IMEANDIKWA NA : DEOKING PETER
*********************************************************************************
Simulizi : Nini Hatima Ya Maisha Yangu
Sehemu Ya Kwanza (1)
Iikuwa siku ya jumamosi nilikuwa narudi nyumbani mida ya saa mbili usiku nilipo karibia nyumbani niliona gari aina ya Noh nyeusi kwa mbali imepaki mbele ya nyumba yetu. Sikujua ile Noh ilikuwa ya nani na ilikuwa imekuja kufanya nini. Mimi nilijua ni wageni wa Baba, niliamua kuzunguka nyuma ya nyumba yetu ambaop kulikuwa na mlango wa kuingilia ndani, kuepusha usumbufu wa wageni waliokuwa wamefika pale nyumbani. Nilipokaribia mlangoni kwa mbali nilisikia sauti na maneno ya kutisha ikanibidi niangalie sauti inatoka wapi, nilipozidi kusogea nilifanikiwa kujua ile sauti ilikuwa inatokea sebleni ambayo ilinifanya nichungulie dirishani, kujua niwakina nani wanaongea yale maneno.
“Nahisi kazi imeisha, hawa wapumbavu walijua wataendelea kukuwa hai huku wakimiliki fedha nyingi namna hii”
Ni maneno ambayo niliyasikia na kunitamanisha nichungulie dirishani. Nilipo chungulia dirishani nilishangaa kutokuona mtu yeyote pale ndani. Nilipo angza angaza vizuri nilifanikiwa kuwaona wazazi wangu wakiwa wamelala chini, huku Baba akiwa anatokwa na damu sehemu za kifuani.
Mama nae alikuwa amelala pale chini akiwa anaonekana mwenye kujawa na maumivu mengi. Wakati nashangaa nilisikia gari ambalo lilikuwa limepaki Pale nje linaondoka, nikaamua kutokanakimbia kwenda kuingia ndani ili kuhakikisha kama nikweli nilicho kiona dirishani.
Kwakweli sikuamini kile nilicho kiona wazazi wangu wamelala chini huku damu zikiwatoka niliwatingisha wote huku machozi yakinitoka, lakini hakuna hata moja ambae aliamka niliwaza kuwa ni wakina nani ambao walio fanya kitu kama kile kwa wazazi wangu na nikwasababu gani. Nilibaki najiuliza maswali bila kupata majibu. Wakati nawaza niliona kikaratasi mezani nilijua bila shaka ilikuwa inanihusu mimi.
“Pole sana John kwa kupoteza wazazi wako wote wawili, najua utaumia sana kwa kilichotokea, lakini na wewe ukitaka uwe salama na uishi maisha mazuri usije ukajaribu kuja kutoa taarifa polisi, na kama utafanya hivyo basi utaishi maisha mazuri. Kingine utakapoojiwa na polisi usijaribu kujifanya mjuaji, maana kabla ya mimi kwenda jela wewe utatangulia kuzimu ukaishi na wazazi wako huko”
Yale maneno yalikuwa yakutisha ikuweza kuamini kitu kama kile, machozi yalizidi kunitoka. Sikutaka kusikia kilichokuwa kimeandikwa kwenye lile karatasi, niliamua kwenda kuchukua simu ili nijaribu kutafuta msaada, lakini kabla ya kupiga ile simu nilisikia suti ikiniita, niligeuka haraka na kukuta ni mama yangu ndiye alikuwa ananiita, huku akiongea kwa shida.
“John mw.an.ang..u…..”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliachia ile simu na kwenda kumsikiliza mama yangu kile ambacho alikuwa ananiambia. “Mwa..nang…u. pole kwa kupoteza wazi wako wote wawili, maana Baba yako amekufa muda mrefu uliopita na mimi hata mimi sinto weza kupona kupona, ila mwanangu kabla Baba yako hajafa kunakitu aliniambia nikuambie ilikukusaidia katika maisha yako, kuna kadi ya benki ambayo nilimpatia mjomba wako Faraja akupe, maana kuna pesa benki ambazo zitakusaidia katika maisha yako ila namba za siri unaanza na mwaka wako unafuta na mwaka wa mdogo wako sophia na umwambie mjomba wako Denis, kunakitu nimempa mjomba wako umwambie akupe”
Aliongea mama huku ananalia kitu ambacho kilinifanya nipatwe na uchungu na hasira kali zilinipanda. Nikataka kumuuliza ni wakina nani ambao wamefanya hivyo nilishangaa mama analegeza shingo na kutulia kama mtu ambae amelala usingizi, nilimwamsha lakini hakuamka.
Kiukweli sikuamini kama mama yangu kipenzi amefariki.Niliona kama naota,Nililia sana huku nikiwa sijui nifanye nini,Maana kupoteza wazazi wote wawili alafu kwa umri niliokuwa nao kuanza kuishi maisha ya upweke nisinge yaweza, kiukweli niliumia sana maana wazazi wetu walivyo kuwa wanatupenda na kutujali, walikuwa wakitupa tulicho kihitaji,mimi pamoja na mdogo wangu Sophia ambae kwa wakati huo alikuwa kwa Bibi alikwenda kumsalimia.
Kiukweli ilikuwa pigo kubwa sana katika maisha yetu maana watu ambao tulikuwa tunawategemea hawakuwapo tena.
Baadhi ya majirani walio sikia kilio changu walikuja na ndio waliotoataarifa kwa polisi, Kila nilipokuwa nawaona nilihisi bado wazima maana niliwapenda wazazi wangu lakini Mungu kawa penda zaidi. kiukweli sikuamini kama Mungu ndiyo aliepanga wazazi wangu kufa kifo cha kinyama namna ile.
Polisi waliwachukua na kuwaingiza kwenye gari na mimi walinichukua kwaajili ya mahojiano, lakini ilikuwa ni usiku sana maana ilikuwa inaendea saa saba usiku, Baadhi ya majirani waliwakatalia na kuwaambia.
"Atakuja hasubuhi, maana sasa hivi ni usiku sana na hayo mahojiano ya usiku yanatoka wapi?"
Aliuliza mzee mmoja baada ya kuona polisi wanataka kunipeleka kwenye mahojiano na usiku ule.
Baada ya yule mzee kuzungumza, kuna Afande mmoja alinyanyuka na kusema.
"Mna huakika gani kama hawa wazazi wake wameuawa na majambazi au yeye ndiyo alie fanya hivyo"
Aliongea yule afande baada ya yule mzee kumkatalia mimi kwenda kwenye mahojiano usiku ule. Yale maneno yalinichanganya na kunizidishia hasira.
"yaani mimi niwauwe wazazi wangu ambao walikuwa tegemeo langu, hicho ni kitu ambacho hakiwezekani"
Nilijikuta naongea kwa hasira na kwajazba bila kujua.
lakini yule Afande alisema.
"Msinifundishe kazi mtanisamee bure maana hii ni moja ya kazi yangu" Aliongea yule Afande na kunichukua.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilichukuliwa na kupanda kwenye gari lao ambalo walikuja nalo.
Tulipofika kituo cha polisi nilishangaa nilingizwa mahabusu na mlango ulifungwa na yule askari aliondoka, nikawa najiuliza maswali mengi.
"Hayo mahojiano ndio yanafanyika huku mahabusu?"
lakini sikupata jibu, nilikaa mahabusu mpaka asubuhi bila dalili ya askari kuja, nilianza kuona sasa hapa kuna mtu katengeneza hili jambo lakini sikuwa na huakika kamili, wakati nawaza niliona mlango unafunguliwa nilimuona yule askari aliye niingiza pale ndani, anaingia aliniamuru nimfuate nami nikawa namfuata kwa nyuma, nilimfuata yule afande mpaka ofini kwake.
Nilipoingia aliniambia niketi kwenye kiti ambacho kilikuwa kinaangaliana nae.
Aliniuliza maswali mengi juu ya kifo cha wazazi wangu, nilimweleza yote niliokuwa nayajua, wakati ananiuliza maswali kulikuwa kuna kamera ikiwa imewekwa kwa upande wa pili ikichukua mazungumzo tuliokuwa tunaongea na yule afande. Tuilipo maliza mahojiano yule afande alinyanyuka na kuzima ile kamera lakini chakushangaza
Yule afande kwa jina lake aliniambia anaitwa Afande Kazi Kazi au Ngumi Nyeusi. Alimuita afande moja alikuwa nje na kuja kwenye ofisi ya yule Afande ambae sisi tulikuwepo, akaambiwa.
"Mrudishe huyu kule kwenye makazi yake mapya alio yaanza jana"
Yule afande alitii na kuniambia nitangulie. lakini mimi sikuelewa yale maneno ya yule Afande
"Mpeleke kwenye makazi yake aliyo yaanza jana"
yale maneno kiukweli sikuyaelewa na kuamua kugeuka nyuma kumuuliza.
"Ni makazi gani ambayo nimeanza jana" Nili muuliza yule Afande, kwa kutaka kujua alikuwa anamaanisha nioni kusema maneno kama yale.
Yule Afande alicheka na kuniambia "Wewe unareta mchezo kwenye kazi za watu we kwani hujui jana umelala wapi, au unanipima akiri yangu, Embu peleka hilo lijambazi huko ndani"
"Yale maneno yalinifanya nishtuke na kutaka kujua nimefanya kitu gani kitu gani cha kialifu.
"Inamaana mimi nimefanya nini labda mpaka mnishikilie"
Niliuliza baada ya kuona yule afande anataka kunirudisha mahabusu.
"Maelezo yako hayajaridhisha polisi. kulingana na tukio lililo tokea.
"tembea" yalikuwa maneno ya yule afande alieambiwa anirudishe, kwenye makazi yangu ambayo nimeanza jana.
Nilipofika mlango ulifunguliwa na mimi niliingizwa. Nilikaa kule mahabusu siku mbili bila kuona mtu yeyote na kule mahabusu, hakuna hata mtu ambae alikuwa ananiletea chakula. Nilikuwa nimechoka mwili mpaka akili, kutokana na matatizo yalio nipata. Hata ndugu yangu sikuona hata moja wakati nawaza hayo nilisikia geti la mahabusu linafunguliwa, alikuwa yule afande alie kuwa amenileta aliniambia.
"Kuna ndugu zako wamekuja kuonana"
Alichukua pingu na kunifunga mikononi, nilitembe huku nikiwa napepesuka kwa njaa niliokuwa nayo. Nilipo fika nilimuona bibi yangu yuko na mdogo wangu Sophia, wakiwa wamesimama pembeni ya yule afande alienikamata siku ile ya tukio. Walipo niona mdogo wangu alikuja kunikumbatia huku akiwa analia. Kiukweli nilipata uchungu nilipokuwa namuona mdogo wangu analia.
"Kwanini kaka. kwanini kwanini?" mdogo wangu alikuwa analia hadi anashindwa hata kuongea, aliishia tu kusema kwanini kwanini.
"Kaka nikweli wewe ndiye umewauwa Baba na Mama ili upatekurithi mali" Kwakweli yale maneno ya mdogo wangu yalinifanya na mimi nianze kutokwa na machozi, maana nilikuwa najua sijafanya hivyo na nilianza kupata hofu, kwa kujua hapo nipo kwenye wakati mgumu.
Kwakweli yale maneno ya mdogo wangu Sophia yalinishtua sana, nilipo geuka upande wa pili nilimuona Bibi yangu akiwa analia. Nipomuona Bibi yangu analia, kiukweli nishindwa kuvumilia na mimi nilianza kulia.
Nilikuwa na uchungu wa kuuwawa kwa wazazi wangu, alafu leo hii naambiwa mimi ndiyo nimefanya hivyo. Kwa kweli nikuwa kama mtu alie changanyikiwa, lakini niliamua kumuachia Mungu, maana yeye ndiyo anaejua ukweli wa mambo yoto.
Kwa umri nilio kuwa nao na kesi ambayo ilikuwa inanikabili na kukaa jela ikuwa mateso makubwa. Yule afande aliwaambia Bibi yangu na mdogo wangu kipenzi, muda wa mimi kuongea nao ulikuwa umeisha, sikupata hata nafasi ya kuzungumza zaidi ya kiliotu kutawala. Nilichukuliwa na kupelekwa kulekule mahabusu kusubiri kwenda mahakamani kwa kosa nisilo lijua.
Nililala mahabusu mpaka asubuhi huku njaa nayo ikiendelea kunisumbua. Muda wa saa tano nilichukuliwa na kupelekwa kizimbani, kwa mara ya kwanza toka nizaliwe ndiyo nilikuwa nimeingia mahakamani. Watu walikuwa wengi, wengine nilikuwa nawafahamu na wengine walikuwa wageni machoni mwangu, lilikuwa ni jambo la kushangaza kwa umri niliokuwa nao kusimama kizimbani kwa kesi ya mauwaji.
"Kijana unatuhumiwa kwa kosa la mauaji ya wazazi wako wote wawili kwa kuwa kuwachoma vis....
"Hapana hakimu mimi sijafanya kitu kama hicho"
Nilijikuta naongea bila mpangili na kufanya watu wote wageukie upande wangu.
"Usije ukajaribu kutoa taarifa kwa polisi maana kabla ya mimi kwenda jela, wewe utatangulia jela"
Nilikumbuka baadhi ya maneno ambayo yalikuwa yameandikwa kwenye kile kijikaratasi na kunifanya niwe na hofu ya mimi kuuawa.
Nilitaka kutoa lile karatasi maana lilikuwa mfukoni lakini moyo ulisita, wakati huo Hakimu alikuwa ananiangalia kwa hasira kama mtu ambae nilikuwa na chuki nae, mpaka nikawa nashindwa kumuangalia na kuangalia chini, lakini wakati naangalia chini nilishangaa kusikia sauti kama nilikuwa naifahamu, ikanifanya ninyanyue uso wangu juu kuhakikisha kama nikweli au nimefananisha sauti.
Kiukweli sikuamini macho yangu yalipo tua kwenye uso wa Mjomba Denis, ambae kwa wakati huo alikuwa masomoni nchini Amerka. Nilijiuliza amekuja lini na mama alimpa kitu gani anipatie nilishangaa, kwenye lile karatasi lilikuwa kimeandikwa, mjomba faraj na mjomba Denis.
Mimi nilikuwa namfahamu mjomba Denis, lakin mjomba Faraj nilikuwa simfahamu, ila niliambiwa alikuwa ni Dokta.
Nilipo muona mjomba niliona kama Mungu kashusha mvua jangwani, maana niliona mjomba wangu ndio mkombozi wangu na kuona furaha inarejea tena..
Nilifurahi sana kwa kile kitendo cha kumuona mjomba wangu Denis, kwa kuwa nilijua lazima nitatoka tu kwa kuwa sijafanya kosa lolote ilikuwa nasingiziwa tu.Mjomba alianza kwa kutoa heshima hakimu na watu wengine. waliongea mengi na walibishana na baadae ikaonekana mimi sina kosa lolote ni watu walipanga niishie jela, lakini Mungu sio athumani kesi tulishinda na kilicho nifanya nishinde kesi ni kwasababu ya mjomba Denis.
Kusomea sheria na kuijua vizuri sheria, ndicho kitu kilicho tupa ushindi. lakini licha ya kushinda mimi bado nilikuwa na dukuduku moyoni mwangu, kuhusu kifo cha wazazi wangu na ni nani ambae alikuwa amefanya hayo yote na nikwasababu gani.
Tulipofika nyumbani, nikiwa na mjomba sebleni nilianza kumuuliza maswali, baada ya kuona hajaniuliza kitu chochote kuhusu kifo cha wazazi wangu.
"Mjomba?"
"Naam mjomba!
"Hivi unafikiria mimi na mdogo wangu Sophia tutaishi maisha gani mbeleni?" Nilimuuliza mjomba, maana nilianza kuona hali ya pale nyumbani, inaanza kubadilika.
"John unajua haya ni maisha. Ndiyo maana kuna kufa na kuzaliwa, ingekuwa tunazaliwa tu bila kufa sidhani kama tungekuwa tunasehemu hata za kuishi"
Aliongea mjomba Denisi na kunifanya nishindwe kuelewa alikuwa anamaanisha nini kusema. "Kuna kufa na kuzaliwa"
"Mjomba Denis ila kifo cha wazazi wangu Mungu hakupenda wafe kifo kama kile cha kikatili namna ile. Ila nakuambia na naapa kwa Mungu mjomba lazima nimuuwe huyu mtu alie wauwa wazazi wangu kwa mikono yangu mwenyewe"
Niliongea kwa hasira na machungu niliokuwa nayo.
"Usiseme hivyo John we mwachie Mungu yote"
"Kwangu hilo litakuwa ngumu kumsamehe, mtu ambae ni katili namna hii hata ukimuachia Mungu haisaidiiKwa"
Kwa umri nilio kuwa nao na maneno ambayo nilikuwa nayaongea yalikuwa kama vichekesho.
"Najua ni utoto unakusumbua, nenda kakoge maana bado unanuka harufu ya mahabus"
Aliongea Mjomba na kufanya kuangua kicheko.
Maongezi yalipo isha mimi nilienda kukoga, nikweli kama mjomba wangu alivyo sema nanuka harufu ya mahabusu, maana toka niende kule polisi nilikuwa sijawahi kukoga hata siku moja.
Niliamu kuingia bafuni ili kukoga, nilipo maliza kuoga nikaenda kubadilisha nguo maana hata nguo zilikuwa chafu sana.Wakati natoa vitu vyangu vya muhimu kwenye mfuko wa suruali yangu, niliona kile kikaratasi niliamua kumpelekea mjomba ili nione ananishauri nini, Nilimkuta mjomba yupo seblen, Nilimkabizi lile karatasi ambalo nililikuta kwenye tukio la kuuawa kwa wazazi wangu, lakini cha kushangaza. Nilishangaa kumuona mjomba anashituka kama mtu alie pigwana shoti baada ya kusoma lile karatasi...
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwakweli nilishangaa kwa kitendo cha mjomba wangu Denis kushtuka bada ya kumpa kile kikaratasi mawazo yalinijia kuwa huenda kashtuka kutokana na yale maneno ambayo yalikuwa yameandikwa kwenye kile kikaratasi wakati nawaza mjomba wangu aliniuliza "hikikikaratasi umekipata wapi na sehemu gani"
Aliuliza mjomba baada ya kusoma lile karatasi.
"Nilikipata wakati Baba na Mama wameuwawa na kukuta kikaratasi kipo mezani ndiyo nikaamua kukiweka mfukoni kwaajili ya ushaidi ila nilishindwa kukitoa mahakamani kutokana na maneno ambayo yameandikwa ndani ya hicho kikaratasi"
"Kwani mjomba kunanini mbona nilipo kupa hicho kikaratasi umeshtuka,.,
Ilinibidi kumuuliza mjomba maana alionekana kuwa na wasiwasi.
"Hamna kitu ila haya maneno yamenitisha sana"
"Lakini mjomba kama unajambo lolote niambie tu maana mimi na mdogo wangu tunakutegemea wewe.
Maongezi yalikuwa marefu ila mjomba angu kunakitu alikuwa anakijua ila hakutaka kutuambia.
Mazishi yalifanyika kila mtu aliekuwa anamfahamu Baba yangu pamoja na mama yangu walilia sana, mdogo wngu alikuwa mtu wa kuzimia kila wakati.
Kiukweli niliumia sana nilipowaangalia kwenye jeneza walilo wekwa walionekana kama wamelala tu, nilitamani kuwaamsha lakini sikuweza, nilibaki na kovu kubwa moyoni mwangu, nilijiona nimebaki yatima katika hii dunia, hadi mazishi yanaisha sikuwa naamini kama kweli wazazi wangu hawakuwa tena Duniani.
Siku zilienda hadi muda wakurudi shule ulifika nakumbuka siku hiyo inilikwenda kununua vitu vya shule kariakoo nikaingia kwenye duka ambalo walikuwa wanauza viatu na vitu vingine nilipo ingia nilichagua viatu na kutoka nilipo toka kama mita hamsini niliona ile Noh ikiwa imepaki na kutoka watu ambao walikuwa wa miraba minne.
Kiukweli wale watu walikuwa wamejazia ile mbaya walipo shuka walifungua mlango wanyuma akatoka mtu ambae sikuamini kama ni kweli au nilikuwa naota nilimuona baba mkubwa Derrick akiwa anashuka na kuingia kwenye lile duka ambalo nilitoka kununua viatu vya shule, nililiangalia lile gari vizuri na kwaumakini kutaka kutambua kama ni lile lilokuwa nyumbani siku ile wazazi wangu walipouwawa.
Mimi kwa wakati huo nilikuwa nimejificha kwenye ukuta wa duka la simu nilikaa kama nusu saa ndiyo nikaona Baba mkubwa anatoka na wale watu alio ingia nao wanatoka na mfuko mweusi wakaingia kwenye gari na kuondoka baada ya kuondoka nilipatwa na wasiwasi kwani ile Noh ndiyo ambayo siku ya vifo vya wazazi wangu vinatokea nilijikuta narudi kwenye lile duka ambalo nilinunua viatu.
Nilipo ingia sikuamini macho yangu kile ambacho nilikuwa nimekiona nilianza kujiuliza maswali mengi
"Inamaana nimekosea duka ama au yule nilie muona alikuwa siyo baba mkubwa, itakuwa niliona vibaya maana Baba mkubwa hawezi kuuwa mtu kwanza ni mtu wawatu na hawezi kufanya jambo kama hili"
Kiukweli wale watu walikuwa wameuawa kikatili mno alafu hakuna hata mtu mmoja ambae alikuwa ameona lile tukio zaidi yangu niliamua kutoka kimya kimya na kwenda kupanda daladala kwaajili ya kurudi nyumbani, maana nilihisi nikikutwa pale ningeweza kuambiwa mimi ndiye niliefanya vile.
Nilipo fika nyumbani nilishangaa kumkuta Baba mkubwa akiwa anaangalia tv na mdogo wangu sophia kile kitendo cha kumkuta baba mkubwa akiwa anaangalia tv na mdogo wangu nilibaki nimeduwaa tu,
Nilikuwa na maswali mengi "ni kwanini baba mkubwa hakuja kwenye mazishi ya wazazi wangu" lakini sikupata jibu "na amefika nyumbani saa ngapi mbona nilipoondoka hakuwepo nyumbani?"
Niliamua kuingia ndani kwangu na kuanza kupanga vitu vyangu kwaajili ya safari..
Nilipo maliza kupanga vitu vyangu nilitoka kwenda sebleni lakini nilikuta hakuna mtu lakini tv ilikuwa imewaka wakati naangalia tv niliona koti la Baba mkubwa lipo kwenye kochi, nipoangalia vizuri niliona kitu kama kinang'aa nilipata tamaa ya kutaka kujua kilikuwa ni kitu gani.
Niliangalia huku na kule kuangalia kama kuna mtu aliekuwepo, nilipoona hamna mtu nikasogelea lile koti na kuingiza mkono kwenye mfuko wa lile koti. kwakweli nicho kitoa sikuamini niliona kama nitoi la watoto na sio bastola ya ukweli, wakati nazidi kuangalia niliona kilekikaratasi ambacho nilimpa mjomba angu nilijiuliza kakipata aje wakati nilimpa mjomba Denis "sasa kapata aje" niliendelea kujiuliza maswali mengi na kusahau kuwa nilikuwa natakiwa kuangalia alafu niache lakini niliendelea kusachi wakati naangalia nilishtukia mlango wa sebleni unafunguliwa.
Niligeuka haraka na kutaka kujua ni nani aliekuwa ameingia. kumbe alikuwa mjomba Denis alipo nikuta nimeshika ile bastola alishtuka na kutaka kukimbia
"Wewe John umepata wapi hiy...... "Kabla hata ajamaliza kuongea mlango uligongwa nilichofanya ni kurudisha kila kitu kama vilivyo kuwa na kumwambia mjomba wangu afungue mlango.
Kwakweli isingekuwa mjomba Denis kusimama mlangoni nilikuwa nakutwa pale na Baba Mkubwa alipoingia cha kwanza aliangalia kwenye kochi ambalo alikuwa ameweka koti lake, alipoangalia niliona kama ameshtuka alichukua koti lake na kwenda chumbani kwake kwa wakati huo nilikuwa na maswali mengi hasa kuhusu kile kikaratasi kakipata aje mjomba kwa wakati huo alikuwa kama mtu alie pigwa na butwaa niliamua kumshitua
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mjomba? mjombaaaaa?"
"Naam"
"Mbona uko hivo unamwa au?"
"Hamna mimi niko sawa ila hivyo vitu vimenitisha sana nilivyo kuona umeshika vitu vile niliona kama ndiyo mwisho wa maisha yangu!!!!!
"Hahahahaaa mjomba mimi siwezi kufanya kitu kama hicho ila nataka nikuulize kitu....
"uliza tu john"
"Hivi mjomba wewe ndiyo ambae ulie mpatia baba mkubwa kile kikaratasi nilichokupa"
"Kikaratasi kipi tena john?"
"mjomba kweli msaulifu kile kikaratasi ambacho nilikipata kwenye tukio la kuuawa kwa wazazi wangu"
"hapana mimi sijampa mbona kipo ndani kumbe wakati tunaongea Baba mkubwa alikuwa amesimama kwenye mlango wa sebleni nilipomuona niliamua kukaa kimya huku mjomba wangu akiendelea kulalamika. alipo niona nimenyamaza ikabidi aniangalie, alipo niangalia aliniona naangalia mlangoni na yeye aliamua kugeuka nyuma kuangalia nilikuwa naangalia nini..
Alipo angalia mlangoni akakutana uso kwa uso na Baba mkubwa....
Alivyo geuka mjomba kuangalia mlangoni nilimuona kama mtu aliepigwa na butwaa
"Lakini mdogo wangu sophia yukwapi" nilijikuta nauliza swali bila kutarajia lakini licha ya kuuliza hakuna alie nijibu, wakati tunaendelea kutazamana nilisikia sauti ya mdogo wangu huku akiwa kama mtu ambae alikuwa anaomba msaada. nilitaka kunyanyuka niende nje ambako ndiyo sauti ilipokuwa inatokea lakini nilishangaa kuona mlango unafunguliwa.
Waliingia watu wanne wakiwa wamemshika mdogo wangu wakiwa wamemwekea bastola kichwani, mimi nilivyo ona hivyo niliona kama mchezo wa kuigiza, kwajinsi walivyokuwa wamemshikilia ilikuwa kama igizo flani, lakini nilimuona mjomba Denis ananyanyua mikono juu kama wanavyo fanyaga kwenye movie.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliendelea kuwashangaa wale watu ndipo kumbukumbu zikanijia tukio ambalo lilitokea kwenye duka nilioenda kununua viatu vya shule, nipowaangalia wale watu nikagundua kuwa wale ndio walie fanya tukio kwenye lile duka na kuuwa wale watu., Muda huo ulikuwa imesha fika saa mbili usiku ambapo Taarifa ya habari ilikuwa inatangazwa, kumbe kwenye lile duka walilo enda kuvamia kulikuwa na kamera (camera) ambayo ilichukua tukio zima hata wakati nilipo rudi napo nilichukuliwa wakati taarifa ya habari inaendelea nilishtukia tv imepigwa risasi na kupasuka.
Nilipo geuka na kuangalia ninani ambae alikuwa amepiga risasi tv nilikuta ni Baba mkubwa akiwa amesha vaanguo zake ambazo nilimuona alikuwa anafanyia matukio yake..
Kwakweli nilishangaa baba mkubwa amebadili nguo saa ngapi wakati alikuwa tulikuwa nae seblen sema yeye alikuwa amesimama mlangoni.
Wakati nawaza na kujiuliza maswali ambayo kwangu yalinichanganya nilishtushwa na mlio wa bunduki ambao ulikuwa kama baruti nilipo geuka nyuma kuangalia niliona mjomba Denis akiwa chini huku damu zikimtoka kwenye kifua chake kwakweli ile hali ilinichanganya sana, nilitoka mbio mpaka alipo kuwepo mjomba wangu ameangukia, kabla hata sijafika nilisikia sauti ya Baba mkubwa akisema "simama kabla sijamwaga ubongo wako na kunywa supu".
"Kwa vile mmeshajua siri hampaswi kuendelea kuishi ili siri iendelee kuwa siri itanibidi na nyinyi muelekee walipotangulia wenzenu. Lakini nyie sitawauwa kwa kutumia bastola nitawauwa kwa mikono yangu mwenyeme!!".
Alipomaliza kuongea nilishangaa anaweka bastola chini na kuanza kumfuata mdogo wangu sophia alipomkaribia alitoa kisu kidogo ile hali ilinitisha na kunifanya nipatwe na hofu na kujua mdogo wangu kipenzi sophia alikuwa anaenda kufa nilikimbia na kwenda kumvaa Baba mkubwa na kumwangusha chini, sikujui hata nguvu nilitoa wapi.
Kumbe tulivyo anguka niliangukia kile kisu kikanichoma kwenye mbavu nilisikia maumivu makali sana na huku damu zikinitoka ndipo nilipo muona Baba mkubwa ananyanyuka huku akiwa ana hasira sana, alipo nyanyuka alininyanyua na kuanza kunipiga ngumi za tumbo na kichwani alivyoona haitoshi alinibamiza ukutani na kuanza kuona nyota nyota mara nikaanza kupoteza nguvu na kuona kiza sikujua kilicho endelea.
Nilikuja kushituka nipo sehemu ambayo kwa
haraka haraka sikujua nipo wapi lakini nipotaka
kunyanyuka nilisikia maumivu makali sehemu
ya tumboni na kichwani, nilipoangalia vizuri
niliona nimepakwa vitu kichwani ambavyo
vilikuwa kama majivu. Nilianza kuwaza nipo
wapi lakini sikupata jibu.
Nilipo jaribu kuvuta kumbukumbu mara ya mwisho nilikuwa wapi lakini hakuna hata lepe ya kumbukumbu niliofanikiwa kukumbuka, wakati nawaza hayo mara nikamuona mdada ambae alionekana kuwa uchi, nilishtuka sana, nilipomuangalia vizuri ndipo nilipogundua alijifunika na majani sehemu zake muhimu katika mwili wake, alipo niona nimefumbua macho alipiga kelele kama mtu ambae kaona kitu cha kutisha hazikupita hata dakika tano watu kama hamsini walikuwa wamenizunguka lakini walikuwa wanaongea lugha ambayo mimi sikuielewa.
"Mzee mmoja wa makamo alinisogelea na kuniuliza unaitwa nani kwa lugha ya kiswahili
"Kwa wakati huo hata jina langu nilikuwa nimesahau. Walivyoona sijajibu walichuka uji ambao sikuelewa umetoka wapi na niuji waaina gani.
Wakati ananiwekea ule uji ulimwagika na kuniunguza kwenye mguu.
Nilishangaa yule Kijana aliye nimwagia uji nilishangaa ana pigwa mateke na ngumi walivyoona haitoshi walimbamiza kwenyemti ambapo alianza kutokwa na damu kichwani na kuanguka chini mzima mzima kama mzigo, nilishangaa sana kwa kile kitendo, kipigo alichokipata hakikufanana na kitu alicho kifanya. NIlibaki nawaangalia wale watu bila kupata jibu.
"Ili siri iendelee kuwa siri haina haja ya kuendelea kuishi"
Nilikumbuka baada ya kumuona yule Kijana alie nimwagia uji alivyo bamizwa kwenye mti na kuanguka kama mzigo.
"Sophiaaaaaa!!!!!!
Nilijikuta namuita mdogo wangu ambae kwa asilimia asilimia nyingi nilijua ni lazima atakuwa amekufa kwa maana baba mkubwa kama aliweza kumuuwa mdogo wake ambae kutoka yeye ndiyo anafuata baba yangu, nilishindwa kuyazuia machozi, nilijishangaa kwanii sikuweza kufa.
Nililia sana nilijuwa nitakuwa nimebaki mwenyewe katika hii Dunia.
Nililia na kutaka kujua nimefika aje apa wakati nawaza nilisikia mlio kama wa baruti ukisikika maeneo yale nikajua apa sasa Baba mkubwa alishajua kuwa bado nipo hai, maana mliouliosikika ni kama ule uliosikika wakati mjomba alivyo pigwa risasi na Baba mkubwa.
Ili sauti ilinifanya nipatwe na hofu sana maana nilitokea kumuogopa sana Baba mkubwa maana kila nilipokuwa nikikumbuka jinsi alivyo waua wazazi wangu kikatili bila hata huruma, ndivyo nilizidi kumuogopa, ukilinganisha na kipigo nilichokipata hadi kupoteza fahamu.
.Lakini wale watu walio kuwa wamesimama pale na yule mwingine akiwa amelala chini kama mtu ambae alikuwa amekufa.
Kitendo cha wale watu kusimama bila woga wowote kilinifanya nianze kuwaza huenda na hawa ni kundi moja na Baba mkubwa au wametumwa kuja kunimalizia. "lakini mbona watu wenyewe wamevaa kama wawindaji maana ile sauti ilikuwa niya bomu"
Wakati najiuliza na kujijibu mwenyewe nilishangaa yule Kijana alie kuwa kapigwa na wale wenzake ananyanyuka kwa kasi ya ajabu na kuanza kutembeza kipigo kwawale walie mpiga. Kipigo kilitembea kwa muda, ghafla wakatokea watu wengine na kuanza kumsaidia yule kijana, mwishowe yule kijana ambae sikufanikiwa hata kujua jina lake, akawa amewauwa wale watu walio mpiga kwa kunimwagia uji wa moto kwenye mguu.
Kile kitendo cha yule Kijana kuwauwa wale watu kiliniogopesha sana maana alipigwa kwaajili yangu. "sasa kama kawauwa marafiki zake je mimi nitapona kweli" hayo ni baadhi ya maswali ambayo nilikuwa nayo kichwani.
Wakati naendelea kuwaza nilishangaa yule Kijana anachukua rungu na kuanza kunifuata maali nilipo.
Kwakweli kile kitendo kilinifanya nipatwe na hofu na kujua leo ni siku yangu ya mwisho kuona jua maana yule Kijana alikuwa mkakamavu, mwili wake ulionekana kuwa na nguvu, alipo fika kwangu hata hakuongea alinyanyua rungu lake na kutaka kunipiga nalo kichwani, nilishangaa anaanguka chini kama mzigo.
Kile kitendo kilinishangaza sana mtu kuanguka bila kupigwa wakati nashangaa nilisikia sauti ya yule kijana alie taka kunipiga rungu akiongea kwa shida.
"Chukua hii itakusaidi kwenye safari ya kutoka kwenye huu msitu maana kuna wanyama wakali sana na mimi nilikuwa sina nia ya kukuuwa walio taka kukuuwa ni hao unao waona wamelala hapo chini"
Yale maneno yalinishangaza wakati nazidi kumshangaa yule jamaa niliona kisu kimeingia kwenye mbavu zake huku damu zikimtoka ndipo nilipo gundua kuwa alikuwa katika maumivu makali.
Nilipokea kile kikaratasi ambacho sikujua kilikuwa kina nini ndani au kimeandikwa nini wakati napokea kile kikaratasi yule Kijana ambae sikumjua kwa jina lakini yeye alinijua aliniambia niondoke maeneo yale maana sio salama kwangu.
Kwawema ambao alinifanyia yule kijana wa kuniokoa kwa wale watu ambao aliniambia kuwa walitaka kuniuwa yalinifanya nitokwe na machozi nikatamani nimsaidie lakini ilikuwa ngumu kutokana na mimi mwenyewe kuwa na maumivu makali ya kichwa na tumbo.
Wakati nawaza yule kijana aligeuza shingo na kuangalia juu na kukaa kimya nilinyanyuka bila kumgusa maana kumgusa kungeniletea matatizo kwa polisi nilinyanyuka na kuanza safari ambayo sikujua mwisho wake ni wapi.
Niliondoka pale nikiwa na maumivu makali sehemu za kichwani na tumboni, nilitembea huku na kule bila kuona mtu yeyote wala nyumba kile kitendo kilinifanya kuchoka hadi akili maana nilikuwa nimetembea umbali mrefu bila mafanikio yoyote, huku njaa nayo ikazidi kuniandama, ukichukulia toka hasubuhi sikuwa nimekula kitu kitu chochote kila.
Njia ambayo nilikuwa napita kulikuwa hakuna hata matunda na miti ile ambayo nilikuwa naiona ilikuwa ni migeni machoni mwangu, niliendelea kutembea huku nikijivuta lakini nilishindwa kuendelea mbele kutokana na njaa niliokuwa nayo, nikaamua kutafuta mti angalau nitulie pale pengine nguvu zitarejea, nilikaa chini ya mti mkubwa ambao ulikuwa kama mti wa mbuyu lakini haukuwa mbuyu.
Nilikaa pale huku njaa ikiendelea kunitesa na kiu nacho kilichukua nafasi nilikaa pale mpaka usiku bila kupata msaada wowote nikakata tamaa ya kuishi na kuona nakufa kifo cha kizembe kama kile, sikupenda kufa kabla sijalipa kisasi kwa baba mkubwa na kutaka kumuona mdogo wangu kipenzi sophia.
Nilijaribu kunyanyuka lakini ilishindikana nilihisi kizungu zungu na kuona kiza kinazidi machoni kwangu ghafla nilimuona mtu ambae sikujua alikuwa mwanaume au mwanamke baada ya kumuona yule mtu nilishangaa kiza kikaongezeka na sikujua kilicho endelea.
Nilipo kuja kushituka nilijikuta nipo kwenye kanyumba cha nyasi kipo kama tembe lakini haikuwa tembe, nilinyanyua kichwa lakini nilishindwa nilipo angalia vizuri niligundua nilikuwa nimefungwa kamba kwenye miguu na mikononi huku usoni nikiwa na vitu kama Sindano vilivyo ingia kwenye mashavu yangu nilijaribu kugeuka angalau upande mmoja niangalie niko wapi maana nilikuwa nimelazwa kwa kuelekea juu.
likuwa ngumu sana kuona pembeni zaidi ya kuangalia juu nilikaa pale kama nusu saa ndiyo nikasikia sauti za watu wakiimba nyimbo ambazo nilikuwa sizielewi hata lugha ambayo walikuwa wanatumia siku ifahamu maana haikuwa kiswahili wala kingereza zile sauti nilianza kuzisika kwa karibu na kujua kuwa walikuwa wanakuja kwangu.
Walipofika karibu na mimi kuna mmoja alikuja na kuanza kutoa zile sindano na kufungua zile kamba ambazo nilikuwa nimefungwa na kuninyanyua nilipo nyanyuka nilishangaa sana kuona watu wafupi alafu walikuwa wengi sana huku kila moja akiwa na ngoma yake mkononi nipo geuka upande wa pili nilishangaa na kutaka kupoteza fahamu baada ya kuona simba wengi wakiwa wapo nyuma ya mtu, ambae nilikuwa nakumbuka kama nilisha wahi kumuona lakini kumbukumbu zangu hazikupata jibu kamili.
Kile kitendo kiliniogopesha sana maana katika maisha yangu nilikuwa najua kuwa simba ni moja ya wanyama ambao ni hatari sana, kile kitendo kiliniogopesha sana kuanza kujiuliza nipo wapi, na nimefika aje apa, lakini sikuwa na kumbukumbu. Kitu ambacho kilinishangaza ni pale walipokuwa wanaongea lugha ambayo sikuielewa hata kidogo.
Walikuwa wananiongelesha lakini hakuna hata neno moja ambalo nilikuwa nalijua walivyoona sijibu walichukua maji na kuyaweka kwenye kitu kama ndoo na kuchanganya na majani ambayo siku yafahamu na kunimwagia baada ya kunimwagia wali sogea pembeni, mimi kwa wakati huo sikujua nini kinaendelea na nikwanini wamenimwagia yale maji wakati nawaza nilishtukia mwili wangu unajaa kama puto kuanzia kichwani mpaka miguuni kile kitendo kiliniogopesha sana.
Kiukweli nilishangaa sana na kuogopa maana hazikupita hata dakika tano nilikuwa nimejaa mwili mzima kama puto, kile kitendo kilinifanya nigundue kuwa wale watu sio wazuri kwangu wakati nawaza. nifanyaje kumbukumbu zilinijia kuwa nilipewa kikaratasi ambacho niliambiwa kitanisaidia kutoka ndani ya ule msitu. Lakini nisinge weza kutoroka kwa wale watu maana walikuwa wengi mno, kitu kingine kilicho nitia hofu kubwa ni wale simba ambao walikuwa wakubwa alafu nawenyewe walikuwa wengi na mimi sikuwa naelewa lugha ambayo walikuwa wanatumia hata mahali nilipo kuwa sikuwa napafahamu na hapo ndipo nilipo gundua kifo changu kimefika.
Wakati nipo pale huku nikizidi kuwa mkubwa nilishangaa simba moja ameachiwa na kuja kunirukia kabla hajanirukia nilisikia sauti kama ya baruti ikilia na kuona yule simba anaangukia pembeni yangu huku akitokwa na damu kichwani, nilitaka kugeuka kuangalia ninani ambae amenionea huruma na kuniokoa kwenye mdomo wa simba, lakini nilishindwa kugeuka kutokana na mimi kujaa miguu ilikuwa mizito sikujua ni dawa gani ambayo inaweza kumfanya mtu kuwa vile. "au niuchawi?" nilijiuliza maswali mengi bila kupata majibu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati nawaza na kujiuliza maswali yasiyo na majibu nilishangaa yule jamaa ambae alikuwa mrefu ambae aliachia simba kuja kuning'ata ananyanyuka na mkuki kuja kwangu, nilimwangalia nikiwa nasali sala zangu za mwisho, nil;ifahamu fika ule ndio ulikuwa mwisho wangu, lakini kabla hajafika nilisikia sauti kutoka nyuma yake nilipo angalia vizuri nilimuona yule kijana alie nipa kile kikaratasi akiwa kakaa kwenye kile kiti alicho kuwa amekaa yule mtu mrefu ambae sikumjua kwa jina.
Alipo geuka kuangalia kule alipo toka alishtuka sana kama mtu alishtushwa na kitu cha ajabu na kupiga magoti. Kiukweli nilishangaa maana yule Mtu yeye ndiyo aliekuwa kiongozi na yeye ndiye alie amuru mimi nimwagiwe maji yenye dawa mpaka nikavimba mwili mzima, "alafu leo anampigia magoti mtu ambae yupo kama mimi na wala hafanani na jamii yao" kile kitendo kilizidi kunishangaza lakini kwa upande wa pili wa moyo wangu nilipata furaha kidogo na kujua sitakufa tena maana yule alikuwa ananifahamu ila kumbukumbu zilinijia kuwa yule aliniokoa na alichomwa kisu cha mbavu na siku niliyo muacha alikuwa ana hali mbaya ya mauti uti na sidhani kama angepona na apa kafika aje.
Kile kitendo kilinifanya nijiulize maswali mengi maana yule Kijana hakuwa na asili ya wale watu na hata lugha alikuwa anatumia yule kijana alieniokoa ilikuwa tofauti na wale watu, ambao sikujua ni watu wa wapi lakini cha kushangaza kundi la wale watu wote niliona wananyanyuka na ngoma zao na kuanza kuja mahali nilipo kuwa walipo fika walianza kuimba lugha ambayo sikuifahamu huku wakipiga ngoma zao wakati wakipiga zile ngoma nilianza kuhisi mabadiliko ndani ya mwili wangu, na hata sehemu nilizo kuwa nifutuka kama puto nako palianza kupungua walipo kuwa wanapiga ngoma zao na kuimba ni kama mtu alikuwa anapunguza upepo kwenye mpira ulio jaa.
Nikiwa pale huku hali yangu ikiwa inarejea niliona wale simba walio kuwa nyuma ya kile kiti ambacho alikuwa amekaa yule kijana alieniokoa wanaanza kunguruma, kile kitendo kiliniogopesha maana sauti ilio kuwa inatoka mpaka ardhi ilikuwa ina vabret lakini wenyewe walikuwa hawaogopi na walivyo ona hivyo ndiyo kwanza walianza kupiga ngoma na kurukaruka.
Kiukweli ile hofu nilio kuwa nayo ilinifanya hadi mapigo ya moyo wangu kwenda mbio lakini nilijipa moyo kwa kuwa yule kaka alikuwa ananifahaamu. Waliendelea kupiga ngoma zao mpaka ikafika usiku huku na mimi nilipoona hamna dalili yoyote ya kupewa chakula niliamua kumwambia yule kaka kuwa sijala toka asubuhi
Lakini cha kushangaza yule kaka baada ya kumuambia kuwa njaa inaniuma alinitandika kibao na kuniambia. "tulia kwanza unapenda kula sana wakati hujui apa utatoka vipi, na wewe ndiyo umesababisha mpaka tupo hapa maana nilikupa kile kikaratasi kwaajili ya ramani ya huu msitu maana mimi nina matatizo ya macho na karatasi lenyewe lilikuwa dogo na nisinge weza kuona sasa wewe umenifanya hadi nije nirudi huku kuja kukuokoa".
Kiukweli nilitokea kupigwa na butwaa maana maneno aliokuwa anayaongea yalinichanganya sana lakini kwa upande mwingine yalinikumbusha kuhusu karatasi nililo pewa bila kuchelewa nilingiza mkono mfukoni na kukutana na lile likaratasi lakini niliamua kukaa kimya maana nilijua endapo ninge mpatia lile karatasi angeweza kuniacha..
Lakini nilishindwa kuvumilia maana njaa ilikuwa kali sana na ilikuwa ngumu kuvumilia na kuanza kuzunguka zunguka huku na kule kujaribu kutafuta angalau hata matundaa, lakini ilikuwa ngumu kuona matunda na kuona mti wa matunda kutokana na kiza kilichokuwepo ile hali iliendelea hadi asubuhi nilipo shtuka asubuhi niliona nyama zikichomwa kutokana na njaa nilio kuwa nayo nilizirukia zikiwa kwenye moto na kuanza kunyofoa haraka haraka bila kujali moto...
Wakati nikiwa nakula zile nyama nilishtukia kitu kizito kinatua juu ya kichwa changu na kunifanya kukosa nguvu na kupata maumivu makali yalio pelekea kupoteza fahamu.Nilipo kuja kushtuka nilijikuta nimefungwa kamba huku nikiwa kichwa chini miguu juu nilipo shituka sikuona mtu yoyote pale ambapo nilikuwa nimefungwa na sikujua nilikuwa wapa, nilipo angalia vizuri niliona damu zikiwa zinatiririka kama maji kile kitendo kilinishangaza sana maana damu zilikuwa nyingi sana, mpaka nikaanzakupata hofu maana sio kitu cha kawaida damu nyingi kiasi kile kutiririka.
Nikiwa palehuku nikiwa nawaza zile damu zilikuwa zinatoka wapi nilishtukia kamba za miguuni zinafunguliwa.Nilitaka kupiga kelele maana nilijua huenda na mimi muda wa kuchinjwa umefika maana nilipo ona zile damu nilipata hofu kubwa, ndiyo maana hata yule mtu alie kuja kukata zile kamba nilipiga kelele lakini alinizuia kwa mikono yake na kufanya sauti isitoke.
Kile kitendo kilinifanya nimkanyage teke la tumbo na kuanguka chini. Alivyo anguka chini kumbe alikuwa yule Kijana ambae aliniokoa kutoka kwenye mikono ya wale majambazi wa baba mkubwa, nilipo muona yule kijana nilibaki nashangaa maana alikuwa kama msukule alikuwa kachafuka kama mtu alie changanyikiwa, wakati namshangaa alinishika mkono na kunivuta pembeni na kuniambia.
"mimi naitwa Gerad wewe huna haja ya kujitambulisha maana nakufahamu vizuri ila kwa sasa fanya jambo moja ondoka maeneo haya maana hawa watu sio wazuri na kama unavyoona damu zinatiririka hizi damu ni za binadamu wenzako na hawa wanachinja bila huruma na kile kikaratasi nilicho kupa kina vitu vingi sana kuhusu huu msitu na hicho kikaratasi ndicho kilicho nipa mbinu na nguvu za kukaa kwenye huu msitu.
Ila nakuomba ondoka maeneo haya maana utauawa na mimi sipo tayari wewe mwenzangu upoteze maisha na kuna vitu vingi nahitaji kutoka kwako. Kiukweli nilitokea kuchanganyikiwana kushangaa maana yule jamaa alie jitambulisha kwa jina la Gerad sikuwahi kumuona katika maisha yangu alafu leo ananiambia ananifahaamu kingine ambacho nilitaka kujua kutoka kwake kuhusu maali ambapo tulikuwa tupo.
"Kaka Gerad tupo wapi hapa?"
"Hapa tupo Nigeria, ila kwa sasa sio wakati wa maswali cha muhimu ondoka maeneo haya siku tukikutana nitakujibu maswali yako yote ambayo unataka kuniuliza. Ila kwa sasa ondoka hapa kunusuru maisha yako.
Sikutaka kubisha kwa maana mimi mwenyewe niliziona zile damu zilizo kuwa zinatiririka pale chini. Nilimuaga na kuanzasafari mpya ambayo sikujua mwisho wake ni wapi maana nilisha jua nipo wapi na sijui baba mkubwa alitumia nini kunitoa Tanzania mpaka Nigeria na hakuna nchi ambayo nilikuwa naiogopa kama Nigeria kutokana kwa kusifika kwa uchawi na mimi "hakuna kitu ambacho nilikuwa sikipendi kama ushirikina"
Niliondoka pale nikiwa na maswali ambayo yalikuwa hayana majibu.nilitembea takribani saa nane huku nikiwa nimechoka na njaa ikiwa imeniandama huku kiza kikiwa kimeanza kuandama anga, niliamua kutafuta mti ili nipande kwaajili ya kupumzika, maana nilihisi chini ningeweza kutafunwa na wanyama wakali. Nilikaa kwenye mti mmoja na kuanza kusubiri pakuche, ili kuendelea na safari, nilikaa pale mpaka kiza kilipo anza kuacha anga ndiyo na mimi nilipo shuka kwenye ule mti.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipo shuka niliendelea na safari yangu wakati nikiwa natembea nilisikia sauti ya jogoo kuwika ile sauti ilinishangaza sana maana pale palikuwa porini.
"sasa huyu kuku anae wika yuko wapi?"
Nilijiuliza huku nikiwa najaribu kusikiliza vizuri ile sauti, niliamua kuifuata ile sauti na kuhisi bila shaka kulikuwa na watu maeneo yale, maana kuku huwa hawakai porini nilitembea umbali wa kama nusu kilometa ndiyo nikaona moto ulio kuwa umewashwa pembeni ya mti mmoja mkubwa
Nilipo ona ule moto nikashtuka maana nilijua huenda wale watu ambao walitaka kuniuwa nika wakimbia ndiyo wako maeneo haya, nilijibanza pembeni ya mti ilikuangalia kama nikweli wale watu wapo maeneo haya.
Wakati nikiwa pale pembeni ya mti nilisikia sauti kama mtu alikuwa anakuja kutoka nyuma yangu, niligeuka haraka nilipo geuka nilishtuka na kutaka kukimbia baada ya kugongana uso kwa uso na Bibi kizee ambae alikuwa kajifunga kitambaa chekundu na cheusi.
Nilipo muona yule bibi nilikimbia kwa kasi ya ajabu lakini nikiwa nakimbia nilisikia yule bibi akiniita jina langu, kile kitendo kilizidi kunishangaza.
"uyu bibi kajua aje jina langu au ni mchawi?" Nilijiuliza huku nikiwa naongeza mwendo wa kukimbia.
"John usiniogope mimi siyo mtu mbaya kwako na huko unapo kwenda siko, njoo nikusaidie mjukuu wangu"
Yale maneno yalinifanya nisimame na kuacha kuendelea kuendelea kukimbia na kuanza kwenda kwa yule bibi ambae nilijua anaweza kunisaidia ila swali ambalonilikuwa najiuliza kuhusu jina langu amelifahamia wapi.
Nilijiuliza maswali mengi huku nikielekea mahali ambapo alikuwa amesimama yule bibi nilipo mfikia alinirukia na kunikumbatia huku akiwa analia. nilipo muona yule bibi akiwa analia nilizidi kushangaa na kutaka kujua nini kilikuwa kina mliza.
Alinichukua na kunipeleka ndani ya kijumba cha udongo ambacho kilikuwa kama kichuguu, nilikuwa namuogopa nikihisi si mtu mzuri kwangu nilipo ingia kule ndani nilishangaa sana.
maana kule ndani ya kile kijumba nilikuta taaza umeme zikiwa zimewaka huku pembeni kukiwa kuna redio pamoja na TV, nilishangaa sana maana pale kulikuwa porini sasa "huu umeme umetoka wapi?huku porini"hayo ni baadhi ya maswali ambayo nilikuwa najiuliza bila kupata majibu, yule bibi aliniletea chakula ambacho nilikula haraka haraka kutokana na njaa nilio kuwa nayo, nilijipa moyo na kuhisi Bibi huyo pengine hakuwa mtu mbaya.
Nilikula kile chakula huku nikijisemea kimoyo moyo niwe salama, nilipo maliza kula nilimshukuru kwa chakula alicho nipa.Baada ya kumaliza kula nilianza kumuuliza maswali na swali la kwanza ni kutaka kujua yeye ninani na kajua aje jina langu.
"John mimi ni bibi, yako huyo Frank ambaye ni Baba yako mimi ni mama yake, hata huyo mwanaharamu mshenzi asie kuwa na huruma na utu hata kwa mzazi wake, Derrick nae nimwanangu ila ni Baba yako na baba mkubwa wako baba ni tofauti na huyo Baba mkubwa ako na yeye ndiyo ambae alinitupa kwenye huu msitu ila yote nimemwachia Mungu kwa maana mungu ndiyo muweza wa yote, Mtoto niliemlea na kumuweka tumboni kwa taakribani miezi tisa, leo hii ananifanyia unyama kama huu"
Aliongea Bibi huyo huku machozi yakiwa yanamtoka, nilimuonea huruma kwa jinsi alivyokuwa anaongea kwa uchungu
na wewe mbona huko hapa kulikoni?Yule bibi alinijibu swali langu la kwanza kuwa yeye ninani na baada ya kunijibu tulijikuta kunatokwa na machozi ""inamaana huyu ni bibi yangu?"
Hapo ndipo nilianza kugundua kuwa baba mkubwa sio mtu mzuri kama ameweza kumfanyia hivi mama yake mzazi kwanzia hapo nilitokea kumchukia baba mkubwa na niliahidi siku nikikutana nae ama zangu ama zake lazima nimuuwe kwa mikono yangu mwenyewe."Mjuku wangu wazazi wako wanaendelea aje na wewe umemfanyaje baba mkubwa ako mpaka kukutupa mahala hapa?""yale maswali alio niuliza bibi yangu yalikuwa kama mwiba moyoni mwangu maana nikikumbuka mama na baba walivyo uawa kikatili nilishindwa nimjibu nini bibi yangu nikabaki tu nalia""
"mjukuu wangu kuna nini mbona nakuuliza unaanza kulia?""au baba mkubwa wako kawauwa niambie tu mjukuu wangu""kweli bibi baba pamoja na mama wameuawa na baba mkubwa na hata mimi pamoja na mdogo wangu tulitakiwa kuuawa ila namshukuru mungu maana mungu bado anamakusudi na mimi ndiyo maana sijafa nipo hai""Ila mdogo wangu sophia yeye ndiyo sijui alikufa au yupo hai ila mimi siamini kama mdogo wangu amekufa ila mtu ambae sinahuakika kama alipona ni mjomba Denis maana yeye alipigwa risasi kifuani nilishindwa kuendelea kuongea nikabaki nalia kwa uchungu.
Bibi alinibembeleza lakini haikusaidia aliniacha na kwenda chumba kingine ambacho nilipo kuja sikukiona kiukweli ile nyumba ilikuwa nyumba ya aina yake yaani nyumba ipo porini lakini inaumeme alafu ukiitazama kwa nje unaweza kusemawanakaa vicheche maana palikuwa kama kichuguu hata mimi nilishindwa kuielewa ile nyumba nilijiuliza maswali mengi ambayo sikuyapatia majibu nilipoona sielewi niliamua kumuita bibi ili nimuulize niliita lakini sikuitikiwa nikaamua kurudi kwenye kochi na kuendelea kumsubiri bibi wakati nikiwa pale kwenye kochi nilikumbuka lile karatasi ambalo nilikuwa nimepewa
Bila kuchelewa niliingiza mkono mfukoni ili kuangalia lile karatasi nilipo litoa nililifungua kutaka kujua nini ambacho kilikuwa kipo kwenye lile karatasi nilipo fungua nilishangaa sana maana lile karatasi lilikuwa limechorwa ramani ambayo nilijua itakuwa ni ramani ya lile pori kutokana na ramani za miti kuonekana kwenye lile karatasi nilipo liangalia lile karatasi lilikuwa tofauti na makarata mengine yaani ilikuwa kama inaonekana mara mbili mbili kitu kilicho pelekea nisiielewe ile ramani ilio kuwa imechorwa kinamna gani maana ilikuwa haieleweki.
Niliamua kwenda kumuita bibi kwa kujua bibi atakuwa anafahamu bibi alipo kuja na kumuonesha alishangaa sana na kuanza kuruka ruka huku akicheza cheza kwa furaha.
"Mjukuu wangu asante sana na hongera maana uhakika wa kutoka kwenye huu msitu tukiwa salama upo asilimia tisini na tisa maana hili karatasi alikuwa nalo baba yako kipindi tumetupwa humu mstunitulikutana na bibi mmoja ambae alikuwa amezeeka sana na yeye ndiyo alikuwa anaishi hapa kwenye hii nyumba ambayo tunakaa hadi sasa""http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo bibi yangu alikuwa anaongea huku akitokwa machozi ya furaha
"john mjukuu wangu huu msitu wanaishi viumbe wa aina mbali mbali wakiwemo wale vimbilikimo wanao kula watu hata babu yako nae walimchukua na kumuuwa, ila mimi siwezi kuwalaumu wao me lawama zangu zituwe kwa derrick maana yeye ndiyo aliofanya hadi sisi tunateseka hadi leo
""Bibi kwani hilo karatasi limechorwa kitu gani maana mimi silielewi" Nilimuuliza bibi baada ya kuona anafurahiya lile karatasi.
"Unajua mjukuu wangu hili karatasi ndiyo "direction" ya hili pori, maana hili pori ni kubwa sana, hata baba mkubwa ako huwa anawatuma watu waje wawatupe huku, lakini yeye hawezi kuja huku kutokana na historia ya hili pori kuwa ukiingia huwezi kutoka.
Hata watu alio kuwa anawatuma alijua hawawezi kurudi. Alinijibu bibi huku akiwa anapepesa macho kwenye lile karatasi.
"Kitu kingine ambacho nataka kujua kutokakwako ni kuhusu hii nyumba? Niliamua kumuuliza swali ambalo kila nikifikiria nilikuwa silipatii jibu.
""Nyumba imefanyaje tena!?"
"Kama unavyo jua hapa ni porini naona umeme unao waka na sijajua unatoka wapi?'
"kama nilivyo kuambia mwanzo kuwa hii nyumba tulipewa tu mimi mwenyewe nimekaa hapa takribani miaka kumi na moja na sijawai kupata jibu ila hii nyumba inasadikika ilikuwa ni ya magaidi ambao walikuwa wanajificha wakati wa vita hata hilo karatasi tulilikuta humu ndani ila walivyo mkamata babu yako ndiyo na hili karatasi ikapotea ila namshukuru mungu atimae limerudi mikononi mwangu.
yale majibu ya bibi yangu yalizidi kunishangaza, nilikosa swali la kumuuliza tena nikabaki nimekaa kimya, alivyoona kipo kimya aliamua kuingia ndani.Baada ya dakika kama tatu nilimuona bibi akiwa anatoka chumbani kwake akiwa na mifuko miwili, ambayo bila shaka ndani ya hiyo mifuko kulikuamo na vitu kutokana nauonekano wake.Alinikabidhi mfuko mmoja kati ya ile mifuko aliokuwa nayo.
"Bibi huu mfuko ni wanini?' nilimuuliza bibi huku nikipokea ule mfuko.
"Mjukuu wangu hapa hatuna muda wa kupoteza, safari ya kutoka kwenye huu msitu ndiyo imeanza"alinijibu bibi huku akiwa anaelekea nje ya ile nyumba.
Kwa wakati huo sikuwa najua nini kilikuwa kinaendelea.Ilinibidi nimfuate nyuma maana yeye ndiye alie kuwa anajua vitu vingi kuliko mimi, hata hivyo mimi mwenyewe nilikuwana hamu ya kutoka kwenye ule msitu nikiwa salama ili nikalipize kisasi kwa babamkubwa, maana nikikumbuka jinsi alivyo itesa familia yetu licha ya kuitesa na kuamua kuwauwa kabisa ndicho kitu ambacho kilikuwa kinaniumiza na kunitia hasira na kutaka kulipiza kisasi.
tuliondoka pale kwenye ile nyumba tukiwa na lile karatasi ambalo lilikuwa limechorwaramani ya lile pori, kutokana na bibi yangu kuwa mzee ilitubidi kutembea polepole.wakati tukiwa tunatembea bibi alikuwa analalama kuwa amechoka kitendo kilicho tulazimu kupumzika kila wakati, tuliendelea na safari hadi pale anga lilipo badilika na kuwa kiza.
ndipo tulipo amua kutafuta mti mkubwa na kwenda kuwasha moto pembeni ya ule mti kwaajili ya kusubiri Kiza kuachia nafasi ili Nuru itawaleanga.tulipumzika pale kwenye ule mti mpaka pale tulipo ona nuru ikiwa imesha chukua nafasi yake, tulitembea takribani masaa matano tukiwa tunafuata maelezo ya lile karatasi, tulipofika mbele kidogo nilimuonabibi yangu akiwa anaanguka chini mzima mzima, ile ilitokana na kutembea kwa muda mrefu bila kupumzika.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilinilazimu nimchukue bibi yangu nimlaze chini ya mti mkubwa na kuanza kumpepea,nilitoa chakula ambacho kilikuwa kwenye ile mifuko ambayo tulikuwa tumeibeba na kumpatia bibi yangu, bibi alipo maliza kula aliniambia anahisi kiu."Sasa bibi maji mimi nitayatoa wapi?
nilimuuliza bibi baada ya kuniambia kuwa anahitaji maji ya kunywa.
tuliondoka pale
"John mjuku wangu hapa nilipo ninahisi kiu sana.
Aliniambia bibi huku akiwa amekaa pale chini ya mti.
"Lakini bibi kwanini tusitembee wote pengine huko mbele tutakutana na maji maana mimi huku sijui chochote na hata hayo maji sijui yanapatikana wapi?'
nilimwambia bibi maana kumuacha pale nisinge weza kutokana na lile pori kuwa nawanyama wakali pamoja na viumbe wengine ambao wanaweza kumdhuru."Siwezi mjukuu wangu wewe nenda utanikuta hapa hapa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment