Search This Blog

Friday, October 28, 2022

BEYOND PAIN - 1

 







    IMEANDIKWA NA : PATRICK CK



    *********************************************************************************



    Simulizi :Beyond Pain

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ni saa kumi jioni nikiwa maeneo ya Kimandolu nikielekea Usa river katika baa iliyotulia ya Roterdam garden mahala panapofanyika vikao vya harusi yangu.Wanakamati ya maandalizi walichagua mahala hapa kutokana na utulivu wake kwani kuna bustani nzuri na hata huduma zake ni nzuri sana.Nikiwa maeneo haya ya Kimandolu gari ikienda taratibu kutokana na magari mengi kukaa pembeni ya bara bara kwa muda mrefu kwa kupisha misafara ya viongozi wa jumuia ya Afrika mashariki waliokuwa na kikao chao hapa Arusha.Siku zote kunapokuwa na mikutano ya namna hii jijini Arusha huwa kunakuwa na adha kubwa kwa watumiaji wa bara bara hii ya Moshi - Arusha kwa sababu ndiyo bara bara kuu waitumiayo viongozi hawa wakitokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).Mara simu yangu ikaita nikaitazama na kukuta ni Mr Cheleo mmoja kati ya wanakamati.

    “Haloo kaka” nikasema

    “Haloo ,uko wapi? Sisi tumeshafika tunakusubiri wewe tu.”

    “Niko njiani kaka si unajua leo njia ilikuwa imefungwa viongozi walikuwa wanaondoka.Ndani ya dakika kumi nitakuwa nimefika hapo Usa river.”

    “Ok kaka tunakusubiri”

    Hiki kilikuwa ni mojawapo ya kikao cha maandalizi ya harusi yangu inayotarajiwa kufanyika muda wa kama mwezi mmoja ujao.Harusi ambayo kila mmoja wa rafiki zangu alikuwa akiisubiri kwa hamu sana.Nimekuwa mchangiaji mzuri wa harusi za rafiki zangu na kuhakikisha zinafana safari hii walikuwa wamepania sana kufanya sherehe ya harusi yangu kuwa ya kihistoria.

    Tulipofika maeneo ya madukani gari zikaanza kwenda kasi na dakika tano baadae nikawasili usa river katika baa tulivu ya Roterdam.Nikapaki gari na kuelekea bustanini.Nikawasalimia wanakamati na kuwaomba radhi kwa kuchelewa kisha kikao kikaendelea.Kilikuwa ni kikao kirefu .

    Wakati kikao kikiendelea nikachukua simu na kumtumia mpenzi wangu Emmy ujumbe mfupi.Kwa siku tatu nilikuwa na shughuli nyingi na sikupata hata muda wa kuonana naye.Kwa sasa emmy anasoma digrii ya sheria katika chuo kikuu cha Tumaini makumira.Kila jioni huwa ana desturi ya kupita kwangu na hata kama sipo kwa kuwa ana ufunguo wa nyumbani kwangu huwa ananisubiri mpaka nikirudi tunakaa wote kisha namrudisha kwake.



    “Hallow sunshine,niko kwenye kikao hapa roterdam.Baada ya kutoka hapa nitapita kwako.Missing you soooo much.” Huu ndio ujumbe mfupi niliomtumia Emmy kipenzi cha moyo wangu.



    Tukaendelea na kikao.Baada ya kama robo saa hivi tangu niutume ule ujumbe mfupi wa maandishi kwa mpenzi wangu Emmy simu yangu inaita kuangalia zilikuwa ni namba za emmy.Nikainuka na kwenda mbali kidogo ili niweze kuongea naye.

    “Halloo Darling “Nikasema kimahaba.kwani ndivyo tulivyozoea wakati tunaongea simuni.

    Nusura moyo unipasuke kwa mstuko pale nilipoisikia sauti nzito ya kiume ikijibu.

    “Mwanaharamu wewe,mpenda wake za watu.Huna haya unamwita nani Darling? Kumbe ndio mchezo wako huo wa kudandia wanawake wa watu.Leo nimekupata.”

    Nilibaki nimeduwaa kwa sekunde kadhaa nisijue nini cha kusema.sikuelewa yule jamaa alikuwa akimaanisha nini.Huku nikitabasamu nikauliza

    “Mbona sikuelewi wewe.Unasemaje? samahani kama simu zimeingiliana”

    ‘Simu hazijaingiliana we juha.We si ndio Wayne? Wayne mkotela….

    “yah ndio mimi” Nikajibu huku mapigo ya moyo yakinienda kwa kasi baada ya yule jamaa kulitamka jina langu

    “ Wewe si ndio umemtumia Sarafina ujumbe wa maandishi sasa hivi ukisema unakuja kumuona ukitoka kwenye kikao?

    “Mimi nimemtumia ujumbe Emmy na sio sarafina”

    “sasa sikiliza wewe mjinga….”Nilihamaki baada ya kuitwa vile lakini nikavumilia nimsikie alichotaka kusema

    “Iwe ni huyo Sara au Emmy kama unavyojua lakini nakwambia kuwa huyu ni mke wa mtu na mimi ndio bwana wake.”..

    “Unasemaje wewe??..Nikauliza kwa hamaki

    “Hebu mpe Emmy simu yake haraka.Mpuuzi wewe” Nikasema tena kwa hasira

    “Mpumbavu wewe ! hivi nikwambie mara ngapi Hakuna Emmy hapa…Huyu anaitwa Sarafina.Kama alikwambia anaitwa Emmy alikudanganya.Huyu ni sarafina na mimi ndio mumewe,mimi ndio ninayemlipia hii nyumba anayoishi na ni mimi ndio niliyemtafutia kazi pale AICC na baadae nikamtafutia nafasi ya masomo pale Makumira.Mimi ndiye ninayemlipia ada na kila kitu.Mimi ndiye ninayemuweka mjini.Nilikuwa nje ya nchi nilikuwa napata taarifa kuwa kuna mtu anatembea na mke wangu nikajua ni utani.Leo ndio nimegundua kuwa ni kweli” akasema Yule jamaa.

    “Mjinga mkubwa wewe,huna haya mimi ndie ninayemlipia Emmy ada zote za masomo na hata nyumba anayokaa mimi ndiye ninayelipa.Na kwa taarifa yako mpumbavu wewe,sasa hivi tuko katika maandalizi ya harusi yetu na kesho jumapili kanisani wanasoma tangazo la kwanza la ndoa yetu.Hivyo nakuomba usijaribu kwa namna yoyote ile kuleta upumbavu wako “ Tayari hasira ilikwisha nipanda nikatamka maneno yale kwa hasira.

    “Sikiliza we mjinga yaani pamoja na kukueleza kote huku bado hunielewi sasa Emmy huyu hapa hebu ongea naye”

    Nikasikia akimpa mtu simu na kumlazimisha

    “Hebu ongea na huyu mbwa mwenzako mweleze ukweli mimi ni nani na mkanye akome kuanzia leo kukufuata fuata la sivyo nitamfanyia kitu kibaya sana ,hanijui mimi ni nani mjinga huyu” maneno haya nikayasikia kwa mbali.Mara nikasikia kitu ambacho sikukitegemea kukisikia maishani mwangu.Niliomba ardhi ipasuke niingie ndani.Nilitamani nijimalize pale pale.sikuona thamani tena ya kuendelea kuishi katika dunia hii.

    Niliisikia sauti ile tamu na nyororo iliyozoea kuniburudisha kila siku na kunifanya nione kama niko peponi,sauti ambayo niliamini ni sauti nzuri kuliko zote duniani,sauti ya mpenzi wangu,bibi harusi mtarajiwa Emmy.Huku akilia kwa kwikwi akatamka maneno ambayo yalinifanya niichukie dunia na watu wake na hasa wanawake.

    “Wayne I’m sorry mimi ni mke wa mtu,na ninaomba usiendelee tena kumtukana mume wangu”

    Ilikuwa ni kama niko ndotoni nikazubaa kwa sekunde kadhaa kisha nikajikaza kiume na kuuliza tena.

    “Emmy is that you??…….

    “Yes Wayne please leave me alone.Usinipigie simu tena.Mimi nina bwana wangu”

    Machozi yalianza kunitoka.Sikuamini kile nilichokisikia.

    “Please Emmy tell me its not true ” Nikasema tena huku machozi yakinitoka.

    “My name is not Emmy…..Akashindwa kuendelea alikuwa akilia.Yule jamaa akachukua tena simu

    “Sasa umeamini we kijana.Tafadhali usiendelee kumfuata fuata sarafina.Kitakachokupata usije kumlaumu mtu………..”Akamalizia kwa tusi zito na kukata simu

    Nikahisi miguu ikiisha nguvu nikaakaa chini.

    Christopher rafiki yangu mkubwa alihisi lazima nitakuwa na tatizo akanifuata .Akastuka baada ya kunikuta nimekaa chini.

    “Wayne.. “Akaita nikamuangalia sikuwa na nguvu za kujibu.

    “Wayne una tatizo gani?

    Akawaita wanakamati wote wakaja mbio na kuanza kunipepea.Nikaletewa maji nikanywa.Dakika kama tano hivi baadae nikaweza kuongea

    “Take me home” Nikamwambia Chris

    “Wayne una tatizo gani.Twende hospitali” Akasema Chris

    “No ! take me home” Nikasema huku nikijaribu kuinuka.Wakanisaidia kutembea hadi garini kisha Chris akawasha gari na kuondoka kunipeleka nyumbani.

    Picha mbali mbali zikawa zinakuja na kupotea.Nilihisi kama vile niko ndotoni .Chris aliendesha kwa kasi bila kunisemesha.Tulipofika maeneo ya sanawari nikafungua mdomo na kumwambia Chris.

    “Nipeleke kwa Emmy” Chris alikuwa akipafahamu anapoishi Emmy hivyo tulipofika maeneo ya Ilboru akakata kushoto na moja kwa moja akaelekea nyumbani kwa Emmy.

    Alisimamisha gari nje ya nyumba ya Emmy.Sikuongea kitu nikafungua mlango nikashuka garini.Mlinzi wa kimasai wa nyumba ya Emmy alinifahamu hivyo aliponiona akanisalimia nikapita zangu hadi ndani.Chris naye alikuwa akinifuata kwa nyuma.Nilisimama mlangoni na kusikia watu wakinong’ona kwa ndani.Nilikuwa na funguo ya mlango nikaufungua bila kugonga na kuingia ndani.Sebuleni nilimshuhudia Emmy akiwa kifuani kwa baba mmoja mnene wakiwa katika mahaba mazito.Nikaanguka na kupoteza fahamu.



    * * * *



    Nilizinduka na kujikuta mahala nisipopafahamu.Nilikuwa katika chumba chenye harufu ya dawa.Ndani ya chumba hiki kulikuwa na watu kadhaa.Mtu wa kwanza kumtambua alikuwa Chris.

    “Pole sana Wayne”.Akasema huku akinishika kichwa.”Tafadhali usiinuke , endelea kupumzika.” Muda huo huo akaja daktari akiwa ameongozana na wauguzi wawili,nikajua hapa nipo hospitali.daktari akanipima kisha akasema

    “Kwa sasa unaendelea vizuri.Itabidi ulale hapa leo ili tuendelee kukuangalia zaidi”

    Sikuwa na ubishi ingawa sikuhisi kuumwa sehemu yoyote ile zaidi ya kichwa kuwa kizito mno.Daktari akatoa maelekezo kadhaa kwa wale wauguzi akaandika pia katika kijikadi kisha akatoka.Pale mlangoni nilisikia akiongea kama na kundi la watu.na dakika hiyo hiyo watu zaidi ya ishirini wakaingia mle chumbani.Walikuwa ni wanakamati ya maandalizi ya harusi yangu pamoja na baadhi ya rafiki zangu.Walinipa pole nami nikawahakikishia kuwa niko salama wakanitakia usiku mwema wakaondoka.pale hospitali nikabaki na Chris

    “Chris nini kilitokea mpaka nikaletwa hapa?

    Chris akanitazama kisha akajibu

    “Wayne ulianguka ukapoteza fahamu ,ikanibidi nikulete hapa katika hospitali hii .Usijali kila kitu kinakwenda vizuri.Daktari anasema kesho asubuhi atakuruhusu”

    Niliposikia kuanguka na kupoteza fahamu ,ndipo nikalikumbuka tukio zima lililotokea.Ghafla fahamu zikanipotea tena.

    Nilirejewa na fahamu baadae sikujua ni saa ngapi.Ukiacha yule daktari mmoja aliyekuwapo mida ile sasa walikuwapo watatu.hali hii iliniogopesha sana.Nikaogopa pengine hali yangu si nzuri.Daktari mmoja mzee mwenye miwani akanisogelea na kuniuliza

    “Wayne unajisikiaje sasa hivi?…

    “Najisikia safi ila kichwa ni kizito sana.Nahisi kama kizungu zungu kwa mbali”

    “Ok sawa.Hali yako inaendelea vizuri,vipimo vyote vinaonyesha uko sawa ila unachotakiwa kwa sasa ni kujaribu kutokuwaza kitu chochote kinachoweza kukusababishia ukapoteza fahamu kwa mara nyingine.Jaribu kupata mapumziko ya kutosha na jitahidi sana kutokuwaza…..”

    Nilimtazama yule daktari sikuwa na jibu la kumpa.Nafikiri hakujua kitu gani kilichonipata.Hakuyaelewa maumivu yaliyokuwa moyoni mwangu.

    “Ok dokta nitajitahidi”.Nilisema huku machozi yakinilenga.

    Madaktari na wauguzi wakatoka na kuniacha chumbani mimi na Chris.hawakutaka Chris aniache peke yangu kwa kuwa waliogopa pengine ningeweza kujidhuru.

    Niliinuka na kukaa kitandani.Chris akanisaidia nikakaa sawa.

    “Chris I hate the world”Nikasema kwa sauti ndogo

    Chris akanitazama akasema.

    “Wayne jitahidi upumzike.Usiwaze lolote kwa sasa.Everything will be ok”

    “No Chris.Nothing is ok.Emmy lied to me…………………”Nikasema huku machozi yakinitoka.

    “Don’t cry buddy,be strong” akasema chris huku akinipiga piga mgongoni

    “ I loved her .I loved her Chris more than I love myself.Lakini ona kitu alichonifanyia…..Nitauweka wapi uso wangu mimi?.”.Uso wote ulijaa machozi.Iliniuma kupita kiasi.

    “Wayne lala kwanza.Tutaongea asubuhi” Akasisitiza Chris.

    “No Chris siwezi lala wakati mwanamke niliyempenda amenisaliti….why me????? Why this pain???”

    “Ok brother let it out……let it out….”Akasema Chris.

    “Emmy amenidanganya muda wote huu kumbe ni mke wa mtu….”

    “what!!!!!!!!” Akahamaki Chris

    “Yah! ana bwana wake.Ndiye yule tuliyemkuta amelala naye kwenye sofa pale sebuleni kwake.Kwa mdomo wake mwenyewe ameniambia nisimsumbue yeye ana mume wake ”

    Chris akainuka na kuanza kuzunguka mle chumbani huku ameshika kichwa.

    “Is this true brother”Akauliza

    “Yah..kwa mdomo wake amenitamkia maneno haya….It hurt Chris it hurt so much.”

    “Mwanaharamu huyu…….”Akasema Chris kwa hasira

    “Kesho ndoa yetu inatangazwa kanisani kwa mara ya kwanza…….nikashindwa kuendelea.Nilishindwa kujizuia kuangusha machozi.

    “Wayne its gonna be ok.Jitahidi ulale kesho tutayaongea mambo haya.Usiwaze sana kilichotokea.Hii ni mitihani tu ya maisha”

    Chris alijaribu kwa kila njia kunibembeleza ili niweze kuwa katika hali yangu ya kawaida lakini kwa hali halisi jinsi ilivyo ni ngumu sana.

    Ni Jumatano ya wiki hii tumetoka kuandikisha ndoa kanisani na kesho tangazo la kwanza linaanza kusomwa.tayari maandalizi yote ya harusi yamekamilika .Nitauweka wapi uso wangu mimi.Nitawaeleza nini watu wanaoisubiri harusi yangu??Nitawaleleza nini wazazi na ndugu zangu? Simlaumu mtu.Emmy nilimchagua mwenyewe.Hakunichagulia mtu yeyote.Iwapo ningechaguliwa na wazazi au mtu mwingine , ningekuwa na kila sababu ya kuwatupia mzigo wa lawama wao kwa uchaguzi wao usiofaa.Lakini hili lilikuwa ni chaguo langu mwenyewe..Huu ni mzigo wangu na inanibidi nisimame kidete niukabili.Nilijilaza kitandani na sijui hata saa ngapi nilipata usingizi.

    Saa tano asubuhi tayari nilikuwa nyumbani kwangu maeneo ya majengo.Nilikuwa najisikia mzima wa afya isipokuwa kichwa kilikuwa kikiniuma kwa mbali.Chris ndiye aliyenichukua hospitali na kunirudisha nyumbani.

    Mpaka sasa hivi hakuna mtu mwingine aliyekuwa akijua nini kilichotokea na kupelekea kupoteza fahamu na kulazwa hospitali zaidi yangu na Chris.Sikutaka kuharakisha kuliweka wazi jambo hili gumu.Nilitaka kuacha kwanza akili yangu itulie.Nilikaa kidogo sebuleni ,halafu nikamwambia Chris aniache nikapumzike.

    “Brother naomba nikapumzike,halafu tutaongea jioni.Ila tafadhali naomba usimwambie mtu yeyote nini kilichotokea..”

    ‘Ok wayne nenda kampumzike ila tafadhali don’t do anything stupid”Akasema Chris huku akitoa tahadhari kwani madaktari walimuonya asikubali kuniacha peke yangu kwa kuhofia pengine ninaweza kujidhuru.

    “C’mon Chris,I’m not a kid.Haya ni mambo ya kawaida katika maisha.Let me have a rest then I’ll know what to do next.”

    “Ok wayne..nitapita mchana kukuangalia.Nikuletee chakula gani mchana?

    “Nothing Chris.Usiniletee chochote.I don’t feel like eating anything.”

    “Unatakiwa ule Wayne.unatakiwa uwe na nguvu.”

    Sikumjibu kitu nikamtazama na kuondoka kuelekea chumbani kwangu.

    Nilikaa kitandani,nikalifungua kabati langu na kutoa albamu kubwa la picha.Humu kuna picha nyingi ambazo nimepiga na emmy tangu tulipoanza mapenzi yetu .Picha yetu ya kwanza mimi na yeye ikanikumbusha tulikwenda picnic Ziwa Duluti.Ni siku tuliyofurahi sana.Siwezi kuisahau siku hii.Nikaendelea na kuzifunua picha nyingine.Wakati nikiendelea na kuzitazama picha simu yangu inalia.Alikuwa ni mama yangu.

    “mama shikamoo” nikamsalimu

    “Marahaba baba ,hamjambo”

    “hatujambo mama,vipi mnaendeleaje?

    “Huku wote wazima.Ni baba yako tu kichwa chake kile kinamsumbua sana lakini anaendelea vizuri”

    ‘Mpe pole sana “Nikajibu kwa ufupi.

    “Vipi mkwe wangu hajambo?

    Nikasita kujibu.

    “eenh jamani hajambo mama mkwe? Mama akauliza tena baada ya kuona sijamjibu

    “Hajambo mama”Nikajibu huku nikiuma meno kwa hasira.Mwanamke huyu amewadanganya hadi wazazi wangu.Iliniuma sana.

    “nashukuru kama ni mzima.Vipi mnaendeleaje na maandalizi ya harusi?

    “mama maandalizi ni mazuri.Tunaendelea vizuri”

    “sawa baba.Leo huku wamesoma Tangazo la kwanza..Hivi ninavyokwambia watu wanajiandaa isivyo kawaida,kila ndugu anataka aje kwenye harusi yako.”

    Sikuwa na cha kusema.Machozi yalikuwa yananitoka.

    “Mama nashukuru.Nitakupigia baadae tutaongea vizuri zaidi”

    “Sawa baba”

    Nilikata simu na kuitupia kitandani.hasira zikanipanda.

    “Damn you Emmy…..”

    Nilizungunguka zunguka mle chumbani nikijaribu kuwaza na kuwazua bila kupata jibu.Nikatoka na kurudi sebuleni.Nikafungua kabati ninamoweka cd na kuchukua moja ya cd niipendayo sana ya mmoja kati ya wanamuziki mahiri kwenye mziki wa bongo fleva,Hamis mwinjuma au Mwana F.A .Huu wimbo wake niliona ni kama vile alinitungia mimi kwa sababu ulinihusu mimi.Ubeti wa pili ndio uliniumiza zaidi ukanifanya niurudie tena na tena

    “hata nikitaka kuoa niambie ntamuoa nani?/

    watu wana watu wao wengine toka zamani/

    ukiambiwa we ni boyfriend haimaanishi uko peke yako/

    wadogo usoni wanahifadhi wazee wako/

    sijui ni dhiki au tamaa tu??/

    watoto wanaanika njaa tu/

    hawafikirii mapenzi wanachoona wao ni mkwanja tu/”

    Maneno haya yalinichoma moyo.Kijana huyu aliimba vitu vya kweli kabisa na yote aliyoyaimba yamenikuta mimi.

    Nikarudi tena chumbani sikujua nini cha kufanya.Nilikuwa kama nimechanganyikiwa vile.Nikaona ni bora nijilaze kitandani na kijiusingizi kikanipitia.

    Nilistuka na mlio wa simu iliyokuwa kichwani kwangu,alikuwa ni Chris.

    “ Haloo” Nikasema

    “Wayne umelala?”

    “Ndiyo nilikuwa nimelala”

    “Ok .Sasa wayne naomba uwe na moyo mgumu na usihamaki tafadhali.Ni kwamba Emmy amenifuata na hapa nilipo niko naye na ni yeye ndiye alinisisitiza nikupigie simu hii.”

    “Unasemaje Chris????? “Nikasema kwa ukali.Sikutegemea kusikia kitu kama kile.

    “Wayne niko na Emmy hapa.amenitafuta na kuomba nafasi ya kuongea na wewe”

    “Chris…………..”Nilidakia,sikutaka aendelee tana kunipa habari za yule baradhuli

    “Chris tafadhali.Kama na wewe unataka tukosane hamna shida ila tafadhali naomba usinipe habari zozote kuhusu huyu mwanamke.”

    Nikakata simu.Mwili wote ulikuwa unanichemka kwa hasira.Sikutaka kumsikia tena emmy katika maisha yangu.Nilikuwa na hasira mbaya mno kwa kitendo alichonifanyia na kama angekuwa karibu yangu sijui hata ningemfanya kitu gani.



    “Hana haya mwanamke huyu.Kwa hiki kitu alichokifanya halafu leo anataka kuongea na mimi!! Aongee na mimi kitu gani? Kwanza si ana nguo zake humu .Zote nazipiga moto.Sitaki kumuona tena machoni mwangu huyu mwanamke.Amenifanyia kitendo cha kikatili sana.”

    Nikalifungua kabati kwa hasira na kuanza kutoa ngo zote za Emmy.Nyingi nilimnunulia mimi mwenyewe na ni nguo za thamani kubwa.

    “Nguo zote hizi nimegharamia hela nyingi kumbe alikuwa akiniona mimi mjinga namna hii…….”

    Nikazikusanya zote na kwa hasira nikaenda nazo katika shimo la taka taka na kuzichoma moto.Sikuondoka mpaka nikahakikisha zimeteketea kabisa .

    Nikarudi sebuleni na kuangalia kama kuna kitu chochote kinachoweza kumuhusu Emmy,nikaiskia geti linagongwa.haraka haaka nikafuta uso na kujiweka vizuri ili mtu asije gundua nilivyosawajika.

    Nilifungua geti na kukuta ni rafiki yangu anaitwa Erasto.

    “karibu Erasto “ilijilazimisha kuchangamka.

    “Ahsante sana wayne”

    “Nimekuja kukujulia hali ,niliambiwa na akina mangi jana ulipata matatizo ukalazwa hospitali” Akasema Erasto tukiwa tumekaa sebuleni

    “Ndiyo,jana nilipatwa na matatizo ya mstuko nikaanguka na kupoteza fahamu.Ni mambo ya uchovu.Si unajua tena ,mambo yamekuwa mengi sana.” Nikadanganya.Sikutaka mtu yeyote agundue kilichotokea kati yangu na Emmy

    “Du! Pole sana.lakini hivi sasa unaendeleaje?

    “Kwa sasa naendelea vizuri.Madaktari wamenipima na hakuna tatizo lolote,wameniomba niongeze muda wa kupumzika.”

    Nilishukuru kwa erasto kuja kunitazama kwani kidogo kichwa changu kilitulia.Tuliongea na kucheka nikaona kichwa kinakuwa chepesi.Mida ya kama saa nane hivi Chris naye akaja akiwa amefungasha chakula,tukajumuika wote kula.Kwa masaa haya machache nilifarijika sana na kujiona kama vile sina matatizo.

    Ilipata saa kumi na moja jioni tukiwa katika maongezi na rafiki zangu ,geti langu likagogwa.Nikainuka na kwend akumuona mgongaji.Nilistushwa na ujio usio wa kawaida wa mwalimu wangu wa dini.katekista Nzomola ndiye mwalimu wetu aliyetufundisha mafundishoya ndoa mimi Emmy na watu wengine kama nane hivi.

    “Ouh Mwalimu,Shikamoo” Nikamsalimia kwa furaha,sikutaka kuonyesha aina yoyote ya mstuko kwa ujio wake.hajawahi kuja nyumbani kwangu hata mara moja.

    “Marahaba Wayne.Habari za Jumapili?

    “Nzuri katekista.”

    “Leo sijakuona kanisani,hata mwenzio naye sikumuona “

    “Leo sikuwa najisikia vizuri ndio maana sikuja.Si unajua mwalimu nyakati hizi mambo yanakuwa mengi “

    Katekista akatabasamu.nikamkaribisha ndani.Nikamtambulisha kwa Chris na Erasto amabo baada ya kuona nimepata mgeni wakaaga na kuondoka.

    “Ndio mwalimu karibu sana.hapa ndio nyumbani kwangu.”

    “Ahsante nimeshakaribia.”

    Kimya kikapita cha kama dakika moja hivi ,katekista akaanzisha maongezi

    “Wayne nimekuja hapa ili tuzungumze juu ya matatizo yaliyotokea”

    Kauli ile inanistua.

    “Matatizo?” yapi hayo” ikauliza

    “yaliyotokea kati yako na mwenzako”

    “nani kakwambia kuna matatizo? Nikauliza tena

    “Mwanzako amenifuata nyumbani .Tangu saa saba mpaka mida hii ndio tumeachana.Amekuja analia na kutaka tukae tuyaongee masuala haya”

    Nilimtazama mwalimu yule kwa hasira mpaka akaogopa.

    “Mzee Nzomola nakuheshimu mno kama mzee wangu,umenijenga sana kiroho.Lakini kwa hili lililotokea naomba usiingilie kabisa.Hakuna kitu tunachoweza kuongea hapa.Halafu mpaka hapa nilipo kichwa changu bado hakijatulia,bado nina hasira na hatuwezi kuongea lolote na tukafikia muafaka .Mzee wangu naomba uniache kwanza nitulie halafu kwa heshima yako nitakuita mimi mwenyewe tutakaa ,tutaongea.Usione kama nimekudharau mzee wangu ,hali niliyonayo sasa hatuwezi kuongea tukafikia muafaka.Niachie siku mbili tatu,kichwa kitulie halafu nitakutafuta mimi mwenyewe.Nakuahidi hivyo.”

    Nashukuru mzee Nzomola alinielewa na akaondoka.

    Jumatatu sikwenda kazini,nilituma taarifa kwa wakuu wangu wa kazi kuwa ninaumwa.Mida ya kama saa tano nikiwa nimepumzika sofani nikitafakari simu yangu inalia.Nikaangalia mpigaji alikuwa ni baba mkwe yaani baba yake na Emmy.Niliiangalia simu ile ikiita na kukata ,ikaanza kuita tena.Nilikuwa na hasira na sikutaka kusikia lolote juu ya Emmy.Mwishowe nikakata shauri niipokee tu.

    “Haloo mzee shikamoo”

    “Nzuri baba hujambo?”

    “Sijambo mzee wangu ,sijui nyie mnaendeleaje?

    “Sie huku wazima.Vipi ali yako kwa sasa unaendeleaje?

    “Naendelea vizuri tu mzee.Nashukuru Mungu”

    Kimya kikapita cha sekunde kadhaa ,halafu akasema.

    “sasa Wayne nimekupigia simu hii nilikuwa na maongezi na wewe ya muhimu sana.Tafadhali ni muhimu mno.Uko kazini?

    Nikasita kujibu ,nilijua hakuna kingine kinachoongelewa hapa zaidi ya suala la Emmy.

    “Niko nyumbani mzee” Nikajibu kwa ufupi.

    “Ok vizuri .Basi nitakuja mida ya saa kumi za jioni ili tuongee mwanangu.Tafadhali naomba unisubiri”

    “Sawa mzee wangu nitakusubiri hapa hapa nyumbani”

    Nikakata simu na kuirushia katika kiti.Nadhani hata huyu mzee aligundua kuwa sikuwa katika hali yangu ya kawaida.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    * * * *



    Saa Tisa kama na nusu hivi za jioni nikasikia honi ikipigwa nje ya geti langu.Nilikuwa nimejilaza chumbani nikaamka na kwenda kufungua mlango.Ilikuwa ni gari ya baba yake Emmy pamoja na gari nyingine mbili jumla gari tatu.Nikawakaribisha ndani.Sikutegemea kama kungekuwa na ujumbe mkubwa vile.Watu zaidi ya kumi.Wengine nilikuwa nawafahamu kama shangazi yake zake Emmy na baba zake wadongo lakini wengine ikawa ni mara yangu ya kwanza kuwaona.Kwa picha ile ya ule ugeni nilielewa dhahiri kuwa hapa linaloongelewa ni suala langu na Emmy hakuna lingine.

    Katika friji kulikuwa na vinywaji,hivyo nikamkirimu ila mmoja na kinywaji alichohitaji.

    Nilisikia wakiongea kichaga,kana kwamba walikuwa wakielekezana jambo.Halafu mzee mmoja mwenye mvi na kitambi akakohoa kidogo na kusema.

    “Bwana Wayne tunashukuru sana kwa ukarimu wako na kwa jinsi ulivyotupokea.hatukutegema kabisa kama ungeweza kutukirimu kwa upendo namna hii.Unaowaona hapa mbele yako ni baba,mama ,mashangazi na wajomba wa mchumba wako emmy”

    Alipotaja neno “mchumba wako Emmy” nikauma meno kwa hasira,nikainama chini.Nafikiri hata wao waligundua kitu.

    “Bwana wayne kwa ufupi tumekuja hapa sisi kama wazazi wa emmy ili kujaribu kuweka sawa mambo yaliyotokea.Hatukuwa tunajua nini kinaendela.Sisi tulikuwa katika maandalizi ya harusi.hatukujua kilichojificha nyuma ya pazia.Jana usiku ndio baba yake akatupigia simu na kutukusanya na kutueleza kuwa kuna tatizo limetokea.Emmy alitueleza yote mwanzo hadi mwisho bila kuficha hata kitu kimoja.Kwa kweli tulistuka sana sana.mama yake presha ikapanda ikabidi apelekwe hospitali.Tunashukuru Mungu hali yake imeendelea vizuri na mpaka sasa tunaye hapa.Kwa kweli kwanza sisi kama wazazi na wanafamilia ya Emmy tunakupa pole sana kwa yaliyotokea na vile vile tunakupongeza kwa ujasiri na uvumilivu wako.Umeonyesha uvumilivu na busara ya hali ya juu sana.Angekuwa ni mtu mwingine sijui tungekuwa tunaongea nini saa hizi.Ni wazi angefanya mambo ya ajabu sana.”

    Akatulia akakohoa kidogo halafu akaendelea.

    “ Wayne narudia tena kuwa hata sisi suala hili limetuuma mno.hatukutegemea kama tungepata aibu ya namna hii.Hii ni aibu kubwa na hata kuja kukuona na kuongea na wewe leo hii ni kwa sababu hatuna jinsi.Lengo letu kubwa la kuja hapa sisi ni kujaribu kuona nini tufanye ili kuweza kuokoa kile ambacho tumekwisha kianza.pamoja na kuwa inauma na bado una hasira lakini najua ndani kabisa ya moyo wako bado kuna kiasi Fulani cha upendo kwa emmy.Emmy Amelia sana na kuomba msamaha mno na kuahidi kuwa amekwisha achana na yule mtu wake aliyemsababishia haya yote.Amelia sana na ametutuma tuje sisi kama wazee tuombe msamaha kwa niaba yake .pamoja na shetani aliyepita kutaka kuvuruga mipango mizuri ya mbeleni ya maisha yenu lakini nina tumaini kuwa bado kuna kila dalili ya upendo wa kweli kati yenu.Suala la nyumba ni gumu na mambo kama haya huwa yanatokea.hakuna nyumba inayokosa majaribu na misuko suko.Na mnapojaribiwa ni wazi yupo atakayeanguka au mkaanguka wote.lakini sikuzote upendo wa kweli husimama panapo majaribu na hata mkijaribiwa mwisho wa siku mtabaki mnapendana na kusimama imara.Sikuzote wapendanao kweli hata kama wakianguka hushikana mikono ,wakasimama na kusonga mbele.Upendo wa kweli siku zote haushindwi na lolote.Ninaona picha ya upendo wa kweli ulio kati yenu.Ni upendo hu wa kweli ndio uliokuzuia kufanya lolote mpaka leo hii.Roho wa Mungu yuko pamoja nawe na ndiye anayekuongoza katika kufanya maamuzi haya yenye busara.kwa maana hiyo Wayne sisi wazee wako tumekuja rasmi kama wazazi kukuangukia na kuomba msamaha na kufuta kila kilichotokea ,tusimame pamoja tushikane mikono na tusonge mbele.Tumekosa sisi tunaomba utusamehe sisi.Emmy yuko tayari kuja kuomba msamaha mbele yetu sisi wazee wake.hatukuweza kuja naye mpaka tutakapoongea na wewe na tuone kama utakuwa tayari kumsamehe mwenzako”

    Akamalizia mzee yule ambaye alikuwa akiongea kama mchungaji vile.Sijui wazee hawa walikuja na nini manake nilijisikia maneno yao yakiniingia moyoni na kujikuta licha ya hasira nilizokuwa nazo kutaka kumsamehe Emmy.Kuna wakati ulikuwa unakuja moyo wa kusamehe lakini papo hapo inakuja picha ya Emmy akiwa amekumbatiana na lile libaba.Ikija picha hii hasira zinarudi tena.

    Niliinua kichwa niliposikia baba yake Emmy akikohoa na kutaka kuongea machache.

    “Wayne mwanangu,na mimi naona niongezee machache katika yale aliyoyasema mkubwa wangu.Kwa kweli pamoja na uzee wangu huu nilikuwa nimeishiwa maneno ya kusema ndio maan nikamuachia mkubwa wangu.Ameeleza kila kitu na sitaki kurudia yale aliyoyasema ila nata kusema machache kuwa Emmy ni binti niliyemlea katika maadili mazuri ya kiroho na kwa kweli alikuwa ni binti mwenye heshima kubwa.Sikutegemea kwa jinsi nilivyomlea aje afanye yale aliyoyafanya.Ndio maana hata mama yake aliposikia mambo haya presha ikapanda kwa sababu hatukumlea awe mtu wa namna hii.Nina imani tabia hii aliyoifanya ni mambo ya tamaa na kuiga.Tena ni baada ya kutoka nyumbani.Pale alipoanza maisha yake ya kujitegemea.Mwanzoni alipotaka kuhama nyumbani na kwenda kuishi mwenyewe nilikataa kwa kuhofia asije akaambukizwa kufanya mambo yasiyofaa katika jamii lakini aliomba sana kuwa anataka ajifunze maisha ya kuishi mwenyewe ndipo nikamruhusu.Hii si tabia yake hata kidogo.Hakuwa na tabia hizi.Ni tamaa tu ya kuwa na pesa na vitu vizuri vizuri.Toka akiwa mdogo nilimfundisha kutambua mara moja anapokosea na kuomba msamaha.Kweli amelitambua kosa alilolifanya na kuomba msamaha.Mimi kama baba yake nilikataa kabisa kabisa kuishughulisha tena na masuala yake baada ya kusikia aibu aliyoifanya.Aliniomba sana sana nimsamehe na nimsaidie kuomba msamaha kwako.Kwa macho yangu niliona katika macho yake kuwa alikuwa akimaanisha toba ya dhati.Ni hilo ndilo lilinisukuma mie nimsamehe na kunifanya nifike hapa leo pamoja na wenzangu hawa kuomba msamaha kwa niaba yake kwanza na baadae yeye mwenyewe atafika hapa na kuomba msamaha kwako mbele yetu.Wayne hatutaki katika hatua kubwa mliyofikia mshindwe kuendelea.Mkisameheana katika hili nina imani mtakuwa mmejenga kitu kikubwa sana na nyumba yenu itajengwa katika kusameheana hata likitokea kubwa la aina gani.Kwa hayo machache Wayne mimi kama baba yake naomba sana niko chini ya miguu yako msamehe mwenzio na muendelee na mipango yenu ya ndoa kama kawaida.”

    Baada ya baba yake Emmy kumaliza kuongea akafuata shangazi yake na baba zake wadogo.Du ! niliombwa kila aina ya msamaha.Kila aina ya ushawishi ilitumika ili niweze kumsamehe Emmy.Kwa kweli sijui wazee hawa walikuwa na kitu gani manake niliwasikiliza na kujikuta ninakuwa na moyo mweupe tena wa kumsamehe Emmy.Pamoja na kwamba zile picha mbaya zilikuwa bado zikinijia nilijawa na moyo wa kusamehe.Hatimaye ikaja zamu yangu kuongea.Kila mmoja akatulia kutaka kunisikiliza nitasema nini.

    “wazee wangu nimewasikilza vizuri.Ujio wenu leo umenipa faraja sana.Sijui mmekuja na kitu gani lakini kwa kweli najiona mwepesi na mwenye furaha sana.Mmenisaidia kuutua mzigo mzito niliokuwa nimeubeba.Ahsanteni sana.Wazee wangu kwa kweli lililotokea ni pigo kubwa kwa moyo wangu.Nimeumia sana.Kwa kweli sikutegemea jambo kama lile kutokea kwa mtu kama Emmy tena kwa wakati kama huu.kama mzee pale alivyosema ni kwa maongozi ya Mungu niliamua kutumia busara zaidi katika suala hili.Sijamueleza mtu yeyote zaidi ya rafiki yangu wa karibu.Sikuwa na haraka ya kutaka kuutangazia ulimwengu nini Emmy kafanya.Sikutaka dunia imchukie.naamini kama mzee alivyosema ni tamaa za pesa ,mali na vitu vizuri vizuri ndio ilmponza.Iwapo ningeamua kumdhalilisha Emmy kwa kutangaza aliyoyafanya ,nisingekuwa nafanya hivyo kwake tu bali hata kwa wazee wake waliomlea katika madili mema,ndugu zake,ndugu zangu na hata wazazi wangu .Pamoja na yote yaliyotokea,machungu yote niliyoyapata,maumivu ya ndani na nje,bado ninathubutu kusimama nakutamka mbele yenu wazee wangu kuwa nimemsamehe Emmy na niko tayari kurudiana naye tena na mipango ya ndoa yetu kuendelea kama kawaida”

    Hawakuamini ,wakanitaka nirudie tena kauli yangu.Nikarudia tena na kuwahakikishia kuwa Emmy nimemsamehe kwa moyo mmoja na wala sina kinyongo naye tena.

    Wazee wakainuka na kuja kunipongeza.Kilikuwa ni kipindi cha furaha sana.Baada ya kupongezana baba yake mkubwa Emmy akasimama na kusema.

    “Wayne wewe ni kijana wa ajabu .Katika kuishi kwangu mpaka nimefika uzee huu sijawahi kuona mtu mwenye moyo wa ajabu kama wako Wayne.laiti dunia ingekuwa na vijana 100 kama wewe basi pangekuwa ni sehemu nzuri sana kwa kuishi.Mimi binafsi sijui hata niseme kitu gani.Sijui hata nikushukuru vipi kwa ujasiri wa kumsamehe mwenzako.Narudia tena kijana unaongozwa na roho wa Mungu.Kwa ulimwengu wa sasa si rahisi mtu kumsamehe mwenzake aliyemfanyia kitendo kama alichokufanyia emmy.Ahsante sana kijana.ahsante sana wayne”

    akanishika mkono tena.Akawageukia wazee wengine na kuwaambia kuwa ni wakati muafaka kwa Emmy kuitwa .Ikapigwa simu na baada ya kama dakika kumi hivi Emmy akaingia ndani.Moyo wangu ukastuka tena baada ya kuiona sura ya Emmy ikiwa na macho mekundu yaliyovimba ikiashiria jisni alivyokuwa akilia.hakutaka kuniangalia usoni.Uso wake alikuwa kuinamisha chini.Nilishindwa kuwa na hasira nikamuonea huruma.

    Baba mkubwa wa Emmy akasimama na kuongea machache.

    “Kijana wetu Wayne,na ndugu wote ambao mko hapa leo,napenda kuchukua nafasi hii kuongea machache kwa sababu mengi yamekwisha semwa na nisingependa kuyarudia tena.Tumemsikia kijana wetu alivyosema.Toka ndani ya moyo wake amekubali kumsamehe Emmy .Kwa kuwa kijana wetu Wayne si mtenda kosa basi hatuna budi sasa kumpa nafasi mtenda kosa yeye mwenyewe kwa mdomo wake akiri kosa na kuomba msamaha kwa mchumba wake,wazazi wake na kwa Mungu wake.Emmy uwanja ni wako ,waangukie wazazi wako uwaombe msamaha pamoja na mchumba wako”

    Kimya kikatanda mle sebuleni.Emmy huku akilia akainuka na kwenda kupiga magoti mbele ya baba yake na kulia akiomba kusamehewa.Baba yake akamshika kichwa na kumuombea kwa Mungu amsamehe na kumtangulia katika kila jambo alifanyalo,halafu akatangaza kuwa tayari amemsamhehe mwanae kwa kosa alilolifanya.Emmy akaenda tena kwa mama yake na kuomba msamaha kama alivyofanya kwa baba yake.Naye halikadhalika akamsamehe.Kazi ikawa kwangu.Akasita kuja kwangu pale tulipogonganisha macho.Nadhani ni nafsi yake ilikuwa ikimsuta kwa mambo aliyoyafanya.Wazee wake wakamuangalia kwa ukali hali iliyomlazimu kujikaza kisabuni na kunisogelea.akapiga magoti mbele yangu na kunishika miguu.

    “Wayne, nakosa hata neno la kusema.Nashindwa nikwambie kitu gani cha kuweza kulifuta doa nililoliweka moyoni mwako kwa tamaa zangu.Nimekuumiza Wayne,na sistahili hata huruma yako.lakini pamoja na hayo yote niliyokufanyia naomba ufahamu kitu kimoja kuwa toka ndani ya moyo wangu bado nakupenda sana na ninaomba msamaha wa dhati kabisa .Naomba unisamehe na tuendelee na mipango yetu ya ndoa kama tulivyokuwa tumepanga.naahidi sintafanya tena kosa kama hili katika maisha yangu.nakuahidi kuwa mke mwema kama utanisamehe.naomba msamaha wako Wayne..”

    Emmy macho yalikuwa yamejaa machozi,akilia kwa kosa alilokuwa amelifanya.Hata mimi ilikuwa ikiniuma sana na nilikuwa nikijiuliza mara mbili mbili kama ni kweli nimeamua kwa dhati kumsamehe? Nikakubaliana na moyo wangu kuwa nikubali kumsamehe.Nikamshka mkono nikamuinua na kumtazama usoni.

    “Emmy,nakubali ulinikosea.Lakini kama tunavyofundishwa kila siku nav iongozi wetu wa dini na kama maandiko yanavyosema kuhusu kusamehemana,mimi kwa moyo wangu wote nimekubali kukusamehe.Nakuombea kwa Mungu naye akusamehe na tuendelee na mipango yetu ya ndoa kama kawaida “

    Maneno yale machache yakampa Emmy faraja kubwa na kumfanya ainuke na kunikumbatia kwa furaha.Sebule yangu ikageuka sehemu ya furaha kubwa.Watu tukashikana mikono na kupongezana.Lilikuwa nitukio kubwa na la kihistioria katika maisha yangu.Vinywaji vikaletwa tukaendelea kuburudika hadi ilipotimu saa mbili za usiku tukaagana wakaondoka.Walipoondoka nikabaki mwenyewe nikitafakari juu ya kilichotokea.Pamoja na kumsamehe Emmy lakini bado roho yangu haikuwa ikimtazama kama nilivyokuwa nikimtazama hapo zamani.

    “Hivi ni kweli roho yangu imekubali kwa dhati kumsamehe Emmy kwa kitu alichonifanya?? Nikajiuliza tena kwa mara ya pili.Saa chache zilizopita sikutamanai kkumuona tena Emmy katika maisha yangu kuokana na kitendo kile lakini sasa nimeamua kumsamehe.

    “Kwa vile nimamua kumsamehe acha tu nimamehe.Nahisi amekiri toka moyoni mwake.”Nikajisemea mwenyewe.

    Maisha mapya yakaanza tena.Penzi letu likaonekana kama vile limechipua upya.Upendo ukaongezeka mara dufu.Enmmy alionekana kubadilika sana na hiyo ikanihakikishia kuwa hawezi kurudia tena kosa alilolifanya.

    Taratibu jeraha lililokuwa moyoni mwangu likaanza kufutika.Nikaanza kusahau yote yaliyokuwa yamepita.





    Ni siku yetu ya kufunga ndoa.Sikuweza kupata usingizi usiku mzima.Nilikuwa nikiwaza kama ni kweli baada ya kupitia msuko suko mkubwa hatimaye ninakwenda kufunga ndoa.Ilikuwa ni kama ndoto.

    Asubuhi nilikuwa ni mtu mwenye mawazo na wasi mwingi.Mpambe wangu aliliona hilo ,akajaribu kunitoa wasi wasi na kunifanya nichangamke.Kwa mara nyingine tena nikajikuta niukijiuliza kama ninalokwena kulifanya leo hii ni sahihi na nina uhakika nalo.Baada ya tafakari ya kina nikaona hakuna haja ya kuendelea kujiuliza maswali mengi.Maji nimekwisha yavulia nguo hivyo sina budi kuyaoga.

    “mwenzangu,pokea pete hii iwe ishara ya upendo na uaminifu kwako.Kwa jina la baba nan mwana na la roho mtakatifu.Amina” Nilitamka maneno haya huku nikimvisha pete ya Ndoa emmy kama mke wangu halali mbele ya kanisa lililofurika watu wakiwa kama mashahidi.Wakati nayatamka maneno haya bado ndnai ya nafsi yangu kuna kitu kilikuwa kikiniuliza “Wayne are you sure with what you are doing? Sauti ile ilikuwa ikiniuliza kama ninayatamka manenoyale kwa dhati toka moyoni mwangu..Sikuijali sana sauti ile ,kwa sababu nilijua nimekubali kwa dhatiya moyo wangu kufunga ndoa na Emmy.Niliamini mwangwi ule ulitokana na tukio lililotokea na ambalo bado jeraha lake halijapona sawa sawa..Tukio ambalo kusema ukweli haliwezi kufutioka kiurahisi.

    Baada ya kumalizika kwa shughuli za kanisanii,shghuli kubwa ikafanyika ukumbini.Ilikuwa ni sherehe ya aina yake na kila mmoja aliyehudhuria alisuuzika moyo.Saa sita za usiku tukaondoka ukumbini na kuwaacha bado watu wakishereheka,tukaenda katika hoteli tuliyoandaliwa maalum kwa ajili ya kulala kwa usiku huo kabla ya kuelekea katika fungate letu tuliloamua kwenda Zanzibar.

    Huo ukawa ni usiku wetu wa kwanza kama mke na mume.Ni usiku huo ambao naweza nikasema kuwa maisha yangu yalianza upya.



    * * * *



    Maisha ya ndoa yalikuwa mazuri na yenye furaha.Nilionyesha kila aina ya upendo kwa Emmy.naye hali kadhalika alionyesha upendo wa kila namna kwangu ilimradi ilikuwa ni furaha na mashamsham kila siku.Kila asubuhi ni kama penzi letu lilianza upya.Miezi hii sita ya kwanza sikuona kitu chochote kibaya cha kunikwaza na ambacho kingenifanya niseme ule msemo uliozoeleka wa ndoa ndoano.Sikuyaona magumu ya ndoa.Niliwashangaa wale wote wanaodai kuumizwa na ndoa zao.Sikuelewa ni kwa nini wengine hawakutaka kabisa kusikia kitu ndoa.Kwa furaha niliyokuwa nayo nikwa ndani ya ndoa sikuweza kufikiri kama iko siku ninaweza kutembea nje ya ndoa.Niliwashangaa wale watu ambao wamekuwa na wapenzi nje ya ndoa zao.Sikuhitaji mpenzi wa nje kwa sababu nilipata kila kitu nilichohitaji toka kwa mke wangu Emmy.Kwa muda huu mfupi nikanawiri na kuvutia zaidi.Nikawa mshauri maarufu wa kuwashauri vijana wenzangu ambao bado walikua wakisita na kuogopa ,kufanya maamuziya kufunga ndoa kwa sababu ndoa ni tamu ajabu. .Nilitolea mfano wa raha nizipatazo mimi .

    Mwezi wa saba toka tufunge ndoa Emmy akanitaarifu kuwa tayari alikuwa mjamzito.Hii ikaongeza furaha na upendo mara dufu ndani ya familia yetu.



    Furaha hii haikuwa tu baina yetu bali hata kwa ndugu na jamaa zetu.Nilimshukuru Mungu kwa kunipa mke kama Emmy.Nilimpenda mno mke wangu na hasa katika kipindi hiki cha ujauzito.Siku zikazidi kusonga na hatimaye siku ya kujifungua ikafika na Emmy akafanikiwa kujifungua mtoto mzuri wa kiume aliyekuwa na afya bora.Nilifurahi kupita kiasi kwa zawadi ile ya mtoto.Ndugu ,jamaa na marafiki wakaungana nasi katika furaha ile kubwa ya kupata mtoto.Kwa furaha niliyokuwa nayo nilimzawadia Emmy zawadi ya gari jipya kabisa kama shukrani zangu kwake kwa kumleta duniani mtoto wetu mpendwa ambaye nilipendekeza aitwe Baraka.niliamini mtoto yule alikuwa ni baraka za mweneyezi Mungu kwetu.Emmy akafurahi mno kwa zawadi le niliyompa.

    Ukurasa mpya wa malezi ukaanza nikiwa baba na Emmy akiwa mama.Nilifurahi kushirikiana na mke wangu katika malezi ya mwanetu Baraka.Muda wa mapumziko ya uzazi ulipokwisha ikatyulazimu kumtafuta msaidizi atakayetusaidia kumlea mtoto wakati tukiwa kazini.Tulifanikiwa kumpata msaidizi kwa msaada wa jiani yetu.

    Siku zilikatika kama mvua na ikafika miezi sita.Tukajadili tukaona kuwa huo ndio muda unaofaa kwa ajili ya kumbatiza mwanetu.maandalizi yakafanywa na hatimaye tukafanikiwa kumbatiza mwanetu kwa jina la baraka.Mtoto akaendelaa kukua akiwa na afya njema mno.



    * * * *



    Miaka minne ilipita.Maisha yakiwa ni yenye furaha na upendo mkubwa.Mtoto wetu baraka alikuwa anasoma katika shule ya awali ya Maria Theresa academy.Baraka alikuwa akiendelea kukua kwa furaha na upendo mkubwa.

    Kwa muda wa miaka yote hiyo hali ya upendo ndani ya ndoa yetu ilikuwa kubwa na hii ilitufanya tuwe mfano wa kuigwa.Nilikwisha sahau yote yaliyotokea kipindi cha nyuma.Nilichokuwa nikiangalia kwa sasa ni malezi ya mtoto wetu na kumtengenezea maisha mazuri ya baadae.

    Ilikuwa siku ya Ijumaa siku ambayo sikuwa na shughuli nyngi za kufanya nikaamua kuwahi kurudi nyumbani ili kujumuika na famili na yangu .Siku zote huwa nikipata nafasi hupendelea kuwahi kurudi nyumbani na kuitumia nafasi hiyo nikiwa na familia yangu tukifurahi pamoja.

    Nikiwa mita kadhaa kabla ya kufika nyumbani kwangu nikaona geti likifunguliwa na gari ya mke wangu ikitoka.Tulipokutana akasimamamisha gari,akashusha kioo tukasalimiana.

    “Hello Darling” akasema mama Baraka

    “Hello honey” nikajibu

    “Mbona leo mapema hivi kulikoni? Akauliza

    “Nimeamua kuja kukaa na familia yangu.Sikuwa na kazi nyingi.Safari ya wapi tena? Nikauliza

    “Kuna mama mmoja jirani yetu ni mjamzito sasa ameanguka ghafla ndio tunataka tumkimbize hospitali”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ouh ! basi wahini mara moja.” Nikajibu naye akaliondoa gari kwa kasi kumuwahi mgonjwa..Nikaingiza gari ndani nikasalimiana na mwanangu Baraka halafu nikamwacha akicheza mimi nikaelekea chumbani kwangu.Kitandani kulikuwa na kompyuta aina ya Laptop ya mke wangu.Kwa kuwa nilikuwa nikihitaji kupumzika nikaamua kuitoa na kuiweka pembeni.Kompyuta ile ilikuwa imechomekwa katika umeme na ilionyesha kuwa muda mfupi uliopita alikuwa akiitumia.Kwa haraka haraka nikaona kama alikuwa akiwasiliana na watu wake kwa kutumia Yahoo messenger.Kuna meseji ilikuwa ikikonyeza kuashiria kuwa haikuwa imesomwa,nikang’amua kuwa Mama Baraka alikuwa ameondoka ghafla na kumfanya asahau kuizima kompyuta yake.Nikaamua kufunga ile Yahoo messenger ili watu wale aliokuwa akiwasiliana nao wajue kuwa hayupo.Kabla sijaifunga kabisa ile Yahoo messenger,nikaliona jina moja limeandikwa My special one.nikapata udadisi Fulani.Nikafungua ule ukurasa waliokuwa wakiwasiliana nikaanza kuusoma .Meseji ya mwisho ilisema

    “Vipi Darling mbona kimya? Are you there??”

    Baada ya meseji hiyo zikafuata BUZZ nyingi..Nilikuwa nimesimama nikaamua kukaa na kusoma sawa sawa.Nikaanza kuisoma tokea mwanzo.Kutokana na muda ilionyesha kuwa walikuwa wameanza kuwasiliana kama dakika ishirini zilizopita.Mfululizo wa mawasiliano yao ulikuwa hivi

    EMMY: Nimeshafika nyumbani dear

    MY SPECIAL ONE : Ouh ! good.Mimi bado niko ofisini

    EMMY: Unatoka saa ngapi leo

    MY SPECIAL ONE : Leo nitachelewa kutoka kidogo.

    EMMY: Ok poa Darl ,sasa hebu tuendelee kujadili lile suala la mtoto manake mimi linalipa wakati mgumu sana

    MY SPECIAL ONE: Darl ni kama nilivyokueleza kuwa mtoto ni lazima nikamtambulishe kwa babu zake.Nataka mtoto aanze kunizoea taratibu ili hata baadae akielezwa kuwa huyu ndiye baba yako mzazi asishangae.Nataka aanze taratibu kuwafahamu ndugu zake.

    EMMY: Darl unanipa wakati mgumu sana.Nashindwa hata nifanye nini

    MY SPECIAL ONE: Usiogope Darl.Unajua mtoto anakua kwa kasi na anazidi kupata akili.Kwa maana hiyo inabidi aanze kujua toka mapema ,nani baba yake nani siye.Nashukuru kwa ile safari ya mbuga za wanyama imeniweka karibu naye sana.

    EMMY: Yah hata mimi nimefurahi kwa hilo kwa sababu kila siku ni lazima akuulizie.

    MY SPECIAL ONE: Hivyo ndivyo ninataka.Jaribu kwa kadiri uwezavyo kumuweka karibu zaidi na mimi.

    EMMY: Nakubali Honey mtoto ni wako lakini siku huyu jamaa akigundua najua ataumia mno.Hujui ni jinsi gani anavyompenda Baraka

    MY SPECIAL ONE: Yah ! I now that.Ni wazi ataumia lakini hakuna jinsi.Ni lazima ifike mahala akubaliane na ukweli kuwa mtoto si wake.Na kwa kweli darling sitaki tuendelee kulificha hili kwa muda mrefu.nataka ifike wakati tuchukue uamuzi wa kumueleza ukweli kuwa mtoto si wake.Tukiendelea kukaa kimya tutakuwa hatumtendei haki mtoto.

    EMMY: Lakini darling ni wazi siku Wayne akiufahamu ukweli hakutakuwa na jingine zaidi ya kuachana.Niliwahi kumuumiza mara moja miaka kadhaa ya nyuma na nikamuahidi kuwa sintamuumiza tena.Sasa akigundua hili sijui nini kitatokea.

    MY SPECIAL ONE: Honey usijali kitu chochote.bado naendelea kuweka mazingira mazuri ili kama kutatokea la kutokea pindi utakapomueleza ukweli basi moja kwa moja unahamia kwangu na tunaanzisha familia,mimi ,wewe na mtoto wetu baraka.

    EMMY : (smiley) Are you sure darling?

    MY SPECIAL ONE :Yes baby I’m sure.Lengo langu mimi sikuzote limekuwa kuishi na wewe.Nataka kuishi na mwanangu.nataka mwanangu akasome Ulaya.Nataka siku moja sisi sote tukaishi Ulaya.

    EMMY : Ingawa nakupenda na niko tayari kufanya lolote kwa ajili yako lakini kila ninapomfikiria mume wangu nafsi inanisuta sana.Wayne ananipenda kupita maelezo.

    MY SPECIAL ONE: Usijidanganye baby kuwa mumeo anakupenda.Unachotakiwa ni kuangalia wapi unapata furaha ya maisha.Fuata moyo wako unavyokutuma.

    EMMY : Ok tuachane na hayo.Umepanga lini umpeleke mtoto kwa babu zake?

    MY SPECIAL ONE: Jumamosi ya wiki ijayo.Anza kuandaa tararibu mazingira ili

    Mumeo asiweze kugundua chochote.

    EMMY: Nitajitahidi darling

    MY SPECIAL ONE: Vipi weekend hii una ratiba gani?

    MY SPECIAL ONE: BUZZ

    BUZZ

    BUZZ

    BUZZ

    MY SPECIAL ONE : “Vipi Darling mbona kimya? Are you there??”

    BUZZ

    BUZZ

    BUZZ



    Mawasiliano yakaishia hapa.nadhani ni wakati huu Emmy alipopata taarifa ya ugonjwa wa jirani yetu na kumfanya aondoke ghafla bila hata kukumbuka kuizima kompyuta yake.Ilikuwa ni kama ndoto ya mchana.Sikuamini nilichokuwa nimekisoma,nikakaa vizuri na kurudia tena na tena .Nikafungua archive na kukuta kumbukumbu ya mawasiliano kati ya Emmy na my special one.Jasho lilikuwa likinitiririka,mapigo ya moyo yakaanza kwenda kwa kasi isiyoelezeka.Nikakaa kitandani huku nikihisi kuishiwa nguvu taratibu.



    No this must be a joke.Its not true” Nikasema mwenyewe huku nikijifuta jasho

    “Emmy cant do to me something like this” Nikasimama na kuzunguka zunguka mle chumbani ,nikapata wazo.Nikachukua flash disk yangu nikaichomeka katika ile kompyuta ya Emmy na kurekodi kumbukumbu zote za mawasiliano baina yake na huyo special one.baad ya hapo nikaiacha kompyuta ile kama ilivyokuwa .Sikutaka Emmy aje agundue kuwa nilikuwa nimezisoma meseji zake.Mambo yakle niliyoyasoma amabayo nilihisi ni kama utani vile ni makubwa na yalihitaji uchunghuzio wa hali ya juu.Nilipohakikisha kuwa hataweza kugundua kitu chochote nikatoka,na kwenda kukaa sebuleni.Sikuwa na nguvu hata za kuendesha gari.Nikaanza kutafakari yale niliyoyasoma.

    “MY SPECIAL ONE” Who is my special one? Nilihitaji kumfahamu huyo aliyeandikwa kama my special one.

    “I need to find out the truth.I’ll find out the truth.And if its true,you’ll cause me another pain … this will be BEYOND PAIN” Nikasema mwenyewe huku nikiuma meno kwa uchungu.

    Sikumbuki usingizi ulinipitia saa ngapi ila nilistuka kwa busu zito nililopigwa katika paji la uso.kwa haraka nikafumbua macho ,kumbe alikuwa ni mke wangu Emmy amerudi toka hospitali.Moyo ukastuka sana nilipomuona.Ghafla kumbukumbu ya nilichokisoma katika kompyuta yake ikaja kwa kasi .Hasira ikanipanda kwa ghafla sana lakini nikajikaza kiume na kuonyesha sura ya tabasamu ili kumfanya asiwe na wasi wasi.Sikutaka kupeleka mambo kwa haraka hadi pale nitakapokuwa na uhakika wa kutosha kama yale niliyoyasoma ni mambo ya kweli au si kweli

    “hello darling” Nikasema kwa sauti ya chini na ya uchovu

    “Ouh my love,mbona umenyong’onyea hivyo ,unaumwa? Akauliza emmy huku amekaa karibu yangu na kunishika kichwa.

    “Siumwi kitu honey ni uchovu tu unanisumbua” Niliumia tena moyoni kutamka neno honey.lakini kwa kuwa nimeshaamua kuliendea suala hili taratibu sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kuonyesha mapenzi kwa Emmy ili asije kung’amua kama ninafahamu lolote kuhusu siri zake.

    “Baba baraka kwa nini hujaenda kulala chumbani ?.Toka umerudi umelala hapa kwenye kochi ? Akauliza emmy

    “Kuna kipindi nilikuwa naangalia katika Tv nikajikuta nimepitiwa na usingizi.Vipi mgonjwa anaendelaje? Mbona mmewahi kurudi namna hiyo?

    Nikauliza na kumfanya Emmy ajibu kwa wasi wasi kidogo

    “Tumemfikisha hospitali ,nimeacha anashughulikiwa mimi nikaondoka”

    “Yaani mama baraka unaondoka na kuwaacha wenzako hospitali bila hata kujua mgonjwa anaendeleaje?

    “baba Baraka nilikuwa nakuwahi wewe,nilijua ungekuwa mwenyewe ungeboreka sana”

    Nilitabasamu baada ya kujua kuwa ananidangaya.Nafikiri alipofika hospitali alikumbuka kuwa hakuizima kompyuta yake na ndio maana akarudi haraka namna ile.

    “Ngoja nikabadili nguo nioge,pengine nitajisikia vizuri “Nikainuka kuelekea chumbani kwangu na kumuacha mama Baraka akiwa kwene sofa akionekana mwingi wa mawazo.Chumbani sikuikuta ile kompyuta yake kitandani ,alikuwa ameishaitoa na kuizima kabisa halafu akaifungia katika kabati lake.Nikatabasamu nikavua nguo na kwenda kuoga kisha nikarudi na kijilaza kitandani.Mlango ukafunguliwa Emmy akaingia,akanifuata pale kitandani nilikokuwa nimelala akanikumbatia na kunibusu.

    “Honey nikupikie chakula gani leo? Akauliza

    “Chochote utakachopika mi nitakula tu” Nikajibu huku nikitabsamu

    “Ok honey nitakupikia chakula kitamu ajabu.Halafu honey kuna jambo nataka tuongee”

    “Jambo gani hilo “ Nikauliza

    Emmy akakaa kimya akafikiri kwa sekunde kadhaa na kusema

    “unajua kuna rafiki yangu mmoja tuko naye ofisi.moja ana harusi ya mdogo wake jumamosi ijayo na inafanyikia nyumbani kwao Same .Ameniomba nimsindikize .Sijampa jibu lolote nikaona ni bora nije nikuombe ruhusa wewe..”

    Emmy akasema.

    Nusura chozi linidondoke baada ya kusikia maneno yale.Nilianza kuamini kile nilichokisoma .Emmy na mu aliyemwandika kama my special one walikuwa wamepanga kwenda nyumbani kwa huyo special one kumtambulisha Baraka kwa babu zake yaani baba na mama yake huyo special one.Iliniuma kupita kiasi.Nikakaa kimya nikifikiri nini cha kusema.

    “Darling niambie basi,utaniruhusu kwenda?” akasema Emmy

    Sikujibu kitu nikaendelea kufikiri

    “Honey say yes please” akanibembeleza Emmy.

    “hakuna shida ,waweza kwenda”nikajibu kwa ufupi.

    “Ouh honey thank you..mwaaahh” akasema na kunibusu mdomoni.akatoka na kuelekea jikoni

    “Ee Mungu kwa nini mambo haya yananikuta mimi? Nikawaza kwa uchungu huku machozi yakinilenga lenga.Nilikuwa nimejilaza kitandani ikanilazimu niinuke na kukaa.

    Kichwa nikaanza kukiona kizito mno.Mateso na maumivu niliyoyapata miaka kadhaa iliyopita yamerudi tena.

    “Daddy !!….’Nikastuliwa na sauti ya Baraka aliyekuwa amerudi toka shuleni

    “Ouh Baraka.umerudi ! Nikasema.

    “Ndiyo baba.pole na kazi”Akasema

    “ahsante mwanangu.Habari ya shule?

    “Nzuri baba”

    Mtoto hyu akaniongezea tena machungu.Nilimpenda Baraka kupita kitu chochote kile katika maisha yangu.

    “ This cant be.Baraka is my son” Nikasema kimoyo moyo.

    “daddy mbona unalia? Akaniuliza Baraka na kunifanya nistuke.Nilikuwa nimeshindwa kujizuia kutokwa na machozi nilipomuona baraka.

    “macho yananisumbua sana leo” Nikajibu na kujilazimisha kutabasamu.

    “Haya Baraka nataka nipumzike,nenda kabadili nguo halafu baadae uje unionyeshe umejifunza nini shuleni leo”

    “Ok Daddy” baraka akasema na kutoka mle chumbani.Nilimsindikiza kwa macho mtoto yule mzuri mwenye akili nyingi ,niliyemkuza katika adabu na tabia njema kiasi cha kumfanya kuwa mfano wa kuigwa mtaani na hata shuleni kwao.

    “Kwa nini Emmy anifanyie mimi mambo haya?Kwa nini anitese namna hii? Nikawaza.

    “.Ni lazima nifanye utafiti nigundue ukweli uko wapi..halafu huyu mtu anayemuita special one…Ni nani? Lazima nimfahamu mtu huyu”

    Mawazo yakawa mengi nikaona ni bora nikakae sebuleni .Nikaanza kutazama televisheni lakini hakuna kitu nilichokuwa nikielewa.Bado mawazo yangu yote yalikuwa katika suala zito linaloniumiza kichwa.Muda wa chakula ulipofika tukakaa mezani,tukala chakula huku nikijilazimisha kutabasamu na kucheka ili kumfanya emmy asihisi lolote.

    “baraka kesho ni weekend,siku ya mapumziko,right? Nikamuuliza baraka mara tulipomaliza kula chakula cha usiku.

    “Yes daddy ,kesho ni jumamosi’ Akajibu

    “Ok pretty boy,now take you guitar.We’re going to play out in the moon and have fun”

    Nilikuwa nimemfundisha Baraka kupiga gitaa.Naye kama mimi alikuwa mpenzi sana wa nyimbo za country.Kila mara tupatapo wasaa huwa tunakaa bustanini na kupiga magita yetu .

    Tukaelekea bustanini,mimi ,Baraka emmy na mbwa wetu aitwaye Chesa.

    “Daddy leo tunapiga wimbo gani? Baraka akauliza

    “Leo tunaimba I believe in you wa Don Williams.This song is special for your mother ,the love of my life.I want to show your mother how much I do believe in her” Nikasema na kumfanya Emmy atabasamu lakini nikagundua tabasamu lake lilikuwa na uoga ndani yake.

    “One,two,three….Tukaanza kupiga huku nikiimba.Nilikuwa mpigaji mzuri sana wa gitaa

    “I don't believe in superstars,

    Organic food and foreign cars.

    I don't believe the price of gold;

    The certainty of growing old.

    That right is right and left is wrong,

    That north and south can't get along.

    That east is east and west is west.

    And being first is always best.



    But I believe in love.

    I believe in babies.

    I believe in Mom and Dad.

    And I believe in you.



    Well, I don't believe that heaven waits,

    For only those who congregate.

    I like to think of God as love:

    He's down below, He's up above.

    He's watching people everywhere.

    He knows who does and doesn't care.

    And I'm an ordinary man,

    Sometimes I wonder who I am.



    But I believe in love.

    I believe in music.

    I believe in magic.

    And I believe in you.



    I know with all my certainty,

    What's going on with you and me,

    Is a good thing.

    It's true, I believe in you.



    I believe in Mom and Dad.

    And I believe in you…………………

    “Honey its enough.This song is so touching.” Emmy akanikatisha nisiendelee kuimba.Nilikuwa ninaimba kwa hisia kali sana huku machozi yakinitoka.Nilipomtazama Emmy naye alikuwa akifuta machozi.Nadhani hata yeye wimbo ule ulimgusa.

    Usiku ule ulikuwa ni moja kati ya usiku mrefu ambao sikuwahi kuupata katika maisha yangu.Sikuweza kupata usingizi.Kichwa changu kilikuwa kimejaa mawazo.Hostoria ya maumivu yaliyonipata miaka kadhaa ya nyuma yakanirudia tena.



    Siku iliyofuata ilikuwa jumamosi,niliamka asubuhi na mapema nikamuaga Emmy kuwa ninaenda ofisini kuna kazi nilitakiwa nikaifanye asubuhi hii na nisinge chelewa kurudi.Siku ya leo ni mapumziko hivyo ofisini nilikuwa mwenyewe.Nikaiwasha kompyuta yangu nikachomeka ile flash disk niliyokopi mawasiliano kati ya Emmy na my special one,mtu ambaye sikumjua ni nani.Nilianza kupitia tarehe moja baada ya nyingine,nikagundua kuwa mawasiliano yao yameanza muda mrefu.Kwa mujibu wa mawasiliano yao ilionesha kuwa walikuwa katika kipindi cha mapenzi mazito.Walikuwa wakiongea mambo mengi kuhusiana na raha na starehe wanazopeana.Nikagundua kuwa huwa wanakutana katika mahoteli makubwa makubwa na kupeana maraha.Kumbe mara zote Emmy akiniaga kuwa wana semina au makongamano huwa anakwenda kuponda raha na huyo special one.Yote haya niliyagundua katika meseji walizokuwa wakiandikiana.Iliniuma mno siwezi ficha.Nilitamani kutokuendelea kuzisoma meseji zile lakini ilinibidi nizisome zote ili kuupata ukweli wote.

    Mpaka nilipomaliza kuzisoma chat history zote nikajikuta sina hata nguvu za kuinuka kweye kiti.Jasho lilikuwa likinitiririka.

    “God where are you? Please help me” Nikasema kwa uchungu mwingi.



    * * * *

    Wiki iliyofuata ilikuwa ni wiki ngumu kwangu kupita maelezo.Nilijitahidi kutokuonesha dalili zozote zile kuwa kuna jambo lolote linanisumbua kichwani kwangu.Kila nilipomuona Baraka furaha yote ikapotea.Masikini malaika yule hakuwa na kosa lolote,hakuwa akifahamu kilichokuwa kikiendelea.Alifahamu fika kuwa baba yake mzazi ni mimi.Hata mimi bado niliendelea kuamini hivyo bado sikuwana na uhakika wa kutosha kwa yale niliyoyanasa kati ya mke wangu emmy na my special one ni ya kweli.Nilihitaji ushahidi wa kutosha..Jumanne jioni baada ya kazi nikaenda kuonana na rafiki yangu mmoja aitwaye beka anayefanya biashara ya kuuza magari.Nilimuomba anisindikize kwenda Same siku ya jumammosi tukitumia gari lake.Japokuwa alitaka kufahamu kwa undani juu ya safari hiyo lakini sikumpa jibu la moja kwa moja.Kutokana na ukaribu wetu akakubali kunisindikiza Same kwa kutumia gari lake.

    Siku zikaenda kwa kasi na hatimaye ikafika siku ya Ijumaa.Usiku tukiwa kitandani Emmy huku akikichezea kifua changu bila kujua kama alikuwa akinikera kupita kiasi ,akasema

    “darling ,kesho ndio ile safari niliyokwambia .Nasikitika kukuacha mwenyewe,utakuwa mpweke sana.”

    Nikatabasamu na kusema

    “Ni kwa nini usimuache baraka ?

    “hapana honey .Unajua Baraka kuna wakati anakuwa msumbufu sana.Acha tu niende naye asije akabaki akakusumbua .”

    “Hawezi kusumbua.Yupo dada yake wa kazi atakuwa akimlea.”Nikajibu.

    “Siku hizi Baraka amekuwa mtundu sana.Honey acha niende naye.Siku mbili tu si nyingi .”

    “Mtaondoka na usafiri gani? Nikauliza

    “Mimi nitaondoka na gari yangu”

    Akajibu Emmy huku usoni akionesha dalili za kutopendezwa na jinsi nilivyokuwa nikinga’ngania Baraka abaki.Nilikuwa nikielewa kila kitu hivyo haikunipa shida yoyote.

    “Ok nadhani hat mimi kesho nitaondoka asubuhi na mapema kuna kazi ninawahi kwenda kuifanya “ Nikasema

    “Ok baby” Akajibu Emmy akanibusu na kulala.Alipogeuka upande wa pili nikafuta mdomo wangu mahala aliponibusu kwa kiganja cha mkono.

    Emmy hakujua kilichokuwa kikiendelea moyoni mwangu lakini ukweli nilikuwa namchukia kupita kiasi kwa mambo anayonifanyia.Pamoja na hayo niliendelea kujifanya mjinga ili niweze kupata ukweli wa mambo.Sikutaka kuyaendea haraka mambo haya mazito.

    Asubuhi na mapema,nikaamka ,nikaoga na kuagana na Emmy.Nikapanda gari langu na kuelekea nyumbani kwa Beka maeneo ya Sakina.Nilimkuta tayari amejiandaa ananisubiri.

    Hatukupoteza muda tukaingia katika gari lake na safari ikaanza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Beka najua bado unajiuliza maswali mengi toka nilipokwambia kuhusu safari hii.lakini ukweli ni kwamba kuna gari ambayo itabidi tuifuatilie inakwenda Same.” Nikasema

    “Tunaifuatilia gari?”Beka akauliza

    “yes..kuna gari tunakwenda kuisubiri Bomang’ombe na tutaifuatilia mpaka Same.”

    Beka akakaa kimya akabadili gia na kulipita lori la mafuta halafu akanigeukia.

    “Wayne whats going on? Toka nimekufahamu sijawahi hata siku moja kukuona ukiwa katika hali kama hii.Kuna kitu unanificha .Hebu kuwa muwazi kama kuna tatizo ili tusaidiane jinsi ya kulitatua. Wewe ni rafiki yangu na tatizo lako ni la kwangu”

    Ni kweli Beka alikuwa mmoja kati ya marafii wangu amabao naweza kusemea ni wa kweli.Sikuona sababu ya kumficha tatizo langu Nikatabasamu na kujibu

    “beka,kusema ukweli nina tatizo kubwa lakini siwezi kukueleza kwa sasa hadi hapo nitakapokuwa na uhakika wa kutosha.Kwa sasa naomba tu unisaidie kulifuatilia hilo gali nitakalokuonesha.”

    Beka hakujibu kitu tena,akakubaliana nami.Akakanyaga mafuta hadi tulipofika eneo la Boma,tukasimamisha gari pembeni ya bara bara.

    Mpaka saa nne za asubuhi bado Emmy alikuwa hajapita ,nikawa na wasi wasi pengine anaweza akawa amepanda gari jingine,nikaamua kumpigia simu.

    “hallow Emmy,umeshaondoka?

    “yes’ darling nimeondoka muda si mrefu,kwa sasa nelekea maeneo ya KIA”akasema Emmy.

    “Unatumia usafiri gani,wa kwako au umepanda basi? Nikauliza ili kupata uhakika zaidi

    “Ninatumia gari yangu”

    “Ok honey Mimi ndio natoka kazini muda huu,msalimu baraka”

    Nikakata simu huku beka akiniangalia kwa jicho kali.

    “unaongea na mkeo?

    “yah ! ni mke wangu” Nikajibu

    “Tunamfuatilia mke wako?

    Sikujibu kitu nikakaa kimya

    “Wayne tell me please.Tunamfuatilia mke wako.?

    “Yes Beka tunamfuatilia mke wangu.”

    “ouh My God whats going on Wayne? Beka akauliza

    “Nitakwambia Beka lakini sio sasa.Ni habari ndefu sana.”

    Beka akajua lazima liko tatizo kati yangu na Emmy.akawa na subira akisubiri muda ukifika nimueleze mimi mwenyewe kwa mdomo wangu nini kinaendelea.Tuliendelea kusubiri huku tukiburudishwa na muziki ,mara nikaliona gari la mke wangu mama baraka likija.Nikamstua Beka aliyekuwa nje akiongea na simu.Akaingia garini tukaanza kulifuatilia gari lile.

    Beka alilifuatilia gari lie kwa ustadi mkubwa ili tusije shukiwa kuwa tunawafuatilia.gari la Emmy likaongoza hadi katika hoteli moja mpya na ya kisasa sana ijulikanayo kama Uhuru white peak hotel.Hatukuweza kuingia mle ndani ya ile hoteli kubwa ya kifahari tukabana sehemu tukiwasubiri watoke.Baada ya kama saa moja hivi wakatoka na safari ya kuelekea Same ikaanza.Nadhani walikuwa wameenda kupata mlo wa mchana

    Tulifika Same saa nane za mchana,.Pale hatukutaka kuendelea kulitumia gari letu hivyo ikatulazimu tulipaki mahala penye usalama tukakodisha gari aina ya Noah,tukaendelea kuifuatilia ile gari ya Emmy.Gari ya Emmy ikasimama nje ya nyumba moja kubwa yenye geti la kijani,na kupiga honi.Mara mlango ukafunguliwa na akashuka mwanaume mmoja ambaye sura yake haikuwa ngeni kwangu.Nikavua miwani myeusi niliyokuwa nimeivaa ili nimuangalie vizuri mtu yule .Sikutaka kuamini kuwa akili yangu ilikuwa sahihi.Sikutaka kuamini mtu niliyemuona toka ndani ya ile gari ni yeye kweli au wamefanana.Nilibaki mdomo wazi.

    “No Its not true.Chris!!!! Nikasema kwa uchungu.

    Ndugu msomaji aliyeshuka toka ndani ya ile gari ya Emmy alikuwa ni rafiki yangu wa siku nyingi aitwaye Chris ambaye alifanya kazi kubwa katika kufanikisha harusi yangu mimi na emmy.Ni mmoja kati ya watu ambao mchango wao kwangu sina uwezo wa kuulipa.Chris mtu ambaye nilimhesabu kama mmoja wa ndugu zangu kabla ya uhusiano wetu kuanza kupungua taratibu kiasi cha kuweza kumaliza hata mwaka mzima hatujaonana.

    Nikiwa naendelea kushangaa nilichokiona,geti linafunguliwa na gari linaingia ndani..Nilikuwa nimelowa jasho mwili mzima.

    “Tuondoke eneo hili Wayne” akasema Beka

    Tuliondoka eneo lile na kurudi hadi mahala tulipoacha gari letu.Tukamlipa yule jamaa mwenye ile gari tuliyoitumia akaondoka zake

    “Tunaelekea wapi baada ya hapa? Beka akauliza

    Sikujibu kwa haraka.Nilitafakari nini kifuate baada ya hapo.Niendelee kumfuatilia Emmy au nirudi nyumbani? Nikajiuliza mwenyewe na mwishowe nikaamua kurudi nyumbani.

    “Twende turudi nyumbani Beka.tayari nimeshaujua ukweli” Nikasema huku Beka akiniangalia na kisha akaondoa gari.

    Safari yetu ilikuwa ya kimya kimya .Nilikuwa na mawazo mengi mno .Tulipofika maeneo ya kwa Sadala Beka akauvunja ukimya.

    “Wayne najua si vizuri kuingilia mambo yasiyonihusu lakini wewe ni rafiki yangu na kama una jambo lolote linalokusumbua basi hata mimi linanihusu.Hebu niambie kuna tatizo gani?

    Sikuona sababu yoyote ya kumficha Beka juu ya tatizo linalonikabili.Nikaamua kumweleza ukweli wote ulivyo.Beka akasimamisha gari pembeni ya bara bara baada ya kuusikia ukweli.Hata yeye alistuka sana.

    “Wayne ni ya kweli hayo unayonieleza? Beka akauliza

    “kwa nini nikudanganye Beka.Haya yote ni ya kweli kabisa.”Nikasema.Beka akavuta pumzi ndefu na kusema kwa sauti ndogo

    “ I cant believe this.”

    Akanyamaza kidogo halafu akasema

    “Kwa jinsi ninavyomfahamu mke wako niliamini ni mmoja kati ya wanawake waadilifu mno katika ndoa zao.”

    “hata mimi nilikuwa naamini hivyo na sikujua kama anaweza akanifanyia kitu kama hiki.Namsikitikia mtoto kwa sababu hajui lolote.Ninampenda mno Baraka.Niliamini yeye ndiye mrithi wangu na ndiye furaha ya maisha yangu.baada ya kugundua kuwa si mwanangu sijui hata nifanye nini.Ninampenda mno mtoto yule Beka” Nikasema kwa uchungu.

    “Kwa hiyo umepanga kufanya kitu gani? Beka akauliza.Swali hili kwangu lilikuwa moja kati ya maswali magumu kujibu.Sikuwa nimepanga kufanya chochote na wala sikujua ningefanya nini.Kwa kitendo alichokifanya Emmy sikuona hata adhabu gani inayomstahili.

    “Beka sijapanga bado nifanye kitu gani.bado nahitaji ushahidi wa kutosha ili niweze kujiridhisha na hatua nitakazozichukua..I think I need more time” Nikasema

    “More time?….Beka akauliza kwa mshangao.

    “More time? Akarudia tena.

    “ Wayne naona kama unafanya utani na suala kama hili.Hili si suala dogo kama unavyolichukulia.Ni suala zito mno.Mkeo ameisaliti ndoa yenu na ushahidi wa uhakika unao.Umemfuatilia mkeo hadi Same na umegundua kuwa anaetembea na mkeo ni rafikiyo sasa ushahidi gani tena unaouhitaji? Hebu chukua hatua stahili mapema” Beka akasema kwa hasira.Beka alikuwa sahihi kwa upande Fulani lakini bado moyo wangu ulikuwa mzito kuchukua hatua za haraka.Beka alikuwa ameukunja uso kwa hasira.Kitendo kile ni wazi kilikuwa kimemuumiza mno.

    “Beka uko sahihi kuwa ushahidi unajitosheleza kwa kiasi kikubwa.lakini bado nahitaji muda zaidi wa kufikiri nini cha kufanya.Sitaki suala hili limuumize baraka.Nataka suala hili niliendee taratibu” Nikasema

    “Taratibu? Beka akauliza tena.

    “Wayne sidhani kama suala hili linakuumiza.Naona unalifanyia mzaha.Taratibu wakati mkeo bado anaendelea kukudanganya ,bado anakuona hayawani,anatembea na rafiki zako halafu unasema unachukulia mambo taratibu..Be serious my friend” beka akasisitiza.

    “nakuelewa Beka,lakini hizo hatua unazonisisitiza nichukue ni hatua zipi? Hebu nishauri” Nikasema

    “Hakuna ushauri hapa.Fukuza tu aende kwa huyo hawara yake.” Beka akajibu kwa hasira kali.

    Nilishindwa kukasirika ikanibidi nicheke .

    “sasa unacheka nini Wayne? Wanawake wa namna hii dawa yao ni kuwatimulia mbali ili wakafunzwe na dunia.Sipendi watu wasiokuwa na hisani”

    “Huo ndio ujinga wa wanawake.kwa jinsi ninavyofahamu ni kwamba Chris ana mchumba wake na tayari amezaa naye mtoto mmoja.Kwa sasa binti huyo yuko nje ya nchi kimasomo.Kwa maana hiyo ahadi kwamba atamuoa Emmy na kwenda kuishi naye nje ya nchi ni uongo mtupu.Chris akisafiri na kwenda nje ya nchi huwa anakwenda kumtazama mchumba wake na si vinginevyo.Iwapo nikimtimua Emmy hatakuwa na mahala pa kwenda kwa sababu ninamfahamu vizuri Chris.Hii ndiyo tabia yake kuwahadaa wanawake.Ninayemuonea huruma hapa ni Baraka.”

    Beka bado hakuridhika na maelezo yangu

    “Wayne mimi nakuonya ,mwanamke huyu si mzuri na hafai katu kuishi naye.Sikushauri uendelee kuishi naye.Mtimue haraka sana.”

    “Beka najua unachokiongea lakini kumbuka Emmy bado ni mke wangu wa ndoa na kama tulivyoelezwa siku tunakula kiapo cha ndoa kuwa kilichofungwa duniani kimefungwa na mbinguni.Hilo ndilo tatizo kubwa linalonifanya nisite kuchukua maamuzi.Nitawezaje kutengua ndoa hii? “ Nikasema huku nikishika kichwa.

    “Hivi Wayne huyu mwanamke amekupa kitu gani? Kuna dawa amekulisha wewe si bure.Haiwezekani ugundue mtu amekufanyia kitendo kama hiki halafu bado unamruhusu kulala ndani ya chumba chako.” Beka akasema kwa hasira

    “hahahaha Beka achana na mambo ya dawa.Unajua mimi huwa sipendi kuchukua maamuzi ya haraka haraka.Hili ni jambo zito linahitaji utulivu na busara ya hali ya juu kulitatua.usiwe na wasi wasi rafiki yangu suala hili litakwisha.Suala kama hili ni lazima washirikishwe wazee,viongozi wa dini n.kTwende tuendelee na safari tutaongea zaidi tukifika.”

    Beka akawasha gari tukaendelea na safari ya kurudi Arusha huku akionyesha dhahiri kuchukizwa na msimamo wangu.





    Jumapili jioni nikiwa nimepumzika bustanini nikitafakari Emmy akarudi.Baraka aliposikia niko bustanini akaja mbio akanikumbatia na kunisalimu.Emmy naye akaja bustanini haraka .Nilipomuona tu nikahisi hasira kali moyoni.Picha ya Chris ikanijia tena.Nikabadilika ghafla.Emmy akanibusu shavuni .Nilitamani nimkate shingo kwa hasira nilizokuwa nazo.Alionyesha mapenzi mazito kumbe ulikuwa ni unafiki mtupu.Huku akinipapasa kifuani akamwamuru Baraka aende ndani akapumzike .Nadhani hii ilikwa ni janja yake ili nisiweze kumuuliza Baraka kuhusu safari yao.

    “Honey habari ya toka juzi? Akasema kwa sauti laini ya kimahaba.

    “Nzuri .Pole kwa safari” Nikasema

    “Safari nzuri.Jamani honey I missed you so much.” Akasema na kunibusu tena.

    “Unajua kukaa mbali nawe hata kwa siku moja naumia sana.Nilipata wakati mgumu mno kwa kuwa mbali nawe.” Akasema huku moyoni akinizidishia hasira.

    “Mwanamke shetani huyu..” Nikasema moyoni kwa hasira.

    “baby are you ok? Akauliza baada ya kuniona nimekaa kimya

    “yah I’m ok” Nikajibu kwa kifupi.Akainua kichwa na kunitazama usoni halafu akakilaza kifuani kwangu.Sikuwa na msisimko wowote kama alivytarajia.Laiti angejua kilichokuwa moyoni mwangu katu asingethubutu kunisogelea karibu.

    Baada ya mlo wa usiku nikamuaga baraka na kumtaka aende akalale ili kesho asichelewe shule.Haikuwa kawaida yangu kuingia chumbani kulala mapema vile.Dakika chache baadae Emmy akanifuata.Akavaa nguo za kulalia na kuja kujilaza pembeni yangu.

    “baba baraka una tatizo gani? Akauliza

    Nilimtazama kwa makini usoni nikaona jinsi alivyokuwa na wasi wasi.

    “Sina tatizo lolote “ Nikajibu

    “hapana mume wangu .nakufahamu vizuri una tatizo.Kuna kitu kinakusumbua.Hebu nieleze mume wangu.haipendezi kama una kitu kinakuumiza halafu hutaki kukisema.Mimi ndiye mke wako sasa usiponiambia mimi utamwambia nani tena?

    Nilitamani kucheka kwa jinsi alivyokuwa akijibalaguza pale kitandani.

    “Ni kweli nina tatizo.” Nikasema.

    “tatizo gani hilo mume wangu? Akauliza huku akinishika kichwa.

    Nilikaa kimya kwa sekunde kadhaa nikatafakari kisha nikasema

    “Jumamosi ijayo tunasafari ya kwenda dar es salaam.nataka tukafanye DNA test”

    Emmy akastuka kama vile ameona jini.Akainuka kwa kasi na kukaa huku kijasho kikianza kumtoka usoni.Akaniangalia kwa macho makali.

    “DNA test? Akauliza kwa ukali.

    “Yes DNA test.Nataka nijue Baraka ni mwanangu au si mwanangu” Nikasema

    “Unajua bado sijakuelewa baba Baraka.Unamaanisha nini unaposema unataka ujue Baraka ni mwanao au si mwanao?

    “Kwani kuna tatizo gani la kutaka kuwa na uhakika wa mwanao? Nikauliza

    “baba Baraka hivi umepatwa na kitu gani? Iweje ukampime mwanao wa kumzaa ? Ina maana umefikia mahala pa kutokuniamini hata mimi mkeo wa ndoa?

    “si hivyo mama baraka.Ni katika kujiridhisha tu.Nakuamini sana mke wangu lakini kwa hili utanisamehe kwa sababu nahitaji kufahamu kama Baraka ni mwanangu au si mwanangu”

    Emmy akakaa kimya.akainuka pale kitandani akasimama na kuanza kuzunguka mle chumbani.Ghafla akageuka huku uso wake umejaa machozi.

    “Nasema hivi kama mimi ni mke wako wa ndoa hufanyi hiyo test.Hivi mimi nitakuwa mjinga kiasi gani nikudanganye kuwa Baraka ni mwanao wakati si mwanao?Nasema baraka ni mwanao na hiyo Test haifanyiki”

    “na mimi nasema hivi ,kama mimi ni mumeo wa ndoa nitafanya hiyo Test.Lazima nijue Baraka ni mwanangu au si mwanangu”Nikasema kwa ukali.

    “Kitu gani kinachokupa wasi wasi kuwa Baraka anaweza kuwa si mwanao? Emmy akauliza.

    “Hakuna kitu chochote Emmy nimeamua tu nifanye hivyo ili niwe na uhakika”

    Emmy akaanza kulia kwa kwikwi huku akilalama kuwa nimevuka mipaka kwa kumuona yeye ni msaliti wa ndoa yetu.Sikumjali nikavuta shuka nikajifunika na kulala.



    * * * *



    Ni wiki ambayo naweza kusema ilikuwa ni nyeusi ndani ya nyumba yangu.Maongezi na vile vicheko vilivyozoeleka vilikuwa nadra sana kusikika.Emmy hakutaka maongezi na mimi kwani muda mwingi alipotoka kazini alikuwa analala chumbani kwa kisingizio cha kazi nyingi.Sikuijali hali hiyo ,ila nilikuwa makini sana ili hali kama ile isije kumuathiri Baraka..Mtoto hakuwa na kosa na hakutakiwa kusulubishwa kwa makosa ya wazazi wake.Nilijitahidi kuwa naye karibu,kumsaidia kazi za shuleni zilizomshinda,na wakati mwingine tulikwenda bustanini kupiga magitaa yetu.Sikutaka aone kama kuna tofauti yoyote imetokea kati ya wazazi wake.Siku ya ijumaa usiku tukiwa mezani tunapata chakula nikakumbushai juu ya safari ya Dar es salaam kesho yake na kuuliza kama kila kitu kiko tayari..

    “Kila kitu umekwisha kiweka tayari kwa safari” Nikauliza

    Emmy hakujibu kitu akaniangalia kwa jicho kali .

    “Hivi ni kweli umemaanisha kwenda kufanya hiyo DNA test au unanitania? Emmy akauliza

    “mama baraka sikutanii.Kesho tunasafri kwenda Dar kwa ajili ya DNA.It’s a serious issue.”Nikasema

    “Kama unakwenda nenda mwenyewe.Mimi wala mwanangu Baraka hatutakwenda” Emmy akasema kwa kiburi

    “Mama Baraka ,mimi ndiye mwenye kauli ya mwisho katika nyumba hii na ndiye mwenye kuamua nini kifanyike na nini kisifanyike.Kwa maana hiyo basi nasema kuwa kesho alfajiri na mapema wote tunakwenda Dar es salaam.Hili halina kipingamizi na wala sihitaji mjadala tena” Nikasema kwa sauti iliyoashiria hasira ndani yake .Nilifahamu ni kwa nini Emmy hakutaka kwenda kufanya kipimo cha vinasaba.Nina uhakika mkubwa kuwa Baraka hakuwa mwanangu wa damu lakini nilikuwa nataka kuwa na ushahidi mkubwa zaidi wa kibaolojia.

    “Kama mnakwenda nyie nendeni lakini mimi sintakwenda Dar es salaam.Mimi ndiye mwenye ukweli wote na hata kama ukienda kupima bado ukweli hautabadilika “Emmy akasema huku akiubetua mdomo wake kwa dharau akakiweka kijiko chini na kuondoka mezani kwa hasira.Niliumia sana moyoni kwa majibu yake ya kiburi namna ile lakini sikutaka kuonyesha mbele ya mtoto.



    * * * *



    Siku ya jumanne nilirejea toka jijini Dar es salaam nilikokuwa nimekwenda kwa ajili ya kufanya kipimo cha vinasaba ili kubaini kuwa Baraka ni mwanangu au si mwanangu.Emmy alikataa kata kata kuungana nasi kwenda Dar kwa ajli ya vipimo hivyo ikanuilazimu kwenda mimi na Baraka.Majibu niliyopewa yalinitoa machozi kwani yalionyesha dhahiri kuwa Baraka hakuwa mwanangu wa damu.Japokuwa nilikuwa naelewa kabla kuwa Baraka hakuwa mwanangu lakini sikuwa na uhakika sana hadi majibu haya yaliponidhihirishia wazi .Majibu haya yalinifanya nifikie hatua ya mwisho ya kuutafuta ukweli kama Baraka ni mwanangu au sivyo.Kila nilipomuangali mtoto yule niliyempenda kuliko kitu chochote kile roho iliniuma sana.Emmy alinifanyia unyama mkubwa sana.Ni bora Emmy angenieleza toka mapema nikafahamu kuwa yule si mwanangu.Ameuficha ukweli miaka hii yote na kwa sasa Baraka amekwisha kuwa mkubwa na ana akili za kutosha na hivyo kuambiwa ukweli kuwa mimi si baba yake ni kitendo ambacho kitamchanganya akili na kumuathiri kisaikolojia.

    Saa moja za za jioni tukawasili Arusha na kuelekea moja kwa moja nyumbani.Nyumbani alikuwepo mtumishi wa ndani peke yake.Nikamuuliza alikoenda Emmy akasema kuwa siku tulipoondoka kwenda Dar es salaam na yeye akaondoka na hajarudi tena hadi leo hii na wala hakusema anaelekea wapi.Sikushangaa wala kuumia rohoni kwa kitendo kile kwa sababu kuendelea kumuona Emmy machoni pangu kungeniongezea hasira.Nikaingia chumbani na kukuta baadhi ya vitu vyake havipo.Nadhani alitambua kuwa kwenda kwangu Dar es salaam kungeweka ukweli wa mambo kuwa baraka hakuwa mwanangu na kwa maana hiyo akaamua kuondoka mapema kabla sijarudi ili kuepusha matatizo..

    Nilikaa kitandani nikitafakari kwa kina juu ya maisha yangu na matatizo ambayo Emmy amenisababishia.Toka nimegundua uchafu alionifanyia Emmy nimekuwa nikijipa ujasiri mkubwa kuwa haya ni masuala madogo ambayo katu hayawezi kuniumiza kichwa lakini nikiwa pale kitandani kwa mara ya kwanza nikahisi kitu kama kisu kikali kikiupenya moyo wangu .Nilihisi maumivu makali ya moyo.pamoja na ujasiri wangu wote nilioahidi kuwa nao lakini nilishindwa kuyazuia machozi kunitoka.Hayakuwa maumivu ya kawaida.Ilikuwa ni zaidi ya maumivu..

    Kesho yake nikadamka asubuhi na mapema na kujiandaa kumpeleka Baraka shule.Emmy hakurejea na wala sikusumbuka kumtafuta katika simu na kumuuliza yuko wapi ingawa nilipaswa kujua aliko akiwa kama mke wangu.Kwa hasira niliyokuwa nayo moyoni sikuwa tayari kumuona tena akitia mguu nyumbani kwangu.Macho yalikuwa yamevimba na mekundu kwa kukosa usingizi .Baraka alipokuwa tayari akaingia garini nikampeleka shule halafu nikaelekea ofisini.Japokuwa nilijitahidi kuuficha ukweli kuwa kuna jambo linanisumbua lakini wafanyakazi wenzangu walihisi sikuwa sawasawa.Nikiwa ofisini niliegemea kitini na kuanza kutafakari kwa kina juu ya maisha ya furaha niliyoishi na Emmy kumbe nyuma yake kumejaa usaliti na uchafu wa hali ya juu mno.Niliufikiria pia urafiki kati yangu na Christopher ulivyokuwa wa karibu.Tulikuwa ni marafiki tulioshibana sana na tuliishi kama ndugu.Ni Christopher ndiye aliyesaidia mpaka mimi na Emmy tukarudiana tena baada ya Emmy kunifanyia usaliti miaka ya nyuma kabla hatujaoana.Leo mke wangu wa ndoa anadiriki kuzaa na rafiki yangu wa karibu.Sikuwa tayari kuendelea kuteseka na kuumia moyo kwa ajili yao tena.Nikaamua kuliweka wazi suala hili.Nikachukua simu na kumpigia baba mkwe wangu yaani baba yake Emmy na kumuomba kama ana nafasi nionane naye jioni yeye pamoja na mama.Hakuwa na tatizo mzee yule ,halafu nikampigia tena simu rafiki yangu Beka na kumuomba aje nyumbani kwangu jioni kwa ajili ya maongezi mafupi , nikampigia pia simu mwalimu wa dini ambaye amekuwa karibu nasi na kutulea kiroho kwa muda mrefu.Niliwataarifu vile vile wasimamizi wetu wa ndoa kuwa wafike jioni hiyo kuna masuala muhimu ya kuongea.Nilihitaji na Emmy awepo katika kikao cha jioni hiyo wakati nikiusema ukweli mbele ya wazee na mashahidi lakini sikuwa na hamu hata ya kuongea naye simuni.Baada ya kufikiri mara kadhaa nikaamua kumpigia simu japokuwa moyo ulikuwa hautaki .

    “Unasemaje wewe? Akauliza kwa ukali mara tu alipoipokea simu.Nilistushwa na ukali ule na kauli ile ya dharau kwani hakutaka hata kunisalimu.Nilisita kidogo kuongea kutokana na hasira zilizonipanda ghafla.Leo emmy amefikia hatua ya kuniita mimi “wewe”

    “Sema unachokitaka kama husemi nitakata simu” Akasema tena kwa ukali baada ya kuona nimekaa kimya.

    “nakuhitaji nyumbani jioni” Nikasema

    “Nije kufanya nini? Hivyo vipimo ulivyoenda kufanya si vimeshakupa ukweli sasa unataka nije kwako kufanya nini tena?

    “nataka uje tuongee”

    “Tuongee nini tena? Hatuna cha kuongea wayne.tayari ukweli unaufahamu kwa hiyo sioni kama kuna kitu tunatakiwa kuongea mimi na wewe.Umeshatambua Baraka siyo mwanao kwa hiyo hata mimi si mkeo.Sifikirii tena kuishi na wewe .Nimechoka mimi maisha ya kubanwa banwa na kufugwa fugwa ndani kama njiwa.Nahitahi maisha ya uhuru,maisha ya kufanya nitakacho.Naomba uniache Wayne.Mimi sifai kuwa mkeo.Unahitaji mwanamke bora wa kuishi naye na si mimi.”

    Nilivuta pumzi ndefu baada ya maneno yale mazito.Sikutegemea Emmy mwanamke niliyempenda na mbele ya mashahidi kanisani akala kiapo cha kuwa nami katika maisha yote mpaka kufa lakini leo ananitamkia maneno kama haya.Ni shetani gani amemwingia mwanamke huyu hadi akabadilika na kuwa namna hii?

    “Emmy mimi sina ugomvi na wewe na hata kama ukitaka kuondoka kwangu mimi sikuzuii kwani ni uamuzi wako.Ninaujua ukweli wote.Ninafahamu Baraka si mwanangu wa damu.Ninafahamu Baba yake ni nani kwa hiyo ninachotaka tukae chini tuongelee suala la huyu mtoto .Tukilimaliza hilo mimi sina tatizo na wewe hata kidogo.You can do anything you want” Nikasema huku moyo ukiniuma kupita maelezo.

    “Ok kama nitapata muda nitakuja.” Emmy akajibu kwa dharau na kukata simu.Nilihisi kama dunia inazunguka .sikuwa nimetegemea kama itatokea siku mimi na Emmy tungefikia mwisho wa namna hii.



    * * * *



    Saa kumi na moja za jioni Baba mkwe akiwa ameongozana na mkewe wakawasili nyumbani kwangu.Niliwakaribisha kwa furaha japokuwa nyuso zao zilikuwa na wasi wasi mwingi.Nadhani mwito ule wa dharura ulikuwa umewastua sana.Tayari Beka,mwalimu wangu wa dini na wasimamizi wetu wa ndoa walikuwa wamekwisha fika muda mrefu na waliokuwa wakisubiriwa ni wakwe.Zaidi ya Beka hakuna aliyekuwa akijua nini niliwaitia jioni ile,hali iliyowafanya wote wazidi kuwa na wasi wasi .Baada ya salamu na maongezi mafupi,nikafanya utambulisho kwa wageni wote halafu nikafungua kikao.

    “Baba na mama mkwe,kwanza kabisa ninapenda kuchukua nafasi hii kuwaomba samahani kwa kuwasumbua jioni hii.Najua mna majukumu mengine mengi ya kufanya .Nashukuru sana kwa kuitikia mwito wangu na kufika hapa.Nawashukuru pia wengine wote mliofika,rafiki yangu Beka,mwalimu wangu wa dini, na wasimamizi wetu wa ndoa.”

    Kabla sijaendelea mbele zaidi,baba mkwe akadakia.

    “Samahani kwa kukukatisha Wayne.Mbona simuoni Emmy hapa?

    Swali lile linanipa wakati mgumu kidogo kulijibu.Nikafikiri kwa sekunde chache na kusema

    “ Emmy atakuja si muda mrefu.amepata dharura kidogo” Nikadanganya.Sikutaka kuharakisha mambo.Nilitaka kwanza niwape picha kamili ya mambo jinsi ilivyo.Nikawatazama wote na kila mmoja alikuwa na sura iliyoniashiria niendelee na maongezi.

    “Nimewaiteni jioni hii ya leo kuna mambo muhimu ya kuongelea.Nadhani nyote mnafahamu kuwa ndani ya ndoa migongano,mikwaruzano huwa haikosekani.Kunapotokea mikwaruzano au migongano ndani ya ndoa na wanandoa mkashindwa kuisuluhisha basi hamna budi kuwashirkisha watu wa karibu kama wazazi na ndugu wengine wa karibu.Kwa ufupi ni kwamba ndani ya ndoa yetu kumetokea matatizo kidogo ambayo sisi kama wanandoa tumeshindwa kuyatatua ikanilazimu kuwaita na kuwashirikisha katika suala hili.”

    Nikanyamaza na kuwaangalia wote mle ndani ,kila mmoja alikuwa na hamu ya kutaka kujua nini kimetokea.

    “nafikiri nyote mnakumbuka kuwa kipindi kifupu kabla ya ndoa yangu na Emmy kulitokea mtafaruku ambao ulichangiwa na mwenzangu kutokuwa mwaminifu katika uchumba wetu.Sitaki kurudia kulielezea hilo kwa sababu lilikwisha pita na limesahaulika,ila nimelisema tu ili kuweka kumbukumbu sawa.Baada ya usuluhishi wa wazazi na ndugu tulilimaliza suala lile na ndoa ikafungwa.Tumeishi vizuri na mwenzanguu hadi tukabahatika kupata mtoto mmoja.Maisha yetu yamekuwa ni ya furaha kubwa siku zote.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikanyamaza tena na kuvuta pumzi halafu nikaendelea

    “Siku chache zilizopita,niligundua kuwa mwenzangu amekuwa si mwaminifu katika ndoa yetu.Labda kwa kuelezea tu ilimpate picha halisi ni nini ninakiongea ni kwamba kuna siku niliwahi kutoka kazini,sikuwa na kazi nyingi za kufanya hivyo ikanibidi kuwahi kazini na kuja kukaa na familia yangu .Nilipofika getini nikakutana na mke wangu akitoka nikamuuliza alikokuwa akielekea kasema kuwa wanampeleka jirani yetu hospitali.Nikaingia ndani na kuikuta kompyuta yake iko kitandani,nikaona ni bora niizime.Kabla sijaizima nikagundua kuwa kabla hajatoka alikuwa akiwasiliana na mtu .Kwa kuligundua hilo nikaona ni bora mtu huyo aliyekuwa akiwasiliaana naye nimjibu kuwa asubiri hadi baadae.Nilipatwa na udadisi wa kusoma zaidi baada ya kuona jina la mtu aliyekuwa akiwasiliana mke wangu limeandikwa my special one.Nikajiuliza huyu my special one ni nani? Hata kama ungekuwa ni wewe ni lazima ungepatwa na udadisi wa kutaka kujua huyo special one ni nani.kwa sababu mimi kama mume mke wangu ndiye mtu wangu muhimu,ndiye my special one.Kwa mantiki hiyo hata mke wangu mimi ndiye special one wake kwa sababu aliamua kuwaacha wanaume wote na kuolewa na mimi.Sasa nikastuka baada ya kujua kuwa mwenzangu ana special one mwingine ambaye si mimi.”

    Nikatulia na kuwaangalia watu wote mle sebuleni.walikuwa kimya kabisa wakiniskiliza.mama yake Emmy alikuwa ameinama ameshika shavu .Nikaendelea.

    “Baada ya uchunguzi nikagundua kwamba walikwisha anza kuwasiliana muda mrefu toka Emmy akiwa kazini,na aliporudi nyumbani wakaendelea tena kuwasiliana.Na hiyo haikuwa mara yao ya kwanza kuwasiliana.Baadae nikagundua kuwa kulikuwa na message za kimapenzi walizokuwa wakitumiana.Nikabaini kuwa Emmy ana uhusiano na mtu huyu wa kimapenzi kwa sababu kwa mujibu wa meseji wanazotumiana walikuwa wakikumbushana juu ya siku za nyuma wanazokutana katika mahoteli makubwa na kufanya mapenzi.Si mara moja Emmy huwa ananiaga kuwa anakwenda semina au katika makomngamano au kikazi nje ya mji kumbe huwa anautumia muda huo kukutana na huyo mtu wake muhimu.Ushahidi wa meseji zote hizo ninao toka walipoanza kuwasiliana.”

    Mama mkwe akainama chini kwa aibu .Baba mkwe yeye akatoa kitambaa na kufuta jasho lililoanza kumtoka.Kila mmoja mle sebuleni sura yake ikabadilika.Sikutaka kumung’unya maneno,nikaendelea.

    “Niliumia sana baada ya kuligundua hilo lakini nashindwa hata kuelezea maumivu niliyoyapata baada ya kugundua kuwa ……….” Kabla sijaendelea mbele mlango ukagongwa.Nikaomba samahani na kwenda kuangalia ni nani aliyekuwa akigonga.Alikuwa ni jirani yetu mama Mwantumu.Mama yule akaniambia kuwa Emmy alikuwa akihitaji kuonana na mimi nje ya nyumba.Amegoma kuinia ndani baada ya kuliona gari la baba yake liko mle ndani.Nikaingia ndani na kumwita mama mkwe nje.





    “Mama samahani,Emmy amekuja yuko nje lakini amegoma kuingia humu ndani baada ya kuliona gari la baba.Ninaomba ukamshawishi aingie ndani kwa sababu kama nikienda mimi hatakubali kuingia ndani” Mama mkwe akakubali na akaenda nje ya nyumba kuonana na Emmy.

    “Wayne vipi,uko salama? Kuna tatizo lolote? Akauliza baba mkwe baada ya kuniona nimerudi ndani na kukaa kimya kimya

    “Hapana mzee.Ni mambo ya kawaida ,mama anayashughulikia” Nikasema

    Baada ya dakika tano hvi mlango unafunguliwa,mama mkwe akiwa ameongozana na Emmy wanaingia ndani.Emmy akiwa ni mwenye sura ya aibu akamsalimu baba yake na mwalimu wa dini halafu akakaa sofani huku amekiinamisha kichwa chake chini.hakutaka kumuangalia mtu yeyote usoni.

    “Nadhani tunaweza kuendelea.” Nikasema na kuwatazama watu wote mle ndani.Baba mkwe alikuwa akimuangalia Emmy kwa jicho la hasira mpaka nikaogopa .

    “Endelea Wayne” Akasema baba mkwe.

    “Kabla hatujasimama nilikuwa nasema kwamba,niliumia sana baada ya kugundua kuwa mwenzangu alikuwa akitoka nje ya ndoa yetu.Mwenzangu hakuwa mwaminifu hata kidogo.Kikubwa zaidi ya yote ni kwamba niligundua kuwa mtoto Baraka hakuwa mwanangu wa damu.Alikuwa na baba yake……”

    “Yarabi toba….” Mama mkwe akasema kwa sauti kubwa huku ameshika kichwa chake.baba mkwe akamshika mkono na kumtoa nje.Mama mkwe ana matatizo ya shinikizo la damu.Baba mkwe aliamua kumtoa nje baada ya kuona hali yake inanza kubadilika.

    Baada ya dakika kadhaa,baba mkwe akarudi ndani.

    “Tuendelee…mama yenu huwa ana matatizo ya shinikizo la damu na habari kama hizi huwa zinamstua sana ndiyo maana nimemtoa nje apumzike.”

    “Mwanzoni sikuamini hata kidogo kuwa ni kweli Baraka anaweza kuwa si mwanangu.Kwa mujibu wa meseji nilizozipata ,walizokuwa wakitumiana Emmy na My special one ni kwamba kwa kuwa Baraka tayari amekwisha kuwa mkubwa, anapaswa kuanza kuwafahamu ndugu zake na kwa kuanzia walipanga waanze kumpeleka kwa babu zake huko Same.Ni kweli siku hiyo kama walivyokuwa wamepanga Emmy aliniomba ruhusa kuwa anamsindikiza rafikiye kwenye sherehe ya ndugu yake.Nilimfuatilia bila ya yeye kujua mpaka Same ndipo nilipogundua kuwa huyo mtu aliyemuita kama special one alikuwa ni rafiki yangu wa siku nyingi sana aitwaye Chris.Nilipolitambua hilo nikataka nipate uhakika zaidi nikamuomba emmy tuende tukapime DNA ili tuwe na uhakika mtoto ni wangu au si wangu.Emmy alikataa kata kata ikanilazimu kuondoka mimi na Baraka hadi Dar es salaam na kufanya kipimo hicho cha DNA na majibu ylidhihirisha kuwa ni kweli Baraka si mwanangu.Niliporudi toka dar es salaam nikiwa na majibu ya vipimo vya DNA Emmy tayari alikwisha ondoka nyumbani na nilipompigia simu ni kwa nini aliondoka nyumbani bila ruhusa yangu akaniambia kwamba kwa sasa sina nguvu yoyote ya kuweza kumzuia,na akaenda mbele zaidi kwa kunitaka nisiendelee kumfuatilia.Nilimuelewa lakini nikamuomba aje katika kikao hiki cha jioni ya leo kwa ajili ya kujadili kuhusu suala la mtoto.Kwa ufupi hayo ndiyo niliyowaitia jioni hii ya leo na imekuwa vyema mhusika mkuu naye amefika”

    Nikamaliza na kuwatazama watu wote mle ndani.Kila mmoja alikuwa kimya .Ukimya mkuu ukatanda mle sebuleni halafu babamkwe akasema kwa hasira.

    “Emmy ,japokuwa umechelewa ,lakini umeyasikia yote aliyoyaongea mwenzio.Je una lolote la kuongea?

    Emmy hakujibu kitu akakaa kimya huku machozi yakimtoka

    “nakuuliza tena Emmy una lolote la kuongea kutokana na haya aliyoyasema mwenzio? Naomba usikae kimya nijibu haraka” baba mkwe akasema kwa ukali

    Emmy akiwa ameuficha uso wake kwa viganja vya mikono akasema

    “Yote aliyoyasema ni kweli baba”

    Baba mkwe akashika kichwa kwa mstuko.

    .Alipatwa na mstuko wa ghafla.Kila mtu mle ndani alikuwa amepigwa na butwaa.baba mkwe akainama akatafakari kwa sekunde kadhaa halafu akainua kichwa na kusema

    “Emmy naomba urudie tena,haya aliyoyatamka mwenzako ni mambo ya kweli?

    Huku akifuta machozi akiwa ameinama chini akasema bila kusita

    “Ni ya kweli baba”

    Ghafla baba mkwe akainuka kwa kasi ya ajabu na kutaka kumvaa Emmy kwa kipigo,nashukuru mwalimu wa dini alikuwa karibu akawahi kumshika na kumketisha chini.

    “Mtoto una laana wewe.Unawezaje kufanya upuuzi kama huu ? Baba mkwe akasema kwa hasira

    “Mzee.Punguza hasira tuyaongee haya mambo kiutu uzima tuyamalize.Najua inauma kama mzazi lakini jitahidi kujizuia mzee wangu ili tuyamalize mambo haya magumu kwa amani”Mwalimu wa dini akasema taratibu akijaribu kumtuliza baba mkwe aliyekuwa amewaka kwa hasira.

    “Mwalimu hebu niachieni nafasi nimshikishe adabu baradhuli huyu .Amenitia aibu kubwa .Tutaziweka wapi sura zetu sisi? ..Ouh My God…..” Akasema kwa hasira baba mkwe.

    “Aibu hii si yako peke yako.Suala hili limetugusa sisi sote.Wote tunaumia mioyoni mwetu.lakini tunajitahidi kujizuia .Nakuomba mzee wangu tuliza hasira tuyaongee mambo haya na kuwasaidia hawa vijana.”

    Baba mkwe akatulia lakini alikuwa akihema kwa hasira.Emmy uso ulikuwa umejaa machozi.Mambo haya mimi niliyaona kama ya kawaida kwa sababu nilikwisha yazoea tayari.Nilikwisha umia vya kutosha kwa hiyo sikuwa mgeni wa maumivu haya.Wote tulikuwa kimya tukisubiri kusikia baba mkwe atasema kitu gani.

    “Emmy nataka uniambie.Ni kitu gani kimepelekea wewe ukafanya uchafu wa namna hii.Nataka uwe wazi ili tujue na tuone jinsi gani tunaweza kulimaliza suala hili”

    Emmy alikuwa ameinama akilia.Hakuweza kuinua uso wake kwa aibu.Sebule yote ikawa kimya ikimsubiri yeye aweze kujibu swali aliloulizwa na baba yake.

    “Emy nimekuuliza,na ninataka unijibu sasa hivi ni kitu gani kimepelekea wewe ukafanya uchafu wa namna hii ? Hii ni aibu kubwa kwetu kama familia,umetuumiza sana siwezi kukuficha na hasa mama yako ameumia mno.Umemuumiza mwenzako pia kiasi ambacho hakielezeki.Bado kuna mtoto Baraka ambaye ataumia kupita kiasi atakapoelezwa kuwa huyu si baba yake mzazi.Tafadhali usikae kimya hebu tueleze ni kwa nini ulifanya mambo kama haya? Baba mkwe akauliza tena huku hasira zikianza kumpanda. Emmy akafuta machozi kwa kitambaa chake halafu akainua sura yake na kusema kwa kwikwi.

    “ baba …kusema ukweli..nilifanya hivi kwa sababu………’ Emmy akashindwa kuendelea akaanza kulia.

    “Emmy naomba tafadhali usipoteze muda wetu hapa.hebu tueleze ni kitu gani kimekufanya wewe ukamfanyia mwenzako namna hii? Baba mkwe akasema kwa sauti kali

    “baba ..niliamua kutoka nje ya ndoa kwa sababu sikuwa naridhika….Wayne haniridhishi”….

    Kauli ile inanifanya nihisi kama vile moyo wangu unataka kupasuka kwa jinsi ulivyoyabadilisha mapigo yake na kuanza kwenda kasi.Katika maisha yangu sikuwa nimetegemea kama iko siku Emmy atakuja kutamka kitu kama kile.Nilijitahidi kwa kila niwezavyo kumridhisha kwa kila kitu alichokihitaji bila kujali gharama yake.na hata katika mapenzi ya kitandani nilikuwa mjuvi wa mambo na kila tulipofanya mapenzi siku zote hunisifia na kuniita kidume huku akiapa na kuwatukana wanaume wengine kuwa hawana hadhi ya kumgusa mtu kama yeye kutokana na raha ninazompatia.Sasa iweje tena leo mbele ya wazee atamke kuwa sikuwa namridhisha?Baada ya tafakari fupi nikagundua kuwa alisema vile kama utetezi wake.Uongo ule ukaniuma sana.baba mkwe akamtazama Emmy kwa hasira na kuuliza.

    “Emmy unadai kuwa ulifanya uchafu huu kwa sababu mumeo hakuwa akikuridhisha,je kuna siku yoyote uliwahi kukaa naye na ukamueleza kuhusu suala hilo?

    Emmy hakujibu kitu akakaa kimya.Nilijua alikuwa akiongopa ndiyo maana hakuwa na jibu.Alipoona Emmy amekaa kimya hana jibu baba mkwe akanigeukia mimi

    “wayne hebu tuelze.Kua siku yoyote mkeo alikwisha wahi kukueleza kuwa humridhishi?

    “Hapana baba hakuna hata siku moja aliyowahi kuneieleza kuwa haridhiki.Kinachonishangaza ni kwamba mara zote amekuwa akinisifia kuwa hajawahi ona mwanaume kama mimi ,kwa maana hiyo ni kwamaba alikuwa akiridhika saa iweje leo atamke kwamba hakuwa akiridhika? Zaidi ya yote hakuna kitu alichowahi kukitaka mke wangu akakosa hata cha gharama gani.Kuna siku nyingine akiwa nyumbani huwa ananipigia simu na kunieleza kuwa ananihitaji,kwa kumridhisha huwa natoroka kazini na kuja kukaa naye.Hebu muulizeni kama ninasema uongo”

    “Emmy umemsikia mwenzio alivyosema.Ni kweli?

    Emmy hakujibu kitu.Baba mkwe akawagekia wasimamizi wa ndoa yetu na kuwaliza.

    “Au alikuwa kushitaki kwenu wasimamizi?

    “hapana baba.Hakuna hata siku moja Emmy amewahi kuja kushitaki kwetu kuhusu jambo lolote lile linalohusiana na masuala ya ndani ya ndoa yao”

    baba mkwe akatafakari kwa muda na kusema

    “Inaonekana Emmy umeamua kutunga uongoHuna sababu yoyote ya msingi iliyopelekea wewe kuamua kutoka nje ya ndoa yako,na hata kufikia hatua ya kuzaa nje ya ndoa na kumdanganya mumeo.Mara ya kwanza mwenzio alikufuma na mwanaume akakusamehe na mkafunga ndoa.Niliamini kuwa ulijifunza na ukabadilika .Siku zote hizi umekuwa ukiishi kama mke mwema kumbe ni chui ndai ya ngozi ya kondoo.Inaonekana hii tabia ya umalaya imekwisha kuingia ndani ya damu yako na hautaweza kuiacha.Sasa nakuambia hivi kwa kosa hili ulilolifanya mimi sintakuwa na kusema .Nitamuachia wayne yeye ndiye atakaye amua afanye nini.” Baba mkwe akasema kwa ukali.mwalimu wa dini ambaye alikuwa amekaa kimya muda wote akakohoa kidogo na kusema.

    “Jamani naomba na mimi niseme kidogo.Nakubali kuwa Emmy amefanya kosa kubwa sana.Amemkosea mwenzake na hata kuvunja ahadi ya ndoa aliyoiweka mbele ya altare ya bwana.Lakini kama Mungu anavyotuagiza kwamba tusiwe na mipaka katika kusamehe kama yeye anavyowasamehe hata wale wanaomkosea kupita kiasi.kwa maana hiyo kabla hatujaendelea mbele na kikao hiki ningeomba kwanza tujenge mazingira ya kusameheana.Ni kwa njia hiyo pekee tunaweza kuyamaliza mambo haya kwa amani.Halafu kitu kingine ni kwamba tunataka Emmy atueleze nani ni baba wa mtoto ili tuone ni vipi tutafanya kuhusu mtoto huyu.” Mwalimu wa dini akasema lakini kabla hajaendelea zaidi baba mkwe akadakia

    “Mwalimu,nafahamu wewe ni mtu wa Mungu na siku zote kazi yenu ni kuhubiri upendo na kusameheana.Lakini nadhani wewe hujaguswa na jambo hili.maumivu ya kufanyiwa kitu kama hiki hayapimiki..Suala la kusameheana naona tumuachie Wayne yeye ndiye atakayeamua kama atamsamehe huyu mke wake au vipi.Tuendelee na kikao chetu.Emmy hebu tueleze huyu mtoto Baraka baba yake ni nani?

    Kwa upande Fulani nilimuunga mkono baba mkwe kwa kauli yake.Kumsamehe Emmy ilihitaji moyo wa ajabu sana.haikuwa rahisi kusamehe .Emmy hakuwa tayari kusema nani alikuwa ni baba wa Baraka.ote tukakaa kimya tukimsubiri.

    “Emmy tunakusubiri wewe ,hebu tueleze ni nani baba wa mtoto ?

    Emmy hakuwa tayari kusema lolote kuhusiana na mtu aliyezaa naye.Kwa kuwa nilikuwa nikimfahamu ni nani baba wa Baraka nikaona ni bora niwe wazi.

    “ Baba mkwe hawezi kutujibu huyu.Lakini tayari ninamfahamu baba wa mtoto.”

    “unamfahamu baba wa mtoto? Baba mkwe akauliza kwa mshangao

    “Ndiyo tayari ninamfahamu” Nikajibu

    “Hebu tutajie ni nani huyo?

    “Ni rafiki yangu Chris” Kimya kikatanda mle sebuleni.Kila mmoja hakuamini kama Emmy angeweza kuzaa na rafiki yangu.

    “Yaani Emmy anadiriki kuzaa na rafiki yako? Baba mkwe akauliza.

    “Si tu rafiki yangu,bal ni mtu aliyekuwa rafiki yangu wa karibu sana.Ni Chris ndiye aliyekuwa muandaaji mkuu wa harusi yangu na Emmy.Nilimwamini na kumuona kama ndugu.Sikujua kama iko siku anaweza akafanya kitu kama hiki alichokifanya.” Nikasema kwa uchungu.Ilikuwa inauma sana.

    “mambo haya yanazidi kuwa magumu.Na huyo rafikiyako mmekwiha wasilia ana kwa siku za hivi karibuni? Aba mkwe akauliza

    “Hapana baba.Ni kitambo kirefu sijawasiliana naye.Mawasilaiano baina yangu na yeye yalianza kufiifia na hatimaye kufa kabisa.Kwa sasa sina mawasilano naye yoyoite yale”

    Baba mkwe akamgeukia Emmy

    “Emmy ni kweli umezaa na rafiki wa Wayne?

    Kwa sauti yenye kitetemeshi Emmy akajibu

    “Ni kweli baba,nimezaa na Chris” jibu lile linampandisha baba mkwe hasira

    “Mtoto una laana wewe.Unawezaje kuzaa na rafiki wa mumeo?

    “baba Chris ninampenda .Sitaki kuendelea kuishi na Wayne.Nataka nikaishi na Chris tulee mtoto wetu.”

    Chumba chote kikawa kimya kwa kauli ile ya Emmy.Kila mmoja alikuwa amepatwa na mshangao mkubwa .Kwa wale waliokuwa pale sebuleni ilikuwa ni kama wanaangalia mchezo wa kuigiza lakini ilikuwa kweli.

    “baba wewe una mawazo gani ? Baba mkwe akanigeukia na kuniuliza.Watu wote mle sebuleni macho yao yakanielekea mimi ili kunisikia ninatoa wazo gani.Kila mmoja alikuwa akikwepa kutoa hukumu kwa kesi ile ngumu.Nililitambua hilo na nikaamua kuweka wazi yaliyokuwa moyoni mwangu

    “baba nadhani nyote mmesikia kwa kauli yake kuwa hana haja ya kuishi tena na mimi.Hili amelitamka mbele yako wewe baba ambaye ni mzazi wake na mbele ya mashahidi ambao walishuhudia ndoa yetu.Mpaka hapa ilipofika mimi nina imani huyu mke wangu amekwisha nichoka na hana mpango na mimi tena.hata kama tukiamua kuyamaliza mambo haya kwa kusameheana na kuanza maisha mapya ni wazi ndani ya nyumba hakutakuwa na amani yoyote wala upendo tena.Mimi kwa moyo mweupe mbele yenu ninyi wazazi na mashahidi ninapenda kuweka wazi lililo moyoni mwangu.” http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikatulia kidogo huku kila mmoja akisikiliza kwa makini sana ili kusikia nitaongea kitu gani

    “Kama tulivyoapa siku ya ndoa yetu na padri akatamka kwamba kilichofungwa duniani kimefungwa pia mbinguni kwa maana hiyo ndoa yangu mimi na Emmy haitaweza kuvunjika hadi pale kifo kitakapotutenganisha.Pamoja na yote aliyonitendea lakini bado Emmy ni mke wangu na siku zote sintalisahau hilo.Pamoja na hayo lakini yeye kwa upande wake amelisahau hilo na kutamka wazi kwamba hajisikii tena kuwa na mimi mume wake wa ndoa na kwamba anahitaji kwenda kuishi na mwanaume mwingine ili walee mtoto wao.Natamka wazi kwamba yuko huru kwenda huko atakako kwenda.siwezi kumzuia kufanya atakavyo hata kama tunafungwa na ahadi ya ndoa.Kwa hiyo Emmy mimi nakuruhusu uende huko unakotaka kwenda,ukaishi kwa amani.Inaniuma sana lakini sina namna nyingine ya kufanya.Naamini mateso haya uliyonisababishia Mungu anayaona na iko siku atanipa faraja.Kwa hiyo mama uko huru kwenda unakotaka kwenda.Una ruhusa ya kuchukua chochote ukitakacho humu ndani.Mimi ya kwangu ni hayo tu” Nikasema na kuinama.Nilihisi maumivu makali ya moyo.



    Wote wakakaa kimya ni baba mkwe pekee aliyethubutu kufungua kinywa chake na kusema

    “Wayne tumeyasikia mawazo na maamuzi yako.Wote tulikuwa tukisubiri kusikia kauli yako ya mwisho kwa sababu wewe ndiye mwenye mke na sisi ni washauri tu.Wayne najua ni maumivu kiasi gani uliyoyapata kwa kitendo hiki alichokufanyia mwenzio.najua umeumia kupita kiasi japokuwa ni wewe mwenyewe unayejua ni kiasi gani umeumia.Pamoja na hayo yote Wayne napenda nipendekeze jambo moja kwamba bado kuwe na fursa ya majadiliano na kusameheana.Sisi sote ni binadamu na sote tunakosea.Baba wa mbinguni anaagiza kwamba mara zote tuishi kwa kusameheana hata pale ambapo mioyo yetu inakuwa migumu kusamehe.Sijui wenzangu mnalionaje suala hili? Baba mkwe akauliza

    Mwalimu wangu wa dini akasema kwa haraka

    “Mzee hata mimi nakuuunga mkono kwa hilo.Japokuwa masuala haya bado ni magumu na yanaumiza moyo lakini bado tunapaswa kusameheana kwa kila jambo.Hata mimi napendekeza hivyo kwamba tupate fursa ya kulijadili suala hili kwa undani na kusameheana ili maisha yaendelee na mtoto asiweze kuathiriwa na haya yaliyotokea kwani yeye ndiye atakayekuwa muathirika mkubwa”

    Mawazo yao yalikuwa mazuri lakini moyoni sikuwa hata na hamu ya kumuona tena Emmy.Nikainua kichwa na kusema kwa haraka.

    “wazee wangu mna wazo zuri lakini naomba niweke wazi kwamba mimi nilikwisha msamehe Emmy siku nyingi.Najua aliteleza kitu ambacho kila binadamu kinaweza kumtokea.Pamoja na kufanya hayo yote aliyoyafanya , bado Emmy ndiye aliyekuwa wa kwanza kuondoka hapa nyumbani bila kufukuzwa.Kwa maana hiyo ni kwamba hata tukikesha usiku na mchana tunajadili tayari mwenzangu hana mpango wa kuwa na mimi tena.Angekuwa ni mtu mwenye busara na mwenye kulitambua kosa lake angeweza kuomba msamaha lakini mpaka leo hajafanya hivyo.Ninyi wenyewe mmekuwa mashuhuda wa majibu anayoyatoa hapa mbele yenu.Mzee tusipoteze muda yeye aende tu anakotaka kwenda.” Nikasema huku hasira tayari ikianza kunipanda.Baba mkwe akamgeukia Emmy

    “Emmy umeyasikia aliyoyasema mwenzako? Baba mkwe akauliza .Emmy kwa sauti ndogo akajibu.

    “baba mimi nimekwisha sema siwezi tena kuishi na Wayne.hakuna haja ya kupoteza wakati kwa usuluhishi.Yeye amekwishanipa ruhusa niende kwa hiyo hakuna kitu cha kuendelea kujadili hapa.hata mkisema nini mimi siwezi kurudiana na Wayne.” Emmy akasema kwa kiburi.

    Baba mkwe akatafakari kwa sekunde chache halafu akasema

    “sawa Emmy tumekusikia.Tumekuelewa unataka kitu gani.nenda unakotaka kwenda lakini ukumbuke kwamba hii ni dunia.mambo uliyomfanyia mwenzio leo na wewe yatakukuta kesho.Siku zote asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na dunia.nakutakia kila la kheri huko uendako.” Baba mkwe akasema kwa hasira

    Baada ya kama dakika moja hivi ya ukimya baba mkwe akasema.

    “ Wayne vipi kuhusu mtoto Baraka.Kuna utaratibu gani kuhusu yeye?

    “Baraka ana haki ya kumfahamu baba yake mzazi.Haitakuwa jambo la busara kama tutamficha ukweli mtoto.Ni jambo zuri ikiwa atafahamu mapema kwamba baba yake si mimi.Iwapo tutamficha na akaja kufahamu tayari akiwa amekuwa mkubwa sana itamuumiza mno.Mimi naona ni bora kama tutafanya utaratibu ili aweze kufahamishwa na kwa baba yake.Hata kama nikiendela kumlea lakini awe akifahamu kwamba mimi si baba yake mzazi.Bado nampenda sana Baraka.Na endapo wazazi wake watakubali wanaweza wakamuacha hapa mimi nikaendelea kumlea……”

    Sikumaliza sentensi yangu emmy akajibu kwa haraka

    “Siwezi kumuacha mtoto wangu hapa.Ninapoondoka hapa leo ninaondoka na mwangu.Siwezi kuruhusu mwanangu aje kulelewa na mwanamke mwingine.Mwanangu nitamlea mimi mwenyewe.”

    Emmy alisema kwa ukali halafu akainuka na kuelekea chumbani kwa baraka.Kila mmoja alikuwa akishangaa

    “Wayne hivi huyu mwenzio amepatwa na matatizo gani? Kwa sababu naona si yule Emmy niliyemlea mimi.Amebadilika ghafla” Baba mke akauliza

    “baba hata mimi mwenyewe ninashangaa kwa mabadiliko haya .”

    Wakati tukiendelea kujadiliana kule sebuleni nikasikia Baraka akipiga kele chumbani kwake.Nikainuka na kuelekea chumbani kwa Baraka

    Emmy alikuwa akipakia nguo na vitu vya Baraka katika begi huku Baraka akilia kwa nguvu.

    “Baraka kuna nini ? Nikauliza baada ya kumkuta Baraka akigalagala chini.

    Aliponiona akakimbia na kunikumbatia.

    “Daddy ,mama anasema eti leo tunahama mimi na yeye tunakuacha peke yako.Halafu anasema eti anataka kunipeleka kwa baba yangu” Nilimuonea huruma malaika yule asiye na kosa. Nikambembeleza akanyamaza kulia halafu nikamwambia.

    “Baraka ni kweli mama yako anakupeleka ukamfahamu baba yako mzazi.Hatukukutaarifu toka mapema kwamba mimi si baba yako mzazi.Kwa hiyo B…….” kabla sijamalizia sentensi yangu baraka akachoropoka na kukimbia akajifungia bafuni akilia.

    Nikamfuata na kukuta tayari amekwisha ufunga mlango kwa ndani.Alikuwa akilia kwa nguvu

    “Baraka fungua mlango..Nikasema.

    “Sifungui mlango hadi uniambie wewe ndiye baba yangu.”

    Nikakosa jibu la kumpa.Roho ikaniuma sana kwa malaika yule kuteseka bila kosa.

    “Fungua mlango Baraka” Nikasema tena .

    “daddy sifungui mlango hadi uniambie wewe ndiye baba yangu.Mimi simtaki baba mwingine zaidi yako……….”

    Nilichomwa na maneno yale ya Baraka nikasimama na kuuma meno kwa hasira

    “Kwa nini Emmy unafanya hivi? Nikajisemea moyoni.

    .Kwa jinsi nilivyokuwa ninampenda mtoto yule sikutazamia kama itakuja tokea siku ambayo ataumia kama hivi.Nilisimama pale mlangoni nikiwa na hasira huku Baraka akiendelea kulia mle ndani bafuni.

    “Baraka fungua mlango ,nataka kuongea na wewe.Fungua mlango mwanangu” Nikaendelea kumbembeleza Baraka afungue mlango.Bado aliendelea kulia.

    “Baraka mwanangu nyamaza kulia na ufungue mlango.” Nikasema tena

    “baba sifungui hadi uniambie kwamba hautanipeleka huko mama anakotaka kunipeleka.Simtaki baba mwingine.wewe ndiye baba yangu” Baraka akasema.

    Wakati nikiendelea kumbembeleza baraka afungue mlango wa bafuni baba mkwe akatokea.

    “Wayne nini kinaendelea huku? Akauliza baba mkwe.

    “Mzee,Baraka amekimbia na kujifungia huku bafuni.Hataki kwenda sehemu yoyote ile.Nimejaribu kumbembeleza afungue mlango lakini amekataa hadi nitakapomuhakikishia kwamba mimi ni baba yake”

    baba mkwe akainama na kufikiri kwa sekunde kadhaa halafu akasema

    “Emmy amesababisha mambo makubwa mno.Sikutegemea kama itakuja tokea siku Emmy atakuja fanya mambo kama haya.” Baba mkwe akanong’ona.

    Kwa muda wa kama dakika moja tulikuwa tumesimama pale mlangoni huku Baraka akiendelea kulia mle bafuni.

    “Kwa hiyo umeamua nini Wayne? Baba mkwe akauliza.

    “Ni kama tulivyoamua pale sebuleni.Emmy ataondoka na Baraka na kwenda kumkabidhi mtoto kwa baba yake mzazi,halafu taratibu nyingine za kisheria na kikanisa zitafuata baadae.lakini kwanza baraka amfahamu baba yake”Nikasema

    “Sawa Wayne mimi siwezi kupingana na uamuzi wako japokuwa Emmy ni mwanangu lakini kwa dharau aliyoionyesha leo kwetu sisi wazazi wake na kwako wewe mume wake wa ndoa sina budi kukubali uamuzi wako huo kwamba aende anakotaka kwenda lakini ni dunia ndiyo itakayomfundisha.Mpaka umefikia uamuzi huu nina imani atakuwa amekufanyia mambo mengi ambayo huwezi kuyaweka wazi.lakini pamoja na hayo nina wazo moja.”

    “wazo gani baba?Nikauliza

    “Nataka nimpeleke Emmy huko anakotaka kwenda.Nataka nikamkabidhi kwa huyo mume wake mpya ambaye yeye ametamka mbele yetu kwamba ndiye anayemfaa kuishi naye.Kwa sababu yeye ameamua kuachana na kiapo chake cha ndoa alichoapa mbele ya mwenyezi Mungu,nitampeleka kwa huyo mwanaume ambaye yeye anamuona ni wa muhimu kwake .Inaniuma sana kufanya hivyo kama mzazi ambaye nilipaswa kuhakikisha mambo haya yanakwisha na mnakuwa pamoja tena lakini hata kama tukijaribu kuyaweka sawa mambo haya ili muishi pamoja Emmy atakuumiza sana na anaweza hata kukutoa uhai wako.Wayne acha tu niende nikamkabidhi huko halafu nitanawa mikono.Huyo Chris ndiye atakayekuwa ni baba na mama yake.” Baba mkwe akasema

    Nikakaa kimya kwa muda halafu nikasema

    “Baba tutakwenda sote”

    ‘Hapana Wayne nadhani ingekuwa vizuri kama ungebaki hapa halafu mimi na huyu mzee wa kanisa tutampeleka Emmy huko anakotaka kwenda.”

    “Nalijua hilo baba.Lakini ninaomba niongozane na ninyi .Hakuna chochite kitakachoharibika.Chris alikuwa rafiki yangu mkubwa sana.Sintamweleza chochote isipokuwa nataka aione sura yangu ili aendelee kuikumbuka katika maisha yake yote.”

    “sawa wayne kama umesisitiza basi hakuna shida.Sasa tunafanyaje kuhusu huyu mtoto aliyejifungia humu bafuni? Muda unazidi kusonga.”Baba mkwe akauliza

    “Nimekumbuka kuna ufunguo wa akiba.Ngoja nikauchukue “ Kwa haraka nikaelekea chumbani nikauchukua ufunguo wa akiba .Emmy bado alikuwa akikusanya nguo pamoja na vitu vyake vidogo vidogo.Sikusumbuka kumsemesha nikatoka chumbani na kurudi kule bafuni alikokuwa amejifungia Baraka.Nikachomeka ufunguo na kuufungua mlango.Baraka alikuwa amejikunyata katika pembe ya bafu akilia.Nilimuonea huruma sana mtoto yule lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya.

    Nilimfuata pale chini alipokuwa amekaa nikapiga magoti na kumfuta machozi.

    “baba naomba usinipeleke huko mahala mama anakotaka kunipeleka.” Baraka akasema

    “Nyamaza kwanza kulia baraka” Nikambembeleza

    “Baba mimi sitaki kuwa na baba mwingine.wewe ndiye baba yangu” Baraka akasisitiza

    “Nalijua hilo Baraka ,lakini huko mama yako anakotaka muende ni muhimu sana.Ila usijali tutakwenda wote.Mimi pia ninakwenda.”

    “na wewe unakwenda baba? Akauliza Baraka

    “Ndiyo Baraka.hata mimi ninakwenda huko.Inuka basi twende ukajiandae”

    Baraka akakubali ,akainuka nikamshika mkono na kumuongoza kwenda chumbani kwake.Nguo zake pamoja na vitu vyake vilikuwa tayari vimepakiwa katika masanduku .Niliumia sana moyoni .Sikutegemea kama ingetokea siku ningeachana na mtoto huyu niliyempenda kupita kitu chochote.Machozi yalikuwa yakinilenga lakini nikajikaza ili baraka asigundue chochote.Alipokuwa tayari nikamfuata mama yake kule chumbani.

    “baraka yuko tayari.Vipi uko tayari? Nikamuuliza Emmy lakini hakunijibu kitu.

    “kama kuna vitu vitabaki kesho nitamtuma dereva akuletee kila kitu unachohitaji” Nikasema

    “Sihitaji kitu chochote toka kwako Wayne.Nilichokuwa nikihitaji nimeshakipata.Nilikuwa nahitaji kuondoka tu hapa ndani.na tafadhali wayne nakuomba nikitoa mguu ndani ya nyumba hii usiendelee kunifuata wala kunipigia simu.Forget if I exist.Na wala usimfuate fuate Chris.hana kosa lolote mimi ndiye niliyemchagua”

    Emmy akasema huku amenikazia macho.Sikutaka kuendelea kubisha naye.Nikainua mabegi yake mawili nikaanza kuyatoa nje na kuyafungia katika gari lake.Mama yake aliyekuwa amekaa ndani ya gari baada ya kutolewa mle sebuleni kutokana na hali yake kuanza kubadilika alianza kulia aliponiona nikitoka na mabegi na kuyapakia katika gari la Emmy.nadhani alifahamu fika kwamba mambo yalikwisha haribika.

    “wayne baba usijali Mungu atakulipia.Mambo aliyokufanyia huyu mwenzio ni mambo mabaya sana” Akasema mama mkwe.

    “usijali mama hii ndiyo dunia na hii ni mitihani ambayo hatuna budi kuishinda.Nitakuwa salama mama usijali” Nikasema huku nikipiga hatua kurudi tena ndani.Nilijitahidi kutokuonesha hali yoyote ya huzuni japokuwa nilikuwa na maumivu makubwa ndani ya moyo.Nikachukua mabegi ya Baraka na kuyapakia pia ndani ya gari ya Emmy.

    “baba naona kila kitu kiko tayari.nadhani tunaweza kuondoka sasa” Nikamwambia baba mkwe.

    “Emmy tunakwenda wote hadi kwa huyo mume wako mpya.Tunataka tukakukabidhi huko” baba mkwe akamwambia Emmy aliyekuwa amesimama mlangoni akiwa na Baraka.

    “baba mimi nakwenda peke yangu.Sitaki mtu yeyote anifuate” Emmy akasema na kumfanya baba mkwe akunje uso kwa hasira

    “Emmy nakuonya kwa mara ya mwisho kwamba sintaendelea kuvumilia dharau zako kwetu.Umetudhalilisha kiasi ambacho wewe huwezi jua,lakini kama haitoshi bado unaendelea kutudharau.Nakwambia sintavumilia zaidi dharau zako.Kuanzia sasa nataka unisikilize mimi kama baba yako.Nakuonya usiendelee kunijaribu tena…” baba mkwe akasema kwa hasira huku akitoa kitambaa na kujifuta jasho.

    “wayne kama hakuna tunachokisubiri tena ,funga nyumba twendeni “ baba mkwe akaamuru.tayari alikuwa amekasirika .Nilimsifu sana baba huyu kwa ustahimilivu wake mkubwa kwa dharau za mtoto wake wa kumzaa.Dharau za Emmy hazikuwa zikimithirika.Sikujua sababu ya mabadiliko yale ya tabia ya Emmy.

    Nilifunga milango ya nyumba yangu huku roho ikiniuma kila nikimfikira baraka.Mimi na Beka pamoja na wale wasimamizi wetu wa ndoa tukaingia katika gari la Beka,halafu mzee wa kanisa akapanda gari moja na baba na mma mkwe ,Emmy akapanda gari lake akiwa na Baraka.Safari ikaanza ya kuelekea Njiro mahala anakoishi Chris.

    Usiku huu hakukuwa na msongamano mkuwa wa magari katika barabara iendayo Njiro.Kwa wakazi wa Arusha wanaufahamu msongamano mkubwa wa magari uliopo siku hizi katika barabara za jiji hili linalokua kwa kasi. Haikutuchukua muda mrefu sana toka maeneo ya Majengo ninakoishi mimi hadi maeneo ya Njiro. Safari yetu ilikuwa ni ya kimya kimya.Kila mtu alikuwa akiwaza lake.Tulikuwa tukilifuata gari la Emmy ambaye ndiye aliyekuwa akituongoza njia.Hatimaye gari ya Emmy ikasimama nje nyumba moja yenye geti kubwa jeusi.Akafungua mlango na kushuka garini.Baba mkwe naye akashuka garini.Kuona hivyo na sisi ikatubidi tushuke.

    “nadhani ni hapa” baba mkwe akasema.Nilipatazama mahala pale nikapatambua kwamba pale hapakuwa kwa Chris.

    “Mzee hapa si nyumbani kwa Chris.Ninapafahamu nyumbani kwake.Emmy anataka kutuchezea mchezo” Nikasema.Ni wazi pale hapakuwa nyumbani kwa Chris.Haraka haraka baba mkwe akamwita Emmy ambaye alikuwa getini akisubiri geti lifunguliwe.

    “Emmy nilikuonya toka mwanzo kwamba sintavumiia tena dharau na michezo yako ya kijinga.Hebu niambie hapa ndipo nyumbani kwa Chris?

    Babamkwe akauliza.Emmy hakujibu kitu akabaki kimya.Tukiwa hatuna hili wala lile tulitahamaki baba mkwe akimchapa Emmy kofi kali la shavuni linalompeleka Emmy chini.Alitaka kumfuata tena pale pale chini ili aendelee kumuadhibu lakini kwa jitihada zangu na Beka tukafanikiwa kumtuliza.

    “Haya ingia garini sasa hivi tunaelekea kwa Chris.Wayne ongoza njia kwenda kwa huyo mshenzi mwingine” baba mkwe akatamka kwa hasira.Emmy akasimama huku akilia akaingia garini na kuligeuza gari lake.Mimi nikatangulia mbele halafu gari la Emmy likafuatia na mwisho lilikuwa ni gari la baba mkwe.Dakika chache baadae tukawasili katika nyumba ya Chris.Gari zikasimama nikashuka na kumfuata baba mkwe.

    “baba ,Chris anakaa hapa” Nikasema

    “una uhakika Wayne? Baba mkwe akauliza

    “Nina ukakika baba” Nikajibu.Baba mkwe akashuka na kumfuata Emmy ambaye alikuwa ameuinamia usukani akiliahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hebu tuambie hapa ndipo nyumbani kwa Chris? Baba mkwe akauliza kwa ukali

    “Ndiyo .Ni hapa” Akajibu huku akijifuta machozi.

    “haya wapigie simu ndani watufungulie mlango”

    Sekunde chache geti likafunguliwa tukaingiza magari ndani.Baada tu ya kushuka ndani ya Gari Baraka akaja na kuung’angania mkono wangu.hakutaka kuniachia.Emmy akatuongoza na kuelekea sebuleni.Mara tu tulipoingia sebuleni nilipatwa na kitu ambacho siwezi kukielezea kama ni hasira au ni nini baada ya kumuona aliyekuwa rafiki yangu mkubwa Chris akiwa amekaa sofani akiangalia luninga huku mezani kukiwa na chupa kubwa ya mvinyo. Mapigo ya moyo yalibadilika na kuanza kwenda kwa kasi ya ajabu.Nikahisi jasho likilowanisha shati langu jepesi.Kichwa kiliwaka moto kwa hasira.Chris aliponiona nimesimama alipatwa na mstuko mkubwa akainuka na kusimama huku akiwa na wasi wasi mwingi.Niliushuhudia uso wake ukivuja jasho jingi.

    “Hallow…W..way.ne..” Akasema kwa sauti yenye kutetemeka.







    ITAENDELEA

    0 comments:

    Post a Comment

    Blog