Search This Blog

Friday, October 28, 2022

AHADI YA MAISHA - 5

 

     





    Simulizi : Ahadi Ya Maisha

    Sehemu Ya Tano (5)







    Miaka Sita Iliyopita.

    ****

    Frank Joseph kijana king’ang’anizi na asiyekubali kushindwa bado alikuwa hayuko tayari kushuhudia George na Winnie wakifunga harusi hata kidogo. Ukorofi wake ungeweza kuwafanya wajiitao vijana wa kijanja wa miaka hii kumbatiza Frank jina la ‘Jembe’. Mara baada ya kutoroka katika hoteli aliyokuwa akilindwa na vijana walioajiriwa na baba yake, waziri wa nchi mzee Joseph, aliongoza mpaka katika jimbo la Ontananarivo ukiwa mji mkuu wa kisiwa hicho cha nne kwa ukubwa duniani cha Madagascar. Hakujali hata kidogo tatizo aliloliacha nyuma katika hoteli aliyokuwapo jimboni Antseranana ambako aliwaacha vijana waliokuwa wakimlinda na alitambua vijana hao wangempigia simu baba yake na kumweleza kila jambo lililokuwa limetokea.

    Ulikuwa ni wakati ambao Frank Joseph alihitaji kutimiza ndoto yake pekee iliyobakia, ndoto ya kumuua George na Winnie na kujisalimisha mikonomi mwa vyombo vya dola au kujiua pia. Akiwa katika jimbo la Ontananarivo aliweza kufanikisha taratibu zote za kusafiri kwa vile alikuwa na kila kitu kilichohitajika. Siku ya Jumamosi mosi mwezi Juni, Frank Joseph alikuwapo katika moja ya ndege ya shirika la Ethiopia Airways na safari ilikuwa imeanza kuelekea nchini Uholanzi, walitarajia kupita katika jiji la Addis Ababa kabla ya London na mwishoe alitarajia kuingia katika nchi ya ndoto zake, Uholanzi ambao alitarajia kwenda kutimiza kila aliloliwaza. Akiwa anawaza kufikia katika jimbo la Tilburg hakuhofia jambo kwa vile rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Hussein ambaye alimweleza juu ya uwepo wa George na Winnie nchini Uholanzi alishamwahidi kumpokea na kutimiza mipango yake, na ikawa hivyo.

    Baada ya saa hamsini ndege ya shirika hilo la Ethiopia Airways ilikuwa ikiburuza matairi yake katika uwanja mkuu wa ndege wa jimbo hilo la Tilburg, mapigo ya moyo ya Frank yalionekana kushuka na alihisi ndoto zake zingetimia baada ya masaa kadhaa. Mara baada ya kukamilisha taratibu zote za uwanjani hapo Frank Joseph alitoka eneo la mapokezi na kupokelewa na rafiki yake wa siku nyingi, Hussein kijana aliyeonekana mtanashati na mtulivu, sura yake ilionesha kama alikuwa mpole na mwenye huruma. Mara baada ya kuchukua teksi na kuondoka uwanja wa ndege waliendelea na maongezi yao “aah! Brother Frank kwa nini usiachane na mpango huu, aah! Wewe ni mtoto wa kiongozi mkubwa sana nyumbani Tanzania kwa nini usiachane na huyu mwanamke, wako wengi pia utampata mwingine” alisikika Hussein kwa sauti ya chini, alionekana kutopendezwa na jambo ambalo lingefuata baada ya saa kadhaa. Frank hakujibu kitu zaidi sura yake ilibadilika kama alikuwa na maumivu fulani na alionekana akishika kifua chake katika eneo la moyo, bila shaka alikuwa ameumia.

    “kwani shida yako nini ni Hussein?, tatizo hujui kitu naomba usiniudhi nipeleke kwenye hiyo hoteli waliyofikia” alijibu Frank akiwa na sura yenye mwonekano wa hasira hata Hussein alilitambua hilo akaamu kutulia. “sawa hakuna shida ila kwa wakati huu sikusaidii kitu hata kidogo” alijibu Hussein na , Frank alitikisa kichwa. “hey guys you’re just talking, where are you heading to?” (“hey nyie mnaongea tu, kwani mnaelekea wapi?”) alisikia dereva wa taksi hiyo baada ya utulivi wa muda mrefu. Hussein ambaye alikuwa akiendelea kuongea na Frank alikatishwa na kauli hiyo kabla ya kusikika akimwelekeza dereva huyo awapeleke katika hoteli ya Moleneind Motel ambayo ilikuwa maarufu kwa watalii, iliyokuwapo katika kitongoji cha Goirle kilometa kadhaa kotoka eneo la uwanja wa ndege.

    Dereva wa taksi alitikisa kichwa baada ya kutambua eneo walilokuwa wakielekea wakati huo maongezi kwa lugha ya Kiswahili yaliendelea baina ya Frank na Hussein. Baada ya dakika arobaini na tano teksi yao ilikuwa imeegeshwa nje ya geti la hoteli hiyo ya kifahari ya Moleneind Motel.

    Hussein na Frank waliendelea kuongea huku Hussein akionekana alikuwa akimpa maelezo kadhaa Frank. “ sasa shika hii simu na business kadi ya kijana mmoja mtanzania anashirikiana na kundi la wahalifu ndani ya nchi hii linaitwa Blackpino in Europe, linahusisha vijana wengi weusi na wazungu kadhaa, ukihitaji silaha wasiliana na kijana huyu atakusaidia bila kusahau nimekwambia George na Winnie walikuwa katika chumba namba kumi na tatu cha ghorofa ya kwanza, Kila la kheri na sihusiki tena, uwe mwangalifu hapa siyo Tanzania, ulinzi ni wa hali ya juu” alimaliza kuongea Hussein, Frank aliyeonekana kuwa na shauku ya kufanya jambo hakujibu kitu zaidi ya kushuka kwenye gari hilo. Hussein alimuamuru dereva wa gari hilo akaliondoa.

    Frank Joseph alikuwa tayari amefika katika hoteli aliyotambua angetimiza haja zake, Hakuwa na haraka aliamua kuzungua kidogo katika eneo hilo, nia yake ilikuwa ni kuwasiliana na kundi la wahalifu la Blackpino in Europe ili waweze kumsaidia kupata silaha kadhaa. Hakuchelewa alipiga namba ya simu aliyokuwa amepewa kupitia simu ambayo Hussein alikuwa amempa. Aliwasiliana vizuri na kijana mtanzania wa kundi hilo ambaye alikataa kujitambulisha, zaidi alihitaji kuonana na Frank baada ya saa mbili, ikawa hivyo.

    Baada ya saa mbili Frank aliwa amevaa sweta lake kubwa alilolinunua ambalo pia lilikuwa na kofia yake iliyofunika kichwa chake, alionekana katika mgahawa mmoja akiwa amevaa miwani iliyopoteza mwonekano wa sura yake pia. Upande wa pili alikuwa amkekaa kijana wa kitanzania aliyezamia katika nchi hiyo aliyekuwa na kifua kipana ambaye alijitambulisha kwa kina la Moses. Alionekana kuwa ni kijana ambaye hakuwa na huruma hata kidogo. Frank alimweleza kijana huyo kuwa alikuwa akitaka bomu moja lililoweza kuongozwa na rimoti.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jambo hilo lilikuwa dogo kwa Moses ambaye ilimchukua dakika arobaini na tano kwenda kulitafuta na kulifikisha katika mgahawa huo. Wakati huo alikuwa amerudi na kijana mholanzi aliyekuwa malifu wa kundi lao la Blackpino in Europe. Alilifumua bomu hilo na kuliweka katika vipande vidogo vidogo, lengo likiwa vipande hivyo viingie kwa awamu katika hoteli ya Moleneind Motel iliyokuwa na ulinzi mkali ili wasishtukiwe. Kipande cha kwanza cha bomu hilo alipaswa kuingia nacho Frank Joseph wakati akienda kuchukua chumba, kipande cha pili kilipaswa kufuata kupitia kwa kijana mholanzi aliyefanya kazi na Moses, na mwishoe mtanzania huyo alieleza angefuatia ili aweze kukamilisha zoezi la kuliunganisha tena bomu hilo. Frank alifurahishwa na mpango huo kabambe na alikuwa tayari kwa kila kitu.

    Moses na kijana huyo walihitaji dola elfu tano zilizokuwa sawa na milioni sita na nusu za kitanzania kwa wakati huo, jambo hilo halikuwa gumu kwa Frank Joseph aliyekuwa na zaidi ya dola elfu ishirini mahususi kwa kufanikisha zoezi hilo. Aliwalipa nusu na nyinigne aliahidi kumalizia mara baada ya bomu lake kufungwa akiwa katika hoteli ya Moleneind Motel. Bila kupoteza muda, Moses alimkodia teksi Frank na safari ikaanza kuelekea katika hoteli hiyo, ilimchukua dakika kumi tu kufika katika hoteli hiyo. Alikaguliwa na walinzi kadhaa na kuonekana salama kisha alionekana akiongoza kuelekea katika eneo la mapokezi kulikokuwapo dada mrembo. Alikuwa amefunika kichwa chake na kofia ya koti lake pia alikuwa amevaa miwani ‘tinted’ ambayo haikuruhusu kumtambua vyema. Aliitoa miwani hiyo mara baada ya kufika katika meza hiyo ya mapokezi. Baada ya dakika tano alikuwa katika chumba chake chenye hadhi kilichokuwa na kila kitu ndani na wakati huu alikuwa akimpigia simu Moses, alimweleza kuwa alikuwa ameshapata chumba chumba nambari ishirini na tano cha ghorofa ya kwanza ya hoteli hiyo ya Moleneind Motel. Nusu saa baada ye mholanzi ambaye alikuwa akifanya kazi na Moses alifika hotelini hapo na alijieleza kama alikuwa ni mgeni wa Frank, naye alikaguliwa na kuonekana salama, kijana huyo alienda kuwakilisha kipande cha pili cha bomu hilo lililokuwa likiendeshwa kwa rimoti kabla ya kuondoka hotelini hapo.

    Frank alibaki katika chumba chake akiwa na shauku ya kipande cha mwisho kufika ili zoezi lake lianze, saa mbili baadaye Moses alifika hotelini hapo kwa staili ile ile na hakushtukiwa na wakati huu akiwa katika chumba cha Frank alifanikiwa kuliunganisha bomu lile likawa sawa tayari kwa kazi, alichukua malipo yaliyobakia kabla ya kuondoka. Miadi ikawepo baina yao, Frank aliahidi kumpigia simu Moses kuomba msaada zaidi endapo zoezi lake lingeshindikana, akaondoka. Mara baada ya kuondoka ikiwa yapata saa kumi jioni, Frank alitoka katika chumba chake akiwa mwangalifu sana na alioneka kuwa na nia ya kuutambua uwepo ya George na Winnie, Ilimchukua dakika tano kuwaona wapendanao hao. Walikuwa wakicheza pamoja katika eneo la kuogelea la hoteli hiyo, aliumia sana na kutamani kuwafuata ili awafanyie vurugu lakini alijikaza alibaki ametulia katika ukuta aliokuwa amesimama kwa muda wa dakika kadhaa huku akiwaangalia, machozi yalikuwa yakimtoka pasipo kujitambua, aliumia kwa kiasi kikubwa.

    Baada ya nusu saa Winnie na George walitoka katika eneo hilo la kuogelea na walionekana wakitembea pamoja wakiwa wamekumbatiana kuelekea katika chumba chao walichokuwa wamefikia. Frank alibaki amejiinamia katika eneo la ukuta alilokuwa amesimama, Hatimaye George na Winnie wakawa wakipita kando yake pasipo kumtambua. “ So by tomorrow, we will be leaving to Steenwijk national park, we have five more days for our holiday before we go back home…. Tanzania” (“kwa hiyo kesho, tutaondoka kuelekea hifadhi ya taifa ya Steenwijk, tuna siku tano zaidi za mapumziko kabla ya kurudi nyumbani …. Tanzania”) alisikika George, “yes, sound good sweetie” (“ ndiyo imekaa vizuri mpenzi”) Winnie alijibu. Ni wakati ambao kwa uangalifu wa hali ya juu Frank naye alianza kuwafuata kwa nyuma lengo lake lilikuwa ni kuhakikisha kama kweli walikuwa wakikaa katika chumba namba kumi na tatu cha hoteli hiyo. Aliwafuata kwa umakini kabla ya kwenda kuwashuhudia wakiingia katika chumba hicho namba kumi na tatu kama alivyoelezwa awali na Hussein, bila kupoteza muda na yeye aliongoza mpaka katika chumba chake huku akiwaza kukamilisha zoezi lake. Chumba chake namba ishirini na tano na cha kina George havikuwa na umbali mrefu sana na aliweza kuwafuatilia kama angehitaji.





