Simulizi : Nini Hatima Ya Maisha Yangu
Sehemu Ya Tano (5)
Nilibaki namwangalia bila kusema lolote maana sikuwa namfahamu zaidi ya kumuona kwenye picha, na kile alichokuwa ananiambia kilikuwa ni kigeni masikioni mwangu. Kiukweli nilikuwa nimechanganyikiwa kwa kile nilichokuwa nakiona mbele yangu.
Wakati nikiwa najiuliza nini chakumjibu, nilisikia sauti ikiniita hakuwa mwingine alikuwa ni Mama yangu. Kichwani kwangu nilitawaliwa na mawazo mengi nilijihisi ni mtu alie kufa na kwenda kukutana na watu waliokufa kitambo, akili yangu bado haikuamini pale tulipokuwa ni Duniani. Niliamini kama pale patakuwa ni Duniani basi wale waliokuwa pale walikuwa ni mizimu, ndivyo akili yangu ilivyokuwa inanituma. Ile sauti ya Mama yangu ilinikumbusha kipindi Mama yangu anapoteza maisha na maneno alio yatamka wakati anakata roho.
"John najua wote hapa tuna makosa, ila tunaomba utusamehe maana tulijaribu kutumia njia mbaya na ndefu kukuambia ukweli kuhusu wewe na familia yako"
Yalikuwa ni maneno ya Mjomba Denis ambae kwangu alikuwa ndiye mtu niliekuwa namuamini kuliko mtu yeyote, lakini kwa wakati ule akili yangu haikuwa sawa sikuweza kumwamini mtu wa aina yoyote. Mawazo yangu yalikuwa wale waliokuwa pale ni mizimu, maana wale waliokuwa wamepoteza maisha wote ndio waliokuwa pale.
“John najua ni muda mrefu ulikuwa hujui ukweli na nafikiri wakati wa kujua ukweli ndio huu”
Alizidi kuongea Mjomba huku akiwa anampa nafasi ya kuongea mama yangu mlezi, Mama nae alionekana kuwa na kigugumizi ikabidi aongee Yule Afande na kuanza kusema.
“Yapata takribani miaka kumi na nane (18) toka ulipo zaliwa katika familia ya Bwana Derrick. Ni mtoto wa pekee katika familia hiyo, toka umezaliwa hukuwahi kujua ukweli kuhusu familia yako. Ukiwa na umri wa miaka sita Baba yako aliondoka na kuelekea Marekani kikazi, wakati akiwa kule kulitokea tatizo la tege waliokuwa wamepanda kusemekana ilipata ajali mbaya na walikuwamo kwenye ile ndege walikuwa wamepoteza maisha wote. Hakuna alieamini kwamba Baba yako amepoteza maisha kila mtu zile taarifa zilimpa wakati mgumu kuzipokea na kuziingiza akilini. Baba yako alikuwa ni mtu wa watu kila mtu aliepata zile taarifa alionekana kuwa na mawazo mengi na masikitiko mengi”.
Aliongea yule afande maneno ambayo yalizidi kunichanganya na kuanza kuhisi Baba yangu hayupo Duniani. Nilimwangalia yule afande jinsi alivyokuwa anaonge kwa makini na utulivu wa hali ya juu.
“Kwa kipindi hicho Mama yako alikuwa kwenye masomo yake Nchini Afrika kusini, tuliona zile taarifa tulishwa kumpatia Mama yako maana tulihisi pengine zingemfanya asifanye vizuri katika masomo yake, tuliamini zile taarifa zinge muumiza sana ikabidi kukaa kimya tukisubiri akimaliza masomo yake tungeweza kumpati zile taarifa, hatukufanikiwa kuona mwili wa Baba yako mpaka Mama yako alipomaliza masomo yake ndipo tulipompati taarifa za Mmewe kupata ajali mbaya ya Ndege”.
Alipofika hapo alitulia kidogo na kuanza kumwangalia yule msichana nilieambiwa ni Mama yangu kisha kuendelea.
“Taarifa zile zilimuumiza Mama yako hadi zikapelekea Mama kudhohofika kiafya na kuwa mtu wa mawazo kila wakati, hazikupita siku nyingi Mama yako alihitisha kikao cha familia na kuzungumzia kuhusu maisha yake ya baadae, jambo ambalo aliokuwa nalo ni kuhusu mtoto ambae ni wewe. Kwa kuwa Mama yako alikuwa bado msichana mdogo hakupenda kuwa mwenyewe aliamini hakukuwa na mwanaume angeweza kumuoa angali ana mtoto, jambo ambalo lilikuwa gumu maana wewe ulihitaji matunzo ya Mama yako ili ukuwe katika malezi mazuri, ilitulazimu kukubaliana na Mama yako kwa kile alichokuwa anakihitaji. Tulikubaliana tukubadili jina la Baba na kukupa la Baba yako mlezi, kila kitu tulifanikiwa kukibadili na wewe ukafahamika kuwa ni mtoto wa familia uliokuwa umelelewa nayo.
Alipofika hapo alitulia kidogo na kuanza kumwangalia yule msichana nilieambiwa ni Mama yangu kisha kuendelea.
“Taarifa zile zilimuumiza Mama yako hadi zikapelekea Mama kudhohofika kiafya na kuwa mtu wa mawazo kila wakati, hazikupita siku nyingi Mama yako alihitisha kikao cha familia na kuzungumzia kuhusu maisha yake ya baadae, jambo ambalo aliokuwa nalo ni kuhusu mtoto ambae ni wewe. Kwa kuwa Mama yako alikuwa bado msichana mdogo hakupenda kuwa mwenyewe aliamini hakukuwa na mwanaume angeweza kumuoa angali ana mtoto, jambo ambalo lilikuwa gumu maana wewe ulihitaji matunzo ya Mama yako ili ukuwe katika malezi mazuri, ilitulazimu kukubaliana na Mama yako kwa kile alichokuwa anakihitaji.
Tulikubaliana tukubadili jina la Baba na kukupa la Baba yako mlezi, kila kitu tulifanikiwa kukibadili na wewe ukafahamika kuwa ni mtoto wa familia uliokuwa umelewa nayo”
ENDELEA………
Yale maneno yaliniumiza sana hadi machozi yakaanza kunitoka kwa kile kilichokuwa kinazungumziwa na yule afande.
"Nahisi mmeamua kuyafanya maisha yangu ya maigizo kila mnapojisikia kunidanganya mnajipanga kuja kunidanganya kwa maneno yenye kuonekana ni yakweli angali ni uongo mtupu, mwanzo mliniambia Baba yangu alikuwa mlinzi wa getini leo mnaniambia Baba yangu alipata ajali ya ndege. Hivi kweli mlinzi wa getini toka lini akapanda ndege, au zilikuwa ndege za promosheni"
Niliongea maneno ambayo yalikuwa hayaendani na wale watu waliokuwapo pale lakini sikuwa na jinsi maana kila wakati walikuwa wakiniambia vitu tofauti, nilihisi hata wale waliokuwapo pale hawakuwa ni watu wema kwa upande wangu. Sikuwa na jambo la kuwaamini maana kila mmoja alionekana kuangalia chini baada ya kuuliza lile swali. Kimya kilitawala huku kila niliekuwa namwangalia alikuwa alikuwa akikwepesha macho yake na kuangalia sehemu nyingine.
Nilishindwa kupata jibu kwa kile kilichokuwa kinaendelea hata mdogo wangu alionekana kuwa na aibu kuniangalia usoni, kiukweli nilijihisi kuchanganyikiwa maana wale watu niliokuwa nawaamini walionekana kuto kuzungumza kitu chochote zaidi ya kukaa kimya.
Yule Afande alionakana kuwa mjuaji kuliko wale waliokuwa pale maana kila kitu alikuwa akizungumza yeye.
Nilifikiria vitu vingi kichwani mwangu bila kupata jibu, mapigo ya moyo yalianza kwenda kasi kitu ambacho kilinigharimu kukaa chini kwa muda. Wakati nilipokuwa nakaa chini nilisikia sauti ya kike inaniita, nilinyanyua kichwa changu kuangalia ni nani aliekuwa ananiita. Nilishangaa kukuta ni mdogo wangu ndiye aliekuwa ananiita, kiukweli nilistaajabu maana haikuwa ile sauti niliokuwa naifahamu.
Nilibaki nikiwa namkodolea macho bila kumjibu huku nikiwa najaribu kuifananisha na sauti niliozowea kuisikia, kabla sijapata chakufanya simu ya Mdogo wangu iliita ikabidi kukaa kimya. Mlio wa ile simu pamoja na ile simu vilikuwa vigeni kwenye macho yangu.
Alipokea ile simu na watu wote tukabaki kimya kitu ambacho haikuwa kawaida yake, maongezi nilioyasiki kutoka upande mmoja ambao ni upande wa mdogo wangu yalinifanya nishangae.
Yalikuwa yanahusu Namba za siri za Bank kwenye account ya Baba, nilishindwa kuelewa ninani aliekuwa anongea nae na alikuwa anataka namba hizo kwaajili gani. Nilipomwangalia mdogo wangu alionekana kukwepesa macho yake na kuangalia pembeni, nilianza kupata wasi wasi juu ya wale watu.
Niliwaza huenda walikuwa wamepewa fedha na kuweza kuamia upande wa Baba mkubwa, sikuwa na huakika na hilo maana hakuna mtu niliekuwa namuamini kama mdogo wangu pamoja na Mjomba Denis.
Nilimwangalia Mama pamoja na Baba walivyokuwa kimya.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mama yule meneja amesema umtumie namba za siri maana anadai amesubiri muda mrefu"
Aliongea mdogo wangu baada ya kumaliza kuongea na simu, lile swali kwa mama lilionekana kumfanya aangalie chini huku akiwa kama mtu aliekuwa akivuta kumbukumbu kwaajili ya kitu flani. Vitu vilivyokuwa vinaendelea vilikuwa kama maigizo maana kilakitu kwao kilikuwa kama kigeni.
Niliamua kukaa kimya huku nikiwa namwangalia mama na kutaka kujua alikuwa anatoa jibu gani, kwa upande wa Baba mkubwa yeye alikuwa akibonyeza bonyeza simu yake huku mguu mmoja ukiwa juu ya meza.
"Mwanangu John mbona kama nimeanza kupoteza kumbukumbu maana sizikumbuki zile namba, naomba unikumbushe maana ni muhimu sana"
Aliongea mama na kunifanya nishangae na kuanza kumshanga. Nilimshangaa sana maana hata kama yeye amesahau alitakiwa amuulize Baba maana Baba ndiye mwenye akauti.
"Sasa Mama si ungemuuliza Baba maana yeye niye anaejua hata mimi naona kama nianza kupoteza kumbukumbu"
Niliongea kwa kumtania mama maana kipindi cha nyuma alikuwa anapenda sana utani. Yale maneno yalionekana kumchanganya Mama na kuonekana hakutarajia swali kama lile. Nilibaki nikiwa nasubiri ni jibu gani angelitoa Mama.
Kabla hajajibu Baba Mkubwa aliingilia na kuanza kunitupia lawama na kudai kuwa siwasikilizi wakubwa, yale maneno ya Baba mkubwa yalinifungua akili na kuanza kuona wale waliokuwapo pale walikuwa wananipima akili.
“Hata mimi sikumbuki vizuri ila kuna sehemu niliandika na kuzihifadhi” Nilongea kwa nia ya kupata nafasi ya kutoka pale. Baba mkubwa aliposikia yale maneno aliniangalia n kuanza kutabasamu akiwa anaonekana kuwa na uchu wa kutaka kujua namba hizo. Alininiambia niende nikazilete hapo nilipozificha, nilifurahi sana maana nilijua ile ndiyo jia ya kuwaepuka. Nilipofika chumbani nilituliza akiliyangu na kuelekea upande wa dirishani kuangalia hali halisi ya pale nyumbani.
Nilipochungulia dirishani nilishtuka na kuhisi macho yangu yalikuwa yakiona vibaya, maana hapakuwa ni pale nyumbani kwa siku zote, nilizidi kuchanganyikiwa nakubaki nimesimama palepale dirishani. Wakati nikiwa nazidi kushangaa nilifanikiwa kuona watu wakiwa wamesimama kila kona ya ile nyumba. Nilihisi mwili wangu unakufa ganzi, taratibu nilianza kuhisi mwisho wangu umefika.
Sikujua ni nani alienileta pale ndani lakini kila kitu kilikuwa ni kile kile kasoro mazingira ya nje, nilisogea upande wa kabatini ili kuangalia vitu vyangu. Kiukweli nilishangaa sana maana nilikuta kila kitu change kikiwa kipo kama nilivyokuwa nimekiweka, nilianza kuhisi pengine niliangalia dirishani kimakosa, ikanibidi kurudi na kwenda kuangalia kwa mara nyingine, ilikupata uhakika kwa kile nilichokuwa nimekiona hapo kabla. Nilipochungulia mara yapili hali ilikuwa ni ile ile hapakuwa pamebadilika, palikuwa kama nilivyoona mara ya kwanza.
Nilishindwa kuyaelewa yale mazingira maana nyumba yetu ilikuwa haina uwanja mkubwa kama palivyokuwa pale kwenye ile nyumba. Wakati nikiwa nawaza khusu hali halisi ya pale nyumbani nilisikia sauti ya Baba mkubwa ikiniita. Nilishindwa cha kufanya nikawa nisahau kilichokuwa kimenilete pale ndani, nilianza kutoka taratibu huku nikiwa najua wazi watu wote hawakuwa upande wangu tena bali walikuwa upande wa Baba mkubwa.
Nilijua nia na madhumuni walitaka kunipima akili kama bado nilikuwa nikizikumbuka namba hizo, nilipofika sebleni ndipo akili yangu ikawa sawa na ndipo niliposhtuka kuwa nilifuata nini kule chumbani. Nilijiangalia mkononi sikuwa na kitu chochote nikaamua kutumia akili ya kuzaliwa na kuamua kuwapima akili, kama ambavyo walikuwa wakinipima mimi.
“Kiukweli zile namba ninazikumbuka vizuri lakini sitoweza kuwaambia na mkitaka niwaambie niambieni ukweli juu ya maisha yangu na kuhusu wazazi wangu. Kama mtafanya hivyo nitaweza kuwaambia kila kitu” Niliongea kitu ambacho kiliwashangaza wengi na kubaki midomo wazi, Baba mkubwa alivyosikia hivyo akajifanya yeye ndiye mwenye uchungu na mwanae akaanza kunifuata huku akiwa anajaribu kukamua macho yake ili ikiwezekana macho yaweze kumtoka. Kilichokuwa kinafanyika ilikuwa ni kama utani ndipo nilipoamua kujifanya mjinga ili kupata urahisi wa kujaribu kuwaepuka.
Baada ya kunifikia alinikumbatia huku akiwa anaongea maneno mengi yasiokuwa na maana kamilil, nilijisikia vibaya sana kumshika mtu kama yule.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Pole sana John kwa kupoteza wazazi wako najua inauma ila yakupasa kuvumilia. Lakini kama wewe unapendelea kuendelea kuwa hai na kuishi maisha mazuri, basi usijaribu kutao taarifa hii kwa polisi au kujifanya mjuaji, maana kabla ya mimi kwenda Jela wewe utatangulia kuzimu”
Nilikumbuka maneno ya vitisho siku ambayo Wazazi wangu walipoteza maisha, lakini chakushangaza bado walikuwa hai. Taratibu nilianza kuona Baba mkubwa pengine hakuwa mtu mbaya lakini swali likuwa “Nikwa nini waliamua kunifanyia vile?” Nilijiuliza mwenyewe wakati nikiwa nimemkumbatia Baba mkubwa. Nilijihisi mwenye makosa maana yamkini nilikuwa nimemuhisi vibaya na kumuona muuaji, nilishindwa kuvumilia maana nili muhukumu kwa kosa asilo lijua maana wale watu waliokuwa wameuwawa walikuwa mbele yangu.
Japo sikuwa najua kwa wale nilikuwa nikiwashuhudia ila kwa uwepo wa wale niliamini yote hayakuwa kweli.
“Baba naomba uniambie ni kwanini mliamua kufanya vile hadi nikapelekea kukuchukia na kukuona muuwaji kitu ambacho hakikuwa kweli” Nilimuuli Baba mkubwa na ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuita Baba, hata yeye alionekana kushangaa maana hakuna hata siku moja nilikubali au kumsikiliza zaidi ya siku ile. Nilipogeuka kwangalia wakina mjomba na watu wengine nilishindwa kuwaelewa maana waliponiona nimegeuka walipeleka macho yao china ambapo hakuwapo na kitu cha muhimu cha kutizama. Nilizidi kupata maswali mengi na kutaka kujua nini kilikuwa kimetokea hadi wale watu kuwa kwenye hali kama ile.
“John mwanangu cha muhimu kwanza ni hizo namba najua unataka kujua vitu vingi na leo naona ndiyo itakuwa suluhisho la matatizo yako yaliokuwa yanakusumbua, kabla sijakuambia chochote ungefanya kile alichokuwa anakitaka mama yako, ili tuendelee kukupa ukweli juu ya maisha yako pamoja na wazazi wako. Ninajua utafurahi kuishi na wazazi wako maana ni kipindi kirefu mlikuwa hamjaonana”
Aliongea Baba huku akiwa anarejea mahali alipokuwa meketi awali, sikutaka kuwa mkaidi niliamua kumtajia zile namba maana nilikuwa nazikumbuka vizuri maana ilikuwa ni mwaka wangu wa kuzaliwa ukifuatiwa na mwaka wa mdogo wangu Sophia. Baada ya kutaja zile namba nilibaki nikiwa nasubiri kupata kujua ukweli kuhusu maisha yangu pamoja na wazazi wangu, kimya kilitawala kwa muda kitu ambacho kilinishangaza maana kila mtu alikuwa akinitumbulia macho, mara ghafla simu ya Baba Mkubwa iliita alipoipokea aliweka laudspika na kuiweka mezani.
“Mkuu imekubali” Nilishindwa kuelewa yale maneno yalikuwa yanamaanisha nini..
Nilibaki nikiwa nashangaa maana baada ya ile simu kukatika kila mtu alibaki akiwa ananiangalia kwa jicho la hasira, nilishindwa kuwaelewa na kufahamu walikuwa wanamaanisha nini kuniangalia kwa staili ile. Baba mkubwa alinyanyuka na kuniangalia kisha akatoa msunyo mkali.
"Pumbavu sana ulifikiri sitoweza kujua namba hizo, nilikwambia toka zamani ukajiona wewe unaakili kuliko mimi. Kingine si ulikuwa unataka kujua historia ya maisha yako, basi usijali maana utaijua na muda wenyewe ndiyo huu, tena watakao kupa historia yako ni wazazi wako ambao kwa sasa wapo kuzimu"
Yale maneno ya Baba mkubwa yalikuwa kama utani, kwajinsi aluvyokuwa akizungumza. Lakini nilishindwa kuelewa alikuwa anamaanisha nini kusema wazazi wangu walikuwa kuzimu, wakati wazazi wangu walikuwa pale mmoja wapo akiwa ni yeye.
"Mbona unanitimbulia macho kanakwamba unifahamu, au kuna kitu kimebadilika kwangu. Najua ulikuwa hujui na hautajua maana unaenda kufa na ndiyo njia rahisi kukutana na wazazi wako ambao wao ndiyo wanaojua historia yako vizuri"
Yale maneno yalianza kunipa wasiwasi maana alikuwa akiongea kwa kumaanisha. "Baba acha utani mimi nipo siriazi, natamani kujua history ya maisha yangu" "Baba?, Baba yako nani hapa kuna Baba yako hapa?"
Nilibaki nikiwa namshangaa Baba mkubwa kwa jinsi alivyokuwa amebadilika, niliamua kuchukulia utani na kuhisi yeye ni mtu wa utani.
"Ila kabla hujafa nakuomba ukifika kule waambie wazazi wako kwamba. Kile walichokuwa wamekificha kwa muda mrefu kwa sasa nimefanikiwa kukipata, na uwaambie ndugu zake wengine watafuata punde wewe utakapo wafikia"
Nilibaki nikwa namtizama huku nikicheka kwa jinsi alivyokuwa anazungumza kanakwamba ilikuwa kweli. Nilianza kuona maisha yangu yameanza kurudi kama kipindi tulipokuwa pamoja na wazazi wangu ambao walikuwa wazazi walezi. Kitu ambacho kilikuwa kinanishangaza ni jinsi walipokuwa wakiniangalia kwa kunikazia macho, kitu ambacho si kawaida.
"Kijana bajisikia furaha sana kupata kile nilichokuwa nakitafuta zaidi ya miaka sita. Nimetumia gharama nyingi kiasi kwamba nilihisi kupatwa na kichaa, ila kwa sasa najua kila kitu kitaenda kama nilivyokipanga. Kama ulikuwa hujui kwa sasa nataka niweze kuwa mtu mmoja mwenyeckuogopwa na kuheshimika kama mfalme, hakuna kitu kinachompa mtu heshima zaidi ya fedha. Vijana embu fanyeni kazi niliowapa na hakikisheni mnammaliza kabisa, maana mimi siwezi kuona damu chafu ikiwa inatapakaa mbele yangu. Mkimaliza muhakikishe hakuna hata chembe ya kiungo kinabakia au kuonekana"
Yale maneno yalianza kunipa wasiwasi na hofu na kuanza kuona kama yanaukweli ndani yake, alipomaliza kuongea alinitizama kwa jicho la hasira na kunipungia mkono kwa idhara ya kuniaga. Nilishikwa na mshangao kwa kile nilichokuwa nakiona na kukisikia, sikuweza kuamini lile jambo. Baba mkubwa alipotoka nje akiwa ameambatana na yule Afande mjomba pamoja na watu wengine walisimama huku wakiniangalia kwa macho makali. "Nimeamini mbio za sakafuni huishia ukingoni na ndege mjanja hugia kwenye kiota kibovu, umekimbia kote umekuja kufa kizembe"
Yalikuwa ni maneno ya mjomba Denis ambae alikuwa ndiye mtu niliekuwa namuamini kupita maelezo, niliposikia yale maneno nilijua moja kwa moja walikuwa wananitania maana mjomba Denis hawezi kunifanyia jambo baya. "Mjomba mbona leo mn....."
Kabla sijamaliza kuzungumza nilishtukia napigwa ngumi ya tumbo hadi nikaanguka chini, nilishangaa sana kuona mjomba ananifanyia kitu kama kile. Sikuamini kama ipo siku mjomba angekuja kunifanyia kitu kama kile. Nilibaki nikiwa namuangalia mjomba kwa jinsi alivyo badilika hukuvnikiwa naugulia maunivu makali kwenye tumbo langu kutokana na ile ngumi niliopigwa.
Nilihisi kama ndoto lakini maumivu yale yalinijulisha kuwa haikuwa ndoto, nikiwa nazidi kujiuliza nini kimempata Mjomba hadi kuwa katika hali ile nilishtukia naongezwa teke la kifua kitu ambacho kilinifanya nihisi maumivu makali kiasi cha kushindwa kuvuta pumzi vizuri. Kiukweli nilishindwa kuelewa nini nilichokuwa nimekifanya hadi kupata adhabu kama ile, nilihisi Mjomba amechanganyikiwa kwa kile alichokuwa anakifanya, nilipo muangalia mdogo wangu naye alionekana kuwa na hasira juu yangu. Nilikuwa kama mtu aliechanganyikiwa, maana waliende kunipiga mateke, ngumi na makofi, damu zilizidi kunitoka.
"Subiri, subiri, subirini naombeni mtoe hizo sura mbaki na sura zenu za kawaida"
Yalikuwa ni maneno ya Mjomba Denis ambae yeye ndiye alikuwa ndiye muongozaji wa kunipiga. Baada ya kuongea vile watu wote waliokuwa pale walipeleka mikono yao kwenye nyuso zao, haikupita hata dakika moja nilishangaa kila mtu anabandua ngozi yake na kubaki na sura nyingine, nilishangaa sana maana walikuwa ni watu ambao sikuwahi kuwaona hapo kabla. Nilibaki nikiwa naduwaa nisijue chakufanya.
Nilizidi kuchanganyikiwa kwa kile nilichokuwa nakiona, nilihisi kama ilikuwa ni filamu au maigizo kwa kile nilichokuwa nakiona mbele yangu. Kitu ambacho kiliniogopesha na kunifanya nianze kuwa na hofu ni pale nilipomuona mmoja wa watu ambao walikuwa ni watu wa Baba mkubwa. Nilishindwa kuyazuia macho yangu na kuhisi yalikuwa yakiona vibaya.
"Yukowapi huyo Mjomba yako ambae ulikuwa ukimtaja taja hapa embu tazama vizuri kama kuna ndugu yako maeneo haya. Hivi unafikiri maisha yanaenda kama unavyotaka wewe, embu jiangalie wewe unaweza kumiliki fedha nyingi kiasi kile, Mabilioni ya fedha yasiyo hesabika uje utumoe mpumbavu kama wewe"
Aliongea mmoja kati ya wale watu waliokuwapo pale huku akiwa ananipiga makofi. Nilijua ule ndiyo ulikuwa mwisho wangu, maana wale watu hawakuwa na hata chembe ya roho ya kibinadamu. Nilipigwa huku wakiniamuru nisimame na kukaa, maumivu niliokuwa nayasikia hayakuwa yakawaida, kila kona ya mwili wangu nilihisi maumivu.
Nguo zangu zililowa kwa damu, pale chini palekuwa pametapakaa damu nyingi. Pumnzi ilikuwa ilikuwa ngumu kuingia kwenye pua zangu maana zilijaa damu nyingi, mdimoni damuzilikuwa nyingi huku zikiambatana na meno kadhaa ya kutoka kinywani kwangu. Hata nafasi ya kuzungumza chochote sikupata, kipigo kiliendelea huku safari hii hali ikiwa imebadilika na sikuwa na uwezo wa kusogeza au kunyanyua mguu wala mkono, mwili wangu ulikuwa umekufa ganzi.
Nilihisi ule ndiyo ulikuwa mwisho wangu, niliahindwa kuelewa kwanini Baba mkubwa alinipa adhabu kama ile ya kupigwa kiasi kile. Macho yalikosa uwezo wa kutazama, nguvu nazo ziliniisha, kiza kikaanza kutawala macho yangu sikujua nini kiliendelea..
Nilipokuja kushituka nilijikuta nipo mahali ambapo sikuweza kupatambua kwa haraka maana kiza kilikuwa kikubwa, nilitamani kunyanyuka lakini mwili wangu ulikuwa na maumivu, maumivu yalikuwa makali kiasi kwamba nilihisi baadhi ya viungo vyangu vilikuwa havifanyi kazi.
Nilijiuliza maswali mengi na kuhusu pale nilipokuwa, nilijaribu kuvuta kumbukumbu ya vitu vilivyotokea hapo kabla lakini sikufanikiwa kukumbuka chochote, nilijaribu kujikaza kunyanyuka lakini hali yangu haikuwa nzuri, niligeuza macho kila pande kungalia kama kulikuwa na mtu maeneo yale.
Nilishindwa kuelewa yale maumivu yalikuwa yamesababishwa na nini, kiukweli sikuwa nakumbuka chochote kilichotokea hapo kabla, mwili mzima ulikuwa una maumivu nilibaki njia panda huku nikizidi kupata maswali mengi katika akili yangu, juu ya yale maumivu.
Nikiwa nimetulia nikiwa sijui cha kufanya nilisikia sauti za viatu, nilitega masikio kupata kujua alikuwa ni nani, yule mtu alipoingia alikuwa kama anaongea na simu baada ya kumaliza kuongea na simu nikaamua kumuita. Nilipomuita na kusikia sauti yangu alishtuka sana, hadi simu yake ikawa imeanguka chini, nilishangaa sana, niliamua kuita kwa mara nyingine maana mara ya kwanza hakufanikiwa kuitika.
Safari hii aliitika na kusogea karibu yangu na kuonekana kushangaa, nilishindwa kuelewa nini kilichokuwa kinamshangaza na kumshtua.
"John umepona, siamini kama umeiona Dunia tena.Ama kweli muache Mungu aitwe mungu"
Aliongea yule mtu na kunifanya nisiyaelewe maneno yake, nilibaki kimya maana sikuwa nafahamu nini kilichokuwa kinaendelea, nilishindwa kumtambua yule mtu maana kiza kilikuwa kingi, sauti ya yule mtu ilionekana kuwa ni kijana, japo sikuwa na huakika.
"John ndugu yangu naomba unisamehe maana sikuwa nauwezo wa kuzuia wewe usipigwe kiasi kile, ila namshukuru Mungu wewe ni mzima. Ila nina taarifa mbaya lakini sitaweza kukuambia saa hivi mpaka pale utakapo pona kabisa"
Aliongea yule kijana ambae sikujua ni nani, nilibaki kimya nikiwa najaribu kukumbuka nini kilitokea mpaka mimi kuwa kwenye hali ile niliokuwa nayo.
''Kaka samahani kwani wewe ni nani?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliuliza baada ya yule kijana kuongea yale maneno, alichokifanya yule kijana aliwasha taa ya kwenye simu na kujimulika na kuniambia nimwangalie. Nilishindwa kuelewa alikuwa anamanisha nini kusema kitu kma kile, Nilipomwangalia nilihisi kumbukumbu kurudi japo sikujua yule kijana ni nani.
Nilipomwangalia vizuri niliweza kumtambua ila sikuweza kujua nilishawahi kumuona wapi, nilimwangalia huku nikiwa najaribu kukumbuka nilimuona wapi ule kijana lakini sikuweza kukumbuka.
"kaka samahani, sijui unaweza kunikumbusha ni wapi nilipokuona au tulipokutana maana kama nakumbuka nimewahi kukuona lakini sikumbuki ni wapi nilipokuona"
Niliuliza baada ya kutofahamu mahali tulipokutana na kijana huyo.
Yule kijana alionesha kusikitika kwa kile nilichokizungumza na kuonesha huzuni, niliendelea kumwangalia yule kijana bila kupata jibu na ndipo yule kijana aliponiambia kila kitu mpaka mimi kuwa kwenye hali kama ile. Kiukweli nilipokumbuka kile kipigo nilishindwa kuelewa kwanini sikuweza kufa, nilimwangalia yule kijana kwa mara ya pili na ndipo nilipopata uhakika kama yule alikuwa ni moja ya watu wa Baba mkubwa na alioshiriki kunipiga mpaka nikawa kwenye hali ile.
Nilipatwa na hasira nilitamani kumrukia lakini uwezo huo sikuwa nao.
"John naomba unisamehe ndugu yangu, najua unaumia sana na mimi sikuwa mwema kwako ila nakuomba punguza hasira. Pole sana na hata hivyo sikupenda kukufanyia hivyo bali nililazimisha na kuambiwa familia yangu ingeweza kuteketea kama ilivyoteketea familia yako"
Aliongea yule kijana ambae aliniambia jina lakeni Joram na kunifanya nishtuke.
"Familia. Familia yangu imepatwa na nini, Usije ukaniambia familia yangu imepatwa na matatizo kama yalionikuta mimi"
Niliongea huku najaribu kujivuta ili niweze kukaa, yule kijana aliweza kunisaidia nikawa nimeweza kukaa na kuuliza tena yule kijana juu ya familia yangu.
Yule kijana aliniangalia na kuanza kutokwa na machozi, nilibaki nikiwa najiuliza nini kilichokuwa kinamliza yule kijana.
"John najua upo kwenye wakati mgumu ila nitakacho kwambia naomba unisamehee maana sikuwa na uwezo wa kuzuia yote yasitokee"
Alionge kijana Joram na kunifanya nihisi kitu kibaya kimeikuta familia yangu, haswa haswa mdogo wangu pamoja na Mjomba, watu ambao ni muhimu sana katika maisha yangu, nilimwangalia yule kijana huku nikiwa namuomba Mungu familia yangu iwe salama. Joram aliniangalia na kutingisha kichwa chake na kuanza kuongea.
ENDELEA...........
"Nashindwa hata nianzie wapi, ila ni lazima ujue ukweli kuhusu familia yako" Alaongea kijana Joram huku machozi yakimtoka, kitu ambacho kilizidi kunipa wasiwasi na hofu. Joram alishindwa kuendelea kuongea kutikana kwikwi ya kilio, nijua huenda familia yangu haikuwa salama.
"Kiukweli Mdogo wako pamoja na Mjomba wako, hatupo nao tena"
Aliongea Joram na kunifanya mwili wangu kusisimka kwa yale maneno ya Joram, nilihisi nimesikia vibaya na kumuliza kwa mara nyingine, lakini ukweli ulibaki pale pale.
Sikuweza kuamini yale maneno, niliamini ndugu zangu wapo wazima nilihisi alikuwa ananiongopea. Siku ile nilihisi Dunia imenilemea, hali yahewa nilihisi kubadilika na kuwa joto angali hapo awali kulikuwa baridi. Nilijihisi kutokuwa na thamani katika hii Dunia, watu ambao walikuwa ni wamuhimu kwangu na ndiyo ndugu waliobakia nao hapa Duniani. Sikutaka kuamini kuwa hawakuwa tena Dunia, nilibaki nikiwa natokwa na machozi huku kila nilipojaribu kujisogeza nilihisi maumivu makali yasiyo elezeka.
"Najua inauma sana ila nakuomba ujaribu kujizuiya ili kupunguza maumivu uliokuwa nayo, maana unavyozidi kulia ndivyo maumivu nayo yanavyozidi kuongezeka"
"Kaka Joram nakuomba kama kweli Ndugu zangu wamepoteza misha, nakuomba ukanionyeshe angalau makaburi yao ili niweze kuamini maneno yako. Nakuomba sana tena sana"
Nilibaki nikiwa nalia hukunikiwa najaribu kumtaka kaka Joram anipeleke kwenye kaburi la Mjomba pamoja na Mdogo wangu. Kaka Joram alibaki akiniangalia kwa huzuni huku akitingisha kichwa chake, kuonekana kusikitika.
"John ndugu yangu sijui nikuambie vipi ili unielewe, ila cha muhimu ni wewe kuwa salama maana hata hapa tulipo si...."
Kabla hajaendelea simu yake iliita, aliiangalia kwa muda na ndipo akaamua kuipokea na kunyanyuka pale alipokuwa amekaa na kusogea kando, nilibaki nikijiuliza maswali huku kichwa changu kikitawaliwa na mawazo. Pale nilipokuwa nimekaa sikuwa nafahamu ni wapi maana kulionekana kuwa na kimya na penye giza nene.
Kaka Joram alipomaliza kuongea na simu alirejea na kukaa pale aliko kuwa mwanzo, huku akionekana kuwa na mawazo mengi.
"Kaka samahani kwani hapa ni wapi?"
Nilijikuta nauliza swali lile bila kutarajia, kiukweli hali ya pale na ukimya ulinifanya kumuuliza Kaka Joram juu ya mahali pale, maana kiza kilikuwa kikubwa ikwa ngumu kutambua mahali pale.
""Kuna kitu ambacho sikukuambia hapo awali, kiukweli hapa tulipo siyo kwetu"
Nilishindwa kumuelewa kaka Joram kwa yale maneno aliyokuwa akiyazungumza.
"Siyo kwetu kivipi kaka maana umeniacha njia panda?"
Niliuliza nikiwa natamani kujua alikuwa anamaanisha nini kwa kusema pale tulipokuwa si kwetu.
"Nikweli kabisa hapa tulipo siyo kwetu"
Nilisikia sauti nyingine ikiitikia na kunijibu nilichokuwa nimekiuliza, nilishangaa sana na ndipo nilipogundua kuwa kaka Joram hakuwa mwenyewe.
Niliguka upande ule sauti ilipokuwa inatokea ili kutaka kujua ni nani aliekuwa akizungumza, ila kutokana na kiza kuwa kikubwa nikashindwa kuona chochote.
"Kwanza napenda kuku omba radhi kwa yote yaliotokea kuhusu wewe pamoja na familia yako. Nina kila sababu ya kukuomba msamaha maana kwa kiasi kikubwa tumeshiriki kuiteketeza familia yako, ila unatakiwa ukumbuke hata sisi hatukupenda kufanya vitu kama vile. Nimambo mengi yameweza kutokea katika maisha yetu ila kwa sasa naweza kusema mwanzo wa kisasi umeanza na ningependa utusamehe na tuwe pamoja maaana najua hata wewe unauchungu kama tulionao sisi"
Alongea yule mtu na kunifanya nishangae sikuweza kumtambua yule mtu zaidi ya kuona kimvuli kutokana na mwanga wa simu kumulika, yule mtu alionekana kupiga magoti huku kukionekana kuwapo na watu wengine pembeni yaki wapatao kama wane. Nilitamani kuwatambua lakini kiza kilikuwa kizuizi.
Nilijiuliza maswali mengi huku nikimwangalia Kaka Joram ambae alionekana kuinamisha kichwa chake huku akionekana mwenye mawazo mengi.
"Nikweli hayasemayo na hata hapa tusipo si nchini kwetu, hapa tulipo tupo nchini kenya, ni hitoria ndefu ya sisi kuwa hapa pamoja na wewe"
Aliitikia kijana mwingine na kunisisitizia pale tulipokuwamo hapakuwa nchini kwetu. Nilibaki nimeduwaa na kushindwa kuuliza chochote.
Yale maneno yalinifanya nishangae, nilishindwa kukubaliana na maneno ya wale watu.
"Mnamaanisha nini kusema hapa ni Kenya na si Tanzania, embu nielewesheni vizuri na tumefika fikaje hapa?"
Nilishndwa hata kuongea kigugumizi kilinishika nikabaki nikiuliza maswali.
"Wakati ulipokuwa unaugulia maumivu ya kupigwa, kiukweli naweza kusema Mungu anamakusudi na wewe. Kwa kipigo utichokipata hakuna mtu alieamini kama leo hii ungalikuwa ukichangia hewa na viumbe wengine, kila mtu aliamini wewe ulikwisha kuwa marehemu"
Aliongea kijana huyo huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini huku akiahindwa kuendelea kutokana na kwikwi ya kilio. Kaka Joram aliliona hilo na yeye alionekekana kutokwa na machozi na kwa na sura ya huzuni.
"Wakati ulipokuwa unapigwa siku ile Baba Mkubwa ako alikuja na kukuangalia kama tumesha maliza kazi aliotupa, baada ya kukuangalia na kuridhika na kipigo tulichokupatia aliamuru tukuchukue na kwenda kukutupa kwenye mapori makubwa ya wanyama wakali ili upate kuliwa na wanyama wakali kuondoa ushahidi" Yalikuwa ni maneno ya Kaka Joram, aliongea na kukaa kimya kwa muda na kuendelea.
"Tulikuchukua kama ilivyotolewa amri na kuanza safari ya kwenda kukutupa, tukiwa njiani tulilipata wazo la kukusaidia ni baada ya kukusikia ukikohowa. Tulikubaliana kwa pamoja maana sisi sote tulikuwa ni kitu kimoja na tulilelewa kwa pamoja, katika kituo cha yatima alichokuwa anakimiliki Baba mkubwa ako" Nilishangaa sana kusikia maneno kama yale na kuanza kujiuliza maswali na kuanza kuona wale wote ni yatima. Nilishangaa sana maana nilipokuwa nakutana nao kwa Baba mkubwa walionekana nadhifu, watu wenye heshima zao. Kila mara walikuwa wamevalia suti za gharama na za heshima, walionekana mfano wa maafsa.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Derrick ndiye mtu alietulea mpaka kufikia hii leo, katika kutulea kwetu ndiyo nyenzo aliotumia kama kati ya sisi kufanya kile alichokuwa anakitaka. Bila kufikiria na sisi tulikikuta tunaingia katika ulimwengu wa wauwaji, naweza kusema siku ni kifa sijui nitajibu nini mbele ya watu niowaondoa bila hiyari yao"
Kaka Joram aliendelea kuongea huku akilia kama mtoto mdogo na kuonekana kuwa na machungu mengi. Nilishindwa kuvumilia nami machozi yalianza kunitiririka, nilikumbuka jinsi tulivyoishi maisha mazuri na familia yangu, lakini hawakuwamo tena nilitamani nifanye kitu juu ya Baba mkubwa lakini uwezo huo sikuwa nao.
Sikuwa na uwezo hata wa kunyanyuka nilihisi pengine siku zinapozidi kwenda nisingali tembea tena, maana kila kona ya mwili wangu ilionekana kuwa tifauti na Mungu alivyo niweka. "Tulikubaliana tukusaidie kimya kimya bila Derrick kufahamu na tulipanga kumdanganya kuwa wewe tulikwisha kutupa kwenye moja ya mapori ya wanyama wakali. Tulufanikiwa kwa hilo, tulikuchukua na kukupeleka hospital ya siri na huko ulianza kupata matibabu.ajibu ya Dokta yalituchanganya na kuhisi muda wowote ungalipoteza maisha. Kwa kudra ya mwenyezi Mungu mapigo ya moyo yalionekana kudunda na kuwa sawa, lakini wakati wewe unapata matibbu huku matumaini ya kupona yakiwa yameanza kujionyesha tulishangaa hospitali uliokuwa umelazwa imevamiwa na watu wasiojilikana"
Alikuwa ni yule kijana alienijibu swali nililokuwa nimemuuliza Kaka Joram. Nilibaki nikiwa nimeachama mdomo wangu huku nikiwa nasikiliza kwa makini kile nilichokuwa nasimuliwa na wale vijana. "Naweza kusema siku ile ilikuwa ya miujiza maana walisachi kila chumba lakini chumba ulichokuwa wewe hakikuguswa hata kitasa chake, tulipoona hali kama ile ndipo tulipogundua mmoja wetu alikuwa ametugeuja na tayari taarifa za kuwa wewe upo hai zilikuwa zimefikishwa kwa Baba mkubwa ako. Mzee Derrick ambae ni baba yako mkubwa alituma watu kwajili ya kuondoa maisha yako pamoja na wewe, tarifa hizo tulipozipata tuliamua kutafuta utaratibu wa kumuepuka mtu yule, tuliamua kukimbilia Zanzibar ambapo tuliamini asingalijua, lakini yote yalikuwa sawa na bure maana huko ndipo tulipojikuta tumeingia mikononi mwa Mtu tuliekuwa tukimuepuka.
Yale maneno yalinipa wakati mgumu kusikiliza maana dhidi nilivyokuwa nasikiliza ndivyo machozi yalivyokuwa yakinitoaka kwa wingi huku yakiambatana na makamsi, nilipokuwa nakumbuka kipigo nilichokipata kutoka kwa Baba mkubwa nilishindwa kuvumilia nilibaki nikilia na maumivu kuongezeka mara dufu. Ilifika wakati nilitamani kifo kuliko kuishi maisha ya kuteseka kama yale, niliapa na kuahidi endapo siku moja nikawa mzima basi nilazima ningeweza kulipiza kisasi kwa yote alionifanyia Baba mkubwa. Niliahidi huku nikiwa nahisemea kimoyoni "Atalipa kwa gharama yoyote" Ni maneno yaliokuwa yakisikika kutoka kwenye fahamu za bongo zangu.
"Tulivyo fika zanzibar tulijikuta tunaingia mikononi mwa Derrick kilaini, Derrick ni mtu mwenye dharau na roho mbaya. Nakumbuka siku hiyo alitoa bunduki yake na kumkabidhi yule mwenzetu aweze kutumaliza, lile jambo lilikuwa la kushangaza lakini ndiyo lilikuwa limetokea kwa wakati huo. Yule mwenzetu japo alitusaliti ila bado alikuwa na moyo wa kibinadamu,alishindwa kufanya kama alivyoambiwa na kubaki amesimama mbele yetu bila kuonyesha kitu chochote. Derrick alisimama na kumwangalia misha akamyang'anya ile bastola na kumpiga ya kicha na pale pale alipoteza maisha"
Nibaki nikiwa nasikiliza huku ikionekana kama movie lakini haikuwa movie, kwa mtu asiye tambua haya ukimwambia vitu kama hivi anaweza kukuambia haya huonekana kwenye movie na si kwa maisha halisi. Walichokuwa wakizungumza kilinifanya nitamani kujua nimefika fikaje pale, nilikuwa kama mtu aliechanganyikiwa.
"Lili kuwa ni jambo la kushangaza sana, tulijua kama yule alifichua siri ya sisi kumsaliti ameuwawa mbele yetu, tulijua ule ndiyo mwisho wetu. Tulibaki na vigugumizi huku tukiwa tunatamani kuomba msamaha lakini tulipo kumbuka kauli ya Derrick yakuwa mtu atakaye tamka neno la msamaha mbele yake basi alikuwa ameomba kifo na si msamaha, nibaadhi ya sheria zake alizo jiwekea. Tukiwa pale huku wewe ukiwa chini kama mtu aliepoteza maisha, alisogea Baba yako mkubwa mahali ulipokuwamo na kukugusa na kiatu kwa kukukanyaga, huku akitamka baadhi ya matusi. Alikuangalia kwa muda na kumuita mtu wake mmoja na kumwambia kitu, hatukuweza kusikia kitu chochote zaidi ya kimya kutwala.
Baada ya dakika kadhaa tulishangaa wanaletwa mbwa watatu wakubwa, wale mbwa tuliwatambua vizuri maana kipindi cha nyuma sisi ndio tuliokuwa tunawapatia chakula. Chakula chao kikubwa ilikuwa ni watu, watu ambao walikuwa wanaenda kinyume na Derrick waliuwawa kinyama kwa kuliwa na mbwa hao. Tulishtuka sana tulipowaona wale mbwa, tulijua muda wa sisi kuwa chakula cha mbwa hao umefika. Tulibaki tukimuomba Mungu kimoyo moyo, ikiwa ndiyo mara yetu ya kwanza tukimkumbuka Mungu toka tulipoingia mikononi mwa Derrick"
Aliongea Kaka Joram na kumeza fundo la mate na kuendelea kuongea.
"Wale mbwa waliamuriwa kutushambulia, hatukuweza kuamini maana wale mbwa waliachiwa na kuturukia na kuanza kututafuna. Nilivyoona wale mbwa wameanza kutushambulia nilikurukia na kukaa juu yako na ili wasiweze kukudhuru zaidi, lakini wakati wale mbwa wakiwa wanazidi kutyshambulia tulisikia sauti kama ya Baruti, haikuwa sauti ya baruti, ilikuwa ni sauti ya bunduki maana tuliifahamu vizuri kutokana na kuizoea na kuitumia.
Sauti ile ilivyosikika tulishangaa wale mbwa wote watatu wanaenda chini huku wakiwa wanavuja damu. Ulijinyanyua na kuangaza ili kujua ni nani aliekuwa amefanya vile, tuliponyanyuka tulikuta ni Mjomba yako akiwa na mdogo wakiwa wameambatana na watu watatu wakiwa wameshikilia bunduki mikononi mwao. Derrick alivyoona vile hata hakushtuka bali alikasirika kwa kitendo cha kuuliwa kwa mbwa wake, Mjomba yako pamoja na mdogo wako walijikuta wazubaishwa na Derrick na kujikuta wanataitiwa na kunyang'anywa silaha zao, likini kumbe hawakuwa wenyewe walikuja na baadhi ya watu na ndipo ilipoamka vurugu ya kubwa.
Tulipoona vurugu ya silaha za moto imezidi tuliamua kutafuta njia ya kuondoka maeneo yale na ndipo tulipokutana na msamaria mwema akatusaidia kutupeleka hospitali maana majeraha tulioyapata yalikuwa makubwa. Baada ya kupata matibabu huku hali yako ikiwa mbaya tuliweza kukutana na rafiki yetu ambae anaishi kenya na yeye ndiye alietuleta hapa tulipo sasa" Alimaliza huku akionekana kuloa kwa machozi, kilio kilitawala kila mtu alionekana kuwa na machungu mengi, kwa mimi binafsi sikutamani hata kuishi, nilijiona sina thamani maana nilihisi kama sikuwa na ndugu sikuona thamani ya kuendelea kuishi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimwangalia Kaka Joram alivyokuwa akitokwa na machozi, huzuni ilitawala, kila mmoja wetu alionekana kuwa na hasira juu ya Baba mkubwa Derrick. Tulikaa pale bila kuongea chochote hadi nikawa nimepitiwa na usingizi, asubuhi na mapema mimi nilikuwa macho nilijigeuza upande wa pili kuangalia walipokuwa wale watu pamoja na Kaka Joram. Nilipogeuka sikufanikiwa kumuona mtu yeyote, nilipojaribu kunyanyuka nilishindwa.
Kiukweli hali yangu haikiwa nzuri, mwili wangu ulitawaliwa na maumivu makali. Sikuwa na uwezo wa kujinyanyua, nilihisi pengine baadhi ya viungo vyangu havikuwa vikifanya kazi.
Nilikaa muda mrefu bila kuona mtu yoyote, niliamua kujaribu kuita kwa jina ambalo nililikariri la Kaka Joram. Niliita kwa muda mrefu bila kujibiwa, nijaribu mara kadha wa kadha lakini sikupata jibu lolote, uwezo wa kufanya jambo lolote sikuwa nalo.
"John umeamka?"
_Nilisikia sauti ya Kaka Joram ikisikika, nilikaa kimya nikiwa naaubiri aweze kuingia ili niweze kumjibu.
"Nimeaka kaka, vipi wewe?"
Nilimjibu baada ya kuingia, pale nilipokuwa nimelala.
"John kama unavyoona hali yako ilovyo, tumejaribu kutafuta jinsi ya kukusaidia, hapa ninavyoongea nimeweza kupata Dokta ambae ataweza kukusaidia hadi utakapo pona"
Aliongea kaka Joram huku akiwa ananinyanyua pale nilipokuwa nimelala, niliponyanyuka nilianza kuelekea nje huku nikisaidiwa na kaka Joram. Nilipofika nje nilishangaa sana yale mazingira, nilipogeuka kutazama nilipotokea nilishangaa sana, palikuwa ni kontena la magari makubwa.
Lilionekana kuchoka sana, nyumba nilizoziona zilionekana kwa za muda mrefu. Safati ya kuelekea kunako matibabu ilianza, nilitembea umbali mrefu huku wakati mwingine Kaka Joram alikuwa akinibeba. Tulitembea kwa muda mrefu kutokana na mimi kuwa mgonjwa, tulifika sehemu ambayo tulikutana na magari na piki piki, huku pembeni ya barabara kukiwa kumezungukwa na ghorofa zikizo enda juu. Mazingira yale yalipendeza hayakuwa na tofauti kubwa sana na jiji la Dar es salaam.
Kiukweli nilikuwa nilikuwa nimechoka kupita maelezo, mwili mzima nilihisi kuwaka moto, hali yangu ilianza kubadilika na kuanza kuhisi baridi kali mwilini mwangu. Kile kitendo kikamlazimu Kaka Joram kunibeba, kwa jinsi alivyoonekana kaka Joram hakuwa na fedha za kulipia usafiri. Hatukuchukua muda mrefu tukawa tumefika katika hiyo hospital, niliingizwa hadi ndani na kupelekwa moja kwa moja kwenye chumba cha wagonjwa wenye kuhitaji huduma za haraka.
Haliyangu ilionekana kuwa mbaya hadi yule Dokta tuliemkuta alishtuka, kwa wakati huo sikuwa na uwezo wa kutambua kilichokuwa kinaendelea, yule dokta aliamua kunichoma sindano ya usingizi. Nilipokuja kuzinduka nilijikuta nipo kwenye chumba chenye hewa safi, nikinyanyuka na kukaa kitandani ambapo ndiko nilipokuwa nimelala, nilishangaa sana maana nilivyo keti kitandani sikuhisi maumivu yoyote. Nilijiangalia baadhi ya sehemu nilizokuwa nimeumia, sikufanikiwa kuona kidonda cha aina yoyote zaidi ya makovu, nilijinyanyua kitandani maana sikuwa naamini kama ningaliweza kupona.
Wakati nikiwa naendelea kujishangaa ndipo Dokta naye aliweza kuingia, alinikuta bado nipo kwenye mshangao mkubwa, yule Dokta alivyoingia alionekana kuwaza jambo katika akili yake, nilimwangalia huku naye akiniangalia na kuangalia karatasi alilokuwa amelishikilia. Nilimsogelea na kumshukuru kwa wema aliokuwa amenitendea, nilijisikia furaha sana kurudi katika hali yangu ya mwanzo, lakini yule Dokta hakunijibu kitu zaidi ya kuendelea kunitizama usoni.
Nilishindwa kuelewa alichokuwa akikiangalia kwenye uso wangu, tukiwa pale wakina kaka joram na watu wengine waliingia na kunikuta nimepiga magoti nikiwa namshukuru Dokta huyo kwa msaada wake.
Walivyofika walikaa kitandani na wengine waliendelea kusimama maana walikuwa wengi. Walinipatia gazeti ambo huwa linatoa taarifa mbalimbali, nililichukua na bila kusita na kuanza kulisoma, nilipolisoma nilishangaa sana.
"Mfanya biashara maarufu hapa nchini ali maharufu kama Derrick amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi na mtu asiye julikana, polisi wanamshikilia msichana alieonekana eneo la tukio kwa mahojiano zaidi"
Ni kwa mujibu wa gazeti hilo, nilipoangalia sura ya msichana alie semekana kushikiliwa nilishtuka baada ya kugundua ni sura ya mdogo wangu Sophia. Nilijikuta nikitokwa na mchozi maana akili yangu ilikuwa inatambua mdogo wangu hakuwa Duniani.
"John?"
Aliniita yule dokta na kunifanya nigeuke upande wake na kumwangalia.
"Unajisikiaje kwa sasa?"
"Najisikia vizuri Dokta na nashukuru kwa msaada wako" Nilimjibu huku nikiwa naangalia lile gazeti, nilifurahi kuona mdogo wangu bado anaishi, nilijua huko alipo atakuwa anapata tabu ya kutumikia kifungo cha mauwaji, lakini niliamini kama nilikwisha kupona ningaliweza kumsaidia mdogo wangu kutoka kwenye kifungo chake. Nilinyanyuka na kumsogelea kaka Joram, kabla sijafika kwa kaka Joram niliona mlango unafunguliwa, nilishangaa kukutana uso kwa uso na Mdogo wangu Sophia.
Nilishangaa sana kumuona mdogo wangu, nilimwangalia vizuri huku nikiwa kama nimemfananisha. Nilinyanyuka na kwenda kumkumbatia mdogo wangu huku nikiwa siamini kama mdogo wangu alikuwa hai. Machozi yalinitoka, hayakuwa machozi ya majonzi bali yalikuwa machozi ya furaha. Nilimwangalia mdogo wangu na kukuta hakuwa na kovu lolote, lakini cha kushangaza mdogo wangu hakuonekana kuwa na furaha hata kidogo. Nilizidi kushangaa pale nipomuona mdogo wangu anatokwa na machozi, kwa jinsi alivyokuwa akilia ilionyesha wazi yale machozi hayakuwa machozi ya furaha. Nilishindwa kuelewa kitu kilishi msibu mdogo wangu, nilijiuliza maswali mengi juu ya kilio cha mdogo wangu, nilivyo muuliza ndiyo nilizidi kuona anazidisha kulia. Nilihisi huenda kukawa na tatizo kubwa limetokea, nilihisi huenda mjomba Denis alikuwa amepoteza maisha.
Machozi yalianza kunitoka maana mtu tuliekuwa tunamtegemea kama Baba kwetu ni Mjomba Denis, nilijua tumebaki yatima. Machozi yalitoka kwa wingi huku yakiambatana na makamasi, kimya kilitawala huku mdogo wangu akizidi kulia, tukiwa pale mlango ulifunguliwa na aliingia mtu aliekuwa na magongo mawili huku akijikongoja, nilipomwangalia usoni nilishangaa kukutana na sura ya Baba mkubwa Derrick. Kiukweli nilishtuka hadi kikaanguka chini, mshituko niliokuwa nimeupata haukuwa wa kawaida, nihisi macho yangu hayakuwa yanaona vizuri. Nilijaribu kuangalia mara mbilimbili lakini ukweli ulibaki pale pale kuwa yule aliekuwamo pale alikuwa ni Baba mkubwa Derrick.
Sikuweza kuamini kile nilichokiona, nilihisi ni ndoto lakini haikuwa ndoto, nilimwangalia jinsi alivyokuwa, alionekana kuwa na maumivu na vidonda vilivyozungushiwa bandeje, kila kona ya mwili wake.
Kitu cha kwanza nilienda kuangalia lile gazeti lililo kuwa na taarifa juu ya kifo cha Baba mkubwa Derrick, niliposoma sikukuta kitu kilichobadilika bai ilibaki vile vile kuwa Derrick ameuwawa kwa kupigwa risasi, nilishindwa kuelewa walikuw na maana gani kunifanyia vile, nilibaki njia panda, yule dokta alimsogelea Baba mkubwa na kumsaidia kumsogeza hadi pale kitandani na kumketisha, alipoketi tuliona mlango unafunguliwa na kuingia mtu mwingine akiwa na magongo kama alivyokuwa Baba mkubwa Derrick, macho yangu yalitua kwenye uso wa Mjomba, niliona kama maajabu, nilifuta macho yangu nikiwa naamini lile nililokuwa naliona lilikuwa ni ndoto. Nilibaki nikiwa nimeduwaa nisijue nini cha kufanya. Nilibaki nikiwa namuangalia mjomba nihisi kumfananisha, sikuamini kama mjomba alikuwa hai.
"Karibu kaka"
Alionge yule Dokta akiwa anamsogeza karibu na moja ya viti vilivyokuwa pale ndani, yule Dokta alionekana kuwa mkarimu na mwenye kujali watu.
"John mbona hivo, unaangalia nini huko?"
Ilikuwa ni sauti ya mjomba Denis na kunifanya niache kuangalia mlangoni amboapo nilibaki niganda baada ya kumuona mjomba Denis, niligeuka na kumwangalia mjomba huku pembeni kukiwa na Baba mkubwa akiwa katika hali ya kujutia na masikitiko makubwa, nilijawa na hasira kila nilipokuwa namwangalia Baba mkubwa akili yangu ilikuwa ikirejea katika matokio kadhaaa yalionitokea na kusababishwa na Baba mkubwa. Nilibaki na mwangalia Baba mkubwa nikiwa nafikiria ni kitu gani ninge mfanyia. Kiukweli nilikuwa na asira isiyo zuilika, kila nilipokuwa nikikumbuka matukio yaliotokea na msababishaji alikuwa ni baba mkubwa.
"John embu keti kwanza hapo"
Aliongea yule dokta huku akiwa ananionyesha mahali pakuketi, nilimwangalia yule dokta na kuanza kujiuliza maswali, katika maisha yangu sikuwahi kukutana na mtu mtulivu na mwenye busara kama yule dokta.
"Sophia jaribu kupunguza jazba na utambue yote haya yaliotokea hayazuiliki tena"
Yule Dokta alimweleza mdogo wangu kitu ambacho sikupata kujua walikuwa wakimaanisha nini, mdogo wangu uso wake ulijawa na machozi, huku macho yake yakiwa yamevimbiana. Nilimwangalia mdogo wangu kikweli alikuwa amedhoofika, hakuwa na mwili kama ule aliokuwa nao hapo kabla. Nilishindwa kuelewa kilichokuwa kikimsibu mdogo wangu.
"Nasikitika sana kwa hiki ulichokifanya kwa ndugu zako, tena nisiseme ndugu bali hawa ni kama watoto wako, wewe ndiyo ulitakiwa kuwajibika na kuwalelea watoto hawa vizuri. Sijui wewe ni mwanadamu wa namna gani, kweli unaweza kumbaka mtoto wa mdogo wako ambae ni kama mtoto wako, pengine hawa ni wadogo kuliko na watoto wako. Nimeishi na kukutana na watu wa aina tofauti tofauti, wenye taabia za kila aina ila taabia kama ya kwako sijawahi iyona"
Alionge yule Dokta kwa sauti iliojawa hasira na jazba nyingi, maneno alikuwa akiyazungumza yule Dokta yaliniacha njia panda. Nilibaki nikiwa natafakari yale maneno bila kupata jibu, nilitamani kujua walikuwa wakimaanisha nini kutamka maneno kama yale.
"Amembaka nani"
Niliuliza bila kutarajia huku nikiwa nasubiri jibu kutoka kwa yule Dokta aliezungumza maneno yale, kimya kilitawala kwa dakika kadhaa bila kupata jibu. "Mimi sistahili kubaki hai, nakiri dhambi zangu mbele za Mungu, najua nimefanya mengi mabaya nimeweza kumzalilisha mtoto wa mdogo wangu na kibaya zaidi nimeweza kumuwa. Kweli kabisa sitakiwi kuishi, kama hamtaniuwa basi nitajiuwa mimi mwenyewe. John mwangu naomba usije ukanisamehe maana mpaka sasa wewe huwezi kuendelea kuishi ukiwa na viungovyako vyote maana unaumwa sa...." Kabla hajamaliza Nilishtukia anakanyagwa teke la kifua na kuanguka chini, Damu nyingi zilimtoka mdomoni ukijumlisha na majeraha aliokuwa nayo ilitosha kabisa kutambua maumivu aliokuwa akiyapata yalikuwa ni makali sana. Nilibaki nikiwa namwangalia Baba mdogo na kujiuliza alikuwa amemuuwa nani, na kitu kingine ni kutaka kujua mimi nilikuwa na ugonjwa gani ambao ulikuwa unanikabili na ungeweza kunifanya nisiwe na viungo vyangu vyote.
Nilifikiria vitu vingi na kuhisi kulikuwa na kitu walikuwa wananificha, sikuwa naelewa ni kwanini Baba mkubwa alivyotaka kuniambia mimi nilikuwa nasumbuliwa na nino. Kile kitendo kiliweza kufungua akili yangu na ndipo nilipopata wazo la kuuliza kwa hali ya utulivu, nilipouliza kila mmoja alionekana kuwa na wasiwasi.
"Bora tu tumwambie ukweli maana tunavyomficha haitasaidia, najua hamtaki kumwambia ukweli ila tambueni ipo siku atajua ukweli maana ukweli wenyewe ataujua siku ya kukakwa mguu wake" Nilishindwa kuelewa alikuwa anamaanisha nini kusema siku ya kukatwa mguu, nilibaki njia panda nisijue maana kamili ya yale maneno. Alivyo zungumza yale maneno kila mmoja alibaki kimya kanakwamba aliwashangaza kwa yale maneno.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kiukweli ningependa kabla sijapoteza uhai wangu ningependa kusema ukweli wa maovu yangu yote, Sophia nakumba unisamehe sana maana hata nikiwa hai sijui uso wangu nitauficha wapi. Wewe ni kama mwanangu lakini nilikufanyia kitu ambacho hakistahili katika huu ulimwengu, Najua nimekupa jeraha la milele sistahili kuishi. John najua muda siyo mrefu hautakuwa na mguu mmoja hii ni kutokana na kuwa na Kansa ambayo imeweza kushambulia mguu wako wa upande wa kulia" Yale maneno yalikuwa kama radi kwenye upande wa moyo wangu, nilihisi Baba mkubwa alikuwa amechanganyikiwa kuzungumza maneno kama yale, nilimwangalia huku nikiwa kama mtu niliechanganyikiwa.
"Mguu? Mguu upo? Wa kwangu au wa kwako?"
Niliuliza maswali mengi huku yote nikihitaji kupata jibu lake, kiukweli nilikuwa naendea kuchanganyikiwa, yale maneno yalinifanya niangalie miguu yangu yote miwili, hakukuwa na tofauti yoyote kwenye miguu yangu. Ni baada ya kuangalia na kukuta makovu, nilinyanyua shingo yangu ili kumuuliza Baba mkubwa juu ya ukweli wa yale maneno. Badala ya kunijibu aliomba yule Dokta aongee ukweli juu ya yote yaliotokea, yule Daktari hakuwa tayari kuzungumza, hakuma aliekuwa tayari kuzungumza ndipo mjomba Denis alivyoamua kuzungumza huku akiniambia nisiongee chochote hadi atakapo maliza maongezi. "Kiukweli naweza kusema familia hii muda siyo mrefu inaenda kuteketea, sisemi hivyo kuwatisha maana kila mmoja wenu anajuwa kilichotokea, na kwa wale ambao hawakuwa wafahamu kilichotokea naombeni mnisikilize kwa makini, maana maji yakisha mwagika hayazoleki na hata yakizoleka hayawezi kuwa sawa na yale ya mwanzo" Alianza kuonge Mjomba Denis huku akiwa ameshikilia magongo yake, maneno yale yalio ongelewa kimafumbo yaliniacha kwenye wakati mgumu kuyafumbua mafumbo hayo.
"Kama mnavyo niona hapa naonge na kutembea na haya magongo, sikutamani kuwa hivi ila yole haya yamesababishwa, kila kitu kimeharibika. Ndoto za familia hii haziwezi kutimia tena. Kuna watu wanaishi kama binadamu lakini si binadamu, wanaonekana na sura za kibinadamu lakini si binadamu. Naongea haya nikiwa na maumivu makali moyoni mwangu, najua huu ndio mwanzo wa mateso makali katika maisha yangu" Alishindwa kuendelea kuongea kutikana kukabwa na kwikwi za kilio, machozi aliokuwa yakimtoka hayakuwa ya furaha, uso wake ulitawaliwa na huzuni kitu ambacho kilitufanya wote kuanza kutokwa na machozi. Yale maneno yalikuwa kama maigizo kwa jinsi ilivyoonekana lakini hakukiwa na maigizo yoyote, kila kitu kilikuwa ni kweli. "Inaniuma sana ndugu yangu ananifanyia mambo kama haya, ona sasa sitoweza tena kutembea nimebaki wakufa mimi, wajomba zangu naombeni mnisamehee sana kwa kuongea maneno kama haya. Kiukweli hata nyinyi mpo kwenye wakati mgumu sana.
Nikweli kabisa kama alivyo zungumza Baba mkubwa wako kiwa wewe utakatwa mguu wako, hatuwezi kukuficha maana hili halina kizuwizi, yote haya msababishaji ni huyo, ameweza kumbaka mdogo wako na tunavyoongea sasa hivi mdogo wako ni mjamzito. Mbaya zaidi mdogo wako ni muathirika wa ugonjwa wa UKIMWI" Nilishtuka kusikia yale maneno, akili yangu nilihisi haikuwa ikifanya kazi, kwakile nilichokisikia kilitosha kabisa kunifanya nijihisi kuchanganyikiwa.
Nilihisi hali ya hewa kubadilika, mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio. Kiukweli yale maneno yalinifanya mwili wangu kuishiwa nguvu, nilimwangalia Mjomba Denis alivyokuwa akiongea huku akitokwa na machozi mengi.
Roho iliniuma sana nilijiona mimi si kitu tena, nilianza kuwaza maisha ya kuishi bila mguu mmoja, lilikuwa kama jambo la utani kwa kile kilichokuwa kikizungumziwa. Machozi ya Mjimba yalinifanya niamini kile alichokuwa akikisema, mdogo wangu alikuwa akilia hadi kubadilika rangi na kuwa mwekundu. Hasira zilinijaa hadi mwili wangu ukaanza kunitetemeka, nilimwangalia Baba mkubwa kwa hasira na kuanza kumfuata huku nikidhamiria kumuuwa kabisa, kila nilipokuwa nakumbuka matukio alioyafanya katika maisha yangu ndivyo hasira zilivyozidi kuniongezeka. Nilipomfukia bila kuchelewa nilimnyang'anya gongo moja na kumpiga la kichwa, nilimpoga kwa hasira na lile gongo hadi akawa ameanguka chini huku damu nyingi zikimvuja kwenye kichwa chake. Nilipotaka kumpiga kwa mara nyingine nilishtukia kitu kama mwiba unaingia kwenye mwili wangu na hapo sikujua kilichoendelea. Nilipokuja kushtuka nilijikuta nimelala kwenye kochi, bilikurupuka kana kwamba kulikuwa na mtu amenishtua.
Niliposhuka kwenye lile kochi nilijukuta nikianguka chini, nilishindwa kuelewa kilichonifanya kuanguka chini, hata nilipojaribu kunyanyuka nilijikuta nashindwa. Ndipo nilipo jiangalia na kugundua mguu wangu wa kukia haukuwamo, nilihisi ile ilikuwa ndoto, nilijaribu kugusa mahali palipokuwa na mguu wangu lakini sikufanikiwa kuuona.Ndugu msomaji nilihisi kuchanganyikiwa, sikiweza kuamini kama kweli mguu wangu haukuwamo. Machozi yalinitoka huku nikiwa bado siamini kama mguu wangu haupo. Nilikumbuka maneno nilioambiwa mara ya mwisho kabla ya kukosa mguu wangu, nilishindwa kuelewa ni kiti gani nilimkosea Mungu hadi kupelekea kunipa adhabu nzito kama ile. Nililia sana huku nikitamani ikiwezekana mguu wangu urejee tena, nilizidi kulia hadi pale nilipomuona Mdogo wangu anaingia pale ndani.
"Kaka umeamka tena? Vipi kaka unajisikiaje na mbina unalia kaka yangu?"
Aliuliza mdogo wangu baada ya kugundua kuwa nilikuwa nikilia, nilishindwa kumjibu na kubaki na kigugumizi cha kwikwi.
"Namshukuru Mungu muumba mbingu na nchi kwa kuendelea kunipa uhai na pumzi, sina kikubwa cha kukupa zaidi ya asante. Nakushukuru kwa kunipa uhai na pumzi ya bure, najua hata hiki koungo kilicho ondolewa naamini ipo siku kitarudi" Nilibaki nikimuomba Mungu na kumshukuru huku machozi yaki nitoka kwa wingi. Baada ya siku tatu nilikuwa tayari naweza kutumia magongo na kutembea umbali mrefu kiasi, tarifa za Baba mkubwa sikupata kuzisikia wala kujua chochote kutokea siku niliokuwa nimempiga na lile gongo. Hali ya maisha ilibadilika sikuweza kufanya vitu vingi kutokana kiuwa na mguu mmoja. Sasa imepita miaka miwili toka matatizo yale kunikuta Mungu amenijalia watoto wawili, ni baada ya kupata msichana alienipenda na kuridhia hali niokuwa nayo. Juliet na Junnio ni majina ya wanangu, Mungu amezidi kunilonda kila hatua na hadi sasa nipo salama. Kikiondoka kiungo kimoja katika mwili wako jua Mungu bado anamakusudi na wewe, yamkini kile kiungo ndicho kilichosababisha Juliet na Junnio kuwa hapa walipo. Sasa maisha yangu yamebadilika ni baada ya kumpata mke mwenye kunijali na kunipenda kuliko chochote, nami nampenda hivyo hivyo milele daima.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment