Search This Blog

Friday, October 28, 2022

MSHUMAA - 1

 

     





    IMEANDIKWA NA : RAMADHANI K HUSSEIN



    *********************************************************************************



    Simulizi : Mshumaa

    Sehemu Ya Kwanza (1)







    YAPATA Majira ya saa tatu usiku. Giza halikuwa kubwa sana kutokana na mwangaza wa mbalamwezi uliokuwa ukiangaza katika jiji hilo la Tanga. Pamoja na kuangaza kwa mwezi. Pia taa zilizofungwa kwenye majumba ya mtaa huo wa Magaoni zilisaidiana kuliondosha giza hilo.



    Katika nyumba moja iliyopo kwenye mtaa huo wa Magaoni palisikika kelele. Hapana sio kelele tu. Ni kelele za vilio. Bilashaka kulikuwa na jambo kubwa lililotukia kwenye nyumba hiyo. Maana sio rahisi mtu apige kelele za kilio halafu pasiwe na jambo la kuhuzunisha au kuumiza moyo. Ndio lazima iwe hivyo na si vinginevyo.



    Majirani waliokuwa karibu na nyumba hiyo walijongea kuifuata nyumba hiyo kwa hatua za haraka haraka huku mioyoni mwao wakiwa na shauku kubwa iliyochagizwa na wahka tele wakitaka kujua nini kimetukia huko. Msiba!. Hapana maana nyumba hii hakukuwa na mgonjwa. Nini sasa kama sio?. Wakabaki na maswali yao huku wakiendelea kupiga hatua kuifuata nyumba hiyo.



    Vilio ndio vilizidi kupita maelezo utafikiri kulikuwa na mashindano ya kulia yaliokuwa yakifanyika ndani ya nyumba hiyo.



    “Kuna nini?” Mama mmoja mnene alimuuliza kijana mmoja mwenye mwili mwembamba. Kwa kumuangalia tu utamdhania ya kuwa mlo kwake huenda ukawa ni wa kutafuta kwa manati. Kijana huyo alimuangalia mama yule mnene pasi na kumjibu chochote. Amjibu nini wakati wote walikuwa wakienda kwenye nyumba hiyo kujua kuna nini? Alihamisha macho yake kutoka kwenye uso wa mama mnene na kuachia sonyo fupi huku akiendelea kupiga hatua kuufuata mlango wa nyumba hiyo. Hawakuwa pekeao. Walikuwa wameongozana na kundi kubwa la watu wengine.



    Waliufikia mlango na kuusukuma. Wakajikuta wakiwa ndani ya nyumba hiyo. Walipokelewa na sebule pana yenye thamani nyingi za samani zilizopangwa kwa ustadi mzuri kwenye sebule hiyo. Vyote hivyo hawakuwa na shuhuli navyo. Macho yao yalikuwa kwenye miili ya watu wanne. Wawili wakiwa wamelala chini huku wawili wakiisukuma kama sio kuitingisha miili ile iliyolala chini.



    “........Mamaaaa......Babaaaaaa. Nini kimewakuta wazazi wangu tenaaaa. Am...keenii baa..siii hii hii hii” Msichana mmoja kati ya wale wawili waliokuwa wakiitingisha miili ile aliyanena hayo huku machozi yakimtiririka machoni mwake. Na yule mwengine alikuwa akilia huku akiyanena maneno yasiyoeleweka. Pengine labda alinena kilugha!.



    Wazee wawili walienda hadi pale ilipo ile miili huku wanawake wengine wawili majirani wa nyumba hiyo wakienda kuwatoa wasichana wale waliokuwa wakilia karibu na miili ile. Wakawasogeza pembeni huku bado wasichana wale wakiendelea kulia. Wazee wale waliokuwa karibu na miili ile. Wakajaribu kuangalia mapigo ya moyo kwenye miili ile miwili iliyokuwa imelala chini mapovu yakichuruzika kutoka kwenye midomo yao ikianguka chini sakafuni.

    Kimya!.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Mmmh!” wakaguna wote kwa pamoja.



    Wakasogeza masikio yao karibu na pua miili ile na kusikilizia kwa sekunde kadhaa. Kisha wakainuka na kuangaliana machoni. Miguno ikawatoka utafikiri walipanga kufanya hivyo kwa pamoja. Wakautazama umati wa watu uliokuwa unawaangalia wao. Kisha macho yao yakaenda kwa wale wasichana wawili waliokuwa wakilia muda mfupi uliopita. Ila hivi sasa walikuwa kimya utafikiri sio wao waliokuwa wakilia mwanzo. Pengine labda hawakuwa na uhakika na kile walichokuwa wakidhania mwanzo na hivi walikuwa tayari kupokea taarifa ya uhakika kutoka kwa wazee wale. Macho ya wasicahana wale yalikuwa yamewakazia wazee wale waliokuwa wamepiga magoti kwenye miili miwili iliyolala chini.



    Wazee wale bila kusema kitu waliyafumba macho ya miili ile iliyokuwa imekodoa macho utadhani inaangalia kitu cha kuogofya sana.

    “Innalilah wainnailaih rajjiun” wazee wale walisikika wakitamka maneno hayo kwa sauti ndogo lakini iliyosikiwa na wote waliokuwa ndani ya nyumba hiyo.



    Ebwana eee!. Yowe kubwa lilisikika lililochagizwa na kilio kikuu. Yowe hilo na kilio hicho kilitoka kwa yule binti mmoja kati ya wale wawili waliokutwa wakilia karibu na miili ile ambayo sasa wazee wale wamethibitisha kwamba ilikuwa ni wafu tayari.



    Mmoja wa mabinti wale alikuwa akilia kwa sauti kuu huku akijaribu kujinasua kwenye mikono ya mwanamke mtu mzima aliekuwa amemshikilia. Mara nyingi alisikika akitaja majina mawili. Mama, Baba. Alionekana kuwa na uchungu mwingi zaidi ya yule binti mwengine.



    Wazee wale na baadhi ya majirani wengine wakashauriana na kupitisha wazo la kuzipeleka maiti zile hospitali maana hazikufaa kuwa ndani ya nyumba hiyo tena. Hata hivyo haikujulikana chanzo cha vifo hivyo ni nini. Kwahiyo pia wakizipeleka hospitali maiti zile huenda wakajua chanzo kilichopelekea vifo vile. Kabla ya kuziinua maiti zile. Kwanza wakamuuliza yule binti ambae alikuwa akilia sana kuliko hata yule mwenzie nini kimetokea hadi kuwa hivyo.



    “Wa...kati tumekaa me..zani tuna...tuna kula. Tulisha....ngaaa ghafla Ba..ba ameangu..uka chi..ni mapovu yaki..mtoka mdo..moni. Kabla hatujajua ni..ni ta..ti...zoo. Mama nae akaanguka na kuwa ka...ma Babaaa haa haa haa!” Binti yule akashindwa kuendelea kuelezea na kujikuta akipiga kelele za vilio. Alikuwa na uchungu baada ya kuondokewa na wazazi wake wote wawili tena kwa wakati mmoja akiwa anashuhudia kwa macho yake. Ilimuuma sana. Ilimuumiza sana wazazi wake kufa kwa pamoja. Tena kifo asichokijua chanzo chake.



    Wanawake wale watu wazima walimuacha yule binti mwengine na kumbembeleza yule ambae ni mtoto wa wafu wale waliokufa muda mfupi uliopita. Yule mwengine alikuwa ni mfanyakazi tu.



    Zile maiti zikabebwa baada ya kupatikana dereva atakae endesha gari kwaajili ya kuzipeleka hospitali ya Bombo. Mtoto wa marehemu wale anaejulikana kwa jina la Shery alitaka kuchomoka kwenye mikomo ya watu wale waliokuwa wakijitahidi kumtuliza ama kumbembeleza baada ya kuona wazazi wake wakiinuliwa wakitolewa nje kwajili ya kupelekwa hospitali. Walimzuia huku wakiendelea kumbembeleza.



    Maiti zilipelekwa hospitali huku nyuma wakiwaacha majirani wakipungua mmoja mmoja kuondoka hapo huku nyuso zao zikisawajika na huzuni ya dhahiri. Majira hayo wakabakiwa wale wamama wawili wakiendelea kupoza mabinti wale kwa kuwapa maneno ya faraja hadi pale walipotulia. Ila uchungu haukuondoka hata punje kwenye mioyo yao. Na hiyo ilidhihirishwa na kilio cha chini chini walichokuwa wakikitoa huku machozi kwenye macho na kamasi kwenye pua zikiwatoka na wala pasiwe na jitihada zozote za kuziondosha.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Wamama wale walijaribu kuwauliza kwa uzuri ni kipi kimetukia hadi ikawa hivyo? Walichojibu ni kwamba hata wao hawajui na walishangaa tu watu wale wakianguka kila mmoja kwa wakati wake lakini hawakupishana sana dakika. Ni kama walipishana dakika moja tu tena hiyo ni baada ya kuanguka Baba na Mama alipoona hivyo ikabidi aache kula na kumuendea mume wake pale chini ajue ni kipi kilichomkuta. Hata hakuzungumza kitu na yeye akaangukia upande wake akafanana na mumewe.

    Wote wakatokwa na mapovu midomoni!.



    Sumu kwenye chakula!. Ama ni nini? Maswali hayo yakazunguka kwenye vichwa vya wamama wale. Lakini kama ni sumu mbona hawawengine hawakudhurika? Na kwa maelezo ilivyosemekana walikuwa wakila wote japokuwa kila mmoja na sahani yake. Au waliekewa sumu kwenye chakula chao? Lakini hiyo haiwezekani kwasababu chakula chote kilikuwa kwenye ‘Hot Pot’ na kila mmoja alikuwa anapakuwa kiasi chake. Sasa ni vipi wafe wawili tu na sio wote wanne?.



    Baada ya kutulia, ikachukuliwa simu ili kuwajulisha ndugu wa wazee wale vifo vyao. Zoezi hilo alilifanya Shery japokuwa ilimpa shida sana kutamka kuwa wazazi wake wamekufa. Hakutaka kuamini hata kidogo wazazi wake waliokuwa wakila wote muda mfupi eti wamekufa. Watakufaje sasa ilhali walikuwa wote? Kwahakika ili muuma sana. Zoezi likakamilika na baada ya nusu saa pakaanza kuingia watu ndani humo huku vilio vikiwa nao pamoja. Kitendo hicho kilimfanya Shery na yeye aanze kulia upya huku akiwataja wazazi wake.







    Nikama vile ndio kilifunguliwa kilio ndani ya nyumba hiyo. Ikawa ni kelele mtindo mmoja za vilio. Na viliongezeka kila baada ya watu au ndugu kuingia ndani ya nyumba hiyo. Kwa hakika usiombe ukakutwa na majanga kama yaliyoikuta familia hii. Hasa hasa kwa Shery ambae alikuwa ni mtoto wa wazee wale. Alilia kiasi kwamba aliwachosha wale wabembelezaji waliokuwa wakimbembeleza yeye. Ilifikia kipindi wakamuacha alie tu pekeake maana hakukuwa tena na namna nyengine sasa ya kumfariji.



    Walishamfariji sanaa. Walishamnyamazisha sana. Ilifikia muda wakamtolea hadi mifano ya watoto wadogo waliofiwa na wazazi wao na hata bado wanaishi bila wasiwasi wowote. Sembuse yeye mtu mzima mwenye kujua baya au zuri. Mwenye uwezo wa kujihudimia mwenyewe. Tena mwenye uwezo wa kuziendesha mali zilizoachwa na wazazi wake. Sasa ni vipi awe na majonzi mengi kiasi hicho?

    Uchungu wa mwana aujue ni mzazi.

    Na uchungu wa mzazi aujue mwana.



    Hawakujua. Hawakujua ni kiasi gani binti huyo anauchungu mtimani mwake. Hawakujua uchungu alionao binti huyo. Kuondokea na wazazi wote wawili kwa wakati mmoja tena ikiwa hakuna ugonjwa wowote waliokuwa wakiugua. Hicho ndicho kilichomfanya binti huyo kuwa na uchungu mwingi. Pengine labda ingejulikana kwamba wazazi hao walikuwa kitandani kwa miezi mingi wakiwa wanaugua ugonjwa fulani. Bilashaka uchungu usingekuwa mkubwa sana kiasi hicho.

    Lakini kifo cha ghafla! Mbele ya macho yake akishuhudia wazazi wake wanakata roho.

    Tusiombe yatukute ndugu msomaji.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Matanga yakafungwa siku hiyo huku wakisubiria ndugu wengine waje kwenye msiba huo. Majira haya Shery alikuwa chumbani kwake akiwa na yule dada wa kazi. Jukumu lile lililoshindikana na wale waliokuwa wakimbembeleza, sasa lilibebwa na yule dada wa kazi aliejulikana kwa jina la Mkasi. Alikuwa akimbembeleza kimya kimya huku kilio cha kwikwi kutoka kwa Shery bado kikiwapo. Kichwa cha Shery alikuwa amekilaza juu ya mapaja ya Mkasi huku akiendelea kutiririsha machozi. Mara chache Mkasi aliwahi kuyafuta machozi yake ili yasimdondokee Shery maana alidhani kama Shery akiona kuwa na yeye alikuwa akilia basi anaweza akaamsha kilio tena ilhali muda huo ameanza kutulia japo si sana.



    Siku hiyo ikapita japokuwa ilibeba machungu mengi sana kwenye mioyo ya wafiwa wale. Na hii ni siku mpya ambayo ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo waliongezeka zaidi. Ikawa ni vilio tu kila baada ya ndugu wengine kuwasili hapo. Shery alilia sana kiasi kwamba hadi sauti ikamkauka. Macho yakamvimba huku sura ikiwa haitamaniki kwa huzuni. Ikashauriwa kwamba binti huyo aondolewe nyumbani hapo apelekwe mbali na nyumba hiyo akatulie maana kwa kulia kwake inaweza msababishia matatizo maana kila mgeni anaeingia hapo basi nilazima ataangua kilio tu. Hilo likaonekana ni tatizo.



    Alipoletewa shauri hilo. Akalipinga kwa nguvu zote huku akiahidi kuwa endapo watalazimisha kumtoa hapo na kumpeleka huko wanapotaka wao. Basi hatoshindwa kujidhuru mwenyewe. Hawakuwa na budi wakamuacha hapo akiendelea kulia kimya kimya. Pengine labda alikuwa akisubiria mgeni mwengine aje ili wasaidizane kulia.



    Nusu saa mbele waliingia watu wawili. Wote wakiwa na umri wa makamo. Bibi na Bwana. Shery alipowaona watu wale wakiingia kwenye nyumba hiyo. Akajikuta akitoka mbio huku akipiga kelele za kilio zilizo washtua watu waliokuwa wamekaa hapo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Bamdogooo Baba yangu hayupoo Mama yangu mimiiii. Bamdogo kaka yako amekufaa hayupo tenaaaa dunianiiiii” Shery alikuwa akilia hivyo na kwenda kumkumbatia yule mwanaume aliekuwa akiingia na yule mwanamke pale ndani. Ilihuzunisha sana kuangalia. Watu waliokua hapo walisikitika na wengine kuthubutu kulia kabisa. Mwanaume yule wa makamo alimpokea Shery aliekuwa akilia na kumkumbatia. Mwanaume yule alidondosha chozi la huzuni huku akimfariji binti huyo ambae ni mtoto wa kaka yake.



    * *



    Mazishi yalifanyika siku mbili mbele baada ya ndugu waliokuwa mbali na mji huo kuhudhuria. Miili ile miwili ilihifadhiwa katika makaburi ya Kichangani. Watu walirudi kuendeleza matanga. Na mwisho matanga yalivyokwisha. Ndugu wengi wakaondoka na wakabaki wale ambao wapo karibu zaidi na familia hiyo ili kuweka kikao wajue nini wanafanya baada ya kumaliza msiba huo.



    Siku ya kikao ikafika na ndugu hao wakakutana kwenye nyumba ya marehemu Fransisi ambae ni baba wa Shery. Pakajadiliwa mambo mengi ikiwemo la kusimamia mali za mzee huyo kwa wakati wote ambao Shery akisubiria amalizie elimu yake ya chuo ndipo akabidhiwe mali zake. Wakatafuta msimamizi na kupatikana kuwa ambae atakae simamia mali hizo ni mdogo wa marehemu ambae ni yule siku ya msiba Shery alienda kumkumbatia baada ya kumuona akiingia hapo.



    “Frank kikao kimekuona wewe. Kwahiyo tunataka kujua upo tayari kuzisimamia mali hizo?” Aliuliza mzee mmoja baada ya kupita shauri hilo. Baba mdogo wa Shery akanyamaza kimya kwa dakika kadhaa. Kisha akaja na jibu kuwa yupo tayari kusimamia mali hizo.



    Jambo hilo likapita baada ya kuwa limeshaafikiwa hapo. Likafuatia jambo jengine ambalo hilo lilitakiwa kwanza litolewe maamuzi na Shery kabla ya kukabidhiwa kwa wazee hao. Na jambo hilo ni kuwa. Je atakuwa tayari kuishi mwenyewe kwenye nyumba hiyo au patafutwe mtu yoyote ambae atakuja kuishi nae hapo au Shery ahame hapo aende akaishi na yoyote kati ya watu hao waliokuwepo hapo.



    Akatulia kimya. Akainamisha shingo yake chini akiwa bado anatafakari jambo hilo. Na wazee wale hawakutaka kumsumbua kwa lolote. Walitaka atoe maamuzi mwenyewe ndipo yaafikiwe hapo. Alikuwa akiwaza sana. Iweje niondoke hapa nikaishi kwengine ilhali hapa ndipo nilipo pazoea? Ama itakuaje nikiishi pekeangu katika hali ya upweke? Akainua kichwa na kuwa tayari kulitolea maamuzi swala hilo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naombeni mnipe muda nifikirie kwanza na nikipata majibu sahihi nitawajulisha. Kama nitaamua kuhama hapa kwenda kwa mtu yoyote kati yenu, basi nitawajulisha au kama nitaamua niishi hapa hapa pia nitawaambia. Ila kwa sasa acheni kwanza nifikirie” alitoa jibu hilo na watu wote humo wakaliafiki. Wazee wale wakaondoka wakimuacha Shery na Mkasi wakishi wenyewe.



    Frank baada ya kutoka kwenye kikao. Safari yake iliishia moja kwa moja nyumbani kwake. Huko alipokelewa na mke wake ambae ni yule alienda nae msibani siku ile . Wakachukuana mpaka mezani. Mke akafanya majukumu yake kama mama wa familia. Akaanda chakula mezani na baada ya dakika saba kila kitu kikawa tayari. Wakati wakiwa wanaendelea kula. Mke wa Frank alionekana kama kuna jambo anataka kulizungumza. Akavunja ukimya na kuamua kuongea.



    “Mume wangu, nini kimeendelea huko kikaoni?” aliuliza akiwa anamuangalia Frank usoni.



    “Tulikuwa tunajadili mambo ya kifamilia tu” Akajibu Frank kirahisirahisi. Jibu ambalo Mke wake hakulifurahia hata kidogo. Akaleta mapozi yake ya kike akijifanya amenuna.

    Ilishangaza!.

    Inakuaje anune wakati yale ni mambo ya familia yangu? Akajiuliza Frank.



    “Mbona umenuna ghafla? Au ulitaka kujua yaliyotukia huko?” akauliza Frank huku tabasamu likiwa usoni mwake akiuondoa ule mshangao. Alijua ni hila tu za mke wake.



    “Kwani kama nikijua kuna nini? Kwani mimi pia si nimeshaingia kwenye familia yenu?” Mwanamke huyo aliuliza kwa kudeka.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Basi mke wangu” Frank alimtuliza. Akaweka kijiko chini na kumuambia. “Maamuzi yaliyotolewa ni kwamba. Mimi ndio nitakuwa msimamizi wa zile mali za marehemu hadi pale Shery atakapo maliza elimu yake. Na amuzi jengine lililopangwa kuwa Shery apewe muda wa kufikiria kwamba atahitaji aiishi pale pale mwenyewe au atafutwe mtu aishi nae. Ni hivyo tu” Frank alimaliza kutoa maelezo. Tabasamu kwenye uso wa mke wake lilionekana. Frank akashangaa.

    Amaa!

    Inakuaje mwanamke huyu anafurahia maamuzi hayo? Mwanamke yule alipoona akishangaliwa na mume wake. Akaondoa lile tabasamu haraka na kumuuliza swali.











    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog