Simulizi : Nenda Na Moyo Wangu
Sehemu Ya Pili (2)
Aliponyanyuka Jafary Hiza, ndipo na yule mwanamke aliifikia meza tuliyokaa
na nikauona mshangao wa Jafary Hiza aliomtazama mwanamke yule kuanzia chini
mpaka juu naamini pia alivutiwa naye. Mwanamke yule akatabasamu hapo
akazidi kuvutia kutokana na lile tabasamu lake muruwa. Akasalimiana na
Jafary Hiza kisha akajitambulisha kwake.
"Naitwa Vanessa Noel" Huku tabasamu likiwa pana usoni mwake.
"Naitwa Jafary Hiza"
Kisha Jafary Hiza akamruhusu akae na yeye akaondoka. Vanessa alinitazama
kwa makini kwa sekubnde zisipongua dakika 10 kisha akaivua miwani yake
akazungumza nami.
"Siamini kama unaweza kumuuwa mpenzi wako" akatoa karatasi kadhaa na
kuziweka mezani kisha akatoa tepurekoda akaiweka pia mezani na kuongea tena
"kwanza kwanini umuuwe mwanamke uliyempenda? Pia ulikuwa hufahamu ukimuuwa
utaingia katika matatizo makubwa na mheshimiwa Oscer Valerian?" Hilo
lilikuwa ni jina la baba yake Beatrice ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa
umoja wa mataifa.
"Dada yangu hata nikikueleza vipi huweza kuamini ninachozungumza lakini
sina ukweli mwingine ninaoweza kukuambia zaidi ya kwamba sijamuuwa
Beatrice"
Akafanya kitu cha dharau sana na sijapenda na pia nilichukia ila kwa kuwa
nilikuwa mtuhumiwa, basi sikutaka kufanya fujo yeyote. Kisha akaniambia
"Naitwa Vanessa Noel nakufahamu unaitwa Ramon Lameck, mimi ni mpelelezi wa
kesi hii kwa upande wa mlalamikaji na ni mpelelezi binafsi. Mlalamikaji
ambaye ni mteja wangu amenilipa pesa nyingi sana za kung'amua kitendawili
hiki. Hataki tu kukufunga pia anataka kujua sababu ya wewe kumuua mtoto
wake. Hivyo mbali ya kuwa mpelelezi wa kesi nimesimama hapa kama
mwanasheria wako ambaye nitakutetea kutokana na vifungu vya sheria
vitakavyoniruhusu kufanya hivyo na ukweli utakaonieleza"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikahisi ni mtego. Mpelelezi wa kesi ya mauaji aliyemtuma ni Mlalamikaji na
hapo hapo ananieleza kuwa yeye ameletwa na mlalamikaji ili anitetee!!
Nikamuuliza Mungu, Ulinikutanisha na Beatrice ili maisha yangu yaishie
hapa? Kwanini kile nilichokiota na kutamani kukifanya katika maisha yangu
kinayeyuka kama mshumaa? Chozi likanidondoka kisha nikameza donge zito la
mate. Nikiwa katika kulia, Vanessa Noel akaipiga meza ile ya bati na
kuniambia.
"Huna sababu ya kulia sasa nitakuuliza mambo kadhaa na ninaomba unieleze
kile nitakachokuuliza"
Nikatingisha kichwa kwa kukubali, akaiwasha tepurekoda yake akaanza kuongea
huku akiwa amebonyeza kitufe cha kuruhusu sauti zetu kuingia katika kifaa
kile kwa ajili ya kumbukumbu.
Vanessa Noel akaniuliza swali la msingi ambalo sikutarajia kuulizwa katika
mazingira kama hayo. Akaniuliza kama nimeshakula tangu nikamatwe? nikamjibu
kuwa si tangu nikamatwe tu majira ya saa sita, yaani tangu asubuhi mpaka
sasa saa 9:38 alasiri(kulingana na saa iuliyopachikwa juu ya ukuta mbele
yangu ilivyokuwa ikisema) sijapata muda wa japo kunywa maji.
Vanessa alisikitika sana nilipomueleza hivyo, kisha akazima ile tepurekoda
na kubonyeza kitufe kile chekunde kwenye meza na kuzungumza na mtu wa
upande wa pili.
"Nahitaji chakula kwa ajili ya mteja wangu"
"Dakika chache" sauti ile nzito ikajibu.
Dakika chache baadaye, kweli lango lile likafunguliwa na toroli
lililosheheni hotpot tatu za vyakula na jagi kubwa la kuvunjika lililobeba
maji ya matunda, lilikuwa likisukumwa na askari wa kike mrembo .
Hotpot zikafunguliwa, Vanessa akaitwaa sahani yake na glass ya kujimiminia
maji yale ya matunda ya embe na pansion, kisha akachota tambi akachanganya
na nyama roast pamoja na zile za kukaangwa wa kuku. Nikapata nafasi ya
kumuuliza Vanessa baada ya kila mmoja akiwa anashughulika katika kung'ata
minofu ile.
"Hapa ni wapi? Na kwanini nimeletwa hapa na si mahabusu kama
nilivyotarajia?"
"Hapa panaitwa Safe house watu kama wewe huletwa sehemu kama hii kutokana
na makosa yenu mliyoyatenda. Kama unamkumbuka yule kijana aliyemuua Mtoto
wa Raisi Baraka katika ule mkasa ulioibua hadithi iliyouza nakala nyingi ya
kitabu kilichoitwa NISAMEHE MWANANGU, aliletwa hapa kabla hajapelekwa
Mwanza kwa ajili ya hukumu. Hata yule aliyemuua Waziri mkuu Peter Chongola,
katika mkasa uliandikwa na mwandishi mashuhuri mwenye njaa stallone na
kuita TAKSI YA KIJIVU(MUUWAJI ANAYETAFUTWA), yeye pia aliletwa hapa. Hivyo
na wewe uliyemuua mtoto wa kigogo wa Un umelazimika kuletwa hapa kwa ajili
ya mahojiano kabla ya kesi yako kunguruma"
Hapo nikawa nimemuelewa sana Vanessa kisha tulipomaliza kula alikuja askari
yule yule akatoa vyombo tulivyolia mazungumza yakaendelea.
"Anafanana na Beatrice kwa mbali?" Vanessa akanitoa katika mawazo ya
kumtazama askari yule akaniuliza kiuchokozi. Mimi sikumjibu, bali nilicheka
kiasi na kumtazama Vanessa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Vanessa ni mwanamke mrembo sana niliyewahi kukutana naye katika maisha
yangu. kwa ufupi si rahisi kumuelezea Vanessa nikamaliza. Vanessa akawa
anaweka kifaa kile cha kurekodia sawa na akaniuliza swali.
"Nataka nianze kufahamu mlikutana wapi na Beatrice"
Nikaanza kusimulia tangu siku ya kwanza nilipopelekwa na baba chuoni pale-:
CHUONI UDOM
kilikuwa ni kipindi cha kipupwe na baridi kali ilivuma kiasi cha kila
mwanafunzi pale chuoni alikuwa amevaa sweta la kumkinga na baridi. Mimi
nikiwa mtoto wa pekee katika famili yetu, baba yangu mzee Lameck alikuwa na
furaha sana kwa kuwa sikumuangusha tangu nilipomaliza kidato cha nne,
nikapata alama nzuri za kuniwezesha kuchaguliwa na serikali kwenda shule ya
Tambaza kisha baada ya hapo ndipo nikachaguliwa kwenda Udom.
Naweza kusema kuwa baba yangu ni rafiki yangu wa karibu sana katika maisha
yangu. Alifurahia mafanikio yangu na kuhuzunika kwa shida zangu hakika
najivunia sana kuwa na baba kama yeye. Siku hiyo ya kwanza akaniacha niende
kuripoti ofisini na kupewa chumba changu akaniambia kuwa
"Soma kwa bidii sana mwanangu, wewe ni mtoto wa kiume wa kike ataolewa wewe
utaowa hakikisha unaposoma ukitazama daftari unamuona mke na watoto wako
pale" akawasha gari na kuondoka.
Mimi nilienda kwa Den of student kisha akanikabidhi kwa warden ambaye
atanipa ufunguo wa chumba changu pale hostel za chuo. Nikakaa katika hostel
za watu wa social huku mimi nikiwa nasomea Public administration. Huko
nikakutana na vijana wawili Steven Ngonyani pamoja na Michael Stambuli.
Hapo ndipo nilianza kumfahamu Beatrice.
Tukiwa tumetoka dinner na wale vijana wenzangu yaani steve na michael,
tulienda katika Carteen ambayo Michael alituelekeza kwa kuwa yeye alikuwa
ni mwenyeji pale chuoni kabla yetu. Huyu Michael alikuwa mwaka wa pili huku
mimi na Steve tukiwa mwaka wa kwanza steve akiwa amenitangulia wiki moja
kabla mimi sijawasili pale chuoni.
"Huku kuna watoto balaa" Michael akaendelee kutudokeza kama alivyoanza
kutushawishi mpaka tukaja katika mgahawa huu. "Nyinyi rukeni kote ila kuna
mtoto anaitwa Beatrice huyo niachieni, chombo changu hicho"
Nikapatwa na hamu sana ya kumuona huyo Beatrice ambaye Michael alikuwa
haachi kumtaja. Niliagiza wali samaki huku wenzangu wakila ugali na samaki
mkavu. Ghafla Michael akatushitua wote tutazame kule alipokuwa akitazama
yeye.
Alipokuwa akitazama Michael, kulikuwa na wasichana watatu waliokuwa
wakiingia pale katika ule mgahawa tulipo sisi. Kutokana na mgahawa ule kuwa
mrefu sana, japo walikuwa mbali niliweza kuuona urembo wao sawia.
Mmoja alikuwa chotara bila shaka, kutokana na nywele zake za singa zilizo
ndefu kiasi zilifika mgongoni zilipeperuka peperuka; alikuwa akicheka na
mmoja aliye kuwa upande wake wa kushoto huyu alikuwa mweusi wa kawaida
mwenye shepu ya kibantu kwa mbali nilifanikiwa kuuona mwanya wake yeye
alivaa sketi fupi hivyo miguu yake minene niliweza kuiona kwa ukaribu
zaidi. Msichana huyo mwingine ndiye ambaye Michael alitaka tumuone bila
shaka. Maana alipoona tu tumegeuka, akaropoka kama aliyewehuka.
"Huyo anakuja, huyo hapo anayeongea na simu"
Kwa mara ya kwanza nikawa nimemuona Beatrice, ilikuwa ni siku ya kwanza ya
mimi kuingia hapo chuoni na ndiyo siku ya kwanza kukutana na Beatrice.
Itachukua kitabu kizima endapo nikitaka kuelezea uzuri wa msichana huyu.
Niliacha kula nikimtazama. Alikuwa ni mrembo kweli, mrembo haswa. Sasa
nikagundua kilichokua kikimchanganya Michael.
Kwa ufupi tu ni kwamba Beatrice alivaa sketi kama yule mbantu, yeye hakuwa
mweusi wala mweupe rangi yake wala haikuwa maji ya kunde, ila alikuwa
anaukaribia weupe. Siwezi kuelezea kwa ufasaha rangi hiyo ukanielewa. Sura
yake ilikuwa ya mviringo lakini alikuwa ana asili ya nywele kwa sababu
alijaa vinyweleo juu ya ngozi yake kiasi cha kunivutia zaidi kwa kuwa mimi
ni mmoja kati ya wanaopenda aina ile ya ngozi. Vinyweleo laini vilivyolala
juu ya ngozi. Kifuani alikuwa amebeba embe sindano ambazo ziliendelea
kusimama wala hazikutaka kulala hivi karibuni. Kiuno kilikatika kikike huku
hipsi zikijichora sambamba na makalio yaliyovimba na kuinua sketi ile na
kuifanya iwe ndogo zaidi. Alikuwa akiongea na simu mpaka alipovuta kiti
akakaa na mara nikashituka nikishikwa.
"Hoya brother, ndio ushachanganyikiwa?" Alikuwa ni Michael huku Steven
akinicheka "Haya ulikuwa ukimtazama nani? Yule Alisia, Prisca ama Beatrice?"
"Duh! Kaka! Mtoto Beatrice namba nyingine" nikaishia hapo nikachota kijiko
cha wali nikakitupia mdomoni, nikavuta mrija wa juisi nikautia mdomoni
nikawa nanyonya juisi taratibu nikimtazama Michael.
Chuki!! Nikaiona hasira katika uso wa Michael iliyozaa chuki. Ndita
zikaharibu paji lake la uso kisha akasonya na kufinya kidogo macho yake
kama atiaye mkazo kwa jambo alilotaka kuzungumza, hakuongea bali midomo
iliishia hewani akatupa kidole chake cha shahada kama akinionya jambo.
Steve akawa anatazama hali hiyo kwa mshangao sanjari na ilivyokuwa kwangu.
Sikuwa na shaka kwa kuwa moyoni mwangu sikumaanisha kumpenda Beatrice kwa
wakati ule ila kama ujuavyoa wavulana tumuonapo mwanamke mzuri lazima nafsi
zetu ziwake tamaa. Wao waliumbwa kwa ajili yetu.
Tuliendelea kula huku mimi nikiibia ibia kutupa jicho katika meza ya sita
aliyokaa Beatrice na wenzake. Mara ya kwanza, ya pili na ile ya tatu
niligongana macho kwa maho na Beatrice halafu kama waliyekuwa wakiniteta na
yule chotara ambaye baadaye nilikuja kufahamu kuwa ndiye Alisia. Sikujua
walichozungumza lakini walikuwa wakitazama meza yetu. Nikazuga kumtazama
Michael nikamkuta yeye akiachia tabasamu pana huku akiwapungia mkono
akiwasalimia. Nilitamani kucheka ila nilijizuia kwa kujifanya nakunywa
juisi.
Nikanyanyuka kwenda kunawa mikono kwenye ndoo itiririshayo maji kama
bombani, ghafla nikagongana na mtu, mtu yule hakuwa mwingine bali ni
Beatrice. Akanimwagia juisi iliyobaki kidogo kwenye glass yake na kuchafua
shati langu nililovaa.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MAHOJIANO NA VANESSA SAFE HOUSE
Kabla sijamaliza kueleza kila kilichokuwa kikiendelea, Vanessa
akanikatisha.
"Sasa ni saa 11 jioni naomba tuishie hapa kwa leo kesho tena nitakuja
kukutembelea ili niweze kujua kilichoendelea. Naomba usiache hata moja
unalolijua niweze kujua jinsi ya kukusaidia"
"Sawa" nikamkubalia, kisha tukaagana na Vanessa.
Vanessa alipoondoka askari wawili waliingia katika kile chumba na mnyororo
fulani uliunganisha pingu za miguu na mikono ambao nilifungwa mimi kisha
nikavalishwa kitambaa cheusi mfano wa kofia ya mzula kisha nikatemnbezwa
taratibu kutoka katika chumba kile.
Nilipokuja kuvuliwa kile kitambaa, nilikuwa ndani ya selo ya peke yangu
lakini ni chumba chenye hadhi ya kulaliwa na mtu mzito. Chumba hicho
kilikuwa na hewa ya pekee na utofauti wa chumba hiki hakikuwa na dirisha
wala mlango.
Hapana! Sasa mimi nilipita wapi? Sikushuka ngazi wala kupanda ila kuna
mlango ulifunguliwa, uko wapi sasa? Mauzauza!!!
Nilijaribu kugusa kuta za pande zote nne za chumba kile baada ya kufanikiwa
kufunguliwa kile kitambaa cheusi, sikufanikiwa kuona chochote kinachofanana
na mlango. Hapo nikakumbuka kile chumba nilichowahi kukiona katika
tamthilia moja pendwa inayoitwa 'The legend of the seeker' sasa nikajiona
mimi nikiwa ni muhanga mmoja wapo kama wale wasichana wawili ndani ya
tamthilia ile.
Nilijaribu kupiga kelele lakini chumba kile kikameza sauti yangu hata
mwangwi haukurudi kama nilivyotaraji. Niligusa hapa na pale sikufanikiwa
kupata chochote ninachokitafuta. Nikaamua kukaa pembeni mwa kitanda kipana
chenye godoro zito pana kutoka chini kwenda juu na kulia kwenda kushoto
lenye mashuka meupe pee! Kisha usingizi ukanipitia. Nikiwa hapo hapo bila
kujitambua.
Niliamka mara baada ya kuamshwa na askari wa kike ambaye alibeba sahani ya
chakula pamoja na glass ya juisi. akaniambia
"Kesho kuna ndugu zako watakuja kukuona"
Nikamshika mkono, nikamuuliza mara alipotaka kuondoka.
"Mlango wa hiki chumba uko wapi? Kwanini nipo hapa na si mahabusu yeyote
chafu kama wafanyiwavyo wavunjaji wa sheria kama mimi?"
Msichana yule alitabasamu kisha akauputa mkono wangu na kunieleza.
"Hapa ni Safe house, wewe ni mtu katili sana na inabidi ulindwe kwa
uangalifu sana kabla hatujajua chanzo cha wewe kufanya mauaji yale.
Unalindwa kwa kuwa inaaminika kama umeweza kumuuwa mwanamke ambaye usiku
uliopita uliweza kudanganya wazazi wake kwa kumvisha pete ya uchumba na
mbele za watu wengi ukakiri unampenda yeye tu huku ukitabasamu kinafki, je
tutajuaje kama umetumwa kumuangamiza mheshimiwa Oscer? Nimekusaidia
kukueleza siri nyingi ila sijilaumu kwa kuwa huoneshi kuwa katili kama
inavyotangazwa huko nje" akatoa gazeti na kunitupia katika mapaja yangu
"Nilipoitazama sura yako katika gazeti hili, sikukubaliana na kichwa hicho
cha habari"
Mara, mara!! Nini hiki? Nasinzia jamani, mara nikalala wala sikumuona yule
askari wa kike wakati anatoka.
Nilipokuja kuamka nililikuta gazeti lile pale pale mapajani mwangu pembeni
kukiwa na sinia la chakula. Nilitazama huku na kule sikumuona yule mwanamke
wala sikuona chochote kilichobadilika katika kuta zile. Nilipotazama katika
sinia lile la chakula, sikukitamani chakula kwanza kabla sijasoma
kilichoandikwa katika gazeti hilo.
"MUUWAJI WA MTOTO WA KIGOGO WA UMOJA WA MATAIFA AKAMATWA NDANI YA NYUMBA YA
MAREHEMU"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kisha picha kubwa ikinionesha nikiwa ndani ya nyumba ya mpenzi wangu
Beatrice. Picha hiyo alinipiga yule askari ambaye hakuvaa sare za kipolisi
kisha akanicheka mara nilipokuwa nimejikojolea. Niliitazama picha ile kwa
uchungu na kuisoma habari ile kwa hasira kisha nikameza donge zito la mate
lililonikaba kwa uchungu. Nikakunja kunja lile gazeti na kulitupa kisha
nikapiga kelele za maumivu kutokea ndani ya moyo wangu kutokana na kesi
hiyo mbaya ya kusingiziwa.
Nikalipiga teke sinia lile la chakula nikapiga magoti kwenye kitanda changu
cha kulalia kisha nikalia kwa uchungu. Hakika hakuna kipindi kigumu
nilichokuwa nikipitia zaidi ya hiki katika maisha yangu. Wakati nikiwa
nimejiinamia pale, askari watatu wakaingia.
"Wewe muuwaji! Una nini?"
Ilikuwa ni sauti ya askari mmoja mnene mrefu kiasi, kidevu chake kilikuwa
chakavu kutokana na ndevu na mapele yake yaliyokomaa. Nilipoinuka na
kumtazama ila sikumjibu kitu.
"Mtoeni humu labda hapendi Ac mpelekeni mahabusu za kawaida kule napo kuna
ulinzi mkali"
Wale askari wawili ambao walisimama pembeni yangu wakanibeba msobemsobe kwa
kunishika makwapani kwangu huku mimi nisisimame, hivyo walikuwa
wakiniburuza. Hapo nikawa nimeuona mlango ulivyokuwa wazi na jinsi ya
kuufungua na kuufunga ilinishangaza teknolojia ya namna hii. Sikutegemea
kama hapa hapa Tanzania nilipoishi zaidi ya miaka 26 kungekuwa na sehemu ya
namna hii.
Nikaburuzwa mpaka katika sehemu yenye selo nyingi ambazo zilikuwa tupu na
kutupwa katika moja ya mahabusu hizo bila huruma, kisha wakaniacha hapo
bila kusema lolote. Baada ya dakika chache baadaye, alikuja yule askari wa
kike aliyeniletea chakula mwanzo akaniambia.
"Nimekuletea chakula ule ukikimwaga na hiki shauri yako sintakuonea huruma
tena"
Uso wake haukuwa na mzaha, akakisukumiza kile kibakuli kilichojaa wali,
paja la kuku na ndizi mbivu kwa mguu wake kisha yeye akaondoka.
Nilikula kile chakula mpaka nilipomaliza kisha nikaenda kujitupa katika
kitanda kidogo kipatacho futi 4 kwa 6 cha chuma, nikasinzia.
Ilikuwa asubuhi, alikuja yule askari wa kike na kuniamsha kwa kirungu.
"Wewe, wewe!!"
Nikaamka.
"Embu njoo! Una mgeni wako"
Niliamka haraka haraka kwenda kukutana na mgeni huyo. Sikujua ni nani,
lakini nilitamani sana kukutana na ninayemfahamu ili niweze kupata faraja
ya moyo japo kujua ni vipi watu wanachukulia kesi yangu. Yule askari
akanifunga pingu mikono yangu kwa nyuma kisha akaniongoza mpaka ilipo
sebule ya nyumba ile.
Hapo mwanzo sikuweza kufahamu kabisa kama nilikuwa ndani ya nyumba ya
kifahari namna hii. Samani za gharama zilisheni katika sebule ile. Kila
kona kulikuwa na vitu vya thamani sana. Sikuvalishwa tena kile kitambaa
cheusi ila ulinzi wa kuvalishwa pingu mfano wa minyororo haukukoma.
Nilipotokeza nikiwa katika mshangao wa nyumba ile, niliweza kuwaona walinzi
lukuki wakitembea tembea huko nje na nilipoyatupa macho yangu kwenye
makochi ya pale ukumbini, mgeni aliyekuwa akinisubiri ni Michael rafiki
yangu. Yule askari akazungumza
"Dakika mlizopewa ni 30 tu za kuzungumza"
Nikatazama ukutani kulipokuwa na saa ilikuwa ni saa 3:14 asubuhi siku ya
pili tangu Beatrice auwawe. Nasema auwawe kwa kuwa si mimi muhusika wa
mauaji hayo licha ya kuwa kila mtu anaamini ni mimi ndiye niliyeua.
Nikamtazama Michael nikiwa na furaha lakini Michael alionesha wasiwasi mara
aliponiona. Wasi wasi ule wa Michael ukanitisha sana. Hakuzungumza wala
mimi sikuzungumza kama kwa sekunde kumi hivi, kisha akaniuliza.
"Ramon" kama aliyekuwa akiniita lakini hakumaanisha kuniita, akaendelea
"Umekuaje rafiki yangu?"
Sikujibu haraka, nilimtazama Michael moja kwa moja katika macho yake kama
niliyekuwa nikimsoma jambo kisha nikamuuliza "Michael wewe una amini
nimeua?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Unadhani mimi nitaamini vipi Ramon?" Alinijibu huku akiitupa mikono yake
miwili hewani na uso wake ukiwa katika hali ya msisitizo.
Hapana! Kuna kitu nakiona katika macho ya Michael si kizuri. Kwanini
Michael anayenifahamu mimi kwa miaka 4 zaidi leo anaamini mimi nimeua? Mimi
nina sura ya kuua? Michael anaigiza na kuna kitu anafahamu. Nikapatwa na
wasiwasi na Michael juu ya kifo cha Beatrice.
"Kiukweli habari hizi zimenishangaza sana Ramon. Sikutegemea mtu kama wewe
unaweza kufanya jambo la kikatili namna ile"
Sikumjibu kitu ila kuna kitu kikawa kimenikaba ndani ya koo yangu na
machozi yakinilenga kwa uchungu.
"Sina cha kukusaidia au kukushauri katika hili kwa kuwa unafahamu fika mzee
Oscer(baba yake Beatrice) ana nyadhifa gani hapa Tanzania. Cha ajabu na
kinachonishangaza wakati umeua na bado ukaendelea kubaki eneo la tukio.
Ramon pombe ulizokunywa, pombe mbaya rafiki yangu nilikuwa nikikuambia kila
siku"
"Unasema nini wewe Michael? Kwanini unanituhumu moja kwa moja bila kuwa na
uhakika Michael? Mimi wa kuuwa?" Uvumilivu ukanishinda sasa nikawa naropoka
kwa hasira huku sauti yangu ikipaa juu hata niipoinyanyuka ikaongezeka
zaidi "nakuuliza, mimi naonekana muuwaji kwako leo? Au kwa kuwa msichana
yule ulikuwa unampenda? Ina maana nilidhani huna chuki tena nami kumbe
ulikuwa mnafki? Michael.." Nikamuinamia mpaka ulipo uso wake na kunyoosha
kidole katika kifua changu nikamwambiwa kwa dhati na hisia kali kwa sauti
ya chini "Mimi sijamuuwa Beatrice lakini muuwaji atapatikana"
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walinzi waliovalia sare nyeusi ambazo si za askari niliowazoea wa hapa
Tanzania, walikuja na silaha nzito na mmoja wao alituuliza
"Kuna nini? Ustaarabu umewashinda?"
Michael alinyanyuka huku akinitazama, akacheka kwa dharau na kutingisha
kichwa. Akaniambia
"Pole rafiki yangu nitakuja kukuona siku nyingine"
Michael akaondoka.
Nilibaki pale sebuleni wale walinzi nao wakaondoka. Machozi sasa
yakadondoka kwa uchungu. Rafiki yangu amenisaliti. Vipi kuhusu wazazi
wangu? Mama yangu ataniamini?Sina shaka na baba kwa kuwa yeye hunijua vyema
mimi. Nikatupa jicho pembeni nikakutana na gazeti la udaku.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment