Search This Blog

Friday, October 28, 2022

MSAMAHA BILA MALIPO (FORGIVENESS WITHOUT PAYMENT) - 3

 

     





    Simulizi : Msamaha Bila Malipo (Forgiveness Without Payment)

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Alisema binti Sophia akiwa katika hali ya ukiwa sana mpaka Robert akabakia kushangaa sana kwani alizoea kumuona Sophia mara nyingi akiwa mtu mwenye furaha mno si kama siku zote. Mtu huwa na furaha na siku zote huwa hazifanani. Haya ni maneno tu ya wahenga ingawa kuna muda yana maana na kuna muda hayana maana kabisa, hasa kwa mtu ambaye anajulikana yuko vipi muda wote.

    Robert mdomo ukamuwasha akamuuliza, kwa nini siku hii umekuwa mpole na

    mwenye mawazo kiasi hicho? Sophia akamwambia hakuna kitu kimsumbuacho bali ameamua kuwa hivyo siku hiyo.

    Robert haikumwingia akilini kabisa maana alikuwa anamfahamu vyema Sophia. Hapana, unanifumba tu nisijue tatizo ulilonalo bwana.” Alisema Robert huku akizidi kumwangalia Sophia usoni na kumdadisi kiundani zaidi.

    Robert hapana kweli mi ndivyo nimeamuwa kuishi hivi huwezi amini eti. Alisema Sophia muda huu kwa kutabasamu kidogo kufuta sura ya huzuni kwenye paji lake la uso. Kweli Sophia siamini bado naona kama unanipaka mafuta kwa kutumia mgongo wa chupa.” Alisema Robert huku akiondoka kwenda kufungua ofisi yake kama meneja masoko wa kampuni.

    Akawa amemuacha Sophia pale stooni ambako ndipo palikua mahali pake anapokaa. Na daima ndipo alipokuwa anapatikana awapo ofisini. “Dah! Yaani Damiani kunidanganya kote leo ananikana na kunifokea! Acha nimsamehe tu bila kulipiza.” Aliongea mwenyewe akirudia kauli hiyo kwa mara ya pili.

    Pindi anaongoea hayo mara Damiani akatia timu na gari lake akiwa amejawa na jaziba kubwa sana kupita maelezo kama awavyo siku nyinginezo moja kwa moja anaenda hadi stooni kwa Sophia kwa jaziba.

    “Nakuuliza unataka kuendelea na kazi ama unataka kuondoka mara moja?” aliuliza Damiani kwa jaziba! Sophia akashuka na kuwa mpole mno kisha akamwambia Damiani bosi samahani yameisha naomba unisamehe naomba bosi.” Alisema kwa utaratibu. “Kama unataka kuendelea na kazi naomba tafadhari tusifuatiliane sana sawa Sophia? Sijui kama unanielewa.

    Baada ya kusema vile Sophia akaanza kutokwa na machozi huku akisema “Sikutegemea kama ingekuwa hivi Damiani” Kisha Damiani anacheka kwa dharau huku akisema kwani ulizanije wewe? Sophia akajibu, Nilizani kuwa utakuwa na huruma ya kunisaidia kwa kuwa unafahamu matatizo yangu kuanzia kwangu mimi hadi ngazi ya familia.

    Damiani akajibu kwangu hayo siyo matatizo ila wewe ndiye uliyeyataka yote hayo. Baada ya muda mfupi Robert anaingia ndani kwa Damiani anamkuta Sophia ana majonzi kisha anawapa salamu kila mmoja. Shikamoo Damiani, anajibu Marahaba Robert. Baadaye Sophia anamsalimia Robert.

    Kwa kuwa Robert alimpenda sana Sophia basi maongezi kati ya watu watatu mara nyingi macho ya Robert yalikuwa yakimuangalia Sophia. Sophia naye akiwa mtu mwenye aibu kwa kuwa alikuwa kati ya watu wawili waliokuwa wakimpenda sana.

    Robert anaanza kumsifu Sophia kwa kusema “Ila we mtoto wa kike ni mrembo na mwenye heshima na sifa zote za kuwa mtoto wa kike unazo. Sophia anajibu kwanini umesema hivyo Robert?

    Huku Damiani akicheka kama alivyozoea kucheka.Sophia akarudia swali lile lile kwa Robert. Robert akajibu wewe naye hata husahau? Jibu la swali lako ni refu kidogo ila nitajitahidi kukueleza.

    Haya nieleze. Kwanza una mwendo kama mnyama mmoja hupatikana maporini na mwenye shingo ndefu lakini jina nimelisahahu, Damiani akasema kwa haraka, Twiga. Robert basi kama ulivyosikia Damiani akimtaja jina lake ndilo hilo. Sophia akasema kweli hiyo siyo sifa bali inaonyesha kuwa mimi sifai kuishi na wanadamu wenzangu kama nyie.

    Hakuna mrembo mwenye sifa hii, haina maana kama unavyodhani wewe. Sophia sifa hii ndiyo inayonifanya nikuite hivyo Damiani anasema kwa shingo upande mbona sifa hiyo nishamwambia zamani sana ila sema yeye ni mpenda kusikia sifa hiyo kama mbaya kwake Sophia ama kweli, tembea uone.

    Bali hayo yote matendo kati ya Robert na Sophia yalikuwa yakionekana kama hayana usawa mzuri ndio maana Damiani aliamua kukatisha maongezi yale kwa kusema “Robert maisha yanaendeleaje?

    Robert anajibu maisha kwa sasa ni mazuri hasa mwezi huu biashara ilikuwa nzuri sana. Kisha Sophia anaamua kuondoka na kuwaacha Robert na Damiani wakiendelea na maongezi yao.

    Wakati akitoka nje macho ya wote wawili yalikuwa mgongoni kwake. Maongezi yao baada ya muda mfupi wakaendelea kwa kuhojiana maswali kama hivi:-

    “Robert mbona unapata hela lakini hufikirii kupata mke wa kukupatia watoto kama mimi?

    “Rafiki yangu, wanawake wa siku hizi wanajipenda na kuwa wanampenda mtu mwenye uwezo mkubwa.Alijibu Robert.

    “Si kweli Robert mbona mimi nilimpata mke bila hata kuwa na akiba yeyote benki lakini nilimuoa yule mke wangu.

    “Damiani si unaona kuwa mimi bado ni mdogo’’alisema Robart.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya Sophia kupewa vitisho na bwana Damiani sasa anaamua kutulia kabisa tena bila hiyana na mtu kabisa. Mke wa Damiani naye kamvalia kidedea Damian akidai mmewe anamdanganya kwa sababu hamwambii mambo ya ofisini kwake na nia na malengo ya mke wa Damiani ni kujua kama yule mfanyakazi ni mwanaume au ni mwanamke.

    Haikuwa bure kabisa kwa mke wa Damiani kutaka kujua hivyo akiwa nyumbani mke wa Damiani anaamua kufanya kazi zake mapema na kwa haraka zaidi ili aende ofisini kwa mmewe kumwona huyo mfanyakazi mpya ambaye ameajiliwa na mmewe katika kampuni yao ya kusindika matunda.

    Mke wa Damiani aligundua mumewe anaanza kumficha baadhi ya mambo hataki ayajue kabisa ndivyo alivyohisi na roho yake ikamtuma kabisa kwenda ofisini kwa mmewe. kule ofisini wafanyakazi waliendelea kuchapa kazi.

    Damiani alikuwa ofisini akijaribu kutafakari hali yake.Ila kweli mimba itakuwa yangu lakini dah! anatulia na kuanza kuwaza sana kiasi kwamba anajisahau kabisa kufanya kazi pale ofisini lakini roho ya ukatili inamuingia Damiani “Aaah! Atajijua mwenyewe bwana” alisema Damiani kimoyomoyo akiwa mwenyewe ofisini kwake.

    Kisha anaamua kumuita Sophia ofisini kwake kuja kumpa maneno mengine ambayo ni ya kumtisha zaidi na dhihaka mbaya, Sophia anaitwa na mfanyakazi mwenzie.Sophia alikuja mbio baada ya kuitwa na kusukuma mlango wa kuingilia ofisini kwa bwana Damiani kwa nguvu.

    Kumbe kitendo hicho kilimuudhi sana bwana Damiani kisha anaanza kumfokea Sophia. “unafungua fungua mlango kwa nguvu au unadhania ni ya kwenu pale, mpuuzi wewe.” Aliongea kwa ukali kabisa na ukatili kisha anamwambia akae chini ampe somo.

    Baada ya kukaa Damiani anamwambia kuwa anaomba anapokuwa nyumbani kwake anapata starehe asiwe anampigia simu kabisa na akamwambia akirudia tabia hiyo ataondoka na kuacha kazi ndani ya ofisi yake. Damiani anaongea akiwa na sura ambayo haina huruma hata kidogo.

    Sophia anaanza kujuta huku machozi yakimtililika kwa wingi usoni.Nakuomba nyamaza na ondoa mkosi ndani ya ofisi yangu sawa.Alisema Damiani bila kuangalia usawa wa macho ya binti Sophia.Hilo ndilo halikumwingia akilini kabisa bwana Damiani aliona kama mchezo wa kuigiza kabisaa.Sophia anaamua kutoka mule ofisini akiwa hana raha kabisa.

    Kuanzia uso wake mpaka nafsi yake pia alikuwa hana amani kabisa.Wakati Sophia anatoka ofisini huku analia alikutana uso kwa uso na mke wa Damiani ambaye alikuwa akipanda ngazi za kuingia ofisini kwa mmewe.

    Mke wa Damiani anashangaa kumuona binti huyo ambaye anadhani si mfanyakazi katika kampuni yao na yuko katika hali kama hiyo akitokea ofisini kwa mmewe. Anamuuliza kwa upole. “na wewe hapa una kazi gani?

    Huku akizunguka kumuangalia kwa umakini kabisa.Sophia pasipo kutambua kama huyo ni mkewe Damiani, akamwangalia na kumwambia aache dharau kama ana shida ama anataka huduma aseme sio kuleta dharau.Kisha Sophia anamsonya kwa dharau ambayo mpaka mke wa bosi wake anajiona choo cha shimo kabisa ambacho hakina thamani mjini.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kisha mkewe Damiani anaondoka kwa dharau akijua huenda ni mpita njia tu kaja pale ofisini na njaa zake.Mke wa damian anaingia ofisini kwa mmewe.Baada ya kuingia Damiani alibaki kumshangaa sana mkewe. “Na wewe si ulikuwa nyumbani huku umeijia nini? Alisema Damiani huku bado akimshangaa kabisa. Nia na madhumuni yangu ni kutaka kumuona huyo mfanyakazi ambaye hutaki kuniambia wala kunionyesha kabisa”

    alisema mkewe akiwa katangulizana na watoto wake wote watatu ambao ni wakike wote maana hakuwa na mtoto wa kiume hata mmoja. Damiani akacheka.

    Ilikuwa ni muda wa mchana jua likiwa linawaka sana mama yake Sophia bado anaendeleza ile mila na desturi yake kama ilivyo ada, muda huu anatumia kuomba kwa aina ambayo ni tofauti kabisa.

    Kuna baadhi ya siku aliondoka hata bila kuacha sumni kabisa.Baada ya kutumia njia hii walau aliweza kupata riziki kidogo japo si kama ilivyokuwa mwanzoni. Utata na uwalakini ulianza kutawala kabisa akili ya mwanamama huyo ambaye anaishi maisha ya anasa mjini.Sasa akili yake ilianza kumuwaza Sophia tu.

    Yaani kumtegemea Sophia kwa kila kitu. Kumvisha Sophia gunia la majukumu pale nyumbani kwa maana ilikuwa haina jinsi wala namna kabisa ya kufanya.

    .Huku Sophia kule ofisini hali na uelewano ulikuwa ndivyo sivyo kabisa kwani baada ya mke wa bosi wake kuingia ofisini na kumwambia mmewe kuwa kaja kumuona mfanyakazi mpya alimbana sana Damiani na kumpa usumbufu uliogeuka kero na kumfanya Damiani aone aibu. Aliwaza kuwa iwapo mgeni yeyote akija pale ofisni na kukuta zogo kama hilo ndani ya ofisi yake itatia aibu, “unataka kumjua si ndiyo?” alimuuliza kwa upole mkewe ambaye naye alijibu kuwa ndiyo shida kubwa iliyompeleka pale ofisini.

    Kumbe huku nje Robert anasikia kila kitu jinsi bosi wake anavyozozana na mkewe. Robert anacheka sana kule nje kama chizi vile au mtu aliyepungukiwa na akili. Sophia anamkuta akicheka, kisha anamuuliza kwa kutabasamu. “mbona Robert unacheka mwenyewe, niambie basi na mimi nijuwe kama wewe” alisema binti Sophia.

    Wakati bado anahoji kinachomchekesha Robert, akafika mtu katumwa kumuita Sophia ili aende kutambulishwa kwa mke wa bosi.“Sophia unaitwa na bosi kule ndani.” Alisema secretary ambaye alikuwa ametumwa na bosi wao kuja kumuita Sophia. “Nakuja sawa” alisema Sophia huku akijaribu kumpeleleza kwa kina bwana Robert amwambie kilichomchekesha.





    Robert akamwambia aende kwanza kumsikiliza bosi akirudi atamwambia ni nini kilimchekesha namna ile.Kisha Sophia anaamua kwenda kumsikiliza bosi wake.Nasema lazima nimjue, unajifanya kunificha mimi”

    “Mke wangu mbona ustaarabu kwako haupo siku hizi?

    “Kama ungeniambia ungeniona hapa?

    “Mimi ningekwambia kwa nini nikufiche mke wangu”

    “Hapana ngoja aje nimuone” alisema mke wa Damiani kwa ukali mpaka bwana Damiani aliamuwa kutulia na kuwa mpole kabisa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Punde si punde Sophia akaingia ofisini kisha mke wa Damiani akaanza kushangaa na kumuuliza Damiani kwa umakini. “Ndiyo huyu mme wangu? Huku akimuangalia kwa usoni Sophia.

    Damiani akamwambia kuwa ndiye kisha akamuuliza kwani kuna nini? Roho ya bwana Damiani ikashtuka nakuanza kuzani kuwa labda mkewe atakuwa anamjua Sophia kiundani zaidi kuliko yeye anavyomjua. Na ukizingatia pia ana ujauzito wake.

    “kwani unamjua huyu?

    “hamna bosi

    Alisema Sophia akiwa ameanza kushituka kisha Damiani akamwambia yule ndiye Mkewe na wale ndiyo Watoto wake. Dah! Sophia akaishiwa nguvu kabisa kisha Damiani akamtambulisha Mkewe kwa Sophia. Mkewe akaonesha dhihaka na kusema kwamba Sophia ni Mtu mwenye dharau sana wala hafai.

    “Sophia umemfanya nini huyu? akajibu“nimetofautiana naye kauli hapo nje” Hebu muone, uwe unauliza kwanza” alisema Damiani kisha wote yeye na mkewe wakaanza kumtupia maneno machafu na kumuonyeshea kwamba hafai kufanya kazi pale. Sophia akatoka nje na machungu kibao huku machozi yakitiririka kama maji mapolomokoni. Robert akamfuata pole pole na kumuuliza kwa nini analia machozi namna ile. “Yaani Robert mambo naona hapa yamekuwa ni mengi kabisa” alisema kwa huzuni binti Sophia. “Kwa hiyo wewe una mpango gani labda kwa kauli yako uliyotumia?

    Aliuliza Robert kwa dharau akimwangalia Sophia. Sophia akamwambia kama hali ndiyo hiyo nitakuja kuacha kazi pale kwenye ofisi ya bwana Damiani. Robert akamwambia haina maana kwa mtu mwenye shida kama yeye kuacha kazi kwani ataambulia shida zaidi. Baada ya kusikia kauli ya bwana Robert Sophia akagundua kumbe pale ofisini hana thamani kabisa na wameshamdharau kabisa. Sophia akabakia akiwa ameshika shavu na raha ikiwa imetoweka kabisa ndani ya moyo wake na hata uso wake pia.

    Ni muda wa asubuhi, Edward ambaye ni mdogo wa Sophia aliona mabadiliko nyumbani alipokuwa analelewa, kulitokea kutofautiana kati yake yeye na mke wa Mfadhili wake, vitendo vya ajabu vilianza kuonyeshwa mbele yake, asubuhi hiyo Edward alikuwa anataka kwenda shuleni lakini mke wa yule bwana ambaye alikuwa akimfadhili alinyanyuka na kumwambia Edward kwa hasira unaenda shuleni leo? aliuliza huku akiwa ameshika kiuno, Ndiyo nataka kwenda shuleni, alisema Edward kisha akaendelea kujiandaa kwenda shuleni.

    Yule mwanamke akakata ule mshipa wa aibu kwa kijana huyu, alikuwa akihitaji awe anafanya kazi ndipo aende shuleni, “Hivi wewe Edward kila siku mimi ndiyo niwe nafanya kazi za hapa nyumbani wewe ukirudi unastarehe tu, sasa hiyo tabia naomba iishie leo, sijawa mkeo kabisa.’’ Alisema mke wa yule bwana.

    Edward alibisha akidai hawezi kufanya kazi kwanza ndipo aende shuleni. Edward alizidi kumwambia kuwa hata nyumbani kwao huwa hafanyi mambo kama hayo. Mke wa yule bwana akamwambia kuwa sasa ndiyo atafanya kwa sana tu kama hataki arudi nyumbani kwao. Kumbuka haikuwa bure yule mama alikuwa na kijimimba kama cha miezi miwili na nusu hivi ambacho kilijenga chuki kubwa kwa Edward ambaye alikuwa hajagundua kitu chochote kabisa kuhusu hilo jambo. Edward akaenda zake shuleni.Wakati akienda shule, mke wa yule bwana alimwangalia kwa jaziba kubwa sana kiasi kwamba Mungu angempa mamlaka katika dunia angelimpoteza kabisa.

    Mke wa Damiani alitoka ndani ya ofisi kisha akamkuta Sophia nje na kumwambia aondoke hapo,’’ wewe huendani kabisa na ofisi hii’’“Sawa’’ alisema. Kwa huruma binti Sophia ambaye alikuwa kama anang’ang’ania pale ofisini.Ingawa kipindi anaingia pale ofisini alionekana kama dhahabu kwa sasa ule udhahabu umepotea kabisa tangu apewe mimba na bwana Damiani.

    Mke wa Damiani alimsogelea Sophia ili kumpa vidonge zaidi, Sophia alihama na kwenda pengine mbali naye maana alikuwa amechoka kusikia maneno yao pale ofisini. Baada ya kumhama, mkewe Damiani alianza kumpa matusi makubwa ya nguoni. Sophia akabaki kumuangalia huku machozi yakitiririka.

    Mke wa Damiani hata huruma haikumuingia kabisa bado aliendelea kumporomoshea matusi makubwa makubwa. Damiani ikabidi atoke nje kuja kuona nini kilichokuwa kinatokea ,“Nakwambia wewe, hebu lione” alisema mke wa Damiani, haijulikani kwa nini mwanamke huyu hakumpenda Sophia sijui ni damu hazikupatana. Damiani baada ya kutoka nje alisimama kwanza kwenye ngazi kuangalia mpambano huku akimtupia jicho zaidi Sofia ambaye alianza kulia huku akimfuata Damiani pale ngazini.

    Damiani baada ya kuona akifuatwa na akijua kabisa mkewe ni mcharuko wa hali ya juu aliamua kumtusi na yeye ili mkewe asimuhisi vibaya wewe mpuuzi, pumbavu kisha akamuuliza anachomfuatia ni nini haswa!

    Baba nanii huyu ana matatizo haoni kama mkeo niko hapa anakufuata ili iweje”

    Sophia akaishiwa hoja na hamu kabisa ya kunena chochote akabakia kulia tu kama mtoto mdogo.

    Damiani kwanini usimkataze mkeo kunitukana, ‘’mke wangu ndiyo ulitaka awe nani” Damiani alijibu.Sophia akawa katika wakati mgumu sana ambapo alishindwa afanyeje na angali bado alikuwa mjamzito na maisha yalikuwa magumu mno pale nyumbani kwao.

    Damiani alishuka katika ngazi na kumwambia mkewe arudi nyumbani. Damiani alionesha hali ya kutomjali kabisa Sophia na kumuona kama mdoli au sanamu fulani iliyochoka na kuwekwa barabarani.

    Ilikuwa ni asubuhi sana yapata kama saa kumi na mbili Sophia akiwa kaamka na mawazo mapya. Alikuwa kapanga kwenda kumsabahi Viviane rafiki yake kipenzi sana na ndiye aliyemsaidia kupata kazi pale kwa bwana Damiani. Sophia alikuwa kapanga endapo atamkuta Viviane, basi atakuwa hana budi kabisa kumwambia vituko na changamoto ambazo zinamkabili yeye pale ofisini kwake. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya ijumaa.

    Sophia aliamua kuacha kwenda kazini, akaenda nyumbani kwao na Viviane kumwambia ukweli wa mambo kuhusu yeye na Damiani wanavyoishi wawapo ofisini kwao. Na mbali na hayo pia walikuwa Viviane na Sophia hawajaonana siku nyingi sana tangu kwenye kutafutiana kazi bado walikuwa hawajapata muda wa kutembeleana au kuonana kabisa.Hivyo Sophia akaona ule ndiyo muda mzuri haswa wa kuonana na rafiki yake huyo ambaye walisoma pamoja.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kule alikokuwa akiishi mdogo wake Sophia, matatizo yakawa yamepamba moto zaidi kwani Edward alianza kuzozana tena na yule mama ambaye alikuwa ni mke wa mfadhili wake. Fujo ilitokana na ule ugomvi wao wa kila mara wakutaka Edward awe anafanya kazi ndipo aende shuleni kwao kusoma.

    Asubuhi hii Edward alipigwa na yule mwanamke kwa kutumia vyombo vichafu kabisa, lakini bado Edward alibisha na kugoma kufanya kazi. “Pumbavu mkubwa wewe” alitukana yule mwanamke “Mpumbavu mwenyewe bwana” Edward alimjibu.

    Unaniambia nini? Aliuliza mwanamke huyo, huku akimbonda bonda Edward na sufuria kichwani. “sawa nipige bwana ninyanyase si uko kwako” alisema kwa huruma kijana Edward,“ ndiyo kwani hapa ni kwenu?

    ‘’Haya mamba sitaki kusikia, kelele Edward nenda shuleni” alisema yule mme wa mwanamke huyo.“Mke wangu wewe tatizo lako ni mvivu sana kazi si atafanya akirudi? ‘’Kumbe unamtetea eti sawa sasa utafanya mwenyewe” alisema kwa hasira. Ama kweli mimba si ugonjwa bali yaweza kuwa chanzo cha mifarakano ndani ya nyumba.

    Ilikuwa ni muda wa saa tatu asubuhi Sophia akawa tayari ameshawasili nyumbani kwao na Viviane ambapo siku hiyo alifanikiwa kumkuta Viviane mwenyewe nje akipika chai ili anywe ndipo aende kazini kwake.

    Mama Viviane hakuwepo pale nyumbani hivyo alikuwepo Viviane peke yake akiendelea na shughuli za pale nyumbani.Viviane baada ya kumuona Sophia alitupa majani na kwenda kumkumbatia rafiki yake kipenzi Sophia. “Waooo sophia” kisha waka angaliana na kuanza kuchekeana kwa roho kunjufu kabisa, Baadae wakaingia ndani.Viviane alikuwa akimwangalia Sophia kwa makini. Aligundua kuwa Sophia ni mjamzito waliendelea kuongea habari nyingine kabisa ambazo ni za kawaida.

    Viviane alianza kumuuliza maswali ya kusanifu kuhakiki kama kweli ana mimba. “Mwenzangu sijui nani kakupa huo mzigo! Kisha akatulia na kumsikiliza Sophia atasema nini. Baada ya kusema hayo tu Sophia alianza kudondosha machozi kwani Viviane alimkumbusha uchungu ulioko ndani ya moyo wake. Baada ya kuona hivyo aliamua kumuuliza nini kilimsibu mpaka akaamua kulia vile.

    Sophia alianza kumpa hali halisi ya mimba yake na mpaka aliyempa kisha akamueleza jinsi anavyofanyiwa na Damiani. Roho ilimuuma sana Viviane.’’Yaani kweli ninavyomwamini Damiani anathubutu kufanya hivyo.” Alisema Viviane kwa uchungu kabisa huku akianza kumchukia kabisa Damiani ambaye waliheshimiana sana.

    Baada ya hayo Sophia alimwambia Viviane hajui atakacho mfanyia Damiani. Viviane anaamua kumpa njia ambayo ni nzuri na salama ya kumbana bwana Damiani ili amuhudumie mpaka atakapojifungua.

    Njia yenyewe ni kwenda kivulini shirika ambalo hutetea akina mama pamoja na watoto. Sophia alikuwa halijui shirika hilo hivyo akawa katolewa usingizini. Liko wapi? hapa hapa Mwanza? Aliuliza Sophia Viviane akamwambia liko hapa hapa mwanza, Dah! Ikawa furaha kubwa kwa Sophia. Viviane akamuhaidi kumpeleka siku ya Jumatatu, ‘’usiende kazini huyo Damian akuhudumie wala usipate hofu sana” alisema kwa kumpoza.

    Kisha Viviane alitoka nje kwenda kuangalia chai. Wakati akitoka tu mara Damiani akampigia simu Sophia. ‘’Viviane, Damiani anapiga” alisema Sophia kwa uwoga, ‘’ebu pokea usikie ana nini” Viviane alisema huku akiendelea na uandaaji wa chai kule nje.





    B

    aada ya mwezi kupita Edo mdogo wake Sophia alikuwa kazua mgogoro mkubwa sana na yule mama mke wa mfadhiri wake. Edo akawa anaishi bila amani. Mda huo Edo alikuwa shuleni, yule mke wa mfadhiri wake sasa alikuwa kabakia ndani mwenyewe. Ukiwa ukawa umemzidia kabisa ndani ya nyumba kisha anaamuwa kwenda kwa majirani zake ambao wanaishi nae karibu pale dah! Na ujauzito aliokuwa nao alikuwa anajikongoja pole pole kwenda kwa jirani yake nyumba ya pili. Jirani yake alikuwa mmbea sana katika waongo ni mbari moja. Na angeliweza kupata tuzo ya uongo bora na unafiki, pamoja na masengenyo juu ya maisha ya watu. “karibu jirani mwema” alisema mbali kabisa ki umbile la nje ungeweza kusema ni mtu ambae ana tabia nzuri labda na mpenda watu, mwenye hekima kubwa sana. Asante jirani yangu, kijacho ananisumbua tumbon jirani. Alisema yule mama mke wa mfandhiri wa bwana Edo ambaye maisha yake kama utakumbuka ni shida sana. Hakuna mfano, mama omba omba, lakini walau dada yake anajituma ila maisha yanampa changamoto kubwa sana kiasi kwamba mpaka anajuta kwanini alizaliwa duniani hapa. (dunia ya ngurue). Basi baada ya kuingia pale nyumbani kwa jirani yake walianza kuongea maongezi yao ya kawaida. Baadae yule mama ambae alikuwa muongo sana alianza kuongea maneno ambayo dhahiri yalikuwa ni yakumtega yule mke wa yule mfadhiri wake na Edo ili kujua ndani wanaishije kwa kuwa nae hakuwa na akili ambayo inazunguka sawasawa. Na ajue kutegua mambo lipi zuri na lipi ni baya/linamukhutaza gani. Alianza kumwambia mambo yote ya ndani kisha akaingia upande ambao ndio gumzo pale nyumbani kwake kati yake na bwana Edward ambae silipendi” alisema yule mwanamke bila kuwa na haya kabisa. “Kwanini humpendi jirani ana tabia mbaya sana ama ni mshari sana ila binadamu jamani! Alisema huku akikaa vizuri kusikia atakavyoanza kuambiwa na yule mwanamke mwenzie asiejuwa kutunza ya ndani mwake kabisa “Yaani ndie anaturudisha nyuma kimaendeleo kabisa toto lina kula mithili ya mchwa. Alisema yule mama mke wa mfadhiri wake Edo. Kisha anaanza kumwambia mpaka kwao Edo kuwa wanashida sana. Mpaka Edo huwa anachota unga na mchele anawapelekea nyumbani kwao wapate kula. Yule mama muongo nae alikuwa makini kuyanukuu yale maneno ambayo alio kuwa akiambiwa pale. Dah! Kumbe mimi nilidhania kwamba ni ndugu yenu kumbe? Alisema kwa upole mwana mama yule ambae ni muongo kupindukia kabisa. “Ndugu wapi, acha nilipendezeshe, dada yake ndio kidato cha nne wale waliofeli. Mtoto alikuja anamachacha na hata sanduku la nguo alikuwa hana kabisa” alisema huku mpaka mdomo ukimtetemeka. Waliongea mengi sana kuhusu Edo na kumpa kashifa mbaya kabisa kijana Edo ambae alikuwa hana ubaya kabisa ili yule mwanamke wa mfazili wake na Edo ndie alikuwa na mambo ambayo hayafai hata kidogo kabisa kwani kutoa siri ya ndani ni jambo ambalo halifai kikawaida labda mtu wa namna hii atakuwa ana kasoro kichwani mwake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huko kazini kwa yule bwana anae mfazili Edonae akiwa ofisini nae pia anadiriki kumuongea vibaya Edo ambae alitowa pesa zake kumsomesha kumbe hata hakutowa kwa roho moja kabisa bali zilikuwa ni roho mbili, roho ya kwanza ilikuwa ni watu wajue na kumtambua kuwa ana roho nzuri, pili ilikuwa ni ya kumfanya ajulikane kwa watu kuwa ana pesa nyingi sana mpaka anaamua kumsaidia Edo. Muda huo bwana huyu anakuwa na wafanyakazi wake wakiwa wamepumzika. Yaani ndugu zanguni nyumbani sasa hivi hapakaliki kabisa, alisema bwana huyu. “Kwa nini bosi kwako alafu tena pasiwe na amani?” aliuliza moja kati ya wafanyakazi wake ambae yuko karibu nae kabisa. Kuna mtoto natoa msaada wa kumsomesha ili aisaidie famila yake maana hawana uwezo kabisa na yule mtoto ana akili sana darasani” wote wakabakia kumuangalia kisha yule mfanyakazi ambae yuko karibu sana na bosi wake akamwambia kuwa amtowe pale nyumbani amsomeshe akiwa nyumbani kwao. Wote wakaunga mkono kauli /jambo la yule bwana. Lakini mmoja kati yao ambae alikuwa (stookeeper) katika kampuni ya huyo bwana yeye alikuwa ana wazo ambalo ni tofauti kidogo kisha anamwambia, “Sikia bosi najuwa umetuomba kama ushauri si ndio, bosi akatikisa kichwa kusikia mawazo ya yuyle bwana. “Kwanin usimuondoe tu nyumbani kwako atakusababishia hata mke akukimbie” bwana huyo alipokuwa akipumzika mida ya mchana hata jioni alipenda kukaa pamoja na wafanyakazi wake bila ubaguzi kabisa na waliongea na kama mtu wa kawaida kabisa, nayeye alipokuwa na jambo gumu ambalo limemuelemea haliwezi alijaribu kuwaambia ili waweze kusaidiana kutatua jambo hilo.

    Alikuwa ni bosi ambae yuko tofauti kidogo si kama wengine ambao wakiwa mabosi basi muda wote ndio wako na mambo yao. Mfanyakazi muda mwingine ndio kwanza unakuta hata hathaminiki. Walimshauri mambo mbalimbali kutokana na jinsi ambavyo mtu alikuwa na uelewa wake tofauti tofauti kabisa. Baada ya pale walitawanyika kwenda zao kazini ikabakia kwake achukue lipi aache jambo lipi kati ya ushauri alioupata kutoka kwa wafanyakazi wake. Maana unapoomba ushauri kwa watu ambao ni tofauti jua pia kuna mkusanyiko wa mawazo mengi pia. Jambo lililopo huwa ni kuchagua wazo moja tu iwe kusuka ama kunyoa, au vyote kwa pamoja. Hapo ndipo tunaingia katika kitu ambacho kinaitwa maamuzi ambayo ni sahihi zaidi kwa mtu ingawa hapa huwa na uwalakini. Kuna kuamua uamuzi ambao si mzuri ambao hauna manufaa mazuri baada ya kutawanyika wote kwa ujumla yule bwana yeye akarudi ofisini kwake. Muda huo kumbe ndio ulikuwa muda wa kutoka wanafunzi kurudi nyumbani. Edo akiwa njiani akitembea huku akicheza mpira na kuimba za makombe ya dunia, ghafla anashangaa na kushtuka kugeuka anamkuta ni rafiki kipenzi wa dada yake yaani Viviane. “Waoooh dada Viviane za siku nyingi dadaangu? Aliuliza Edo akiwa kabeba mgongoni begi ambalo lilikuwa na madaftari ambayo alikuwa anavipindi navyo siku hiyo. “Nzuri mdogo wangu, kila nikija nyumbani kwenu kumsabahi Sophia huwa sikukuti mdogo wangu au masomo yamekubana? Alisema Viviane akiwa na mkoba wake ambao ulikuwa umesheheni vitu mbalimbali kama vipodozi pamoja na simu ya mkononi. Dah! Kwa kweli ilikuwa furaha sana kwa Edo kumuona Viviane na ilikuwa pia furaha kwa Viviane kumwona Edo maana walikuwa na muda kitambo sana hawajapata kuonana. Edo akasogea pembeni kando na barabara ambayo walikokuwa wamesimama. Waliongea sana Edo kwa kuwa alimuona Viviane kama dada yake Sophia. Aliamua kumwambia adha ambazo alikuwa akipambana nazo kule anakoishi kwa mfadhiri wake. Viviane alipata uchungu sana kisha anamuuliza kwa nini huyo mwanamke amsumbue. Edo baada yakuonge mno akaanza kumwambia/kumuulizia dadake Sophia. Viviane alimwambia ukweli kabisa Edo wala hakupindisha jambo kuwa kwa sasa Sophia anamimba tena kubwa sana. Edo akashangaa sana, hata hakuamini kabisa usemi ambao Viviane alimwambia. “Dada sophia anamimba toka lini dada Viviane? Aliuliza kwa umakini Edo na kwa mshangao mkubwa sana. Akiwa haamini kabisa kama Sophia anamimba tena ya Damiani ambaye ni bosi wake, ndie aliyemdanganya na kumpa ujauzito ili apate cheo ambacho ni cha hali ya juu, na urahis wa kupata kazi na alosababisha bwana Damiani kumfanyia Sophia.hivyo tunaweza kusema umaskini ndo chanzo cha Sophia kupata ujauzito huo ambao alikua nao. Damiani ndo kwanza kabisa alikua anamdharau binti Sophia alikua anamuona kama mwanamke ambae asiefaa kabisa hapa duniani. Basi baada ya Edward kujua jambo hilo aliondoka na kuachana na viviani akiwa na wingi wa mawazo mno. Njiani alikua kama mtu asiejitambua maana aalikua anatembea apo alikoswa koswa na magari kumgonga baskeli nazo pia zilikua zikimkosa kosa kabisa kumgomnga maana akili na upeo vilihama kabisa na kuanza kumuwazia dada yake Sophia “hivi dada Sophia anampango gani na uyo mtoto ambae atamzaa na maisha ya nyumbani ndo karaha”aliwaza mwenyewe akiwa anatembea barabarani,mfoko wa madaftali nao ukikua umemzidia uzito maana ulikua na madaftari karibu kumi na kidogo pamoja na ya marafiki zake ambao walikua hawajahudhuria kwa sababu zao ambazo ziliweza kua za msingi zaidi au hata bila msingi wa aina yoyote ile. Bega la Edo la mkono wa kushoto lilikua kama linataka kuchomoka maana alikua kachoka sana,hata tembea yake ilikua ni ya kichovu sana nyuma yake kulikua na binti ambae walikua wanasoma nae yeye alipokua nyuma aligundua Edo alikua kachoka sana maana tembea yake ilikua ni ya tofauti na alivyo mzoea kabisa wawapo darasani “Edo leta nikusaidie mzigo rafiki yangu” alisema yule msichana huku akiwa anatembea kwasababu Edo alikua mbali sana.alimsubilia kwanza msichana yule kisha akalishusha lile begi chini, “wahi basi Mariamu nimechoka kweli nataka kuwahi nyumbani” aliongea kwa uchovu kabisa. Kuna mtu kuchoka mpaka anahisi kwamba kuongea ni shida kabisa. Pengine wengine huona mdomo kuwa mzito kabisa. Anaamua kukaa kimya kabisa. Hali hii huwa ipo sana kwa watu ambao ni wavivu sana ndio hali kama hiyo huwatokea. Na Edo pia ni miongoni mwa watu hao ambao wana asili ya uvivu sana maana kama angelikuwa si mvivu wa kutupwa basi angekuwa hana mzozo na yule mke wa mfazili wake. Ingawa bado yule mwanamke alikuwa ni mjamzito katokea tu kumchukia Edo lakini angepunguza kiasi flani chuki na yule mwanamke, basi baada ya yule msichana kumsaidia Edo mzigo ambao ulikuwa umempa uchovu, walienda mwendo wa taratibu mpaka mwishoe wakafika njia panda moja hivi ambayo ilikuwa ni ya barabara za lami, wakaachana mmoja kulia mwingine kushoto kwenda nyumbani kwao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    ***.





    ITAENDELEA  

0 comments:

Post a Comment

Blog