    Jambo lilolomuumiza kichwa Frank wakati huu lilikuwa ni moja, alihitaji kadi kuu ambayo iliweza kufungua milango yote ya hotelini hapo kwani kadi aliyokuwa nayo iliweza kufungua mlango wake tu. Baad a ya kufikiria kwa dakika kadhaa alipata wazo, alipiga simu eneo la mapokezi na kuagiza chakula na kinywaji. Aliahidiwa kuwa angehudumiwa baada ya dakika kadhaa na ikawa hivyo. Mhudumu mmoja mrembo wa kike alifika katika chumba chake akiwa na chakula, Frank alijongea katika eneo la sebule ndogo ya chumba chake na kumshuhudia akimwekea chakula mezani. Alichukua bia moja ya kopo aliyoiagiza na kuanza kuinywa kwa haraka alijibadilisha na kuonekana kama alikuwa amechoka sana. Wakati huo alikuwa akimwangalia kwa umakini mhudumu huyo na aligundua alikuwa na kadi kuu ya kufungulia milango yote katika mfuko wake wa nyuma wa sketi aliyovaa, hapo alipata faraja kabla ya kusikika huku akishika kichwa chake. “oops! This head sucks damn, aaah! I’m getting out of control, oops! Please help me…” (“oops! Kichwa changu kinaniuma, aaah! Nahisi kuzidiawa, oops! Naomba unisaidie…” hakumaliza kauli yake hiyo alijiangusha chini kama gogo, hali iliyomshtua mhudumu huyo wa kizungu aliyemsogelea kwa haraka akiwa na hofu. “hey what’s the problem, someone help, help he’s in trouble” (“hey kuna tatizo gani?, naomba mnisaidie, mnisaidie, ana matatizo”) alipaza sauti mhudumu huyo wakati akijaribu kumwinua Frank ambaye kwa taabu aliinuka huku akiwa amekumbatiwa na mrembo huyo, ni wakati ambao alitimiza lengo lake, alichomoa kadi kuu ya hoteli hiyo katika mfuko wa nyuma wa mhudumu huyo na kuichomeka kwenye shati alilokuwa amevaa. Aliendelea kuwa katika hali yake ileile ya kulegea. Mhudumu huyo alimkalisha kwenye kochi kabla ya kuanza kumfungua vishikizo vya shati lake, ni wakati ambao kidogo Frank alijifanya amerudiwa na fahamu. “hey what’s up? Can I call our hotel doctor?” (“hey, una nini? Nimuite daktari wa hoteli yetu?”) alisikika mhudumu huyo. “no, It’s all right now, this happens to me several times, I have my pills that I use, thanks for helping me” (“hapana, kila kitu kiko sawa sasa, hii inanitokea mara kadhaa, nina vidonge vyangu ninavyovitumia, ahsante kwa kunisaidia”). Alisikika Frank akiwa amekaa katika kochi hilo ilhali akiwa amelegea. Mhudumu huyo alikaa katika chumba hicho kwa dakika kadhaa kabla ya kuondoka baada ya kuona Frank ametengamaa kidogo na alikuwa hataki aitwe daktari.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara baada ya mhudumu huyo kuondoka Frank alishangilia kama mchezaji akifunga goli na wakati huu kazi iliyokuwa imebakia ilikuwa ni moja tu, alihitaji kuwafuatilia kwa umakini George na Winnie ili atege bomu wakati wakiwa wametoka katika chumba chao. Hakuwa na shaka kwani alikuwa ameiba kadi iliyoweza kufungua kila mlango katika hoteli hiyo. Majira ya saa moja jioni alikuwa akizunguka zunguka eneo la karibu na chumbani kwake huku akiwa amejifunika na kofia ya koti lake bila kusahau miwani yake aliyokuwa ameivaa. Ilimchukia saa mbili kukaa nje hapo, majira ya saa tatu, Winnie na George walitoka katika chumba chao na waliekea upande wa pili wa korido hiyo. Akiwa na furaha alielewa watu hao walikuwa wanaenda kula chakula cha jioni wakati huo, hakupoteza muda aliingia kwenye chumba chake na kuchukua bomu lililokuwa limeunganishwa alitoka kwa haraka na kutembea mpaka katika chumba nambari kumi na tatu. Aliitumia kadi aliyoiiba kuingia katika chumba hicho, na alifanikiwa, aliongoza haraka mpaka katika kitanda cha chumba hicho na alilitega bomu hilo chini ya godoro kubwa lililokuwapo. Alikuwa amelitegua bomu hilo lililoonesha lilikuwa limesalia na masaa kumi na mbili ili lilipuke kama lisingefyatuliwa na rimoti ambayo Frank alikuwa nayo. Hivyo lingelipuka saa nne asubuhi siku iliyofuata.

    Frank alitoka haraka katika chumba hicho kabla ya kukifunga kama awali na aliongoza mpaka kwenye chumba chake akiwa na amani kidogo. Amani yake ilikamilia zaidi baada ya nusu saa kwani aliwaona George na Winnie wakirudi katika chumba chao. Hapo alitabasamu na hakuwa na mpango na kadi aliyoiiba kwani aliirejesha mapozkezi na kueleza kuwa ilikuwa imeangushwa na mhudumu aliyemhudumia awali. Wakati huu Frank chakula kilipita mdomoni baada ya saa kadhaa za kuwapo nchni humo. Alitulia kwa muda mrefu katika chumba chake huku mpango wake ukiwa kuondoka saa kumi na moja asubuhi, muda aliopanga kufyatua bomu alilolitega kwa kutumia rimoti pia, hakulala usiku mzima akiwaza muda huo ufike. Hatimaye ilipotimia saa kumi na moja asubuhi aliondoka hotelini hapo, ingawwaje aliwekewa vikwazo kadhaa vya kuondoka muda huo bila kutoa taarifa awali lakini alijijtetea kama alikuwa amepigiwa simu ya dharura. Frank hatimaye aliondoka kwa mguu katika hoteli hiyo huku akiwa amekataa hata msaada ya usafiri wa bure wa hoteli hiyo ya kifahari ya Moleneind Motel akidai kuna mtu angemfuata eneo hilo. Aliongoza mpaka nje ya hoteli hiyo na kwenda kusimama umbali wa mitaa kadhaa kutoka kwenye uzio wa hoteli hiyo. Alikuwa amesimama chini ya mti mmoja uliokuwa karibu na hoteli hiyo na aliiona vizuri hoteli hiyo kwa ndani hata chumba cha kina George alikiona. Hakuwa na hofu na rimoti yake kwani alielezwa kuwa ilikuwa inaweza kufyatua bomu lililotegwa hata kwa umbali wa mita mia tano na yeye hakuzifikia mita hizo, alikuwa karibu sana. Ilikuwa yapata saa kumi na moja na dakika ishirini wakati ambao Frank aliitoa rimoti hiyo kabla ya kuvuta pumzi, alionekana akiwa tayari kwa kufyatua bomu alilotega, alikiandaa kidolegumba na taratiiiiibu alianza kukishusha tayari kwa kulifyatua…..

    Nini kitafuata? Bomu hilo litalipuka? Na kama halitalipuka Winnie na George wataponaje? Usikose sehemu inayo fuata.

    Ikawa hiyo Frank alibonyeza kitufe cha rimoti hiyo huku akiwa anatabasamu lakini jambo la kushangaza bomu lake halikulipuka, alirudia tena kwa hasira lakini halikulipuka pia. Ni wakati ambao hata kijasho chembamba kilianza kumtoka, hakuamini kilichokuwa kikiendelea. Alitamani kama arudi hotelini na kwenda kulifyatua bomu katika chumba cha kina George ili wafe wote lakini jambo hilo lilikuwa kama ndoto ambazo hazikuweza kuwa na nafasi hata kidogo. Frank aliendelea kutokwa na jasho katika eneo hilo lililokuwa na baridi kali, alikuwa amechanganyikiwa na kila jambo lililokuwa likiendelea, alipojaribu kumpigia simu Moses ili kujua namna yeyote ya kufanya lakini kijana huyo alikuwa hapatikani.

    Aliendelea kuzunguka eneo hilo huku akibonya kwa kukilazimisha kitufe cha rimoti hiyo pasipo mafanikio, kadri muda ulivyozidi kusogea ndivyo alivyozidi kujihisi kuchanganyikiwa. Wakati huo wa majira ya saa moja asubuhi alikuwa amejificha katika miti kadhaa ya urefu wa kimo chake iliyokuwapo kando ya hoteli hiyo ya Moleneind Motel. Wakati huo alikuwa amebakiwa na nafasi moja pekee aliyoisubiri kwa hamu, alikuwa akiombea George na Winnie wachelewe kutoka katika hoteli hiyo ili bomu alilotega lilipuke nao majira ya saa nne asubuhi kama lilivyopaswa kulipuka pasipo kutumia rimoti.

    Alibaki akizunguka zunguka eneo hilo huku akijificha na hatimaye ilitimia saa tatu na nusu, alikuwa amebanwa na haja ndogo ambayo mishipa yake ya fahamu haikuweza kuitambua. Alikuwa akizunguka eneo hilo huku akiwa amebana miguu yake na kichwa chake kikiwa kimeelekezwa kwenye chumba walichokuwa wakikaa George na Winnie, kwa umbali aliokuwapo bado macho yake yaliweza kumhakikishia kuwa kulikuwa na watu katika chumba hicho kutokana na mizunguko ya hapa na pale aliyofanikiwa kuiona kama watu walikuwa wakizungua, ingawaje hakuweza kumtambua hata mmoja. Bado alikuwa akiamini watu hao walikuwa ni George na Winnie, alihisi walikuwa wakijiandaa kwa safari ya kuelekea katika hifadhi ya taifa ya nchi hiyo ya Steenwijk iliyopo katika jimbo la Breda, kama alivyo wasikia wakiongea.

    Ilipotimia saa tatu na dakika hamsini, tabasamu lililoanza kumpotea usoni lilianza kurudi taratibu kwa vile bado aliendelea kuona mizunguko katika chumba cha kina George kwa mbali. Ni wakati ambao alianza kutembea taratibu akiiacha hoteli hiyo ya Moleneind Motel lakini macho yake yakiwa yameelekea katika hoteli hiyo. Alitaka kuwa mbali na hoteli hiyo wakati bomu alilotega likilipuka, alifanya hivyo akijihakikishia ugumu wa kuweza kukamatwa na walinzi wa hoteli hiyo. Ilipotimia saa tatu na dakika hamsini na nane kama alivyoona katika simu yake Frank alianza kukimbia kabisa wakati huo alikuwa umbali wa kilometa moja na nusu lakini bado aliweza kuiona hoteli ya Moleneind Motel kwa vile eneo hilo lilikuwa la tambarare. Mwishoe aliishia kusimama katika eneo lililokuwa kando ya barabara kuu ielekeayo katika jimbo la Breda ambako pia inapatikana hifadhi ya taifa ya Steenwijk. Lilikuwa ni eneo la kilomita kadhaa zilizobakia ili kufika eneo la mjini la jimbo hilo la Tilburg ambako siku moja kabla Frank alikutana na Moses na kuweza kulinunua bomu alilokuwa amelitega bomu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati huo saa yake ilionesha ni saa saa tatu na dakika hamsini na tisa na sekunde thelathini, Frank alikuwa amebanwa na haja ndogo lakini bado alijikaza kama vile alikuwa ameshika kitu muhimu alichoambiwa asikiachie. Macho yake yalikuwa yameelekezwa katika hoteli ya Moleneind Motel huku jasho likimtililika bila shaka baadhi ya mishipa yake ya fahamu ilikuwa haifanyi kazi kwa wakati huo. “ hamsini na tatu, … nne, hamsini na tano, sita, saba, hamsini na nane, tisa ….sitiniii” Alisikia kwa sauti Frank akihesabu kando ya eneo hilo lililokuwa na miti mifupi baadhi iliyokuwa imepandwa kando ya barabara huku likiwa tulivu.

    Wakati huo bomu lake halikumwangusha lililipuka na kwa mbali aliweza kuushuhudia mlipuko huo, ni wakati ambao Frank aliruka na kushangilia. Ni kweli akili yake haikuwa sawa kwani pia huu ni wakati ambao haja yake ndogo ilianza kumtoka bila kujitambua. Bila shaka mishipa yake ya fahamu kupitia akili yake ilielezwa kuwa matatizo yalikuwa yamefika kikomo. “Safiii, kufeni wajinga nyinyi, hata kwenda jela naweza kujipeleka tu washenzi nyie” Alisikika Frank Joseph akiongea na kuruka ruka eneo hilo kwa furaha, kwa mtu ambaye alikuwa akipita ilikuwa ni rahisi kumhisi ni mwehu zaidi kutokana na lugha yake ya Kiswahili aliyoitumia.

    Ikiwa ni sekunde kadhaa tangu mlipuko huo utokee ilhali akiwa bado anashangilia ushindi wake lilionekana gari moja la shirika la utalii likiongoza eneo hilo likitokea barabara iliyoelekea katika hoteli ya Moleneind Motel. Ni wakati ambao Frank alitulia kidogo akiwa na lengo la kuonekana ni mtu sawa tu, ni wakati ambao alikuwa akiwaza jambo la kufanya pia baada ya kifo cha Winnie na George kama alivyoamini. Alibaki akiwa mtulivu barabarani ilhali gari hilo likijongea taratibu, hatimaye lilianza kupita kando yake. Ni wakati ambao Frank alihisi kuchanganyikiwa ghafla, kwani ndani ya gari hilo aina ya Range Rover ambalo lilikuwa limetengenezwa maalumu kwa watalii aliweza kumwona George na Winnie, Walikuwa wamekaa siti ya nyuma ya gari hilo huku wakiwa wamekumbatiana, walionekana kama walianza zoezi hilo ndani ya sekunde kadhaa zilizokuwa zimepita. Ubize wa watu hao na zoezi hilo ndiyo uliowafanya washindwe hata kumwona Frank aliyekuwa nje huku akiwa mdomo wazi. Taratibu alianza kushuka chini pasipo kujitambua na mwishoe aliishia kukaa chini alikuwa amechoka na kila jambo lililokuwa limetokea.





    Machozi na hasira za waziwazi vilionekana katika paji la uso wake, alikuwa amechanganyikiwa kwa wakati mwingine na wakati huu ilikuwa zaidi. Hata hisia za yeye kufa aliona zikimrudia haraka, alitaka kufa na George na Winnie ili wote wakose penzi lililopiganiwa kwa mwanamke mmoja huyo. Wakati huo akili yake ilimcheza na haraka aliamua kumpigia simu tena Moses, wakati huu simu ya kijana huyo iliita. “Dude, I need your help, our plan was not perfect but I want them died today, I don’t care even if it will cost me my life” (“ Ndugu, nahitaji msaada wako, mpango wetu haukwenda sawa lakini nataka wafe leo sitajari hata kama ikinigharimu maisha”) Alisikika Frank mara baada ya simu yake kupokelewa. Moses alimwahidi Frank kumsaidia kutimiza zoezi la kumuua George na Winnie ila kwa sharti moja la kumlipa dola zaidi ya elfu kumi na tano alizokuwa amebakiwa nazo Frank, ambazo zilikuwa sawa na kiasi cha milioni kumi na nane za kitanzania kwa wakati huo. Frank hakuwa na shida na suala la pesa, lengo lake kubwa lilikuwa ni kushuudia watu wake hao wameuawa, aliahidi kulipa fedha hizo kama Moses na vijana wenzie wa kundi la Blackpino in Europe walivyozihitaji.

    Baada ya nusu saa Frank Joseph alikuwa katika mgahawa waliokutana na Moses siku moja iliyokuwa imepita. Moses alikuwa na vijana wenzie wanne wa kundi la Blackpino in Europe na walikuwa tayari kwa kazi. Ni wakati ambao Frank pia alikuwa akikamilisha malipo yao ya awali kabla ya zoezi hilo kuanza. Hatimaye zoezi hilo lilikamilika na waliongoza mpaka katika gari lililokuwa la rangi ya bluu ambalo walifika nalo vijana hao wa Blackpino in Europe, gari ambalo lilikuwa limechakaa pia.

    Wakiwa na Frank safari yao ilianza wakielekea katika jimbo la Breda kwa vile walikuwa wamepewa uhakika na Frank kuwa George na Winnie walikuwa wameelekea katika jimbo hilo ili kwenda kutalii katika hifadhi ya taifa ya Steenwijk. Gari la vijana hao ambalo lilikuwa likiendeshwa na kijana mmoja wa kiholanzi aliyeonekana kuathirika kwa kiasi kikubwa na dawa za kulevya lilikuwa kwenye kasi ya ajabu. Muziki wa Hiphop ulikuwa ukiendela kupigwa kwa sauti kubwa, wakati huo, Frank alipata faraja kwani alitambua kuwa George na Winnie hawangeweza kutoka katika jaribio hilo lililokuwa limekaribia. Uhakika wake huo ulitokana na silaha nzito aina ya AK 47 alizoziona katika gari hilo. Silaha hizo zilikuwa nne na zilikuwa zimewekwa risasi za kutosha na Moses ambaye aliendelea kuzisafisha huku akivuta msokoto wa bangi mdomoni mwake. Moshi uliotoka pamoja na sauti kubwa ya muziki viliwafanya wahalifu hao waone maisha mazuri na pengine walihisi walikuwa wakielea angani, kila jambo lililkuwa rahisi kwao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya gari hilo kuendeshwa kwa kasi kwa saa kadhaa hatimaye waliweza kuliona gari ambalo Frank aliwathibitishia kuwa Winnie na George walikuwapo. Lilikuwa gari la shirika lilokuwa likihusika na watalii, gari lililokuwa aina ya Range Rover. Wakati huo Frank moyoni aliweza kutulia kidogo ingawaje furaha yake ingetimia kama wahusika wake wangekufa kabisa. Gari hilo la shirika la utalii ambalo lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kawaida ndilo lililowafanya hata wao kupunguza mwendo wa gari lao huku wakiendelea kuwafuatilia na hatimaye baada ya saa kadhaa safari hiyo iliishia katika eneo lililokuwa karibu na geti kuu la hifadhi ya Steenwijk. Kwa mbali George, Winnie na wahusika wa kampuni hiyo ya utalii walionekana wakiwasaidia kushusha mizigo yako kutoka katika gari hilo.

    Wakati huo Frank akiwa na vijana wa kundi la Blackpino in Europe wakiongozwa na Moses walikuwa wameshuka kwenye gari lao huku wakiwa umbali zaidi ya mita mia sita kutoka eneo hilo lililokuwa tulivu kwa kiasi kikubwa. Moses alionekana akiikoki bunduki yake aina ya AK 47 tayari kwa kazi, vijana wake pia walionekana wakimeza vidonge vya dawa za kulevya huku wakivuta pumzi, dhahiri kuna jambo zito lilikuwa tayari kutokea. “Dawg just give me machine gun, I will kill them for sure” (“mwanangu nipe mimi bunduki, nitawaua nakuhakikishia”) Alisikika Frank akiongea kwa sauti ya kujiamini. “Hey relax, everything is under control of us now, you have paid your bill then just wait and see, right? Stay here, you have had a chance to kill but you didn’t, let me handle this business”) (“hey tulia, kila kitu kiko chini yetu saa, umetulipa, kwa hiyo subiri na ushuhudie sawa? Subiri hapa, ulikuwa na nafasi ya kuua na hukuweza, hii kazi niachie mimi”) Alisikika Moses akiongea huku akiwakonyeza vijana wake ambao waliingia haraka kwenye gari hilo. Frank Joseph alibakia tu ametoa macho hakupewa hata nafasi ya kuingia kwenye gari hilo, kazi yake ilikuwa kusubiri na kuona Moses akiua kama alivyoahidi, alitamani kuua yeye lakini ukweli unabaki pale pale kuwa hakujua hata jinsi ya kutumia silaha hiyo kubwa ya kivita, alibaki ametulia akiwa na hamu ya kushuhudia watu waliomuumiza kichwa wakiuawa.

    Mara baada ya Moses kuingia kwenye gari, dereva wa gari hilo ambaye alikuwa kijana mholanzi, aliliwasha gari hilo kabla ya kulikanya mafuta kwa nguvu huku akiwa amezuia breki za gari pia, gari hilo matairi yake yalikuwa yakizunguka kwa kasi huku yakitoa moshi lakini bado llilikuwa halijaruhusiwa. Moses alikuwa amekaa siti ya mbele pembeni na dereva huyo huku akiwa ameishika vizuri bunduki yake, mara alionekana akimtikisia kichwa dereva huyo aliondoe gari hilo. Ikawa hivyo gari hilo liliondolewa kwa kasi ya ajabu likielekea usawa wa eneo walilokuwa wakina George ambao bado walikuwa wakiweka sawa mizigo yao iliyokuwa mingi. Ni wakati ambao Moses alikuwa amesimama na kutoa kiwiliwili chake nje ya gari akiwa tayari kwa kuwaua Winnie na George. Baada ya sekunde kadhaa walikuwa usawa husika wa watu hao, awali shabaha yake ilielekezwa kwa Winnie, alifyatua risasi ambayo aliamini ilimpata mwanamke huyo ingawaje alimshuhudia George akirukia usawa wa Winnie, alipiga risasi ya pili na hii ilikuwa maalum kwa George wakati huu bila shaka aliihakikisha imempata sawasawa pia. Kwani alikirudisha kiwiliwili chake ndani ya gari kabla ya kusikika “Hey drive drive, I’m so bad son I got them all down homie” (“Hey endesha, endesha, mi mbaya mwanangu, nimewapiga wote wamenguka chini” Alisikika Moses ambaye alikuwa amegeuza kichwa chake kuangalia eneo ambalo alikuwa amempiga Winnie na George.

    Dereva wa gari hilo huku akipiga kelele naye alikuwa amegeuza kichwa chake akiangalia eneo hilo ambalo George na Winnie walikuwa wamepigwa risasi, vijana wenzao pia wa kundi lao la Blackpino in Europe walikuwa wameelekeza macho yao nje ya gari huku wakishangilia. “damn! that’s my boy you’re so bad” (“huyo ndo kijana wangu, we ni mbaya sana”) Alisikika dereva wa gari hilo ambaye alikuwa ameacha kuangalia mbele. “Aaaaaaaaaaah!.........” Ilikuwa sauti ya mwisho ya Moses ambaye alikuwa wa kwanza kuliona gari la mizigo lililokuwa kwenye kasi ya kupindukia ambalo lililkuwa mbele ya uso wa gari lao, ajari mbaya ndiyo lilikuwa jibu lililofuatia baada ya gari lao kugongana uso kwa uso na gari hilo la mizigo.

    Frank kwa mbali alikuwa ametoa macho akiangalia kila jambo lililokuwa limetokea, tabasamu pana ndilo lililokuwa limetanda usoni mwake, macho yake yalikuwa yameelekezwa kwenye eneo ambalo George na Winnie walikuwa wamepigwa risasi, eneo walillokuwa na waongozaji wa watalii. Alikuwa amesikia sauti nzito upande ambao gari la vijana wa Blackipino in Europe lilikuwa limeelekea lakini aliipuuzia. Kwa jinsi alivyoona aliamini George na Winnie walikuwa wameshafariki, wakati akiwa na shauku ya furaha ya jambo hilo alishuhudia upande mwingine wa barabara hiyo ukiwa unafuka moshi. Ulikuwa ni upande ambao gari la kina Moses lilikuwa limeelekea. Baada ya dakika moja alilishuhudia gari la askari wa hifadhi hiyo ya Steenwijk wakiongoza gari lao kwa kasi kuelekea katika upande huo uliokuwa ukifuka moshi. Hakupoteza muda, alijua azimio lake lilikuwa limekamilia aliondoka akikimbia kwa kasi akifuata barabara kuu iliyokuwa ikielekea katika jimbo la Tilburg, alikuwa akipiga kelele peke yake akishangilia kila jambo lililokuwa limetokea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alitumia muda wa saa moja akikimbia kwa furaha kabla ya kufika katika eneo lilokuwa na makazi ambalo lilipakana kwa kilometa kadhaa na hifadhi ya taifa ya Steenwijk, eneo ambalo lilikuwa likikaliwa na wakazi wachache waliokuwa wawindaji. Akiwa katika makazi hayo hakupoteza muda alikodi gari moja huku akiwa amemweleza dereva wake ampeleke katika kitongoji cha Etten kilichokuwapo karibu na eneo hilo la jimbo la Breda, ikawa hivyo dereva huyo aliliendesha gari hilo kwa kasi kabla ya kuishia kumfikisha Frank katika hoteli moja ya kawaida iliyokuwapo katika kitongoji hicho cha Etten. Wakati huo kijana Frank Joseph alikuwa ametulia akisubiria kwa hamu jambo ambalo lingefuata kupitia vyombo vya habari, ni wakati ambao alibadilika ghafla, hakuwaza tena kujisalimisha kituo cha polisi kama awali. Hakuwaza pia kurudi Tanzania kwa vile alitambua serikali ya jamhuri ya Tanzania ilikuwa ikimtafuta kwa udi na uvumba baada ya kutoweka kwake kwenye jela alilofungwa katika mazingira ya kutatanisha.

    Jambo aliloliwaza ni moja tu baada ya kutambua kuwa George na Winnie walikuwa wamefariki, aliwaza kuhakikisha anamjulisha baba yake kuwa alikuwapo nchini humo Uholanzi. Aliwaza kumwomba baba yake huyo fedha ili aanze maisha akiwa katika nchi yeyote ya Ulaya na kwa wakati huo hakufikiria hata kidogo kurudi Tanzania. Alikuwa chumbani kwake kifua wazi huku akiwa ameitolea macho televisheni moja iliyokuwa ikirusha matangazo yake, lakini pia alikuwa akibadilisha mara kadhaa vituo vya televisheni. Lengo lake lilikuwa ni kujua kila jambo lililokuwa limetokea baada ya tukio la George na Winnie kupigwa risasi lakini pia alihisi kuwa Moses na vijana wake walikuwa wamepata ajali.

    Majira ya saa moja jioni aliweza kupata jibu, kituo kimoja cha televisheni kilianza kuelezea tukio zima lilokuwa limetokea. Aliweza kughadhabika na kuhisi kazi nzito ilikuwa inapaswa kuendelea baada ya kugundua Winnie alikuwa hajapigwa risasi, mtangazaji huyo alieleza kuwa kijana mtanzania George Innocent alikuwa amepigwa risasi mbili mgongoni wakati akijaribu kumkinga mpenzi wake na hali ya kijana huyo ilikuwa mbaya sana. Taarifa hiyo ilielezea pia vifo vya watu saba kwa mpigo waliopata ajali wakiwapo vijana watano waliohisiwa kuwa ni wa kundi la Blackpino In Europe. Na wengine vijana wawili waliokuwa kwenye gari kubwa la mizigo. Bado uchunguzi wa polisi ulikuwa ukiendelea, wakati Frank akiwa na imani kuwa George lazima angekufa hakuumia hata kidogo kusikia vifo vya vijana wa Blackpino in Europe. Alikuwa amebakiwa na dola elfu saba mia tano ambazo alipaswa kumlipa Moses na vijana wake baada ya kuwaua Winnie na George, fedha hizo alikuwa nazo kwenye kibegi chake kidogo.





    Alionekana akizunguka zunguka katika chumba chake ndani ya hoteli hiyo, chumba kilichokuwa katika ghorofa ya pili. Alikuwa akiwaza jambo, wakati huo aliwaza kutumia pesa alizobakiwa nazo ili kuhakikisha anamuua Winnie pia, roho ya kuua ilikuwa imeutawala moyo wake. Aliendelea kuwa katika fikra hizo nzito alhali akiwa ameacha kuangalia televisheni, ghafla alishtushwa na jambo. “…. This anonymous dude who has been named as Ramadhan Abdallah is wanted by police officers all over the country, whoever sees him please contact any neaby police station, the prizes will be awarded, he’s believed to be a terrorst who has murdered two hotel cleaners of Moleneind Motelby bomb explosion” (“Mtu huyu asiyejulikana vizuri ambaye ametajwa kama Ramadhan Abdallah, anatafutwa na maofisa wa polisi nchi nzima, yeyote atakaye mwona anaobwa kutoa taarika katika kituo cha karibu cha polisi, anaaminika kuwa ni gaidi aliyewauwa wafanyakazi wa usafi wawili wa hotel ya Moleneind Motel kwa mlipuko wa bomu”

    Frank Joseph alikuwa ameitolea macho televisheni hiyo ambayo picha yake ilikuwa imejaa kwenye kioo chake. Jina la Ramadhan Abdallah ndilo alilokuwa amelitumia awali wakati akichukua chumba katika hoteli ya Moleneind Motel. Alitumia jina hilo wakati akiondoa uwezekano wowote wa kuweza kugundulika na George na Winnie waliokuwa katika hoteli hiyo awali. Aliamini ni kweli alikuwa ameua watu wawili kwa kutumia bomu lake alilolitega kwa vile mara ya mwisho aliwashuhudia kama watu walizunguka katika chumba walichokuwapo wakina Winnie na yeye aliami walikuwa ni watu wake hao waliomuumiza kichwa.

    Akili yake aliona kama imeanza kushindwa kufanya kazi kwa vile ghafla alijikuta akiogopa hata kutoka nje akihofia kukamatwa. Alibaki akizunguka katika chumba hicho huku akitokwa jasho, alipokumbuka hali ya George aliyeamini kuwa angekufa alipata faraja kidogo. Wakati huu aliyakumbuka maneno ya rafiki yake Hussein ambaye alimpokea kutoka uwanja wa ndege wa Tilburg na kumsihi kuwa makini. Mambo yalivyokuwa yakienda yalimkubusha pia kuwa hakuwepo Tanzania bali Uholanzi. Kwa vile teknolojia ilikuwa imetumika na kuweza kupata picha yake kupitia kamera zilizofungwa katika hoteli ya Moleneind Motel, mpaka wakati huo picha yake ilikuwa kwenye vyombo vya habari tofauti.

    Baada ya saa mbili wakati akiwa katika dimbwi hilo la mawazo ghafla alisikia ving’ora vya magari ya polisi vikisikika, alitembea haraka mpaka katika dirisha la chumba hicho na aliweza kushuhudia magari matatu ya polisi yakiwa yameegeshwa na askari walishuka wakikimbia kuelekea kwenye hoteli hiyo. Frank alisononeka kidogo kabla ya kutabasamu bila shaka tabasamu lake lilitokana imani yake kubwa kuwa George asingepona na wote wangemkosa Winnie, alitembea haraka akielekea chooni huku akiendelea na zoezi la kuivunja kadi yake ya benki, alipoivunja alionekana akichanachana hati yake ya kusafiria iliyotumia jina la Frank Joseph, alipofika chooni alivitupa vitu hivyo kwenye tundu la choo kabla ya kuhurusu maji yaliyovipoteza kabisa. Alibakia na kitambulisho chake bandia kilichomtambulisha kama Ramadhan Abdallah raia wa Kenya. Alitembea akitabasamu kabla kwenda kujilaza kimgongo katika kitanda chake. Mlango wa chumba chake ulikuwa haujafungwa na alionekana yuko tayari kwa kukamatwa.

    Akiwa ametulia kitandani hapo alisikia sauti za makanyagio ya viatu vya askari waliokuwa wa wakikimbia nje ya kordo ya ghorofa hiyo ya pili. Alibakia mtulivu huku akitambua mwanzo wake wa kukamatwa ulikuwa umefika. “Stay calm in your room… everyone doesn’t move” (“tulia kwenye chumba chako…. Kila mmoja usitembee”) Alisikika afisa mmoja wa jeshi polisi akiongea kupitia kipaza sauti, maneno yake yalimfikia Frank pia aliyekuwa mtulivu kitandani kwake. Baada ya dakika tano alihisi zoezi lililokuwa likiendelea katika hoteli hiyo, wakati huo alikuwa amekaa kitandani kwake. Aligundua kuwa askari hao walikuwa wakimtafuta mhalifu wao chumba kimoja mpaka kingine, na alitambua mhalifu wao alikuwa ni yeye alibakiwa akiwa ametulia ihali akiwa muoga sana.

    Mara alisikia askari hao wakigonga mlango wa chumba chake, Frank alisimama akiwa amenyoosha mikono yake akiwa tayari kwa kukamatwa. Hakwenda kufungua mlango kwa vile alitambua kuwa ulikuwa wazi, hatimaye askari watatu wa kiholanzi waliingia katika chumba chake wakiwa wameshika picha mkononi mwao. Frank alibaki ametulia huku akiwa anatetemeka, askari mmoja alimsogelea na kuonekana akimwangaliwa kwa umakini usoni. “Where is your identity card?” (“kitambulisho chako kiko wapi?”) Lilikuwa swali la kwanza la askari ambaye alikuwa akimwangalia kwa umakini Frank Joseph, alionekana kama alikuwa kiongozi wa wenzie. Bila kupoteza muda kijana huyo alitoa kitambulisho chake na kumkabidhi askari huyo ambaye alianza kukiangalia. Askari wengine wawili walikuwa wakikikagua chumba hicho kwa umakini mkubwa.

    Hawakuona kitu chochote walichokifikiria vibaya katika chumba hicho, askari aliyekuwa ameshika kitabulisho cha Frank Joseph bado alikuwa akikiangalia kwa umakini alionekana kama alikuwa amegundua jambo lakini hakuweza kulithibitisha. Kijana huyo alikuwa akitetemeka na hilo lilionekana wazi wazi, askari mwingine alimsogelea mwenzie na kuchukua kitambulisho cha Frank Joseph kabla ya kusikika akikisoma “Ramadhan Abdallah, the coward dude, why are you trembling?” (“Ramadhan Abdallah, kijana muoga, kwa nini uanatetemeka?”). “I don’t know what’s going on” (“Sijui kinacho endelea”) Alijibu Frank ambaye bado alikuwa akitetemeka.

    Wakati askari wa awali akiwa bado amemkazia macho, ghafla askari mwingine aliingia katika chumba hicho cha Frank. “Hey officers, we have caught our German criminals in the other room, let’s go” (Askari, tumewakamata wahalifu wetu wa kijerumani katika chumba kingine, tuondoke”) Alisikika askari huyo na askari hao walianza kuondoka katika chumba hicho, askari aliyekuwa akimwangalia kwa umakini Frank ambaye alionekana kama ni kiongozi wa wenzie pia naye alianza kutoka katika chumba hicho. Alitembea huku akigeuka kumwangalia Frank, bado hakuridhika na maamuzi yao ya kuondoka wakiwa wamemwacha kijana huyo alikuwa akimhisi vibaya.

    Mara baada ya askari hao kutoka Frank alivuta pumzi ndefu, hakuamini jambo lililokuwa limetokea alijihisi kama alikuwa ndotoni. Aliufunga mlango wa chumba chake kabla ya kuelekea dirishani na kuanza kuangalia nje. Aliwashuhudia askari hao wakiwapakia vijana wanne wa kijerumani kwenye gari moja wapo kati ya matatu yaliyokuwapo. Mwishoe askari hao waliingia kwenye magari hayo na waliondoka katika hoteli hiyo, ni wakati ambao Frank hakuamini kabisa alichokuwa akikishuhudia, alikuwa amepona kutoka katika mkono wa askari hao wa Uholanzi. Alibaki amekaa kitandani kwake huku akiwaza jambo la kufanya kwa wakati huo, alikuwa akiwaza kuondoka katika hoteli hiyo haraka iwezekanavyo. Jambo lililomfanya aendelee kusita sita juu ya maamuzi yake hayo lilitokana na ukweli kwamba hakujua eneo la kuelekea wakati huo wa saa mbili usiku, taarifa za kutafutwa kwake nchi nzima ndizo zilimkatisha tamaa kabisa. Bado alikuwa njia panda.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    MWISHO







0 comments:

Post a Comment

Blog