Search This Blog

Friday, October 28, 2022

HOLLY SIN (DHAMBI TAKATIFU) - 1

 

     





    IMEANDIKWA NA : AZIZ HASHIM



    *********************************************************************************



    Simulizi : The Holy Sin (Dhambi Takatifu)

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    Simulizi ya aina yake inayosisimua na kukufurahisha ... fuatilia simulizi hii kujifunza mengi na kuburudika.



    MLIO wa kengele ulisikika kutoka kwenye mnara wa kanisa kuashiria muda wa sala ya Jumapili, waumini mbalimbali wakawa wanaingia ndani ya kanisa kwa ajili ya kumuomba Mungu wao.

    Aidan, mtoto mdogo mwenye umri wa miaka sita, aliteremka kwenye gari lao lililokuwa limepaki nje ya kanisa kabla hata wazazi wake hawajateremka, akaanza kukimbia kuingia ndani.

    “Caro! Caro!” aliita Aidan huku akimkimbilia mtoto

    mwenzake, Carolina aliyekuwa ameshikwa mkono na mama yake, wakielekea ndani ya kanisa hilo. Wakakumbatiana kwa furaha na kushikana mikono, hakuna aliyekuwa na shida tena na wazazi wake.

    Urafiki wa watoto hawa waliokuwa wanasoma shule moja ya chekechekea, uliwafanya hata wazazi wao kuwa karibu kama ndugu. Siku nyingine Aidan alikuwa akilala nyumbani kwa akina Caro, Caro naye akifanya hivyohivyo kwani walikuwa wakiishi mtaa mmoja.

    Misa ilipoanza, watoto hao walitoka nje ya kanisa na kuendelea kucheza kwa furaha bila kujali kitu. Baada ya misa kuisha, wazazi wao walitoka na kuanza kusalimiana kwa furaha huku watoto wao wakiendelea kucheza.

    Baadaye wakaagana lakini Aidan hakutaka kumuacha Caro peke yake, akamng’ang’ania waondoke pamoja mpaka mama wa mtoto huyo alipokubali. Wakaondoka pamoja kwa kutumia gari la akina Aidan mpaka nyumbani kwao ambapo waliendelea kucheza kwa furaha mpaka jioni.

    Siku ziliendelea kusonga mbele, watoto hao wakizidi kushibana utafikiri wamezaliwa kwa baba na mama mmoja. Kila siku Aidan hakwenda shuleni bila kumpitia Caro na kwenda kusubiri basi la shule pamoja, vivyo hivyo kwa Caro.

    Hata walipofikisha umri wa kuanza darasa la kwanza, ilibidi wazazi wao wawatafutie shule moja ya kulipia kwani hakuna aliyekuwa tayari kukaa mbali na mwenzake. Wakaandikishwa pamoja East Africa International School, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

    Maisha yalizidi kusonga mbele huku watoto hao wakizidi kukua kimwili na kiakili, ukaribu wao ukazidi kuimarika hata wakiwa shuleni kiasi cha baadhi ya wanafunzi wenzao kuhisi walikuwa ndugu wa damu.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Miaka saba baadaye, wote walihitimu elimu ya msingi shuleni hapo na matokeo yalipotoka, walikuwa wamefaulu kwa kiwango kikubwa na kuchaguliwa kwenda shule mbili tofauti. Ilibidi wazazi wao waitane na kujadili suala hilo kwani hakuna aliyekuwa tayari kwenda kusoma mbali na mwenzake.

    Kwa kuwa familia zao zilikuwa za kitajiri, waliafikiana kwamba wawatafutie shule moja ya kulipia, wakapelekwa Maritime Secondary School ambako walianza kidato cha kwanza pamoja.

    “Caro!”?“Abee Aidan.”

    “Unajua wewe ni mzuri sana.”

    “Hahaa Aidan, acha utani wako bwana! Hivi umewaza nini mpaka kuniambia hivyo?”

    “Aah! Hapana, sijawaza chochote, nimekwambia tu.”

    “Lakini hujawahi kuniambia hata siku moja.”

    “Si ndiyo nimeanza kukwambia leo, kwa hiyo hutaki kupokea sifa zako?”

    “Haya basi ahsante,” alisema Caro kwa aibu huku akiinamisha sura yake chini. Wakaendelea kujisomea lakini Aidan alionyesha kukosa utulivu kabisa, muda mwingi akawa anamtazama Carolina usoni utafikiri ndiyo mara yake ya kwanza kumuona.

    “Aidan mbona unaniangalia sana, mwenzio nasikia aibu bwana,” alisema Caro huku akiinamisha sura yake chini kama kawaida yake, wakacheka kwa pamoja na kuendelea kujisomea.

    Hata hivyo, Aidan hakuishia hapo, aliendelea kumtazama Caro kwa jicho la wizi bila mwenyewe kujua huku akianza kuhisi hali ambayo haikuwahi kumtokea hata siku moja. Alianza kuhisi hisia za kimapenzi zikizunguka ndani ya kichwa chake na kutaka kuvuka kwenye urafiki wa kushibana waliokuwa nao tangu wakiwa wadogo.

    “Sijui nikimwambia atanielewaje? Lakini naogopa,” Aidan aliwaza wakati wakiendelea kujisomea.

    Huo ukawa mwanzo wa mateso ndani ya moyo wake kwani hakuwa na ujasiri wa kumueleza kilichokuwa ndani ya mtima wake. Kila alipotaka kufumbua mdomo wake na kumueleza Caro kilichokuwa ndani ya moyo wake, ulikuwa mzito mno.

    Siku zikazidi kusonga mbele huku akijitahidi kuonyesha kwa vitendo namna alivyokuwa anampenda na kumhitaji kwenye maisha yake. Hata hivyo, kila alichokuwa anakifanya kwa Caro, msichana huyo alikuwa akichukulia kama ni upendo wa kawaida waliozoeshana tangu wakiwa wadogo.

    Kwa kadiri alivyokuwa anazidi kuwa mkubwa ndivyo Caro alivyozidi kupendeza. Uzuri wake wa asili, rangi ya ‘keki’ aliyojaliwa, tabasamu pana lililoupamba uso wake kila mara, umbo lake lililojengeka vizuri na ‘vifuu’ vilivyochomoza kifuani kwake kama michongoma, zilikuwa ni sifa zilizofanya karibu kila mtu atamani kuwa karibu na Caro.

    Hata hivyo, wavulana wengi shuleni pale hawakupata hata nafasi ya kumsogelea kwani kila mara Aidan alikuwa pembeni yake. Kijana huyo naye aliendelea kuteseka ndani ya moyo wake kutokana na kushindwa kueleza kilichokuwa ndani ya moyo wake.

    Kitu pekee alichoweza kukifanya kila siku ni kuandika katika ‘notebook’ yake jinsi alivyokuwa anampenda Caro, rafiki yake kipenzi tangu wakiwa watoto. Kila alipokuwa anakwenda, notebook hiyo ilikuwa mfukoni. Kila siku akawa anaandika jinsi anavyompenda msichana huyo mpaka kurasa zikakaribia kujaa.

    Baada ya kukaa shuleni kwa kipindi kirefu, hatimaye muda wa likizo uliwadia kwani walikuwa wakisoma shule ya bweni. Wakaanza kufungasha nguo zao kwenye mabegi yao ya kisasa, kila mmoja akiwa bwenini kwake.

    Kwa kuwa wazazi wao walikuwa wakielewana sana, walikubaliana kwamba baba yake Aidan, mzee Kenan Twalipo aende kuwachukua wote wawili kwa kutumia gari lake, jambo ambalo alilifanya. Akaendesha gari lake mpaka shuleni, Maritime Secondary School ambapo aliwakuta mwanaye Aidan na Carolina wakimsubiri kwa shauku.

    Walipomuona, walimkimbilia na aliposhuka kwenye gari walimkumbatia kwa furaha.

    “Naona maisha ya hapa shuleni yamekuwa mazuri sana, mnakua vizuri kama mapacha,” alisema mzee Kenan na kuwafanya wawili hao wacheke kwa furaha.

    Aidan akapakiza mizigo kwenye buti la gari na wakati akiendelea kufanya kazi hiyo, alichomoa notebook yake aliyokuwa akitembea nayo mfukoni na kuichomeka kwenye begi la Caro bila mwenyewe kujua. Safari ya kurudi nyumbani ikaanza.



    Wakiwa njiani, Mzee Kenan alikuwa akiwatania mambo mbalimbali, hali iliyowafanya njia nzima wawe wanacheka kwa furaha. Baada ya muda, wakawasili mtaani kwao. Ilibidi wampitishe kwanza Carolina nyumbani kwao.

    Gari liliposimama, Aidan ndiyo alikuwa wa kwanza kuteremka, akaenda kumsaidia Caro kuteremsha mizigo yake na kuiingiza ndani, wazazi wake wakatoka na kuwalaki wote wawili kwa furaha kubwa.

    Baadaye, Aidan alirudi garini na kuondoka na baba yake mpaka nyumbani kwao ambako alipokelewa kwa furaha na mama yake. Baada ya kutumia muda mrefu kusalimiana na kusimuliana yaliyotokea wakati akiwa shuleni, baadaye Aidan alienda kuoga kisha akaingia chumbani kwake kupumzika.

    Alipojilaza kitandani kwake, mawazo juu ya namna alivyokuwa akiteseka kwa penzi la Caro yalianza kujirudia ndani ya kichwa chake. Akawa anawaza mbinu nyingine atakayoitumia iwapo ile ya kumuwekea ‘diary’ kwenye begi lake itashindikana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nitakunywa pombe ili kutoa aibu kisha nitamueleza ukweli,” aliwaza Aidan akiwa amelala pale kitandani, wazo hilo akaona litafaa zaidi kwani alishawahi kusikia kwamba mtu akinywa pombe, anakuwa hana aibu hivyo anaweza kuzungumza au kufanya chochote bila hofu.

    Upande wa pili, baada ya Caro kusalimiana na wazazi wake na kusimuliana mambo mbalimbali yaliyotokea wakati akiwa shuleni, aliambiwa akaoge kisha apumzike kwani alionesha kuchoka. Akaenda bafuni kuoga kisha akarudi chumbani kwake ambapo kabla ya kupumzika, aliamua kupanga vitu vyake vizuri.

    Akafungua begi lake na kuanza kutoa nguo, vitabu, madaftari na vifaa vingine alivyotoka navyo shuleni. Wakati akiendelea na kazi hiyo, alishtuka kuona diary ambayo aliitambua haraka kuwa ni ya Aidan.

    “Ooh! Amesahau diary yake, ngoja nikipumzika nitampelekea,” Caro alijisemea kisha akaiweka juu ya droo ya kitanda chake, akaendelea kutoa vitu vyote mpaka alipomaliza, akavipanga kila kimoja sehemu yake kisha akarudi kitandani na kujilaza.

    Japokuwa alikuwa na uchovu, usingizi haukumjia haraka, akaanza kutafakari mambo mbalimbali aliyokutana nayo shuleni kwa kipindi chote alichokuwa masomoni.

    “Hivi kwa nini siku hizi Aidan ananiangalia sana usoni na kunisifia kwamba mimi ni mzuri? Kwani nimebadilika nini?” alijiuliza Caro huku akisimama na kusogea kwenye ‘dressing table’ kubwa iliyokuwa ndani ya chumba chake, akaanza kujitazama kuanzia juu hadi chini, akawa anajigeuzageuza kama mwanamitindo, mwisho akaishia kutabasamu.

    “Ana haki ya kunisifia, mimi ni mzuri kwelikweli,” alisema Caro na sura yake kupambwa na tabasamu pana, akawa anatembea taratibu kurudi kitandani kuendelea kupumzika.

    Macho yake yakatua juu ya diary (kitabu cha kumbukumbu) ya Aidan iliyokuwa juu ya droo ya kitanda chake, akaitazama kwa muda kama anayejishauri kitu, akaamua kuachana nayo na kupanda kitandani, akaukumbatia mto wake na kuendelea kujigeuzageuza huku maneno ya Aidan kumsifia yakijirudiarudia kichwani mwake.

    “Lakini hata yeye ni mzuri, mwili wake umejengeka vizuri na anavutia sana. Ngoja nimuandikie kwenye diary yake ili ije kuwa kama ‘sapraiz’ kwake siku akiiona,” aliwaza Caro na kuinuka, akachukua kalamu na ile diary ya Aidan, akarudi kitandani huku akiendelea kutabasamu, akaanza kuifungua.

    “A diary of my love to Caro!” (Kitabu cha kumbukumbu za penzi langu kwa Caro!) ulisomeka ukurasa wa kwanza wa diary hiyo, moyo wa Caro ukalipuka na mapigo yake kuanza kumwenda mbio. Alirudia kuyasoma maandishi hayo zaidi ya mara tatu akihisi kwamba huenda amekosea kusoma lakini bado hali ilikuwa ni ileile.

    Alishusha pumzi ndefu na kufungua ukurasa wa pili, alichokiona kilimfanya apigwe na butwaa akiwa ni kama hayaamini macho yake. Aidan alikuwa ameandika mambo mengi kuhusu yeye na Caro, akielezea ni jinsi gani alivyokuwa anampenda tangu wakiwa wadogo.

    “Nilimpenda kama dada yangu na rafiki tangu tukiwa wadogo, lakini sasa nahisi mawazo yangu yanabadilika kwa kasi kila kukicha. Nataka awe mpenzi wangu lakini kumwambia siwezi, nitaendelea kuteseka…” ilisomeka sehemu ya maandishi aliyokuwa ameyaandika Aidan kwenye ukurasa huo.

    Caro alifikicha macho yake akihisi huenda alikuwa ndotoni, akashusha tena pumzi ndefu na kuendelea kusoma. Alipomaliza alifungua ukurasa mwingine ambapo napo alikutana na maelezo marefu kutoka kwa Aidan akielezea jinsi alivyokuwa anampenda.

    Aliandika mambo mengi ya kumsifia huku akijiwekea nadhiri kwamba siku atakayopata ujasiri, atamweleza ukweli unaomtesa ndani ya nafsi yake. Caro aliendelea kufunua ukurasa mmoja baada ya mwingine, akakutana na mashairi ya mapenzi, sifa kemkemu na kila aina ya maneno ya kimahaba, yote yakiwa yameandikwa na Aidan maalum kwa ajili yake.

    Alijikuta akishindwa kujizua, machozi yakaanza kumlengalenga kwani ilionesha dhahiri kwamba moto mkali wa mapenzi ulikuwa ukiwaka ndani ya mtima wake kiasi cha kumfanya ateseke sana. Alijilaza kitandani huku akiendelea kupitia kurasa za diary ile, machozi yakazidi kumtoka.

    Licha ya kwamba alikuwa akimheshimu kama kaka na rafiki wa tangu utotoni, alijihisi mwenye hatia kubwa kwa kushindwa kuzielewa hisia za Aidan tangu mwanzo kiasi cha kumfanya ateseke kiasi hicho. Aliendelea kuwaza mpaka baadaye usingizi mzito ulipompitia.

    Alipozinduka, tayari ilikuwa jioni, akili zake zikamtuma kujiandaa haraka na kumfuata Aidan nyumbani kwao kwani hakupenda kuendelea kumuona akiteseka kwa sababu yake. Akaingia bafuni kuoga kisha akarudi na kuanza kujipodoa. Alichagua gauni lake zuri lililomfanya aonekane mrembo mithili ya ndege tausi. Akaongeza bashasha kwa kujipulizia marashi mazuri ya kuvutia.

    Alipohakikisha amependeza kisawasawa, alitoka kimyakimya bila hata kuaga na kwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa akina Aidan.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ooh! Karibu mrembo, karibu sana,” baba yake Aidan, mzee Kenan alimkaribisha Caro kwa bashasha, huku akiwa amevaa taulo tu. Ilionesha kwamba alikuwa ametoka kuoga muda mfupi uliopita. Akamshika mkono na kuingia naye ndani.

    “Mwenzako bado amepumzika, inaonesha amechoka sana na mama yako ametoka kidogo, jisikie huru,” alisema mzee huyo kwa uchangamfu, huku akiwa amemkazia macho Caro hasa sehemu za usoni na kifuani mpaka msichana huyo mdogo akawa anajisikia aibu. Akawa anamwagia sifa kemkemu huku akijisogeza karibu naye.





    “VIPI maisha ya shule unayaonaje?” alisema mzee Kenan huku akizidi kujisogeza kwa Caro, kwa kuwa sofa walilokuwa wamekalia lilikuwa ni la watu wawili, Caro hakuwa na ujanja zaidi ya kutulia, mapigo ya moyo wake yakawa yanamuenda kasi kwani alihisi kuna kitu kibaya kinataka kumtokea.

    “Inabidi mjitahidi kusoma kwa bidii, unajua sisi wazazi wenu tunawategemea sana,” alisema mzee Kenan, safari hii akiwa amemgusa Caro begani, taratibu akaanza kuupitisha mkono wake mgongoni kwa msichana huyo huku akijifanya kuendelea kumpa mawaidha ya kukazania masomo kwani ndiyo ufunguo wa maisha yao.

    “Kuna zawadi nzuri nilikuwa nimewaandalia, nilitaka mkirudi tu shuleni niwape, twende nikakupe wewe kwa sababu ndiyo umewahi, mwenzako nitampa baadaye,” alisema mzee Kenan huku akimuinua Caro pale kwenye sofa alipokuwa amekaa na kuanza kuelekea naye kwenye chumba cha wageni.

    Kwa jinsi Caro alivyokuwa anamheshimu mzee Kenan, alimchukulia kama baba yake kiasi kwamba alishindwa kumbishia chochote alichokisema. Huku mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio kuliko kawaida, alitii alichoambiwa na mzee Kenan.

    “Mbona unaonekana unaogopa sana, jisikie huru, unajua tayari umeshakuwa mkubwa wewe, si unajiona mwenyewe,” alisema mzee huyo na kuzigusa nido changa za msichana huyo mbichi, hali iliyomfanya apige ukelele wa mshtuko.

    “Ooh, samahani, ni bahati mbaya,” mzee Kenan alijibaraguza na kudai kwamba kitendo cha kugusa kifua cha Caro kilikuwa ni cha bahati mbaya. Caro alitingisha kichwa kuonyesha kukubaliana na mzee huyo, akaendelea kumkokota kuelekea chumba cha wageni kama kondoo anayepelekwa machinjioni.

    ***

    Aidan aliendelea kuhangaika chumbani kwake, alijitahidi kuutafuta usingizi lakini hakuupata, mawazo juu ya Caro, msichana wa ndoto zake bado yalikuwa yakiendelea kuzunguka kichwani mwake na kumfanya akose utulivu kabisa.

    Wazo alilolifikiria kwa muda mrefu, lilikuwa ni kutoka na kwenda sehemu yoyote kunakouzwa pombe kisha anywe kidogo kutoa nishai kisha amfuate Caro nyumbani kwao.

    “Nikifika nitamwambia nina mazungumzo naye, najua lazima atakubali. Tutaenda kwenye bustani ya maua kule nyuma kisha nitajikaza na kumueleza kwamba nampenda sana na nataka awe mpenzi wangu ili baadaye, nimuoe na kujenga naye familia,” aliwaza Aidan na muda huohuo, aliinuka haraka na kusimama nyuma ya kioo kikubwa kilichokuwa chumbani kwake.

    Akajinyoosha kutoa uchovu kisha akachukua taulo lake na kuanza kuelekea bafuni, alipogusa mlango wa chumba chake tu, alisikia mtu akipiga kelele za kushtuka, kwa kuwa alikuwa anamfahamu vizuri Caro, aliitambua sauti yake.

    Harakaharaka akarudi chumbani kwake na kuweka taulo sehemu yake, akavaa nguo vizuri na kujitazama kwenye kioo, akachukua marashi mazuri na kujipulizia huku akijitahidi kuvaa uso wa kujiamini. Akatoka akiwa na bashasha ya hali ya juu ya kuzungumza na Caro.

    Alipofika sebuleni, alishangaa kuuona mkoba mdogo wa Caro ukiwa kwenye sofa, viatu vyake vikiwa pembeni ya mlango. Aligeuka huku na kule lakini hakumuona, ikabidi apaze sauti na kumuita.

    “Caroo! Caroo!” lakini hakuitikiwa.

    Sauti hiyo ya Aidan ilimshtua baba yake ambaye ndiyo kwanza alikuwa akifungua mlango ili amuingize Caro kwenye chumba cha wageni, harakaharaka akamuonyeshea ishara Caro ya kutosema chochote kisha akamruhusu arudi sebuleni wakati yeye akinyata kuelekea chumbani kwake, akajifungia mlango huku akijilaumu kwa kushindwa kutimiza alichokuwa anakitaka.

    Aidan baada ya kutoitikiwa, alifungua mlango na kutoka nje akiamini atamuona Caro lakini hakukuwa na dalili zozote, akarudi ndani. Wakati anaingia, alishtuka kumuona msichana huyo mrembo akitoka upande wa chumba cha wageni, huku akionyesha kuwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimesikia kama unaniita,” Caro alisema huku akijitahidi kuificha hofu iliyokuwa ndani ya moyo wake.”

    “Ndiyo, nilikuwa nimepumzika chumbani, natoka naona viatu na mkoba wako ndiyo nikawa nakuita.”

    “Nilikuwa msalani,” alisema Caro na kukaa palepale alipokuwa amekaa awali. Kwa kuwa Caro alikuwa ameizoea sana nyumba hiyo kiasi cha kuwa mwenyeji, Aidan hakuendelea kumhoji kwani mara kwa mara alikuwa na uwezo wa kuingia ndani hapo hata kama hakuna mtu na akafanya chochote anachokitaka, kama ilivyokuwa kwa Aidan akiwa nyumbani kwa akina Caro.

    “Nilikuwa nimepumzika kwani bado nahisi uchovu wa kishuleshule,” alisema Aidan huku akikaa vizuri kwenye sofa na kuwasha runinga, wakawa wanatazama muziki huku wakiendelea na mazungumzo ya hapa na pale.

    Kwa kuwa tayari Aidan alikuwa ameshapanga mipango yake ya namna ya kumfikishia ujumbe Caro, alimuomba watoke nje na kwenda kwenye bustani za maua zilizokuwa nyuma ya nyumba yao, wakatembea taratibu huku Caro akionyesha kuwa na mawazo mengi.

    “Mbona unaonekana kama haupo sawa Caro,” alisema Aidan huku akimshika begani. Caro alitamani kumweleza kilichokuwa ndani ya moyo wake lakini aliogopa kuwagombanisha Aidan na baba yake, akaamua kuficha siri juu ya tabia mbaya aliyoionyesha baba yake. Akaamua kubadili mazungumzo.

    “Nimekuletea ‘diary’ yako uliyokuwa umeisahau kwenye begi langu,” alisema Caro huku akimtazama Aidan kwa macho yaliyokuwa na ujumbe, akaitoa diary hiyo na kumkabidhi, Aidan akahisi aibu kubwa ndani ya moyo wake kiasi cha kukwepesha macho yake.

    “Umeisoma?”

    “Hapana, wala sijaisoma,” alisema Caro huku akiachia tabasamu pana, akamkumbatia Aidan kwa nguvu, akamnong’oneza: “Pole kwa kuteseka kwa kipindi kirefu kwa ajili yangu.” Aidan alijihisi kama anapaa angani, akazidi kumkumbatia kwa nguvu. Walibaki kwenye hali hiyo kwa dakika kadhaa, Caro aliyekuwa akitazama upande wa nyumba ya akina Aidan, akashtuka baada ya kugundua kuwa kuna mtu alikuwa akiwachungulia kupitia dirishani. Alipomtazama vizuri, aligundua kuwa ni baba yake Aidan, harakaharaka akamuachia huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio kuliko kawaida.

    “Vipi Caro, mbona umeshtuka ghafla?” aliuliza Aidan kwa mshangao lakini Caro hakumjibu kitu.



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “CARO, si naongea na wewe? Mbona umeshtuka sana?”

    “Aaah! Samahani akili zangu zilikuwa mbali, unajua nimeondoka nyumbani bila kuaga sasa nahisi mama ananitafuta, ngoja nikamuage kwanza halafu nitakuja tuendelee na mazungumzo yetu,” alisema Caro huku akijitahidi kuvaa tabasamu bandia, harakaharaka akaondoka na kurudi nyumbani kwao.

    Aidan alibaki amepigwa na butwaa akiwa haelewi nini kilichombadilisha Caro, hata hivyo, alihisi labda ni aibu za kikekike na ugeni katika medani ya mapenzi ndivyo vilivyomsababishia hali ile, akatafuta sehemu nzuri na kukaa huku akiendelea kuangalia mandhari nzuri ya bustani za maua na matunda zilizotunzwa vizuri.





    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog