Simulizi : Msamaha Bila Malipo (Forgiveness Without Payment)
Sehemu Ya Tano (5)
SURA YA KUMI
B
abu akamwambia razima amfuatilie kwa sababu yuko kwenye himaya ya watu. Mrs Damiani alimwangalia kwa dharau kisha akamwambia, “Pole yako mzee unamjua mwenye eneo hili?,Aliuliza Mrs Damiani huku akiwa bado kamkamatilia kwa nguvu Sophia ambaye hana hata hatia. Wale mababu walimwangalia sana yule Mke wa Damiani. Baada yakuona kawajibu kama eneo lake walimwambia amuanchie Sophia. “haya basi mwachie mwenzio kwani hauoni kama ni mjazito?’ Mke wa Damiani aliendelea kuwa na jeuri.
Dah! Wale mababu wakapandwa na hasira wakamwambia kwa mara ya pili tena amuachie mwenzake. Mke wa Damiani akawajibu kwani wao wanajua ambacho kimefanya mpaka amemkaba?.
Kisha Mrs. Damiani aliamua kuwatukana wale mababu kuwa wana visebengo na pia ni wambea kama wanawake. Dah! Jambo hilo lilimuuma sana hasa yule babu ambae alipita mara ya kwanza na kuongea nae. “Bwana, huyu binti kama ni dharau amenidharau vya kutosha. Ebu nipe fimbo yangu kwanza,’’ alisema babu yule kisha akamsogelea kwa hasira mke wa Damiani nakuanza kumkwanyua sawasawa na ile fimbo yake. Mke wa Damiani akamuachia Sophia na kuanza kuikwepa ile fimbo ambayo alikuwa akipigwa nayo.
Dah! Ilikuwa ni kama mchezo fulani wa kufurahisha lakini kumbe babu yule ndivyo alivyokuwa akimaanisha. “Hivi wewe babu vipi nimekukosea nini mbona hivi lakini? Alisema mke wa Damiani huku akikwepa ile fimbo lakini wapi bado ilimuadhibu vilivyo kabisa wala hakuweza kuikwepa. Kila alipojaribu kusogea pembeni bado shabaha za yule babu zilifanya kazi. “Mpuuzi kabisa binti wa nani wewe usie kuwa na heshima? Hapo mke wa Damiani akiwa kakaa chini anatuliza maumivu ya bakora ambazo alikuwa kapigwa.
Sophia akawa pembeni akiongea na wale akina babu ambao walianza kumuuliza chanzo cha kukabana. “Yaani huyu mbwa ndiye anasababisha mpaka napigwa namna hii! Alisema mke wa Damiani kwa uchungu huku akimwangalia sana Sophia. Tena alimwangalia kwa jicho laubaya kabisa. Sophia ingawa alijua jicho analoangaliwa na mke wa Damiani si la kheri aliamua yeye kujikaza kisabuni ili awaambie ukweli wale akina babu ambao walitaka kujua chanzo cha ugomvi wao. Sophia aliendelea kuwaambia wale Mababu ukweli.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipomaliza kuwaelezea, wale mababu walimdharau kabisa Mke wa Damiani ambaye alionekana dhahiri kabisa kuwa ana jeuri ndani ya moyo wake. Walimwangalia Mke wa Damiani kisha wakamwambia Sophia “Binti toa msamaha bila malipo yoyote sawa? Mungu ndiye mlipaji’’. Yalikuwa maneno ya wale wazee wawili ambao walimchukia sana Mke wa Damiani ambaye alikuwa bado ni kijana wa makamo. Kisha wale wazee wakaondoka na kwenda zao.
Sophia akabakia pale pamoja na mke wa Damiani. Hapo ndipo Sophia alianza kuonyesha kwamba huwa sio mpole pale inapobidi na pia huwa hapendi kuonewa hata kidogo. Mrs. Damiani alimfuata kwa hasira akidai kuwa kwanini apigwe kwa ajili yake vile. Alikuwa na hasira akitaka kumpiga ngumi ya usoni, Sophia akaikwepa na kumshika mkono. “Nadhani upole sasa unataka kuzidi, nitakuharibu dada” alisema Sophia.
Ilikuwa ni siku ya pili Damiani pamoja na Robert wakiwa hospitalini. Nyumbani kwa Damiani watu matumbo joto kabisa. Mke wa Damiani akiwa na wasiwasi zaidi ya ule wa mara ya kwanza. Watoto ndio kwanza wanalia wakimtaka baba yao. Kule ofisini hakujafunguliwa hata kidogo. Mke wa Damiani ndio kwanza alipigana na Sophia alimpa kipigo sawasawa kabisa bila kuogopa kitu chochote. Damiani na Robert wakiwa wodini hoi bin taabani. Damiani alianza kumwambia Robert kuwa bora atoroke aende kuangalia mambo jinsi yanavyokwenda. Maana Robert ndiye alikuwa na nafuu kidogo kuliko Damiani. Robert alimwambia itakukuwa je madaktari wakagundua kuwa anataka kutoroka si itakuwa hatari kabisa. Damiani akamwambia kuwa bila kufanya ujanja huo kazi itakwenda vibaya. “ Lakini Damiani sikia sawa nikienda nitafanya nini cha maana labda nimpe funguo na tumkabidhi Sophia Ofisi” Damiani akakubali na kusema kuwa ni jambo zuri atakapoenda amtafute Sophia kwa hali na mali ili ampe funguo akae ofisini ili kuendelea kuhudumia wateja. Kabla bwana Robert hajaondoka , alinyanyuka kutoka kitandani na kuanza kutafakari jinsi gani anavyoweza kutoroka pale hospitalini, kumbe kipindi wakipanga hayo nesi ambae alikuwa mlangoni alisikia mipango walivyokuwa wakipanga. Baada yakusikia alikimbia moja kwa moja mpaka kwa daktari ambaye alikuwa anasimamia hospital hiyo yeye alikuwa Ofisini akiwa anaangaika na mambo kadha wa kadha ambayo yalikuwa yanapaswa kufanyika muda huo . Mara mlango ukagongwa huku ukisukumwa “Nani”? aliuliza daktari huku akisitisha kazi aliyokuwa akifanya na kwenda kufungua mlango ambao alikuwa ameufunga kwa ndani. Baada ya kufunga tu anakutana uso kwa uso na nesi. “Na wewe mbona umeacha kazi kwani kuna shida gani?” nesi hakuchelewa kumwambia kuwa kuna mgonjwa anataka kutoroka wakati bado wanaonekana kuwa na hali mbaya. “Unasema ukweli aliuliza daktari mkuu. Nesi akamwambia kuwa ni kweli na amemuona mmoja akijiandaa kuondoka . “Basi fanya hivi sawa kambanieni getini sasa ataenda wapi,. Kisha nesi akaenda kuwaambia wenzie wamsaidie kwahilo jambo. Daktari mkuu yeye akaingia ofisini kwake kuendelea na mambo aliyokuwa akifanya. Wakiwa tayari wameshajipamga sawasawa, Robert akavaa nguo vizuri, nguo za pale hospitalini akazivua na kuziachakabisa kisha anafungua mlangoni na kuangalia kushoto na kulia kisha anaondoka kama alikuwapo vile. Kumbe wale manesi wao wakawa tayali wako getini wakmsublia Robert atakapotokea tu basi iwe ndio hatamu yake pale getini. Robert akafanikiwa mpaka kutoka nje kabisa ya jingo la hospitali. Baada yakufika pale nje kwa mbali getini akawaona manesi wakiwa wamesimama kwenye lango la kupitia dah! Ikamuwia vigumu flani bwana Robert kuweza kupenya na kwenda nje kule waliko panga na bwanahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Damiani. Robert akasimama kwanza kuangalia atafanya nini ili aweze kutoweka eneo hilo ambalo ni baya kwake kwa wakati huo. Robert alikata kona kana kwamba anaenda msalani kisha anasogea mbele kidogo. Anakutana na kijiukuta ambacho kilikuwa hakina ugumu kukiruka. “Dah! Afadhari sasa hapa hapa naruka naenda, si wamebana mlangoni hawa manesi” Robert anaruka kishujaa na kudondokea ng’ambo ya pili ambako kulikuwa kuchafu ajabu. Kulikuweko na mfereji wa maji machafu ambayo yalikuwa yanatokea ndani ya hospitali. Dah! Robert baada yakutua hapo alibakia kwanza kuangalia yale mazingira jinsi ambavyo yalivyo. Kwa mbali akaona kama kuna mtu ambae alikuwa anamsogelea. Robert anatoka mbio hata kandambili ambazo alikuwa kava akaziacha pale maana aliona kama zinampa uzito flani ambao hautomsaidia kukimbia kwa haraka. Kule chumbani akawa amebakia Damiani peke yake, mara nesi ambaye ndie aliyekuwa akiwahudumia akawa kaingia na madawa kwenye trei ya madawa. “Damiani” aliita nesi kwa sauti ya chini. Damiani akaitika kwa sauti ya unyonge kabisa. “Mwenzio Robert kaenda wapi” aliuliza nesi huku akiandaa pamba kwa ajili ya kumsafishia Damiani. “Kaenda sijui wapi tu mimi sielewi nimeona kaondoka tu” alisema Damiani kwa sauti ambayo ni ya chini kabisa. Sauti ambayo ni ya kujirazimisha kabisa. “Yaani watu wengine bwana, niliwaambia halizenu ni mbaya sana haitakiwi kwenda nje wala wapi shauri yenu. Alisema nisi huku akianza kumuosha Damiani yale makovu ambayo alikuwa nayo. Robert muda huo kaisha ingia barabarani nay ale makovu yake makubwa usoni pamoja na miguuni, watu walibakia kumshangaa Robert wengine walizania labda ndio katoka kupata ajali. “Mbona naangaliwa sanahivi kwa nini” Alijisemea mwenyewe moyoni huku akijishika pale alipoumia. Robert alikuwa anatembea mithiri ya mtu Fulani ambaye ana amani ndani ya nafsi yake. Wakati huo akiwa njiani akitembea kumbe Sophia nae alikuwa ng’ambo yabarabara ya pili akielekea shuleni kwa mdogo wake Edo. Robert kuangalia kwa mbali akamuona Sophia kisha anaanza kumuita kwa sauti ya juu kabisa. Sophia akasikia sauti ikimuita lakini haoni mtu, akabaki kuangaza angaza huku na kule kuon ni nani ambae anamuita. Kuangalia kwa mbali akawa kama anamfananisha Robert. Lakini kutokana na makovu aliyokuwa nayo hata Sophia hakkujua vizuri kwamba yule ni bwana Robert ambae alikuwa na sura nzuri yenye mvuto sawia sasa amebadirika na kuwa na uso wa kutisha namna hii! Akabaki anashangaa mtoto wa kike akiwa kabebelea mkoba wake begani, pamoja na tumbo lake ambalo lilikuwa kubwa sana pengine anaweza kumshusha kijacho mapema sana. Sophia ……http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Sophia nisubilie basi” aliongea Robert huku akimkimbilia Sophia. Sophia nae akawa kaisha muona kuwa yule ni bwana Robert kabisa. “Robert ni wewe! Umekuwaje?” alisema kwa kushangaa mno. Robert akamwambia kuwa ni yeye huku machozi yakianza kumlengalenga Sophia. Kisha akamwambia ilikuwaje hadi akapata makovu makubwa ambayo yako usoni mwake. Robert alishindwa hata amwambie nini Sophia alichomwambia ni kuhusu habari za funguo za pale ofisini alizoambiwa na Damiani tu. Kumbe funguo zilipotea siku walipopata ajali. Zilipotelea ndani ya gari. Dah! Robert baada yakukumbuka hivyo akaachoka kabisa, akashindwa hata aaseme nini ambacho Sophia atafanya ili kufungua ofisi. Hapo ndipo pakawa na muungiliano wa mambo ambao wote waishindwa wafanye nini wakabakia kungaliana tu. “Nazani Sophia hakuna jambo zuri kama kubomoa ofisi. Damiani kanambia usimamie wewe” Robert aliongea kisha akamuelekeza mpaka hospitali ambayo walikokuwa amelazwa dah! Sophia alisikitika sana kumuona Robert akiwa katika hali hiyo ambay oni mbaya sana. “Sophia pambana kike hakikisha kwamba mambo ya ofisini yanakwenda sawa” alisema Robert kwa msisitizo mkubwa sana. Kisha akaondoka kwenda zake hospitalini kuendelea kupata matibabu. Ambayo walikuwa wanapatiwa katika hosipitali. Sophia akawa kapewa jukumu ambalo alikuwa halitalajii kabisa katika maisha yake hata siku moja kabisa. Akaahirisha mpaka safari ambayo alikuwa akipanga kwenda kumtembelea mdogo wake Edo ambae alikuwa akisoma kwa msaada wa yule bwana ambae alikuwa ana uwezo mkubwa wa kifedha.
Sophia ilibidi aondoke kwenda kule ofisini kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kubomoa ule mlango wa ofisini kwao dah! Haikuwa jambo ambalo ni jepesi kwa Sophia ambae alikuwa ndo mara ya kwanza kabisa kukabidhiwa ofisi tangu kukuwa kwake miaka yote duniani hivyo alikuwa na kitete sana kwa jukumu hilo ambalo alilokuwa kaachiwa. Damiani kule wodini baada yakumalizwa kusafishwa vidonda nakupakwa dawa aliamuwa kulala hapo bado bwana Robert alikuwa bado kabisa hajatia nanga kabisa mule wadini wala hospitalini. Nyumbani kwa bwana Damiani mke wake alikuwa sasa ameshabadili wazo ambalo alikuwa nalo pamoja na hofu kumshuka sana. Alikuwa na wivu sana hivyo basi aliendeleza fikra zake za wivu zaidi alianza kuweza kwamba labda pengine Damiani amekwenda na wanawake wengine. “Ukweli mpaka leo bado hato taarifa kuhusu alipo nimakusudi mazima haya” alijisemea mwenyewe mke wa Damiani huku akipanga kurudi tena ofisini kujua mmewe alipo. Moyo ulikuwa unamuuma sana hata chakula alikuwa anakula kwa shida sana yaani bora kla ili aishi tu wala alikuwa hana furaha na chakula chake. Ambacho alikuwa anpika kwa kula. Mke wa Damiani alikuwa kaishiwa maneno bali alibakiza hasira tu ambayo aliwafanyia hadi watoto wake pale ndani. Sophia ambae alikuwa kapewa mikoba yakuiingoza ofisi sasa alikuwa pembeni akiangalia jinsi ambavyo vijana wakibomoa mlango. Mkoba wake alikuwa kauweka pembeni, mikono kaifunga kifuani kama ndume ambayo inamiliki himaya ile. Alivyokuwa kaka alikuwa kaka kumzidi hata Damiani. Sophia moyo wake ukawa na furaha kubwakupewa nafasikama ile ambayo ilikuwa adimu kwake. Kipindi akiwa anasubilia watuwabomoe ili aweze kuingia na kupanga mule ndani mkewe Damiani huyo akawa kawasili. Sophia una mamlaka gani kubomoa kama nani wewe? Aliuliza mke wa Damiani kwa hasira. Sophia akabakia kumuangalia huku akimcheka. Unanicheka kwa kunidharau si ndio?” alisema huku akimwangalia usoni. Mke wa Damiani akamsogelea huku akilini akijiuliza kwa nini Sophia amejiamini hivyo sana leo. “Mbona Sophia unataka kunipanda kichwani?” alisema mke wa Damiani, lakini wala Sophia hahangaiki kunyanyua mdomowake. Alibakia kumuangalia jinsi anavyobwabwaja kama hana hakili vizuri kichwani. Dah! Mrs. Damiani anapata hasira sana kicha anamsogelea na kuanza kumtikisa Sophia. “Heeee! Ebu niache tena kamuulize mmeo hospitali ndie kanambia nifanye hivi sawa, tena!alisema kwa ugaidi Sophia. Mke wa Damiani akashangaa “Hospitalini!” kisha akapunguza jazba na akaanza kumuliza Sophia kwa upole. Hospitalini kafuata nini? Sophia ndipo alipoanza kumwambia ukweli wa mambo. Mara baada ya kuambiwa vizuri kabisa alianza kumgeuka tena Sophia. “Hapo sawa nimekubali lakini kwa nini hukuniambia ukweli jana wakati unajua fika kuwa yule ni mme wangu ulikuwa na maana gani? Sophia akamwambia kuwa hata yeye amepata taarifa kwa Robert na Robert nae amekuja akiwa na hali ambayo ni mbaya sana. Ingawa aliambiwa ukweli lakini bado alikuwa kmuelewi kabisa binti Sophia. Sophia akamwambia ngoja wavunje pale mlango kisha ampeleke kumuona mmewe. (yaani Damiani). Mke wa Damiani alitaka waende muda huo huo. Akawa anamlazimisha sana Sophia. “Nasema ebu niache kwanza nifanye nilivyoambiwa ndipo twende usinipelekeshe sawa? Alisema Sophia kwa jeuri mno.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SURA YA KUMI NA MOJA
N
i muda wa mchana ambao nitulivu kabisa. Sophia pamoja na mke wa Damiani wakiwa wamekwenda kudhuru hospitalini walipolaza Damiani na Robert. Sophia alikuwa mbele maana ndie alikuwa kama mwenyeji wa mke wa Damiani. Ingawa Sophia alikuwa kaelekezwa na bwana Robert ambae alikutana nae barabarani muda mfupi uliopita. Dah! Sophia alikuwa shapi sana kwenye kutembea. Alitembea kama mchina kiwandani. Mke wa Damiani akawa anaona kama Sophia anamkomoa labda, kisha anasimama na kumwambia, “Sophia mbona unanipelekesha sana mdogo wangu” alisema mke wa Damiani huku akiwa kasimama na kushika kiunoni. Sophia akamwambia yeye alishazoea muda mwingi zaidi kutembea kwa haraka na si polepole. Baada ya kusimama na kuongea kidogo kisha wakazidi kwenda mbele. Sophia alikuwa hajasahau mkoba wake begani. Mke wa Damiani alikuwa kava kitenge kiunoni na kingine katupia shingoni.
Viviane ambae ni rafiki kipenzi na wa dhati kabisa wa Sophia alikuwa njiani mara akamwona mdogo wake Sophia (Edo) akiwa ng’ambo ya pili ya barabara, alikuwa akielekea nyumbani kwao kuwasabahi maana alikuwa ana muda mrefu kidogo hajaonana/ hajawaona mama na dada yake Sophia. Edo alilkuwa kaishatoka shuleni sasa alikuwa kabadili hata nguo za shuleni. Alikuwa kavaa za nyumbani. Viviane baada ya ya kumuona Edo, akamuita, kumbe Edo alikuwa hajamuona kabisa dadake Viviane kwani mawazo na akili yake vilikuwa mbali sana. Viviani akamuita tena kwa mara ya pili na kumuuliza “Edo mdogo wangu unakwenda wapi?” Edo akajibu kuwa anakwenda nyumbani kumsabahi mama na ndugu zake kwani amewakumbuka mno. Viviane alipomuangalia vizuri akamuona Edo akiwa na kijifurushifani cha nguo mkono wa kulia. Na hicho ni nini mdogo wangu? Edo akamwambia kuwa ni cha nguo zake ila hakumfafanulia nguo zake anapeleka/kwenda nazo nyumbani kufanya nini.
Kule wodini Robert ambae alikuwa hayupo wodini alikuwa tayari kaisharudi. Na pia alikuwa kaisha safishwa na kupewa dawa. Na yule nesi ambae alikuwa anawahudimia. Kwa sasa Robert alikuwa akinywa juice pamoja nakula matunda ambayo walikuwa amepewa kama msaada. Damiani alikuwa ndio kwanza yuko hoi kitandani maana maumivu yalimsumbua na pia alikuwa na siku ya pili hajala kitu chochote kile mdomoni. Hivyo hali ilizidi kuwa mbaya zaidi ya mara mbili yake. Robert kidogo alikuwa na hali ambayo ni ya auheni kidogo ambayo ilikuw ainalidhisha japo si sana. Wodini palikuwa kimya sana sauti iliyokuwa ikisikika ni ndege ambao wako nje kwenye miti. Watu walikuwa wametulia ma wodini mwao. http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Baada ya Sophia pamoja na yule mke wa Damiani kuwa sili pale eneo la hospitalini, Sophia likuwa kaishasahau wodi ambayo aliambiwa/alielekezwa na bwana Robert. Mawazo yalikuwa hayapo alichokuwa anakumbuka ni direction ya eneo la hospitalini. “Sijui yuko wodi gani nimesahau kabisa” alisema Sophia akiwa ameanza kumwaya mwaya, mara nesi mmoja akawa katokea na kuwauliza wanaelekea wapi, ama wanataka msaada gani ambao wanahitaji zaidi. Sophia akaongea “Tunawagonjwa wetu lakini hatujui wako wodi gani” alisema binti Sophia kwa upole. Nesi hakuwa na roho mbaya alitaka bado kuwaelewa na kuwaelekeza vizuri. Akawauliza wagonjwa wao n wagonjwa wa namna gani/ wana umwa nini? Sophia akamwambia wanumwa vidonda vya kupata ajali. “vidonda vya kupata ajali! Nesi akapatwa na mshangao kwa lugha ambayo Sophia aliitumia. Kisha anarekebisha lugha yake nesi akamuelewa kisha akawa peleka kwa nesi ambae alikuwa anahudumia wagonjwa wa aina hiyo. Huyo nesi ndiye alikuwa akiwahudumia akina Damiani. Baada ya kufika pale kwa yule nesi, yule nesi wa mala ya kwanza akawa kaisha muona yule nesi kisha akamwambia “Kuna wageni wako hapa” alisema yule nesi aliyewaleta kisha nesi ambae alikuwa ndie mlengwa alichungulia kuwa angalia kwa uzuri “Wageni wangu tena haya waambie wanisubilie” alisema nesi aliyekuwa akiwatibu wakina Damiani. Mda huo alikuwa akipanga madawa ya wagonjwa wengine. Mkononi alikuwa kava groves za rangi nyeupe. Kule chumbani ambako Damiani pamoja na bwana Robert walikuwa wamelazwa, hali ya Damiani ilizidikuwa mbaya maana Damiani alinyanyuka kutoka kitandani. Robert alibakia kungalia nini ambacho Damiani anachotakakkufanya. Damiani alianza kuhangaika na kutapa tapa huku nakule. Baada yakuzunguka sana mule chumbani, mara Damiani akasimama kisha akamwambia Robert “Nakuomba hata kama nisipomwona mke wangu mwambie Sophia ana mimba yangu na ampe heshima na amuachie Sophia asimamie kampuni yangu sawa….” Mara baada ya kusema hivyo Damiani akadondoka china kisha akatikisa mguu kidogo na kufumba macho yake kabisa. Damiani akawa katoweka duniani kabisa. Robert akawa amebakia kuhaha mule ndani. Akawa anajaribu kufumbua macho ya Damiani wapi, akijaribu kumtikisa wapi, Damiani kagand tu. Dah! Robert uzalendo unamshinda anasimama kidogo huku mikono akiwa kaiweka kiunoni kisha anaona kama anapoteza muda pale ndani. Anaamua kutoka nje ya wodi yao/chumba na kwenda nje kutafuta msaada kwa nesi ambae alikuwa anawahudumia ili aje kumpa muafaka wa Damiani.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati Robert akienda kumbe nesi nae pamoja na wale wanawake yaani mke wa Damiani pamoja na Sophia wakawa njiani wakija wodini kuwaangalia Damiani pamoja na bwana Robert. Walipoingia kolido la pili tu, mara wakakutana na Robert. “Na wewe unaenda wapi?” aliuliza nesi wao ambae aliwapa huduma. “Nesi…. Nesi Damiani, twendeni tukamuone twendeni” aliongea Robert huku machozi yakimlenga machoni. Nesi pamoja na mke wa Damiani, Sophia, wote wakakimbia kwa haraka kwenda kumuona Damiani. Kawaje au amekuwa nini kule…
****
fuatilia volume TWO
MWISHO
0 comments:
Post a Comment