Simulizi : Msamaha Bila Malipo (Forgiveness Without Payment)
Sehemu Ya Nne (4)
Edo akiwa kachoka sana na mzigo wa begi la madaftari ambao aliokuwa nao begani sasa alikuwa kauhamishia bega la kulia. Alikuwa kachoka sana pia na njaa nayo ilimuangaisha tumboni maana alikuwa hana kitu ambacho alikuwa kaweka mdomoni. Yule mama ambae alikuwa muongo ajabu alipomuona Edo alimuita, “Kijana ebu njoo mara moja na maongezi kidogo na wewe” alimuita kwa sauti kubwa huku akionyesha uso wa furaha kubwa kabisa. Edo akawa anajiuliza kimoyomoyo, kwanini yule mama kamuita leo kwa furaha kubwa namna ile wakati hana hata mazoea nae hata kidogo kabisa. “lakini ebu ngoja niende yawezakana kuna kitu ambacho ni kizuri kabisa” Edo akaamua kwenda maana alisimama kwa muda mchache kisha akaenda. Moyo wake na kichwa vilimfanya awaze au ajiulize maana vilikuwa havija aafikiana kutoa jambo ambalo ni bora zidi. Edo akamsogelea vizuri kisha yule mama akampa kiti akae maana alikuwa anamaongezi ambayo ni (deep) ni marefu kidogo. Kaa baba kwanza mbona umechoka choka au una njaa mno? Alimuuliza huku akimsaidia kumuwekea mkoba chini. Edo nae hakumwambia ukweli kama ana njaa kweli.
SURA YA NANE
N
i usiku yapata kama saa mbili na nusu usiku, Sophia akiwa nyumbani pamoja na mama yake mzazi ambae kwa sasa amekuwa kichaa kabisa. Mda mwingine anakuwa hatamani hata kuvaa nguo, anaongea maneno ambayo ni magumu na hayajulikani ni lugha gani kabisa dah! Ilikuwa ni shida ndani ya familia hii kwa saasa walikuwa wanamtegemea zaidi Sophia ndipo wapate chakula. Na ile biashara yakwenda kuombaomba mjini kwa sasa alikuwa mama sphia kaiaacha kwa sababu tu ya akili kuwa mbaya. Tatizo halikujulikana ni tatizo gani. Chumbani walipokuwa wakilala ilikuwa ni harufu mbaya kweli maana alifikia hatua ya kujisaidia ndani na kutunza kinyesi uvunguni mwa kitanda. Sophia kwa sasa mshahara alikuwa analipwa mzuri na bwana Damiani ingawa alipewa kwa matusi na kejeli kubwa sana na kashifa mbaya. Lakini kwa sababu alikuwa na shida iliyokuwa nyumbani kwao aliamua kulizana na kufanya kazi hivyo hivo kwa matusi. Na mambo ya usengenyaji. Usiku huu Sophia alikuwa anapika chakula cha usiku. Mama yake muda huo yeye alikuwa anaimba nyimbo ambazo hazieleweki kabisa wala hazina kichwa wala miguu. Kipindi alichokuwa akiimba mama Sophia, Sophia aliacha kupika, machozi yakawa yanamtoka anaamuwa kuacha mpaka sufuria la ugali ambalo alikuwa katenga jikoni likawa linamwagikia mpaka chini yale maji yake. ‘jamani mimi hivi mama yangu amekuwaje sijui ni kitu gani jamani, aliongea kimoyomoyo huku machoozi yakimdondoka kwenye pua yake dah! Sophia alikuwa ni mtu wa huzuni sana. Hata awapo nyumbani au ofisini bado furaha ilikuwa haipo kwake. Alibakia kulia pale mama yake yeye aliendelea na kuimba wala hana muda na Sophia. Tumbo la Sophia lilikuwa kubwa mno kwa sasa “Sijui nitamsaidiaje mama yangu dah! Huku akiendelea kupika chakula mdogo wake Sophia ambae alikuwa mdogo kwa muda huo alikuwa kakaa pembeni mwa Sophia akijaribu kusubilia chakula. Sophia alikuwa anampenda sana mdogo wake. Usiku huo Sophia kipindi akiwa nyumbani anapika Damiani kule ofisini kwake alikuwa kabakia na Robert ambaye walikuwa nae ofisini kwa ajili ya kuandaa mambo ya kesho na kupanga mahesabu ya vitu ambavyo wameuza kwa hasara, pia faida ambayo imeingia katikak kampuni yake. Wakati wakiangalia vitu hivyo kwa umakini usiku huo, Damiani akaanzisha mada ya kumuhusu binti Sophia, Robert ndugu yangu Sophia kama unavyomuona ana mimba na mimba ni yangu kweli, damu yangu haiwezi kupotea. Alisema Damiani kwa upole. Robert akamuuliza kwani alikuwa anataka kufanya nini? Damiani akiwa ana acha kabisa kuandika kisha anamwambia Robert kuwa anataka kumuweka wazi mke wake kuwa Sophia ana mimba yeke. “Aisee kumbe Damiani na wewe sijui vipi tu yaani mwambie. Alisema Robert kwa kumshinikiza Damiani. Hapana naogopa Robert mke wangu anaweza kunifanyia kitu kibaya ana roho mbaya sana. Damiani alizidi kuchanganyikiwa zaidi. Wewe mwambie bwana atakavyochukulia sawa. Robert bado alizidi kumshinikiza Damiani lakini wanawake hawana adabu ebu acha kwanza Sophia ahangaike. http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Alisema Damiani akivua roho sasa ile ya huruma ambayo aliyokuwa nayo. Robert alikuwa ni bendera fuata upepo yeye popote alipoona. Damiani kasema huko huko aliungana nae, lakini sawa tu muache apate shida kidogo. Robert baada yakusema hivyo anatulia kumuangalia Damiani ataongea lipi. Wakati wanapanga mambo hayo ofisini mke wa Damiani alikuwa ameshaanza kujiuliza mumewe yuko wapi usiku huo wote. Anakaa ndani lakini wapi anaona hapakaliki. Yani huyu baba yenu kazini mpaka mida hii kweli leo nahisi atakuwa sio ofisini tena bali….! Alisema mwanamke huyu ambae alikuwa ngangali mno mpaka hata Damiani mwenyewe alikuwa anamuogopa sana. Dah! Alihangaika mno kuangalia nje aliposikia sauti ya gari kwa mbali alijua pengine ni bwana yake Damiani kumbe wala walikuwa watu wengine ambao waliingia majumbani kwao. Mwanamke huyo roho ilikuwa juu juu sana kwenye stuli palikuwa hapakaliki, yule mke wa damiani alikuwa ni mwanamke ambae ana wivu sana. Na pia ukiachilia mbali wivu aliokuwa nao lakini alimpenda sana Damiani ndio maana alimfanyia wivu sana. Watoto nao wakawa hawataki kwenda kulala wanadai mpaka wamuone baba yao kwanza ndipo waridhike na waende kulala. Kule ofisini Damiani machare yalianza kumcheza kuhusu hali ya kule nyumbani. Robert leo tumechelewa sana twende na gari au tukodi tax? Aliuliza daminai. Twende na gari bwana kwanini tukodi…. Wakati gari tunalo? Alisema Robert ili nae Damiani ampitishe nyumbani kwake. Damiani hakuwa na tatizo alipanda ndani ya gari kisha akawasha gari kwa ajili ya kuanza mwendo. Muda umekwenda sana bwana saa tatu na nusu” aliangalia saa yake ya mkononi Damiani “Muda umekwenda wapi; saa tatu na nusu bado sema shemeji ndie huwa anakusumbua.” Alisema bwana Robert ambae alikuwa hana tatizo wala hofu ya kuchelewa.
Kule nyumbani kwa akina Sophia muda huu sasa wanaingia kulala chumbani kwa sababu ya kule chumbani kuwa na harufu ambayo ni mbaya, Sophia aliamua kutandika sebleni chini ili alale pale kama baiskeli ama kabati ndio hukaa sebleni. Sophia alikuwa kachoka sana ata kulala tu alilala kwa kujitupa mithili ya mzigo mkubwa sana . mlango ulikuwa ni wakusukuma tu unaingia nao ndani. Kipindi Sophia akiwa kalala pale sebleni alianza kujiuliza atafanya nini mpaka maisha ayakomboe pale nyumbani kwao. Mimi mwenyewe ndo kwanza mjamzito ila Damiani basi tu mungu atanilipia” aliwaza mwenyewe hata alikosa mpaka usingizi. Alimtupia lawama zote Damiani maana ndiye aliyemharibia kila jambo kabisa. Alikuwa kapanga kusoma lakini kutokana na ujauzito wake aliamua kuhairisha kabisa maana kilikuwa ni kitu ambacho hakiwezekani kusoma wakati angali ni mjamzito maana ujauzito huwa na mambo yake ya usumbufu. Sophia aliamua kuachana nahilo jambo mpaka atakapojifungua na mtoto kukua vizuri ndipo ataanza kusoma. Pesa alikuwa anapata nahali ya chakula si mbaya kama zamani. Kwa sasa ilikuwa ni angalau kidogo ila pesa ya kufanya mambo makubwa ndio ilikuwa haipo kabisa. Damiani walipokuwa ndani ya gari, gali ilianza kama kuleta hitrafu Fulani “Mbona usukani wa gari unasumbua Robert? Alisema Damiani akiwa anajaribu kuendesha kwenda mbele zaidi. Lakini bado uskani unabana breki nazo haziendi kabisa wala hazieleweki kabisa. Damiani nguvu zinamuishia. Kutahamaki mbele kuna gari la mizigo likija kwa kasi sana. Robert yeye ndio kwanza hana hata haraka anakunywa pome tu maana kwenye gari la bwana Damiani alikuwa anaweka na pombe humohumo. Wakiwa wanaenda huku wanakunywa na pombe kidogo. “Lakini Robert unajua hapa tulipo ni pabaya tunaweza kupata lolote ambalo litasababisha ajali” alisema Damiani. Gari la mizigo nalo lilikuwa katika spidi kali, likagonga gari alilokuwemo Damiani kwa mbele, kioo cha gari la Damiani kikapasuka kwa kuingia ndani na kikamkata Damiani usoni, akatokwa na damu nyingi sana. Na Robert akawa kaisha zimia kutokana na hofu na uwoga. Yeye alichanwa mkono. Sura pia ilikuwa haitamaniki kabisa ni ya mtu au nyani alikuwa kachwanwa vibaya na vioo vya gari. Damiani ambae alikuwa anaahueni maana alikuwa bado hajazilai punde tu nae akawa kazirai kabisa hata hajitambui. Askari wa usalama ambao walikuwa doria wakawa wamewasili pale sehemu ambayo ni ya tukio. “Dah atakuwa kaumia huyo sana” alisema dereva wa gari la polisi ambae alimuangalia Robert kwa umakini. Damu kwa wote wawili zilivuja sana ingawa walikuw bado wamezilai lakini bado damu zilivuja kwa sana. Askari wale wa usalama waliamuwa kufanya mawasiliano na watu ambao wanashughulika na ambulance hospitialini ili waje kuwachukua Damiani na Robert ambao wako mahututi. (taabani). Gari lao lilikuwa upande wa mbele halitamaniki kabisa. Lilikuwa limebondeka kama sufuria la kupimia. (aluminiamu). Usukani ulikuwa umepinda, mara ambulance ikawa imewasili pale eneo la tukio dah! Wale wahudumu wa pale kwenye ile ambulance walikuwa ni watu ambao wako shapu kidogo. Waliwaingiza kwenye gari haraka haraka zaidi, na kuwa weka kwenye vitanda vya mule ndani ya ambulance kisha ambulance ikaondoka kwa mwendo wa kasi. Kumbe katika pilikapilika za kuwabeba Damiani pamoja na Robert, pochi ya Damiani ikawa imedondoka chini. Pochi hiyo ilikuwa na vitu vingi sana. Kulikuwa na kadi ya benki pamoja na pesa zilizokuwa ni za mauzo kwa siku hiyo. Pesa hizo zilikuwa ni kiasi cha Tsh. Million tatu na nusu. Baada ya ambulance kuondoka walibakia askari wa usalama katika eneo la tukio kwa ajili ya upelelezi wa kina zaidi. Katika zunguka zunguka ya kuuliza wasamaria wema waliokuwepo eneo la tukio (mashuhuda), askari mmoja ambae alikuwa kitengo cha upelelezi akaiokota ile pochi kisha akaichukua na kuanza kuangalia ndani kuona kuna nini. Ile kufunua tu Dah! Akakutana na burungutu la elfu kumi kumi, mwenzie ambae alikuwa nyuma akawa ameshtukia akajua moja kwa moja lazima kuna kitu. “Jamaa vipi tuambiane bwana mbona kimya sana” alisema askari mwenzie yule askari aliyeokota ile pochi alikuwa ni mpenda pesa sana, hivyo hakutaka kumwambia kuwa ameokoa pochi yenye pesa akawa anabisha. “Vipi wewe mbona unanishangaza mno. Aliificha ile pochi mara baada ya kuongea vile. “Aaaah! Ndugu yangu mbona tunabaniana nimekuona na ….http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Kabisa” askari yule akamuangalia kisha akamuuliza “Kwani nilichookota ni cha kwako? Wakawa wanarumbana pale hata kila mtu kati yao akashindwakufanya wajibu wake ambao ulimpeleka pale. Yule askari aliyeokota hiyo pochi alipoona mwenzie anamsumbua alihama na kwenda upande mwingine ili asiendelee kusumbuliwa kabisa.
Sophia usiku huo ambao Damiani pamoja na Robert wakiwa wamepata ajali barabarani yeye alikuwa ndio kwanza yuko usingizini akijaribu kutuliza akili yake vizuri kabisa. Nyumbani kwa bwana Damiani ndio kulikuwa na hali ya huzuni kwa mke na watoto wake wote watatu walikuwa wameshika shavu zao kwa huzuni maana ilikuwa sio kawaida kuona baba yao akachelewa mpaka mida hiyo. Dah! Watoto walileta hali ambayo ni ya huzuni zaidi. Mke wa Damiani baada ya kuona pale ndani hapafai aliamua kwenda nje kukaa kibalazani. Tena akiwa mwenyewe bila wanawe. Watoto baada ya kuona baba yao hatokezi waliamua kumsubiri na ndipo wakapitiwa usingizi hapo hapo sebuleni kwenye makochi. “Daminai amekuwaje mme wangu, simu haipatikani, au kapita na Robert kwenye mipombe.” Alijiuliza maswali bila majibu mke wa Damiani akiwa pale nje kibarazani.
Usiku huo ulikuwa tofauti kwa upande wa Edward kwani alilala na njaa kwa kosa ambalo lilikuwa halijulikani. Mke wa mdhamini wake aliamua kumfanyia hivyo makusudi kabisa. Edo alipoingia jikoni kutaka kuchukua chakula alizuiliwa na yule mama. Edo akabakia anamshangaa sana. “Lakini mama nimekosa nini ambacho mpka unaninyima chakula? Aliuliza Edo kwa lugha ya upole kabisa nay a unyenyekevu wa hali ya juu kabisa. “Eehe yaani leo kukunyima chakula ndio umediriki mpaka kuniita mama” alisema mwanamama yule ambae alikuwa akimfanyia makusudi kabisa Edo wala kulikuwa hakuja jambo wala sababu kubwa mno ya kufanya Edo anyimwe chakula. Edo alipata uzuri kabisa akumuongelesha jambo lingine kabisa sasa aliamua kwenda chumbani kwake kupumzika huku akiwa na hasira sana na yule mwanamke wa yule bwana. Wakati yote hayo yakitukia yule bwana alikuwa pembeni katulia akimwangalia tu mke wake jinsi anavyomtendea kijana Edo ambae aliondoka kwa unyonge sana na akibakia kumlaumu…
SURA YA TISA
Nhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
i asubuhi yenye kupendeza, Sophia akaingia bafuni kuonga mara baada yakuwa kamaliza kuwaandalia kila kitu pale nyumbani kwao. Ndipo akaingia kuweka mwili safi kidogo. Ilikuwa ni asubuhi ambayo ni ya kawaida sana. Sophia ukiachia umasikini aliokuwa nao alijijali sana kimavazi kiasi kwamba ungeweza kusema nyumbani kwao ni kwa thamani sana au ni pa fahari mno kumbe umalidadi waficha umaskini.Sophia alipokuwa bafuni anaoga, mke wa Damiani alikwisha fika ofisini kwa mmewe, Ama kweli mlala na mwanaume basi huona wivu kulala peke yake.
Mke wa Damiani alikuwa hana raha kabisa, nyumba aliiona kama vile si yake tena. Aliondoka nyumbani akiwa na kanga mbili moja kafunga kiunoni na nyingine alikuwa kafunga ushungi. Baada ya kufika pale ofisini aliaanza kutazama milango ya majengo yale na kugundua kwamba bado imefungwa kabisa na makufuli. “Duh! Sasa huyu Damiani kalala wapi mbona ofisi bado imefungwa? Alisimama kana kwamba anataka kupaa angani, alijiuliza maswali mengi sana hata ambayo yalikuwa hayafai kujengeka ndani ya kichwa chake. Alihisi pengine labda ni Robert ameanza kumshawishi Damiani mambo ya umalaya.
Na hilo ndilo alilokuwa akilifikiria kwa sana. Maana alimwona Robert ni mtu ambae anapenda sana umalaya kuliko mmewe Damiani. “Kama ameanza kumfuata Robert basi hapa sina mme tena” aliongea mwenyewe bila kuangalia upande wa pili, kwa nini Damiani hayupo ofisini. Mke wa Damiani alikuwa bado hajui kitu chochote kinachoendelea kuhusu mmewe.
Sophia nae alikuwa chumbani kwa mama yake pamoja na mdogo wake akijipodoa ili aingie ofisini kwa ajili ya kazi. Pembeni alikuwa kaandaa mkoba mkubwa sana ambao alikuwa tayari kaishaweka simu pamoja na mambo mengineyo yanayomuhusu yeye pamoja na Ofisi kwa ujumla.
Aliporidhika na kuona kuwa sasa yuko sawa bini sawia baada ya kujipodoa, aliondoka na kwenda kazini tayari kwa kazi za siku hiyo. Alivalia gauni lake zuri analopaswa kuvaa mama mjamzito na viatu vyake vyenye kisigino kifupi maana si unajua tena wajawazito na viatu virefu ni vitu viwili tofauti. Mke wa Damiani alizidi kufikiria bila kupata muafaka wa mawazo yake, mwisho akaamua kutafuta sehemu na kukaa chini.
Mwonekano wake ulionesha wazi kuwa ni mtu mwenye mawazo mengi. Akiwa amekaa chini alitokea babu mmoja ambae alikuwa anatembelea magongo. Babu yule alipata kilema akiwa mtu mzima kabisa na wala si kilema cha kuzaliwa. Yule mzee akamsogelea mke wa Damiani kisha akamuuliza, ‘Kwa nini umekaa kwa unyonge kiasi hicho kama mtu mwenye matatizo?’ Mara baada ya kumuuliza hivyo, mke wa Damiani akajifanya kutoka kwenye ile hali aliyokuwanayo kisha akamsikiliza yule babu ambaye alisogea karibu yake. “Babu unasema nini nilikua sijakuelewa’’. Alisema mke wa Damiani huku akijikuna kichwani kama mwehu flani ambae hajitambui kabisa.
Yule babu akarudia kumwambia kwanini umekaa kinyonge hivyo, unawaza nini? Mke wa Damiani bado hakutoa jibu lolote kabisa yaani alibaki kumtizama kisha akasimama na kujinyoosha kidogo, akajivuta mikono yote kulia nakushoto mithiri ya bwana Yesu Kristo msalabani, kisha mke wa Damiani akamwambia kuwa, hana mawazo wala unyonge labda macho ya babu tu ndiyo mabaya, hakumwangalia vizuri na kwa undani zaidi. “Sikia mama unamawazo sana ila unanificha tu, hutaki kuniambia ukweli” alisema yule babu huku akimwangalia mno mke wa Damiani, kisha Mke wa Damiani akaenda pembeni ili kumkwepa babu yule.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Babu alionekana kabisa kama akitaka kumsaidia bibie huyo kitu fulani ambacho ni kizuri zaidi lakini bibie kutokana na kuwa mwenye jeuri aliona kuwa anasumbuliwa na kupotezewa muda wake bure. Babu nae kwa kuwa alikuwa ni mtu mzima alipogundua bibie anajeuri ambayo imo katika akili yake aliamua kuendelea na mambo yake Mke wa Damiani akarudia kukaa kama alivyokuwa amekaa awali. “Huyu babu nae ananisumbua tu.” Alisema mke wa Damiani huku akiendelea kuwaza mmewe atakuwa wapi hadi muda huo.
Akiwa anaendelea kuwaza mara Sophia nae akafika kutoka nyumbani. Sophia baada ya kumuona mke wa Damiani pale nje alipata hofu sana alijua kuna jambo ambalo linaweza kuwa limetokea. Dah! Sophia aliingiwa na uwoga maana anamjua vizuri mke wa bosi wake alivyo mshari na mfuatiliaji wa mambo ya pale ofisini kwa mmewe Damiani. Sophia akamsogelea na kumsalimia akiwa hana amani kabisa. Ile kusogea tu mke wa Damiani akanyanyuka, “Sophia si ulikuwepo jana ofisini?” Sophia akamjibu ni kweli jana alikuwapo ofisini. “Basi nakuomba uniambie Damiani yuko wapi? Sophia akamwambia kuwa hata yeye hajui alipo Damiani. Mi najua yuko ofisini lakini nashangaa kama hayupo na Ofisi ingali bado imefungwa.
Mke wa Damiani bado hakumwelewa kabisa Sophia hivyo akainuka na kumkaba na kumwambia aseme Damiani alipo kabla hajampiga. Sophia alizidi kumwambia kuwa hajui Damiani alipo na aliondoka na kumuacha ofisini hivyo anamsumbua bure. Mke wa Damiani alikuwa ni mfupi sana na Sophia alikuwa kapanda hewani kidogo. Sasa mke wa Damiani akawa kamkaba uku akitaka kumrushia ngumi mke mwenzie.
Sophia alikuwa ni mpole sana ukichangia na ile mimba aliyokuwa nayo, na pia hakuwa na nguvu za kusema atapigana. Alikuwa kachoka mno. “Nasema hivi Sophia haiwezekani uwe Ofisi moja na mtu tena haina watu wengi, lazima unajua alipo. “Ebu acha utani utanambia tu.” Alisema Mrs Damiani huku akisimama juu yajiwe lililokuwepo eneo hilo ili amkabe sawasawa. Dah! Sophia alitia huzuni kabisa, alimuomba Mrs Damiani amuachie, alijishusha lakini wapi, Mrs Damiani alikuwa mgumu kuelewa kabisa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yule babu wa mara ya kwanza kupita pale akatokea, na kushangaa kwa nini tena yule mke wa Damiani kageuka na kumkaba dada mwenye mimba? Babu huyu alikuwa na mzee mwenzie wote wakasogea pale karibu na akina Sophia ili kujua kwanini wamekabana tena eneo la Ofisi za watu. Wale wazee walikuwa wanamfahamu vizuri sana Damiani maana wao ndio waliomsaidia kupata eneo hilo la Ofisi yake. “Jamani kulikoni mbona mnapigania kwenye ofisi za watu? “Duh! Binti mbona nimekupita hapa una mawazo kumbe ulikuwa unawaza kupigana?” Alisema yule babu ambaye alipita mara ya kwanza pale. Mke wa Damiani alimwanglia kwa dharau sana akimshusha chini mpaka juu. “Mzee una matatizo na mimi eti?” Mbona unanifuatilia sana why? Aliuliza na kwa lugha ya Kizungu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment