Search This Blog

Friday, October 28, 2022

MAFANIKIO KATIKA AKILI YANGU [SUCCESS ON MY MIND] - 1

 

     





     IMEANDIKWA NA : PHABIANI ISAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Mafanikio Katika Akili Yangu (Success On My Mind)

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    Ni asubuhi yenye kupendeza jua likiwa lime chomoza,kuashiria siku nyingine, ime wadia noel alikuwa amebeba begi lake mgongoni akielekea shuleni.lakini alionekana kuwa ni mtu mwenye mawazo mengi sana nyuma yake alikuwa akija mzee alikuwa akiendesha baiskeli huku akipiga mruzi.Bahati mbaya aka msogelea na kumukwangua na baiskeri, maeneo ya mguuni noeli hakuongea chochote alikaa kimya ‘’kijana samahani’’ alisema yule mzee huku akishuka kutoka kwenye baiskeri. ‘’bila samahani mzee’’ alisema noeli hukuakitembea kwaku chechemea.yule mzee alipo mwangalia usoni noeli aligundua ana msongo mkubwa sana wa mawazo.’’lakini mbona una mawazo mno?’’ aliuliza Yule mzee lakini noeli akawa mzito kuongea. naakamjibu ‘’hamna mzee’’ aliongea kwakutabasamu kijana noeli ‘’punguza mawazo, mawazo ya nini wewe ungali kijana mdogo’’ alisema Yule mzee mwenye baiskeli kisha aliondoka na kumuacha noeli akiwa amesimama njiani, noeli alikuwa mwanafunzi kidato cha sita katika shule ya sekondari ya nsumba, noeli alikuwa ametokea familia ya watu wa maisha ya chini kabisa.Mama yake alikuwa muuza pombe za kienyeji.Baba yake alikuwa amewatelekeza tangia walipokuwa wadogo, ‘’maisha haya najuwa iposiku nita yaacha’’ aliwaza akilini mwake kisha akaondoka kwenda darasani noeli alikuwa na ndoto kubwa sana, katika mpangilio wa maisha yake alikuwa akiwaza siku moja kuwa mwandishi mzuri wa vitabu. Lakini pia alipenda kuwa mwanamuziki, ‘’noeli?’’ alimuita msichana mmoja ambae aliye kuwa akisoma nae, aligeuka na kumuitikia kwa upole ‘’namm’’ hukuakiwa bado angali amegeuka, Yule binti nae alikuwa kavaanguo nzuri. Madaftari yake alikuwa kayaweka katika mafaili. Nakuya shikilia mkononi,’’duuuh! leo tumechelewa’’ alisema Yule binti.

    ‘’sikuzote hazilingani’’ alisema noeli kwa utaratibu hukuwakitembea mwendo sanjari na ule wa Yule binti, ambae waliyekuwa wakisoma nae.’’kazi ya mwalimu ulifanya?’’ aliuliza Yule binti noeli akamjibu na kumwambia ‘’mimi natamani kumaliza shule’’ alisema noeli hukuakiwa amekata tamaa na maisha ya kuuza pombe ya pale yumbani kwao huku hali ya biashara hiyo ikiwa mbaya sana kutokana na polisi kumsumbua sana mama yake.kila siku polisi walikuwa hawaishi kuja nyumbani kwao na noeli, ‘’sijaifanya kazi yake’’alisema noeli

    ‘’mwalimu ata gombana sana’’aliongea Yule binti aki mwonea huruma noeli.

    ‘’ila baadae nitafanya’’ alisema noeli uwezo wa kimasomo alikuwa nao mkubwa sana, tatizo ni umasikini uliokuwa umekithiri, noeli kila siku jua linapo zama na kuchomoza alikuwa akiwaza atafanya nini iliaweze kulipa deni ambalo alilokuwa akidawaiwa shuleni,’’dah! Maisha magumu’’ aliongea hukuakiwa anashusha pumzi yake kwanguvu. Noeli karibia kila ngazi ya elimu alikuwa akipitia changamoto nyingi mno,walianza kuingia katika eneo la shule, kwambali walianza kuona walimu wakiwa wamesimama. Pomoja na mwasibu wa shule, wao pomoja na kuwa mbali lakini walikuwa wamesha muona noeli, ‘’hivi huyu kijana amegoma kutowa pesa?’’aliuliza mwalimu mmoja,

    ‘’sijui naona yuko kimya mno’’ waliendelea kumjadili noeli na kila iliyoitwa leo noeli alikuwa akiitwa ofisini.kusoma kwake hakukuwa kwa raha hata kidogo,aliishi kwa wasiwasi noeli alipokuwa shuleni.’’nitafanyeje?...... nitafanyeje?’’ ndio lilikuwa swari lake kila siku kijana noeli alipokuwa akitembea alipofika sehemu yenye uwazi walimu wake wakamuita, ‘’noeli?’’

    ‘’nammm mwalimu?’’ aliitikia kwa upole hukuakiwa anageuza shingo yake, alikuta niwale walimu wake ambao kila siku walikuwa waki msumbuwa shuleni.’’aiseee narudi nyumbani’’ ndilo wazo lililomuingia kichwani kijana noeli kwaharaka, pamoja na kupitia mambo yote hayo lakini bado noeli aliamini kuwa ipo siku matatizo yataenda kuisha.’’wewe pesa tunayo kudai umelipa?’’aliulizwa na mwasibu wa shule,

    ‘’hapana’’ alijibu kijana noeli mwalimu mkuu aliweza kutowa amli ya noeli aweze kufukuzwa, ‘’mwalimu huyu arudi nyumbani’’ aliongea hukuakiwa amelishikilia begi la noeli,noeli anafukuzwa kurudi tena nyumbani kwao.kufukuzwa kwa noeli ilikuwa imesha kuwa kawaida hata mwanafunzi mwenzake ilifikia hatuwa waliona kawaida, noeli akiwa njiani alianza kuwaza ‘’nirudi tena nyumbani?’’ alijiuliza swari hilo kichwani akili ya haraka ikamuingia katika kichwa chake ‘’niende mtaani’’ aliwaza hivyo hatimae aliamuwa kwenda mjini rafikiyake alikuwa darasani akimsubilia sana, ’’leo noeli yuko wapi?’’alijiuliza wenyewe tu kichwani huku akiwa anajinyoosha.Rafiki yake noeli alionekana kutokuwa na raha kabisa mwalimu alikuwepo darasani lakini yeye alikuwa hamsikii kabisa.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Noeli baada ya kufika mjini Alianza kujifikilia tena akilini mwake’’ni fanye nini?’’ mala akili ikamjia aende kuvua nguo za shule kwanza.Nakisha aende kufanya vibarua atakavyokuwa akikutana na vyo mtaani,aliingia katika uchochoro na kubadili nguo zake kwa haraka zaidi.Ili mchukuwa kama dakika tano kuweza kubadili nguo zake,alivaa nguo za nyumbani [full]. Akiwa noeli anatembea na kuangaza huku na kule akakutana na watu wakichimba balabara.Wakati akiwa amesimama na kuwa shaagaa wale wachimba balabara, mala mmoja kati ya wale wachimba balabara akamuita noeli. ‘’dogo vipi?’’ alisogea karibu na noeli kisha akamwambia,’’mbona unashangaa hapa kwanini?’’ noeli alisimama kisha akamjibu ‘’namimi nataka kazi’’ aliongea noeli kwakwakujiamini ‘’wewe utaweza kweli kazi yetu?’’ aliongea huku akimtizama kwa huruma mno kijana noeli.’’naombeni hata niwa sombee…..’’ noeli alionekana ni mwenye shauku yakutaka kufanya kazi na baadae aweze kulipwa ujira wake. ‘’kama utaweza ni fuate’’ walitembea kwakufuatana kama kumbikumbi wakienda noeli ambako alikuwa hapajui.Walipofika sehemu moja hivi walikutana na bwana mmoja akamuuliza Yule mwenyeji wake na noeli ‘’unasemaje?’’ aliuliza Yule bwana, ‘’nimekutana na huyu bwana mdogo’’ Yule bwana alimuangalia sana noeli kisha akamuuliza tena ‘’anashida gani?’’ ingawa hakutaja anashida gani Yule bwana alimuelewa kisha akamwambia’’naomba umsikilize’’alisema Yule mwenyeji wake na noeli, Yule bwana alikubalia kisha mwenyeji wake na noeli aliweza kuondoka na kuwaacha wawili hao.Mazungumzo yalianza kati ya Yule bwana na kijana noeli ‘’bwana mdogo ulikuwa unasemaje?’’ alimuuliza noeli, nakisha noeli alimjibu ‘’mimi natafuta kazi’’alijibu kwakujiamni noeli alikuwa ni kijana ambae anajiamini sana Yule bwana akamwambia’’kibarua chakulipwa kwa siku au?’’ ilikuwa kama ni bahati kiuwanadamu lakini ilikuwa kama mpangilio asilia kutoka kwamungu.’’ndio mimi kibarua chochote’’alisema noeli basi Yule bwana ambae alikuwa ni mkubwa pale aliamuwa kumpeleka aweze kumpa kibaruwa cha kusomba moramu na kuwapelekea mafundi.Kazi ile haikuwa nyepesi hata kidogo ilikuwa nikazi ngumu isivyo kawaida.’’fanya kwaleo nita kulipa 35 elfu’’ alisema Yule bosi wapale kisha akaondoka na kumuacha noeli baada ya kusikia atapewa donge nono kama hilo alijituma sana katika kazi yake.Hukuakiwa na matumaini mengi sana,’’kumbe ngoja niji tume’’ mama yake muda huo alikuwa akiuza pombe kirabuni suala la shule kwa mwanae alikuwa halifuatilii hata kidogo.Noeli alijikita katika kufanya kazi yake juwa lote lilikuwa likimuishia mwilini, jasho lilikuwa likimtoka mwilini kwa wingi.Alijitahidi kubeba mifuko mikubwa ya moramu lakini uwamini wake katika mafanikio ulimfanya kujituma bila kuchoka.HUkuakiamini iposiku atakwenda kuuwacha umasikini.Noeli hakuwai kujiwazia mabaya hata sikumoja kila gumu alilokuwa akipitia aliliona kama changamoto tu.

    Mama Noeli alikuwa akifuata maji na huku akiuza pombe alifanya kazi mbili kwa wakati mmoja.Wateja wake wapombe walikuwa ni makuli pamoja na matingo waliokua wakitokea maeneo mbalimbali. ya mji wa mwanza,Mama Noeli alikuwa ni mwanamke ambae mchakalikaji’’mama noeli habari?’’ alimuongelesha mmoja kati ya wateja wake mama noeli akamjibu ‘’salama’’ alikuwa na ukaribu na wateja wake, ‘’niachie ya…….leo’’ waliongea wakiwa wamekutana njiani mama noeli akiwana ndoo ya maji kichwani. kutokana na biashara yake mama noeli alikuwa ni mtu maarufu sana mtaani hakuna ambae aliyekuwa hamjui pesa aliyokuwa akiipata katika bishara yake ilikuwa sawa anagawana na askari.Alikua na siku nyingi sana hajawapelekea pesa polisi kutokana na biashara yake kuwa ngumu sana.Akiwa njiani kurudi nyumbani na skari nao wakawa wameshafika katika kaya yake, tena wakiwa niwenye hasira isiyokuwa na kifani ‘’tuwa ndoo tuondoke’’ walisema askari wakiwa wamemsubilia na mama noeli alikuwa haja tuwa hata ndoo chini.Mama noeli ilibidi aanze kujitetea ‘’biashara ngumu’’ alijitahidi kujitetea lakini hakuna liye msikiliza wala hoja yake waliona kama hainamashiko.



    Askari wale walichokuwa wakikifanya ilikuwa ni haramu ingawa pia biashara ya mama noeli ilikuwa ni haramu pia.Mama noeli kwakutojuwa haki zake na elimukuwa ndogo aliona kama ni sawa.’’nipeni muda’’ alisema mama noeli askari waka mjibu ‘’haiwezekani unatuchezea’’ walisema askari na wote waliweka msimamo wao pamoja au mmoja.’’leo nirazima twende wote haiwezekani’’mama noeli baada ya kusikia hivyo alizidi kuchanganyikiwa zaidi askari walimuangalia kwa sura za kikatili sana huruma juu yake ilikuwa haipo.Mama noeli anaamuwa kutuwa ndoo ya maji kisha akachukuwa kitenge chake.Nakutowa pesa yake ya mauzo madogo aliokuwa kayafanya na kuwapatia, ‘’kumbe unatu chezea akili zetu’’ walimuuliza hukuwakimpa vitisho, ‘’amna jamani pesa hakuna’’ alisema hukuakiwa anajuta sana kutowa pesa karibia yote ya mauzo yake ya siku hiyo.’’sasa tukiwa tunakuijia utatu……’’ walisema wale askari huku wakiwawana weka mfukoni pesa ambayo waliokuwa wamepewa na mama noeli.Baada ya kumaliza walichokuwa wanakitaka waliamuwa kuondoka akabakia mama noeli, akiwa anawaza sana mikono akiwa kaiweka kichwani ‘’dah! Biashara hii sasa mbona ina…….. sana’’ aliwaza mno kichwa kikapata ukungu wa mawazo mengi sana.Siku hiyo ilikuwa ngumu sana kwa mama noeli kuweza kutengeneza pombe wateja wake walianza kuja mmoja baada ya mwingine,Alihisi mwenyezi mungu hathamini uwepo wake katika dunia.Tumboni kwao walizaliwa wawili noeli pamoja na dada yake,dada yake alikuwa ameishia kidato cha nne na akaishia kuwa mama wa nyumbani.Aliolewa na mfanyabiashara mmoja wa level ya kati.

    Ilikuwa ni muda wa mchana juwa likiwa limewaka sana,hata dada yake kule ndani ya nyumba mambo yakawa yake haribika. Alifukuzwa na mume wake,ilikuwa ni vita ndogo ndani ya nyumba, ‘’toka masikini wewe’’ yalikuwa maneno yakuchoma kwa dada yake noeli akiambiwa na yule mumewake ‘’nisamehe mume wangu’’ alijitetea sana binti zawadi ilikulinda ndoa yake.Aliongea huku akiwa ana lia na kumpigia magoti mpaka chini mumewake,Mafurushi yake ya nguo mume wake alikuwa tayari amekwisha kuyaweka sebleni.’’sikutaki’’ aliongea kidume huku akiwa anafoka sana kosa ilikuwa ni matumizi mabaya ya pesa ambayo mume wake hakuya penda.Zawadi alijitahidi kumbembeleza mume wake lakini haikuwezekana,Aliendelea kumtolea matusi ambayo yalilenga ufukara wa nyumbani kwao zawadi.’’umasikini wa kwenu unaniletea’’ wakati mtafaruku huo ukifanyika mama yake noeli alikuwa njiani kuelekea nyumbani kwa zawadi.Pesa askari walichukua alibakia mweupe kanga alikuwa kavaa zimechafuka sana,matobo pia yalikuwa mengi sana hakika ilionyesha dhahiri kuwa anadhiki katika maisha yake.Alipokuwa kaolewa zawadi palikuwa siombali sana nyumbani kwao,ulikua ni umbali wa kilometa au nusu kilometa.’’leo razima uwende kwenu’’ alisema mume wake zawadi’’nisamehe’’ aliongea hukuakimuangukia miguuni kwake zawadi.’’niachie bwana’’ aliongea hukuakienda chumbani kwao, akiwa hataki hata kusikia sauti ya mke wake’’nitaenda wapi mungu wangu!’’aliwaza zawadi mwenyewe hukuakiwa ana zidi kujaza mapigo mengi sana katika moyo wake.Akiwa analia na mikono akiwa ameiweka shavuni mala akasikia sauti ya mtu akibisha hodi nje ya nyumba yao sauti alikuwa ameshaijuwa ingawa ilikua ikitoka kwambali sana.’’hodi hapa?’’ akaitikia ndugu yake na mumewake zawadi alikuwa amekaa kwauzuni na hata nguvu yakwenda kufunga mlango ikawa imekosekana.’’wapo humu ndani?’’ aliuliza mama noeli kwa huku akiwa anawasiwasi sana,’’ndio wapo ingia’’alimfungulia geti huku mama noeli akafunguwa na kuweza http://deusdeditmahunda.blogspot.com/kuingia mpaka ndani.Wakati akiwa anafunguwa tu geti na kuingia alimuona kwambali zawadi akiwa amejawa na machozi mengi katika paji lake la uso.Na raha aliyokuwa nayo zawadi katika kakumkaribisha mama yake ilikuwa niya kawaida kabisa.’’zawadi alimuiti ukuakiwa ana mshangaa’’ zawadi alipomuona mama yake ndio machungu yalizidi katika moyo wake.Maana machozi ndio yaliendelea kutoka mengi sana,’’zawadi unalilia nini?’’ aliuliza mama noeli kwa mala ya pili,huku nayeye alikuwa akitaka kububujisha machozi yake.’’baba……… ananifukuza’’ aliongea hukuakiendelea kulia, ‘’umekosea nini!’’ ilikua hali ya kumshangaza sana mama yake na noeli maana alikuwa hakutarajia kabisa wala kufikilia katika akili yake.Wakati wakiwa wanazungumza zawadi na mama ake mala mume wake akatoka nje hukuakiwa na jaziba kubwa isiyokuwa na kifani.Tena alizidi kuongea kauli yake ileile ‘’ondoka bwana hapo kwangu’’ alishangaa sana mama noeli kisha akamuuliza ‘’mmekuwaje tena jamani’’alisema mama noeli huku akiwa anamuona mkwilima wake hana muda nae kabisa.Alitoka nje na kutowa bastora na kuwaonyehsea,’’wote ondokeni sitaki kuwaona hapa’’alivaa roho ya ujasiri mpaka kwa mama yake mkwe,baada ya kufanya hivyo kilammoja alimkimbia na kumuacha mwenyewe.Hukuakitowa maneno ya kukashifu familia yao.’’mwanangu twende’’ aliongea kwauwoga mama noeli ‘’yani sirudi tena hapo’’alisema zawadi hukuakiwa anafuta machozi yake taratibu.’’leo ametukashifu hivi!’’ alishangaa hukuakiwa anashangaa zaidi akilini mpaka moyoni, njaa nayo ilikuwa ikisumbuwa moyo wake’’nilikuwa sijui kama…….. yuko hivyo?’’ alisema zawadi hukuakiwa ameweka adhimio la kurudi nyumbani kwao ajuwe lakufanya nilipi,

    Muda ulikuwa ukiyoyoma noeli akawa amekwishamaliza kazi yake.Watu walijuwa atakuwa nikijana wamtaani na mpambanaji hawakuweza kuzania kama angekuwa mwanafunzi.’’wewe bwana mdogo?’’alimuita Yule bwana ambae alikuwa kampa kibarua noeli, noeli aliitikia kwa heshima alikuwa amechuchumaa chini maana alikuwa amechoka sana.’’nammm” aliitika hukuakimfuata Yule bwana alipofika Yule bwana hakupoteza muda alimpatia ujira wake noeli ‘’bwana mdogo shika……. Yako kabisa’’ ilikuwa pesa tasilimu shilingi tharathini elfu ilikuwa furaha kwa kijana noeli ingawa kazi ilikuwa ngumu sana.Furaha ilikuja baada yakufikilia kwamba hakutarajia kama angeweza kupata kazi kama hiyo ‘’kesho kama utaweza njoo’’ alimwambia Yule bwana kijana noeli maana alikuwa amependa utendaji wakazi wa noeli.Noeli akamjibu nakusema ‘’nitakuja asubui’’ alipoambiwa hivyo ilimpa moyo na faraja kubwasana aliondoka hukuakiwa anachezacheza na kurukaruka.Noeli alipoondoka kitu cha kwanza aliwaza kwenda sokoni kununuwa chakula.

    USiku ulikuwa umeingia mama noeli pamoja na zawadi walikuwa wamekaa nje.Yanyumba yao wakiwa wamejikunyata mtoto wa zawadi alikuwa analia sana,’’mbembeleze mtoto’’ alisema mama zawadi huku njaa ikiwaimewatafuna mno.Ataongea yake ilikuwa imebadilika ‘’noeli nae mbona hajaja?’’ aliongea hukuakiwa anasonya sonya kumuwaza kwake noeli kumbe ilikuwa nikwakheri maana noeli alikuja kuishibisha familia yake.’’naona atakuwa amepita kujisomea kwa wenzake’’ alisema dada yake noeli zawdi, punde noeliakawa amefika akiwaameshikilia mifuko miwili ya Rambo.Akiwa imejaa vyakula mbalimbali alivyokuwa kanunuwa sokoni, kwajili yakumletea mamayake aweze kupika wale.’’mama……..mama’’alianza kuitia mbali akiwahata ajawezakutulia,ghafla akawa amedondosha chini viazi vyake maana mfuko mmoja ulikuwa umedondoka ‘’noeli ume……nini?’’ aliuliza mama noeli hukuakiwa anainama katika giza usiku huo kuangalia.’’nimekuletea viazi mama’’ alisema noeli huku nayeye akiwa ameyaelekeza macho yakechini kuangalia viazi vita dondokea uwelekeo gani.Mama yake pamoja na dada yake baada ya kusikia ni chakula kitu mabacho hawakutegemea kabisa kutoka kwa noeli waliinama na kuanza kuviokota sambamba na kuviosha walijuwa huwenda sikuingeisha wakiwa lala na njaa matumaini yalikuwa yameisha watoka,rakini noeli anakuja na kuibuwa tumaini kwao.’’



    ’na dada zawadi amekuja sangapi?’’aliuliza noeli hukuakimpatia mfuko mwingine uliokuwa na vyakula vingine tena, mama yake na noeli alikuwa hawezi kumjibu maana njaa ilikuwa ikimsumbuwa sana.Kisha akamwambia ‘’mwanangu umejuwaje kama leo hari ni mbaya’’alisema mama noeli kisha noeli akamwambia,’’mama nilijuwa ndio maana nikafanya hivyo’’ jasholilikuwa likimtoka mwilini noeli anaamuwa kuchukuwa ndoo na kufuata maji ilikuja kuweka mwili safi alipofika bomani alikuta vijana wenzake wakiwa wana teka maji huku wakiongea vijana hao wao nyumbani kwao walikuwa na maisha mazuri kiwastani walianza kumsema na kumg’ong’a.’’hivi huyu sasa hivi yuko……. Gani’’ waliulizana kisha mmoja akawajibu’’yuko kidato cha sita’’ walipokuwa wakiongea yeye noeli alikuwa akiwasikia vizuri’’kwaiyo ndio anataka kui…… familia yake?’’ noeli maneno yaliokuwa yakitoka yalikuwa yakimpa uchungu sana.Akiwa bado angali ameinama mala akasikia mwingine akisema ‘’hatoweza’’ walimuongea na kumcheka kutokana na ule umasikini wa nyumbani kwao.Noeli alikaa pale bombani kwa kujitenga mwenyewe baada ya kumaliza kuteka maji aliondoka na kuwapa kisogo’’huyu ataishia….. tu’’ waliendele kumg’ong’a ‘’wasomi wengi hawana kazi iwe yeye’’ watu wengi wamekua wakikalili maisha au hata wengine kufuata mifano ya watu walioshindwa.Tumeshindwa kujuwa kila mmoja hutusuwa maisha kwanjia yake na kwa muda wake.Unaweza kusoma shahada ya uchumi,au hata ya sharia au hata ya sayansi ya jamii.Lakini yehova asiwe amekupangia huko au usipate maisha mazuri kutumia taaruma uliyo nayo,yote yana wezekana je niwangapi? ambao wametusua maisha pasipo kutumia usomi wao? Tunahitaji kufikili [positive] katika maisha yetu.Noeli akiwa njiani akitembea nandoo yake ya maji mkononi wazo likamjia kichwani.’’the succes it is on my mind’’ Noeli alikuwa ni mtu wakushangaza sana hata alipokuwa akipitia magumu kiasi gani bado aliendelea kuwaza mafanikio yako katika maisha yake.Ilikuwa kama ni sauti ambayo ilikuwa ikimjia katika moyo na akili yake.Noeli alienda moja kwa moja mpaka bafuni alipofika bafuni alianza kuvua nguo kabla hajamaliza kuvua nguo vizuri,alianzakulitizama bafu lao http://deusdeditmahunda.blogspot.com/namna lilivyokuwa lime bomoka upande mmoja akakumbuka alipokuwa akitembelea mji mmoja sikumoja alikuta,mazingira mazuri ya bafu la kuogea hisia kali zikawa zimeibuka katika akili yake.Alipofikilia sana tena wazo na suti ileile vikamjia’’the succes it is on my mind’’ kisha akapigapiga kifuani kwake hukuakiwa anaji mwagia maji kwa speed ya ajabu mama yake alikuwa akiendelea kupika haraka maana njaa iliyokuwa ikimuuma ilikuwa sio ya kawaida hata kidogo.Yule rafiki yake wa shuleni ndie walikuwa wakikaa nae chumba kimoja wakijisomea, alipokua chumbani aliwaza sana kuhusu noeli hatimae aliamuwa kwenda nyumbani kwao.Na noeli kwenda kujuwa noeli anaendelea vipi.Walipokuwa wamepenga chumba kwakujisomea palikuwa sio mbali sana na nyumbani kwao na noeli punde tu akawa tayari ameshafika nyumbani kwao noeli.’’hodi mama?’’ mama noeli akaitikia kwa hraka’’karibu’’ hukuakiwa jikoni akifanya mpango wa chakula na zawadi yeye alikuwa chumbani akimbembeleza mtoto wake maana alikuwa akilia sana.’’noeli yuko wapi mama?’’ aliuliza Yule rafiki yake,’’noeli yuko bafuni akioga’’ alisema mama noeli hukuakikaa chini kwa uchovu, ‘’leo sijaonana nae hata kidogo’’ aliongea rafiki yake na noeli akiwa anasogea na kuegemea mtini.’’shule ngumu sana?’’ alisema mama noeli ingawa kwao noeli ilikuwa ni mjini lakini walikuwa wakipika kwakutumia kuni sio kwakupenda baliilikuwa ni uleukwasi uliokuwa umetawala katika maisha yao.kupikia mkaa kama wengine ilikuwa ni ghrama sana kwao kuweza kukimudu kitu hicho.

    PUnde si punde noeli akawa ametoka bafuni na maji yalikuwa yaki mdondoka kutoka mwilini kwa matone,’’girbeti?’’ aliita noeli kisha girbeti akaitikia ‘’namm noeli’’ kisha akamsogelea na wakaongea na kusalimiana kwaukarimu mno noeli pamoja na girbeti walitokea kupendana na hatimaye wakawa marafiki walisikilizana.Na wote walikuwa wakisoma mchepuo mmoja yani [HGL] ingawa katika [futures] zao kila mmoja alikuwa na zake tofauti na mwenzake.Noeli alipenda kuwa mwandishi mzuri wa habari girbeti yeye alikuwa anataka kuwa mwanasheria mzuri na mtizamo wa ‘’succes on my mind’’ wote pia walikuwa nao,na walipenda kuutumia kama kauli mbiu kila walipokuwa wakipita.’’leo hukuingia darasani’’ alisema girbeti ngoja tutaongea kuna……. Imetukia’’ alisema noeli hukuakisogea kukaa karibu na girbeti.



    SURA YA PILI.

    Baada ya miezi mitatu kupita noeli alikuwa amefanikiwa kuhitimu masomo yake ya kidato cha sita.Wakati huu maisha ndio yalimwendea vibaya sana maana alishinda kutwanzima akiwa amebelea bahasha la kaki,marafiki zake kalibia wote hakuweza kuwanao kwa wakati huo.Juwa lilikuwa likiwaka nakumuishia lote noeli kiasi hata chakuunguza ngozi yake.Alikuwa katikati ya mji wa mwanza alitembea lakini hakuweza kuchoka noeli,alitembea sikuhii na kuamuwa kwenda kwenye eneo moja zuri lililoko katikati ya mji wa mwanza na kuamuwa kukaa.Eneo lilikuwa na bustani nzuri ya majani ya kuteleza mawe yake pia yalikuwa ni ya kihistoria katika taifa la Tanzania.Eneo lilikuwa mwambao wa ziwa victoria ‘’dah! Niliambiwa leo sangapi?’’ alijiuliza mwenyewe akilini mwake,maana sikuiliyokuwa imepita alikuwa kaenda ofisi flani ambayo ilikuwa ni kituo cha redio.Wao walimwambia aweze kwenda siku inayofuata mbayo ilikuwa ndio siku hiyo.Wakati akiwa pale kwenye ufukwe uliokuwa na bustani nzuri noeli alikuwa hana atashilingi mfukoni mwake njaa pia ilikuwa ikimuuma mno lakini ikafikia hatuwa hata akaizoea.Akiwa amekaa mala akaiyona gari nzuri naya kifahari ikiwa imekuja karibu na ule ufukwe na kupaki.Akamuona baba mmoja akishuka kutoka katika ile gari ya kifahari kiujumla Yule baba alionekana kuwa ni mtu mwenye pesa alienda kukaa palepale alipokuwa amekaa kijana noeli.Kisha akamuongelesha noeli,’’bwana mdogo vipi……yako?’’ aliongea Yule baba hukuakienda kukaa’’salama’’ noelialiitikia kwaraha pasipokuwa na furaha kabisa kutoka moyoni Yule baba alikuwa na soda ya kopo aliitowa na kuanza kunywa taratibu ‘’unaitwa nani rafiki?’’alimuuliza Yule baba noeli nae hakusita kumjibu au kumwambia jina lake,’’naitwa noeli’’ hata ongea yake ilikuwa kama anarazimishwa kuongea ‘’noeli mbona unamawazo sana?’’aliuliza hukuakiwa ana muangalia noeli.Noeli alimficha hakutaka aweze kujuwa chochote kuhusu yeye.Kisha anamjibu tu kwakumlidhisha,’’hamna niko kawaida’’ alisema kijana noeli hukuakiwa amegeuza macho yake kuelekea ziwani.yule bwana bado aliendelea kumuuliza maswari,’’unasoma?’’ noeli alimjibu ‘’nimemaliza kidato cha sita,’’inamaana unasubiri kwenda chuo kikuu?” noeli aliitikia ‘’ndio’’ alionekana kumfurahisha Yule baba maana alikuwa akiwapenda sana vijana wasomi.Ingwa yeye alibahatika kuwa na pesa na akawa amekoswa elimu.’’safi sana na sasa hivi unafanya kazi gani?’’ aliuliza Yule baba,

    ‘’natafuta kazi ya muda nifanye” aliongea kwakusononeka sana noeli alikuwa haya pendi maisha ya umasikini hatakidogo. Maana aliona namna umsikini unavyo yagharim u maisha ya nyumbani kwao,’’mmmh! Utapata kweli?’’ alimuuliza Yule bwana hukundio akizidi kumkatisha tamaa noeli lakini noeli kwakuwa alikuwa sio mtu wakukata tamaa alimwambia ‘’najaribu nikishindwa basi’’ Yule baba alitaka kujuwa kwanini anatafuta noeli kazi baada ya kusoma [couse] nyoyoyte ilikujiandaa na maisha ya chuo kikuu,ili [couse] iweze kumsaidia mbeleni.Unajuwa sikuzote katika maisha masikini anavyowaza tofauti kabisa na tajiri.Noeli baada ya kuulizwa hivyo aliamuwa kusema ukweli hasiria wa maisha yake.’’mimi natokea katika familia duni’’ Yule bwana akawa amemuangalia sana noeli kisha anamwambia ‘’wewe unahisi kazi gani itakusaidia’’ aliuliza hukuakimgeukia na kumuangalia kwa umakini.’’nikiwa mtangazaji nahisi nita isaidia familia yangu’’ aliongea kwakujiamini noeli akijuwa utangazaji pamoja na uwandishi ni vitu anapenda kutoka moyoni.



    ’’aisee! lakini sawa’’ alishangaa kumuona kijana kama noeli katika taifa la tanzania’’kwaiyo utaweza utangazaji?’’ alirudia tena kumuuliza noeli Yule bwana, noeli aliendelea kumuaminisha’’naweza sema sijapata media’’ alikuwa akiongea kwahisia maana alikuwa akizungumzia kitu anachokipenda.Hebu pata wazo au jaribu kuwaza namna unapokuwa ukizungumza kitu chenye uharisia kutoka moyoni,kitu ambachokilimfanya noeli aweze kujiamini ni pamoja na kugunduwa yeye ana sauti nzuri sana.’’sasa nitakupeleka kwa……. Flani’’ alimuaidi kwasababu aliona noeli akijiamini sana,’’anaredio?’’ aliuliza noeli kwa umakini uku akigeuza usowake kwa Yule bwana.’’ndio ana redio kubwa sana’’ ilikuwa ni furaha iliyoleta mtikisiko katika moyo wa noeli nakuleta tumaini jipya. ’’una simu?’’ aliuliza Yule bwana noeli akamwambia ‘’hapana’’ nyumbani kwao noeli hatamtu mmoja alikuwa hana simu.wala hata uwezo wakununua simu ulikuwa haupo,Yule baba liwaza kisha akamwambia’’noeli sasa nita kupataje?’’ Yule bwana alikuwa akiumiza kichwa atampataje noeli mala baada yakuachana ikiwa hata simu hana.Noeli nae alikua akiwaza atumie njiagani au ikibidi namba ya ndugu gani aweze kumpatia aweze kuwasiliana kiurahisi.’’nafikili na simu nyingine’’ alikumbukia kuwa anasimu ambayoilikuwa ni mbovu ampe noeli iliaweze kumpata kwaurahisi zaidi, kwanjia ambayo ni rahisi katika mawasiliano. ’’mmm’’aliguna hukuakienda kwenye gari lakekisha akatowa begikubwa lenye rangi nyeusi akaanza kulipekuwa katika kulipekuwa alibahatika kupata ile simu ambayoaliokuwa akiiwazia,kwamuda mchache uliopita ‘’safi hii hapa unaweza kutumia’’ aliongea hukuakiwa anamkabidhimkononi.Rafiki yake girbati aliamuwa kwenda kujikita katika migodi nae maisha yalikuwa yakimwendea vibaya kilakulipo kucha,’’dah!’’ alikuwa akiwaza sana hukuakiwa anapigamiayo na mchana huo njaa ilikuwaikimuuma sana na pesa yakula alikuwa hana maisha ya kahama yalikuwa yamemshinda kijana girbeti.wakumsaidia nae pia alikuwa hamuoni kabisa katika muda huo ulikuwa ni wakati mgumu sana kwake kijana girbeti. ’’kukaa hapa mimi bila kazi siwezi’’ alisema kijana girbeti ‘’wewe mwanaume unachaguwa kazi’’ alisema kijana mwenzake ambae alikuwa mchimbaji mdogo wa madini.’’uwoni kazi chimba hata…..’’ girbeti akighadhabika sana maana hakuna ambacho huyo kijana mwenzake aliweza kumsaidia, ’’hapa kuna pesa’’ alizidi kumwambia girbeti akamuangalia kisha akamwambia ’’zikowapi hizo pesa!’’ alikuwa akimuona kama mtu anae ongea tu pasipo kuchunguza kitu.’’unataka zikufuate! tafuta’’ alimwambia Yule kijana mwenzake. Tena alimjibu pasipokumwone huruma mwenzake,girbeti alikuwa haya wezi maisha ya mgodini maana alikuwa hakuwai kuyaishi.Girbeti aliwaza sana nakufikilia ‘’hivi nini ambacho kili nileta huku?’’ yeye pia alikuwa na ideal ya uwandishi lakini ilikuwa sio sana kama ya noeli alikuwa na kipaji kizuri cha uchoraji na alikuwa kachora michoro mingi na kuitunza ndani.Wakati alipokuwa akiwaza Yule kijna wenzake aliondoka na kumuacha,huku akimwambia ‘’waza mwenyewe hapo’’aliondoka ukugirbeti akiwa anawaza na hata kumkumbuka rafiki yake noeli.Namna walivyokuwa wakipeana mawazo na faraja katika maisha.’’hapa nilipo hapanifai’’ aliwaza girbeti mwenyewe moyoni alikuwa katika msongo mkubwa sana wa mawazo hata mchimbaji mmoja mdogo aliyekuwa akifahamiana nae alimfuata.Na kumwambia, ‘’punguza mawazo’’ alimuongeresha kwakumshitukiza kisha girbeti akashituka ‘’alaaa bwana weee!’’ http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Yule mchimbaji akamwambia, ’’punguza mawazo’’ girbeti akawa mkali sana kisha akamwambia Yule mchimbaji ‘’nomba niache’’ aliongea hukuakiwa amejawa na hasira isiyokuwa na kifani,wakati yeye na noeli wakihangaika wenzao walikuwa nyumbani wakisubilia matokeo ya kwenda chuo kikuu.Lakini kwa girbeti na noeli wao ilikuwa tofauti walipigania kuweza kufanikisha ndoto zao.’’twende chimbo’’ alimwambia Yule kijana mchimbaji mdogo girbeti baada ya kutuliza asira alimwambia ‘’hapana akili yangu haiko sawa’’ alisema girbeti Yule mchimbaji mdogo wamadini alikuwa katokea kuzoeana nae alitowa shilingi tharathini elfu na kumpatia girbeti. ‘’asante sana’’ aliongea girbeti hukuakiwa anatabasamu ilikuwa kama nuru yehova alioamuwa kumshushia.’’kawaida rafikiyangu itakusaidia’’ aliongea hivyokisha akaondoka girbeti akabakia mwenyewe kisha nae alinyanyuka na kwenda hotelini kwajili yakupata chakula.Alimuona hakika nyule kijana ana [humanity] kuliko vijana wengine pale mgodini ‘’dah! amenisaidia sana kwa leo’’ aliongea mwenyewe hukuakiwa anaenda hotelini kiguu na njia.Hebu wazia unapokuwa nanjaa alafu mtu akatokea kukusaidia utamchukulia daima kama mtu muhimu sana na mwenye utu mno ndivyoilivyokuwa kwa kijana girbeti.Ilikuwa yapata saa nane mchana noeli akawa amewasiri pale alipokuwa ameambiwa aende siku hiyo akiwa ameshikilia bahasha yenye vyeti vyake ndani.Alihisi uwenda maisha yakawa na uhafadhari kuliko alivyo hivyo,’’umerudi?’’ aliulizwa na mtu wapale mapokezi kisha akaitikia ‘’ndio bosi wenu aliniambia nije’’ alisema noeli hukuakiwa anamuangalia Yule dada wa mapokezi.Katika ofisi ile ambayo alikuwepo.’’haya ngoja niwasiliane nae’’ kisha ananyanyuwa simu yake na kumpigia bosi yake simuiliita kama dakika tano kisha akapokea.’’mariamu unasemaje?’’ aliuliza bosi wake katika simu,’’yule……. amekuja’’ alimpataalifa kisha bosi akamwambia ‘’ahaa mwambie aingie’’ kisha akakata simu na kumwambia ‘’sawa waweza kwenda’’ noeli sikuhiyo alikuwa kajitahidi kiasichake kuvaa vizuri miguuni alikuwa amevaa viatubila [sox] nguo alizokuwa amevaa pia zilikuwa zimepauka sana.Kiasi hata cha kupoteza rangi yake ya asilia. ‘’hodi’’ aligonga hodi kwa sauti ya chini Yule mkurungenzi akaitikia ‘’karibu….. ingia’’ pembeni mwameza yake alikuwa na kikombe cha chai.Ambachokilikuwa na chai ya moto ambayomkurungezi alikuwa akinywa hukuakifanya kazi zake, ‘’kwiiiiii’’ ilikuwa sauti ya mlango noeliakifunguwa na kuingia ofisini.’’kijana karibu’’ aliongea hukuakinywa chai yake ya moto,alikuwa ameshaliweka jina la noeli kichwani mwake.Alikaa kwenye kiti kwa heshima na nidhamu, ‘’zatangia jana’’ aliitikia noeli na kumjibu ‘’nzuri’’ bosi aliamuwa kumuita mariamu kwanguvu, ‘’emm mariamu?’’ aliitikia kwaharaka na kujambio.’’abee bosi’’ aliitikia mariamu dada aliyekuwa mapokezi kisha bosi akamwambia ‘’msikilize huyu kijana’’ aliongea bosi huku akiwa anabonyeza bonyeza tanakilishi yake.Na kuangalia program zake za kikazi ambazo alikuwa akifanya. ‘’una taka chakula gani?’’ alimuuliza Yule dada wa mapokezi ukuakiwa anamuangalia, noeli alimjibu ‘’naomba ugali na samaki’’http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ alimjibu lakini kwa aibu nyingi sana noeli alikuwa anaaibu mno.Mariamu alitoka akiwa anatoka na kurudishia mlango mkurugenzi akamuita, ‘’mariamu wambie hao wachakula waharakishe’’ ilikuwa sauti yake kubwa na yakusikika kwamariamu,’’sawa bosi’’ mkurugenzi alianza kuongea sasa taratibu na kijana noeli kwautaratibu na hustaha. ‘’umefanya demo nzuri?’’ noeli akamjibu na kumwambia ‘’ndio nimefanya lakini kwachangamoto kubwa sana’’ aliamuwa kuwamuwazi noeli katika jambo hilo mkurugenzi alimsikia kisha akamwambia kwautaratibu, ‘’hamna mdogo wangu kitu chakuja kama miujiza you must struggle’’ aliongea maneno machache lakini yalionekana kumkaa akilini noeli.Noeli akilini mwake alianza kuyafikilia maneno ambayo aliyokuwa akiongea mkurugenzi Yule, ‘’ila yuko sahihi nita yaishi na kuyashika maneno yake’’aliwaza akili noeli hebujiulize katikampito wako au mapito ambayo uliopitia katika maisha yako uliwahi kujifunza nini? Watu wengi sana mpito wamekuwa wakiuwona kama mateso.Napenda kukuambia maisha ulionayo sasa hutokaa nayo daima,ni mpito tu na neema yaja mbele yako.Motivation speaker maarufu duniani rezy- brown, alisema katika moja ya makongamamano yake kuwa hakuna mtu ambae mungu alimuumbia shida mpaka kufa hapa duniani.Wakati wakiongea punde tu mala chakula kikawa kimeletwa, chakula kilikuwa kizuri kama ambavyo noeli alikuwa kaagiza.Kilikuwa kimefunikizwa chula kilikuwa mapokezi kwa dada mariamu, ‘’noeli tuta kuchukuwa’’ alimtamkia [live] Yule mkurugenzi bila kumchengesha hiiili tokana na noeli kutengeneza demo wakati akiwa angali hana kifaa chochote wala hata personal computer, kitendo hicho tu kilimfanya aweze kupewa credty kubwa sana na yule bosi wa kampuni hiyo.Kuna mtu muda mwingine juhudi anayo iyonyesha inaweza kumu insipire mtu kukuamini na kukuta hata kazi uwenda ukawa na shahada au stashahada au hata hukuweza kwenda shule kabisa,unatakiwa kutengeneza mazingira ya watu kukuamini.







    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog