Search This Blog

Friday, October 28, 2022

MSAMAHA BILA MALIPO (FORGIVENESS WITHOUT PAYMENT) - 2

 

     





    Simulizi : Msamaha Bila Malipo (Forgiveness Without Payment)

    Sehemu Ya Pili (2)



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    B

    aada ya kufanya mizunguko kibao sana mjini Viviane sasa anaamuwa kumpeleka Sophia kwa Damiani. Palikuwa si mbali kwa pale mjini na Damiani alikuwa anajulikana mno pale mjini ata kama ungemuulizia mtoto mdogo angekuonyesha kampuni yake ilipokuwa. Baada ya mizunguko mingi pale ofisini bwana Damiani anaamua kutulia nakumpigia simu Viviane kumuuliza yuko wapi. Viviane anapokea na kumwambia yuko pembezoni mwa barabara ya kwenda benki kuu. Damiani akamwambia awahi maana anataka kutoka kwenda bandarini kuangalia kuna vitu katumiwa. Viviane aliongeza mwendo mithiri ya ndege inayotaka kupaaa. Sophia ndio kwanza alikuwa anafurahia kwa sana. Baada ya muda kidogo wakawa tayari wako sehemu husika wakiwa wamechoka kidogo. “Habari za saa hizi kaka” alisalimia kwa heshima Viviane “salama sijui una shida gani nikusaidie?” Aliuliza yule kaka ambae alikuwa pale mapokezi kwa lugha ya wenzetu wanapaita (receiptionist) pale ofisini kwa bwana Damiani. “Naweza kuonana na Damiani nina shida nae” Alisema kwa utii. Hata Sophia alionekana mwenye heshima zaidi maana ofisi ya mtu inapaswa kutunukiwa heshima flani. “Shida gani dada yangu, ya kiofisi au ya binafsi? Aliuliza kwa upole kaka huyu wa mapokezi. Viviane akamwambia yeye anashida nae kiofisi zaidi. Yule kaka akampa daftari la kusaini aingie kuonana na bwana Damiani kule ndani ambako ndio ofisi yake ilipo.



     Viviane alisaini kisha wote waliingia maana alisema hakuna shida kwa Sophia kusaini maana mmoja alitosha kuwakilisha. Baada yakuingia Damiani akawakaribisha vizuri kwa upendo. “Karibuni jamani Viviane karibu sana” Asante Damiani za kazi? aliuliza Viviane kwa upole na upendo. Za kazi kaka yangu” alisema Sophia kwa upole na unyenyekevu mkubwa sana. Siku zote mtafutaji lazima kunyenyekea ili kupata anachohitaji basi ndio falsafa ndogo yenye maana hapa duniani. Baada ya kumaliza kusalimiana Viviane alianza kumtambulisha Sophia kwa Damiani ili wajuane kwa upana kwanza. “Damiani, huyu ndiye rafiki yangu niliyekwambia. Sophia huyu ndio Damiani rafiki yangu sana”. Aliongea Viviane baada ya kuongea akamuachia ulingo wa maongezi bwana Damiani ambaye alikuwa ndie mwenye kampuni hiyo. Damiani akamwambia Sophia anachohitaji katika kampuni yake ni umoja na uwajibikaji katika shughuli zote za pale ofisini. Sophia akamwambia atakuwa tayari kuyatii yote ayasemayo. Damiani akawa anaongea huku akimwangalia vizuri Sophia. “dah mtoto mzuri huyu akiingia kazini hapa lazima nile unyumba” aliwaza kichwani Damiani akiwa tayari ameshakufa na kuoza vibaya kwa mtoto Sophia. Damiani akamuuliza Sophia kiwango chake cha elimu, Sophia akamkabidhi Damiani cheti chake cha kidato cha nne chenye ufaulu wa daraja la nne yenye pointi 26. Damiani akamwambia sio mbaya sana kwa sababu ana cheti chake kizuri anaweza kusoma muda wowote ule. Damiani akamtamkia Sophia mbele ya Viviane kwa kazi ameshapata mambo mengine ya mshahara wataongea wawapo wawili tu yaani yeye Damiani na Sophia. Kisha Damiani akamwambia Sophia kwamba kuanzia siku inayofuata awe ameshaanzakuja ofisini kuanza kazi. Sophia alikuwa haamini kabisa alibakia kukenuwa meno tu nje hajui atamwambia nini Viviane cha kumshukuru, kisha Viviane na Sophia wanaondoka wote.

    **

    Ilikuwa mishale ya saa saba mchana mama Sophia aliamua kuwahi siku hiyo nyumbani kwake. Alirudi na mfuko wa sukari pamoja na pesa kama elfu kumi na mbili mkononi. Sophia nae alikuwa tayari amesharudi yumo ndani na mdogo wake Edward au kwa kifupi [Edo] wakiongea mawili matatu kuhusu hali ya nyumbani na furaha wakiwa nayo kubwa sana juu ya Sophia kupata kazi. “Dah, aisee dadaangu umehangaika sana mungu kasikia kilio chako bwana” alisema Edward mdogo wa Sophia kwa furaha kubwa. Sophia hakuwa nyuma kumsihi Edward asome sana kwani hakutamani aje kuishi kama yeye kwa shida. Edward alikuwa anona kama ndoto vile dada yake kupata kazi kutokana na kuhangaika kwa muda mrefu kutafuta kazi. Mama yao alipofika nje alianza kuwaita kwa nguvu. “Sophia, we Sophia njoo unipokee jamani” alisema mama Sophia huku kichwani akiwa na sukari kilo tano. Sophia na Edward baada ya kusikia sauti ya mama yao walitoka nje. “kumbe Edo umekuja za shuleni? Edo akamwambia ni nzuri, kisha akamsalimia mama yake kwa heshima. Marahaba nimetoka huko mihangaikoni dah! Sophia ingiza ndani hiyo sukari. Sophia akabeba ile sukari akiwa na furaha mno. Mama yake akamuita nje Sophia kisha akamwambia awashe jiko wapike maana ana njaa sana. Njaa ambayo ni ya hatari mno. Sophia akachukua jiko na kuanza kuwasha taratibu kabisa. Siku hiyo pale nyumbani kwao walikuwa na nyuso za furaha kuanzia mamayao, Sophia mwenyewe, Edward na mdogo wao. Kwa Sophia furaha ilizidi zaidi baada ya kutamkiwa na Damiani kuwa aanze kazi kesho yake na pia mama yake kuja kaning’iniza mfuko wa sukari. Siku hiyo hadi panya waliomba uhamisho walisikia furaha na kujongea karibu karibu kupata kitu ambacho kingeachwa holela pale chini. Mama nimepata kazi kampuni moja hivi, nimefanyiwa mpango na rafiki yangu” Alimwambia mama yake huku akiwa anapepea moto ambao ulikuwa umegoma kuwaka. Mama Sophia hakuongea mengi sana kwa sababu pia alikuwa kwenye hesabu kali alibakia kumtikisia kichwa tu bintie Sophia kumpa moyo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ni mida ya saa kumi jioni bwana Damiani akiwa ametoka kazini na uchovu kibao. Anaamua kupita bar na mhasibu wa kampuni yake bwana Robert kwenda walau kupiga mbili tatu moja moto moja baridi. Damiani ndie aliemshinikiza bwana Robert kwenda bar mara baaada ya kutoka kazini kwenye kuumiza akili nyingi mno . Baada ya kufika bar Damiani akaagiza bia mbili “samahani kaka niwahudie vinywaji gani ? Aliuliza mhudumu wa pale bar. Mimi naomba safari baridi, alisema Damiani huku akiwa kashikilia tishu mkononi. Mimi niletee Kilimanjaro ya moto”. Alisema bwana Robert huku akimwangalia muhudumu anavyokwenda na kuacha lawama huku nyuma kwa jinsi ambavyo muhudumu alivyokuwa ameumbika. “Dah! Kwa mtindo huu mabinti watanilia pesa yangu sana” maneno haya yalitoka mdomoni kwa bwana Robert maana alipenda sana akina dada wazuri wenye kunukia unyunyu hasa wenye maumbile ya kuvutia. Akawa amemkumbusha na Damiani kwa binti Sophia aliyekuja kuomba kazi asubuhi kazini. Damiani akamwambia “Robert aisee! Kuna mtoto kaja asubuhi ofisini dah! Ebwana yule ni halali yangu si kesho anaanza kazi utamwona” Alisema Damiani kwa utaratibu. Robert, akamuuliza anamuweka sector gani pale ofisini. Damiani akamwambia anamuweka stoo ili vitu visiopotee na kumpa hasara kama ya mara zote ambayo huwa inatokea pale stoo katika ofisi yake. Robert akanyamaza na kumwambia ampe nafasi ambayo ni nzuri na imara kwa binti. Damiani akacheka na kumwambia Robert, Ndugu yangu na wewe mambo haya yana kugharimu sana alisema bwana Damiani akiwa anaweka chupa ya bia mdomoni mwake. Waliongea mengi sana kuhusu Sophia na ujio wake pale ofisini. Damiani alisisitiza kuwa anahitaji mapinduzi makubwa pale ofisini kwake.



    **

    Muda ukawa unachanja mbuga zaidi Sophia akamchukua mdogo wake Edo waende kwa dobi kunyoosha nguo aliyokuwa anataka kuvaa kesho yake ili aingie akiwa safi na poa kabisa maana umaridadi unatakiwa ofisini hasa ukizingatia ofisi ya bwana Damiani ilikuwa na wageni wa kila aina na wengine wana nyadhifa kubwa tu serikalini na nje ya serikali pia. Hivyo Sophia alikuwa anafanya maandalizi (preparation) angali bado mapema sana. Baraka aliyekuwa anamsubiri Sophia kwa hamu akitegemea kumuona kwani aliamini kabisa Sophia atakuja maana alijua ana shida na nifukara wa kutupwa hivyo lazima angekubali ombi lake kwa urahisi tu kulingana na dhiki zake, ingekuwa kama kumsukuma mlevi au sawa na kushuka mtelemko bila wasi wasi wowote. “Huyu vipi sijui mbona hatokei dah! Alisema Baraka kwa usongo mno akiwa amempania sana. Rafiki yake Baraka akamwambia kuwa Sophia hatoweza kuja kwani muda umeenda hivyo asijisumbue kwa mawazo. Baraka akamwambia haitowezekana kumuacha binti mzuri kama yule. Baraka alikuwa kadhamiria kabisa bila mapuuzo yoyote yale au mzaha mzaha tu. Sophia akawa anatamani sana siku iishe mapema kesho yake aende kazini kuanza rasmi kazi mpya. Damiani ambae ndie bosi wake mtalajiwa wa Sophia, alikuwa yuko nyumbani kwake amepumzika na mkewe pamoja na watoto wake watatu ambao wote walikuwa ni wa kike. Mke wa Damiani alikuwa ni mpole na hakuwa muongeaji sana. Alikuwa na rangi yake nzuri nyeusi ya kuteleza, rangi adimu, rangi isiyoweza kupatikana kwa madawa ya viwandani, rangi wanayoililia wazungu, rangi inayopatikana barani Afrika pekee, rangi nyeusi hakika ni yakujivunia. Mkewe Damiani alikuwa anaitwa Isabella. Damiani badala ya kuwaza familia yake alianza kumfikilia Sophia ambae alimkubalia kufanya kazi katika ofisi yake. “Aisee Sophia ni mrembo kuzidi ata Isabella, lazima nitakuwa nae hata kwa kutumia ubosi wangu”. Aliwaza mwenyewe Damiani kichwani tayari ata mkewe Isabella akawa amegundua kuwa mumewe ana mawazo sana kisha akamuuliza, “Mbona ni kama unawaza sana mme wangu kwanini au ofisini wamekukwaza mno”? Damiani akamwambia hakuna tatizo kisha akashika rimoti ya kuwashia televisheni na kuanza kubofya bofya kuangalia chaneli ambayo ina mambo mazuri kisha Isabella akakumbuka neno akamuuliza mmewe kwa utaratibu. “Mume wangu, uliniambia kuna sector ambayo haina mtu ofisi kapatikana mtu au bado? Aliuliza Isabella ilikujua. Damiani akamwambia tayari ameshapatikana na kesho ataanza kazi. Baada yakumjibu hivyo Isabella akatulia tuli. Damiani akamwambia nimesumbuka sana kupata mtu lakini ukiwa huna shida huwa wanaibuka watu wengi sana wakiomba nafasi ya kazi nawadengulia. Isabella akamuuliza mfanyakazi huyo aliompata ni mwanamke au mwanamme. Damiani akamtega kidogo ili kuona Isabella anatoa maoni gani. Akamwambia ni jinsia gani ambayo anaona ingefaa kwa nafasi hiyo. Isabella kwa kutogundua anategwa yeye akamwambia kuwa anapenda mwanaume ndie yuko sawa mno katika uwajibikaji na uzalishaji pia. Damiani akamwambia hayuko sahihi na kauli ainenayo maana wapo wanawake ni wazuri sana kuliko anavyoweza kuwazania. Baada ya kumwambia hayo akamwambia wazi kuwa mfanyakazi yule ni wakike. Baada yakusema hivyo mke wa Damiani yaani Isabella hakuwa na furaha kabisa huku akimkomalia mmewe amfanye kuwa wa muda tu. Baadae aweke mwanaume ndio sawa.

    N

    i siku ya Jumamosi asubuhi Damiani akiwa amewahi kufungua ofisi yake ili kusudi awahi kufunga maana siku hiyo huwa kazi hainogi kama siku zingine za wiki. Sophia naye alikuwepo tena ndiye mtu wa kwanza kabisa kufika pale ofisini. Damiani akawa anamuelekeza mambo kadha wa kadha ya ofisi kwa ujumla.

    Damian akawa anamuonyesha mpaka jinsi vijana wake wanavyosindika matunda kwa umakini na usafi wa hali ya juu. Sophia alifurahia sana na kumwambia bosi wake kuwa kumbe atajifunza mambo mengi na makubwa awapo pale ofisini kwake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Utajua mambo mengi Sophia ambayo ni adimu huwezi kupata kwingine”.Alisema Damian huku akicheka cheka na kutabasamu.Damiani akaendelea kumwambia achilia mshahara wake mzuri ambao anawapa wafanyakazi wake bado watu huwa wanaondoka katika kampuni yake na ujuzi wa usindikaji matunda na wanaenda kuwa watu mashuhuri zaidi yake.Sophia alizungushwa na Damiani na kupewa sheria mbalimbali za pale kazini,akiwa kazini anatakiwa kuwaje. Awe kwenye muonekano gani kwa siku hiyo ndio kazi aliyokuwa nayo Damiani kwa binti Sophia.

    Baada ya kumaliza kumtembeza Sophia na kumpa sheria na taratibu za kiofisi.Damiani akamkabidhi na ufunguo wa stoo kwa ajili ya Jumatatu kuanza kazi rasmi.Ufunguo ndio huu, hakikisha mali zote humo stooni zina kuwa katika hesabu nzuri sawa”? Sophia akatikisa kichwa kuashilia kuwa Damiani anayomwambia yanaeleweka.Kisha Damiani akaenda naye ofisini ili wapange mshahara wasije kusumbuana mbeleni.



     Damiani alikuwa anatilia suti muda mwingi awapo eneo la ofisini kwake. Baada ya kuingia ofisini bwana Damiani akakaa kwenye kiti na kuanza kumuuliza Sophia . “Najua kazi yako itakuwa tofauti na wengine, ungependa nikupe shilingi ngapi kama mshahara wako? Aliuliza Damiani kwa utulivu mkubwa na umakini. Mimi bosi nakusikiliza wewe tu maamuzi yako kwako. Alisema binti Sophia kwa upole huku akiumauma kucha za vidole vyake kwa aibu na kutojiamini.

    Damiani akamwambia kuwa yeye hapendi kuropoka mshahara anaojisikia kusema. Huwa anawapa uhuru sana wafanyakazi wake.Wakati wa maelewano ya malipo isipokuwa kama akisema pesa kubwa mno huwa anafanya maboresho kidogo ili wasipunjane ama kunyonyana kwa kiasi fulani. Baada ya kumwambia hayo alimpa tena muda mwingine wa kupanga mshahara wake mwenyewe bila kuhofia hofia kwa sana. Sophia akamwambia anataka laki moja na nusu tu. Damiani akacheka na kumwambia hiyo ni pesa ndogo sana ambayo hamlipi mtu yeyote mule ndani.

    Damiani kwa sababu alikuwa ni msomi aligundua Sophia hataki kujiamulia mwenyewe mshahara hivyo Damiani akampangia mwenyewe mshahara.Sophia mimi nitakulipa shilingi laki tatu ili utakapoonyesha juhudi na ubunifu wako mbeleni nitakuongeza donge zuri tu la mshahara”Alisema Damiani kwa umakini.

    Ilikuwa ni mida ya saa saba mchana Damiani akifunga ofisi yake wakiwa na Robert kijana wake wa kazi. Robert alikuwa ana kazi kidogo ile asubui hivyo hakuweza kuonana ama kumfahamu vyema binti Sophia ambaye alikuwa ni mfanyakazi mgeni pale ofisini kwao.

    Kipindi wakifungua ofisi Robert akawa kamuona Sophia lakini akawa hajui kama ndiye Sophia ambaye walikuwa wakimuongelea siku ile iliyopita.Robert akaamua kumuuliza Damiani ambaye ni bosi wake.“Oya bosi ee na huyo binti mrembo mrembo vipi mbona hatuambiani”? alisema Robert akiwa ameshasahau habari za Sophia.

    Hii ni kutokana na bwana robart kuwa na mambo mengi sana kichwani. Nakuwaza mambo ya usambazaji wa bidhaa maana ndiye alikuwa meneja wa masoko katika kampuni hiyo ya kusindika matunda ingawa alipenda sana mabinti ili kupunguza msongo wa mawazo ya ofisini. Uchumi wa kampuni ulikuwa ukiyumba na Damiani alikuwa akimlalamikia sana hivyo alikuwa makini mno katika shughuli yake. Baada ya kuwa ameshasahau Damiani anaamua kumkumbusha.Robert huyo ni mfanyakazi mwenzio sawa” Baada ya kuongea hivyo akaanza kumfafanulia kuwa yule ndiye Sophia aliyekuwa akimwambia jana jioni. Kisha Damiani akamuita Sophia ili kumtambulisha na bwana Robert ambaye ndiye msaidizi wake. Sophia huyu ni meneja masoko wa kampuni hii anaitwa bwana Robert. Pia bado kuna wafanyakazi wengi sana nitakutambulisha pole pole tu sawa”? kisha Sophia akaitikia kwa sauti ya utii wa hali ya juu.Baada ya kumaliza kuwatambulisha wafanyakazi wake Damiani akaingia ndani ya gari lake na kuwaomba Sophia na bwana Robert waingie ndani ya gari ili aende nao.Damiani alitaka kwenda kuwafanyia surprise ya kunywa na kufurahi pamoja yaani kama kupongezana na kumkaribisha binti Sophia kama mfanyakazi mpya kuingia ndani ya kampuni yake.Japo lengo la Damiani halikuwa hilo, yeye alikuwa na lengo mbadala ambalo alikuwa anajua yeye pamoja na moyo wake na akili yake kwa ujumla.Pia kampuni yao ilikuwa inazalisha juice mbali mbali zinazotokana na matunda pamoja na vyakula mbalimbali.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Damiani alipokuwa anaendesha gari yake, alihisi huenda atawahiwa kwa binti Sophia, na hii ni baada ya kumuona Robert amekaa na Sophia. Akamwambia Robert, “njoo uendeshe bwana mimi nimechoka sawa alisema akiwa na moja kichwani.Robert akakubali akijua kweli Damiani labda kachoka, kumbe janja ya sungura ndani ya shamba la migomba.Haya nipishe nishikilie huo usukani” kisha wanasimamisha gari ili kubadirishana. Robert akaingia kuendesha na Damiani akaenda kukaa nyuma na Sophia. Damiani akaanza kumuongelesha Sophia “Hivi unaishi mitaa gani? Sophia anatulia kisha anamwambia mtaa anaoishi. Damiani anagundua kuwa mitaa anayoishi Sophia ni ya watu duni sana kimaisha kwa ujumla.

    Kisha Damiani akaanza kumpeleleza kinaga ubaga ili kujua anaishije.Sophia ambaye kwa umbo na muonekano wake alionekana mtoto wa wenyenazo, lakini kumbe ni tofauti kabisa na mtu anavyoweza kumdhania.

    Sophia naye hakuwa nyuma kumwambia hali halisi ya nyumbani kwao. Sophia alimwambia maisha anayoishi ni magumu sana. Anaona kupata kazi hii itamsaidia kimaisha. Damiani alimwambia awe mchapa kazi tu ataona mambo yatakavyo mbadilikia.

    Damiani akamwambia hata bwana Robert hana elimu kubwa anaelimu kama ya Sophia ya kidato cha nne. Damiani akamwambia lakini juhudi zake zimemfanya aishi maisha mazuri na yenye kupendeza tu.

    Sophia akawa anatamani kuishi kama Robert. “Yaani bosi natamani kuwa kama huyu walau” alisema Sophia kwa matamanio zaidi.Damiani akamwambia atakuwa level kama hiyo tu wala asihofu sana na kuumiza roho yake.

    Lakini Sophia aliamua kuchukulia kawaida maana aliona ni mambo mengine ya ubinadamu tu kisha punde si punde Robert kaendesha mpaka mwisho wa safari yao, ambapo waliingia ukumbi mmoja maarufu sana uliokuwa pembezoni kidogo ya mji.

    Ukumbi huo wanaingia watu wenye pesa zao mjini. Damiani aliingia mule ukumbini akiwa mkabala na binti Sophia. Wakiwa hawaachani kabisa. Robert hebu mwambie mhudumu atupatie bia mbili castle tafadhari.

    Kisha Damiani akatoka na kwenda faragha kidogo kuongea na simu. Muziki ni sehemu ya burudani na ni sehemu pia ya starehe kwa upande mwingine.Kwa kutambua hilo pale baani kulikuwa na muziki miondoko ya taratibu sana, muziki usiokuwa na bughuza pale ukumbini.Sophia ungepeda kuongeza soda nyingine, usione aibu ongeza” alisema Robert kwa niaba ya.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    SURA YA SITA

    B

    aada yakuwa Sophia ameshamaliza wiki moja kazini. Damiani akiwa ameshamtongoza Sophia na kukubaliana bila kipingamizi chochote. Kwa sasa Damiani na Sophia walikuwa mtu na bosi wake lakini pia walikuwa mtu na mpenzi wake kwa uhusiano wa karibu sana.

    Sophia alikuwa anapewa kipaumbele sana kuliko wafanyakazi wengine pale ofisini kwa bwana Damiani. Upendeleo huo ulizidi tena waziwazi kabisa sasa uliwaudhi hadi baadhi ya wafanyakazi wenzake. Khamis pamoja na nduguye Khemed wao walikuwa wamesoma sana kuliko Damiani na ndio walikuwa washauri wakuu na waongozaji wakubwa wa kampuni hiyo walikuwa wakifanya mipango mpaka kodi inapunguzwa huko TRA.

    Kwa sasa wanaona dhahiri kabisa Damiani hawapi hata pesa zao tangu alipoingia Sophia pale. Sasa Khamis na Khemed wakawa wametulia wenyewe wakimjadili kwa upana Damiani. Yaani khamis nakupa wiki nane za kukaa hapa kama silipwi naondoka.”

    Alisema khemed kwa uchungu wakukosa pesa zao. Khamis na Khemed walizungumza mengi sana kumuhusu bosi wao Damiani. Na Damiani muda huo penzi limemkolea kwa binti Sophia.

    Mama Sophia yeye ingawa mwanae kwa sasa alikuwa ana wajali na kuwahemelea vitu lakini yeye hakuacha kazi yake ya kuomba omba kule mjini, kitu ambacho Sophia alikuwa hapendi na kumkemea mara kwa mara aache. Mama Sophia alikuwa mbishi sana hakupenda kuachana na kasumba hiyo hata kidogo

    Ilikuwa ni wiki ya pili sasa tangu Sophia aanzishe mahusiano ya kimapenzi na bosi wake Damian. Sophia akiwa nyumbani kwao tena chumbani kwake mwenyewe anaanza kugundua vitu mbali mbali kuwa huenda akawa mja mzito.

    Anaanza kujishangaa chuchu zake kwa jinsi zinavyokuwa kwa haraka na kubadilika rangi kuwa nyeusi zaidi. “Hivi kuna nini mbona sijielewi elewi.” Alijiuliza mwenyewe kichwani, Sophia akaanza kung’amua moja baada ya jingine.

    Akagundua si bure lazima itakuwa ni mimba tena ya Damiani maana mara zote hakutumia kinga yoyote kila alipokutana kimwili na Damiani.Sophia akajadili katika akili yake akaona ni bora amwambie Damian mapemaa zaidi ili akae akijua ana mimba yake.

    Sophia alikuwa kabadilika sana kwa kiasi kikubwa mno.Umbo lilikuja kama la mama mtu mzima, alikuwa kaanza kubagua vyakula pale nyumbani.Mama Sophia alikuwa hajui kinachoendelea kwa binti yake.

    Yeye aliendelea zaidi kuomba omba wala haya mengine alikuwa hayamo kabisa. Sophia aliamua kupanga kesho yake ni lazima amwambie Damiani hali halisi.Akawaza sana lakini akaona kwa nini asimpigie simu tu amwambie wazi kuwa ana mimba yake.

    Sophia akaamua kuchukua simu na kumjuza Damiani kuwa ana mimba. Damiani baada ya kusikia hivyo alianza kumfokea sana. Nakuuliza Sophia umeshindwa kazi? Haya mimba yako si kimpango wako mimi inanihusu vipi? Alifoka sana Damiani na kumkana kama kweli hajawahi kutembea naye.

    Sophia akaamua kukata simu na kuanza kulia mwenye mawazo yakamuingia mabaya na machafu mno. Tena baada ya bwana Damiani kumaliza kuongea na Sophia alianza kuwa na hasira sana. Chuki ikaanza kujengeka moyoni mwa Damiani dhidi ya Sophia ili hali anajuwa ni ukweli kabisa mimba ni ya kwake ila kaamua kukanusha tu.

    Moyo wa kijasiri ukamuingia Sophia na kuamua kutunza na kuilea mimba ambayo alipewa na bwana Damiani maana alikuwa hapendi kutoa mimba, Sophia akaamua kutuliza moyo nakusonga mbele kimaisha kisha Sophia akatamka neno “Aah, kwa nini nisimsamehe, ngoja nitowe moyo wangu kwa msamaha bila malipo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alisema Sophia akiwa kweli ameshamsamehe Damiani akijuwa labda ni kufanya kitu bila kugundua. Hakumwambia hata mama yake. Aliona ni bora kugangamara bila woga na mashaka mashaka mengi sana. Hakuwa kama mabinti wengine wasiokuwa na ustahimilivu katika maisha. Sophia anaamua kulala ili kupunguza mawazo mabaya kichwani ya kutosamehe watu. Muda huo wote mama yake alikuwa ameshalala.

    Ilikuwa ni asubuhi na mapema Sophia akiwa tayari yuko eneo la ofisi akipanga vitu stooni nakusafisha stoo kuweka mambo katika usawa. Kipindi akifanya fanya usafi Robert akawa amefika na gari lake ambalo lilikuwa la thamani kidogo.

    Robert anafika kisha anaenda kumsabahi binti Sophia.Sophia habari za nyumbani? Aliuliza bwana Robert akiwa anatikisa tikisa funguo za gari lake mikononi,Nzuri tu kaka Robert sijui za huko kwenu.









    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog