Simulizi : Nini Hatima Ya Maisha Yangu
Sehemu Ya Pili (2)
Bibi aliendelea kulalama kuwa hawezi kuendelea na safari kutokana kiu, kiukweli nilishangazwa sana na kile kitendo cha bibikukataa kuendelea na safari kwasababu ya kiu.Sikutaka kubishana na bibi yangu maana niliwaza huenda anamatatizo ndiyo maanahawezi kuendelea na safari, nilipoona bibi yangu amekataa kata kata kuendelea na safari niliamua kukata mti ambao ulikuwa mrefu kiasi, baada ya kuchukua ule mti nilichukua mfuko mmoja kati ya ile ambayo tulikuwa tumebebea vyakula na vitu vingine na kuuchana.
Nilipo maliza niliuchukua ule mfuko na kuufunga kwenyeule mti.Baada ya kuufunga nilipanda juu ya ule mtiambao alikuwa amelala bibi yangu nilipo fika juu ya ule mti nilichukua ule mti uliofungwa mfuko na kuuweka kama bendera, Nia na madhumuni yangu ni kwamba nikiwa narudi nisipasahau sehemu ambayo bibi yangu alipo kuwa..
nilipo maliza nilichukua lile karatasi kwaajili ya kuangalia njia ambayo ningepata maji, nilitembea huku nikiwa na kariri njia ili nisije kupotea, nilitembea umbali mrefu sana bila mafanikio yoyote ya kupata maji, sehemu nyingine kwenye ile ramani kulikuwa kunaonyesha mto lakini ukifika kwenye lile eneo unakuta mchanga.
Wakati nikiwa nazidi kusonga mbele nilisikia sauti kama za watu wakiwa wanaongea, niliogopa sana kitendo kilicho pelekea nigeuke pande zote kwa haraka, moyo ulianza kwenda mbio huku jasho jembamba la hofu likinitoka baada ya kugongana uso kwa uso na bibi kizee ambaye alikuwa ameshikilia fimbo mkononi.
Nilishtuka sana nilipo muona yule bibi ambae alikuwa amezeeka sana, yule bibi wala hakunisemesha alinipita kama anioni,baada ya kufika mbele aligeuka na kuniita kwa ishara kile kitendo kilinishtua sana na kunifanya nitokwe na haja ndogo bila kutarajia.
Upande mwingine wa moyo wangu ulikuwa unakataa mwito wa yule bibi kwa kuofia kuwa huenda ni mtu mbaya na alikuwa anahitaji kunidhuru, ila upande mwingine wa moyo wangu ulikuwa unakubali mwito wa yule bibi.
Muonekano wa yule bibi, Alikuwa mweupekiasi, mrefu kiasi, kwa muonekano wake alikuwa ana umri kati ya miaka themanini hadi tisini, nilivyoona anaendelea kuniita niliamua kumfuata huku nikiwa najihadhari asije akanidhuru.
Nilipo mfikia alinivuta pembeni na kunizibamdogo kwa mikono yake ambayo ilionekana kuwa na nguvu, kile kitendo kilinifanya nipige kelele lakini licha ya kupiga kelele yeye hakujali aliendelea kuniziba mdomo wangu ili sauti yangu isifike mbali.
Nilijitahidi kujitoa kwenye ile mikono ya yule bibi bila mafanikio, sikujua nia ya yulebibi nini maana toka nimezaliwa sikuwahi kumuona hata siku moja.
yule bibi aliendelea kuniziba mdomo kitendo kilicho pelekea mimi kuwaza huenda alikuwa na nia ya kuniuwa, sikupenda kufa kabla sijalipa kisasi kwa baba mkubwa.
Wakati yule bibi akiwa amenishika nilishangaa sana baada ya kuwaona watu ambao hawakuwa wageni machoni mwangu, nilipo waangalia vizuri ndipo nilipo gundua kuwa walikuwa wale watu waliotubwa na baba mkubwa kuja kunitupa pale porini.
kile kitendo kilinishangaza sana maana siku nilivyo toroshwa na gerad ambae yeye ndiye aliowapiga wale watu, kiukweli niliogopa sana na kile kitendo cha wale watu kuonekana tena.
Yule bibi alipowaona wale vijana wa baba mkubwa alinishukuma hadi katikati ya wale watu ambao nilikuwa nawaogopa sana kutokana na ukatili wao, nilijiuliza maswali mengi sana kuhusu wale vijana wa baba mkubwa.
Jambo ambalo lilikuwa linaniumiza kichwa ni kuhusu baba mkubwa, maana nilijua anaweza kuwa hupo maeneo yale na alikuwa anahitaji kuniua.
"John we nikijana mdogo sana na sizani kama nisahihi kufa ukiwa na umri mdogo namna hii" Aliongea mmoja kati ya wale vijana na kunifanya nishangae, nilishindwahata nimjibu nini kutokana na hofu yangu juu yao, Baadhi ya wale vijana waliokuwa pale mmoja wao nilikuwa namkumbuka kipindi nilivyo pelekwa mahakamani kwa kosa la kusingiziwa kuwa nimewauwa wazazi wangu na yeye ndie alikuwa hakimu, kile kitendo kiliniogopesha sana nakuanza kufikiria kuwa baba mkubwa
yeye ndiye alie panga mimi kupelekwa mahakamani na kutaka mimi nifungwe jela, niliwaza mpaka nikaanza kutokwa na machozi.
"Kijana hatujaja hapa kuja kuona machozi yako wala kilio chako, sisi hapa tumekuja na jambo moja la msingi, na jambo hili liko ndani ya uwezo wako na kama utaweza kufuata utakayo ambiwa utakuwa umeokoa maisha ya mdogo wako, ila kama utaenda kinyume na haya utakayo ambiwa basi hatuna budi kumuuwa mdogowako mbele ya macho yako.
Yale maneno yalinifanya mwili mzima kukosa nguvu maana nilikuwa nampenda sana mdogo wangu na huyo ndiyo alie bakia kama ndugu yangu wa pekee.
"Nikitu gani mnacho hitaji kutoka kwangu ambacho kinaweza kulingana na uhai wa mdogo wangu kipenzi?'Niliwauliza huku nikitokwa na machozi."Jambo ambalo limetuleta hapa ni hili hapa.
Walinipatia kakipisi cha karatasi ambacho kalikuwa kamekunjwa vizuri, nilikakunjuwaharaka haraka na kutaka kujua nini kilikuwa kipo ndani ya lile karatasi.
nilipomaliza nilianza kusoma kilicho andikwa kwenye lile karatasi.Kama unahitaji mdogo wako aendelee kuwa hai Basi fanya haya nitakayo kuambia, naomba uwapatie hao vijana wangu namba za siri za akaunt "(account)" ya baba yako za benk, na kama utaenda kinyume nitamuuwa mdogo wako mbele ya macho yako.
Yale maneno yaliokuwa yameandikwa kwenye ile karatasi yalizidi kunitia hasira, nilitamani ardhi ipasuke niingie maana niliona duniani nimateso, nililia sana huku nikiwa nimeshikilia lile karatasi kitendo kilichopelekea karatasi lile kuloana baada ya kunyeshewa mvua ya machozi.
Yale maneno yaliokuwa yameandikwa kwenye ile karatasi yalizidi kunitia hasira, nilitamani ardhi ipasuke niingie maana niliona duniani nimateso, nililia sana huku nikiwa nimeshikilia lile karatasi kitendo kilichopelekea karatasi lile kuloana baada ya kunyeshewa mvua ya machozi…
"Kijana huu siyo wakati wa kulia, kama kweli unampenda mdogo wako fanya kama ulivyo ambiwa, maana yule mzee hana huruma wala utu yeye anachojali ni pesa tu. Nakama unadhani ni utani we pingana nae uone mdogo wako atakacho fanywa.
Nikiwa pale sijui chakufanya, maana hizo namba walizo kuwa wanazihitaji za siri za Akaunti ya Baba sikuwa nazo, Niliumiza kichwa nijinsi gani nitaokoa maisha ya mdogo wangu, na nijinsi gani nitaweza kutoka hapa porini.
"Namba za siri sijazishika kichwani, ila kuna sehemu nilizihifadhi. Niliamua kuwaongopea maana sikuwa najua chochote kuhusu Akaunt ya Baba, mimi niayangu ni kutoka kwenye ule msitu, maana nilijua kuwa wao ndio waliokuwa na uwezowa kunitoa pale porini.
"Kama ni hivyo haina shida ila kama utakuwa unatuongopea basi ujue kichwa chako kitakuwa halali yangu.Yale maneno yaliniogopesha,maana sikuwa nafahamu kitu chochote kuhusu namba za siriza akauti za baba.Tuliondoka pale huku nikiwa na mawazo juu mdogo wangu.
maana nilijua sielewi chochote na ilikuwa ngumu kwa baba mkubwa kumdanganya, Niliwaza mambo mengi mpaka nikapitiwa na usingizi.
Nilikuja kushtuliwa na mmoja kati ya wale vijana wa baba mkubwa, nilishtuka baada ya kumuona Baba mkubwa akiwa kasimama nje ya gari ambalo tulitoka nalo kule porini.Nilijiuliza maswali mengi baada ya kujua tayari nilikuwa jijini Dar es salaam tena na mikononi mwa Muuaji asie kuwa na utu hata kidogo.
Nilipokewa vizur,Nilijua muda sio mrefu ningekuwa marehemu mtarajiwa maana nilijua siwezi kupona kwenye mikono yake.
Nilitamani kukimbia lakini ikawa ngumu maana tayari nilisha shikiliwa mikono hukunikiwa naingizwa kwenye gari kwaajili ya kuelekea nyumbani kwa Baba mkubwa, njia nzima nilikuwa nikiwaza nijinsi gani nitamdanganya Baba Mkubwa ili anielewe.
Nilipokewa vizur,Nilijua muda sio mrefu ningekuwa marehemu mtarajiwa maana nilijua siwezi kupona kwenye mikono yake.Nilitamani kukimbia lakini ikawa ngumu maana tayari nilisha shikiliwa mikono hukunikiwa naingizwa kwenye gari kwaajili ya kuelekea nyumbani kwa Baba mkubwa, njia nzima nilikuwa nikiwaza nijinsi gani nitamdanganya Baba Mkubwa ili anielewe
Tulipofika nyumbani kwa Baba mkubwa geti lilifunguliwa, nasi tukaingia na gari.
Kiukweli nyumbani kwa Baba mkubwa palikuwa pamebadilika sana, maana kulikuwa kumejengwa gorofa kubwa, huku kukiwa kuna magari ya kifahari ya aina mbalimbali.
Wakati nashuka kwenye gari huku nikiwa na hofu juu ya maisha yangu, kuhusu kitu cha kumuambia Baba mkubwa ili anielewe, niliwaza hatimaye nikawa nimepata kitu cha kumuambia.
Tukiwa pale alikuja mdada mmoja ambae mrembo nikaambiwa nimfuate. Nilimfuata hadi ndani, Wakati nikiwa naingia kule ndani huku nikiwa napanda ngazi za ghorofa ambalo lilikuwa lakifahari sana.
Tulifika juu kidogo yule dada aliniambia niingie ndani ya chumba kimoja ambacho kilikua pembeni yake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimwangalia usoni huku nikiwa natabasamu maana nilitokea kumpenda ghafla bila kutarajia, Nilitamani kumuuliza angalau jina lake lakini nilikuwa nimechewa maana alikuwa anameshaanza kushuka ngazi kadhaa kuelekea nje.
Niliingia ndani ya kile chumba huku mawazo yangu yakiwa juu ya yule dada, bila kujua nipo kwenye hatari kubwa kuhusu kile kilicho nileta.Kile chumba kilikuwa kizuri sana,kulikuwa kunakilakitu.
Kitu chakwanza niliingia bafuni, maana kilechumba kilikuwa kina bafu ndani kwa ndani na mimi mwenyewe nilikuwa sijaogomuda mrefu, nilipo toka bafuni nilishangaakukuta nguo zikiwa zimewekwa juu ya kitanda.
Nilizichukua na kuanza kuziangalia nilipoziangalianiliona kama zinanitosha, Nikaamua nizijaribishe wakati nazijaribisha kama zina nikaa mara nikasikia mlango unagongwa.
Nilishtuka maana zile nguo zilikuwa tayari mwilini kwangu, Wakati naangaika kuzivua mara mlango ukafunguliwa.Niligeuka haraka kuangalia ninani ameingia, Alikuwa yule dada alieniingiza pale ndani.
"Umepenza"Aliongea yule dada huku akiwa ametabasamu, Kiukweli alikuwa binti mzuri ambae nilijikuta nampenda ghafla."Ahsante" Nilimjibu huku ni nikiwa nimetabasamu.
"Baba anakuita yupo sebleni anakusubiri" Alivyo sema kuwa baba mkubwa alikuwa akiningoja sebleni yale maneno yalilifanya tabasamu langu lote na furaha yangu kuyayuka.
Ile hali ilifanya hata yule dada kuanza kunishangaa, maana nilikuwa kama mtu aliepewa taarifa za kushitushwa.
"Kwani kunanini kaka mbona umeshtuka baada ya kuambiwa kuwa unaitwa sebleni?" Aliniuliza yule dada huku akiwa ananiangalia usoni.
"Hamna kitu dada yangu mbona nipo sawa tu" Nilimjibu yule dada huku nikiwa nawaza nijinsi gani nitapona katika haya majanga.
Tuliondoka pale chumbani kuelekea sebleni alipo kuwa Baba mkubwa akinisubiri, Nilifika sebleni nikamkuta Baba mkubwa akiwa ananisubiri kwa hamu kubwa.
Pembeni yake kulikuwa na mdada mrembo kuliko yule wa mwanzo,"Karibu mwanangu jisikie upo nyumbani"Alinikaribisha Baba mkubwa huku akiwa ametabasamu.
Yale maneno ya Baba mkubwa yalinichanganyasana katika akili yangu."Nashukuru kwa kunikaribisha kwako"
Nilimshukuru Baba mkubwa huku nikiwa najiuliza vitu vingi katika akili yangu.
Maana nikikumbuka siku ambayo alinipiga mpaka kupoteza fahamu, nikaja kujikuta porini, Kila ninapo kumbuka vile vitendo alivyo nifanyia Baba mkubwa huwa napatahasisa isiyoisha.
Tulikaa pale sebleni huku tukipiga story mbalimbli, lakini mimi nilikuwa mbali kimawazo, huku nikiwa nasubiri niambiwe kilicho nileta kwenye ile nyumba.
Lakini kitu cha kushangaza mpaka tunamaliza maongezi nilikuwa sijaulizwa kitu chochote kuhusu akaunti ya Baba yangu.
Niliondoka na kuenda chumbani kwangu kwa ajili ya kupumzika, Lakini usiku mzima sikupata usingizi.
Nilikuwa nikifikiria jinsi ya kulipiza kisasi kwa Baba mkubwa, maana kila ninapo muona Baba mkubwa, Naona kama nimemuona Izrael mtoa roho za watu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati nikiwa pale kitandani huku usingizi ukiwa umekwenda likizo kwa muda kutokana na mawazo mengi juu ya maisha yangu.
Nilipata wazo la kutoroka,lakinisikujua lile jengo lipo wapi, maana Dar es salaam naifahamu vizuri, Na nakumbuka siku chache kabla ya kupatwa na matatizo ya kutupwa porini.
Maana sehemu ambayo tulikuwa tunaishi mwanzo ndiyo hii iliyojengwa ghorofa hili, nilijiuliza maswali mengi hatimaye usingizi ukanipitia.
Nilikuja kushtushwa na mlango kugongwa, Nilipo fungua nilikuta ni yule dada alie ni alie nipeleka katika kile chumba.
"Habari yako kaka, umeamka salama?" Alinisalimia yule dada huku akiwa anakuja sehemu nilio kuwa nimelala."Nzuri dada yangu, MUNGU nimwema sana" Nilimjibu yule dada huku nikiwa nashuka kwenye kitanda.
"Hivi dada unaitwa nani?, Maana toka nimekuja sijafanikiwa kujua jina lako""Mimi naitwa Debora" Alinijibu huku akiwa ananiangalia usoni.
"Jina na lako zuri kama wewe""Amna bhana mbona kawaida tu kaka, Kwani wewe unaitwa nani"Aliniuliza debora baada ya mimi kumwambia ana jina zuri.
Tulipiga story nyingi, hatimaye nilikwenda kupiga mswaki kwajili ya kwenda kupata kifungua kinywa, Nilipo maliza kupata kifungua kinywa niliamua kuzunguka ile nyumba ya Baba mkubwa ili angala niifahamu kiundani zaidi.
Nilikaa pale kwenye ile nyumba ya Baba mkubwa bila tatizo lolote, lakini nilipo kuwa najaribu kutoka nje ili niangalie mazingira nilikuwa nazuiwa na walinzi.
Hata baadhi sehemu katika ile nyumba nilikuwa nikitaka kuingia nazuiliwa, sikujua nikwanini lakini nilipazowea hatimaye siku zikapita na miezi pia nikiwa nipo kwenye ile nyumba.
Siku ya jumapili huwa baba mkubwa hatokinyumbani, kuanzia asubuhi hadi jioni yeye huwa anashinda nyumbani, na mimi siku hiyo ndiyo nilipanga kumuuliza maswali kadhaa kuhusu familia yangu.
Ilipofika jumapili asubuhi Debora alikuja hadi chumbani kwangu, kile kitendo kilinishangaza sana maana huwa sikawaida yake, huwa anakuja na kugonga mlango.
Lakini siku hiyo ilikuwa tofauti, maana alikuja na kuingia moja kwa moja chumbani kwangu, huku akiwa amejifunga kanga moja, kile kitendo kilinishangaza sana.
Nilijiuliza maswali mengi juu yake, lakini sikupata majibu yalio jitosheleza, sikuwa na lakupinga.
Niliamua kumkaribisha maana nilijua nipo sehemu za watu tena watu wabaya, watu walioniulia wazazi wangu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipoingia alifunga mlango na kusogea karibu na kitanda changu.
"Debora leo kuna nini maana siyo kawaidayako kuing....
"Sio kawaida yangu kivipi john kwani kuingia chumbani kwako bila kubisha hodi nikosa eti john?'.
Alidakia debora na kuniuliza swali ambalo lilizidi kunichanganya, Lakini sikuwa na jinsi ilinibidi kuwa mpole ili nijue shida yake nini.
"John nijibu basi kama nimefanya vibaya, kuingia chumbani kwako bila kubisha hodi"Alirudia tena kuniuliza baada ya kuona sijamjibu.
"Hapana Debora hujafanya vibaya ila siyo kawaida yako" Baada ya kumjibu hivyo nilishangaa kumuona Debora akiwa anapanda kitandani kwangu, huku akiwa anatabasamu tena bila hofu, Nilibaki nimeduwaa na kushindwa hata kuongea.
Nilitaka kuongea lakini Debora alinizuwia kwa kuniziba mdomo kwa mkono wake, Alipopanda kitandani alianza kunipapasa kitendo kilichopelekea kuamsha hisia zangu, ambazo zilipotea kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo yaliotokea hapo nyuma.
Nilishindwa kuvumilia maana Debora alikuwa mtundu sana na alikuwa na mwili mlaini, ambao nilikuwa naogopa hata kuugusa kwa kuhofia unaweza kutoboka, Nilipoona Debora anazidisha mashambulizi huakiwa ameishika maiki yangu na kunifanya nisikie raha flani Amanzing.
Yale mashambulizi yalikuwa makali sana huku yakiwa yakizidi kupamba moto, huku debora hakiwa hajiwezi, nilipoona hivyo niliamua kutoa ile kanga aliokuwa amejifunga Debora na kuitupia pembeni, maana hali ya hewa ilikuwa imeshabadilika pale chumbani.
Kiukweli Debora alikuwa na umbo zuri pengine hata kuliko wanawake ambao nilishawahi kuwa nao, maana alikuwa hana doa lolote ndani ya mwili wake, nilisogeza mikono yangu hadi kwenye tunda la Debora na kuanza kuonyesha "Skill" zangu kwake.
Nilimchezea Debora mpaka nilipoona hali yake imebadilika ndipo nilipoanza kulitafuna tunda lake, kiukweli Debora alikuwa anatunda tamu ambalolilinifanya kusahau shida zangu, na hata kusahau kuwa nipo kwenye hatari kubwa.
Wakati nazidi kulitafuna tunda, huku Debora hakiwa hajitambui yupo bin-tahaban kutokana na vitu nilivyokuwa nampatia, mara mlango ukafunguliwa nilishtuka na kumsukuma Debora pembeni, nilikurupuka bila kuelewa na kutupa macho mlangoni ili kujua ninani ameingia…
Nilishtuka nilipo muona Magreth akiwa ameingia chumbani kwangu, Magreth alikuwa ni moja ya wafanyakazi wa Baba mkubwa, Na muda mwingi huwa yupo na Baba mkubwa, Ndiyo maana huwa sijazoweana nae sana, japo yeye ni mzuri kuliko Debora, na hajawahi kuja chumbani kwangu hata siku moja, hata salamu zangumimi na yeye zilikuwa ni salamu za juju.
Nilishangazwa na kile kitendo cha kuingia chumbani kwangu, tena bila kubisha hodi. Kiukweli nilitokea kuchanganyikiwa, na kuwa kama mtu alie pigwa na bumbuwazi.
Nilipo mwangali Debora nilishtuka, Baada ya kumuona Debora akiwa anatetemeka, huku akiwa anatokwa na jasho jingi.
Nilishangaa sana maana haikuwa kitu cha kawaida kwa mtu kama debora, kutetemeka kama mtu alie kutana na simba mwenye njaa kali.
Kile kitendo cha Debora kuonyesha hofu kilinichanganya, nilipo geuka mlangoni nilimuona Magreth akiwa analia, huku akiwa anamwangalia Debora kwa hasira, Nilizidi kuchanganyikiwana kuona kama maigizo.
Nilijikaza na kuchukua Taulo na kuingia bafuni na kuwaacha pale chumbani, Lakini nilikuwa na maswali mengi juu ya Magreth kuhusu kilio chake.
Nilijiuliza maswali mengi huku nikiwa na hofu kubwa juu ya lile jambo.Nilijua huenda Magreth alikuwa akinipenda na ndiyo maana aliponifuma, nipo na Debora akaanza kulia. Niliumiza akili ili nijue nini chakufanya.
Nilipata wazo la kwenda kumuomba msamaha Magreth, ili zile taarifa zisifike kwa Baba mkubwa. Maana nilijua taarifa zile zikifika kwa Baba mkubwa ingekuwa hatari kwangu.
Nilitoka bafuni nikiwa na mapovu ya sabuni na kutoka hadi chumbani, nilipotoka tu bafuni nilishtuka baada ya kumuona Debora akiwa yupo chini, huku akiwa anatokwa na damu, nilishtuka sana nilipogeuka pembeni.sikumuona Magreth.
Nilikimbia hadi pale chini alipokuwa Debora huku nikiwa natetemeka."Debora nini kimekupata nieleze mpenzi wangu" Nilimuuliza Debora baada ya kumuona Debora akiwa anapumua kwa shida."John na.om..ba unis..amee" Aliongea Debora kwa shida huku akiwa anazidi kutokwa na damu nyingi.
Nilipoona damu zinazidi kumtoka nilitoa iletaulo niliokuwa nimejifunga na kuichana katikati na kumfunga debora pale alipokuwa amechomwa kisu, Kabla sijamfunga nilishtushwa na sauti ya Baba mkubwa akiwa ananiita kwa jina langu.
Niliposikia ile sauti niliona kama kifo kinaninyemelea, Maana nilijua Magreth ameshamfikishia taarifa kwa Baba mkubwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimfunga Debora haraka haraka na kumuweka kitandani kwangu maana sikupenda kumpoteza Debora na nilikuwa nimesha jitoa muhanga kwa lolote.
Nilitoka haraka nje baada ya kuona baba mkubwa ameniita muda mrefu. Nilipotoka nilimkuta baba mkubwa akiwa ameshikilia laptop mkononi.
"John umeanza kuwa kichaa?' Aliniuliza baba mkubwa swali lililo nichanganya na kujua mambo yameharibika."Kwanini Baba" Nilimuuliza Baba mkubwa baada ya kuniambia nimeanza kuwa kichaa…
Nilipo jiangalia ndipo nilipo gundua kuwa
sikuwa nimevaa nguo, kile kitendo
kilinishangaza sana maana nilikuwa nipo kama
nilivyo zaliwa.
Nilijiuliza maswali mengi na nimetoka toka aje
bila kuwa na nguo lakini sikupata jibu. Kiukweli
nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa na nilijua
kuwa siri imesha fichuka.
Bila kupoteza muda nilitoka mbio hadi
chumbani kwangu, nilipofika chumbani kwangu
nilifunga mlango kwa ndani ili asije kuingia
Baba mkubwa, Nilipo mwangalia Debora
niligundua kuwa yupo kwenye hali mbaya
ambapo alikuwa akihitaji msaada wa haraka,
Nilijiangalia nilivyo alafu nikajifananisha na
Baba mkubwa ili nijue yeye ananishinda kwa
kitu gani.
Niliona naanza kuchanganyikiwa maana vitu
nilivyo kuwa navifanya vilikuwa haviendani na
kile nilicho kuwa nakifanya. Wakati huo Baba mkubwa alikuwa akikazana kugonga mlango bila mafanikio, nilizidi
kuchanganyikiwa nilipokuwa namuona Debora
akiwa katika hali ile. Niliwaza mengi na vitu
vilivyo nitokea na nimateso mangapi nimepitia
leo hii yule alie nifanyia visa leo hii anazidi
kuniumiza.
Niliwaza mengi huku nikiwa sijui lakufanya na
wakati huo ndiyo Baba mkubwa alikuwa
ameongeza kasi ya kugonga mlango, Nilizidi
kutetemeka na kutaka hata ardhi ipasuke ili
niingie maana Baba mkubwa akijua mimi ndiye
niliesababisha debora kupata matatizo basi ingekuwa mwisho wangu.
Nilipoona anazidi kugonga mlango huku
akilitaja jina langu, Niliamua kumchukua Debora na kumuweka uvunguni ili Baba mkubwa asimuone, Wakati namwingiza Debora
uvunguni nilishangaa kumuona Magreth akiwa yupo uvunguni.
Nilishtuka nilipo muona magreth uvunguni mwa kitanda changu, jambo ambalo sio la
kawaida na lakushangaza sana.. Niliairisha zoezi la kumuweka Debora uvunguni na kumrudisha pale kitandani, Kwawakati huo
nilikuwa na hasira juu ya Magreth maana nilijua kuwa yeye ndiye alie sababisha mpaka debora kuwa katika hali ya mauti uti.
Nilimtoa Magreth uvunguni kwa hasira huku nikiwa na mvuta kwa nguvu zote, Nilipo mtoa nilianza kumtembezea kichapo, huku nikiwa natokwa na machozi ya hasira, Maana kila mtu
ninaekuwa nae na kuona msaada kwangu ndiyo
anaepata matatizo.
Nilizidi kumpiga hadi nilipo muona Ameanguka chini kama mzigo alivyo anguka chini na hapo
hapo Baba mkubwa akawa amefanikiwa kuingia
ndani kwangu.
Nilishtuka baada ya kumuona baba mkubwa amefanikiwa kuingia ndani, Sikuwa na wasisi maana nilijitoa kufa kupona kwa lolote ambalo lingetokea mbele yangu, Ila nia yangu ilikuwa kulipiza kisasi na kumuona mdogo wangu Sophia, Maana toka nimefika kwenye ile nyumba sikuwahi kumuona japo Baba mkubwa alikuwa akiniambia yupo.
"John mwanangu umekuwa kichaa lini mpaka unataka kuwauwa wenzako" Aliniuliza Baba mkubwa baada ya kukuta nimemfanya mbaya Magreth, Baada ya kuniuliza lile swali nilipata wazo la kujifanya kichaa ilinipone katika lile janga.Jambo ambalo lilikuwa lipo tofauti ni Baba mkubwa kuonekana kuwa mpole.
Kile kitendo cha Baba mkubwa kuongea kwa huruma hadi kupelekea machozi kumtoka kilinishtua, Maana huwa na jua yeye ni katili na siku zote huwa namuona nimuuwaji ila siku ile ilikuwa tofauti.Kitu cha kwanza nilicho waza ni kuanza kuongea maneno yasiyo eleweka nikijifanya mtu alie changanyikiwa.
Nilijitahidi kujikaza ili nisigundulike kama nilikuwa si kichaa maana nilijua ikigundulika basi itakuwa mwisho wa maisha yangu, Nikiwa pale huku nikiendelea kujifanya chizi, Walikuingilia watu watu wa miraba minne pale chumbani wakiwa wamevalia traki nyeusi na tisheti za blue.
Nilishtuka baada ya kuwaona wale watu wameingia pale chumbani, Niliona chumbakimekuwa kidogo na kusahau kuwa nilikuwa kwenye zowezi la kujifanya chizi.Wale watu walivyo ingia walinikamata na kunibeba juu juu kama kiatu cha mtumba hadi nje, Waliniingiza moja ya chumba cha pale nje na kunifungia kule ndani, Nilikaa pale kwenye kile chumba huku nikiwa sijui nitafanya nini ili niokoe maisha yangu, Nilisikia sauti ya Baba mkubwa akiwa anawafokea wafanyakazi wake, Huku akiwa anafoka kwa nguvu hali ilio pelekea mimi kuanza kupata hofu juu ya maisha yangu.
Nilikaa pale kwenye kile chumba ambachonilifungiwa hadi nilipoona mlango unafunguliwa, Mlango ulipo funguliwa aliingia mdada mrembo alie vaa nguo za Hospital, Nilipo muona yule dada nilianza kutokwa na machozi kitendo kilichopeleke yule dada kuanza kunishangaa.
Nilimwangalia vizuri ili kupata uhakika kama ni yeye au nilikuwa naota, Nilipo mwangalia vizuri niligundua ndiye.Yule dada alizidi kunishangaa huku akiwa anaendelea kutoa vifaa vyake vya kazi, Nilipoona anataka kunichoma sindano nilimshika mkono na kumwangalia usoni ilinimwambie mimi ninani na nipo pale kwa sababu gani.
Nilishangaa yule Dada anaanza kupiga kelele kitendo kilichopelekea wale vijana wenye nguvu kuingia ndani na kunikuta nimemshika yule dada mkono, Walipoona nimemshika mkono walianza kuja mbio hadi pale nilipo kuwa, Walivyo fika nilishangaa napigwa ngumi ambayo ilinipeleka hadi chini na kuanza kuona kiza kingi na hatimaye sikujua nini kiliendelea..
Nilikuja kujikuta nipo juu ya kitanda kwenye chumba ambacho kilikuwa kigeni machoni mwangu, Lakini chakushangaza sikuwa nakumbuka chochote na sikujua nijinsi gani nimefika pale chumbani, Nilipojaribu kuamka pale kitandani ili niangalie vizuri kile chumba. Nilishindwa kunyanyua hata shingo, Nilihisi maumivu makali na sikujua yale maumivu yametokawapi na nini kimetokea.
Nilijiuliza vitu vingi bila kupata majibu hukunikiwa sielewi ni kwanini nipo pale.
Nilipoona sielewi chochote niliamua kuondoka pale kitandani ili nitoke nje pengine ningeweza kujua nipo wapi, Lakini nilishangaa mkono wangu unakuwa mzito kama vile mtu ananivuta.
Nilipoangalia mkono wangu ndipo nilipo gundua kuwa nilikuwa nimefungwa pingu na kushikizwa pembeni ya kitanda, Nilishaa sana kwa kile kitendo maana mimi huwa najua wanaofungwa pingu ni waalifu sasa iweje mimi nifungwe, Nilizidi kuchanganyikiwana na nilitamani kumbukumbu zangu zirudi ili nijue nini kimetokea. Nilianza kumuomba Mungu kumbukumbu zangu zirudi ili nijue kitu gani kilitokea kabla ya kufungwa zile pingu.
Sikupata jibu lolote juu ya zile pingu pamoja na sehemu ile nilio kuwa, Na nini kimenileta pale kwenye kile chumba, Na nilifanya kosa gani hadi likapelekea mimi kuwa pale, Hayo ni maswali ambayo nilikuwa nikijiuliza.
Wakati nikiwa sijui hili wala lile niliona mlango wa kile chumba unafunguliwa, baada ya mlango kufunguliwa aliingia kijana aliekuwa amevaa nguo za Polisi huku akiwa ameshikilia vitu kama mafaili kwenye mikono yake, Nilishangaa sana na ndipo nilipo gundua yule kijana alikuwa ni polisi.
Kile kitendo kilinishangaza na kunitia hofu maana nilivyo kuwa ilidhihirisha kuwa nilikuwa nimepigwa sana, maana mwili mzima ulikuwa unaniuma.
Yule kijana aliekuwa amevalia nguo za polisi alipo fika pale alionekana mtu mwenye wasiwasi sana, Nilipomwangalia ni kama mtu ninae mjua ila sikuwa najua nimemuona wapi.
Yule kijana alinisogelea hadi pale nilipo kuwa nimefungwa na kunifungulia ile pingu, Baada ya kunifungulia aliniambia nimfuate ila mimi sikuwa tayari kumfuata, japo sikuwa najua nini kinaendelea, Alipoona ninasita kutoka pale aliamua kutumia nguvu kunitoa pale kwenye kile chumba.
Tulipotoka nje nilishangaa maana lile jengo nililokuwa lilikuwa refu sana hadi ukilitizama unahisi kizungu zungu, niliingizwa kwenye gari lililo onekana kuwala kifahari.
Baada ya kuingia pale ndani nilikutana na kijana na msichana mrembo, wakiwa wameketi siti za nyuma ndani ya lile gari. Nilishtuka baada ya kugundua kulikuwa na watu wengine ndani ya lile gari.
Nilipo ingia ndani ya lile gari yule msichana alikuja na kunikumbatia na kuanza kulia huku akiwa ananita kaka, Yale maneno ya yule msichana yalinichanganya, maana msichana mwenyewe nilikuwa simfahamu japo kumbukumbu zilikuwa zikionyesha kama nilikuwa nimewahi kumuona, lakini sikuwa najua nimemuona wapi.
Mwanzo nilipo muona yule dada akiwa analia niliona kama utani, lakini muda ulivyo kuwa unaenda ndipo nilipo gundua yule dada alikuwa analia kwa kumaanisha,kitendo kilicho pelekea kuanza kumuuliza maswali yule dada, maana nilikuwa sina kumbukumbu yoyote ndiyo maana ilikuwa ngumu kumtambua yule mdada.
"Samahani dada yangu we ninani na tunaenda wapi, maana naona unalia tu bila sababu embu nieleze nini kinaendelea?"Nilimuliza yule dada baada ya kuona kilio kizidi, Yule dada badala ya kunijibu yeye aliendelea kulia huku akiendelea kulitaja jina la kaka.
Safari iliendelea bila kujua nilikuwa naenda wapi, nilipo waangalia wale watu walionekana si wageni machoni mwangu, japo mmoja wao alionekana ni mgeni machoni mwangu, Nilipokuwa najaribu kuvuta kumbukumbu ilikuwa ngumu kukumbuka, japo kumbukumbu zilikuwa zikinijia na kuyayuka kitendo kilicho pelekea kupitiwa na usingizi mzito.
ITAENDELEA…………
*******************************************************************************************
NINI HATIMA YA MAISHA YANGU 27
Mtunzi:DEOKING PETER
+255766788242
+255673788242
ILIPOISHIA……..
Safari iliendelea bila kujua nilikuwa naenda wapi, nilipo waangalia wale watu walionekana si wageni machoni mwangu, japo mmoja wao alionekana ni mgeni machoni mwangu, Nilipokuwa najaribu kuvuta kumbukumbu ilikuwa ngumu kukumbuka, japo kumbukumbu zilikuwa zikinijia na kuyayuka kitendo kilicho pelekea kupitiwa na usingizi mzito.
ENDELEA…………
Nilipo kuja kushtuka nilikuta tayari kiza kimesha tawala anga, nilishangaa kujikuta nikiwa nipo kwenye kitandi, wakati nakumbuka mara ya mwisho nilikuwa ndani ya gari, Nilitaka kuamka ili nipapase angalau ukutani ili niwashe taa.
Nilinyanyuka na kuanza kupapasa wakati nikiwa nimeugusa ule ukuta nilishangaa maana haukua ukuta, Nikile kitendo kilinishangaza maana ukuta huwa ni mgumu lakini ule ulikuwa kama nguo nzito,Nilipoona hivyo sikukata tamaa ya kutafuta swichi ya kuwashia taa, Wakati nazidi kuitafuta swichi nilishangaa naguswa mguu na kitu ambacho nilikuwa sijakielewa, Nilishtuka na kuanza kupiga makelele huku nikiwa nakimbia kimbia bila ya kujua chumba chenyewe ni kidogo.
Kumbe kile chumba kilikuwa kilikuwa ni kidogo kila nilipokuwa nakimbilia nilikuwa nakutana na kizuwizi wakati nazidi kutafuta pakutokea huku nikipiga makelele ghafla nilishangaa kuona mwanga wa kama tochi ukinimulika machoni, Huku ukiambatana na sauti nzito ya mwanaume ikinisisitiza nitulie maana pale palikuwa si sehemu salama na niache makelele niliyokuwa nayapiga, Baada ya kusikia yale maneno nilipata hofu maana yule aliekuwa akinimulika nilikuwa simuoni.
Niliamua kuwa mpole na kutii kile nilicho ambiwa, Alinimulikia hadi nilipopanda kitandani baada tu yakupanda kitandani alizima tochi yake.
Nilikaa pale kitandani huku nikiwa sielewi nini kinaendelea na imekuwaaje nimefika hapa, Nilijiuliza maswali mengi huku nikiwa kama mtu aliechanganyikiwa maana nilikuwa napelekwa pelekwa bila hata kuuliza.
Usiku mzima sikuweza kulala maana akili yangu haikuwa sawa, ila kitu ambacho kilikuwa kinanishangaza ni pale nilipo kuwa nasikia sauti za wanyama wakali, Nilikuwa nikijiuliza sauti zile zinatoka wapi bila kupata jibu.
Palipo pambazuka nilikishangaa kile chumba maana nilikuwa najua nimelala kwenye nyumba ya kawaida kumbe haikuwa hivyo, Nilipotoka nje ndipo nilipo gundua lilikuwa ni hema na si chumba cha kawaida.
Nilipoangalia mazingira ya lile endeo nilitaka kukimbia maana kulikuwa kumezungukwa na miti mingi ya aina tofauti tofauti, Kwa mbele niliona maji yakiwa yanatirika kuelekea mabondeni, Kwa mbali niliweza kuona mawe makubwa pamoya na dege wa aina tofauti tofauti.
Kiukweli palikuwa panatisha na mimi kwa haraka haraka nilijua pale palikuwa ni porini, maana kulikuwa hakuna dalili ya watu kuishi maeneo yale, Nilipoona lile eneo nilikumbuka kama nilishawahi kukaa eneo kama lili, japo nilikuwa sijui ilikuwa ni wapi.
Nilikaa pale huku nikiwa najitahidi kukumbuka ni eneo gani lililo kuwa kama lile ambalo nilisha wahi kuliona, Nilipo kuwa nazidi kukaa pale ndipo nilipoanza kuona kumbukumbu zinarejea na kuanza kukumbuka kidogo kidogo hatimaye nikawa nimefanikiwa kukumbuka vitu vilivyo tokea hadi pale nilipo kuwa.
Nilipokuwa nazidi kukumbuka ndipo hasira zilipokuwa zinazidi kunipanda huku zikiwa zinaambatana na kilio kilichosindikizwa na machozi.
Kiukweli niliumia sana lakini sikupaswa kuendelea kulia maana hata ningelia mpaka machozi ya damu isinge saidia. Nilijipa moyo wa kishujaa maana nilijua malipo ni hapa hapa Duniani.
Niliamua kurudi ndani ya lile hema ili niwatambu wale watu ambao waliekuwa wamenileta pale maana mimi nilikuwa wa kwanza kuamka na wale watu nilikuwa siwajui na kama ndiyo waliotumwa kunimaliza basi nianze nao maana watu karibia wote wa Baba mkubwa wote nilikuwa nawafahamu.
Niliporudi ndani ya lile hema nilishangaa kukuta hakuna mtu hata mmoja, Kile kitendo kilinishangaza maana walikuwa ndani, Katika kuangaza angaza nilifanikiwa kuona karatasi likiwa kwenye kakitanda nilichokuwa nimelala.
Nilisogea hadi pale kitandani ambapo palikuwa na lile karatasi, Nililichukua lile karatasi na kuanza kulisoma ili nijue lilikuwa limeandikwa kitu gani maana wakati nilipo amka sikuona lile karatasi.
Kaka mimi ni mdogo wako sophia mimi pamoja na Mjomba Denis ndio tuliokutoa kwenye hatari ya kuuawa na Baba mkubwa,Ndio tukaamua kukuleta mahali hapa Kama unakumbuka kipindi ukiwa pale nyumbani kwa Baba mkubwa, Alikuwa akionekana kukupenda na kukujali, Yale yote uliokuwa unayaona anakufanyia ilikuwa ni njia ya kupata hela ambazo zilikuwa zimeachwa na Baba katika akauti yake.
Kipindi hicho chote alikuwa akikulinda ili usije kutoka kwenye imaya yake, maana alikuwa anajua ukitoka na kwenda mbali na maeneo yako tunge weza kukuchukua, maana yeye alichokuwa akihitaji ni namba za siri za akauti ya Baba na kama unavyo jua baba alikuwa anapesa nyingi katika akaunti yake na hizo pesa zilikuwa kwaajili ya kutusaidia katika maisha ya baadae.
Najua itakuwa ngumu kwako kukumbuka mambo haya maana walisha kuathiri kisaikolojia, Ila ninacho kuomba kaka yangu ni kutotoka hapo tulipo kuacha maana hapo ndipo kwenye usalama japo si sana ila itakuwa na usalama kwako....Nilisoma lile karatasi kwa uchungu huku nikiwa najikaza maana ilikuwa ni ngumu kulisoma na kulimaliza.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilitamani niwaambie kuwa kumbukumbu zangu zimerudi lakini ilikuwa nimechelewa maana nilikuwa nipo mwenyewe, Nilianza kujilaumu kwa kumwamini baba mkubwa na kujua ni mtu mwema kwangu kumbe haikuwa hivyo bali ilikuwa nimejiweka katikati ya mbwa mwitu wenye njaa kali.
Nilipata hasira kali na kuanza kuona kama naanza kuchanganyikiwa.
Kiukweli nilitokea kuchanganyikiwamaanakila jambo lilokuwa zuri kwangu lilikuwa ni baya, Nikikumbuka kifo cha wazazi wangu ndiyo hasira zinazidi kunipanda, Nilikaa muda mrefu pale huku nikiwa natafakari yale maneno yalio andikwa kwenye lile karatasi huku nikiwa nazidi kutokwa machozi ya kulipiza kisasi.Nilitamani kukutana na Baba mkubwa ili nimuonyeshe ni jinsi gani nilivyo na hasina na machungu juu yake, maana nilitokea kumchukia kutokana na matendo yake.
Hadi kiza kinatawala anga bado sikuwa najua nafanya nini ili kutoka pale, maana ile SEHEMU ilikuwa ngeni kwenye macho yangu maana ilikuwa kama msitu ambao ulionyesha hakuna mtu alie kuwa akiishi yale maeneo, Nilikuwa na hofu sana juu yamaisha yangu maana pale palionyesha kuwa na wanyama wakali, Kutokana na mimi kuwa muoga niliamua kupanda juu ya mti huku mawazo yakiwa yapo kwa mdogo wangu na mjomba wangu maana nilijua Baba mkubwa anaweza kuwauwa kutokana na wao kutokuwa na uwezo wa kupambana na Baba mkubwa.
Nilikaa pale juu ya mti mpaka asubuhi, Asubuhi ilipofika nilichukua baadhi ya vitu ambavyo waliviacha vingi vyao vikiwa ni vyakula. Baada ya kufanya hayo nilianza safari ambayo ilikuwa haina direction maana nilikuwa sielewi mashariki wala magharibi, Nilitembea umbali mrefu bila kukutana na kitu chochote huku nikiwa naamini nitatoka pale hadi ilipofika usiku nilikuwa sijapata hata dalili ya kufanikiwa kuona angalau unyayo wa mtu katika safari yangu.
Niliamua kupanda juu ya mti kusubiri kesho ili niendelee na safari."John mwanangu?'Ilikuwa ni sauti ya mwanamke iliokuwa ikisikika kutoka nyuma yangu, nilipogeuka nilikuta ni mama yangu ndiye aliekuwa akiniita nilishtuka nilipomuona mama yangu akiwa ananiita, wakati mimi nakumbuka mama yangu alikuwa amekufakipindi kirefu kilicho pita, sasa leo iweje awe apa au naota hata nilipo fikicha macho ukweli ulibaki pale pale kuwa ni mama yangu.
Kiukweli sikuamini japo nilikuwa nimeona sura ya mama, lakini cha kushangaza nilipomwangaliayule mtu aliekuwa anafanana,nilipo muangalia nilishangaa kumuona akiwa anatokwa na machozi, kile kitendo kilinishangaza maana kumbukumbu zangu zilikuwa zinajua kuwa mama yangu alisha poteza maisha kipindi kirefu, nikiwa kwenye mawazo huku nikiwa natafakari lile jambo, nilishtuswa na sauti ambayo ilinifanya nigeuke maana sauti ile haikuwa ngeni masikioni mwangu.Nilipogeuka nilishangaa kumuona Baba mkubwa akiwa amepiga magoti huku akiwa anatokwa na machozi.
Kiukweli nilipomuona Baba mkubwa nilipatwa na hasira hadi nilianza kuona kizungu zungu maana nilikuwa nikimuona nakuwa kama nimemuona shetani, nilitamani kumrukia na kumrarua vipande vipande lakini nilipotaka kujaribu kusogea nilisikia sauti nyuma yangu ikiniambia niache ambacho nilikuwa nataka kufanya, nilipo geuka nilishangaa kumuona mjomba denis.
Kile kitendo cha kumuona mjomba denis huku nyuma yake akiwa yupo mdogo wangu kilishtua na kunifurahisha, Kiukweli toka Baba na mama wapoteze maisha sikuwahi kucheka wala kufurahi ila siku ile ilikuwa kama ndoto kuwaona ndugu zangu. Ambao nilikuwa najua sipo nao tena leo nawaona tena.
Nilikuja kushtuka nipo chini ya ule mti niliokuwa nimelala, kumbe nilikuwa naota nilianza kulaumu ndoto maana nilikuwa nafuraha ila sikuwa na furaha tena maana nilikuwa mwenyewe tena sehemu awbayo sijui mashariki wala magharibi.
Kiukweli niliichukia dunia nzima na kuanza kumlaumu Mungu kwanini nilizaliwa katikahii Dunia yamateso, Niliwaza vitu vingi juu ya maisha yangu kila jambo ninaloona msaada kwangu, ndiyo jambo linalo niangamiza.Niliendelea kukaa pale chini huku nikiwa naitafakari ile ndoto, lakini sikuweza kuifafanua.
Ilipofika asubuhi niliendelea na safari ya kutafuta ni jinsi gani ningetoka kwenye ile sehemu. Nilitembea umbali mrefu bila kupata maji, chakula nilichokuwa nacho kilikuwa kimeisha.Niliendelea na safari mpaka nilipoona kiza kimetanda anga.
Nilipanda kwenye mti maana nilikuwa sina sehemu nyingine ya kwenda kulala zaidi ya kupanda juu ya mti.
Nilikaa pale kwenye ule mti huku nikiwa nimejishikiza vizur, hiyo ni kutokana na ule mti kuwa na matawi mengi, ambae mtu akipita chini au mnyama hawezi kukuona. Nikiwa kwenye ule mti nilianza kusinzia hata nilipo jaribu kujizuwia nisisinzie ilishindikana hatimae nikapitiwa na usingizi mzito.
Nilikuja kushtuka baada ya kuhisi kitu kimenipiga kwenye mguu wangu.
Baada ya kile kitu kunipiga nilianza kuhisi maumivu makali, kiukweli yale maumivu yalikuwa hayaelezeki hadi nikawa siwezi kushika hata kipande cha tawi la ule mti.
Niliteleza kwenye ule mti na kuanguka chini, lakini yale maumivu ya kuanguka juu mpaka chini yalikuwa yana hafadhali kuliko yale maumivu niliokuwa nayasikia kwenye mguu wangu.
Sikujua yale maumivu yanatokana na nini na yamesababishwa na nini.
Kwavile kulikuwa na kiza kingi ilikuwa ngumu kujua nini kimenipiga, nilipapasa kwenye ile sehemu niliokuwa nahisi maumivu na kukuta kama nimetobolewa, nilishhndwa kujua nikitu gani kilicho nitoboa. Nilijaribu kunyanyuka ili nirudi kwenye ule mti kusubiri ifike kesho ili nijue nini kimetokea, lakini nilishindwa maana maumivu yalikuwa makali kupita kiasi.
Nilikaa pale chini hadi asubuhi. Kitu cha kwanza nilianza kuangalia pale ambapo nilipokuwa nasikia maumivu, nilipoangalia niligundua kuwa nilikuwa nimetobolewa lakini sikujua nimetobolewa na nini kimenitoboa.
Nilijaribu kusimama lakini hali yangu ilikuwa mbaya. maana yale maumivu ya kwenye mguu nilianza kuyasikia mwili mzima, nilianza kuona nguvu zinaniishia, huku mwili wangu ukiwa unazidi kupoteza nguvu hatimaye mapovu yalianza kutoka mdomoni huku nikiwa nashindwa hata kuongea.
Nilijua mwisho wangu umefika maana kwa hali niliokuwa nayo sikuwa na huakika wa kupona, japo sikuwa najua nimepatwa na kitu gani.
Nilitamani kuongea maneno machache ya kumuomba mwezi Mungu kwa yote nilifanya, lakini hali ilizidi kuwa mbaya nikaanza kuona kiza kingi kikiambatana na nyota nyingi hatimaye sikujua nini kiliendelea…
Nilitamani kuongea maneno machache ya kumuomba mwezi Mungu kwa yo
Nilikuja kushtuka nipo kwenye kakichaka, nilijishangaa maana nakumbuka mara ya mwisho nilikuwa chini ya mti tena nikiwa na hali mbaya.
"sasa nimefika aje hapa na ni nani alie nisaidia na kwanini kanisaidia" Nilijikuta naropoka kwa jazba, maana sikupenda kuendelea kuteseka maana nilijua Duniani ni mateso.
Nilipo jaribu kunyanyuka nilishangaa kutosikia maumivu ya aina yoyote, wala kuhisi mabadiliko yoyote kwenye mwili wangu.
Nilizidi kushangaa nilipogusa ile sehemu nilioumia na kukuta akovu tu na si kidonda tena, ilikuwa kama ni sehemu ilioumia siku nyingi.
Kile kitendo kilinishangaza sana maana kidonda kililikuwa kibichi na hata mazingira yale na yale niliyojikuta yalikuwa na utofauti mkubwa, nilishindwa kuelewa nimefika aje pale na ni nani kanileta pale, lakini sikupata majibu kwa wakati ule.
Niliondoka pale na kuanza kumtafuta mtu alie nisaidia, japo sikuwa najua ni nani alieokoa maisha yangu ila nilijipa moyo huenda akawa maeneo yale. Niliendelea kusonga mbele huku nikiwa nazidi kumtafuta mtu alienisaidia. Nilipo fika mbele kidogo nilishangaa kumuona simba mkubwa, akiwa anakuja kwenye njia upande wangu.
Nilishtuka hadi haja ndogo ikaanza kunitoka bila kutarajia, nilitamani kukimbia lakini miguu ilionekana kuwa mizito.
Hata nilipo jaribu kupiga kelele niliona mdomo unakuwa mzito na kuanza kuhisi joto na baridi kwa wakati mmoja. Nilishindwa nifanye nini maana yule simba alikuwa tayari yupo karibu.
Yule simba alizidi kusogea huku akiwa anakuja kwa kasi na kunirukia. Nilipoona ameruka niliamua kufumba macho ili nisione kile kilicho kuwakinatokea, maana nilijua ndiyo mwisho wa maisha yangu. Nilishangaa kusikia sauti ya mlio wa baruti kitendo kilichonifanya kufungua macho haraka. Nilipofumbua macho nilishangaa kumuona yule simba akiwa pembeni yangu huku akiwa anavuja damu.
Kile kitendo kilinishangaza sana na kuanza kuona kama naota, maana haikuwa kitu cha kawaidi nilipogeuka pembeni nilikutana na mzee wa makamo akiwa ameshikilia gobore mkononi.
Nilijiuliza maswali mengi moja ya swali nililo jiuliza ni kwanini amenisaidia lakin yule mzee alionekana kama mtu anaenijua, maana nilishangaa anakuja kwangu huku akiwa ananishangaa na kuanza kunikagua kama nimeumia.
Kile kitendo kilinishangaza sana na kutaka kujua yule mzee ni nani.
"Samahani mzee we ni nani? na umenijulia wapi, maana mimi sikufahamu na wewe unaonyesha kunifahamu kwa kirefu?"
Nililimuuliza yule mzee baada ya kuona ni mtu anaenijua.
"Ni story ndefu mjukuu wangu. Usiwe na haraka utajua tu mjukuu wangu"
Aliongea yule mzee huku akiwa anatembea kumfuata yule simba na kumuweka bigani kisha kuanza kusonga mbele na kumwambia nimfuate nyuma.
Nilimfuata yule mzee mpaka kwenye kakijumba chake, nilipofika kwa yule mzee,yule mzee alinikaribisha kwenye kajumba chake. Nilipoingia ndani ya kile kijumba nilishangaa sana maana muonekano wa nje na wandani ulikuwa na utofauti mkubwa sana, Yule mzee aliniambia niketi kwenye kiti kisha yeye akatoka nje na kuniambia nimsubiri.
Niliwaza huenda yule mzee akawa mtu mbaya kwangu. "Angekuwa si mtu mzuri asinge niokoa wakati nilipotaka kuliwa na simba" Nilijikuta naongea mwenyewe. Niliendelea kumsubiri yule mzee huku nikiwa nashangaa kale kajumba maana ukiwa ndani utasema ni nyumba ambayo ipo katikati ya mji, ila kwa nje ilikuwa tofauti.Wakati nikiwa nashangaa ile nyumba niliona picha ya Mjomba Denis ikiwa imetengenezewa frem.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kile kitendo kilinishangaza sana, nilisema labda nimemfananisha lakini hata niliponyanyuka na kuisogelea ile picha ukweli ulibaki pale pale kuwa ni Mjomba Denis. Nilishangaa sana na kuanza kujiuliza huyu mzee anajuana na Mjomba Denis au wana mahusiano gani.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment