Search This Blog

Friday, October 28, 2022

KURASA (THE PAGES) - 1

 

     





    IMEANDIKWA NA : RAMAAH MZAHAM



    *********************************************************************************



    Simulizi : Kurasa (The Page)

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    UTANGULIZI



    Siku hiyo waliyo muijia mtoto, walikuwa ni wakali mno

    Nilijitahidi sana kupambana nao, lakini nilishindwa

    Na wakafanikiwa kuondoka na mtoto. Nilikukumbuka sana

    Mpenzi wangu ila sikuwa na jinsi. Nilichanganyikiwa

    Sikuwa na cha kufanya sasa zaidi ya kuomba angalau mawasiliano.

    Mwanzo iliwezekana, lakini baadae… Hebu funua



    “KURASA”

    *****



    Hospitali ya Taifa ya wagonjwa wa akili, Mirembe, pembeni kidogo ya mji mkuu wa Kiserikali wa Dodoma, Mgonjwa mmoja anaonekana akiwa amelala. Hakuwa amelala usingizi, bali alikuwa kajilaza kiubavu ubavu akionekana kuwa na tafakari nyingi kichwani mwake.

    Wakaingia manesi wawili wakiwa wameongozana, mmoja akiwa na umbo zuri linalovutia kuliko la mwenzie na kuanza kukabidhiana majukumu ndani ya sare zao za kazi.

    “Vipi likizo Shoga yangu?”

    “Ilikuwa ni bomba mbaya, lakini tatizo ni fupi sana best,” wakacheka huku wakigonga mikono yao na hayo ndio yalikuwa ni mazungumzo yao huku wakiendelea kupeana majukumu.

    Walimfikia mgonjwa yule aliekuwa kajilaza, Nesi anaemaliza muda wake akamueleza yule anae ingia kuwa mgonjwa yule mbele yao amepoteza kumbukumbu kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, bila kumueleza zaidi wakaendelea kwa wagonjwa wengine.

    Nyuma yao mgonjwa Yule akanyanyuka na kuenda kusimama kwenye fence ya chumba alichopo, ilikuwa ni fence ya Nondo ambazo zilikuwa ni maalum kwa sehemu yote ya hospitali ile ambayo inatibu watu wote wenye matatizo ya akili.

    Ghafla wakamsikia yule mgonjwa akiita jina la Stellah, wakatazamana na kugeuka kwa pamoja kumtazama, nae muda huo alikuwa kasimama kwenye hizo nondo akiwatazama na kupunga mkono mmoja wa kulia, hali ile iliwashangaza, hawakuitegemea kabisa, maana tangu afike pale mgonjwa huyo, hajawahi kuongea hata mara moja ila tu siku hiyo.

    Nesi wa zamu anaetoka akamwambia shosti wake kuwa hayo sasa ndio maajabu, kwani haijawahi kutokea, lakini huyo anaeingia aitwae Stella na mgonjwa huyo, wala hakujali, akamwambia nesi mwenzie wakaendelea na shughuli zao.

    Ajabu yule mgonjwa aliendelea tu kuita jina lile, Manesi wale wamezoea kuitwa majina yoyote ambayo wagonjwa wao wanayojisikia, hivyo kuitwa jina lile la Stellah, wala haikuwasumbua. Hali ile haikuishia pale, bali ikawa inaendelea hivyo hivyo kila Nesi yule anapoingia kwenye wodi ile aliyopo yule mgonjwa.

    Hali yake sasa ilionekana kupata nafuu kubwa sana, maana kila alipokuwa akipata tiba kwa Nesi yule aliekuwa akimuita Stellah, alikuwa akitulia sana, hali iliopelekea apate nafuu kwa haraka tofauti na awali. Lakini muda wote aliendelea tu kumuita yule Nesi kwa jina la Stellah.

    Jina lile halikuwa la yule Nesi, lakini hata nae sasa akajiuliza ni vipi huyu ang’ang’anie jina hili kila siku? Ikamfanya avutike kujua, huyu mgonjwa ni nani na huyo Stellah ni nani pia. Akajaribu kumuuliza jina lake, mgonjwa yule akang’ang’ania tu jina la Stellah.

    Nesi alipoona hawaelewani, akatoka na kumfungia kama kawaida kisha akaendelea kutoa huduma kwa wengine huku akilini akipanga kumchunguza kiundani mgonjwa yule ni nani na yupo pale kwa tatizo gani, kifupi aujue ukweli halisi.

    Muda ukawa unakwenda, mwezi mmoja ukakatika kila akimkaribia yule mgonjwa, anamuita jina la Stellah, alilikana wee na hatimae siku moja akamuitikia akiamini huenda ataujua ukweli wa huyo Stellah ni nani.

    Lakini wala hakuujua kupitia huyo mgonjwa ambae alionesha dalili kuwa hajui lolote kuhusu huyo Stellah na aidha ni jina tu limemuijia kichwani mwake, kitu ambacho ni kawaida sana kwa wagonjwa wa akili.

    Siku hiyo Stellah akaamua kuvunja ukimya, akaenda kwa Daktari mkuu wa hospitali na kuongea nae. Aliomba kusoma file ya mgonjwa yule, akamtajia namba na jina na kuruhusiwa.

    Alilisoma kwa dakika kama 3 tu huruma ikamuingia na hata chozi likataka kumtoka, akalifunga na kulirejesha mahala pake bila hata ya kulimaliza kulisoma, historia na chanzo cha uwepo wa mgonjwa Yule pale ndani, ilimfanya adhoofike. Jioni aliporejea nyumbani ambapo ni eneo lilelile la hospitali, alikuwa ni mpweke na mwenye mawazo mengi sana, alitamani kuwa karibu nae.

    Uamuzi aliouchukua ni kuongea na daktari siku ifuatayo. Na hicho ndio kilichotokea, alimuomba daktari amchukue yule mgonjwa na kukaa nae kwake kwani amegundua ni ndugu yake na hana tatizo kubwa sana, hivyo anaweza kumsimamia.

    Daktari alimhoji sana na aliporidhika, akamruhusu kuondoka nae kwa masharti kadhaa, likiwepo la matumizi ya dawa kwa wakati sahihi na kumfikisha kwake angalau mara moja kila wiki kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nesi alikubali na kusaini baadhi ya makaratasi aliyopaswa kusaini, daktari alimpa pole na kuruhusiwa kuondoka nae huku akimsisitiza juu ya kile alicho mwambia, Nesi na mgonjwa wake wakatoka.

    Hakuwa msumbufu kabisa,aliweza kutumia tiba kwa usahihi na kwa kuwa alikuwa nyumbani, tena kwa nesi wa ugonjwa unao msumbua, alikula chakula kinachopaswa na kwa wakati muafaka kabisa.

    Hali yake ikaanza kuimarika kwa kasi na hata kumbukumbu ikaanza kurejea taratibu mno. Bado yule Nesi hakumkimbilia kwa maswali yake ya kiudadisi, aliendelea tu kumsubiri, japo hamu ilikuwa ni kubwa sana lakini aliidhibiti.

    Siku moja mgonjwa alikuwa ndani peke yake, Nesi alikuwa nje akifua nguo zao, ghafla akasikia sauti ikipiga kelele mara moja tu kisha ikatulia. Nesi akakimbilia ndani ilipotokea sauti ile, alipoingia na kukuta kilichotokea mle ndani, hofu ikamuingia na kujishika kichwa





    Mgonjwa alikuwa kalala pembeni ya makochi, sakafuni akiwa hajitambui kabisa. Kwa sekunde kadhaa kichwa cha Stellah kiliwaza mambo mengi sana, la kwanza lilikuwa ni ule mkataba aliousaini mbele ya daktari, kuwa atamlinda mgonjwa yule kwa gharama yoyote na akishindwa amrejeshe.

    Mawazo hayakumfanya aendelee kutafuta chanzo cha ukelele ule, akamsogelea karibu zaidi na kumkagua kwa umakini ajue huenda ametereza na kuanguka ama ni kipi kilichojiri.

    Akazinduka baada ya kuona pini imechomekwa kwenye Extension ya umeme, hapo aliweza kugundua kilichotokea, mbio mbio akaanza kumpa huduma ya kwanza. Dakika 3 zilitosha kabisa kumfanya azinduke na kumtazama Nesi.

    Nesi alishukuru Mungu na kumnyanyua na kumlaza kwenye sofa, mgonjwa akatoa sauti ya chini kwa kumuita “Stella” Nesi sasa aliisha zoea kuitwa jina hilo, mara nyingi aliitika na mara chache alinyamaza.

    Lakini mwito wa muda ule ulikuwa ni wa ndani zaidi, hakuitika bali alimtazama usoni kwa upole na kuita

    “Ramaah” Mgonjwa hakuitika bali akaita tena jina la Stellah, nae hakuitika bali akamwambia

    “Ramaah mie sio Stellah” Alijibu yule Nesi huku akikaa karibu yake, kwani aliona kama kuna jicho Fulani hivi Yule mgonjwa alimuangalia na yeye Stella kutokana na uzoefu wa kazi yake alihisi kuna unafuu Fulani kwa mgonjwa wake.

    “Wewe sio Stellah? Wewe ni nani sasa?” kabla hata hajajibu, Nesi alihisi furaha ya ajabu sana moyoni, aliamini dawa zimefanya kazi na ule umeme uliomzimisha umesaidia kumrejeshea kumbukumbu yake.

    Mgonjwa akanyanyuka na kuketi.

    “Mimi naitwa Scholler, wewe unaitwa nani?” akamuuliza swali ili kumjaribu

    “Wewe unasema jina lako Scholler, sio Stellah... sawa, nami sasa jina langu nani?” hakuweza kulikumbuka jina lake mapema.

    Alijitahidi sana kuvuta kumbukumbu, lakini ilishindikana, akasema halijui jina lake

    “Unaitwa Ramaah” akamsaidia kumkumbusha jina

    “Mimi ni Ramaah? Jina langu ni Ramaah, eti? Mh! Mbona sikumbuki sasa jina hili?” alijiuliza mwenyewe kwa sauti ambayo hata Scholler aliisikia.

    Kupitia elimu ya saikolojia aliokuwa nayo Scholler, akaona hatua ya siku hiyo inatosha, hakutaka kumchosha zaidi kwa maswali na kumbukumbu nyingi, akanyanyuka na kumpelekea maji ya kuoga, kisha alipomaliza kujiswafi akamtayarishia chakula na dawa vikafuatia na mwisho akampeleka chumbani anapolala na kumuacha huko.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Saa 9 usiku mlango wa Scholler ukagongwa, alihisi ni majambazi, lakini akajiona bwege, majambazi yagonge mlango? Hapana... au atakuwa nni Ramaah? Haiwezekani kuwa ni yeye...

    Sasa huyo mtu anaegonga mlango ni nani usiku wote huu? Akaingiwa na shaka zaidi, akahoji.

    “We nani unaegonga usiku huu?” aliuliza Scholler kwa sauti ya hofu

    “Mimi Ramaah” aliguna Scholler kutokana na jibu la Ramaah na kunyanyuka haraka haraka, akamfungulia mlango na kumuuliza vipi? Mbona usiku mnene?

    “Samahani dada... Uliniambia unaitwa nani vile?” Ramaah alisahau jina la Scholler

    “Scholler” alimjibu kifupi ili aseme sababu ya kumgongea usiku ule.

    “Enhee dada Scholler, mi nimekumbuka jina langu, mimi naitwa Ramaah Mzaham, lakini sijui hapa nilipo ni wapi, ninafanya nini na nimefikaje na nina muda gani hapa? Nimejitahidi kukumbuka, lakini nimeshindwa kabisa, ninaomba unisaidie, hilo jambo linaniumiza mno hadi nakosa usingizi,” aliongea huku akimtazama Scholler usoni.

    Akiwa na tabasamu usoni lililo zingirwa na huzuni moyoni, alikuwa akimuonea huruma sana kijana Yule, akasema

    “Masikini, Pole sana Ramaah nimefurahi kuona kwanza umekumbuka jina lako, nami nakuhakikishia utakumbuka kila kitu, lakini tu unapaswa kutulia”

    “Ndio dada Scholler, lakini...” kabla hajamaliza kuongea kile anachotaka kukisema, Scholler akamsogelea na kusema

    “Muda huu ni usiku sana Ramaah, huu sio muda rafiki kwa sisi kukaa hapa na kuzungumza, tunapaswa kulala ili kupumzisha miili na akili zetu, kesho asubuhi nitakuambia kila kitu ninachokijua kuhusu wewe, Sawa Ramaah?”

    “Hapana dada Scholler si sawa, napenda angalau hata nijue hapa nilipo ni wapi?”

    “Sawa nitakuambia hilo moja, lakini sitajibu tena swali lingine lolote hadi kesho, unakubaliana nami?” alimwambia kimtego na Ramaah akajaa vizuri tu.

    “Ndio nimekubali” alikubali haraka haraka kwa nia tu ya kutaka kujua kwani aliamini akijua tu hapo alipo huenda akajua mengi zaidi, mazingira hayo yalikuwa ni mageni kabisa kwake.

    “Hapa ni hospitali ya wagonjwa wa akili Mirembe...” Scholler hata kabla hajamaliza Ramaah akadakia

    “Dodoma..!” kwa mshangao mkubwa kisha akaendelea huku akimtazama Scholler

    “Ina maana mimi nimechanganyikiwa dada yangu?” aliuliza kwa sauti ya hofu.

    “Wewe hukuchanganyikiwa Ramaah! Hapa wanaoletwa sio wote ambao wamechanganyikiwa, wengine wanakuja na matatizo tofauti na hayo uliyokariri wewe,” alijaribu kumtoa hofu kidogo, lakini Ramaah alikuwa na maswali mengi mno,

    “Sasa kwanini mimi nipo hapa?” lakini pamoja na maswali hayo Scholler akamwambia

    “Ndio sababu nilikwambia tutaongea zaidi kesho, muda huu hautoshi, kuna mengi hapa kati yanahitaji muda Ramaah, nenda kalale kwanza,” alimwambia akimpigapiga mgongoni.

    “Sawa bhana, kesho si mbali, usiku mwema dada Scholler!” Wakaagana.

    Ramaah akaelekea chumbani kwake huku Scholler akimshindikiza kwa macho ya huruma, alipopotea machoni mwake, nae akaelekea chumbani kwake kuendelea kulala akiwa anatamani kuwahi kukucha.





    Ni alfajiri tulivu ya siku ya Jumamosi, siku ambayo huwa ni ya mapumziko kwa Scholler na huitumia kwa kufanya zile kazi kubwa kubwa ambazo alishindwa kuzifanya siku za kazi, hujidamka mapema ili kuwahi kuzimaliza kazi zake na kupumzika akiwa anajisomea riwaya mbalimbali.

    Alikuwa akiamini kwa muda ule ambao ameamka, ni lazima Ramaah atakua bado kalala, akapanga afanye kazi zake mbiombio ili wakati Ramaah anaamka akute kila kitu tayari amemaliza ndio wakae mezani ili kuongea.

    Kumbe alikuwa akijidanganya tu, Mshituko mkubwa sana aliupata mara baada ya kufungua mlamgo wa chumbani kwake na kukuta ule wa kutoka nje ukiwa wazi, alihisi itakuwa wameibiwa.

    Akaenda haraka haraka na kuchungulia nje, huku akikagua mlango kama upo salama, aliweza kumuona Ramaah kwa mbali akiwa amesimama akitazama majengo ya wafanyakazi wenziwe na Scholler.

    Ramaah nae akageuka na kuanza kurejea mlangoni aliposimama Scholler na kufika wakasalimiana kila mmoja akiwa na mshangao juu ya mwenzie kuwahi kuamka. Hakuna aliejaribu kuuliza, maana kila mmoja alihisi shauku aliyonayo yeye, na mwenzie pia ni itakuwa ni vivyo hivyo.

    Scholler alifanya kazi zake haraka haraka na hadi kutimia saa mbili asubuhi, walikuwa tayari mezani wakipata kifungua kinywa, hii ndio sehemu ambayo kila mmoja wao alikuwa akiisubiri kwa hamu kubwa sana.

    Ramaah alitaka kujua ni vipi alifika pale na alikuwa hapo kwa ajili gani, lakini bado na Scholler alitaka kujua maisha ya nyuma ya Ramaah yalikuwaje kabla ya kufika hapo.

    Kazi ya kumimina chai kwenye vikombe ilifanywa na Ramaah katika kugawana majukumu. Awali walianza kwa kunywa kimyakimya, lakini kutokana na shauku ya kutaka kujua, Ramaah akaamua kuvunja ukimyahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mh! Dada Scholler. Mimi naona huu ni muda muafaka wa wewe kunieleza ni kwanini nipo hapa na nimefikaje, naomba dada yangu usinifiche,” aliomboleza Ramaah huku akimtazama machoni.

    “Usijali kama nilivyokueleza hapo awali jina lako na hapa ulipo, hapa ulifikishwa zaidi ya miezi miwili iliopita, ukitoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako nako huko uliisha kaa zaidi ya mwezi mzima ukipata matibabu bila mafanikio”

    “Wewe umejuaje dada Scholler?” aliuliza kwa shauku

    “Ngojea kaka yangu, haya ninayo kueleza hapa ni kutoka kwenye File lako ambalo ndio lina maelezo yote haya, hivyo acha nimalize kwanza, mwisho ndio utauliza maswali, sawa?”

    “Ok! Samahani dada yangu, unaweza kuendelea”

    “Sawa, tatizo kuu lililosababishwa wewe uletwe hapa ni kupoteza kumbukumbu, maana hukuweza kukumbuka chochote hata jina lako” alikatazwa asiulize, lakini akajisahau

    “Samahani dada Scholler, lilianzaje tatizo hilo?” Scholler akatabasamu na kumjibu

    “kutokana na maelezo ya wale waliokufikisha hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ulipoteza fahamu ukiwa nyumbani kwako Ilala na kukimbizwa hospitali ya Amana palepale Ilala kabla ya kuhamishiwa Muhimbili”

    “Dah! Kwa hiyo mie kwangu ni Ilala? Mbona sipakumbuki?”

    “Kutokumbuka ndio tatizo lililokufanya wewe uwepo hapa hadi sasa Ramaah”

    “Sasa litaisha lini?” aliuliza tena huku akimtazama Scholler

    “Kwa kweli sifahamu tatizo hili litaisha lini, kwani hali uliyo nayo leo, hakuna alietegemea kama utakuwa hivi” alimjibu huku akibugia funda la chai

    Ramaah aliendelea kuvuta kumbukumbu, lakini picha ya maisha yake haikuja kabisa. Scholler sasa ndio akamuuliza kama anamjua Stella

    “Stellah.. Stellah namjua, Stellah ndio wewe, nashanga tu sasa, ni kwanini umeamua kubadili jina?”

    “Mie sio Stellah Ramaah, nimekwambia tangu awali kuwa mimi ninaitwa Scholler na hata simfahamu huyo Stellah”

    “Kama si wewe kweli, basi umefanana nae sana Stellah, jamani yupo wapi Stellah?” alijiuliza

    “Kwani ni nani huyo Stellah?” Scholler aliuliza akitegemea kupata jibu litakalompa mwanga

    “Hata sikumbuki” jibu la Ramaah lilitaka kumchekesha Scholler, akajizuia kwa kumuuliza kama amnaikumbuka kazi aliokuwa akifanya hapo awali.

    Ramaah akakanusha kuwahi kufanya kazi, maana alisema yeye hajawahi kufanya kazi yoyote

    “Ramaah Mzaham Jr, wewe ni daktari bingwa wa magonjwa ya mlipuko na uchunguzi wa vifo, ni mwajiriwa wa jeshi la wananchi wa Tanzania..” hapo hapo akamkatiza Scholler

    “Baas basi basi nimekumbuka..” akanyanyuka na kuzunguka huku na kule, akaendelea

    “basi nimekumbuka, dada Scholler nimekumbuka kila kitu, mama yangu wee” akajishika kichwa.

    “Umekumbuka nini Ramaah?” Shauku ilihamia kwa Scholler sasa, alisimama kumfuata

    “Kila kilichotokea, tangu mwamzo hadi kupoteza fahamu..”

    “Nielezee Ramaah”

    “Ni story ndefu sana dada yangu..” huku akitikisa kichwa “..mama yangu wee.. Stellah”

    “Stellah ni mama yako?”

    “Hapana, Stellah si mama yangu, bali yeye ndio chanzo cha yote haya, dah! Amenitoa kabisa katika huu ulimwengu kwa kipindi kirefu sana nikiwa hata sijielewi masikini ya Mungu, hebu tazama, Duniani sikuwepo wala Akhera sikufika, madhila makubwa amenipa yule Ibilisi, basi bwana midhali nimepona!”

    Machozi yalikuwa yakimtoka Ramaah tokana na kumbukumbu kumjia kichwani mwake, Scholler akampoza kwa kumpa moyo na kumtoa chuki na hasira iliokuwa ikijionesha dhahiri usoni. Akamuomba amueleze kisa kamili, si unajua raha ya maongezi? Ni kutazamana…





    Waliondoka hadi sebuleni na kuketi kwenye sofa wakitazamana huku pembeni kukiwa na stuli walioitumia kwa kuweka vikombe vyao vya chai kisha Ramaah akaanza kuelezea kilichotokea wakiwa wanatazamana na Scholler.

    Nilizaliwa miaka 30 iliopita huko mkoani Arusha na kusoma elimu tangu ya awali hadi sekondari huko huko, wakati tukisubiri matokeo wazazi wakapata uhamisho na kuelekea Tabora kisha elimu ya juu nikaisomea huko Jijini Dar Es Salaam kisha nikaenda nchini Urusi kusomea udaktari wa binaadamu, nikizama zaidi katika uchunguzi wa vifo na magonjwa ya mlipuko.

    Nilirejea nyumbani nikiwa tayari ni daktari na kuajiriwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, japokuwa nilitakiwa sehemu mbalimbali za watu binafsi, yakiwepo mashirika na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi, lakini nikaamua kulipa fadhila kwa wananchi wanaolipa kodi na kupitia hizo kodi zao ndio mie nimeweza kusoma bila kukwama ada wala nauli kwa kipindi cha miaka mitano.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitengo changu kikawa ni pale hospitali ya Amana, Ilala. Nikawa ninawajibika ipasavyo bila kutegemea mtu wala nini bali nilijituma mwenyewe hadi nikapewa ukuu wa kitengo nilichokuwepo.

    Kawaida binaadamu hujitafutia furaha yeye mwenyewe wala hailetwi na mtu, nikatoka siku moja ili kuyapa haki yake macho ya kuona viumbe wazuri, majengo marefu, Ardhi yetu yenye wasaa na kila kinachopaswa kuonekana.

    Nikatoka na kuelekea huko maeneo ya Ukonga madafu kwa dada yangu. Wakati narejea nilipofika kwenye kona ya TAZARA, taa nyekundu zikawaka.

    Hivyo hazikuniruhusu mie kuvuka, nikalazimika kusimama. Pembeni yangu ikaja na kusimama gari ndogo aina ya Toyota Nadya, nakumbuka gadi rangi yake ilikuwa ni ya Silver.

    Kikateremshwa kidogokidogo kioo cha dereva huku mie nikitazama, maana gari yake aliekuwa akishusha kioo na ile yangu, zilikuwa zinalingana kimo, hivyo karibu kila kitu ambacho angekifanya kwa umbali ule niliokuwepo basi ningekiona.

    Nikakutanisha macho na kiumbe mmoja wa ukweli sana. Alikuwa kavaa miwani nyeusi na kapelo nyeusi kaiweka upande, masikioni kaweka Earphone.

    Alianza yeye kunipungia mkono mara tulipokutanisha macho kwa kunitikisia vidole vya mkono wa kulia, mie nikatabasamu na kutikisa kichwa kumkubalia salamu yake, kisha akanipa ishara ya kutaka kuingia upande niliopo mie, yaani nae alitaka kuelekea Mandela Road.

    Nikatikisa kichwa kwa mara nyingine nae akaonyesha dole gumba kuashiria kukubaliana nami, taa ziliporuhusu akaingia upande wangu na kuendelea na safari. Nilipenda jinsi alivyo na hasa mambo yake, alionyesha anajiamini mno, nami hayo ni maradhi yangu. Hupenda sana binti anaejiamini tofauti na binti ambae anataka aongozwe kwa kila jambo.

    Hadi namuona siku hiyo licha ya mke sikuwa hata na mchumba, akanivutia na nikaamua kumfuatilia nikidhamiria kwenda nae hata kama ni Morogoro, safari zangu zote zikawa zimeishia pale na kuanza safari mpya ya kumfuatilia aendapo mrembo yule.

    Tuliingia Mandela Road na kukatisha Uhuru hadi maeneo ya Karume, pale alipaki gari na kuingia kwenye duka la sonara, nami nikafanya hivyo pia, ila wakati mie naingia nikakuta tayari yeye ameisha hudumiwa na muda ule alikuwa akilipa pesa.

    Akiwa anatoka kama mtu aliekumbuka kitu, akarudi hadi sehemu zilipowekwa pete, nikaamua kumsogelea maana eneo lile alikuwa peke yake, nikaona hii ndio nafasi muafaka kwangu. Nikamsalimia, nae aliitika vizuri tu, nikajitambulisha, akashukuru na kunipa mkono.

    Muda wote huo nilitegemea nae atajitambulisha kwangu, lakini haikuwa hivyo, bali akamuita muhudumu na kumuuliza bei ya pete iliokuwepo mbele yetu. Muhudumu alimtajia bei kubwa sana iliyotushangaza wote pale, tukajikuta hata tumetazamana, nikarejesha jicho kwa muuzaji na mie nikamuuliza mbona bei ni ghali sana?

    Jibu lake likawa ni kwamba, pete ile ni ya dhahabu, kito chake ni cha Tanzanite na imezungukwa na vipande vidogo vidogo vya Almasi.

    “Ukitazama kwa haraka haraka kaka utagundua kuwa ni haki yake kuuzwa bei hiyo,” Kipindi hicho yule binti alikuwa ameijaribu mkononi na ilimpendeza sana, ilikuwa ni pete ya uchumba lakini ilileta umbo kama la mlima Kilimanjaro, kifupi ilikuwa ni nzuri sana hasa ikivaliwa na msichana mwenye vidole virefu na vyembamba kama vya huyo mrembo.

    Akaivua na kuirejesha mahali pake, kitendo kilichomfanya Muhudumu amuulize kulikoni? Binti akajibu kuwa amepungukiwa pesa na ataiijia siku nyingine atakapokuwa amekamilisha kiwango cha pesa kinacho hitajika, kwani hata nae pia kaipenda.

    Hapo hapo nami nikaingilia kati nikaomba kudhamini pambano na kusema nitaongezea kiasi chochote kilichopungua. Muuzaji alitikisa kichwa akiamini sasa atafanya bishara.

    Akaitoa tena mahali pale alipokuwa ameiweka, lakini binti akamzuia na kushukuru. Sikuridhika, nikamwambia muuzaji ampatie tu kama vipi nitailipia kabisa pesa yote.

    Wakati mie nikiwa na shughulika na kutoa pesa ili kulipa, Muhudumu nae alikuwa akisafisha ile pete na kibox chake pia ili kuiweka pete mahala pake kabla hajamkabidhi yule mrembo.

    Akanipa kwanza mie ile pete baada ya kuilipia, nikaanza kumuangaza mle ndani sikufanikiwa kumuona, muhudumu akaja kunisaidia, wapi hatukumuona hadi pale tulipotazama dirishani na kumuona akipotelea mbele akiwa garini, nikatoka haraka ili kumuwahi, lakini sikufanikiwa kumuona alipoelekea.





    Zikapita siku 3 hivi bila kumuona, nikakata tamaa ya kumuona, nikaamini sitamuona tena hasa baada ya kufika kwa sonara kumuulizia, akasema hajamuona. Nikarudi nyumbani kwangu kuendelea na kazi zangu, ila pete ile sikuitoa garini.

    Siku hiyo nilipita kwa yule sonara ikiwa ni kama mwezi hivi tangu niinunue ile pete, nikaenda kwa jamaa alie nihudumia siku ile ya kwanza. Alinikumbuka baada ya kujitambulisha, nikamuuliza kama aliwahi kumuona tena yule binti pale.

    Roho iliniuma hasa pale aliponiambia aliijia pete ile wiki iliofuata na kuikosa, nae alisikitika baada ya kuambiwa mie niliinunua, hata alipoonyeshwa nyingine hazikumridhisha, akaondoka bila kununua chochote.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilitikisa kichwa na kumpa maelekezo muhudumu yule kuwa siku yeyote atakayotokea tena pale, ampe business card yangu ambayo nitamuachia na kusisitiza kuwa ile pete ninayo na sina mpango wa kuitumia, mwambie nilinunua kwa ajili yake yeye tu, akakubali na nikampa kifuta jasho ili asisahau, mie nikaondoka.

    Sikupata ujumbe mfupi wala simu siku ile na mwezi wote ule, nilipita kwenye lile duka hadi wakanizoea sasa, nikawa nikifika tu wananiita hadi kwa jina, maana tayari kama ni ‘Member’ basi ningekuwa na kadi ya ‘Plutnums’ nikakata tamaa ya kumuona tena yule mrembo.

    Nikajiwekea ahadi kuwa ile Pete sitaiuza wala kuigawa kwa mtu mwingine yeyote tofauti na mrembo huyo bali nitamvalisha yeyote nitakae mpenda na nitafurahi sana kama itamtosha.

    Huyo ambae Pete hiyo itamtosha, basi ndio atakuwa mchumba wangu na ndio atakae kuwa mama wa watoto wangu. Ndio rasmi sasa siku hiyo nikaitoa garini na kuiweka kwenye kabati yangu ya nguo.

    Hiyo ilikuwa ni ishara ya kwanza kuonesha kuwa nimekubali matokeo, matokeo kuwa sitaweza kumuona tena mrembo Yule ambae aliutikisa moyo wangu mara tu baada ya kumuona.

    **********



    Siku moja ya kazi nikiwa ofisini kwangu asubuhi sina mawazo kabisa na binti yule, kwani niliisha kata tamaa kabisa ya kumtia machoni kwa mara nyingine, nikiwa natazama Televisheni ya Taifa, kukawa na habari moja nyeti ya mauaji ya Mwanamama.

    Mwanamama huyo alie uawa maeneo ya Buguruni aliwahi kuwa na cheo kikubwa sana ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa kabla hajastaafu, nikiwa nasikiliza kwa makini chanzo cha tukio lile, mlango wangu ukagongwa. Nikamruhusu aliegonga aingie ndani.

    Siku hiyo hapakuwa na kazi nyingi, hivyo muda mrefu niliutumia kupitia vitabu vyangu vya uuguzi ili kuendelea kujifunza mengi zaidi nikiamini kwamba kuna mengi mno ya kujifunza bado.

    Hamadi! Pasina kutegemea wakaingia watu wa3 nikasalimiana nao na kuwapa viti. Kati ya wale walioingia, mmoja alikuwa ni msichana na wawili walikuwa ni wanaume. Huyo msichana sasa, ndio alikuwa na kila dalili kuwa mimi ninamtambua lakini sikujua nilikutana nae ama kumuona wapi

    Nikaamua ngoja nisubiri, huenda nikakumbuka, maana Dunia hii ina watu kama macho, wamefana sana, yule msichana ndio akawa mtambulishaji wao

    ‘Sisi ni maafisa wa upelelezi kutoka Ofisi ya Upelelezi makao makuu, mie naitwa Inspector Stellah na hawa wawili ni maafisa wasaidizi” alimaliza huku akinitazama mie

    “Nashukuru Inspector Stellah mimi naitwa Daktari Ramaah Mzaham, karibuni sana” alionekana kushtuka kwa mbali sana, sikujali mie nikaendelea

    “Nipo Idara ya Uchunguzi kama Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi wa magonjwa ya mlipuko na vifo, sijui niwasaidie nini?”

    “Tunashukuru sana daktari, Eeeenh kilichotufikisha hapa kwako, nafikiri tayari utakuwa una fununu, maana tumekuta unatazama habari hiyohiyo”

    “Naam nimefungua Televisheni ya Taifa na kukuta habari ya mauaji ya Kanali mstaafu wa Jeshi la kujenga Taifa, sijui nipo sahihi?”

    “Swadakta, na hiyo ndio sababu iliyotuleta kwako, kifupi tumeleta maiti ili kuifanyia uchunguzi zaidi, sasa tunahitaji kauli yako, ni lini tunaweza kupata jibu la uchunguzi utakao fanya?”

    “Eeer, uchunguzi huchukua kati ya masaa 48 hadi 72, hivyo kwa uhakika njooni baada ya siku 3, ila maiti yenu mnaweza kuiijia hata kesho ili mfanye utaratibu wa mazishi”

    “Hapana daktari, jitahidi iwe chini ya hapo maana tayari jeshi la Wananchi wanataka uchunguzi uanze mara moja”

    “Sawa nitajitahidi kuanza haraka kufanya uchunguzi”

    “Tunashukuru sana Daktari” wakapeana mikono na kuagana

    Wakiwa wanatoka, Stellah alikuwa ndio wa kwanza kutoka akifuatiwa na wasaidizi wake, nikamuita na kumwambia nahitaji mawasiliano, hivyo anipe namba ya simu huku mie nikitoa ya kwangu. Yangu akaipokea na kumpa msaidizi wake kisha akatoa kalamu na karatasi, akaniandikia simu ya mezani huko ofisini kwake na kuahidi kunipigia.

    Sikupenda tabia yake, maana mie sikuwa nataka simu ya ofisini bali nilitaka namba ya simu yake. Nafikiri hata nae aligundua kuwa sijaridhika na kitendo chake, maana alimwambia msaidizi wake akifika ofisini ampe ile Business Card yangu, wakatoka

    Nikapatwa na hasira, nikaichukua na kuichana ile karatasi kisha nikaelekea chumba cha upasuaji ili kuifanyia uchunguzi maiti ile. Kwa kusaidiana na wenzangu tuliweza kufanikisha uchunguzi wa awali uliosababisha kifo cha mwanamama yule. Tuliondoka sa 8 usiku kila mmoja akielekea kwake

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Siku iliyofuata mapema sana nilijidamka na kuingia ofisini, lakini hadi naanza kuhudumia wagonjwa saa mbili asubuhi, Sikuwa nimemuona askari yeyote kati ya wale waliokuja siku iliopita.

    Saa 4 asubuhi Stellah ndio alifika ofisini kwangu akiwa kikazi zaidi, alionesha sura ya kazi yenye wasiwasi. Nilimkaribisha na kumpa majibu yao kama walivyohitaji, alielewa vizuri na kunipongeza kwa kazi nzuri akisema nimewapa mwanga mkubwa

    Aliniaga na sikumuacha atoke burebure bali nilimtwanga swali kama ananikumbuka. Akasema tangu siku iliyopita alipoingia pale ofisini alinitambua, alikumbuka jina na hata sura japo hakumbuki aliniona wapi. Nilitabasamu na kumkumbusha ni wapi tulionana mi nae.

    Nae sasa alikumbuka na kutabasamu, lakini lilikuwa ni tabasamu la kuomba aruhusiwe kuondoka kwa amani, maana ilikuwa ni kama namchelewesha tu kwenda kwenye safari zake.

    Bahati nzuri niligundua kabla hajasema, maana masomo ya Saikolojia ni moja kati ya masomo niliofaulu kwa kiwango cha juu, nikaamua sasa nimuombe anipe namba yake ya simu. Akasema tayari aliisha nipa

    Nami nikajitetea kuwa aliyonipa awali ilikuwa ni namba ya simu ya ofisini ila kwa sasa mimi siihitaji tena kwani sina tena kazi nae ya kiofisi. Akaniuliza nataka ipi? Nikamwambia nataka namba yake ya simu ya mkononi.

    Alionekana kutokuwa tayari, nami pia Sikuwa tayari kumruhusu aondoke bila kuniachia namba yake, nikaamua kutumia nahau na methali za kila namna nikitaka tu langu mie litimie.

    Baada ya maongezi marefu kidogo, nikaweza kumshawishi na kunipatia namba yake, nikamuahidi kumpigia simu jioni akiwa amerudi nyumbani, akatoka haraka haraka kuwawahi wenzie ambao tayari walikuwa wametoka nje ya ofisi yangu.

    Ilikuwa ni furaha kwa upande wangu kwa kuweza kupata namba ile ya simu ambayo niliona ni kama aenipa mwangaza juu ya kile ambacho nimelenga kukipata toka kwake.

    Siku sasa nikaona haiendi kabisa, nilitamani mno jioni ifike haraka na niweze kumpigia na kuongea nae, nilichokifanya kwa muda ule kwanza, ni kujitahidi kuimeza ile namba ili hata ikitokea simu imeleta tatizo ama imepotea, basi namba hiyo niwe nayo kichwani muda wote.

    Jioni iliwadia, nami kama nilivyoahidi, nikampigia simu na simu yake iliita sana pasina kupokelewa hadi nikakata tamaa, lakini mwishoni ikielekea kwenye kukatika ndio akapokea

    “Ndio Dr. Ramaah, habari za jioni?” ile hali ya kuijua namba yangu tu ilinipa faraja

    “Nzuri Inspector Stellah, habari za kazi?” nilimjibu kwa kujiamini kutokana na kupokea simu yangu kwa kuonesha kuitambua, hiyo iliniongezea kujiamini.

    “Ni nzuri tu Doctor, ila samahani kwa sasa sipo sehemu nzuri, naomba nikupigie simu usiku kama hutajali,”

    “Ooh pole sana Inspekta, nitasubiri simu yako wala usijali,” hiyo ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuongea nae kwenye simu.

    Nilisubiri simu yake usiku mzima, nikiamini kuwa atapiga tu, lakini hakupiga nami nikajizuia kupiga kwani hatujakubaliana hivyo, makubaliano yetu yalionesha kwamba ni yeye ndio atakaepiga na katu si mimi, nikasimamia hapo japo ni mimi ndio nilikuwa na shida kuliko yeye.

    Siku iliyofuatia nayo ikapita kimya, si asubuhi wala mchana, mpaka usiku nilikuwa sitaki kuiacha simu umbali hata wa mita tatu, ikaisha siku ya pili hali ikiwa ni ileile.

    Hadi mchana wa siku ya 3 ndio Stellah akanipigia na kunitaka radhi akisema alikuwa anakumbuka kwamba aliniahidi kunipigia lakini alibanwa sana na majukumu ya kikazi kwani kazi ni nyingi nao wapo wachache.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimwambia asijali na nikatumia muda ule kumuelezea hisia zangu. Nilimueleza ni jinsi gani najisikia kwake tangu siku ya kwanza nilipomuona na jinsi gani nimeteseka tulipo potezana siku ile kwa sonara hadi hapo tulipoonana tena ofisini kwangu.

    Haikuwa kazi rahisi kumshawishi Stellah awe mpenzi wangu, siku hiyo niliongea kwenye simu hadi nikafikia hatua ya kukopa maneno, lakini hakunielewa. Nilipomaliza kuongea yangu akaniaga kwa kunitakia siku njema.

    Unajua kuchoka? Basi mie nilichoka siku ile, nikalaza kiti cha gari na kuanza kumfikiria, akili ikanituma nimpigie simu, lakini moyo ukanizuia, nikaacha na kuelekea nyumbani kujipumzisha.

    Sikukata tamaa, nikaendeleza mashambulizi ya chini chini, kwa kipindi hicho sikuwahi kupenda kama nilivyompenda Stellah, hivyo kila mwanamke alie nisogelea nilimuona kama maiti tu, sipaswi kuwa nae, kibaya zaidi wengi wakawa wanajileta tu.

    Ila kwa kuwa nilikuwa nimeamua mwenyewe, sikulegeza msimamo, si unajua kuwa moyo ukiamua kitu, hakuna wa kuuzuia.

    **********



    Siku moja ya kazi, nikiwa ndio nimeripoti tu asubuhi, binti mmoja mzuri sana alikuja ofisini kwangu na kujitambulisha kwa jina la Eva. Dalili zilijionesha kuwa hakuwa mgonjwa, nilihisi atakuwa na tatizo binafsi.

    Nikamuuliza kama naweza kumsaidia kile ambacho kimemsababisha awepo pale, alitikisa kichwa kukataa kuwa hahitaji msaada bali akatabasamu na kuniambia ananipenda na amejitahidi sana kujizuia lakini sasa ameshindwa.

    Nilimshangaa mno, ni wapi amepata ujasiri huo wa kuweza kunichana live kitu ambacho ni vigumu mno kwa wasichana kukifanya, akajitetea kwamba ni upendo wake wa dhati kwangu ndio umemuongoza.





    Nilimshukuru na kumwambia hata Mungu Mwenezi ameagiza upendo, kisha nikamwambia nimemsikia na sasa anaweza tu kwenda, muda ule kweli aliondoka na kuniahidi atarudi, mie sikujali.

    Usiku akaniibukia nyumbani, sasa nikamchana kwa kumwambia ana bahati mbaya maana tayari nina mpenzi, akatoka huku akitukana sana, sikujali mie nilicheka tu, maana mie nilikuwa na langu rohoni, mengine waka hayakunisumbua.

    Akili yangu iliisha zama kwa Stellah, hakika sikuona mwanamke mwingine yeyote. Asubuhi moja ya mwisho wa wiki, nikiwa hotelini nakunywa chai, hapo wastani ni kama miezi mi3 imekatika tangu kumfuatilia Stellah na bado sijausoma msimamo wake, nikamtumia sms nikimuuliza alipo.

    Akaniambia yupo kazini kwake, nikamuomba aje tupate kifungua kinywa, akaniambia ana kazi nyingi, sikuongeza neno lolote bali nilirudisha simu yangu mfukoni nikafanya yangu, nilipomaliza nikatoka kurejea ofisini kwangu.

    Saa saba mchana nikiwa katikati ya Jiji simu yangu ikaita, alikuwa ni Inspector Stellah, nikajiuliza kabla sijapokea, sijui ana lipi muda huu, kisha ndio nikapokea. Ajabu baada ya kupokea akaniomba kama nina muda tukutane Jamaa Fast Food eneo la Posta muda ule.

    Nilimpa dakika 10 tu, maana sikujua alikuwa na lipi. Nilifika baada ya dakika chache na kuketi usawa wa lango kuu la kuingilia ili niweze kumuona wakati akiingia, kwani mle ndani sikumuona baada ya kumtafuta kwa macho.

    Nae hakuchelewa, dakika 2 zilizofuata tangu mimi kuwasili mle ndani, akawa amewasili na kuungana nami mezani, aliponikaribia nilinyanyuka na kumpokea kisha nikamvutia kiti na kumuomba akae, kama mimi vile ndio mwenyeji ilhali ni mimi ndio niliekaribishwa kutokana na wito wake.

    Alikuja muhudumu na mimi nikaanza kuagizia chakula, niliagiza wali wa kukaanga na samaki wa kupaka, nae akaagiza Chips Samaki na juice ya Parachichi, sikutaka kupoteza muda sana, nikajidai nami nina shughuli nyingi sana na muda hauniruhusu mie kukaa sana, nikamuuliza sababu ya wito ule.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaniambia ameridhishwa na tabia yangu hivyo amekubali niwe mpenzi wake. Nikashangaa na kumuhoji ameridhishwa vipi na tabia yangu na wakati mie naye hatujawahi kuwa karibu hata kwa nusu saa, sasa hiyo tabia yangu ilio mridhisha yeye kaijulia wapi?

    Leo hakuwa na sura ya kikazi, alikuja na sura ya binti mrembo kama yule nilie muona siku ya kwanza na ama kumzidi yule kidogo. Huku akitabasamu akaniambia yeye ni askari tena mpelelezi, hivyo tangu ile siku ya kwanza kumtongoza, amekuwa akinifuatilia nyendo zangu kwa ukaribu.

    “Hata name sikuwa kwenye uhusiano kwa kipindi hiki, hivyo nilihisi wewe umenipenda tangu siku ya kwanza kule kwa Sonara, sasa tulipokutana mara ya pili ndio nikathibitisha kwa kufanya baadhi ya mambo ili nione matokeo yake baada ya kufanya vitu ambavyo vitakukera,”

    “Kama vipi mfano?’

    “Pale ulipo omba namba ya simu na nikakupa ya mezani, pia kutokukupigia simu japo niliahidi, mfano huo,” akanyanyua juisi yake na kupiga funda kadhaa huku akinipa name wasaa wa kutafakari aliyo yasema.

    Kilicho nishangaza ni kuwa hata Eva eti alikuwa ni mtego toka kwa yeye Stellah, nilimtazama kwa jicho la udadisi huku mapigo ya moyo yakipiga kwa kasi zaidi na kumuuliza ni wapi alimtoa yule binti machachari.

    Akaniambia yule binti wapo nae ofisini kwake na kwa kupitia uzuri wake, ameweza kuwasaidia mambo mengi na kufanya kuwa na mafanikio na hata kwangu aliamini kama nimemtamani yeye basi kwa Eva sitaweza kuchomoka. kitu ambacho hakujua kuwa mie yeye sikumtamani umbo, bali nilipenda jinsi alivyo.

    Nilicheka na kumjulisha hilo na kumwambia huo ndio msimamo wangu na katu haubadiliki. Alitikisa kichwa na kusema ameamini ila tunapaswa kwenda kupima afya zetu kabla ya suala lolote hapa kati kutokea, mie tena nikakubali kwa roho nyeupe, yaani kiroho swaafi.

    “Kama unaweza kuwa na muda tunaweza kupima leo? Maana mimi leo nina nafasi ya kufanya hivyo,” aliposema vile ndio nikathibiti kuwa nimeipata nafasi niliyoitaka, nikamwambia nipo tayari.

    Kwa siku ileile moja tukapima afya zetu mara 3 kwa sehemu tofauti tofauti na kote tulionekana tupo safi. Ilikuwa ni furaha sana upande wangu, maana sasa ndio lilichipuka penzi jipya, penzi lilikuwa ni tamu kuzidi asali, lenye ladha tamu zaidi ya sukari na zudi kuliko mshahara.

    **********

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maisha yakawa mustarehe, tulikuwa kama damu na mwili ama majani na udongo, tulikuwa tunatenganishwa na kazi pekee lakini kila tulipotoka kwenye mihangaiko yetu ya kibinadamu, tulirudi kuwa kama saruji na mchanga kwenye zege.

    Furaha ikawa ndio sehemu ya maisha yetu, karaha ikawa ndio adui yetu namba moja, tulijali maisha na kazi zetu, hatukuwa na muda kabisa wa kufuatilia nani kafanya nini au fulani kasemaje

    Muda mwingine nilichelewa kurudi kazini ila mara nyingi zaidi Stellah ndio alichelewa kuliko mie. Kazi zake zilimlazimu wakati mwingine kurejea kati ya saa 1 magharibi au saa 2 usiku. Kwa sababu hilo suala alikuwa amenieleza tangu awali, nilikubaliana nae.

    **********







    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog