Search This Blog

Friday, October 28, 2022

HOLLY SIN (DHAMBI TAKATIFU) - 2

 

     





    Simulizi : The Holy Sin (Dhambi Takatifu)

    Sehemu Ya Pili (2)





    Aliendelea kumsubiri kwa hamu Caro arudi kwani hakuna siku aliyokuwa anaisubiri kwa hamu kama siku hiyo. Licha ya kusubiri sana, Caro hakutokea, hali iliyoanza kumpa wasiwasi Aidan. Kwa kuwa nyumbani kwao hakukuwa mbali na hapo, aliinuka na kuchuma waridi jekundu bustanini hapo na kulificha ndani ya shati lake.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaanza kutembea taratibu kuelekea nyumbani kwa akina Caro. Kwa kuwa urafiki wao ulipitiliza mipaka na kuwa kama ndugu, aliingia kwa uhuru mpaka ndani kwa akina Caro, akakutana na mama yake aliyekuwa akichagua mchele sebuleni.

    “Mwenzio yupo chumbani kwake amepumzika, anasema anajisikia vibaya,” alisema mama yake Caro huku akiinuka na kwenda kumuamsha Caro chumbani kwake, alipoamka, aliwapisha sebuleni na kuelekea jikoni kuendelea kuandaa chakula cha jioni.

    “Caro, upo sawa kweli?” Aidan aliuliza kwa sauti ya upole huku akimsogelea pale alipokuwa amekaa, akatoa ua alilomchumia bustanini na kumsogezea puani ili anuse harufu yake nzuri, Caro akaachia tabasamu hafifu na kulipokea ua hilo.

    “Ahsante kwa kunijali Aidan, najisikia vibaya mwenzio, sijui nimepatwa na nini kwani hali hii imenitokea ghafla,” Caro alisema huku akiinuka na kwenda kulificha ua alilopewa na Aidan chumbani kwake kwani hakutaka wazazi wake walione akihofia kugundulika kwa uhusiano wao wa kimapenzi ambao ndiyo kwanza walikuwa wanataka kuuanzisha.

    “Niambie kinachokusumbua Caro, nakuona kabisa haupo sawa au nimekukwaza kwa nilichokwambia? Naomba unisamehe kwani hizo ni hisia za moyo wangu tu,” alisema Aidan kwa upole lakini Caro akatingisha kichwa kuashiria kwamba hakuwa amekwazika na alichomweleza wala alichokisoma kwenye ‘diary’ yake bali alikuwa akijisikia vibaya tu.

    Akamuomba Aidan amuache apumzike kwa maelezo kwamba anahisi maumivu makali ya kichwa, wakakubaliana kuonana siku inayofuatia. Kwa shingo upande, Aidan akaaga na kuondoka huku akiendelea kuwa na mawazo tele ndani ya kichwa chake. Tangu alipofahamiana na Caro, wakiwa wadogo kabisa, hakuwahi hata mara moja kumwambia kitu kama hicho kwamba amuache apumzike.

    “Au kwa sababu amejua nampenda? Au hanipendi ndiyo maana ananionyeshea haya yote,” Aidan aliendelea kuwaza wakati akitembea taratibu kurudi nyumbani kwao, kichwa akiwa amekiinamisha, mawazo mengi yakiendelea kukisumbua kichwa chake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipofika nyumbani kwao, alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwake, kabla hajafungua mlango, alisikia baba yake akimuita. Ikabidi arudi sebuleni kumsikiliza.

    “Unaonekana haupo sawa, nini tatizo?”

    “Aaah! Hamna kitu baba,” Aidan alijaribu kuficha hisia zilizokuwa zinautesa moyo wake, baba yake akamkazia macho usoni.

    “Nahisi umeanza kujihusisha na mambo ya mapenzi katika umri mdogo. Nakusihi kwa upole kama ni kweli, bora uache kabisa kwani tumepoteza fedha nyingi kukusomesha, tunategemea utalipa fadhila kwa kuelekeza nguvu zako kwenye masomo na si vinginevyo, nadhani umenielewa,” alisema baba yake Aidan, mzee Kenan kwa msisitizo huku akionyesha kutokuwa na hata chembe ya masihara. Aidan hakujibu kitu zaidi ya kujiinamia, baba yake alipomaliza kumsomea risala yake aliondoka taratibu na kwenda kujifungia chumbani kwake.

    “Amejuaje kwamba mimi nimeanzisha uhusiano wa kimapenzi na Caro? Au ndiyo sababu Caro amechanganyikiwa?” alijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu. Ni kweli alichokisema baba yake kilikuwa na maana kubwa kwake lakini moyo wake ulikuwa unazungumza lugha nyingine kabisa.

    Hakuwa tayari kulipoteza penzi hilo ambalo sasa alikuwa na uhakika nalo, hasa baada ya Caro kufahamu hisia zilizokuwa ndani ya moyo wake. Jioni hiyo ilikuwa ngumu sana kwake, aliwaza mpaka akapoteza hamu ya kula, akalala na njaa.

    Kwa upande wa Caro, naye alikosa raha kabisa kutokana na mambo yaliyotokea siku hiyo. Awali alikuwa na furaha kubwa ndani ya moyo wake baada ya kugundua kuwa kumbe Aidan alikuwa akimpenda. Alifurahi kwa sababu alikuwa akimjua vizuri na zaidi alivutiwa na tabia zake nzuri alizozionyesha tangu alipokuwa mdogo.

    Furaha yake ikazidi kwa kuwa walikuwa wakifahamiana mno, kuanzia wao wenyewe mpaka familia zao. Hata hivyo, furaha hiyo ilidumu kwa muda mfupi, kumbukumbu za vitendo vya kidhalilishaji alivyovifanya baba yake Aidan, mzee Kenan ikiwemo kumgusa kifuani na kumkokota mpaka chumbani huku akionyesha waziwazi jinsi alivyokuwa na uchu wa mapenzi, zilimkosesha kabisa raha msichana huyo mdogo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila alipotafakari cha kufanya, alikosa majibu, akaendelea kuteseka kwa mawazo mpaka usiku sana. Kama ilivyokuwa kwa Aidan, na yeye hakula chakula cha usiku siku hiyo, akisingizia kuwa anaumwa.

    Kesho yake kulipopambazuka, alikuja na wazo jipya, akaona njia pekee ya kuondokana na matatizo hayo, ni kusafiri na kwenda kijijini kwa babu na bibi yake ambako alipanga kwenda kumalizia likizo yake.

    Wazazi wake walishangazwa na safari hiyo ya ghafla aliyoipanga binti yao lakini kutokana na mapenzi ya dhati waliyokuwa nayo kwake, walikubaliana naye. Hakutaka kumuaga Aidan kwani alijua hawezi kukubali kirahisi aende mbali naye, akajiandaa kimyakimya mpaka alipokuwa tayari.

    Wakati wazazi wake wakiwa wanajiandaa kumsindikiza Ubungo ambako angepanda basi la kumpeleka kwa bibi na babu yake, mzee Kenan alisimamisha gari lake nje ya nyumba yao na kuteremka kwenda kuwasabahi kama ilivyokuwa kawaida yao.



    Walipomueleza kuwa wanamsindikiza Caro Ubungo anayetaka kusafiri, mzee Kenan aliwaambia imekuwa bahati nzuri kwani na yeye anaelekea Ubungo hivyo badala ya kuchoma mafuta kwenye gari lao, ni bora yeye ndiyo ampeleke.



    Awali Caro alitaka kukataa lakini akahofia kuonyesha picha mbaya kwa wazazi wake, kwa shingo upande akakubali kuongozana na mzee Kenan. Akaagana na wazazi wake kisha akapanda kwenye gari na kukaa pembeni ya mzee huyo, safari ya kuelekea Ubungo ikaanza huku kila mmoja akiwa kimya.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    WAKATI safari ikiendelea, licha ya kuwa bize kubadili gia na kunyoosha usukani, baba yake Aidan alikuwa akitumia muda mwingi kumtazama Caro usoni kiasi cha kumfanya msichana huyo mdogo kuanza kuona aibu za kikekike. Macho yao yalipogongana, Mzee Kenan hakusema chochote zaidi ya kuachia tabasamu lililokuwa na ujumbe ndani yake.

    “Mungu wangu, hata sijui itakuwaje,” aliwaza Caro huku akijifanya kutazama nje kupitia kioo cha pembeni. Muda mwingine, mzee huyo alikuwa akibadili gia kwa nguvu na kusababisha mkono wake uguse mapaja ya msichana huyo ambaye kiumri alikuwa sawa na mwanaye wa kumzaa.

    “Tutasimama kidogo kwenye lile duka pale kuna zawadi nataka nikakununulie kabla hujaondoka,” alisema mzee huyo huku uso wake ukiwa umejawa na tabasamu. Caro alitingisha kichwa kuashiria kukubaliana na alichoambiwa na mzee huyo aliyekuwa anamheshimu kama baba yake na mtu wa karibu wa familia yao.

    Mzee huyo alipunguza mwendo na kuwasha ‘indiketa’ upande wa kushoto, akatoka nje ya barabara ya lami na kusimama mbele ya duka moja kubwa lililokuwa linasifika kwa kuuza nguo za kisasa.

    “Nisubiri nakuja sasa hivi,” alisema mzee Kenan wakati akishuka kwenye gari, harakaharaka akaingia ndani ya duka hilo. Baada ya dakika kadhaa, alitoka akiwa na mfuko mdogo uliokuwa na vitu ndani yake. Akaingia kwenye gari na kumpa Caro.

    “Utaenda kufungua ukiwa peke yako, hizi ni zawadi zangu kwako, napenda siku moja nikuone ukiwa umependeza,” alisema mzee Kenan. Bila hata kujua kilichokuwa ndani ya mfuko huo, Caro akapokea na kushukuru kwa adabu, akauchanganya kwenye mizigo yake aliyokuwa anasafiri nayo.

    “Samahani, kabla sijakufikisha Ubungo naomba tupitie kwenye Hoteli ya The Paradise kuna rafiki yangu namdai fedha zangu kaniambia nimpitie anipe, unaweza kupata na wewe kidogo za kukusaidia ukiwa safarini,” alisema mzee Kenan.

    “Hatutachelewa kweli baba? Maana muda wa basi kuondoka umekaribia.”

    “Wala usiwe na wasiwasi, wala hatuchelewi,” alisema mzee huyo, Caro akakubaliana naye lakini tayari kengele ya hatari ikianza kulia ndani ya kichwa chake. Mfululizo wa matukio yaliyokuwa yanatokea kati yake na mzee huyo, ulimtia shaka juu ya usalama wake. Hata hivyo alipiga moyo konde na kuendelea kutulia aone mwisho wake.

    Ukimya ukapita kati yao, walipokaribia Ubungo, mzee huyo kama alivyosema, alikata kona na kutoka kwenye barabara ya lami, akaongeza mwendo kuelekea The Paradise Hotel. Akiwa kwenye kasi kubwa, gari likaanza kuyumbayumba huku likitaka kutoka nje ya barabara hiyo ya vumbi.

    “Daah! Mkosi gani tena huu.”

    “Kwani vipi tena baba?”

    “Sijui nimekanyaga misumari? Matairi yote ya mbele yamepata pancha,” alisema mzee Kenan huku akiendelea kuhangaika kulidhibiti gari lililokuwa linayumbayumba, akapunguza mwendo na kufanikiwa kusimama salama kando ya barabara.

    “Sasa si nitachelewa baba? Naomba nikodi hata teksi tafadhali,” Caro alisema baada ya kuona huo ndiyo mwanya pekee wa kumkimbia mzee Kenan, baba wa rafiki yake wa tangu utotoni, Aidan. Mzee huyo alifikiria kwa muda, bila kujibu kitu akateremka na kuangalia jinsi matairi ya mbele yalivyoharibika, akajilaumu sana.

    Hakuwa na cha kufanya zaidi ya kumsimamishia Caro teksi na kumuelekeza dereva ampeleke Ubungo. Wakaagana huku Caro akimshukuru Mungu wake kwani hakujua mzee huyo alikuwa amepanga kufanya jambo gani ndani ya kichwa chake, hasa kutokana na vituko vya kimapenzi alivyokuwa anamfanyia bila kujali kwamba ni sawa na mwanaye wa kumzaa.

    Harakaharaka Caro akateremsha mizigo yake na kusaidiana na dereva teksi kuipakiza kwenye gari, wakaondoka huku mzee Kenan akimsindikiza Caro kwa macho mpaka teksi ilipopotea kwenye upeo wa macho yake. Akachukua simu na kumpigia fundi wake kwa ajili ya kuja kumbadilishia matairi kwenye gari lake.

    Caro alifika Ubungo muda mfupi baadaye, alikwenda moja kwenye ofisi za basi alilokata tiketi. Harakaharaka akasaidiwa kupelekwa kwenye basi hilo ambalo lilikuwa limebakiza muda mfupi kabla ya kuondoka. Ni mpaka alipoingia ndani ya basi na kukaa kwenye siti yake ndipo alipoamini kwamba yupo salama, akashusha pumzi ndefu na kumshukuru Mungu wake.

    Safari ilianza huku kichwani akiwa na mawazo tele juu ya kila kitu kilichokuwa kinaendelea kwenye maisha yake. Safari ya kuelekea Morogoro, nyumbani kwa bibi na babu waliomzaa mama yake ikaendelea. Baada ya saa kadhaa, tayari basi lilikuwa limeshafika Morogoro, akateremka kwenye Kituo cha Mabasi cha Msamvu na kupanda ‘kipanya’ kilichompeleka mpaka Kihonda ndanindani, nyumbani kwa bibi na babu yake.

    Bibi na babu yake ambao licha ya umri wao mkubwa walikuwa wakiishi maisha ya kisasa, wakiwa karibu na kila muhimu kwenye himaya yao, walimpokea Caro kwa furaha na kumkaribisha nyumbani hapo. Baada ya kusalimiana na kupeana michapo ya hapa na pale, walimuandalia Caro maji ya kuoga kisha akaandaliwa chakula maalum kwa ajili yake mgeni.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kula, aliomba kupumzika kutokana na uchovu wa safari ambapo alipelekwa kwenye chumba cha wageni. Akajitupa kitandani na kutulia kwa muda, mawazo juu ya Aidan yakaanza kumjia kwa kasi. Akawa anakumbuka mambo mbalimbali waliyoyafanya pamoja tangu wakiwa wadogo, akaishia kutabasamu mwenyewe.

    Aliendelea kutafakari mambo mbalimbali kuhusu jinsi urafiki wao ulivyokuwa umeshamiri na hatua waliyokuwa wamefikia ya kutaka kuvuka mipaka ya ukaka na udada waliyojijengea tangu wakiwa wadogo na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi.

    “Nampenda sana Aidan, yeye ndiyo atakuwa mwanaume wangu wa kwanza na wa mwisho, tukimaliza shule nataka anioe nimzalie watoto wazuri kama mimi,” Caro aliwaza huku akijigeuzageuza pale kitandani, uso wake ukiwa umejawa na tabasamu pana.

    Ghafla alikumbuka kitu kilichoitibua furaha yake; mzee Kenan na vituko vya kimapenzi alivyokuwa anamfanyia. Akakumbuka kuhusu zawadi alizomnunulia muda mfupi kabla hajasafiri, akashikwa na shauku ya kutaka kuziona zawadi zenyewe. Akainuka na kwenda kwenye mizigo yake, akachukua mfuko aliopewa na mzee Kenan, akaenda nao kitandani na kuanza kuufungua.

    “Haaa! Hivi vitu gani tena?” Caro alipigwa na butwaa baada ya kuanza kuufungua mfuko huo, akiwa ni kama haamini alichokiona. Alirudia kutazama mara mbilimbili huku macho yakiwa yamemtoka kama mjusi aliyebanwa na mlango.

    Mzee Kenan alikuwa amemnunulia zawadi ya nguo kadhaa za ndani zikiwa na ujumbe wa kimapenzi pamoja na mkufu wa dhahabu ambao ulionekana kuwa tofauti na ile ya kuvaa shingoni. Hakuyaamini macho yake, akajikuta akiuachia mfuko huo, ukadondoka chini kisha akajishika tama akitafakari kwa kina mzee huyo ambaye kwake alikuwa ni sawa na baba yake, alikuwa na maana gani kumfanyia kitendo kama hicho.





    LIJIKUTA akizama kwenye dimbi la mawazo kwa kipindi kirefu, akitafakari kwa kina afanye nini ili kuukwepa mtego hatari uliokuwa mbele yake. Kuna wakati alipata wazo kwamba ili kumkomoa mzee huyo, dawa yake ni kuwaeleza ukweli wazazi wake juu ya kila kitu kilichokuwa kinaendelea.

    Hata hivyo, akili nyingine ilimtuma kuwa asifanye hivyo kwani hiyo ingemaanisha kuvunja kabisa urafiki uliovuka mipaka na kuwa kama undugu, baina ya familia hizo mbili. Pia alitamani kumueleza Aidan lakini akili nyingine ikamzuia kwani kufanya hivyo ilikuwa ni kuwagombanisha mtu na baba yake, jambo ambalo hakutaka litokee.

    Licha ya kufikiria kwa muda mrefu, bado hakupata jibu la moja kwa moja, akaamua kuendelea kukaa na siri hiyo ndani ya kichwa chake.

    ***

    Aidan alishtushwa na taarifa za msichana aliyetokea kumpenda tangu wakiwa wadogo, Caro kufunga safari ya ghafla na kuondoka bila hata kumuaga, muda mfupi tu baada ya kumweleza ukweli uliokuwa ukimtesa ndani ya moyo wake.

    “Kwani hajakuaga?”

    “Wala hajaniaga ndiyo maana nashangaa, siyo kawaida yake kabisa.”

    “Hata sisi wenyewe tulishangaa kwani safari ilikuwa ya ghafla mno na aling’ang’ania kweli, ikabidi tumruhusu kwani hatukutaka kumuudhi,” mama mzazi wa Caro alikuwa akizungumza na Aidan ambaye baada ya kusikia taarifa hizo, ilibidi aende kupata uhakika kwa mama yake.

    “Amesema atarudi nini?”

    “Mh! Wala hatujui lakini inawezekana likizo yote akakaa hukohuko kwa bibi yake.”

    Majibu hayo yalimmaliza kabisa nguvu Aidan, akaondoka akiwa mnyonge na kwenda kukaa kwenye bustani ya maua, mawazo mengi yakikisumbua kichwa chake. Alipowaza kwa kina, alihisi lazima kuna tatizo linalomsumbua Caro ingawa alishindwa kuelewa ni tatizo gani kwani alikuwa na mabadiliko ya ghafla.

    Alijaribu kujikagua matendo yake akihisi huenda yeye ndiye aliyemkwaza Caro lakini hakugundua kosa lolote alilolifanya. Akaendelea kuzama kwenye dimbwi la mawazo machungu mpaka machozi yakawa yanamtoka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mbona umejiinamia hapa kwa muda mrefu? Kuna tatizo?”

    “Hapana baba, hakuna tatizo lolote,” alisema Aidan huku akijifuta machozi, akitaka baba yake ambaye ndiyo alikuwa akirejea muda huo asigundue chochote.

    “Unanificha? Unajua siku hizi umekuwa na tabia za ajabuajabu sana?” baba yake Aidan, mzee Kenan alianza kufoka. Aidan alishindwa kuelewa kwa nini baba yake anakuwa mkali kwake bila sababu, hata hivyo hakumjibu kitu zaidi ya kuendelea kujiinamia.

    “Badala ya kujisomea ndani una kazi ya kulialia tu, najua hiyo yote ni kwa sababu unawaza mapenzi badala ya masomo, na kwa taarifa yako lazima nikuhamishe ile shule unayosoma,” alisema mzee huyo na kuondoka, akamuacha Aidan kwenye lindi lingine la mawazo.

    Kuhamishwa shule kulimaanisha kumtenga mbali na kipenzi cha moyo wake, Caro, jambo ambalo hakuwa tayari kuona linatokea. Akajilazimisha kuchangamka ambapo aliondoka na kwenda kuchukua madaftari yake, akakaa sebuleni na kujifanya anasoma ili kumfurahisha baba yake. Hakutaka kabisa kuhamishwa shule.

    Siku zilizidi kusonga mbele, hatimaye likizo ikawa inaelekea ukingoni huku Aidan akijitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kumfurahisha baba yake ili asimhamishe shule. Jioni moja, Aidan akiwa anajisomea sebuleni kwao, alishtuka baada ya kusikia sauti kama ya Caro mlangoni kwao akibisha hodi.

    Harakaharaka akaacha kila alichokuwa anakifanya na kwenda kufungua mlango, hakuamini macho yake kumuona Caro, akiwa amenawiri vizuri na kuzidi kuwa mrembo. Kwa jinsi alivyokuwa amemkumbuka, alimkumbatia kwa nguvu na kumbeba juujuu mpaka sebuleni.

    Wakaangushana kwenye sofa huku kila mmoja akiwa na furaha ya ajabu. Wakaendelea kukumbatiana kwa muda huku wakimwagiana mabusu mfululizo.

    “Kwa nini uliondoka bila kuniaga mpenzi wangu?”“Nisamehe sana Aidan, kuna jambo lilinilazimisha kufanya hivyo lakini elewa kwamba nilifanya kwa sababu ya upendo wangu kwako,” alisema Caro huku akiwa bado amekumbatiana na Aidan, akaendelea kumuomba msamaha kwa kitendo hicho na kumhakikishia kwamba anampenda sana.

    “Kweli unanipenda Caro?”

    “Nakupenda sana Aidan, kutoka ndani ya moyo wangu! Wewe ndiye mume wangu na baba wa wanangu watarajiwa, tukimaliza shule nataka unioe,” alisema Caro huku akimtazama Aidan kimahaba, kauli iliyomfurahisha sana Aidan.

    Wakaendelea kuzungumza mambo mengi huku kila mmoja akiwa na furaha kubwa ndani ya moyo wake. Wakatoka wakiwa wameshikana mikono na kwenda kwenye bustani za maua, walipozoea kucheza tangu wakiwa wadogo. Wakawa wanacheza kama watoto wadogo, kila mmoja akiwa na furaha. Baadaye wakakaa sehemu tulivu na kuendelea kuzungumza mambo yao.

    “Aidan! Aidan,” sauti ya mzee Kenan ilisikika kwa nguvu kutokea ndani kwao, harakaharaka akainuka na kumuacha Caro pale bustanini kwa ajili ya kwenda kumsikiliza baba yake.

    “Umeanza kuingiza wanawake hapa ndani kwangu si ndiyo? Huu mkoba wa kike ni wa nani?” mzee huyo aling’aka huku akimuonyesha mwanaye mkoba alioukuta kwenye sofa.

    “Ni wa Caro, sijaingiza mwanamke yeyote baba.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ni wa Caro? Kwani amesharudi? Yuko wapi? Hebu kamuite,” maneno yalimtoka mfululizo mzee huyo, ile sura ya ukali ikayeyuka ghafla na tabasamu likaanza kuchanua usoni kwake.

    Harakaharaka alitoka na kwenda mpaka pale bustanini alipomuacha Caro, akamwambia kwamba baba yake anamuita. Tofauti na alivyotegemea, Caro hakuonyesha kufurahia wito huo, akainuka kwa kujilazimisha huku lile tabasamu alilokuwa nalo tangu alipofika likiyeyuka.

    Walipoingia tu, alimpokea kwa uchangamfu na kuanza kumuuliza habari za alikotoka.

    “Aidan nenda dukani kaninunulie vocha,” alisema mzee huyo kama gia ya kumtoa Aidan na kumfanya abaki peke yake na Caro. Alipotoka, alisogea kwenye sofa alilokuwa amekaa Caro na kuanza kuzungumza naye kwa upole kwani alionyesha hayupo sawa.

    “Vipi zawadi zangu nilizokupa siku ile ulizifurahia?”









    ITAENDELEA  

0 comments:

Post a Comment

Blog