IMEANDIKWA NA : RAMAAH MZAHAM
*********************************************************************************
Simulizi : Msamaha Bila Malipo (Forgiveness Without Payment)
Sehemu Ya Kwanza (1)
Ni muda wa saa mbili usiku Sophia ambae ana uchu wa maisha akiwa katika dimbwi la mawazo anangalia pembeni na kuwaona wadogo zake wakilia kutokana na njaa waliyonayo baada ya siku hiyo kuwa ngumu kwao baada ya kukosa chakula kwa siku nzima. Kumuangalia Mama yao hali ni ileile maana tayari maisha kwa upande wake yalikua yashampiga na kumfanya Sophia kuanza kuwaza na kujisemea moyoni “ningefaulu kwenda kidato cha tano ningekuja kuwasaidia wadogo zangu,lakini kidato cha tano sio kitu.natakiwa kuwa walau na kibarua,”. Alijiuliza Sophia kichwani mwake. Akimtazama Mama yake ndio anatia unyonge sana na ndipo anapochanganyikiwa na zaidi yeye ndie mtoto mkubwa pale nyumbani na mdogo wake anayefuata alikuwa kidato cha pili na alipokuwa kidato cha kwanza mdogo wake alifanikiwa kupata mfadhili wa kumsaidia katika masomo yake na alikuwa akiishi hukohuko kwa mfadhili ila alikuwa akienda kuisalimia familia yake kila siku za mwisho wa wiki kwani alikua na mapenzi ya dhati kwa ndugu zake pamoja na Mama yake mzazi. Mdogo wake na Sophia hakubahatika kumuona Baba yake mzazi kwani alifariki muda wakati Sophia yupo kidato cha pili.Baada ya kuwaza kwa muda mrefu ndipo Sophia akaamua kwenda chumbani kwa Mama yake ambapo walikuwa wakitunzia vyombo na vitu vingine mbalimbali. Kwa huruma aliyokuwa nayo Sophia aliamua kuchukua maji na kuchemsha chai kwa ajili ya Mama yake na mdogo wake wa mwisho angalau kuwasitiri na njaa waliyokuwa nayo. “Mama Mama…” aliita Sophia Kwa sauti ya upole na unyonge . “Unajua Sophia acha kunisumbua nina njaa au mwenzetu umekula, mbona sikuelewi? Alisema Mama Sophia huku akiwa hajui kama Sophia amewaandalia chai yeye na mdogo wake wa mwisho na wakati huo Sophia alikuwa nyuma ya mgongo wa Mama yake na vikombe viwili vilivyokuwa na chai. Sophia akagundua kuwa Mama yake hajaona kuwa amebeba nini.Kisha akazunguka na kwenda mbele kumpa Mama yake kikombe cha chai. “Sasa Sophia mwanangu chai tu! Ila ngoja tunywe hivyo hivyo. Ila kuna sukari kweli”? Aliuliza mama Sophia huku akiwa na furaha usoni mwake. Sophia akamjibu kuwa hakuna sukari ila ameona bora awachemshie chai hivyo hivyo ilimradi wapashe tumbo japo kidogo.
Kutokana na huruma aliyonayo Sophia aliona bola awape kwanza chai mama yake na mdogo wake kwani aliona wao ndio wanaoumia zaidi kuliko yeye. “Ila mwanangu una huruma sana na upendo wa dhati,sijui kwa nini Mungu hakuoni au kukufikiria”, alisema Mama Sophia huku akiwa anakunywa chai isiyokuwa na sukari.
Sophia alianza kumuangalia Mama yake kwa umakini kutokana na kauli aliyoisema mama yake kisha akamwambia kwa uzuni huku machozi yakimlengalenga machoni. “Mama usijali naamini ipo siku Mungu atanifikiria”, alisema Sophia ambae alikuwa anatoa machozi kwa uchungu sana. Wakati huo Mama yake Sophia alikuwa akiendelea kunywa chai bila hofu ata pale mwanae alipodondosha chozi yeye alichukulia ni jambo la kawaida kwa upande wake haswa ukizingatia Mama huyo alikua na matatizo ya akili. Alipomaliza kunywa chai, Mama yake Sophia aliingia chumbani mwake kupumzika akiwa na mwanae wa mwisho ambae ni mdogo wa Sophia.Sophia alibaki pekee yake sebuleni huku akiwaza sana juu ya mstakabali wa maisha yake. Baada ya kuwaza kwa muda mrefu Sophia akaenda chumbani kwao na kuchukua cheti chake cha kidato cha nne,na kasha akakitazama sana hali liyopelekea machozi kuanza kumtoka kwa mara ya pili mithili ya maporomoko ya maji.Katika kuwaza kwake sana ndipo akili yake ikarudi shule kwa jinsi alivyokua anasoma na kupelekea kuwakumbuka baadhi ya marafiki zake kwa jinsi walivyokuwa wakiishi wakati wakiwa shuleni.”Haki ya Mungu nitapambana kwa hali na mali ili niendelee na masomo, sikubali kuishia hapa”, alisema Sophia kwa sauti ya chini. Kisha akakirudisha cheti chake sandukuni kwani alikua akikitunza humo kwa uangalifu mkubwa licha ya kuwa hakina matokeo mazuri.
Mdogo wake Sophia ambae anaishi kwa kufadhiliwa akiwa kule kwa mfadhili wake alikua akiwaza sana juu ya kwao kwani alikuwa amepakumbuka sana nyumbani kwao haswa Mama yake na mdogo wao wa mwisho. Hii inakuja baada ya kuwa na wiki tatu za mtihani zilizopelekea yeye kushindwa kufika kuwaona sababu ya mitihani hiyo. Mfadhili wake anagundua hali aliyonayo Edward na kumuuliza, mbona hauna raha kipi kinakusumbua labda? Edward kwa kuwa ni mtoto wa kiume aliamua kukaa kimya bila ya kuonyesha kwamba hawazi chochote. Edward alinyamaza kisha mfadhili wake akaingia ndani kwa mkewe maana mkewe ndie alikuwa karibu sana na Edward na kufahamu udhaifu wake . Yule bwana baada ya kufika kwa mkewe akamuuliza “hivi huyu mtoto leo amekuwaje mke wangu mbona hana raha”. alisema yule bwana akiwa na yeye ana mambo mengi kichwani baada ya kuongea hivyo aliamua kwenda chumbani kutuliza akili kidogo. Mkewe nae aliendelea na kazi zake kule jikoni. Edward aliamua kwenda kulala kwani mawazo ya kwenda nyumbani yalizidi sana hivyo akaamua kupumzisha mawazo kwa usingizi.
Nyumbani kwa kina Sophia walikuwa wakilala kwa shida sana na wakiwa wamelala usiku huo Sophia anaamka mida ya saa tisa usiku akiwa katika dimbwi la mawazo kuwa kesho ataenda wapi angalau apate kibarua chochote cha kufanya ili aweze kukidhi mahitaji yake na nyumbani kwao. Lakini ghafla anapata wazo la kwenda katika kampuni moja ambayo inajiusisha na kutoa video za wasanii wa kitanzania katika tasnia mbalimbali. Kampuni hiyo inajulikana kwa jina la Home advertising ambayo ipo Mwanza katika jengo la PPF Plaza.
Hofu inamtoka Sophia baada ya kukumbuka kuwa aliwai kuambiwa na rafiki yake Anna kuwa kampuni hiyo pia uchukua watu ambao kiwango chao cha elimu sio kikubwa. Baada ya kuvuta kumbukumbu hiyo, Sophia ana pata moyo na hamasa kubwa na kujisemea moyoni “kesho nitakwenda kuomba kazi na hata kama nikipata bado ndoto yangu ya kuendelea na elimu ipo pale pale”. Alijisemea moyoni huku akikunja ngumi mkono mmoja na kupiga kiganjani kwa uchungu na kurudi kitandani kulala na kuchukuliwa na usingizi mzito kama wa pono. Ndoto ikamjia “sikiliza Sophia, amini utakuja kuwa na maisha mazuri kuliko hata ya mwanaume” ilitoka sauti tu ndotoni wala si sura ya mtu. Sauti hiyo haikujulikana ni ya nani na kisha ikatoweka. Sophia akiwa ndotoni anaanza kuangazaangaza lakini haoni mtu anajiuliza maswali mengi sana kisha ndoto inaisha. Masaa yanazidi kwenda. Asubuhi nayo ikawa inagonga hodi.
Upande wa pili Edward alikuwa amelala sana na kusahau kama kuna shule siku hiyo. Mke wa yule mfadhili akaenda kumuamsha,lakini kutokana na uchovu aliokuwa nao , Edward akaamua mwambia “ Aunt dah! leo shule hatuendi mimi narudi kulala, bado nina usingizi”. “Yaani wewe mtoto huwa unasumbua sana wakati wa kwenda shule. Chakushangaza sasa wikiendi unawai kweli kuamka sijui kwanini” Alisema aunt yake Edward ambaye ni mke wa mfadhili wa Edward. Baada ya kuongea maneno hayo Aunt akatoka chumbani kwa Edward na kurudi kufanya kazi zake za ndani, huku Edward akijiandaa kwenda shuleni.
Siku iliyofuata Mama Sophia aliamka mapema sana lakini kichwani mwake alikua ameamka na wazo jipya ambapo kwa upande wake aliona ni jambo zuri hivyo ni vyema amshirikishe mwanae . “Sophia mwanangu” Sophia akaitika kwa sauti ya chini kabisa “Abee Mama” Kisha Mama Sophia anaanza kumwambia Sophia ya moyoni mwake, “mwanangu naona leo niende mjini angalau nikakae barabarani ili nikaombe msaada kwa wapita njia kwani hapa nyumbani ndio hivyo mambo magumu na hali inazidi kuwa mbaya”.alisema Mama Sophia huku akikaa kimya kumsikilizia Sophia atasema nini juu ya jambo hilo. Wazo hilo halikumungia Sophia kichwani hata kidogo na akamwambia Mama yake kuwa kufanya hivyo ni kujizalilisha na bora waendelee kuvumilia hali waliyonayo na sio kwenda kukaa barabarani na kuomba. Mama Sophia baada ya kusikia kuwa mwanae yuko kinyume naye anaamua kumgombeza. “ujue nakushangaa sana wewe,pesa hapa nyumbani hakuna na wewe unaleta maswala ya kuona aibu,mimi niache nitaenda na huwezi kubadilisha maamuzi yangu”,alisema Mama Sophia huku akimchukua mwanae mdogo na kwenda nae kuomba huko mjini. Mama Sophia akaenda mjini kutimiza lengo lake la kuwa ombaomba.Baada ya Mama yake kuamua kuchukua maamuzi hayo,Sophia anaenda ndani na kuchukua cheti chake na kisha kujiweka katika hali ya usafi ilikuficha shida zake maana watu wengi mjini huonekana kuwa wasafi ata kama wana shida nyingi na kwa jinsi walivyopendeza uwezi kuamini kama hawana kitu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kujiweka katika hali ya usafi Sophia anabeba cheti chake na kuamua kwenda kwenye ile kampuni kwa lengo la kuomba kazi ili aweze kujikomboa kimaisha.Licha ya shida alizonazo,Sophia kwa namna nyingine alikua ameumbika kwa kweli na alijaliwa kuwa na umbo zuri ambalo lilimvutia mwanaume yoyote rijari pindi anapokutana na binti huyo ambae alikuwa hatumii vipodozi lakini ukimuona kwa kweli mtoto alikua analipa.
Edward kule kwa mfadhili wake baada ya kumaliza kujiandaa kwa safari ya kwenda shule anapewa pesa ya matumizi na Aunt yake ambae ni mke wa yule mfadhili.Mke wa mfadhili alikua na mapenzi ya dhati kwa Edward kwani alimchukulia kama mwanae na hii inakuja baada ya yeye na mume wake kukosa mtoto katika ndoa yao baada ya kuwa na matatizo ya uzazi yeye na mumewe. Baada ya kupewa pesa Edward anatoka nduki mpaka shuleni kwenda kuwahi masomo yake. Siku hiyo aliamka akiwa amechelewa sana.
Nyumbani kwa kina Sophia palikua kimya sana siku hiyo kwani hapakuwa na mtu yeyote. Mlango ulikuwa umefungwa na kufuli dogo ambalo mtu akipushi kidogo tu lazima kitasa kiachie na kufuli kwenda zake. Bwana afya wa mtaa wao alikuwa amewatembelea pale nyumbani kwao kina Sophia kuangalia mazingira kama yako safi na kuona kama pana choo maana alipata habari kutoka kwa majirani zao kuwa hawana choo. Bwana afya alikagua maeneo yote na akagundua kuwa kuna choo tena kisafi kabisa. Bwana afya akagundua hizo zilikuwa ni chuki tu zawatu. Kisha kwa utaratibu akaondoka kuendelea na kazi zake kwa siku hiyo.
I
likuwa ni mida ya saa tano asubuhi, Sophia alikuwa ameshafika katika ofisi za Kampuni ya Home Advertising na sehemu ya mapokezi anakutana na Binti mwenzie ambae kiumri ni kama wanalingana vile. Sophia anasalimiana na yule binti kisha anamueleza shida ya yeye kuwa pale ofisini na ndipo yule binti anamuelekeza mahali wahusika wakuu wa Kampuni ile walipo ili aende kuongea nao vizuri kuhusu shida yake. Baada ya kuonyeshwa walipo wahusika wakuu, Sophia anaingia kwa heshima na kuwakuta kina kaka wawili wakiendelea na kazi zao mle ndani. “Karibu dada, karibu sana” alikaribishwa kwa furaha kubwa sana na mmoja kati ya wale kina kaka.Mwingine akamwambia “Dada acha uoga naona kama unatuogopa” Alisema kaka huyo huku akiondoka mle ofisini. Baada ya yule mmoja kuondoka,mle ofisini wakabaki Sophia na Kaka mmoja ambae ndie mmiliki wa Kampuni ile.Kaka huyu jina lake ni Baraka . “Dada sijui unaitwa nani?” aliuliza Baraka kwa sura yenye huruma na Sophia akajibu kwa kusema anaitwa Sophia Evance. Baraka nae hakuwa nyuma kujitambulisha na kusema yeye ni nani na ana cheo gani pale ofisini katika Kampuni hiyo. Baada ya kufahamiana, Baraka alitaka kujua Sophia ana shida gani haswa ndipo Sophia akamwambia shida ya yeye kuwa katika ofisi zile kwa muda ule ni kutaka kazi. Baraka alitaka kujua kiwango cha elimu alichonacho Sophia na ndipo Sophia akaweka wazi na kumwambia ukweli kuwa elimu yake ni Kidato cha Nne huku matokeo yakiwa sio mazuri. Baraka akatikisa kichwa na kusema,daraja hilo sio baya kwani wao wamekua wakiwachukua watu wenye kiwango hicho cha elimu katika Kampuni yao.Baraka akamwambia kazi umepata. “ Eee Mungu mkubwa ata siamini kaka yangu”? Aliuliza kwa furaha mpaka akanyanyuka kwenye kiti alichokuwa amekalia. Wakati yote yakiendelea hayo, Baraka alikua akimuangalia sana haswa upande wake wa nyuma ambako alikua amefungasha makalio ya kutosha yenye kumtoa mwanaume rijali udenda ata kama nyumbani ana mke . “Huyu Binti mbona mzuri sana,kazi atapata ila lazima nilale nae,siwezi kumuacha mtoto kama huyu utakua uzembe”, Aliwaza Baraka kichwani mwake na kisha akamwambia Sophia kama anataka kazi basi lazima afate masharti yake na mambo atakayotaka Baraka. Sophia akasema kuwa yuko tayari kwa masharti hayo. Baraka akatulia kidogo kisha akamwambia “unaju kuwa wewe ni Binti mzuri sana na itakua sio vyema kwa wewe kukosa kazi ila ninachotaka kutoka kwako ni kufanya mapenzi na wewe kwanza ndipo masuala ya kazi yatafuata,alisema Baraka huku akimchezea Sophia sehemu za vidole vyake vya mikononi. Ghafla Sophia akatoa mikono yake kisha akabaki kumuangalia Baraka usoni. Baraka akakasirika mno kuona Sophia katoa mkono wake kwenye mikono yake, kisha anamwambia,” Sawa kwa hiyo hutaki sio, nenda basi na kama unataka kazi kwenye hii kampuni bila ya kufuata masharti yangu basi hakuna kazi,nenda dada kama kazi tu hapa zipo kibao” alisema Baraka huku akiwa anamuangalia Sophia kwa jicho la uchu wa mapenzi. Sophia anaamua kuondoka akifikiria sana kauli ya Baraka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande wa pili Mama Sophia alikuwa akiendelea na zoezi lake la kuombaomba na wakati huo alikua na zaidi ya shilingi elfu kumi za kitanzania mkononi mwake kitu ambacho ata yeye alikuwa ajaamini jambo hilo. Ilikuwa wakati wa asubuhi tu ambapo Mama Sophia na mwanae mdogo walikua wakihesabu pesa walizokushanya huku akijisemea, “elfu kumi dah! Kumbe kazi inalipa,Elfu kumi sasa hivi tu alisema mama Sophia huku akiwa ameshikilia noti mkononi za mia tano mia tano. Mama Sophia kwa uelewa wake na matamanio aliyokuwa nayo aliona kazi hiyo ndio inamfaa na kuona kitendo cha Sophia hapo awali kumkataza asifanye hivyo ni kama upuuzi na kumuona mwanae hana lolote la maana. Baada ya kumaliza kuhesabu pesa zake alizokuwanazo ana amua kurudi barabarani tena kuomba akiwa na dhamira ya kuongeza nyingine zaidi ya hiyo aliyokuwa nayo mkononi mwake. Mdogo wake Sophia alianza kulia njaa maana ni siku ya pili sasa ajatia kitu tumboni, Mama Sophia anaamua kwenda kumnunulia chai kwenye vibanda vya kina Mama ntilie ili mwanae atulize njaa “ Ebu nipe chai na vitumbua viwili sawa”? Alisema Mama Sophia huku akiwa na haraka ya kwenda kuendelea kuomba kule barabarani ambako kulikuwa na watu wengi sana wenye huruma na wasiokuwa na huruma pia nao walikuwepo. Dah! Mama Sophia alifanya haraka kama anataka kusafiri vile. Muhudumu ambae alikuwa ndio Mama ntilie aliharakisha sana lakini mama Sophia aliona kama anachelewa kisha akamwambia, “Bwana si uharakishe wengine tuna kazi zetu eti”, alisema mama Sophia akimpiga mkwara mzito yule mama ntilie huku akitikisa miguu midhili ya bosi, kumbuka Mama Sophia akili zake huwa haziko vizuri wakati mwingine.
Nyumbani kwa kina Sophia alikuwepo Sophia peke yake akiwaza juu ya yale aliyokutana nayo ofisini kwa Kijana Baraka juu ya kutoa mwili wake ili apatiwe ajira au kugoma kutoa mwili wake na kuendelea kubaki katika hali aliyonayo ya kutokuwa na ajira(Unemployment).Alikuwa amekaa pembeni ya mlango wa nyumba yao huku cheti chake kikiwa pembeni yake na kichwani mwake akiwa na mawazo mawili mawili juu ya jambo alililokutana nalo kwa Kijana Baraka. Kuna upande kilimwambia akubaliane na jambo lile na upande mwingine kilimwambia asifanye jambo kama hilo,kwa kweli alikua katika hali ngumu na njia panda juu ya jambo hilo. Sophia akawa amechoka kiakili na kimwili mpaka jinsi ya kuwaza.Siku zote waswahili wanasema ni bora kuchoka mwili kuliko akili maana akili ndio kila kitu haswa katika maamuzi.Sophia akawa amepigwa na butwaa pale mlangoni asijue la kufanya na kujisemea moyoni”haiwezekani kwani ofisi ipo moja hapa duniani,nitakwenda kutafuta mahali pengine”,alijisemea Sophia. Maisha ya Sophia yalikuwa ni magumu sana kwa wakati huo. Mama yake Sophia baada ya kumaliza kumpatia mwanae mdogo chai anaamua kurudi tena barabarani kuendelea na shughuli yake ya kuomba msaada toka kwa wapiti njia.Na mara hii ndio bahati ilikua kwake zaidi maana idadi ya watu waliomchangia pesa ilizidi kuongezeka na kwa muda mfupi alijikuta akiwa na shilingi elfu 30 mikononi mwake jambo ambalo lilikuwa kama ndoto kwa Mama Sophia. Baada ya kupata pesa hizo, Mama Sophia aliona kama zinatosha hivyo anaamua kumbeba mwanae mgongoni na kurudi zao nyumbani. Ingawa bado alikua hajakula lakini aliona kama ameshiba vile kutokana na kushika elfu thelathini haraka haraka bila ya kuitolea jasho kubwa. Sophia kule nyumbani njaa ilimuuma mpaka akaamua kwenda kwa jirani yao kuomba unga japo kidogo ili apate kupika ata kijiugali ili kuweza kupoza njaa “ hodi… hodi.. Mama” aligonga kwa sauti ya chini kule ndani hawakusikia , Sophia aliendelea kugonga uku akipandisha sauti yake kidogo kidogo na kupelekea Mama mwenye nyumba kusikia kama nje kuna mtu anagonga bila ya kujua ni nani anae gonga muda ule wa mchana. Alinyanyuka kwa haraka sana akijua labda ni mgeni wao wa maana na yawezekana amekuja na jambo la msingi,lakini kufungua akakuta ni Sophia na ndipo Mama yule akasonya kwa dharau na kumtemea mate Sophia na kumuuliza,” kwani una shida gani wewe masikini mkubwa”, alisema yule Mama huku akimuangalia Sophia kwa dharau. Sophia akamueleza shida yake kuwa ni unga ili apate kupika japo kajiugali apate kula maana njaa ilikua imemkabili sana na hakuwa na chochote cha kuweza kupika kwa wakati huo.Yule Mama alimtazama Sophia kwa nyodo kwa mara nyingine na kisha kumuita Binti yake Modesta na baada ya kuja akamwambia kwa sauti ya chini ili walioko ndani wasijue kinachoendelea kuwa huyu Binti anashida na unga,je tumpatie au atazoea na kuja mara kwa mara. Wakati Mama Modesta na mwanae wakiongea juu ya suala la kutoa unga au la,ghafla Baba Modesta anarejea na kumkuta Sophia akiwa nyumbani kwake. Baba Modesta anamuangalia kwa jicho kali sana na kutamani ata kumrukiaSophia usoni.” We binti hapo mlangoni kwangu unafanya nini kwani huna kwenu”?, aliuliza kwa kufoka mno hadi Sophia akaogopa na kuwa kama amenyeshewa na mvua ya mawe, au kama wale mbwa koko waonapo watu na kushusha mikia yao chini. Ndivyo alivyokuwa Sophia na kisha akatoka kabisa pale mlangoni na kusogea mbali sana, kisha Baba Modesta akaanza kumtukana Sophia na kumwambia umasikini ameusababisha mwenyewe haswa baada ya kushindwa kufaulu mtihani wa kidato cha nne. Sophia hakumjibu kitu chochote http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Baba Modesta. Kipindi mama Modesta yuko ndani akawa tayari amesikia sauti ya Baba Modesta na akakumbuka kuwa mumewe alishakataa kutoa kitu ndani kumpa mtu yeyote pale mtaani. Baba Modesta alikuwa ni mtu mwenye roho mbaya sana na mkatili kupita kiasi. Huruma na yeye walikua ni maji na moto, Mama Modesta baada ya kumuona mwanae anakuja na unga akamrudisha nao mikononi. “Rudisha, rudisha Baba yako yuko hapo nje” alisema Mama Modesta huku akiwa anaangalia dirishani kwa umakini, huku kule nje Baba Modesta akawa anamuuliza maswali mengi Sophia kanakwamba hamjui au ndio kamuona kwa mara ya kwanza pale nyumbani. “Kwani ulikuwa na shida gani hapa nyumbani”, alimuuliza Sophia, Sophia akamuangalia kwa uwoga hakutaka kumjibu, mwili ukawa unatetemeka sana.
” Hivi nakuuliza hutaki kunijibu eti nitakuzabua vibao pumbavu”,Baba Modesta alipayuka kwa hasira, na baada Sophia kuona Baba Modesta kapaniki aliamua kuondoka huku njaa ikizidi kushika hatamu yake tumboni na kurudi nyumbani kwao ambako hakuna kitu. Punde si punde mara Mama Sophia akawa ameshafika nyumbani akiwa na furaha sana kwenye paji la uso wake, Sophia akawa hata ameshindwa kuongea kutokana na ukali wa njaa aliyokuwa nayo. “Sophia mwanangu fuata mkaa na mboga, mimi naenda kusaga debe la unga sasa hivi” alisema mama Sophia akiwa anaingia ndani hapo Sophia alitabasamu kwa mbali sana akijua neema imeingia ndani kwao, huku Mama yake akitoka nje na kumuonyesha Sophia pesa alizopata huko kwenye shughuli yake ya kuombaomba. Sophia hakuamini kabisa na kumwambia Mama yake aongeze bidii katika kazi hiyo,ndipo Mama yake akisema, “ si nilikwambia twende ukanidharau sasa hivi hakuna kulala na njaa”, alijinadi Mama Sophia kwa mwanae huku akichukua ndoo yake na kwenda kupima mahindi na kwenda kusaga., Sophia nae alichukua mifuko miwili ya lambo,mmoja wa mboga na mwingine kuchukulia mkaa. Sophia kipindi anataka kuondoka akakumbuka na kumwambia Mama yake yaani mama kumbe tunaishi na ngulu mbili ngoja nikirudi nitakwambia” alisema Sophia kwa hisia kali na huzuni. Mama yake kwa kuwa alikuwa na haraka alimwambia, sawa hiyo baadae utaniambia tufanye kwanza haya sawa mama angu? Alisema Mama Sophia kwa upendo kisha wakatawanyika wote kwenda kwenye hiyo mipango yao waliyokuwa wamepangiana dakika chache zilizopita. Mama Sophia yeye alielekea mashine na Sophia alielekea sokoni kufanya manunuzi ya mboga na mkaa kama walivyokuwa wamepanga. Kila mtu aliondoka kwa haraka kama anafukuzwa na mtu ili waje kupika mapema kula vizuri siku hiyo.
SURA YA TATU
B
aada ya Sophia kumaliza kula chakula na njaa kuisha anaamua kumwambia mama yake ukweli wa mambo. “mama kumbe baba Modesta ana roho mbaya sana” alisema Sophia baada ya kuwa tumbo liko ndii. Mama Sophia akaanza kumwambia kuwa kwani ulikuwa hamjui baba Modesta kuwa ni mtu ambae ana roho ya mbwa mwitu. Kisha mama Sophia akamwambia mwanae kwani ni ulienda kwa mama Modesta. Sophia akajibu kuwa njaa ilikuwa imemuuma mpaka basi. Akaamua kwenda kuomba unga kidogo. Mama Sophia bado hakumwelewa mwanae kwani aliendelea kumuuliza kwa nini aende kuomba unga wakati yeye alikuwa anakuja kununua. Sophia aliendelea kumwambia yeye alikuwa hajui hilo kabisa kwamba atakuja na unga nyumbani. Mama alimwambia mwanae kuwa hampendi sana baba Modesta. Sophia aliguna sana kwa sababu tu ya kumshangaa baba modesta na roho yake mbaya kiasi hicho. Wakati wakimsema baba Modesta, huko kwake alikuwa akiwagombeza mke na mtoto wake. ‘Mimi nawashangaa sana na roho zenu za kanisani wakati wenzenu tunahangaika sana” alisema baba modesta kwa roho na sura ya ukali. Kwa mama modesta na modesta kutoa tu unga mama modesta baada ya kuona mume wake amezidi ukali aliamua kuwa mpole na kuanza kujitetea. “Mume wangu, sisi tumeshangaa yuko mlangoni, tunalifukuza wapi haliondoki yani jamani watu mengine bwana” alisema kwa unafiki mama Modesta ili mumewe asijue kama kweli alitaka kumpa unga hivyo akaamua kujisafisha kwa mmewe. Na kwanini msilitupie hata mawe huko? Alisema kwa sura ya ukatili. Mama Modesta akamkatiza mumewe “mume wangu achana naye huyo bwana na ikitokea akaja tena ataishia kulee” alisema mama Modesta ili kumaliza maongezi yale. Kwa hilo alifanikiwa maana mumewe alinyamaza kabisa hakuongea tena kitu chochote kutoka mdomoni kwake
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kule kwao Sophia mama Sophia anamuonya sana mwanae kwenda kuomba kitu chochote katika mji huo hata kama atakuwa na shida kiasi gani. Sophia naye hakuacha kuyaishi yale aliyoambiwa na mama yake. Mama Sophia alimkataza mwanae kwa sababu za msingi zaidi. Baaada ya kuongea mengi sana kuhusu baba modesta sasa mama Sophia anaamua kwenda kulala ili kesho aende kuomba asubuhi na mapema. Sophia nae aliwahi kulala ili kesho ajue anaanzia wapi. Kulekule kwa bwana Baraka au aende kwingine ambako hawatomuomba unyumba kama ilivyo kuwa kwa Baraka. Lakini hadi anaenda kulala alikuwa hajapata muafaka ikiwa ataenda kwa Baraka ama kwingine. Sophia siku hii analala akiwaza sana juu ya alicho ambiwa na Baraka na anawaza sijui akubali ama atafute kwingine. Sophia akaamua kufunguka kimawazo nakuona ni bora kukuche aende kwa rafiki yake Viviane ili aombe ushauri maana alikuwa kawaza mpaka kuwazua. Sophia binti ambae hakati tamaa mapema, zaidi aliendelea kuuchapa usingizi usiku huo. Wakati binti Sophia akienda kulala aliota njozi ambazo ni imara na nzuri zaidi. Baraka kule nyumbani alikuwa anaishi na jirani zake na vijana wenzie wengi tu maana alikuwa hajaoa na wala hakutegemea kuoa wakati huo, hivyo alikuwa anaishi na baadhi ya jirani zake pamoja na baadhi ya vijana wenzake wenye mazingira ambayo kidogo hayako sawa kwa roho nzuri tu Baraka alikuwa nayo ila pepo wa ngono tu ndio alimsumbua. Baraka muda huu anatumia kuongea na wale vijana wenzie pale ndani uku wakiangalia Televisheni. “Bwana ee dah! Kuna binti ni mzuri ile mbaya kaja pale ofisini laiti akinikubali niutumie uzuri wake basi kazi amepata” alisema Baraka huku akibadili badili chaneli za television. Baada ya Baraka kuongea hivyo Tumaini ambae alikuwa ni mmoja kati ya vijana ambao Baraka anaishi nao aliongea akisapoti uchafu na ujinga ambao Baraka aliongea pale mbele yao. “ aaaah wewe tena Baraka mzee wa kuwachakachua, chakachua kwanza” baada ya Tumaini kuongea hivyo Baraka akapatwa na wazimu kabisa na kudai lazima kama Sophia atataka kazi akubali kuvua nguo maana ukikubali kuolewa ukubali kulala uchi pia. Ndio kauli inayotumika maofisi mengi sana ambayo yamejawa na vijana wadogowadogo ambao ni wasomi. Baada yakuongea hayo bwana Baraka akaanza kuwapa sifa za maumbile ya binti Sophia ili kutaka waone ni mzuri kiasi gani na ni namna gani anamtaka kimapenzi binti Sophia na amesema kesho ataleta barua ili nimsainie mpaka anikubalie umeona raha ya kuwa bosi Tumaini, unafaidi vyote vizuri tu” alisema Baraka kwa kujinadi mbele ya kadamnasi uliyokuwa pale ndani “ hayo ndio mambo matamu na mazuri ukiwa bosi we kesho mmbane sana mpaka akubali” alisema Tumaini ambae alikuwa na akili sawa na tabia sawa na Baraka ya kutamani kuchezea mabinti kwa kutumia nyazifa zao. Baada ya kupewa kichwa Baraka anagangamala kuwa siku inayofuata lazima Sophia amkubali kimapenzi. Moja kati ya changamoto ambazo akina mama na akina dada wazuri wanazokutana nazo kutoa hongo ya ngono au rushwa ya kimapenzi katika suala zima la utafutaji ajira. Vijana wengi sana leo wamekuwa wakipambana na kuhangaika bora ilimradi tu wapate kufaulu kupata mabinti kwa urahisi zaidi. Ndio maana wapo vijana wanadhani ya kuwa umaarufu ili kuibuwa mabinti kwa ulahisi. Ndio maana kuna vikundi vya uigizaji ambavyo vingine viko kwa ajili ya kupatiana wapenzi tu si kwa ajili ya kukuza sanaa na utamaduni wetu Tanzania.
***
Ilikuwa ni muda wa asubuhi watu wakiwa katika mihangaiko mbalimbali kila mtu akijaribu kushika ambako huwa kunampa ridhiki. Mama Sophia yeye aliamka mapema sana kwa ajili tu ya kuwahi watu wanaoenda makazini. Asubuhi awapate kwa urahisi. Siku hii Sophia sijui alipitiwa na malwani gani alikuwa bado amelala usingizi mzito sana wakutojielewa. Mama Sophia alitaka kuondoka na kumuaga mwanae kipenzi lakini baada ya kumkuta bado angali amelala aliamua kwenda kwanza kazini kwake. Bwana ee ngoja niwai mimi sinitarudi tutaonana” alisema mama Sophia huku akimbeba mgongoni kiziwanda chake na kufunga vizuri kitenge chake ambacho alikuwa amekivaa. Kitenge kilikuwa kimechakaa sana utadhania kina mapigano na maji na sabuni. Baada ya saa moja kupita Sophia akaamka kwa ajili ya kwenda kutafuta kibarua. Sophia baada ya kuamka alikuta jua limechomoza kubwa la saa moja asubuhi, akajua pengine muda umekwenda sana akaamka kwa haraka sana kwenda kunawa uso wake, kisha akarudi ndani kuvaa nguo/kuustiri mwili na mavazi. Sophia alifanya chapuchapu akiwa na falsafa kuwa kuwahi asubuhi ndio kupata kazi kwa uzuri zaidi. Sophia baada ya kumaliza tu akabeba cheti chake na kuondoka kwenda kutafuta kazi. Sophia aliamuwa kupita kwanza kwa Viviane nyumbani kwao alijuwa hatoweza kumkosa. Baada ya kufika anamkuta nje mama yake Viviane akipika chai nzuri na nzito. Mama Viviane anaanza kubadilika akizania labda Sophia kaja kuvunja mipangilio yao pale kwake. Sophia baada ya kumsalimia aliitikiwa kwa mbalisana mama Viviane, Sophia akaulizia kama Viviane yupo mama akamwambia yumo ndani kwa sauti ya chini kabisa, Sophia akaingia ndani na kumkuta rafiki yake kipenzi Viviane, walisalimiana kisha Sophia hakutaka kupoteza muda sana maana akufukuzae hakwambii toka ishara alizionyesha mapema sana mama Viviane, hata Sophia angekuwa mjinga kiasi gani tayari alikuwa ameshagundua siku nyingi mno.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Sophia akamuelezea ukweli kabisa Viviane pasipo kusahau hata kimoja kichwani. Viviane akamwambia ikishindikana ni bora kuacha tu kuliko kugawa mwili wake ili apate kazi. Viviane aliongea kwa uchungu lakini jambo la kuacha kutafuta kazi halikumwingia akilini kabisa Sophia. “Maisha haya bila kazi si ni sawa na kuishi London wakati huna pesa!” alisema Sophia kwa unyenyekevu. Viviane hakuongea kitu akabakia kufikiria amshauri nini cha kufanya huyu rafiki yake. Wakati akifikiria sana mama Viviane akamwita Viviane nje. Mama nakuja ngoja kidogo naongea na rafiki yangu hapa. Alisema Viviane ambae alikuwa swaiba sana na Sophia. Mama Viviane alimuita tena Viviane kwa sauti yajuu mno. Mwisho Viviane akaamua kwenda kwa mama yake nje kusikia anataka nini maana kwa sauti kubwa hiyo alikua tu kuwa kunajambo analomuitia na la muhimu sana. Baada ya kufika mamayake akamwambia “Viviane sasa unampango gani na huyo rafiki yako. Mimi nimepanga kila mtu chapati tatu tatu” alisema mama Viviane huku akiwa ameweka uso wa mbuzi hacheki wala kutabasamu hata kidogo walau kuleta (good visual) kwenye uso wake. Sasa Viviane akaishiwa hata neno la kuongea amwambie au amshauri nini mama yake mzazi mwenye roho ya korosho. Viviane akamwambia mama yake kuwa si tabia nzuri anayofanya maana alikereka sana ata akashindwa kunyamaza. Akaona ni bora kumwambia ukweli baada ya kumwambia hivyo mama yake alianza kumgombeza viviani polepole ili Sophia asisikie anacho mgombezea nini haswa, lakini hapo aligonga mwamba kwani Sophia alikuwa anayasikia yote maana alikuwa makini sana na masikio yake yalikuwa ni kama ya sungura mjanja kutoka bandani. Sophia baada ya kusika picha nzima aliamua kusimama na kuanza kujishauri kama aage au abaki pale ndani. “Shida hizi basi tu bwana ipo siku” aliwaza kimoyo moyo akijaribu kuupa moyo tumaini la kupata. Viviane kwa kuwa anampenda sana Sophia aliamua kuzila kunywa ile chai kabisa. Mama yake akamuangalia bila kummaliza binti yake. Viviane baada ya kukasilika akarudi ndani kuongea na rafiki yake kwani mama yake alikuwa mpaka anataka kukatisha (crimax) ya maongezi yao. Viviane baada yakurudi ndani anamkuta Sophia kasimama. “Vipi mbona umesimama unataka kwenda sasa hivi?” aliuliza Viviane kwa mashaka sana akijuwa labda Sophia ameshagundua walichoongea nje na mama yake. (Viviane alikuwa sahihi ingawa alikuwa kama anabashili flani hivi kama kubahatisha bahatisha). Sophia nae alikuwa mjanja sana kupindukia hakutaka Viviane ajue kama ameshawagundua akamwambia kuwa amechoka tu kukaa pale kwenye kochi. Sophia hadi alijinyoosha kinafiki ilikusudi viviani asijue kiendeleacho moyoni mwa Sophia. Kisha Sophia anakaa chini na kutulia. Kipindi akiwa ametulia Viviane akawa anabonyeza simu yake ya mkononi, akiwasiliana na bwana mmoja ambae alikuw ni rafiki yake sana. Bwana huyo alikuwa na kampuni inayojishughulisha na usindikaji wa juisi na matunda. Bwana huyo alikuwa anaitwa Damiani. Walikuwa wakiongea kwa njia ya sms. Damiani alikuwa taklibani miezi mitatu nyuma anatafuta mfanyakazi wa kusimamia hesabu za stooni kwake na alikuwa anataka mwanamke maana wanaume walikuwa wanamwibia sana na kumpa hasara kubwa sana ambayo alikuwa hatalajii kabisa. Akawa tayari alishamwambia mpaka Viviane amtafutie mfanyakazi. Viviane akawa amemkumbusha baada ya kuona Sophia anahangaika mno na kazi hapati mjini. Damiani akamwambia kwa njia ya meseji kuwa bado hajampata mfanya kazi na anahangaika sana kumtafuta lakini hampati kabisa. Viviane akamwambia kuwa ana rafiki yake anamuamini sana anatafuta kazi. Damiani kwa kuwa alikuwa na mambo mengi sana ya kiofisi alimwambia Viviane ampeleke siku hiyo hiyo kama itawezekana. Viviane akamwambia Sophia kwanza ili kumuweka wazi wazi anaenda kufanya nini sio kwenda kama vichaa tu mabarabarani. Sophia baada ya kuambiwa hivyo na http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Viviane aliamuwa kusahau hata yale yaliyofanyika pale muda uliopita na kufungua ukurasa mpya kabisa. “Kweli Viviane au unanitania, acha bwana mini niko siliasi bwana” alisema Sophia akijuwa Viviane anamtania kabisa wala hakutaka kuamini ni kweli. Viviane akaingia chumbani kwake na kubadili nguo ili waanze kwenda mjini kwa Bwana Damiani. Viviane alikuwa anamuamini sana Damiani na Damiani alikuwa anamuamini sana Viviane. Damiani alipomaliza kuongea na Viviane aliendelea kukabiliana na majukumu ya pale ofisini, kule mtaani mama Sophia kazi ilikuwa namuendea vizuri kwani alibahatika kwenda kuomba dukani akapewa sukari kilo tano maana ilikuwa ni siku ya Ijumaa ambayo inajulikana kama siku ya kusaidia wasiojiweza kimaisha. Baada ya kupata sukari hiyo mama Sophia alifurahia mno nakusema kwa uso wa furaha na bashasha kubwa mno. “Maisha ya namna hii kumbe nilikuwa nachelewa sasa na chai nyumbani itakuwa inapikwa kwa sana” aliongea mwenyewe kama hamnazo vile. Ingawa ni kweli alikuwa mpungufu wa akili. Mama Sophia nakuwa bado halidhiki sana na ile sukari anaamua kwenda kuomba tena pesa barabarani. Siku hiyo alikuwa kava kitenge kimechafuka sana, miguuni alikuwa kapauka kama pande la muhogo, kichwani akavaa lemba kubwa sana kama la kinaigeria vile. Wakati haya yote yakifanyika kwa muda huo mdogo wake na Sophia,Edo anaamuwa kurudi nyumbani kwao maana ilikuwa ni ijumaa, na ndio siku aliyokuwa anapenda kwenda nyumbani kusalimia alafu kesho yake anaondoka kurudi alikokuwa anaishi. Sophia ambae anabashasha na shauku kubwa yakupata kazi, sasa walikuwa mjini na best yake mkubwa Viviane. Kwa sababu walikuwa hawajanywa chai hata kidogo, Viviane aliamua waingie supermarket walau wanunue bidhaaa au chochote angalau wale kupooza matumbo yao. Au kufanya minyoo ya tumboni kuwa sawiya kabisa. Sophia ndio ilikuwa mara ya kwanza kuingia supermarket alikuwa anaishia kuziona kwa nje tu na kupita basi.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment