Simulizi : Nenda Na Moyo Wangu
Sehemu Ya Tano (5)
MAMBO HAYO YALIKUWA HIVI
Nikiwa chumbani kwangu siku ambayo Michael
alikuja na mimi ndio kwanza nilikuwa nimetoka kumsindikiza, babaaliingia akiwa na hasira.
"Ni mara ngapi nikuambie sitaki kumuona yule kijana hapa nyumbani?"Nilimtazama baba kwa hasira kila nilipomtazama na kumuona ni mzeeanayezeeka vibaya. Kwanza Michael alipokuwa akija nyumbani,
akimsalimia baba alikuwa haitiki. Sikupenda kumuuliza kwanini alikuwahaitiki salamu ya rafiki yangu huyo na hata hivyo sikumjibu palealipouliza mpaka aliporudia tena
"Nakuuliza, kwanini unamleta yule muhuni nyumbani kwangu?"
"Baba yule sio muhuni na sioni ubaya wowote aliokufanyia naomba umuheshimu"
Baba alicheka kicheko ambacho hakikuwa na ladha ya kuwa kicheko balikaraha, kisha akanizaba kibao kikali na kunieleza"Yule si rafiki mwema kwako na hafai kuwa rafiki yako mshenzi wewe"
Akatoka huku akiniacha nimelishika shavu langu kwa maumivu. sikuwaza
kwanini aliniambia vile, au kwanini alimchukia kiasi kile mpaka siku
ambayo nikiwa nimekaa nje ya nyumba yetu nikijisomea kitabu ndipobaba
aliponijia tena.
"Hujambo!?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nilimtazama na kuitika sijambo kisha nikamsalimia.
"Marahaba, nataka kuzungumza na wewe Ramon"nikakitua kitabu kile kwenye mapaja yangu nikamtazama baba"Mwanangu, wewe ni mwanangu wa pekee na unajua ni kiasi ganinakupenda. Sio kwamba ninapokukataza kuwa na urafiki na Michael ninania mbaya na urafiki wenu. Michael ni rafiki mliyekutana chuo wotemkiwa mmeshakuwa wakubwa na kila mtu ana tabia zake, Michael unazijuazake?" akaniuliza, mimi nikatingisha kichwa"Hapana" nikajibu
"Basi ni hivi, Michael anawatumia wanawake waliomzidi umri kwa
kuwachuna na kuyaendesha maisha yake, miongoni mwa wanawake hao ni
mama yako"
Nilikumbwa na mshituko nikayatoa macho pima nisiamini nilichokisikia
nilibaki kinywa wazi huku nikiendelea kumtazama baba, wala yeye hakuongea
chochote alipoona nimehamanika, akaondoka.Mawazo hayo yalikatishwa na sauti ya Bella yule askari wa kike.
"Chakula tayari"nikala pale na kisha nikarudi pale ukumbini kutazama runinga.
Kesho yake alikuja Vanessa kama alivyoahidi akiwa na ujumbe mzitoulionishitua na kunifanya nijue mengi. Hapo mwanzo sikujua kama Bella alihusika katika
kumuuwa Beatrice, basi ndivyo ilivyo kwenye ripoti ya Vanessa
aliyoshika mkononi mwake.
Mimi na Vanessa tulisalimiana akiwa amebebabahasha pekee ya kaki mkononi mwake. Hakuwa na chochote, hata ulemkoba wa kuhifadhia tepurekoda yake.
"Pole sana kwa matatizo"ghafla kabla sijaitikia salamu ile, nilimsikia yule askari wa kike,
Bella akipiga kelele"Niacheni, niacheni nasema. Mnaniumiza!!"
Nikamgeukia Vanessa kwa macho ya mshangao na kumuuliza
"Vipi, kuna nini?"Vanessa alibitua midomo huku tabasamu laini likimpitia akiwa ameinua
mabega yake kwa dharau. Akanitupia ile bahasha
"Tulipopima ile simu ya mpenzi wako(Beatrice) alama za vidole
vilivyoshika na kutuma ujumbe ule kwako, ni alama za vidole vya huyu
askari"
Wakati nikiyasikiliza hayo, nilikuwa nikimtazama Bella aliyekuwa
akitolewa nje ya jumba lile kinguvu. Alikuwa akilalamika kwa huruma na
majonzi
"Mimi sihusiki jamani, mimi sijauwa"Ndio neno la mwisho kulisikia kutoka kwa Bella na mara nikamgeukia
Vanessa, aliendelea kunieleza"Unajua si rahisi kupata matokeo ya alama za vidole vya mtu ambaye
rekodi yake haipo katika rekodi ya jeshi la polisi lazima mtu huyu awe
ni mtu ambaye amewahi kutenda makosa ya jinai na kukamatwa ama kwa mtu
ambaye ni mwajiriwa wa serikalini ambaye alitia sahihi ya dole gumba
kwa wino katika karatasi zake za mkataba. Hivyo ilikuwa rahisi kupata
taswira ya huyu koplo Bella Daniel Zagamba na uzoefu wake kazini
pamoja na mwaka alioajiriwa"Nikashusha pumzi ndefu kwa uzito wa taarifa ile iliyozidi
kunikanganya, ikabidi nimuulize Vanessa huku nikimrudishia zile
karatasi
"Huyu askari amekua karibu na mimi kwa kipindi chote tangu nimeletwa
humu ndani na alionesha kuyajua mengi kuhusu kesi hii lakini
inawezekanaje yeye awe ndiye muuaji? Vile vile haitwi Bella Daniel Zagamba yeye ni Bella Matondane inakuaje hii?"Vanessa alicheka kwa kebehi na kunieleza kwa umakini"Hili jambo ni zito Ramon si rahisi kuamini ukitajiwa muuwaji lakiniinabidi uvumilie na uyashinde. Wivu wa mapenzi ndio uliosababisha kifocha mwenzi wako na aliyemuua ni mtu wako wa karibu"
Nikamkatisha "nilijua tu, nilijua ni Michael. Michael ndiye alimuuwa
Beatrice kwa kuwa Beatrice alinipenda mimi"
"Usipende kuongozwa na hasira katika jambo kama hili nimekwisha
kueleza Michael hausiki na mauaji haya"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Una maana huyu askari alikuwa anamuonea wivu Beatrice? huyu askarialikuwa ananitaka? mbona mimi nilikuwa simjuhi?"
Vanessa alicheka kwatuo na kunyanyuka kisha alitembea taratibu mpaka
mlangoni akafungua mlango na alipokuwa akirudi ndani, alikuwa
ameushika mkono wa baba yangu. Sikuweza kutambua chochote lakini
nilibaki na mshangao nilipomuona baba yangu ni mzima na mwenye afya
ukiacha kiasi cha siku mbili nyuma alipokuwa akitembelea magongo.
Vanesa alimkaribisha baba katika ile meza yetu maongezi yakaanza mara
nilipomsalimia baba
"Ramon baba yako ana mengi ya kukueleza ndio maana
sikuwa na sababu ya kukueleza yote kuhusu nilichogundua ila huyuatakueleza kila kitu"
Vanessa aliongea yake na baba alikohoa kama anayeitafuta sauti yake,
mimi nikabaki njia panda nikimtazama baba na kisha Vanessa alikuakitabasamu.
"Kuna nini?" Niliuliza"Mwanangu" Baba akazungumza "Nilikueleza nitakapopata nguvu ya
kuzungumza nitakueleza muuwaji wa msichana wako(Beatrice)"
Baba akaanza kunihadithia kila kilichokuwa kikiendelea hapo nyuma
mambo mengi ambayo nilikuwa mimi siyafahamu.
HAPA NAKUHADITHIA KILE AMBACHO BABA ALIKUWA AKINIELEZA.
Ilikuwa ni baada ya miezi miwili tangu niingie pale chuoni nikiwa
tayari nimeshazoeana na Michael, Beatrice akawa mpenzi wangu. Katika
muda ndipo kipindi ambacho hatukuwa na mahusiano ya karibu na Michael,
tuligombana kwa sababu ya Beatrice. Mama aliwahi kuja chuoni na
kuniulizia kwa watu. Sehemu ya watu aliowauliza, wakamuonesha Michael
aliyekuwa akipita kwa mbali na wakimwambia mama kuwa yule ndiye rafiki
yangu na labda amuulize yeye wapi nilipo. Mama alimuita Michael na
kuniulizia, Michael akamuelekeza wapi angenipata kwa muda huo. Ni siku
hiyo ambayo Mama alinikuta tukiwanaBeatrice darasani tunataniana huku
tukifurahi pamoja. Nilimtambulisha Beatrice kwa mama na mama alifurahi
sana kumuona Beatrice. Maisha yakaenda na mara niliporudi nyumbani
baba akaniuliza swali"Mama yako ameshakuja chuoni kwenu mara ngapi?"
"Mara moja"Nilimjibu hivyo na kwenda zangu nje chini ya mti fulani wa mwembe
uliokuwa ukitoa kivuli safi. Hapo chini ya mti nilimkuta mama amekaa
mkekani akifuma vitamba vyake vya makochi kwa sindano ya mkono
"Oh Ramon! njoo ukae"Nikakaa, mama akaniuliza"Hivi yule kijana Michael anakaa wapi?"
"Hapana mama sifahamu" Nilimjibu mama bila kutilia manani maswali yake
"Anaonekana ni kijana mzuri aliyetulia kwanini humkaribishi mwenzio
apajue kwenu?"nilizisikia hatua za mtu ajaye pale tulipo na mara nikafahamu kuwa ni
baba mara alipozungumza"Kwanini Michael?" Baba hakukaa aliendelea kusimama, sasa akiwa mbele
yetu "mbona hukuwahi kuwaulizia rafiki zake wengine na sasa iwe
Michael?"
Nilimuona mama akisonya na kujinyanyua pale mkekani na kishaaliondoka. Ni hapo nilipoanza kuona tofauti kati ya mama na baba. Mama
alionesha kumpenda Michael lakini baba alimpinga sikujua yote hayo
sikujua chochote kwa kuwa nilikuwa nikiwekwa mbali na ukweli. Siku za
kukaa nyumbani zilipokwisha nikarudi chuo.. Ndipo siku moja baba
alikuja chuoni na kunieleza kuwa haupendi ukaribu wangu na Michael, Mimi baba alinishangaza kwa kuwa ukaribu huo hatukuwa nao.
"Baba mbona mimi sipatani na Michael kwa sababu ya Beatrice!"
Nadhani hakuniamini baba akaniambia kuwa mara nyingi mama alipokuwa
akitoka kunitembelea alipokuwa akimuaga baba, alikuwa akimzungumzia
sana Michael kuliko mimi. Niliingiwa na wasiwasi nikamuuliza
"Kwani mama amekuja mara ngapi chuoni kwetu?"
"Ni zaidi ya mara tatu, kwanini wakati ni wewe ndiye alikuja kukutembelea?"
"Mnh hapana baba, mama nimemuona chuoni mara moja tu"
Nilieleza ukweli kwa kuwa nilianza kuwa na mashaka ili nisijiingize
mahali pabaya. Basi baba akanieleza kuwa ni zaidi ya mara tatu alikuwa
akiaga nyumbani kuwa anakuja kunitembelea chuoni. Mimi nilishituka
sana kwa kuwa sikuelewa sababu ya mama kumdanganya baba kuwa anakuja
kunisalimia na alikuwa haji.
"Alikuwa anakuja kukutana na Michael"
Baba alizungumza kwa uchungu na nilielewa uchungu alio nao, nikataka
kumjaribu baba"Lakini baba kuna umuhimu gani wa kunieleza haya yote kuhusu Michael
na mama leo wakati huu ikiwa nina kesi ya kumuua Beatrice?"
nikamgeukia Vanessa na kumuuliza kwa hasira "Na wewe unakaa kaa hapa
ukitabasamu bila kumueleza baba kuwa ninachohitaji ni kujua ukweli wa
mauaji ya Beatrice, nani kamuua Beatrice ndicho ninachohitaji kusikia
nahitaji kukijua kwa sasa na si hadithi ya Michael na mama"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndipo naelekea"Nilimgeukia baba baada ya kuzungumza hayo na kumsikiliza alikuwa
anamaanisha nini. Baba akaendelea
"Japo unasema mlikuwa hampatani baadae nadhani mlikuja kuwa marafiki
kwa kuwa alikuwa anakuja nyumbani nawe"
"Ndiyo kwa hiyo"
"Mama yako na Michael walikuwa wapenzi"
"Wapenzi?" nilihamanika. Vanessa alitingisha kichwa huku tabasamu
liking'ang'ana katika papi zake. Niliumizwa na taarifa hizo lakini
bado sikuwa nimeelewa chochote. Baba akaendelea
"Mama yako alimpenda Michael japo Michael alionekana hampendi mama
yako. nilikuwa nikimsikia mama yako mara nyingi akimlalamikia Michael
kwanini anapoteza pesa nyingi kwake na yeye akawa hampendi. Mara
kadhaa pia nilikuwa nikimsikia akilalamika kuwa atamkomesha huyo
Beatrice anayemfanya Michael asimpende yalikuwa ni mabishano
yaliyotokea wiki moja kabla ya mauaji ya Beatrice hayajatokea, siku
chache baadaye aliweka kikao na watu ambao kwa mimi sikuwahi kuwaona
watu wale pale nyumbani hapo mwanzo, mmoja wa watu hao alikuwa ni huyu
askari wa kike. Nilifuatilia kwa umakini bila wao kujua chochote kama
nilikuwa nikiwafuatilia maongezi yao yalikuwa yakinishangaza maana mara nyingi walikuwa wakimtaja Beatrice sikuweza kukueleza mapema kwa kuwa nilidhani kuwa ningeidhibiti hali ile mwenyewe lakini nathikitika kuwa nimeshindwa mpaka Beatrice amefikwa na mauti”
Nilihisi ni kama utani ama ndoto ambayo nilikuwa nikiota na labda ninakaribia kuamka. ‘Ina maana baba anamaanisha mama ndiye muhusika wa mauaji ya Beatrice?’ nikajiuliza kwa uchungu huku machozi yakinitoka. Nikauinua uso wangu na kumtazama baba, baba pia alikuwa akinitazama mimi kwa uso wa upole. Nikamuuliza “una maana mama ndiye muhusika wa mauaji ya Beatrice?” baba akatingisha kichwa kwa kukukubali kile ambacho nimemuuliza. Nikahisi nachanganyikiwa kiukweli ni hali ngumu niliyokuwa nayo kwa wakati ule na hata sikuwa na uwezo wa kuendelea wa kuwasikiliza tena na hivyo mahojiano yalikatishwa huku Vanessa akiniahidi kuwa atakuja siku ya kesho ili aweze kunieleza mengi ambayo bado nilikuwa sijayafahamu mpaka kwa wakati huo.
Haikuwa rahisi kuelewa ni vipi Bella amehusika na mauaji ya Beatrice. Sawa Bella alionekana kuyajua mengi kuhusu kesi hii sasa ni vipi alihusika? Sijawahi kumuona hapo kabla japo baba anadai kuwa aliwahi kumuona akija pale nyumbani lakini ilikuwaje achukue uamuzi wa kumuua Beatrice akiwa yeye ni askari? Nilihisi nazidi kuchanganyikiwa kwa kuwa sikujua pia mama yangu alihusika vipi na kwanini amuuwe Beatrice.
Kila nilichokitazama katika nyumba hiyo mara baada ya vanessa na baba yangu kuondoka, niliona kama namuona askari yule wa kike, Bella. Nilijiuliza mengi kiasi kwamba nilianza kuelewa kiasi au sehemu ya mambo yalivyokuwa yakienda. Nilianza kuelewa kuwa kulikuwa na uhusiano fulani kati ya mama yangu na yule askari. Niliikumbuka ile siku ambayo mama alikuja na yule askari alimuita pembeni na hivyo walizungumza jambo ambalo mama alisita kunieleza kile ambacho alitaka kunieleza, labda huenda kilihusiana na Michael. Nakumbuka siku ile ndiyo ilizidi kuniongezea hisia kuwa huenda ni Michael alihusika katika mauaji ya Beatrice.
Nilirudi katika chumba changu nikakuta sahani iliyojaa vipande vya mikate vilivyopakwa siagi ya karanga na kikombe cha maziwa. Bila shaka ni Bella aliyeniandalia. Nilikunywa chai ile pale huku nikiwa na mawazo lukuki kichwani mwangu. Machozi yaligoma kutoka kwa kuwa ilikuwa ni kama nimekumbwa na taharuki ama ugonjwa ambao si rahisi kuuelezea. Nikakumbuka mara kwa mara jinsi ambavyo mama alikuwa akimuulizia Michael na kushindwa kuelewa sababu ya msingi yeye kufanya uchafu wa namna ile na mtu tuliyelingana umri tena akiwa sawa na mtoto wake yaani mimi. Kipande cha kwanza niliweza kukimaliza lakini sio cha pili nilichohisi kikinikaba koo kwa uchungu ulionikumba. Niliiacha chai ile na hapo machozi yakaanza kunibubujika kwa uchungu. Siku hiyo sikuoga nilishinda nikilia siku nzima mpaka nilipohisi nikishikwa begani na mikono iliyo laini sana. Nilipoinua uso wangu kumtazama yule aliyekuwa akinitazama, alikuwa ni Vanessa akiwa amejawa na hudhuni na uso wake ukionesha utulivu wa hali ya juu. Alikuwa amerudi mara baada ya ujio ule wa asubuhi akiwa na baba
“Pole sana Ramon” akanyamaza huku akiwa ameinama na kunipatia kitambaa cha kujifuta machozi, akaniambia “kesho utatoka na kuwa huru kwa dhamana baada ya Oscer kuondoa vipingamizi vya dhamana yako lakini hii inatokana na asilimia themanini ya ushahidi kukamilika na sehemu ya wahusika wa mambo haya kukamatwa na kusekwa mahabusu. Hutaruhsuiwa kuzungumza chochote kwa mtu yeyote ili usiharibu taratibu za upelelezi. Yangu ni hayo na kesho nitakuja na baba yako kukuchukua mpaka nyumbani kwenu”
“hapana sitaweza kukubali uondoke siku ya leo mpaka unieleze”nilizungumza kwa uchungu “unieleze ni vipi yule askari anahusika na mauaji haya huku mama yangu akihusika pia na mauaji haya. Kwa kuwa sielewi chochote sielewi yaani nazidi kuchanganyikiwa ni heri ningejua ni Michael aliyehusika lakini si mama yangu. Imekuwaje Vanessa?”
Akanieleza jinsi ilivyokuwa mwanzo mpaka mwisho kwa jinsi na yeye alivyohadithiwa na kuelewa.
YALIYOTOKEA KATIKA KIFO CHA BEATRICEhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa ni wiki mbili zilizopita mama yake na Ramon akiwa amerudi mapema na rafiki zake akiamini kuwa mzee Lameck bado hajarudi kutoka kazini. Alikuwa ni yeye pamoja na washirika wake watatu mwanamke akiwa mmoja kati ya wale aliokuja nao ambaye ndiye Bella, askari aliyekuwa akiishi na Ramon katika nyumba ya Safe house kumlinda ili asitoe yote yale ambayo huenda alikuwa akiyafahamu. Hiyo ilikuwa ni kazi yake baada ya mambo kuharibika au kwenda tofauti na mipango ya kambi yao ya mauaji ya Beatrice. Wanaume wengine wawili waliobakia alikuwamo Moses aliyetoroka jela kipindi kifupi tu akiwa na kesi ya mauaji ya watu wengi wasio na hatia huku aliyebakia akiwa James mattaba kijana aliyetumwa kuipeleleza nyumba anayoishi Beatrice akijifanya kama muuza mchicha na magazeti kwa siku nyingine bila kushitukiwa na mlinzi wa Beatrice, Baraka. Kikao chao kilikuwa kina ajenda ya kumuangamiza Beatrice siku ambayo anavishwa pete na Ramon.
“lakini mama kwanini unataka kufanya jambo hili ikiwa mtoto wako anampenda sana huyu binti?” Bella ndiye alihoji
“kha! We vipi?” Moses aliropoka “acha ujinga, ni mara ngapi madam akueleze kuwa Michael ndiye sababu?”
“kivipi?” Bella akahoji kiushabiki. Ubishani huo ukamshitua Lameck kule alipokuwa na kunyata taratibu kuelekea pale mlangoni karibu na ukumbini walipokutania kusikiliza maongezi yale. Mara akaisikia sauti ya mkewe
“Sikia wewe mwanamke nafahamu kuwa Beatrice ni mpenzi wa mtoto wangu lakini Beatrice amekuwa akininyima usingizi kutokana na kulikosa penzi la Michael kwa muda mrefu sasa. Michael amekuwa na ugomvi na ramon tangu wakiwa chuo kwa sababu ya Beatrice na hata nikiwa nimeshamkanya mara nyingi sana kuwa aache mahusiano hayo na Beatrice akawa hanisikii kwa kuwa niliwahi kumkuta akibusiana na Beatrice nyumbani anapoishi Michael” Bella alishituka kusikia hayo na hakuongea chochote akabaki kuwa msikilizaji wa kila kilichopangwa. Moses ndiye alikuwa mratibu wa mchezo mzima baada ya kumsikiliza James jinsi ramani ya nyumba ile na muda ambao mbwa wa nyumbani kwa Beatrice wanafunguliwa. Mpango ulisukwa vyema na hivyo mauaji yale yalipangwa kutekelezwa na james akishirikiana na Moses pamoja na Bella.
Dakika chache mara baada ya Ramon kumuacha Beatrice pale pale getini, hakutambua kuwa kulikuwa na watu watatu waliokuwa wakitambua ujio wao huku wamejibanza katika giza zito nyumba nne kutoka pale walipo wao. Watu hao walikuwa ni Moses, Bella pamoja na James waliokuwa wakiwasiliana muda wote na mama yake Ramon ili kutambua muda gani Beatrice atatoka katika sherehe ile.
Katika mifuko ya Moses, kulikuwako na chupa yenye kilevi kilichotiwa sumu kali ya kukausha maini huku akiwa ameviweka visu vinne vyenye makali kote kuwili kwa ajili ya mauaji. Kiunoni mwake akiwa amepachika bisu kubwa la kimasai aina ya sime. Bella alikuwa ameshikilia nyama kilo tatu alizozikata kwa vipande vipande huku akiwa amepakaza sumu pia kwa ajili ya kuwatupia mbwa wale. James hakushika chochote James alikuwepo pale kwa kazi maalumu.
“Dogo ndiyo anasepa sisi tunaingia” Moses akatuma ujumbe kwa mama yake Ramon akajibiwa “kuweni waangalifu”
Jambo la kwanza kufanywa kabla ya kuingia ndani, ni kuzima umeme wa zile kamera ambazo ni James pekee alijua kamera nne zilizopachikwa kwa ajili ya ulinzi wa nje tu na jinsi ya kuzikata nyaya zake. Baada ya kufanya hivyo kwa kitendo kisichozidi dakika kumi. James mwenyewe tena, ndiye aligonga getini. Baraka mlinzi aliyevalia sare za ulinzi kutoka Jinja Security, aliuliza kwa lafudhi ya watu wa shinyanga(sukuma)http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nani?”
“James yule muuza magazeti kaka”
Hakuwa na wasi juu ya kuulizwa amefuata nini usiku wote huo kwa kuwa asubuhi ya siku hiyo alimpitishia magazeti na akawa ameisahau chenchi yake kwa makusudi kwa ajili ya faida ya baadaye. Hakuzisahau ndevu zilizokuwa zikimdanganya Baraka mara tatu alizokuja hapo akijifanya kama muuza magazeti na mara muuza mchicha. Wakiwa wamesimama pale nje, walimsikia Baraka akilalamika juu ya zile kamera ambazo haziwaki
“haya ngoja nakuja ndugu yangu”
Ujinga alioufanya mlinzi yule mweusi na mfupi wa kimo, ni kufungua geti dogo lililomruhusu Moses kummwagia pombe ile yenye kilevi kidogo sehemu ya usoni Baraka na hivyo alipovuta tu kimiminika kile cha baridi hakuweza kupiga kelele wala hatua alizojaribu kutaka kupiga kwa hofu aliyokumbana nayo kwa kushuhudia watu watatu asiowafahamu usiku wa saa nane kama ule. Akiwa bado anaipigania roho yake pale chini alipoanguka, Bella akawa amekwishawarushia mbwa wale yale mapande ya nyama huku mbwa hao wakali wakiyafakamia kwa uroho bila kujua kuwa ndani yake kuna sumu iliyowafanya wanyong’onyee mithili ya mlenda na kunguka chini mmoja mmoja kama kuku mwenye kideri. Ukimya uliokuwepo nje ukamtisha Beatrice kwa kuwa bado hakuwa hajapitiwa na usingizi. Na kwakuwa alikuwa na shida ya kumuuliza jambo Fulani Baraka, akaipiga ile simu ya mezani ambayo iliita tu na haikupokelewa, akahisi hali ya hatari, ndipo kwa wakati huo alimpigia Ramon. Ramon naye hakupokea simu kwa wakati ule kutokana na usingizi uliokolezwa na wingi wa pombe alizokunywa akatika sherehe.
Beatrice akafanya kosa la kufungua mlango na kukutana na mtu mrefu tofauti na Baraka anayemjua yeye, akaita kizembe “Baraka” hakuitikiwa kwa kuwa hakuwa yeye bali kimiminika kile chenye kilevi lakini chenye sumu kali ya kukausha maini akarushiwa na kuivuta sumu ile iliyomo ndani yake. Kilevi kile kilikuwa ni pombe ya kawaida tu lakini iliyochangwa na sumu kali ili kuupoteza ushahidi, ilitengenezwa na Moses. Beatrice alianguka chini na kuishiwa nguvu mara baada ya kuvuta kimiminika kile cha hatari.
James akiwa amekishika kiwiliwili cha Baraka kilichotenganishwa na kichwa chake huku damu nyingi zikiwa zimemtapakaa mikononi mwake, ndipo alishika pale ukutani na alama ya kiganja chake kutokea karibu na mlango wa kuingilia ndani kwa Beatrice. James akishirikiana na Bella walimburuza Baraka mpaka kilipo chumba kilichofanyika kama stoo ndani ya nyumba ya Beatrice na kumuweka huko.
Moses alikuwa akiendelea kung’ang’ana na mwili wa Beatrice kuuingiza ndani ya chumba chake huku akiwa ameshamkata sehemu ya koromeo lililokuwa likivuja damu nyingi, ndipo Bella alipomsaidia kwa kumbeba miguuni huku Moses kwa mikono aliyovaa gloves akiwa amemshika sehemu ya kichwani. Moses alikuwa makini sana katika kazi hizo labda huenda kwa kuwa alikuwa ni muuaji mzoefu lakini si kwa James na Bella walioacha acha ovyo alama zao za vidole kutambulikana hapo baadaye. Mara walipomlaza Beatrice sakafuni kwake katika chumba chake, akaumalizia uhai wa Beatrice kwa kulichomeka sime kubwa alilolipachika kiunoni mwake katika tumbo la Beatrice bila kutumia vile visu vine katika moja ya mifuko ya koti lake. Ilikuwa ni picha mbaya kuitazama na ndiyo aliyoikuta Ramon saa aliyokuja. Bella akaiona simu ya Beatrice pembeni ya kitanda, akawaza jambo kiaskari Zaidi. Mara baada ya Moses kutoka huku akimuamrisha waondoke haraka eneo hilo kwa kuwa ilikuwa ni usiku mno yeye akabaki nyuma kuichunguza simu ile ya Beatrice. Alifungua sehemu ya meseji hakukuta meseji yoyote ya kumgusa ila alipofungua sehemu ya simu zilizpoigwa simu ya juu iliyopigwa muda mchache uliopita ilikuwa ikipigwa kwenda kwa Ramon. Katika akili yake akaamini kuwa mambo yamekwishaharibika. Yeye pia akaona ni bora aharibu Zaidi tofauti na mpangilio wa jinsi walivyopanga. Akapanga kuirudisha kesi hiyo kwa mtoto wa bosi wake ambaye yeye ni kama rafiki yake. Akamtumia meseji ile Ramon mwenyewe iliyoandikwa kuwa “kwanini unaniuwa Ramon?’ akiamini huo ni ushahidi wa kutosha kumuingiza Ramon katika matatizo. Na ndivyo ilivyokuwa hapo baadaye mpaka alipodanganya wenzake kwa kuwatumia meseji akijifanya kuwa ni msamari mwema anayetoa taarifa za tukio la mauaji yaliyotokea huko mikocheni. Baada ya wao kutokomea alirudi nyumbani kwake akiwa anajiandaa kuitwa ofisini kwa ajili ya kwenda kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ambaye ni Ramon.
Mama yake na Ramon alikuja kuelewa kuwa lameck mumewe, amekuwa akimfuatilia kwa mambo mengi aliyokuwa akiyafanya. Alifahamu hata kuwa kifo cha Beatrice anakifahamu na hivyo aliwatumia watu wake kumuonya ili afunge mdomo wake asije kuitoa siri ile. Ni siku ile ambayo alivnjwa mguu na watu wa mama yake Ramon wakishirikiana na Moses.
SAFE HOUSEhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kusikia hayo yote, nilizidi kulia huku nikiona dunia ni chungu na sistahili kuishi ikiwa mama yangu mwenyewe aliyenizaa ndiye aliyesababisha haya yote kutokea. Nilimuomba Vanessa aniache peke yangu kwa muda nipate nafasi ya kutafakari mambo mengi yaliyotokea huku nikiamini kuwa sina muda mrefu wa kuendelea kuishi. Vanessa akaniaga huku akinieleza kuwa
“Michael pia amekamatwa huku ukitakiwa kwenda kutoa ushahidi kati ya mama na rafiki yako ni nani aliyemuuwa mpenzi wako”
“vipi kuhusu mama yangu, amekamatwa pia?”
“ndiyo”
“sawa nakusubiri kesho acha sasa nikalale”
Sikwenda kulala kama nilivyomuomba Beatrice aniache nikalale bali niliutumia muda wote wa usiku kuandika sehemu ya hadithi ya maisha yangu yaliyoniumiza kuliko yote. Nitawezaje kumtazama Michael ikiwa nimeshamshutumu kuwa ndiye muuaji ikiwa mama yangu ndiye aliyehusika na mauaji haya? Nitawezaje kumnyooshea bwana hakimu kuwa muuaji ni yule pale huku nikitazamana na uso wa mama yangu aliyenizaa baada ya kuniweka tumboni kwake miezi tisa tena kwa uchungu na kisu cha operesheni kikipanua njia yake baada ya mimi kushindwa kupita kwa hali ya kawaida? Hapana yanipasa moyo wangu uende na yule nimpendaye. Ninachoamini kuna maisha baada ya kufa kama ilivyoandikwa na mwandishi mashuhuri mwenye ujuzi wa pekee stallone joyfully katika kitabu chake cha msitu wa wafu. Kwanini nisiende kukutana na mpenzi wangu kuliko kuishi katika dunia ya dhuruma na manyanyaso kama hii ya kifedhuli? Namkumbuka Christian aliweza kukutana na Munira tena katika msitu ule, acha na mimi nife nikiwaachia kitendawili kiziro walimwengu ni vipi utathibitisha kuwa mama yako ndiye muuaji wa mpenzi wako Betarice eti kwa kuwa alikuwa anampenda rafiki yako? Mimi siwezi kusimama kizimbani ndio sababu ya kuchukua uamuzi huu. Siku ya leo jumapili ya saa 11 alfajiri ya mwezi wa saba tarehe nne ndio siku ya mwisho ya uhai wangu duniani. Mnisahamehe kwa wote niliowakwaza kwa uamuzi niliouchukua ila naiombe sharia ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ichukue mkondo kwa kila dhulumu ya haki iwe ya kuishi na yeyote iwayo ifuatwe kwa mujibu wa katiba ya nchi hii yenye Amani na upendo inavyosema.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MWISHO
“Ramon alikufa kwa kujinyonga na shuka kukiwa na walinzi wachache waliopunguzwa kutokana na ushahidi kukamilika. Michael alichiwa huru mara baada ya kuthibitika kuwa mama yake Ramon ndiye aliyehusika na mauaji yale huku Bella na mama yake Ramon wakihukumiwa kifungo cha maisha jela ikiambatana na mateso makali. Moses na James hawakukamatwa.
0 comments:
Post a Comment