Simulizi : Wabeba Ndoto (Dream Holders)
Sehemu Ya Tano (5)
"Una uhakika kwamba atakuwa sawa ukienda naye Groto?" aliuliza Daniel "sijui inabidi tujaribu huku madaktari watajua kuwa alikuwa haumwi na hata hizi alama za ngumi za Kronos zitazua maswali.Asante sana unaweza kwenda Daniel" aliongea Sebastian na kumpokea Gerald kutoka mikononi mwa Daniel.Muda huohuo Kylie aliwasili pamoja na Paul na kusimama mbele ya Sebastian na Daniel huku wakimtazama Gerald aliyekuwa amepoteza fahamu."Sebastian!" aliongea Kylie kwa mshangao na hasira "naondoka" aliongea Daniel na kuondoka "Sebastian tena! ukiwa na Daniel wewe ni nani Sebastian na unataka nini kutoka kwa Gerald?" "sikia Kylie huu sio muda wa kuongea haya angalia Gerald yupo katika hali mbaya inabidi nimpeleke mahali akasaidiwe kama kuna matibabu apewe" "mahali gani unataka kumpeleka! eeh! kama kweli ana matatizo kwa nini usimpeleke hospitali ambapo atakuwa chini ya uangalizi wa mama yake na sisi rafiki zake" "sikia Kylie naakiwa kumpeleka Gerald sehemu iliyo salama na si..." "wapi huko! amabako ni salama kuliko hospitali.Na inaonekana unamjua Daniel kumbe! kama ni tatizo la kimatibabu Gerald atatibiwa hapahapa na humpeleki popote" aliongea Kylie kwa msisitizo "Kylie unajua wewe huelewi kinachoendelea ni...."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ "kinaendelea nini! humjasikia alichosema kuwa Gerald atatibiwa hapahapa na haendi popote na mtu tusiyemfahamu.Fanya jambo la busara tuachie Gerald na uondoke zako"alidakia Paul akiongea huku akimsogelea Sebastian mpaka usoni na kukunja uso wake."Okay hamna shida kama mtamtibu.Nitakufuata kwenye ndoto Gerald" alingea Sebastian na kumnong'oneza Gerald karibu na sikio lake.Alimsogeza Gerald na kumpatia Paul ambaye alimpokea na kumshika vizuri "na kitu kingine nikikuona tena karibu na Gerald nitakushitaki polisi" aliongea Kylie kwa hasira.Sebastian alinyoosha mikono yake na kuondoka.Kylie aligeuka na kunyanyua uso wa Gerald "Gerald! Gerald! unanisikia?" "Kylie nafikiri nenda kamuite kocha ili afanye mpango tumpeleke hospitali" aliongea Paul na Kylie alikimbia haraka na kumpasha habari kocha juu ya tatizo la Gerald.
Ndani ya zahanati kubwa katika moja ya chumba cha wagonjwa Gerald alionekana akiwa amelala juu ya kitanda akiwa bado hajarudia fahamu zake,mama yake alisimma karibu yake huku akitiririka machozi.Kylie lijaribu kumfariji kwa kumkumbatia.Muda huohuo daktari aliwasili na kumsogelea mama yake Gerald "habari yako mama.Pole sana juu ya mwanao.Kwa kweli tatizo ambalo linamsumbua mwanao ni tatizo ambalo hatujawahi kuliona kabisa.Kuna kitu kinatokea ndani ya mwili wa mwanao inaonekana seli zake ziliathirika na mionzi fulani ambayo hatujui imetokea wapi hiyo mionzi.Je mnajua lolote kuhusu hili?" "hapana dokta hatujui lolote kuhusu mionzi Gerald alikuwa kwenye mashindano ya rugby wakati tatizo hilo limemkuta.Na hiyo mionzi kaitolea wapi! hakuna mazingira yeyote ambayo yanaweza kuleta mionzi na kama ni uwanjani ina maana basi wachezaji wote wameathirika na mionzi amabyo sina uhakika na chochote juu ya mionzi maana ni jambo kubwa sana" "hujakosea hata sisi tunashangaa tumewafanyia uchunguzi wachezaji baadhi na hakuna ambaye amegundulika kuathiriwa na mionzi yeyote na cha kushangaza zaidi mionzi hiyo inaonekana kutokea ndani ya mwili wake.Nandiyo ambayo imesababisha seli zake kuachana kwa kiasi kikubwa lakini zitachukua mda paka kurudi katika hali yake kama siku tatu hivi hasa seli zake za ubongo.Na vipi kuhusu hizo alama za ngumi na majeraha usoni mnajua chochote kuhusu hilo pia?" aliuliza daktari tena "hapana dokta hatujui chochote" "nafikiri akiamka unahitaji kuzungumza sana na mwanao ujue nini kinaendelea" aliongea daktari huku akitabasamu na kuondoka.
Mlango ulifunguliwa kwa nguvu kiasi cha kumshitua Kate aliyekuwa chumbani kwake na kuamua kushuka chini sebuleni kwa haraka.Aliduwaa alipomuona kaka yake Sebastian akiwa na amembeba Gerald mikononi mwake "Sebastian! nini kimetokea!" aliongea Kate kwa mshituko baada ya kumuona Gerald akiwa hajielewi mikononi mwa Sebastian "Kate mtafute dokta Richie aje haraka" aliongea Sebastian huku akimlaza Gerald juu ya kochi refu lililokuwa sebuleni pale.Kate alikimbia haraka na kunyanyua simu yake kumpigia dokta Richie huku Sebastian akiendelea kumuhudumia Gerald."Nini kimetokea Sebastian mbona Gerald yupo hivi?" "alikuwa akipigana na Kronos" "na?! Kronos ndio kampiga kiasi hiki! nilifikiri uliniambia kuwa Gerald ni supreme.Kama hamna uhakika kwa nni mnahatarisha maisha ya Gerald!" alongea Kate kwa uchungu kiasi cha kumshangaza Sebastian huku akimtazama Kate usoni na kushindwa kuelewa ilikuaje Kate alihisi vile "sio kwamba Kronos amempiga.Alimpiga Kronos lakini hali hii imemtokea ghafla baada ya Kronos kukimbia.Umeshampigia dokta Richie?" "tayari yuko njiani anakuja" alijibu Kate.
Paul alifungua mlango taratibu na kuingia taratibu huku akimuangalia Gerald aliyekuwa amelala kitandani bila fahamu yeyote.Kylie alionekana kusimama pembeni ya kitanda akimuangalia Gerald aliyekuwa amelala hajielewi.Paul alimsogelea Kylie na kumbusu shavuni "anaendeleaje?" "dokta amesema anaweza kuamka baada ya siku tatu au zaidi" alijibu Kylie kwa sauti ya unyonge "tatizo ni nini?" "wamesema ni kwa sababu ya kitu kama mionzi hivi imempiga.Ndio nashangaa mionzi gani hiyo na imetokea wapi mbona wachezaji wengine hawajaathirika" maneno hayo yalimduwaza Sebastian aliyeonekana kuwaza sana.Alimgekia Kylie aliyekuwa makini sana akimtazama Gerald kitandani huku uso wake ukionekana kuwa na majeraha mengi "siku ile wakati Daniel anamchukua Gerald niliona shingo yake ilikuwa na rangi ya bluu" "una maana gani?" "huenda madaktari wakawa wako sahihi Kylie" "kama ni mionzi mbona wewe uko sawa!" aliuliza Kylie kwa mashaka "labda mionzi hiyo ilitakiwa kumpiga yeye au labda kuna watu walitaka kumpiga Gerald na mionzi hiyo.Anayejua hilo ni Daniel na yule jamaa Sebastian itakuwa wanajua kila kitu.Hapa kuna kitu kinaendelea Kylie lazima tutafute kinachoendelea kama Gerald hatatuambia basi tutafuta wenyewe" aliongea Paul huku akimtazama Kylie usoni aliyekuwa amenyong'onyea kwa huzuni."Umekula?" "hapana" "Kylie unatakiwa kula siku ya pili hii hujala hata kidogo au unataka na wewe ulale kitandani.Nikuletee nini?" "usijali niko sawa wala usisumbuke" "lakini baby una..." "niko sawa husikii!" alijibu Kkylie kwa sauti ya juu "niko sawa usijali wewe nenda kale nitakaa hapa kumuangalia Gerald" aliongea tena Kylie kwa sauti ya chini.Paul alitembea taratibu kuondoka aliufungua mlango taratibu na kumtazama Kylie aliyekuwa amesimama akimtazama Gerald.Jambo hilo lilijaza wivu kw Paul ilikuwaje Gerald rafiki tu wa Kylie asababishe mpaka kylie kutokula kwa siku mbili,ulikuwa ni urafiki gani huo!.Paul alifunga mlango na kuondoka zake.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"inaonekana kuwa seli zake za mwili hasa za ubongo zimeachana sana na zinajiunga taratibu.Imesababishwa na mionzi labda kitu kama hicho" aliongea dokta Richie baada ya kumchunguza Gerald aliyekuwa kitandani kwenye moja ya vyumba katika nyumba ya Sebastian "huyu ni supreme na huwa anabadilika rangi anakuwa wa bluu anang'aa" "oh! kumbe ni supreme! inawezekana pia huo mwanga anaotoa wakati anang'aa unasababisha seli zake kutengana pia.Sikuwahi kufikiria kama kuna siku nitakuja kumuona supreme huwa nasikiaga mababu zetu wakituhadithia kuhusu huyu supreme lakini leo nimemuona,ni heshima sana kwangu" aliongea daktari yule kuonyesha furaha yake "sawa usimuambie mtu yeyote kuhusu hili" "usijali,pia mrudishe duniani ulivuomleta huku Groto unazidi kuziathiri seli zake za ubongo.Mrudishe tu duniani ili apone haraka" alishauri daktari Richie.Sebastian alirudi na kumshika dada yake Kate kwenye mabega baada ya kumsindikiza dokta Richie nje "umekula?" "unafikiri nitaweza kula wakati Gerald yupo katika hali hii" alijibu Kate "oh! unajali sana kuhusu Gerald! basi muangalie kama huna njaa wacha mimi nile nikimliza nimrudishe duniani" aliongea Sebastian na kuondoka zake kuelekea jikoni.
Katika moja ya klabu kubwa ya usiku Harrison alionekana akibugia pombe kwa hasira kali huku mawazo yake yakiwa juu ya mama yake aliyekuwa akimtesa sana pamoja na Kylie ambaye alikamata hisia zake na kumchanganya sana.Pembeni yake walikaa mabinti wawili ambao Harrison alikuwa akiwatazama kwa macho ya matamanio hasa kwa kuwa wasichana wale walikuwa wamevalia mavazi yalioacha sehemu zao kubwa za miili wazi.Harrrison aliwasogelea kwa ukaribu huku akiwa anapepesuka kutokana na kulewa sana "mambo zenu warembo" alisalimia Harrison huku akibugia kinywaji chake.Wasichana wale walitabasamu na hawakutegemea mtoto wa tajiri mkubwa katika mji ule angekuwa klabu usiku ule tena akiwa amelewa chakari "ongezeni vinywaji warembo nitalipa tu.Msijali mko na Harrison tajiri mtoto kwa hiyo agizeni chochote.Mhudumu waongezee wadada hawa pombe kali" aliamuru Harrison "asante lakini tumetosheka tayari kwanza hatukai sana tunamsubiri mtu tu" alijibu mmoja wa wasichana wale "aaah! mmetosheka okay! naitwa Harrison sijui mnaitwa nani wenzangu" aliongea Harrison uku akiwapa mikono.Wasichana wale walimpa mikono yao huku wakitabasamu na kujitambulisha "aisee Lilian mimi naondoka ngoja niwahi wewe si Steve atakufuata" aliaga mmoja wa wasichana wale akiondoka na kumuacha mwenzake pale "mbona mwenzako anaondoka!" "anawahi nyumbani unajua usiku huu kwa mtoto wa kike sio mzuri" "wewe vipi hutaki kuwahi au wewe huogopi usiku?" "hapana,naogopa usiku sema kuna mtu namsubiri ndio atakuja kunifuata ndio maana bado nipo" alijibu Lilian huku akitabasamu "nani? baba yako au!" "hapana actually I am waiting for my boyfriend" "oh! your boyfriend.Una boyfriend? yah msichana mzuri kama wewe unakosaje boyfriend.Okay Hope atawahi" alijibu Harrison na kuendlea kunywa pombe zake kali.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwenye kituo cha mabasi ya abiria Lilian alionekana akiwa amesimama huku akiangalia saa yake ya mkononi na kuhema kwa hasira kwa kuwa mda ulikuwa umekwenda sana.Muda huohuo gari ya kifahari aina ya range rover ya rangi nyeusi ilipaki mbele yake taratibu,vioo vilifunguliwa karibu na uso wa Lilian "oooh Lilian! bado unamsubiria boyfriend wako tu" aliongea Harrison kwa sauti lakini Lilian hakujibu chochote hasira za kusimama muda mrefu kituoni hakikumfurahisha "oooh come on! Lilian utamsubiri mpaka saa ngapi? huoni kama giza kubwa sana.Ingia ndani nikupe lift mpaka nyumbani kwako" aliongea Harrison "no its okay namsubiri my boyfriend atakuja" "atakuja saa ngapi tokea umeniacha klabu sasa hivi ni lisaa limepita huyo boyfriend wako atakuja saa ngapi.Acha utoto bwana ingia twende sasa hivi usiku utaporwa" alibembeleza Harrison na kufanikiwa kumvuta Lilian kuingia ndani ya gari yake.Gari ilitembea kwa kasi sana huku stori tamu zikiendelea ndani ya gari zilizomfurahisha Lilian.Ufundi wa Harrison katika kuongea na kupangilia maneno matamu vilimlegeza kabisa Lilian na kujisahau kwamba alikuwa ndani ya gari na mtu asiyemjua vizuri.Harrison alipaki gari yake pembezoni mwa barabara iliyokuwa tulivu usiku huo mnene "vipi mbona unapaki!" "ili tuongee vizuri" alijibu Harrison "lakini..." alishindwa kumalizia baada ya Harrison kujirusha na busu zuri la kimahaba juu ya mdomo wa Lilian na kumfanya Lilian ashindwe kuzuia mihemko yake.Mikono ya Harrison ilipapasa kwa nguvu maziwa ya Lilian huku akiyakusanya kwa nguvu huku midomo yake ikishuka taratibu juu ya shingo ya Lilian na kumfanya Lilian kutoa sauti za kimahaba.Harrison libetua kiti cha Lilian vizuri na kukifanya kilale chini zaidi kwa haraka aliivuta sketi fupi ya Lilian na kuiteremsha wakati huo akifungua mkanda wake kwa haraka.Taratibu Harrison alimuingilia Lilian na kumfanya kwa kasi na kumfanya Lilian kulia kama mtoto mdogo.
Baada ya siku tatu nje ya zahanati kubwa Gerald alionekana akitembea kwa shida huku akiwa anasaidiwa na Paul huku Kylie na mama yake Gerald wakiwa nyuma wakimsindikiza kuelekea kwenye gari ndogo ya Paul.Muda huohuo Harrison aliwasili na gari yake aina ya range rover na kuisogeza kwa kasi mbele yao,alishuka kwa haraka na kuwasogelea "unatafuta nini hapa?" aliuliza Paul kwa hasira "eeh! hiyo ndio salamu!" "seriously Harrison unafanya nini hapa?" aliuliza Kylie "okay,nimekuja kumcheki Gerald nimesikia leo kwamba alikuwa anaumwa naona amepona" "well amepona unaweza kwenda" alijibu Kylie "naweza kuwapandisha kwenye gari yangu ni kubwa mtakaa vizuri hata mgonjwa atakaa vizuri zaaidi "hatuhitaji msaada wako tuko sawa unaweza kwenda au mpaka nikulazimishe" aliongea Paul "haina haja ya kujibishana,Harrison nashukuru sana kwa kuja kunijulia hali nashukuru Mungu nimepata nafuu.Tuko sawa kwenda na gari yetu hiihii" aliongea Gerald na kutembea taratibu kupanda gari yao "okay haina shida get well soon.Shikamoo Mrs Johnson" aliongea Harrison na kupunga mkono kumsalimia mama yake Gerald "eeh Kylie naweza kuongea na wewe tafadhali" "hatuna cha kuongea mimi na wewe" "tafadhali dakika moja naomba unisikilize ili Gerald awahi nyumbani" alibembeleza Harrison.Kylie alitembea na kumsogelea Harrison na kusimama pembeni "eeh eleza shida yako haraka" "Kylie nilikuwa naomba usahau yaliyotokea siku ile unisamehe na tuwe marafiki tena kama mwanzo" "yaani umeniitia hili jambo unanipotezea muda tu" alijibu Kylie na kuondoka na kumuacha Harrison akiduwaa.
Kadiri siku zilivyozidi kwenda afya ya Gerald iliimarika na kuweza kurudi hata shule kuendelea na masomo na kila muda Kylie alipojaribu kumuulizia kuhusu nini kilichotokea siku ya fainali hakumpa majibu yaliyoridhisha "Gerald mimi najua kuna kitu kinaendelea ambacho unanificha kwa nini lakini" "Kylie kama kungekuwa kuna kitu chochote kinachoendelea ningekuambia mbna ila hakuna kitu kinachoendelea" "wewe na Daniel mmeanza lini kuwa marafiki?" aliuliza Kylie kwa shauku "mimi na Daniel siyo marafiki kwani hujui kuwa Daniel ni mpinzani wetu" alijibu Gerald "Gerald mimi siyo mtoto mdogo na kama nyie ni maadui mbona alikusaidia siku ile" "halafu kumbe hamjui Daniel ana roho mbaya uwanjani tu lakini ni mtu mzuri kwa hiyo sikushangaa alivyonisaidia pale" alijibu Gerald na kutabasamu.Kylie hakuridhishwa sana na majibu ya Gerald ila aliyakubali kwa kuwa Gerald hakuonyesha kuwa tayari kumueleza Kylie ukweli wowote.Mwalimu Ngeze aliingia kwa haraka mda huo na kusalimiwa na wanafunzi wote "marahaba eeh ntumaini wote wazima" aliongea mwalimu Ngeze huku akitembeza macho yake mpaka alipomtazama Gerald "oh! Gerald natumaini umepona sasa eeh maana nilisikia unaumwa sana" "yah niko sawa mwalimu" alijibu Gerald huku akitabasamu "vizuri, baada ya vipindi unione" aliamuru mwalimu Ngeze na kuendelea kufundisha kama kawaida yake.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Gerald na Kylie walionekana kukaa pamoja kwenye bustani nzuri iliyokuwepo maeneo ya shuleni,walionekana kuzungumza na kucheka kwa pamoja huku wakifurahia maongezi yao "vipi kuhusu wewe na Paul?" "tuko sawa tu kwa nini umeuliza hivyo?" "sina nia mbaya Kylie ila naona kama haumpi muda wa kutosha Paul sisemi kwa nia mbaya na nina imani hata yeye atakuwa anafikiri hivyo.Sidhani hata kama ningekuwa mimi ningejisikia vizuri" "sijui Gerald nahisi kama nahitaji kila mara kukaa na wewe" "Kylie mimi siyo mtoto mdogo hutakiwi kuwa na mimi kila saa hayo matatizo naweza kuyahimili usiwe na shaka" "moyo wangu hautaki kukuacha peke yako Gerald" aliongea Kylie huku akishika mkono wa Gerald taratibu" "Gerald!" aliongea Paul aliyewasili ghafla,Kylie aliutoa mkono wake haraka kwa kushituka "vizuri kukuona tena ukiwa na afya" aliongea Paul na kukaza macho yake "Paul unafanya nini hapa?" Kylie alikosa utulivu na kujikuta akiuliza swali bila kutegemea "nafanya nini! hapa si shuleni! kwani naulizwa nikimuona girlfriend wangu nisimsalimie au rafiki yangu!" "yah,nimekosea kuuliza" alijibu Kylie "uko sawa kweli?" aliuliza Paul kwa mashaka "anyway tuyaache hayo nahitaji kuongea na wewe Kylie" "basi ngoja mimi niwaache nikamalize kazi zangu kukopi notes" aliongea Gerald na kuondoka "kuna tatizo gani tena Paul?" "nataka tuongee kuhusu Gerald na jinsi ya kumsaidia,inaonekana ana matatizo makubwa yanayomsumbua" "yah nilikuambia Gerald kuna itu haviko sawa na kuna watu wanamuharibu Gerald nafikiri wanamuingiza matatizoni" "basi inabidi tumsaidie wewe endele kumlazimisha Gerald akuambie ukweli huenda akakuambia maana wewe ni rafiki yake a karibu sana tofauti na mimi.Halafu mimi nitashughulika na yule Sebastian kujua ni nani na anamfanya nini Gerald" aliongea Paul "nafikiri hilo ni jambo zuri kumsaidia Gerald maana inaoneka anaogopa kuna mtu anamtisha" aliongea Kylie.Muda huohuo kengele iligongwa ya wanafunzi kurudi madarasani "ooh kiranja ngoja nirudi darasani nitakuona tukitoka" aliongea Kylie na kuondoka huku akimuacha Paul akimshangaa na kukaza macho yake.
Katika jengo kubwa ambalo lilikuwa ni hospitali kubwa ya watu wenye matatizo ya akili au vichaa.Kwenye moja ya chumba alionekana kijana mmoja ambaye alivalia nguo nyeupe ambazo zilibana mikono yake kwa nyuma.Uso wa kijana huyo ulijaa ndevu nyingi na kumfanya aonekane kama mzee ingwa alikuwa bado ni kijana mdogo kabisa.Detective James pmoja na daktari maalum wa wagonjwa hao walisimama nje y chumba hicho huku wakimtazama mgonjwa huyo kupitia ukuta mkubwa wa kioo ambao uliwatenganisha na mgonjwa huyo "nataks kuingia ndani nikaongee naye"aliongea detective James "detective huyu mgonjwa hajawahi kuongea hata mara moja ni yupo hivyohivyo kimya na ukijaribu kuongea naye ni kama utamtibua tu na kumuongezea ugonjwa.Ningeshauri labda muache kwa leo" alijibu daktari huyo "hapana nitajaribu kuongea naye nifungulie niingie" aliamuru detective James.Daktari hakuwa na sababu zaidi ya kukubali kufungua alibonyeza kitufe kilichokuwa pembeni ya mlango na kutoa sauti kubwa kama ya honi ya gari.Mlango ulifunguka taratibu na detective James aliingia taratibu huku akiwa ameweka mikono yake mfukoni "naomba uniache niongee naye" aliamuru detective na daktari yule aliondoka kumuachia usiri."Habari yako Mathias" alisalimia detective lakini kichaa yle hakujibu chochote wala kumuangalia "mmh naona hutaki kuongea na watu ambao tumekuja kukusalimia" aliongea detective huku akizidi kumsogelea kwa ukaribu zaidi.Kichaa yule hakujibu chochote wala kugeuza uso wake "mimi nimekuja kwa jambo moja tu,nataka uniambie kilichotokea usiku wa tarehe 14 najua na wewe ulikuwepo ndani wakati baba yako mzee Max anauliwa.Niambie ulichoona" aliongea detective James lakini kichaa yule Mathias hakujibu chochote wala kupepesa kichwa chake.Jambo hilo lilimtia hasira James na kujikuta akifoka "mimi najua kama wewe huumwi na kwamba unanisikia na una akili tosha ya kuweza kunijibu na kunipa maelekezo ninayoyahitaji.Ukikaa kimya hatutaweza kutafuta haki kwa baba yako na hatutaweza kumtafuta mtu aliyemuua baba yako.Onyesha ushirikiano ili tuweze kukusaidia na sio kukaa kimya,hivyo basi niambie kile ulichokiona usiku w tarehe 14" alifoka detective James.Mathias aligeuka na kuanza kuhema kwa nguvu na kutoa sauti za ajabu kanak kwamba alikuwa akinguruma,uso wake wa kutisha uliojaa ndevu ulimtisha James na kumfanya arudi nyuma taratibu akimkimbia kichaa Mathias aliyekuwa akimsogelea "hakuna mwenye uwezo wa kunisaidia,toka!" aliongea Mathias kwa sauti ya ukali huku akipiga kelele kama mtu mwenye mapepo hukuakionekana kuogopa kitu.Alizidi kumsogelea James na kumpigia kelele nyingi huku akimfukuza na kuangusha vitu kwa kutumia miguu yake na kujaribu kumpiga mateke.James alikimbia na kujaribu kufungua mlango ambao ulikuwa umefungwa kwa nje "daktari! daktari!" alipiga kelele James huku akipiga mlango kwa nguvu.Daktari pamoja na wasaidizi wake walikuja haraka na kufungua mlango na kumtoa Mathias ambaye alikuwa amemkamata James kwenye koo lake.Walitumia mashine ndogo ya umeme kumpiga shoti kichaa Mathias ambaye alianguka chini na kumbeba mpaka kitandani kwake.Detective Mathias alitoka nje taratibu huku akitazama madaktari walivyokuwa wakihangaika kumfunga Mathias atulie,aliweka shati lake vizuri.Daktari alitoka na kumsogelea James na kumkazia uso wake "siku nyingine sitakuruhusu kusumbua wagonjwa wangu na kuleta usumbufu" aliongea daktari yule na kuondoka na kumuacha Detective James akihema kwa nguvu huku akimtazama Mathias aliyekuwa amelala baada ya kuchomwa sindano.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Usiku huo Gerald alioneken kutembea kwa haraka kurudi nyumbani,alishuka kutok ndani ya basi kwa sababu ya foleni kubwa iliyokuwepo barabarani.Alitazama saa ake ya mkononi na kuona kuwa mda ulikuwa umekwenda sana na mama yake alimkataza kurudi nyumbani usiku.Alitembea na kukatisha mitaa mingi alipita pembezoni mwa majengo marefu ya kiofisi na biashara.Alikaribia jengo refu ambalo ilikuwa ni hoteli kubwa ya nyota tano katika mji huo.Aliikaribia hoteli hiyo na kupotea ghafla.
Aliangalia huku na huko na kukutana na miti mirefu ambayo ilikuwa pembezoni mwa barabara ya vumbi,alisikia sauti ya mwanamke akikimbia huku akilia na kupiga kelele.Alisikia pia sauti kubwa ya mngurumo kama wa simba.Alitaza vizuri na kumuona mnyama kama mbwa mkubwa mweusi akimkimbiza mama yule.Mnyama yule alitisha sana huku mngurumo wake mkubwa ukiashiria njaa kali aliyokuwa nayo.Gerald alijificha pembeni ya mti mkubwa na mwanamke yule alikimbia haraka kumpita Gerald aliyekuwa amejificha pembeni ya mti.Aliokota tawi kubwa la mti na kulitoa majani pamoja na vitawi mkubwa mpaka lipopata gongo kubwa.Alitoka kwa ghafla mbele ya mnyama yule ambaye alisimama ghafla.Alinguruma kwa nguvu kuashiria Gerald atoke mbele yake lakini Gerald aliendelea kusimama kwa kujiamini huku akinyosha gongo lake.Alipigwa konde zito juu ya uso wake na mnyama yule na kuanguka chini.Mnyama yule aliendelea kukimbia kumkimbiza mwanamke yule lakini Gerald alimkamata mkia.Mnyama yule alilia kwa hasira.Mwanamke yule alisimama na kugeuka nyuma na kushangaa kumuona kijana asiyemjua akijaribu kupambana na mnyama yule.Gerald alimvuta mnyama yule na kumuangusha chini.Mnyama yule alinyoosha makucha yake kuelekea juu ya uso wa Gerald lakini Gerald aliinama vizuri na kukamata sehemu ya juu ya mkono ule na kuruka juu ambapo alikwaruza sehemu ya juu ya bega la mnyama yule.Alinguruma kwa maumivu na kuamua kukimbia.Gerald alihema kwa nguvu na kutupa gongo lile chini.Ghafla alitokea mbele ya hoteli ile na kujishangaa "nini kinanitokea?" alijisemea Gerald na kujitazama.
Gerald aliingia ndani akiwa amechelewa na kumkuta mama yake akiwa sebuleni akitazama luninga "wewe mtoto huwa husikii ukiambiwa mda wa kurudi nyumbani" "shikamoo mama,tatizo foleni mama leo kulikuwa na foleni kubwa sana njiani" aliongea Gerald kwa haraka na kujaribu kuondoka "hebu rudi hapa adabu gani hiyo" aliongea mama yake huku Gerald akimsogelea taratibu "na huo uso vipi?" "kuna mtu alinichokoza shuleni" "ndio mkapigana.Sasa utapigana na kila mtu anayekuchokoza.Unajua siku hizi sikuelewi wewe mtoto hivi kuna nini kinaendelea isije ikawa umeingia kwenye makundi ya kuhuni huko" aliongea mama yake kwa kufoka "hapana mama" alijitetea Gerald na kuondoka baada ya kusemw kwa muda.
Detective James alionekana ofisini mwake akipekua makaratasi mengi yaliyokuwa mezani kwake.Aliziangalia picha nyingi zilizokuwa za maiti ya marehemu Maxx,baba yake Mathias.Picha hizo zilionesha maiti ikiwa ina mikwaruzo mikali ya kucha za mnyama mkali sana ambaye hakujulikana.James alikusanya picha zile na kuondoka kwa haraka.Gari ndogo ya James ilipaki mbele ya zahanati ndogo ya wanyama "unaweza kuzitambua hizi alama ni za mnyama gani?" aliuliza James "ni vigumu kuzitambua ila inaonekana huyu mnyama ni jamii ya mbwa na kwa jinsi zinavyoonekena ni mbwa mkubwa sana maana kucha zake ni ndefu.Na sidhani kama tuna huyu mnyama wa aina hii hapa kwetu wala duniani kote.Sina uhakika sana kama yupo mnyama wa aina hiyo hapa kwetu" alijibu daktari wa mifugo aliyekuwa akitazama picha zile alizoletewa na James "hii maiti ni ya raia wa hapahapa na alikutwa akiwa amekufa nyumbnai kwake sasa ukiniambia huyu mnyama hayupo mahali hapa nashindwa kukuelewa" "mmh kwa kweli sijawahi kuona kitu kama hicho tokea nimeanza hii kazi yangu.Na kama huyo mnyama yupo basi atafutwe haraka ili adhibitiwe na inavyoonekana ni muuaji na siyo kama anatafuta chakula" "huwezi hata kukisia ni aina gani ya wanyama wanaokaribia labda na aina hii" "hapana kwa kweli" alijibu daktari yule.
Kesho asubuhi sana mama yake Harrison alirudi nyumbani mapema.Gari yake ya kifahari ilionekana kuwasili nyumbani huku dereva wake akisaidia kushusha masanduku.Mume wake alimuona tokea ndani na kushangazwa na ujio wa ghafla wa mke wake "Harrison!" aliita kwa sauti ya juu na Harrison alitoka haraka akitokea chumbani kwake "hebu nenda kamsaidie mama yako mizigo naona amerudi" aliongea baba yake huku akisimama na kumlaki mke wake nje ambaye hakuonekana kuwa na raha hata kidogo "karibu,vipi tena mkutano umeisha?" "hapana haujaisha bado unaendelea" "sasa mbona umerudi wakati uliniambia utakuwa unakaa hotelini mpaka mkutano utakapoisha" "nimebadilisha tu maamuzi" alijibu mke wake na kuingia ndani akionekana kuwa na uwoga fulani.Harrison alimtazama mama yake huyo wa kambo na kutabasamu.Chumbani mme wake alionekana kujadiliana sana na mke wake kwa kuwa alitambua hayuko sawa huenda kuna kitu kilimkosesha amani "mke wangu kuna tatizo gani tokea umerudi nakuona huna raha" "ni uchovu tu" alijibu "hapana uchovu gani huo,siku zote unafanya kazi tena nzito lakini sikuoni ukichoka hivi,niambie kwa nini umerudi nyumbani au hupendi ile hoteli?" "nafikiri siipendi hoteli" "kwa nini,sasa si ungenipigia simu nimtume mtu akupeleke mahali pengine kama hujaridhishwa na huduma zao" aliongea mume wake "hapana huduma zao nzuri tu,sema huwa naota ndoto za kutisha ndio maana" maneno hayo yalimmaliza nguvu mume wake na kujikuta akicheka "yaani unakimbia hoteli kisa ndoto za kutisha kwani unakoenda hutaota" alizidi kucheka "ndoto zilionekana kama kuwa kweli kabisa,jana nimeota nakimbizwana mnyama gani sijui leo nimeamka asubuhi nimeona mchubuko kwenye mkono wangu" aliongea mke wake huku akitazama kijimkwaruzo kidogo juu ya mkono wake "basi uoga wako unakufanya ukimbie hoteli sikutegemea" aliongea mume wake huku akicheka na kuelekea uwani na kumuacha mke wake akihema kwa hofu.
Aliamka taratibu baada ya kusikia minong'ono na sauti ikimuita jina lake.Alitembea taratibu huku akiifuata sauti ile ambayo ilionekana kutokea nyuma ya nyumba yao.Alijaribu kuisikia kwa makini sauti ile "Harrison! ni wewe au?" aliongea polepole na kuzidi kusogea mbali na nyumbani mpaka alipokaribia mahali ambapo lilikuwa giza tupu huku akizidi kusikia sauti ya Harrison ikimuita lakini hakuweza hakumuona "Harrison!".Ghafla alisikia mngurumo mkubwa nyuma yake,aligeuka na kushtushwa baada ya kumuona mnyama mkubwa na aliyetisha mbele yake.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment