Simulizi : Mshumaa
Sehemu Ya Tano (5)
Nusu saa mbele walimaliza kula na kuendelea na maongezi mengine. Muda wote Suma alikuwa akifikiria ni jinsi gani ataliingiza lile swala lake. Alipopata nafasi akamkumbusha na kuulizia majibu yake. Shery aliingiwa na kigugumizi cha ghafla. Akainama chini kwa tafakuri asielewe amuambie nini kijana huyo.
“Lakini Suma mi sijawahi kuwa na mtu hata mara moja na sielewi nitaanzaje...” Akaikata sentensi yake asijue aiendeleze vipi.
“Najua kinachokuogopesha ni maumivu. Shery naomba nikuhakikishie kuwa mimi sipo na sitaweza kuwa kama unavyofikiria. Haki nimekupenda kweli na wala sijakutamani kwasababu nakujua ulivyo. Naijua heshima yako. Naitambua thamani yako. Sitoweza kukuumiza pindi ukinikabidhi moyo wako. Imani yako kwangu ndio nitaitumia kama kigezo cha kukupenda kweli. Elewa niongeayo Shery. Amini maneno yangu ili uniifadhi kwenye moyo wako ukiwa na amani. Nakupenda. Nakupenda kweli”
Suma aliyazungumza hayo akiwa anamuangalia binti huyo usoni akimaanisha ayasemayo. Shery aliangalia chini kisha akainua uso wake na kutazama pembeni. Hakuwa na ujasiri wa kumtazama Suma usoni hata kidogo. Akajikakamua na kumtazama akiwa anataka kusema kitu. Akashindwa na kuangalia tena pembeni. Alitabasamu na kusikitika kidogo.
“Shery..” Suma aliita na Shery akaitikia kwa mguno. “Najua nimekupa mtihani mkubwa. Lakini sasa sina budi.... Unanipenda?” Shery hakuelewa akubali ama akatae. Lakini ujasiri wa kukataa anautoa wapi? Akakubali!.
Ukurasa mpya wa mapenzi ukafunguliwa na wawili hao. Suma akafurahi baada ya ombi lake kukubaliwa na mnyange huyo mwenye kila sifa ya urembo. Furaha ikatawala kwao wote huku wakiahidiana kuto salitiana. Maongezi yaliwanogea mpaka Shery akapitisha muda wa kuwapo nyumbani kwao. Kuja kushtuka ni saa mbili usiku. Shery akachanganyikiwa si mas'hara. Muda huo ni dhahiri baba yake atakuwa amesharudi nyumbani. Je asipomkuta? Kizazaa!.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akamuharakisha Suma kuwa waondoke mahala hapo. Suma akamuelewa na kumuitia bodaboda itakayomuwahisha nyumbani kwao. Akapanda na safari ya kwenda kwao ikaanza huku akimuharakisha zaidi dereva kuwa akazane. Dakika kumi na tano zilitosha kuwafikisha. Shery akashuka kuingia ndani ya nyumba huku akiwa na hofu maana tangu ahamie hapo hakuwahi kukutwa nje na Frank hata mara moja.
Ndani ya nyumba Frank alionekana kughadhibika kwa kitendo cha Shery kutokuwapo nyumbani majira hayo. Pengine asingekuwa hivyo kama asingeongezewa maneno ya uongo na mkewe Rebeka ambaye yeye ndie muasisi wa hasira za Frank muda huo. Alikuwa akitembea huku na huko hapo sebuleni akimsubiri Shery arudi.
Shery aliingia akiwa na hofu yake na alipomuona baba yake akiwa hivyo ndio akazidi kuchanganyikiwa. Frank alimtazama kwa hasira Shery. Hakutaka kumuuliza chochote badala yake kipigo ndio kilifuatia. Rebeka alimzuia na kumuambia hiyo ni kesi endapo atamjeruhi kama si kumuua kabisa. Akatoa ushauri kuwa Shery aondoke tu hapo maana anaweza leta mimba zisizo na baba.
Frank akaacha na kuelekea chumbani kwa Shery na baada ya muda alirudi akiwa na begi kubwa la nguo. Akamtupia Shery na kumtaka aondoke nyumbani kwake. Shery aliomba msamaha huku akilia lakini ndio kwanza Frank alizidi kupambwa moto na maneno ya mkewe. Hakutaka wa kuwaza kumsikiliza Shery. Badala yake alimtaka aondoke nyumbani kwake. Alipoona Shery anagoma kuondoka. Alichomoa mkanda na kutaka kumshushia kipigo zaidi.
Unadhani Shery hakuyakumbuka yale maumivu aliyoyapata siku mbili nyuma? Hakutaka yajirudie tena. Akainuka kinyonge na kuvuta begi lake. Akamtazama kwa chuki Rebeka ambae alikuwa akicheka kwa siri. Akageuka na kutoka. Nje ya nyumba hiyo hakujua aende wapi. Akafikiria arudi kwao lakini alipokumbuka kuwa nyumba mzima waliipangisha. Akakata tamaa. Wapi aelekee kwengine? Kwa Suma ndipo alipoona chaguo sahihi kwa muda huo!.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alitoa simu yake na kumpigia. Simu iliita kisha akapokelewa. Shery akamuelezea yote yaliyomkuta mpaka kufukuzwa. Akamuambia kuwa hajui aelekee wapi majira hayo ya usiku ilhali hana sehemu nyengine ya kuenda. Labda kama angesema aende kwa nduguze wengine lakini kulikuwa na umbali mkubwa sana. Suma akamtoa hofu na kumuambia atafute usafiri kisha ampesimu dereva ili amuelekeze ni wapi atampeleka.
Shery akafanya hivyo na punde akapata usafiri wa bodaboda. Akampigia simu Suma na simu ile akampa dereva ili aelekezwe ni wapi atampeleka. Baada ya muda akarudishiwa simu yake na kutakiwa apande. Akapanda yeye na begi lake na wakaanza kuondoka mdogo mdogo mahala hapo kuelekea huko walipotakiwa wafike.
Dakika kadhaa wakafika mahala hapo na kumkuta Suma nje ya nyumba moja akiwa amesimama akiwasubiri wao. Dereva wa bodaboda akalipwa hela yake na kutembea. Kisha Suma na Shery wakaingia ndani ya nyumba hiyo ambayo Suma alikuwa amepanga chumba kimoja. Akamkaribisha ndani na baada ya muda Shery alimuelezea yote yaliyomkuta.
Suma akampa pole. Akamtazama mwilini hakuwa na majeraha makubwa. Alikuwa na alama ndogo ndogo za kichapo. Suma akataka kwenda kumtafutia chakula ila Shery alikataa na kumuambia kuwa hakuwa na njaa. Shery amani ya moyo ikamrejea tena. Siku iliyofuata alipanga kwenda kwa mchungaji wa kanisa lao walilokuwa wakisalia kwaajili ya kwenda kumuelezea matatizo yake. Siku hiyo ikaisha huku wakiwa wamelala kitanda kimoja.
* *
Siku iliyofuata Shery alienda nyumbani kwa mchungaji wao nakumuelezea kila kitu kilichotokea kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Mchungaji alimuonea huruma na kumpa pole nyingi. Maana alikuwa akimuelezea huku akilia kudhihirisha uchungu alionao. Kwakuwa siku hiyo ni Jumamosi. Siku ambayo Frank hutoka kazini mapema. Walisubiri mpaka muda saa kumi jioni ndipo mchungaji alipompigia simu Frank akimtaka afike kwake akiwa na mkewe.
Frank hakujua kama Shery alifika kwa mchungaji. Hata Rebeka hakulijua hilo. Wakajiandaa haraka haraka kutoka na heshima aliyonayo mchungaji kwao. Kisha wakaelekea huko wakiwa hawajui ni nini wameitiwa. Dakika kadhaa walifika kwenye nyumba hiyo na kushangazwa na uwepo wa Shery mahala hapo. Hapo ndipo walipojua ni nini wameitiwa. Rebeka akataka kuondoka ila alizuiwa na mchungaji maana alishajua ni nini kitafuata mahala hapo.
Macho ya Frank na Mchungaji yalikuwa yakimtazama yeye. Hakuwa na budi kukaa. Mchungaji alianza kuwasalimia kisha hapo akaingia kwenye jambo lililofanya kuwaita hapo. Akawaeleza yote aliyoelezwa na Shery. Kisha akawauliza kama kuna ukweli wowote. Wote wakawa kimya kwa aibu. Hawakujua wajibu nini. Wakabaki wakitazama chini.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Naona shetani anataka kuivuruga amani kwenye mioyo yenu. Hapana, nakosea kusema anataka bali ameshaivuruga amani na kupelekea vurumai kutokea. Lakini Mungu mwenye mamlaka yote ardhini na juu mbinguni. Atakwenda kuudhihirisha utukufu wake punde tu tutakapo muomba ateketeze na kuangamiza hila za shetani muharibifu. Hakuna kinachoshindikana chini yake maana yeye ndie mwenye mamlaka yote na alisema tusimpe nafasi shetani akatutawala hata kwa bahati mbaya. Tunakwenda kumuomba yeye ataleta majibu ya maombi yetu. Tusemeni Eimen”
Mchungaji alizungumza hayo na kuanza kushusha maombi ambayo Shery alichagiza huku Frank akishadadia kwa kiasi kidogo ikiwa Rebeka hana amani moyoni mwake. Hakupenda kitu hicho kwasababu anakumbuka alichokifanya nyuma.
Punde alianza kunguruma kama simba huku akijinyonganyoga kama nyoka aliemwagiwa mafuta ya taa. Hali ile ilizidisha maombi zaidi kwa mchungaji. Alizidi kuomba maana kile walichokuwa wakikitaka kilishaanza kuonekana. Rebeka akiwa katika hali ile ile alianza kuropoka yote aliyoyafanya nyuma. Alizungumza kwamba alienda kwa mganga ili kumuua Baba na Mama yake Shery nia yake kuu ni kutaka zile mali zao. Huku akidai kuwa angezipata kupitia kwa mumewe Frank maana na yeye pia alimroga asipinge chochote atakachoongea. Mwisho aliomba msamaha akidai anaumia sana kwa maombi hayo.
Wote waliokuwapo hapo waliyasikia yote aliyoyazungumza. Ghafla Frank alidondoka chini na kuanza kutokwa na mapovu mdomoni. Shery aliacha kuomba na kwenda kumkumbatia Baba yake huku akimlilia. Mchungaji akamzuia na kumtoa pale akimuambia kuwa amuache vile vile alivyo. Muda huo hata Rebeka pia alizimia baada ya kuropoka yote. Shery alikuwa na kazi ya kulia tu muda wote.
Mchungaji alimaliza maombi yake na kuwatazama wale watu wawili waliokuwa wamelala pale chini. Aliwatazama kwa kitambo muda huo Shery akiwa analia. Baada ya dakika kadhaa. Rebeka aliinuka pale chini. Kichwa kilikuwa kikimuuma sana. Akawatazama waliokuwa mbele yake. Aibu ikamvaa. Akajinyanyua pale chini na kutoka nje bila kuzungumza chochote. Shery na mchungaji walikuwa wakimtazama tu pasi na kumuambia chochote. Mchungaji akasikitika na kumuambia Shery waendelee na maombi.
Majira ya saa kumi na mbili za jioni. Shery na Frank walikuwa wakiingia nyumbani kwao. Ndani hawakumkuta Rebeka. Hata pale Frank alipoenda kumtazama chumbani kwao hakumkuta bali alihisi Rebeka atakuwa ameondoka. Kabati lilikuwa wazi ikiwa nguo za Rebeka hazikuwapo ndani yake kumaanisha kuwa ameondoka. Katika tazama yake alikutana na karatasi aliyoiacha juu ya kitanda. Akaitazama na kuichukua kisha akaanza kuisoma.
Alikutana na maandishi ya Rebeka aliekuwa akimuomba radhi kwa yote aliyomfanyia. Pia alimjulisha kuwa yeye ameondoka ameenda kwao. Akaongezea kuwa ni vile dini yao hairuhusu kuachana lakini angeomba Frank amuache maana hakustahili kuwa mke wake. Akaomba radhi kwa kumuulia kaka yake na shemeji yake huku yeye akimroga. Mwisho alimalizia kwa kumtakia maisha mema.
Frank aliikunja ile karatasi na kuiweka kwenye mfuko wa suruali yake. Akatoka nje na kumkuta Shery akiwa amesimama sebuleni akiwa hajui cha kufanya. Maana alifukuzwa kwenye nyumba hiyo siku iliyopita na hapo alikuja tu kwa shinikizo la Frank aliemtaka waongozane wote kuja hapo. Frank alimuomba msamaha kwa yale aliyokuwa akiyafanya na Shery akamuambia kuwa alishamsamehe maana alijua hazikuwa akili zake. Kisha akamjuza kuwa Rebeka ameondoka. Shery hakuwa na cha kujibu wa kuongezea.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku iliyofuata Frank alifunga safari mpaka nyumbani kwa kina Rebeka. Rebeka alipomuona alilia huku akimuomba msamaha. Hata hivyo waliitwa ndani na wazazi wa Rebeka kwenda kuyaongea. Huko waliyazungumza na kuyamaliza. Frank alimsamehe Rebeka na kutaka yaishe kabisa. Pamoja na kusamehewa kwa Rebeka. Pia wazazi wake walitaka abaki hapo kwa siku kadhaa ndipo atarudi nyumbani. Frank alikubali na kuwaaga wazee hao. Akaondoka akiamuacha mkewe kwa siku kadhaa ndipo arejee nyumbani kwake.
Siku hii mpya Shery aliitumia kwenda kwenye makaburi ya wazazi wake. Aliongozana na Suma kwenda huko. Huko alipofika alilia sana juu ya makaburi hayo ambayo yalikuwa karibu karibu. Mwisho aliweka mashada na Mishumaa kama ishara ya kuwatakia heri huko walipo. Kisha hapo wakaondoka.
Siku mbili zilipita ikiwa siku hizo Frank akifanya jitihada za kuvunja mkataba na wale waliopangisha kwenye nyumba ya Shery aliyoachiwa na wazazi wake. Maana alijua hata Rebeka atakaporudi nyumbani hapo. Hatokuwa na amani japokuwa Shery alishamsamehe kwa moyo mmoja. Akafanikiwa kuuvunja mkataba na watu wale na kuwarudishia pesa zao zote.
Shery akarudi katika nyumba yake rasmi huku Frank akitakakumkabidhi mpaka na kampuni iliyoachwa na mzazi wake kama urithi wake. Shery alikataa kwa kumuambia aendelee kumshikia mpaka pale atakapo maliza elimu yake. Ikawa rasmi anaishi na Suma katika nyumba yake.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku ya kwanza kulala wote katika nyumba hiyo. Ndio siku ambayo Shery aliondolewa usichana wake na Suma kwa ridhaa yake mwenyewe. Mashuka yalidhihirisha hayo pale yalipochafuka kwa damu zilizomtoka. Walijitoa kitandani na kwenda maliwatoni kwenda kujisafisha. Waliporudi wakajitupa kitandani ikiwa pia wameshapafanyia usafi mahapa hapo. Walilaliana huku wakipiga soga zao.
“Hivi Ismaili. Utanioa kweli?” Shery alimuuliza Suma.
“Kwanini unasema hivyo?” Suma nae akauliza.
“Kwasababu sisi dini zetu ni tofauti” Shery alisema. Suma alikuna kichwa baada ya kusikia maneno ya Shery. Pengine hakuwa na jibu sahihi la kumpa.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment