Search This Blog

Friday, October 28, 2022

MAFANIKIO KATIKA AKILI YANGU [SUCCESS ON MY MIND] - 3

 

     





    Simulizi : Mafanikio Katika Akili Yangu (Success On My Mind)

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Aliendelea kumpa moyo na mifano ya watu wengi sana ambao aliwaona katika maisha. ‘’mimi siwezi’’ alisema Yule mama mwenzake na mama noeli, ‘’sawa lakini mimi nitaendelea’’ aliongea mamanoeli kwaujasiri hukuakiwa nimwenye kujipa moyo sana.Yule mwanamke mwenzake na mama noeli alikuwa akimshangaa sana mama noeli kwa moyo aliokuwa nao wakufanya kazi bila ya kukataa tamaa na kuwa ni mwenye uthubutu.

    Nimuda wa saa tisa alasiri katika mji wa mwanza upepo ukiwa unavuma kutoka katika ziwa victoria.Ndege kubwa iliyokuwa imebeba watu waliokadiliwa kuwa,[60] ilikuwa ikituwa katika uwanja wa ndege wa mwanza.Nje ya uwanja watu walikuwa kisubilia ndugu zao waweze kushuka, kutoka katika ndege na waweze kuwa pokea ndugu zao hari ya hewa ilikuwa niyenye kuvutia, upepo ulivuma kwambali juwa nalo, lili tia nakshi ilikukamilisha hari nzuri ya hewa katika mkowa wa mwanza.Wale wakorea walikuwa wameshuka kutoka katika ndege, lengo lao kubwa ilikuwa nikutaka kuonana na kijana noeli ambae alikuwa akiwafurahisha sana.Nakukonga nyoyo zao ilikuwa niwakati muwafaka wakuweza kuonana nae walipofika walichukuwa gari la kuwapeleka moja kwa moja mpaka hotelini.Na hoteli ambayo walifikia ilikuwa ni gold crest ambayo ilikuwa katikati ya mji wa mwanza.’’hoteli itakuwa nzuri?’’ aliuliza mmoja kati ya wakorea ‘’hoteli ni nzuri’’ aliwajibu dreva wa gari hilo la hoteli hiyo, ‘’haya twende’’ walipokuwa wakipita barabalani walifurahiya madhari nzuri ya mji wa mwanza waliokuwa wakikutana nayo,milima mizuri ambayo ilikuwa na nyumba za watu.’’mwanza kumbe kama brazili’’ alisema mkorea mmoja ‘’nipazuri sana hakuna njoto kama la dar eslaamu’’ waliongea kwa lugha ya kingeleza.Wakati wakorea hao wakiwa wameingia katika mjiwa mwanza kuonana na noeli ikiwemo kumpa pongezi nakuonyesha ufuatiliaji mzuri katika kipindi chake muda huwo noeli yeye alikuwa maktaba ambayo na yenyewe ilikuwa karibu na hoteli hiyo ambayo wakorea wale walikuwa wamefikia.Alikuwa maktaba akiandaa makala iliaweze kutuma katika gazeti flani ambalo alikuwa kawaomba kuwaandikia makala, noeli alikuwa akiandika makala mbalimbali za kijamii na alikuwa na uwezo mzuri sana katika hilo pia. Changamoto pia zilikuwepo nyingi sana katika kazi hiyo nyingine ambayo alijipa kijana noeli.Kompyuta ya kuchapia alikuwa hana kwaiyo alilazimika kwenda kuchapa [stationary].ILikuwa ni kazi ya changamoto kwa kijana noeli ingawa alikuwa amejaribu kuthubutu, alikuwa amekaa mkao wakula hukuakiwa akiwaza kwa mapana na marefu kile alichokuwa akikiandika.Akiwa katika harakati za kuandika mhariri wa lile gazeti alilokuwa akiandikia akampigia simu. noeli anaamuwa kupokea ile simu hukuakitokanje, ‘’halooo’’ aliongea noeli kwa sauti ya juu sana, kisha mhariri akamwambia katika simu ‘’saa kumi mwisho kupokea makala tunaingia production’’ alisema mhariri, dah! Noeli alihisi kuchanganyikiwa kilichompamoyo alikuwa ameandika katika karatasi na kuweza kutamatisha kilichokuwa kinatakiwa nikuweka katika maandishi ya kompyuta na aweze kuituma kwa barua pepe.Aliondoka haraka nakwenda kuchapa kazi yake internet naaweze kuituma kwa Yule mhariri wa lile gazeti.Ilikuwa kama muujiza maana noeli alikuwa anaenda kuchapa kazi yake katika internet café ambayo ilikuwa karibu na hoteli ya gold crest alafu alipita maeneo ya hotelini palepale wakati akipita wale wakorea walikuwa wametoka nje ya hoteli wakiwa wana uwangalia mji wa mwanza namna ulivyo.Noeli alikuwa ameshaanza kuwa maarufu na watu wengi walianza kuiyona kazi zake nakupendezwa nazo, alipokuwa akipita ghafla mtu mmoja akamuita mtu huyo alikuwa ni moja ya watu ambao walipenda noeli alichokuwa akikifanya. ‘’noeli… noeli’’ alimuita kwa sauti maana alikuwa mbali na noeli, noeli kabla haja itika wale wakorea wakabakia kutahamaki sana. ‘’noeli ndio yupi?’’ walijiuliza waokwa wao wenyewe, lakini mmoja wao akawambia, ‘’ngoja tuone ataitikia yupi’’ waliongea wakorea hao hukukila mmoja akitaka kumuona noeli, mwenzake noeli aliyekuwa akimuita alikuwa amesimama mbele yao akiwa amesimama umbali wa mita[30] tu ‘’nammm’’ aliitikia noeli hukuakiwa anageuka kumuangalia aliyekuwa anamuita.Ndipo wale wakorea walipomjuwa noeli ni yupi, Yule aliye muita noeli alimsogelea na kuanza kuongea. ‘’umeadimika noeli’’ aliongea Yule aliyemuita noeli hukuakiwa amesimama na noeli, ‘’mambo yana zidi kuwa mengi’’ aliongea noeli kwa upole huku Yule aliyemuita akatowa pesa shilingi elfu kumi na kumpatia noeli ‘’nitakuona baadae’’ aliongea hukuakiwa anaondoka, ‘’sawa mimi naenda kuchapa makala yangu’’ aliongea noeli akionekana kuwa na haraka zaidi.Alipotaka kuondoka tena wale wakorea wakamuita tena kwajina lake harisi, ‘’hey noeli?’’ walimuita wote kwa pamoja hukuwaki mpungia mkono. ‘’hawa wameni Julia wapi!’’ alikuwa akishangaa mno ‘’noeli hi!’’ walimsogelea na kumpa mkono, kila moja wao ‘’yes how is it?’’ aliwajibu noeli kisha nawao wakamjibu kwa pamoja ‘’fine’’ noeli alikuwa anahraka sana aliwambia kuwa ana wai [deadline] ya gazeti na anatamani kuweza kukaa nawao aongee na akawaweka wazi kwakile anachokwenda kukifanya. ‘’tutaweza kwenda wote?’’ waliongea huku wakitabasamu noeli hakuweza kuwakatalia, alipoingia stationary na kuanza kazi ya kuchapa na kuhariri makala yake.Wale wakorea walikuwa makini sana kumuangalia kila alichokuwa akifanya kadili walivyozidi kukaa na noeli ndivyo walizidi kumfurahiya zaidi.

    Walianza kujitambulisha kwa noeli pamoja na madhumuni waliokuwa nayo.’’nashukuru sana’’ aliongea noeli hukuakitabasamu, nuru ya kupenda anachokifanya ikazidi kuongezeka kwa noeli.Waliendelea kumuuliza maswari ‘’jounalism ndio taaruma yako?’’

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ’ walimuuliza hukuwakiwa nae sambamba hawakutaka kuwambali nae, ‘’hapana’’ alikanusha kisha akawambia kilicho tokea katika michakato yakutaka kwenda chuoni.Noeli alikuwa ni mkweli katika maisha yake, ‘’alaaa! Kumbe sasa una mpango gani kusoma’’ aliuliza mkorea mmoja hukuakiwa anamuangalia machoni noeli.Noeli akamwambia, ‘’tatizo ni pesa’’ alisema noeli ‘’ukipata chance ya kusoma journalism utafanya viruzi zaidi’’ walikuwa wakiongea wakorea hao hukuwaki onafahari kuweza kukaa pamoja na noeli.Walizdi kumuhamasisha noeli ukuwaki endelea kumuamini sana noeli walijuwa wazi noeli alikuwa ni [born to be] yaani noeli alikuwa na uwezo mzuri wa uwandishi wa habari tangia kuzariwa kwake.’’Nacho kiona anatakiwa kuendelezwa asome’’ alisema mkorea mmoja ambae alimuona noeli kama kijana mwenya kupigania ndoto zake na kuweza kuziishi. ‘’unakipaji kikubwa sana’’ wale wakorea waliendelea kumsifu sana noeli ingawa lugha waliyoitumia kuongea ilikuwa ni lugha ya kikorea.Walianza kujadiliana namna ya kuweza kumsaidia noeli aweze kupata shahada yake ya journalism wakorea walikuwa watatu mmoja alikuwa mwanaume na wengine walikuwa ni wanawake, kati ya wale wawili alikuwepo mkorea mmoja ambae alikuwa na baba yake nae alikuwa mkufunzi katika chuo kimoja huko urusi.Alikuwa ni mhadhiri katika chuo kilichokuwa mjini mosco, alipanga kuweza kumwambia baba yake amsaidie noeli kupata udhamini katika chuo chochote mjini mosco. ‘’tuta hakikisha unapata shahada’’ walimuakikishia katika hilo,noeli hakuweza kuwaamini kwa haraka ‘’nikweli?’’ aliongea noeli kwa mshangao hukuakitowa macho yake kwa nguvu, ‘’kuna mtu tuna fanya nae……. atakusaidia’’ noeli baada ya kuambiwa hivyo aliinamisha kichwa chake chini na kuanza kunyoosha mikono yake hukuakiwa anashukuru vilivyo, ‘’ooooh! Nitafurahi sana endapo itakuwa hivyo, noeli mungu kwa wakati wake alikuwa ameamua kumfungulia milango kupitia watu wengine ambao ni tofauti na watanzania wenzake. ‘’nijambo dogo’’ alisema Yule mkorea wakike hukumwingine nae akisema, ‘’unatufurahisha na unakipaji’’ ilikuwa ni hari ya kumfurahisha sana nakuzidi kumpa moyo. ‘’nyumbani wapi?’’ walimuuliza ‘’ nihapahapa mwanza’’ walitamani hata kupafahamu nyumbani kwao noeli walianza kupata uharisia wa maisha ya noeli walitaka kuweka ukaribu mkubwa nae. Ilikuwa ni kama neema kutoka mbinguni.

    Noeli baada yakuambiwa hivyo na wale wakorea dah! Sikuilimwendea vyema sana kwatumaini kubwa mno, likamjia moyoni mwake ‘’tunaweza kwenda nyumbani leo?’’ walimuuliza kama inawezekana mazingira ya nyumbani kwao noeli yalikuwa ni mabaya sana.Aliamuwa kuwambia ‘’apana kesho itakuwa vyema zaidi’’ alikuwa akiongea nae kwa lugha ya kingeleza, alifanya hivyo noeli ilikuweza kuandaa mazingira yakuwakaribisha rasimi nyumbani kwao noeli alikuwa akiwathamini na kuwapa au kuwatunuku heshima kubwa sana.Na alikuwa akihisi ametembelewa na watu wenye uthamani mno.Giza lilikuwa limetanda wakorea walikaa na noeli hatimae waliamuwa kwenda kulala pale hotelini walipokuwa wamefikia.Waliagana na noeli vizuri kisha wakaondoka noeli siku hiyo alikuwa hana kazi yakwenda kufanya studio lakini pia alikuwa hana kipindi redioni, ebufikilia unapata watu wanakuwa wanakiamini unachokifanya alafu wanakuwa mbali na wewe hatimae wanaamuwa kupanga safari kwa sababu yako wewe fikilia hilo nifuraha ya aina gani itakayo kupata ndivyo.Ilikuwa kwakijana noeli ambae alipatwa na furaha kiasi cha kushindwa kuizuiya.Tayana mpenzi wake nae muda huo alikuwa katoka katika shughuri zake za kushona nguo, noeli na tayana walikuwa wamezoeshana kukutana katika hoteli ya victoria lakini kutokana na uwezo haba wa kifedha walikuwa wakiishia nje.Uwezo wakuingia ndani walikuwa hawana tayana alikua akimsubilia noeli nje ya hoteli hiyo.Alisimama kwa muda mrefu sana akimsubili noeli hukuakijiuliza ‘’mbona haji huyu’’alijiuliza mwenyewe wakati huo noeli alikua akiwai ilikufika mapema katika eneo hilo.Zawadi dada yake noeli alikuwa katika basi wakija mwanza kuranguwa samaki awapeleke jijini dar eslaamu,akiwa ndani ya basi katika siti aliyokuwa amekaa alikuwa amekaa na dada mmoja ambae nae alikuwa mfanya biashara na mpambanaji.Yeye alikuwa mzaliwa wa shinyanga makazi yake yalikua mwanza dar eslaamu alikuwa akienda kibiahsara zaidi.Alikuwa ni mdada mwenye juhudi sana katika kila alichokuwa akikifanya. ‘’dah! Nimechoka’’ alisema Yule dada akimwambia zawadi ‘’hata hivyo dar to mwanza mbali’’ aliongezea kwakuongea zawadi dada Yule alikuwa akijinyoosha mala kwa mala ‘’unakaa mwanza?’’ alimuuliza zawadi, nae zawadi hakuchelewa kumjibu, ‘’ndio’’ alikubalia kwa haraka sana zawadi pia alikuwa anaupenda mji wake ambao alizaliwa. ‘’unajishughulisha na nini?’’ yalikuwa maongezi yakutaka kufamiana zaidi hasa ukizingatia, wote walikuwa pamoja katika safari moja. Zawadi alimwambia ‘’nauza samaki’’ alimfafanulia anawatowa mwanza nakuwa peleka jijini dar eslaamu, ‘’aisee nibiashara nzuri’’ maongezi yao katika safari yalikuwa yakizidi kuwanogea zaidi, ‘’lakini inakulipa?’’ zawadi hakuona shida kumwambia ukweli kuhusu biashara yake ‘’inalipa kiasi chake’’ alisema zawadi ukweli ulikuwa nikwamba Yule dada alikua kafanyabiashara nyingi katika mpito wa maisha yake.Alikuwa kaisha fanya biashara ya kuuza samaki sawana alivyokuwa akifanya zawadi,

    Ni usiku ya pata kama saa mbili unusu noeli akawa amewasili nyumbani.Na wingi wa furaha ukiwa umetawala, ‘’noeli?’’ aliita mama yake ukuakiwa ameshikilia koroboi mwanga wa koroboi ndio ulikuwa umetawa katika maisha yao ya pale nyumbani tangia kuzaliwa kwao yeye na dada yake zawadi walikuwa hawajawai kuona umeme nyumbani kwao, ‘’nakuja mama tuongee’’ alisema noeli maana alikuja na kuingia tu ndani pasipo kumtaarifu mama yake kama yumo ndani mama ake akaingiwa na wasiwasi akijuwa uwenda akawa mtu mbaya. Punde noeli aliweza kutoka nje kuongea na mama yake, ‘’mama kesho weka mazingira safi’’



     alianza kwakumwambia mama yake. ‘’kuna nini kwani?’’ aliuliza mama noeli hukuakili ikiwa imemtuma mbali sana.Huwenda mwanae noeli alikuwa anataka kuleta mwinga nyumbani, ndiko akili yake iliko mtuma zaidi. ‘’sija amini bado mama’’ alisema noeli nakumuacha mama yakenjia panda. ‘’huja amini nini?’’ aliuliza mama yake hukuakiwa njia panda, ‘’mama nimepata wadhamini wazungu’’ aliongea noeli na mama yake alimshangaa sana. ‘’noeli mwanangu umeanza kuwa na wazimu?’’ aliuliza mama ake noeli kisha noeli akaendelea kumwambia, ‘’mama amini kweli na kwambia’’ mama noeli wazungu aliwachukulia kama yehova vile maana hakuamini kile ambacho mwanae alichokuwa akimwambia. ‘’mmmmh!’’ aliguna na kutikisa kichwa mno.Wakati huo noeli alikuwa ameshakutana na mpenzi wake tayana na akampa taarifa kuwa kuna wakorea wanao taka kumsomesha, tayana hakumkubalia kutoka na dhana ya watu wa ughaibuni kuweza kuwachukuwa watu na kwenda kuwafanyia mabo mabaya.Dhana hiyo ilimkaa akilini nakusababisha hata aweze kuwafikilia vibaya watu wa mataifa ya ughaibuni.Wakati wakiwa katika maongezi pindi walipokuwa wamekutana tayana alimsihizaidi noeli, ‘’usiende, usiende kabisa’’ lakini hilo alikuweza kumfanya noeli awe na mtizamo ahasi bado aliendelea kuwa na mtizamo chanya.Maongezi kati ya noeli na mama yake yaliendelea wakiwa wamekaa sebleni kwao, ‘’ume wapatia wapi?’’ bado mama noeli aliendelea kumuuliza maswari mengi sana mwane tena kwaumakini wa hari ya juu, ‘’niwasikilizaji wazuri wa kipindi changu’’ bado ilikuwa ngumu kumuamini alichokuwa akikisema noeli mzungu kwamtizamo wa mama noeli alimwona kama mtu wa utofauti sana na hawezi kuja kumfuata noeli mwanae kutoka familia ya kimasikini. ‘’kesho watakuja tuta waona’’ alisema mama ake noeli kwa furaha aliyokuwanayo noeli alimuacha mama yake na kufunga safari ya kwenda nyumbani kwao dausoni ambae alikuwa akikaa nae jirani na pia alikuwa akisoma nae yeye alibahatika kupata mkopo wa kusoma chuo kikuu.Lakini pia wazazi wake walikuwa nauwezo wakifedha, nandicho kitu kilicho muuma noeli nakuona mungu anaupendeleo.Noeli hakujuwa mungu ni mungu wa upendo na haki pia, nakila aombae nakujishughulisha yeye humpa mwanga na nuru sambamba na mibaraka dausoni alikuwa ndani akitizama runinga usiku huo nje walikuwa wamekaa kina mama na akina dada ambao walikuwa ni ndugu wa dausoni, ‘’hodi hapa?’’ aliongea kwasauti noeli akiwa amesimama ‘’karibu’’ alijibu mama mdogo wake dausoni ‘’ahsante’’ aliitikia kisha akaulizwa ‘’wewe ninani?’’

    ‘’naitwa noeli’’ alipokwisha kutaja jina lake tu watu wote wakashituka huku mama zake na noeli wengine wakisimama na kuuliza vyema, ‘’noeli mtangazaji?’’ noeli hakujificha aliwajibu na kuwambia, ‘’ndio mimi’’ walinyanyuka na kuanza kumuangalia walianza wenyewe kumtunuku uthamani mkubwa sana. ‘’lakini dausoni alishatwambia tukabisha’’ waliongea hukuwakimpisha njia aweze kuingia ndani, noeli aliposikia dausoni aliwambia ‘’dausoni nimesoma nae’’ alisema noeli kwa utaratibu huku akiwamekaziwa macho akiangaliwa na kilamtu.Mala punde si punde mala dausoni akawa ametoka nje akiwa nimwenyefuraha maana.Alifurahi kusikia noeli amekkuja kumsalimia nyumbani, ‘’noeli’’ aliita dausoni kisha noeliakaitikia ‘’nammm’’ wakakumbatiana na kupeana mikono.Hukukila mmoja akiwa ni mwenye furaha, ‘’uwonekani’’ alisema dausoni ‘’kazi wana nibana sana’’ aliongea kwautaratibu ‘’karibu ndani’’ kisha wanaingia ndani baba yake dausoni alikuwa amekaa kwenye makochi ya sofa.Akiangalia televisheni akibadilishana na mawazo na kijana wake dausoni, ‘’baba huyu ndie dausoni’’ alimtambulisha noeli kwa baba yake ‘’alaaa! Karibu’’ alimkaribisha kwafuraha kubwa sana isiyokuwa na kifani.Noeli aliitikia kwa ukarimu ‘’ahsante’’ baba ake dausoni alikuwa akimuuangali malambili mbili kijana noeli akishindwa kujuwa amefanyanini mpaka kufikia alipokuwa.’’zakazi noeli’’ baba ake dausoni mwenyewe alikuwa akiona furaha kukaa na kijana noeli,’’nzuri’’ noeli alikuwa amekaa kiheshima sana baba dausoni alikuwa akimuona noeli kama kijana mwenye bahati.Kichwani alikuwa akiwaza mwenyewe ‘’hivi kweli atakuwa kapambana kwa nguvu zake huyu kijana?’’ alikuwa akimuangalia na kumfikilia akilini mwake.Aliamini noeli atakuwa ana mtu ambae amemfanyia mpango kuweza kufikia hatuwa ya kutangaza kituo kikubwa kama kile.Akifikilia wataaruma wa habari walikuwa wengi mtaani na walikoswa ajira alimfikilia kwa mapana zaidi kijana noeli [kwakeli mungu ni mwema huwa nyanyuwa wanyonge na kuwapa uthamani].

    ***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SURA YA TANO

    MUNGU KATIKA NJIA YA MAFANIKIO[GOD ON THE WAY TO MY SUCCES]

    Ni muda wa saa mbili asubui noeli akiwa ametoka nyumbani na kuelekea kazini.Aliamuwa kupita hoteli ya gold crest kuwasalimia wale wakorea, ambao walikuja mwanza kwajili yake.Alafu badae aweze kwenda ofisini maana siku hiyo ofisini kulikuwa na kikao kikubwa sana, alipofika gold crest alikuta wakorea wako nje ‘’waoo karibu noeli’’ waliongea kwatabasamu kubwa lenye furaha isiyokuwa na kifani. ‘’asante’’ walikuwa wamesimama nje lakini baadae waliweza kwenda nae mpaka ndani ya hoteli. ‘’za tangia jana?’’ walimuuliza wote watatu huku wakiwa na nyuso za tabasamu, ‘’nzuri’’ wao walikuwa ni watu wenye imani ya kidini sana, ata walipokuwa katika mji wa dar eslaamu asubui ilikuwa razima waweze kwenda kusali ibadani.Mwanza pia kulikuwa na pastor wao ambae alikuwa akiwapa elimu ya kiimani pamoja na [inspiration] katika mambo na maisha yao yakila siku, pastor huyo alikuwa ni mzungu kutoka Canada walipokwishafika waliwasiliana nae na kumwambia kuwa wako mwanza.



    Pastor aliwaelekeza alipokuwa akipatikana kwa muda wote.Pastor alikuwa anakaa mtaa wa pasiasi, huko pia alikuwa akifanya kazi ya kuhudumia watu na kuwapa elimu ya kidini kuhusu masuala ya kiimani. ‘’noeli?’’ alimuita mmoja kati ya wale wakorea ‘’nammm’’ aliitikia noeli hukuakiwa anawaangalia, ‘’pasiasi iko wapi?’’ aliulizwa noeli kisha noeli akawajibu kuwa pasiasi ni nje kidogo ya mji wa mwanza.Wakorea hao wao hilo awakuliona wao walikuwa wakitaka kufika pasiasi ilikuonana na pastor, ‘’okey nita wapeleka’’ alikubalia maana ilikuwa haina njia yakuweza kuwa katalia wakati yeye ndie alikuwa mwenyeji wao.Siku hiyo pia gazeti lilikuwa limetoka na makala ya noeli ilikuwa imetoka.Makala yake ilikua ikizungumzia masuala ya kijamii, iliweza kumuongezea wigo mkubwa wa watu pia.Aliweza kupigiwa simu nyingi sana kwa asubui tu ujumbe wamaandishi pia uliingia kiasi cha kupitiliza, ndoto na malengo yake sasa zilikuwa zikienda kutimia.Safari ya kwenda pasiasi kuwa peleka wakorea iliweza kuanza, zawadi nae alikuwa ameshafika katika mji wa mwanza na akiwa amewasili tangia usiku wa kuamkia siku hiyo.Zawadi baada ya kutoka tu kitandani kabla ya yote alipata wazo. ‘’nimepata faida kubwa sana katika biashara kwanini nisiende kumshukuru mungu’’ suala hilo liliibuwa maswari mengi katika kichwa chake kisha ana mwambia mama yake. ‘’mama?’’ aliita kwasauti ya upole sana, ‘’abee zawadi’’ kisha zawadi akamwambia mama yake, ‘’naenda kanisani’’ mama yake alimkubali na zawadi alipanga atakapo fika atataka kuongea na pastor wake.Ambae aliachana nae takribani miaka minne kutokana na harakati alizokuwa nazo zakusaka maisha ilikuwa ngmu sana kuweza kwenda kanisani, wakati ambapo watu wengi huwa katika dhiki huwona niheri kuweza kufanya mambo yao kwanza.Alafu yehova kumpa fursa ya mwisho na ibirisi amekuwa akiwashikilia watu wengi hapo. [yeremia;33,3] ndivyo ilikuwa kwa zawadi alivyokuwa katika mfumo wa maisha yake. ‘’unaenda sangapi?’’ aliuliza mama noeli zawadi binti yake akamwambia, ‘’asubui hii’’ aliongea hukuakiwa amesimama na mama yake, ‘’nakwenda kuchukuwa samaki’’ aliuliza mama noeli hukuakimwambia kuwaataweza kufanya mambo yote mawili, aliongea na baada ya muda mfupi aliagana na mama ake na kuondoka.

    Noeli alikuwa ameshafika pasiasi akiwa na wale wageni wake,ambao walikuwa wamekuja kumtembelea. ‘’mkowa mzuri huu’’ waliongea huku waki geuza geuza shingo zao, huku na kule walikuwa wamesimama wakimsubilia pastor ajekuwachukuwa walizidi kuuangalia mkowa wa mwanza kiumakini. Mji wa mwanza ulionekana kuwavutia sana wale wakorea wakiwa bado wangali wamesimama mala ikaja gari aina ya [range] yenye rangi nyeusi ghafla akashuka Yule pastor ambae alikuwa amevaa suti yake yenye rangi nyeusi kisha akasalimiana na wale wakorea, ‘’twende nyumbani alisema pastor huyo mzungu, ‘’mungu ni mwema ametukuta nisha tena’’ walisema wakorea wale hukuwakiwa wanaingia ndani ya gari. ‘’mimi mtumishi acha nikae mbele’’ alisema mkorea mmoja ambae alikuwa na shauku kubwa sana yakutaka kukaa karibu na yule pastor wakizungu ilikuwa ni kiu na shauku yake kubwa sana. ‘’hapana ukumbele muachie huyo kijana aweze kukaa’’ alisema pastor huku akiwa amemchaguwa noeli kuweza kukaa nae karibu, tayari alianza kuendesha gari lake kuwapelekka nyumbani kwake.Wakati alipokuwa akiendesha gari lake alikuwa akimuangalia sana noeli na kumsemesha. ‘’unaitwa nani kijana?’’ alimuuliza noeli hukuakiwa anamuangalia sana, ‘’naitwa noeli’’ alijibu noeli ukuakiwa anaangalia mbele namna gari lilivyokuwa likitembea, ‘’safi noeli nakuona mungu amekupa….. flani’’ aliongea kwautara tibu sana Yule pastor wa kizungu.’’kitu!’’ alishangaa kwanza noeli ukuakijiuliza maswari kuntu kichwani mwake.Noeli alikuwa akishangaa sana alijuwa pengine kuna kitu kina endelea baina ya wale wakorea na Yule pastor wa kizungu, kumbe roho mtakatifu alikuwa amemshukia pastor na kumuonyesha mambo ambayo noeli alikuwa ametunukiwa na mungu kama kipawa.Niswari unapaswa kujifikilia je mungu wewe amekutunuku nini ambacho ulicho nacho? Yaweza kuwa kuimba au yaweza kuwa mambo mengine uwe kijana ama mzee unapaswa kujiuliza swari hili tena kwa mapana,Watafiti wa mambo ya kidini na kiimani waliingia katika utafiti mkubwa zaidi.Nakugunduwa hakuna mwanadamu ambae ameubwa na kukoswa kipawa chochote, jiulize unauwezo gani ambao mungu amekujalia? Yehova aliamuwa kumuonyesha Yule pastor mzungu uwezo ambao aliokuwa nao noeli, kristu pia aliendelea kutembea juu ya Yule pastor kisha pastor akamwambia,’ ‘’hakika utukufu unatembea juu yako’’ aliendelea kuongea pastor hukuakiwa ana mpa maneno mazuri noeli.Noeli aliweza kufarijika na maneno ya Yule pastor na yakawa yamempa nguvu kubwa ya kiimani. ‘’naona mungu njiani amekuandalia mambo mazuri na kila atakae shinda na wewe atashindwa, umeumbwa wa kushinda nasio kushindwa noeli’’ dah! Noeli alijikuta kutamani nishwa na Yule pastor kwa maneno yake, picha yamungu alianza kuiyona katika akili yake.Punde tu wakawa wamefika pastor akafunguwa mlango wa gari kisha akatoka nae noeli pamoja na wale wakorea wakawa wameshuka nao kutoka katika gari. ‘’jamani tukaribieni ndani’’ alisema pastor hukuakifunguwa mlango wa kuingilia ndani, kisha wakaingia alipokuwa akikaa Yule pastor palikuwa ni pazuri sana.Noeli alitembea macho yakiwa juu juu sana ‘’noeli utaanguka’’ alisema mkorea mmoja kwa lugha ya kingereza hukuakiwa kamshika mkono noeli asiweze kuteleza na kuanguka. ‘’hapana naangalia humundani namna kulivyokuzuri’’ alisema ukweli noeli.Noeli alikuwa muwazi sana hata akuweza kuhofia kuchekwa na alipenda sana kujifunza mambo mengi kutoka kwa wengine, noeli kila uchao alikuwa akipenda kujifunza kitu kipya kingie katika akili yake.Hebu jiulize pia swari lingine kila siku huwa unaingiza kitu gani kichwani? Au ndio siku inaisha ujajifunza kitu chochote kama ndivyo inakupasa ubadilike na uwekama noeli.



    .Nime pata kuwaona vijana wengi wa kitanzania na baadhi ya nchi za kiafrika kuwa wajuwaji angalia hawa jui vitu sikitu chema tuna paswa kujifunza ilitujuwe vingi kama alivyokuwa noeli,Walielekea kukaa katika viti mala baada ya kuingia ndani.pastor yeye alienda moja kwa moja mpaka jikoni huko alimkuta mfanya kazi wake akiwa anafanya usafi, mfanya kazi wake alikuwa anaitwa martina alipofika tu alimuita, ‘’martina?’’ aliita pastor martina aliitikia ‘’abee pastor’’ pastor alikuwa anampenda sana martina na hata hafla mbalimbali ulaya na nchi kadhaa za Africa alienda nae pamoja. Martina alikuwa mtoto wa mitaaani alichukuliwa na pastor huyo ambae alikuwa na roho nzuri naya utu. ‘’kuna wageni andaa chai, na juice za wageni’’ alikuwa akiongea pastor hukuakiwa ameshikilia mlango, ‘’sawa pastor’’ alimjibu martina pastor kwalugha ya kingerza martin aalikuwa akiijuwa vyema lugha ya kingereza kutokana na kwenda nchi za wazungu mala kwa mala.Baada yakumaliza kumpa maagizo pastor alirudi kuongea na wageni wake kule sebleni, ‘’eheee za dar eslaam jamani?’’ aliongea ukuakienda kukaa katika kiti, ‘’nzuri’’ waliitikia wote kwa pamoja wale wakorea waliongea na pastor kisha baada ya muda mfupi kupita waliamuwa kuanza kumtambulisha kijana noeli na kazi yake ambayo aliokuwa akiifanya. Lakini pia hawakuacha kumwambia [obstacles] ambazo alizokuwa akikumbana nazo kijana noeli, pastor alitikisa kichwa chake kisha akamwambia noeli, ‘’your born to wine not tobe faire’’ aliongea pastor hukuakiwa ana tabasamu na kumuangalia noeli usoni. Bado pastor aliendelea kuongea maneno yenye nguvu na yenye kumtia moyo noeli, baada ya pale alimuuliza noeli ‘’uko tayari tusali?’’, ‘’niko tayari’’ alisema noeli kisha wote wanapiga magoti chini na kuanza kusali.Maombi yalikuwa ni marefu na yenye[ motivation] kubwa ndani yake, punde waliweza kutamatisha maombi yao na kusimama kisha wakaanza kupeana mikono. ‘’asante sana’’ alisema pastor hukuakiwapa mikono wote na kuwakumbatia, walirudi kukaa katika nafasi zao ‘’mimi najuwa utasoma tena nje ya taifa lako’’ aliendelea kumwambia noeli maneno ambayoa ni adimu sana na hakuwai kuyafikilia kuyapata nje na mama yake mzazi. Mala martina akaleta chai pamoja na vitafunwa alikuwa amebeba sinia ambalo lilikuwa na sahani nyingi juu yake,’’karibuni’’ alisema martina hukuakichuchumaa kupiga magoti kama ilivyokuwa mila na tamaduni za mabinti wa kiafrika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zawadi akiwa nae ameenda kumtembelea pastor aliyekuwa kaachana nae sikunyingi sana.Alifanikiwa kumkuta pastor lakini akiwa na watu wengi mno waliokuwa wakimsubilia kuzungumza nae kwashida mbalimbali. pastor akiwa anaongea na waumini wake mala dhalula ya simuikaingia na simu ilitoka kwa mtu wake wa msingi sana, ikawa hainabudi pastor kuweza kutoka nje ilikuweza kuongea na simu yake.Akiwa anaongea na mtu katika simu mala akamuona zawadi akiwa amekaa akimsubilia nae aweze kuongea nae. ‘’mmmh!’’ alishangaa na kugunia moyoni ilikuwa nisiku nyingi zimepita hakuwai kuonana na zawadi, baada ya kumaliza kuongea na simu alimuita ‘’zawadi?’’ aliita pastor hukuzawadi akiwa amesimama katika ngazi. Kisha zawadi akaitikia, ‘’abee mtumishi’’ aliitikia kwaunyenyekevu sana kule alikokuwa kaolewa zawadi na kuondoka sasa hari ya uchumi ilimuendea mume wake vibaya.Mume wake alikuwa akihisi kuchanganyikiwa muda huu alikuwa amekaa na ndugu zake sebuleni akiwaomba ushauri. ‘’nataka zawadi arudi’’, ‘’yani mwanamke kawa na……… zake unazania atakukubalia’’ aliongea mmoja kati ya ndungu zake hukukila ndugu yake akimpa maneno yenye kumkatisha tamaa.Zawadi baada ya kuitwa alimfuata pastor wake, ‘’wewe mwanampotevu ulikuwa wapi?’’ aliongea kwakutabasamu kabla ya zawadi kuolewa na kuanza kupambana na maisha pastor huyo alikuwa akimsaidia zawadi mambo mengi sana. ‘’hamna ni maisha tu pastor’’ alisema zawadi hukuakitabasamu, ‘’mbona unabadilika na kumpa mgongo mungu wako?’’ aliuliza pastor ukuakiwa anamuangalia usoni zawadi. Pastor aliangaliwa na zawadi pia kwa huruma pastor alianza kuwa na wasiwasi na maisha ya zawadi akihisi amekuwa wadunia.

    Ilikuwa ni siku ya jumapili noeli akiwa barabalani akiwaona wenzake wakienda chuoni kwajili ya kuripoti na kuweza kuanza masomo.Nakipindi hicho ndio kilikuwa kipindi cha vyuo vingi kufunguliwa na kupokea wanafunzi wapya, noeli alikuwa amejitolea kumsindikiza rafiki yake, ‘’mtaani nabakia mwenyewe!’’ alijiuliza swari hilo kichwani mwake huku raha ikimuondoka kabisa moyoni mwake.Mwenzake walipofika stendi ya mabasi aliingia ndani ya basi hukuakimuaga noeli kwa sauti maana kelele zilikuwa zimetawala kwawingi stendi, ‘’noeli ubakiae salama’’ noeli hakuongea chochote alipunga mkono wa wivu ilikuwa nisiku ambayo asingeweza kuisahau katika maisha yake.Noeli alitawaliwa na unyonge mwingi sana hatatembea yake ilikuwa niya utaratibu sana, alikuwa akielekea studioni wale wakorea walikuwa tayari wamesha rudi dar eslaam akiwa anatembea njiani mala sauti ikamjia ‘’noeli utafanikiwa’’ sauti hiyo ilikuwa inataka kufanana na ile ya Yule pastor aliyekwenda kumtembelea na wale wakorea.Noeli alijikuta akiona hatakile alichokuwa ameaidiwa akikipuuzia, ‘’nafasi ya kusoma si wanipe sasa hivi’’ alijifikia nakuona alikuwa akidanganywa akifikilia walimwambia watakwenda nyumbani kwao na hawakwenda.Hapoa ndipo alizidi kutokuwa na imani nakile alichokuwa ameaidiwa.Aliwaza sana naku [reason] maana noeli alikuwa nikijana ambae anapenda ku [reason] mno lakini bado hakuweza kupata jibu.Biashara ya zawadi ilikuwa imechanganya vizuri sana alikuwa tayari amesha chukuwa mzigo mwingine wa samaki na akitarajia kurudi tena jijini dar eslaamu, mwenyeji wake Yule wa jijini dar eslaam akampigia simu zawadi akapokea wakati huo alikuwa katika soko kubwa la samaki jijini mwanza [mwaloni], ambakokelele zilishamili zawatu pamoja na magari, ‘’zawadi mbona umechelewa sana?’’ zawadi alimjibu kwa sauti, ‘’ninalanguwa mzigo nita kuja siku ya……….’’ Alisema zawadi kule jijini dar eslaam watu walikuwa wameweka tenda katika hoteli mbalimbali, pamoja na migahawa wakitaka samaki kutoka mwanza.Aliendelea kumsihi aweze kuwai wafanye biashara walikuwa wametokea kuelewana zawadi na Yule mwenyeji wake na kuaminiana sana kibiashara, hakuna ambae aliyekuwa na shaka na mwenzake wala wasiwasi hata mmoja.



    Noeli akapanda dardara kuelekea studio zilipokuwa akiwa kwenye daradara akapigiwa simu na mhariri wa gazeti ambalo alilokuwa akiandikia. ‘’noeli?’’ aliita mhariri katika simu ‘’namm kaka’’ aliitikia noeli hukuakiweka umakini katika kusikiliza mhariri anacho mwambia ni nini, ‘’aisee makala yako nzuri sana’’ alisema mhariri akiwa anampongeza kijana noeli, ‘’nashukuru’’ barua pepe ambazo alikuwa akizipokea zilikuwa nyingi sana, na baruwa pepe zote zilikuwa za kumsifu kijinsi noeli alivyokwakuweza kuandaa makala nzuri na yenye kuigusa jamii.Noeli alikuwa na skills za kuandika na skills zake zilikuwa za uwandishi wa uchunguzi na kutafakali sana kwa mapana na marefu, kwaakile alichokuwa akikiandika. ‘’naitunza makala yako’’ alisema mhariri akiwa amerenga kujakuipeleka katika mashindano ya uwandishi wa makala bora nchini Tanzania, shindano ambalo liliwashindanisha wa ndishi wa habari pamoja na makala mbalimbali za kijamii.Noeli alifurahiya sana na akamuaidi mhariri kuzidi kuandika makala nyingi zaidi za kijamii na zenye kuelimisha jamii kwa ufundi zaidi.Watu waliokuwa wasomaji wazuri wa magazeti walianza kumuona kama kijana nyota katika uwandishi anaechipukia.Ingawa alitoka katika familia masikini lakini bado watu wenye heshima walianza kumtambuwa kupitia makala hiyo moja tu.Ofisi za gazeti zilikuwa dar eslaamu wakati noeli akifurahiya kuona alichokiandika kwaakili yake kina pokelewa kwautashi mkubwa na watu.Ilikuwa yapata saa nne asubuhi muda wa ofisinyingi kuwaruhusu.Watumishi wao kuweza kwenda kupata kifunguwa kinywa, maofisa wawili walionekana kuwa busy sana kusoma. Makala ambayo alikuwa kaiyandika kijana noeli waliisoma hukuwakiwa wanajadiliana, ‘’’’dah! Kijana huyu anaandika sana’’ walikuwa hawaamini hasa ukichangia na umli aliokuwa nao kijana noeli ‘’nimdogo rakina ana hekima flani alitunukiwa na mwenyezi mungu’’ walizidi kuongea mada kuu ilikuwa ni kijana noeli na uwandishi wake mahili. ‘’sikuzambeleni atafanya vizuri sana’’ noeli anazidi kupata jina kwakile alichokuwa akikifanya.Hebujiulize kama ni kijana, mama,baba,au hata dada n.k mpaka ulipo ukifa kama leo jamii itakuchukulia kama mtu gani? Umeiyachia nini jamii yako au hatafamiliya yako, tunaposema umeiyachia nini hatuna maana ya fedha au kitu chochote chenye uthamani.Hapana tuna maanisha umeachanini aidha kitabu yaweza kuwa hata mshauri na mwenye harakati kwa masuala ya vijana yapo mengi tu.Wale maofisa waliendelea kusoma wakati mmoja akiwa anasoma akamuuliza mwenzake, ‘’hebu muangalie wawapi huyo?’’http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ akimuonyesha na kisha aliangalia na kumwambia, ‘’wa mwanza huyu kijana’’ walitunza namba zake za mkononi ambazo zilikuwa kwenye gazeti.Ili wapatapo muda waweze kuwasiliana nae.Noeli akiwa katika daradara hatimae waliweza kufika katika kituoni kisha noeli alishuka na kwenda studio.Kama una uwezo flani mungu amekujalia yaweza kuwa kuimba, yaweza kuwa mwaandishi mzuri napengine hukwenda shuleni.Alafu ukajikuta umezaliwa pia katika familia masikini usikate tamaa, kifanye kitu hicho yamkini mungu ndio atakunyanyuwa kupitia hichokipaji chako au huwo uwezo wako uliokuwa nao.Kinacho waangusha watu wengi ususani sisi waafrika nikuto tambuwa uwezo tulio patiwa na mungu waziada tofauti na wengine,ndio maana bara letu limekuwa kila siku likiandamwa kwa umasikini.Hebutujiulize tunawezaje kuitwa bara masikini wakati tungali na uwezo waziada.Ambao tunaweza kuutumia kuzalisha pesa na kuliinuwa bara letu.Tafiti nyingi zimekuwa zikitubeza kwamba afrika tunaongoza kwakuwa naufikiliaji mdogo, kama ufikiliaji mdogo mbona kunawatu afrika wanabuni vitu vikubwa[tuna paswa kuwa na mawazo chanya katika kila tunachokifanya].

    Nisiku ya jumamosi noeli akiwa njaa hajui atafanya nini pesa alizokuwa nazo zilikuwa zimekwisha alifikilisha sana akili yake.Akikumbuka wenzake wako chuoni wameanza masomo yao ya juu huzuni ndio ilizidi zaidi.Ahadi yakwenda nje kusoma ilikuwa ikishugulikiwa lakini kwakijana noeli kwa muda huwo aliona kama ameaidiwa ahadi feki tumaini katika ahadi hiyo likawa lime toweka. ‘’dah! Maisha gani haya’’ alisema noeli hukuakiwa ameshika kichwa chake nakukitikisa mno, aliona ukata ulikuwa ukiendelea kama ilivyokuwa mwanzoni kipindi akiwaza hayo alikuwa amekaa ndani na mama yake alikuwa ameenda kuchota maji ya kwenda kupikia pombe bombani.Pesa katika simu yake ilikuwa haipo alitamani angeweza kumpigia Yule pastormzungu na kuongea nae, amuombe msaada angalau maana hali aliyokuwa nayo ilikuwa inatisha ‘’leo hata nauli sina!’’ alikuwa akiongea mwenyewe chumbani kwake kijana noeli huku, siku hiyo alikuwa na kipindi redioni, na ilikuwa ni razima aweze kufika redioni hari ya kulipwa ujira wake ilikuwa kama vile zamani alikuwa halipwi kama ilivyokuwa zamani.Kalibia kila kitu alikuwa akiji tutumuwa noeli mwenyewe.Alikuwa akifikilia na akagunduwa muda nao ukizidi kuyoyoma, noeli ana amuuwa kuvaa nguo zake na kuondoka ‘’ itajulikana mbele ya safari’’ alijisemea mwenyewe kisha akatoka ndani na mwendo wa mawazo kutawala katika moyo wake ukizidi kushamili zaidi.Umasikini sio kitu chema noeli alijikuta kuwaza mpaka kufikia hatuwa ya kumkufulu mwenyezi mungu pasipo yeye kujuwa.Punde si punde noeli aliingia balabarani akitembea kwamiguu, katika kutembea noeli alikutana na kijana mmoja noeli ana amuwa kumwambia shida ambayo aliyokuwa nayo. ‘’’samahani ndugu’’ alisema noeli kwaustalaabu, ‘’bila samahani nakusikiliza’’ alisema Yule kijana aliye simamishwa na noeli ‘’naomba nisaidie nauli’’ aliongea noeli japoilikuwa kwa kujikaza sana maana alikuwa hakuzoea kuomba mtu.yule kijana alimwangalia sana noeli na kumnyari kisha ana mwambia, ‘’mimi sina hela’’ noeli aliamuwa kumjibu na kumwambia, ‘’asante’’ lakini alikuwa amechukia na kujishusha sana hasa pale alipoona Yule kijana amemnyari waziwazi na kujuwa.Msongo wa mawazo ulizidi maana aliwaza mno juwa lili waka lote na kumuishia, kichwa kilianza kumuuma kutokana na mchanganyiko wa mawazo pamoja na juwa kumuwakia kari na kumuishia mwilini. ‘’leo nitafikaje studioni?’’ bado ilikuwa kitendawili kikubwa sana kwa noeli kuweza kufikilia namna ya kufika studioni.Akiwa amekaa katika nguzo ya umeme wazo lingine likamjia ‘’muda mwingine aibuweka pembeni omba nauli kwa mtu yoyote uwende studioni’’ likawa limeweza kumjia wazo kama hilo.Alipofika kituoni aliishia kuwaona wengine ambao waliokuwa wakipanda daradala kwasababu walikuwa na nauli zao. ‘’pasiasi ilemela………. Pasiasi ilemela’’ alitowa sauti yake kwanguvu konda pamoja na mpiga debe wake.Akiwa amesimama kalibu na noeli alitamani kumwambia konda kuwa hana nauli lakini kutokana na konda alivyokuwa kwanza amekaa kikatili sura yake ikiwa imemjaa jereha nyingi usoni noeli aliogopa kumwambia.



    .Aliamini makondakta wengi huwa na tabia sawa mtazamo ambao ulikuwa chanya alishindwa kujuwa sio wote wana tabia sawa au mienendo sawasawa, wakati akiwa amesimama noeli nakushindwa kumuelezea kondakta ukweli wake konda alimuuliza ‘’vipi dogo?” noeli nae alimjibu, ‘’safi’’ hukuakiwa na wasiwasi na uwoga mwingi, ‘’panda twende bwana’’ alisema kondakta noelialishangaa kisha akaguna, ‘’mmmm’’ napatwa na kigugumizi konda aliingiwa na wasiwasi na kuhisi noeli uwenda hana nauli na anashindwa kusema.Kondakta alimwambia ‘’kama huna nauli sema nikupe msaada’’ alipokwisha kusema hivyo noeli alimwambia, ‘’nikweli brother’’ kondakta alimruhusu kupanda noeli aliingia kwenye gari na kukaa.Tunapaswa kuwa namitazamo chanya hata katika makundi flani ya watu,wakiwa ndani ya daradala mmjadala ukaibuka ‘’masikini atakuwa masikini tu’’ alisema mama mmojamnene aliyekuwa amekaa karibu na alipokuwa noeli. ‘’apana mungu huwa nyanyuwa wanyonge’’ aliongea kijana mmoja ambae alikuwa akiwa ni muhamasishaji mkubwa wa vijana katika maendeleo, wakati wakibishana mala noeli nayeye akawa akitaka kuchangia naakaipiata ile nafasi ya kuweza kuongea, ‘’mchawi wa mtu ni mtu mwenyewe http://deusdeditmahunda.blogspot.com/unavyosema……. Ndivyo itakavyokuwa’’ alisema noeli na watu walikaa kimya kuweza kumsikiliza na mala nyingi maneno ya noeli yalitawaliwa na khekima na busara isiyokuwa na kifani.Lakini pia noeli alikuwa na [high influencing power] katika kila alichokuwa akiongea au akifanya basi ni razima angepata mtu au kundiflani la watu ambao wange msapotia. ‘’lakini huyu kijana ameongea ukweli’’ alimuunga mkono mzee mmoja kauli ambayo aliisema noeli, baba huyo alikuwa amekaa siti ya nyuma. Noeli punde si punde aliweza kushuka katika kituo ambacho alikuwa anatakiwa kushuka, aliweza kushuka nakuelekea studio nakuacha kwenye iledaradala mabishano yakiendelea.Kule studio siku hiyo kulikuwa na mkanganyiko usiokuwa wakawaida kulikuwa na vifaa ambavyoviliibiwa na aliyeiba alikua hajulikani.Kili ibiwa mpaka kifaa muhimu kwakurushia na kurekodia matangazo.Mkurugenzi alikuwa ameteuwa majina ya watu aweze kuwaondowa kazini kutokana na wizi huo kutukia.

    ***





    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog