Search This Blog

Friday, October 28, 2022

MAFANIKIO KATIKA AKILI YANGU [SUCCESS ON MY MIND] - 4

 

     





    Simulizi : Mafanikio Katika Akili Yangu (Success On My Mind)

    Sehemu Ya Nne (4)





    SURA YA SITA.

    Ni saa 2;30 asubui noeli anawasili katika studio anafika na kukutana na mkurugenzi wake akiwa ameweka mikono mfukoni.Nabahasha kadhaa akiwa amezishikilia mkono wake wa kushoto, ‘’bosi shika moo’’ alimsalimia noeli ‘’marahaba’’ aliitikia kwahali yake ambaayo ilikuwa sii kawaida yake kabisa.Noeli alianza kuonea utofauti hapo wakati sikuzilizopita alikuwa akimuamkia aliitikia kwa furaha na bashasha kubwa sana, ‘’mmmh! Leo kuna nini?’’ alijiuliza mwenyewe kichwani lakini noeli alishindwa kupata jibu aliendelea na shuguli zake za kiofisi alipoingia chumba cha production alikutana na nyuso za huzuni kwa wafanyakazi wenzake.’’dada fatuma vipi?’’ aliuliza noeli fatuma alikuwa akikaa pamoja mno ingawa fatuma alikuwa, ni mtaaruma akiwa na shahada ya mawasiliano kwajamii yani [masscommunication] ‘’noeli kuna…… hapa leo’’ aliongea kwa utaratibu fatuma nae jina lake lilikuwa limo katika orodha ya watu ambao wanaotaka kuondolewa ofisini.Majina mkurungenzi aliyaanda kwa siri sana alikuwa hayupo mfanyakazi ambae aliyekuwa hajui kilichokuwa kikifanyika haukuweza kupita muda mrefu sana, mkurungenzi aliingia ofisini kwake na kuwaita wote kwa pamoja. ‘’mpo wote?’’ aliuliza mkurugenzi ‘’ndio’’ waliitikia kwapamoja kwasauti iliyokuwa na muungurumo usiokuwa na kifani, kisha akawaambia kile alichokuwa amedhamilia kukifanya. ‘’mmeona upotevu uliotokea?’’ aliwauliza mkurugenzi hukuakionekana kitofauti sana aliongea kwa vituo vituo kisha akaendelea kuongea ‘’kuna watu nitaenda kuwatowa hapa ofisini’’ taarifa hiyo ilikuwa imewashituwa watu karibu wote mule ndani na kuweza kunyog’onyea sana, alipomaliza alitowa bahasha zilizokuwa na ameshikilia mkononi mwake.Nakuanza kuwaita majina mmoja baada ya mwingine, na fatuma ndilo lilikuwa jina la kwanza kuitwa nalapili lilikuwa nila noeli baada yakuya taja hayo majina.Alinyanyuka kutoka katika kiti chake na kuwambia, ‘’nilio waita kwanzia sasa ofisi yangu haiwaitaji tena’’ kisha akawaamuru waweze kuondoka ilikuwa niwakati wa huzuni hata kwaambao walibakia pale pia, ilikuwa nipigo kubwa sana kwafatuma lakini noeli kwake ndio ilikuwa pigo kubwa zaidi.Maana hakuwa na lakufanya wala mbadala wowote ule, noeli alitembea akiwa amejitwika mikono kichwani mithiri ya mtu ambae aliyefiwa. ‘’nitaenda wapi mimi na nitafanya nini?’’ ndio maswari nyaliokuwa yakimtawala kichwani mwake noeli, walitembea jiani kama wagonjwa fatuma ambae alikuwa gwiji wa habari za michezo na uchunguzi alijuwa sasa hana nafasi yakuweza kusikia tena katika media.Kutokana na mawazo aliyokuwa nayo akijuwa sehemu aliyopo ndio itakuwa suruhu kwa taaruma yake.Nime pata kusikia vijana flani waliowasomi wakiamini taaruma zao zinaweza kutumika sehemu flani tu.Hayo ni mawazo hasi pia katika mapambano yakuelekea mafanikio. ‘’naenda kuteseka na shahada yangu’’ aliongea fatuma akimwambia noeli huku wakitoka nje ya geti la studio hizo, noeli alikuwa ni mwenye huzuni mno alimwambia fatuma, ‘’mimi ndio sito sikika tena’’ alisema noeli baada ya kufikilia kwamba wapo wataaruma wakihangaika kusaka kazi hiyo na wamekoswa, nakubakia kuzunguka na vyeti sasa yeye ataweza kweli kumudu ushindani? Alipowaza hilo alijikuta kujikatia tama mwenyewe.

    Kila mmoja alikuwa akiwaza lake kipindi walipokuwa wakitembea.Hatimae waliweza kufika katika kituo cha daradala.Fatuma alielekea uelekeo wake na noeli nae alielekea uelekeo wake, kupanda gari kurudi nyumbani ilikuwa mtihani mwingine tena kwa kijana noeli maana alikuwa hana nauli yakuweza kumfanya aweze kufika nyumbani kwao, yakuja kazini aliweza kusaidiwa sasa atarudi vipi? Juwa nalo lilikuwa kali sana lakini njaa nayo ilikuwa ikimsumbuwa sana. ‘’aiseee! Nitarudi vipi nyumbani’’ aliwaza sana.Alijuwa endapoangeendelea kukaa studio asingeweza kukoswa nauli yakurudi nyumbani, kutoka na kufahamiana na watu wengi mno.Aliendelea kukaa katika kituo cha daradala noeli alikuwa hapendi kabisa kuomba pesa hususaniakina dada huwo ulikuwa utamaduni wake ambao aliokuwa kajiwekea, akiwa amekaa katika kituo cha daradala alimuona mdada mmoja ambae alikua mzuri sana.Alivuka baraba nakuja palepale kwenye kituo cha daradala nakukaa pale alipokuwa,amekaa noeli kisha ana msalimia ‘’mambo’’ alimsalimia Yule dada noeli kisha noeli nae akaitikia, ‘’safi dada’’ aliitika noeli halafu Yule dada kwaharaka alifanikiwa kumgunduwa kuwa noeli anamawazo mengi sana yanayo usumbuwa moyo wake.



     ‘’unaenda wapi?’’ aliuliza Yule dada hukuakitengeneza nywere zake kichwani ‘’naenda hapo tu’’ Yule dada alijisikia tu kumuongeresha noeli muda mfupi tu alipopita noeli aliona daradala likipita na kusimama pale kituoni, kisha Yule dada anaenda kupanda daradala na kuondoka ‘’oya unaenda?’’ alimuuliza konda hukuakimyooshea mkono noeli, alitikisa kichwa kuonyesha kuwa haendi.’’dah! sasa utangazaji naacha!’’ alikuwa haamini alihisi uwenda maisha yake yatakuwa magumu sana atakoswa hata pakuweza kujishikiza.Noeli alikuwa pia na mtizamo sawa na wa fatuma aliwaza kisha wazo lingine lika mjia akilini. ‘’naingia katika uwanda wa shida’’aliwaza kichwani mwenyewe noeli.Baada ya kusubilia sana hatimae noeli aliweza kupata lifti ya gari kwenda katikati ya mji, ingawa alikaa kwamuda mfefu sana akiandamwa na mawazo.Akiwa bado ndani ya gari alijikuta bado akiwa kwenye dimbwikubwa la mawazo.Aliye mpa lifti ya gari alikuwa hamfahamu wala walikuwa hawafahamiani na hawakuwai kuonana popote. ‘’unashukia wapi?’’ alimuuliza mwenye gari hukuakiwa anaendesha, ‘’nitashuka samaki’’ alimjibu noeli kwakujirazimisha ingawa kiukweli alikuwa mbali sana kimawazo.kwakuwa gari lilikuwa likikimbia sana walijikuta kufika kwa haraka mjini, walipofika noeli alishuka na kumshukulu sana Yule aliyempa lifti. ‘’asante sana kaka’’ alisema noeli hukuakiwa anashuka nyumbani hakutamani kwenda alihisi kuchanganyikiwa. ‘’baba yangu angekuwepo’’ alijiwazia mwenyewe moyoni hukuakiwa kasimama katika kituo cha daradala mjini kilichokuwa maarufu kwa jina la samaki.Akiwa bado angali akiwaza akilinyingine ikamjia, ‘’kwanini nisijiuwe tu nahangaika hivi mpaka lini mimi ni hizi shida mpaka lini’’ alipowaza kaulihiyo aliuma meno yake kwa msisimko masaa aliyaona yakienda taratabu siku nayo aliiyona kwake nindefu sana kutokana na mambo yaliokuwa yamemkuta.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Anaamuwa kupanda ghorofa ya ppf gorofa lililokubwa sana katika mji wa mwanza.Ana panda mpaka gorofa ya sita, lengo ilikuwa ni aweze kujirusha na aweze kutoka duniani.Alifikia mpaka hatuwa yakuona hana umuhimu katika hii dunia noeli aliona akiishi katika dunia ambayo niya mateso. ‘’nitoke duniani maana mimi sina maana ya kuishi katika dunia hii’’ aliongea maneno hayo noeli kwa sauti ya nguvu, hukuakipandisha ngazi kwakupanda.kuelekea gorofa ya saba alipofika gorofa ya saba alisimama na kuregeza viungo vyake vyamwili.Ilikuweza kuruka kwenda chini, kumbe alipokuwa akipanda gorofani kuna walinzi wakawa wakimfuatilia kwanyuma kutaka kujuwa alichokuwa akitaka kukifanya.Alipokuwa akitaka kuruka walimfuata na kumshikilia kwanguvu huku kila mmoja akiwa ana mshangaa kwakile alichokuwa akitaka kukifanya, ‘’wewe una matatizo gani’’ aliuliza mmlinzi mmoja, ‘’amekuaje huyu kijana?’’ kila mmoja alianza kumshangaa nakuanza kumfikilia kwa namna tofauti.Watu wote ndani na nje ya jengo la ppf walijazana kuweza kushuhudia kilichokuwa kimetukia katika gorofa ya saba, wapita njia pia waliokuwa wakipita katika barabara ya nyerere pia walisimama hata ambao hawakujuwa, kile kilichokuwa kikiendelea walisimama nakuuliza ilikutaka kujuwa vyema. ‘’kuna mtu anataka kujirusha huko gorofa ya saba’’ alipishana na watu wakiongea habari hiyo pastor Yule mzungu ambae alikuwa kaisha kutana na noeli, nakufamiana nae pastor alikuwa amekuja kumtembelea moja kati ya marafiki zake waliokuwa wakifanya kazi katika jengo hilo. ‘’mtu anataka kujiuwa!’’ alishangaa sana pastor nae akaanza kupandisha ngazi kuelekea kulikokuwa na tukio kuweza kushuhudia. Ile anapanda tu akakutana na watu wakiwa wamemshikilia noeli hukunakule, noeli akiwa amejawa na simanzi hukujasho zikiwa zina mtoka.Mwili mzima hofu nayo ya macho ya watu ikiwa imemtawala.Pastor alishangaa sana kiasi hata cha yeye kuweza kukosa raha kabisa wakati hawa wakiwa wamemshikilia noeli, kutaka kumfikisha katika hatuwa nyingine za kisheria.pastor akaibuka nakuwauliza. ‘’amekuwaje huyu kijana?’’ aliuliza pastor kisha watu ambao walikuwa wamemshikilia noeli wakamjibu, ‘’anamatatizo ya akili’’ pastor aliwashangaa kusikia wakisema hivyo, kwani alimuamini noeli ni timamu wa akili na hakuweza kuliafiki hilo kisha alimshika mkono na kuondoka nae, wale waliomshikilia walimuuliza Yule pastor mzungu ‘’unaenda nae wapi?’’ kwakuwa pastor alikuwa amejawa na ustaalabu, ‘’huyu kijana wangu na mjuwa’’ alijibu pastor akiwa analengwalengwa na machozi, akashuka nae kisirisiri mpaka ndani yagari kisha wakaondoka nae wakiwa njiani pastor alianza kumuuliza maswari noeli. ‘’noeli imekuwaje tena?’’ alikuwa akiuliza hukuakiendesha gari na huzuni ikimjaa, ‘’pastor nahisi mungu anipendi’’ alisema noeli huku uzuni ikizidi kujidhihirisha usoni mwake.’’ooooh! kwa nini unasema hivyo noeli?’’ pastor aliongea kwa imani sana hakutegemea kama noeli angeweza kufikia hatuwa kama hiyo aliyokuwa nayo. ‘’nimefukuzwa kazi bila ya hatiya yoyote’’ aliongea noeli akitamani kulia pastor alimwangalia sana usoni kisha akamwambia noeli, ‘’noeli wewe ni mshindi haijalishi unapitia mambo gani na wakati gani’’ pastor aliendelea kumpa [motivation] na kumfanyia ushauri na saha wa nguvu ili noeli asije kufanya kitu cha kuishangaza jamii na kuacha majonzi katika familia yake.’’dah! pastor sijui kama nita pata tena kazi nayo ipenda kama hii’’ alisema noeli majonzi pamoja na huzuni vilizidi kumtawala noeli. ‘’usikate tama unajuwaje kama mungu je anataka kukufungulia njia kupitia mlango mwingine’’ alisema pastor Yule wakizungu ambae alikuwa kweli anatumiwa na mungu kuwa inuwa watu kiimani na kimaisha pia.Kadili walivyokuwa wakiendelea kuongea na pastor na pastor kuendelea kutowa [motivation].Hali aliyokuwa nayo noeli ikawa inatoweka taratibu, nakuanza kurudia hari yake ya mwanzoni, ‘’noeli katika macho yangu nakuona unakuwa mtu flani’’ kwa maneno aliyokuwa akiyanena pastor alijikuta noeli kutabasamu, tuna takiwa kuwapa maneno mazuri marafiki zetu au hata ndugu zetu wanapokuwa katika wakati mgumu, itatusaidia katika jamii zetu na taifa na hata bara letu afrika,[napenda kuona jinsi motivation speaker wanavyojitokeza na kuhamasihsa watu afrika]. Waliongea wakiwa katika gari lakini pia pastor alikuwa amepanga sikuhiyo aweze kukaa sikunzima na noeli ilikuomba na kujifunza zaidi maandiko matakatifu yana sema nini kuhusu maisha.







    Punde si punde waliweza kufika, kwa pastor walizungumza maongezi machache.Baada ya kumaliza kuongea pastor alimuomba noeli wapige magoti na waweze kusali. ‘’nitaenda kuomba kwajili yako’’ alisema pastor kisha noeli akakubalia pastor alianza kusali mpaka misuri ya shingoni ilimsimama, alisali kwangvu na kutowa sauti kubwa sana, akiwa anasali simu yake nayo ikawa inaita na haikuwa simu ya Tanzania.Au simu kutoka ndani ya taifa la Tanzania ilikuwa ni simu kutoka nchini urusi, simu ilikuwa ikiita mno hatimae pastor aliamuwa kuweza kukatisha maombi, nakwenda kuipokea ile simu alihisi uwenda ikawa simu muhimu sana. ‘’hellow’’ aliongea huku simu akiwa ameiweka kwa mfumo wa sauti kubwa [loud speaker] ‘’yes ni mimi mr alisoni kutoka mosco urusi’’ alipokwisha kujitambulisha pastor akawa alishamuelewa vizuri ‘’alaaa za siku?’’ walisalimiana kwa furaha maana ilikuwa nisiku nyingi walikuwa hawajaweza kuwasiliana, ‘’ulisema una…… unataka apate udhamini wa kusoma’’ pastor alikubalia na kumwambia, ‘’ndio nisaidieni kwa hilo’’ alizidi kuweka mkazo zaidi pastor juu yahilo jambo.Wakati wakiongea noeli yeye alikuwa amebakia akiwa amefumba macho lakini pia kila kilichoongelewa alikuwa anasikia. ‘’nafasi imepatikana anataka kusomaa couse gani?’’, pastor akamjibu kwaharaka ‘’anataka kusoma jounalism’’ mr alison aliweza kutokwa jibu la ujumla, ‘’sawa muandae tarehe 26 juni aweamewasili jijini mosco’’ dah! Ilikuwa furaha kwa pastor kuweza kupata taarifa kama hiyo.Ambayo mwenyewe pia hakuitarajia kwa wakati huo. ‘’sawa asante sana mr alison’’ mr alison alikata simu yake kisha pastor akasimama na kusema ‘’mungu ni mwema’’ maana hakuweza kuamini kama jambo hilo lingetukia kwa wakati huo.Mr Alison alikuwa ni profesa wa chuo kikuu flani huko mosco urusi, Alison alikuwa ni rafiki sana wa pastor noeli alifurahiya sana na alijuwa anae takiwa kufanyiwa taratibu hizo ni yeye.26 JUN ndio ilikuwa mtihani wa kupimwa na endapo noeli ataenda kufaulu ndipo watakwenda kumchukuwa. ‘’noeli?’’ alimuita pastor ‘’namm’’ noeli aliitikia kwa furaha zaidi kisha pastor akamwambia, ‘’umeona sasa’’ aliongea pastor hukuakiwa anamuangalia noeli na kutabasamu noeli nae alikuwa akimwangalia nakutabasamu, ‘’umepata nafasi ya kwenda kusoma mosco urusi’’ noeli alisimama na kurukaruka kwafuraha, ‘’asante sana’’ aliongea ukuakimpatia pastor mkono wa pongezi na furaha kwakile alichokifanya. ‘’ilakuna mtihani wa majaribio’’ alisema pastor akimuweka sawsawa katika hilo. ‘’nitafanya na kufauru’’ alisema noeli kwakujiamini, ama kweli kumbe ukiona dhiki imezidi juwa raha zimekalibia.Noeli aliyekuwa akitaka kujiuwa hakutarajia kama atapata taarifa nzuri na njema kama hiyo.

    Zawadi akiwa dareslaamu biashara imekubalika,Wazo jingine lakibiashara likawa limemuungia.Aweze kuanzisha kilimo hii ilikuwa baada ya kugunduwa kwamba hata kilimo, kumbe anaweza kufanya.Maisha yake yalikuwa mazuri maana hata nyumbani yeye ndie kwa sehemu kubwa ndio alikuwa akiwa hudumia. ‘’zawadi hii ndio dar ina pesa’’ alisema mwenyeji wake na zawadi, ‘’nikweli’’ alimsapoti kwa kile alichokuwa kakiongea ‘’tufanye hata kilimo’’ aliamuwa kusema kile alichokuwa akikihisi, mwenyeji wakena zawadi akihisi zawadi ajaweza kuwaza kabisa. ‘’dah! Uwezi kuamini nilisha waza hilo tayari’’ zawadi alicheka kisha akamwambia Yule mwenyeji wake wazo lilimjia baada ya kwenda eneo la mkuranga na uwanda wote wa pwani.Nakukuta maeneo mengi yakiwa wazi, na watu wakiwa wame yaangalia zawadi alitaka kuichukuwa fursa na kuweza kuifanyia kazi.Walikuwa wakizungumza huku wakiwa wanakula, katika eneo la chalinze ilipokuwa [center] ya mji huo mdogo ‘’wanawake wamekaa tu’’ alisema zawadi, http://deusdeditmahunda.blogspot.com/‘’hawa ni wanawake wa kipwani’’ alimwambia Yule mwenyeji wake. ‘’wao wanapendelea nini?’’ aliuliza zawdi alikuwa ni mdadisi sana kila alichokiona alitaka kukijuwa kiundani.Nikwa nini kimekuwa hivi au vile alitamani kujuwa zawadi, ‘’wao hukaa nyumbani tu’’ alisema mwenyeji wake ‘’aisee!’’ alishangaa sana binti zawadi hukuakitamani sikumoja aje kuwa [motivation speaker] kwa watu ususani kwa wanawake na mabinti wenzake.Ambao wanaoishikatika mitizamo hasi, wakati huo bado zawadi alikuwa akifanya biashara yake ya samaki hukuakifunguwa akili yake katika Nyanja mbalimbali za kibiashara.Zawadi alikuwa ni binti watofauti maana alikuwa akijikita kusoma pia vitabu vya kuhamasisha. [motivation books] Yule mwenyeji wake alikuwa amemuona na kitabu kwamuda wasiku kadhaa akiwa amekishikiilia aliamuwa kumuuliza, ‘’zawadi kwanini umeshikilia kitabu kwa muda mrefu?’’ aliuliza zawadi alimjibu, ‘’napenda sana kusoma vitabu ilikupata maarifa’’ alijibu zawadi hukuakikishikilia kitabuchake vizuri.Kusoma vitabu pia vya uhama sishaji kulimpa zawadi mitizamo chanya na fikra chanya pia katika kila alichokuwa akikifanya zawadi alikuwa ni binti watofauti, na mabinti wengine wa kitanzania[ukitaka kuwa na mafanikio jitofautishe na wengine].

    **

    SURA YA SABA.

    Nimuda wa usiku koroboi ikiwa kwamwanga mkari na kutowa moshi juu. sebleni kwao na noeli, mama yake alikuwa amekaa kwakujikunyata kwa ubaridi.Ambao uliokuwepo siku hiyo pembeni alikuwa amekaa na mtoto wa zawadi, ambae alikuwa ameshaanza kukaa noeli alikuwa na furaha kubwa sana akawa akikaa huku akiwa anatabasamu.Kila mmoja kati ya watu hawa alikuwa na hisiya tofauti, na katika ukuwaji kila mmoja alikuwa na aina yake, mama noeli alikuwa amekaa kichwa akiwa kakiinamisha chini.Wakati huohuo noeli yeye noeli alikuwa na furaha isiyokuwa na kifani. ‘’mama nina habari njema’’ alisema noeli hukuakitabasamu, ‘’habari gani?’’ aliuliza mama noeli akiwa ametulia na kupooza sana aliwaza mno maana biashara yake ilikuwa imekufa.Askari walikuja na nyumbani kwa mamanoeli na chukua kila kitu ambacho alikuwa akipikia pombe, ‘’mwanangu hebu acha nikwambie’’ alinyanyuwa shingo yake na kunyanyuwa miguu yake, ‘’umekuwaje mama’’ alikaa kimya kwa muda kisha akamjibu ‘’biashara yangu imekufa’’ noeli alikuwa akishangaa sana, ‘’kwa nini?’’ bado mama noeli alikuwa kimya akifanya tafakali kuweza, kumudu maisha yake ‘’askari wamechukua kila kitu’’ dah! Noeli alisikitika kisha akamwambia, ‘’mama usihofu umasikini umekwisha’’ aliongea hukuakimshika mama yake mabegani.Mama ake alikuwa ajaelewa kabisa noeli ana niniau kitugani, ‘’nimepata nafasi ya kwenda kusoma mosco urusi’’ mama yake nae gafla akapatwa na furaha, ‘’urusi!’’ alishangaa na kujiuliza malambilimbili maana hata urusi alikuwa hajui iko wapi na bara gani. ‘’ndio mama urusi’’ alimjibu noeli mama yake ‘’nakazi?’’ noeli alikuwa muwazi sana kwa mama yake.Alimwambia namna mungu alivyomfungulia mambo kwanjia ambayo niya ajabu na hakuweza kutarajia kabisa kama ingekuwa namna hiyo.





    yehova kweli anatenda pale unapoona giza limetanda mbele yako yeye ndio hapo anapokwenda kuonyesha nuru yake.’’mama kwanza kabisa naomba ujuwe nimefukuzwa kazi’’ alisema noeli hukuakiwa kawaida na mwenye furaha, ingawa mama yake alikuwa amepunguza mawazo aliposikia hivyo tu furaha ikaweza kumuishia kabisa kutokana na taarifa hiyo mbaya.Noeli aligunduwa mama yake amenug’unika sana kisha anamwambia, ‘’ila mama usihofu nitaenda urusi yehova atanipa wepesi tu’’ noeli alijuwa sasa ndio ulemuda ambao alikuwa akiuwazi miaka mingi iliyokuwa imepita tangia alipokuwa kidato cha tatu, alipokua akiwaza sikumoja aje kufanya kazi ya uwandishi nje ya taifa lake na kusomea pia nje ya taifa lake.Alijaribu kumshawishi mama yake kuondowa dhana ya kuhangaika tena na maisha,

    Wakati noeli akiwa nyumbani kwao usiku huo pastor yeye alikuwa ameisha lala.pastor akiwa usingizini anapata ndoto, alijikuta akitembea sehemu yenye madhari sawa na mwezini.Akiwa ana tembea alikutana na mtu aliyekuwa akig’aa kama miare ya jua. ‘’mbona una tembea……. Unafuata nini?’’aliulizwa pastor na Yule mtu aliyekuwa akig’aa kama miare ya juwa, kisha pastor akamjibu kwakujiamini, ‘’nimeshangaa niko hapa’’ pastor alimjibu lakini moyo wake ulikuwa umegubikwa na uwoga usiokuwa na kifani.Kisha Yule mtu akamwambia ‘’namuona kijana flani akija kuwa mtu mkubwa barani afrika na mashuhuli’’ kisha mtu huyo akatoweka pastor akajikuta akiwa mwenyewe kama ambavyo ilivyokuwa mwanzoni.Gafla upepo ukavuma kwanguvu kiasi cha kumzidia nguvu pastor akaanguka chini baada ya kudondoka chini alishindwa kusimama kutokana na upepo kuwa na nguvu sana.Akashituka kutoka usingizini akatupa shuka pembeni kisha, anaenda sebleni alipofika sebleni alisikia kengele ya alamu ikiita kutoka getini, alianza kujiuliza maswari mengi kichwani.Kikubwa alichokuwa akijiuliza ninani aliyekuja kumtembelea usiku huo.Gafla roho ya ujasiri ikaweza kumuingia pastor kisha anaamuwa kufunguwa mlango na kutoka nje alipotoka nje alimkuta mlinzi akiwaamesimama na bwana mmnoja mwenye kitambi. ‘’ehe kuna nini?’’ aliuliza pastor kwa haraka hukuakiwa anahofu mlinzi akamjibu na kumwambia, ‘’pastor kuna mgeni wako’’ alisema mlinzi, ‘’pastor za siku nyingi?’’ aliongea Yule bwana na tayari pastor akawa ameisha mjuwa/ kumtambuwa. ‘’ahaaa lucasi’’ aliweza kumtabua haraka maana walikuwa wakikutana sana. ‘’nammm pastor samahani kwakuja usiku’’ aliongea kwakujitetea lucasi, ‘’usijali bwana karibu ndani’’ wakaingia ndani nakumuacha nje mlinzi.Lucasi alikuwa ni rafiki mwingine wa pastor ila lucasi alikuwa ni mtanzania, lucasi alikuwa akifanya kazi katika ofisi ya mambo ya ndani. ‘’nammm pastor’’aliongea hukuakiwa anakaa vizuri katika kiti, ‘’nilikuita unifanyie mpango kuna kijana wangu anatakiwa kwenda mosco urusi’’ aliongea pastor hukuakiwa anamuangalia lucasi, ‘’sawa kwa muda gani?’’ aliuliza lucasi, ‘’wikimbili tu’’ lucasi alikuwa akiangalia nakutikisa kichwa chake kisha anamwambia, ‘’nimtanzania?’’ pastor alimjibu nakumwambia, ‘’ndio ni mtanzania’’ lucasi alitowa orodha ya vitu ambavyo vilivyokuwa vinatakiwa ili aweze kumkamilishia kijana huyo masuala yake na aweze kwenda nchini urusi. ‘’anaenda kufanya nini?’’ aliuliza tena lucasi ‘’anaenda kimasomo’’ alijibu pastor kwakuwa lucasi ilikuwa sio mala yake ya kwanza kumfanyia pastor [process] za kwenda nje ya nchi, hakuwa nashaka na pastor kisha anamwambia, ‘’alete vitu hivyo tumfanyie…… haraka’’ pastor pia alikuwa akimwamini sana lucasi maana hakuwai kumuangusha katika kazi alizokuwa akimfanyia hapo nyuma.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati noeli akiwa amekaa na mama yake hukuhuzuni ikiwa imetawala.Kwa wingi zaidi akiwaza atafanya nini kununua vifaa vingine tena,Alijuwa itamgarimu pesa nyingi nae pesa alikuwa hana, polisi walimchukulia kila kitu na kitenge cha pesa.Nakuweza kuondoka nacho ‘’mwanangu zawadi si tuta muuwa?’’ alisema mama noeli hukuakiinamisha kichwa chake chini. ‘’mama kwanini umesema hivyo’’ alimuuliza mama yake kutaka kujuwa kwanini mama yake amesema maneno kama yale, ‘’unajuwa mpaka leo….. ndio anatulisha’’ alisema mama noeli, noeli alikuwa halijui hilo alijuwa mama yake ndio kilakitu kwake.Maana noeli alikuwa na kipindi kirefu akiwa ajafanya mazungumzo ya kina zawadi dada yake, walikuwa wakikutana na kusalimiana kila mmoja alijikuta akiwa na mabo yake/ akiwa katika kuhakikisha ndoto zake zina kwenda kutimizika.Noeli alishangaa sana ilikuwa ni taarifa ambayoa alikuwa hakuitegemea kabisa katika akili yake, ‘’ina maana zawadi amekuwa na…… kiasi hicho?’’ aliuliza noeli maana hata safari za dada yake alikuwa akiziona hazina maana yoyote.Noeli alionekana mnyonge sana hakufurahiya atakidogo baada yakuambiwa na mama yake kuwa zawadi ndie anawalisha yeye pia akiwa mmoja wao. ‘’hivi uwanaume wangu na ujana wangu uko wapi?’’ alijiuliza mwenyewe noeli akilini swari hilo, aliona kama anauzembe flani na ujinga ambao ulikuwa umegubika kichwa chake.Wakiwa wanaongea ndani mala barozi wa nyumba kumikumi pamoja na mwenyekiti wa mtaa wakawa wame simama nje na kuanza kuita, ‘’mama noeli?’’ kisha mama noelialiitikia kwa haraka ‘’abee!’’ aliitikia kwakushituka sana maana ilikuwa adimu mno yeye kuitwa usiku hata majirani zake ilikuwa sikawaida yao.Mwenyekiti pamoja na barozi walikuwa wameshilikilia mafaili pamoja na baruwa ambazo zilikuwa ndani ya bahasha.punde tu mala noeli na mama yake wakawa wametoka nje, kwakuwa kulikuwa na giza kubwa mama noeli alianza kwakuuliza, ‘’nyie akina nani?’’ aliuliza hukuakiwa anatembea sanjari na mwanae. ‘’kuna nini nyie?’’ aliuliza noeli hukuakiwa anawaangalia kama watakuwa ni watu salama kwao, ‘’ni mimi mwenye kiti’’ barozi nae alijitambulisha kwaharaka noeli alishusha hali ya kuwa na hofu pamoja na wasiwasi katika moyo wake vivyo hivyo mama yake pia.Walimpa mama noeli barua nae mama noeli baada ya kuipokea alimpa noeli mwanae, baada ya pale mwenyekiti pamoja na barozi waliondoka.

    Ilikuwa ni asubuhi yenye kupendeza zawadi akiwa ametoka kulala siku hiyo joto lilikuwa kali sana.Lilikuwa joto kali mno hasa kwa waliokuwa wageni wa mji wa dareslaamu, ‘’aisee joto kali sana’’ alisema zawadi hukuakiwa anajipepea kwa kitenge ambachoalikuwa amekitundika mabegani. ‘’ndio nature ya mji huu’’ alisema Yule mwenyeji wake, hukuakiwa anatirilikwa na jasho usoni mwake. ‘’huu mji siupendi kwa joto tu’’ aliongea zawadi hukuakiwa anajipepea ‘’leo inatakiwa kwenda kudai madeni yaliobakia’’ alisema zawadi kisha mwenzake akamuuliza, ‘’kwanini mbona haraka?’’ zawadi alinyamaza kwadakika kadhaa kisha akamjibu, ‘’nataka kurudi mwanza’’



     ukweli ilikuwa zawadi alikuwa amemkumbuka sana mwanae pamoja na mama yake kule nyumbani akitaka kuwai iliarudi kuwajulia hali nyumbani kwao zawadi alikuwa, anapenda nyumbani kwao.Wakati zawadi akiwa anawaza hayo bwana ake ambae alizaa nae watoto alikuwa akipanga kujakumchukuwa mtoto wake, alikuwa amekaa na ndugu zake wakimpa ushauri kuhusu suala hilo ‘’benja mwanao vipi?’’ aliulizwa na ndugu yake mmoja, ‘’yuko na mama yake’’

    ‘’amekuwa sana?’’

    ‘’ndio’’ benja alimuowa zawadi kwakumtorosha kwenda kuishi nae na kumrubuni kwa maneno ya ulaghai.Nabaadae aliamuwa kumuacha kwa sababu zisizokuwa na msingi, alikuwa na rafiki yake waliyekuwa wakishibana sana. ‘’unamuacha vipi amchukue mwanao?’’ alikuwa akimshangaa sana, ‘’nitaenda kumchukuwa kwao zawadi’’ rafiki yake alikuwa akimwambia afanye kila awezalo amchukuwe mwanae. ‘’twende leo’’ alizidi kumshawishi huyo rafiki yake wana amuwa kufunga majadiliano na kuanza safari yakwenda nyumbani kwao zawadi ili waweze kumchukuwa mtoto wa benja.

    Noeli baada ya kuamka asubuhi walibakia kuangaliana na mama ake.Maana hawakuwa na pesa hata kidogo matumbo yaliwaunguruma, kwanjaa kari mtoto wake zawadi nae alilia kwanjaa iliyokuwa ikimsumbuwa.Noeli anaamuwa kuondoka nyumbani akiwa anaondoka mama yake akamuita, ‘’noeli’’ aliamuita mama yake. ‘’namm mama’’ hukuakisimama mithiri ya gari lililo shika breki kwagafla. ‘’unaenda wapi?’’ aliuliza mama yake kisha noeli akamjibu, ‘’naenda kufuatilia mambo yangu flani’’ alimficha mama yake noeli akiwa hataki kabisa mama yake ajuwe anapo kwenda, ‘’haya sawa nenda’’ alimruhusu mama yake aweze kwenda alikokuwa akienda, wakati noeli alipokuwa akiondoka alikuwa amepanga kwenda nyumbani kwa Yule pastor.Lengo la kwenda ilikuwa ni kuweza kukaa nakuongea na pastor huyo.Siku hiyo noeli alikuwa na nauli iliyokuwa imekamilika alienda moja kwamoja mpaka katika kituo cha daladala akaingia ndani ya gari nakukaa akiwa ametulia, ‘’leo siombi mtu’’ alijisemea moyoni abiria wa kwanza katika gari hilo alikuwa ni noeli.Wakati akiwa kwenye gari alikaa dirishani nakuangalia mambo ya nje, mala akamuona fatuma akiwa na bahasha lake la kaki, ameshikilia mkononi noeli uzalendo wakutulia na kumuacha fatuma apite ulimshinda.Ana amuwa kumuita kwanguvu, ‘’fatumaaaa’’ aliita noeli huku kichwa chake akiwa kakiweka nje ya dirisha ilifatuma aweze kumuona vizuri, ‘’nani anae niita?’’ aligeuza shingo yake fatuma kuangalia aliyekuwa akimuita.Lakini sauti alianza kuitambuwa mapema mno ‘’lakini sauti kama ya noeli’’ aliendelea kuangaza hatimae alimuona noeli akiwa ametowa kichwa chake nje ya dirisha la gari.Fatuma ana mfuata mpaka alipokuwa noeli hukuaki tabasamu, ‘’noeli unaenda wapi?’’ aliuliza fatuma akiwa mbali hukuakitembea kwenda kule noeli alikokuwa.’’naenda pasiasi’’ aliongea hukukichwa chake akiwa bado amekitowa nje, ‘’pasiasi kufanya nini?’’ aliuliza fatuma huku akiegemea dirishani alikokuwa amekaa noeli na kuelekeza kichwa chake. ‘’naenda kwa pastor wangu’’ aliongea hukuakiwa anatabasamu noeli, fatuma yeye alimwambia kuwa ana taka kwenda kujaribu katika makampuni mengine ya utangazaji fatuma kufukuzwa kwake katika kituo cha redio kuliweza kumrudisha nyuma sana kwakiasi flani fatuma alikuwa ametoka katika familiya ya watu wenye pesa.Lakini hakuwa na wazo lakuweza kufikilia kukaa nyumbani, ‘’harakati tu’’ alisema fatuma kisha noeli akamsapoti kwahiyo kauli yake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ ‘’nikweli dada yangu pambana’’ alizidi kumtia moyo noeli mwana dada fatuma, ‘’haya maisha usitegemee nyumbani’’ alisema fatuma wapo ambao walimshangaa sana wakati nyumbani kwao kungali na mali na maisha mazuri pia. ‘’mmmh! amependa mwenyewe tu’’ yalikuwa maneno ya mabinti wenzake ambao waliosoma na fatuma ambao walitegemea mambo ya kusaidiwa kuliko, kutumia akilizao au uwezo wao ambao mungu aliwajalia, fatuma na noeli waliongea maneno machache na kisha waliachana ‘’tuzidi kuonana’’ lilikuwa neno la fatuma lamwisho kwa noeli.Fatuma alitembea kwamiguu sana kisha anaamuwa kufika sehemu na kukaa, hukuakifunguwa na chupa yake ya maji nakuanza kunywa akiwa anakunywa maji yakishuka kooni mala wazo flani likawa limemuingia akilini. ‘’hivi naangaika kutafuta kazi weee hivi sina kabisa nachoweza kufanya mimi kama fatuma?’’ alijiuliza swarihilo kichwani mwake mwenyewe, ‘’hivi siwezi kuwa mwana mitindo mkubwa au mkulima mkubwa?’’ bado alikuwa akijiuliza maswari hayo kichwani mwake.Fatuma alijikuta kuwaza hivyo pasipo kuangalia hali ya nyumbani kwao wala nini, ‘’mbona kuna wanawake matajiri why mimi naweza bwana’’ aliendelea kuwaza hukuakitia fundo la maji tena katika kinywa chake.Fatuma baada ya kuwza hivyo alihisi kuthubutu kwakitu au vitu ambavyo alikuwa amewaza, Nae alikuwa na ndoto sawa naza dada yake noeli zawadi akitaka siku moja Tanzania iweze kumjuwa na awe mwana mke au mwana dada wakuigwa katika taifa lake.Fatuma alifikilia juu ya hayo mambo mawili, na alitaka afanye uchunguzi wakina sana, kuweza kujuwa utaratibu wa kilimo au kuanzisha kampuni yake ya ubunifu wa mitindo.Fatuma alikuwa hakuwaza pesa kwanza maana aliamini kwamba siku zote katika maisha, wazo ndio huanza na badae pesa ndio hufuata aliamini ata bilionea wakwanza duniani na mwanzilishi wa kampuni ya[ Microsoft] birgert alianza na wazo ndipo pesa zika futa ndivyo ilivyokuwa farisafa yakuamini kwa binti fatuma binti mwenye akili na msomi.Wakati alipokuwa akiwaza mala baba yake akawa amempigia simu fatuma, fatuma aliipokea simu kwa haraka ‘’fatuma?’’ alimuita kwakufoka katika simu baba yake, ‘’abee baba’’ aliitikia fatuma ‘’uko wapi?’’ aliuliza baba yake ‘’niko kwenye……. Ya kazi’’ aliongea kwakujiamini fatuma baba yake alimshangaa sana, mwanae fatuma kusema hivyo wakati fatuma anajuwa baba yake angali na uwezo mkubwa tu wa kipesa.Aliona kwamwanae atakuwa akimdaririsha akiwa anahangaika kutwa nzima na bahasha yake. ‘’ebu rudi nyumbani’’ alisema baba yake katika simu, ‘’haya sawa baba’’ alisema fatuma kwakumtii baba yake lakini nafsi yake ilikuwa ikimpeleka katika masuala mengine kabisa.Fatuma ukiachia elimu yake kuwa kubwa pia alikuwa ni mbunifu mzuri katika suala zima la kuchola, alipokuwa [highschool] alishinda katika shindano moja la kikanda akawa mchoraji bora wakati huo alikuwa nchini Uganda akisoma, ‘’kama niliweza kuwapiku watu mianne nikiamuwa iwe seriously busness inakuwa’’ aliendelea kuwaza mwenyewe kichwani.Akijaribu kujitafutia namna yakuweza kufanya mambo yake mwenyewe, akawa akipata hoja nyingi sana ambazo zilianza kumfunguwa akili yake kiasikikubwa sana.Wakati fatuma akiwaza hivyo zawadi nae dada yake noeli alikuwa ni mchoraji mzuri sana tena alichora michoro ya kiafrika yenye kuvutia zawadi michoro yake ilikuwa ni yaki mataifa ingawa hakuwai kushindana katika kinyang’anyiro chochote.



     Cha masuala kuhusu uchoraji katika namna yoyote ile, zawadi akiwa jijini dar eslaamu akiwachumbani amekaa mwenyewe aliingiwa na hari ya kutaka kuchora maana ilikuwa yapata kama miezi mitatu akiwa hajachora, ile hari yakutamani kuweza kuchora ikawa imemuingia.Tena kwashauku kubwa sana zawadi alipenda kuchora ukiachia mbali kwamba ana uwezo pia wakubuni biashara. ‘’nasiku nyingi sana sija chora’’ alipata wazo hilo baada yakuona karatasi kubwa, nyeupe ilivyokuwa mbele yake, akaangaza na karamu kisha anachukuwa na kuanza kuchora picha ya mwanamke mrembo ambae alikuwa akionekana wa kiafrika kwa mavazi aliokuwa kamtilia katika ubunifu wa uchoraji.Mwenyeji wake alikuwa ametoka kwenda kuteka maji alipo rudi alimkuta zawadi akiwa ameshikilia ile picha, ‘’umeipatia wapi hiyo picha?’’ aliuliza mwenyeji wake ‘’nimeichora mwenyewe’’ alisema zawadi ‘’hapana kweli zawadi!’’ alikataa kwanamna mvuto wa picha ulivyokuwa pili alikuwa haamini kama zawadi anauwezo mkubwa kama ule wakuchora picha yenye ubora kama ile, ‘’una uwezo kweli kama huu?’’ aliuliza Yule mwenyeji wake akiwa haamini, ‘’ndie mimi nilie chora’’ aliongea zawadi hukuakiona fahari kushikilia picha yake. ‘’mmmh!’’ aliguna huku akishangaa mwenyeji wake, ‘’huwamini au nichore nyingine?’’ ilibidi aweze kukubalia maana picha hakuweza kuiyacha ndani kisha akamshauli, ‘’kama unaweza kuchora na mna hii omba magazetini’’ lilikuwa wazo jipya ambalo zawadi hakuwai kufikilia ‘’siunaona katuni’’ alizidi kumpa maarifa iliaweze kutumia kipawa chake. ‘’huwa naziona tuu gazetini’’ alijibu zawadi ‘’sasa kumbe hata wewe unaweza’’ baada yakuambiwa hivyo zawadi alikuwa akizidi kumchimbuwa mwenyeji wake iliampe, namna yakufanya ‘’ofisi za magazeti ziko wapi?’’ aliuliza zawadi, ‘’nitakupa namba za mr simba’’ alisema mwenyeji wake ‘’mr simba yeye ni nani?’’ alikuwa akitaka kumjuwa vyema huyo mr simba. ‘’nimhariri mkuu’’ zawadi alifikilia mno kisha akamwambia, ‘’ataweza kuni saidia?’’ mwenyeji wake alimtoa hofu na kumwambia, ‘’tena atakusaidia sana’’ zawadi bado aliendelea kujiuliza ‘’hivi inawezekana kweli?’’ akawa akijipa maswari mengi ndani ya moyo wake hukuakitikisa kichwa, ‘’ila itawezekana tu’’ roho nyingine ya uthubutu na ujasiri ikamuingi zawadi.****

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SURA YA NANE

    Baada ya wiki kupita noeli akawa amekamilisha kila kitu, Ambacho alikuwa akitakiwa kukifanya.Katika safari yake ya nchini urusi katika mji wa mosco ilikuwa ni muda wamchana, pastor akiwa anamfanyia [shoping] noeli katika maduka mbalimbali ya mji wa mwanza. Hatimae wanaingia duka la dada mmoja liyeitwa Irene, Irene alikuwa ni [africast] mwenye utanzania pamoja na uswideni, ‘’pastor nichukuwe…..?” aliuliza noeli hukuakiwa anaangalia nguo ‘’hapana chukuwa nguo nzito mosco kuna baridi’’ noeli alikuwa ni mwenye furaha iliyopitiliza. ‘’dah! Humu nguo ni nzuri’’ alisema pastor hukuakiwa anamuangalia Yule dada ‘’wewe binti unatolea wapi nguo nzuri kama hizi?’’ alimuuliza hukuakigeuza shingo yake kuangalia nguo kwakweli nguo ndani ya duka hilo zilikuwa niza kuvutia katika kila aina yanguo. ‘’natolea south Africa au dubai’’ alimjibu Yule binti muafrikasti ‘’noeli umeona lakini?’’ alipotaja jina noeli Yule Irene akashituka na hata sauti ya noeli alianza kuhisi alishaisikia sehemu flani. ‘’wewe ni noeli?’’ aliuliza Yule mdada muafrikasti, hukuakimuelekezea noeli kidole, ‘’ndio mimi’’ alikubalia kijana noeli pasipokuwa na wasi wasi ‘’ulikuwa ukitangaza redioni?’’ bado aliuliza Yule binti muafrikasti kisha noeli akamjibu ‘’nikweli nilikuwa niki tangaza’’ Yule binti alifurahiya kisha akamuuliza tena, ‘’mbona sikuizi sikusikii?’’ noeli alimjibu akamwambia kuwa yeye alishaacha kazi.yule binti muafrikasti aliweza kukaa kimya nakubakia kutabasamu kisha akamwambia, ‘’ulikuwa ukitangaza vizuri sana noeli’’ noeli alimshukulu baada ya kumpatia sifa kama hiyo, alizidi kuandika makala katika gazeti lile ingawa walikuwa hawampatii ujira wowote.Noeli alikuwa akitafutwa katika simu mno na watu walikuwa wakimpongeza kwa makala zake nzuri ambazo alikuwa akiandaa,kilichokuwa kikimbeba noeli ilikuwa ni ukubwa wa maarifa aliokuwa nayo kijana noeli. ‘’aisee nimebahatika’’ alisema Irene pastor akawa akimshangaa binti Irene kwanini amesema amebahatika, kisha anaamuwa kuumuuliza ‘’umebahatika kwa ninia labda?’’ aliuliza pastor noeli yeye alikuwa kimya hatamwenyewe akujuwa kwanini Yule dada amesema vile, ‘’nimekutana leo na mtu maarufu kama noeli’’ alisema yulebinti wa kiafrikasti, noeli alishangaa sana pastor nae alikuwa akishangaa sana, ‘’mimi mbona mtu wa kawaida’’ alisema noeli kisha Yule binti muafrikasti ‘’hapa wewe noeli ni mtu maarufu sana’’ ilikuwa ni habari yakumfurahisha noeli pia alikuwa akifurahiya kimoyoni.Kisha akaguna ‘’mmmm!’’ hukuakitabasamu na kumwambia noeli, ‘’wewe una hadhina yakuja kuwa mtu maarufu sana’’waliendelea huku wakizunguka duka zima.Kuweza kuchaguwa nguo ‘’napenda iwe hivyo’’ alisema noeli. zawadi alikuwa amesha rudi mwanza, alirudi akiwa na kasi ya biashara na kuwekeza katika kila kitu alichokuwa akifanya.Kuchora alikuwa akijitahidi sana kila iliyoitwa siku alikuwa akijitahidi kuboresha michoro yake kuchora kulimfanya hata aweze kujikuta akiwa anachelewa kulala nyakati za usiku.Mama yake zawadi alikuwa akimshangaa sana kuona zawadi akichelewa kulala kwa sababu ya kuchora, usiku mmoja alinyanyuka kutoka usingizini na kumkuta zawadi akiwa anachora yapata mida ya saa tisa usiku.Aliamka na kumwambia ‘’zawadi ulali?’’ zawadi nae alimjibu na kumwambia, ‘’mama na chora’’ alimjibu zawadi mama yake na kisha aliendelea kuchora michoro yenye hadhi ya kiutamaduni na mienendo ya kimataifa.Ingawa zawadi alikuwa na elimu ndogo na ufaulu wa matokeo yake kuwa wa wastani.Lakini hilo alikumfanya aweze kushindwa kuchora michoro ya kimataifa alichora micholo ya kimataifa [think big] kuna muda hatupaswi kujidharau kufanya vitu kwakuhofia elimu zetu pengine au hata kuhofia kutokana na uwezo wakifedha katika familia zetu.Inatupasa kufikilia vikubwa ili tuwe watu wa kubwa haijawai tokea mtu akafikilia hasi na akaja kupata matokeo chanya biblia inasema [ajionavyo mtu ndani ya nafsi yake ndivyo alivyo].

    Wakati noeli akiwa anafanya shoping zawadi dada yake yeye alienda ofisi ya gazeti moja la mwanza.Kupeleka michoro yake alikuta watu wakiwa [busy] sana alisimama akiwa ameshikilia bahasha yake, ‘’dada vipi mbona umesimama?’’ alimuuliza bwana mmoja ambae alikuwa pia mfanya kazi wa mule ndani, ‘’nashida na wahusika’’ alisema zawadi hukuakiwa amesimama bado ‘’unashida gani?’’ aliyekuwa akimuhoji alikuwa ni muhariri msaidizi wa gazeti hilo.







    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog