Simulizi : Mshumaa
Sehemu Ya Nne (4)
Njaa ililisumbua tumbo lake. Miungurumo isiyoeleweka aliiskia tumboni mwake. Alikumbuka tangu alipokula mchana wa siku iliyopita chuoni ndio hadi muda huo hakula tena chakula kinachoeleweka zaidi ya shurubati tu kipindi alipokuwa na kijana Suma kule Reustaurant. Majira hayo yalikuwa ni saa saba kasoro mchana. Akajiinua kiuvivu pale alipokuwa huku maumivu yakiwa nae. Akaingia chooni walau aoge ili apunguze uchovu aliokuwa nao.
Alipotoka. Akabadili nguo na kuchukua pesa kwenye mkoba wake. Akatoka nje ambapo alimkuta Rebeka akiandaa chakula muda huo. Chuki aliyonayo kwa mwanamke huyo ilipelekea mpaka kutomsalimia kwa mara ya kwanza tangu amjue. Akapitiliza mpaka nje na huko ndani kilisikika kicheko cha dhihaka kutoka kwa Rebeka. Akapuuza na kuendelea na safari yake.
Dakika kadhaa akarudi akiwa amebeba kimfuko cheusi ambacho ndani yake kulikuwa na chakula alichoenda kununua. Akaingia ndani kwake akimuacha Rebeka mezani akila chakula alichotoka kupika. Majira hayo Frank alikuwa kazini.
Majira ya saa tisa alasiri. Suma hakupata ujumbe wowote kutoka kwa Shery wala kupigiwa simu tu. Akawaza labda huenda Shery amekwazika na yeye kutokana na yale waliyoongea siku iliyopita. Maana hata ondoka yake siku hiyo haikuwa yenye kutafsirika kirahisi kama amekwazika ama laa! Akiwa chumbani kwake. Akachukua simu yake na kuitafuta namba yake. Alipoipata, akaipiga.
Shery akiwa amejilaza kitandani kwake. Aliona simu yake iliyokuwa pembeni ya mto alioulalia ikiita. Akaivuta na kutazama ni nani mpigaji. Jina Suma likaonekana kwenye kioo. Alibaki akiiangalia tu pasi na kuipokea. Sio kwamba hakupendezwa na upigaji wa Suma muda huo. Ila mkanganyiko wa mawazo aliyokuwa nayo ndio unamfanya afikirie kuipokea simu hiyo. Simu ikaita mpaka ikakata. Lakini bado hakuitoa kiganjani kwake. Ni kama vile alikuwa akisubiri ipigwe tena ama anategea aone kama atapiga tena ama laa!
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Simu yake ikaita tena. Mpigaji akiwa ni yule yule. Aliitazama kwa muda na mwisho alikata shauri kuipokea. Maongezi ya salamu yakafuata na katika huko kusalimiana. Kijana Suma akagundua kuwa Shery hayuko sawa. Akajitahida kumuuliza nini tatizo lakini Shery alikana kwa kusema yupo sawa. Suma nae alikataa kata kata kuwa Shery asimdanganye ati yupo sawa. Akauliza labda kwamba ni yale maongezi ya siku iliyopita ndio yamemfanya awe hivyo?
Shery alikataa!.
Akamuuliza tena tatizo ni lipi ikiwa sio hilo. Shery alikaa kimya kwa muda akifikiria amuambie ama asimuambie. Mwisho alikata shauri kuwa amuambie huenda ikawa akapata wazo lolote kutoka kwa kijana huyo. Akamuambia!. Suma alikaa kimya kwa muda akitafakari amshauri vipi Shery. Baada ya kutafakari sana. Akamuambia kuwa siku inayofuata afanye juu chini wakutane ili ajue amshauri vipi.
Hata kuulizia juu ya ombi lake siku hiyo alishindwa baada ya kujua kwamba Shery hayupo sawa. Akamezea. Wakaagana kwa minijali ya kuonana siku inayofuata na simu ikakatwa.
Frank akiwa kazini kwake. Alikuwa akifikiria yale yaliyotokea jana. Hivi ni kweli zilikuwa ni akili zangu zile? Alijiuliza. Ni kosa lipi hasa hadi limepelekea kumpiga vile Shery? Siamini kama ni kweli ati amemtukana mke wangu. Hapana bwana. Shery hajafikia kuwa na tabia mbovu kiasi hicho cha kumtukana mtu yoyote sembuse Mama yake mdogo. Hapana. Zile hazikuwa akili zangu hata kidogo. Sasa nifanyeje ili niweke mambo sawa? Nimuombe msamaha? Hahaha mkubwa hakosei bwana siwezi kumuomba msamaha. Lakini Shery ni mkubwa yule ataelewa tu kwamba nilikosea na kuyaacha yapite.
Frank aliendelea kujiwazia mwenyewe. Mwisho akainuka pale alipokaa. Akachukua kilicho chake na kutokomea nje ya jengo lile. Akapanda kwenye gari lake na safari ya kurudi nyumbani kwake siku hiyo ikaanza. Ila alipanga ampelekee zawadi ishara ya kuwa amani iyendelee kati yao. Zawadi hiyo ni ipi?? Laptop akaiona itakuwa poa sana kwasababu Shery alikuwa bado ni msomi.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipitia kwenye maduka yanayouzwa vifaa hivyo na kununua moja. Baada ya kukamilisha kila kitu. Akatoka na kuingia garini kwake. Akaitazama ile Laptop kwa muda kisha akasikitika. Akawasha gari na safari ya kurudi kwake ikaanza. Dakika kadhaa akawa yupo nyumbani kwake. Akashuka kwenye gari na kuingia ndani.
Sebuleni alimkuta mkewe akiwa amekaa kwenye sofa akiangalia tamthilia. Rebeka alipomuona Frank akiingia hapo. Akainuka na kwenda kumpokea. Ila ule mfuko ambao ndani yake kuna ile Laptop Frank alikataa nao. Rebeka hakuhoji chochote kwasababu hakujua ndani yake kunanini. Frank alitoka hapo na kuuendea mlango wa chumba cha Shery. Akagonga hodi.
Muda huu Rebeka ambae mwanzo alipeleka ile mizigo ya mumewe ndani ndio alikuwa anatoka. Akaona Frank akigonga mlango kwenye chumba cha Shery. Akabana kutega aone Frank atafanya nini. Shery aliekuwa chumbani kwake muda wote. Alisikia mlango wake ukigongwa. Akakaa kimya maana alidhani ni Rebeka anataka kumletea chokochoko. Ila baada ya kusikia sauti ya Baba yake mdogo akijitambulisha. Aliinuka na kwenda kufungua.
Frank aliachia tabasamu ili kumtoa hofu Shery. Shery akamsalimia na alipoona Frank alikuwa na shida ya kuingia ndani. Akampisha. Mlango ukafungwa wakawa wenyewe ndani. Rebeka alipoona hivyo. Haraka haraka aliwahi kwenye mlango wa chumba cha Shery na kubana akisikiliza kitakachoongelewa humo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Frank japokuwa alipinga kumuomba msamaha Shery kwa yale aliyomfanyia siku iliyopita. Ila hapo alijikuta tu akiomba msamaha. Shery roho ilimuuma baada ya kujua kuwa hazikuwa akili za baba yake kumfanyia vile. Hapo akahisi kuna hila imetendeka tu kwa namna yoyote Rebeka kumfanyia baba yake. Shery akamsamehe kwa moyo mmoja baada ya kuombwa msamaha wa dhati na baba yake.
Frank baada ya kusamehewa. Alimtolea ile laptop aliyomletea kama zawadi na kumkabidhi. Shery alifurahi na kumkumbatia Frank. Kisha hapo akamuachia na kuitazama ile laptop. Frank baada ya kuhisi amesamehewa kabisa. Aliachia tabasamu kisha akamuaga Shery. Akainuka kwaajili ya kuondoka.
Rebeka kule nje ya mlango. Alisikia kila kitu kilichoongelewa na wawili wale. Alikasirika na kupanga mashambulizi zaidi dhidi ya Shery. Akatoka mbio mpaka sebuleni kwenye sofa na kwenda kukaa. Alikuwa kishari shari tu akimsubiria Frank atoke. Frank alienda mpaka pale alipo mkewe. Akamshika bega akitaka kumuuliza kulikoni.
Rebeka aliutoa ule mkono na kuutupilia pembeni. Frank alishangazwa na kitendo hicho. Alimtazama mkewe ambae yeye alikuwa akitazama pembeni kabisa. Akamuuliza nini tatizo na Rebeka akakaa kimya. Frank akarudia kumuuliza tena na Rebeka alimtazama kishari shari na kumuuliza.
“Chumbani kwa Shery ulienda fanya nini?” Frank alishangazwa na swali lile. Akakaa kimya huku akimuangalia Rebeka aliekuwa akimuangalia yeye kwa chuki.
“Nimeenda kumsalimia mwanangu. Ama kuna ubaya?” Frank alijibu huku akitabasamu, kisha akauliza. Rebeka hakuwa na cha kuongeza tena. Alikaa kimya kisha akaja na swali jengine.
“Vipi kuhusu ile hati ya nyumba? Hujui kama mimi ninashida na pesa?” Ebwana ee! Frank ni kama vile aliminywa sehemu fulani na kufanya asiwe na nguvu. Alianza kutetemeka na asijue ajibu nini kwenye hilo swali aliloulizwa. Baada ya muda akapata ujasiri na kuongea.
“Tutaongea baadae. Embu kwanza sasa niwekee chakula maana nina njaa” Rebeka alisonya kwa nguvu na kupotelea ndani.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku hiyo ikaisha bila kuwa na maelewano mazuri kati ya Frank na mkewe Rebeka. Rebeka alitaka kuelezwa kuhusiana na hati ya nyumba aliyoachiwa Shery huku Frank akibabaika asijue ajibu nini. Kila mmoja akalala upande wake na kuupitisha usiku huo pasi na maelewano mazuri.
Siku iliyofuata. Shery hakuweza pia kwenda shule japokuwa hali yake haikuwa mbaya sana. Hata hivyo alishatoa taarifa toka jana kuwa alikuwa akiumwa sana. Siku hiyo pia alikuwa chumbani kwake hakutaka kushirikiana chochote na mama yake mdogo. Alikuwa na hofu anaweza kumfanyia chochote kibaya maana alishona chuki za waziwazi alizoonyeshwa na Rebeka.
Alikuwa na laptop yake mpya aliyoletewa akirekebisha baadhi ya vitu. Alipohisi njaa, alitoka nje kwenda kununua alichokihitaji na kurudi kula chumbani kwake. Siku hizo hakutaka kabisa hata kumsalimu akihofu huenda salamu yake ikawa chanzo cha kudhurika. Maana hakuwa na imani nae tena, alishaanza kumuhisi tofauti.
Majira ya saa kumi na moja jioni. Alitoka baada ya kupigiwa simu na Suma kuwa aende Sizler Corner wakakutaniane kwenye mgahawa huo. Hata hivyo hakutaka kumuaga Rebeka kuwa anaenda wapi. Mpaka muda huo alishajiamulia kuwa mbali na mwanamke huyo ambae kwake alimuona kama shetani.
Dakika kadhaa akawa maeneo hayo. Akapiga hatua kuuendea mgahawa huo ambapo kwenye meza iliyokuwa kando kidogo aliweza kumuona Suma akiwa amekaa anamsubiri yeye. Kama kawaida ya kijana huyo aliinuka pindi tu alipomuona Shery akiingia hapo. Akamlaki na kumkaribisha kwenye kiti chengine na Shery alipokaa ndipo na yeye alikaa.
Pakafuata mazungumzo ya kawaida kabla ya kuingia kwenye mazungumzo yaliyowafanya wakutane mahala hapo. Salamu za hapa na pale huku wakiulizana hali. Kisha Shery akamuhadithia mwanzo mwisho kilichotokea mpaka kufikia siku iliyopita. Suma alimtazama kwa huruma Shery ambae kwa muda huo alikuwa akilia kwa uchungu.
Suma akavuta kiti na kukaa karibu yake kwaajili ya kumfariji. Akamvuta karibu yake na bila hiyana Shery alivutika. Akalala kwenye bega la Suma huku akilia kwa uchungu. Suma alianza kumbembeleza huku akimfariji kwa kumtolea maneno mazuri. Dakika kadhaa mbele Shery akatulia na utulivu ukapatikana.
“Siwezi kumuhisi vibaya mama yako ila kwa hayo maelezo yako uliyoongea. Inaonekana kuna nguvu flani anatumia kumuendesha baba yako. Maana...” Suma aliongea ila akakatishwa na sauti ya Shery.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unajua nini Suma. Hivyo unavyohisi hata mimi nimehisi hivyo hivyo. Maana mimi namjua sana. Tena sana baba yangu Frank jinsi anavyonihusudu. Sasa iweje mara hii abadilike ghafla?” Shery aliongea hivyo huku akimtazama usoni Suma utafikiri ana majibu ya hayo anayoyauliza.
“Mi naona tumshatakie Mungu hili swala” Suma aliongea.
“Kivipi?” Shery aliuliza.
“Kwasababu haya sio mambo ya kawaida. Inabidi umtafute mchungaji umueleze haya. Naamini atalipatia ufumbuzi” Suma aliongea hayo. Shery aliinamisha kichwa kwa tafakuri ya hayo aliyoelezwa na Suma. Alipoinua kichwa, alikuwa akitabasamu huku akimtazama Suma usoni. Hakika umenipa ushauri yakinifu sana. Alijiwazia.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hilo ni wazo zuri sana umenipa. Na sikuwahi kufikiria kitu kama hicho hata mara moja. Nashukuru sana Suma kwa ushauri wako”
Kwakuwa mchana wa siku hiyo hakuwa ametia chochote tumboni tangu alipokula asubuhi. Tumbo nalo lilimsumbua kwa njaa. Ikabidi aagize chakula. Wakati wanasubiria chakula kiletwe. Walikuwa wakiendelea na maongezi huku Suma akijitahidi kumuweka sawa Shery ili apate nafasi ya kugusia lile swala lake.
Hivyo alifaulu. Shery alirudi katika hali yali yake ya kawaida na kusahau kabisa visa vya Rebeka. Muda wote alikuwa na furaha kutokana na maneno ya kijana huyo ya ucheshi aliyokuwa akiyatoa. Muda kidogo chakula kililetwa na wakaanza kula taratibu huku wakipunguza uongeaji ili kuyapa nafasi nzuri makoo yao kupitisha chakula hicho.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment