Simulizi : Zari La Ndoa
Sehemu Ya Tatu (3)
Saa 12 na nusu asubuhi, Sungura akamtumia sms Zainab na kumwambia iwapo huyo jamaa atampigia simu na kumtaka waonane nae sehemu yoyote tofauti na kwao, basi asikubali na amwambie yeye hawezi kutoka bila ruhusa ya wazazi.
Akarudi kulala baada ya kumaliza kutoa maelekezo ambayo yeye aliamini kuwa ni ya msingi sana. Zainab nae alichapa usingizi hadi saa mbili alipoamshwa na simu yake iliyokuwa ikiita kwa fujo sana.
Namba aliyoiona mbele kwenye kioo cha simu yake ilikuwa ni ile ile aliyoongea nayo usiku uliopita na kuihifadhi kwa jina la Bodi ya mikopo, akaipokea na kusalimiana kisha jamaa akamuelekeza Zainab ni wapi alipo.
Kauli ya mpenzi wake ikamuijia kichwani, kauli ambayo ilionesha kabisa kumtilia shaka mtu yule, akaipa nafasi na na kulazimika kufuata ushauri wake. Matwiga nae akagoma na kumwambia hawezi kuondoka pale kuelekea popote, maana muda haumruhusu.
Zainab akaamua kukata mzizi wa fitina na kumwambia awasubiri dakika chache zijazo anaongea na baba yake ili waje nae hilo eneo alilopo. Moyo wa Matwiga ukafa ganzi lakini akazuga zuga tu kwa kusema anatoa robo saa wawe wamefika.
Dakika 10 tu Zainab akamwambia zinawatosha wao kuwa wamefika huko. Baada ya kukata simu ile akampigia Sungura na kumwambia wanapaswa kuonana eneo ambalo alitajiwa na Jamaa ambalo Sungura pia alilitambua.
Wakapanga dakika chache zijazo wawe ndani ya eneo hilo, lakini wakati bado wao wakijipanga kupitia simu zao, Zainab akasikia kuna ujumbe mfupi wa maandishi umeingia, hakujali akaendelea tu kuongea na mpenzi wake.
Sms iliyoingia kwenye simu ya Zainab ilikuwa imetoka kwa Matwiga ikiuliza bado tu?
Zainab akamjibu kuwa wanasubiri bodaboda, muda mchache ujao watakuwa wamefika eneo hilo walilokubaliana yeye wala asikonde.
Hapo sasa Matwiga akajua Zainab yupo Serious kuhusu hiyo issue na kweli anakuja na baba yake, akachukua simu yake na kumjtumia ujumbe mwingine wa maandishi na kumwambia asiende tena kwani muda uleule wanaondoka kuelekea sehemu nyingine, kwani wamechelewa sana kufika.
Mwisho wa ujumbe ule aliandika kuwa iwapo atapata nafasi ya kurejea Songea, basi watawasiliana, hakuhangaika hata kuijibu sms ile bali alicheka sana na kumpigia simu Sungura.
Cha kwanza kuongea ni kumsifu mno Sungura kutokana na kuwa na akili za ziada, akahoji ni vipi? Zainab akamuhadithia yote, Sungura alitabasamu na kumwambia yeye alihisi kuwa wale sio watu wazuri kabisa kwake.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tangu muda ule wakaiua rasmi safari ya kuelekea kule hotelini walipokuwa wakijitayarisha kwenda na kila mmoja akashika yake aliyopanga kufanya kabla ya kuzuka kwa safari ile.
Sasa ndio matokeo ya Sungura yakawa yametoka alikuwa amechaguliwa kwenda kujiunga chuo kikuu cha Dodoma kwa ajili ya kuchukua diploma ya masomo ya Ugavi na ununuzi (Procurement).
Alimjuza Zainab pamoja na kumpa baadhi ya mipango yake ambayo alimwambia itasimama hadi wakati atakapomaliza chuo na wakati huo nae atakuwa yupo chuoni. Walikubaliana kuwa wavumiliane tu na umbali wala usiwe ni kigezo cha kutengana.
Mtu wa kwanza kuondoka Songea kwenda chuo alikuwa ni Zainab ambae kila kitu chake kilikua tayari kimetayarishwa na mzazi wake, ambae aliondoka nae hadi Iringa kwa ajili ya kukamilisha yaliyokuwa hayajakamilika, siku ya pili Mzee akarejea Songea akiwa amemuacha mwanae Iringa kwa ajili ya kuanza masomo yake.
Wiki moja mbele, Sungura nae akaondoka Songea kuelekea Dodoma, lakini kwanza akapita hadi Iringa kumuona mpenzi wake. Walifurahi kuonana ugenini, hata muda waliona kama vile hauwatoshi.
Walielekea hadi chuoni kwa kina Zainab kutembea ili Sungura ayaone mazingira ya chuo anachosoma mpenzi wake. Usiku kabisa ndio Sungura akaondoka kuelekea huko mtaa wa Legeza Mwendo ambapo kuna nyumba ya wageni iitwayo Kisimba, ndio alipofikia.
Asubuhi mapema, Sungura akajidamka na kuanza safari yake ya kuelekea Dodoma ili kujiunga na chuo ili kukamilisha ndoto zake.
Maisha ya upweke kwa wapendanao wale wawili, yakaanza tena upya baada ya kuyasahau kwa muda. Awamu hii walikuwa na unafuu kiasi fulani, kwani walikuwa na mawasiliano na muda wote waliwasiliana.
Kila jioni waliwasiliana hadi usiku wa manane, tena huku wakiwa na wasaa mpana zaidi wa kuchat na kuongea muda wote watakao. Sungura hakuhofu kuwa kero kwa ndugu yake wala Zainab hakuogopa wazazi, ilikuwa ni nafasi adhwiim kwao.
Ukakatika mwezi mmoja na kila mmoja sasa akaanza kuikubali hali halisi na kuyazoea mazingira ya eneo alilopo na upweke akiuchukulia kama changamoto, ambao suluhisho lake lilikuwa ni simu tu pekee.
Ikapita miezi mitatu bila wapendao wale kuonana, vituko vikaanza sasa kwa Zainab, akaanza kupokea ujumbe wa kimapenzi, hakujua unatoka wapi, Mwanzo akawa wala hazijibu, lakini mtumaji akawa anaendelea tu kutuma bila kuchoka.
Kila akipiga ili aweze kuongea nae, mtu yule anakata simu nakumtumia sms za kumtaka asome kwanza, wataongea sana muda utakapofika, ila kwa sasa akamwambia ajiweke busy na masomo tu lakini ajue kuna mtu yupo sehemu anamsubiri tu hadi atakapomaliza.
Hali ile ikawa inamchanganya sana, akawa anataka kumuuliza Sungura kama ni yeye ndie anaefanya vile, lakini nafsi yake ikawa inakataa kumuuliza, maana akiwa si yeye itakuwa ni sawa na kujichoresha kwa Mpenzi wake, akaamua tu ngoja akomae hadi mwisho wake ataujua.
Uamuzi akaufikia kuwa ni kudharau tu juu ya mtumaji yule ambae yeye binafsi aliamini kwamba yule ni mtu anaemjua vizuri ndio maana hataki waongee, kwani huenda sauti akaitambua pindi atakapomsikia.
Siku moja ya kuzaliwa kwake akiwa yupo Hostel hana hili wala lile, akakuta mlangoni kwake kuna box kubwa sana la zawadi na juu ya lile box limeandikwa jina lake kwa herufi kubwa ambazo zilionekana hata kwa mbali.
Kwanza alijua huenda ule ukawa ni mtego, lakini akiwa amesimama kwa mashaka, ikaingia sms kwenye simu yake ikimtakia siku njema ya kuzaliwa kwake huku ikimuarifu juu ya uwepo wa box mlangoni kwake.
Ujumbe ulimwambia mle ndani kuna zawadi yake ya Birthday, hivyo kila kilichomo mle ndani ni mali yake na kila kitu kina uthibitisho ambao utamuhakikishia kuwa ni mali yake, hivyo afungue tu bila kuogopa na kutumia bila wasiwasi wowote, maana vitu vyote pale ni vyake yeye.
Zainab akamuita shoga yake mmoja na kumshirikisha, nae pia akaogopa. Wakamuita mtu wa 3, huyu sasa ndio alikuwa ni chakaramu hasa, hata kabla hajaelezwa chochote, alivyoona tu jina la Zainab Mapunda, akafungua box na kutoa Computer.
Ilikuwa ni Computer mpya kabisa aina ya Dell ikiwa na kila kitu, ilikuwa na Charger, Phones yenye mic palepale, mouse ya nje, warranty card na Risiti ambayo ilikuwa imeandikwa kwa majina yake yote mawili, bila kukosea.
Hakuamini Zainab, lakini hiyo ndio ilikuwa ni hali halisi, akatoa simu na kupiga namba ile ambayo ilimtumia sms, namba ambayo sasa alianza kuizoea kuchat nayo. Kama kawaida haikupokelewa, bali ikamtumia sms.
'Tafadhali Zainab, usipige simu, tuma tu ujumbe mfupi,' mara zote mtumaji wa sms zile hakuonesha dalili yoyote ya kimapenzi. Zainab akamtumia sms na kumwambia yeye binafsi hawezi kupokea vitu asivyojua ni wapi vimetoka.
Jibu lililorudi kutokana na ujumbe wake, lilikuwa ni jibu la kebehi, sms ilisema 'Zainab wewe ni mkubwa sasa, usipende kuongozwa kwa kila kitu, vingine kichwa chako chenyewe kijiongeze, risiti ina jina la duka iliponunuliwa hiyo mashine.'
Sms haikuendelea zaidi ya hapo, hata Zainab mwenyewe akajiona ni bonge la bwege, kwa aibu akarudisha vitu vyote kwenye box na kuliingiza ndani akisaidiwa na shoga yake mmoja aliekuwa nae pale.
Alipoingia chumbani, akjilaza kitandani na kuchukua ile risiti na kuisoma vizuri. Aliona namba ya simu, akapiga ili kujiridhisha, alipokea mwana dada mmoja na kusema hana uhakika na kile anachotaka kujua.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Cha msingi alimuambia ni heri siku ifuatayo afike dukani mapema ili waikague, maana inawezekana ikawa ni feki japo ina namba yake yeye ambae ndio mmiliki wa duka. Zainab akakubali na kuanza kuchat na Sungura pasina kumueleza lolote lililotokea.
Bado alikuwa akiamini mtu anaefanya hivi ni mtu ambae anamfahamu vizuri, japo hakumjua ni nani lakini kila aliemjua alikuwa hamuamini kwa asilimia mia moja, hivyo alikuwa akimtega hata Sungura, aliamini kabisa muda tu utawadia kama ni Sungura basi lazima atajichanganya mwenyewe.
Ndio maana muda wote alikuwa kimya pasina kumwambia kuwa kuna kitu gani kinaendelea, aliamini kama ni yeye ipo siku atajisahau na kuongea tu, walichat bila kuonesha dalili yoyote ya kupokea kitu kile cha thamani.
Mwisho akamuuliza Sungura ambae alikuwa hajamtumia salamu yoyote ya kumtakia furaha ya siku ya kuzaliwa kwake. Sungura akamwambia tayari ameisha mtumia kupitia Facebook, akamuuliza kuhusu zawadi.
Sungura akajitetea kuwa bado hajapata pesa, amvumilie hadi boom ikitema, Zainab akamwambia wala asijali kwani anamtania, kumbe akili yake ilikuwa wala haikuwa pale, yeye alitaka tu kumpima kama atakuwa ni yeye basi lazima angemwambia amemfanyia Suprise.
Wakaagana na kulala huku akiwa na maswali kibao kichwani, huyu mtu kaipata wapi siku yangu ya kuzaliwa? Akamuuliza kwa njia ileile ya msg, nae akajibu kifupi tu 'FB' Zainab akatikisa kichwa na kumjibu poa, akavuta shuka na kulala.
Asubuhi ya siku iliyofuata, aliamka na kufanya yake hadi saa nne asubuhi na kutoka kuelekea dukani ambapo ile Laptop ilinunuliwa. Alibeba risiti yake hadi sehemu yalipo maduka ya vitu vya umeme.
Kwa kuwa risiti ilikuwa imeandikwa jina na mtaa duka lile linapo patikana, alifika kwa urahisi na kukaribishwa. Aliulizia kama Laptop yenye risiti ile ilinunuliwa pale huku akimpa dada mmoja risiti ile.
Dada alieipokea risiti ile aliisoma na kufunua kitabu kuangalia Serial Number. Akafunga kitabu baada ya kuiona na kumwambia kuwa risiti ile ni halali na mteja wao aliinunua juzi jioni na kuiacha hadi siku ya jana ndio aliifuata.
Zainab akatikisa shingo yake kukubali kisha akanyoosha mkono kuiomba risiti yake, yule dada akamuuliza kama ina tatizo lolote, akamwambia hakuna bali alitaka tu kujua kama ni mali ya halali. Dada yule akamthibitishia vile na kumkaribisha tena kununua vifaa pale dukani kwao.
Wakati akitoka ikaingia msg ikimpongeza kwa uamuzi wake wa kuamua kuhakiki, kisha ikaingia sms nyingine wakati hata ile ya kwanza hajaifuta
"Hiyo bodaboda nyeusi aina ya Boxer, ambayo dereva wake amevaa Jaketi jeusi, itumie, mimi tayari nimeilipia kwa ajili yako!" Sms hii ya pili ilimtesa kidogo, akaanza kuangaza kule na huku, huenda akamuona mtu anaetuma sms zile.
Hakuweza kumuona mtu yeyote anae shughulishwa na simu zaidi ya kuona kijana wa boda boda alieambiwa, akimsogelea na pikipiki yake na kumsalimia, kisha akamuuliza
"Dada, nakurudisha chuo ama bado una mizunguko mingine?" Alihoji bodaboda.
"Kwani wewe ni nani hadi uniulize hivyo?" Zainab aliuliza kwa mshangao na hali anajua fika yule kijana ni nani.
"Mimi ni bodaboda na nimelipwa pesa na yule kaka uliekuwa nae dukani humo, ameniambia nikupeleke popote."
"Kaka gani aliekulipa pesa wakati mimi nimekuja peke yangu hapa?"
"Si yule aliekuwa na Prado nyeusi akapaki hapa wakati wewe ukiwa ndani!"
"Samahani kaka yangu, mie simfahamu huyo mtu," alisema huku akiondoka kwa miguu.
"Ha! Haya sasa maajabu..." Bodaboda akatoa simu na kufungua sehemu ya sms.
Huku akimfuata Zainab ambae alionekana kuwa na haraka, akamsogelea na kumuuliza kama anaijua ile namba, mwanzo Zainab akataka kukataa kusimama, lakini akili yake ikafanya maamuzi ya haraka na kusimama.
Alitamani sasa kujua, namba hiyo iliyomlipia pesa kwa bodaboda ndio ileile anayo wasiliana nayo yeye ama hii ni nyingine, akasimama. Yule kijana akamuonesha msg kutoka kwenye kampuni moja iliyotumika kumrushia pesa.
Thamani ya pesa ilionekana ni Shilingi Elfu Kumi na mbili ambazo kijana aliwmwambia amelipwa ili kupeleka popote hadi pesa ile itakapo kwisha. Zainab aligundua namba ni ileile, ikiwa imesajiliwa ka jina la MAKOS MAKOS.
Ghafla jazba ikampanda sana Zainab kuona anafuatiliwa na mtu asiemjua kila hatua anayofanya, kwani sasa alijua fika kabisa, mtu huyo sio Sungura. Akasonya na kumwambia yule kijana kwamba yule mtu alietuma pesa ni ile ni mpumbavu.
Akamshauri yeye aile tu na bodaboda ile wala yeye hapandi, kisha akaondoka eneo lile huku akimtumia sms Makos akimuasa akae nae mbali. Makos akapiga simu, lakini hakuongea baada ya Zainab kupokea.
Bali aliweka sauti ya muziki ndio ulisikika, ulikuwa ni wimbo wa Mariah Carrey uitwao My All ambao ulikuwa na maneno
'I would give U my all, to have just one more night with U, I risk my life to feel your body next to mine, coz I cant go on living in the memory of our song...'
Zainab akakata simu kwa hasira na kuita bodaboda nyingine iliompeleka hadi chuoni kwao akiwa ni mwenye hasira kedekede, wakiwa wanalikaribia geti kuu la kuingilia chuoni, aliweza kuiona Prado nyeusi ikitoka mle ndani na kuelekea upande mwingine, yaani ikwa kama vile imewatangulia mbele yao.
Iliondoka kwa kasi sana kama vile inakimbia kitu fulani hivi. Zainab akamwambia dereva wa bodaboda aiwahi ile gari. Kijana akakataa na kusema hana mafuta ya kutosha kulifukuza gari lile, kwani yeye anaweka mafuta kiasi tu kwenye pikipiki yake.
“Dada yangu pamoja na kuwa ninaweza kuipata gari ile, lakini tambua ile ni mashine ingine, hatari sana, akifunguka Yule…”
Basi ikabidi tu akatishe kuingia chuoni, lakini alipofika tu getini, mlinzi akawazuia na kumuuliza dereva wa bodaboda ni kiasi gani anadai kwa ajili ya kumleta chuo yule binti mrembo?
“Leo nina hela… Sema unamdai kiasi gani huyo malkia wa nguvu?”
Kijana dereva wa bodaboda akabaki anashangaa tu huku akumtazama Zainab ambae nae alikuwa akimkata jicho la hasira yule mlinzi. Hakuna aliemjibu yule mlinzi bali yeye mwenyewe tu akatoa shilingi Elfu 10 na kumpa dereva wa bodaboda.
Akamwambia akate pesa ya nauli ya kumtoa binti yule kule mjini hadi pale na chenji yake amrudishie, kijana hapo tena wala hakujiuliza, akapokea pesa na kukata, chenji akamrudishia mlinzi na kuwasha pikipiki yake.
Zain alikuwa bado hajateremka, akashuka kwa ghadhabu huku akiondoka kwa miguu akiwa amefura kwa hasira hata wao, yaani mlinzi na dereva aliemleta, wakiwa hawajui amemnunia nani.
Alielekea moja kwa moja hadi kwenye majengo ya chuo hali akiwa hana furaha kabisa. Aliingia chumbani kwake na kujifungia, akalia sana kwa kuhisi uhuru wake wa faragha unaingiliwa bila ridhaa yake.
Kilio kile wala hakikumsaidia lolote, kwani mambo yaliendelea hivyo hivyo, hakukuwa na mabadiliko yoyote. Sasa akaamua kula nae sahani moja, akampigia simu Sungura aje chuoni kuna dharula.
Hilo nalo likakwama, Sungura alishindwa kuja kwa sababu masomo yalikuwa ni magumu mno hasa kwa wanachuo wa mwaka wa kwanza. Lengo la Zain alitaka aje kumuumiza mtu huyo anaemtumia sms, maana kila kitu afanyacho yeye alimwambia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kutokuja kwa Sungura kukafanya lengo la Zain lishindwe kutimia. Hilo pia likamliza, aliona dhahiri hata Sungura ameshindwa kumliwaza? Ila alisahau kuwa hajamwambia Sungura sababu ya kumuitia huko wala hakukumbuka kwamba Sungura anasoma na anatakiwa kujituma sana.
Mwenyewe alikaa na kufikiri kuhusu kulia kwake, mwishoni akajiuliza hivi atalia hadi lini? Hivyo akaacha kulia na kuizoea hali ile, ikamlazimu tu sasa kuwa anachat tu na mtu huyo.
Hapo aliamini huenda itakuwa ni njia itakayo mpeleka kwenye kumjua mtu huyo kama si kupitia chatting, yaani kujitambulisha vizuri, basi mazungumzo atakayo zungumza nae, yatampa mwelekeo.
Hakuna tatizo lolote alilolipata kwa kuwa nae karibu ama kuchat nae, ila kilicho msumbua ni ile hali ya jamaa kujua shida zake nyingi kabla hajamwambia mwenyewe ama kujua matukio kadhaa yanayo muhusu.
Hicho kitu kilimtesa mno na akashindwa kujua kabisa ni kwa nini. Mawasiliano baina yake na Sungura hayakukatika wala kupungua, alimpa msaada mkubwa sana mpenzi wake bila kumueleza ni wapi anapata pesa ile ya kumsaidia.
Kichwani mwake Sungura alijua ni wazazi wake Zain ndio wanao muwezesha mtoto wao na vumbi ndio ile inayo muangukia na yeye, ili kupunguza mzigo kwa Simba ambae alikuwa ni mtoto wa mjini 'Mission town'.
Ukakatika mwaka mmoja pasina Zain kumuona Makos wala kusikia sauti yake, alitamani sana kumuona, aliamini kabisa huyo ni mtu anaemjua vizuri mno, lakini hakujua ni wapi anaweza kumuona ama ni sehemu gani anaweza kupata habari za kumuhusu yeye.
Alikata tamaa kwa kuamini Makos ni mtu alie karibu nae mno kiasi ambacho kila anachopanga anamjulisha bila yeye mwenyewe kujua, lakini bado aliamini ipo tu siku nae Makos atachoka na kujitokeza mwenyewe.
Siku moja akiwa amekaa na wenzie wakiwa wanafanya discusssion, simu ya Zain ikaita, namba iliompigia ilikuwa ni ya Matwiga ambayo aliihifadhi kwa jina la 'Bodi ya Mikopo' Aliipokea na kuongea nae.
Ilikuwa imepita muda mrefu mno hawajawasiliana, hivyo leo ilikuwa ni kama bahati tu kupigiwa na namba ile, pia tuseme ilikuwa ni bahati zaidi kwa upande wapili kwa simu yake kupokelewa.
Mpigaji alimuomba waonane nae, maana yupo Iringa kwa muda ule. Zain akakataa na kusema hayupo Iringa kipindi hiki, ameondoka kwenda Dodoma kwenye Field. Jamaa wa bodi ya mikopo akakubali na kumuomba iwapo atarejea Iringa, amjulishe ili waonane.
Zain akamwambia iwapo itatokea nafasi na akakumbuka, basi atamwambia, kwani haamini kama kitu hicho kinaweza kutokea kwake, kisha akacheka kwa kebehi na kukata simu, akawageukia shosti wake na kuwahadithia walicheka kwa sauti ya juu na kugonga mikono kwa furaha tele.
Wiki moja mbele akiwa kwenye mishemishe za kujipanga kwa ajili ya kutafuta sehemu ya kufanyia field, akapokea sms ikimwambia ajaze fomu ya maombi ya kufanya field kwenye shirika la Umeme Tanzania.
Mkoa alioambiwa natakiwa kuuandika kwenye fomu ni mkoa wa Mbeya, kwani kule kila kitu kilikuwa kimeandaliwa tayari kwa ajili yake, msg ile pia aliipokea toka kwa Makos. Kwa sasa Zain hakuwa na uwezo wa kumkatalia chochote Makos.
Pamoja na kuwa alikuwa bado hajamjua, lakini alitekeleza. Utaratibu ukaandaliwa kama alivyotaka Makos japo awali tayari walikubaliana na Sungura waende wakafanye field wote kwa pamoja mkoani Morpogoro, lakini akafuata mpango wa Makos.
Alichomwambia Sungura kuwa ni pendekezo la wazazi wake ambao ameshindwa kuwapinga, Sungura akamuelewa na kumtakia mafanikio ili afanye vizuri. Siku iliyofuata ilikuwa ndio siku ya Zain kuondoka kuelekea Mbeya.
Akatoka kwenda Stand ili kukata tiketi ya kuelekea Jijini Mbeya, akiwa njiani akapokea sms ikimueleza ni wapi aende kuchukua tiketi. Akatii amri, ajabu kufika kule akakuta tiketi ya Songea ikiwa na jina lake.
Akashangaa na kumuuliza wakala imekuwaje tena? Wakala akiwa hajui lolote, akamuuliza kama jina lile ni la kwake? Zaina kajibu ndio lake, basi wakala akamwambia kwamba yule aliekuja kukata tiketi ile ndio alieacha maagizo hayo.
Lakini Zain kabla hajaondoka, yule wakala akamwambia yule jamaa aliekata tikelti ile aliacha pia maagizo dirisha la pili, aende tu kuonesha tiketi ile watampa maelekezo mengine ya ziada.
Zain akasogea na kuwaonyesha ile tiketi kama alivyo ambiwa. Akashangaa zaidi baada ya kupewa tiketi ya Songea hadi Mbeya ikiwa ni ya siku 3 mbele. Akabaki amesimama tu hajielewi hadi alipokumbuka kutoa simu.
Akamtumia sms Makos na kumuuliza mbona hajielewi, Makos akamwambia Zaina yeye afuate tu maelekezo kila kitu kimeandaliwa wala asiwe na shaka yoyote. Tena Makos akamtoa shaka kwa kumwambia hapaswi kujiuliza suala la kwenda kwao.
Makos akamwambia kuwa kuna sababu 3 zinazomfanya amshauri kwenda Songea na kumwambia moja tu ambayo ni kubadili mazingira, zingine mbili akamuahidi akiwa Songea atamueleza zilizobakia.
Akawa mpole na kukubaliana na Makos, hata kabla ya kurejesha simu mfukoni, ikaingia msg ya pesa kutoka mtandaoni, alipoifungua ilikuwa ni pesa kiasi cha shilingi laki 1, toka kwa Makos, akamshukuru na kurejea chuoni kujiandaa.
Akiwa chuoni akampigia simu Sungura ambae siku ile tayari alikuwa amewasili Morogoro kuanza field, akatumia nafasi ile kumuaga kwa kumwambia anaenda Field Mbeya lakini kwanza anarudi nyumbani Songea.
Sungura akataka kujua kama kuna usalama, Zain akamwambia ni salama tu ila anaenda kwa siku kama mbili ili kuchukua kiasi kidogo cha pesa kwa wazazi ili akifika kule asisumbuke hasa ukizingatia yeye ni mtoto wa kike.
Utetezi wake ulikuwa unajitosheleza sana, Sungura akamwambia anafurahi mno kuona mpenzi wake amemaliza mwaka wake wa kwanza kwa ushauri wake yeye. Lakini bado Zain hakuwa amemwambia kuhusu mahusiano yake na Makos.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Moyo ulitamani mno kumwambia kinacho endelea, kwani alikuwa akimpenda Sungura kwa dhati, lakini mdomo nao ukawa ni mzito kutamka juu ya jambo hilo, akili ndio ilikuwa ikiongoza kwa kumpa sababu muhimu ya kutolisema jambo lile.
Sababu ilikuwa ni kwamba asimwambie jambo hilo kwa kipindikile hadi kipindi ambacho watakapokuwa pamoja, yaani kwa kuishi na sio kwa kila mmoja kuwa mbali na mwenzie kama walivyo sasa.
Wakaagana kwa mabusu motomoto na mwisho Zain akamrushia mpenzi wake kiasi kidogo cha pesa ambacho kiukweli kilimpiga sana tafu, maana alikigawa na kumtumia kaka yake pia ambae alikuwa ni mgonjwa.
Siku iliyofuata Zain aliondoka Iringa kuelekea kwao Songea na kupokelewa na wazazi wake ambao walifurahi mno kumuona, lakini alikuta baba yake ameumia mguu wa kushoto. Akauliza tatizo ni nini? akajulishwa kuwa aligongwa na bodaboda wakati akivuka barabara.
Hali haikuwa mbaya sana, Zain akamshukuru Makos kwa kuratibu safari ile na kumueleza juu ya ajali ya mzazi wake. Makos akamjibu anajua na ndio sababu ya kumwambia aanzie kule, kwani wazazi hawakutaka yeye ajue, Alishangao mno Zain.
“Ha!” alishangaa mno Zain na akamuhoji Makos alijuaje kama mzazi wake kaumia na hataki yeye ajue na hali hata kwao hapajui na hajawahi kumuelekeza. Makos akamjibu kuwa yeye alikuwepo hapo nyumbani kwao siku ya pili baada ya ajali.
Kwanza Zain akashtuka kusikia vile, na kuhoji kama Makos anapajua kwao, anasahau kwamba swali lake amelijibu tayari hapo juu, akauliza tena kama kwao wanamtambua, Makos akamwambia ndio.
“We kwetu wamekujulia wapi? Ama nawe umeishi mtaani kwetu nini?” Zain alimuuliza na Makos akaendelea tu kufunguka
Makos akamjuza kwa kumwambia kwamba amekwenda huko kwa nia moja ya kujitambulisha tu na kweli amefanikiwa kwani amejitambulisha na kuwaambia ukweli kuwa hawajaongea wao bado na kuomba nafasi ya kutekeleza majukumu yote kama mchumba, na hiyo ndio sababu ya pili ya yeye kwenda kwao.
'Nawe nimetaka uende ukakae chini na wazazi na kulizungumzia suala hilo mbele ya wazazi nikiamini muafaka utafikiwa vizuri tu ili name nichukue jukumu langu kama mchumba halali wa Zain, malkia wangu wa nguvu.' Ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Makos kwenda kwa Zain.
Alipigwa na butwaa Zain na kumuuliza tena Makos, kuwa hiyo ndio sababu ya misaada ile ambayo amekuwa akimpatia? Makos akamjibu kwamba ile sio misaada bali ni haki yake akiwa kama mtu ambae amechunukiwa na moyo wake.
Zain akamuuliza kama hajui kuwa yeye Zain ana mpenzi wake? Makos akamjibu kuwa watu huwaacha wazazi wao tena wakiwa wanawapenda na wanawahitaji ije kuwa mpenzi tu ambae wamekutana tu wakiwa ni wenye akili?
Kauli ile ilimtia hasira sana Zain na kujikuta akimtukana Makos na kumwambia kwamba tangu muda ule hataki tena mawasiliano nae. Makos hakuonesha kukasirika, bali alimkumbushia kwamba ana siku mbili tu za kuwepo pale Songea.
Mambo ya Makos yalimchanganya mno Zain hasa pale alipomwambia siku moja ya kuwepo Songea tayari imeisha, imebaki moja tu ambayo ni kesho, hivyo ajiandae kwa safari yake ya Iringa kuripoti kwenye field.
Akakasirika Zain na kumwambia asimpangie, kisha kazima simu yake na kutoka chumbani alipokuwa amejilaza kitandani kuelekea chumbani kwa mama yake. Bahati nzuri akakutana nae mlangoni.
Mkononi mama yake alikuwa ameshika kibox cha simu, muonekano wa kibox kile ilionesha kuwepo kwa simu mpya kabisa tena ilio onekana ni ya kisasa mno, Zain akaipenda na kumpokonya mama yake huku akiisifu ni nzuri.
Mama yake akiwa anamtazama mwanae na tabasamu usoni, wakati huo Zain alikuwa akiitoa simu ile kwenye box lake, kisha mama akamuuliza mwana
"Mwanangu kuna mpango gani kati yako na Sungura?" Swali hilo lilimshitua Zain, lilikwa ni swali ambalo hakulitarajia kwa muda ule, akaacha kukagua simu na kumtazama mama yake kwa mshangao kama ndio leo anamuona kwa mara ya kwanza vile.
"Mama mbona umeniuliza hivyo?"
"Nimekuuliza kwa sababu ninataka kujua..."
"Mama itakuwa ni mapema mno kwa mimi mkuzungumzia jambo hilo, je nikisema kitu fulani na kesho kisitokee ama kikatokea tofauti na nilicho kisema, nitaeleweka vipi?"
"Sawa, lakini si unajua aliewahi kuripoti kituoni ama kushitaki, ndio mwenye haki zote za awali?"
"Ndio mama lakini baada ya uchunguzi kila mmoja hupata haki zake," alikataa Zain.
“Hapo kwenye uchunguzi sasa ndio pagumu…”
“Unamaanisha nini mama?” kauli ilikuwa tete sana, hakuielewa Zain
“Kuna vitu vingi hutokea hapo katikati, likiwepo suala la muda kama hamjielewi wewe na huyo Sungura, shauri yenu, ipo siku mtalia kilio cha samaki," Mama alisema huku akiondoka na kumuacha mwanae akiwa kama vile hajielewi.
Zain akajishika tama huku akitafakari maneno ya mama yake, alishindwa kabisa kuupata muafaka na kichwa chake kutokana na maneno ya mama yake, akaona jambo jema kwake ni kumfuata alipo ili kumuuliza maana ya maneno yale makali.
Maana aliona kama kuna kitu hivi kati yake na Sungura, hakujua hata yeye hatma ya penzi lao, lakini alitambua vema kwamba hakuna kati yao hata mmoja ambae angeweza kuishi bila ya mwenzie.
Safari yake iliishia jikoni, alimkuta mama yake akiwa na kazi zake, akamuuliza mama yake maana ya maneno yake yale, mama akamwambia anapaswa kutulia hadi muda utakapofika ndio atajua maana ya maneno yale na kila kitu kitakuwa wazi.
Kisha mama nae akamuuliza mwanae kama ile simu kaipenda? Zain alijibu kwa kutikisa kichwa huku akiwa na tabasamu usoni mwake, mama akamwambia ile simu ni yake, Zain akafurahi na kumkumbatia mama yake na hakusahau kumshukuru.
Mama nae alikuwa katabasamu na kutikisa kichwa kukubali shukrani za mwanae, kisha akauliza huku akimtazama usoni
Kawaida macho huongea mapema kuliko mdomo, kizuri zaidi kwa upande mmoja, yaani upande wa ukweli na kibaya kwa upande mwingine, yaani upande wa uongo ni kuwa, macho yanaweza kuongea kile ambacho mwenye macho anaweza akashindwa kuongea
"Zain unamjua Makos?" Zain aliekuwa kaifungua simu ile kwa nia ya kuweka Sim Card, akaacha na kumuangalia mama yake kwa jicho la udadisi mno, na badala ya kujibu swali lile, nae akamuuliza mama yake;
"Mama kwani nawe unamjua Makos?" Alishangaa na kusahau kama tayari Makos aliisha mwambia zamani kuwa alifika kwao kujitambulisha.
"Kwani wakati nakuuliza kuhusu Sungura hukunielewa ninamaanisha nini?" Wakawa kimya wote, ndio sasa Zain akaamini Makos alifika kwao, japo awali alichukulia kama ni maneno tu ili awe karibu yake.
Ukimya ulivyokuwa ukiendelea, mama ndio akauvunja kwa kumwambia mwanae
"Hata hiyo simu ulioipenda nami kukupa, wala sijakupa mie, hiyo ni yako na ni yeye ndio alieileta na alinikabidhi tu tukiwa hospitali, sasa hebu niambie ukweli wote ulivyo," alisema huku akiweka kwenye stuli ndogo iliyokuwepo pale sahani aliyokuwa nayo mkononi na kumtazama mwanae kwa umakini.
Ni kama mtu aliekuwa akitaka kusikia kitu cha muhimu sana, Zain akashusha pumzi kwa nguvu na kufikiri kidogo, kisha akajipangusa uso na kusema
"Mama yangu, kiukweli huyo Makos mimi binafsi sijawahi kumuona hata siku moja na hata mara moja hajawahi kunitamkia suala la mapenzi na huwezi kuamini hata sauti yake siijui,ila nimekuwa nikiwasiliana nae kwa mwaka sasa lakini kifupi mama mimi ninampenda sana Sungura," sasa ikawa ni zamu ya mama kushusha pumzi kwa nguvu na kufikiri kidogo, nae akasema kuuliza
"Wewe na Sungura mna mpango gani, hili ni swali ambalo unalikwepa sana Zain lakini unapaswa tu kulijibu?"
"Mama mipango yote itapangwa mara tu baada ya kuwa tumemaliza masomo yetu na muda huu itakuwa ni kama vile tunadanganyana tu," Alijibu Zazam kwa sauti ya upole sana lakini yenye kumaanisha kile akisemacho.
"Mwanangu jiangalie sana, kutokua na maamuzi ni kujiweka kwenye wakati mgumu wewe mwenyewe, jitazame vizuri, baadae utakuwa kwenye hali ngumu zaidi iwapo hutaamua sasa, sawa Zain?" Mama yake akamuasa huku akigeuka kuendelea kupakua chakula.
Zain akabaki akitikisa kichwa peke yake kukubali lakini akiwa tayari kaisha zongwa na mawazo mengi, alikuwa akiwaza jinsi mama yake anavyomshawishi kufanya maamuzi.
Akarejea chumbani kwake na kujitupia kitandani kwake akiwa kachoka kabisa tena kwa ghafla. alikuwa kifikiria sana kuhusu huyu mtu aitwae Makos, Huyu Makos ni nani? Na kwanini hataki kujionesha? Pia ni kwanini hapendi kuongea nae?
Akanyanyuka na kuchukua simu yake mpya aliyopewa na kuamua kumpigia simu Sungura ili kujua mpenzi wake anaendeleaje huko alipo. Waliongea kwa takribani dakika 20 hivi. Sungura alimshukuru mno kwa kile kiasi cha pesa alichompatia.
Kwani alimwambia ni kiasi gani imesaidia kumtibu kaka yake ambae yupo huko anaumwa na hakuwa na pesa kabisa hadi ile pesa aliyompa ndio akamtumia na kwenda hospitali. Zain akampa pole na kisha akamuaga na kukata simu, kilichofuatia ni kuchapa usingizi.
Makos hakutuma ujumbe wowote siku ile waliyokwaruzana na Zain hadi siku ya pili. Siku hiyo mara tu baada ya kuamka, Zain akapanga kwenda kumuona Simba bila hata ya kumjulisha yoyote kati ya ndugu wale wawili.
Alifika na kumkuta Simba alkiwa kalala nje kwenye mkeka akiwa na baadhi ya wachezaji mpira wenzake wakipiga story tu huku mzazi mwenzie na Simba akiwa pembeni yake. Wote walimuona wakati akija lakini hawakujua kama alikuwa akienda pale.
Hivyo hadi anafika hakukuwa na maandalizi yoyote ya kumpokea, Simba pekee ndie aliekuwa akimjua na alikua akijua wazi kuwa Zain hawezi kuja pale wakati Mpenzi wake Sungura akiwa hayupo, hivyo waliendelea tu kupiga soga.
Aliwasalimia na kufanya Simba aanze kuwapanga wengine ili Zain apate pa kukaa. Alimjulia hali yake na kumtakia afya njema. Hakukaa sana akaaga, akatoa pesa tena kiasi kidogo na kumpa shemeji yake, kisha akaondoka.
Alitokea kuipenda sana familia ya kina Sungura ambayo kiuwezo wala haikuwa na kipato kikubwa. Familia yao nayo ilikuwa na kipato cha kati lakini sasa yeye alikuwa na uwezo wa kipesa kupitia Makos ambae alimtumia tu pesa wakati wowote aliojisikia kutuma pesa.
Wakati akiwa njiani anarejea nyumbani, akahisi kama kapungukiwa na kitu fulani, akagundua tatizo ni Makos, alikua amemzoea sana, akamtumia ujumbe mfupi. Nae Makos ni kama mtu aliekuwa akitegemea ujumbe muda ule, akaujibu haraka sana.
Wakaendelea kuchat kwa muda kidogo, mwisho Makos akamuuliza kama yupo tayari kuondoka siku ifuatayo. Zain akamuuliza ni kwanini anataka kujua? Akamjibu kuwa anahisi labda bado anataka kuendelea kukaa na wazazi.
Zain akamjibu kuwa ameishi na wazazi kwa zaidi ya miaka 20 na sasa ni muda wake wa kuandaa maisha yake binafsi. Makos akamjulisha kuwa maisha yake tayari yameisha andaliwa, bila kumueleza zaidi akaomba muda wa kufanya kazi na kuaga.
Siku iliyofuata Zain aliondoka kuelekea Iringa. Mawasiliano baina yake na Makos yakazidi maradufu kuliko awali, lakini hakuacha kuwasiliana na Sungura, aliwasiliana nae asubuhi na usiku. Muda mrefu mchana alichat na Makos kupitia WhatsApp lakini hakuwahi kumuona picha yake.
Aliomba kumuona hadi akachoka mwenyewe, kila siku alikuwa akimwambia atamchoka tu kwa suala la kumuona ama kumsikia, maana watakuwa wote muda wote wa maisha yao uliobaki, avute tu subira. Zain akazoea sasa na hakusumbuka tena kumuuliza kuhusu kumuona wala kumsikia.
Ikiwa imesalia miezi miwili kutimia miaka miwili ya masomo, kwa mara ya kwanza Makos alimpigia simu Zain na kuongea nae. Hakuamini siku hiyo, waliongea takriban nusu saa nzima, ajabu Zain alijisikia amani na faraja tele.
Alitamani waendelee kuongea zaidi lakini muda ulikuwa hauwaruhusu kufanya hivyo, baada ya kumaliza kuongea na kukata simu, Zain akaanza kuulaumu moyo wake, kwa nini umeanza kuonesha nia ya kumpenda Makos?
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akazuga kwa kumpigia simu Sungura, maana alihisi kabisa moyo wake unaweza kumsukuma nje Sungura. Waliongea kwa dakika chache na Zain akamuahidi kumtumia nauli ili aende kwenye sherehe yake ya kumaliza chuo, walikubaliana hivyo na kuagana.
Sungura sasa kajipanga kwelikweli kwa ajili ya siku hiyo, aliamua ajinyime kweli hadi ikifika siku hiyo nae akafanye mambo ambayo watu wote hawatoamini. Alijipanga kuanzia mavazi hadi zawadi bila kusahau mambo kibao aliyomuandalia mpenzi wake.
Siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa ikawadia, ndugu, jamaa na wazazi wakajumuika na familia zao kwenye sherehe ya kuwapongeza kumaliza masomo baadhi ya vijana wao. Simba na Sungura nao walikuwepo kama waalikwa.
Zain alituma pesa kwa Sungura ambae alimtumia na ndugu yake ili aje kushuhudia shem wake akivaa joho na kutunukiwa cheti akiwa ni mmoja kati ya wahitimu wa mwaka ule.
Kama alivyokuwa amedhamiria Sungura, alipendeza hasa na aliweza kununua zawadi ambazo zilivutia wengi, lakini hawakujua kuwa mwenzao alijipanga kwelikweli hadi kutimiza vile. Alijinyima mno hadi kutimiza vile.
Ulipofika wakati wa kutoa zawadi wakatoa zawadi na kupiga nae picha, walikuwa wana furaha sana wao waalikwa, lakini mualikaji alikuwa na sura ya wasiwasi, kipo kilicho sababisha hali ile.
Makos hakuwepo siku hiyo, hicho kitu ndio kilicho mkwaza mno Zain ambae alikuwa akitegemea uwepo wa Makos siku hiyo kwani ndivyo alivyokuwa ameahidi kuonana nae kwa mara ya kwanza.
Zain akiwa na jazba akajiapiza kuwa hatopiga simu kwa Makos wala kumuuliza ni kwa nini hakutokea kwenye sherehe yake.
Kile ambacho yeye alikuwa amekitegemea hakikutokea, alitegemea kumuona Makos siku hiyo kwa mara ya kwanza lakini ndio hivyo hakutokea na hakutoa taarifa yoyote. Sherehe ilikamilika na kila mtu akashika njia yake kurejea kwake ikiwa ni jioni kabisa.
Familia ya Mzee Mapunda ililala kwa ndugu yao maeneo ya Mianzini, wakati Simba na nduguye Sungura walilala Guest iliokuwa maeneo ya palepale jirani na walipofikia familia ya Mzee mapunda.
Hata usafiri walitumia mmoja ambao ulikuwa ni Noah iliyokuwa chini ya Zain kama kivuli, kwani Makos alikuwa akihusika na uwepo wa gari ile pale japo mwenyewe hakuonekana kabisa kwenye shughuli ile.
Saa 6 za usiku akiwa katikati ya usingizi, simu ya Makos ilimuamsha Zain. Akajishauri sana kuhusu kuipokea, baada ya kuiacha iite hadi ilipo kata, Makos akapiga tena, Zain safari hii akaikata, Makos akarudia tena kupiga.
Zain akaikata tena nae na sasa akaizima kabisa na kulala usingizi wa raha. Aliamka mapema asubuhi ile na kusahau kuiwasha simu yake hadi pale mama yake alipomfuata chumbani alipokuwepo na kumpa taarifa ya wito.
Alikuwa bado yupo kitandani wakati mama yake alipoingia ndani na kumwambia wamepokea ofa ya chakula cha mchana kutoka kwa Makos, ambae amewaalika kwenye tafrija hiyo itakayofanyika nyumbani kwake hapo hapo Iringa mjini.
“Amesema ni hapa hapa mjini panaitwa Ruaha, we alikupigia ukawa hupatikani, mimi amenipigia mama yake kunialika chakula hicho cha mchana,” aliongea mwenyewe Zain akimsikiliza tu.
Mwanzo Zain alionekana kutaka kuipotezea ofa ile ikiwa ni kama kujibu apigo ya kile alichofanyiwa na Makos, lakini baada ya kujifikiria kwa sekunde kadhaa, akamkubalia mama yake kuwa watakwenda.
Kichwani mwake alitafakari kitu kimoja kabla ya kuamua kwenda ama kutokwenda, alijua vizuri kuwa yeye anatakiwa kumuona Makos, kwani kwa miaka miwili hakufanikiwa kumtia machoni. Alikuwa na hakika kabisa Makos anamfahamu vizuri na wakati wowote ina maana akihitaji anamuona, yeye je?
“Saa nyingine ninapishana nae njiani pasina kumjua kama ndio yeye, huenda tunasalimiana nae humuhumu uswazi, nisipoenda nitakuwa nimemkomoa nani?”
Akaamka na kumpigia simu Sungura kutaka kujua usiku uliopita ulikuwaje upande wake hapo ugenini? Sungura akamwambia upande wake ulikuwa ni usiku mzuri tu na ameufurahia hasa kwani amemuona mpenzi wake, pia ameshuhudia akimaliza masomo.
Sasa Zain alijihisi kuwa na furaha, alihisi kidogo kupata faraja kutoka kwa mpenzi wake baada ya kukerwa na Makos siku iliopita. Mwisho Sungura akatumia fursa ile kumuaga kuwa anarudi Singida ambapo yupo field kwa sasa.
Kama kawaida huwa hamuachi mikono mitupu mpenzi wake, akamtumia pesa kiasi na kumtaka wawasiliane kila baada ya muda fulani ili ajue walipofika kutokana na ajali nyingi za sasa hapa nchini.
Alishukuru mno Sungura maana alikuwa hata hata mia ya kuanzia pindi atakapofika Singida, hakuwa na chanzo kingine cha kupata pesa zaidi ya Boom, hivyo pesa ile ilimpiga tafu sana. Alipopokea tu akamtumia ujumbe wa shukrani.
Makos bado aliendeleza mambo yake yaleyale, pamoja na kuwa sasa walikuwa wameanza kuongea, lakini akamtumia ujumbe na kumtaarifu kuwa kuna Taxi ameituma hapo imfuate kumpeleka dukani kununua nguo.
Alimwambia dereva yule analijua ni duka gani ampeleke, hivyo atampeleka na kumsubiri ili kumrejesha. Anachopaswa yeye kufanya ni kuchagua tu nguo tu na kuchukua kwani tayari yeye ameisha weka order na amepewa vocher.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hapo kuna Voucher ya thamani ya laki 3 anayo huyo dereva wa Taxi anaekuja kukuchukua, usihofie chochote, nadhani itakutosha, na kama kutakuwa na tatizo jingine lolote nijulishe Zain,” ilikuwa ni sauti ya taratibu ya mwanaume akionesha jeuri ya pesa, hakusema maneno mengi akakata simu.
Uwezo wa kukataa Zain hakuwa nao, akatoka nje na kukuta gari ikimsubiri, akaingia na kutoka ikiwa ni saa 3 asubuhi. Alikwenda hadi dukani, lilikuwa ni moja kati ya maduka makubwa kwa pale Iringa mjini, ni wachache mno walioingia mle, maana paligharimu pesa nyingi mavazi yake.
Mwanzo hata nae alipokabidhiwa ile voucher yenye thamani ya pesa ile alijua atarudi na mzigo, lakini kumbe alikuta nguo ghali lakini zenye ubora mkubwa na kuchagua nguo atakazo ambazo aliona zitamfaa kwa mtoko ule wa mchana anao utegemea.
Walirejea saa 4 na baada ya dereva Taxi kuondoka akawaambia wazazi wake kuwa watafuatwa pale na dereva yule waliekuwa nae siku iliyopita pindi itakapo timu saa sita mchana, hivyo wajiandae kwa ajili ya kutoka.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment