Search This Blog

Friday, October 28, 2022

NENDA NA MOYO WANGU - 4

 

     





    Simulizi : Nenda Na Moyo Wangu

    Sehemu Ya Nne (4)





    Nikaanza kulia kwa uchungu kwa kuwa nilihisi mambo yanazidi kuwa mazito katika kichwa changu. Unadhani ingekuwa rahisi kumsikiliza baba kuwa nisimuamini mama kwa atakachonieleza? Yaani mwanamke aliyeniweka tumboni kwake miezi tisa kisha akanizaa kwa uchungu? Hakika nilijihisi naukaribia uchizi. Yule askari wa kike akanieleza. "Michael ahusiki na mauaji nakusaidia kidogo ili usichanganyikiwe zaidi"



    Kisha akanipapasa kwa mikono yake laini akaondoka.

    "Huyu naye!?" Nikajiuliza, ina maana anamtetea Michael kwa kuwa anamjua muuwaji? Ina maana yeye ananifahamu basi kabla mimi sijakamatwa na kukutwa na kesi hii?



    "Ni nani mwanamke huyu?" Nikaanza kuingia katika uchunguzi wangu. Nikahisi kuwaza sana kichwa kitaniuma, wazo la mwisho ndio nililiona nafuu. Kumchunguza huyu askari wa kike.



    Nilikuwa na nia ya kumchunguza kwanza katika uhusiano wake yeye na mama yangu mzazi, kwa kuwa nakumbuka mara ya mwisho mama kuja alimvuta pembeni na kuna mambo walizungumza kwa siri, ni nini hicho walikuwa wakizungumza? Ndio nilitaka nianze hapo. Kwa kuwa mara baada ya mama kutoka pale aliondoka akiwa na haraka huku akiwa ameacha lile alilotaka kuanza kuniambia hewani na mwisho akilikana.



    Kisha nitataka kujua amenijuaje mimi na kujua mambo mengi yanayonihusu, si rahisi kwa askari wa kawaida ambaye si mpelelezi wa kesi yangu kugundua watu wanaonihusu. Ningeweza kumuhusisha na mauaji haya lakini kwa kuwa alikuwa na ukaribu na mama nilijua fika huenda mama alimueleza mengi nikataka kuyajua. Pia nikachanganya ile hali ya aksari kuja pale nyumbani kwa Beatrice nikazidi kusisimkwa na vinyweleo vyangu huku akili ikizidi kuwa makini na yote yaliyokuwa yakiendelea.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kisha alionekana kuvutiwa hivyo nilifahamu fika isingekuwa shida kutumia hila zangu katika udhaifu wake kumpata na kumteka kimapenzi na kisha atanieleza mengi. Nikaingia katika njama za kumpeleleza askari yule wa kike. Nikarudi zangu mahabusu nikimsubiri aniletee chakula cha usiku. Saa 2:14 haikuwa mbali na wakati niliusubiri akawa anaingia amebeba sinia lenye sahani ya chakula. "Leo kuna ugali, kisamvu na samaki"



    Akaniambia huku akiweka sinia lile chini mbele ya meza yangu. "Ahsante nitakula"

    Nikamshika mkono kwa minajiri ya kumpapasa nikiwa nimeanza rasmi kuingia kazini kujua ni kitu gani anafahamu.Mpapaso muruwa wa mikono yangu laini hakika ukamchanganya yule askari wa kike. Niliona akilegea na kunitazama kwa jicho la huba. Zilidumu sekunde kadhaa kisha akauputa mkono wangu akaropoka.



    "Niache, usithubutu tena kufanya hivyo nitakushitaki" Akaondoka huku akiwa ametazama uso wake juu sehemu zilipo kamera za ulinzi wa eneo hilo. Nikaelewa kwanini hata uso wake haukonesha ile hasira aliyoiigiza. Nikajipa moyo siku bado zipo

    Siku iliyofuata aliniletea gazeti lenye kipande cha karatasi ndani yake. Sikuweza kujua mwanzo sababu ya kunitupia gazeti lile, aliponikonyeza nikakionana kikaratasi kilichoanguka.

    Kiliandikwa hivi

    "Hii si sehemu sahihi ya mimi na wewe kuwa kama unavyotaka iwe. Jitahidi kucontrol hisia zako ili wasishitukie chochote wakubwa"

    Nilipomaliza nikatabasamu na kukikunja kunja kipande kile cha karatasi nikakitupia mdomoni. Yule askari wa kike aliona nilichokifanya akatabasamu kule alipo na mimi nilimuona pale nilipo. Tabasamu langu lilikuwa la kikebehi kwa kuwa huenda hakutambua kua mimi sikufanya vile kwa lengo la kimapenzi bali kumchimba nipate kile alichokuwa akikificha.

    Majira ya saa saba mchana alinijia tena yule askari wa kike akiwa ameongozana na Michael, walinikuta nikiwa nimekaa kwenye makochi ya sebule ya nyumba ile nikitazama kipindi cha Tusker project fame. Nilitabasamu nilipomuona Michael lakini yeye uso wake ulikuwa wenye huzuni na hasira iliyoambatana nayo.

    "Karibu"

    "Siamini kama umeona unisingizie upumbavu wako"

    "Una maanisha nini?" Nikamuuliza Michael kwa kuhamanika kiasi.

    "Ina maana si wewe uliyemuelekeza yule malaya(akimaanisha Vanessa) nyumbani kwangu? Amekuja kuniuliza na kunishitumu kuwa mimi ndiye muhusika wa mauaji ya Beatrice, ina maana Ramon umedhamiria kuniangamiza? Kweli?"

    Nikacheka kwa kebehi na wala sikuona kama Michael alikuwa hana hatia, macho na uso wake huku sauti yake ikimtetemeka ilionesha dhahiri ni kiasi gani alikuwa akificha jambo alilojitahidi kulificha lakini alishindwa kutokana na uoga.



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sina cha kukuambia lakini sheria itafuata mkondo wake na ukweli hautajificha"

    Akaniambia jambo lililonishangaza "Laiti kama ungemjua muuaji, usingethubutu kunipakazia ujinga wa namna hii ninachopenda kukuambia kuwa usitamani kumjua muuaji wa mpenzi wako maana hutatamani kumuhukumu na wala hutatamani kuishi"

    Akanyanyuka na kuondoka huku maneno yake yakaja kufanya kazi baada ya siku ishirini na moja. Siku ya leo nikiwa naandika barua hii huku nikiwa nimemjua muuaji wa Beatrice na kweli dakika chache baadaye na dhamiria kuitoa roho yangu nikapumzike na Beatrice. Inauma! Inauma sana...

    "Basi tuendelee wewe ukisoma barua hii yenye kisa cha kweli kwa mtiririko sahihi ili hadithi ya mambo mabaya kuliko yote niliyowahi kuyapitia yasikuchanganye" Ikabidi niwe mpole mara baada ya Michael kuondoka. Yule askari wa kike akanijia akiwa amepishana na Michael pale mlangoni alipokuwa anaingia na Michael akitoka.



    "Huyu rafiki yako vipi? Mbona ana hasira hivi?" Alikuwa amesimama wala hakutaka kukaa karibu yangu. Nikaona uso wake kama wenye kunipa ujumbe fulani lakini sikuutambua. Ikabidi nimuulize swali.

    "Unaitwa nani?"

    "Jina langu wewe la nini?"

    "Unadhani najisikia vizuri kuishi na mtu nisiyemfahamu? Kwanza huna kwenu?" nikamtazama kisha nikaendelea "maana haiwezekani wewe ushinde na mimi tu kila siku na sikuoni ukienda kwako ina maana wewe hujaolewa" Yule askari akacheka kisha akanijibu huku nusu akicheka nusu akijitahidi kutaka kuongea

    "Naitwa Bella"

    "Bella!? Yule msichana aliyezungumza na shetani?" Yeye akacheka zaidi na mimi nikatabasamu tu, akanijibu "kile ni kitabu tu cha kubuni hakina uhalisia wowote. Unadhani ni rahisi kuzungumza na lucifa? Utazungumza na pepo wake lakini sio yeye mwenyewe bwana" Nikaona uelekeo wa kuelewana na huyu askari sasa ulikuwa mzuri, nikafurahi kumfahamu kuwa anaitwa Bella.

    "Ni jambo zuri kukufahamu, acha nikalale"

    "Haya usiku mwema" Nikamuacha mimi nikaelekea zangu kulala.

    Asubuhi iliyofuata niliamshwa na moshi wa sigara uliokera pua yangu, ile kuamka tu nikakutana uso kwa uso na yule mpelelezi Jafari Hiza.

    "Za siku nyingi?" Kwa mang'amung'amu huku usingizi bado ukiendelea kung'ang'ana katika macho yangu nikaitika huku nikipikicha macho kutoa tongotongo.

    "Salama habari yako"

    "Nimekuja kuzungumza na wewe muda wa kuchezeana akili na kuulizana kuhusu habari umepitwa na wakati jiandae kisha kuna chumba utaletwa mimi nitakuwepo huko nakusubiri"

    Akatoka akiwa ameizima sigara yake pale mlangoni aliposimamiahuku akiwa aaisaga kwa kisigino cha mguu wake. Wakaja askari wawili kutoka nyuma ya mgongo wake na kunifunga pingu, Bella akaingia.

    "Naomba kuzungumza naye" Wale askari wawili hawakuzungumza chochote wakaniacha kisha walitoka wakiniacha mimi na Bella katika chumba kile cha mahabusu.

    "Unajua unapoenda?" Bella akaniuliza uso wake ukionesha wasiwasi.

    "Sio katika chumba cha mahojiano?"

    "Ni cha mahojiano lakini si kile ulichokizoea huko kuna hatari zaidi ya uijuavyo hatari yenyewe. Jitahidi kila neno ulilokwishazungumza usilibadilishe zaidi ya kuliongea lile lile ulijualo"

    Hofu ikanikumbatia na kunipa joto kiasi cha kunitoa jasho. Bella akatoka na kuwaita wale askari wawili waliondoka mwanzo na kunifunga ile pingu ya myororo, wakanipeleka katika chumba fulani hivi. Huko wakanivua shati nikabaki kifua wazi na kukalishwa katika kiti ambacho sikufahamu hapo mwanzo sababu ya kuletwa hapo licha ya kujuwa kwa kuambiwa kuwa ni chumba cha mateso.

    "Leo utaeleza ukweli" Jafary Hiza akazungumza huku wale askari walionileta ndani ya chumba hiki nilichokuwa nikikiogopa, wakinifunga kwa kukaza kamba zao miguu yangu na mikono kwa kuniunganisha na kiti kile.

    "Mfungeni vizuri asilete shida baadaye" Niliisikia sauti kutoka nyuma ya mgongo wangu huku mlango ukiwa unafungwa. Jafary hiza akawa anatabasamu kwa kebehi akimtazama mgeni huyo aliyeingia kwa sasa. Nilipogeuka kumtazama alikuwa ni Oscer Valerian, baba yake Beatrice. Yeye akanitazama kwa dharau zaidi.

    "Kwanini mnanifanya hivi?"

    "Kwa kuwa wewe ni muuwaji na unastahili kuuwawa" Mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakienda kasi kuliko kawaida ya mapigo yake. Nilitamani kulia lakini sikuona sababu ya kulia mbele za watu wasio na huruma.

    Mbele yangu askari wale wakaleta vifaa ambavyo sikuvifahamu kazi yake, Jafary hiza akainua kifaa kimoja kinachofanana na bisibisi na kukifunua na kubana sehemu ya chuchu zangu.

    "Nitakuuliza na utajibu niliochokuuliza" Nikiwa naugulia maumivu, niliuma meno huku nikiitikia kwa kichwa kwa kumaanisha kukubali.

    "Yule msichana alikukosea nini?" Hapo alipunguza ukali wa kukibana kile kifaa huku Oscer akiwa pembeni ya Jafary hiza akitazama kila kinachoendelea.

    "Hatukuwahi kugombana hata siku moja" nikasema na alipobana tena nikapiga kelele "ayyyy!!!"

    "Sasa inawezekanaje ukamuua kinyama kiasi kile? Ulirukwa na akili?"

    "Mimi.. Mimi sifahamuuuuu yalaaaaaaa!!"

    "Kwanini umeuwa pumbavu!" Oscer alizungumza kwa hasira na kuninasa kibao. Jafary hiza akahama kutoka kwenye chuchu zangu na kuhamia kinywani.

    "Nitakung'oa meno usipowataja washirika wenzako wengine mlioshirikiana kumuuwa Beatrice na kusema sababu ya kumtoa roho yake"

    "Kwanini mnamchelewesha? Hana anachoeleza yeye na mpuuzi mwenzake Michael lazima damu ya mwanangu ilipwe" Oscer alifoka kwa hasira.

    "Nipo tayari kufa kama mmekosa imani nishamkabidhi Beatrice moyo wangu muda mrefu na kufa kwake kunanishangaza hata iweje moyo wangu bado unafanya kazi nifanyeni mtakacho kama mnadhani mnatenda haki"

    Kisha kilichofuata sikukitambua kutokana na lile lililofanyika ghafla bila kutarajia. Niliona giza zito likitanda mbele yangu na kila kiungo changu cha mwili kikikosa nguvu. Kumbe kile kiti nilichokalia kina umeme na swichi yake iliwashwa na Oscer mwenyewe, nilimuona nilipokuwa nikifunga macho taratibu huku nikijaribu kupambana na hali ile. "Nakufa!? Hapana siamini sio sasa, bado sijamaliza kuandika bado sijamjua muuwaji kwanini nalala? Sitaki kufa sasa hivi" nilijisemea hivyo na kisha nikapokelewa na usingizi.

    Nilipofumbua macho yangu kwa mara ya kwanza kitu cha kwanza kukiona mbele yangu anha! Hapana ulikuwa ni uso ulionitazama kwa chini ulipo uso wangu mimi nikimtazama juu ulipo wake.

    "Baba"

    nikaita kwa sauti ya utulivu na kavu bila shaka.

    "Pole sana mwanangu utapona" Kitendo cha kupewa pole kutokana na kukumbuka kuwa nilipigwa na yule askari Jafary Hiza akishirikiana na Oscer Valerian kuniadhibu, roho yangu iliniuma na kuanza kubwabwaja "Acha waniue baba acha nife kwa ajili ya Beatrice najisikia fahari kufa kwa ajili ya Beatrice. Nimemkabidhi yeye moyo wangu hawezi kuondoka mpaka na mimi nife acha baba"

    Niliongea maneno ya uchungu kiasi kwamba mimi na baba tulilia kama watoto pale wodini. Pia nikaona kitu ambacho kabla sijaendelea sana na mtiririko wa kisa hiki nisije nikasahau kukueleza, nilishangaa kumuona baba akitembelea gongo huku hali yake ikionesha kuwa ni dhaifu sana, nikahisi anaumwa au amepata ajali. Nikamuulizahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Baba unaumwa?"

    "Hapana mwanangu" Sauti yake ikakaa mbali na ukweli mara nikahisi kitu kikubwa kimejificha ndani ya nafsi yake. Sikuking'amua wakati huo ambao na mimi nilikuwa katika matatizo ni mpaka hapo baadaye alipokuja kunieleza mkasa mzima ambao sikuwa nikiujua hapo mwanzo. Lakini kabla sijafika huko ambako ndiko mwisho wa story hii nikueleze tu kuwa baba alipigwa na watu waliohusika kumuua Beatrice wangu, kwa kipindi hicho ambacho nipo hospitalini, sikuweza kujua kwa kuwa hakunieleza chochote.



    "Baba kuna kitu unanificha" nikamdodosa nikijaribu kumkazia macho kwa ukali kidogo.

    "Kila kitu kina wakati wake utakuja kuelewa baadaye mwanangu pole kwa mateso yote unayoyapata"

    "Ahsante baba lakini mbona unafahamu mengi ambayo hutaki kunieleza?"

    "Nikikueleza yote sasa nitakufa! Subiri nipate nguvu ya kupambana"

    Nilishituka na kushangazwa sana sikutaka baba afe kabla hajanieleza ukweli nikanyamaza kimya nikimtazama kwa kustaajabu. "Unataka nikueleze sasa? Nipo radhi kufa kwa ajili yako?"

    "Hapana baba, bado nakuhitaji" "

    "Basi subiri muda utakapofika" Baba akaniambia, kisha aliingia Vanessa pamoja na daktari aliyevalia joho jeupe la kiuuguzi. "Du ana bahati sana. kuzimia siku mbili kutokana na shoti ya umeme?nilidhani angekufa. Ana maisha marefu sana huyu kijana" alisema yule muuguzi na kunichanganya zaidi.

    'Ina maana mimi nililala hapa kitandani siku mbili mnh!!' Nikajiuliza kwa wasiwasi nikimtazama baba kisha Vanessa aliyekuwa akitabasamu nikamgeukia yule muuguzi akiwa anafunga dripu mpya ya maji.

    "Umepona wewe ni jasiri mwenye nguvu" muuguzi yule alinieleza maneno ya kunitia nguvu kiasi nikafarijika. Baba akaniaga "Nitarudi tena siku nikipata nguvu zaidi"

    "Njoo mapema kabla hawajaniua baba"

    "Hauwezi kufa mpaka uijue haki yako" baba akaondoka mimi nikamtazama mpaka alipoishia. Yule muuguzi akamfuata nyuma baba yangu nikabaki mimi na Vanessa.

    "Hapa ni hospitali ama wapi?"

    "Safe house" Vanessa akanijibu kiuwepesi.

    "Ina maana hii nyumba ni kubwa hivi? Nilidhani ni hospitali"

    Vanessa akacheka hakunijibu jambo. Akakaa pembeni yangu akinipa pole kwanza na mimi nilipoitikia mahojiano mafupi yakaanza tena hapo hapo nikiwa kitandani mara tu baada ya kutoa ile tepurekoda yake.

    "Nilikutana na Michael" aliniambia huku akiitengeneza tepurekoda yake.

    "Alinieleza na kunijia juu sana kwamba kwanini nimemchoma kwa mpelelezi kuwa yeye ndiye anahusika na mauaji"

    "Inawezekana akawa ama asiwe bado kuna utata"

    Nikamtazama Vanessa kwa mshangao mkubwa macho yakinitoka pima na kuanza kunichanganya upya. 'Iweje Vanessa naye abadilike sasa na kuwa upande wa Michael'

    "Sipo upande wa Michael" ni kama kwamba aliweza kuyasoma mawazo yangu, akaendelea "Nilipomuhoji Michael sikuona hatia katika maelezo yake lakini sitaki kuthibitisha ni hakika kuwa hajahusika ila uchunguzi bado unaendelea lakini nilipochukua alama za vidole vya Michael havikurandana na vile vilivyokutwa katika mwili wa Beatrice. Sifahamu nini sababu au nini kimetokea lakini Michael hakuna kidhibiti cha kumuhusisha na mauaji yale hivyo bado uchunguzi unaendelea huku utata mwingi ukiendelea kugubika mauaji haya"

    "Kivipi"

    "Kuna alama nyingine ya vidole tulipozipima na vyako vimeshabihiana kwa asilimia tisini hivyo unaendelea kuwa muuaji namba moja uliyeshirikiana na wenzako katika kutekeleza jambo lile. Hutapelekwa mahakamani mpaka uchunguzi utakapokamilika. Jopo la wapelelezi nikishirikiana nao pia tumepewa siku kumi na nne tu kukamilisha zoezi hili kuanzia leo nasubiri ukipata nafuu niweze kuendelea kukusikiliza maisha yako kwa ujumla na Beatrice ili niweze kuangalia ni nani mwingine ambaye anaweza akawa amehusika na mauaji yale"

    Nikashusha pumzi nzito kwa kuwa niliyaona maji shingoni mwangu. Sikuwa na jinsi sasa maana hata tumbo nilihisi likinguruma kwa uoga huku nikitoa hewa chafu kwa mbali. Vanessa akanyanyuka na kuniaga huku akinieleza "Sasa ni saa 4 na dakika ishirini asubuhi nitakuja saa 12 jioni kuzungumza na wewe kwa kuwa hatuna tena muda mrefu wa kukaa na kuzungumza"Wakati Vanessa ametoka hazikupita dakika nyingi na Bella akawa ameingia. Aliingia akiwa amebeba chupa ya maji makubwa ya kilimanjaro na hotpot la kuhifadhia chakula. Alipolifunua, kulikuwako na vipande vya nyama ya kukaangwa na wali hotpot la pili kulikuwa na mchuzi wa maharage.

    "Umeamini sasa nilichokuwa nikikueleza?"

    "Nini?"

    "Kuhusu Michael!"

    "Anha! Mi nachanganyikiwa tu hata sielewi"

    "Unaonaje ukisikia muhusika ni baba yako?"

    "Unasemaje?" Kiukweli nikahamanika kwa jambo hilo aliloniuliza. sidhani kama kipo ambacho kingetokea na kunifanya niamini kuwa baba au mama yangu anaweza akahusika na mauaji.

    "Haiwezekani" nikasema huku nikikaa vizuri "baba yangu hawezi kumuua Beatrice"

    Bella akacheka kwa kebehi na kunieleza. "Ngoja nikupe kama hadithi tu ya kubuni halafu upime maelezo yangu na uchambue utakavyoweza. Lakini huu ni msaada mdogo tu ninaokupa usinihusishe kama shahidi katika kesi yako" aliniambia hivyo huku mimi nikiwa nimelala nikabaki kimya kumsikiliza.



    "Mama na baba yako wamekuwa na ugomvi wa mara kwa mara"

    "Ndiyo ni kweli" nikamjibu.

    "Baba yako amekuwa akiuchukia ujio wa Michael nyumbani kwenu na mara kwa mara amekuwa akikuambia usimuamini mama yako kwa lolote atakalokueleza"

    "Ndiyo" nikaendelea kumjibu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwanini baba yako amekuwa akificha mambo kwa visingizio kuwa atauwawa"

    "Nini?" Nikaanza kuingiwa na wasiwasi. Huyu Bella amejua mambo mengi sana yanayonihusu mimi na familia yangu amejuaje yote hayo? "Wewe ni nani? Na umejuaje mambo haya yote?"



    Bella akacheka na kuniambia "Mimi ni Bella Matondane ni askari wa jeshi la polisi la jamhuri ya muungano wa Tanzania umenisahau? Kufahamu hayo ni sehemu ya jukumu langu kufanya uchanguzi katika kutaka kukusaidia juu ya tatizo hili linalokukabili. Ninachoamini mimi na wachache kati yetu ni kuwa wewe hujauwa ila hapa kuna mkono wa mtu na mkono huo ni mtu wako wa karibu sana na anayekuhusu ndiye amehusika amka Ramon usipende kuamini vitu nusu nusu chunguza kwa umakini utambue nani mbaya wako"



    "Huna unachoniambia nikakuelewa" nilihisi naanza kuchanganyikiwa. Sikutaka kuamini kuwa huyu askari sasa anamuhusisha baba yangu na mauaji ya Beatrice, nikabaki nikiwa nimeikunja midomo yangu na macho pia





    "Ni kweli unachanganyikiwa haswa ukisikia kuwa anayehusika ni ndugu yako sina shaka ukija kumjua utaumia zaidi na kuchanganyikiwa kuliko hata hivyo hivi karibuni mambo yatatimia"



    Akawa anatoka na mara mlango ukafunguliwa. Alikuwa ni baba akiwa ameongozana na Oscer baba yake na Beatrice. Bella alipowaona wakiingia watu wale alishituka sana, nilishangazwa kushituka kwake kwa kuwa kama Oscer wameshakutana mara kadhaa hapo katika nyumba salama iweje ashituke wakati yule ni baba yangu aliyekuwepo katika chumba hiki dakika arobaini na tano zilizopita. Baba pia alishituka vivyo hivyo huku akijitahidi kumtazama kwa makini Bella bila kupata jawabu la msingi ambalo lilimfanya aulize kwa sauti

    "Bibi, nadhani tuliwahi kukutana sehemu?" Akawa anamtazama juu mpaka chini na kuendelea "Sikujua kama wewe ni askari"

    Oscer alikuwa akiwatazama baba na Bella kama nilivyokuwa nikifanya mimi kwa mshangao.

    "Nini kinaendelea!?"

    Bella akajibu kwa sauti ya kitetemeshi “Hapana mzee, umenifananisha”

    Nikajiuliza huku nikisubiri ujio wa Oscer na Baba chumbani kwangu una ujumbe gani kwa mara nyingine niliyodhani baba amekwishaondoka.

    Bella alipojibu hivyo, alifanya haraka akatoka nje huku baba akibaki akimtazama kwa nyuma akiwa ameshikilia magongo yake. Kisha alipogeuka akawa kama ananong'ona na mzee Oscer



    "Huyu binti namfahamu na niliwahi kumuona sehemu ambayo si nzuri sasa sikumbuki ni wapi kabisa yaani"



    Oscer akamshika bega baba kiurafiki kitu ambacho kikanifaraji huenda kuna mapatano kiasi ambayo sikuyafahamu.



    "Habari yako ndugu" Oscer akanisalimia

    "Salama shikamoo"

    "Marahaba, pole kwa yote”

    "Ahsante" nikajiulliza ina maana si yeye aliyenifanyia? Mbona hana dalili za kuomba radhi?

    "Ona unavyotesa wazazi wako? Wanabaki kugombana huko nje kwa sababu yako? Naomba uniambie tu mwanangu kwa urafiki sasa achana na yale yaliyopita siku chache zilizopita, kwanini umemuua mwanangu, mwanangu mpendwa na wa pekee ambaye alibaki badala ya mama yake kwanini umemuuwa!"



    Akaanza kushika shati yangu huku akinitingisha tingisha kwa hasira machozi yakimtoka yaliyoongozana na kamasi jepesi. Baba alijitahidi kumzuia lakini alionekana kuelemewa na ulemavu wake.



    "Naumia sana Lameck mtoto wangu wa pekee? Shenzi nitamuuwa Ramon. Hatonyongwa nitahakikisha namuuwa kwa mkono wangu"

    "Niue sasa hivi usichelewe ukamuumiza baba yangu"

    "Pumbavu nyamaza!" Ikawa patashika ndani ya chumba hicho. Baada ya Oscer kuninyamazisha, baba akanizaba kibao. Ikabidi ninyamaze kutazama kinachoendelea.

    "Niambie kwanini umemuuwa mwanangu" Oscer akazungumza kwa tuo aliouwekea msisitizo.

    "Mzee wangu mimi sijamuuwa nakuhakikishia mimi sijamuuwa"

    "Na alama za vidole vilivyokutwa shingoni na mikononi mwake vilikuwa ni vya nani?"

    "Sifahamu mzee wangu mimi sijauuwa" nikaanza kulia kwa uchungu huku baba akinitazama akiwa analia. Oscer akanitazama kwa hasira akiwa amekunja ngumi akanieleza "Mimi hutaniona tena, siku utakayoniona jua kuwa ndio siku ya kifo chako kwa heri" Akatoka baba akimfuata kwa nyuma.

    walipokuwa wakitoka, nikawa katika hali ya hudhuni huku hali hiyo ikinikosesha rah asana. Nikajaribu kukumbuka kila hatua zangu na vipi niambiwe ni mimi nahusika hata alama za vidole vyangu vikutwe katika shingo na mikono ya Beatrice. Akilini mwangu kukagonga kengele, ndioyo ni kengele ya kunikumbusha jambo. Nilikumbuka siku niliyopata taarifa kutokana na ujumbe uliotoka kwa Beatric akiniuliza kuwa kwanini namuuwa na hali ya uoga iliyonikumba siku hiyo. Nimekumbuka jambo, nimekumbuka, nimekumbuka jamani. Nikapata picha ya siku ile ya mwisho naukuta mwili wa mpenzi wangu ukiwa chini unaelea juu ya dimbwi la damu. Nimekumbuka sababu ya mimi kuhusishwa na mauaji. Nikatamani kunyanyuka nimuite baba yake Beatrice na baba yangu pamoja na Vanessa awepo niwaeleze jambo hili mara nikagundua kuwa mkono wangu umefungwa kwa pingu kwenye kitanda kile, harakati zangu zikapoa nikaendelea kuwaza tukio lile kwa nikiwaza uzembe nilioufanya.Niliwaza kuwa, siku ambayo nilifika nyumbani kwa Beatrice, mara nilipomkuta amelala kwenye dimbwi la damu na bila shaka roho ilikuwa imekwishamtoka; niliogopa sana na hivyo nilichanganyikiwa na kila nilichokifanya nilifanya kwa kuongozwa na uoga nilio nao. Vidole vile vilivyokutwa katika mwili wa mpenzi wangu, ni kweli zilikuwa ni alama za vidole vyangu lakini si kweli mimi nilihusika kumuuwa Beatrice. Nilimshika mara nilipoingia katika chumba kile ili kuhakikisha kama amekufa kweli, hapo ndipo nilipoacha alama za vidole vyangu. Lakini ninani atakayeamini? Ni nani atakayenisikiliza kama kila mtu ananiona

    mimi ni muuaji? Nikakumbuka jambo lingine. Beatrice alinitumia ujumbe usiku ule kuwa mimi nimemuua na kwanini namuua, si kweli kama Beatrice atakuwa alituma ujumbe ule kwa mkono wake mwenyewe, na kama siye yupo aliyehusika. Hapo ndipo nilipokuwa nikipataka kwa hamu, nikalivua

    shuka nililofunikwa kisha nikakaa kitako nikaitazama ile dripu iliyokuwa ikitiririsha maji katika mishipa yangu, kasha na mkono ule mwingine niliofungwa pingu katika kitanda kile cha chuma, nikaendelea

    kuliwazia jambo lile kwa undani zaidi nikiona kuwa lilikuwa lina mantiki kubwa ya kumshirikisha pia na Vanesa. Basi nikaona endapo kamasi ujumbe ule ulioandikwa kwa kutumiwa simu ya Beatrice uliandikwa na mtu mwingine, kuna uwezekano mtu huyo aliacha alama za vidole katika simu ya mpenzi wangu. Lazima apatikane na ajulikane ni nani na hiyo ndiyo njia ya kuvua kitanzi cha lawama na fedhea iliyonikumba kuwa nimemuua Beatrice.

    Bado wasiwasi wangu ukaganda kwa Michael huku nikitabasamu kwa ushindi na mara mlango katika wodi ile ukafunguliwa.Alikuwa ni dokta ambaye alikuja kuniambia kuwa nimekwishapata nafuu, hivyo baada ya dripu hiyo ningeruhusiwa kutoka katika chumba hicho. Daktari mwenyewe hakuwa mbali na uaskari kutokana na ukakamavu wa sura yake na ujamali wa misuli ya mikono yake. Hiyo ikawa habari njema kwangu kutoka katika chumba hicho kinachonuka madawa lakini pia nilitaka kumuomba Vannesa aipeleke kesi mahakamani haraka ili nipate kujua hatima ya maisha yangu. Nimechoka kuishi kwamawazo, hisia na wasiwasi. Hali hiyo ikasukumwa na hamu iliyojaa huku shahuku ikimwagika nilipotaka kumuona Michael akiadhibiwa kwa kosa la kumuua Beatrice. Niliamini upelelezi ukikamilika utaangukia kwa

    Michael. Pia jambo nililowaza la kupima alama za vidole kutoka kwenye simu ya Beatrice lilikuwa wazo zuri, nilitaka kumshirikisha Vanesa pia.

    Masaa matatu baadae niliruhusiwa kutoka hapo nikiwa katika ulinzi mkali wa polisi. Baada ya kula chakula cha usiku nikiwa nimejipumzisha katika mahabusu yangu, Bella akanijia na mimi wazo

    fulani likaniingia. Nikamwambia "Hivi ninaweza kuwasiliana na Vanesa?"

    "Unataka kumwambia nini?" Aliniuliza kwa mshituko uliojitengeneza

    katika uso wake kisha alizuga nisiweze kumuona, nikaonesha kutojali

    nikamwambia "Kuna kitu nimeanza kugundua nahitaji kuzungumza nae"

    nilizungumza hivyo kumpima kama ataamua kunisaidia au lah! Lakini

    alinisaidia kwa kunipa usiku huo huo tena kwa usiri mkubwa. Alioondoka

    kisha alirudi dakika chache baadaye na mto mweupe msafi na akaniambia

    jambo ambalo nilimuelewa kwa haraka "Utumie mto huu" akiushika kwa

    msisitizo "Usiku wa manane sana kwa kuwa huu ni msafi tofauti na

    uliolalia hiyo ni baada ya kwenda kuoga" nikatingisha kichwa kwa maana

    ya kuonesha kuwa nimeelewa kisha yeye akaondoka. Nikauweka mto

    ule wenye simu chini yake

    kwenye kitanda changu nikisubiri muda wa

    kuwasiliana na vanesa.

    Nilipoegesha kichwa changu kwenye tendegu ya kitanda, nikapitiwa nausingizi mwepesi ule wa mang'amung'amu. Muda mchache baadaye niliamshwa na kelele za mbwa waliokuwa wakibweka ovyo nje ya nyumba hiyo. ilikuwa yapata saa saba na dakika zake kwa mujibu wa saa ya kwenye simu niliyokabidhiwa na Bella. Ilipowaka nikairudisha ile simu chini ya mto na mimi nikanyanyuka kwa

    hatua za kunyata mpaka katika geti la mahabusu il. nilijitahidi kutazama kushoto, kisha kulia

    nikauona moshi ukitoka upande ule kilipo chumba kilichotumika kama jiko. Nikarudi pale kitandani

    na kuitoa ile simu; kitu cha kwanza nilichofanya ni kutazama salio, ilikuwemo ya kutosha. Nikajaribu

    kuzikumbuka namba za Vanesa alizonipatia siku za nyuma endapo nitahitaji kuzungumza naye kwa

    wakati ambao hatakuwepo. Nikaijaribu ya kwanza sauti ya kike ikanijibu kuwa

    "namba unayopiga haipo, ..."Sikutaka kumalizia kusikiliza nikasonya kwa hasira huku nikinakili namba nyingine, hiyo ikaita. Sekunde chache sauti ya kike ikakoromachomboni huku ikiwa katika utulivu wa uchovu wa usingizi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Halo"

    Nikajikohoza kidogo kuirekebisha sauti yangu ilianisikie kwa ufasaha nitakapozungumza kwa sauti

    ya chini kabisa. kisha nikasema "Ramon hapa tafadhali naomba tuzungumze kwa

    meseji" nilimsikia akishituka mara aliposikia jina langu, bila shaka alikuwa na maswali mengi ya kuniuliza

    lakini sikumpa nafasi hiyo nikakata simu. Punde ukaingia ujumbe kutoka kwake

    "umepata wapi simu ya mkononi?"

    "huku huku ndani ya nyumba salama, kuna jambo nimegundua nadhani litasaidia" nikamjibu

    huku nikiwa makini kuuficha mwanga wa simu ile usije ukawashitua walinzi, nilikuwa nikituma na kusoma jumbe zile chini ya mto

    "kesho nitakuja huna sababu ya kumuamini yeyote kuanzia sasa kwa kuwa kuna mengi nimegundua ya kukushitua lakini wewe ni mwanaume yapasa ujipe moyo na kuukubali ukweli. usiku mwema"

    Nikatamani kumuuliza mambo mengi lakini ikawa ni kama kwamba hakuitaji kuendelea kuchati na

    mimi, hivyo nikaizima simu nikalala.

    kesho asubuhi niliamshwa na sauti ya Bella "Nipatie mto na foronya yake nitakuja jioni tena"

    Nilipoelewa alichomaanisha, mimi nilimwambia "Hapana huu wangu unatosha usiniletee tena"

    akatingisha kichwa na kuondoka, mara nikashituka. Nikakumbuka kuwa zile jumbe

    nilizokuwa nikichati na Vanesa sikuzifuta hali ya wasiwasi na uoga ukanivaa kwa kuwa bado sikuwa

    nikimuamini askari yule moja kwa moja. "potelea mbali" nikaitupa mikono hewani na

    kuelekea zangu sehemu ya kunawia uso na kusafisha meno. Nilipomaliza na kuoga, ndipo

    niliambiwa kuwa kuna mgeni wangu ananisubiri ukumbini. Nilifanya haraka haraka nikijua kuwa ni

    Vanesa.

    Nilipofika pale ukumbini, nilimkuta Vanesa amesimama eneo la dirishani huku akitazama nje. Alikuwa ameikunja mikono yake kifuani nakama aliyekuwa ameikalia meza ya vitabu iliyopo pale. Mchakacho wa

    hatua zangu huenda zikamfanya ageuke kule nilipokuwa natokea mimi, kisha nikafunguliwa zile pingu za mikono zilizounganisha mpaka miguu yangu kisha wale askari wakaondoka. waliniacha mimi na Vanesa pekee,

    Vanesa akanisalimu. "Nimeshapoa dada yangu ila nahitaji unisaidie jambo hili kabla ya

    yote" Baada ya salamu nikamwambia Vanesa. Yeye alivuta kiti kilichopo pale karibu yake na kuutua mkoba begani mwake huku nami nikikaa mkabala naye. Vanesa alionekana kuwa mtulivu zaidi na kuniambia

    "Nieleze unahitaji msaada upi na kisha usinifiche jambo" Akayakaza macho yake na vituta vya mistari juu ya uso wake vikajichimba,akaendelea "Ni nani aliyekupa simu ama wapi ulipata"

    Nikacheka niliposikia hivyo na sikuwa na sababu ya kumficha jambo, ilakule kuwa na sura siriazi kukanifanya nimuone kama kituko. Nikamueleza ukweli "Kwanza nashukuru kwa kuamua kunitetea au kuisimamia kesi hii japo ni upande wa mlalamikaji uliokutuma kusikiliza utetezi wangu. Hivyo

    sijajua nia na sababu ya mzee Oscer lakini naamini hana nia mbaya

    kabisa na mimi. Vanesa kuna alama za vidole katika faili la kesi hii

    vilivyopatikana katika mwili wa marehemu Beatrice, basi naamini

    nikikueleza hili hutaweza kuamini"

    "Nieleze kila kitu" vanesa alinikatisha huku akiwa amekwishawasha tepurekoda yake. Nikaendelea kumueleza jinsi ilivyotokea mpaka nilipomshika Beatrice aliyekufa na alama za vidole vyangu vikabaki katika mwili wake

    "Hiyo ni kesi mbaya na ngumu sana"

    "Sasa nitafanyaje Vanesa na imeshatokea?" Nikauliza kwa kukata tamaa

    na nikaamua kuitupa kete yangu ya mwisho, nikamueleza "Kuna jambo nimelifikiria nadhani litanisaidia"

    "Lipi?" akauliza huku akinitazama kwa makini.

    "Kama unakumbuka inasemekana Beatrice alinitumia ujumbe kwenye simu yangu kuwa kwanini namuuwa je unadhani kulikuwa kuna uwiano wa yeye kuituma meseji ile kama ni mimi kweli nilimuua?"

    nilimuona Vanesa akiwa amebung'aa na huenda alikuwa akisisimukwa na kile

    nilichokuwa nikimueleza, nilimuona akivutiwa na mkondo wa maongezi

    lakini alishindwa kuzungumza neno, nikaendelea

    "Basi kama kulikuwa hakuna ulazima kuna aliyefanya jambo lile na mtu

    huyo ndiye amehusika na mauaji haya kwa asilimia kubwa lakini je

    unadhani tutampataje?"

    "Wewe umefikiria nini kwanza? maana umenipa mwanga mpya" alisema nusu akifurahi kwa raha huku akiwa amejawa na shahuku

    "Aliyetuma ujumbe ule aliiacha simu eneo la tukio?"

    "Ndiyo" Vanesa akanijibu

    "Simu ile ipimwe alama za vidole kisha itakuwa rahisi kumjua muhusika

    wa tukio hili kwa kuwa naamini atakuwa ni muhusika ambaye askari

    wanayo rekodi ya mambo yake ya kijambazi hapo nyuma. muuaji mgeni

    hawezi kufanya tukio la kijasusi kama hili na baada ya hapo tutajua pa

    kuanzia"

    Vanesa alisimama na mimi nikasimama, akawa anaizima tepurekoda ile kisha akanipa mkono wa pongezi.

    "Nafurahi kumtetea mtuhumiwa mwenye kunuka upelelezi naomba nikafanye

    jambo hilo sasa hivi na jioni ama kesho nirudi na majibu kamili"

    "Je yale uliyogundua wewe ni yapi?" Nikauliza nilipomuona akifungasha

    "Nishamjua muuaji lakini si sahihi kukwambia sasa ila nilizungumza na

    Michael pia hausiki na mauaji haya acha niukamilishe ushahidi ili

    keshokutwa upande mahakamani"

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikaa na mawazo mengi mara baada yaVanessa kuondoka. Nilijiuliza kwanini Vanessa aone Michael tenaahusiki katika mauaji haya? sasa kama si yeye, ni nani basi anahusika?amesema anamjua, atakuwa ni nani huyo ambaye mimi sijamjua katikamaelezo yangu yote niliyoyatoa? Nilipokuwa nimekaa peke yangu, nikawanimezama katika tafakuri iliyonikumbusha mambo kadhaa nyuma

    yaliyopita.









    ITAENDELEA  

0 comments:

Post a Comment

Blog