Search This Blog

Friday, October 28, 2022

WABEBA NDOTO (THE DREAM HOLDERS) - 3

 









    Simulizi : Wabeba Ndoto (Dream Holders)

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Mechi ilianza huku timu ya the thunders ikimiliki mpira,kelele zilizidi kila mara Paul aliposhika mpira.Pasi nzuri ilitolewa kwa Paul ambaye aliipokea vizuri na kukimbia kwa kasi huku akikwepa mabeki wa timu pinzani kwa ustadi mkubwa na kufunga goli zuri lililowashangaza watu wote.Uwanja mzima ulipiga kelele na kuimba jina la Paul,kasi yake na chenga zake za ajabu zilikuwa kivutio kwa watu wengi,alikuwa na kipaji cha ajabu.Kylie alishangilia sana kila mara Paul alipokamata Mpira na kufunga goli,beasts walitawaliwa sana kimichezo na hilo lilichangiwa sana na uwezo binafsi wa Paul.Mpaka wanaelekea mapumziko timu ya the thunders ilikuwa kifua mbele ikiongoza kwa tofauti ya magoli matatu kwa sifuri.

    "Safi sana,tuendelee hivyo hivyo,Paul Safi sana na Daniel umefanya kazi kubwa.Nani anajua chochote kuhusu Gerald sijamuona leo" muda huo huo Gerald aliingia akiwa ameshika vizuri begi lake mgongoni,kocha aligeuka kwa haraka "shikamoo kocha" " ooh Gerald! karibu ndio nilikuwa nakuulizia mda si mrefu vipi unaweza kucheza leo?" Gerald alitikisa kichwa chake kuonyesha kukubali "vizuri,basi badilisha utaingia kumalizia ushindi,kama nilivyoawambia mwendo uleule ni kufunga magoli mengi" alizidi kuongea kocha wao kuwatia wachezaji wake moyo.Paul alimtazama Gerald aliyekuwa akivaa jezi zake.Gerald hakuonekana kuwa na furaha na hilo Paul alilitambua kwa haraka "mda tayari" aliongea msimamizi mkuu wa mechi hiyo alipoingia ndani kuwaita "okay boys,mda tayari tukajaze ushindi" aliongea kocha wao kuwahamasisha kushinda magoli mengi zaidi.Wote walisimama na kuelekea uwanjani ambapo walidhamiria kushinda zaidi.Kelele za mashabiki zilisikika kushangilia wachezaji wakiwa wanaingia,Gerald aliingia taratibu na kuketi kwenye benchi la wachezaji wa akiba.Kwa mbali Kylie alimuona Gerald akiwa makini kuangalia wachezaji wenzake wakijipanga uwanjani,moyo wa Kylie ulipata ahueni baada ya kumuona Gerald akiwa mzima na kuonekana mwenye afya.Kipenga kilipulizwa kuruhusu awamu ya pili ya mechi kuanza.Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote mbili zikishambulia kwa kasi,timu pinzani ilidhamiria sana kumdhibiti Paul asifurukute kabisa ni kama timu nzima ilikuwa ikimkaba Paul peke yake "Gerald jiandae" alisema kocha na Gerald alisimama haraka na kufanya mazoezi mepesi pembeni ya uwanja kuandaa viungo vyake "Paul! Paul!" aliita kocha na kunyoosha mkono wake kuashiria Paul atoke ili kumpisha Gerald.Hakufurahishwa na jambo hilo lakini aliamua kutoka taratibu huku akipiga makofi,uwanja mzima alisimama kumpigia makofi wakati akitoka kuelekea nje ya uwanja.Paul aliingia uwanjani kwa haraka huku akihema kwa nguvu kwa kuwa kuchukua nafasi ya Paul halikuwa jambo dogo,alijua kuwa alitakiwa kufanya aliyokuwa akifanya Paul uwanjani,kushinda magoli tuhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Daniel alikamata mpira na kuurusha kwa kasi Sana upande wa Gerald,aliruka juu na kuudaka vizuri lakini ghafla alipigwa kikumbo kikubwa sana kilichomburuza chini,watu wote walipiga kelele za mshangao,Kylie alishika moyo wake kwa mshituko huku midomo yake ikionekana kutamka sala.Paul alimtazama Kylie na alihisi Kylie huenda alimpenda Gerald,Kylie hakuwa na sura ya shabiki bali sura yake ilijaa upendo na mapenzi ya dhati kwa Gerald " twende Gerald" kocha alisikika akisema kwa sauti,alinyanyuka taratibu na kushika kichwa chake huku alikunja uso wake kwa maumivu "Gerald unafikiri nitakuacha ushinde leo" alisikia sauti ukiongea ndani ya kichwa chake "wewe ni nani! uko wapi!" aliongea Gerald huku akiangalia huku na huko uwanja mzima na kuona wachezaji wote wakimsubiri anyanyuke na mashabiki waliokuwa walimpigia makofi "jitazame! uko chini! timu nzima inakuangalia wewe na mimi niko hapa kuhakikisha hushindi lolote" "Kronos! ni wewe!" "Kronos! Kronos! mimi siyo Kronos Gerald mimi ni kama wewe wote tupo uwanjani nakuona Gerald,nyanyuka" ilijibu sauti ile.Gerald alinyanyuka huku mashabiki walimpigia makofi,alikimbia pembeni ya uwanja na kupokea pasi nzuri ambapo alikimbia kwa kasi na kumrushia Daniel aliyekuwa katikati ya uwanja,Gerald alikimbia mbele kwa haraka na kupewa pasi fyongo kutoka kwa Daniel lakini alijinyoosha vizuri na kuukamata mpira.Aliwatoka mabeki kadhaa lakini kabla ya kuvuka mstari alipigwa kikumbo na beki wa timu pinzani na kuanguka chini "ni wewe sio!" aliuliza Gerald akiwa amelala chini.Timu pinzani waliwahi mpira na kufunga bao Safi ambalo lilikuwa goli la tatu na la kusawazisha kutoka kwa timu ya the Beasts.Gerald alitazama ubao wa matokeo na kutikisa kichwa chake "Gerald unapoteza mechi leo ona! magoli yote yamerudi unaiangusha timu yako Gerald" "kaa kimya,popote ulipo kaa kimya sitaki kusikia ukiongea" alijibu Kylie huku akiangaza macho yake.Kutoka jukwaani Kylie alimuona Gerald akitikisa midomo yake kana kwamba anaongea na mtu,alishangaa na kutomuelewa Gerald.Sekunde chache zilisalia kwa mchezo kumalizika,Gerald alikimbia mbele kwa kasi na kunyoosha mkono wake kuomba mpira,Daniel aliurusha mpira vibaya lakini Gerald alijitahidi kuruka juu sana na kuukamata mpira ule.Akiwa hewani alikutana na kikumbo kingine kikubwa kilichomuangusha chini,mpira uliwahiwa na timu pinzani ambao walipeana pasi ndefu kwa haraka na kufunga goli lililowapa ushindi the beasts.Kipenga kilipulizwa kumaliza mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa,timu ya the beasts pamoja na mashabiki zao walishangilia sana kwa furaha.Gerald alinyanyuka taratibu huku akitikisa kichwa chake na kutembea kuelekea walipokuwa wachezaji wenzake "usijali Gerald umecheza vizuri" aliongea mchezaji mwenzake huku akimshika mgongoni "no hujacheza vizuri" alidakia kocha wao "umepoteza nafasi nyingi sana kila nafasi uliyopoteza uliwapa wapinzani nafasi na wakashinda,umetunyima ushindi wasikudanganye wenzio hujacheza vizuri "nini! hivi kocha uliangalia mechi vizuri nimejitolea na kuumia kwa ajili ya timu halafu unasema nimecheza vibaya! hata hivyo pasi zingine nilikuwa napewa vibaya lakini nilijitahidi kuzifikia" "usimlaumu mtu yeyote Gerald hakuna aliyekupa pasi mbaya" alidakia Daniel "ndio Daniel ulimpa pasi mbaya hata mimi niliona" alidakia Paul "narudia tena hakuna niliyempa pasi mbaya" alizidi kujitetea Daniel.Paul alinyanyuka na kumsogelea Daniel usoni "unajua tatizo lako ni nini!" unafikiri wewe ni bora kuliko mimi hapo ndipo unapokosea..." "mmmh sio tena,huu sio muda wa kugombana wote,nimechoka kuona mnagombana kila siku" alidakia kocha " kama hutaki tugongane chagua mmoja Kati yangu na Daniel mmoja wetu afutwe katika timu" aliongea Paul kwa kujiamini huku akimuangalia kocha wake usoni.

    Mgeni rasmi bwana Harrison alitoa zawadi kwa washindi wote ikiwemo timu ya the beasts.Ghafla kundi la watu liliingia huku likiongozwa aliyekuwa mbele kabisa akilindwa na watu wa miraba minne,walitembea haraka na kumkaribia Harrison "shikamoo mama" alipokea kofi zito shavuni kutoka kwa mwanamke yule lililomuaibisha kwa watu wote "mama!" "mama nini! huu ndio muda wa kuwa hapa?" aliongea mwanamke yule na kumuongezea kofi lingine "nakuulizia huu ndio muda wa kuwa hapa! nimekutuma nini eeh kazi niliyokupa hujafanya uko hapa unagawa zawadi,ndio kazi niliyokupa hii!" alifoka mama yule "hii ni shule ya baba yangu na nimekuja hapa kwa niaba yake" "mpumbavu!" alifoka na kumuongezea kofi "mimi nilikupa kazi sikukuambia uje huku.Toka hapa nikukute nyumbani mbwa mkubwa wewe!" aliongea mwanamke yule na kuondoka haraka akimuacha Harrison akiwa amedhalilika mbele ya watu wote.Alijitahidi kutabasamu lakini alikunja uso wake kwa hasira.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gari ndogo ilionekana kutembea barabarani,barabara iliyokuwa katikati ya miti mirefu "..yah! yaani karibu tunafika.. hatuwezi kusahau.. tumebeba kila kitu.. watoto? watoto wapo hapa wanafurahi wenyewe..aya Harrison ongea na baba yako" aliongea mwanamke aliyekuwa akiendesha gari hilo.Aligeuka nyuma walipokaa watoto wake na kumpatia simu mtoto wake wa kiume aliyeitwa Harrison "shikamoo baba.. nzuri..eeh ndio.. nimebeba kila kitu na mdoli wangu wa Ben ten..eeh yupo..aya Lisa ongea na baba" aliongea Harrison na kumkabidhi simu mdogo wake wa kike aliyeitwa Lisa ili aongee na baba yao.Baada ya mazungumzo ya kwenye simu walianza kuimba nyimbo ambazo ziliongeza furaha katika safari yao.

    SEHEMU YA NNE+



    YOU'LL ALSO LIKE

    Kararan Bulutlar  by Arimeary

    Kararan Bulutlar

    30

    0

    Hayat bir sinavdi ve bazi engeller vardi ben ise hayatimi bu engelleri asmaya harcamistim

    .

    .

    SB [1] NAGATA by HayatulFitri6

    SB [1] NAGATA

    45

    1

    Terkadang kamu harus dengarkan kata hati, jangan tanyakan siapa yang kamu cintai. Tapi siapa yang membuatmu bahagia dan dihargai

    ~Nagata

    My Boy Friend by jerapahsipit

    My Boy Friend

    22

    5

    Masa masa SMA adalah masa masa paling indah

    di mana pada saat itu kita baru mengenal apa yang namanya cinta

    Sepertiku dan kelima temanku

    Yang baru saja merasakan cinta.

    Sama na parapecie  by ZosixOfficial

    Sama na parapecie

    20

    0

    Mel to 14 letnia dziewczyna, której zycie obrócilo sie o 180 stopni. Jej tata 2 lata temu wyjechal do Barcelony w dodatku klóci sie z mama i w szkole przesladuja ja dzie...

    Gari ilikatisha na kuingia kwenye kichochoro chenye barabara ya vumbi,walipita kibao kikubwa kilichoandikwa 'BROODVILLE HILLS TOURISM CENTRE'.Ilitembea na kupaki mbele ya jengo kubwa lililojengwa kwa mbao ngumu,gari ilizima huku mama pamoja na watoto wake wakishuka kwa furaha.Kutoka jengo lile alitoka baba wa makamo aliyevalia kaptula fupi huku akiwa amevaa shati lililombana lililochora kitambi chake "hey karibuni..Mrs Raymond karibu sana naitwa Max,nitakuwa msimamizi wenu siku zote mtakazokaa hapa.Watoto mpo tayari kufurahi!" aliongea Max na kuwageukia watoto wale "ndioo!" walijibu watoto wale kwa pamoja,mama yao na Max walitabasamu "karibuni ndani" aliongea Max na kuanza kuwasaidia kushusha mizigo iliyokuwa ndani ya gari "hii ni mara yenu ya kwanza hapa?" "ndio,rafiki yangu ameshawahi kuja hapa na mumewe ndiye aliyenielekeza basi na hawa watoto wakawa wanalilia safari nikaamua niwalete" "vizuri hujakosea kabisa Broodville hills ni sehemu nzuri kwa familia na ina mazingira mazuri sana ya kitalii nina imani mtafurahi" aliongea Max huku akiwaonyesha sehemu za kukaa "muda si mrefu kuna gari litakuja tutaondoka"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya saa moja na nusu gari kubwa aina ya Land Rover iliwasili eneo hilo tayari kuichukua familia hiyo mahali pale,Harrison na Lisa walikimbia haraka na kupanda gari hilo "mmh msikimbie kimbie" aliongea mama yao.Max alipanga mizigo vizuri na kuingia ndani ya gari baada ya familia nzima kuingia.Land Rover ilishika njia kuingia barabara ya vumbi iliyokuwa ikielekea milima ni.Ilipofika saa mbili usiku gari ilisimama kwenye eneo lile na kuzima "tutalala hapa leo halafu kesho tutaendelea na safari" aliongea Max.

    Walishuka na Max alianza kufunga hema zao ili wapumzike usiku huo.Max aliwasha moto na wote waliketi kuuzunguka moto huo ili kuwapa joto.Watoto walifurahi n kucheka sana wakati Max akijaribu kuwahadithia Hadithi za vichekesho,mama yao alitabasamu kila mara alipoona watoto wake walicheka.Usiku mnene uligonga hodi huku kila mmoja akiwa amelala usingizi mzito,Harrison na dada yake walilala kwenye hema moja na mama yao alilala kwenye hema nyingine huku Max akiwa amelala ndani ya gari "kaka Harrison unasikia? kaka Harrison!" aliongea Lisa akijaribu kumuamsha kaka yake.Harrison alinyanyuka na kujaribu kusikiliza kama angeweza kusikia chochote "sisikii chochote Lisa,hebu lala kesho tutaendelea na safari" " kweli kaka Harrison kuna kitu huko nje" "unajua nini Lisa ni bo.." alikatisha baada ya kusikia sauti ya mngurumo mkubwa "yah nasikia!" aliongea Harrison "ni nini hiyo?" aliuliza Lisa "sijui inabidi twende nje tukaangalie" "hapana usiku sana saa hizi" alijibu Lisa.Harrison alifungua hema na kutoka nje taratibu huku Lisa akimfuata kwa nyuma.Walitembea mpaka katikati ya msitu huo mnene na kusikia sauti ya miguu ya viumbe wakikimbia,walijaribu kutazama huku na huko bila kuona chochote.Mingurumo mikubwa kama ya simba ilisikika Kwa nguvu "Harrisoooon!" alilia Lisa aliyechukuliwa ghafla na wanyama wale "Lisaaaa!" aliita Harrison huku hofu ikimuingia na kuanza kukimbia kuelekea mahali zilipowepo hema zao.Mama yake na Max waliamka baada ya kushitushwa na kelele za Harrison "mama,wanakuja" alilia Harrison "Harrison! Mungu wangu!" alishituka mama yake na kumsogelea karibu "mama wanakuja tuondoke" "hebu tulia, Lisa yuko wapi?" "wamemchukua mama,tuondoke wanakuja" aliongea Harrison huku akilia kwa hofu "nani wamemchukua? ni kina nani hao!" aliuliza mama yake kwa hofu.Ghafla wanyama wakubwa weusi kama mbwa mwitu wenye sura za kutisha walitokea mbele yao.Hofu iliwaingia na kila mmoja alianza kutetemeka kwa uwoga,Max alikimbia haraka ndani ya gari na kuliondoa mahali pale kwa haraka.Mmoja wa mbwa wale alimkaba koo mama yake Harrison na kulinyofoa na kuanza kumtafuna kwa njaa Kali.Harrison alilia sana huku akishuhudia mama yake akibaki mifupa tu.Walipomaliza kumtafuna mama yake walimsogelea Harrison taratibu na kunguruma kwa hasira,Harrison alirudi nyuma na kudondoka chini huku akilia sana kwa hofu.Walisogelea uso mdogo wa Harrison na kunguruma,matone ya damu yalidondoka juu ya uso wa Harrison na kutoka kwenye meno makali ya wanyama wale.Waliondoka na kukimbia haraka bila hata kumdhuru wala kumjeruhi.Ulikuwa usiku wa kutisha sana kwa Harrison.

    "Shikamoo mama" alisalimia Gerald aliyekuwa na begi lake mgongoni "marahaba,unajua kama umechelewa shule!" "najua" alijibu Gerald na kuangalia saa yake ya mkononi na kuona ilikuwa saa mbili kamili,alikimbia kuhawi shule na kuingia ndani sekunde chache kabla ya mwalimu kuingia,aliangalia saa yake tena na kuona ilikuwa saa mbili na dakika mbili,alitabasamu.Aliketi juu ya kiti na kumsalimia Kylie lakini Kylie hakujibu chochote.Gerald alitoa madaftari yake na kuanza kumsikiliza mwalimu akifundisha.Alisinzia na kila mara mwalimu wake alimuamsha na kumgombeza.

    "Gerald! Karibu" aliongea Kate akijaribu kumkumbatia lakini Gerald alimzuia "sina muda huo Kate,Sebastian yuko wapi?" "huna muda na mimi baada ya yote tuliyofanya!" "Kate sikia tulichofanya kimepita usikiweke akilini,samahani sana,Sebastian nimemkuta?" "Gerald!" alishangaa Sebastian aliyewasili ghafla akitokea chumbani kwake "unafanya nini hapa! si ulitakiwa uwe shule!" "mazoezi" alijibu Gerald na kuelekea kwenye uwanja mkubwa uliokuwa nyuma ya nyumba.Alijaribu kupiga ngumi nyingi sanamu zilizokuwa uwanjani hapo,alipiga sana na kufanikiwa kuvunja moja baada ya kurusha konde zito,alifurahi sana baada ya kuona kwa mara ya kwanza aliweza kuvunja sanamu zile "umeendelea sana siku hizi,ukiendelea hivyo kumshinda Kronos itakuwa kazi rahisi sana" aliongea Sebastian aliyemsogelea kwa ukaribu "unaogopa kwamba nitaweza kukupiga na wewe" "unafikiri utaweza?" Gerald aliruka juu sana na kumporomoshea Sebastian ngumi nyingi ambazo aliziondoa vizuri.Mateke mfululizo ambayo Gerald aliyarusha hayakumpa taabu Sebastian ambaye aliyakwepa vizuri.Sebastian aikamata Shingo ya Gerald na kumrusha mbali ambapo alidondokea sanamu zile na kuzivunja,aliweka mkono Chini na kuserereka.Alimtazama Sebastian kwa mbali aliyekuwa amekunja mikono yake "aaa..h!" alipiga kelele Gerald na kumkimbilia Sebastian ambaye alirusha ngumi iliyoteleza juu ya bega la Gerald,alikamata mkono wa Sebastian na kumpiga ngumi nzito ya ubavuni iliyomrusha mbali sana.Jambo hilo lilimfurahisha sana Gerald hakuamini kama alimpiga ngumi ile Sebastian.Sebastian alinyanyuka taratibu huku akishika mbavu zake "vizuri,nafikiri kwa leo inatosha twende ndani,tufurahie".

    Gerald aliendelea kuzurura ndani ya Grotto na kushangaa mitaa mizuri ambayo watu walikuwa wakiishi kupitia ndoto zao,ghafla Gerald alisimama na kushangaa sana "Kronos!" alishangaa Gerald baada ya kumuona adui yake mkubwa."Kronos!" aliita Gerald kwa nguvu,Kronos aligeuka na kumtazama Gerald kwa mshangao "Gerald! unafanya nini hapa Grotto!" "baba yangu yuko wapi Kronos.Niambie ulipomuweka baba yangu au nikulazimishe" aliongea Gerald kwa hasira na kujiamini "oo..h! Gerald napenda sana unavyojiamini siku hizi.Siwezi kukuambia nilipomuweka baba yako kama usionilazimisha" aliongea Kronos na kutabasamu kwa dhihaka.

    Gerald alikimbia na kurusha ngumi lakini ilidakwa vizuri na Kronos ambaye alimpiga ngumi ya uso iliyomtupa chini.Tukio hilo lilishangaza wapita njia wengi ambao waliacha shughuli zao.Gerald akiwa chini akiugulia maumivu yake ghafla alijiona akiwa katikati ya msitu mnene "umenileta wapi huku Kronos!" "huku ni sehemu ambayo nitakuua bila watu kuona" alijibu Kronos huku akimsogelea Gerald taratibu.Alikamata koo la Gerald na kumpiga ngumi nyingi za tumbo na kumrusha mbali ambapo Gerald alijibamiza kwenye mti mkubwa "Gerald,supreme gani wewe!" aliongea Kronos na kumnyanyua Gerald na kumrusha tena upande wa pili.Gerald alinyanyuka na kurusha ngumi nyingi lakini Kronos alizikwepa kwa ustadi na kumpiga ngumi nzito ya tumbo ambayo ilimuangusha Gerald chini."Sikia Gerald naweza kukuua hapa nikitaka umenitia hasira,ila kabla sijakuua nifanye hiki" aliongea Kronos na kumnyanyua Gerald shingoni.

    Ghafla walitokea kwenye chumba kidogo ambacho kilikuwa na giza na kilionekana kichafu sana kilichojaa nyasi nyingi na kilinuka sana.Walisimama mbele ya baba mmoja aliyefungwa mdomo na kitambaa kikubwa huku mikono yake ilifungwa na minyororo mikubwa,ndevu zake nyingi zilizojaa usoni zilionyesha alifungwa pale kwa miaka mingi.Kronos aliekuwa bado amemnyanyua Gerald kwa kumkamata Shingo "Gerald ulitaka kumuona baba yako,yule pale! unaona sijamuua lakini nitamuua hivi karibuni" aliongea Kronos na kumgeukia baba yule "hello Donald unamuona mwanao,eti ni supreme! uliyekuwa unamtegemea kwamba ipo siku atakuja kukuokoa,usiwe na hayo matumaini Donald kwa sababu mwanao hana uwezo huo.Gerald nenda kamsalimie baba yako" aliongea Kronos na kumuachia Gerald aliyeanguka chini kama mzigo.Alimkimbilia baba yake na kushika uso wake huku akilia kwa uchungu "baba uko sawa?" baba yake alitikisa kichwa,hakuweza kuongea kwa sababu ya mdomo wake kufungwa na kitambaa kikubwa "baba samahani sana kuwa na nguvu nivumilie nakuahidi nitakuja kukuokoa ipo siku" aliongea Gerald huku akilia sana " no usiamini Donald hawezi kukuokoa" aliongea Kronos na kumpiga ngumi ya tumbo "Gerald sitakuua leo mda wako bado."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Gerald uko sawa,unaweza kuamka?" aliuliza mwalimu wake baada ya Gerald kupiga kelele kwa muda mrefu.Wanafunzi wengine walishitushwa na tukio hilo na wengi kudhani kuwa Gerald alisumbuliwa naapepo "Gerald unatoka damu!" aliongea Kylie huku akimshangaa Gerald aliyekuwa akitoka damu nyingi mdomoni.Alinyanyuka upesi na kukimbilia chooni ambako alisukutua mdomo wake na kutema damu nyingi "Kronos nitakupata na nitakuua" aliongea Gerald huku akijitazama kwenye kioo,alishika tumbo lake lililokuwa na maumivu makali baada ya kupigwa sana na Kronos makonde ya tumbo.Alirudi darasani na kuketi taratibu juu ya kiti chake,Kylie alimtazama na kumuonea huruma,alichana kipande kidogo cha karatasi na kuandika ujumbe mfupi wa maneno uliouliza kujua tatizo la Gerald. Gerald alimtazama Kylie na kugeuza Shingo yake kumtazama mwalimu wake.

    Saa kumi na moja jioni masomo yalikuwa yameisha kwa siku hiyo,wanafunzi wote walishika njia zao kurudi nyumbani isipokuwa wachezaji tu ambao walikuwa na masaa mawili ya ziada kwa ajili ya kufanya mazoezi.Kylie alitembea taratibu na Paul "Paul inabidi nikuambie kitu" "nini?" "hivi hujagundua kuwa Gerald amebadilika he is acting weird" "hapana sijagundua,namuona kawaida tu" alijibu Paul "kweli,mchunguze hayupo kawaida hukumuona hata siku ile siku ya mechi alikuwa kama anaongea na mtu.Nafikiri kuna jambo anatuficha pengine..."pengine nini!" alidakia Paul "kwani kuna tatizo gani kama alikuwa anaongea na mtu,eeh! sawa labda hayuko sawa pengine ana matatizo yanakuhusu nini! au kuna nini unajali!" aliongea Paul kwa jazba "sio kama najali lakini..." "lakini nini! unampenda sio! unampenda Gerald si ndio Kylie!" "Paul!" "sikia Kylie nenda nyumbani huu ni muda wa wachezaji tu,sawa" aliongea Paul na kuelekea uwanjani.Kylie alihema kwa nguvu na alijua kuwa Paul alisema ukweli alimpenda sana Gerald na ndio maana alijali sana.

    Baada ya mazoezi makali ambayo timu ya the thunders ilifanya kocha wao aliwaita wachezaji wote kwa pamoja "okay boys,tumekuwa pamoja kipindi chote cha mazoezi tukijiandaa na michuano mikubwa ya kitaifa inayokuja mbele yetu.Nimechagua wachezaji ishirini tu ambao watatuwakilisha kwenye michuano hiyo na siyo kama nisipokuchagua ina maana wewe hujui hapana ila idadi kamili inahitajika kwa hiyo nikisoma jina lako ujue haupo tena kwenye timu" aliongea kocha huku wachezaji wakihema kwa hofu ya kutemwa kikosini "Gasper,Anthony na...Daniel you guys ni wachezaji wazuri lakini..." "unafki kocha" alidakia Daniel "umeniacha mimi siyo kama sijui,najua unajua na wote hapa wanajua kwamba mimi ni mchezaji mzuri na bora kuliko wote hapa ambaye hakuna kocha duniani ambaye angethubutu kuniacha,wewe! eti umeniacha! najua ilibidi uchague kati yangu na Paul kama alivyokwambia ukaamua kumchagua Paul nyota wa timu yako" aliongea Daniel kwa hasira "siyo hivyo Daniel..." "ndio hivyo usiwe unafki bwana,kwaherini" aliongea Daniel na kumtazama Paul "naona umepata ulichokitaka Paul,unayeniogopa nimetemwa" "bye Daniel tuache tuendelee na mazoezi" alijibu Paul kwa dhihaka na kutabasamu.Daniel aliondoka kwa hasira "okay kwa leo tumeishia hapa tukaoge".

    Wachezaji wote walikuwa bafuni kusafisha miili yao,Gerald alikuwa katika loka lake kifua wazi,alichukua tisheti yake na kuivaa taratibu huku akikunja uso wake kwa maumivu.Paul alimsogelea Gerald na kushangaa kuona alama nyekundu za majeraha ya ngumi juu ya tumbo la Gerald.Alishusha tisheti yake na c kushituka baada ya kukutana na uso wa Paul "Paul! vipi!" "safi tu vipi wewe uko sawasawa kweli?" "yah mimi niko poa tu" alijibu Gerald "hongera kwa kuchaguliwa kwenye timu unastahili" "asante" alijibu Gerald na kuondoka.Paul alikunja uso wake na kumtazama Gerald akiondoka aliamini maneno ya Kylie kuwa Gerald hakuwa sawa kuna mambo yalikuwa yakimsumbua.

    Nje ya duka kubwa lililoandikwa 'BROODVILLE BEST AUTO SPARE PARTS ' mlango wake ulifunguliwa kwa ajili ya kutoa huduma siku hiyo.Sebastian alisafisha bidhaa zake pamoja na duka lake ili livutie wateja,ghafla alisikia sauti laini ya koo likikwanguliwa,aligeuka haraka kukutana na mteja wake "karibu,nikuhudumie nini?" aliongea Sebastian huku akimshangaa mteja wake ambaye alionekana binti mdogo sana kumiliki chochote cha usafiri "nina shida na wewe" "mimi! una shida gani? kama siyo kuhusu biashara labda nikuelekeze kwangu maana saa hizi ni saa za kazi" "nina shida muhimu,ni kuhusu Gerald" "Gerald! Gerald nani?" aliuliza Sebastian kujifanya kutomjua Gerald "ooh usijifanye humjui nimewaona wote mara mbili unakujaga shuleni,unamjua" " wewe ni nani?" aliuliza Sebastian "naitwa Kylie ni rafiki yake,na wewe je?" "mimi ni rafiki yake Pia" "sikia wewe na Gerald mna uhusiano gani zaidi ya urafiki,rafiki tu hawezi akaja mpaka shuleni akamtorosha rafiki yangu.Siku hizi Gerald haeleweki maana anatokwa na damu,anakuja na mashuka shule siku nyingine haonekani kabisa shuleni,unamfanya nini rafiki yangu! unamuingiza kwenye biashara gani rafiki yangu!" aliongea Kylie kwa sauti ya hasira "mimi na Gerald ni marafiki tu kama wewe na yeye" "sasa kwa nini yuko hivyo?" "kwa nini hilo swali usimuulize mwenyewe,samahani sana niko kazini inabidi nifanye kazi" aliongea Sebastian na kuondoka.Kylie alipumua kwa nguvu na kutoridhishwa majibu ya Sebastian.

    Kylie aliondoka na kuingia ndani ya duka jirani lililoandikwa 'PAUL NOVELS STORE' alitazama vitabu vingi vilivyokuwa vimepangwa kwenye makabati makubwa "karibu dada nikusaidie nini?" aliuliza muuzaji wa duka hilo "una kitabu chochote cha paulnovels?" "Paulnovels...mmh..yah kuna hiki hapa" alijibu muuzaji huyo na kutoa kitabu na kukiweka juu ya meza mbele ya Kylie "shilling ngapi?" "hicho elfu kumi na tano tu".Kylie aligeuka upande wa makabati na kuendelea kutazama vitabu vingine.Mda huohuo aliingia kijana mwingine aliyesogea karibu kabisa na meza ya mauzo "karibu".Kijana yule aligeuza Shingo yake na kutazama kitabu kilichokuwa juu ya meza "oh! aisee! hiki kitabu niuzie hiki kitabu" "aah kimeshanunuliwa na yule dada pale" "kiasi gani? nitazidisha mara mbili" "hapana hatuna hiyo aina ya biashara,ila bado sijapokea pesa unaweza kuongea naye mkakubaliana" kijana yule alimgeukia Kylie "etii..samahani sana sista" Kylie alimgeukia "samahani nina shida na hiki kitabu" "nimeshanunua tayari" "si bado hujampa pesa nitakulipa na wewe" aliongea kijana yule.Kylie alishangaa na kumsogelea zaidi kijana yule "nina shida na kitabu siyo hela.Hey! halafu nakujua wewe Harrison si ndiyo!" kijana yule aliduwaa kidogo na kushitushwa "yah naitwa Harrison sijui nakujua?" "hapana huwezi kunijua,naitwa Kylie ni mwanafunzi wa Broodville high school,form five" "Broodville! okay sasa naelewa umenijuaje" "yah kila mwanafunzi pale anakujua najisikia fahari sana kukutana na wewe,tena naitwa Kylie" aliongea Kylie na kumpa mkono.Harrison alitazama uso wa Kylie uliokuwa ukipendeza kwa uzuri,macho yake yaliyorembua yalimlainisha kabisa Harrison,hakusita kumpa mkono wake "naitwa Harrison,well... nafikiri umenunua kitabu sikihitaji tena" Kylie alitabasamu na kuingiza mkono wake ndani ya pochi ndogo kutoa pesa "no! no! it's okay nitalipa tu,tunza pesa yako" aliongea Harrison na kutoa noti mbili za elfu kumi na kumkabidhi muuzaji "asante sana" alishukuru Kylie na kuondoka.Harrison alivuta pumzi kwa nguvu kwa sekunde chache na kuamua kumkimbilia Kylie "hey Kylie" Kylie alisimama na kugeuka kumtazama Harrison aliyekuwa akimkimbilia,alipomkaribia alimuangalia usoni "yes" "mm..h eeh..labda nikupe lifti nimekuja na usafiri" "asante sana nitapanda basi tu" "tafadhali" alibembeleza Harrison.Kylie alijaribu kukataa lakini ushawishi wa Harrison ulikuwa mkubwa sana.Kylie alikubali na kuingia ndani ya gari ambapo liliondoshwa kwa kasi.Sebastian alitoka dukani kwake na kulitazama gari lile lililokuwa likiondoka kwa kasi.

    Ndani ya gari Kylie alishika begi lake vizuri huku akitazama nje ya dirisha,Harrison alimtazama huku akibadilisha gia kwa haraka "so,unaipenda shule?" "nini?" "unaipenda Broodville I mean your school" aliuliza Harrison "yah kawaida naipenda ndio maana niko pale" "uko sahihi,baba yangu aliniambia wakati yeye anakuwa hakuwahi kwenda shule na ndio maana alipofanikiwa aliamua kujenga shule ili vijana wasipate taabu kufanikiwa kama yeye" aliongea Harrison huku akitoa tabasamu zuri,mashimo madogo yalionekana juu ya mashavu yake "aah ni vizuri kwa baba yako.Hivi unasoma kweli! maana sisi tungekuwa na pesa nisingesoma "nini!" alishituka Harrison na kucheka "elimu bado ni muhimu,nasoma mambo ya biashara,siyo kama eti sisomi kabisa" Kylie alitikisa kichwa chake na kumtazama Harrison aliyekuwa akibadilisha gia kwa haraka na kwa ustadi mkubwa "unakimbiza gari kweli yaani!" "Khaa! nakimbiza! mbona naendesha kawaida sana sema hii gari inakimbia sana,Range ni hatari" alijibu Harrison huku akikunja usukani kwa ustadi mkubwa.Gari ilipunguza mwendo baada ya kuona kundi kubwa la polisi na gari zao mbele yakiwa mbele barabarani,gari mbili za wagonjwa zilionekana kuingiza maiti ndani.Gari ilitembea taratibu "unaweza kushusha kioo kidogo" aliongea Kylie na kutoa kichwa chake nje baada ya kioo kushushwa "jamani tunaomba mpite haraka eneo hili liko chini ya polisi" aliongea polisi mmoja aliyewakaribia "kuna nini afande" "kuna mauaji yametokea" alijibu polisi yule,Kylie alirudisha kichwa ndani na kioo kilifungwa "was that a murder!" "yah nafikiri familia kwenye ile nyumba wameuawa" alijibu Kylie baada ya kuulizwa na Harrison.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gerald alipiga ngumi nyingi kwa hasira,pumzi nyingi alizokuwa akitoa ziliashiria kuwa alikuwa na hasira sana.Sababu ya hasira kali alizokuwa nazo rangi yake ya ngozi ilibadilika na kuwa ya bluu.Kate aliingia taratibu katika chumba cha mazoezi alichokuwemo Gerald,alishangaa na kushituka baada ya kuona rangi ya ngozi ya Gerald ilivyokuwa ya bluu aliamini mda huohuo kuwa Gerald ndiye alikuwa supreme.Mfuko ule mkubwa wa kibondia ulianguka chini baada ya kupigwa ngumi nzito na Gerald,Kate alishituka na kumfanya Gerald ageuke.Gerald alimtazama Kate huku rangi yake ya bluu ikianza kufifia na kuondoka kumpita mbele yake akimuacha Kate akiwa ameduwaa.Kate alikamata mkono wa Gerald na kumfanya Gerald kusimama "nini Kate" aliuliza Gerald lakini Kate hakujibu kitu,kubadilika rangi ya ngozi ya Gerald kulimshitua sana "kama hauna cha kuniambia niache" aliongea Gerald "una tatizo gani Gerald?" "niko sawa" alijibu Gerald "no,hauko sawa umekuwa wa bluu na ninavyojua mimi supreme akiwa ana hasira ngozi yake inabadilika kuwa ya bluu.Kuna tatizo Gerald niambie" "Gerald aliangalia chini na kupumua taratibu "juzi nilikutana na Kronos hapa Grotto na nilifikiri naweza kumpiga baada ya kumpiga kaka yako lakini kumbe nilikuwa nimekosea.Kate mimi ni dhaifu sina nguvu kama mnavyofikiria labda mimi ni dream holder wa kawaida,supreme gani mimi siwezi kumpiga hata creator mmoja! baba yangu amepalalaizi miaka kumi na Saba Kronos amemteka na kumtesa sana.Niliona baba yangu akikosa imani mwanaye aliyenitegemea,supreme! akipigwa na Kronos.Kate mimi ni dhaifu" aliongea Gerald huku akitoa machozi.Kate alimwaga machozi hakuwa na cha kujibu zaidi ya kupeleka mdomo wake juu ya mdomo wa Gerald na kumpa mabusu motomoto,Gerald alionyesha ushirikiano mzuri kwa kurudisha mabusu yale na kumfanya Kate aheme kwa nguvu kana kwamba alibanwa na pumu.Walizungushana wakipeana mabusu mpaka pale Kate alipoegemea ukuta,Gerald aliingiza mkono wake ndani ya sketi fupi ya Kate ambaye alinyanyua mguu mmoja vizuri kurahisisha tendo hilo.Aliteremsha taratibu nguo ya ndani ya Kate na kuingia taratibu kumfanya Kate ajinyanyue taratibu kama mtu aliyepigwa ngumi ya mgongo.Haikuwa mechi rahisi kwa wote wawili,baada ya tendo hilo Gerald alirudi duniani na kumuacha Kate akiwaza na kufurahia tendo hilo.Moyo wake ulimpenda sana Gerald na hukumuona tu kama mtu aliyekutana naye na kufanya naye mapenzi,alihisi jambo la tofauti upendo wa dhati.

    Asubuhi na mapema Gerald aliamka na kujiandaa kuelekea shule "mama baadae nitaenda kwenye birthday party ya rafiki yangu" aliongea Gerald huku akitafuna kipande kikubwa cha mkate kilichokuwa mezani "ndio salamu hiyo" aliongea mama yake huku akimkaribia na bilauri kubwa la juisi kutoka jikoni "shikamoo,kama nilivyokwambia mama baadae naenda kwenye party ya rafiki yangu" "aah utajijua mwenyewe uende usiende " "kwa hiyo umeniruhusu" "nenda tu" aliongea mama yake.Grald alivuta gazeti lililokuwa mbele yake 'AFISA UTALII AUAWA NYUMBANI KWAKE' lilisomeka gazeti hilo "mama unamjua huyu afisa utalii aliyeuawa?" "Yah namkumbuka si yule Maxmillian nilisoma naye" alijibu mama yake.Gerald alikunywa chai haraka na kuelekea shuleni.

    "Kylie naomba unisamehe kwa niliyoyasema siku ile,sikuyamaanisha" aliongea Paul wakati akitembea na Kylie kwenye mazingira ya shule "usijali potezea" "no Kylie namaanisha kusema hivyo" "potezea Paul nimeshasahau ukizingatia Gerald ni mtu mzima anajielewa haina haja ya mimi kujali matatizo yake" aliongea Kylie huku akimuangalia Paul usoni "nafikiri Gerald atakuwa na matatizo maana nilimuona ana majeraha tumboni na yalionekana siyo ya kawaida" "ulimuuliza lolote?" "nilimuuliza kama yuko sawa akanijibu yuko sawa lakini hakuonekana kama yuko sawa,labda tuchunguze tatizo lake" aliongea Paul kwa msisitizo.

    Kylie aliingia darasani taratibu huku kelele za wanafunzi ziliashiria kutokuwepo kwa mwalimu darasani,aliketi kwenye kiti chake karibu kabisa na Gerald aliyekuwa akisoma madaftari yake "Gerald hi" alisalimia Kylie,Gerald alitikisa kichwa chake kujibu salamu ile "you look more handsome leo" alizidi kuongea Kylie.Gerald alitabasamu na kuangalia chini "eeh Gerald nimekaa nimefikiria nimeona kuwa kuchuniana na kutoongea siyo jambo zuri.." aliongea Kylie huku Gerald akinyanyua uso wake taratibu "...sisi kama classmates na marafiki hatupaswi kuchuniana" alizidi kuongea Kylie lakini Gerald aliduwaa macho yake mbele kwa mshangao mkubwa "Gerald unanisikia,Gerald!" sauti ya Sebastian ilisikika kichwani mwake.Alinyanyuka taratibu na kutoka nje ya darasa kwa haraka "Gerald!" aliita Kylie ambaye naye alisimama kumfuata Gerald nje ili kujua Gerald alikuwa akielekea wapi.Gerald alielekea mpaka nyuma ya jengo hilo na kumkuta Sebastian akizunguka huku na huko kama mtu aliyechanganyikiwa "Sebastian nini hiki! hujui kwamba huu ni muda wa mimi kuwepo shuleni!" "Subiri kwanza Gerald" aliongea Sebastian na kumshika bega na kusogea sehemu ambapo Gerald alitokea "nisubiri hapa Gerald" aliongea Sebastian na kuelekea alipotoka Gerald.Kylie alishituka baada ya kukutana na Sebastian kwenye korido "aah! Sebastian!" "Kylie uko shule na ukiwa shule unatakiwa kusoma kwa bidii siyo kupoteza muda kama unavyofanya,rudi darasani usome muache Gerald yeye ni mtu mzima anaweza kujiangalia mwenyewe" "kumbe unajua umuhimu wa shule na kusoma sasa kwa nini humuachi Gerald asome.Sikia mimi sijui unamfanya Gerald au unamtumbukiza kwenye makundi mabaya nitakushitaki polisi nafikiri mwalimu mkuu anapaswa kujua hili" "Kylie usiwe msumbufu,ukifanya hivyo utahatarisha maisha yako na ya Gerald,sidhani kama unapenda hilo litokee huu sio muda wa kuwa shujaa nenda darasani kasome " aliongea Sebastian na kuondoka kumuacha Kylie akiwaza zaidi.Aliamua kuwafuata zaidi na kunyata mpaka waliokuwepo "Gerald usimsikilize" alipiga kelele Kylie alipofika haraka nyuma ya jengo alipokuwepo Gerald na Sebastian.Alishangaa hakuona mtu yeyote Gerald na Sebastian walitoweka ghafla "wameenda wapi!" aliongea Kylie kwa sauti ya chini na kushangaa Gerald na Sebastian walipoteaje ghafla wakati muda mfupi uliopita alisikia sauti zao.Kylie alishituka baada ya kuguswa bega na Paul "uko sawa kweli! unafanya nini hapa ulitakiwa uwe darasani" "niko sawa tu,wewe unafanya nini hapa?" aliuliza Kylie "mimi ni kiranja hujui hilo,ulitakiwa uwe darasani.Unaonekana hauko sawa una tatizo gani?" "Gerald" "Gerald kufanya nini?" "hayupo darasani kuna mtu kaja amemtorosha" aliongea Kylie "mtu! mtu gani,unajua Kylie hii ishakuwa hatari kama mtu anakuja na kutorosha wanafunzi hapa itakuwa hatari.Nafikiri tumwambie mwalimu mkuu" "no,usimwambie kwanza labda wanajuana tumuulize kwanza Gerald" "aah sawa basi twende darasani" aliongea Paul.

    Moto mkubwa ulionekana kuteketeza nyumba ya Sebastian "Sebastian nini hiki!" alishangaa Gerald "Kate yuko wapi?" ghafla Kate alianguka chini akitokea juu kabisa ya nyumba hiyo,mbele ya Gerald "Kate!" alishituka Sebastian na kumsogelea,Kate alinyanyuka taratibu huku akihema kwa nguvu "wako wengi Sebastian wako wengi mno" "kina nani? nani hao?" aliuliza Gerald "hao ni HELL DREAMERS ni dream holders wabaya sana wapo hapa kutuua creators wote,wanataka kulipa kiasi" aliongea Sebastian huku akijaribu kupigana na mmoja wa adui aliyekuja mbele yake "tunafanyaje sasa?" "pigana pigana nao" alijibu Sebastian.Gerald,Sebastian na Kate wote kwa pamoja walipigana na adui hao ambao miili yao ilionekana kuwaka moto.Moto iliyowaka kwenye miili yao iliwasaidia kupaa angani.Walipigwa sana na kujeruhiwa vibaya.Kate,Gerald na Sebastian walishindwa kabisa kuwadhibiti adui hao na kila mara walipojaribu walipigwa sana.Wakiwa wote chini wakihema juu juu na kwa maumivu makali "watatuua!" aliongea Gerald kwa maumivu "hapana ndio maana nimekuleta huku Gerald unaweza kutusaidia kuwapiga wewe ni supreme" "nitawezaje wako wengi sana siwezi kuwapiga wote" "hao wengine ni dhaifu wanamtegemea mkuu wao yupo hapohapo mtafute,ukimdhibiti huyo hao wengine hawana shida" aliongea Sebastian kwa maumivu "nitamjuaje?" "moto wake usoni ni mwekundu sana kwa sababu hapo ndio chanzo.Jiamini Gerald unaweza" Gerald alinyanyuka taratibu huku akishika tumbo lake kwa maumivu " kama wewe ni mwanaume njoo hapa peke yako usijifiche kwa hao shetani wenzako" alipaza sauti kwa ukali.Ghafla alipigwa kikumbo kilichomtupa mbali sana.Gerald alimtazama adui yule aliyekuwa akimsogelea taratibu huku mwili wake ukiwaka moto "creator mwingine tayari kwa kufa safi sana" aliongea adui yule kwa sauti ya kutisha sana "unafikiri unaweza kuniua hebu jaribu" alitishia Gerald.Alinyanyuliwa na kupigwa ngumi nzito ya uso iliyomtupa mbali "kumbe rahisi hivi" aliongea adui yule huku akimsogelea taratibu.Gerald alinyanyuka taratibu huku akiyumbayumba,alirushiwa ngumi ya kasi iliyoambata na moto lakini Gerald aliikwepa kwa ustadi na kuruka juu ambapo alitua na mateke yaliyomkuta adui yule usoni.Upiganaji wa Gerald ulifanana sana na mpiganaji maarufu wa China marehemu Bruce Lee.Konde zito lililotua usoni mwa adui ulijaza hasira zaidi na kuzidi kumsogelea Gerald.Alirusha ngumi nyingi zilizomkuta Gerald kifuani na kumuumiza "yeah" alifurahi adui yule.Gerald akiwa chini alipigwa ngumi nyingi za mgongoni zilizoambatana na moto,Gerald alilia kwa maumivu makali.Alijibetua kwa sarakasi na kurusha teke lililomkuta adui juu ya kidevu.Gerald alisimama wima huku akihema kwa nguvu na kumtazama adui aliyekuwa akimkimbilia kwa kasi.Walisukumana kwa mikono huku kila mmoja akitumia kiasi kikubwa cha nguvu kumsukuma mwenzake.Gerald alibadilika rangi na kuwa wa bluu kwa hasira na kumpiga ngumi tatu za haraka zilizomrusha mbali.Adui alilia kwa hasira huku akimtazama Gerald aliyekuwa wa bluu na kupaa kukimbia huku wafuasi wake wakimfuata nyuma kama miale ya moto.Sebastian na Kate walimsogelea Gerald "umeweza" aliongea Kate "amekimbia" "kwa sababu amejua wewe ni supreme,ila ipo siku huyo FLAME DEVIL atarudi tena" aliongea Sebastian kwa maumivu "huyo flame devil ndio nani?" aliongea Gerald kwa hasira huku rangi yake ya bluu ikiwa imekolea "nitakuambia siku nyingine sasa nina kazi ya kuiumba tena nyumba yangu" alijibu Sebastian.

    Ndani ya Choo cha shule ambacho kilikuwa kinatumiwa na wanaume tu,walishangaa kuona moshi ukitoka kwenye moja ya choo kilichofungwa vizuri huku harufu kama ya kitu kuungua ilisikika.Gerald alifungua mlango na kutoka huku wanaume wengine wakimshangaa Gerald alikuwa akifanya nini chooni kiasi cha harufu kali ya moshi kusikika.Gerald alisimama ghafla kwenye korido baada ya kuona kundi la wanafunzi wakimbeba mwanafunzi mmoja aliyezirai kumpeleka zahanati ya shule "nani huyo amezirai?" aliuliza Gerald "Paul nafikiri anaumwa" alijibu mmoja wa wanafunzi wale aliyekuwa akisindikiza msafara ule.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SEHEMU YA TANO



    Usiku huo kelele za shangwe na mziki mkubwa ulisikika kutoka nyumba kubwa ya Emily,mwanafunzi aliyekuwa akisoma shule moja na Gerald.Ilikuwa ni sherehe kubwa ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Emily.Gerald aliwasili akiwa amechelewa na kutembea haraka mpaka kwa Emily na kumpongeza kwa kutimiza miaka kumi na saba tokea amezaliwa.Mziki mkubwa uliendelea kupigwa huku vijana wakionekana kucheza midundo hiyo na baadhi yao walionekana kuvuta bangi na kutumia vilevi vikali.Kwa mbali Gerald alimuona Kylie akiwa amekaa peke yake mbele ya meza kubwa iliyokuwa mbele kidogo na alipokuwa Gerald,alivuta pumzi na kumsogelea taratibu huku akiwa ameshika glasi kubwa iliyojaa mvinyo "hey Kylie" alisalimia Gerald lakini hakupokea majibu "mbona uko peke yako,Paul yuko wapi!" "Paul anaumwa alizirai leo mchana,hujui hilo! oh nimesahau kumbe ulitoroka shule" aliongea Kylie "hapana sikutoroka shule Kylie" "sasa ni nini kama sio kutoroka!" aliongea Kylie kwa sauti ya ukali kidogo "Gerald unajua siku hizi sikuelewi unatega shule mara unaumia au huyo Sebastian anakufanya nini!" "Sebastian! Umemjuaje!" alishangaa Gerald "namjua wewe elewa hivyo,hivi Gerald una tatizo gani kama kuna tatizo niambie,mimi nakuganda hivi kwa sababu nakujali lakini wewe unaonekana hujali wala huthamini upendo wangu kwako" "Kylie sikia kungekuwa kuna tatizo lolote ningekuambia lakini hakuna kinachoendelea" "kama hakuna kinachoendelea mbona uko hivyo" "mbona nipo kawaida Kylie" "hapo unaona upo kawaida eeh! naona Gerald hunijali nachohisi juu yako wewe ni walewale" aliongea Kylie kwa sauti ya hasira na kuondoka kuelekea nje na kumuacha Gerald akiduwaa huku akitafakari maneno ya Kylie kwa muda.Alivuta pumzi na kuamua kumfuata Kylie nje "Kylie! Kylie nime..." alishindwa kumalizia baada ya kumuona Kylie akiwa amesimama karibu kabisa na Harrison ambao waligeuka na kumtazama Gerald "oh! hey! hello" alisalimia Gerald huku akishika kichwa chake "hello" alijibu Harrison kwa sauti tulivu huku akitoa tabasamu zuri Sana.Alipendeza sana na suruali yake ya jeans iliyomkaa vizuri huku akiwa amevalia koti jeusi aina ya leather "tunaweza kutoka?" aliuliza Harrison huku alimtazama Kylie usoni "tutoke! wapi? usiku huu!" "mahali tu,ni surprise" "lakini Harrison niko kwenye birthday ya rafiki yangu si unaona" "tafadhali utapenda" alibembeleza Harrison "Harrison labda siku nyingine" aliongea Kylie na kumgeukia Gerald "subiri kwanza" aliongea Harrison na kumsogelea Gerald aliyekuwa amesimama mlangoni "oya tunatoka na Kylie tunaenda mahali faragha kidogo nafikiri utamruhusu,usijali atakuwa salama nimekuja na gari yangu ile SUBARU iko salama pia" "oh..ah..Kwa nini unaniambia mimi! si umuombe mwenyewe Kylie..ni mtu mzima kutoa maamuzi yake mwenyewe" aliongea Gerald kwa kujiuma uma huku akimtazama kylie,Harrison aligeuka na kumsogelea Kylie "okay jamaa pale ameturuhusu twende,please twende Kylie" Kylie alishindwa kukataa zaidi na kujikuta akiingia ndani ya gari ya Harrison na kuishia zao.

    "Hivi kwani tunakwenda wapi?" aliuliza Kylie aliyekuwa ndani ya gari ya Harrison wakielekea asipokujua "relax nimekuambia ni surprise utapenda tu.Nani yule?" "nani? oh yule ni rafiki yangu anaitwa Gerald" "ni rafiki yako! nafikiri atakuwa anakupenda kwa jinsi alivyokuwa akikuangalia inaonyesha anakupenda" aliongea Harrison huku akivua koti lake na kubaki na singlendi "hapana ndivyo alivyo,tumekuwa marafiki kwa muda mrefu" alijibu Kylie huku akimtazama Harrison kwa mshangao "una tattoo!" "yah,ni tattoo ya mama yangu na hiyo hapo ndogo ni ya dada yangu anaitwa Lisa wote ni marehemu sasa" "ina maana yule siku ile hakuwa mama yako!" "Baba yangu alioa mwanamke mwingine baada ya mama yangu kufa" alijibu Harrison na kuonyesha hasira kidogo usoni mwake.Gari iliwasili kwenye mtaa mmoja uliojaa vijana wengi walioonekana kuwa wahuni,baadhi walionekana kuvuta bangi na kunywa pombe kali wengine walionekana kupakata wanawake waliovaa nusu uchi na kuwapapasa maungo yao,mziki mkubwa ulisikika kutoka kwenye magari ya kifahari ya vijana hao.Harrison alipaki alipaki gari vizuri pembeni "tushuke" "no nitakusubiri humu ndani" "come on Kylie! unaogopa nini! uko na mimi,shuka bwana" aliongea Harrison.Kwa pamoja walishuka na kulisogelea kundi lile la vijana waliokuwa wakipiga kelele "ooh Harrison!" baadhi ya vijana walimsalimia kwa kugonganisha ngumi zao "huyu ndio demu wako mpya nini aisee unajua kuchagua mtamu kise#*" Kylie alikunja uso wake kuonyesha kukasirishwa na kauli ile "no Fredy kausha usinilazimishe nikuumize huyu siyo kama hawa malaya wako" alijibu Harrison.Mda huohuo wanawake waliovalia chupi tu walimsogelea Harrison na kumkumbatia lakini Harrison aliwasukuma mbali "tokeni zenu!.Rondo yuko wapi?" aliuliza Harrison.Mda huohuo mngurumo mkubwa wa gari ulisikika na kufanya watu wageuke kuitazama gari aina ya ALTEZZA iliyowasili na kupaki pembeni kidogo ya gari ya Harrison.Alishuka mwanaume mmoja aliyekuwa na upara huku mwili wake ukiwa umechorwa sana na tattoo "ooh Harrison umekuja! nilijua unaniogopa lakini unaonekana kumbe nilikosea.Na huyu msichana mrembo hapa ni nani!" aliongea Rondo huku akijaribu kushika uso wa Kylie lakini mkono wake uliondolewa kwa nguvu na Harrison" "ooh easy Harrison" aliongea Rondo huku akicheka "unajua Harrison unajua sana kuchagua wasichana warembo utanialika basi utakapomgonga na huyu mmh" "Rondo tumalize kilichotuleta hapa.Kylie ingia ndani ya gari" aliongea Harrison huku akikunja uso wake na kuingia ndani ya gari.Aliwasha gari yake na kuichochea kwa hasira huku akimtazama Rondo ambaye alikuwa ameingia ndani ya gari yake.

    Wakati huohuo kwa kina Emily sherehe kubwa iliendelea,Gerald aliketi kwenye meza huku akinywa pombe taratibu zilizoonekana kumlewesha "Gerald!" alinyanyua uso wake baada ya kuitwa na kushituka "ooh Paul! umekuja nilisikia unaumwa!" "hapana lilikuwa ni joto tu kali lilipanda.Kylie yuko wapi?" "eeh Kylie.. Kylie ametoka" alijibu Gerald "ametoka! kaenda wapi?" "sijui" Paul aligeuka na kumsogelea Gerald "una maana gani hujui! ametoka na nani?" "Harrison yule mtoto wa mwenye shule inaonekana wanafahamiana" alijibu Gerald.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Tunaondoka au?" aliuliza Kylie huku akimuangalia Harrison aliyekuwa akimtazama Rondo ambaye alikuwa ndani ya gari yake ya ALTEZZA "funga mkanda Kylie maana speed kubwa ni hatari" aliongea Harrison huku akichochea gari yake "no Harrison tuondoke tu this is not safe" aliongea Kylie kwa uwoga lakini Harrison alikuwa bize akimtazama Rondo kwa hasira "you know what mimi nashuka nitachukua taksi " aliongea Kylie huku akijaribu kufungua mlango wa gari lakini Harrison alimdaka kwa nguvu na kumvuta "sikiliza Kylie huendi popote umekuja na mimi na tutarudi wote.Trust me Kylie you going to be safe I'll keep you safe.Funga mkanda tushinde tuchukue gari yake." aliongea Harrison na kugeuka mbele kumuacha Kylie akifunga vizuri mkanda huku akihema kwa nguvu.Mwanamke aliyevaa chupi tu huku kifuani akiwa wazi alisogea taratibu mbele ya magari hayo huku mkononi mwake akiwa na bendera kubwa,aliipandisha na kuishusha na ghafla gari ya Rondo na Harrison zilitoka kwa kasi eneo lile.Harrison alikuwa hodari mkubwa wa kuendesha gari kwa kasi huku akibadili gia kwa haraka na kwa ustadi Kylie alikuwa roho juu huku akitetemeka sana ilikuwa mara yake ya kwanza kuwa ndani ya gari iliyokuwa ikikimbia kasi kiasi kile.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog