Search This Blog

Friday, October 28, 2022

NINI HATIMA YA MAISHA YANGU - 4

 





    Simulizi : Nini Hatima Ya Maisha Yangu

    Sehemu Ya Nne (4)





    Nilishtuka sana baada ya kuona sura ya Babu ndani ya lile gari. "Pengine nimemfananisha tu. Babu hawezi kufanya hivi"

    Nilijikuta nikiumiza kichwa kwa kile kitendo kilichokuwa kimetokea.



    "Itakuwa katumwa na Baba mkubwa. Maskini mzee wawatu anakosa gani, mpaka wamuuwe kikatili hivi, yaani binadamu tunaroho mbaya sana tena sana"

    Nilijikuta natokwa na machozi ya hasira kwa kile kilichotokea, japo sikuwa namfahamu yule mzee ila kwa jinsi alivyogongwa na lili gari alihitaji kuonewa huruma sana.

    "Kaka mbona unalia. Huyu mtu unamfahamu"



    Aliniuliza mdogo wangu na kunifanya kuondoka kwenye mawazo niliokuwa nayo. Nilishindwa kumjibu kitu zaidi ya kumwambia tuingie ndani, maana tayari watu walikuwa wameshajaa.



    Nilijua pengine mdogo wangu alikuwa hajamuona yule mtu, alie sababisha ile ajali. Laiti angeliona sijui angefanyaje.

    Siku inayofuata ilikuwa siku ya mapumziko. Tulipanga tutoke kama familia, lakini Naomi alionekana hayupo sawa.



    Ilitubidi tumpeleke hospitali ili kujua tatizo nini. Tulipofika hospitali ilitubidi sisi kubaki kwenye gari, maana tusingeweza kuingia hospital wote. Tukiwa ndani ya gari tuliona gari moja ya kifahari inaingia pale hospital.



    Kiukweli lile gari lilikuwa zuri sana. Alishuka kijana mmoja aliekuwa amevalia suti nyeusi, aliposhuka alifungua mlango wa nyuma. Alipofungua mlango, alitoka mzee mmoja mwenye mwili wa kibabe huku akiambatana na mwanae wakike.



    Nilipomwangalia yule msichana, alionekana kutokuwa na furaha na alionekana mtu mwenye mawazo mengi sana. Kabla hawajaondoka kuelekea kwenye mlango wa hospital, kuna kijana mmoja alitokea mlango wa nyuma.



    Nilivyo mwangalia yule kijana nilishtuka kumuona maeneo yale, maana yeye alikuwa ni bodigadi au mlinzi wa Baba mkubwa. Nilivyoona vile sikutaka kuumiza kichwa changu. Nilijua pengine yule ni mdogo wake pamoja na Babu yake. Waliingia ndani huku yule mmoja wao akiwa amebaki ndani ya lile gari.



    Tukiwa bado tupo ndani ya gari tukiwa subiri wakina Naomi, ambao wao kwa wakati huo walikuwa ndani ya ile hospital. Tulingoja muda mrefu sana pale kwenye gari bila kuwaona wakina mjomba pamoja na Mzee Solomon na mwanae.



    Tulipoona hakuna mtu alieonekana kurudi ilinibidi nitoke na kumwacha mdogo wangu ndani ya gari.



    Nilipokuwa naingia ndani ya hospital, mlangoni nilipishana na yule mzee akiwa na yule kijana pamoja na yule msichana. Muonekano wa yule mzee ulinipa wasiwasi sana, maana alionekana ni mtu mwenye haraka na alie kuwa na hofu kubwa. Siku mtilia maanani sana.



    Hiyo ni kutokana na kutomfahamu yeye pamoja na watu wake. Nilipokuwa nazidi kusonga mbele nilianza kupata wasiwasi juu ya yule mzee, hiyo ni kutokana na kuona michirizi ya damu ikiwa inatoka kwenye moja ya chumba vilivyokuwa pale hospital.



    Nilishtuka sana baada ya kuziona zile damu, sikutaka kuwa shaidi wa lile jambo zaidi ya kuamua kuelekea walipo Mjomba.



    Niliwaza huenda mjomba pamoja na Mzee solomon watakuwa hawapo salama. Nilizidi kusonga mbele huku nikiwa kama mtu nilie changanyikiwa maana nilikuwa nikipiga kelele huku nikiita bila kujali pale ni hospital na kuna wagonjwa.



    Nikiwa nazidi kusonga mbele nilifanikiwa kuwaona wakina mjomba na mzee Solomon pamoja na Naomi wakiwa wanatoka kwenye chumba cha Dokta, walionekana ni watu waliokuwa hawatambui nini kilichokuwa kinaendelea pale hospital. Nilimshukuru Mungu kuwakuta wapo salama wote. Tulirejea nyumbani huku akili yangu ikiwa bado inawaza juu ya lile tukio lililotokea pale hospital.



    "Inamaana yule mzee ni muuwaji" Nilijikuta nikiropoka kwa sauti bila kujijua. "Yule mzee aliekuwa na yule msichana?" Alidakia mdogo wangu baada ya kusikia. Nilitahamaki kusikia mdogo wangu kuniuliza vile. "Amejuaje kwamba ni yule mzee" Nilijiuliza kimoyo moyo bila kupata jibu kamili.



    Nilikosa jibu la kumjibu ikabidi kukaa kimya, huku nikiwa nazidi kutafakari lile tukio lililokuwa limetokea muda mfupi uliotokea. Usiku wa siku hiyo Mjomba aliniambia nijiandae kuna sehemu aliitaji kwenda na mimi. Nilifanya kama alivyotaka, baada ya kumaliza kujiandaa alikuja hadi chumbani kwangu na kuniambia tuondoke.



    Sikutaka kuuliza maswali mengi, maana nilimwamini Mjomba sana. Tulitoka hadi barabarani ambako kulikuwa na daladala pamoja na bajaji, tuliingia ndani ya bajaji na safari ilianza.



    Tukiwa kwenye bajaji story za hapa na pale zilikuwa zikiendelea. "Mjomba ni wapi tunapoelekea, maana hujaniambia na ukichukulia ni usiku na siyo kawaida yako kutoka usiku" Nilimuuliza Mjomba baada ya kuona anipi taarifa zozote za tunako kwenda.



    Mjomba alinisihii nisiwe na haraka nitafahamu, niliamua kukaa kimya na kusubiri kufika hiyo sehemu aliyokuwa ananipeleka Mjomba.

    "Tuache hapo kona" Aliongea Mjomba kumwambia dereva wa ile bajaji, maana mjomba alisema tumeshafika.



    Tulishuka na kuelekea kwenye nyumba moja ya kifahari, nyumba ile ilionekana ni nyumba ya mtu ambae yupo juu kifedha. Nilipoiona ile nyumba ya kifahari nilianza kupata hofu kwa kujua mjomba alikuwa ameniuza kwa Baba Mkubwa.



    Nilimgeukia mjomba na kumuuliza "hapa ni wapi na ni kwanani?" Nilimuuliza mjomba baada ya kuona ile nyumba japo sikuwa naamini kuwa mjomba hawezi kuniuza kwasababu yeye ni kama Baba kwangu. Mjomba hakunijibu kitu yeye aliendelea kusonga mbele. Nilimfuata hadi tukaingia kwenye ile nyumba.



    Tulipoingia ndani nilikaribishwa na mwana dada mrembo, nilipoingia niliketi kwenye moja ya sofa pale ndani. Baada ya muda kidogo alikuja kijana wa makamo, nilipomuona yule kijana nilishangaa sana kumuona yule kijana akiwa anafanana na Mjomba Denis.



    Nilipigwa na butwaa kwa kile nilichokiona, nilihisi huenda naota tena ndoto za mchana lakini haikuwa hivyo ilikuwa ni ukweli mtupu. Niliwatizama mara mbili mbili nisipate jibu kamili, nilibaki tu nimeduwaa. Niliwaza na kuwazua ila bado sikupata jibu kamili.



    Wakati nikiwa namshangaa yule kijana huku nikiwa bado namtathimini, nilishangaa namuona Babu yangu akiwa ametokea kwenye mlango ule alieingilia yule kijana. Nilipomuona Babu yangu nilishtuka na kutaka kukimbia. Lakini mjomba aliniwahi na kunirudisha na aliniondoa hofu kwa kuniambia kama yeye yupo basi hakuna kinacho haribika. Kiukweli nilikuwa nimechanganyikiwa sana, akili yangu niliona kama inataka kusimama.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Karibu mjukuu wangu na mbona unaniogopa sana nini tatizo?"



    Aliuliza Babu baada ya kuniona nina hofu sana, nilikosa cha kumwambia nikabaki kimya lakini mawazo yangu hayakuwa pale kabsa, nilikuwa nikikumbuka tukio la kugongwa na gari la yule mzee ambalo lilitokea karibu na nyumba yetu, na alifanya tukio lile alikuwa Babu yangu maana nilimshuhudia kwa macho yangu mawili.



    Kila nikumbukapo tukio hilo huwa namchukia sana Babu.

    Kabla hatujaketi alikuja mzee mmoja ambae bila kukosea alikuwa ametokea mule ndani, alikuwa ni mzee wa makamo.



    Alitusalimia kisha akaketi, nilivyo mwangalia yule mzee nilishtuka sana. Alikuwa yule mzee niliemuona pale hospitalini wakati tulipo mpeleka Naomi hospital, nilimkumbuka vizuri pamoja na lile tukio lililo tokea pale hospital.



    Nilipata wasiwasi na hofu kubwa, lakini Mjomba yeye wala hakuwa na hata chembe ya kuogopa, alionekana mtu alie juwana na wale watu kwa kipindi kirefu.









    Wakati nazidi kuwashangaa wale watu huku nikiwa na tahamaki juu ya uwepo wangu kwa watu wale, nilishangaa kumuona mdogo wangu anaingia pale ndani tena akiambatana na kijana ambae kwa haraka haraka sikuweza kumtambua.

    Niliona kama ni ndoto kwa yale niliyokuwa nayaona, nilikuwa kama mtu aliechanganyikiwa.



    Nilizidi kushangaa tu bila kujua nini kilikuwa kikiendelea.

    Walianza kusalimiana huku wakiwa wanachekeleana. Kitendo cha kumuona mdogo wangu pale tena akiwa mwenye kujawa na furaha kilinishangaza sana na kunipa maswali mengi.



    Kwa upande wangu wasiwasi na hofu zilinijaa. "Vipi kaka John mbona upo hivyo, unaonekana mtu mwenye mawazo mengi. Nini shida kaka yangu" Aliniuliza mdogo wangu baada ya kuniona nipo kimya. Nilishindwa kumjibu nikabaki nimekaa kimya nikiwa nazidi kuwatafakari wale watu.

    "Mjomba hapa ni wapi na umenileta hapa kuja kufanya nini?" Nilimuuliza Mjomba huku nikiwa nawaangalia wale watu, lile swali lilionyesha kumshtua Mjomba na ilionekana hakutarajia kukutana na lile swali. Wote walianga kunishangaa kana kwamba lile swali lilikuwa halieleweki, walikaa kimya ndipo nikaamua kuuliza kwa ukali kidogo huku nikiwa nimewakazia macho.



    Waliendelea kukaa kimya huku wakizidi kunishaa kama vile hawakuwahi kuniona hapo kabla, ile hali ya kunishangaa huku wakiwa kimya ilinipa hasira, lakini mjomba alinituliza na kuniambia mambo mazuri hayahitaji haraka hivyo niwe mtulivu ili tuende sawa. "Mjomba hawa siyo watu wazuri kabisa japo huyu ni Babu yangu lakini siyo mtu mzuri.



    Huenda hawa ndiyo walishirikiana na Baba mkubwa kuwauwa wazazi wangu. Niliongea kwa hasira huku nikiwa sina huakika na yale niliyo kuwa nikiyasema. Nilishangaa Babu ananyanyuka kwa hasira na kuanza kunifuata huku akionyesha dhahiri kukasirishwa na yale maneno.



    Nilitamani kukimbia ila tayari alisha nifikia ila kabla hajanipiga au kunifanya chochote Mjomba aliingilia na kumshika Babu ambae kwa wakati huo alionekana kufura hasira. Nilijua nimefanya makosa lakini yote nilifanya kutokana na hasira, niliona aibu hata kumwangalia Babu maana nilihisi kumkosea sana.



    "Embu jaribuni kuwa watulivu maana hiki sicho kilichotuleta hapa" Aliongea yule kijana alifanana na Mjomba Denis, lakini Babu yeye alionekana mtu mwenye hasira huku akinitizama kwa jicho la hasira. Walizidi kuongea mambo mengi huku mimi akili yangu ikiwa haipo pale, kitu ambacho kilinifanya nishtuke na kutoka kwenye mawazo ni pale walipo sema Baba yangu alikuwa hai.



    Nilihisi kusikia vibaya lakini nilizidi kushangaa zaidi walipo nambia kuwa yule kijana aliefanana na Mjomba ndiye Baba yangu. Kiukweli nilistaajabu kusikia kitu kama kile, nilihisi bado nipo kwenye ndoto lakini haikuwa ndoto, ilikuwa ni kama magizo tena igizo lisilokuwa na maana kamili.



    Nilikaa kimya kidogo huku nikiwa najiuliza "Huenda watu hawa wamechanganyikwa. Eet huyu ni Baba yangu mtu mwenyewe simfahamu ndiyo mara yangu ya kwanza kumuona leo awe Baba yangu" Niliongea kwa kujiamini huku nikicheka na kuhisi wale watu wamechanganyikiwa.



    Haikuniingia akilini kitu kama kile.

    "Kwahiyo huu ndiyo ujinga mlioniitia hapa kwamba huyu ni Baba yangu"

    Niliongea huku nikiwa najiandaa kunyanyuka ili nitoke nje, ila kabla sijanyanyuka nilishtukiza kapigwa kibao kikali, kilichonifanya nirudi mdogo mdogo kwenye kitu.



    Nilipoangalia ni nani kanipiga nilishangaa alikuwa ni Mjomba Denis huku nae akionyesha kuwa na hasira. Nishangaa maana watu wote walionekana kunitizama kwa hasira nisijue nini cha kufanya.



    Niliona nikiendelea kuwa mkali na mwenye hasira ningeleta ugomvi, niliamua kuwa mpole na kubaki kama mtu aliemwagiwa maji ya kwenye mtungi.

    "John hapa unapotuona si kwamba hatuna akili au hatujakosa kazi za kufanya. Nakuomba jaribu kuwa na heshima usiwe kama alivyo Baba yako!"

    Aliongea yule kijana aliesemekana ndiye Baba yangu na kufanya watu wote washangae.



    Nilianza kupata wasiwasi yakuwa huenda hawa si watu wazuri maana waliesema ni Baba yangu nae ilionyesha si Baba yangu.

    "Mbona nashindwa kuwaelewa kwa maneno mnayo yazungumza, mmeniambia huyu ndiye Baba yangu. Sasa mbona kwa maneno anayo yaongea yanaonyesha yakwamba si Baba yangu?"

    Niliuliza kwa kutahamaki huku nikiwa nasubiri jibu ya lile swali.

    "Kama ulivyo sema hujakosea kabisa maana ni kweli mimi siyo Baba yako"



    Alinijibu yule kijana na kuwafanya wakina mjomba kuzidi kushangaa na kutahamaki, huku nao pia wakitamani kujua nini kinaendelea.

    Watu wote tulikaa kimya kusubiri alichotaka kusema yule kijana.

    "Najua wengi wenu hamjui ukweli kuhusu hawa watoto, kiukweli hii ilikuwa ni siri ya kipindi kirefu ambayo ilikuwa baina ya watu watatu tu, ambae ni mimi pamoja na wazazi walezi wa hawa watoto"

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliongea kijana yule huku akiwa anatutazama mimi pamoja na Mdogo wangu Sophia.

    "Polani sana wajomba zangu maana mmeishi maisha magumu angali Baba yenu ana fedha nyingi, uwezo aliokuwa nao Baba yenu ni mkubwa ni tofauti na maisha mnayoishi leo. Ila ukweli ni kwamba wale waliopoteza maisha kipindi cha nyuma siyo wazazi wenu wa kuwazaa!"



    Alizidi kuongea yule kijana huku maneno yake yakizidi kunipa maswali mengi.

    "Yule aliekuwa Mama yenu kwangu mimi alikuwa ni Dada yangu na huyu mnaemuona hapa ni mdogo wangu. Nistori ndefu sana na itanichukua muda mrefu kuwaambia hii siri ambayo ilidumu zaidi ya miaka kumi na tisa na kama mnavyoona muda ulivyeenda. Ni vema kama tungeenda kupumzika alafu kesho tuzungumze jambo hili"



    Kiukweli yale maneno yalikuwa mazito kwa upande wangu, sikuwahi kufikiria katika maisha yangu kama nina mzazi katika hii Dunia. Siyo mimi pekee nilie stajabika kusikia maneno yale. Hata Mjomba na wengine wakionekana kushangazwa na lile jambo.

    Nilishindwa kuelewa yale maneno japo alitumia lugha fasihi ya kiswahili lakini mimi niliona ametumia lugha tofauti, nilipo waangalia Mjomba pamoja na Babu walionekana ni watu waliokuwa na mshangao mkubwa juu ya kile alichokisema mjomba.



    Hatukuwa na budi ilibidi kila mtu aingie chumbani kwaajili ya kupumzika, ilikuwa kama ndoto katika maisha yangu kwa kile nilichoelezwa na mjomba. Ile nyumba ilikuwa kubwa na ilikuwa na vyumba vingi, niliingia kwenye chumba kimoja kwenye ile nyumba ili kupumzika kwaajili ya siku inayofuata.



    Usiku wa ile siku sikuweza kupata usingizi kabisa, nilikuwa na mawazo mengi juu ya utata katika maisha yangu. Nilikumbuka maisha ya nyuma kipindi tukiwa na Wazazi wetu, nilikumbuka jinsi tulivyoishi maisha ya furaha, kiukweli nilitamani maisha siku zijirudi ili niendelee kuyafurahiya maisha yale ya nyuma.



    "Hivi ni kweli wale waliopoteza maisha siyo wazazi wangu na kama siyo wazazi je wazazi wangu ni kina_nani?"

    Kichwa changu kilizidi kutawaliwa na mawazo na maswali mengi, huku maswali hayo yakiwa magumu kuyajibu. Usingizi ulinisumbua ukiambatana na uchovu, japo nilikuwa na mawazo mengi na maswali ila usingizi ulinizidi hatimae nilipitiwa na usingizi.



    "Hivi ni kweli wale waliopoteza maisha siyo wazazi wangu na kama siyo wazazi je wazazi wangu ni kina_nani?"

    Kichwa changu kilizidi kutawaliwa na mawazo na maswali mengi, huku maswali hayo yakiwa magumu kuyajibu. Usingizi ulinisumbua ukiambatana na uchovu, japo nilikuwa na mawazo mengi na maswali ila usingizi ulinizidi hatimae nilipitiwa na usingizi.



    Nikiwa kwenye usingizi niliota ndoto, ndoto ambayo ilikuwa na maswali mengi sana, maana niliota nikiwa na wazazi wangu pamoja na mdogo wangu tukiwa pamoja tukiwa tunasherekea sikuku ya mwaka mpya. Siku iyo ilikuwa ni siku ya furaha sana, majirani, jamaa na marafiki walikuja nyumbani kwetu maana siku ile tulikuwa na sherehe ndogo pale nyumbani.



    Wengi walionekana kuwa na tabasamu katika nyuso zao, nilifurahi sana kuona kila mtu anatabasamu lakini wakati muda ulivyozidi kuenda ndivyo nilianza kuona lile tabasamu kwa wale watu likiwa hafifu. Sikulifikiria sasa lile jambo niliona ni kitu cha kawaida. Ikiwa inaendea saa tano usiku alikuja mzee wa makamo, ambae alionekana kula chumvi nyingi ni kutokana na muonekano wake.



    Yule mzee alikuwa ni mtu nadhifu na mwenye heshima zake, alipoingia alisogea hadi mahali alipokuwa ameketi Baba yangu pamoja na Mama yangu. Alipomfikia alimsogelea na kumnong'oneza kitu, mimi binafsi sikuwa nafahamu yule mzee ni nani na anauhusiano gani na Baba yangu. Kitu ambacho kilinishangaza ni pale yule mzee alipomnong'oneza Baba na Baba kuonyesha kushtuka. Sikutaka kujua sana maana nilijua ni watu waliofahamiana, waliendelea kuongea huku wakiwa wanaelekea nje.



    Lakini kabla hawajafika mlango wa kutokea nje nilishangaa kumuona Baba anaanguka chini na kuanza kutokwa na mapovu mdomoni. Nilishangaa sana lakini kabla sijasogea pale Baba alipoangukia nilishangaa Mama nae anaanguka kama Baba alivyoanguka na kuanza kutokwa na mapovu mdomoni. Nilistaajabu na kubaki nimesimama katikati huku nikiwa sijui cha kufanya huku nikiwa kwenye mtihani mzito, sikuwa najua nianzie wapi na niishie wapi.



    Kabla sijapata jibu nilishtuka kutoka usingizini, pale kuwa pamepambazuka jua nalo lilikuwa tayari lilisha tawala anga. Nilitoka kitandani na kuingia bafuni ambapo palekuwa ni pale pale chumbani. Nilipomaliza kupiga mswaki na kukoga nilitoka hadi sebleni, ambapo wakina mjomba walikuwa tayari wapo mezani wakipata kifungua kinywa. Nilisogea taratibu hadi mezani na kupata kifungua kinywa kwa pamoja, baada ya tumbo kuwa safi swali la kwanza kwa mjomba ni juu ya wazazi wangu.



    Lile swali halikuwashtua sana watu waliokuwamo pale maana kila mmoja wetu alikuwa anatamani kufahamu ukweli ambao mjomba anadai ilikuwa siri. Mjomba aliniangalia kwa jicho la upole akionekana kusikitishwa na kile alichotaka kutuambia.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nawashukuruni kwa uwepo wengu hapa, najua mnashauku kubwa ya kupata kufahamu ukweli kuhusu ili jambo"



    Aliongea mjomba hukakiwa anaketi vyema kwa kutupa mkasa mzima wa maisha yetu.



    "Katika familia yetu tulizaliwa watoto watatu mmoja wetu akiwa ni wakike, ambae ndiye Mama yenu mlezi, kiukweli hatukuwahi kujuta katika maisha yetu, maana tulilelewa maisha mazuri na ya dini, hatukuwahi pata shida zaidi ya kuona kwa majirani na watu wa karibu, au nasema uongo?"



    Aliongea mjomba na kumuuliza mjomba Denis na Mjomba Denis alitingisha kichwa kuashiria alichokuwa anaongea ni ukweli.



    "Dada yangu ambae kwa sasa ni marehemu, alibahatika kuolewa katika familia ya watu wenye uwezo kifedha. Maisha ya Dada yangu yalibadilika sana hakuwa tena mtu wa kawaida maana Mumewe alikuwa ni mtu mkubwa serikali. Japo elimu aliokuwa nayo Dada yangu haikuwa ya juu sana ila alipata kibaki cha kutembelea nchi mbali mbali na mataifa mengi, hali ile ilimfanya Dada yangu kuwa mtu maharufu na mwenye maendeleo makubwa, mume wake alimpenda sana Dada yangu na kumthamini hadi ikafika wakati akatamani kuwa nae kila wakati"



    Alizidi kuongea Mjomba na kuchukua glas ya maji na kumeza fundo mbili za maji na kuendelea.







    "Licha ya kuwa na furaha kati ya Dada yangu na Mume wake lakini kuna kitu kilipungua katika nyumba yao, zaidi ya miaka kumi ndani ya ndoa yao hawakubahatika kupata mtoto kitu ambacho kiliwaumiza sana. Kila siku walikuwa wakimuomba Mungu afungue milango yake ili angalau wapate hata mtoto mmoja, lakini bado hawakupata mtoto. Naweza kusema Mungu alikuwa na makusudi yake, waliendelea kuwa na imani ya kuwa ipo siku watapata mtot.."



    Kabla hajaendelea simu yake ilita na kumfanya akae kimya na kuichukua simu yake kwa ajili ya kuipokea lakini alichofanya Mjomba kilikuwa tofauti maana alibonyeza kitufe cha kukata simu na kuizima kabisa. Kile kitendo kilinishangaza na kujua lile jambo alilokuwa analiongelea lilikuwa lina umuhimu sana.



    "Mungu aliwasaidia na kuwapatia mtoto wa kike ambae walimpa jina la Sophia, furaha na tabasamu iliyopotea kwa muda mrefu vilirejea katika familia hiyo. Wanandoa hao walimshukuru Mungu kwa kuwapa mtoto mzuri na mwenye afya njema huku wakiamini bila Mungu wasingefanikiwa au kufika hapo walipokuwa, maisha yafuraha yaliendelea huku mtoto wao akiendelea kunawiri na kuwa na afya njema.

    Kwakuwa wanandoa hao walikuwa na majukumu mbalimbali ya kitaifa hivyo iliwagharimu kutumia muda mwingi kulitumikia Taifa, walikubaliana kuleta mfanyakazi wa kike kwaajili ya kumwangalia mtoto wao na pia waliweza kupata kijana ambae alikuwa kama mlizi katika nyumba ya familia hiyo. Kijana huyo ambae alionekana mzoefu kwenye kazi hizo na mwenye uelewa mkubwa aliejulikana kwa jina la Derick"



    Aliongea mjomba huku akionekana kuwa na hali ya huzuni, kwa yale maneno aliokuwa anayaongea Mjomba yalianza kunifungua akili juu ya familia yangu japo sikuwa na uhakika kwa yale niliyokuwa nikiyawaza.



    "Derrick alikuwa ni kijana mwenye kujiamini sana na ndicho kitu kilichomfanya kupata kazi katika familia hiyo. Elimu yake ilikuwa ni darasa la nne, kila alichokiona kwenye ile nyumba kilikuwa kigeni machoni mwake.

    Kiukweli alikuwa kama mtu aliezaliwa leo, lakini kwa upande wa msichana wa ndani, yeye alionekana kuwa mwelewa wa baadhi ya vitu katika nyumba ile. Maisha ya familia ile yalikuwa tofauti na familia nyingie maana hawakuwa na ubaguzi wa kuwatenga wafanyakazi wa familia ile, waliwapenda kama watoto wao, kila walichotaka waliwapatia.

    Wakiwa kazini huku nyuma mazowea kati ya kijana Derric na msichana wa kazi yalianza kujengeka kwa kasi, walikuwa na muda mzuri wa kufanya yao. Kiukweli walifurahiya maisha yale wakiwa ndani ya penzi zito, haswa kijana Derrick ndiye alieonekana kumpenda msichana huyo kupita kiasi.

    Penzi lao halikujificha hadi Baba na Mama wa familia hiyo waliliona jambo hilo. Haikupita siku nyingi msichana huyo alikuwa tayari ni mjamzito, kile kitendo kiliwaumiza wanafamilia wale maana maisha ya kijana Derrick yalikuwa mabaya sana kiasi kwamba hata chakula kwake ilikuwa ni tatizo kwake"



    Kila aliekuwa pale alionekana kutokwa na machozi kwa yale aliekuwa akiyasema Mjomba.



    "Kwakuwa wale wanafamilia walikuwa wakimwamini Mungu, ilikuwa ngumu kumwamuru yule msichana kutoa ule ujauzito na walijua kufanya hivyo ni sawa na kuuwa. Familia ya yule msichana ilikuja juu kwa kuanza kuitupia lawama familia ile na kudai yale yaliotokea waliamua kuwafanyia kwakuwa wao ni maskini, yale maneno yalimwingia vilivyo na kumuumiza moyoni kwake kwa kuwa hakupenda kulaumiwa kwa kitu asicho kifahamu.

    Baada ya kuongea na ile familia aliahidi kumwangalia msichana huyo hadi pale atakapo jifungua na mtoto kuwa mkubwa.

    Waliporudi nyumbani walimkuta Derrick akiwa ameshakusanya kila kichokuwa chake na kutaka kuondoka katika familia hiyo bila sababu ya msingi. Derrick aliamini mapenzi yake na msichana huyo yatakuwa yameisha, kama alivyoamua ndivyo ilivyokuwa na Derrick aliondoka katika familia hiyo na kwenda kuanza maisha yake"



    "Huyo msichana alitwa nani? maana toka mwanzo sijasikia jina la huyo msichana?"



    Aliuliza mdogo wangu na kufanya Mjomba na watu wengine kubaki kimya huku wakimtiza Mjomba ili awape jibu. Lile swali lilimshtua Mjomba na kuonekana kuwa hakutarajia kukutana na swali kama lile, nilipomwangalia mjomba nilishangaa kuona anatokwa na machozi.



    Sikuwa nafahamu kilichokuwa kinamliza Mjomba na hiyo ni baada ya kuulizwa swali na mdogo wangu.

    "Kuhusu jina la huyo msichana mtalijua ila cha muhimu ni kuwa wavumilivu na wasikivu"

    Aliongea Mjomba kwa kigugumizi kilichoambatana na kwikwi ya kilio.



    "Dada yangu pamoja na Mume wake kama walivyokubaliana kumtunza msichana yule na kumpatia mahitaji yake ya msingi mpaka pale atakapo jifungua japo kunawakati msichana huyo alikuwa akimkumbuka sana kijana aliempenda kupita maelezo Derrick, kiukweli walimpenda na kumfanya kama mwanafamilia wa ile familia, ilifika wakati wageni wakija kwenye nyumba yao wakimkuta msichana huyo walidhani ni mtoto wa familia hiyo.

    Siku zilisonga miezi nayo ikapita hatimaye msichana yule alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume na kumwita John"



    Aliongea Mjomba na kunifanya nishtuke na kustaajabu kwa yale niliyo yasikia.



    "Inamaana Sophia sio mdogo wangu?"

    Nilijikuta nikitamka bila kutarajia nilihisi huenda naota kwa yale niliyokuwa nayasikia lakini haikuwa ndoto, kiukweli sikuwahi kuwaza kitu kama kile katika maisha yangu.



    "Baada ya yule msichana kujifungua mtoto wake na kumpa jina, Msichana yule alitoweka katika familia ile na kumtelekeza yule mtoto mdogo. Najua kile kitendo kilikuwa cha kinyama ila siwezi kumlaumu. Familia ile ilichukua jukumu la kumlea mtoto yule na kwakuwa Dada yangu alikuwa bado ananyonyesha hivyo ikawa rahisi kupatia maziwa bora, mtoto huyo akiwa na miaka mitatu kulitokea uvamizi katika ile nyumba pamoja na ofisini kwao na vilibiwa vitu vya muhimu vya serikali. Lile tukio lilisababisha Dada yangu pamoja na Mme wake kuonekana wazembe na waongo kwa kudanganya serikali kuwa vitu vya umma vimepotea kwa mazingira ya kutatanisha. Haikufahamika aliefanya tukio lile ila kwa kuwa Dada na Mume wake walikuwa na fedha za kuwatosha na kujikimu waliamua kuachana na mambo ya serikali na kuanza kuishi maisha ya kawaida kama walivyo raia wengine. Maisha yao yalikuwa mazuri sana na waliamua kufungua kampuni ya usindikaji ambayo iliwaingizia kipato kikubwa na kuwafanya waendelee kuwa na maisha mazuri zaidi na zaidi. Mtoto huyo alipofikisha miaka saba alianza shule, alikuwa ni mtoto mwenye uelewa mkubwa kiasi kwamba alimpita uwezo mtoto wa Dada yangu na ndiyo mwanzo wa Sophia kuanza kumwita John Kaka, japo Sophia alikuwa mkubwa kwake. John akiwa darasa la tano huku Sophia akiwa darasa la nne palitokea tukio kubwa na lakutisha pale nyumbani, kwani walivamia kwa awamu ya pili huku awamu hii wakiwa na lengo la kuondoa uhai wao na kuchukua mali zote walizokuwa nazo. Walifanikiwa kuchukua walicho_kihitaji na kuondoka bila kuwadhuru. Marehemu Dada yangu pamoja na Mumewe waliamua kuishi maisha ya hali ya kawaida kwa kuhofia siku moja wangepoteza uhai wao kwasababu ya fedha. Waliamini wataishi maisha mazuri bila kusumbuliwa na mtu yoyote. Ilipita miaka saba wakiwa wanaishi maisha ya kawaida huku wakijaribu kuwaleo watoto wao vizuri, lakini wale watu hawakuwa waacha waliendelea kuwafuatilia hatimae walimuuwa Dada yangu pamoja na Mme wake, hili tukio najua hata wewe una lifahamu na unamjua vizuri aliefanya haya?"

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliuliza mjomba nami nikatikisa kichwa kuashiria aliyokuwa anayasema yalikuwa ni yakweli.



    "Yote haya aliefanya ni Baba yako mzazi Derrick ambae wewe unamwita Baba mkubwa"



    Aliongea Mjomba kwa uchungu huku machozi yakimtiririka. Nilishtuka sana na kutaka kuanguka kwa yale niliyo yasikia.



    "Baba yangu ndiyo huyu muuwaji! Hahahaaaa nilianza kukuamini lakini sasa naona umekosa story kwakuwa umetushika masikio kwa muda mrefu ndio ukaamua kutudanganya kwa njia hiyo?"



    Niliongea kwa hasira huku nikimwangalia Mjomba kwa jicho la hasira, maana nilihisi amenitukana kwa maneno yake ya kuniambia Baba yangu ni muuwaji tena mtu alienitesa mpaka nikawa kama mkimbizi, leo hii isemekane kuwa Baba yangu ni jambo ambalo halikuniingia akilini.



    "Baba yangu ndiyo huyu muuwaji! Hahahaaaa nilianza kukuamini lakini sasa naona umekosa story kwakuwa umetushika masikio kwa muda mrefu ndio ukaamua kutudanganya kwa njia hiyo?"



    Niliongea kwa hasira huku nikimwangalia Mjomba kwa jicho la hasira, maana nilihisi amenitukana kwa maneno yake ya kuniambia Baba yangu ni muuwaji tena mtu alienitesa mpaka nikawa kama mkimbizi, leo hii isemekane kuwa Baba yangu ni jambo ambalo halikuniingia akilini.





    Hasira na jazba zilinijaa kwa yale aliyo niambia Mjomba, kiukweli katika maisha yangu hakuna mtu niekuwa namchukia kama Baba mkubwa. Naweza kusema baada ya shetani anaefuata ni Baba mkubwa, muonekano wake na alivyokuwa alikuwa hafananii na alichokuwa akikifanya.



    "John huwezi kupingana na ukweli maana ukweli haufichiki, hata hivyo Baba yako bado anakupenda sana lakini kitu kinacho muumiza na kumfanya asikufuate ni kwakuwa hakufahamu kwa sura ya ukubwani, yeye anakufahamu kwa sura ya utotoni maana kipindi Mama yako ameondoka aliondoka na picha zako, ila siwezi kujua walikutana au la ila nacho kifahamu ndicho hicho maana mimi unaeniona ni Spy au mpelelezi na muda sio mrefu Baba yako atakuwa akiyalipia makosa yake na maovu yake aliyo yafanya, nina ushahidi wa kutosha juu ya huyu mtu na nimeona ni vizuri kama ningekuambia ukweli. Kiukweli kabla ya Dada yangu na Mumewe hawajapoteza maisha walifanikiwa kuacha mali na mali hizo zilikabidhiwa kwenu na mrithi wa mali hizo ni wewe, kila kitu kipo chini yako na moja ya vitu hivyo ni Dada yako Sophia. Naweza kusema wewe ni mtoto mwenye bahati sana ila nakuomba endelea kumpenda Sophia na kumjali kama ilivyokuwa awali, najua ni ngumu kuamini nilichokwambia ila pengine hichi kinaweza kukufanya uamini ninayo yasema"



    Aliongea Mjomba kwa unyonge machozi yakiwa yanamtirika. Alinipatia karatasi lilokuwa limeambatanishwa na picha mbili, sikuwa na fahamu alikuwa anamaanisha nini kwa kunipatia vile vitu. Nilichukua lile karatasi na zile picha, nilianza kutizama picha zile na kunifanya nishtuke kwa nilichokiona.

    Picha zile zilikuwa za Baba na Mama wakiwa na Baba mkubwa huku Baba mkubwa kuonekana amevalia nguo za ulizi, nilipoangalia picha ya pili nilimuona Baba mkubwa akiwa ameketi kwenye sofa ya kifahari pembeni kukiwa na msichana mrembo.



    Nilipoziangalia zile picha nilianza kuhisi huenda aliyokuwa anayasema Mjomba yalikuwa ni yakweli, sikutamani yale maneno yawe ya ukweli na sikutaka kuamini kama inawezekana mimi nikawa mtoto wa Muuwaji. Nilimuomba Mungu kimoyo moyo nikiwa namuomba yale maneno yasiwe ya kweli, machozi yalianza kunitoka kwa kuanza kulaumu kuwa na Baba kama yule.

    Nilichukua lile karatasi na kuanza kulisoma huku mwandiko uliokuwa umeandika ujumbe ule nikiwa naufahamu ni wa Mama yangu. Niliyo ya soma kwenye lile karatasi yalinifanya machozi kuzidi kunitoka kwa wingi, maana kile alichokisema Mjomba ndicho kilichoandikwa kwenye lile karatasi.



    Kiukweli nilihisi kuchanganyikiwa kwa taarifa zile, niliona kama nachezewa akili yangu maana kitu kama kile sikukiruhusu kuingia kwenye akili yangu. Watu wote walikuwa wameinamisha vichwa vyao chini na walionekana kushangazwa na zile taarifa. Nilipo muangalia mdogo wangu nilimuona akiwa anatokwa na machozi, roho yangu iliniuma sana kuwa na Baba kama yule.

    Wakati tukiwa pale simu ya Mjomba ilita

    alipoipokea alionekana kuwa kama mtu aliepata za kushitusha, nilizidi kushangaa maana mjomba alipata wasiwasi mkubwa na hofu, watu wote tulipigwa na bumbuwazi ni baada ya mjomba kuanguka chini mzima mzima huku simu yake ikiwa bado ipo hewani.



    Tulianza kumpepea mjomba huku Mjomba Denis akichukua ile simu ili kujua ni taarifa gani alizozipata mjomba. Mjomba alipochukua ile simu na kuiweka kwenye sikio lake ili kupata kusikia kilichokuwa kinaongewa, nilishangaa simu aliokuwa ameishika mjomba inaanguka chini. Nilishangaa sana kwa kile nilichokiona maana mjomba nae alianguka chini na kubaki kimya kama mtu alie lala.



    Nilishtuka sana na kuhisi walikuwa wananitania, maana sikuwahi kuona kitu kama kile cha mtu kupokea simu na kuanguka chini bila sababu za msingi. Nilipoona hali kama hile niliamua kuchukua ile simu ili nisikilize kile` kilichokuwa kinakungumziwa, na kuwafanya wakina Mjomba kuanguka chini na kupoteza fahamu. Lakini nilipoichikua ile simu sikufanikiwa kusikia chochote wala kuona chochote , nilishangaa na hata nilipoangalia simu zilizopigwa hivi karibuni, sikufanikiwa kuona namba yoyote iliopigwa muda mfupi ulio pita.



    Niligundua ule ulikuwa mchezo kwa kile kilichokuwa kinaendelea, niliamua kuiweka simu juu ya meza ila kabla sijaifikisha mezani nilisikikia ile simu inaita, bila kuchelewa niliiangalia nani aliekuwa anapiga ili ikiwezekana kuipokea kabisa. Kabla hata sijaangaza ninani aliekuwa anapiga nilishtukia simu inachukuliwa kwa kasi, na nilipo angalia ninani nilikuta ni mjomba ndiye alie ichukua.

    Sikuwa nafahamu nini kinaendelea maana muda siyo mrefu walijifanya wame poteza fahamu, baada ya muda lirejea maana alipo chukua ile simu alitoka nayo nje.



    Aliporudi alituaga na kusema atarejea muda sio mrefu. Kiukweli mimi bado nilikuwa na mawazo mengi juu ya maneno noliokuwa nimeambiwa kuwa Baba mkubwa ndiye Baba yangu. Mimi pamoja na Mdogo wangu tulirejea nyumbani ambapo tuliwaacha Naomi pamoja na Baba yake, tulipofika nyumbani tulikuta hali ya pale nyumbani imebadilika sana, tofauti na tukipo paacha jana. Mlango wa kuingilia ulikuwa wazi, tulipofika ndani tulishangaa kukuta damu nyingi zikiwa zime tapakaa sebleni, kile kitendo kilianza kunipa wasiwasi na hofu maana damu zile zilikuwa ni nyingi sana.



    Tulianza kuwaita Naomi pamoja na Baba yake bila mafanikio, tuliogopa kuingia ndani kwa kwa hofu tuliokuwa nayo. Wakati tukiwa pale sebleni tukiwa hatujui nini cha kufanya, tulishangaa wanaingia watu walio valia nguo za polisi. Walipoingia walituambia tupo chini ya ulinzi kwa kosa la kuuwa kwa kukusudia, tulishangaa sana kwa zile taarifa kitu ambacho kilinishangaza ni kuona wale polisi wakiwa wanayatambua majina yetu vizuri.



    Nilitamani kukimbia lakini wale polisi walikuwa ni wengi hivyo ikawa ngumu kuwatoka, ukiangalia nisingeweza kumwacha mdogo wangu nyuma. Tulichukuliwa na kupelekwa kituoni bila kuambiwa chochote, tuliingiza kwenye chumba kimoja mimi pamoja na mdogo wangu na kufungiwa. Tulikaa pale chumbani hadi ilipofika saa kumi ndipo askari mmoja alipokuja kututoa na katupeleka ofisini kwa mkuu wake.



    Tulipofika ofisini tuliambiwa tuketi kwaajili ya kumsubiri mkuu wa afike. Hatukuchukua muda mrefu aliingia mkuu wa kituo hicho na Yule alietuleta alitoka na kutuacha na mkuu wake. Nilishtuka baada ya kumuona Yule askari, nilimwangalia mara mbili mbili ili kujua kama nimemfananisha, kiukweli sikuwa nimemfananisha alikuwa ndiye. Alikuwa ni Yule afande aliekuwa anasimamia kesi ya mauaji ya wazazi wangu nay eye ndiye aliefuta kesi ya wazazi wangu.



    “Ndiyo vijana nasikia nyie ni wauwaji wa kimya kimya na taarifa zenu tumezipata, mnaweza kuniambia ni nani anaewapa kazi hizo, maana mimi najua nyie hamuwezi kufanya kazi bila sababu za msingi”

    Aliuliza Yule Afande na kunifanya nipatwe na hasira na kuanza kumwangalia kwa jicho la hasira.

    “Tena wewe wa kiume ndiyo lijambazi likubwa liangalie linavyo angalia, wewe unafikiri unaweza kufanya nini hapo ulipo, hiki ni kituo cha polisi ukiingia ukitoka ni mpya unakuwa kama mtu aliezaliwa kwa mara ya pili”



    Aliongea Yule afande huku akijitamba kwa kututisha kwa maneno yake yaliojawa na jazba nyingi, hatukuwa na lakusema maana hatukuwa tunatambua chochote, mimi binafsi nilikuwa na hasira maana Yule afande ndiye mtu aliekuwa anashiriki sisi kuteseka na kupata mateso makubwa katika maisha yetu.

    “Wewe unavyosema sisi ni wauwaji na kaka sisi ni wauwaji tuonyeshe kithibitisho au unaongea kwa vile una mdomo wa kuongea, we unafikiri hii nchi ni ya Baba yako. Ulinitesa nikiwa mdogo kipindi wazazi wangu wameuawa ukanipa kesi mimi, ulifikiri kila kitu kinajificha na ninafahamu wewe unashirikiana Baba mkubwa Derrick na nyie ndiyo mliouwa wazazi wangu”



    Nilionge kwa hasira bila kuju ni makosa kumwambia Afande maneno kama yale. Yule afande aliniangali kwa hasira kiasi kwamba nilianza kuogopa, nilihisi nimefanya makosa japo ilikuwa kweli ila sikuwa na uthibitisho wowote. Yule afande alinyanyuka huku akionekana kukasirishwa nayale maneno alianza kunipiga vibao, wakati ananipiga mlango ulifunguliwa nilipogeuka kuangalia ni nani aliekuwa ameingia, nilishangaa kukuta ni Baba mkubwa.



    Nilishtuka sana baada ya kumuona Baba mkubwa akiwa pale kituoni, kiukweli hakuna mtu niliekuwa namuogopa kama Baba mkubwa. Nilihisi ndiyo mwisho wa maisha yangu maana ni kwakipindi kirefu Baba alikuwa akitaka kutuwa lakini kwa huruma za mwenyezi Mungu alituepusha na matukio mabaya. Hali ya hewa pale ndani nilihisi imebadilika ni baada ya Baba mkubwa kuingia, nilipoangalia upande wa pili nilimuona mjomba akiwa ameshikwa na vijana wawili huku akiwa anatokwa na damu nyingi mdomoni na sehemu za kichwani.



    "Hivi nyie mbwa wadogo wadogo mlifikiri mtanichezea mchezo ambao mimi siufahamu, huyu mnaemuona hapa nimtu mwenye bahati kubwa sana. Naweza kusema pengine ana roho za paka kwakuwa amepata mateso makali lakini bado yupo tu. Afande naomba usiumize mikono yako kwa kupiga wapumbavu kama hawa, hawa ni wauwaji tu hawastahili kupigwa makof. Hawa adhabu yao ni kifo tu maana alieua kwa upanga atakufa kwa upanga"



    Aliongea Baba mkubwa kwa sauti ya kukejeli huku akionekana kushirikiana na yule Afande, wakati huo nilikuwa nikimwangalia Mjomba jinsi alivyo vimba kwa kuonekana amepigwa sana na alionekana kuwa na maumivu makali kiasi kwamba hakuwa na uwezo wa kunyanyuka au kusogea. Hasira zilinijaa lakini hazikusaidia kitu maana mikoni mwangu nilikuwa na pingu, nilimwangalia Baba mkubwa kwa hasira huku nikiwa nakumbuka maneno ya Mjomba

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Huyo unaemuita muuwaji ndiye Baba yako na ndiye alie wauwa wazazi wako walezi ambae ni pamoja na Dada yangu, mimi unavyo niona ni mpelelezi na muda siyo mrefu atalipia kwa maovu aliyo yatenda"

    Kiukweli yale maneno yalikuwa ni kama fimbo kwangu, maana kila wakati nilipokuwa nikiyakumbuka yalikuwa yakiniumiza na kunikosesha amani. Baada ya Baba mkubwa kumwambia yule Afande asiangaike kupigana sisi maana alikuwa anaumiza mikono yake, yule Afande alituacha kurudi kwenye kiti chake na kuanzamaswali.





    Maswali ambayo yalikuwa magumu kuyajibu maana kila tulichokuwa tunaulizwa kilikuwa kigeni kwetu, kila kilichokuwa kinaulizwa kilikuwa kikiandikwa kwenye karatasi. Baada ya maswali tulionekana tuna hatia maana hatukuwa tumejibu chochote zaidi ya kuitikia kila kitu ni kutokana na hofu ya kuuwawa na Baba mkubwa. Wakati tunarudishwa ndani tulitakiwa kuacha vitu vyote pale ofisini, wakati natoa vitu vyangu zile picha pamoja na lile karatasi kumbe wakati naondoka kule kwa mjomba nilichukua na kuweka mfukoni na nilivyokamatwa zilikuwamo mfukoni.



    Nilitamani kuvificha lakini sikupata nafasi ya kuficha maana nilikuwa nimesha viweka juu ya meza pale ofisini, sikutamani Baba mkubwa kutambua chochote juu ya maisha yangu. Wakati naweka vile vitu mezani Baba mkubwa yeye alikuwa wakwanza kuangalia vile vitu akihisi huenda tulikuwa na mipango juu yake.

    Sikuweza kumzuia kuangalia ilibidi kuwa mpole maana sikuwa na uwezo wowote, nilibaki nikiwa namwangalia Baba mkubwa kwa vile kila kitu kilikuwa kimeandikwa kwenye lile karatasi ikiambatana na picha mbili.



    Baada ya kuangalia zile picha nilimuona Baba mkubwa anarudi kwenye kiti taratibu na kuonekana kupoteza tabasamu, muonekano wa Baba mkubwa ulibadilika hata yule Afande alikuwa akimshangaa sana. Baada ya kuangalia zile picha aliamua kufungua lile karatasi na kuanza kulisoma, alipokuwa anasoma tulianza kuona machozi yanaanza kumtoka ni baada ya kusoma lile karatasi.



    Kiukweli nilishangaa kumuona Baba mkubwa analia ama kutokwa na machozi ila siku ile ilikuwa tofauti, alikuwa akinitizama kwa muda mrefu huku machozi yakimtoka. Nilijua huenda nilichoambiwa ni kweli na ilionyesha Baba mkubwa amejua ukweli yakuwa mimi ni mwanae.

    Yule afande alibaki ameduwaa na kuzidi kushangaa kwa kile alichokuwa anakiona, ilionyesha ni kwa mara ya kwanza yule Afande kumuona Baba mkubwa akiwa anatokwa na machozi. Yule Afande alimwita afande mwingine ili atupeleke kwenye chumba cha waalifu, wale afande walituchukua na kutupeleka ndani ambako kulikuwa na hali ya hewa tofauti mle ndani ya kile chumba.



    Hazikupita hata dakika mbili tulishangaa kumuona Baba mkubwa akiwa mbele ya chumba tulichokuwa tumefungiwa, macho yake yakiwa yamebadilika na kuwa ya rangi nyekundu, hakuwa na lakuongea zaidi ya kulia. Akiwa amesimama huku akiwa anatokwa na machozi walikuja Afande wawili na kutufungulia na kuturudisha ofisini, tulipofika ofisini tulimkuta mjomba Denis akiwa anatungoja na alionekana kuwa na hasira kwa kile kilichotokea.



    Bila kupoteza muda Mjomba alituchukua na kutoka nje ya kile kituo, wakati tunatoka tulisikia sauti ikiita, nilipogeuka nilikuta ni Baba mkubwa akiwa nyuma yetu huku mkononi mwake akiwa na zile picha na lile karatasi. Kiukweli nilikuwa na hasira sana sikutaka hata kumuona, nilijifanya kama sijasikia na kuanza kupiga hatua za haraka haraka.



    Kabla sijafika kwenye gari Baba mkubwa alikuwa tayari alishafika kitu ambacho kilinishangaza sana, sikuwahi kufikiria hata siku kama ipo siku Baba angekuja kunifuata akiwa katika hali ile. mjomba alichofanya alifungua mlango na kutuambia tuingie ndani ya gari na kisha kuondoka.



    Nilimwangalia Baba mkubwa kupitia kioo cha dirisha la gari na kumuona akiwa anajipiga piga na kulia kama mtoto mdogo, sikuweza kumuonea huruma hata kidogo, kwa yale alio yafanya hakustahili kupata msamaha. Nilijua ukweli alio upata ulimuumiza maana alioyo yafanya kwa mwanae wa damu na kumfanya ateseke na kuchukia uwepo wake hapa Duniani.



    Hasira nilizokuwa nazo zilikuwa ni nyingi kiasi kwamba hadi mwili wangu ukawa unatetemeka. tulipofika nyumbani niliingia chumbani kwangu nikiwa na hasira, nilipofika ndani nishangaa kukuta chumba hakuna kitu chochote zaidi ya kitanda. Nilitoka na kumfuata mjomba ili kumuuliza nini kilichotokea.



    Nilipotoka nilimkuta mjomba akiwa anaongea na simu, sikufahamu alikuwa anaongea na nani, baada ya kumaliza kuongea na simu nilimuuliza juu ya kile nilichokikuta chumbani kwangu, alinijibu na kuniambia polosi walifika pale nyumbani na kuchukua kila kitu chako na kusema wanafanya uchunguzi juu ya kifo cha Naomi pamoja na Baba yake.



    Yale maneno ya mjomba yalinifanya nishtuke na kushangaa kwa kile alichosema Mjomba.

    "Na mjomba yupo wapi maana nilimuona kituoni akiwa kwenye hali mbaya?".



    Nilimuuliza Mjomba Denis ili kufahamu hali ya mjomba, lakini jibu la mjomba lili nikosesha furaha na kunifanya nikose nguvu, na kunza kuona kiza kizito hatimaye sikufahamu nini kiliendelea.

    Nilipokuja kushtuka nilijikuta nikiwa nipo kwenye chumba ambacho kwa haraka haraka sikutambua palikuwa ni wapi, nilipoangalia pembeni nilimuona baba mkubwa akiwa amekaa kwenye kiti akiwa anaonekana kuwa na mawazo mengi. Kwenye akili yangu sikufikiria kama ipo siku ningekuja kumuita Baba mkubwa “Baba” Nilitokea kumchukia sana bila kufahamu alifanya yale kwasababu gani.



    Moyo wangu ulikuwa ukikosa amani pale neon la Baba mkubwa ni Baba yangu, kiukweli nilikuwa na mawazo mengi. Baba mkubwa aliponiona nimeamka alisogea hadi pale kitandani na kuanza kuniuliza naendeleaje, sikuwa na jibu la kumpa zaidi ya kumwangalia kwa hasira.



    Kiukweli nilikuwa nikikumbuka zile taarifa alizoniambia mjomba denis kuwa mjomba amepoteza maisha kwa kupigwa na polisi na alie fanya yote hayo nilijua iwe isiwe alikuwa ni Baba mkubwa, maana kipindi tukiwa pale kituo cha polisi yeye ndiye alionekana kumkejeli mjomba.



    Hasira zilinijaa mara dufu, nilitamani kumrukia na kumchana chana vipande vipande Baba mkubwa, lakini uwezo huo sikuwa nao. Niliendelea kuwa kimya huku nikizidi kumwangalia vibaya Baba mkubwa.

    “John mwanangu naomba unisamehe maana haya yote yaliyo tokea hayak…….”



    Kabla hajamaliza kuonge mlango ulifunguliwa wakaingia Mjomba pamoja na Mdogo wangu, kitu ambacho kilinishangaza ni pale mjomba alipoingia na kumsalimia Baba mkubwa huku wakiwa wenye kujawa na tabasamu, kile kitendo kilinipa maswali mengi.



    Maswali ambayo yalikuwa magumu kupata jibu, nilimwangalia mjomba na mdogo wangu walivyo kuwa wanaongea na Baba mkubwa, nilipatwa na hasira maana Yule waliokuwa wanaongea nae ni kama shetani. Hasira niliokuwa nayo ikapelekea kunzisha vurugu na kusababisha uaribifu wa vifaa vilivyokuwa mle ndani. Kwa kiasi kikubwa nilikuwa nimeharibu vitu vingi kiasi kwamba nilianza kujiona mkosaji.



    Dokta alipofika na kukuta hali yangu imerudi kam hapo awali, aliongea na mjomba ili ikiwezakana niruhusiwe, niliruhusiwa na kutoka pale hospitali na kuelekea nyumbani. Kitendo cha Baba mkubwa kuongozana na mimi huku akizidi kuongea na Mdogo wangu bila uoga wowote kilinipa hasira, na kukosa amani na kuanza kuhisi mambo mabaya.



    Hakuna hata siku moja ambayo niliwaza au kufikiria kuwa na baba mkubwa na kufungua mdomo wangu kuongea nae.

    Hasira nilizokuwa nazo dhidi ya Baba mkubwa zilikuwa ni zaidi ya samba aliekosa mawindo, lakini niliamua kuwa mpole kwa kuwa hasira zile ndizo zilizonifanya kuaribu vitu pale Hospital.



    Tulipofika nyumbani Baba mkubwa alinifuata ili kutaka kuongea na mimi,lakini moyoni nilihisi kama Napata dhambi kukaa na mtu kama Yule. Mtu alie uwa Baba na Mama yangu mlezi na kunifanya niishi maisha yalikuwa na mateso ndani yake, sikutamani kukumbuka mateso nilioyapata kupitia Baba mkubwa ambae ayafanya kwa motto wake wa damu bila kumonea huruma, kingine kilichokuwa kinaniumiza ni kifo cha mjomba, mtu aliejitoa na kunilinda kwa kipindi kirefu bila mimi kujua.



    Niliamini katika maisha yangu sikuwa na ndugu zaidi ya mdogo wangu pamoja na mjomba Denis.

    “John mwanangu naomba punguza hasira ninajua ni jinsi gani unavyo umia ila tambua haya yote nilifanya kwaajili yako”

    Aliongea Baba mkubwa kitu ambacho kilinifanya nishangae na kubaki mdomo wazi.





    Yale maneno ya Baba mkubwa yalinishangaza na kunifanya ni cheke kwa sauti.

    “Umefanya kwaajili yangu? Kwahiyo unataka kuniambia ulikuwa unauwa kwaajili yangu, ukataka kuniuwa na mimi nayo ni kwasababu yangu. Leo naona Mungu amenishukia na kunifunika na mbawa zake, maana sikuwahi kuwaza kama ipo siku ningekuja kuongea na mtu kama wewe pengine leo ndiyo umekuja kuchukua roho yangu, kwakuwa wewe ninakufananisha na Izrael mtoa roho japo izrael hana roho mbaya kama uliokuwa nayo wewe”



    Niliongea kwa kumaanisha huku nikiwa namwangalia Baba mkubwa kwa hasira. Hakuweza kunijibu chochote zaidi ya kubaki kimya na kuendelea kunitazama kwa macho ya huzuni. Kimya kilitawala nikajua hakuwa na chochote cha kuniambia nikaamua kutoka nje maana nilihisi pengine alikuja kunipima akili. Wakati natoka kuelekea nje kabla sijafungua mlango nilishangaa mlango unafunguliwa, nilimwangalia ni nani aliekuwa amefungua nilishituka sana na kutaka kukimbia.



    Alikuwa ni mjomba ambae nilipata taarifa zake kawa amepoteza maisha baada ya kupigwa sana na askari na hata hivyo mimi mwenyewe nilishuhudia mjomba akiwa kwenye ali mbaya. Ndugu msomaji nilishangaa na kustaajabu kwa kile nilichokiona, siona kovu lolote kutoka kwa Mjomba, nilihisi kama macho yangu hayaoni vizuri lakini hata nilipo fikicha macho yangu ukweli ulibaki pale pale yakuwa Yule alikuwa ni Mjomba.



    Sikuweza kuamini kwa kile nilichokiona, mjomba aliponiona alinitizama na kuanza kucheka.

    Alipofika aliketi kwenye sofa na kukaa kimya akiwa kama anamsubiri mtu, nilishindwa kuelewa nini kilikuwa kinaendelea. Haikupita muda mlango ukafunguliwa. Nilipogeuka kuangalia ninan nilishangaa kukuta ni Yule Afande tuliekuwa nae kule kituo cha polisi, na yeye alipofika alitafuta nafasi na kukaa kimya kama alivyofanya Mjomba.



    Nilizidi kushangaa na kujiuliza maswali mengi kwa wakati mmoja juu ya Yule Afande. Nilikumbuka jinsi alivyonipiga na kunitamkia maneno mabaya yakuwa mimi ni muuwaji kwa amri ya Baba mkubwa.

    “Wewe huwezi kuwa Baba yangu kamwe, ni Baba gani anawezakumtafuta mwanae wa kumzaa ili amuuwe bila hatia, mtu usiekuwa na hata chembe ya ubinadamu. Kama haya yote umefanya kwa Mwanao, je kwa mtu usiemfahamu ungefanya kitu gani?”.



    Niliongea kwa uchungu huku machozi yakiwa yananitoka, nilikuwa ni mwenye kujawa na majonzi na huzuni, ilifika wakati nikawa najihisi sina thamani hapa Duniani. Kila nilipokuwa nawaona watu ambae walinitendea ubaya na kuniona mimi kama mnyama, wakati nazidi kuwaza mambo yalio nikuta na kunifanya nisitamani kuishi nilishangaa kuona anaingia mtu ambae sikutegemea katika maisha yangu kama ningekuja kumuona tena au kupata kusikia sauti yake.



    Nilizidi kushangaa na kujiuliza maswali mengi kwa wakati mmoja juu ya Yule Afande. Nilikumbuka jinsi alivyonipiga na kunitamkia maneno mabaya yakuwa mimi ni muuwaji kwa amri ya Baba mkubwa.

    “Wewe huwezi kuwa Baba yangu kamwe, ni Baba gani anawezakumtafuta mwanae wa kumzaa ili amuuwe bila hatia, mtu usiekuwa na hata chembe ya ubinadamu. Kama haya yote umefanya kwa Mwanao, je kwa mtu usiemfahamu ungefanya kitu gani?”.



    Niliongea kwa uchungu huku machozi yakiwa yananitoka, nilikuwa ni mwenye kujawa na majonzi na huzuni, ilifika wakati nikawa najihisi sina thamani hapa Duniani. Kila nilipokuwa nawaona watu ambae walinitendea ubaya na kuniona mimi kama mnyama, wakati nazidi kuwaza mambo yalio nikuta na kunifanya nisitamani kuishi nilishangaa kuona anaingia mtu ambae sikutegemea katika maisha yangu kama ningekuja kumuona tena au kupata kusikia sauti yake



    ENDELEA......................

    Nilishangaa sana kimuona Mama, mtu ambae alikuwa amepoteza maisha kwa kipindi kirefu kilicho pita. Ndugu msomaji nilistaajabu kuona kitu kama kile, nilihisi nipo kwenye ndoto, lakini haikuwa ndoto ilikuwa ni ukweli mtupu.

    Nilishindwa kuzuia macho yangu kuona kitu kama kile. Hata ingekuwa ni wewe unae soma huu mkasa usingeweza kujizuia kushangaa ama kuamini kitu kama kile. Nilimtizama mtu yule aliekuwa amefanana na Mama yangu, kuanzia sura na kila kitu kilifanana na Mama, ikuweza kuamini lile jambo.



    Nilishindwa kuongea lolote na kubaki nikiwa nimeduwaa huku kichwa changu kikiwa kimetawaliwa na mawazo mengi. Nilizidi kushangaa maana sikuwahi kuwaza kitu kama kile au kufikiria kama ingetokea jambo kama lililo tokea leo. Nae alipofika alinipita pale mlangoni na kwenda kukaa kwenye sofa na kutulia kama walivyofanya wakina mjomba.



    Nilihisi kuchanganyikiwa kwa kole nilichokiona mbele yangu, nilianza kuona kama akili yangu inaanza kuruka. Nilibaki nashangaa bila kujua nini kilikuwa kinaendelea, nilijua kuna jambo lilikuwa linaendelea ambalo mimi sikuwa nalifahamu. Niliamua kutoka nje maana pale ndani kila mtu alikuwa kimya kukiwa kama kuna jambo la muhimu lililotakiwa kuzungumziwa pale. Kwa wakati wote macho yangu yalikuwa yakimtizama yule mtu alifanana na mama.



    Nilipofungua mlango wa kutokea nje nilishtuka na kuanza kurudi nyume nyume. Nilitamani kukimbia lakini nilihisi nguvu kuniishia, nilianza kuhisi kizungu zungu huku macho yangu yakiwa mazito kutazama ama kuangaza kilicho mbele yangu, hali ile iliendelea kunishambulia huku nikiwa najitahidi kumwangalia yule nilie muona kwa makini nikiwa nahisi nimemfananisha. Hatimaye nilipoteza fahamu pale pale.



    Nilipokuja kushtuka nilishangaa sana kwa kile nilichokiona, nilijikuta nikiwa nimelala kwenye moja ya sofa yaliokuwa pale ndani. Nilipoangaza huku na kule nilifanikiwa kuona sura za watu ambao siku waingiza akilini mwangu. Sura nilizokutana nazo zilinipa wakati mgumu kufafanua kilichokuwa kinaendelea.



    Baba, Mama na watu wengine ambao walipoteza maisha muda mrefu uliopita wote walikuwa pale, niliona kama nipo kwenye ndoto ikanibidi kuamka pale kwenye sofa na kuangalia vizuri wale watu. Kiukweli nilistaajabu kwa kile nilichokiona maana walikuwa ni wale wale niliokuwa nawafahamu.

    Nilizidi kuwatizama mara mbili mbili ilikupata uhakika kama niwale, jibu lilikuja ni lile lile walikuwa ni wao.



    Nilipozidi kuangaza angaza nilifanikiwa kumuona mtu ambae nilimuona kwenye zile picha nilizokuwa nimepewa na mjomba na kuambiwa ni Mama yangu, nilishangaa sana sikuwa nafahamu nini kinaendelea zaidi ya kubaki nashangaa huku nikiwa nazidi kuchanganyikiwa. Hakikuwa ni kitu cha kuamini, haikuniingia akilini kwa watu waliopoteza maisha kuoneka tena Duniani wakiwa wanaishi.



    Watu wote walikuwa wakinitizama, kila upande niliokuwa nageuka nilikutana na macho yakinitizama. Sikufahamu ninikilitokea hapo kabla hadi nikawa pale nilipokua na sikujua wale watu wamefika pale muda gani.

    “John mwanangu naomba unisamehe”

    Nilisikia sauti, nilipogeuka nilikuta ni yule msichana ambae nilimuona kwenye picha, nilishindwa kuelewa alikuwa ananiomba samahani kwa kosa gani.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilibaki namwangalia bila kusema lolote maana sikuwa namfahamu zaidi ya kumuona kwenye picha, na kile alichokuwa ananiambia kilikuwa ni kigeni masikioni mwangu. Kiukweli nilikuwa nimechanganyikiwa kwa kile nilichokuwa nakiona mbele yangu.

    Watu wote walikuwa wakinitizama, kila upande niliokuwa nageuka nilikutana na macho yakinitizama. Sikufahamu ninikilitokea hapo kabla hadi nikawa pale nilipokua na sikujua wale watu wamefika pale muda gani.



    “John mwanangu naomba unisamehe”

    Nilisikia sauti, nilipogeuka nilikuta ni yule msichana ambae nilimuona kwenye picha, nilishindwa kuelewa alikuwa ananiomba samahani kwa kosa gani.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog