Search This Blog

Friday, October 28, 2022

WABEBA NDOTO (THE DREAM HOLDERS) - 4

 









    Simulizi : Wabeba Ndoto (Dream Holders)

    Sehemu Ya Nne (4)





    "Kwa nini uliruhusu Kylie aondoke na huyo jamaa!" aliongea Paul kwa hasira huku akishushia kwa glass ya pombe kali "walikubaliana wenyewe kama nilivyokwambia walionekana kufahamiana ilikuwa vigumu kuwakataza "ungenipigia hata simu" "simu! nilifikiri unaumwa na hata Kylie aliniambia hivyo.Unajua nini Paul relax! Kylie she'll be just fine usiwaze sana" aliongea Gerald lakini Paul kwa hasira alirusha kopo la pombe juu ya picha kubwa na kuipasua jambo lililomshitua Gerald.Paul aliondoka kwa hasira huku Gerald akimshangaa.Aliisogelea picha ambayo Paul aliipasua na kuitazama ilivyoharibika aliinama na kuokota kopo ambalo Paul alirusha,alishitushwa baada ya kuona alama nyeusi ya vidole juu ya kopo lile kana kwamba vidole vya Paul vilikuwa na masizi.

    Gari ya Rondo ndiyo ilikuwa ya kwanza kurejea kwenye umati wa watu na kumfanya kumshinda Harrison kwa mita chache sana.Harrison alikasirika sana na kushuka ndani ya gari yake pamoja na Kylie "Harrison nafikiri sasa umeamini kwamba huwezi kunipita hata siku moja " aliongea Rondo kwa majivuno huku akimsogelea Harrison "najua unajua kwamba umebahatisha tu" alijibu Harrison na kumfanya Rondo acheke kwa dharau "nini! nimebahatisha! unanichekesha sana Harrison ujue nini wewe nipe tu gari yangu" aliongea Rondo.Harrison alitoa funguo za gari na kumkabidhi Rondo ambaye alizipokea kwa haraka.Rondo alimsogelea Kylie aliyekuwa pembeni mwa Harrison na kuushika uso wake "au nipe na huyu mwanamke Harrison nakuachia gari lako" "no Rondo ushapata gari yako just leave man.Huyu ni mwanamke wa heshima siwezi kukupa kisa gari!"alijibu Harrison "tangu lini umeanza kuheshimu wanawake wewe! huyu naye ni malaya kama wengine usijali nitamtomba vizuri kwa sababu yako" kauli hiyo iliwasha hasira ndani ya Harrison na kurusha ngumi nzito iliyotua juu ya uso wa Rondo na kumdondosha chini.Wafuasi wa Rondo walimkaribia Harrison na kumpiga sana huku Rondo akisimama kwa maumivu "muueni huyo msenge " aliamuru huku Harrison akiendelea kupigwa sana.Kelele za vijana zilisikika kushangilia ugomvi huo,Kylie alipiga kelele kubembeleza Harrison aachiwe bila mafanikio.Sauti ya ving'ora vya polisi ilisikika na vijana wote walitawanyika kumuacha Harrison akigaagaa chini.Kylie alimsogelea na kumsaidia kunyanyuka "Harrison we have to go" "hapo hapo mlipo wote wekeni mikono kichwani na mpige magoti" waliongea polisi waliowasili eneo lile.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndani ya selo Kylie alijiinamia kwa uchungu na hofu juu ya kuwepo kwake selo usiku ule.Harrison alizunguka huku na huko akiwaza juu ya tukio zima "usijali Kylie nimeshaongea na mama yangu utatoka hutalala humu leo" "suala si Kulala humu Harrison sijui kwa nini nilikusikiliza ningejua ningebaki na Gerald tu" alifoka Kylie "samahani sana Kylie sikupanga hivi kama ulivyoona jamaa alikuwa anakuongelea vibaya nisingemruhusu.." "hao ni marafiki zako mimi hawanihusu usijifanye ulikuwa unajali na kuniweka matatizoni" aliongea Kylie huku akimwaga machozi.Harrison alimsogelea Kylie na kumshika mkono "usinishike Harrison! usinishike!" alikataa Kylie kwa hasira.Muda huohuo askari wa kituo hicho cha polisi pamoja na mama yake ya Harrison waliwasili mahali pale,askari yule alifungua geti kubwa la selo lililokuwa na kitasa kikubwa cha chuma.Harrison alinyanyuka na kumlaki mama yake lakini alipokea kofi zito "mama!" "ndio party hii eeh!" alifoka mama yake na kumuongezea kofi lingine "samahani mama ilikuwa ni bahati mbaya" alijitetea Harrison na kuongezewa kofi zito "shenzi wewe! bahati mbaya kukimbiza gari usiku! na gari liko wapi?" "nimelipoteza,mshindani wangu amelichukua" aliongea Harrison na kuongeza hasira zaidi kwa mama yake ambaye alimpiga kofi lingine "nalihitaji hilo gari haraka iwezekanavyo "mama tulikubaliana mshindi angechukua gari hivyo..." "sitaki kujua mlikubaliana nini nachohitaji gari lirudi" aliongea mama yake na kutoka selo kwa hasira huku Kylie na Harrison wakimfuata kwa nyuma.Askari alinyoosha mkono na kumzuia Kylie kutoka nje ya rumande na kumrudisha ndani.Harrison aligeuka na kumbwatukia askari "hey! yupo na mimi umesahau kama mlitukamata wote" "hapana,mama hapo amekulipia wewe peke yako huyu hajalipiwa kwa hiyo mpaka na yeye atakapolipiwa ndio ataweza kutoka" aliongea askari yule na kumfungia Kylie rumande.Kylie alirudi ndani taratibu kwa masikitiko,Harrison alisimama mbele ya geti lile na kumtazama Kylie aliyekuwa akilia "I'm sorry Kylie ila nitatafuta njia ya kukutoa humu leo" "nenda Harrison please niache mama yako anakusubiri" "I'm sorry Kylie I'm really sorry" "nenda bwana Harrison just go!" alipiga kelele Kylie kwa hasira.Harrison aligeuka na kuondoka kuelekea nje ya kituo hicho.Alielekea na kumkuta mama yake akiwa amekaa ndani ya gari kifahari katika siti za nyuma huku dereva wake akiwa amekaa kwenye siti yake.Alisogea dirishani na kukaribia uso wa mama yake "mama nakumbuka vizuri nilikuambia kwamba tulikamatwa wawili mimi na rafiki yangu lakini rafiki yangu bado yupo ndani na inaonekana hujamlipia" "kwa nini nimlipie hana wazazi" "mama mimi ndiye niliyemsababishia haya matatizo na ni jambo la uungwana mimi kuwajibika juu yake ulitakiwa kumlipia" alifoka Harrison "ingia ndani ya gari tuondoke naona huna cha maana cha kuongea" aliongea mama yake na kuangalia mbele.Harrison alijawa na hasira na hakufurahishwa kabisa na tukio la mama yake kutolipa faini kwa ajili ya Kylie.

    Asubuhi na mapema Kylie na mama yake walionekana kutoka ndani ya kituo cha polisi huku Kylie akionekana kuwa mchovu sana na kushikwa begani na mama yake kumsaidia kutembea.Mda huo ghafla Paul na Gerald walionekana kuwasili mahali hapo kwa kukimbia sana kiasi cha kuhema kwa nguvu "Kylie uko sawa!" aliongea Paul kwa wasiwasi "shikamoo mama Kylie" walisalimia kwa pamoja "Gerald! Paul! mnafanya nini hapa!" "tulisikia kilichotokea jana usiku kwa hiyo tulipanga tuje kukutoa" aliongea Gerald "uyo Harrison yuko wapi?" aliuliza Paul kwa hasira "mpotezeeni tu kwa bahati mbaya mama yake alimlipia yeye peke yake hakutegemea lakini.Mama nimechoka tuondoke" aliongea Kylie kwa sauti ya chini.Waliondoka wote kwa pamoja na kumsindikiza Kylie mpaka nyumbani kwao,Kylie aliwashukuru sana na mama yake aliwaalika chai lakini walikataa kwa kuwa asubuhi hiyo walikuwa wanawahi kwenye mazoezi ya kujiandaa na michuano mikubwa ya rugby ambayo ingefanyika ndani ya siku zijazo.

    "Nataka wote mshirikiane kumuua Gerald,muumizeni na ikiwezekana ua kila mtu aliyepo upande wake nitakuwa nyuma yangu nitawasaidia kwa kuwa nyie wote ni wangu na mtamuua Gerald kwa ajili yangu" aliongea Kronos kwa hasira huku akitazama wafuasi wake.

    Timu ya the thunders ilikuwa ikiendelea na mazoezi makali kujiandaa na michuano,kama kawaida Paul alionyesha juhudi kubwa na iliyofanya kila mtu kuamini kuwa Paul ndiye alikuwa moyo wa timu.Gerald hakuwa nyuma kiwango chake kilipanda siku hadi siku japokuwa hakuwa tegemeo lakini juhudi zake zilionekana.Kylie alikaa pembezoni mwa uwanja ambapo kulikuwa na mabenchi makubwa alikuwa akiwapa sapoti rafiki yakehttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Gerald na mpenzi wake Paul.Muda huohuo Harrison alikaribia taratibu uwanjani huku mikono yake ikiwa mifukoni alisogea taratibu mahali alipoketi Kylie na kukaa karibu yake "hi Kylie" "please go" alijibu Kylie na kuendelea kutazama uwanjani.Katikati ya uwanja Gerald alitazama nje na kumuona Kylie akiwa anazungumza na Harrison aliangalia kwa makini na kuendelea na mazoezi "look here Kylie nimekuja kuomba samahani kwa yaliyotokea siku ile,kwa maana hata simu zangu hutaki kujibu" "sitakiwi kujibu chochote kwako Harrison,can you please go now!" "ninachotaka uelewe Kylie ni kwamba sikudhamiria kufanya vile mama yangu nilimwambia alipe lakini..." "mmh hayo ya mama yako sitaki kuyasikia wewe nenda tu Harrison" alidakia Kylie.Gerald aliendelea kumtazama Kylie huku akihema kwa nguvu kwa sababu ya mazoezi makali.Ghafla aliguswa bega na Paul "yule ndio mtoto wa director sio ndiye aliyeondoka na Kylie siku ile" Gerald alitikisa kichwa chake kukubali.Paul alitembea kwa hasira kumkabili Harrison "Paul unataka kufanya nini subiri!" aliongea Gerald akijaribu kumzuia bila mafanikio.Paul alipomkaribia Harrison alikunja shati lake na kumvuta Kwa nguvu mpaka alipokaribia uso wake "sikia wewe mpumbavu ngoja nitumie fursa hii kukuonya stay away from this girl na yeyote anayenihusu". Jambo hilo lilimshitua Kylie ambaye alijaribu kumzuia Paul amuachie Harrison kwa kuwa alijua hasira kali za Paul.Gerald aliwasili wakati huo na kusogea karibu "Paul muache" "hapana Gerald huyu mtu inabidi aonywe ili asirudie tena.Umesikia wewe mpumbavu sijali wewe ni mtoto wa mwenye shule mimi nitakuvunja taya hilo" aliongea Paul kwa hasira.Harrison alijitoa na kumsukuma Paul kwa nguvu "huna haki ya kuja hapa na kunikunja kama vile tunajuana.Mimi na Kylie ni marafiki na nimekuja hapa kuongea na rafiki yangu.Unafikiri wewe ni nani uje hapa na kunikunja mmh" "huyo ni boyfriend wangu Harrison wewe nenda tu usijitafutie matatizo atakudhuru" alidakia Kylie "ooh! naona sasa naelewa,wivu! usijali bro huyu ni demu wako wala simuhitaji ila sikulaumu huwezi sana kumuamini demu wako akiwa na mimi nani anajua labda siku itatokea nikakupokonya" aliongea Harrison na kumsogelea Paul usoni huku akitabasamu kwa dhihaka.Paul alirusha ngumi iliyotua juu ya uso wa Harrison na kumuangusha chini,Gerald na wachezaji wengine walimsogelea Paul na kumshika.Kylie alikunja uso wake kana kwamba alihisi maumivu.Harrison alisimama na kushika uso wake kwa maumivu "utafanya nini eeh utanipiga!" aliongea Paul kwa jazba huku akijaribu kujitoa mikononi mwa Gerald na wachezaji wengine.Ghafla mda huo polisi wawili pamoja na mwalimu mkuu waliwasili mahali pale "kuna nini hapa?" "hakuna kitu" alijibu Paul huku akihema.Mwalimu mkuu aliwageukia polisi wale "okay tuko hapa tuna shida na Mr Harrison" aliongea mmoja wa polisi wale.Harrison alishituka huku kushika uso wake "mimi ni Harrison,vipi kuna tatizo?" "unamjua Rondo James?" "ndio namjua" "mara ya mwisho umemuona wapi?" "Juzi usiku kwani kuna tatizo gani?" alizidi kuhoji Harrison "well,amekufa jana usiku amekutwa nyumbani kwake akiwa amekufa" alijibu mmoja wa polisi wale "kwa hiyo mnahisi mimi ndiye niliyemuua!" "hatujui,gari yako Subaru iko wapi?" "nilimpa yeye" "haipo tunafikiri labda unayo,ila usijali siku njema" waliongea askari wale na kuondoka pamoja na mwalimu mkuu "kumbe wewe ni muuaji au unataka kumuua na Kylie pia" alidhihaki Paul "Paul acha bwana" alidakia Kylie.Harrison alishika uso wake kwa maumivu na kumnyooshea kidole Paul "hii ngumi uliyonipiga leo nitalipa siku" aliongea Harrison na kuondoka kwa hasira "nasubiri hiyo siku ku** wewe" alitukana Paul huku Kylie akijaribu kumtuliza.

    Gari kubwa iliyobeba vijana wengi wapatao nane wanawake Kwa wanaume huku mikononi mwao wakiwa na chupa kubwa za pombe kali,baadhi yao walionekana kuvuta bangi na kufurahia mziki mkubwa uliokuwa ukipigwa kwenye gari hilo.Gari hiyo ilitembea kwa kasi katikati ya barabara tupu katika usiku huo mnene.Ghafla dereva aliona mtu katikati ya barabara na kujaribu kumkwepa lakini gari ilikosa kutulia na kupinduka mpaka kwenye kichaka kikubwa kilichokuwa na nyasi ndefu pembezoni mwa barabara."Kila mtu yuko sawa?" aliuliza dereva yule huku akitoka taratibu nje ya gari ile iliyopinduka "yah nafikiri kila mtu yuko sawa hatujaumia sana" alijibu msichana mmoja Kati ya wale vijana "John hujamgonga kweli!" "sijui lakini nina uhakika sijamgonga" "nafikiri turudi tukamuangalie tuwe na uhakika" aliongeza mwanaume mmoja Kati yao.Walianza kutembea taratibu kurudi barabara kuu kuhakikisha kama hawakugonga mtu "lakini guys nina uhakika sijamgonga hapa tupige simu kuomba msaada hata wa fundi mekanika" ghafla walisikia sauti za hatua za wanyama "nini hicho!" aliuliza mmoja wa vijana wale kwa hofu.Sauti kubwa za mngurumo kama wa simba ulisikika na ghafla wanyama wakubwa kama mbwa weusi walitokea wasipojulikana na kuwararua vijana wale na kuua wote.Baada ya kitoweo hicho wanyama wale walinguruma kwa sauti kubwa.Upande wa pili wa barabara kijana mmoja ambaye hakuonekana vizuri aliangalia wanyama wale waliokuwa wakiunguruma na kuondoka.Vijana nane waliiuawa usiku huo na wanyama wakali.

    Helikopta kubwa ya chaneli kubwa ya televisheni iitwayo NATIONAL SPORTS CHANNEL iliruka juu ya uwanja mkubwa wa PETER LONELL ARENA uliokuwa umefurika watu kutoka maeneo mbalimbali "michuano mikubwa ya kitaifa ya rugby imefunguliwa rasmi leo,mashabiki wana msisimko wa ajabu ndio maana wamejaa kushabikia timu zao.Macho yote ni kwa bingwa watetezi the thunders je watatetea taji lao.Nisiongee mengi naitwa Mercy Pearlson.Enjoy" aliongea mwanamke mrembo mtangazaji wa kituo hicho cha TV.Timu ya the thunders haikupangiwa kucheza siku hiyo kwa hiyo walikaa juu ya jukwaa maalum ili kushuhudia wapinzani wao wakipambana "timu ya kwanza kuingia uwanjani ni Portland timbers makofi tafadhali" aliongea mtangazaji na sauti yake kusikika kwenye spika kubwa zilizokuwa uwanjani hapo.Timu ya Portland timbers iliingia kwa haraka huku ikiwa imevalia jezi zao za kijani "wapinzani wao kwa leo hii ni timu mpya kabisa inaitwa the beasts,makofi tafadhali" timu ya the beasts iliingia ikiwa imevalia jezi zao za rangi nyeusi zilizowapendeza vizuri.Timu zote zilijipanga vizuri kukabiliana.Timu nzima ya the thunders pamoja na kocha wao walishituka baada ya kumuona Daniel ndani ya uwanja akiichezea the beasts,wote walijua uwezo mkubwa ambao Daniel alikuwa nao hivyo walisali kimoyo moyo kuomba timu ya the beasts itolewe mapema.Daniel aliangaza macho yake juu ya uwanja uliofurika watu na kupeleka macho yake mpaka kwenye jukwaa ambalo timu ya the thunders walikaa alitabasamu kwa dhihaka "anatuangalia,Daniel anatuangalia msiogope huyo jamaa mimi hanisumbui" aliongea Paul kwa kujiamini "hello! Gerald tumekutana tena,kunifukuza kwenye timu yenu wakati nilikuwa mchezaji bora ni kosa kubwa sana lisilohitaji msamaha.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Salini sala zenu za mwisho maana tutakutana tu na msiombe kitakachowapata" . Sauti ya Daniel ilisikika ndani ya kichwa cha Gerald na alishindwa kuamini kama Daniel alikuwa ni dream holder na muda wote huo waliishi pamoja."Unafikiri naogopa Daniel! niko tayari kwa ajili yako" alijibu Gerald kwa kunong'ona.Paul alimtazama Gerald aliyekuwa akinong'ona peke yake na kutomuelewa kiasi cha kumshangaa zaidi.Kipenga kilipulizwa na mechi ilianza kasi sana huku timu ya the beasts ikitawala mchezo mzima.Kasi na nguvu waliyokuwa nayo wachezaji wa the beasts ilimshangaza kila mtu na kujenga hofu kwa timu pinzani.Shughuli nzito na uchezaji wa kipekee wa Daniel uliwashangaza wengi na kuzua hofu kwa wachezaji wa the thunders kiasi cha kocha kujutia uamuzi wa kumtimua.

    Kila siku timu ya the thunders pamoja na timu ya the beasts ziliibuka videdea katika mechi zao.Uwezo wa timu hizi mbili ulivutia mashabiki wengi na wengi walitabiri kuwa timu hizi zingefika fainali na mojawapo kuibuka na ubingwa.Paul kama kawaida ndiye aliyekuwa nyota wa timu yake akiisaidia timu yake kushinda kwa kiasi kikubwa sana.Majina mawili tu ndiyo yaliyotawala kwa mashabiki jina la Paul na Daniel ndiyo ambayo yalikaa midomoni mwa mashabiki kiasi cha kuwagawa katika pande mbili ambao waliamini Paul ni bora na ambao waliamini kuwa Daniel ni bora.Timu ya the thunders pamoja na timu ya the beasts ndio zilizokuwa na ushindani mkubwa na kufanikiwa kukutana fainali.Fainali hiyo ilikuwa ya kihistoria kuliko fainali zote kwa kuwa ilijaza watu wengi mno na wengine walikosa nafasi uwanjani.Baa zote nchini zilifurika wateja ambao hawakutaka kukosa fainali hiyo.Nyumba zote zilikuwa tulivu kwa kuwa familia zilijikusanya kuangalia mechi hiyo kwenye luninga zao.Wamiliki wa michezo ya kamali waliingiza fedha nyingi sana siku hiyo.Kwa hakika ilikuwa ni mechi ya aina yake.Timu zote zilijipanga vizuri kwa ajili ya fainali hiyo.Paul alimuangalia Daniel kwa hasira na kudhamiria kuwa kwa namna yoyote ile lazima amuoneshe Daniel nani alikuwa bora kati yake na yeye mwenyewe.Daniel alimtazama Paul usoni na kutabasamu na kisha kumgeukia Gerald aliyekuwa amekaa kwenye benchi la wachezaji wa akiba kwa hofu kwa kuwa alijua timu yake inaweza kuwa hatarini "jitazame Gerald huna hata raha kwa nini! ooh kwa sababu unajua naenda kushinda mechi! au kwa sababu naenda kuua kila mchezaji leo na itakuwa mwisho wao na wako.Naenda kuleta msiba wa kitaifa leo" sauti ya Daniel ilisikika kichwani mwa Gerald huku akitabasamu "nakuonya Daniel usijaribu kufanya kitu chochote cha kipumbavu na ukifanya lolote mimi mwenyewe nitakuua Daniel" alijibu Gerald kwa kunong'ona "tutaona basi" alijibu Daniel.Wakati huo Kylie hakuwa mbali na benchi la wachezaji wa the thunders alimuona Gerald akinong'ona peke yake huku akiangaza macho uwanjani na kushindwa kuelewa kwa nini Gerald alikuwa akionekana akiongea peke yake.Kipenga kilipulizwa na mechi ilianza kwa kasi sana huku kila mchezaji akidhamiria kushinda mechi hiyo.Paul aliruka juu sana ili kuudaka mpira uliokuwa ukija upande wake,aliudaka na kutua nao chini vizuri huku akikimbia kwa kasi sana.Wachezaji wa nne wa the beasts walimvamia kujaribu kumzuia lakini aliwapita kwa ustadi mzuri sana.Alikimbia kumkabili Daniel aliyekuwa mbele yake alimzunguka kulia na mara moja kurudi kushoto kwa kasi sana.Chenga ambayo ilimshinda Daniel na kuanguka chini.Paul alivusha mpira kwenye mstari na kuiandikia timu yake bao la kwanza.Uwanja mzima ulipiga kelele kushangilia bao safi lililofungwa na Paul ambaye alitanua mikono yake kwa majigambo.Paul alimsogelea Daniel usoni na kutabasamu kwa dharau lakini mwamuzi wa mchezo aliwahi na kuwatenganisha.Timu ya the beasts ilianza mpira kwa kasi kubwa na kupeana pasi nyingi nzuri na ambapo mpira ulirudi katikati ya uwanja na kumkuta Daniel ambaye aliudaka vizuri na kuwapiga chenga wachezaji wa the thunders.Paul alimkimbiza kwa kasi na kutua juu ya mgongo wake na kumdondosha Daniel chini.Mpira ulitambaa chini ambapo kwa haraka Paul aliukamata na kutoa pasi safi kwa mwenzake aliyeandika bao la pili kwa timu ya the thunders.Kelele nyingi zilisikika uwanja mzima kushangilia bao hilo,mechi ilianza kuonekana rahisi hasa kwa Paul ambaye aliwatesa sana wapinzani wake kwa chenga zake za maudhi kwa hakika alikuwa katika ubora mkubwa usiku ule.

    Mchezaji mwingine wa the thunders aliudaka mpira vizuri lakini ghafla alipigwa kikumbo kizito na Daniel na kuondoka chini huku akivuja damu mdomoni kwa wingi,wahudumu wa afya walimkimbilia kwa haraka kwa ajili ya kumpatia matibabu lakini ukubwa wa jeraha lake ililazimika mda huo akimbizwe hospitali kwa matibabu ya umakini. "Huyo wa kwanza Gerald,naweza kuacha nisiue tena kama ukijisalimisha kwa Kronos,Grotto" "siwezi kufa kizembe hivyo Daniel mwambie Kronos hivyo" "sawa uamuzi ni wako mimi sina tatizo naua tu" alijibu Daniel.Mchezo uliendelea kwa kasi ambapo baada ya dakika kadhaa mchezaji mwingine wa the thunders alipigwa kikumbo na mchezaji wa the beasts na kuanguka chini kwa kishindo kikubwa na kumfanya agalegale kwa maumivu.Wahudumu wa afya waliwasili kumsaidia lakini ilishindikana huyo naye alikimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.Paul na watu wote walishangaa ilikuwaje kila mchezaji aliyepigwa kikumbo aliumia vibaya na kukimbizwa hospitali! baadhi ya mashabiki waliamini kuwa huenda wachezaji wa the thunders walikuwa wamechoka "wa pili huyo Gerald namba inazidi kuongezeka na mimi na enjoy tu" sauti ya Daniel ilisikika kichwani mwa Gerald na kumtazama Daniel aliyekuwa akimuangalia na kutabasamu kwa dhihaka "tafadhali acha,hao hawana kosa hao" alinong'ona Gerald huku akimtazama Daniel kwa hasira.Kwa mbali Kylie alimuona Gerald akinong'ona peke yake na kushangazwa na jambo lile kuwa Gerald alikuwa akinong'ona kana kwamba alikuwa anaongea na mtu "kumbuka Gerald unaweza kuwaokoa" aliongea Daniel "Gerald jiandae unaingia sasa hivi" aliongea kocha ambaye kwa muda huo alikuwa akibadili wachezaji baada ya wachezaji muhimu kuumia "eeh..! kocha hapana sitacheza maana sijisikii vizuri leo" kocha wake alihema kwa nguvu na kumgeukia Gerald "basi sawa naelewa kama unaogopa".Dakika zilisogea huku timu zikiwa sare mpaka muda huo Paul alihema kwa nguvu kwa kuwa alibebeshwa mzigo mkubwa,alitazama glovu zake na kuzishangaa kwa kuwa zilitoboka kana kwamba zilikuwa zimeungua moto.Gerald alinyanyuka taratibu kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo Kylie alipomuona naye alisimama na kumfuatilia Gerald kwa nyuma.Gerald alitembea kwenye korido ndefu lakini ghafla Sebastian alitokea mbele yake "nini tatizo Gerald linaonekana ni kubwa kuliko ulivyonieleza mwanzo" aliongea Sebastian baada ya kumuona Gerald akiwa anahema kwa nguvu "Gerald embu tulia tatizo ni nini?" "inaonekana Daniel ataua wachezaji wote tayari ameanza na wawili" aliongea Gerald kwa hofu "Mungu wangu kwa nini!" "amesema nijisalimishe kwa Kronos la sivyo ataua wachezaji wote" aliendelea kujibu Gerald kwa hofu.Kylie alijibanza vizuri kwenye kona na kusikiliza maongezi baina ya Sebastian na Gerald na kushituka kwa hofu baada ya kujua kuwa kuna mauaji yalikuwa yakiendelea usiku huo.Sebastian alikaza macho yake na kuangalia huku na huko "umekuja na mtu?" "hapana kwa nini unauliza?" "tuingie changing room" aliamuru Sebastian na Gerald alitangulia ndani.Sebastian alitazama huku na huko kana kwamba alihisi mtu na kisha kuingia "umeniambia Daniel anauwa wachezaji na tayari wawili wapo hospitali lakini inawezekanaje!" "Daniel ni dream holder" "nini!" alishangaa Sebastian "yah ni dream holder na sijui anauwaje wachezaji kwa mtindo huo.Labda na yeye ni creator" "no Daniel siyo creator, creators tuko sita tu,hamna namna ya kwamba yeye ni creator" "la..la..labda kuna wengine wengi sisi hatuwajui wapo tu huko" alihoji Gerald kwa hofu.Sebastian aliwaza sana huku akizunguka huku na huko "no nafikiri hawa the beasts wote ni dream holders na wako chini ya Kronos.Ndiye anayewapa hizi aina ya nguvu na uwezo.Hao wachezaji wameumiaje?" "yaani ni kama wamejeruhiwa ndani kwa ndani ya miili yao.Wameumia zaidi ndani ya miili yao na siyo nje" alijibu Gerald "ina maana kila aliyepigwa kikumbo ndo alikuwa amejeruhiwa kiasi hicho! siyo kwamba wachezaji wenu wamechoka hapa kuna kitu cha ziada" aliongea Sebastian "ndio nashangaa uliniambia kuwa dream holders hawana nguvu duniani zaidi ya Grotto sasa ina..." http://deusdeditmahunda.blogspot.com/"yah Gerald hawana nguvu duniani na hili kuwajeruhi hivyo ina maana waliwajeruhi Grotto na siyo pale uwanjani" "lakini dream holders hawawezi kwenda Grotto mpaka wewe wamelala!" "ndiyo uko sahihi na ndiyo maana Kronos yuko pale anawasaidia kuwavuta Grotto bila wao Kulala" aliongea Sebastian na kumchanganya zaidi Gerald "lakini mbona wachezaji waliojeruhiwa walikuwa pale uwanjani na kuumia sasa ukiniambia wanapelekwa Grotto nashindwa kuelewa" "tendo hilo linatokea kwa kasi na haraka sana huwezi kuliona kwa macho ya kawaida.Ila kwa vyovyote usijisalimishe kwa Kronos" alijibu Sebastian "hapa naona nazidi kuchanganyikiwa tu.Sasa nafanyaje mana Daniel atazidi kuua watu wasio na hatia yeyote "rudi uwanjani ukacheze ila hakikisha Daniel anakupiga kikumbo maana lazima atajaribu kukuua huku Grotto.Wewe ni supreme Gerald akikumbatia jitoe mara mbili mwili wako mmoja ubaki uwanjani mwingine uende Grotto.Kwa kuwa wewe ni supreme hata Daniel naye atajitoa mara mbili.Hiki kitendo ni cha haraka na kasi sana kwa hiyo na wewe uwe mwepesi.Mimi nitabaki huku kucontrol mwili wako" aliongea Sebastian.Gerald aliwaza kwa muda na kuona ugumu wa jambo hilo "usiogope Gerald kila kitu kitakuwa sawa inabidi umzuie huyu Daniel.Unaweza."

    "Kocha niko tayari kucheza,naweza kusaidia" "una uhakika tuko nyuma goli tatu ila kama unaona unaweza kucheza vaa Viatu" alijibu kocha na kutoa ishara kwa mwamuzi kuwa Gerald alitakiwa kuingia.Kylie alirudi jukwaani huku akiwa ana hofu na kushindwa kuelewa nini kilikuwa kinaendelea nyuma ya mechi hiyo.

    Gerald aliingia uwanjani kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine aliyeumia vibaya sana.Gerald alimtazama Daniel na kuwaza kichwani mwake "nilikuambia Daniel siwezi kufa kizembe na umefanya makosa makubwa sana kuwaua watu wasio na hatia.Na unajua nini hili limenitia hasira hivyo basi nakwenda kukusimamisha hapa hapa uwanjani" "basi vizuri" alijibu Daniel.Gerald alimsogelea Paul na kumpa mkono "glovu zako vipi mbona zimetoboka?" "hata sijui mimi mwenyewe nashangaa sijui imekuwaje" alijibu Paul.Mechi kali iliendelea ambapo Gerald alipata mpira na kukimbia nao kwa kasi,aliwakwepa walinzi wawili wa timu pinzani kwa ustadi na kupenyesha pasi safi iliyomkuta Paul na kufunga goli kirahisi.Mashabiki wa the thunders walipiga kelele kushangilia bao hilo na kuona kuwa uhai ulirudi kwenye timu yao "come on Daniel unaniogopa au!" aliongea Gerald huku akimtazama Daniel kwa mbali.Mechi iliendelea kwa kasi huku Gerald akionyesha hali ya kupambana kwa kuwapiga sana vikumbo wapinzani na kuzima mashambulizi yao.Pasi ndefu ilipigwa kwa Gerald ambaye alikuwa katikati ya uwanja,aliwazunguka mabeki vizuri na kurusha mpira kuelekea mbele kabisa mpaka ulipomkuta Paul aliyeruka na kuudaka vizuri.Alikimbia na mpira kwa kasi lakini Daniel alipomuona alimkimbiza kwa kasi ili ampige kikumbo kizito.Gerald alizisoma vizuri njama za Daniel aliyekuwa tayari kwenye mbio za kasi kumkabili Paul.Gerald alikimbia akitokea nyuma ya uwanja upande wa mashariki kuelekea kumkabili Daniel.Paul aligeuka nyuma na kumuona Daniel akimkaribia.Daniel aliruka juu sana na akiwa juu aliona mgongo wa Paul kabla ya kutua juu yake.Ghafla Gerald alimrukia Daniel huko huko juu na kuanguka naye chini huku wakiserereka mbali sana.Gerald alimuokoa Paul na kumfanya ashinde kirahisi.Gerald na Daniel walinyanyuka kutoka chini na Paul alimsogelea Gerald na kumpiga begani "fresh Gerald umecheza vizuri" timu ya the thunders kwa mara nyingine iliukamata mchezo kwa kiasi kikubwa.Kila mara Gerald alipokamata mpira alimpa pasi Paul ambaye alikuwa akishinda kirahisi.Uwanja wote ulifurika kwa furaha,Gerald na Paul walitengeneza kombinesheni nzuri.Akili nyingi za Gerald zilizojua kutumia kasi ya Paul ndiyo ilikuwa nguzo kubwa ya ushindi.Kipenga cha mwisho kilipulizwa na timu ya the thunders iliibuka mshindi na kuweza kutetea taji lake.Kelele nyingi zilisikika kutoka kwa Kylie aliyekuwa akiruka kwa furaha.



    Kwa nguvu Gerald na Daniel walidondoka chini huku wakihema kwa nguvu.Walipigana sana huku Daniel akionekana kulemewa sana na ngumi nzito na zenye kasi kutoka kwa Gerald.Gerald alimkaba koo Daniel na kumrusha mbali sana ambapo Daniel alidondoka na kuhema kwa maumivu akijitahidi kunyanyuka "nilikuambia Daniel kwamba nitakuweka mikononi mwangu na nitakuua,umeshachelewa kwa maana tayari the thunders wameshashinda mechi" aliongea Gerald na kuzidi kumsogelea Daniel aliyekuwa amekwisha nyanyuka na kuyumba kwa uchovu.Daniel alirusha ngumi ya kizembe ambapo Gerald aliinama na kuikwepa bila matatizo alimgeuza na kumkaba na kumsogelea karibu na sikio lake "unajua umewajeruhi watoto wa watu wasiokuwa na hatia ili tu umfurahishe Kronos.Sasa hata Kronos hawezi kukusaidia" aliongea Gerald kwa hasira huku akimkaba Daniel kwa nguvu "Gerald! unataka kuua mtu leo!" aliongea Kronos aliyekuwa amewasili ghafla na kuonekana kutembea kuwakaribia.Gerald alishituka na kumuachia Daniel aliyedondoka chini kama mzigo mzito "Kronos bora umejileta nilikuwa sina mpango wa kumuua mtu yeyote ila sasa ninao na nitaenda kukuua" aliongea Gerald kwa hasira na kumkimbilia Kronos na kumrushia ngumi nyingi sana ambazo Kronos alizikwepa kwa ustadi,kila ngumi aliyorusha Gerald ilionekana kuambatana na hasira kali sana ndani yake."Gerald unajitahidi sana siyo kama nilivyokuacha mwanzo siku hizi unajitahidi hata kurusha ngumi ila kwa bahati mbaya huwezi kunipiga kama ilivyokuwa kwa baba yako" aliongea Kronos kwa dhihaka.Gerald alirusha teke lakini lilidakwa vizuri na Kronos na kuuzungusha mguu wa Gerald kwa kasi kitendo kilichomrusha Gerald juu na kumuangusha chini.Alikamatwa shingo kwa nguvu na kurushwa upande mwingine ambapo alijibamiza kwenye mti na kuanguka chini "yaani ni rahisi sana kukuua wewe Gerald hta sijui ni kwa nini najisumbua kuwatuma hawa dream holders wadhaifu wasiokuwa na msaada wowote" aliongea Kronos huku akimtazama Daniel aliyekuwa amelala chini kwa uchovu huku akimtazama Kronos akimsulubu Gerald.Kronos aliweka mkono wake juu ya koo la Gerald na kumnyanyua juu kwa nguvu huku akimkaba "yeees Gerald sasa nimekuweza hakuna wa kukusaidia shida yangu haikuwa kwenye mechi yenu ya kipumbavu laiti kama ungejisalimisha mapema nafikiri sasa hivi ungekuwa na kifo chenye amani lakini kwa sababu umekuwa msumbufu haina budi kufa kwa usumbufu na wewe" aliongea Kronos huku akizidi kumkaba http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Gerald kwa nguvu sana.Gerald alijitahidi kukamata mkono wa Kronos ili auondoe huku pumzi yake ikionekana kukata "unakufa sasa Gerald ninabaki mimi na baba yako.unajua nini kitatokea wewe ukifa mimi ninakuwa supreme na hawa dream holders wote nitawatawala na baba yako nitamuua na mama yako atakuwa mke wangu" maneno hayo yalijaza hasira ndani ya Gerald na ghafla rangi yake ya ngozi ilibadilika na kuwa ya bluu iliyong'aa sana.Jambo hilo lilimshitua Daniel na kumshangaza na kutoamini kuwa mda wote alikuwa akijaribu kupigana na supreme! "yeah unabadilika"aliongea Kronos huku akimshangaa Gerald.Kwa nguvu Gerald alijitoa mikononi mwa Kronos na kumpiga ngumi za haraka zilizomuangusha Kronos chini.Alimnyanyua na kumrusha juu sana na kisha alipomdaka alimkandamiza zaidi juu ya barabara kiasi cha barabara kupata ufa mkubwa.Hasira nyingi zilimjaa Gerald ambapo alimfuata Kronos aliyekuwa chini akiugulia maumivu na kumkaba koo kwa nguvu.Roho ya Kronos ilianza kutoka huku Gerald hasira nyingi zikiendelea kumpa nguvu ya kumkaba Kronos "Gerald ukimuua hutaweza kumuona baba yako yeye peke yake ndio anajua mahali  alipomuweka baba yako" sauti ya Sebastian ilisikika kichwani mwa Gerald.Alipiga kelele za hasira na kumuacha Kronos akikohoa baada ya kuachwa kukabwa "nisikilize Kronos sasa hivi unakwenda kunionesha baba yangu alipo" aliongea Gerald kwa hasira.Kronos alisimama taratibu huku akishika koo lake na kumtazama Gerald aliyekuwa akihema kwa nguvu "ndiyo supreme nitakuonesha baba yako alipo" "sasa hivi" aliamuru Gerald.Ghafla Kronos alipotea mbele yake na kutoweka Gerald aliangalia huju na huko kwa hasira "ameenda wapi? ameenda wapi? noooo...!" alipiga kelele kwa hasira.Aligeuka taratibu na kumtazama Daniel aliyekuwa akitetemeka kwa hofu kuogopa kuuliwa mda huo na supreme,taratibu Gerald alimsogelea huku rangi yake ya bluu ikiwa inafifia kuashiria hasira zilikuwa zikipungua kabla hajamkaribia alianguka chini kwa uchovu jambo lililomshitua Daniel.+



              Uwanja uliendelea kupiga kelele kumpongeza Gerald kwa ushindi mkubwa na mabadiliko makubwa aliyoyaonyesha kwenye fainali hiyo.Wachezaji wote wa the thunders walimzunguka Gerald katikati huku wakimshangilia kwa nguvu ghafla Gerald alianguka chini kwa uchovu huku kila mmoja akimshangaa kwa mshituko "nafikiri tuite gari la wagonjwa tumkimbize hospitali" aliongea Paul "hapana" alidakia Daniel aliyeingia katikati yao na kumsaidia Gerald kunyanyuka na kuondoka naye.Jambo hilo lilimshitua kila mtu kwa kuwa walijua kuwa Daniel alikuwa adui yao na ilikuaje mpaka alikuja na kumnyanyua na kuondoka naye.Kwa mbali Paul aliona alama za kuumia juu ya shingo ya Gerald na rangi ya shingo yake ilikuwa ya bluu iliyokuwa ikififia.Hilo lilimshitua Paul na kumpa maswali mengi kichwani kama Gerald alikuwa anaumwa na kama alikuwa anaumwa je ni ugonjwa gani ambao ulifanya rangi ya ngozi yake kubadilika kiasi kile!.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



            Kwenye korido huku Gerald akiwa ameshikwa begani akisaidiwa kutembea na Daniel baada ya uchovu mkubwa sana,alihema kwa nguvu na kutetemeka sana kama mtu aliyekuwa anaumwa "Daniel nafikiri uende sasa utazua maswali mengi ambayo nitakosa majibu" aliongea Gerald kwa shida huku akihema kwa nguvu "hapana Gerald siwezi kukuacha hapa inabidi tutafute mahali upumzike umepoteza nguvu nyingi sana umekuwa dhaifu sana" aliongea Daniel huku akitembea taratibu na kutafuta kuingia kwenye moja ya vyumba vilivyokuwa kwenye korido hiyo.Mda huo Sebastia alitokea mbele yao "Gerald! uko sawa! amepatwa na tatizo gani?" aliuliza Sebastian kwa hofu "sijui alikuwa akipigana na Kronos na rangi yake ilipokuwa ya bluu alimpiga sana Kronos lakini Kronos bahati mbaya amekimbia.Ghafla tu alidondoka chini! nikaamua kumrudisha huku duniani na kumtoa uwanjani kumsaidia kwa sababu yeye ni supreme na anastahili msaada wangu mimi kama mtumwa wake" alijibu Daniel akiwa wamesimama.Sebastian alimuangalia Gerald aliyekuwa ameinamisha kichwa chake kama mtu aliyekuwa amekata roho "vizuri,sasa wewe nenda zako niachie mimi nitaenda naye Groto kuangalia tatizo lake ni nini hasa" aliongea Sebastian



             Kylie alishuka kutoka kwenye jukwaa na kuingia moja kwa moja hadi ndani ya uwanja ambapo wachezaji walikuwa na furaha na kushangilia huku wakimrusha kocha wao juu na kumdaka kuonyesha furaha waliyokuwa nayo mioyoni mwao "Paul! Paul!" aliita Kylie aliyekuwa mbali kidogo na wachezaji.Paul aligeuka baada ya kusikia sauti ya Kylie iliyokuwa ikimuita na kuamua kumsogelea kwa ukaribu zaidi "hey baby"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ "Paul, Gerald yuko wapi?" "baby kuna tatizo gani? hufurahii kuona  mpenzi wako kuwa nimeshinda ubingwa!" "Paul hatuna muda wa haya mambo sasa,Gerald yuko wapi?" aliongea Kylie kuonyesha kuwa alikuwa makini kutaka kujua alipokuwepo Gerald "sijui alikuwepo mda si mrefu lakini Daniel alikuja akamchukua wakaondoka wote" "na wewe ukaacha Daniel ambaye ni adui yenu amchukue Gerald na kuondoka naye nani anajua atamfanya nini huko alikompeleka!" alifoka Kylie "Kylie mbona unajali sana kuhusu Gerald! sikia inavyoonekana Gerald na Daniel wanajuana vizuri walikuwa wanatuchezea akili zetu kipindi chote hiki!" "umeona sasa! hilo ndilo tatizo lako Paul!" alifoka Kylie na kuondoka kuelekea ndani ya vyumba ya kubadilishia ngua huku akikimbia "Kylie!" aliita Paul kujaribu kumsimamisha Kylie bila mafanikio mpaka alipoamua kumfuata kwa nyuma.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog