Search This Blog

Friday, October 28, 2022

BEYOND PAIN - 3

 









    Simulizi :Beyond Pain

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Meserani park moja kati ya sehemu nzuri kutembelea iko kilometa 25 magharibi mwa jiji la Arusha katika barabara ya kuelekea hifadhi ya taifa ya Serengeti na bonde la Ngorongoro.Hifadhi hii imejumuisha nyoka wa kila aina wanaopatikana mashariki na kusini mwa afrika.Ukiwa katika hifadhi hii ya Meserani utapata pia kuwashuhudia mamba wenye ukubwa wa zaidi ya meta tatu na vile vile utafurahia safari za ngamia kuelekea katika maboma ya wamasai na utabahatika kujifunza utamaduni wa kimasai.

    Saa kumi za jioni tulirejea jiijini Arusha.Ilikuwa ni siku niliyofurahi mno.Tulipanda ngamia na kwenda katika kijiji cha wamasai ,tulikaa na kujifundisha mambo mengi kuhusiana na utamaduni wa kimasai pamoja na kununua badhi ya vitu walivyokuwa wakiviuza.Kwa miaka yangu yote ya kuishi Arusha sikuwahi hata mara moja kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo hapa jijini.Nilijisikia furaha sana baada ya kugundua faida ipatikanayo kutokana na utalii wa ndani.

    “Clara bado naendelea kukushukuru kwa sababu kupitia kwako nimejifunza mambo mengi.Katika miaka yote hii niliyoishi hapa Arusha sijawahi kutembelea hata kivutio kimoja ha utalii.Nimehamasika sana kwa ziara tuliyoifanya leo na kila nipatapo nafasi nitakuwa nikifanya utalii wa ndani na kuliongezea taifa mapato” Clara hakujibu kitu alinitazama na kutabasamu

    Clara hakutaka tena kukaa pale hotelini .Hakutaka tena kuwa mbali nami.Akaniomba kwa siku hizi chache ambazo atakuwepo hapa Arusha azimalizie akiwa nyumbani kwangu.Nilifurahi sana kwa uamuzi ule

    Pale hotelini Clara hakuwa akidaiwa chochote akapakia vitu vyake na tukaelekea nyumbani kwangu.Furaha ikaingia tena ndani kwangu.

    **********************

    Siku mbili kabla ya safari ya kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mapumziko nilipokea taarifa kwamba ninahitajka katika ofisi za taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa.Walikuwa wakihitaji kunihoji .Tayari Emmy alipeleka mashitaka kama alivyokuwa ameahidi kama nisingetimiza matakwa yake.Sikuwa tayari kutimiza matakwa ya Emmy.Nilimweleza Clara kuhusiana na mwito ule na akanipa moyo kwamba nisiwe na wasi wasi hata chembe kwa sababu suala hilo liko ndani ya uwezo wake na nihesabu kama limekwisha.

    Saa tatu za asubuhi katika siku niliyotakiwa nifike pale ofisini ilinikuta nikiwa katika chumba maalum kwa ajili ya mahojiano.Watu tatu wakaingia pale wakiwa na mafaili yenya nyaraka mbali mbali tukasalimiana na mahojiano yakaanza.

    Nilihojiwa mambo mengi sana kuhusiana na fedha zile zilizokuwa benki.Niliwaele

    za ukweli kuhusiana na ugomvi wangu na Emmy na jinsi gani Emmy anavyotaka kuhakakisha kwamba ninaporomoka.Ni

    liwaeleza vile vile kwamba si kweli kwamba fedha zile zilitokana na ufisadi nilioufanya wakati nikiwa mfanyakazi wa halmashauri ya jiji la Arusha bali fedha zile zimetokana na biashara tuliyokuwa tukiifanya kwa ubia kati yangu mimi na Clara.Clara akaitumia nafasi hiyo pia kulezea kwa upana kuhusiana na biashara tunayoiendesha kwa ubia .Aliwaonyesha vithibitisho mbalimbali vilivyokuwa katika kompyuta yake ndogo vilivyoonyesha kwamba nimekuwa nikipokea mgao wa fedha toka katika kampuni ile.Kitu kilichowaumiza kichwa ni kwamba ni wapi basi Emmy alizitoa nyaraka zile alizokuwa nazo? Nyaraka kuhusiana na fedha iliyokuwepo benki nilikiri ni zangu na Emmy alizichukua wakati nikiwa sipo nyumbani lakini nyaraka mbalimbali ambazo alikuwa nazo kuhusiana na ufujaji wa fedha za halmashauri nilizikana na kuwaomba waende wakapate taarifa sahihi kutoka halmashauri nilikokuwa nikifanya kazi.Baada ya masaa takribani sita ya mahojiano,tukaondoka na kuwaacha wakiumiza vichwa vyao na kumlaani Emmy kwa kuwasumbua pasi na faida yoyote.Nilimshukuru sana Clara kwa kuniokoa katika sakata lile.

    “Pamoja na kulimaliza suala hili bado nitabaki na msimamo ule ule kwamba fedha zile ni za wananchi na itabidi tuzirudishe kwa wananchi kwa kuzipeleka katika miradi ya maendeleo” akanikumbusha Clara.

    “Clara nalikumbuka hilo.Mara tutakaporejea kutoka Zanzibar fedha zile zote tutazipeleka katika miradi .Tutapanga na kuamua ni kitu gani tunaweza tukaifanyia jamii kwa fedha zile”

    Nikamwambia Clara akatabasamu na kunibusu.

    ***********************

    Ni Siku ya tano sasa toka tumefika hapa Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Serena Inn.Baada ya misuko suko iliyotupata Arusha tuliamua kuja huku mbali kwa ajili ya mapumziko na kupanga maisha yetu.Ni mida ya saa tisa za alasiri tukiwa katika ufukwe wa Mangapwani unaomilikwa na hoteli hii ,simu yangu ikaita.Niijilaumu sana kwa kutembea na simu sehemu kama hii.Nikaitoa simu na kuangalia mpigaji.Zilikuwa ni namba ngeni kabisa.

    “hallo “ nikaita

    “hallo Wayne” Ikajibu sauti ya upande wa pili ambayo nilihisi kama ninaifahamu.

    “nani mwenzangu? Nikauliza

    “Ni mimi Chris”

    “Chris !! nikastuka mno.Sikuitegemea kama Chris angeweza kunipigia simu hasa baada ya kitendo alichonifanyia.

    “Wayne najua hukutegema kama ningeweza kukupigia simu tena.Nimelazimika kukupigia kuongea na wewe mambo mawili makubwa”

    “Chris tafadhali naomba usiniharibie siku.Kwa sasa niko Zanzibar mapumzikoni na mpenzi wangu mpya.Sitaki unisumbue Chris” Nikasema kwa ukali

    “Wayne tafadhali naomba unipe dakika mbili tu za kuongea na wewe na baada ya hapo sintakusumbua tena.” Chris akasema

    “Unataka kuniambia kitu gani Cris? Nikauliza kwa ukali

    Clara aliyekuwa amebaki nyuma yangu akanikaribia na kuniuliza

    “Darling mbona unaongea kwa ukali namna hiyo.nani huyo aliyekupigia simu ?

    “Ni mume wa Emmy” nikamjibu Clara ambaye akasogea pembeni na kunipa nafasi niongee na Chris.

    “Wayne kwanza kabisa nachukua nafasi hii kukuomba msamaha japokuwa nafahamu kwamba si rahisi kunisamehe kwa mambo niliyokufanyia.Nimekuwa sina amani maishani mwangu.jambo hili limenikondesha mno.Japokuwa ni ngumu kwako kunisamehe lakini naomba nikiri kwamba nilikukosea sana na ninaomba unisamehe.”

    “Chris mimi sina tatizo na wewe hata kidogo. Nimekwisha kusamehe muda mrefu sana na nikaendelea na maisha yangu.Nilikupa Emmy kwa kuamini kwamba ndiye mwanamke pekee anayekufaa maishani.Mimi kwa sasa niko na mpenzi ambaye ndiye niliyeandikiwa na Mungu.Ninayafurahia maisha yangu tofauti na nilipokuwa na huyo mke wako” Nikasema huku nikitabasamu

    “nashukuru sana Wayne kama umekwisha nisasemehe.Jambo la pili ninalotaka kukueleza ni kwamba mimi na Emmy tumeachana.Niligundua kwamba mtoto yule ambaye alisema ni wa kwangu hakuwa mtoto wangu.Kutokana na matendo yake nilipata shauku ya kwenda kupima DNA na majibu yakaonyesha kwamba Baraka si mwanangu kama alivyodai.Sikuweza kuvumilia nikaamua kumfukuza kwangu na kwa sasa amesema kwamba anarudi kwako kwani bado ni mkeo halali.Hivi tunavyongea tayari amerejea nyumbani kwako anadai ni nyumbani kwake na wewe ni mume wake halali wa ndoa.Nimeona nikufahamishe kuhusu jambo hilo ili ujue nini kinaendelea huku na uchukue tahadhali.Mwanamke yule ni baradhuli na hafai katika jamii..kwa heri wayne” Chris akakata simu

    “bastard !! nikasema kwa hasira.Nilihisi kijasho chembamba kikinitoka

    Clara aliniangalia jinsi nilivyobadilika ghafla akahisi mambo hayakuwa sawa akanisogelea na kunishika bega.

    “Wayne huyo mume wa Emmy amekuambia nini cha kukuudhi namna hiyo? Akauliza Clara.Nilikuwa nikihema kwa nguvu kwa hasira

    “Clara ninajuta kwa nini nilimfahamu Emmy.Nashindwa kuelewa ni mwanamke wa aina gani yule”

    “Nini kimetokea tena? Kwa nini anaendelea kukufuata fuata wakati kila mmoja ana maisha yake kwa sasa? Clara akauliza

    “Chris amenipigia simu na kuniambia kwamba yeye na Emmy wametengana .Amegundua kwamba yule mtoto Baraka ambaye Emmy alisema ni wake kumbe si wake.Jambo hilo limemfanya amtimue Emmy na hivi tunavyoongea amerudi nyumbani kwangu akidai bado ni nyumbani kwake.Nashindwa kuelewa nitamfanya nini huyu mwanamke ili aachane na mimi.Nimechoka sasa na matukio ya Emmy”

    Clara akaniangalia kwa makini usoni na kisha akasema

    “ Suala hili limekuwa gumu sana kwa sasa.Ukiangalia kisheria Emmy bado ni mkeo wa ndoa.Kwa mujibu wa ndoa za kikristu ni kwamba mkisha funga ndoa kanisani hakuna kitu kinachoweza kuwatenganisha zaidi ya kifo.kwa maana hiyo wewe bado ni mume halali wa ndoa wa Emmy.Kwa Emmy kurudi katika nyumba yenu ni halali yake kwa sababu bado ni mke wako.” Clara akasema taratibu lakini nilijua ndani ya moyo wake alikuwa ameumia sana.Nilijaribu kutafakari kwa kina ni kwa nini Emmy amekuwa akinifanyia vituko vya namna hii.Kwa nini hataki kuniona nikiwa na furaha katika maisha yangu? Niliuma meno kwa hasira na kusema

    “Clara pamoja na yote uliyoniambia lakini ni ukweli ulio wazi kwamba ndoa kati yangu na Emmy ipo katika makaratasi tu.Lakini katika uhalisia hakuna ndoa baina yetu.Hata Mungu mwenyewe analiona hilo na hata hao viongozi wa dini nikiwaelezea watakubaliana nami kwamba Emmy hafai kuwa mke.Nimekwisha mtoa Emmy moyoni mwangu na sintarudi nyuma tena.Simtaki Emmy maishani mwangu.Sitaki kabisa kumuona mbele ya macho yangu.” Nikasema kwa ukali

    “punguza hasira Wayne.Suala hili linatakiwa kushughulikiwa taratibu na kwa umakini mkubwa ili kupata suluhisho la kudumu la mgogoro huu usiokwisha.Mimi nina wazo moja” Clara akasema

    “Wazo gani hilo Clara?

    “Ninakushauri kwamba uwaite wazee wa pande zote mbili ili muweze kukaa na kutafuta suluhu kwa sababu kuivunja ndoa yenu ni jambo ambalo haliwezekani.Kinachotakiwa kufanyika hapa ni kuitafuta suluhu ya kudumu ili muweze kuishi kwa amani tena.”

    “Una maanisha nini Clara? Nikauliza

    “Nina maana suluhisho hapa ni wewe kurudiana na Emmy .Inavyoonekana ni kwamba Emmy bado anakupenda na kwa maana hiyo hata mfanye nini katu hamuwezi kutengana”

    “Tafadhali usiseme hivyo Clara” Nikasema.Nilikuwa nimestushwa sana na kauli ile ya Clara

    “Wayne suala hili mbona liko wazi kwamba wewe na Emmy kamwe hamuwezi kutengana.Mnachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kutafuta suluhu ili muweze kuishi kwa amani katika ndoa yenu.”

    “Clara naomba tafadhali usiseme hayo maneno.yananiumiza sana moyo wangu.Macho yangu kwa sasa nimeyaelekeza kwako tu.Ninachokihitaji ni kuwa nawe maishani.”

    Clara akanishika mikono miwili,akanitaz

    ama usoni na kusema taratibu

    “Wayne Nakupenda sana .Toka moyoni mwangu nakiri kwamba nakupenda zaidi ya unavyoweza kufikiri.Nakupenda zaidi ya ninavyojipenda mwenyewe.Sijawahi kupenda kama nilivyotokea kukupenda.Wewe ni kila kitu kwangu.Wewe ni mwanaume wa pekee kabisa ambaye hujawahi kutokea maishani mwangu.Kila nikiwa nawe najihisi kama niko juu mawinguni.nasikia furaha ya ajabu kila ninapokuwa nawe.Nilipokuona kwa mara ya kwanza niliweka ahadi kwamba nitafanya kila niwezalo kwa ajili ya kulipigania penzi lako.Nilikuwa tayari kwenda hadi mwisho wa dunia kwa sababu yako.Niliweka ahadi ile kutokana na jinsi ninavyokupenda Wayne.Kutokana na hali halisi ilivyo ninasikitika kusema kwamba Wayne mimi na wewe hatuwezi katu kuwa pamoja tena.Katu hatutaweza kuwa na furaha katika maisha yetu.Wewe ni mume halali wa Emmy.hata kama ndoa yenu iko katika mgogoro mzito kwa sasa lakini ukweli utabaki pale pale kwamba wewe ni mume wa mtu.Nimekuwa nikilifikiria sana jambo hili na limeniumiza sana moyo.Mwanzoni nilijipa moyo nikitegemea labda mambo haya yanaweza yakatulia na hivyo tukapata nafasi ya kufurahia maisha tukiwa sisi wawili bila bughudha ya aina yoyote ile lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo karaha na vituko toka kwa mkeo vinazidi.Kusema ukweli nimekuwa nikiumizwa sana na mambo anayoyafanya mkeo lakini nimekuwa nikivumilia kutokana na upendo wangu kwako.Kwa muda huu mfupi tulioonana kila siku limekuwa likiibuka jambo jipya toka kwa Emmy ambaye hataki kukuona ukipumzika.Hataki kukuona ukifurahi.Wayne naomba nikuambie ukweli kwamba nimevumilia na sasa nimechoka.Ninaona itakuwa vyema kwetu sisi kuusitisha huu uhusiano wetu ili usiendelee kuumia zaidi.Iwapo nitaendelea kuwa nawe Emmy hatatuacha hata kidogo.Ataendelea kutuandama usiku na mchana.Kwa maana hiyo ni bora kama nitajiweka pembeni na kukuacha uendelee na Emmy”

    Clara akasema kwa uchungu huku machozi yakimtoka.Alikuwa ameumizwa mno na mambo aliyokuwa akiyafanya Emmy.Alikilaza kichwa chake kifuani kwangu na kukilowesha kifua changu kwa machozi.Nilisikia uchungu mwingi kwa machozi aliyoyamwaga malaika wangu ,nikapandwa na zisizomithilika

    .Laiti kama Emmy angekuwa karibu yangu wakati ule ningeweza kumfanyia kitu kibaya sana.Sikujua ni kwa nini niendelee kuteseka kwa mambo anayonifanyia Emmy.Sijui nimemkosea nini Emmy kiasi cha kuwa na chuki nami ya namna hii.Niliumia sana kwa aumuzi ule wa Clara.Baada ya kuachana na Emmy nilitegema kwamba Clara ndiye furaha ya maisha yangu.Nilimuona ni kama malaika aliyeshushwa kwa ajili ya kuja kunirudishia furaha ya maisha iliyokwisha potea.Kwa muda huu mfupi niliokuwa na Clara nimekuwa ni mtu mwenye furaha kubwa maishani na nilikuwa na mipango mingi ya siku za usoni nikiwa na Clara. Kwa upande mwingine sikulaumu sana uamuzi huu aliouchukua Clara kwa sababu ni kweli alikuwa amechoshwa na karaha zinazoendelea. Toka siku ya kwanza tuliyoanza mapenzi yetu imekuwa ni matukio moja baada ya jingine.Clara hakuwa ametaka kujiingiza katika mambo ya mahusiano kwa sababu ya kuogopa mambo kama haya yanayotokea sasa.Aliufuingua moyo wake baada ya kuamini kwamba mimi ni mwanaume wa pekee ambaye ninaweza kumpa furaha ya maisha lakini kumbe alikuwa akielekea mahala ambako alikuwa akipakimbia miaka hii yote aliyokuwa akiishi peke yake.Alikuwa akiyakimbia matatizo na karaha zilizomo ndani ya mahusiano lakini badala yake amejikuta akitumbukia katika shimo lililojaa kila aina ya matatizo.

    “Wayne nakupenda sana na sitaki kuachana nawe lakini sintaweza kuendelea nawe kwa sababu ya ukweli ulio wazi kwamba Emmy anakuhitaji .Emmy ana kila sababu ya kunifanyia vituko kwa sababu wewe ni mume wake halali wa ndoa.Siwezi kuendelea kupambana na Emmy kila kukicha .Ninamuachia mume wake na kujiweka pembeni.Nimeamua kuyarudia maisha yangu niliyokuwa ninaishi yaani maisha ya kuwa peke yangu.Sitegemei kama nitaingia katika mahusiano tena kwa sababu baada ya miaka mingi ya kuwa nje ya mahusiano nimeufungua moyo wangu na kujaribu kupenda tena lakini kilichotokea ni kitu kile kile nilichokuwa na kikwepa kwa miaka mingi yaani mumivu ya moyo.Ninaumia sana Wayne..Moyo wangu umeumia sana na sijui kama kidonda hiki kitaweza kupona.Nitateseka kwa maisha yangu yote kwa sababu mtu niliyetokea kumpenda naye akanipenda hataweza kuwa nami.Inaniuma sana ….” Clara alizidi kumwaga machozi.Nikamuonea huruma .Alikuwa amemumia moyo.Alikuwa akiteseka kupita kiasi.Nilimlaani Emmy kwa laana zote za dunia hii.kwa machungu na hasira nilizokuwa nazo sikuwa tayari kumuona tena Emmy katika maisha yangu.Nilimchukia kupita kiasi.Nilimtaza

    ma Clara alivyokuwa akilia na kuteseka kwa maumivu ya moyo nikasikia uchungu sana.Huku machozi yakinilenga nikamwambia

    “Clara nafahamu ni uchungu kiasi gani ulio nao kwa uamuzi huu mgumu uliouchukua.Nafahamu vile vile mateso na maumivu makali unayoyasikia moyoni kwa mambo yote ambayo yametokea katika kipindi hiki kifupi tulichokuwa pamoja.Mateso na maumivu haya hata mim ninayasikia kwa sababu sipendi kukuona ukitoa machozi au ukiumia moyo wako.Ninapokuona katika hali hii ninapatwa na uchungu mwingi kwa sababu lengo langu ni kukuona ukiwa ni mwenye furaha na matumaini siku zote.Hata hivyo Clara uamuzi huu umeuchukua haraka sana.Nadhani bado nina nafasi ya kuweza kuyaweka sawa mambo haya ili mimi na wewe tuweze kuishi kwa amani katika maisha yetu.Naomba tafadhali unipe nafasi nyingine ili niweze kuyamaliza mambo haya na sisi tuweze kuishi kwa amani bila bughudha ya aina yoyote ile.Nitafanya lolote linalowezekana kufanyika ili mimi na wewe tuweze kuwa pamoja.” Nikamwambia Clara ambaye akainua kichwa na kunitazama

    “Wayne nakuamini kwamba unaweza ukafanya unavyoweza na sisi tukaishi kwa furaha.Ndiyo ! tutaishi kwa furaha lakini hatutakuwa na amani katika maisha yetu.Hatutaweza kufunga ndoa kwa sababu kisheria wewe bado ni mume wa mtu.Pamoja na hayo Emmy hataweza kukuacha uishi kwa furaha.Ataendelea kukuandama mpaka mwisho wa uhai wake.Jambo la msingi ninaloliona hapa ni sisi kuusitisha huu uhusiano wetu ili Emmy aweze kuwa na amani.Ninahisi vituko vyote hivi anavyovifanya ni kwa sababu anakupenda.” Clara akasema .

    Nilijaribu kuendelea kumshawishi abadili maamuzi yake lakini ilikuwa ngumu sana.Msimamo wake haukutetereka.Kwa mara nyingne tena nilikuwa nimeumizwa na Emmy.Nilisikia maumivu makali sana tofauti na hata pale mwanzo Emmy aliponiacha na kwenda kwa Chris.kwa sababu yake nilikuwa nimemkosa mwanamke niliyempenda zaidi maishani mwangu.Nilikuwa nimeikosa furaha ya maisha yangu.





    Hatimaye siku tuliyopanga kurejea Arusha ikawadia.Ilikuwa ni siku ya jumamosi yenye kijua kitamu.Kila kitu tulikwisha kiweka tayari kwa safari .Clara alikuwa amevaa miwani mikubwa kwa ajili ya kuyaficha macho yake yaliyokuwa mekundu na kuvimba kutokana na kulia.Kila alipokuwa akinitazama alishindwa kujizuia kutoa machozi.Alikuwa amenizoea sana na alifahamu kwamba baada ya muda mfupi ujao hataweza kuwa nami tena.Jambo hili lilimuumiza mno.Alitamani kuwa nami muda wote.Hata mimi nilisikia uchungu mwingi kila nilipomtazama malaika huyu ambaye nilimpenda zaidi ya ninavyoweza kuelezea..Ilikuwa ni kama nimeonjeshwa asali kisha nikanyang’anywa.Niliumia sana.

    Clara aliamua kunisindikiza hadi Arusha ili aweze kujaribu kupata walau muda wa kuongea na Emmy na kumweleza kwamba yeye na mimi tumeachana na kwa hiyo awe na amani ya moyo.Sikulipenda sana wazo hili la Clara kutaka kukutana na Emmy kwa sababu ninamuelewa vizuri Emmy ni mwanamke ambaye ninaweza kusema ana roho ya kikatili sana.Pamoja na kulipinga wazo hilo la kuonana na Emmy bado Clara aliendelea kusisitiza na ikanilazimu kumkubalia atakavyo.

    Saa tano juu ya alama tulipanda ndege na kuelekea mkoani Kilimanjaro.Tuk

    ashuka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na kisha tukakodisha taksi hadi jijini Arusha.Nilitaka tufikie hotelini lakini Clara alisisitiza tupite kwanza kwangu ili aniache nyumbani kwangu na baada ya hapo yeye angeelekea hotelini ambako angelala hadi siku ya pili yake ambayo alipanga kuondoka kurejea katika makazi yake afrika kusini.

    Geti halikuwa limefungwa.Niliamini maneno ya Chris kweli Emmy alikuwa amerejea nyumbani kwangu.Tukashusha mabegi yetu na kuingia ndani.Sebuleni tulimkuta Emmy akiwa amejaa tele akitazama luninga huku akinywa mvinyo.Nilipomuona ghafla nilipandwa na hasira za ajabu nikatamani nimrukie na kumpa kipigo kikali lakini Clara akaligundua hilo na kunisihi nisifanye jambo lolote baya.Emmy alipotuona akasimama akashika kiuono chake .

    “Huyo Malaya wako unampeleka wapi? Akasema Emmy kwa sauti kali

    “Naomba umtoe ndani ya nyumba yangu haraka sana”

    Niliinua mkono juu kwa dhumuni la kumtandika kibao lakini Clara akanishika mkono

    “wayne please don’t do that” akanisihi

    “nani amekurudisha katika nyumba hii wewe shetani? Nikafoka.Nilikuwa nimepandwa na hasira kali.

    “Nimerudi nyumbani kwangu.hapa ni nyumbani kwangu na ninaweza kuingia na kutoka muda wowote ule.Au umesahau kama mimi ni mkeo? Emmy akasema huku akiibetua midomo yake

    Nilichukua begi langu na kulipeleka chumbani halafu nikarudi sebuleni na kumkuta Emmy amefura kwa hasira.

    “Naomba tafadhali umtoe huyu kikaragosi wako nje ya nyumba yangu kabla sijamfanyia kitu kibaya” Emmy akafoka.

    Kwa kasi ya aina yake nikamrukia na kumkaba shingo yake kwa mikono yangu miwili.Juhudi za Clara kuninasua nisimuumize Emmy zilisaidia kwa sababu ningeweza kufanya jambo baya kutokana na hasira nilizokuwa nazo.

    “Wayne tafadhali punguza hasira unaweza ukamuua mwenzio.” Clara akasema huku akihema kwa nguvu.

    Nilimtazama Emmy ambaye alikuwa akihema kwa nguvu huku akilia .

    “Na iwe ni mwanzo na mwisho kumnyooshea kidole Clara.Huyu ndiye mwanamke ninayempenda na si wewe kunguru . Na ukithubutu tena kumuinulia mdomo Clara nitakukata shingo yako.” Nikamwambia Emmy ambaye alikuwa akifuta machozi.

    “ Wayne mimi naomba niondoke.Hakuna jambo lolote litakaloendelea hapa Nyote mna hasira na hatuwezi kuongea lolote.Nitakutaarifu nitaondoka saa ngapi siku ya kesho.kwa heri Wayne” Clara akasema huku akilichukua begi lake na kuanza kupiga hatua kutoka nje.

    “Clara subiri kwanza” Nikamwambia na kumfanya asimame.Nikaingia chumbani na kutoka nikilisukuma begi langu.

    “I’m going with you” Nikamwambia Clara.Sikuwa tayari kumuona Clara akiondoka kiurahisi rahisi namna ile. Clara akabaki akishangaa

    “Wayne !! “ Clara akasema kwa mshangao

    “I’ve made up my mind Clara.I’m going with you.Hakuna anayeweza kunitenganisha nawe.” Nikasema huku nikilikokota begi langu.

    “Wayne tumekubaliana kwamba urudi na utafute suluhisho na mkeo.That’s for the best of us all.Tafadhali Wayne naomba ukae na mkeo na mtafute suluhisho la matatizo yenu “ Clara akasema

    “Clara siwezi kuwa na mke mwenye roho ya kishetani kama huyu.This is not my wife” Nikasema kwa hasira huku nikimshika mkono Clara .

    “Wayne humu huondoki leo. Leo utachagua ama mimi ama huyo kahaba wako” Ikasikika sauti ya Emmy ikisema kwa ukali.

    “Twende tuondoke Clara.Usimjali huyo mwenda wazimu” Nikamwambia Clara na kuanza kulivuta begi lake kutoka nje.Kabla sijaufikia mlango nikamsikia Emmy akiita kwa ukali

    “Wayne nimekwambia hutoki humu ndani leo.”

    “Go to hell” nikasema bila kugeuka

    “Wayne !! Emmy akasema kwa sauti kali

    tayari tuliufikia mlango wa sebuleni nikageuka na ghafla Emmy akairusha ile chupa kubwa ya mvinyo akimlenga Clara.Kwa kasi ya ajabu nikamsukuma Clara akaanguka pembeni na chupa ile ikanipiga kichwani nikaanguka chini.Likatokea giza nene.

    ***********************

    Macho yangu yalikuwa mazito kufunguka .Nilihisi usingizi mzito sana.Nilijitahidi kuyafumbua macho yangu lakini bado yalikuwa mazito.Nilijihisi kama vile niko ndotoni.Nililifumbua jicho la kushoto lakini sikuweza kuona vizuri.Bado nilikuwa usingizini.Nilikuwa nikiona vitu viwili viwili na sikuweza kutambua kitu chochote.Nikafumbua na jicho lingine la kulia na kujaribu kuamka katika ule usingizi mzito niliokuwa nimelala lakini bado macho yalikuwa na ukungu.Nikainua mkono wangu na kuyafikicha macho na hatimaye nikaona kama niko katika sehemu yenye mwanga mkali.Nikajaribu kuinua kichwa lakini nikakirudisha chini kwa haraka baada ya kuhisi maumivu makali sana sehemu ya nyuma ya kichwa .Maumivu niliyokuwa nikiyahisi ilikuwa ni kama nimekatwa na kitu chenye ncha kali.Nikausogeza mkono kichwani ili niweze kuona sehemu niliyoumia nikakutana na bandeji kubwa iliyokuwa imefungwa nyuma ya kichwa changu.Hapo ndipo fahamu zilipoanza kunirudia vizuri na kukumbuka tukio lililokuwa limetokea mchana wa siku ile.Nilikumbuka kwamba Emmy alinipiga na chupa ya mvinyo kichwani iliyonipelekea kupoteza fahamu.Nilipoku

    mbuka jambo hili nikajikuta nikiuma meno kwa hasira.

    Kwa mbali nikahisi kama kitu cha baridi kikiyagusa mashavu yangu.Nikainua mkono na kuupeleka shavuni ili niweze kuona ni kitu gani kilichokuwa kimenitembelea nikakutana na kitu kama mkono wa mtu.Nikayakaza macho ili kuweza kuona vizuri zaidi nikaiona sura ya mwanamke ambaye sikuweza kumtambua kwa haraka alikuwa nani.Bado macho yangu yalikuwa yakiona vitu kama ukungu ukungu.

    “Wayne unajisikiaje? Iliniambia sauti ya mwanamke yule aliyekuwa amekaa pembeni yangu kitandani na mara moja nikaitambua sauti ile ilikuwa ni ya Clara.

    “Ouh Cla..ra ....ki….ki…kichw…kichwa kinauma sana” Nikatamka kwa taabu.

    “Pumzika Wayne.Endelea kupumzika.” Clara akasema huku akiinama na kunibusu.Nilipata faraja ya aina yake baada ya kufahamu kwamba Clara alikuwa pembeni yangu.Nilimpenda na kumthamini Clara kuliko kitu chochote kile.Clara alikuwa ndiye kila kitu kwangu kwa sasa.Ni mwanamke pekee ambaye ameweza kunirejeshea furaha ya maisha yangu ambayo sikuwahi kuipata katika siku zote nilizokuwa nimeishi na Emmy.Nilikwisha weka nadhri kwamba nitafanya kila niwezalo ili niweze kuwa na mwanamke huyu mwenye kila sifa nzuri.

    Kwa namna mikono ile laini ya Clara ilivyokuwa ikipita katika mashavu yangu nilihisi kama niko sehemu moja nzuri sana yenye upepo mzuri.Nilihisi kama vile niko katika bustani nzuri yenye wanyama na ndege wa kila aina.Nilihisi raha ya ajabu.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Picha ya Emmy ikanijia tena nikauma meno kwa hasira.Maumivu niliyokuwa nayasikia yalinizidishia hasira juu yake.Taratibu nilianza kuwa na mawazo labda Emmy ana matatizo ya akili kwa sababu vitendo anavyovifanya haviendani kabisa na mtu mwenye akili ya kawaida.Nilikubaliana na mawazo yangu kwamba yawezekana kabisa Emmy akawa na matatizo ya akili.Sijawahi kumtendea kitu chochote kibaya lakini yeye amekuwa mstari wa mbele sana katika kupambana na mimi kila kukicha.Amekuwa akinisababishia maumivu makali kila uchao.

    “Nahitaji kumuepuka huyu mwendawazimu Emmy kwa sababu bila hivyo anaweza akanitoa uhai.Nahitaji sana kuwa mbali na Emmy kwa namna yoyote ile kwa sababu nisipofanya hivyo anaweza hata akamdhuru Clara.Huyu mwanamke anaonekana kabisa ana mapungufu ya akili.Sitaki kumuona tena Emmy katika maisha yangu” Nikawaza na kuyafumba macho yaliyokuwa mazito nikalala.

    ************************

    Nilifumbua macho na kwa sasa niliweza kuona vizuri. Miale ya jua iliyokuwa ikipiga ukutani kupitia dirishani iliniashiria kwamba jua lilikuwa likielekea kuzama.Taratibu nikainua kichwa changu na kisha nikakaa kitandani.Nilikuwa katika chumba cha peke yangu na hakukuwa na mtu yeyote mle chumbani.Katika meza ndogo iliyokuwa pembeni ya kitanda niliiona saa yangu ndogo ya mkononi.Nikanyoosha mkono nikaichukua na kutazama muda.Ilipata saa kumi na mbili kasoro dakika kadhaa.Bado niliendelea kusikia maumivu makali ya kichwa katika ile sehemu niliyokuwa nimepigwa na chupa.Nikainama na kutafakari kwa kina juu ya mwisho wangu na Emmy.

    “Kama nisipochukua hatua za haraka anaweza akaniua huyu mwanamke.Lazima nimuepuke haraka sana.” Nikawaza na mara mlango ukafunguliwa akaingia daktari .

    “Unajisikiaje Wayne? Akaniuliza yule daktari

    “najisikia vizuri japokuwa bado nasikia maumivu makali sana kichwani” nikamweleza daktari

    “Pole sana.Yule mwanamke hakuwa na nia njema na wewe.Una bahati sana kwamba jeraha halikuweza kuingia ndani sana vinginevyo tungekuwa tunaongea mambo mengine sasa hivi.” Daktari akanieleza huku akinifanyia vipimo.Nilikosa neno la kumjibu kutokana na hasira nilizokuwa nazo juu ya Emmy .

    “Wayne unaendelea vizuri sana na hatuna sababu ya kuendelea kukuweka hapa hospitali.Unaweza ukarejea nyumbani kwako lakini utaendelea kuja hapa kwa ajili ya kusafisha na kufunga kidonda chako.Kuna kitu kimoja ambacho ninataka kukuasa kama mwanaume mwenzangu ni kwamba jaribu kuwa makini sana na huyu mwanamke aliyekusababishia jeraha hili kwa sababu inaonekana wazi alikuwa na lengo la kukuua.Sehemu aliyokupiga si sehemu nzuri hata kidogo.”

    “Nitajitahidi daktari .Nashukuru sana “ nikasema .

    “Nimekwisha mtaarifu rafiki yako Clara na tayari amekwenda dirishani kulipa gharama zote pamoja na kuchukua dawa ambazo utakuwa ukizitumia”

    “Nashukuru sana daktari “ Nikasema na kisha daktari yule akatoka mle chumbani.Dakika mbili baada ya daktari kuondoka mle chumbani nilimokuwa nimelazwa mlango ukafunguliwa akaingia Clara.Akatabasamu baada ya kuniona nikiwa nimekaa kitandani.Katika bega lake la kushoto alikuwa amefungwa bandegi.

    “Ouh Wayne..Unajisikiaje mpenzi wangu? Akauliza Clara huku akikaa kitandani karibu yangu na kunibusu

    “Ninajisikia vizuri Clara ila kichwa ndiyo bado nakisikia kinauma sana huu upande wa nyuma” Nikasema

    “Pole sana Wayne.Nashukuru sana kukuona unaendelea vizuri .Nilikuwa na wasi wasi mwingi kwa sababu sehemu aliyokupiga Emmy ni sehemu mbaya sana na ambayo inaweza kusababisha mtu akapoteza uhai wake.” Akasema Clara

    “Hata daktari amenieleza kwamba mahala hapa Emmy aliponipiga na chupa ni pabaya sana. Mbona bega lako limefungwa bandeji? Nikauliza

    “baada ya kukupiga na chupa kichwani ulianguka ukapoteza fahamu na damu kuanza kukutoka,ikanilazimu kurejea ndani kwa dhumuni la kukusaidia na ndipo hapo nilipokutana na Emmy akiwa na kisu mkononi akataka kunichoma nacho nikawahi kumdhibiti na akafanikiwa kunikata bega.Nilikimbia nje nikaomba msaada wa majirani ambao walifika mara moja na kumkamata Emmy kisha kwa pamoja tukaelekea polisi ambako aliwekwa rumande hadi hapo utakapopona ili aweze kufikishwa mahakamani.

    Wayne nina wasi wasi mkubwa kuhusu Emmy.Sina hakika kama atakuwa mzima wa akili.Nina wasi wasi anaweza akawa na matatizo ya upungufu wa akili.” Clara akasema

    “hata mimi nimekuwa nikiwaza hivyo kwa sababu vitendo anavyovifanya Emmy haviendani kabisa na vitendo vya binadamu wa kawaida.Nashukuru sana kama tayari anashikiliwa na vyombo vya dola.Mwanamke yule hafai kabisa kukaa katika jamii iliyostaarabika.Nitahakikisha anafungwa na kuozea gerezani.Sintaw

    eza kumsamehe kamwe kwa hili alilolifanya.Pamoja na hayo nimefikiria kwa sasa itanibidi kuishi mbali naye.Nitajitahidi kumuepuka Emmy kwa gharama zozote zile.Kama nikiendelea kukaa hapa karibu naye iko siku atanitoa uhai wangu” Nikamweleza Clara ambaye bado alikuwa amekaa kitandani karibu yangu akinitazama kwa huruma

    “Wayne nilikwisha fanya maamuzi ya kuachana nawe na kuondoka zangu lakini kwa kitendo alichokifanya Emmy kimenifanya niogope kukuacha peke yako.Nina hakika mwanamke huyu hana nia njema nawe.Iko siku atakufanyia jambo baya sana .Siwezi kuondoka na kukuacha peke yao Wayne.bado nakupenda na nitakuwa nawe siku zote. Sikuachi tena mpenzi wangu” Clara akasema na kunikumbatia.Siwezi kuelezea ni jinsi gani nilivyopatwa na furaha ya ghafla kiasi kwamba sikuhisi hata maumivu ya kichwa tena.

    “nashukuru sana Clara kwa uamuzi wako wa kubaki nami.Hata mimi sikuwa tayari kukupoteza kirahisi rahisi namna hii kwa sababu ya mwanamke mwendawazimu kama Emmy.Nakuahidi nitakuwa nawe siku zote na sintakubali yule kichaa akuguse tena.Safari hii nimedhamiria kumfundisha adabu.na kama anahitaji kuufahamu ubaya wangu basi ajaribu kunifuatilia tena.Iwapo atanifuata fuata tena sintakuwa na huruma kwake hata kidogo.” Nikasema na kumfanya Clara atabasamu.

    “Wayne muda unakwenda kwa kasi .Jiandae ili tuweze kuondoka hapa hospitali kwa sababu daktari amekwisha toa ruhusa” Clara akasema huku taratibu akinishika mkono na kunishusha kitandani.Akanisaidia kuvaa nguo zangu halafu taratibu tukatoka pale hositali na kuondoka.Sikutaka kwenda na Clara nyumbani kwangu tena kwa kuepusha mtafaruku mwingine.Niliichukia mno nyumba ile licha ya kwamba ni nyumba yangu mwenyewe.Badala yake tulikwenda kuchukua chumba hotelini ili tupumzike kwa usiku mmoja kabla ya kupanga nini kinaendelea.



    Ni usiku wa saa saba.Chumba kilikuwa na mwanga mdogo uliotoka katika taa iliyokuwa pembeni ya kitanda.Muziki laini wa ala ulikuwa ukisika kwa mbali.Clara alikuwa amekiegemeza kichwa chake karibu na kifua changu huku mkono wake mmoja ukinichezea kifuani.Sikuhisi tena maumivu ya kichwa.Nilisikia raha ya ajabu mno.

    “Wayne umefikiria kufanya nini ili kujiepusha na kadhia zisizokwisha za Emmy? Clara akauliza kwa sauti ndogo

    Nikamtazama usoni mrembo yule mwenye uzuri uliotukuka nikanyoosha mkono na kuzishika nyewe zake ndefu

    “Nimefikiria kuachana naye kisheria.Nina maana kwamba nitampa talaka yake mahakamani ili hata sheria isimtambue kama mke wangu halali.”

    “Unadhani atakubaliana nawe kuhusu suala la talaka?

    “Hayo ni mamuzi yangu na ni lazima ayakubali.Hii ndiyo njia pekee ya kuweza kuachana naye.Bila hivyo atanisumbua sana kwa sababu kisheria bado anatambulika kama mke wangu halali wa ndoa.”

    Clara akaniangalia kwa makini usoni kisha akasema

    “Wayne pamoja na mambo yote aliyoyafanya Emmy kuna kitu kimoja nataka kukuomba”

    “Sema chochote Clara nitakupatia” nikamwambia na kumfanya atabasamu

    “Naomba kesho ukamtoe Emmy polisi na ufute kesi inayomkabili”

    Nilistushwa sana na ombi lile la Clara ikanilazimu kuinuka na kukaa kitandani na kumtazama kwa makini

    “Unasema nini Clara !! Nikauliza

    “Nasema hivi naomba kesho ukamtoe Emmy polisi na ufute ile kesi .Usipofanya hivyo anaweza akafungwa gerezani”

    Nilishindwa nimjibu nini Clara ikanilazimu kucheka kidogo

    “Usicheke Wayne.Kweli ninaomba ukamtoe na ufute ile kesi”

    “Clara ninacheka kwa sababu hilo ni jambo ambalo haliwezekani hata kidogo.Mimi ninataka afungwe tena kifungo kirefu gerezani kwa sababu ndiko mahala pekee anakostahili kuwepo,Mwanamke baradhuli yule anastahili kifungo gerezani.” Nikasema nikiwa na uchungu mwingi nikikumbuka kila jambo ambalo Emmy amenifanyia.

    “Wayne nafahamu ni jinsi gani Emmy alivyokuumiza moyo wako.Nimekuwa nawe kwa kipindi hiki kifupi na nimeyashuhudia mambo ya Emmy.Amenitukana na kuniumiza sana lakini pamoja na hayo yote aliyoyafanya bado moyo wangu unakuwa mzito sana kuacha afungwe gerezani.Sielewi ni kwa nini imenitokea hivi .Namuonea huruma sana .Wayne sintakuomba kitu kingine chochote zaidi ya hiki.Naomba umsaidie Emmy aweze kutoka “

    Niliinama nikatafakari kwa muda.Nilimshangaa sana Clara kwa uamuzi ule.Niliyatazama macho yake wakati akiongea na nilihakikisha kwamba alikuwa akimaanisha kile alichokisema.Lengo langu lilikuwa ni kuhakikisha kwamba Emmy anafungwa gerezani na hivyo kuniachia uhuru wa kujivinjari na malaika wangu Clara.Kitendo cha kumfutia kesi Emmy kingemfanya aendelee kuniandama kila kukicha na kunifanya niishi maisha ya ndege.

    “Unaniahidi nini Wayne? Clara akaniuliza tena na kunistua toka mawazoni

    “Ok ! kwa vile ni wewe umeomba basi nitafanya hivyo.Tutakwenda sote kesho kumtoa Emmy na kuifuta kesi.Baada ya hapo nitawakusanya wazee na kuwataarifu rasmi kuhusu azma yangu ya kuachana na Emmy kisheria na kisha nitaanza kushughulikia taratibu zote za kumuacha kisheria.Ila napenda kukuonya kitu kimoja kwamba Emmy ana roho ya kikatili sana,si mtu wa kuonea huruma hata kidogo.”

    “Ouh ! Wayne thank you so much my love.Umenifanyia kitu kikubwa sana.Maandiko yanatufundisha kwamba tuwe na moyo wa kusamehe.Mimi nimemsamehe Emmy “ Clara akasema huku akiiweka mikono yake yote miwili kifuani Nilisikitika sana kwa Clara kuwa mwepesi vile wa kumsamehe Emmy.hakuwa akimfahamu Emmy kiundani.Emmy hakuhitaji msamaha.Emmy alikuwa na roho ya kinyama sana.

    ***********************

    Saa tatu za asubuhi siku iliyofuata ilitukuta tayari tumekwisha wasili katika kituo cha kati cha polisi.Tulienda kushughuikia kufuta kesi ya Emmy kama Clara alivyokuwa ameomba Haikuwa kazi rahisi sana kufanya hivyo hasa ukizingatia ukubwa wa kosa alilolifanya Emmy ambalo lingeweza hata kusababisha kifo.Tulihangaika sana na mpaka ilipotimu saa saba za mchana ndipo tulipofanikiwa zoezi letu la kuifuta kesi na kumtoa Emmy .

    Hakutaka kuongea nasi badala yake aliponiona nimesimama na Clara alituangalia kwa chuki ,akasonya na kupiga hatua kuondoka maeneo yale

    “Clara nilikwambia huyu mwanamke ni shetani.Ona dharau anazozionyesha.hata shukrani hana.Hakukuwa na sababu yoyote ya kumuonea huruma.Tulitakiwa tumuache kwanza aende jela ili akajifunze adabu.” Nikasema nikiwa na hasira

    “Usijali Wayne.Asikuumize kichwa Pamoja na dharau zote alizozionyesha lakini nashukuru kwa kuwa moyo wangu una amani .Najisikia furaha sana kwa Emmy kutoka.Nashukuru sana kwa jambo hili.Usiumize kichwa kwa suala hili.twende tukapumzike kabla hujakutana na wazee jioni ya leo” Clara akaniambia huku amenishika mkono.Tukawaaga maafisa wa polisi waliokuwa wametusaida kulifanikisha jambo lile ambao kila mmoja alishangaa kwa namna Emmy alivyoondoka kwa dharau pale kituoni.Kisha maliza kuagana ,tukaingia garini na kuondoka zetu kurudi hotelini kupumzika ..

    saa kumi na moja za jioni tayari nilikwisha jiandaa kuelekea katika kikao kinachofanyika nyumbani kwa wazazi wa Emmy.Clara alikuwa ameniomba kuongozana nami akiwa na wasi wasi kwamba pengine Emmy anaweza akanifanyia vurugu..Kutokana na mambo aliyonifanyia Emmy sikuwa na hamu hata ya kuiona nyumba yangu tena.Nyumba ambayo kwa miaka mingi imekuwa ni sehemu ya maisha yangu leo hii niliiona ya moto na sikuwa radhi hata kutia mguu ndani yake.Kabla sijaingia katika ndoa nilikuwa nikisikia toka kwa watu mbali mbali au kupitia nyimbo na simulizi mbali mbali kwamba kuna nyakati ndoa hubadilika na kuwa ndoano.Sikuelewa usemi huu ulimaanisha kitu gani hadi yalipokuja kunikuta ndipo nilipotambua maana ya usemi ule.Ndoa ni tamu kama ukimpata mtu aliye sahihi lakini ukimpata ambaye si sahihi ndoa huchacha na hupoteza utamu wake wote na hutatamani kuisikia tena maishani mwako..

    “You look so nervous” akasema Clara wakati akijifunga mkanda na kunistua toka mawazoni.Nikageuza shingo na kumtazama ni katabasamu

    “Yah..I’m a bit nervous .Nimekwisha choka kabisa na maisha haya ya vurugu kila kukicha.Nataka kuishi maisha ya amani na furaha .Najaribu kutafakari ni lini mambo haya ya vurugu na chuki yatakwisha na nikawa huru” Nikasema taratibu

    “Usife moyo Wayne,mambo haya yatakwisha tu.Mungu atakusaidia.” Akasema Clara huu amenishika bega

    “Yah ..nadhani kuanzia jioni ya leo nitakuwa na uhuru na amani.” Nikasema na kuinama chini.Clara akanitazama na kusema

    “Wayne sidhani kama litakuwajambo la busara mimi kwenda pamoja nawe.Yule mwanamke anaweza akanitolea maneno machafu na nikashindwa kuvumilia halafu tukaanzisha zogo mbele ya wazee.Sitaki jambo hilo litokee.Mimi naona ni bora kama nitabaki hapa hapa hotelini “ akasema Clara.Nikafikiri na kuona maneno yake yana busara kwa sababu Emmy ni mwanamke mwenye tabia chafu sana na hasiti kumtukana mtu yeyote hata mbele ya wazazi wake.Nisingeweza kuvumilia kuona Clara akitukanwa na Emmy na hivyo nikaona ni bora abaki.

    “Sawa Clara.Hilo ni jambo la msingi sana.Ngoja niende mimi peke yangu nitahakikisha kila kitu kinakwisha leo mbele ya wazee.Mwanamke yule ni nusu kichaa na kama ulivyosema anaweza akakukutukana mbele za wazee kitu ambacho siwezi kukivumilia .” Nikasema na kumvutia Clara kwangu nikambusu

    “Nakutakia kila la heri mpenzi wangu.Mambo yote yatakwenda sawa.Usiwe na hofu hata kidogo” akasema Clara akiwa amekiegemeza kichwa chake kifuani kwangu

    “Thank you so much my angel.I love you”Nikasema na kumbusu tena

    “I love you too Wayne.Drive safe” akasema Clara nikashuka na kumfungulia mlango akashuka akanibusu tena na kisha akaanza kutembea kuelekea hitelini.Nilisimama kwa muda huku nikitabasamu nikimuangalia malaika huyu akitembea kwa madaha ule mwendo wanaopenda kutembea wanamitindo wengi.

    “Ee Mungu nakushukuru kwa kuniletea mrembo huyu .Kwa kuwa naye ninajihisi kama ninaishi tena.Baada ya Emmy kunitenda nilijiona kama mfu.I felt dead but now I feel life.” Nikaomba kimoyomoyo kisha nikaingia garini.

    “Ninampenda Clara toka moyoni.Kwa mara ya kwanza ninahisi kupenda toka moyoni.Hata Emmy sikuwahi kumpenda kama ninavyompenda Clara.” Nikawaza nikiwa

    garini kuelekea nyumbani kwa wazazi wa Emmy katika kikao.

    “Leo ni mwisho wangu na Emmy.Nataka akome kabisa kunifuatilia na aniache niishi maisha yangu kwa amani na Clara.Najuta sana kufahamiana na Emmy.Nimepoteza muda mwingi nikitegemea nina mtu maishani kumbe nilikuwa naishi na shetani ndani.Mwanamke yule hafai kabisa kuwekwa ndani kama mke, na kwa vituko alivyonifanyia hakuna mwanaume yeyote duniani ambaye anaweza akamvumilia.Kweli nimeamini si kila mwanamke anafaa kuwa mke.Namsikitiki

    a sana Baraka.Mtoto yule mpaka sasa hivi hajui aelekee wapi,hamfahamu baba yake ni nani.Toka amezaliwa alijua kwamba mimi ni baba yake mzazi.baadae amekuja kuambiwa kwamba baba yake ni Chris na sasa anaambiwa tena kwamba Chris si baba yake.Mtoto huyu lazima ameathirika kisaikolojia na maisha yake lazima yatayumba sana.Damn you Emmy ! “ Nilishikwa na hasira za ghafla baada ya kufikiria kuhusu mateso na machungu aliyonayo mtoto Baraka.

    ************************

    Niliwasili nyumbani kwa wazazi wa Emmy nikapokelewa na baba yake Emmy .Mara Baraka akaja akikimbia na kunikumbatia.Akanisalmu.Nilishindwa kuyazuia machozi kunidondoka baada ya kumuona Baraka.Nilimpenda sana mtoto huyu ,niliamini yeye ndiye maisha yangu .Hata baada ya kugundua kwamba si mwanangu Baraka ameendela kuwa sehemu ya moyo wangu.Namuwaza kila dakika ya maisha yangu tatizo ni kwamba mama yake amekuwa hataki kabisa Baraka akaribiane nami.Nilimshika Baraka na kukumbuka mbali sana jinsi nilivyokuwa nikiishi naye kama mwanangu.

    Baada ya maongezi mafupi na baba mkwe pale nje akanikaribisha sebuleni ambako kulikuwa na watu ambao kwa hesabu ya haraka haraka hawakupungua thethili.Wengi walikuwa ni wazee wa heshima.Niliwasalimu wote kwa pamoja na kisha nikaelekezwa mahala pa kukaa nikapatiwa kinywaji.Dakika kama nane hivi toka nimewasili pale ndani Emmy akaingia .Alikuwa amevaa miwani mikubwa kuyafunika macho yake ,akawasalimu watu wote mle ndani na kisha akatoka nje ambako alikuwa na maongezi kidogo na baba yake Mama yake Emmy hakuonekan akujishughulish

    a na suala lolote kuhusiana na Emmy,yeye alikuwa amekaa pamoja na akina mama wengine wakiongea na kucheka pale sebuleni .

    Emmy na baba yake wakaingia tena sebuleni na Emmy akaenda kukaa pembeni ya zuria walilokuwa wamekalia akina mama.Baba yake akanong’onezana jambo na mzee mmoja mwenye mvi nyingi na kisha akakohoa kidogo na kusema

    “Ndugu zanguni napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisheni sana katika kikao hiki cha dharura.Wengi mmepata taarifa kwa kuchelewa na ninashukuru sana kwa kuweza kufika.Ni mzee Mmasi pekee ambaye bado hajafika mpaka mida hii lakini nina imani atakuwa njiani kwani alinihakikishia kwamba lazima atafika.Ndugu zangu najua mtakuwa mkijiuliza sana kuhusu dhumuni la kuitana hapa mida hii.Kwa ufupi tu ninaweza kusema kwamba watoto wetu hawa wawili Wayne na Emmy wana matatizo katika ndoa yao Nadhani nyote mmekwisha yasikia sina haja ya kuyarudia tena hapa.Mgogoro huu umekuwa ukichukua sura mpya kila kukicha.Leo linazuka hili ,kesho linazuka lile ilimradi kila siku kumekuwa na matukio .Ndoa ya watoto wetu naweza kusema kwamba imepapigwa na dhoruba kali na sijui kama inaweza ikahimili dhoruba hilo.Nasikitika sana kwa sababu ni mapema sana kwa wao kuingia katika matatizo makubwa ya namna hii.Kutokana na hali kuendelea kuwa mbaya kila kukicha kijana Wayne aliniomba niitishe kikao cha wazee akadai kwamba kuna jambo anataka kutueleza.Yeye wazazi wake wako mbali kwa maana hiyo sisi tuliopo hapa tunasimama kama wazazi wake na wazazi wa Emmy.Naombeni tumsikilize kijana wetu kwa analotka kutueleza.Karib

    u sana Wayne.” Akasema baba mkwe na kunikaribisha.Nikasimama na kuwasalimu tena wazee wale kwa mara ya pili.

    “Wazee wangu napenda kutoa shukrani zangu za dhati sana kwa kuahirisha shughuli zenu mbalimbali na kufika hapa kunisikiliza mimi kijana wenu.Kama baba mkwe alivyowadokeza ni kweli kwamba ndoa kati yangu na mwenzangu Emmy Imepigwa na dhoruba kali sana na ninaweza kusema kwamba imeshindwa kuhimili dhoruba hilo na sasa inaelekea kuzama baharini “ Nikanyamaza na kuwatazama wazee wale waliokuwa kimya kabisa wakinisikiliza.Emmy alikuwa ameinama akichezea simu yake.Sikumjali nikaendelea.

    “Nina hakika nyote mtakuwa mnafahamu au mmesikia mambo yaliyoipata ndoa yetu.Kwa kweli ni mambo ya aibu na nisingependa kuendelea kuyaongelea hapa kwa sababu yanafahamika kwa kila mtu.Labda kwa kuweka kumbu kumbu sawa na kwa faida ya wale ambao hawakuwa wakifahamu kilichotokea ni kwamba baada ya miaka kadhaa ya ndoa yetu niligundua kwamba mwenzangu hakuwa mwaminifu katika ndoa yetu.Niligundua kwamba mtoto ambaye siku zote nilikuwa nikiamini na kumpenda kama mwanangu si mtoto wangu.Nililigundua hilo baada ya kunasa mawasiliano kati ya Emmy na rafiki yangu wa karibu sana aitwaye Chris nafikiri wengi mnamfahamui kwa sababu ndiye aliyeisimamia harusi yetu.Mke wangu Emmy na Chris walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na kwa mujibu wa mawasiliano niliyoyanasa Chris alidai mtoto Baraka ni wake.Awali sikuliamini suala hilo nikafanya uchunguzi na kugundua kwamba ni kweli Chris na Emmy ni wapenzi.Ili kujiridhsha zaidi ikanilazimu kutumia kipimo cha DNA ili kuhakiki kama Baraka ni mwanangu na kipimo kikaonyesha kwamba Baraka si mwanangu .Nilipotoka katika vipimo nilimkuta mwanzangu tayari amekwisha hama nyumbani.Nilimtaarifu baba mkwe na kwa msaada wake tukafanikiwa kwenda hadi kwa huyo Chris ambako ndiko Emmy alikwua amehamia na kumkabidhi mwanae ili amlee.Hivi majuzi nikiwa Zanzibar nilipigiwa simu na Chris ambaye alikuwa akiishi na Emmy kwa wakati huo akaniambia kwamba yeye na Emmy wametengana baada ya kugundua kwamba Emmy amekuwa akimdanganya na yule mtoto Baraka si wa kwake pia.Baada ya kuachana na Chris,Emmy hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda ikamlazimu kurudi katika nyumba yangu..” Ghafla nikakatizwa na sauti ya juu ya Emmy



    “Wewe mwanaume ukome kusema ile ni nyumba yako.Pale ni kwangu.Tumejenga wote na nina uhuru wa kuingia pale muda wowote ninaotaka.Mbona unakwepa kusema ulikuwa Zanzibar na Malaya wako? Sema ukweli watu wote wakusikie..” akasema Emmy kwa sauti kali

    “Emmy naomba uwe na adabu mbele ya wazee wako.Naomba ukae kimya hadi utakaporuhusiwa kuongea” baba mkwe akasema kwa ukali

    “baba mnamsikiliza sana huyu muongo mkubw………..”akasema Emmy lakini akazuiwa ghafla na baba yake aliyeinuka kwa hasira

    “kelele !! nitakunasa vibao sasa hivi ..” Baba mkwe akawa mkali na kuinuka kutaka kumfuata Emmy pale chini alipouwa amekaa lakini akazuiwa na wazee wenzake.

    “Hapa ni nyumbani kwangu na ni mimi ndiye mwenye amri nani aongee ndani ya nyumba hii.Kama ni huo ufidhuli wako ni huko huko mtaani na si hapa.Wayne endelea” akasema baba mkwe nikakohoa kidogo na kuendelea.

    “Baada ya kusikia kwamba Emmy amerudi nyumbani kwangu ikanilazimu kurejea Arusha mara moja kwa sababu nilitaka kufahamu ni kitu gani kilichomrudisha kwangu baada ya mambo yote aliyonifanyia.Nikiwa nimeongozana na rafiki yangu niliyekuwa naye Zanzibar Emmy alinitukana sana na kunitolea vitisho nikaamua kuondoka.Kabla sijaufungua mlango akanipiga na chupa kichwani nikapoteza fahamu .Namshukuru sana rafiki yangu huyo niliyekuwa naye kwani ni yeye ndiye aliyekimbia na kuwaita majirani ambao walinikimbiza hospitalini na Emmy akakamatwa akapelekwa polisi.Baada ya kutibiwa nikatoka hospitali .Kwa kumuonyesha kwamba mimi si mtu mkatili kama alivyo yeye imenilazimu kwenda polisi na kufuta kesi iliyokuwa ikimkabili.Baada ya hapo nikaona niwaite wazee wangu ili niwaeleze kwa ufasaha nini kinachoendelea kati yangu na Emmy” Nikanyamaza na kumeza mate.Mara mzee mmoja akaniuliza swali

    “Huyu rafiki yako unayesema kwamba ulikuwa naye Zanzibar ni nani? Kwa sababu tumemsikia mwenzako hapa akimlalamikia”

    “Huyu rafiki yangu anaitwa Clara.Ni mtanzania ambaye anaishi na kufanya kazi nchini afrika ya kusini.Nilikutana naye hapa hapa Arusha siku kadhaa zilizopita .Ni yeye ndiye aliyenisaidia katika kuyatenegeza upya maisha yangu yaliyokuwa yameharibika.Ni yeye ndiye alinifanya nijione kama mtu ninayeishi tena baada ya kukata tamaa na maisha haya kutokana na vituko vya Emmy.Huyo ndiye niliyekuwa naye Zanzibar na huyo ndiye aliyenipeleka hospitali baada ya Emmy kunipiga na chupa kichwani.” Nikasema na kuwafanya wazee wote mle sebuleni kutikisa vichwa vyao kukubaliana nami.Nikaendelea

    “Wazee wangu mahala nilikofika mimi na mwenzanu ni pabaya kwa sababu tumefikia mahala pa kuhatarisha uhai wetu.Kwa hatua tuliyofikia naweza kukiri kwamba hakuna namna tunayoweza kufanya ili kuweza kutuweka tena pamoja.Hapa nina maana kwamba kuishi pamoja kati yangu na Emmy haiwezekani tena na kwa maana hiyo basi ninaomba kuchukua nafasi hii kuweka wazi kwamba nimefikia uamuzi wa kuachana na Emmy rasmi.” Nikanyamaza na kuyaacha maneno yale niliyoyaongea yaweze kuingia masikioni mwao kisha nikaendelea

    “ Nimeamua kuachana na Emmy.na kila mmoja aendelee kuishi maisha yake.Nimeona niwafahamishe kwanza wazee wangu ili muweze kufahamu na msishangae mtakapolisikia shauri hili mahakamani.Nitafuata taratibu zote za kisheria za kutoa talaka.Jambo jingine ambalo nataka kuliweka wazi kwenu ni kwamba hata kama sheria itatutaka tugawane mali zote sawa kwa sawa lakini mimi ninamuachia mwenzangu kila kitu tulichonacho.Ninamuachia nyumba zetu mbili,magari yetu mawili,maduka yetu ya nguo pamoja na duka kubwa la vipodozi.Mimi ninaondoka na nguo zangu tu.Sitaki kuwa na kitu chochote kitakachonikumbusha kuhusu Emmy.Nataka kuyaanza maisha mapya kabisa yenye amani ya moyo.Kwa hiyo wazee wangu nimeona niwataarifuni kwani tayari mwanasheria wangu amekwisha anza kulishughulikia kisheria suala la kuachana kwetu.Ni hayo tu niliyotaka kuwafahamisha.Ahsanteni sana” Nikasema na kukaa chini.Watu walikuwa wakijifuta majasho .Kila mmoja aliuona ugumu wa suala hili.Baba yake mkubwa Emmy akakohoa kidogo na kusema.

    “Wayne tumekusikia na kukuelewa. Mambo uliyotueleza ni makubwa na ninapenda kukupa pole sana kwa matatizo yote yaliyokupata ndani ya ndoa yenu.Hiyo ndiyo mikiki mikiki ya ndoa ambayo tunakutana nayo.Usituone sisi tumeishi na ndoa zetu hadi tumekuwa wazee namna hii,tumepitia mambo mengi sana lakini tulisimama imara na ndiyo maana mpaka leo hii bado tuko na mama zenu.Pamoja na yote yaliyotokea bado nina imani lazima iko fursa ya majadiliano kati yetu na nyie ili kujaribu kuzuia ndoa hii isianguke. Bado kuna uwanja mpana sana wa majadiliano na mambo haya yote yanaweza yakasawazishwa na mkaendelea kuishi kwa amani.Mnapitia katika kipindi kigumu cha majaribu na ambacho lazima msimame imara ili msije mkaanguka.Mimi napendekeza yafanyike maongezi.Sisi wazee tupo hapa na hakuna chochote kinachoweza kuharibika.Tutawasuluhisha na mtaendelea kuishi kwa amani katika ndoa yenu.Hakuna binadamu mkamilifu.Sisi sote tuna mapungufu yetu.Au mnasemaje wazee wenzangu? Akasema baba yake mkubwa na Emmy.Wazee wote mle ndani wakamuunga mkono isipokuwa baba mkwe yaani baba yake Emmy.Nilimshangaa sana mzee yule kwa mawazo kama yale hata baada ya kusikia vituko alivyokuwa akivifanya Emmy.Wakati wakiendelea na mjadala wa chini chini Emmy akasimama

    “Wazee wangu naomba mnipe nafasi na na mimi niseme ya kwangu.Huyu mwanaume ni mlaghai na ni yeye ambaye amekuwa si mwaminifu.Mara nyingi tu nimemfuma na wanawake kibao .Sasa nasema hivi mimi sina maneno mengi ya kusema.kwa sababu yeye amekwisha sema kwamba amefikia mwisho mimi siwezi kumlazimisha na wala sitaki kuendelaa kuishi naye.Yeye aniache huru niishi maisha yangu na yeye akaendelee na maisha yake na wanawake zake.Sitaki usuluhishi wa namna yoyote ile na huyu mwanaume.Nakwambia hivi Wayne ukitaka usiende hata mahakamani na kupoteza wakati wako.Wewe ondoka zako na ukaishi na huyo Malaya wako.Mimi sintakufuatilia tena na ninaomba usinifuatilie katika maisha yangu.Sahau kama mimi na wewe tuliwahi kulala kitanda kimoja.Lakini nakuapia kwamba iko siku moja utakuja kunipigia magoti kunguru wewe” akasema kwa kiburi Emmy na kuondoka kwa kasi mle sebuleni akapanda gari lake na kuondoka.

    “Jamani mmeona kiburi cha huyu mtoto? Mmeona mtoto alivyo shetani huyu? “ akasema baba mkwe.Babamkubwa wa Emmy akitikisa kichwa.na kusema

    “Sikujua kama Emmy amebadilika na kuwa na kiburi namna hii.Emmy niliyemfahamu mimi si Emmy huyu niliyemuona dakika chache zilizopita.Nilihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    fanya makosa makubwa sana kutaka kumtetea ili aweze kurudiana na mumewe.Kwa hatua aliyofikia tayari ameshindikana kabisa.”

    Baba mkwe akasimama na kusema

    “wayne wewe ni kijana wetu ,tunakupenda sana.Wewe ni kijana ambaye ninaweza kusema kwamba ni wa pekee kabisa.Kwa mambo aliyoyafanya Emmy ingekuwa ni mtu mwingine saa hizi tungekuwa tukiongea mambo mengine ,lakini wewe umevumilia mambo yote.Nimekuwa nawe toka mwanzo wa vituko vya huyu mtoto na ninafahamu ni uchungu kiasi gani aliokusababishia.Kwa hapa ilipofika mimi nakubaliana nawe kabisa Wayne kwamba imetosha.Achana na Emmy.Sisi kama wazi tunakupa baraka zote na tunakuombea kwa Mungu ili aweze kukupa furaha na mafanikio katika maisha yako mapya.Huyu mwana kulaanika atafundishwa na ulimwengu.Una baraka zote toka kwetu wazazi na endelea na taratibu zote za kisheria ili sheria isiendelee kumtambua kama mke wako. Kwa sababu kuna uwezekano mkubwa akaja kukusumbua sana siku za usoni.Mimi sina mengi ya kusema zaidi ya kukutakia baraka nyingi na Mungu akutangulie katika kila jambo unalolifanya.Hapa bado ni nyumbani kwako na siku zote unakaribishwa .Sisi bado ni wazee wako na siku zote ukipatwa na tatizo lolote lile usisite kututaarifu na tutakupatia kila aina ya msaada unaouhitaji” akasema baba mkwe.Ninampenda sana mzee huyu kwa sababu ni mzee mwelewa na siku zote amekuwa upande wangu.Niliwashukuru wazee wale ambao waliniasa mambo mengi sana .Ilipofika saa nne za usiku nikawaaga na kuondoka kurejea hotelini kuonana na barafu wa moyo wangu Clara nikiwa ni mwingi wa furaha nikiamini kwamba Emmy hatanisumbua tena maishani.Nikiwa njiani nikapokea ujumbe mfupi wa maandishi katika simu yangu

    “Mapambano bado yanaendelea.Huu si mwisho wako.Your life will be a living hell” Nilihisi moja kwa moja ujumbe ule ulitoka kwa Emmy.Nikaupuuza na kuufuta katika simu yangu

    “Its your turn to get pain Emmy…anza kujiandaa” Nikasema taratibu nikiwa na tabasamu usoni.

    Nilifika hotelini na kumkuta Clara barafu wa moyo wangu akinisubiri kwa hamu kutaka kufahamu kilichojiri katika kikao kile.Alikuwa na wasi wasi mwingi.Aliponiona tu alinikumbatia kwa nguvu na kunipa mabusu kemkem.Sikuwahi kufanyiwa hivi na Emmy katika miaka yote niliyoishi naye.Nilizidi kumshukuru Mungu kwa zawadi hii ya kunipatia mwanamke ambaye anafahamu mapenzi.Anajua kupenda .Nilimkumbatia Clara kwa mahaba mazito ,nikafumba macho na kupumua kwa nguvu na kumshukuru Mungu kwa kuniletea malaika huyu ambaye amenifanya niifurahie dunia na kila kitu kilichomo ndani yake.Ndugu msomaji mapenzi ni matamu kama ukimpata mtu ambaye unampenda naye akakupenda na si mtu mwenye tabia kama za Emmy ambaye anaweza akakufanya ukaichukia dunia.

    “Ouh My darling..I missed you soo much “ akasema Clara na kunibusu mdomoni.

    Haraka haraka akachukua koti na kunivalisha kwani hali ya Arusha usiku huu ilikuwa ni ya kiubaridi baridi na malaika wangu hakutaka kuniona nikitetemeka kwa baridi.Baada ya kuhakikisha nimevaa koti akaleta kikombe cha kahawa

    “Karibu kahawa mpenzi wangu” akasema Clara.Nlishindwa nijibu nini,nikabaki nikitabasamu.

    “Nini..mbona unanishangaa hivyo? Akauliza Clara

    “Ninakushangaa kwa sababu kila dakika nakuona kama mpya..nakuona kama unazidi kuwa mrembo..sichoki kukutazama ..kwa jinsi ninavyosikia raha nikiiona sura yako niko tayari kukesha nikikutazama usiku kucha….” Kauli ile ikaamsha kicheko mle ndani.Clara akacheka kwa nguvu sana.

    “Enhee hebu nipe habari za huko ulikotoka” akasema Clara

    “Ulifanya jambo zuri sana kuamua kutokwenda katika kikao kile.Mwanamke yule sina hakika kama ana akili timamu.” Nikasema

    “Nilikwisha lisoma hilo toka awali na ndiyo maana nikakuomba kwamba uende peke yako.Nimekwisha usoma ubongo wa Emmy “ akasema Clara huku akitabasamu.

    “katika maisha yangu yote niliyoyaishi hapa duniani,nilifanya kosa moja kubwa sana na ambalo nitaendelea kujilaumu hadi siku ninaingia kaburini .Nilifanya kosa kubwa sana kumuoa Emmy..That’s the biggest mistake of my life” nikasema .Clara akanisogelea ,akanibusu na kusema

    “Usiseme hivyo Wayne.Sisi wote tunafanya makosa katika maisha yetu lakini tunapogundua kwamba tulifanya makosa tunajitahidi sana kutoyarudia tena.Tafadhali nakuomba usahau yote yaliyotokea na endelee na maisha yako mapya.Siku zote makosa tuliyoyafanya nyuma yanatufana tuishi maisha bora zaidi huko tuendako ..kwa hiyo usijilaumu kwa kutokufanya chaguo sahihi..I think this time you have chosen the right one…” akasema Clara akiwa karibu yangu..

    “Safari hii sikufanya chaguo mimi..bali baada ya kumlilia Mungu kutokana na shida na mateso niliyoyapata toka kwa Emmy.aliamua kunichagulia mtu yeye mwenyewe..kwa maana hiyo wewe ni chaguo langu toka kwa Mungu na siku zote huwa hakosei katika kila jambo analolitenda.Mungu ametukutanisha kwa sababu anazozifahamu yeye mwenyewe.Sikuota katika maisha yangu kama nitakuja kupata mapenzi na furaha kama niipatayo nikiwa nawe.Naona ni kama muujiza mkubwa sana ambao Mungu amenitendea.Thamani yako kwangu hailinganishwi na kitu chochote kile katika hii dunia.Hi ndiyo sababu niko tayari kwa lolote lile kwa ajili yako pekee.Nakupenda Clara.Nakupenda zaidi ya unavyofikiri..Nakupenda zaidi ya ninavyojipenda mwenyewe.nakupenda sasa na daima” Maneno yale yalimtoa machozi Clara.Ni kweli nilitamka maneno yale toka uvunguni kabisa mwa moyoni mwangu..Nilimpenda Clara kupita ninavyoweza kuelezea.

    “Maneno yako yananifanya nijione ni mwanamke mwenye bahati kubwa sana kumpata mtu anayenipenda kupita nafsi yake mwenyewe.Katika maisha yangu nimekutana na watu mbali mbali ambao wamekuwa wakijaribu kupata bahati ya kuwa na nafasi ndani ya moyo wangu.Wengi wa hao ni watu matajiri wakubwa na wenye majina makubwa lakini wote hawa walinipenda mimi kwa sababu ya jina langu kubwa ,mafanikio yangu na wengine lengo lao ni kutaka kuweka historia ya kuwa na mtu kama mimi.Sikuwa tayari kutoa nafasi kwa mtu yeyote ambaye alionekana kuwa na chembe chembe za kuvutiwa nami kutokana na aidha uwezo wangu,jina langu au uzuri wangu.Nilikwisha umizwa hapo awali na safari hii sikutaka tena kufanya makosa.Nilihitaji mtu ambaye atanipenda mimi kama Clara na si kama mrembo au mwanamitindo au tajiri.Baada ya kukutana nawe Wayne nimegundua kwamba wewe unanipenda mimi kama mimi na si kwa sababu ya uzuri,jina au uwezo wangu.Moyo wangu umekuchagua wewe kati ya mabilioni ya wanaume wa dunia hii.Nakuahdi kwamba nitakupenda na kukuenzi hadi siku naingia kaburini.Siku zote utakuwa mwanaume wa pekee ambaye umeuteka moyo wangu kwa namna ya ajabu sana kiasi kwamba umenifanya niisahau dunia..Ninajiona ni kama ninaishi katika dunia yenye watu wawili .mimi na wewe tu.Nakupenda sana Wayne na nitazidi kukupenda hadi mwisho wa uhai wangu” Clara akasema na kunikumbatia,ak

    anipiga busu zito na kukilaza kichwa chake mapajani mwangu.

    “Tuachane kwanza na hayo…niambie nini kimeendela katika kikao? Akauliza Clara.

    “Kikao kilikwenda vizuri.Wazee walihudhuria wengi..Nilianza kwa kuwapa historia nzima ya wapi nimetoka na Emmy,mambo gani amenifanyia .Niliwaeleza kila kitu bila kuwaficha vitendo vyote vichafu vya Emmy na kila mmoja alionekana kufumba macho kutokana na vitendo vya aibu alivyokuwa akivifanya mtoto wao.Mwisho nikawaeleza kwamba kutokana na hali ilivyo hivi sasa mimi na Emmy hatuwezi kupikwa chungu kimoja tena kwa maana hiyo nimeamua kuachana naye kisheria na tayari wanasheria wangu wamekwisha anza kulishughulikia suala hilo.Nikaweka wazi mbele ya wazazi kwamba ili kumfanya Emmy asiendelee kunifuata fuata katika maisha yangu ninamuachia kila kitu nilichonacho.Sihitaji kitu chochote kutoka katika mali nilizonazo.Vyote ninamuachia Emmy ili aweze kuyaendesha maisha yake kwa raha na amani bila kubughudhiwa na mtu yeyote yule.” Nikanyamaza na kumtazama Clara aliyekuwa kimya akinisikiliza.

    “Emmy akasemaje uliposema hivyo?

    “Ingawa hakusema wazi lakini nina imani moyoni mwake alifurahi sana kwani atakuwa huru sasa kufanya kila anachotaka kukifanya.Kitu cha kushangaza kwa mwanamke yule aliinuka na kuongea kwa kiburi sana na kuondoka zake kitendo ambacho kiliwaacha hoi baadhi ya wazee ambao hawajawahi kuvishuhudia vibweka vya Emmy wazi wazi.baada ya hapo kikao kikaendelea kati yangu mimi na wazee na wamenipa baraka zote za mimi kumtaliki mtoto wao na wote wako upande wangu”

    “Stupid woman…sijawahi kuona mwanamke mwenye akili mbovu kama yule.Badala ya kushukuru ameachiwa kila kitu ili aweze kuyaendesha maisha yake lakini badala yake anaondoka kwa kiburi na tambo..” akasikitika Clara

    “Nadhani sikufanya jambo baya kufanya maamuzi nliyoyafanya.Nilifanya vile ili kumuondoa kabisa katika maisha yangu na kuanza maisha mapya na kila kitu kipya.Maisha mapya,mpenzi mpya,nyumba mpya na kila kitu kipya,au unasemaje malaika wangu? Nikamuuliza Clara aliyekuwa amechanua tabasamu pana.

    “Wayne naweza kusema kwamba wewe ni mwanaume wa kipekee sana na nina bahati kubwa sana kukutana nawe.Una roho ya kipekee ambayo wengi hawana.Umefanya jambo la busara sana kumuachia kila kitu.Nyumba magari,mali pesa ni vitu vinavyotafutwa kwa maana hiyo tutaunganisha nguvu na kwa juhudi zetu tutayaanza upya maisha yetu mapya.Kitu kikubwa cha kushukuru ni kwamba roho yako iko salama salimini.Mimi niko tayari kuishi nawe hata katika nyumba ya udongo kwa sababu pesa mali na kila kitu si vitu vinavyotengeneza penzi la kweli.Niko tyari kuwa nawe katika maisha yoyote yale kwa sababu ninakupenda na kukujali.Lakini naomba nikukumbushe kwamba bado makubaliano yetu yanasimama pale pale kwamba zile fedha tulizopanga kuzipeleka katika miradi ya kijamii bado zitafanya kazi ile ile iliyokusudiwa.”

    “Usihofu kuhusu hilo Clara..makubaliano yetu hayajabadilika na kila kitu kitafanyika kama kilivyopangwa.Zile pesa zote ambazo sikuzipata katika njia zilizo halali zitarudi kwa wananchi kwa kupitia miradi ya maendeleo.” Kauli ile ikamfurahisha Clara akanivuta karibu yake na kunipa busu zito.Tuliongea mambo mengi sana siku hiyo kuhusiana na maisha yetu ya baadae hasa baada ya suala la kuachana na Emmy kisheria kukamilika.Tulipochoka kuongea tukaenda zetu kulala.



    Wakati Wayne na Clara wakiyafurahia mapenzi yao na kupanga mikakati mingi ya kufanya juu ya maisha yao ya mbele Emmy alikuwa bado amekaa sebuleni akiwa na katika meza ndogo,chupa kadhaa za mvinyo zilikuwa zimetapakaa .Kisahani kidogo kilichokuwa pale mezani kiliku kimejaa vichungi vya sigara alizouwa akizivuta kwa fujo.Toka amerudi kutoka katika kikao amekuwa hapa mezani akinywa mvinyo na kuvuta sigara kwa fujo.

    "Hatimaye niko huru sasa.Nina uhuru wa kufanya kila nilitakalo.Nina mali za kutosha kuyaendesha maisha yangu mwenyewe bila kupelekwa kama ng'ombe na mwanaume yeyote." akawaza Emmy huku akimimina mvinyo katika glasi yake akanywa funda moja na kuirudisha chini.

    " Acha ninywe ,leo ni siku yangu kubwa sana..natakiwa niifurahie.Hawa shoga zangu nimewapigia simu muda mrefu waje tusherehekee kuwa kwangu huru lakini mpaka mida hii sijawaona.Ngoja niwapigie tena simu nijue kama hawaji mimi nielekee zangu viwanjani nikale bata hadi asubuhi." akawaza Emmy huku akiichukua simu yake na kuzitafuta namba za shoga yake mkubwa Sheila.

    "We Sheila mko wapi ninyi? Mbona hamfiki? kama hamji niambieni ili nitoke zangu niende viwanjani" akasema Emmy kwa sauti ya ukali kidogo

    "Usijali shoga yangu,tunakuja sasa hivi .Gari ya Salama ilkuwa imepatwa na hitilafu kidogo ikabidi tumsubiri fundi aje arekebishe.Tuko hapa karibu na kwako.Ndani ya dakika mbili tutakuwa tumeshafika hapo nyumbani." akasema Sheila na kukata simu

    Emmy akainuka akaenda kabatini na kutoa chupa nne za pombe kali akaziweka mezani.Mara akasikia kengele ya mlangoni inalia.Akajua tayari shoga zake wamekwisha wasili.Akatoka na kwenda kufungua geti.

    "Waoohhhhh.............." Akafurahi Emmy huku akikumbatiana na shoga zake.Haraka haraka akafungua geti na gari likaingizwa ndani kisha akawaongoza rafiki zake kuelekea sebuleni

    "Nilikwisha anza kukata tamaa pengine hamuwezi kuja tena leo." akasema Emmy

    "Kwa nini tusije Emmy? Kamwe hatuwezi kufanya hivyo hata mara moja.Ulipotupig

    ia simu kuna wateja ambao tulikuwa tukimalizia kuwaremba wana sherehe yao ya kmuaga bibi harusi,tulipowa

    maliza ikatubidi kuanza moja kwa moja safari ya kuja huku.Tukiwa njiani gari ikapata matatizo ikabidi Salama amuite fundi aje arekebishe." akasema Sheila

    "Karibuni ndani shoga zangu" Emmy akawakaribisha rafikize sebuleni

    "Leo ni mwendo wa kula na kunywa hadi asubuhi.Leo ni sherehe usiku kucha" akasema Emmy akiwaonyesha rafiki zake chupa zile za pomkbe kali zilizokuwa zimepangwa pale mezani.

    "waoohhhh !! Emmy ..." akasema kwa furaha Sheila huku akikumbatiana na Emmy.

    "kuna sherehe gani leo? Salama akauliza

    " Mbona haraka hivyo ya kutaka kufahamu mambo.? Emmy akasema huku akicheka.

    "Kila mmoja achukue kinywaji anachokipenda.Tutakunywa hadi asubuhi .Katika friji kuna kuku atakayejisikia njaa atajisaidia yeye mwenyewe." Emmy akasema huku akimimina mvinyo katika glasi yake.

    " Emmy wewe ni shoga yetu lakini mbona unatuficha leo umefurahi kitu gani? Tushirikishe na sisi shoga zako ili tufurahi pamoja.Au umeshinda bahati nasibu? " akaendela kusisitiza sheila.Huku akitabasamu Emmy akasema

    "Shoga zangu leo nina furaha sana.Siwezi kuwaficha furaha niliyonayo leo.Ni sawa tu na kama nimeshinda bahati nasibu " akasema Emmy

    " Hebu tuweke wazi shosti mbona unatuficha namna hiyo? Salama akasema na kumfanya Emmy atabasamu na kusema

    " I'm a milionare "

    " What !!... a millionare? akauliza Sheila kwa mshangao

    'Yes a millionare"akajibu Emmy

    "Enhee tupe siri ya kuwa millionare...um

    eokota fedha au umempata bwana mwenye kisima cha mafuta uarabuni? Pili akauliza

    "Wayne ameamua kunipa talaka yangu kwa hiyo kuanzia sasa hivi mimi ni mwanamke huru" akasema Emmy huku akifurahi

    "Waoohh !! " wakasema shoga zake wote kwa pamoja.

    " Tena si kuniacha tu bali ameniachia na kila kitu.Mali zote tulizokuwa nazo ameamua kuniachia mimi.Kwa hiyo I'm a free woman and a milionare too"

    "Ouh Emmy !! Sheila akasema huku akiinuka na kwenda kumkumbatia shogaye kwa furaha na shoga zake wengine nao wakafanya hivyo

    " Hongera sana Emmy." akasema Pili ambaye kwa kawaida si muongeaji sana kama wale wengine

    " Kwa maana hiyo kuanzia sasa ni mwendo wa kula bata tu.Pesa ipo ya kutosha tunatakiwa tuitumie.Sitaki kusikia mtu akilalamika shida ndogo ndogo ......" akasema Emmy na kuzifanya sura za shoga zake zichanue kwa tabasamu pana sana.

    "jamani tugonganishe glasi zetu tumtakie Emmy mafanikio katika maisha yake mapya" akasema Sheila.Wote wakainua glasi zao na kugonganisha wakimtakia Emmy maisha marefu na yenye furaha.

    "Welcome to the real world girl" Sheila akasema huku akitabasamu

    Pili akawasha muziki na kuanza kucheza.

    "Jamani leo ni kujiachia tu .ni sherehe kubwa..hatimaye tumempata milionea katika kundi letu" akasema Pili huku akicheza kwa furaha.Salama akajiunga naye katika kucheza.Emmy na Sheila wakabaki wamekaa katika sofa wakiongea hili na lile.

    " Unajua Sheila wewe ni shoga yangu mkubwa na siwezi kukuficha kitu.Leo nina furaha sana kuachana na yule mwanaume lakini moyoni najihisi vibaya sana.Sina amani ya moyo"

    "kwa nini unasema hivyo Emmy" Sheila akuliza

    "Kila mara sura ya Wayne inanijia akilini na kunifanya nijutie mambo niliyokuwa nikimfanyia.Katika dunia hii siwezi kumpata tena mwanaume mwenye moyo wa uvumilivu kama Wayne.Nimemfanyia mambo mengi sana mabaya na hata kuna wakati alinusurika kufa baada ya kumpiga na chupa kichwani.Siku ile niliogopa sana shoga yangu.Nilijua nimeua.Nilijua maisha yangu yanakwenda kuishia gerezani.Kwa bahati nzuri hakufa.Alivyokuwa na moyo wa ajabu yule mwanaume baada ya kutoka hospitali bado alikwenda polisi akajitahidi mpaka akanifutia kesi iliyokuwa ikinikabili.Nikikumbuka mambo niliyomfanyia naumia sana moyoni.Sikustahili kumtenda vile"Emy akaongea kwa masikitiko

    " Emmy shoga yangu,kwa sasa unachotakiwa kukifanya ni kumsahau kabisa Wayne.Yeye amekwisha amua kuanza maisha mapya.Amechoka na aina ya maisha mliyokuwa mnaishi.Na wewe halikadhalika jaribu kumsahau na uendelee na maisha yako mapya.sahau yote yaliyotokea huko nyuma.Kwa sasa jipange ili uone namna utakavyoweza kuendeleza miradi yote aliyokuachia Wayne.Kwa sasa una pesa na uwezo wa kutosha .Una uwezo wa kumpata mwanaume yeyote yule umtakaye.Una uwezo wa kupata furaha ya nama yoyote ile uitakayo.Achana kabisa na mawazo ya kuhusu Wayne" akasema Sheila

    "Hapana Sheila.Sidhani kama itakuwa rahisi kumsahau Wayne namna hiyo.Nimemfanyia mambo mengi mabaya na ya kusikitisha.lakini bado aliendelea kunipenda na kunivumilia.Katika dunia hii hakuna mtu kama Wayne.Yule ni mwanaume wa pekee kabisa.Pamoja na kwamba kaniachia kila kitu lakini sintaweza kumpata kama yeye" akasema Emmy na kumfanya shogaye Sheila kukaa kimya na kumtazama kwa makini

    "Sheila kuna kitu ninataka kukwambia ambacho sijawahi kumwambia mtu yeyote" Emmy akasema

    "Kitu gani hicho Emmy? Sheila akauliza

    Emmy akafikiri kidogo na kisha akasema

    "Pamoja na yote niliyomfanyia Wayne lakini huwezi kuamini kwamba moyoni nahisi bado ninampenda sana.Wayne bado yuko moyoni mwangu...........

    " unasema ? !!! ... Sheila akastuka na kuuliza kwa mshangao.Mstuko ule wa Sheila ukawafanya Pili na Salama waliokuwa wakicheza mziki kupunguza sauti ya mziki.

    "kulikoni Sheila mbona umestuka namna hiyo? akauliza Salama

    "haya makubwa tena..kuna jambo kaniambia Emmy limenifanya nistuke .Nahisi hata mapigo yangu ya moyo yameanza kubadilika" akasema Sheila.

    "Emmy kuna nini? Salama akauliza

    "Eti Emmy anasema kwamba bado anampenda Wayne...." Sheila akasema na kuwafanya salama na Pili kustuka

    "Eti Emmy hayo anayosema Sheila ni ya kweli? akauliza Salama akiwa amejishika kiuno

    "Sikilizeni shoga zangu.Ninyi ni rafiki zangu wakubwa na siwezi kuwaficha kitu.Ukweli ni kwamba bado ninampenda sana Wayne.Sidhani kama nitakuja kumpata mwaname kama yeye.Ninahisi kuna mtu alikuwa akinifanyia mchezo mchafu.Kuna mtu alikuwa akiniroga ili mimi na Wayne tusiweze kuishi kwa amani,kila siku nimfanyie vitimbi Wayne na mwishowe tuachane.Kuna mtu aliyekuwa akinionea kijicho kwa maisha yangu mazuri na Wayne.Kila nikifikiria mambo niliyokuwa nikiyafanya nashindwa kuamini kama ni mimi ndiye nilikuwa nafanya mambo ya ajabu namna ile.Lazima kuna mtu alikuwa akiniroga ili niweze kuachana na Wayne" Emmy akasema na kuwafanya shoga zake waangue kicheko kikubwa.

    "Hahahahaaaa......halooooo ........."

    Kicheko kile kilionekana kumkasirisha Emmy akauliza

    "Emmy kweli umetuchekesha.Hivi kweli shoga yangu wewe ndiye wa kusimama leo hii na kusema kwamba unampenda Wayne? Umemfanyia mambo mengi sana na akakuvumilia.Sina hakika kama mtu unayempenda unaweza ukamfanyia vitendo kama ulivyomfanyia.Umezaa nje ya ndoa na bado ukamtukana matusi yote ya dunia hii.Ulimvua nguo ,ukamdhalilisha kwa matusi uliyomtukana,leo hii inakuaje useme eti unampenda? Sheila akasema

    " Sheila ninayokwambia ni ukweli mtupu.lazima kuna mtu ananiroga.Kesho asubuhi nina safari ya kwenda kwa babu Tanga nikamfahamu mchawi wangu ni nani.Nina hakika atakuwa ni yule mwanamitindo aliyenichukulia mume wangu.Nitapambana naye na nitahakikisha Wayne anarudi hapa ndani."Akasema Emmy.

    "Hahahahaaa...shoga umeula wa chuya..usimtafute mchawi kwa sababu mchawi ni wewe mwenyewe.Umeshi

    ndwa kumtunza bwana wajuzi wa mambo wakamchukua.hah

    aaaaa...msahau Wayne huyo si wako tena." akasema Salama huku akicheka kicheko kikubwa.Wenzake pia wakaungana naye kucheka kitendo kilichomkera Emmy

    "sasa mnacheka nini? Nini cha ajabu kinachowachekesha? ninasema hivi kesho asubuhi na mapema aliye shoga yangu wa ukweli ataungana nami kwenda Tanga kwa babu.Atakayekataa ndiye mchawi wangu.Mimi nimemaliza sitaki tena mjadala nakwenda zangu kulala.Tayari mmekwishaniharibia siku yangu" Emmy akainuka kwa hasira na kuelekea chumbani kwake.Shoga zake wakabaki na mshangao

    " Jamani haya makubwa.Yaani baada ya kumfanyia mwanaume vituko vya namna ile leo hii anadiriki kusema kwamba eti kuna mtu anamroga? Ina mana wakati akifanya vitendo vile vyote hakufahamu thamani ya mwanaume hadi leo hii mwanaume amechoka ndipo anasema kwamba bado anampenda? Hahahahaa halooooooooo...Haya ni maajabu ya Musa " akasema Pili huku akigonganisha mikono na wenzake na kucheka kicheko kikubwa sana.

    " Hata mimi namshangaa sana huyu shoga yetu.Nadhani ni pombe tu zinaongea.Ameshalewa yule" akasema Sheila huku akicheka na kuichukua glasi yake ya mvinyo akanywa.

    "Thamani ya mwanamke mume bwana..yeye amepata mume aliyempenda ,akamvumilia katika mambo yote lakini hakuiona thamani yake,akamtukana ,akamfanyia kila aina ya vitimbi vya hii dunia leo hii baada ya kuachwa ndipo anakumbuka kuwa mume ana thamani.Alifikiri sisi tunaokaa bila waume tunapenda...Hii zamu yake...Leta mvinyo hapa tunywe hadi asubuhi." akasema Salama.



    Usiku huu ni usiku ambao nilihisi kama vile niko peponi.Nje mbalamwezi ilikuwa ikiangaza na kuifanya dunia ing'ae kwa nuru safi na adhimu ya mbalamwezi.Chumba kilikuwa na mwanga hafifu.Mimi na mwanamke niliyempenda kuliko wanawake wote Clara tulikuwa tumejilaza kitandani.Clara alikuwa amekilaza kichwa chake katika kifua changu.Nilikuwa nimemkumbatia kwa mahaba mazito.Nilifumba macho nikamshukuru Mungu kwa mara nyingine tena kwa zawadi hii aliyoniletea ya mwanamke mzuri pengine kupita wote duniani.Clara alikuwa ametulia mikononi mwangu.Nilijihisi kama siko tena katika dunia hii iliyojaa kero na karaha za kila aina.Nilijihisi kama vile niko katika ulimwengu mwingne kabisa ,ulimwengu wenye utulivu na mahaba mazito,ulimwengu usiokuwa na kero wala husuda za wanadamu.Baada ya mateso makubwa niliyoyapata toka kwa Emmy mtu niliyeweka ahadi ya kuwa naye katika shida na raha ,hatimaye nimeweza kupata kitulizo cha moyo wangu.Clara alikuwa ni kila kitu kwangu.Nilimpenda kuliko maelezo.

    Mkono wangu ulikuwa ukiichezea shingo laini ya Clara.Ngozi ya kimwana huyu ilikuwa laini ,nikapatwa na hisia kwamba pengine sikuwa nikiigusa ngozi ya binadamu wa kawaida.Nilihisi kama vile ninaigusa ngozi ya malaika kwa jinsi ilivyokuwa laini na ya kung'aa hata katika mwangaza huu hafifu uliokuwemo chumbani kwetu.

    "Wayne.." akasema Clara kwa sauti laini sana iliyoyafanya maungo yangu yasisimke

    " Unasemaje malaika wangu? Nikasema huku nikimuangalia usoni

    " Unafahamu ninakupenda kiasi gani? Nikatabasamu na kumuangalia usoni nikasema

    " Clara malaika wangu nafahamu kwamba unanipenda sana,sioni kitu cha kulinganisha na upendo wako kwangu.Ni upendo ambao hauwezi kupimwa wala kulinganishwa na kitu chochote kile" Nikasema taratibu

    "Nashukuru kama unalifahamu hilo.Napenda kuongezea kwamba ninakupenda kupita hata ninavyojipenda mimi mwenyewe.Nimezama katika bahari ya penzi lako na siwezi kutoka tena.Tafadhali naomba unishike vyema niweze kuogelea katika bahari hii bila kuzama.Naomba unisaidie kuyafurahia maisha yangu yaliyobakia hapa duniani.Nakukabidhi moyo na mwili wangu ,uvilinde na kuvichunga kama unavyojipenda wewe mwenyewe..Wewe ni kila kitu kwangu.naomba unitawale ewe mfalme wangu nami nitatii.." Clara akasema taratibu na kwa hisia kubwa Alikuwa katika hisia kali sana za huba.Nilimkumbatia kwa nguvu zaidi na kumbusu katika paji la uso wake .

    "Clara wewe ni malaika wangu uliyeshushwa maalum kwa ajili yangu tu.Niwapo nawe najihisi kama niko katika dunia nyingine kabisa.Ninapatwa na furaha ya ajabu ambayo sijawahi kuipata toka nimezaliwa.Wewe ni lulu ya pekee na ya thamani kubwa katika maisha yangu.Sintakutawala kama unavyotaka bali nitakupenda kwa moyo wangu wote hadi mwisho wa uhai wangu.Kuna nyakati ninakosa hata neno la kukuambia ni namna gani ninakupenda Clara zaidi ya unavyoweza kufikiri.Siku zote nitakulinda,kukuheshimu na kukuthamini......" Nikasema huku nikimtazama Clara usoni ambaye machozi ya furaha yaliendelea kumchuruzika

    " Wayne.........." akasema Clara.

    "naam mpenzi wangu" Nikaitika

    "What do you want tonight? akauliza nikamuangalia kwa macho yaliyojaa huba zito,nikambusu shavuni na kusema

    "All I want is for you to be by my side tonight and forever..." Nikasema na Clara akanikumbatia kwa nguvu na kunibusu.

    "Here I am..I'm all yours...tell me anything and I'll do.." akasema Clara

    "Sina cha kukwambia Clara zaidi ya nakupenda sana" nikasema na kumbusu.

    "Mimi ninalo la kukwambia" akasema Clara

    "Niambie mpenzi wangu" Nikasema

    "Wayne kuna jambo nimekuwa nikilifikiria."

    "Jambo gani Clara?

    "Sitaki tena kurudi afrika ya kusini.Ninataka kuishi nawe hapa hapa nyumbani Tanzania.Nafahamu kwamba unaweza ukastuka kwa jambo hili lakini kwa ajili yako niko tayari kwa kila kitu.Sioni tena sababu ya mimi kuendelea kukaa afrika ya kusini wakati mtu anayeutunza moyo wangu yuko Tanzania.Nimefikiria sana na kufanya maamuzi kwamba nitabaki hapa hapa tanzania.Sitaki kuishi mbali nawe hata kidogo.Sitaki kuwapa wanawake wengine nafasi ya kukupata.Wewe ni mwanaume adimu sana kupatikana na kwa vile tayari nimekupata sintakubali kukupoteza.kwa maana hiyo makazi yangu nitayahamishia hapa hapa Tanzania." Clara akasema na kunitazama usoni .Nilishindwa niseme nini kwa furaha niliyokuwa nayo.Suala hili la umbali uliopo kati yetu lilikuwa likinila akili sana lakini kwa upendo wake mkubwa Clara ameamua kuhama kutoka nchini afrika ya kusini alikokuwa akiishi na kuja kuishi tanzania kwa dhumuni moja tu la kuwa nami karibu.Huu ulikuwa ni upendo usiopimika.Nilitaka kusema kitu lakini Clara akaniziba mdomo.

    "Please Wayne dont say anything.....na

    jua bado huamini lakini huo ndio ukweli .Kwa ajili yako niko tayari kupoteza kila kitu.Niko tayari hata kwenda kuishi baharini mradi tu niwe na wewe.Jioni ya leo nimezungumza na wanasheria na washauri wangu na wameafiki suala langu la kuhamia nchini Tanzania.Makao makuu ya kampuni yangu nitayahamishia hapa hapa Tanzania na kule afrika ya kusini kutabaki na tawi..." Clara akasema na kunibusu .Nikamkumbatia na kumbusu mfululizo.

    "Clara nashindwa hata niseme nini kwa upendo huu mkubwa ulionao juu yangu..........."

    "Shhhhhhhhhh............." Clara akaniwekea kidole mdomoni na kunizuia kusema chochote

    " Wayne mpenzi wangu niambie unapenda twende tukaishi wapi hapa Tanzania? Clara akauliza

    Huku nikitabasamu nikamjibu

    "Nakupa wewe nafasi hiyo ya kuchagua ni sehemu ipi hapa Tanzania unaipenda na ungependa kwenda kuweka makazi.Kokote kule utakaposema mimi niko tayari kwenda kuishi nawe."

    Clara akatabasamu na kusema

    "kweli Wayne unanipa nafasi ya kuchagua mahala pa kuishi mimi na wewe?

    "ndiyo Clara"

    "kokote nitakapochagua uko tayari kwenda kuishi?

    "kokote kule utakochagua mimi niko tayari kwenda nawe,hata kama ni mashambani mimi niko tayari kwenda nawe."

    Clara akainuka kidogo akanitazama huku akicheka akasema

    "Nataka twende tukaishi......." akanyamaza,akafikiri kwa muda kisha akasema

    " nataka twende tukaishi....mbona unaniangalia kwa wasi wasi namna hiyo" akatania Clara huku akicheka

    "Kuna sehemu moja tu ambayo ninaipenda sana na siku zote nimekuwa nikifikira iwapo ningeamua kuweka makaazi yangu nchni tanzania ningeishi huko...Nikwambie ni wapi? akaendelea kutania Clara na kuzidi kuniweka roho juu.

    "Niambie malaika wangu.."Nikambe

    mbeleza

    "Ninataka mimi na wewe tuishi hapa hapa Arusha." akasema Clara na kunifanya nimkubatie na kumbusu kwa furaha.

    "Ouh thank you my angel..thank you soo much."Nikasema huku nikiendelea kumbusu.

    "Nafahamu kwamba unapapenda sana Arusha,umepazoea na shughuli zako zote ziko hapa Arusha,hata mimi pia ninapapenda sana Arusha na siku zote nimekuwa nikitamani kuweka makazi yangu ya kudumu hapa.Nashukuru Mungu kwamba ile ndoto yangu ya siku nyingi sasa imetimia.Hatimaye muda si mrefu nitahesabika kama mkaazi wa Arusha." akasema Clara.

    " Ahsante sana malaika wangu kwa uchaguzi huu mzuri.Ninaupenda sana mkoa huu wa arusha kuliko mikoa yote ya hapa tanzania.Arusha is wonderfull..Arusha is amazing...na kuwa pamoja nawe hapa Arusha tutatengeneza dunia ya peke yetu ndani ya mji huu uliobarikiwa...Ahsante sana mpenzi wangu...Karibu sana Arusha" Nikajikuta maneno yakinitoka mfululizo na kumfanya Clara acheke kicheko kidogo.

    "wayne I love you and I'll do anything for you..Its hard to find love like this these days..I thank God because I have foud love and I'm a happiest woman n the world..I'll never let you go..Come here my darling I'm all yours tonight and for the rest of my life" akasema Clara na kunivuta kwake tukaanza kupeana mabusu mfululizo.taratibu maongezi yakaanza kupungua na kilichobaki kikisikika ni miguno ya kimahaba.Ulikuwa ni usiku usiosahaulika katika historia yangu na Clara.Ulikuwa ni usiku wenye kila aina ya raha.Tulihama kutoka katika ulimwengu huu wa taabu na kuhamia katika ulmwengu mwi ngine kabisa wa peke yetu na kujivinjari huko usiku kucha.

    *************************

    Kengele ya saa ndiyo iliyomstua Sheila toka katika usingizi.Wenzake wote walikuwa wamelala fofofo kutokana na pombe nyingi walizokunywa usiku.Wote walikuwa wamelewa na hakuna aliyejua alifikaje katika chumba cha Emmy.KItandani alikuwa amelala Emmy ,Sheila na Salama.Pili yeye alikuwa amelala chini.Sheila akawatazama wenzake akatabasamu baada ya kuiona chupa ya mvinyo ikiwa pembeni ya kitanda.

    " Inaonekana Emmy aliendelea kunywa pombe baada ya kutuacha sebuleni.Naona kuna chupa hapa pembeni yake.Mh ! haya si maisha hata kidogo.Huu si unywaji mzuri wa pombe " akawaza Sheila huku akiinuka na kuhisi kizungu zungu kutokana na pombe kuwa bado kichwani.Akaenda jikoni akafungua friji na kuchukua chupa ya maji akanywa yote

    " Sasa najisikia afadhali.Jana tulikunywa pombe nyingi sana" akawaza Sheila wakati akiweka sawa vitu sebuleni vilivyokuwa vimepanguliwa hovyo kutokana na pombe walizokuwa wamekunywa jana yake.

    " Jana ilikuwa si mchezo.Kweli ilikuwa ni sherehe" Sheila akakaa sofani akaanza kuwaza

    " Kuna kitu alikiongea Emmy jana kikainishangaza sana na sijui kama alikiongea akiwa amelewa au alikuwa akimaanisha alichokisema.Nakumbuka alisema kwamba bado anahisi anampenda Wayne pamoja na vituko vyote alivyomfanyia vilivyopelekea ndoa yao kuvunjika.Nakumbuka tulicheka sana tukamuudhi Emmy akaondoka kwa hasira .Vile vile alisema kwamba leo atakwenda Tanga kwa mganga kwa sababu anahisi kuachana kwake na Wayne lazima kuna mkono wa mtu.Huyu shoga yangu anakotaka kwenda si kwenyewe kabisa.Hakuna mtu aliyekuwa akimroga ili aachane na mumewe.Mchawi ni yeye mwenyewe .Yeye mwenyewe kwa tabia zake chafu ndiye amekuwa akiiroga ndoa yake.Ninamfahamu Emmy kwa muda mrefu kwani nimesoma naye darasa moja.Hawezi akaishi na mwanaume hata siku moja yule.Siku zote yeye ametaka kuwa juu ya mwanaume na kumtawala.Wayne alivumilia mno na mwisho akachoka.Emmy hawezi kutulia na mwanaume mmoja na hii tabia yake sasa kwa nini leo hii aseme kuna mtu anamroga?Kuna kila ulazima wa kumweleza ukweli kwamba asihangaike kutafuta mchawi kwani mchawi ni yeye mwenyewe.Alitaka kuwa huru sasa amekuwa huru kufanya kila anachokitaka.Wayne amekwenda kutafuta furaha ya maisha yake na asiendelee kumsumbua tena.Aliyomfany

    ia yanatosha sana.Amuache apumzike sasa kwani amemuachia kila kitu kwa nini basi aendelee kumuandama hadi kumuendea kwa waganga? Kama alifahamu thamani yake basi angemthamini na kumjali wakati bado yuko naye ndani.Huyu Emmy asituletee mambo yake ya kipuuzi akatusababishia matatizo mengine.Yeye akubali kushindwa na aendeleze miradi yake aliyoachiwa.Mbona sisi hatuna waume lakini tunaishi? Tunakula tunakunywa na tunapata kila aiana ya starehe tunayoitaka.Anatakiwa ajifunze kuishi kama sisi kwa sababu alipata bahati ya kuolewa akaichezea.Laiti ningeipata mimi bahati kama aliyoipata Emmy ya kuolewa na Wayne naapa nisingemuacha akaenda sehemu yoyote peke yake.Ningeambat

    ana naye kama kumbi kumbu.Mwanaume kama Wayne ni adimu sana kumpata kwa miaka hii.Emmy ameula wa chuya......." Sheila akatabasamu halafu akachukua chupa ya mvinyo akapiga funda kadhaa



    " Ngoja nizimue Sheila mimi manake ile ya jana ilikuwa si mchezo " akasema Sheila huku akiendelea kupiga funda za mvinyo halafu akainuka na kurudi chumbani akamuamsha Emmy.

    " Mhhhhhh.!!!.......we Sheila hebu niletee maji ya kunywa..kichwa kinaniuma sana" akasema Emmy akiwa amekunja uso kutokana na maumivu ya kichwa aliyoyasikia.Sheila akamletea maji ya kunywa akanywa.

    " Amka shoga yangu uzimue kidogo.utajisikia vizuri" akasema Sheila huku akimpa Emmy chupa ya mvinyo iliyokuwa pembeni ya kitanda Emmy akapiga funda kadhaa na kuiweka pembeni.

    " Jana mlilala saa ngapi? manake niliwaacha mnaendelea kunywa" akauliza Emmy

    " Mhh ! Jana ilikuwa balaa tupu,sielewi hata tulifikaje humu chumbani" akasema Sheila huku akitabasamu baada ya kumuona Pili namna alivyokuwa amelala pale sakafuni.

    " Mhhh ! Inaonekana Pili alilewa sana hadi akashindwa kupanda kitandani." akasema Emmy

    " Achana nao hao watoto wadogo pombe hawaziwezi hebu njoo huku tuongee shoga yangu" akasema Sheila na kuongoza kuelekea Sebuleni. Emmy akainuka na kumfuata Sheila sebuleni.Bado aliendelea kuhisi kichwa kikimuuma sana

    " Sheila kichwa kinaniuma sana" akasema Emmy

    " Usijali Emmy..unatakiwa kwanza uzimue halafu tukapate supu safi ya kongoro au mkia utajisikia vizuri" Akasema Sheila

    " Kweli kabisa Sheila.Waamshe akina Salama tukatafute supu ya mkia"

    " Kabla hatujaenda huko kuna jambo nataka unieleze shoga yangu wakati bado hujaweka pombe kichwani"

    " Jambo gani hilo Sheila?

    "Jana uliniambia kitu ambacho kilinistua kidogo.Wakati tukinywa ulisema kwamba ulikuwa na mpango wa kwenda kwa mganga ili kumtafuta mtu ambaye unahisi alikuwa akikurogha ili usiweze kuelewana na Wayne.Sasa nataka uniambie ukiwa bado mkavu kabisa maneno yale yalikuwa ya kweli au zilikuwa ni pombe tu?

    Emmy akainama akafikiri na kusema

    " Sheila wewe ni rafiki yangu mkubwa na wa siku nyingi sana na siwezi kukudanganya kitu.Nilimaanisha nilichokiongea na wala sikuwa nimelewa kiasi cha kuongea mambo nisiyoyajua.Sheila, nimekuwa na mawazo hayo kwamba lazima kuachana kwetu kuna mkono wa mtu kwa sababu nikiyafikiria mambo niliyokuwa nikimfanyia Wayne nashindwa kuamini kama ni mimi kweli ndiye niliyeyafanya mambo hayo.Sielewi nilipata wapi ujasiri wa kufanya mambo yale kwa sababu kuna nyakati niliweza hata kutamka maneno machafu mbele ya wazazi wangu.Nikifikiria hivyo moyo unaniuma sana.Nina uhakika lazima kuna mtu ambaye hakupenda kuniona nikiwa na Wayne ambaye alikuwa akinichezea ili nimfanyie vituko vya kila aina na mwisho tuachane.Sheila shoga yangu,kutoka moyoni napenda nikiri kwako kwamba ninampenda Wayne.Ninampenda sana lakini sijielewi ni shetani gani aliyenipitia hadi nikamfanyia vituko vile.Wayne amenivumilia mambo mengi sana kwa sababu alikuwa akinipenda na ninahisi ndani ya moyo wake bado ananipenda.Nimeligundua kosa langu na ninahitaji Wayne anipe tena nafasi nyingine.Siwezi kumpata mwanaume mwingine kama Wayne hata kama nikizunguka dunia nzima.Ni yeye tu ambaye anaweza akaishi na mimi .Hakuna mwanaume mwngine ambaye anaweza akanivumilia hata kwa siku moja lakini Wayne nimekaa naye kwa miaka mingi na kwa muda wote huu amenivumilia na kunijali.Sheila nataka kumrudisha Wayne kwangu.Niko tayari kwa lolote lile lakini si kumpoteza Wayne.Baada ya kuniacha nimeanza kuliona pengo lake.Ninajihisi mtupu ndani yangu.Kwa mara ya kwanza ninahisi kumuhitaji Wayne katika maisha yangu.Naomba unisaidie shoga yangu katika kumrudisha Wayne kwangu..." akasema Emmy huku akichukua chupa yake ya mvinyo na kupiga mafunda kadhaa akizimua ili kujiweka safi.Sheila ambaye alikuwa kimya akimsikiliza Emmy akasema

    " Sikiliza Emmy..Tena naomba unisikilize vizuri sana.Wewe ni rafiki yangu wa siku nyingi toka tukiwa shuleni.Ninakufahamu vizuri kuliko mtu yeyote yule.Emmy hakuna mtu aliyekuroga.Kuachana kwako na Wayne hakuna mkono wa mtu kama unavyodhani. Usihanganike kumtafuta mchawi shoga yangu utakakuja umbuka hapa mjini kwa sababu mchawi ni wewe mwenyewe.Umeiroga ndoa yako wewe mwenyewe.Mume anatakiwa kutunzwa Emmy.Sasa hivi kumpata mume kama Wayne ni sawa na kuwa na dhahabu ndani kwa hiyo unatakiwa kumlinda kwa kila namna.Unatuona sisi tunaishi bila waume unafikiri tunapenda? Hatupendi lakini nani wa kutuoa? Wengi wanatuchezea na kutuacha lakini wewe ulimpata mwanaume akakuweka ndani ukashindwa kumlinda na matokeo yake amechoka na ameamua kuondoka zake akakuachia kila kitu.Uliivuruga ndoa yako wewe mwenyewe Emmy na huna haja ya kundelea kumfuatilia Wayne kwa sababu tayari ameanza maisha mapya.Tayari ameipata furaha ya maisha aliyoikosa kwa miaka mingi.Amempata mtu ambaye anampa kila anachokihitaji.Mtu anayemjali na kumthamini.Muache Wayne apate raha na aendelee na maisha yake bila kero zozote toka kwako tena.Muonee huruma ameteseka vya kutosha " akasema Sheila na kumfanya Emmy ainamishe kichwa akiwaza.

    " Sheila unayoyasema yanaweza yakawa na ukweli ndani yake.Lakini nitafanya nini na mimi bado nampenda Wayne? Ni kweli nilimfanyia Wayne vituko vingi na nilimnyima kabisa raha lakini hebu nipe ushauri nitampataje tena Wayne kwa sababu bado moyo wangu unamuhitaji? Nifanye nini ili mume wangu arudi kwangu? akasema Emmy

    " He's not your husband any more.he is your x naomba usijichanganye kwa hilo...." akasema Sheila kwa haraka

    " Naomba ulitambue hilo kwamba Wayne si mumeo tena.Kwa sasa hauko moyoni mwake tena.Kitu cha kufanya kwa sasa msahau kabisa Wayne na uendelee na maisha yako.Amekuachia kila kitu endeleza miradi yako na utapata kila unachokihitaji.Kama unataka mwanaume basi utampata mwanaume yeyote yule umtakaye.Achana na mawazo ya ulimwengu uliopita.Ingia katika ulimwengu mpya kabisa.Tayari una mtoto wako mmoja unataka nini zaidi? Una mali za mamilioni ya fedha.bado unamtaka na Wayne tena? Achana na Wayne.Sisi tuendelee kula bata na kuyasongesha maisha.Maisha mafupi haya Emmy." akasema Sheila

    " Sheila wewe ni shoga yangu wa ukweli na mara zote huwa unanieleza ule ukweli.Pamoja na yote uliyonieleza lakini bado moyo wangu unakuwa mzito sana kumuacha Wayne aende hivi hivi.Bado natakiwa kupambana hata kidogo nijaribu bahati yangu pengine anaweza akarudi kwangu.Dunia ina maajabu mengi na lolote linawezekana." akasema Emmy

    " Unafikiria kufanya nini? Akauliza Sheila

    " Bado nafikiria kwenda kwa babu ili anifanyie mambo na Wayne aweze kunirudia.Nakuhakikishia shoga yangu kwamba kama nikifanikiwa kumrudisha Wayne kwangu nitatulia sana na nitabadilika kabisa.Sintakuwa yule Emmy mliye mzoea.Nitaanza maisha mapya kabisa."akasema Emmy

    " Emmy mimi ni rafiki yako tu na sina mamlaka ya kukuzuia usifanye kitu chochote unachokitaka kukifanya.Mimi ninapenda kukuona ukiwa na furaha siku zote na ndiyo maana nikakushauri kwamba achana na Wayne na uendelee na maisha yako hii ni kwa ajili ya furaha ya maisha yako.Kazi yangu ni kukushauri tu na ni juu yako kama utaukubali ushauri wangu ama la.Na wala si lazima uukubali ushauri wangu kwani mwisho wa siku wewe ndiye mwenye uhuru na maisha yako.Enhee huko kwa babu umepanga kwenda kufanya nini? akauliza Sheila akionekana kuchukizwa kidogo na maamuzi ya Emmyhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Naomba usikasirike shoga yangu.Ni kweli bado nampenda Wayne na ninahitaji kumrudisha kwangu kabla hajapotea kabisa na yule mwanamitindo.Ushauri wako siku zote umekuwa mzuri na wenye manufaa makubwa kwangu na kamwe sintaweza kuupuuza lakini bado nahitaji kujaribu japo kidogo kumrudisha Wayne.Hata kama tumeachana lakini bado ni mume wangu kwani kidini ndoa hutenganishwa pindi mmoja akifariki.Kwa babu nataka akanisaidie kumrejesha Wayne kwangu.Uwezo huo anao si unakumbuka Kidawa aliachana na mumewe lakini alikwenda kwa babu na muwe akarudi na sasa wana watoto wawili na wanaishi kwa furaha.Kama kwa kidawa iliwezekana hata kwangu itawezekana pia.Nakuhakikishia Sheila Wayne atarudi kwangu." akasema Emmy kwa kujiamini

    " Emmy naomba nikwambie kitu kimoja kwamba hata kama mganga akikusaidia kumrudisha Wayne kwa njia anazojua yeye mwenyewe bado hautakuwa moyoni mwake.Hakutakuwa na penzi la kweli na hii ni hatari zaidi kwa sababu utakayeumia zaidi ni wewe.Lakini kama uko tayari kwa hilo mimi sikuzuii kwenda kwa mganga." akasema Sheila

    " Kwa hiyo Sheila uko tayari kunisindikiza.kwa babu?

    " Niko tayari kwenda nawe kokote shoga yangu" akasema Sheila na kumfanya Emmy afurahi

    " Basi shoga yangu hakuna haja ya kupoteza muda.Tujiandae tuondoke zetu." akasema Emmy

    " sasa hivi? mimi sina hata nguo za kuvaa" akasema Sheila

    " Ndiyo ! sasa hivi...usijali kuhusu nguo .Chagua nguo yangu yoyote uvae tuondoke." akasema Emmy kisha akamshika mkono shoga yake wakaenda chumbani kujiandaa kwa ajili ya kuondoka.

    Baada ya kuoga na kuwa tayari kwa kuondoka Sheila akamuamsha Salama.

    " Salama ninatoka kidogo kuna mahala ninakwenda na Emmy.Msichelewe kwenda kufungua saluni si mnakumbuka kuna wale maharusi wa kuwapamba? Msichelewe sana" akasema Sheila.

    " Salama funguo za nyumba hizi hapa.Mkitoka mtafunga nyumba na mtaondoka na funguo.tutawataarifu muda tutakaorudi" akasema Emmy huku akimshika mkono Sheila wakatoka na kuingia katika gari wakaondoka kuelekea kwa mganga Mombo

    **********************

    Saa sita za mchana waliwasili eneo la Mombo ambako ndiko mganga anayemfahamu Emmy alikuwa akiishi.Emmy akaegesha gari lake nje ya nyumba ya mganga na kushuka garini.

    " Emmy una hakika kwamba hapa ni penyewe? akauliza Sheila

    "Ni hapa hapa .Siwezi kupotea.Niliwahi kuja mara moja na Kidawa." akasema Emmy na mara akatokea mama ambaye aliwakaribisha kwa furaha.Mwanamama huyu alionekana kama msaidizi wa mganga.

    " Karibuni sana" akasema mwanamama yule aliyekuwa amevaa nguo nyeusi akiwakaribisha akina Emmy katika mkeka.

    " Ahsante sana" wakajibu kwa pamoja

    " mama tumekuja kumuona mtaalamu.Tumemkuta? akauliza Emmy

    " Yuko ndani tena mna bahati kwa sababu leo alikuwa akitaka kusafiri lakini akaahirisha safari yake baada ya mizimu kumtaarifu kwamba kuna wageni wawili wenye shida kubwa toka Arusha watafika leo.Nyie ndo wageni wake toka Arusha? akauliza yule mama na kuwafanya Emmy na Sheila watazame kwa mshangao

    " Ndiyo sisi..amejuaje kama tutakuja leo toka Arusha? akauliza Emmy kwa mshangao

    " Hapa ndo mmefika kwa mtaalamu asiyeshindwa na kitu chochote.Kuanzia masuala ya mapenzi,kesi ,uzazi,utajiri na kila kitu hapa ndio suluhisho lake.Mganga huyu anajua matatizo ya kila mtu ajaye hapa bila hata ya kuambiwa na kabla hata hujafika hapa yeye tayari anakuwa amekwisha fahamu na kukutafutia tiba " akasema mwana mama yule huku akizidi kuwashangaza akina Emmy.Mwana mama yule akainuka pale mkekani na kuondoka .

    " Shoga haya mbona makubwa? Ina maana huyu mganga amejua kwamba leo hii tutakuja? akauliza Sheila kwa mshangao

    " Nilikwambia Sheila mganga huyu huwa hashindwi na kitu chochote kile Huyu ndiye alimrudisha mume wa Kidawa.Nina uhakika hata mimi wayne atarejea kwangu" akasema Emmy kwa sauti ndogo huku akitabasamu.

    " Shoga yangu haya mambo mimi kwangu mbona mageni sana." akasema Sheila akiwa katika hali ya uoga

    " Usiogope Sheila hakuna tatizo lolote" akasema Emmy na mara yule mama akarejea.

    " Mganga amenituma niwataarifu kwamba amekwisha anza kulishughulikia tatizo lenu ambalo kwa mujibu wa melezo yake ni kwamba ni tatizo gumu sana lakini haliwezi kumsinda.Kwa maelekezo ya mizimu ni kwamba tiba lazima ifanyike usiku wa leo.Kuanzia saa tano usiku hadi saa tisa..Kwa maana hiyo itawalazimu leo kulala huku huku.Vile vile kuanzia sasa mnatakiwa kuyatoa hayo mavazi yenu mliyovaa na kuvaa nguo mtakazopewa yaani kaniki kama hii niliyovaa mimi hapa kwa sababu tayari shughuli imeshaaanza.Mnatakiwa kuvaa kaniki pekee iliyopakwa dawa bila ya nguo ya ndani au nguo yoyote ile ambayo haijawekwa dawa.Twendeni nikawaonyeshe chumba mtakachokaa wakati uganga ukiendelea" akasema yule mama na kuwaongoza akina Sheila kwenda kubadilsha nguo.

    " Shoga haya ya leo mbona makubwa..." akasema Sheila huku akicheka kichini chini.

    " Shhhhhhhhhhhhhhh.....!!! nyamaza Sheila.Ukiongea kitu huyu mganga anakusikia" akasema Emmy

    Emmy na Sheila wakapelekwa katika mojawapo ya vyumba vilivyokuwamo katika nyumba ile iliyoezekwa kwa makuti.Chumba kile hakikuwa na mlango bali pazia kuu kuu lililochakaa sana.Ndani kulikuwa na mkeka mmoja tu kuu kuu.Mama yule akawakaribisha Emmy na Sheila wakaingia ndani wakakaa katika mkeka.

    " Sasa mnatakiwa muyatoe hayo mavazi yenu ili yakapakwe dawa kuondoa aina yoyote ile ya mkosi na mnatakiwa mjifunge nguo hizi ambazo tayari zimekwisha wekwa dawa." akaamuru yule mama na kusimama pembeni.Emmy akaanza kuvua nguo zake .Sheila naye akavua nguo lakini akaogopa kuvua nguo yake ya ndani.Yule mama akamuangalia kwa jicho kali na kusema.

    " Mwanangu kama umekuja hapa una matatizo na unahitaji kutatuliwa matatizo yako unatakiwa ufuate kila utakachoambiwa na mganga.Masharti aliyoyatoa mganga ni kwamba mnatakwa mzitoe kabisa nguo zenu zote mlizotoka nazo mjini na mvae nguo hizi ambazo tayari zimekwisha wekwa dawa." akasema yule mama .Emmy akamshika bega shoga yake na kumwambia.

    " Sheila vua nguo zote shoga..Usiogope kitu" akasema Emmy na kwa shingo upande Sheila akavua nguo yake ya ndani akabaki mtupu na kujifunga ile nguo nyeusi waliyopewa na yule mama msaidizi wa mganga .Mama yule akazikusanya nguo zote za akina Emmy

    " Kaeni pumzikeni hapo katika mkeka msubiri maelekezo mengine" akasema yule mama na kuondoka na zile nguo.

    " Shoga hii ya leo kali.Mi mwenzako naogopa kukaa namna hii.Asije yule babu akatubaka bure" akasema Sheila huku akicheka

    " Usiogope shoga yangu ,mtafuta cha uvunguni sharti ainame.Hawezi kutufanyia kitendo kama hicho.Ninamfahamu vizuri mganga huyu" Akajibu Emmy.

    Baada ya kukaa mle chumbani kwa zaidi ya saa moja hivi yule mama akarejea tena na safari hii akiwa na sinia lililosheheni chakula.Ulikuwa ni wali safi wa nazi pamoja na kisamvu.

    " Karibuni chakula.Mnatakiwa mle mshibe kwa sababu dawa mtakazopewa ni kali na mnatakiwa muwe na nguvu ya kutosha." akawakaribisha yule mama halafu akatoka na kuwaacha akina Emmy wakiendelea kula chakula.

    Walipomaliza kula kile chakula akaja yule mama na kuondoa vyombo akawaambia wapumzike na wajiandae kwa sababu mganga atakuja kuwaona muda si mrefu.Emmy alifurahi sana , aliamini mganga yule ndiye suluhisho la matatizo yake.Aliamini kabisa kwamba mganga yule alikuwa na uwezo wa kumrudisha Wayne mikononi mwake.



    Dakika thelathini baadae mganga akajitokeza akiwa amevaa nguo nyeusi aliyoifunga hadi kiunoni.Kichwani alivaa kofia yenye manyoya.Kifuani alivaa ngozi ya chatu na mkononi alishika usinga mweusi.

    mara tu mganga alipoingia mle chumbani Emmy na Sheila wakasimama na kumsalimu mganga kwa adabu.

    " Marahaba wanangu.habari za mjini?

    " Nzuri babu,habari za hapa?

    " habari za hapa nzuri.Karibuni sana "

    Mganga akaupunga usinga wake hewani kisha akasema

    " Nilikuwa na safari ya kwenda Pangani siku ya leo lakini mizimu yangu ilinikataza kwenda na kuniambia kwamba kuna watoto wangu watakuja wana shida kubwa sana inayohitaji msaada wa haraka.Ninalifahamu tatizo lako Emmy na hata Sheila ninalifahamu taizo lako ingawa hukuja hapa kutafuta tiba bali kumsindikiza mwenzako lakini mizimu imenielekeza nikusaidie na wewe pia" akasema mganga na kuwafanya Sheila na Emmy watazamane kwa mshangao mkubwa.Kilichowashangaza ni namna mganga alivyoyafahamu majina yao kwani hawakuwahi kumtajia majina yao.

    " Msijiulize sana nimewafahamu vipi.Mimi ndiye mzee Mtuguru ninayefahamu kila kitu.Kila mgonjwa anayekuja hapa ninakuwa nimelifahamu tatizo lake kabla hata hajapanda gari kufika hapa.Kabla hamjafika hapa tayari nilikwisha fahamu matatzo yenu yote na namna ya kuwasaida." Akasema mganga na kuzidi kuwashangaza akina E mmy.

    "Emmy tatizo lako ni kutaka kurudiana na mumeo Wayne ambaye tayari amekwisha tangaza kuachana nawe.Ninafahamu kwamba bado unampenda sana mumeo lakini ndoa yako ilitawaliwa na migogoro mingi sana hali iliyopelekea Wayne kuchoka na kuamua muachane. Migogoro yote ndani ya ndoa yako ninaifahamu chanzo chake na nitakusaidia kumfahamu mtu ambaye aliifanya ndoa yako iweze kutawaliwa na migogoro kila kukicha.Nafahamu kwamba kilichokuleta hapa kwangu ni kutaka kumrudidha Wayne kwako na muendelee kuishi kwa amani na furaha.Hilo ni suala dogo sana kwangu na nitahakikisha ndani ya muida mfupi Wayne anarejea nyumbani kwako na kuachana na mpenzi wake wa sasa ambaye wanapanga kufunga ndoa.nakuhakikishia kwamba mapenzi yao hayatafika mbali na Wayne atarejea kwako." akasema mzee Mtuguru.Emmy akamuangalia Sheila akatabasamu.Mga

    nga akamgeukia Sheila akamuita.

    " Sheila .."

    " Naam babu" akaitika Sheila kwa adabu.

    " Ninafahamu tatizo ulilonalo.Sheila una tatizo la kukimbiwa na mabwana kitu ambacho kimekufanya ukate tamaa tena ya kuolewa na kuamua kuishi maisha ya peke yako.Kuna mtu ambaye anakuonea kijicho kwa uzuri wako na hivyo akakufunga kabisa ili usiweze kuishi na mwanaume yeyote yule.Mizimu imeliona hilo na imenituma nikusaidie na wala sintataka unilipe chochote ila mambo yako yatakapokuwa safi basi utaamua wewe mwenyewe kama utakuja kuishukuru mizimu.Nitakufanyia dawa na muda si mrefu utafanikiwa kumpata bwana tena mwenye uwezo mkubwa kipesa.Mizimu imenionyesha mwanaume ambaye utampata ambaye ni mwarabu ." Sheila akajikuta akitabasamu baada ya maneno yale ya mganga.

    " Kwa sasa endeleeni kupumzika wakati tukijiandaa na tiba itakayoanza saa tano za usiku." akasema mganga halafu akamuita yule mama msaidizi wake akamuomba amletee chombo chenye moto pamoja na ubani.Haraka haraka yule mama akakiweka kile chombo chenye moto kati kati ya chumba halafu mganga mzee Mtuguru akaanza kufukiza ubani huku akisema maneno ambayo si Sheila wala Emmy aliyeyaelewa.

    " Mnachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuendelea kufukiza ubani kwani mizimu inapenda sana harufu ya ubani.Kila baada ya muda mtakuwa mkichukua ubani na kuutupia juu ya huu moto huku kila mmoja akisema kile ambacho anataka mizimu imsaidie." akasema mganga halafu akaondoka mle chumbani.

    " Shoga ! hii ya leo kali..mpaka nimeogopa.Huyu babu kiboko.Amejuaje matatizo yetu? Shoga nakwambia wakati ananiambia matatizo yangu nilikuwa natetemeka kwa uoga." akasema Sheila

    " Sheila nilikwambia huyu babu ni kiboko.Anafahamu kila kitu.Ninamfaham

    u sana kwa sababu ndiye aliyemsaidia shoga yangu Kidawa mpaka akarudiana na mumewe.Ninaamini hata mimi pia nitarudiana na Wayne.Halafu Sheila nilikwambia kwamba migogoro yangu na Wayne haikuwa ya kawaida.Niliamini kabisa kwamba kulikuwa na mkono wa mtu.Si unaona babu amesema kwamba ni kweli kuna mkono wa mtu ! Nina hasira na hyo mtu ambaye amenisababishia haya matatizo yote.Nitamfanyia kitu kibaya sana " akasema Emmy

    " Hunishindi mimi Emmy.Nina hasira sana na huyo shetani aliyenifunga ili nisipate bwana.Unajua nimekuwa ninajiuliza sana nina tatizo gani kwa sababu kila bwana niliyekuwa nikimpata sikuwa nikidumu naye kwa muda mrefu.Shabani nilikaa naye kwa miezi sita na tukaachana katika mazingira ya utata utata..nikampata Malick naye nikadumu naye kwa miezi miwili tu..Jonathan naye nilikaa naye kwa miezi mitatu.lakini aliyeniumiza zaidi ni Samir ambaye nilimpenda sana na nilidumu naye kwa muda wa wiki mbili tu.Nilipolala naye mara moja tu hakurudi tena kwangu.Mpaka leo ninaumia roho sana kila nikimkumbuka Samir.Ninataka babu anionyeshe huyo hasidi mkereketwa wa maisha ya watu ambaye hataki kuona wenzake wakifurahi.Nina

    taka nimfunze adabu" akasema Sheila huku uso wake ukionyesha hasira za wazi

    *********************

    Saa tatu za usiku mama msaidizi wa mganga akaingia katika kile chumba walichokuwamo Emmy na Sheila.

    " Binti zangu mambo ndo yanakwenda kuanza sasa hivi.Mmekula mmeshiba lakini? akauliza yule mama

    " Ndiyo mama" wakajibu kwa pamoja Emmy na Sheila.

    " Sawa . Sheila ni nani hapa? akauliza

    " Ni mimi hapa."

    " Wewe Sheila subiri kwanza hapa hapa wakati namtanguliza mwenzako katika sehemu itakapofanyikia dawa." akasema mama yule kisha akampa Emmy kibuyu na kumuamuru akishike kwa nguvu.

    " Haya nifuate " akasema yule mama huku akiongoza njia kuelekea sehemu iliyokuwa na giza nene.Alikuwa akitembea huku akiupunga usinga wake na kuimba wimbo wa kiganga.Walipita katika njia yenye majani mengi.Ni sauti za wadudu na madege ya kutisha ndizo zilizokuwa zikisikika na kumuogopesha sana Emmy.Hatimaye baada ya mwendo wa dakika kumi hivi wakawasili katika eneo moja lililokuwa na kibanda kidogo.Nje ya kibanda kile kulikuwa na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka.Emmy akakalishwa katika kiti kidogo kilichokuwa karibu na ule moto halafu yule mama mganga akamzungushia usinga kichwani na toka ndani ya kile kibanda akatokeza mganga mzee Mtuguru.Akamuita yule mama maidizi wake na kuongea naye katika lugha yao .Ilionekana kana kwamba kuna maelekezo anampa halafu yule mama akaondoka zake na kuwaacha Emmy na mganga na hapo ndipo shughuli ikaanza.Mganga akaingia katika kile kibanda chake akatoka na ndoo iliyokuwa imejaa maji ya moto yaliyokuwa na harufu kali ya dawa .Akamuamuru Emmy kuvua ile nguo aliyokuwa amejifunga.Bila ubishi Emmy akaivua ile nguo na kubaki mtupu halafu mganga akaanza kumuogesha dawa ile iliyokuwa katika ndoo.Emmy aliogopa sana kuwa vile mbele ya yule mzee lakini kwa vile alikuwa ana shida ilimbidi kupiga moyo konde kwa lolote lile litakalotokea.A

    likuwa akitetemeka mwili kutokana na uoga mwingi.Baada ya zoezi lile la kuoga dawa kukamilika mganga akamumuru avae ile nguo yake halafu akamletea dawa nyingine katika kibuyu akampa anywe na muda huo huo kutetemeka kukakoma.Emmy akabaki akishangaa.Mzee Mtuguru akaingia tena kibandani na safari hii akatoka na vifaa vyake vya kiganga na kuanza kuongea maneno mengi ya kiganga.Zoezi lile likachukua zaidi ya saa moja.halafu akamuomba Emmy asogee karibu.

    " Huyu ndiye bwana unayetaka arudi kwako?" akauliza mganga akimuonyesha Emmy sura ya mtu iliyokuwa ikionekana katika beseni la maji.Emmy akaitambua sura ile kwamba ni ya Wayne na kwa haraka haraka akasema

    " Ndiyo mzee.ni huyu huyu mume wangu"

    " Na huyu mwanamke wake unataka tumfanye nini? tumuue?

    Emmy akasita kujibu akamtazama mganga.

    "Sema unataka tumfanye kitu gani?

    " Nataka aondoke hapa Tanzania na asirudi tena na amsahau kabisa Wayne" akasema Emmy

    " Vizuri.Mizimu imesikia ombi lako na sasa naituma ikafanye kazi hiyo" mzee Mtuguru akaanza kuongea maneno mengi ya kiganga na kila alipokuwa akinyoonsha mkono kulielekea lile beseni la maji moto ulikuwa ukiwaka ndani ya beseni.Emmy akaogopa sana.Baada ya muda mganga akampa Emmy kibuyu akishike na kumwambia

    " Mizimu imesema bado hujaitolea sadaka yoyote ile ya kuifurahisha.Kwa maana hiyo ahidi kwamba uko tayari kutoa sadaka wanayoitaka mizimu kwa ajili ya kukufanikishia mambo yako.Mumeo atarudi nyumbani na wewe utakuwa mwanamke tajiri na mwenye nguvu " akasema mganga na kumfanya Emmy atabasamu kwa mbali.

    " Niko tayari mganga kutoa sadaka yoyote ile ambayo mizimu itaitaka ili mradi mambo yangu yafanikiwe." akasema Emmy kisha mzee Mtuguru akakaa pembeni ya beseni lake lenye maji akaingiza mikono yake na kuyazungusha maji halafu akampa Emmy kisu kikali na kumuamuru akichome katika yale maji.Bila ubishi Emmy akakiinua kisu na kukichoma ndani ya yale maji na mara tu alipofanya kile kitendo akasikia sauti fulani ikilia.Sauti ile haikuwa ngeni masikioni mwake.Baada ya sekunde kadhaa maji yale yaliyokuwamo ndaniya lile beseni yakaanza kubadilika rangi na kuwa damu.

    " Mizimu imefurahi kwa sadaka hii nzuri sasa naituma tena kwenda kuifanya kazi hii" akasema mganga na kuendelea na uganga wake.Baada ya muda akamgeukia Emmy na kumwambia akae pale pale juu ya jiwe na aendelee kukishika kile kibuyu kwani kazi ilikuwa inaendelea.Mganga akaondoka na kumuacha Emmy peke yake.

    " Mambo haya yanatisha sana..lakini maji ukisha yavulia nguo huna budi kuyaoga.Wayne lazima arudi kwangu..Halafu ile sauti niliyoisikia ikilia mbona si ngeni masikioni mwangu? Ni kama ninaifahamu sauti ile ..ni kama ya.." Emmy akakatisha mawazo yake baada ya mama msaidizi wa mganga kuwasili.

    Mzee Mtuguru baada ya kuondoka kwa Emmy akaelekea moja kwa moja katika sehemu aliyokuwa amewekwa Sheila.Sehemu hii nayo ilikuwa na kibanda na moto mkubwa ulikuwa ukiwaka nje .Mganga akaingia ndani akachukua maji yenye dawa na kumuamuru Sheila atoe ile nguo yake halafu akaanza kumuogesha ile dawa.Alipomaliza kumuogesha ile dawa akachukua tena ndoo nyingine yenye maji safi akamsuuza mwili wote na kisha akiwa vile vile mtupu akamuamuru kuingia katika kile kibanda ambacho kilikuwa na taa ya chemli na chini kulitandikwa mkeka msafi.Kati kati ya kile kibanda kulikuwa na chombo chenye moto na mganga akamuamuru Sheila kupiga magoti pembeni ya kile chombo halafu akaanza kurushia ubani huku akiongea maneno ambayo Sheila hakuyaelewa.Alipomaliza akamwambia Sheila

    " Mizimu inataka kuanza kufanya kazi yake kwa hiyo inakubidi unukie marashi kabla haijaingia hapa na kukushughulikia

    .Inamia chombo hicho na ujifukize ." akasema mganga na kumpatia Sheila chombo cha ubani na yeye akainuka akasimama nyuma yake.Sheila akainama na kuanza kujifukiza ubani.Mganga mtuguru aliyekuwa amesimama kwa nyuma jasho likaanza kumtoka alipolishuhudia umbo la Sheila kwa nyuma.Mate yakamdondoka na kujikuta akiangusha usinga wake.Mwili ulikuwa ukimtetemeka .Akaanza kuongea maneno yake ya kiganga .Kila alipolishuhudia umbo la Sheila mate yakazidi kumtoka.Haraka haraka akaenda sehemu ambayo huwa anahifadhi vibuyu vyake akachukua kibuyu kimoja na kumimina dawa iliyoko ndani yake na kisha taratibu akammwagia Sheila kichwani.Mwili ukazidi kumchemka kwa ashki na kwa kasi akavua ile nguo aliyokuwa amejifunga kiunoni na kumuendea Sheila pale chini alipokuwa ameinama.

    " Mizimu imekuja sasa na inaanza kufanya kazi yake.Ipe mizimu nafasi ifanye kazi yake." akasema mzee Mtuguru huku akimshika shika Sheila maungoni na kumfanya atoe miguno iliyozidi kumchanganya mzee Mtuguru.Mganga akashindwa kusubiri na kwa kasi akaanza kumuingilia Sheila.Ile dawa aliyommiminia kichwani ilikwishampumbaza na kumfanya afurahie kitendo kile.Mzee Mtuguru jasho lilikuwa likimtoka kwa mapigo ya Sheila ambaye kwa wakati huo hakuwa na ile akili yake ya kawaida kutokana na kupumbazwa na dawa za mzee Mtuguru.Baada ya kumaliza mizunguko miwili mzee mtuguru na Sheila walikuwa hoi wakalala juu ya ule mkeka wamekumbatiana.mganga alikuwa akihema kama ng'ombe aliyetoka kulima.

    " duh ! ni muda mrefu sana sijapata faraja kama hii..mtoto ameumbika huyu sijawahi kuona..." akawaza mganga mzee Mtuguru.

    Ni sauti ya mama msaidizi wake ndiyo iliyomstua mzee Mtuguru katika kile kibanda.Haraka haraka akainuka na kuvaa nguo yake kwa aibu.Walikuwa wakifokeana na yule mama.Mzee Mtuguru alikuwa amelewa kwa penzi alilopewa na Sheila na akajisahau kuhusu dawa iliyokuwa iikendelea ya Emmy.Muda ulipozidi kusonga bila kurejea kule alikokuwa amemucha Emmy ,yule msaidizi wake aliamua kumfuata kule ilikokuwa ikifanyika dawa ya Sheila ambako alimkuta mzee Mtuguru ameanza kupitiwa na usingizi kwa uchovu.Huku wakizozana kwa lugha yao wakaanza kuondoka kwa kasi kuelekea kwa Emmy.Sheila bado alikuwa amelala usingizi mzito hajitambui.

    ********************

    Saa nane za usiku tukiwa kitandani nilimshuhudia malaika wangu Clara akiamka kwa kasi toka usingizini.Alikuwa akihema kwa nguvu.

    " Clara what's wrong my dear? nikamuuliza kwa wasi wasi.Sikuwahi kumuona akiwa katika hali ile.Jasho jingi lilikuwa likimtiririka.Nikachukua haraka glasi la maji na kumpa

    " Kunywa maji Clara and calm down.." Nikasema huku nikimpa Clara lile glasi la maji akanywa.Nikachukua kitambaa na kumfuta jasho.

    " Nini kimetokea Clara? Una tatizo gani? nikamuuliza huku nimemkumbatia.

    " Wayne nimeota ndoto mbaya sana...Ouh gosh it was so terrible.." akasema Clara kwa sauti ya uoga.

    " a dream !! ..NIkauliza kwa mshangao.

    " Ndoto ya kutisha sana .." akasema Clara

    " And it was so real..." akasema

    " Ndoto yenyewe ilikuwaje? Nikamuuliza.

    Clara akakaa kimya na kisha akasema.

    " Wayne do you believe in God?

    " Ofcourse I do" nikajibu

    " Ok let us pray" akasema Clara

    Tukapiga magoti na Clara akaongoza sala.Baada ya kusali kwa saa moja na nusu tukapanda tena kitandani.Nilijaribu kumshawishi Clara anieleze ndoto ile aliyoota ilikuwa inahusu nini lakini aligoma kata kata kunieleza zaidi ya kusisitiza kwamba ilikuwa ya kutisha sana.

    " Wayne kuanzia sasa inatubidi kujiweka karibu na mikono ya Mungu..something isn't right" akasema Clara na kuzidi kunichanganya.

    " Kwa nini unasema hivyo Clara ? Nikamuuliza

    " Ouh Wayne my love just forget it..lakini ni muhimu kujikabidhi kwa Mungu ..just for protection" akasema Clara na kunikumbatia kwa nguvu.

    " Please my angel dont ever leave my side..I'm so scared" akasema Clara nami nikamkumbatia kwa nguvu.Nilikuwa na mawazo mengi sana na sikuweza tena kupata usingizi .Ndoto aliyoota Clara ikazidi kunipa maswali mengi.

    Saa tisa na robo simu yangu ikaita.Nikaichukua na kuangalia mtu aliyenipigia simu nikakuta ni baba mkwe yaani baba yake Emmy.Nikapatwa na wasi wasi kidogo kwa sababu hajawahi kunipigia simu katika muda kama ule.

    Nikaipokea simu ile na kuongea naye.Taratibu nikajikuta mkono ukiisha nguvu na simu yangu kuanguka chini.Clara alikuwa ameamka akinitazama.

    " Wayne my love nini tena? akauliza Clara huku akiiokota simu yangu na kuiweka mezani.

    " Baraka" Nikasema taratibu

    " baraka ? akauliza Clara

    " yah ! Baraka is dead" Machozi yakanitoka

    Clara naye akashindwa kujizuia kulia.

    " Wayne tell me its not true..Baraka huyu mtoto wa Emmy?

    " Ndiye huyo huyo" nikajibu huku machozi yakinitoka.

    " Hebu nieleze vizuri Wayne ili nielewe..amekufaje?

    " Kwa mujibu wa baba mkwe ni kwamba Baraka ameanza kuumwa ghafla usiku huu ikawalazimu kumkimbiza hspitali lakini kabla hawajafika hospitali Baraka akafariki dunia.Na....." Nilishindwa kuendelea kuongea kwani nilisikia uchungu mkubwa moyoni.Kwa mara nyingine tena nilipata maumivu makali ambayo yalipita maumivu ya kawaida.

    Clara akashika kichwa chake alishindwa kuyazuia machozi kumtoka.

    " Wayne I cant believe this...Baraka is dead? akasema Clara huku akilia.

    Mwili wangu uliishiwa nguvu.Nilikaa kitandani machozi yakinitoka.Kwa kawaida mimi huwa ni mvumilivu sana lakini kwa habari hii ya kifo cha baraka nilishiwa nguvu kabisa.Nimepitia magumu mengi na sikuweza kuangusha chozi lakini kwa hili la Baraka nilishindwa kuvumilia.

    " Baraka...why you my son ?.... Nikalia kwa uchungu.Nilisikia uchungu mkubwa ambao sijawahi kuupata.Nilihisi kama vile moyo wangu unakatwa vipande vipande.Nilisikia uchungu ambao siwezi kuelezea maumivu yake.Clara akaja na kunikumbatia.Alikuwa akilia.Akachukua kitambaa na kunifuta machozi.

    " Nyamaza kulia Wayne....Jipe moyo mpenzi wangu..kaza moyo" akasema Clara huku akinipiga piga mgongoni.Si kitu cha kawaida kwa mwanamke kumbembeleza mwanaume asilie kwa sababau imezoeleka kwamba wanaume ni watu majasiri na huwa wanalia kwa ndani lakii leo hi mambo yalikuwa tofauti .Nilishindwa kuwa na ule ujasiri wa kiuanaume.Nilishindwa kujizuiq kububujikwa na machozi.

    " Clara I cant ..Let me cry..Ninasikia uchungu mkubwa..Wish like I'm going to die too...."

    " Usiseme hivyo Wayne..jipe nguvu hii yote ni mipango ya Mungu" akasema Clara kwa uoga.

    " Clara hujui moyo wangu una uchungu kiasi gani kwa taarifa hizi.Baraka amezaliwa nikimuangalia.Nimemlea mimi mwenyewe kama mwanangu na kumsomesha shule.Nimemlea katika mapenzi makubwa kama baba.Baraka alikuwa rafiki yangu mkubwa .Baraka alikuwa ni kila kitu kwangu.Nilimpenda Baraka kupita kitu chochote hapa duniani.He loved me so much...We used to play guitars every evening...:" Niikashindwa kujizuia kuangusha machozi.

    " Mungu wangu kwa nini umemchukua Baraka akiwa mdogo namna hii? Alikuwa na ndoto nyingi sana katika maisha yake.Alikuwa na ndoto za kuwa mwandishi wa vitabu..why you took him so soon?..." Nilikuwa nikiongea kila neno lillokuwa mdomoni mwangu.

    " Emmy I hate you !!!!..I hate you so much Emmy..wewe ndiye chanzo cha haya mambo yote yaliyotokea.Kama isingekuwa wewe ningekuwa na maisha mazuri na Baraka.Ouh Baraka my son nitakupata wapi tena.!!!"..machozi yaliendelea kunibubujika.Clara akaniletea glasi ya maji nikanywa.Akakaa karibu yangu akinihurumia.Hata yeye pia aliumia sana kwa taarifa zile.Alionana na Baraka siku chache zilizopita na wakatokea kuelewana sana.Taarifa za kifo cha ghafla ni wazi zilimstua mno.

    " Clara my love Nimepitia matatizo mengi sana na nimevumilia yote lakini kwa hili nimesindwa kuvumilia.Ninasikia kama moyo wangu unakatika vipande vipande.Ninasikia maumivu ambayo siwezi kuyaelezea." Nikamwambia Clara.

    " Wayne jipe moyo yote hii ni mipango ya Mungu.Kaza moyo haya ndiyo maisha ya mwanadamu" akasema Clara. Nilimwelewa Clara alivyokuwa akisema lakini kila nilipoikumbuka sura ya Baraka machozi yakanitoka.

    " Yote haya yamesababishwa na Emmy.Kama si yeye haya yote yasingetokea.I'll never forgive Emmy..I'll hate her till the day I die" Nikasema kwa uchungu.Clara alikuwa amekaa pembeni yangu akijaribu kunipa moyo katika wakati ule mgumu niliokuwa nao.

    " Clara twende hospitali nkahakikishe kama ni kweli Baraka amefariki dunia" Nikasema huku nikiinuka pale kitandani nikavaa viatu tukatoka.Clara ndiye aliyekuwa akiendesha gari. Nilikuwa nikimuelekeza njia ya kupita kuelekea katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru.



    Tukiwa njiani nilimpigia simu baba mkwe na kumuuliza mahala walikokuwa akaniambia kwamba bado walikuwepo katika hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya taratibu za kuuhifadi mwili wa marahemu.Tulifika pale katika hospitali ya Mount Meru tukashuka nikampigia simu baba mkwe kwamba tayari tumekwisha wasili bila kupotea muda akatufuata.Baba mkwe aliponitazama machoni aligundua kwamba macho yalikuwa mekundu kwa sababu ya kulia.

    "Baba naomba uniambie ni kweli Baraka amefariki? nikauliza haraka haraka.Nilikuwa ni kama nimechanganyikiwa,

    " Pole sana Wayne.Nafahamu ni jinsi gani tukio hili limekustua na kukuumiza.Hata sisi sote bado hatuamini lakini ndiyo hivyo ilivyotokea.Mipango ya Mungu siku zote huwa haipingiki.Kitu cha msingi ni kujipa moyo na kukubaliana na hali halisi japokuwa inauma sana " akasema baba mkwe na kunifanya machozi yanitoke tena.Nikachukua kitambaa na kujifuta.

    " Baraka is too young to die..Hebu nieleze baba kifo chake kimetokea katika mazingira gani? nikauliza.

    " Kifo cha huyu mtoto kimetokea katika mazingira ya ajabu ajabu sana kiasi kwamba hata sisi bado hatuamini kama ni kweli Baraka hatunaye tena.Baraka hakuwa akiumwa kitu chochote.Alikuwa ni mzima wa afya .Amecheza na wenzake na ilipoingia jioni akaingia ndani akafanya kazi walizopewa shuleni.Baada ya hapo tukapata chakula cha usiku wote pamoja kisha tukasali sala ya jioni halafu Baraka akenda chumbani kwake kulala akiwa mzima wa afya.Mida ya kama saa sita za usiku Baraka akagonga mlango wetu na kusema kwamba kichwa kinamuuma sana.Bibi yake akampa dawa ya kutuliza maumivu ya kichwa tukiamini baada ya muda mfupi kichwa kitapona .Baada ya kunywa dawa ile ya maumivu Baraka akarejea tena chumbani kwake kulala.Dakika thelathini baadae akagonga tena mlango wetu akasema anasikia homa kali.Ni kweli mwili wake ulikuwa na joto kali sana Nikamwambia bibi yake tumkimbize hospitali .Tukaingia garini na kuanza safari ya kuelekea hospitali lakini kwa bahati mbaya alifariki tukiwa njiani.Tulipofika hapa madaktari wakasema kwamba mtoto alifariki kitambo.Kwa kweli hata mimi mwenyewe siamini mpaka hivi sasa ju ya tukio hili.Kifo cha Baraka kimetustua sana.Bibi yake yeye anasaidiwa na madaktari kwa sababu mpaka sasa hivi amekwisha zirai mara mbili.Kwa kweli ni tukio la kustusha sana"

    " Ouh Baraka .why you my son.why so soon...." Nikasema kwa uchungu sana halafu nikasogea pembeni kidogo ili nifute machozi.Sikutaka baba mkwe anione nikilia.

    " Emmy yuko wapi..? Ana taarifa za tukio hili? Nikamuuliza baba mkwe

    " Emmy hana taarifa bado.Simu yake haipatikani na hatuelewi yuko wapi." akasema baba mkwe.Nikapatwa na hasira sana kwa uzembe wa yule mwanamke.

    " Mwanamke mzembe sana huyu .Yaani anathamini starehe na kumuacha mwanae hadi akafariki....I'll never forgive you Emmy for this " Nikasema kwa hasira.Nikamuomba baba mkwe anipatie namba za simu za Emmy nijaribu kumpigia .Nikapiga namba nilizopewa na baba mkwe lakini hazikuwa zikipatikana.Nikauma meno kwa hasira.

    " Huyu mwanamke atakuwa wapi mida hii? ..Nikajiuliza bila kupata jibu.Wazo likanijia nijaribu kuwasiliana na Chris ili nimuulize kama anaweza kufahamu mahala alipo Emmy.Chris aliwahi kuwa rafiki yangu mkubwa lakini urafiki wetu ulikufa pale aliponisaliti kwa kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na Emmy na baadae Emmy akahama kwangu na kuhamia kwake.Bado nilikuwa na hasira naye lakini kwa wakati kama huu niliamua kuyaweka masuala yote kando na kutafuta mshikamano.Niliamini kweli matukio kama ya msiba yanasaidia sana kumaliza tofauti za watu.

    Niliziandika namba za Chris.Nilikuwa nimeziweka kichwani.Niliziandika katika simu yangu nikapiga.Simu ikaita lakini haikupokelewa.Ikaita tena mara ya pili haikupokelewa.Ikaita kwa mara ya tatu ikapokelewa.

    " Hallow" Ikasema sauti niliyoitambua ilikuwa ya Chris.

    " Hallow Chris habari yako ndugu yangu"

    " Habari nzuri ..naongea na nani" akauliza Chris nikajua tayari amekwisha zifuta namba zangu za simu katika simu yake.

    " Unaongea na Wayne hapa" Nikasema halafu kikapita kimya kifupi.Nina imani lazima Chris alikuwa amestuka sana kusikia nikimpigia simu muda ule.Hakuwa ametarajia kama ningempigia simu tena

    "Wayne !!!.....akauliza kwa mstuko

    " Ndiyo ni mimi Wayne." Nikajibu nikasikia akivuta pumzi ndefu .

    "Chris samahani kama nimekusumbua lakini imenilazimu kukupigia simu kwa jambo la muhimu sana." Nikasema

    "Nakusikiliza Wayne" akajibu Chrishttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Chris unaweza kufahamu mahala alipo Emmy kwa sasa? nikauliza

    " Hapana siwezi kufahamu alipo Emmy kwa sababu nilikwisha achana naye kitambo.Mbona nilikupigia simu nikakufahamisha kwamba Emmy siko naye tena? akasema Chris.

    " Nalifahamu hilo Chris lakini imenilazimu kukupigia kukuuliza pengine unaweza ukafahamu mahala alipo.Tumemtafuta kila mahala hapatikani na simu yake amezima." Nikasema

    " kwani kuna tatizo gani Wayne hadi umtafute Emmy usiku wote huu ? akauliza Chris

    "Kuna matatizo makubwa yametokea.Baraka amefariki dunia"

    " Baraka !!!!!..baraka huyu mtoto wa Emmy..? akauliza kwa mstuko Chris

    " Ndiyo ." nikajibu

    " Wayne najua mimi na wewe hatuna mahusiano mazuri siku hizi lakini naomba tafadhali uniambie kama taarifa hizo ni za ukweli " akasema Chris.Niliisikia sauti yake ni wazi alikuwa akiongea huku akitetemeka.

    "Ni kweli Baraka amefariki dunia .Kifo hiki kimetustua sote.Kimetokea ghafla sana." nikasema na kumsikia Chris akivuta pumzi ndefu

    " Kwa sasa uko wapi Wayne? akauliza Chris

    " hapa niko Mount Meru hospital" Nikajibu

    " Ok nakuja sasa hivi" Chris akajibu.

    Nilipomaliza kuongea na chris simuni nikamuona baba mkwe akiwa amesimama na daktari mmoja wakiongea nikamshika mkono Clara tukawafuata.

    "madaktari wamemaliza kuufanyia uchunguzi mwili wa Baraka na wamegundua kwamba kilichomuua Baraka ni moyo wake kushindwa kufanya kazi ghafla." akasema baba mkwe na sote tukastuka.Toka nimekaa na Baraka sijawahi kusikia hata mara moja kwamba Baraka ana matatizo ya moyo.Ikanilazimu kuuliza

    " Baba hili tatizo la moyo limemuanza muda gani kwa sababu ni muda mrefu nimekaa naye na sijawahi kusikia kwamba Baraka ana matatizo ya Moyo."

    " Hata mimi nimeshangaa sana kwa taarifa hii ya daktari." akasema baba mkwe akiwa ameinama.Ilionyesha wazi kwamba naye amechanganyikiwa.

    " Emmy bado hapatikani hewani? akauliza baba mkwe

    " Hapana bado hapatikani hewani .Ana shoga yake mmoja anaitwa Sheila lakini kwa bahati mbaya nimezifuta namba zake.Huyu ni rafiki yake mkubwa sana." nikasema wote tukajikuta hatujui tufaye nini.

    " Baba tunaweza kuruhusiwa kuuona mwili wa Baraka? nikauliza

    " Twendeni huku" akasema baba mkwe tukaelekea katika chumba cha kuhifadhia maiti ambako ndiko mwili wa Baraka ulipelekwa.Baba mkwe alitufanyia ishara tusimame pale nje yeye akaingia ndani akaongea na wale wahudumu wa kile chumba halafu akatuita tuingie ndani.Kile nilichokuwa nikiamini labda ni ndoto hakikuwa ndoto tena bali ni kweli.Baraka alikuwa amefariki dunia.Alikuwa amelala juu ya kitanda akiwa amefumba macho.Ukimuangalia ni kama alikuwa amelala.Nilihisi kuishiwa nguvu.Niliumia mno moyoni.

    " Ouh Baraka..its true..Ouh son" Nilishindwa kuyazuia machozi kunitoka.baba mkwe akanishika .

    " kaza moyo Wayne.Najua inauma lakini lazima tukaze mioyo." akasema baba mkwe.Nilimsogelea baraka pale alipokuwa amelazwa nikamkumbatia na kumlilia.Nilimpenda mno Baraka lakini kwa sasa hakuwa tena na kauli.Alikwisha fariki.Baada ya dakika kama kumi hivi wahudumu wa chumba cha maiti wakatuomba tutoke mle ndani kwani kuna maiti walihitaji kuziingiza.

    Machozi bado yaliendelea kututoka mimi na Clara.Baba mkwe akatufariji.Tulipotoka katika chumba cha maiti mara nikakutana uso kwa uso na chris.Mwili ukanisisimka nikafuta machozi.Baba mkwe naye akamtazama Chris kwa jicho kali lakini kwa muda kama ule hakuna mtu aliyethubutu kumsemesha kitu.

    " Poleni sana" Chris akatuambia.

    " Baraka yuko wapi? akauliza Chris akiwa bado haamini kama ni kweli Baraka amefariki dunia.

    " Amekwisha ingizwa katika chumba cha maiti na haruhusiwi mtu kuingia tena"

    " Ouh Baraka..masikini Baraka .." akasema Chris ambaye ni dhahiri alikuwa ameishiwa nguvu .

    " Emmy amekwisha patikana ? akauliza Chris

    " Mpaka dakika hii hajulikani yuko wapi" Nikajibu

    " Ouh Mungu wangu ! huyu mwanamke ni maisha ya namna gani anaishi haya? Mpaka mida hii anahangaika na starehe hajui kama mwanae ameaga dunia" akasema Chris huku akikaa chini.Muda ule ule likaingia kundi kubwa la watu wakiwemo ndugu na majirani .Kila mmoja hakuamini kama ni kweli Baraka amefarki dunia.Wote walikuja kuhakikisha kama ni kweli.Eneo lile likageuka la vilio.Ikatulazimu kuwatuliza akina mama Tukasogea pembeni na baba mkwe na kujadiliana nini kifuate.Kilichoendelea ni kurudi nyumbani kuendelea na taratibu za msiba.

    " Kama ni hivyo basi mimi na Chris tunakwenda kumsaka Emmy hadi tumpate.Tutaingia katika kila klabu ya burudani hapa Arusha hadi tuhakikishe tumempata." nikamwambia baba mkwe halafu nikamuendea Clara.

    " Clara utaondoka na gari letu.Mimi nitaondoka na Chris tunakwenda kumtafuta Emmy hadi tumpate.Tutakutana msibani"

    " Are you sure you are ok Wayne? akauliza Clara kwa wasi wasi.

    " I'm ok Clara" Nikajibu kisha nikaagana na baba mkwe nikaingia katika gari la Chris tukaondoka maeneo ya hospitali.

    " Tunaanzia wapi kumtafuta Emmy? akauliza Chris.Alikuwa na wasi wasi mwingi lakini kwa wakati huo haukuwa muda wa magomvi tena.

    " Tuanzie nyumbani kwangu..Yawezekana akawa amejifungia mle chumbani na mwanaume " nikasema

    " Wayne hebu nieleze nini kimemuua Baraka? kwa sababu bado siamini kama ni kweli Baraka amefariki" akasema Chris.

    " Mimi nimepigiwa simu usiku huu na baba mkwe akanipa taarifa hizo na hata mimi sikuamini hadi nilipokuja hapa nikashuhudia kwa macho yangu Baraka amekufa.Its so hard to believe" Nikasema

    " Inauma sana ..nashindwa hata niseme nini..Najua mimi na Baraka hatukuwa marafiki and I didnt have a time to say I'm sorry"Akasema Chris kwa masikitiko makubwa.Sikujibu kitu.

    Tulifika nyumbani kwangu na kusimamisha gari nje ya nyumba.Taa za nje ya nyumba zilionekana kuwaka lakini taa za ndani zilikuwa zimezima.Nikabonyeza kengele ya mlangoni.Baada ya dakika kumi hivi geti likafunguliwa na msichana mmoja ambaye ninamfahamu kama rafiki wa Emmy.Aliponiona alistuka mno.

    " Karibu shemeji" akasema msichana yule huku akitetemeka.Sikuhitaji maongezi mengi nikamuuliza

    " Emmy yuko wapi ? Nikauliza kwa ukali kidogo na msichana yule akaogopa kunijibu

    " Emmy yuko wapi? Yuko ndani? Nikauliza safari hii kwa ukali zaidi

    " Emmy hayupo" akajibu yule msichana

    " Amekwenda wapi?

    "Alisafiri amekwenda Tanga"

    " Tanga? Nikastuka

    " Ndiyo"

    " Amekwenda kufanya nini Tanga?

    " Mimi sifahamu lakini aliondoka na Sheila na sisi akatuambia tumlindie nyumba yake hadi hapo atakapokuwa amerudi" akasema yule msichana.

    " Una uhakika Emmy hayuko ndani?

    " hapanaShemeji .Emmy hayumo humu ndani.kwani kuna tatizo gani?

    " Mkiwasiliana naye mwambieni kwamba mwanae Baraka amefariki dunia ghafla usiku huu"

    Msichana yule akastuka na nusura aanguke chini kwa mstuko alioupata.Akashika kichwa kwa mikono yake

    " Ouh Masikini Emmy kamuua mwanae...!!! akasema msichana yule kwa sauti ndogo lakini niliyoweza kuisikia vizuri

    " Unasemaje ? Nikamuuliza tena kwa ukali.Msichana yule akastuka na kutaka kurudi ndani haraka nikawahi kumdaka mkono.

    " Nimesikia ulivyosema.Naomba unieleze ukweli tafadhali.Emmy amefanya nini !!! "Nikauliza kwa ukali

    Huku akitetemeka akasema

    " Shemeji naomba nikueleze ukweli.Emmy na Sheila wameenda Tanga kwa mganga "

    " Mungu wangu !! " nikajikuta nikisema huku nikihisi mwili wangu ukiloa jasho

    Niliinua mikono yangu nikaiweka kichwani.Nilihisi kama kichwa kinazunguka.Taratibu nikakaa juu ya tofali.Nilihisi kuishiwa nguvu.Chris ambaye alikuwa amesimama nyuma ya gari akiongea na simu akanifuata pale chini nilipokaa juu ya tofali akaniuliza.

    “ Wayne nini kinaendelea hapa? Emmy yuko wapi?..

    Nilikosa jibu la kumpa kwa haraka.Akili yangu bado haikuwa ikifanya kazi sawa sawa.Nilikuwa katika mstuko mkubwa.

    “ Wayne..Emmy yuko wapi? Akauliza tena Chris lakini sikumjibu kitu.Midomo ilikuwa mizito kufunguka kutokana na hasira nilizokuwa nazo.Chris akamfuata yule msichana ambaye alikuwa amesimama nyuma ya geti naye akilia akamuuliza mahala alipo Emmy lakini msichana yule hakumpa jibu lolote zaidi ya kuendelea kulia.Chris akanifuata tena pale nilipokuwa nimekaa.

    “ Wayne nafahamu kwamba mimi na wewe tunatofauti kubwa lakini naomba kwa sasa tuziweke tofauti zetu pembeni na tuangalie kwanza suala la muhimu lililoko mbele yetu.Tunatakiwa tusaidiane kumtafuta Emmy .” akasema Chris huku akiniangalia kwa wasi wasi.Nikainama chini kwa sekunde kadhaa halafu nikainua kichwa na kumtazama nikasema

    “ Emmy amekwenda kwa mganga Tanga.Emmy amemuua mwanae “ nikasema kwa uchungu mkubwa.

    “ Sijakuelewa vizuri Wayne..Emmy amefanya nini? Akauliza Chris.

    “ Emmy amekwenda kwa mganga Tanga .Amemuua mwanae.Emmy kamuua baraka” Nikasema kwa sauti ndogo.Chris akavuta pumzi ndefu akaliegemea geti.

    “ This woman is a monster “ akasema Chris kwa hasira.

    “ Nina uhakika mkubwa lazima atakuwa amejiingiza katika masuala ya kishirikina ndiyo sababu ya Baraka kufariki ghafla.” Akasema tena Chris.Kikapita kimya kifupi halafu Chris akauliza

    “ kwa hiyo tunafanya nini Wayne?

    “ Hatuna cha kufanya..Twende tukaendelee na taratibu nyingine za msiba.Atakapokuja atakutana na msiba wa mwanae.Stupid woman” nikasema huku nikiuma meno kwa hasira.Tukaingia garini na kuondoka kurejea msibani.

    “ Sababu gani iliyompelekea Emmy aende kwa mganga? Akauliza Chris wakati tukielekea nyumbani kwa wazazi wake Emmy ambako ndiko msiba wa Baraka ulikuwepo.

    “ Sifahamu sababu hasa ya kumfanya aende huko kwa mganga .Ninahisi pengine kitendo cha mimi kuamua kuachana naye kisheria kimemchanganya kichwa zaidi na kumfanya aende huko alikoenda ingawa sijafahamu ni kwa malengo yapi.” Nikasema na kumfanya Chris ageuze shingo na kunitazama.

    “ mmeachana kisheria? akauliza Chris

    “ Ndiyo.Nimeamua kuachana naye kisheria ili asitambulike tena kama mke wangu.Nafikiri suala hili ndilo lililopelekea aamue kwenda huko kwa mganga.Ninadhani lengo lake kubwa ni kulipiza kisasi kwangu mimi na kwa mpenzi wangu wa sasa Clara.Ninakumbuka mara ya mwisho tulipofanya kikao pamoja na ndugu na wazazi wake alitamka kwamba atayafanya maisha yangu kuwa magumu sana.Nadhani kwenda kwa mganga ilikuwa ni moja ya plani zake za kutaka kupambana nami na kuyafanya maisha yangu kuwa magumu.Ninakumbuka muda mfupi kabla sijapokea simu toka kwa baba mkwe akinitaarifu kuhusu kifo cha ghafla cha Baraka Clara alistuka toka usingizini alikuwa akiweweseka.Alisema kwamba aliota ndoto mbaya sana lakini hakunisimulia ndoto hiyo ilihusu nini.Baada ya muda mfupi baba mkwe akanitaarfu kwamba Baraka amefariki dunia.Nina hasira sana na huyu mwanamke laiti kama ningemtia machoni muda huu ningeweza hata kumkata shingo yake..” nikasema kwa uchungu.

    “ Baraka nimemlea mimi mwenyewe nikidhani ni mwanangu wa damu lakini kumbe sivyo nilivyokuwa nikifikiria.Nilimpenda sana yule mtoto na hata baada ya mambo haya kujitokeza nikatambua kwamba si mwanangu bado nimeendelea kumpenda sana na kumjali kama mwanangu.Alikuwa na ndoto nyingi akiwa mkubwa lakini ndoto zake zote zimemeyuka kama mshumaa.Amekatishwa uhai wake na mwanamke mwenye roho ya kikatili mfano hakuna.Mama yake aliyemzaa ameamua kumtoa uhai wake..Inaniuma sana Chris..Inaniuma mno” nikasema na kuinama chini nikashindwa kuyazuia machozi kunitoka.

    “ kaza moyo Wayne..Nafahamu ni jinsi gani ulimpenda Baraka. Hata yeye alikupenda kupita kiasi na siku zote hakutaka kusikia kwamba wewe si baba yake mzazi.Emmy amefanya ukatili mkubwa sana.Amewadhulumu na kuwaumiza watu wengi kwa vitendo vyake vya kikatili anavyovifanya.Sijawahi kukutana na mwanamke mwenye roho ya kikatili kama huyu.Ninajuta hata kumfahamu “ akasema Chris…..

    “ Kuna nyakati ninahisi ni bora kama nisingeufahamu ukweli ningeendelea kuishi maisha ya raha na amani nikiwa na baraka.Siku zote nikiwa naye nilikuwa nasahau taabu na maudhi yote ya Emmy.Masikini Baraka…” Nikasema

    “ Kwa hiyo tutafanya nini kuhusu huyu shetani Emmy? Akauliza Chris

    “ Bado sijapata jibu nini cha kufanya.Tushughulikie kwanza msiba umalizike halafu nitajua nini cha kufanya..Safari hii amevuka mpaka..I’ll make her life a living hell.She’ll feel the pain zaidi ya ninavyohisi sasa..Yatakuwa ni zaidi ya maumivu” nikasema kwa hasira.Chris hakujibu kitu.akanitazama halafu akaendelea kuendesha gari .

    Nilikuwa nikisia maumivu makali ya moyo.Kifo kile cha ghafla cha Baraka kilinipa machungu mengi.Kilinikumbusha karaha na vitimbwi vyote vya emmy toka nilipoonana naye hadi leo hii.Nikazidi kumchukia mwanamke huyu ambaye kwa sasa nilimuona kama ni kiumbe asiye na roho..

    " Kama amejiingiza katika masuala haya ya uganga basi hata malaika wangu Clara atakuwa hatarini..Lazima atataka kulipiza kisasi kwa Clara akiamini kwamba ndiye chanzo cha yeye kuachana na mimi.Siamini katika uchawi na nitamtegemea Mungu siku zote.Yeye hashindwi na jambo lolote." Nilikuwa nikiwaza nikastuliwa na mtetemo wa simu yangu.Nikaitoa mfukoni na kuangalia mpigaji alikuwa ni Clara..http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Hallo Clara" Nikasema baada ya kuipokea simu.

    " Hallo Wayne habari za huko?mmefanikiwa kumpata Emmy? akauliza Clara

    " Emmy hatujafanikiwa kumpata lakini tuliyoyagundua huku yanasikitisha sana" nikajibu

    " Mmegundua kitu gani? akauliza Clara kwa wasi wasi

    " Nitakueleza tukifika.Hivi sasa tuko njiani tunakuja"

    "Ok mpenzi naomba ufike salama unifahamishe hicho mlichokigundua huko kwa Emmy..Nimeanza kuwa na wasi wasi mkubwa kwa mambo ambayo yameanza kuongelewa hapa msibani" akasema Clara

    " mambo gani yanaongelewa hapo msibani? Nikauliza

    " Tutaongea ukifika hapa Wayne.." akajibu Clara na kukata simu

    Nikavuta pumzi ndefu na kuirudisha simu mfukoni.



    ***************************





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog