Search This Blog

Friday, October 28, 2022

MSHUMAA - 2

 

     





    Simulizi : Mshumaa

    Sehemu Ya Pili (2)





    “Kwahiyo kuanzia sasa wewe ndio utakuwa ni msimamizi wa hizo mali?”



    “Yeah! Hadi pale Shery atakapo maliza elimu yake” Frank alijibu.



    “Mi nakushauri tumchukue Shery tuishi nae pia”



    “Siwezi nikamchukua bila mwenyewe kutaka. Ni lazima kwanza atoe maamuzi yeye”



    “Sawa..” Akatulia na kuangalia chini. Baada ya sekunde kadhaa. Akainua kichwa na kumuangalia Frank“Mume wangu kesho ninataka kwenda kumtembelea Shangazi yangu Msambweni. Kwahiyo nilikuwa naomba ruhusa yako”



    “Unaenda saa ngapi na utarudi saa ngapi?” Akauliza Frank.



    “Asubuhi na nitarudi mchana” Akajibu na Frank akakubali. Tabasamu likajiunda kwenye uso wa Rebeka. Wakaendelea kula.



    * *



    Siku iliyofuata majira ya saa tatu asubuhi. Rebeka ilimkuta maeneo ya Msambweni. Huko alikutana na mtu aliedai kuwa ni shangazi yake.



    “Mwenzangu wee! Nimesikia taarifa ya vifo vyao” aliongea mwanamke huyo.



    “Basi ndio hivyo na hapa nimekuja unipeleke kule kwa yule mtaalamu nataka nimtengeneze na mume wangu afanye vile nitakavyo” Rebeka aliongea.



    “Basi subiri nijiandee haraka”

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya dakika ishirini. Walikuwa ndani ya Bajaji wakielekea huko walipopanga kwenda. Iliwachukua dakika Arobaini na tano wakawa wamefika maeneo ya Machui. Wakamuambia dereva bajaji awasubiri pahali na wao wakaondoka hapo kuelekea wanapo pajua wao. Walikatisha njia hii na kutokea njia ile na mwisho wa safari yao ikaishia kwenye kijumba cha udongo kilichoonekana kuelemea upande mmoja. Wabisha hodi mlangoni na wakapokelewa na sauti ya chafya. Wakavua viatu na kuzama ndani.

    Bilashaka walikuwa wenyeji hapo.



    Huko walimkuta mzee akiwa amejifunga tambara jekundu kichwani akiwa kifua wazi huku katikati ya kifua hicho pakiwa na tambara jeupe lililopita begani hadi kiunoni na kupita kwa nyuma ya mgongo. Chini akiwa amevaa kaniki nyeusi. Na shingoni akiwa amejivisha mahirizi mengi. Chumba hicho lilikuwa kikinuka harufu ya madawa ya hovyo hovyo iliyochagizwa na udi. Mzee yule akawaambia kwa ishara wakae kwenye msalwa. Yule mwanamke aliekuja na Rebeka. Akakaa kushoto huku Rebeka akikaa kulia kwa yule mzee. Chafya nyengine tatu zikasikika kutoka kwa yule mzee na akawambia waeleze shida zao.



    “Kwanza nikushukuru babu kwa zile dawa zako. Zimefanya kazi..” Yule mzee akatabasamu huku akitingisha kichwa.



    “Ila leo nimekuja na jengine. Nataka nimfanye mume wangu asiongee kitu juu yangu. Yani kila nisemalo asilipinge” Akaeleza shida yake Rebeka.



    “Mmefika. Umefika kwa mtaalamu wa mambo hayo Kilunge wa Kilungeni. Zoezi lako dogo sana kama punje ya unga wa ngano. Muhimu tu nikutimiza masharti. Baasiii” Hilo neno la mwisho alilitoa kwa sauti kubwa mpaka wanawake wale wakashtuka. Wakakaa vizuri huku wakiangaliana usoni hofu ikionekana kwa mbali. “Je uko tayari kutimiza masharti?” Akamalizia. Rebeka akaitikia kwa kichwa kukubali. Yule mzee akachekelea huku akitingisha kichwa. Mara ghafla alitulia kimya na kule kucheka kukimuondoka na hivi sasa alikuwa kauzu kama vijana wa mtaani wasemavyo. Akaangalia huku na huko huku akiupunga usinga wake pande zote nne za dunia. Macho yake akayakaza kwa Rebeka.



    “Kumbuka. Umeshaingia kwenye kiapo cha wakubwa. Ukishindwa kutimiza masharti lazima udhurike kama sio kufa basi utageuzwa Fungo na sijui utaishi wapi.. Je uko tayari nikupatie masharti?” Yule mzee aliongea. Rebeka alikuwa akitetemeka si mchezo. Akamuangalia rafiki yake na kumuona rafiki yake akimtaka kukubali. Rebeka akaitikia kwa kichwa kuwa amekubali. Ila alishtuliwa na sauti kali ya yule mzee iliyomtaka aitikie kwa maneno na si kwa ishara.



    “Ta..tawile” Rebeka aliitikia. Yule mzee akachekelea huku akitingisha kichwa chake. Akainamisha kichwa chini kama dakika moja ama mbili. Alipokuja kukiinua. Macho yake yalikuwa mekundu mithili ya nyanya mbivu. Rebeka alitaka kukimbia ila alizuiwa na rafiki yake. Akakaa tena ila hivi sasa akirudi nyuma kidogo mbali na yule mzee.



    “Sharti la kwanza litaanzia leo usiku. Inakubidi ulale hapaa” Yule mzee aliongea kwa sauti ya kuogofya tofauti na ile ya mwanzo. Hivi sasa ilikuwa ikikwaruza sana kama mtu anaetaka kukata roho. Rebeka macho yalimtoka pima asiamini masikio yake. Yani nilale hapa? Na nyumbani je? Mume wangu nae? Alijiuliza.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Najua kinachokuchanganya ni mume wako. Usijali nitakupa dawa ambayo unatakiwa umuwekee kwenye chakula cha usiku. Jua kwamba akikila atalala na hatoweza hata kushtuka hadi siku ya pili majira ya asubuhi. Na muda huo itakuwa tumeshamaliza kazi na utarudi nyumbani kwako utamkuta akiwa bado amelala. Kwahiyo ondoa hofu kuhusu hilo” Alitoa maelezo mzee. Kisha akampa dawa ambayo ilikuwa ndani ya karatasi dogo. Rebeka akaipokea huku akitetemeka. Baada ya hapo wakaaga na kuondoka.



    Majira ya saa mbili usiku Rebeka ndio alikuwa akimaliza kupika chakula. Kama alivyoambiwa na yule mzee nae akafanya vile vile. Dawa ile akaichanganya kwenye chakula ambacho alihakikisha lazima akile Frank. Baada ya hapo akahamisha chakula na mezani ambapo alimkuta mume wake akiwa hapo akichezea simu yake. Akamtengea chakula. Chakula ambacho alikiweka ile dawa. Frank bila kujua alikula na baada ya kumaliza kula. Alijihisi kuwa na usingizi mwingi. Akajiondoa pale mezani na kuhamia sebuleni. Akatafuta sofa na kujilaza. Akavuta rimoti na kubadilisha chanel kwenye Tv. Akawa anaangalia taarifa ya habari na kujikuta akisinzia pale pale kwenye sofa.



    Rebeka aliingia chumbani kwake na kwenda kujiandaa haraka haraka. Dakika kumi na tano zilimtosha kujiandaa. Akatoka na kumkuta mumewe akiwa bado amelala vile vile. Akazima taa ya sebuleni. Kisha akafunga milango yote na kuondoka nyumbani hapo. Akatafuta tax iliomfikisha kule kwa yule mzee. Tax ikarudi mjini na yeye akaenda kwenye kile kijumba. Akabisha hodi na kupokelewa na sauti iliyomtaka kuingia ndani. Akataka kuvua viatu kam alivyo zoea ila akakatishwa na sauti iliyomtaka kuingia ndani akiwa hivyo hivyo. Akazama ndani.



    Alimkuta yule mzee mara hii akiwa na mavazi ya kawaida. Pia hakuwa mzee sana kama alivyoonekana mchana wa siku hiyo. Sasa alikuwa na umri unaokaribia na uzee. Akamkaribisha sehemu iliyoonekana kama sebule hivi. Akakalishwa kwenye kochi chakavu na kuambiwa asubiri hapo. Akakaa huku hofu ikiwa nae. Baada ya muda yule mzee alirudi tena na hivi sasa akiwa kwenye mavazi yake yale yale ya kiganga. Akamuambia Rebeka aache kila alichokishika hapo na watoke akiwa hana chochote cha kubebeka. Akaacha kila kitu ikiwemo mkoba wake ambao ndio alikuwa ameweka vitu vyake vingi humo. Wakatoka wote.



    “Umefanya la maana kuja na haya mavazi mekundu huku. Sasa hapa chukua hiki kitambara cheusi, jifunge kiunoni..” akampatia kitambara hicho na yeye akajifunga. Akaendelea. “...chukua na hiki cheupe jifunge kichwani” na yeye akafanya hivyo. Safari ikaendelea kusikojulikana.



    Walitembea umbali mfupi tu na safari yao ikaishia kwenye mti mrefu na mkubwa. Yule mzee akamuambia Rebeka akae upande wake wa kushoto kisha akatoa usinga wake na kuanza kupunga kila pande. Akatulia kimya na kuanza kuinamisha kichwa na kukiinua mara saba kuulekea mti huo. Alipokuja kukiinua macho yake yalibadilika rangi na kuwa mekundu zaidi yalivyobadilika mchana. Giza tu ndilo lililofanya Rebeka asiyaone macho ya mganga yule.

    Pengine angekuwa na hofu zaidi ya hiyo aliyonayo sasa.



    Baada ya hapo akaongea maneno yasiyoeleweka ambayo haikujilakana ni lugha gani. Akayaongea sana na alipokuja kukoma. Akamtaka Rebeka wauzunguke huo mti mara tatu. Wakafanya hivyo na walipokuja kutulia. Akachukua kibuyu na kukipunga punga kwa juu na ule usinga wake na kumpatia Rebeka. Akamtaka anuie chochote akitakacho kwenye kibuyu hiko. Rebeka alikipokea huku akitetemeka nusra akiangushe. Akafanya kama alivyotakiwa kisha akamrudishia mganga kibuyu chake. Alikipokea na kukipunga punga tena kisha akaachia cheko kubwa lililomuacha hoi kwa hofu Rebeka. Kisha akamuambia.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    “Agano na wakubwa limetimia. Hupaswi kupinga sharti lolote nitakalo kupa kuhusiana na hiki ulichokiomba.....” akamuangalia usoni japo uso huo aliuona kwa tabu kutokana na kigiza kilichogubika mahala hapo na macho yake mekundu yakutisha. Kisha akamuambia. “.....sharti la kwanza litaanzia nyumbani kwangu. Nikukumbushe tu kuwa huna namna ya kupinga na vinginenvyo utadhurika wewe na kizazi chako..... Tuondoke, tushamaliza kazi”



    Mganga alipunga usinga pande nne za dunia. Kisha akainama kama anatoa heshima fulani. Baada ya hiyo akamtaka Rebeka waondoke. Walipofika kwenye nyumba ya yule mganga. Rebeka akatakiwa asubiri pale pahali palipoonekana kama sebule. Mganga akaingia kwenye kile chumba alichokuwa ameingia mwanzo. Baada ya dakika kadhaa akafungua pazia lililokuwa kama kizuizi cha mlango na kumtaka Rebeka aingie na yeye mule. Muda huu alikuwa kifua wazi na chini alivaa kaniki.



    Rebeka alingalia huku na huko kama ni yeye kweli alietakiwa kuingia chumbani humo. Hakuona mtu wala kitu isipokuwa yeye mwenyewe. Kuna nini? Nikafanye nini? Akajiuliza. Yule mganga alikuwa bado akimuangalia. Akainuka kiuoga huku akitetemeka kwa chini chini. Mganga aliachia pazia. Rebeka alienda kufunia pazia lile na kuzama ndani. Huko alikuta chumba kilichotisha tofauti na mazingira aliyoyazoea yeye. Kilikuwa ni chumba kidogo lakini kirefu. Chenye makorokoro mengi yasiyoeleweka kwa haraka. Kulikuwa na kibatali kilichotoa mwanga hafifu ambao haukuwa ukitosheleza kuangaza ndani humo.



    Mganga alimkaribsha kwenye kitanda. Hapana ni mfano wa kitanda. Kitanda ambacho kilionekana kuchoka na kwa haraka haraka unaweza jua ni kichanja cha kuwekea mahindi. Rebeka alipiga hatua ndogo ndogo kukiendea kitanda kile huku akijaribu kuchunguza huku na huko ndani humo. Palitisha!. Paliogepesha!. Na hata hapakufaa kuishi kiumbe aitwae binadamu labda kuishi wanyama kama Kuku, Bata Mbuz....... Aaagrh acha nisipaongelee sana nisije nikadhuriwa na mganga huyo au hata kufanya mazingaombwe yake utashi huu wa uandishi wa riwaya ukaniondoka ki mazingara.



    Hofu bado ilikuwa nae Rebeka baada ya mganga yule kumsogelea pale kitandani akikaa karibu nae huku mkono wake wa kulia ukipita kiunoni mwake. Nabakwa!. Aliwaza Rebeka. Akataka kupinga jambo hilo, ila alikatishwa na ishara aliyopewa na mganga kuwa atulie kimya. Nae akakaa Kimya!. Mganga aliendelea kufanya yake taratibu bilawasiwasi wowote ilhali wasiwasi ukiwa na Rebeka.



    Kufamba na kufumbua. Nguo yake ya juu ilikuwa pembeni yake. Haikujulikana na hata yeye pia hakujua nguo yake imetolewa saa ngapi. Pengine imetolewa kimazingara pia!. Nani anaejua? Hakuna!. Hivi ni sahihi mimi kulala na huyu babu? Akajiuliza Rebeka. Hapana si sahihi. Kwanza mimi ni mke wa mtu. Eee ni mke wa mtu lakini mzee huyo pia si mtu? Nikajiuliza.



    “Ukijaribu kupinga hili nakugeuza Mbwa sasa hivi ukae nje ya nyumba yangu unilinde” Mganga akampa onyo baada ya kumuona akileta tabu ilhali yeye alishaanza kupandwa na hashki za kufanya ngono. Unadhani Rebeka angetaka kugeuzwa mbwa ailinde nyumba hiyo? Katu asilani! Akakaa kimya na kumpa wasaha mzuri mganga kufanya kile kilichopo mawazoni mwake muda huo. Ngono!.



    * * * *



    Majira ya alfajiri yalimkuta Rebeka akiwa amekaa kwenye kochi lililokuwa ndani mule. Akiwa amejikunyata kimya huku akitetemeka. Mtetemo ule haukuwa wa uoga kama aliokuwa nao usiku wa siku iliyopita. Mtetemo wa sasa hivi ulikuwa ni wa ubaridi uliokuwa ukipiga kwa kasi yake. Akiangalia nguo alizovaa ni nyepesi sana ambazo zilimuwezeshe baridi kumpiga haswaa. Je achukue mashuka yaliyozagaa ndani humo ajifunike? Nani kasemaa!. Mashuka yalikuwa yakitoa harufu kali. Sio kwamba yalitoa harufu nzuri? Thubutu!.



    Yalikuwa yakitoa harufu kali isiyoeleweka. Na sio harufu tu. Na rangi isiyoleweka kama ni nyeusi ama zambarau huku ikichora ramani mbali mbali za kijiji alichowahi kuishi mganga huyo. Chakushangaza. Yule mzee alikuwa amelala pale kwenye kitanda ambacho sitoona haya kukiita kichanja huku akiwa amejifunika moja ya mashuka yale gubi gubi. Rebeka alikuwa akitamani mzee yule ainuke hata muda huo ili ampe ruhusa ya kuondoka hapo maana akiangalia saa kwenye simu yake ilimuonyesha ni saa kumi na moja na dakika arobaini.



    Ni kama vile dua zake ziliitikiwa na muumba. Mganga aliinuka pale kitandani na kumuangalia mteja wake. Kisha akaachia tabasamu lisilojulikana kama ni salamu za kikwao ama ndivyo alivyozoea kuwaangalia watu pindi amkapo. Akamuuliza ameamkaje na Rebeka alijibu kwamba ameamka salama. Kimya kikachukua nafasi kwa zaidi ya dakika mbili. Rebeka akavunja ukimya na kumuambia kwamba alihitaji kuondoka ili amuwahi mume wake kabla hajaamka.



    Alikuwa na uhakika kwamba mume wake hadi majira hayo hakuamka. Na hiyo ilitokana na kuacha simu yake hewani makusudi ili mume wake atakampo amka. Alijua lazima atamtafuta. Mzee aliinuka pale kichanjani na kuiweka kaniki yake vizuri. Akapiga myao mrefu huku akikuna tumbo lake. Akamuangalia tena Rebeka. Rebeka akakwepesha macho yake na kuangalia pembeni. Mganga akatabasamu na kutoka ndani humo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliporudi alikuwa ameshika kijungu ambacho ndani yake kulikuwa na vikaratasi viwili vilivyofungwa vizuri. Akamuambia atie mkono achukue kimoja na yeye akafanya hivyo. Hapo akamuambia kuwa hiyo ni dawa. Na dawa hiyo anatakiwa amuwekee mume wake kwenye chakula atakacho kila mchana wa siku hiyo na ahakikishe chakula hiko awe amekipika yeye mwenyewe. Hilo halikuwa tatizo kwake maana hakuwa na mfanyakazi wa kupika chakula nyumbani kwake. Kwahiyo kama ni kupika basi atapika yeye mwenyewe.



    Akamuambia atie mkono tena achukue kile kilichobaki. Na yeye akafanya hivyo. Hiyo nayo akamuambia kuwa ni dawa. Na dawa hiyo anatakiwa ampake mume wake pale atakapolala baada ya kula chakula kile chenye ile dawa ya mwanzo. Alimuambia kuwa anatakiwa ampake juu ya macho, katika tundu za pua zake na amalize juu ya mdomo na kwenye masikio. Hiyo ilikuwa ni kumfunga asione, asisikie, asinuse wala asiongee chochote kwenye kauli yake. Akamruhusu aende huku akimsisitiza kukumbuka masharti hayo. Rebeka akaondoka.



    Saa kumi na mbili na nusu asubuhi ilimkuta Rebeka nyumbani kwake. Akafungua mlango kwa wasiwasi na kuzama ndani. Akashusha pumzi za ahueni baada ya kumkuta Frank akiwa amelala vile vile alivyomuacha kwenye sofa. Akapitiliza mpaka chumbani kwake na kuvua nguo zote. Akakiendea kioo cha kabati na kujitazama akiwa mtupu kabisa. Hivi ni kweli nimetoka kulala na mzee? Tena mganga? Akajisikitikia kulala na mganga lakini asisikitike kwa yale aliyoyasababisha hadi umauti ukawakuta Bibi na Bwana Fransisi. Wazazi wa Shery.



    Akaingia maliwatoni. Huko akafanya anayoyajua yeye na baada ya dakika kadhaa akatoka huku mwili wake ukichirizika maji. Bilashaka alitoka kuoga. Akavaa nguo alizozoea kulala nazo na kutoka hadi pale sebuleni. Akatumia wasaa huo kuzuga kama anatoka kulala. Akamuamsha Frank kwa sauti ya uchovu. Frank aliinuka na kujishangaa kiwa sebuleni na si chumbani kama alivyozoea.



    “Kumbe nililala hapa? Mbona hukuniamsha? Kwanza imekuaje nikapitiwa na usingizi namna hii?” Frank aliuliza maswa mfululizo.







    “Hata mi’nashangaa kukukuta hapa. Mi nilijua basi tume lala wote ndani. Naja kuamka asubuhi. Sikuoni! Na sio kawaida yako kuwahi kuamka. Nd’o nikaona nije kuangalia huku. Mara nashangaa umelala kwenye sofa sijui tatizo nini?” Rebeka aliongea na mwisho alimalizia na muayo wa kuigiza akijifanya ana uchovu mwingi.



    Frank aliinuka kiuvivu pale kwenye sofa. Akajinyoosha kidogo kisha macho yake akayapeleka kwenye sofa alipotoka kulala muda mfupi uliopita. Akapaangalia na kurudisha macho yake kwa Rebeka. Akamsaili kwa sekunde kadhaa. Akashangaa! Huyu anatoka kulala au kuoga? Kama anatoka kulala mbona anaonekana ana maji maji kwenye mwili wake? Ama ni jasho? Hakupa jibu!.



    “Sasa mke wangu fanya basi uniandalie chai haraka maana nataka kutoka saa hii” Frank aliongea.



    “Unataka kutoka? Unaenda wapi? Leo si jumapili?” Rebeka aliuliza maswali mfululizo. Ila uliza yote ni ile kuwa na hofu. Itakuaje endapo Frank asiporudi mchana ilhali masharti yalimtaka amuwekee ile dawa kwenye chakula cha mchana? Hofu!. Wasiwasi!. Ama Uoga!. Pengine hata vyote kwa wakati mmoja vilikuwa nae.



    “Aarhg! Rebeka unajua kama leo ni jumapili siku ya ibada. Sasa unaniuliza vipi nataka kwenda wapi ilhali wajua kabisa kwamba leo ni kanisani? Au kwavile wewe huendi ndio maana?”



    “Hapana sio ivyo. Ila umenishangaza kusema unataka kutoka saa hii wakati muda bado kabisa” Rebeka alijibu huku hofu ikimpungua taratibu nafsini kwake.



    “Kuna sehemu nitapitia kabla ya kwenda kanisani... Fanya hivyo basi ili usinicheleweshe” Aliongea hivyo na kuanza kupiga hatua kukifuata chumba chao.



    Majira ya mchana. Rebeka alikuwako jikoni akianda chakula. Sebuleni Frank alikuwa amejilaza kwenye sofa huku akisoma kitabu cha Riwaya kiitwacho. ‘ SIKU TATU KABLA YA KIFO CHAKE’ Kilichoandikwa na mtunzi mahiri katika tasnia hiyo ya utunzi. Ahmed Ramadhani Jiriwa. Kitabu ambacho kilimuhamisha katika sayari hii ya tatu na kumpeleka katika sayari ya Riwaya isiojulikana ni sayari ya ngapi. Mpangilio mzuri wa matukio na maneno matamu yaliyoandikwa kwa ustadi mzuri huku vikichagizwa na kisa chenyewe cha kuvutia na kuteka akili ya msomaji. Vilimfanya asikumbuke chochote hata alipo ni wapi.



    Alikuja kushtushwa na sauti ya Rebeka ambae alikuwa muda mrefu hapo akimuangalia jinsi alivyo topelea kwenye kitabu hiko. Rebeka akatabasamu na kumuambia kuwa chakula kilikuwa mezani na ilikuwa ni yeye tu asubiriwaye ili wakakishambulie chakula hiko. Akatamani asile ili aendelee kusoma kitabu kile. Ila akajua kufanya hivyo itapelekea kumuuzi mkewe. Akasimama, kitabu mkononi.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa hicho kitabu unaenda nacho wapi? Si ukiache tu hapo utarudi kumalizia kusoma ukimaliza kula” Rebeka alisema. Frank alimuangalia Rebeka usoni kisha macho yake akayarudisha kwenye kile kitabu ambacho kwa sasa alikuwa amekipitishia kidole cha shahada pale alipoishia kusoma huku akiwa amekifunga. Juu ya jalada la mbele akapokewa na maandishi ya jina la mtunzi wa kitabu hilo. Ahmedy Ramadhan Jiriwa. Akasikitika huku akitabasamu. Bilashaka alifurahishwa na utungaji wa mtunzi huyo. Ama kweli kuna watu wana vipaji vya ajabu. Yani kama vile maisha ya kweli? Alijiwazia mwenyewe kisha akakitupa kitabu kile kwenye sofa alilokuwa amejilaza mwanzo. Akaongozana na Rebeka kuifuata meza.



    Rebeka alimuandalia chakula kile ambacho amekiweka ile dawa. Bila kujua chochote. Frank alikula kwa haraka kidogo ili amalize au hata akiishia njia sio mbaya ili mradi tu asimuudhi mke wake. Yote nikuwahi kuendelea kusoma kitabu kile. Dakika nane zilitosha kufika pale alipotaka kufika. Akanawa mikono huku akimshukuru Rebeka kwa kumtengenezea chakula kizuri. Akaondoka mezani na kulifuata tena lile sofa. Akachukua kile kitabu na kukifungua ile kurasa aliyoishia.



    Taratibu alianza kuona mabadiliko. Kichwa kilikuwa kizito mithili ya kiroba cha ‘Cement’. Macho yalitaka yafumbe ilhali yeye akiyalazimisha kuyafumbua ili aendelee kusoma kitabu chake. Mikono taratibu ilianza kushindwa kuhimili uzito wa kitabu kile. Akapiga kite cha ghadhabu. Akapikicha macho ili walau ajiweke katika hali ya kawaida. Ikashindikana!. Akaweka kitabu pembeni. Muda huo akapitisha wazo la kulala maana aliona usingizi ukimshinda. Akalala!.



    Rebeka alimuona Frank alivyokuwa akipata tabu kushindana na usingizi wa kimazingara. Mwisho alimuona kama amelala hivi. Akataka kujihakikishia. Akamfuata mpaka pale. Akamuamsha kidogo kidogo huku akimtingisha kwa mbali. Frank ndio kwanza alikuwa akijigeuza upande wa pili. Nusra adondoke kwenye lile sofa. Rebeka akatabasamu na kuingia chumbani kwao. Baada ya dakika moja akatoka na ile dawa ambayo alipewa na yule mzee wa kiganga.



    Akafika nayo pale kwenye sofa. Akafanya kama alivyoambiwa. Akampaka ule unga wa ile dawa kidogo juu ya ngozi ya macho. Akahaimia kwenye pua, napo akafanya hivyo. Akashuka mdomoni napo akampaka, kisha akamalizia na masikioni. Frank alipiga chafya kisha akafumbua macho yake kidogo. Alionekana kuzidiwa na usingizi si mas'hara. Akafumba tena na kulala moja kwa moja.



    * * * *



    “Mi nadhani ungeenda tu kuishi na baba yako mdogo. Kwasababu wewe bado ni mdogo na unahitaji malezi” Alishauri Mkasi baada ya Shery kuumiza kichwa sana na asipate uamuzi wa kipi afanye.



    “Na wewe je utaenda kuishi wapi?” Shery alimuuliza.



    “Narudi nyumbani. Nahitaji kwenda kuanzisha familia yangu na mimi” Shery akatulia kimya akifikiria ushauri wa Mkasi. Ni kweli ni waki sasa tangu alipoomba kupewa muda wa kufikiria ni amuzi lipi atalichukua. Atafute mtu kati ya watu wale waliokuwepo kwenye kikao siku ile aishi nae hapo nyumbani kwao. Au akaishi nyumbani kwa huyo mtu.



    Wazo la Mkasi akalipitisha ya kuwa akaishi kwa Frank ambae ni baba mdogo wake. Akachukua simu na kumpigia. Simu ilikuwa ikiita tu pasi na kupokelewa. Alipojaribu mara ya pili. Simu ikapokelewa. Lakini sio na yule aliemtarajia. Alipokea Rebeka mke wa baba yake mdogo. Wakasalimiana kwa furaha na Shery akamuulizia baba yake mdogo. Rebeka akamuambia kuwa muda huo amelala. Shery akamuambia kuwa majira ya jioni atakuwa hapo maana kuna jambo anataka kuzungumza nae. Simu ikakatwa baada ya maafikiano.



    Majira ya saa kumi na mbili za jioni. Shery alikuwa nyumbani kwa Frank. Muda huo walikuwa wapo kwenye bustani ya nyumba hiyo baada ya Frank kuamshwa kwenye usingizi uliomkuta kiajabu. Walikuwa wapo wenyewe sehemu hiyo. Moja kwa moja Shery hakutaka kupoteza muda. Akaenda kwenye swala lililomleta hapo. Akamueleza kuwa alifikiria na kupitisha uamuzi wa kuja kuishi hapo kwake. Frank alifurahi sana baada ya mwanae huyo mtoto wa kaka yake kutaka kuishi nae.



    Wakapanga na kukubaliana kuwa, nyumba ile ambayo alikuwa akiishia Shery. Waipangishe na kodi itakayopatikana isaidie kwenye elimu ya Shery. Japokuwa wazazi wake wameacha mali nyingi tu. Frank alimuuliza kuwa ni lini alionelea aje kuanza kuishia hapo. Shery akajibu kuwa ni siku inayofuata baada ya kwisha kuwa ametoka chuoni. Wakazungumza machache na Shery akaaga kuwa anataka kuondoka. Akaruhusiwa. Akaingia ndani kwenda kumuaga mama yake mdogo. Akaondoka akiahidi kuwa siku inayofuata atatokea hapo baada ya kuwa ameshaweka mambo sawa kule nyumbani kwao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Frank akiwa bado na furaha baada ya Shery kutaka kuja kuishi kwake. Alimpigia simu yule mzee ambae ile siku ya kikako yeye ndie aliekuwa kiongozi. Akamjulisha uamuzi wa Shery na mzee yule nae akabariki. Akakata simu na kuingia ndani. Huko alimpa taarifa hizo mke wake. Rebeka alizipokea kwa furaha kama alivyozipokea yeye. Frank alikuwa akifurahia kuwa katika kikao alipewa jukumu la kusimamia mali za kaka yake na leo hii Shery ametaka waishi wote nyumbani kwake. Aliona ni jinsi gani mtoto wa kaka yake alivyokuwa akimpenda. Lakini kwa upande wa Rebeka ilikuwa ni tofauti na Frank.









    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog