Search This Blog

Friday, October 28, 2022

WABEBA NDOTO (THE DREAM HOLDERS) - 1

 







    IMEANDIKWA NA : PAUL M CHALE



    *********************************************************************************



    Simulizi : Wabeba Ndoto (Dream Holders)

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Alikuwa akikimbia huku akihema kwa nguvu,hofu kuu ilimjaa na uwoga wa kuogopa kufa ilichangia yeye kukimbia zaidi.Alizidi kukimbia huku akiangalia nyuma kumtazama mtu aliyekuwa akimkimbiza usiku huo.Kasi yake ilionyesha wazi kuwa alikuwa akimkimbia mtu hatari sana aliyekuwa akitaka maisha yake.Ghafla alidondoka chini baada ya kumgonga mtu aliyesimama mbele yake.Akiwa chini huku akijiburuza mbali na mtu yule aliyekuwa akimsogelea taratibu.Mtu yule alionekana kuvaa koti kubwa lenye rangi nyeusi huku mikono yake ikiwa imefungwa vizuri na glovu za rangi nyeusi "tafadhali usiniue,tafadhali nakuomba" alilia na kuomboleza maisha yake,hakutaka kufa "naombeni msaada jamani! nauliwa!" alipiga kelele kuomba msaada kwa mtu yeyote aliyekuwa karibu na eneo lile "unapiga kelele Gerald,unapiga kelele za bure tu,tuko katikati ya msitu mnene na saa hizi ni saa tisa usiku unafikiri kuna mtu?! hakuna mtu hapa tuko mimi na wewe tu na nitakuua" alitetemeka kwa hofu kwa kujua hakuna namna angeepuka kifo usiku ule.Sura katili iliyojaa ndevu nyingi ya baba yule aliyesimama mbele yake hakuonyesha hata chembe ya huruma,bundi walilia kwa sauti kushangilia kifo cha Gerald usiku huo "tafadhali" alizidi kulia na kuomboleza.Baba yule hakuonyesha kujali alitoa kisu chake mfukoni na kukifungua vizuri "una bahati sana Gerald inabidi nikuchome kisu ufe utakufa kwa maumivu sana" aliongea huku akimsogelea,alinyanyua mkono wake ulioshika kisu juu,Gerald alifunga macho yake kujiandaa na kisu kuingia tumboni mwake.

    Alishituka kwa nguvu kutoka kitandani na kukaa vizuri huku akihema kwa nguvu,alinyanyua nguo yake juu na kutazama tumbo lake kuona kama lilikuwa na jeraha lolote,alipumua kwa nguvu baada ya kutoona jeraha lolote juu ya tumbo lake.Aliangalia saa juu ya ukuta na kuona ya kuwa muda ulikwenda sana na alikuwa amechelewa shule,alivua nguo zake haraka na kukimbia bafuni ambako kulikuwa mita kadhaa kutoka kitanda chake.Alifungulia maji na kuanza kuoga kwa haraka,mikono yake iliganda kichwani baada ya kuhisi vijiti vidogo vilivyokuwa kichwani mwake,alivitoa na kuvishangaa hakutaka kuamini alichojaribu kuamini.Alitoka bafuni huku akijikausha mwili wake kwa taulo,alitembea taratibu mpaka mahali alipotupa nguo zake,alichuchumaa na kuzinyanyua,alishangaa baada ya kuona majani madogo yaliyokuwa juu ya suruali yake.Ghafla mda huo hodi iligongwa mlangoni mwake na aliweza kusikia sauti ya mama yake ikimuita "mama subiri kidogo" alinyanyuka haraka na kuokota nguo zake na kuzitupia ndani ya kabati,aliyakusanya vizuri majani yale na kuelekea dirishani na kuyatupa majani yale,kabla hajafunga dirisha kwa mbali alimuona kijana asiyemjua akimtazama kijana huyo alivalia suruali aina ya jeans na koti kubwa jeusi lilimtosha vizuri huku mikono yake ikiwa mfukoni,alikuwa akimtazama Gerald kwa umakini.Gerald alimtazama na kuamua kufunga dirisha lake na kuliziba kwa pazia.Alielekea mlangoni na kuufungua taratibu huku mama yake akiingia taratibu ndani "shikamoo mama" "marahaba ulikuwa unafanya nini mda wote huo!" "Aah..nilikuwa najiandaa kwenda shule" alijibu Gerald huku akishika kichwa chake "shule!mbona umechelewa sana! tuyaache hayo baadae mchungaji Jackson atakuja hapa,nimemwambia tatizo lako la ndoto nafikiri atakuja akuombee huenda tatizo lako likaisha.Vipi na Leo umeota tena?" aliuliza mama yake "hapana Leo sijaota kabisa" "una uhakika?" aliuliza mama yake kwa wasiwasi "yah,leo sijaota".Mama yake aligeuka mlangoni na kuondoka zake,Gerald alibamiza mlango na kurudi dirishani kwa haraka ili aweze kumuangalia kijana yule aliyemuona wakati akitupa majani,alifungua pazia haraka na kuangalia huku na huko lakini hakuona mtu yeyote.Alifungua pazia zaidi kuruhusu mwanga uingie alivaa nguo zake haraka kuelekea shuleni.

    "Please sir may I come in" aliongea Gerald akiwa nje ya darasa kuomba ruhusa kuingia ndani maana alikuwa amechelewa sana,Mwalimu Ngeze alimtazama kwa macho ya ukali na kutazama saa yake "Gerald umechelewa tena!" "Sorry sir" "sorry sir! hizo sorry sir zako hazisaidii kitu,ujue wewe ndio mwanafunzi unayeongoza kwa kuniambia sorry,siku nyingine sitakusikiliza,pita ukakae" alifoka mwalimu Ngeze mwalimu mzuri wa kemia katika shule ya MIDTOWN.Gerald aliketi taratibu juu ya kiti chake na kutoa madaftari na kuyaweka juu ya meza "Gerald unaweza kunitajia Goldberg and Wages law" aliuliza mwalimu Ngeze huku akimtazama Gerald,Gerald alisimama huku akishika kichwa chake,minong'ono ya wanafunzi wenzake ilisikika kuashiria kumbeza "keep quite! enhee Gerald" "the rate of chemical reaction is directly proportional to the molar concentration of reactants raised to their power of molecules" "good! clap your hands for him" aliamuru mwalimu Ngeze.Darasa lote lilipiga makofi na Gerald aliketi taratibu juu ya kiti chake.Mwalimu Ngeze aliendelea kufundisha kwa nguvu zote na juhudi kuhakikisha wanafunzi wake walikuwa wanaelewa kila kitu alichokuwa akifundisha.Mawazo ya Gerald yalikuwa mbali sana,alikuwa akiwaza juu ya ndoto alizokuwa akiota kila siku na kumnyima usingizi.

    Baada ya dakika kadhaa ukimya ulitawala darasani wanafunzi waligeuza nyuso zao kutazama mlangoni kumtazama msichana aliyeonekana kuwa mgeni shuleni hapo na kwenye darasa hilo "morning sir! Is this science class?" "Yah,welcome" alijibu mwalimu Ngeze na kuangalia darasa zima kumtafutia nafasi ya kukaa "Gerald pembeni yako kuna mtu?...Hamna eeh? Karibu ukakae pale".Uzuri wa msichana huyo ndio ulichangia kwa kiasi kikubwa ukimya ndani ya darasa huku kila mtu akimshangaa huku baadhi ya wavulana wakinong'ona,alipita taratibu na kuelekea kwenye sehemu ya wazi karibu kabisa na Gerald.Gerald alikaa vizuri na kumtazama "hey" "hey" "karibu,I'm Gerald,Gerald Donald and you can...." "mmmh no! Gerald unawahi sana kusalimia wasichana lakini hata siku moja hujawahi kuwahi darasani" aliongea mwalimu Ngeze na kusababisha kicheko kikubwa darasani kilichodumu kwa muda mfupi.Gerald aliinamisha kichwa chake kwa aibu na kuendelea kuandika,msichana yule alimgeukia Gerald na kumtazama "thanks naitwa Kylie" aliongea msichana yule na kumpa mkono Gerald ambaye aliitikia na kuinamisha uso wake kwa aibu.Sura nzuri ya Kylie ilikuwa ishapenya kwenye moyo wa Gerald,aliwaza mengi kwa muda na kulaza kichwa chake juu ya meza mpaka usingizi ulipomchukua.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gerald aliingia taratibu ndani huku akirudishia mlango wa nyumba polepole,ukimya alioukuta ulimsababishia Gerald aanze kuita "mama!mama!" aliita sana lakini hakupokea majibu,alielekea moja kwa moja mpaka jikoni lakini hakumkuta mama yake,alifungua jokofu na kutoa boksi dogo la juisi na kuimimina ndani ya bilauri ambapo aliinywa taratibu.Ghafla alisikia mlango kutoka sebuleni ukifunguliwa "mama huyo"alijisemea kwa sauti ya chini.Aliweka bilauri juu ya meza na kuelekea sebuleni kumlaki mama yake.Alishtuka baada ya kumuona mwanaume mwenye sura ya kutisha iliyojaa ndevu huku amevalia koti kubwa la rangi nyeusi"Gerald tumekutana tena,tena nyumbani,usijali mama yako hayupo nafikiri akirudi atajisikia vibaya sana kukuta maiti yako" Gerald alitetemeka na kukimbia jikoni ambapo alichukua kisu ili kujihami "oooh! una akili sana,umeshika kisu!" aliongea baba yule kwa dhihaka na kucheka "usiwe msumbufu Gerald maana usumbufu ni kitu ambacho kinanitiaga hasira sana huwa sipendi vijana wanaonisumbua" alizidi kuongea baba yule kwa dhihaka kwa kasi sana alimkaba Gerald kwa nguvu na kuchomoa kisu mikononi mwake.Ghafla kisu kile kilipita mkononi mwa Gerald na kumchana.Gerald alilia kwa maumivu "tafadhali niache..."

    "Gerald!Gerald!" aliita kwa nguvu mwalimu Ngeze na kugonga meza kwa nguvu iliyomshitua Gerald kutoka usingizini.Alishituka huku akiwa amelowa jasho na kutetemeka alitazama huku na huko na kuona wanafunzi wenzake wakimcheka "Gerald unaota tu eeh!,sio! Kwa hiyo mimi hapa mbele nafundisha unaona kama nakuimbia nyimbo nzuri mpaka unalala" alifoka mwalimu Ngeze kwa hasira "I'm sorry sir" "sorry sir,tena sorry sir" aliongea mwalimu Ngeze na kuhema kwa nguvu.Gerald aliangalia mkono wake uliokuwa ukivuja damu kutoka eneo la juu lililokuwa limechanika,Kylie alimshangaa Gerald na kushituka "gosh! Gerald uko sawa!" "Yah niko sawa ni..ni..kidonda kidogo tu" alijibu huku akitoa kitambaa kwenye mfuko wa suruali "no Gerald hicho siyo kidonda cha kawaida!" aliongea Kylie kwa mshangao.Gerald alinyanyuka kwa nguvu na haraka na kukimbia nje ya darasa kuelekea chooni,mwalimu Ngeze pamoja na wanafunzi walishangaa tukio hilo.Alifika chooni na kufungua bomba kuosha kidonda chake lakini damu nyingi iliendelea kuvuja,alishangaa kuona kidonda chake kilikuwa kikubwa alitoka haraka kuelekea kwenye zahanati ndogo ya shule kupata matibabu zaidi "umefanya nini?" aliuliza tabibu aliyekuwa akiangalia kidonda chake "nimechanika bahati mbaya kwenye dawati" "hilo siyo dawati,mbao na misumari ya dawati haviwezi kukuchana kiasi hiki,panaonekana ni jeraha la kisu" "kisu! hapana hapa ni shule kwa nini nichanike kwa kisu! hakuna anayekuja na kisu shule" aliongea Gerald huku akikunja sura yake kwa maumivu makali "nani anayejua! nyie wanafunzi siku hizi mmekua wahuni sana,sasa nenda pale maabara kwa nesi akisafishe na kukifunga halafu utapitia dawa pale dirishani,nimekuandikia hapa" "aah asante dokta" "haina shida kuwa mwangalifu sana" aliongea daktari.Baada ya matibabu ambayo hayakuchukua muda mrefu Gerald alitembea taratibu kurudi darasani,alipandisha ngazi zilizokuwa mbele yake alikutana na korido ndefu ambayo ilikuwa na madarasa kila upande,aliinua kichwa chake na kumuona mtu mwingine aliyesimama mbele na mwisho kabisa wa korido hiyo,alikuwa ni kijana yuleyule aliyemuona asubuhi wakati akitupa majani kutoka dirishani chumbani kwake.Hilo lilimshitua Gerald kwa kuwa kijana yule hakuwa mwanafunzi wa shule hiyo na alionekana kumfuatilia Gerald kila wakati,hayo yalimchanganya akili Gerald "hey!hey!" aliita Gerald huku akijaribu kumkimbilia kijana yule ambaye aliondoka kwa haraka,Gerald alimkimbila bila mafanikio maana hakumuona kijana yule alipotea kwa haraka na kwa muda mfupi sana!.Alirudi darasani,kelele ziliashiria kuwa mwalimu Ngeze hakuwepo darasani,aliingia taratibu na kuketi vizuri kwenye kiti chake "Gerald uko sawa kweli?" aliuliza Kylie,Gerald alitikisa kichwa na kutabasamu "no Gerald you were just okay then all of the sudden ukaanza kutoka damu!" "nipo sawa,huwaga na hili tatizo la kutokwa na damu lakini niko sawa can we not talk about this?" aliongea Gerald huku akitazama bandeji iliyofungwa vizuri mkononi mwake.Dakika zilipotea Gerald alikuwa makini na madaftari yake huku akiwaza juu ya ndoto alizokuwa akiota kila Siku,alishindwa kuelewa ilikuwaje mambo aliyokuwa akiyaona ndotoni yalitokea kweli katika maisha yake,alishindwa kuelewa yule baba ambaye anamuona kila siku kwenye ndoto alikuwa ni nani na kwanini alijaribu kumuua.Maswali mengi bila majibu,zaidi alijiuliza yule kijana ambaye humuona kila Siku baada ya ndoto alikuwa ni nani.Kylie alimuangalia Gerald na kumshangaa,alianza kumuonea huruma na kuona huenda Gerald alikuwa na matatizo makubwa yaliyomsumbua akili na kumfanya kuwa na mawazo mara kwa mara.

    "....huwa namuona huyu baba akijaribu kuniua kila Mara nikiota huwa kama naongea naye" "unamjua huyo baba,unamfahamu? labda ushawahi kumuona mahali au kuzungumza naye?" aliuliza mchungaji Jackson "hapana,sijawahi kumuona kabisa,kama navyokwambia huwa namuona kwenye ndoto tu akijaribu kuniua" "aisee nafikiri kuna roho za kuzimu zinakufuatilia,hapa cha msingi ni maombi tu kila siku kabla ya kulala.Nimeleta na haya maji ya baraka utakuwa ukiyanyunyiza kila siku kabla ya kulala.Sasa tufunge macho tuombe" aliongea mchungaji Jackson,wote walifunga macho na mchungaji Jackson aliomba kwa nguvu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku zilisogea taratibu na Gerald hakuonekana kusumbuliwa tena na ndoto za ajabu,alilala usingizi mzito kila siku na kuongeza furaha yake hata sura yake ilianza kung'aa na kuonesha uzuri kila alipotabasamu "kumbe wewe ni kijana mzuri tu" aliongea Kylie huku akitabasamu huku akishindwa kumuangalia Gerald usoni "kweli! sijawahi sikia hilo" "kweli,maybe ulikuwa hujui kwa sababu before you were always alone,quite,maramara unaotaota tu.You were weird you know" "thanks,sasa hivi niko sawa,hata wewe ni mzuri sana" aliongea Gerald na kumuangalia Kylie kwa macho ya aibu "mmmh!" "hutaki au! Yaani Midtown nzima wewe ndio namba one" aliongea Gerald wakati wakitembea taratibu mpaka dukani na kununua juisi ambazo walianza kunywa taratibu "asante kwa juisi" "ah asante na wewe kwa kushukuru" alijibu Gerald.Walitembea taratibu mpaka kwenye bustani nzuri ya shule na kuketi kwenye moja ya mabenchi yaliyokuwa hapo "natamani ningekuwa kama wewe Gerald mzuri,nafaulu darasani yaani mama yako na baba yako must be very proud" Gerald alitabasamu "yah I wish my dad angeona haya yote na kunisifia" aliongea Gerald kwa sauti ya chini "is he dead?" "No! Ila ni kama amekufa tu,amepalalaizi mwili mzima tokea nazaliwa sijawahi kuongea na baba yangu.Yuko hospitali tu amelala kwa miaka yote kumi na saba" "pole sana naamini Mungu anaweza kutenda miujiza ni swala la kumuomba Mungu tu" aliongea Kylie kumfariji Gerald.Gerald alimtazama Kylie usoni na kutabasamu "nashukuru" "unajua Gerald tokea tumekuwa marafiki huwa najisikia raha tu kuongea na wewe,nakuwa huru like I'm free to talk anything yaani ningekuwa na zawadi ningekupa" Gerald alitabasamu na kucheka "zawadi!zawadi ya nini sasa! Hata ungenipa zawadi wewe unafikiri ungenipa nini?" aliuliza kwa utani huku akimsukuma Kylie na bega lake "wait" aliongea Kylie na kufumba macho " mmmh ningekupaa..BMX! baiskeli mpya uachane na kibaiskeli chako kile kibayaaa" aliongea Kylie na kucheka "kibaya eeh" alijibu Gerald na yeye akifumba macho yake "mimi ningekupa mkufu mzuri wa dhahabu wenye herufi ya jina langu nikuvalishe shingoni mwako ili kila mda ukiutazama ukumbuke jinsi gani mimi wa muhimu kwako.Na uache kuvaa mikufu yako mibaya iliyochakaa chuma chakavu" "nini!" alishituka Kylie na kumpiga Gerald Kofi dogo kwenye bega na wote walicheka huku wakiangaliana kwa muda,sura zao zilisogeleana taratibu na kubadilisha ndimi zao kwa mahaba "Kylie I'm sorry this is not right,I shouldn't have done this" "noo! Its okay its okay Gerald" alijibu Kylie huku sura zao zikigusana kwa ukaribu na mikono ya Kylie ikiwa juu ya mashavu ya Gerald.Gerald alishusha taratibu mikono ya Kylie "no its not okay unatoka na Paul and he really loves you" aliongea Gerald kwa sauti ya chini " yah uko sahihi Paul loves me and its not right,I'm sorry" alijibu Kylie,baada ya muda walisimàma na kuelekea majumbani kwao huku kila mmoja akiwaza juu ya tukio hilo.

    Siku zilizidi kusogea huku maisha ya Gerald yakiendelea kuwa vizuri,hakusumbuliwa tena na ndoto za ajabu,mama yake alikuwa mwenye furaha sana kuona mwanaye hasumbuliwi na ndoto mbaya alishukuru sana kwa maombi aliyofanya mchungaji Jackson.Gerald alikuwa chumbani kwake akichezea kompyuta yake ghafla mama yake aliingia "Gerald,natoka naenda mbali kidogo halafu nitapitia kumuona baba yako hospitali kwa hiyo nitachelewa kurudi hivyo basi hakuna kutoka leo" "mamaa!" "umenisikia,halafu hizo nguo chafu hapo chafu vipi?! Kwa nini huzifui unataka ziozeane hapo" "nitazifua" "nikirudi nikute zimefuliwa" aliongea mama yake na kuondoka.Gerald alihema kwa nguvu kuashiria kusumbuliwa,alinyanyuka taratibu na kusogelea rundo la nguo chafu lililokuwa juu ya kitanda chake.Alichambua moja moja na kunyanyua suruali,ghafla mkufu ulidondoka kutoka kwenye mfuko wa suruali ile,aliibwaga suruali ile juu ya kitanda na kuunyanyua mkufu ule kutoka chini.Ulikuwa wa dhahabu! Herufi kubwa 'G' ilichongwa vizuri kwenye mkufu ule "huu mkufu umetoka wapi tena!" alijiuliza,alijaribu kuvuta kumbukumbu ni wapi alipoupata mkufu ule lakini hakufanikiwa kukumbuka chochote.Alinyanyua simu yake na kuibofya kwa haraka na kisha aliiweka taratibu juu ya meza.Alinyanyua nguo zake na kuzipeleka kwenye chumba cha kufulia ambapo aliziingiza kwenye mashine na kubofya kitufe kuruhusu mashine ianze kazi ya kufua nguo zile.Alishinda siku nzima nyumbani kama alivyoamriwa na mama yake wala hakutoka kwenda popote zaidi ya kuoga vizuri na kutulia nyumbani kwake.Usiku ulipowadia huku mama yake akiwa bado hajarudi alisikia kengele ya mlangoni ikilia kuashiria kulikuwa ba mtu mlangoni.Alishuka kwa haraka mpaka sebuleni na kufungua mlango kwa haraka "hey" "heeey" alijibu Kylie aliyekua amependeza sana "umependeza sana" "asante" "karibu" aliongea Gerald huku akimuongoza Kylie kuingia ndani "mama yako hayupo?" "mama hayupo ametoka atachelewa kurudi kwa hiyo usijali sana" Kylie alitembea taratibu na kuketi juu ya kochi kubwa lilionekana ghari "nyumba yenu nzuri" "kawaida,tumehamia hivi karibuni ndio maana unaona bado mpya.Utatumia nini Maji,juisi auuu..bia?!" "Wewe! bia tena! usinichekeshe Mimi maji tu yatanitosha" alijibu Kylie Gerald aliharakisha na kurudi na bilauri la maji na kumpatia Kylie "here you go!" "thank you" "so umeniitia nini maana nimeona meseji yako wakati niko kwa kina Janeth" aliongea Kylie baada ya kupiga fundo dogo la maji "funga macho" "what!" "funga macho trust me" "Gerald what is this!" "Come on funga macho " alisisitiza Gerald.Kylie alifumba macho yake Gerald alisimama na kuingiza mkono wake mfukoni na kutoa mkufu alioukuta ndani ya suruali yake,alizunguka nyuma ya kochi ambalo alikuwa amekalia Kylie.Aliufungua mkufu ule na kuufunga vizuri shingoni mwa Kylie.Kylie alifumbua macho yake na kustaajabu mkufu wa dhahabu ambao ulitiririka kifuani mwake "oh my God Gerald!" alishangaa Kylie na kusimama,Gerald alitembea na kumsogelea karibu "mzuri sio?" "Of course its beautiful halafu hii ni dhahabu umepata wapi?" "nilifanya vikazi nikapata pesa nikaamua nikunulie zawadi kama nilivyokuahidi "kwa hiyo na mimi nina deni la BMX nafikiri" aliongea Kylie na kutabasamu.Waliketi chini na kuzungumza mambo mengi kwa muda mrefu furaha na upendo vilijaa katikati yao kikwazo kikubwa kilikuwa ni Paul mwanaume aliyekuwa na mahusiano na Kylie na lisingekuwa jambo jema kwa Kumuacha Paul bila kosa kwa maana Paul alimpenda sana.

    Mlango ulifunguliwa Gerald na Kylie walitoka nje baada ya maongezi ya muda mrefu,ulikuwa ni muda wa Kylie kuondoka kwa kuwa ulikuwa usiku sana.Wakiwa wanaagana gari ndogo iliwasili taratibu "oh shit! Mama huyo!" alishituka Gerald "nani! Mama yako!" "tulia kuwa kawaida kila kitu kitakuwa sawa" aliongea Gerald.Mama yake alishuka na kushika njia kuelekea ndani ya nyuma lakini alisimama na kushituka kidogo baada ya kuona Gerald na Kylie mbele yake "oh!" "Oh! Mama umerudi karibu shikamoo" "shikamoo" alisalimia Kylie "marahaba,Gerald huyu msichana mzuri hapa ni nani? Glory au?" aliongea mama yake baada ya kuona mkufu wenye herufi 'G' shingoni mwa Kylie "Kylie,naitwa Kylie" "oh Kylie! samahani sana jina zuri nilipoona hiyo herufi nikajua ni.." "anaitwa Kylie no rafiki yangu,tunasoma wote" alidakia Gerald "oh! sawa hamna shida,karibu sana Kylie mimi ndiye mama yake Gerald" "asante" alijibu Kylie kwa uchangamfu "haya mimi nipo ndani" aliongea mama Gerald na kuingia ndani.Kylie alihema kwa nguvu "nilikwambia kila kitu kitakuwa sawa" aliongea Gerald huku akitabasamu "mama yako ni mtu mzuri.Well..I gotta go its geting late" "yah sure"alijibu Gerald.Waliangaliana kwa muda "bye" aliaga Kylie na kuondoka.Gerald alimsindikiza kwa macho huku akitabasamu mpaka alipopotea gizani.Aligeuka na kurudi ndani kwa haraka na kumkuta mama yake akitafuta kitu ndani ya jokofu "Gerald" "mama nimeshafua tayari" alidakia Gerald "ni mzuri sio" Gerald alikunja sura kwa mshangao "nani?,unamaanisha Kylie! Mama Kylie ni rafiki yangu kwa hiyo sitakiwi kumuona kama yeye ni mzuri" "lakini tayari unamuona yeye ni mzuri.Unajua ni nini hicho? love! Mapenzi!" aliongea mama yake huku akinywa fundo la juisi aliyomimina kwenye bilauri "love! Mama unaongea kuhusu nini! Mimi na Kylie ni marafiki tu" "labda uniambie ile G kwenye mkufu inafanya nini" "mamaaa! ni..." "au potezea usijali sana" alidakia mama yake "nilienda kumuona baba yako daktari amesema hamna dalili zozote za kuamka inabidi tuwe wavumilivu inawezekana akaamka tena" aliongea mama yake kwa sauti ya chini na kumkumbatia mwanaye.

    Usiku huo Gerald alitembea taratibu barabarani kupunga upepo huku akiwaza hatima ya baba yake,ghafla alisikia sauti Kali kama ya mtu aliyekuwa akiruka,aligeuka nyuma lakini hakuona mtu yeyote barabara ilikuwa tupu na tulivu,wala hakuwa mbali na nyumba yao.Ghafla alipigwa konde zito juu ya shingo na kudondoka chini,alipiga kelele kwa sababu ya maumivu makali ambayo aliyahisi kwenye shingo yake.Alijitahidi kunyanyuka huku akishika shingo yake kwa maumivu.Alisikia sauti za hatua za miguu zikimkaribia,alihema kwa maumivu na kutetemeka kwa hofu huku akijitahidi kunyanyuka ili kumtazana mtu aliyempiga konde hilo "Gerald maumivu unayoyapata hayatapotea hivi karibuni" Gerald alishituka alikuwa ni baba yuleyule aliyekuwa akimuona kwenye ndoto zake "wewe!" "ndio mimi Gerald,tatizo wewe Gerald unafikiri kila kitu ni ndoto tu" aliongea baba yule na kuingiza mkono wake mfukoni "oh damn! nimesahau kisu changu,ila hamna shida nitakuua kwa mikono yangu mwenyewe" Gerald alijaribu kukimbia lakini baba yule alitokea ghafla mbele yake na kumkaba koo na kumnyanyua juu.Gerald alijaribu kujiondoa bila mafanikio huku akiona uhai ukimtoka, ghafla alitokea kijana mwingine aliyeruka kwa juu sana na kutua na ngumi nzito juu ya mgongo wa baba huyo, ngumi ile ilisababisha baba yule amuangushe Gerald chini "Gerald kimbia "Gerald alikohoa alijaribu kumtazama kijana yule aliyemwokoa lakini hakumuona sawasawa baada ya kijana yule kuendelea kupewa kichapo na baba yule "Gerald kimbia, unataka kufa au!" Gerald alinyanyuka na kukimbia haraka kuelekea nyumbani kwake maana hapakua mbali na maahali ambapo alivamiwa, alifungua mlango wa nyumba kwa haraka ......Alishituka kutoka kitandani huku akihema kwa nguvu jasho jingi lilimtoka, alikunja uso wake na kushika shingo yake iliyekuwa inauma, aliangalia saa yake na kuona mda ulikuwa umeenda sana, alinyanyuka kitandani huku shingo yake ikimuuma sana alijisafisha vizuri mwili wake na kuelekea shule, kwa kuwa ilikuwa Jumamosi, haikuwa Siku ya masomo shule ilitenga Jumamosi kuwa Siku maalum ya michezo na mazoezi ya timu mbalimbali za shule na mtaani. Gerald aliwasili katika viwanja vya michezo akiwa amevalia jezi zake vizuri kwa mbali alimuona Kylie akiwa pembeni Paul katika mapozi mazito ya kimahaba, alisogea kwenye benchi kubwa lililokuwa umbali wa mita ishirini kutoka eneo lilipokuwepo benchi alilokalia Kylie na Paul.Alikaa na kuanza kufunga vizuri kamba za viatu vyake,alikunja uso wake kwa maumivu makali ya shingo.Alinyanyua kichwa chake baada ya kumuona Kylie na Paul wakisogea kwenye benchi lake "hi" "mambo Gerald" aliongea Paul huku wakigonganisha ngumi zao "mzuka tu upo tayari kwa mechi" "kama kawa mwanangu si unajua shughuli yangu" aliongea Paul na kutabasamu huku akimuangalia Kylie usoni "nakuaminia baby" "unajua mchezo wa American football au rugby huu tunaocheza hauna mambo mengi kasi na nguvu ndiyo nguzo muhimu,vyote ninavyo hivyo" alijisifu Paul.Maumivu ya shingo yaliendelea kumpa taabu Gerald ambaye alikunja uso wake kwa maumivu kila wakati "Gerald uko sawa?" "Yah,uchovu tu Jana nilichelewa sana kulala".Filimbi ilipulizwa na kocha wa THE THUNDERS ambayo ndiyo ilikuwa timu aliyokuwa akichezea Gerald na Paul.Paul ndiye alikuwa nyota mkubwa wa timu hiyo kipaji chake kilikuwa chachu kubwa ya mafanikio ya timu hiyo,hilo ilikuwa tofauti kwa Gerald hakuwa na kipaji kikubwa lakini aliupenda sana mchezo wa rugby japokuwa hakuwa na bahati ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza."Twende pangeni mstari" wachezaji walijipanga vizuri kama kocha wao alivyowaamuru "sikia nakupa mpira unakimbia nao mpaka mbele ambapo mtakutana na Muddy nadhani mnaijua shughuli yake,hakikisheni asiwaguse mtamkwepaje sijui lakini nachotaka Mimi mpira uvuke mstari.Tumeelewana? haya Paul anza uwaoneshe wenzako" aliongea kocha wao na kupuliza filimbi yake kwa nguvu.Mpira ulirushwa kwa Paul ambapo aliudaka vizuri na kukimbia nao kwa kasi,kasi yake ilikuwa ni kama kumuona Usain Bolt akikimbia,alifanya vizuri na kufanikiwa kuvusha mpira kwenye mstari.Watu wote walimpigia makofi"yeah" sauti ya Kylie kwa mbali ikisikika.Gerald alivuta pumzi akiangalia wenzake wakikimbia vizuri na kumfurahisha kocha wao,Gerald aliwaza kama angeweza kuyafanya yale ilihali ana maumivu ya Shingo "zamu yako Gerald nataka kuona kasi na akili zaidi lakini.." alikatishwa baada ya gari ya kifahari lenye rangi nyeusi kuwasili pembeni ya uwanja.Alishuka kijana mmoja mrefu na mweusi kiasi aliyeonekana na umbo kubwa na kuvalia jezi zake vizuri,alitembea taratibu mpaka katikati ya uwanja,kila mtu alimshangaa kwa kuwa hakuwa mwenyeji kwenye timu hiyo "shikamoo kocha" "marahaba,na wewe ni..." "Daniel,naitwa Daniel Davis ni mgeni hapa" alijibu kijana yule "uko mahali sahihi kweli hapa?" "ndio,nataka kuwa kwenye timu hii ya The Thunders" "ooh! Unafikiri ni rahisi hivyo,okay unacheza nafasi gani?" "zote" alijibu Daniel kwa kujiamini "ooh vizuri zote sio! kwa sasa nenda ukakae defence zuia hawa wanaokuja na mpira wasivuke mstari huo.Hey! wewe Muddy rudi huku muache Huyu Mr Daniel anioneshe alichokuwa nacho" aliongea kocha na kumtazama Daniel usoni "nenda".Gerald alihema kwa nguvu alihema kwa nguvu huku akimtazama Daniel aliyekuwa mbele yake kujiandaa kumkabili,filimbi ilipulizwa "haya Gerald twende kimbia" Gerald alianza kukimbia kwa kasi huku akiugulia shingo yake,alimkaribia Daniel ambaye alionyesha yuko tayari kukabiliana naye.Gerald alipigwa kikumbo cha nguvu na Daniel ambacho kilimrusha juu na kudondoka chini umbali mrefu kitendo ambacho kilitonesha shingo yake na kuongeza maumivu zaidi.Tukio hilo lilimshangaza kila mtu,Kylie alifunga mdomo wake kwa mikono kuonyesha mshangao na mshituko "yeah hiyo ndiyo defence nayoitaka" alipiga kelele kocha. Kwa muda mrefu Gerald alibaki chini akigaagaa na kushindwa kuamka kitendo ambacho kilifanya wenzake kumsogelea na kumzunguka "Gerald uko sawa?" aliuliza mmoja wa wachezaji.Kylie alikimbia na kukaribia mahali pale na kumtazama Gerald aliyekuwa chini "Gerald are you okay?" Gerald alitikisa kichwa chake lakini hakujibu lolote.Kylie alikaza macho yake kwa mshangao baada ya kuona alama za vidole juu ya shingo ya Gerald "hebu mbebeni mpelekeni zahanati sidhani kama ataendelea tena " aliamuru kocha wao.Walimbeba mpaka zahanati ambapo walimpatia matibabu kwa muda mrefu mpaka jioni sana.Jioni hiyo mama yake Gerald alifika zahanati haraka na kumkuta akiwa amekaa kitandani huku pembeni yake akikaa Kylie pamoja na Paul aliyekuwa amesimama "ooh! Gerald uko sawa mwanangu?" aliongea mama yake baada ya kuingia na kugeuza uso wa mwanaye "ndiyo mama usijali niko sawa" alijibu Gerald.Mama yake alishangazwa na alama ya vidole juu ya Shingo ya Gerald "umepigana!" "hapana sijapigana" "na hizo alama shingoni je? hebu au unaota tena!" alihoji mama yake "hapana mama ni..." "hapana nini sasa wakati alama zinaonekana,unaota tena eti?" Gerald alitikisa kichwa kuashiria kukubali "Mungu wangu! sijui hata tufanye nini?" aliongea mama yake na kusimama huku akiwaangalia Kylie na Paul "asanteni sana wanangu kwa kukaa hapa na rafiki yenu.Mmh,Kylie!" "hamna shida mama, Gerald ni rafiki yetu na sisi kama marafiki zake inatupasa kukaa naye" aliongea Kylie.Maneno hayo yaligusa moyo wake na kutabasamu.Muda huohuo daktari aliingia akiwa ameshika karatasi zake,Gerald alishangaa kwa sababu kijana aliyekuwa akimuona kila Siku,aliyemuona wakati akitupa majani dirishani na aliyemuona wakati akitoka zahanati Siku alipoota darasani ndiye kijana yuleyule ambaye mda huo alisimama mbele yake kama daktari!."Gerald,sasa hivi uko sawa ni maumivu tu ya shingo yalikudhoofisha,nimekupa dawa.Chochote kitakachotokea sasa hivi usiogope komaa siyo rahisi wewe kupata madhara" aliongea daktari yule huku akimkazia Gerald macho yake.Alimgeukia mama yake na kutabasamu "wewe ndiyo mama yake nafikiri!.Sasa usiwe na shaka mwanao yuko safi na atakuwa salama.Labda niwaache" aliongea daktari huku akimtazama Gerald na kuondoka.Mama yake alimsogelea na kumfariji mwanaye.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya siku mbili maumivu yalimuisha kabisa,Gerald hakusumbuliwa na maumivu yoyote.Aligeuza shingo yake na kuona ilikuwa vizuri kabisa huku akiwa amevalia jezi zake alishika njia taratibu kuelekea uwanjani kwa ajili ya mazoezi ya peke yake kwa kuwa Mara ya kwanza hakufanya mazoezi vizuri baada ya kujeruhiwa shingo yake.Alijitafutia mda wa peke yake kwa kuwa baada ya miezi michache kulitarajiwa kuwa na michuano ya kitaifa.Alianza na mazoezi mepesi ya kunyoosha viungo vyake na kuviweka sawa.Nguzo muhimu wa mchezo huo ilikuwa ni kasi ambayo kila mchezaji alitakiwa kujifunza hilo,kutambua hilo Gerald alianza kukimbia uwanja mzima huku akikwepa fimbo ndefu zilizosimamishwa uwanjani hapo.Alihema kwa nguvu na kukimbia kwa kasi sana.Ghafla alipigwa kikunbo kizito kilichomrusha na kumdondosha umbali mrefu na kuserereka chini mpaka kwenye dimbwi kubwa la maji "ukiendelea hivyo Gerald utaweza kumtoka beki yeyote kwa maana hiyo hutashinda magoli" Gerald alishituka na kumshangaa baba ambaye anamuona kwenye ndoto kila siku.Alimsogelea na kumnyanyua kwa mkono mmoja na kumrusha tena umbali mrefu "Gerald kwa nini inaonekana rahisi hivyo kukuua! rahisi sana" aliongea huku akimsogelea Gerald taratibu.Gerald alijitahidi kunyanyuka lakini alikamatwa shingo yake "umepona eeh nafikiri natakiwa kuivunja sasa hivi" aliongea huku akikandamiza shingo ya Gerald kwa nguvu "muache aende Kronos,unajua huwezi kumuua" alimuachia Gerald chini na kumgeukia kijana aliyekuwa nyuma yake akimkaribia taratibu "na wewe je unafikiri siwezi kukuua! mmh Sebastian!" aliongea baba yule,Kronos."Kuniua mimi siyo rahisi hivyo muache dogo aende hutopata unachokitaka" Gerald alinyanyuka na kumshangaa kijana yule ambaye huwa anamuokoa "wewe!" "ndio mimi,acha kunishangaa na uende nyumbani maana huyu jamaa yuko hapa kukuua kama kwaida yake"alijibu Sebastian.Kronos alicheka kwa dharau "Sebastian unamuambia nani arudi nyumbani! tazama mtu mwnyewe hata kurudi nyumbani hawezi hivyo nitawaua wote wawili leo" aligeuza teke kwa kasi lililomkuta Sebastian usoni na kumdondosha chini.Alitemba na kumsogelea Gerald aliyeanza kurudi nyuma kwa hofu alimkaba koo kwa nguvu huku akimnyanyua juu sana.Sebastian alinyanyuka akakimbia alipomkaribia Kronos aliruka juu na kutua na ngumi nzito iliyomrusha Kronos mbali sana,Gerald alidondoka chini "kimbia Gerald nenda nyumbani tulia kuwa makini ili urudi nyumbani" aliongea Sebastian huku akimfuata Kronos aliyekuwa bado akizagaa chini,alipomkaribia alimshika shingo na kumrusha juu ambapo Kronos aligonga tawi kubwa la mti na kudondoka chini.Sebastian alizidi kumsogelea Kronos aliyekuwa bado akizagaa chini.Sebastian aligeuka na kupokea ngumi nzito kutoka kwa Kronos mwingine wakati huohuo Kronos mwingine alikuwa chini akigalagala kwa maumivu "Kronos utajiumba Mara ngapi ili uweze kupigana na mimi!" alidhihaki Sebastian huku akishika uso wake.Kronos alinyanyuka huku akishikilia mgongo wake kwa maumivu "unataka kujua! nazidi kuwa na nguvu Sebastian,niko kila sehemu hata ukitaka niwe mara millioni" aliongea Kronos.Ghafla wanaume wengi walijaa uwanja mzima wakimsogelea Sebastian,wanaume wote hao walikuwa wakifanana kimuonekano na hata sura zao zilifanana na sura ya Kronos."ooh! Gerald nimekwambia urudi nyumbani" alifoka Sebastian huku akirudi nyuma taratibu.Alikuwa katikati akizungukwa na watu hao "ooh Kronos! umekuwa nani wewe!" aliongea kwa sauti ya chini huku akiwatazama watu wote waliokuwa wakizidi kumsogelea.

    Gerald alishituka kitandani huku akipiga kelele kitanda chake kililowa sana na maji huku shuka lake likionekana kuchafuka sana na matope.Mama yake aliingia haraka baada ya kusikia kelele za mwanaye "Gerald " alimkimbilia na kumsogelea mwanaye aliyekuwa akitetemeka sana "Mungu wangu!" alishangaa baada ya kuona kitanda cha mwanaye kikiwa kimelowa sana na kuchafuka " ni ndoto gani mwanangu unazoota kila siku!" aliongea mama yake na kumkumbatia mwanaye huku akisali na kumwomba Mungu ayaondoe mateso kwa mwanaye ya kuota ndoto mbaya kila siku na kumsababishia kutolala kwa amani.Alielekea jikoni na kurudi na bilauri iliyojaa maji ya kunywa na kumkabidhi Gerald ambaye aliyanywa gubigubi."Pole sana nwanangu ipo siku utakuwa sawa,unafikiri unaweza kuendelea kulala?" Gerald alitikisa kichwa chake kukubali "una uhakika?" "ndiyo mama nitalala usijali we kapumzike" alijibu Gerald.Mama yake alimtolea shuka jingine safi na kumkabidhi atandike na kuondoka huku akimuacha mwanaye akijifunika shuka tayari kwa kulala "Sebastian! Kronos! ni kina nani hawa!" aliongea Gerald na kuwaza kabla ya usingizi mzito kumchukua.



    SEHEMU YA PILI



    "Twende! twende! kimbieni! toa pasi hakikisha inafika.Changamka Gerald" alipaza sauti kocha wao.Gerald alipigwa kikumbo cha nguvu na kubwagwa chini kama mzigo "safi Daniel,Gerald umelegea sana! nyanyuka". Mazoezi yaliendelea huku kila mara Gerald akipata mpira Daniel alikuwa akimzoa kwa nguvu.Wakati mwingine Gerald alipata mpira kutoka kwa Paul na kuanza kukimbia huku akiwapiga chenga mabeki kwa ustadi mkubwa sana,hiyo ilikuwa tofauti kwa upande wa Daniel ambaye alikuwa beki asiyepitika kirahisi na punde tu alipomuona Gerald akija upande wake alimkimbilia kwa kasi kubwa sana na kumsukuma vibaya na kumsababishia Gerald kudondoka chini na kuumia.Jambo hilo lilimtia hasira Paul ambaye alimfuata Daniel kwa jazba kubwa na kumsukuma "una matatizo na Gerald !" alifoka Paul huku akiendelea kumsukuma zaidi "Mimi ni beki nafanya defence tu" "defence! defence gani hii! unataka kuumiza watu hii siyo defence" alifoka Paul huku akiendelea kumsukuma.Daniel alishindwa kuvumilia kusukumwa na kuamua kurudisha kwa kumsukuma Paul "nini! au una wivu mmh! kwa sababu unajua mimu ni bora kuliko wewe nina nguvu,kasi zaidi na akili pia.Kwa hiyo usinifuate kana kwamba unamtetea Gerald wakati unajizungumzia mwenyewe,come on! kuwa mwanaume jiongelee nafsi yako" "hey! wote wawili yaishe la sivyo nitawapa adhabu,huu siyo mda wa kugombana mnatakiwa kushirikiana tuna michuano mikubwa mbele yetu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Daniel punguza kidogo na wewe Gerald unajilegeza sana hutacheza kwenye timu yeyote kama umelegea hivyo" alisema kocha wao.Gerald alisimama na kukimbia taratibu kuendelea na mazoezi.Baada ya dakika kadhaa kocha alimtoa na kumwambia apumzike.Gerald alivua glovu zake na jezi zake kwa hasira na kuelekea bafuni kunawa.Kylie alimuona Gerald akielekea bafuni huku akiwa amenyong'onyea aliamua kumfuata nyuma kumtia moyo.Kwa mbali Paul alimuona Kylie akimfuata Gerald lakini aliamua kuendelea na mazoezi.

    Kylie aliingia taratibu bafuni huku ukimya ukitawala hakusikia chochote zaidi ya sauti ya maji yaliyokuwa yakimwagika kutoka kwenye mabomba "Gerald!" aliita Kylie bila majibu huku akiingia ndani zaidi "Gerald uko sawa?" aliongea baada ya kumuona Gerald akiwa amejiinamia mbele ya kioo huku akiwa amejifunga taulo kiunoni.Gerald aligeuka na kumtazama Kylie "naam" Kylie alimeza mate kwa kuwa hakutegemea kumkuta Gerald akiwa na taulo tu "nilikuwa nataka kujua kama uko sawa,naenda.Sorry" " no siko sawa,nina vitu Vingi kichwani mwangu vitu vinanitokea ambavyo sivielewi kylie.Vitu Vingi sana" Kylie alimsogelea Gerald kwa ukaribu na kuweka mikono yake juu ya kifua kikubwa cha Gerald na kushusha mkono wake taratibu mpaka tumboni "usijali kila kitu kitakuwa sawa Gerald jikaze".Mikono ya Gerald ilishika kiuno cha Kylie na kumvuta kwa nguvu karibu yake.Walisogeleana na kubadilishana mate,Gerald alishusha mikono yake mpaka chini na kuyashika mapaja mazuri ya Kylie yaliyojaa vizuri na kumnyanyua juu.Alimgeuza na kumuweka juu ya sinki lilokuwepo mahali hapo huku wakiendelea kubadilishana mate.Kylie alishusha mkono wake na Kujaribu kushusha taulo la Gerald kiunoni "no Kylie tusifanye hivi Paul yuko uwanjani halitakuwa jambo zuri akitukuta hapa" aliongea Gerald.Kylie alishuka kutoka juu ya sinki huku akimtazama Gerald kwa macho yaliyolegea sana,aliweka nywele zake vizuri na kumtazama Gerald Kwa muda na kuondoka kurudi uwanjani.Mazoezi ya nguvu yaliendelea uwanjani kwa mbali Paul alimuona Kylie akitoka bafuni huku akiweka nywele zake vizuri na baada ya dakika kumi alimuona Gerald akitoka akiwa amebadilisha nguo.

    Gerald alishika njia tatatibu kurudi nyumbani huku akitabasamu kila mara alipokumbuka tukio la yeye na Kylie bafuni."Gerald!" aligeuka nyuma baada ya kusika sauti ya mtu ikiita jina lake " Sebastian!" "yah inabidi tukae tuongee" alijibu Sebastian.Gerald alikunja uso wake na kumeza mate kwa hasira "ndio inabidi tuongee unieleze kwa nini nimekuwa nikiota ndoto za ajabu na huyo kichaa Kronos kwa nini nimekuwa nikiwaona nyie kwenye ndoto zangu!" "Punguza jazba Gerald kuwa mpole nisaidie nikusaidie.Tafadhali tukae tuongee" "sina cha kukusaidia Sebastian kama huwezi kunijibu hayo maswali yangu sina cha kukusaidia ila naomba mniache niwe na amani nifurahie usingizi wangu.Sina msaada."alifoka Gerald "kama huwezi kunisaidia vipi kuhusu baba yako huwezi kumsaidia?" "Unaongea nini! baba yangu kivipi! baba yangu amepalalaizi kwa miaka kumi na saba sasa na sijui cha kumsaidia pia" alijibu Gerald.Sebastian aliangalia saa yake "sasa hivi ni saa sita mchana twende mahali tuongee tukale,niamini mimi unaweza kumsaidia baba yako siyo kila unachokiona kipo kama kilivyo na ndio maana unaota ndoto hizo za ajabu kila Siku.Uko tayari tuongee?" "tunaongelea wapi?" aliuliza Gerald huku akikaza macho yake.

    Mlango wa kioo wa mgahawa mkubwa ulioitwa 'EAT HERE RESTAURANT'ulifunguliwa.Gerald na Sebastian waliingia taratibu na kuketi kwenye moja ya meza " huu mgahawa ni ghali sana Sebastian unaweza kulipa?" "usijali" muda huohuo mhudumu aliwasili na karatasi pamoja na peni mkononi mwake "karibuni niwasaidie nini naomba utuletee juisi ambayo ni bora na ghari kuliko zote,mhudumu aliandika maelezo yale na kuondoka "Sebastian usitake tuburuzwe kwa kushindwa kulipa Mimi mwenyewe mwanafunzi sina hela.Sebastian alifumba macho kwa sekunde chache na kuyafumbua "usijali nimekwambia" alitoa mkono wake uliokuwa juu ya meza.Gerald alishangaa kuona hela nyingi zikiwa juu ya meza "" aaisee umefanyaje hivyo!" mazingaombwe au uchawi!" alishangaa Gerald "natakufundisha baadae". Mhudumu aliwasili na bilauri mbili za juisi na kuwakabidhi kila mmoja wa kwake "asante,kunywa Gerald twende mahali pazuri zaidi ambapo tutaelewana" aliongea Sebastian.Gerald alipiga fundo dogo la juisi na kurudisha bilauri mezani "kwa hiyo utaniambia au tunakunywa tu juisi!" alihoji Gerald.Kwa ghafla dada aliyekaa nyuma ya Gerald alimwagiwa juisi bahati mbaya na mhudumu "aisee nini hiki! gauni ghali hii!" alifoka dada yule.Gerald aligeuka na kutazama tukio lile,Sebastian alifumba macho yake na kuweka mkono wake juu ya mdomo wa bilauri,kidonge kidogo kiliingia ndani ya bilauri na kuyeyuka mara moja.Alitoa mkono wake haraka baada ya Gerald kugeuka "maliza haraka tuondoke" aliamuru Sebastian.Gerald alikunywa ile juisi gubigubi na kubamiza bilauri mezani kwa nguvu.Sekunde chache baadae Gerald alianza kusinzia "umeniwekea nini Sebastian?" hakuona vizuri macho yake yalifumbwa na ukungu wa usingizi "inabidi ulale Gerald,lala" aliongea Sebastian huku akimtazama Gerald aliyekuwa akirembua kutokana na usingizi mzito.Haikuchukua dakika nyingi Gerald alidondosha kichwa chake juu ya meza kama mzigo na kupotea usingizini.

    Ghafla Gerald alisimama ukingoni mwa barabara kana kwamba alikuwa akijiandaa kuvuka,magari hayakuonekana kupungua barabarani huku milio ya honi ikipokezana.Gerald alishangaa kwa kuwa mji huo haukutulia watu walipishana huku na huko kwa shughuli zao pia alishangaa majengo makubwa yaliyojaa ndani ya mji huo.Alizidi kushangaa kwa kuwa hakuwai kuuona mji huo mahali popote hata kwenye luninga ulikuwa ni mji mgeni machoni kwake."Hutamaliza kuushangaa mji huu Gerald hata kama ukipewa Siku nzima" aliongea Sebastian aliyekuwa nyuma yake akitembea kumkaribia.Gerald aligeuka kumtazama Sebastian "uko tayari?" aliuliza Sebastian " subiri kwanza Sebastian,hapa wapi?" "tuko GROTTO ni sehemu yetu nyingine ya maisha mimi ,wewe na wengine wa jamii yetu "una maana gani? hapa wapi? Sikia Sebastian mimi nataka kurudi nyumbani tupo sijui kwenye mji gani huu! nata.." "kaa kimya Gerald na unisikilize kama unataka kurudi nyumbani nakumsaidia baba yako" aliongea Sebastian.Walivuka barabara na kuingia kwenye mgahawa mkubwa mahali hapo "hey Linda mambo alimsalimia mhudumu mrembo aliyekuwa akizunguka kwenye baadhi ya meza.Walisogea kwenye moja ya meza na kuketi,baada ya muda mfupi Linda alielekea kwenye meza yao "mambo Sebastian,Gerald" Gerald alishangazwa na jambo la mhudumu kujua jina lake "tafadhali Linda tuletee chakula kizuri sana kama kawaida yangu na huyu bwana mdogo mletee hivyohivyo"aliongea Sebastian na kumgeukia Gerald "sasa ndio tutakula sahau ile juisi" aliongea Sebastian na kuhema kwa nguvu "okay sikia Gerald sasa hivi unaota na uko ndani ya ndoto yako mwenyewe unaishi kama hivi.Sasa hivi umelala na unaota ndoto kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee ya wewe kuja huku,Grotto". "nini!" "Grotto ni kama dunia nyingine sema huku ni tofauti kwa sababu tunaishi kwa kutegemea ndoto zetu.Kila mtu unayemuona humu yuko mahali amelala na hii ndiyo ndoto anayoota,kila kitu humu ni ndoto.kuna watu huku ndiyo wanaishi maisha na kuyaendesha siyo kama huko duniani,kuna watu huku ni matajiri na wana kazi zinazo wasaidia kuendesha maisha yao duniani.Asante Linda" alitabasamu huku akimshukuru Linda baada ya kuwaletea chakula."Mfano Linda bado ni mwanafunzi wa chuo wazazi wake in masikini Sana lakini tokea amejua kuwa ana maisha mengine Grotto ada,pesa havijawa tatizo kwake" aliongea Sebastian "na wewe ni nani?" na Kronos ni nani? kwa nini alitaka kuniua?" aliuliza Gerald kwa haraka.Sebastian aliingiza kijiko mdomoni na kuanza kutafuna taratibu huku akimtazama Gerald "mimi? mimi ni 'dream holder' kama wewe Kronos na kila mtu humu Grotto.Tofauti ya Mimi na wewe ni kwamba sisi ni 'creators' ndiyo dream holders wenye nguvu kuliko wote ila nguvu zetu zinatofautiana.Dunia nzima tuko creators sita tu ambao ni Mimi,wewe Kronos,baba yako Mr Donald na mwingine ambaye hakuna anayemjua ila.." "subiri,subiri kwanza umesema baba yangu ni creator!" aliuliza Gerald kwa mshangao "ndio baba yako ni creator ila kwa bahati mbaya Kronos amemfunga mbali sana kwa miaka yote hii kumi na saba na ndio maana inabidi nikusaidie ili umuokoe baba yako" aliongea Sebastian kwa msisitizo.Gerald alihema kwa nguvu kuonyesha kutoelewa sana alichokuwa akiambiwa "una uhakika naweza kumsaidia baba yangu?" "asilimia mia moja" "Kronos yuko wapi?" "oooh! tulia siyo haraka na siyo rahisi hivyo! Kronos anaishi kwenye ndoto za watu kwa muda mrefu anajificha kwa hiyo hajulikani alipo.Kwa hiyo tunaanzia hapo kutafuta hao watu "ujue unanichanganya umesema watu wanaota na kuja huku Grotto sasa inakuaje watu wengine wakaota tofauti na huku Grotto mpaka Kronos ajifiche huko!" "dream holders wanaoweza kuota ndoto ndani ya Grotto ni wachache sana tena hao wenye matatizo sana mara nyingi wanaota ndoto za kutisha" "sasa tutawajuaje?" "sijui hakuna anayejua ni jukumu letu kuwatafuta. Kwanza inabidi ujifunze kuja huku bila kulala kama sisi creators wengine ila sasa hivi itabidi tu ulale ili uje huku mpaka utapojifunza" aliongea Sebastian na kumalizia kijiko cha mwisho.Gerald aliangalia pembeni huku akiwaza sana "usiwaze sana Gerald wewe una nguvu sana kuliko unavyofikiri,wewe ni supreme creator mwenye nguvu kuliko wote duniani unahitaji muda tu kujifunza na kutambua hill.Nafikiri kwa leo tumemaliza".http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kaka! Kaka! Kaka!" alishituka Gerald baada ya kuamshwa na mhudumu aliyegonga meza yake,aligeuza shingo yake na kutazama nje na kuona kwamba ilikuwa ni usiku "samahani n saa ngapi?" "saa mbili na nusu umelala hapa tokea saa Saba mchana.Vipi unaumwa?" "aah! nafikiri,samahani sana kwa usumbufu ngoja niende" aliongea Gerald na kunyanyuka,alitembea kwa haraka na kufungua mlango wa mgahawa huo na kuondoka alishika njia kurudi nyumbani huku mama yake akiwa anamsubiri kwa hofu kwa maaana hakuna aliyejua alipokuwepo.Alifika na kuingia taratibu na kumkuta mama yake akiwa anatazama luninga "ulikuwa wapi?" mmmh nilikuwa.." "usiniambie ulikuwa kwa kina Kylie maana alipiga simu kukuulizia "nilikuwa kwa..kina Daniel rafiki yangu mwingine wa shule ndio nimechelewa huko "sipendi hiyo tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani na hata kama ukiona utachelewa ni jambo zuri ukitoa taarifa si una simu wewe!.Usirudie tena "sawa samahani" alijibu Gerald na kuingia chumbani kwake.Alitumia muda mwingi kuwaza juu ya yote ambayo Sebastian alimueleza kuhusu Grotto na uwezekano wa yeye kumsaidia baba yake aliyekuwa amefungwa kifungo cha ndoto na kufanya apalalaizi kwa miaka kumi na saba tokea Gerald alipozaliwa..Sasa alijua kuwa ana uwezo wa kumuokoa baba yake japo hakuwa na uhakika ni kwa namna gani ila aliamini maneno ya Sebastian ambayo yalimfungua macho na kumpa ufahamu kwa nini alikuwa akiota ndoto zile.Aliamini ipo siku atamsaidia baba yake na kurudisha furaha kwenye familia yao.

    Alitembea taratibu kwenye korido za shule na kushika njia kuelekea ofisini kwa mwalimu Ngeze,alifungua mlango taratibu na kumkuta mwalimu Ngeze akiongea na binti mmoja ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa shuleni hapo "Gerald! subiri kidogo nje" Gerald alirudisha mlango taratibu "hayo mambo yanawapata wasichana wengi...." aliweza kusikia maneno hayo kutoka kwa mwalimu Ngeze akimwambia binti yule.Alikaa juu ya benchi refu lililokuwa pembeni kidogo na mlango was ofisini akisubiri zamu yake ya kuingia.Baada ya muda mlango wa ofisi ulifunguliwa na binti yile alitoka huku akiwa analia na kuondoka kwa haraka,Gerald alisimama na kumtazama binti yule kwa mshangao na kisha akageuka na kuingia ofisini "siku nyingine kwenye ofisi yoyote unagonga kwanza ukisharuhusiwa ndio unaingia siyo unaingia tu kama chooni.Kaa chini" "samahani mwalimu alijibu Gerald na kuketi taratibu "mmmh Gerald una matatizo gani siku hizi?" "una maana gani mwalimu?" "siku hizi maendeleo yako yameshuka darasani,huudhurii vipindi na hata ukihudhuria una chelewa ,unalala darasani! vipi kuna tatizo? labda naweza kukusaidia" "hapana mwalimu sina matatizo yoyote nafikiri labda nipunguza umakini tu lakini kila kitu kipo sawa "alijibu Gerald "nasikia huwa una matatizo ya kuota ndoto za ajabu sana ambazo zinakutesa huenda hilo likawa ndio tatizo unafikiri?" "ndoto! ndoto gani hizo! sijiu chochote kuhusu ndoto kuchangia kufeli hata hivyo kila mtu anaota ndoto sidhani kama ndoto ndio chanzo cha matatizo ya watu.Kama nilivyosema mwanzo nafikiri ni umakini tu umepungua" alijibu Gerald.Mwalimu Ngeze alitabasamu na kumuangalia Gerald usoni "haya kama umesema hakuna tatizo ni vizuri zaidi ila kama ulivyosema ongeza umakini katika masomo suala la kuchelewa vipindi halikusaidii jitahidi kuwahi maana unakuwa unapitwa na vingi........" mwalimu Ngeze aliongea vingi kumshauri Gerald kuhusu kupandisha matokeo yake na kumruhusu aende.

    Aliingia darasani huku begi lake likiwa mgongoni kelele nyingi darasani ziliashiria hakukuwa na kipindi kwa muda ule,alielekea moja kwa moja kwenye meza yake ambapo alimkuta Kylie akiwa makini sana kujisomea kiasi cha kutotambua uwepo wake "hey" "oh! hey! umechelewa tena!" "nilikuwa oifisini kwa mwalimu Ngeze alikuwa akinisema kuhusu matokeo yangu.Vipi unasoma nini?" "chemistry nafanya maswali kadhaa" alijibu Kylie "je unajua Agness amepata matatizo gani au kapatwa na nini?" "Agness! hapana kwa nini unauliza hivyo!" "alikuwa ofisini kwa Ngeze baada ya muda akawa ametoka analia,nafikiri labda amepatwa na tatizo" "kwa kweli sijajua nitajaribu kumchunguza na kumuuliza" alijibu Kylie kwa mashaka.Gerald alitoa madaftari yake na kuyaweka juu ya meza na kusoma taratibu lakini kila Mara alipoteza umakini na kuonekana kuzama kwenye dimbwi kubwa la mawazo "uko sawa kweli!" "yah niko sawa nilikuwa nafikiria maneno ya mwalimu Ngeze.Vipi umezungumza na Paul?" "ndio niliongea naye Jana nilienda mpaka kwao sema nilimkuta anaunwa sana" "aisee! kwa hiyo atakosa mazoezi leo!" "aliniambia atakuja nimejaribu kimkataza lakini hataki anapenda sana rugby" aliongea Kylie huku akiendelea kuandika juu ya daftari lake "vipi utakuwa mazoezini leo?" aliuliza Kylie "ndio,unataka uje kuniangalia!" "mmmh kwa nini nikuangalie yaani niache kumuangalia Paul nije kukuangalia wewe" "najua huwa unaniangaliaga hilo halina ubishi" aliongea Gerald huku akimtazama Kylie usoni,Kylie alitabasamu na kushika mkono wa Gerald taratibu huku akimuangalia usoni.Wote wakicheka kidogo huku sura zao zikionyeshana upendo mkubwa katikati yao.

    Baada ya masaa mengi ya vipindi daraaani kengele iligongwa kwa sauti ya juu kuashiria kuwa vipindi kwa Siku hiyo jioni vilikuwa vimekwisha na wanafunzi waliruhusiwa kurudi majumbani kwao.Kwenye korido ndefu Gerald na Kylie walionekana wakitembea polepole huku wakizungumza,walishika njia mpaka uwanjani kwa kuwa ulikuwa ni muda wa timu kufanya mazoezi kujiandaa na michuano mikubwa ya kitaifa. Walielekea moja kwa moja mpaka mahali alipokuwa Paul akinyoosha viungo vyake "hey hun" aliita Kylie huku akimkumbatia na kumpa busu zuri mdomoni "Kylie! Gerald inakuwaje?" http://deusdeditmahunda.blogspot.com/"freshi tu,Kylie aliniambia ulikuwa unaumwa,uko poa?" "niko sawa kabisa ilikuwa ni homa tu" alijibu Paul na kuweka mkono wake juu ya bega la Kylie na kumvuta karibu yake na kumpa busu la mdomoni "I miss you babe" "mmmh I miss you too sweety" alijibu Kylie kwa sauti ya kudeka na kutia wivu mkubwa ndani ya Gerald.Gerald alitabasamu kwa mapenzi mazuri ambayo Kylie na Paul walioneshana,aligeuza shingo yake pembeni na kumuona Agness akitembea peke yake huku akiwa na mawazo mengi "Kylie Agness yule pale unafikiri unaweza kuongea naye sasa hivi?" "huh! ngoja nijaribu" aliongea Kylie na kuondoka mahali pale kumfuata Agness huku Paul na Gerald wakimsindikiza kwa macho "Agness ana tatizo gani?" aliuliza Paul" "hakuna anayejua tokea asubuhi amekuwa na mawazo na kulia nafikiri kuna tatizo kubwa litakuwa limempata" alijibu Gerald huku wakiendelea kumtazama Kylie ambaew alishaanza kuongea na Agness "utashinda mangapi Leo?" aliulia Gerald "leo sitashinda sana nataka nimuoneshe yule mpumbavu Daniel nani bora hapa,nani wa kuogopwa Midtown linapofika suala la rugby"aliongea Paul kwa msisitizo huku akimtazama Daniel kwa mbali aliyekuwa akinyoosha viungo vyake.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog