Search This Blog

Friday, October 28, 2022

NENDA NA MOYO WANGU - 3

 

     





    Simulizi : Nenda Na Moyo Wangu

    Sehemu Ya Tatu (3)





    "RIPOTI YA KIfO CHA BEATRICE MTOTO WA KiGOGO WA UN YASIKiTISHA"

    Nikavutika na maandishi hayo, kisha nikachukua gazeti lile na kusoma

    kilichoandikwa ndani. Habari ile ilinishangaza na kunishitua sana,

    mwandishi aliandika kilichotolewa na daktari baada ya uchunguzi.

    "Katika damu ya binti huyo wa Bw Oscer, kumekutwa na sumu kali aliyoinywa

    katika bia" sehemu ya habari hiyo ambayo ilinishitua. Ni saa ngapi Beatice

    alikunywa pombe? nilirudi naye mpaka nyumbani kwake kisha mimi nikaondoka,

    hakuna sehemu ambayo Beatrice alikunywa pombe.

    "Haiwezekani" nikasema kwa nguvu kisha mapigo yangu ya moyo yakaenda mbio

    sana "kuna mchezo"

    Nikarudishwa mahabusu na yule askari wa kike na kukuta nimekwisha andaliwa

    chai ya maziwa pamoja na mkate uliopakwa Blueband na jam. Nikiwa mwenye

    mawazo mengi juu ya ujio wa Michael na habari ile ya kifo cha Beatrice,

    ilinibidi nile haraka haraka kabla sijapoteza hamu ya kula kisha nikashinda

    njaa. Nilipomaliza kula, nikapanda kitandani kwangu miguu nikaikunja na

    kuikumbatia katika kifua changu. Hapo nikawa nawaza.



    SIKU YA TUKIO LA MAUAJI YA BEATRICE.

    "Usiku ule wakati tunatoka pale katika sherehe, Beatrice hakuwa na kilevi

    chochote kichwani mwake wala kinywa chake hakikutoa harufu ya pombe. pombe

    aliinywa saa ngapi kwa kuwa hata nilipokuwa nikimbusu, sikusikia harufu ya

    kilevi"



    INAENDELEA HAPA Nikakunjua miguu yangu na kuifunga mnikono yangu kifuani

    kisha nikasimama nikawa nazunguka zunguka katika kile chumba.

    "Vipi Michael? Kwanini haoneshi kuumia kwa mimi kupata kesi kubwa namna

    hii? Kwanini yeye ni kama anashiriki kunihukumu kuwa mimi nimeuwa?

    Inawezekana Michael akawa anahusika ama anamjua muuwaji? Muuwaji ni nani na

    Michael afurahie kufungwa kwangu? Ama Michael ameamua kufanya kitendo cha

    heri tukose wote?"

    Hapo nikakaa tena kitandani nikashika kichwa changu kwa mkono niliopegemea

    katika paja langu.

    "Tukose wote? Yaani Michael anaweza kumuua Beatrice ili tukose wote? Ina

    maana hana roho ya huruma kiasi cha kutazama hisia zake? Na kama si Michael

    ni nani basi? Nani awezaye kuwaza kuwa Beatrice ana uhusiano na mimi?"

    Niliwaza mengi na kukiri kwa sauti ya juu mara baada ya kushusha pumzi

    ndefu nikajisemea "Nimekamatika"

    Sauti ya yule askari wa kike ikanizindua aliposema "Muda wa kuoga na

    kubadilisha nguo zako za kiraia"
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijitazama nikakumbuka kuwa tangu nilipokamatwa jana, sikuwa

    nimebadilisha nguo wala kuoga. Nikavua ile shati niliyovaa kisha suruali

    nikajifunga taulo lililopo pembezoni mwa mto katika kitanda changu. Yule

    askari alirudi tena akiwa na nguo yaani suruali na shati nyeupe

    zilizokuinjwa vizuri na kunipatia pamoja na sabuni na mswaki kisha mimi

    nikaziweka zile nguo pale kitandani na kutoka naye nikiwa na sabuni na

    mswaki mkononi. Akanipeleka katika vyoo vya mahabusu huko nikaoga kwa muda

    wa nusu saa. Nilioga kwa muda mrefu kutokana na mawazo yaliyoandama kichwa

    changu kwa muda mrefu.

    Nilipotoka na mara baada ya kuvaa, alikuja Jafary Hiza aliyeongozana na

    Vanessa Noel.

    "Habari yako Ramon"

    Vanessa alinisalimu huku Jafary Hiza akinitazama kwa jicho baya ambalo

    sijapata kuliona kamwe.

    "Nzuri tu sister za tangu jana?"

    Vanessa akatabasamu kisha akanijibu "Nzuri pia, naona leo umechangamka

    tofauti na jana?"

    Sikumjibu. Wakaingia askari wawili wakataka kunifunga ile pingu yenye

    mnyororo Vanessa akawasihi.

    "Msimfunge tafadhali kuna ulinzi wa kutosha kuliko kumfanya hivyo" Vanessa

    akamtazama Jafary Hiza kisha akasema "Unajua unapomtuhumu mtu haina ulazima

    wa kufanya hivi tunavyomfanya kwa kuwa kama ni kesi ya kusingiziwa

    itamuondolea kujiamini na kujihisi kuwa yeye ni mhukumiwa tayari. Tumpe

    uhuru kiasi"

    Jafary Hiza hakujibu kitu na uso wake ulionesha kukereka na jambo hilo

    akaondoka na kutuacha mimi na Vanessa. Vanessa alinichukua mimi mpaka

    katika chumba kile cha mahojiano tulichokaa siku ya kwanza mimi naye.

    Nilikaa na yeye akakaa, akaniambia huku akiwa na uso wenye tabasamu.

    "Ramon, nilipokuwa nyumbani nilitamani sana muda huu. Naomba uendelee na

    ile hadithi ya wewe Beatrice na Michael"





    AKAWASHA ILE TEPUREKODA YAKE NA MIMI NIKAANZA KUZUNGUMZA-:



    "Unakumbuka nilipoishia?"

    Nilimuuliza Vanessa. Kisha akaniambia

    "Mlikuwa carteen mkila mara Beatrice akakumwagia juisi mlipogongana"



    SASA NIKAWA NIMEKUMBUKA, NIKAENDELEA.



    Beatrice aliniomba msamaha kwa kunichafua na ile juisi kisha akatoa kitambaa chake cheupe chenye maandishi yaliyoandikwa kwa wino mwekundu ambayo sikuweza kuyasoma, akawa ananifuta pale juisi iliponimwagikia. Wakati huo Michael na Steven walikuwa wakinitazama, Lakini Michael alinitazama kwa jicho baya sana tofauti na Steven aliyekuwa akitabasamu na kunioneshea dole gumba la poa. Sikujali kuhusu Michael.

    Nilimshika Beatrice mkono ambao alikuwa akinifuta futa pale nilipochafuka, kisha akauinua uso wake na kunitazama. Nikamwambia kwa sauti ya upole

    "Usijali nitaenda kuifua"

    "Naomba unisamehe sana ilikuwa ni bahati mbaya" akanisihi kwa sauti laini ya kubembeleza na mimi ikaniteka sauti yake nikabaki nikimtazama. Kisha kwa sekunde kadhaa akautoa mkono wake kutoka kwangu na kuniambia "Naitwa Beatrice" akanipatia mkono wake kama ananisalimia na mimi nikaupokea nikajibu.

    "Ramon"

    Niliona macho yake yaking'aa kama aliyesikia nikiwa nimezungumza jambo la ajabu sana, nikatoa lile tabasamu ambalo huwa ni nadra sana kulitoa kwa kila msichana kwa kuwa si wote walistahili zawadi hiyo adhimu kutoka kwangu. Lakini Beatrice alistahili.

    Nilipomuona Beatrice kwa mbali sikuwa na chochote nilichohisi kutokana na ukweli kwamba nilishagundua kuwa Michael anampenda msichana huyu lakini nilipokuwa karibu yake tukitazamana, moyo wangu ulibadilisha mapigo yake ya kawaida na kwenda kasi sana. Jasho lilikuwa likinitoka huku mikono yetu ikiwa hewani imeshikana.

    "Nimefurahi kukufahamu Ramon" akatoa tabasamu laini na kubahatika kuliona jino la rangi ya madini ambayo kwa kipindi kile sikuweza kuyajua ni madini ya aina gani kisha akanieleza "Mimi nipo Ba wewe uko wapi?"

    "Social leo ndio nimewasili chuo"

    Akatabasamu tena kisha akautoa mkono wake kwangu na kuniambia "sawa Ramon tutaendelea kuonana na si vibaya siku moja ukaja kunisalimia katika hostel zetu"

    "Poa"

    Kisha kila mmoja akarudi katika meza yake. Kwa Beatrice ile kusimama na mimi ikawa kama sherehe kwa kuwa niliona wenzake wakifurahia jambo ambalo mimi sikulijua huku kwangu ikiwa kasheshe kwa Michael.

    "Umefurahi sasa we boya?" Michael akaniuliza akiwa amekunja ndita kwa hasira. Kabla sijamjibu chochote akanyanyuka na kuondoka zake. Mimi nikabaki nikimtazama Steve kwa mshangao huku nikipandisha mabega yangu juu kisha nikayashusha chini steve akautupa mkono wake hewani na kunieleza.

    "Mpotezee boya tu"

    Baada ya kumaliza kula tukanyanyuka na Steven kisha tukaondoka.



    BAADA YA KUAMALIZA HADITHI HIYO YA CHUONI NIKAKUMBUKA JAMBO LINGINE MUHIMU:-"Halafu nisisahau jambo Vanessa!" Vanessa akanitazama na kuacha kile alichokuwa akikiandika "Michael alikuja leo asubuhi"

    "Alikuja? Enhe ilikuaje?"

    Nikamuelezea Vanessa kila kitu kilichotokea asubuhi juu yangu mimi na Michael lakini hakuzungumza chochote bali aliguna tu na kuniambia niendelee kuhusu Beatrice.

    Nikaendelea kumueleza maisha yangu ya siku ya kwanza pale chuoni. Siku hiyo yote Michael hakuniongelesha licha ya kuwa ndio siku ya kwanza kukutana na Michael katika maisha yangu. Nikaifahamu tabia ya Michael vyema. Niimuona kuwa ni mtu asiye na busara mwenye wivu kupindukia na pia ni mtu asiye na ustahimilivu. Nikajichekea nilipomuona kajinunisha akitazama movie ya mwanadada Angelina Jolie "salt" moyoni nikajisemea 'unatazama kwa macho lakini huna unachoelewa wala kufurahia kwa kuwa una hasira na mimi' nikatoa mguno wangu wa kebehi ambao bila shaka ulimkera Michael, nikamsikia akisonya wakati nikipanda juu ya kitanda changu.

    Siku ya kwanza ikawa imeisha nikiwa ndio mgeni katika chuo kikuu cha dodoma.

    Ikawa ni siku ya kwanza kukutana na Beatrice mwanamke aliyebadilisha maisha yangu kutoka katika hali ya kutamani kila mwanamke na kufanya naye ngono na kuwa naye yeye peke yake. Mwanamke ambaye leo ameniweka katika kitanzi ambacho sielewi nini hatima yangu hapo baadaye mwanamke niliyempenda kuliko kitu chochote katika maisha yangu. kwasababu unajua kuna kipindi niliwahi kukorofishana na Michael hadi kutaka kukatana visu kwa sababu ya Beatrice.

    Hapo kukamshitua Vanessa akainua uso wake akanitazama na kuniuliza

    "Ilikuwaje?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nitakuhadithia kila kitu kama unataka kujua kila kitu

    SIKU HIYO IlIIKUWA HIV ISiku moja tukiwa chumbani, nilikuwa nikichart na Beatrice baada ya wiki moja tangu ile siku ya kwanza tuliyoonana. Najua unajiuliza ni vipi nilichart naye na siku hiyo hatukupeana namba za simu, lakini ukweli ni kwamba nilimfuatilia Beatrice binafsi kwa kuwa sikutaka kuanzisha ugomvi na Michael. Sikutaka kuanzisha ugomvi kwa kuwa nilimjua anampenda na penzi lake lingeweza kuzua tatizo kama akigundua na mimi ninampenda Beatrice. Katika kumfuatilia, niliingia mpaka chumbani kwao siku iliyofuata mara baada ya siku ile. Alifuarahi sana kuniona nikiwa naranda randa chini ya ghorofa kilipo chumba chao.

    "Romy"

    Aliniita kwa kifupi na wala hakuendelea kuniita Ramon hivyo hilo likawa kama jina langu jipya kwake. Nilipogeuka na kuinua uso wangu kwa juu, nilimuona Beatrice akiwa ana khanga aliyoifungia kuanzia kifuani na bila shaka ikaishia magotini. Nilimpungia mkono na kuvunga kuwa nilikuwa kama simfuatilii yeye ila ukweli wa jambo hilo nilikuwa nao moyoni mwangu. Akaniita.

    "Njoo upaone chumbani kwangu basi"

    Akaniambia akiwa na furaha, hivyo sikutaka kupoteza nafasi hiyo hadhimu nikapanda ngazi na kwenda mpaka kilipo chumba chao. Huko nikakutana na Alicia pamoja na Prisca wakiwa wanasukana. Tukasalimiana huku wao wakiniachia tabasamu zao nzuri. Nilikaa katika kiti ambacho alikikalia Prisca alipokuwa akimsuka Alicia, kisha yeye akakaa kwenye kitanda.

    "Karibu Romy"

    "Ahsante sana Beatrice" Akanitambulisha kwa Alicia kisha kwa Prisca, nikajichekelesha na kusema

    "Nafurahi kuwafahamu sana"

    "Na sisi pia" kisha wakagongana wakaachia kicheko cha haya. Sikupenda kukaa kwa kuwa nilihisi kama walikuwa wakinichora. Nilihisi walikuwa wakinichora kwa kuwa niliona wakiwa na kitu ambacho walikuwa wakinizungumzia kabla ya mimi kuja tena. Ina maana tangu jana bila shaka walikuwa wakinizungumzia kwa muda mrefu na imekuwa kama bahati ya mimi kuja kwao.

    "Oh! Unakunywa nini Romy?"

    "Hapana sinywi chochote nilikuwa napita tu kuelekea kimwaga"

    Nikamuona Alicia akimsuka Beatrice mimi nikajifanya kama sijaona jambo lile, Beatrice akaniambia.

    "Romny upo whatsapp?"

    Nilishituka lakini nikajua janja hiyo, nikaitika kwa kichwa nikimtazama akiachia tabasamu laini la furaha.

    "Niandikie namba yako"

    'Mtoto wa kishua' Simu yake ilitangaza ufahari na hapo nikamtazama Beatrice kwa jicho la tofauti zaidi. Simu aliyokuwa akiitumia kwa kipindi hicho ni Iphone sijuhi Iphone ipi hivyo ikanionesha ufahari wa Beatrice. Nikaandika namba yangu kisha akaniambia jibipu na wewe uipate na yangu, hiyo ndiyo ikawa sababu ya mimi na yeye kuanza kuwasiliana. Wiki moja ilitosha mimi na yeye kuwa na mawasiliano ya karibu kiasi kwamba hakuna ambaye angekataa kuwa tulianza kuwasiliana zaidi ya mwaka mmoja uliopita, lakini haikuwa hivyo. Kisha baada ya kubadilishana namba ya simu hizo, nikaaga kuondoka. Nilichokuwa nikikitamani ndio hicho, nikae kupoteza muda zaidi nini? Prisca na Alicia wakanitania,

    "He ina maana zetu huchukui" Nikahisi aibu sana nikataka nibaki nichukue na zao wao wakajua wamenipata wakaniambia nisijali tu niende walikuwa wakinitania.

    Sasa siku hiyo wakati tukiendelea kuchati mimi nikicheka kwa kila meseji iliyokuwa ikiingia, Nilikuwa nikimsikia Michael akisonya sonya kwa hasira. Mimi sikuzungumza nikaendelea kufurahi kuchati na Beatrice. Mara nikatoka kwenda chooni nikaiacha simu kitandani kwangu huku akiwa amebaki Michael peke yake. Sikujuwa kama alikuwa amesoma meseji zangu, niliporudi nikawa naendelea bila kuwa na shaka yeyote. Katika sehemu ya meseji hizo, tulikuwa tumepanga kukutana maeneo ya Kwa mama wajasiriamali. Kumbe yote Michael alikuwa ameshasoma na alipanga kunifuatilia ahakikishe. Jambo hilo ndio likazua utata wa kutaka kunikata visu.

    Muda ambao tulipanga mimi na Beatrice ulipofika, nilitoka nikiwa nimehakikisha kuwa nimependeza sana sanajari na kunukia manukato yangu safi. Kwa kuwa nilifahamu fika ilikuwa ni sehemu ya gizani basi manukato yangu yangu kuwa silaha tosha ya kuniona "smart" nikatoka wakati ambao Michael naye alikuwa ametoka. Kwa mama wajasiriamali ilikuwa ni mita chache tu kutoka katika hostel zetu.

    "Habari yako Beatrice?"

    "Salama tu Romy nilitegemea ungechelewa sana" alisema Beatrice akiwa amesimama kunikaribisha.

    "Mimi sikutegemeakama ungewahi kuja kabla yangu nashukuru kwa kuwahi"

    Kisha tulikumbatiana, nikakaa pembeni yake akiwa ametandika khanga chini pembeni ya mti fulani. Tukawa tunapiga hadithi mbalimbali na kufahamiana kwa ufupi.

    "Mimi ni mtoto wa pekee katika familia yetu. Baba yangu anaitwa Oscer kama unamfahamu"

    Sikujuwa sababu ya yeye kuniambia kuwa kama namfahamu, nikakataa lakini Beatrice hakupenda makuu ya kuzidi kunifahamisha ni Oscer yupi alikuwa akimzungumzia, japo nilikuwa namfahamu Oscer kabla hajawa naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa.

    "Mimi ni mtoto wa pili lakini kwa sasa nipo peke yangu kwa kuwa kaka yangu alifariki kwa ajali ya gari iliyowahi kutokea chato katika lile gari lilokuwa likienda Rwanda"

    Beatrice akawa amenyamaza na mimi ni kama hadithi zikawa zimeniishia, ukimya wetu uliotupitia tukasikia mchakato wa kitu chenye uhai katika nyasi zilizopo karibu yetu.

    "Nini hicho?"

    Beatrice alitoa macho pima sanjari na pumzi zake kupishana kwa hofu. Mimi nikasimama kutazama kile kilichokuwa kikifanya zile nyasi kutingishika, alikuwako mtu. Mtu huyo alivaa shati nililolifahamu na nilimfahamu mtu huyo fika, nikamtoa hofu Beatrice.

    "Hapana mtu usiogope"

    "Haya" aliongea lakini sauti yake haikuwa na dalili zozote za kuwa kama aliamini nilichozungumza. Mimi na Beatrice tukasimama na kushikana mikono kwa sekunde kadhaa.

    "Nimefurahi sana kukuona Romy"

    "Nimefurahi pia Beatrice"

    Tulikumbatiana tena kisha Beatrice akanitupia busu zito la kuzivamia papi zangu. Tukaondoka moyoni nikiwa nimehakikisha kumkomesha Michael kwa kuwa ndiye aliyekuwa akitutazama kule alipojificha kwenye nyasi.

    "Kwanini unatabasamu"

    Beatrice alifahamu kuwa nilikuwa nikitabasamu lakini si tabasamu la kile alichonifanyia kwakuwa halikuwa tabasamu halisi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Una lips za moto" nikamdanganya yeye akacheka, tukaondoka. Nilipofika hostel nikiwa ndio kwanza nimekaa natafakari kuhusu tukio la Michael kuja kututazama kule tulipo mimi na Beatrice, Michael aliingia. Alikuwa akihema kwa fujo macho yamemtoka pima.

    "Ramon, Ramon" Akawa ananiita kwa hasira. "Wewe sio wa kunifanyia mambo ya(akatukana tusi zito la kunidhalilisha)nasema huwezi kunifanyia hivi" Akapanda kitandani kwangu na kuanza kuniangushia makonde. Mimi niliziba uso wangu kwa kuwa sikutaka kupigana na Michael. Michael aliendelea kunipiga mpaka tukaanguka kutoka juu ya doubledeker mpaka chini mkono wangu ukateguka lakini aliendelea kunipiga. Mezani kukawa na kisu kidogo kilichotumika kukatia embe, nikiwa nimesimama huku michael naye amesimama akihema kwa nguvu mimi nikiugulia maumivu, akawa anapanga kunichoma na kisu kile. Nilishuhudia hilo na niligundua kwa kuwa machale yalinicheza mapema, nikamkwepa kisha nikakimbilia nje ya chumba chetu. Michael hakuwa mtu kabisa, michael alikuwa tayari kuuwa kwa ajili ya Beatrice. Michael alimpenda sana Beatrice.

    Mara mpaka hapo, Vanessa akanikatisha "Dah kuna mambo mazito sana katika kesi yako, nilipopewa kuhusu habari za kifo cha mtoto wa mteja wangu nilidhani ingekuwa ni kazi nyepesi lakini kuna mazito"

    Hofu ikanivaa kwa kuwa sikufahamu kwanini aseme hivyo, kwanini aanze kuingia na uoga wa kuifuatilia kesi yangu? Sikuwa na nafasi hata ya kumuuliza hayo yote kwa kuwa muda ulikuwa umekwisha kwa wakati ule.

    "Acha niende Ramon, lakini kuna umuhimu wa mimi na wewe kukutana kila siku kwa ajili ya uzito wa kesi yako. Kuna jambo moja nimelipata kutoka katika maelezo yako lakini inabidi nisikie zaidi huenda fikra zangu zikanidanganya kutokana na kusikia upande mmoja wa shilingi" Akaniaga na kuondoka zake. Siku hiyo nilibaki mwenye mawazo sana. Nikasema yawezekana nilichowaza ni sahihi ndio maana hata Vanessa alisema vile. Sikuwa nimekosea kuelezea kila kitu kweli nilichofahamu kuhusu Michael.



     Hisia zangu zikanifanya kumshinikiza Vanessa aamini kama nilichoamini mimi ili Vanessa apate muda wa kumchunguza Michael na kugundua kila kitu. Nilipotazama saa sikujua kama ilikuwa imeshafika saa 10:48 jioni, yule askari wa kike akaniletea chakula ugali na maharage kwa samaki wa kukaanga na mchuzi wa maharage. Nilipokula nikashiba, nikalala mpaka majira ya saa 2 usiku. Niliamshwa na kirungu cha askari aliyekuwa akiniita kwa kebehi. "We jambazi" Nilipoinuka na kumtazama alikuwa ni yule askari ambaye alinikamata nyumbani kwa Beatrice. Akaniambia "Una mgeni" Nilitoka nikiwa najiuliza ni vipi mgeni aruhusiwe kuniona kwa wakati huo ambao sidhani kama ilikuwa ni sahihi. Nikatoka na kwenda kumuona. Sebuleni pale alikuwako mtu ninayemfahamu. Mtu huyo ni mtu mzito sana. Mtu huyo nilimzoea kumuona katika mikutano mingi mikubwa ya kitaifa mtu huyo hakuwa mwingine bali ni baba yake Beatrice, mzee Oscer.Kwa kueleza tu kiufupi unaweza ukahisi ni kiasi gani nilikuwa na hofu juu ya kutazamana ana kwa ana na Oscer. Sikumbuki fika kama niliweza kumsalimia au kuzungumza chochote mara nilipokutana naye macho kwa macho tena mara baada ya sherehe ya juzi usiku wa kifo cha Beatrice. Zilipita dakika mbili kwa kadirio chini mpaka alipoanza kuzungumza tena nami.

    "Umeshindwa kunisalimia?" Kwa sauti ya kigugumizi bila kuelewa fika kile nilichokuwa nikikizungumza, nikamsalimu "shikamoo mzee!" "Nashindwa kuelewa kitu gani kimekupata kijana. Kwanini umeukatisha uhai wa binti yangu mpendwa siku niliyokukabidhi mbele ya wazazi wako. Ni hivi walivyokufundisha ama nini alikukosea Beatrice, mwanangu? Kwanini umeamua kumuhukumu hata kama lipo alilokukosea?" Nikayaona machozi yakilowesha mashavu yake huku akivuta kamasi jepesi na kunitia simanzi hata mimi. "Sina sababu ya kukueleza ni nini nitafanya mara baada ya kuthibitika wewe unahusika na mauaji ya binti yangu lakini naomba ujieleze vizuri ili yule mwanasheria akuelewe usije ukaenda nje na ukweli utakaokutia kitanzini. Nimempangia adhabu nzuri yeyote aliyehusika na mauaji ya binti yangu" Akanyanyuka mara baada ya kumaliza aliloongea na mimi nikanyanyuka na kumtazama alipotaka kuongea na maneno aliyotaka kuzungumza kuishia mdomoni kwake. Mimi nikazungumza mara aliponipa mgongo na kutaka kuondoka. "Mheshimiwa, ukweli ni kwamba mimi sihusiki na mauaji ya Beatrice kwa kuwa pia ninampenda na nilimpenda sana Beatrice kuliko kitu chochote. Nitajitahidi kueleza kila kitu kinachohusu kazia hii lakini iwapo itathibitika n'nastahili adhabu hii sina sababu ya kukubali nipatiwe adhabu yeyote ili moyo wangu uende na yule nimpendaye" Sauti yangu ikakumbwa na kitetemeshi cha kuzungumza kwa hasira iliyokaba koo yangu na kutengeneza donge fulani la hasira. Oscer hakugeuka kunitazama lakini alinijibu huku akianza kupiga hatua za kuondoka. "Auwaye kwa upanga... " Hakumalizia kile alichotaka kuongea akawa ameshafunguliwa mlango na kutoka nje. Mimi nikajibu kwa sauti ambayo haikusikika na mtu "Atakufa kwa upanga. Atakufa kwa upanga au nitakufa kwa upanga!!" Kisha nikarudi katika mahabusu yangu baada ya kuletewa chakula kule kule na askari yule yule wa kike.

    "Nadhani juisi ya rozela niliyotengeneza utaipenda" Kisha akaondoka. Nilikila niliposhiba nikaenda kuoga kwa ajili ya kwenda kulala. Siku iliyofuata asubuhi na mapema mara baada ya kunywa chai, nilielezwa leo siku ya nne ni siku maalumu ya kukutana na wazazi wangu. Nilifarijika sana kwa kuwa nilitamani sana kukutana nao nisikie wao pia wanamaono gani juu ya kesi yangu na vipi wameichukulia kesi hii iliyonikuta mtoto wao. Alipokuja yule askari wa kike akanieleza kuwa hawakuja wazazi wangu wote wawili bali mama yangu peke yake. Ilinishangaza kwa kuwa sikutegemea kama baba angeweza kukaa nyumbani ikiwa mimi nina kesi nzito inayonikabili ya mauaji. Sikuwa na la kufanya nikatoka katika mahabusu ile nikaelekea kule alipo mama. Askari yule wa kike akaninong'oneza jambo

    "Mama yako anaonekana kijana! Anayajua mambo mengi ya mjini" Nikampuuza kwa kuwa aliongea kwa kunikejeli na kama ningejua maana ya maneno yake tangu mwanzo leo nisingeweza kuandika haya ninayoandika saa chache kabla ya kifo changu. Saa chache kabla sijaamua uamuzi mgumu wa kuitoa roho yangu na kumkabidhi Beatrice moyo aende nao kule popote aendako yeye.

    Nikafika pale alipo mama yangu tukasalimiana na alionesha kuwa na furaha sana kuniona. Mama alinitazama baada ya mimi na yeye kukaa kwenye kochi, kisha akazitazama kwa kuzigusa gusa nguo nilizovaa akatoa tabasamu fulani dhaifu. "Habari yako mwanangu?" Akanisalimu kwa sauti ya upole "Salama mama, shikamoo!"

    "Marahaba" kisha akawa kama anataka kuongea tena, akaendelea "Imekuaje ukafikwa na jambo kama hili mwanangu?"

    "Mama ina maana na wewe unaamini kuwa nimeua?" Nilimuuliza "Hapana sitaki kukuuliza kama umeuwa au hujauwa kwa sababu sitaki kuamini kama unaweza kumuuwa Beatrice na siwezi kuamini kamwe lakini ilikuwaje wewe ukakamatwa kama muuwaji wa Beatrice na baba yake akithibitisha kuwa umekamatwa na vithibitisho vyote kuwa wewe ndiye muuwaji! Hicho ndicho n'nachotaka kufahamu ilikuwaje ukakamatwa kwa kesi hii?" Nikashusha pumzi kwanza kwa kushukuru kuwa mama yupo upande wangu na anaamini kuwa mimi siwezi kumuuwa Beatrice pili nilihisi kuwa nina mzigo mpya wa kumuelezea upya juu ya kila kilichotokea lakini sikuwa na sababu ya kuacha kumuhadithi kwa ufupi kila kilichotokea bila ya kuacha la maana hata moja. Nikamueleza kwa ufupi tangu nilipopata ujumbe mfupi kutoka kwa beatrice kuwa ninamuuwa kisha nikaja kuupata asubuhi ya siku ya pili nikiwa n'na hangover ya pombe nyingi kichwani mwangu kisha nikachukua uamuzi wa kwenda nyumbani kwa Beatrice huko ndipo nilipokutana na madhira haya yaliyonifanya niwe mbali na kitanda changu, nyumbani kwangu kule mtoni kijichi. Hadithi hiyo haikuonesha kumshitua sana mama yangu, akaropoka jambo ambalo sikulielewa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Yule mtoto mshenzi sana" kisha akanitazama kwa chati kana kwamba alikuwa akisubiri nimuulize swali, akaendelea kuongea "Ngoja kwanza nikuulize, hivi Michael ameshakuja kukuona?"

    "Ndiyo mama alikuja juzi lakini yeye alinishitumu kuwa mimi nimemuuwa na sikutegemea kabisa kama rafiki yangu wa siku nyingi kiasi hiki asinijue hata kuniamini kuwa mimi ni muuwaji, mimi ninaweza kuwa muuwaji kweli?" Nikaanza kulia mbele ya mama.

    "Usilie mwanangu, wewe ni mtoto wa kiume. Inabidi ujikaze na upambane kutafuta haki yako, yule Michael ni mtoto mshenzi sana na usije kumuamini kabisa ndio maana siku zote nilikuwa nikikueleza kuwa Michael asimzoee kabisa mpenzio sasa nadhani utakuwa umenielewa"

    Wakati mama akizungumza hayo yule askari wa kike alikuwa ametujia na kumtoa pembeni mama na kumueleza mama jambo, sikuweza kujua nini alizungumza naye. Nikakaa kitambo kidogo nikimtazama mama na askari yule walivyokuwa wakizungumza huku wakinitazama kwa kuniibia kama vile walikuwa wakinizungumzia mimi. Mimi pia sikuelewa maana ya mama kumsema Michael ni motto mshenzi na vipi ilihusiana na kesi yangu juu yay eye kunikataza Michael kuwa na mahusiano ya karibu na Beatrice.



    ...

    Mama aliporudi pale nilipo mara baada ya kumaliza kuzungumza na yule polisi wa kike, aliniaga kuwa anaondoka. Alionesha kuwa mwenye haraka na kusahau kabisa kuna kitu ambacho aliniambia kabla hajaenda kwa yule askari wa kike.

    "Mama" nikamuita kisha akageuka aliponipa mgongo na kutaka kuondoka "kuna jambo la kushangaza umenieleza naomba uniambie ukweli"

    Mama akageuka na kukaa tena kochini kisha na mimi nikakaa baada ya yule askari wa kike kuondoka akiwa ametuacha wawili mimi na mama.

    "Kitu gani hicho? Muda wa kukuona umeisha"

    "Kuhusu Michael" nikamtazama kwa makini mama kupitia machoni kwake "umejuaje kuhusu mauaji ya Beatrice naina maana unataka kusema kuwa Michael ndiye muhusika?"

    Nilimuona mama akiyatoa macho pima na akaunda tabasamu la uongo. Ndiyo tabasamu la uongo, tabasamu ambalo halikuwa na ladha yeyote ya raha niliona hivyo. Akanieleza "Mwanangu, zile ni hisia tu naomba uachane nazo hazina maana yeyote katika kesi hii ila ukweli ni kwamba nishakukataza mara nyingi kuhusu urafiki wako na Michael tuongeze maombi tu ili hii kesi ipate ufumbuzi lakini ni mbaya sana na imekukalia vibaya " akasimama kisha akaniambia "acha niende namuwahi baba yako, huenda akaja wiki ijayo"

    Sikuwa na sababu ya kumng'ang'ania mama anieleze chochote kwa kuwa mama alipoamua kufanya jambo lake, basi hakuna ambaye angeweza kumbadili mawazo yake, mama akaondoka.

    ....



    Zilipita siku kadhaa nikiwa mahabusu. Nikiwaza kila aina ya jambo linalonipitia kwa umakini zaidi. Nilitumia muda mwingi kuwaza mengi kipindi ambacho Vanessa aliukata mguu kuja kuzungumza nami. Ni hapo nilipofuatwa na yule askari wa kike na kunieleza jambo la kushangaza

    "Ramon wewe ni kijana mdogo sana uliyeingia katika matatizo ambayo si yako lakini anayepigana vita hii anajuta sasa kukuingiza wewe katika matatizo ya namna hii" kisha akanitazama kwa tuo kana kwamba alisubiri nimuulize jambo, akaniuliza yeye "je! Ukimfahamu utamsamehe?"

    "Siwezi kumsamehe abadani, amemuuwa mwanamke ninayempenda amenifanya nikose imani kwa watu wangu wote wa karibu siwezi kumsamehe zaidi ya mimi kumuua na yeye ili astahili linalomfaa"

    Nikamjibu kwa hasira kutokana na hali ambayo imenikuta na inayoendelea kunitafuna kutokana na kutokujua ukweli ambao umeniweka katika giza hili zito la kutofahamu kinachoendelea.

    Askari yule akabetua mabega yake kwa kebehi mimi nikaendelea na ratiba yangu ya siku hiyo.

    Siku hiyo nikiwa nimejipumzisha katika chumba changu baada ya chakula cha jioni, alikuja Vanessa. Niliingizwa katika chumba kile kile cha kila siku nikiwa najihisi huru zaidi. Tukasalimiana na Vanessa kisha akanitaka radhi kutoonana takribani siku nne.

    "Kulitokea nini hata usije?" Nikamuuliza

    "Nilikuwa katika uchunguzi wa awali juu ya ripoti ya kifo cha beatrice. Kwanza nikuulize, Beatrice alikuwa akinywa pombe?" Akanitazama akisubiri jibu langu. "Hapana si mnywaji kabisa"

    "Lakini siku ile alikunywa kutokana na furaha ya siku yenyewe? Na alikunywa akiwa na wewe au nani mwingine?"

    "Unajua Vanessa, nashindwa kuwa na jibu kamili juu ya swala hilo kwa kuwa hiyo habari ya kukutwa na pombe ndani ya mwili wake Beatrice na kuwa kama chanzo cha awali ya kifo chake nilisoma katika gazeti. Lakini ukweli wenyewe ni kwamba siku hiyo baada ya kutoka katika sherehe mimi na Beatrice nikamsindikiza mpaka pale kwao. Nilishuka katika gari nikamfungulia mlango na tukasimama pale getini kwao kama dakika ishirini au zisizopungua hizo. Kisha nikamuaga baada ya kuongea naye mengi juu ya mapenzi yetu. Hakuwa amekunywa pombe wala nini na nilihakikisha anaingia ndani ingawa ni mimi nilikuwa nimelewa siku hiyo"

    Vanessa akashusha pumzi ndefu kisha akatoa kalabrasha lenye karatasi kadhaa akalitupa mbele yake akafunua funua pale huku akijaribu kuzisoma karatasi kadha wa kadha akagota katika moja wapo. Akauinua uso wake na kunitazama, kisha akaanza kuongea

    "Ndani ya damu yake, kumekutwa pombe hiyo yenye sumu ya nyoka kwenye kilevi hicho iliyompelekea kumuozesha maini yake ghafla na kusimamisha mapigo ya moyo yaliyopelekea Beatrice kupoteza fahamu na kufa taratibu kabla hawajatenda unyama walioutenda wa kumtoboa tumbo kisu kile kikubwa kilichokutwa eneo la tukio huku alama ya vidole ikionekana ni ya mwanaume kisha wakamkata sehemu ya shingoni" kisha akanitazama kwa hali ya huzuni akaniambia "Beatrice ameuwawa kinyama sana, kwa yeyote aliyeyafanya yale, hastahili kuishi"

    Akaniangalia nilivyokuwa nikisisimuka kutokana na taarifa zile ikawa zamu yangu kuvuta pumzi nyingi kisha nikazitoa kama zilivyo, nilihamanika. "Sijuhi walimkosea nini mpenzi wangu" Nilisema kwa huzuni nikitazama karatasi ile mbele ya Venessa ambayo bila shaka ndiyo iliandikwa ripoti aliyonisomea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Alama ya vidole katika nyumba na maeneo yote ya mauaji ni za mkono wa kiume kutokana na vina saba vilivyotoa ripoti yake ya awali" Vanessa akanitazama kisha akaniambia "kuna kila sababu ya kesi hii kuendelea kuwa ngumu kwako kwa kuwa unayehusishwa na mauaji haya wewe ni mwanaume"

    Hofu ikazidi kunipanda tumaini likapotea. Nikamuuliza Vanessa kwa unyonge “Na wamejuaje kama alama za vidole vile ni vya mwanaume?”

    “Ramon, hayo ni mambo ya kisayansi na ni ngumu kujibu kiurahisi lakini inawezekana kupimwa alama na kugundulika ni mkono wa mtu gani”

    Vanessa akanieleza huku akifunga kalabrasha lile lenye karatasi ya ripoti "Sasa tuachane na hayo tuendelee na maelezo yako. Kuhusu maisha yako chuoni mahusiano yako na Beatrice pamoja na Michael"



    Nikavuta pumzi kwa kile tulichotoka kuzungumza punde. Kiukweli mawazo ya kesi hii, yaliniumiza nafsi na kunifanya ninyong'onyee kila dakika jinsi majibu kadhaa yanayokuja juu ya upelelezi wa mauaji ya Beatrice. Nikatazama juu nikijaribu kukumbuka kila kilichotokea hapo zamani. "Kiukweli uhusiano wangu mimi na Michael ulipungua kama si kupotea kabisa. Alikuwa akinifanyia visa sana pale chumbani mpaka nikapaona pachungu"





    Vanessa akiwa anaitazama tepurekoda aliyoiwasha wakati naanza kuzungumza akanikatisha kwa swali "Visa gani alikuwa akikufanyia"

    "Kuna wakati nilikuwa nikikuta godoro langu lina maji, wakati mwingine nguo zangu nilizoziandaa kabisa nataka kuzivaa nazikuta kwenye beseni la kufulia, ni mengi ambayo si rahisi kuelezeka na kuisha ila ikafikia hatua mimi kuhama baada ya kukubaliana na Steven kuhama kuelekea kule jirani na ghorofa alilokuwa akiishi Beatrice. Maisha yangu mimi na Beatrice ndiyo yakazidi kuwa matamu haswa tulipokuwa na hakika ya kila siku kuonana na kila dakika tunayotamani kukutana hiyo ikazidi kumuumiza Michael"

    Vanessa akanihoji “Na je Beatrice alikuwa akifahamu ugomvi wenu?”

    “Ndiyo kwa kuwa ilikuwa ni ngumu kwa Michael kuficha chuki zake kwangu”

    Nikiwa nataka kuendelea kumuelezea mengine Vanessa, kwa kuwa hatukuendelea na uhasama ule mpaka tunamaliza chuo, nilimuona akitazama saa yake mkononi ilipobidi ninyamaze yeye akauinua uso wake kunitazama

    "Sasa muda umekwenda lakini jambo hili nitalifanya kesho. Unayo ramani ya nyumbani kwa Michael" Sikuwa nimemuelewa nikamjibu "Mimi sijuhi kuchora ramani za nyumba ya uswahilini kiasi kile" Vanessa akacheka na kujisahihisha pale alipohisi amekosea mpaka akanikanganya mimi. "Nina maana unapafahamu anapoishi Michael" Nikakenua meno nikitabasamu mara baada ya kumuelewa vizuri, nikamuelekeza.

    "He msewe? Kwani alikuja kusoma chuo cha Ud(University of Dar es salaam)?"

    aliniuliza kwa kuchanganyikiwa. "Hapana hakuwa na pesa na hapo nilimlipia mimi pesa ya pango kwa kuwa chumba hicho kilikuwa chumba cha rafiki yangu Nambode Issack Njinjo, yeye alipokuwa akihama alinieleza na mimi nikamchukulia Michael"

    "Ina maana Michael hakuwa na wazazi? Na ilikuwaje wewe umlipie wakati mlikuwa mna ugomvi?"



    Nilipotaka kumjibu, akanizuia. Akanyanyuka na kuanza kupiga hatua za kuondoka mara aliponiaga.

    "Kesho sitakuja ila nitakuja baada ya kesho kukueleza wapi nilipofikia na nitakusikiliza zaidi maana una zaidi ya kunieleza"

    Nilikaa siku hiyo bila kuwa na mawazo yoyote. Nahisi nilikwishazoea maisha ya humu ndani. Kwanza sikuona utofauti wa maisha haya na maisha wanayoishi watoto wanaoishi maisha ya kifahari ambayo hakuna uhuru lakini kila nilichokitaka nilikipata. Nikaenda kwenye meza iliyojaa vitabu huku nikitazama wingi wa askari walioletwa kunilinda. Wengi wao wakiwa wamebeba silaha nzito za moto.



    "Psiii"

    Nikamuita mmoja wapo aliyesimama mita chache namimi nilipokuwa nimekaa mimi.

    "Una fegi?" Hakuzungumza bali alitoa kasha la sigara aina ya embassy na kunipatia kiberiti cha gesi nikaiwasha kisha nikaanza kuuvuta moshi wake. Mimi sikuwahi kupenda kuvuta sigara lakini si kwamba sikuwahi kuivuta katika maisha yangu. Niliwahi kuvuta katika wakati ambao nilikuwa nimelewa ama nikiwa katikati ya marafiki zangu ambao sikupenda wanione kama mtoto wa mama sana.

    "Naomba kukuuliza jambo" hilo ndio likawa lengo langu la kuomba sigara "kwanini mnanilinda wengi tofauti na idadi ya askari wa mwanzo?"

    Yule askari akanitazama na wala hakuwa na dalili yeyote ya utu wema. Alionesha sura ya ukatili na mbaya kuliko nilizowahi kukutana nazo kisha akanijibu kwa mkato na sauti iliyojaa hasira

    "Wewe ufahamu fika kuwa wewe ni mtu hatari? Unataka kutoroka?"

    Nikajichekesha na wala sikujibu chochote. Nikaigeukia meza ile kisha nikakitwaa kitabu kimojawapo mezani pale hicho kiliitwa SIRI kitabu hiki sikuwahi kukutana nacho mtaani lakini kilinishangaza uhodari wa Vanessa jinsi alivyoweza kupambana na nguvu za giza katika kuwaumbua wauaji waliosababisha uchonganishi kati ya Khatib na Ubwa katamba.

    "Hapana inawezekana Vanessa ninayemsoma humu si huyu ninayekutana naye"

    "Ndiye" ile sauti ya askari wa kike ikanijibu nikageuka kumtazama. Alikuwa ameshika mkonga wa simu na kunipatia "Baba yako mzee Lameck yupo hewani"

    Niliipokea simu ile haraka haraka na kuiweka sikioni kwangu.

    "Halow, halow baba!" Nikaisikia sauti ya baba katika hali ya utulivu ikiniuliza naendeleaje "Naendelea vizuri baba mbona hujaja kuniona?"

    "Nitakuja mwanangu ila siendelei vizuri kiafya. Mama yako ameshakuja kukuona? Kuna chochote amekueleza kuhusu kesi yako?"

    "Hapana baba hajanieleza chochote kuna nini kwani? Maana nahisi kuna kitu anafahamu"

    "Usimwamini..."

    Simu ikawa imekatika na kuniacha njia panda. Niliita, baba baba kuhakikisha kama simu ilikuwa hewani, nilikuwa naongea na chombo kitupu.

    Nikiwa naitazama ile simu iliyokatikia sikioni mwangu kana kwamba ilikuwa na uwezo wa kuzungumza nikashikwa na bumbuwazi hata nisizungumze chochote kwa nusu dakika. Yule askari wa kike akanishika bega na kuniambia

    "Huna sababu ya kushangaa kwa kuwa ni mengi utasikia na mengi utaelezwa cha msingi ni kuvumilia kama mwanaume na kujua kuwa hayo ni majukumu yako na inabidi ujitetee kuondoa kitanzi ulichoandaliwa kwa ajili ya hukumu ya kunyongwa"

    Akanipokonya ile simu na alianza kupiga hatua za kuondoka. Nikamuuliza swali akasimama

    "Kitanzi? Ina maana hukumu yangu ni hiyo?"

    "Unadhani hukumu ipi inakufaa muuwaji wa mtoto wa kigogo?"Nikamuacha aende kwa kuwa nilihisi anazidi kunichanganya. Kasha nilijiuliza mengi ni vipi huyu askari ambaye aliondoka mara baada ya kunikabidhi simu na arudi akiwa anajua nini nimeambiwa? Japo hakunieleza kuwa amesikia lakini kwa jinsi alivyoongea nilielewa kuwa alifahamu kitu ambacho baba alinieleza na vipi aje mara baada ya simu kukatika? Nililala juu ya mikono yangu niliyoilaza juu ya meza nikaingia katika tafakuri fupi.



    'Mama anamjua muuwaji na anamuhisi ni Michael, mimi na Vanessa tumekuwa tukimuhisi Michael pia lakini baba anasema nisimuamini mama kama ameniambia kuwa anamfahamu muuwaji! Haya yote yanatoka wapi? Kwanini inakuwa hivi?'

    "Ahaaa"

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikapiga kelele mpaka wale waliokuwa wakinilinda wakashituka. Walikuja mbio kwa kuwa walikuwa hawakai ndani mara kwa mara, nyakati za usiku. Nyakati hizi huwa wanaongeza nguvu ya ulinzi huko nje. Niiwasikia wakizungumza

    "Ana nini huyo mwehu?"

    Nilipogeuka nikamkuta yule askari wa kike akicheka kisha akawajibu kwa kebehi huku akinitazama "Na amekuwa mwehu kweli, kwa kuwa ameanza kuongea mwenyewe" Sikujua kabisa kama yule askari alikuwa nyuma ya mgongo wangu sikujua kama nilikuwa nawaza kwa kuzungumza sikujua jamani! Sikujua mimi ah!! Nini sasa kilichokuwa kinataka kunitokea? Jasho jingi lilikuwa likinitoka na wala sikutambua nini kilikuwa kinaendelea katika kichwa changu. Ilikuwa ni hali mbaya kuliko kuumwa hata malaria.







    ITAENDELEA  

0 comments:

Post a Comment

Blog