Search This Blog

Friday, October 28, 2022

HOLLY SIN (DHAMBI TAKATIFU) - 3

 

     





    Simulizi : The Holy Sin (Dhambi Takatifu)

    Sehemu Ya Tatu (3)





    BADALA ya kujibu, Caro alijiinamia huku aking’atang’ata kucha kwani alikuwa akihisi aibu kubwa kwa mtu anayemheshimu kama baba yake, kumpa zawadi za aina hiyo.



    “Naongea na wewe Caro! Mbona hunijibu mama,” alisema mzee huyo akijisogeza na kumshika begani msichana huyo, akazidi kujisogeza kiasi cha kuanza kusikia pumzi na mapigo ya moyo ya msichana huyo mbichi.

    Kwa upande wa Aidan, alipotumwa na baba yake aliona kama amevurugiwa furaha yake ya kukaa jirani na Caro, akatoka mbiombio na kwenda dukani huku akikimbia, muda mfupi baadaye tayari alishapata vocha alizotumwa, akarudi mbio nyumbani kwao kwa lengo la kumuwahi Caro wake.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa jinsi alivyokuwa na haraka, aliingia ndani kwa kasi, akakutana na picha ambayo hakuitegemea. Baba yake alikuwa amekaa jirani mno na Caro, mkono mmoja akiwa amemshika begani huku msichana huyo, kipenzi cha moyo wake akiwa amejiinamia, aking’atang’ata kucha zake.



    “Vipi umepata? Nilikuwa nampa ushauri mwenzako hapa juu ya kukazania masomo, sitaki mje kututia aibu hapo baadaye kama ninavyokwambiaga kila siku,” mzee huyo alijivunga na kusimama, akapokea vocha na kuondoka kuelekea chumbani kwake.

    Aidan alibaki bado ameduwaa kwani japokuwa familia hizo mbili zilikuwa zimezoeana sana, hakuwahi hata siku moja kuona kitendo kama hicho, maswali mfululizo yakaanza kupita ndani ya kichwa chake kiasi cha kumfanya ajihisi kama amebeba mzigo mzito kichwani mwake.



    “Kwani baba alikuwa anakwambia nini?” Aidan aliuliza huku bado akiwa ameduwaa, Caro akashindwa cha kujibu zaidi ya kuchukua mkoba wake na kusimama, usoni akionyesha kukosa kabisa raha. Akawa anataka kutoka nje lakini Aidan alimzuia na kumkalisha kwenye sofa akitaka kujua kilichotokea.



    Wakiwa katika hali hiyo, mama yake Aidan ambaye muda mwingi alikuwa akiutumia kazini, aliingia na kuwakuta wanaye wamekaa sebuleni. Kwa kuwa zilikuwa zimepita siku nyingi bila kuonana na Caro, alimkumbatia kwa furaha na kumuuliza habari za safari.

    Ile furaha iliyokuwa imetoweka kwenye moyo wa Caro, ilirejea ghafla, akatabasamu na kuanza kumsimulia mama yake Aidan mambo yote yaliyotokea akiwa safarini. Baada ya kuridhika, mama yake Aidan aliwaacha wanaye sebuleni, akaenda chumbani kuungana na mumewe.

    Hata hivyo, Caro hakutaka kuendelea kukaa sebuleni hapo, akamtaka Aidan amsindikize nyumbani kwao na kama ni kupiga stori, wakapigie hukohuko. Bado hakuwa tayari kueleza chochote kilichotokea wakati alipobaki peke yake na baba yake Aidan.

    Siku hiyo ilipita, baada ya siku kadhaa mzee Kenan alikuja na hoja mpya ya kujifanya anataka kuwapeleka Aidan na Caro ufukweni kupunga upepo wa bahari. Awali Caro alikataa kabisa ofa hiyo mpaka mama yake akawa anamshangaa lakini alipohakikishiwa kwamba watakuwa na Aidan, alikubali kwa shingo upande.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hatimaye Jumamosi ikawadia, siku ambayo walipanga kwenda ufukweni. Japokuwa mkewe hakwenda kazini siku hiyo, mzee Kenan hakutaka kuongozana naye ufukweni pamoja na Aidan na Caro kwa madai kuwa siku hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya watoto wao, yeye asubiri siku yake.

    Kwa kuwa alikuwa akimuamini sana mumewe, alikubali na kushiriki kuwaandalia vitu vyote muhimu. Wakaondoka kwa gari la familia na kwenda mpaka Msasani Beach, sehemu ambayo mzee huyo alikuwa anapendelea kwenda kupumzika.

    Baada ya kufika ufukweni, mzee Kenan alijifanya ana mambo yake, akawaacha Aidan na Caro wastarehe wanavyotaka, wakaenda kuogelea na kucheza mchangani huku mzee huyo akiwa amekaa pembeni akinywa pombe kali kama kawaida yake.

    Aidan na Caro waliendelea kufurahi ingawa bado moyo wa Caro haukuwa na furaha kutokana na uwepo wa mzee huyo kwani alijua chochote kinaweza kutokea wakati wowote.

    “Aidan! Aidan hebu njoo mara moja,” alisema mzee huyo kwa sauti iliyoonyesha kuwa tayari pombe zilishaanza kumkolea kichwani.

    “Mama yako amenipigia simu anasema amepata dharura inayohitaji fedha na kadi ya benki nimetembea nayo mimi, hebu chukua Bajaj umpelekee mara moja, utatukuta hapahapa,” alisema mzee Kenan kwa sauti ya kilevi, kengele ya hatari ikalia ndani ya kichwa cha Caro.

    “Nitaenda naye baba, wala hatutakawia,” alisema msichana huyo, wazo lililopingwa vikali na mzee Kenan kwa madai kuwa wakiongozana wote, watachelewa kufika. Mvutano uliendelea lakini mzee huyo aliendelea kushikilia msimamo wake, Aidan na Caro wakawa hawana cha kufanya zaidi ya kukubaliana na maagizo hayo.

    Akatoa kadi ya benki pamoja na nauli ya Bajaj na kumkabidhi Aidan huku akimsisitiza awahi kurudi, akaondoka kwa shingo upande na kuwaacha na Caro. Muda mfupi baada ya kuondoka, mzee Kenan alisogea pembeni na kumpigia simu mkewe, akamwambia kwamba amemtuma Aidan ampelekee kadi ya benki ili aihifadhi kwani anaogopa kuipoteza kwenye mchanga wa bahari.

    “Sasa kwa nini usingeiweka kwenye gari? Huoni kama umemsumbua bure mtoto?” alilalamika mama yake Aidan, mzee huyo akamuweka sawa kwa maneno matamu kisha akakata simu.

    Harakaharaka akaanza kutembea kurudi mahali alikomuacha Caro ambaye bado alikuwa amevaa nguo za kuogelea na kujifunika kwa mtandio mwepesi juu ya nguo hizo.

    “Umewahi kunywa juisi ya kopo inayoitwa Redds?”

    “Hapana sijawahi.”

    “Basi ngoja nikuagizie uionje wakati tunamsubiri Aidan, naamini utaipenda,” alisema mzee huyo huku akimuita mhudumu na kumnong’oneza sikioni. Akaondoka na baada ya muda mfupi, alirudi na sinia lililokuwa na makopo matatu ya Redds pamoja na mzinga mkubwa wa pombe kali aliyokuwa anakunywa mzee huyo.

    “Yaani ukimaliza hizi zote nitakupa bonge la zawadi, we mwenyewe utafurahi,” alisema mzee huyo wakati akimfungulia Redds moja na kummiminia kwenye glasi, na yeye akafungua mzinga wake na kuanza kunywa taratibu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Bila kujua kama ile siyo juisi kama alivyoambiwa bali ni bia, Caro aligida glasi ya kwanza mpaka ikaisha huku akiisifia kutokana na ladha yake nzuri. Mzee Aidan akammiminia glasi ya pili na kumpa. Alipoimaliza, tayari alishaanza kubadilika, akawa anachekacheka huku akiyarembua macho yake kama amekula kungu, hali iliyomfurahisha sana mzee huyo.

    Alipomaliza chupa ya pili, tayari alikuwa tilalila, akamuinua na kuanza kumkokota kuelekea mahali alikopaki gari lake.

    “Leo ndiyo leo, asemaye kesho mwongo,” alisema mzee huyo huku akijilamba midomo kutokana na uchu aliokuwa nao.





    ALIPOMFIKISHA kwenye gari, alimpandisha kisha akamfunga mkanda, harakaharaka na yeye akapanda na kuliwasha gari. Akaondoka kwa kasi kuelekea mafichoni kutimiza azma yake. Caro hakuelewa chochote kilichoendelea kwani kutokana na kuzidiwa na kilevi, aliuchapa usingizi mzito.

    Aidan akiwa ndani ya Bajaj akiwahi nyumbani kumpelekea mama yake kadi ya benki kama alivyoagizwa na baba yake, alishtuka baada ya simu yake kuanza kuita mfululizo. Harakaharaka akaitoa simu yake na alipoangalia namba ya mpigaji, aligundua kuwa ni mama yake.

    “Haloo mama, nipo njiani nakuja kukuletea kadi ya benki.”

    “Kwani umefika wapi mwanangu?”

    “Ndiyo tupo hapa kwenye daraja la Msasani, kuna foleni lakini tutawahi,” Aidan alisema kwa kujihami akidhani mama yake alikuwa akitaka afike haraka nyumbani. Hata hivyo, tofauti na alivyotegemea, mama yake alimwambia kitu tofauti:

    “Sikia mwanangu, hiyo kadi we itunze utakuja nayo baadaye, rudi ukaendelee kufurahi na mwenzako ufukweni, baba yako akikuuliza mwambie mimi ndiyo nimekwambia urudi.”

    “Sawa mama, ahsante sana,” alisema Aidan na kumuamuru dereva wa Bajaj apunguze mwendo na kugeuza. Japo dereva alishangazwa na uamuzi wa ghafla wa mteja wake, hakutaka kuhoji sana kwani alichokuwa anakitaka ni fedha tu.

    Akageuza Bajaj na kuanza kurudi Msasani Beach Club huku Aidan akiwa na furaha ndani ya moyo wake kwani kiukweli japokuwa hakuwa na uwezo wa kubishana na baba yake, hakufurahishwa kabisa na kitendo cha baba yake kumtibulia starehe na kumtuma nyumbani.

    Akili yake yote ilikuwa kwa Caro, alitamani waendelee kucheza kwenye mchanga na kuogelea baharini, akajikuta akitabasamu wakati Bajaj ikiendelea kupenya kwenye foleni kurudi Msasani.

    Baada ya kufika kwenye njia panda ya kuelekea ufukweni, wakati dereva wa Bajaj akiiacha barabara ya lami na kuingia ya vumbi, Aidan aliona gari kama la baba yake kwa mbali likielekea upande wa Kawe lakini hakutilia maanani sana akiamini huenda amelifananisha.

    Baada ya kufika Msasani Beach Club, alimlipa dereva wa Bajaj fedha yake kisha harakaharaka akashuka na kuanza kuelekea upande wa nyuma alikowaacha baba yake na Caro. Cha ajabu, alipofika kwenye meza aliyokuwa amekaa baba yake, alikuta ikiwa tupu, akahisi huenda na yeye ameenda kutembea kwenye mchanga wa bahari.

    Harakaharaka akatoka kwenye geti na kuelekea baharini lakini Caro hakuwepo pale alipomuacha, akaanza kuangaza macho huku na kule lakini hakumuona Caro wala baba yake. Alirudi ndani na kuendelea kuangaza huku na kule akidhani labda wanaweza kuwa wamehama meza lakini hakufanikiwa kuwaona.

    “Au lile gari nililoliona kule barabarani kweli lilikuwa la baba? Lakini kwa nini waondoke ghafla wakati tumekubaliana nikirudi nitawakuta hapa?” Aidan alijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.

    Ikabidi aende kwenye meza aliyokuwa amekaa baba yake akiamini wanaweza kuwa hawajaenda mbali, akakaa na kuanza kusubiri huku muda wote akiangaza macho huku na kule.

    Licha ya kuendelea kusubiri kwa muda mrefu, Aidan hakumuona baba yake wala Caro huku giza nalo likianza kuingia. Hakuwa na cha kufanya zaidi ya kutafuta usafiri wa kumrudisha nyumbani kwao, akili nyingine ikimtuma kuamini kwamba huenda wamepishana na wao wamesharudi nyumbani.

    Wakati akiondoka, alijaribu kumpigia baba yake simu yake lakini haikuwa ikipatikana hewani, jambo ambalo siyo kawaida yake. Alitamani Caro naye angekuwa na simu ampigie na kumuuliza yuko wapi lakini haikuwezekana kwani msichana huyo alizuiwa na wazazi wake kumiliki simu mpaka atakapokuwa mkubwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huku akiwa na mawazo mengi ndani ya kichwa chake, Aidan alienda kupanda Bajaj na kumuelekeza dereva sehemu ya kumpeleka.

    Furaha yote aliyokuwa nayo siku hiyo iliyeyuka kama theluji iyeyukavyo juani, akaendelea kuwaza kwa muda mrefu mpaka alipowasili nyumbani kwao, akashuka kwenye Bajaj na kumlipa dereva fedha zake, breki ya kwanza ilikuwa nyumbani kwa akina Caro kumuulizia kama amesharudi.

    “Sasa Aidan, wewe unamuulizia Caro si mliondoka pamoja? Kwani umemuacha wapi mwenzako,” mama yake Caro alimuuliza Aidan huku na yeye akionyesha kupatwa na mshtuko.

    “Tulipishana kidogo, yeye akaondoka na baba, nadhani watakuwa wamekwama kwenye foleni,” alijibu Aidan kwa kifupi huku akianza kuondoka. Mama yake Caro alimrudisha na kuendelea kumhoji maswali mbalimbali, alipomhakikishia kwamba yupo na baba yake, angalau aliridhika na kumruhusu aondoke.

    Akatoka na kuelekea nyumbani kwao alikomkuta mama yake akiandaa chakula cha jioni. Nako alikutana na maswali kama yaleyale aliyoulizwa na mama Caro. Mama yake alishangaa kwa nini amerudi peke yake wakati alishamwambia akaendelee kujumuika na Caro na baba yake kisha warudi pamoja.

    “Tulipishana nao, nafikiri wamekwama kwenye foleni kwa sababu mimi nilipanda Bajaj,” Aidan alijibu kwa kifupi na kwenda chumbani kwake, akajitupa kitandani huku mawazo yakiendelea kukisumbua kichwa chake.

    Mama yake naye alibaki na mawazo mengi kwani mfululizo wa matukio yaliyokuwa yanatokea tangu jioni, ulimfanya ahisi kuna jambo halipo sawa kati ya Aidan na Caro ingawa hakumuwazia kabisa mabaya mumewe.

    Muda ulizidi kuyoyoma bila baba Aidan wala Caro kurejea nyumbani, hali iliyoanza kuwapa wasiwasi wazazi wa pande zote mbili. Muda mfupi baadaye, mama na baba Caro wakafika nyumbani kwa akina Aidan kumuulizia binti yao.

    Kilichowashangaza zaidi ni kwamba wakati Caro alikuwa hafahamiki mahali alipo, Aidan alikuwa chumbani kwake amejifungia, jambo ambalo halikuwa kawaida kwani tangu wakiwa wadogo, walizoea kuongozana popote wanapokwenda na mara zote wazazi wao hawakuwa na wasiwasi wanapokuwa wawili.

    “Ni saa nne na nusu sasa bado mtoto hajarudi nyumbani, siyo kawaida yake,” alisema mama yake Caro, mumewe naye akakazia lakini mama Aidan aliwatoa wasiwasi kwamba hakuna kitakachoharibika kwa sababu yupo na mzee Kenan.

    “Au inawezekana wamepata ajali? Foleni gani hiyo muda wote wawe hawajafika nyumbani?”

    “Hebu ngoja nijaribu kumpigia simu mzee mwenzangu nijue nini kimetokea,” alisema baba yake Caro lakini alipojaribu kumpigia simu mzee Kenan, hakuwa akipatikana hewani, hali iliyozidi kuwachanganya wote.





    AKAWAAMBIA wazazi wake jinsi alivyopewa juisi za kwenye makopo na mzee Kenan na jinsi alivyoleweshwa na juisi hizo.

    “Baada ya hapo nini kiliendelea?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sikumbuki baba, nilijihisi mwili wote ukiishiwa nguvu na sikuelewa tena kilichoendelea mpaka nilipozinduka na kujikuta nimelala chumbani kwangu.”

    SASA ENDELEA…

    “MUNGU wangu, mbona sitaki kuamini macho yangu?” alisema baba yake Caro baada ya kusikia maelezo hayo ya mwanaye, akamgeukia mkewe ambaye alikuwa amejiinamia akilia kwa uchungu.

    Kwa jinsi walivyokuwa wakiheshimiana na mzee Kenan, hakuna aliyekuwa tayari kuamini kwamba anaweza kumfanyia ukatili huo binti yao ambaye kimsingi ni sawa na mwanaye. Ikabidi wasogee pembeni na kuanza kujadiliana nini cha kufanya, Caro akawa anaendelea kulia.



    “Haiwezekani mume wangu, lazima tuchukue hatua, siwezi kukubali mwanangu aharibiwe kirahisi namna hii wakati nimehangaika sana kumlea mpaka amekuwa mkubwa,” alisema mama Caro huku naye akiendelea kulia kwa uchungu.



    Uamuzi ambao waliufikia kwa pamoja ilikuwa ni kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi haraka iwezekanavyo. Wakamchukua binti yao na kwenda mpaka kwenye gari lao, wakaingia na kuondoka kuelekea kituo cha polisi.



    Walipofika waliandikisha maelezo kisha wakapewa fomu maalum kwa ajili ya kwenda hospitali ili Caro akapimwe na daktari ili kuthibitisha kama kweli amebakwa. Wakaondoka pamoja mpaka hospitali.

    “Baada ya tukio ulienda kuoga?”

    “Ndiyo dokta.”



    “Ulikosea sana kwani umevuruga kabisa ushahidi, itakuwa vigumu kumtia hatiani mbakaji kwani hakuna tena ushahidi, pole sana binti,” alisema daktari wakati akiendelea kumfanyia vipimo Caro. Wazazi wake waliendelea kuhuzunika, kila mmoja macho yakiwa mekundu kutokana na kulia.



    Baada ya daktari kumaliza kazi yake, walirudi kituo cha polisi ambapo mipango kwa ajili ya kwenda kumkamata mzee Kenan ilianza. Mkuu wa kituo akatoa gari pamoja na askari watatu kwa ajili ya kwenda kumkamata mzee huyo mwenye roho ya kinyama.

    ***

    Mzozo mkubwa uliendelea ndani ya nyumba ya mzee Kenan kati yake na mkewe, wakawa wanalumbana vikali kuhusu tukio lililotokea usiku. Mzee Kenan alikuwa akisisitiza kwamba hakufanya jambo lolote baya zaidi ya kunywa pombe mpaka usiku.



    “Hujafanya kitu? Hata aibu huna mwanaume wewe.”

    “Sijafanya kitu kweli mke wangu, mi nilikuwa nakunywa pombe tu.”

    “Na mtoto wa watu? Yaani umemlewesha mtoto wa watu ili ufanikishe lengo lako, mwanaume muuaji wewe sijapata kuona, nataka talaka yangu,” alisema mama Aidan huku na yeye akianza kulia.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Japokuwa hakuwa na uhakika wa kilichotokea, ushahidi wa mazingira ulimfanya aamini kwamba lazima mumewe alimuingilia kimwili Caro.

    Mzozo ulipoendelea, ilibidi mzee huyo aamke na kuanza kujiandaa kuondoka huku akiwa bado na pombe kichwani. Akatoka na kumuacha mkewe akiwa anaendelea kulalama na kulia kwa uchungu.



    “Nitauficha wapi uso wangu mimi? Mwanaume umenitia aibu wewe sina hamu. Lazima utatoa talaka yangu,” alisema mama Aidan wakati mumewe akitokomea kusikojulikana. Hakutaka hata kuondoka na gari, akatembea kwa miguu mpaka barabarani alikosimamisha teksi.

    ***

    “Sisi ni maafisa wa polisi kutoka kituo cha kati, hivi ni vitambulisho vyetu,” askari watatu wenye silaha walijitambulisha kwa mke wa mzee Kenan, wakamueleza kuwa walikuwa wakimhitaji mumewe.

    “Amefanya nini tena?”

    “Ataenda kujua mwenyewe kituoni,” alisema askari mmoja huku akionyesha kutokuwa na hata chembe ya masihara. Wakaingia mpaka ndani lakini hawakumkuta mzee huyo.

    “Ameenda wapi?”



    “Wala hajaniaga, ameondoka muda si mrefu,” alisema mama Aidan huku akiwa bado amepigwa na butwaa. Kwa kuwa mtuhumiwa hakuwepo, walimwambia kuwa itabidi wamchukue yeye mpaka kituoni ili iwe rahisi kumpata mzee Kenan.



    Aidan aliyekuwa bado amelala, alishtuka baada ya kusikia mzozo sebuleni kwao, mama yake akibishana na watu. Harakaharaka akaamka na kuvaa nguo zake, akatoka mpaka sebuleni.

    “Mungu wangu, kuna nini tena,” alijiuliza huku akiwa amepigwa na mshangao kuwaona askari wenye silaha wakijibizana na mama yake, akasogea kutaka kujua kinachoendelea.

    “Tunamchukua mama yako mpaka baba yako aje kujisalimisha kituoni,” alisema askari mmoja huku wakimchukua mama Aidan. Wakatoka naye hadi nje na kumpakiza kwenye ‘difenda’, wakaondoka naye kwa kasi kubwa.



    “Kwani kumetokea nini? Kwa nini baba anatafutwa na polisi?” Aidan alijiuliza bila kupata majibu, ikabidi atoke mbio mpaka nyumbani kwa akina Caro kuwapa taarifa ili kama kuna uwezekano wawasaidie.

    Alishangaa kukuta mlango umefungwa kuashiria kwamba hakukuwa na mtu yeyote ndani. Hali hiyo ilizidi kumchanganya, akawa anajiuliza wameenda wapi asubuhi yote hiyo? Hakupata majibu. Harakaharaka akarudi mpaka nyumbani kwao, akachukua simu yake na kuanza kutafuta namba ya baba yake.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipoipata alianza kupiga lakini iliita bila kupokelewa. Akatoka na kusimama mlangoni, akaendelea kupiga lakini simu ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa. Alipopiga kwa mara ya tatu, aligundua kuwa simu ilikuwa ikiita kutoka ndani ya gari la baba yake.

    “Kwani baba ameenda wapi mpaka aache simu yake?” alijiuliza lakini bado hakupata majibu, ikabidi aingie ndani na kwenda kuchukua ufunguo wa gari, akatoka na kulifungua kwa lengo la kuchukua simu ya baba yake.



    Ghafla aliona kitu kwenye siti ya nyuma kilichomshangaza sana. Akiwa ni kama haamini, alisogea taratibu huku akikichunguza vizuri kitu hicho. Ilikuwa ni nguo ya ndani, tena ya kike ikiwa kwenye siti ya nyuma ya gari hilo la baba yake. Alipoichunguza vizuri, aligundua kuwa ilikuwa imechanwachanwa, akazidi kujiuliza maswali yaliyokosa majibu.

    “Mungu wangu? Kwani nini kimetokea? Mbona sielewielewi?”







    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog