Search This Blog

Friday, November 18, 2022

CHUNGA SAANA LAAZIZI WANGU - 3

 





Simulizi : Chunga Saana Laazizi Wangu
Sehemu Ya Tatu (3)




Maisha yalizidi kuaonga mbele.Mahusiano yao yalizidi kupamba moto Zaidi na hayakuishia tu kwenye mahusiani ya kimapenzi,bali hata katika masomo yao walishirikiana kwa pamoja.Walikuwa wakikutana jioni kwenye majadiliani ya kundi waliloliandaa la takribani wanafunzi watano.Tuntu alikuwa na rafiki yake mmoja aliyeitwa Said Mipawa pia Salma alikuwa na rafiki zake wawili.Walikuwa wakikutana maeneo ya chuo kikuu cha Muhimbili na kuanza majadiliano yao katika mosomo ya biashara na mengine.

Wakati wa majadiliano walikuwa hawana masihara.Waliendesha midala yao bila ya kuingiza masihara.Baada mijadala yao ndipo mambo mengine yalifuatia.Siku moja baada ya majadiliano,Salma na Tuntu walishirikiana njia kuelekea kituoni.

“Jumamosi naomba tutoke out.Unasemaje?”Tuntu alimuuliza Salma wakati wakiwa njiani.

“Sina pakwenda Zaidi ya kufua na kufanya shughuli ndogondogo asubuhi,so tutatoka.”

“Sawa nataka twende sehemu moja amazing”Tuntu aliongea huku akitabasamu.Walikubaliana na walipofika kituoni kila mmoja alichukua gari lake na hapo waliachana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Jumamosi ilifika.Ilikuwa ni mida ya saa tatu asubuhi walielekea maeneo ya Mlimani city.Baada ya kufika,waliimgia upande wa mavazi ya kike ambapo Salma alichagua mavazi mbalimbali aliyoyapenda.Iligharimu kiashi cha shilingi laki tatu.

Tuntu alijali sana muonekano wake hivyo hakuhitaji mchumba wake awe katika hali isiyovutia.Pia alijitoa kwa moyo wake na alikuwa tayari kupoteza gharama yoyote kwa ajili ya Salma.Baada ya kutoka Mlimani city,walielekea maeneo ya Sinza mapambano.

Lengo la kumpeleka huko,ilikuwa ni kumuonesha kwanini aliweza kutumia pesa yake kumlipia ada ya mitihani pamoja na kugharamia mavazi hayo.Tuntu alikuwa na akili ya kutafuta pesa.Alifungua vituo vya kuchezesha gemu maeneo hayo ya Sinza.Alikuwa na vituo vinne kwenye mitaa tofauti.Aliwaweka vijana waaminifu ambao walikuwa wakisimamia vituo hivyo kwa makini.

Katika kila kituo kulikuwa na tv tatu.Kutokana na kuchangamka kwa eneo la Sinza,kila kituo kilikuwa kikiingiza elfu kumi na tano mpaka elfu ishirini kwa siku hivyo ilikuwa ikipatikana elfu themanini kwa siku.Walielewana wawe wanampatia elfu hamsini kwa siku halafu wao walibaki na shilingi elfu therathini au zaidi kama itazidi elfu themanini.

“Hongera sana baby!”Salma alimsifu kwa ubunifu wake wa kusaka pesa.

“Asante sana mpenzi.Aaah! Kuna kitu ambacho napenda kukumbusha.Naomba usije ukawaza kunipenda kwa sababu ya uchumi nilionao.Ila nipende kama nilivyo.Umeelewa?”Tuntu aliongea kwa hisia sana.

“Usijali.haya ni ya kupita tu,nakupenda sana!”Salma aliongea kwa kumaanisha alichokuwa akikisema.Salma alikuwa na mapenzi ya dhati kwa Tuntu.

Baada ya kumuelekeza baadhi ya vitega uchumi,ilibidi waondoke nyumbani.Tuntu alimwita dereva wa Bajaji ili ampeleke Salma nyumbani kwao Magomeni Mikumi.Alimpatia Salma kiasi cha shilingi elfu kumi na tano kisha alimpa na dereva pesa yake ya ujira na safari ilianza.

Katika kipindi chote hicho cha mahusiano yao,hakuna aliyewahi kumgusia mwenzake suala la kufanya mapenzi.Tuntu hakuwa na nia ya kumchezea msichana huyo aliyekuwa moyoni mwake.Bali alihitaji kufanya naye tendo hilo mpaka pale atakapokuwa mke wake halali kwa mujibu wa sharia ya dini yake ya kiislamu.Kwa upande wa Salma yeye hakuwa na pingamizi lolote.Chochote ambacho Tuntu angetaka,yeye alikuwa radhi kukifanya hivyo alikuwa ni bendera kufuata upepo.

Maisha yalisonga mbele huku ikiwa ni kawaida yao kuonana kila siku kwenye majadiliano ya masomo yao.Siku moja Salma alimkera Tuntu na ndiyo siku alimfahamu Tuntu ni mtu gani.Baada ya kumaliza majadiliano wakiwa wanataka kuondoka,Salma alibaki na Tuntu huku wenzao wakitawanyika na kurudi nyumbani kwao.

Walipokuwa wamebaki wenyewe tu,Salma aliaga na kuelekea msalani.Kutokana na shughuli zake za kiuongozi,mara nyingi Salma alikuwa akija na simu yake shuleni ili atakapotaka kuwasiliana na viongozi wenzake wa UN wilaya ya Ilala aitumie.Akiwa anaelekea msalani,aliiacha simu yake ikiwa mikononi mwa Tuntu.

Ghafla ujumbe mfupi uliingia.Tuntu aliusoma ujumbe huo uliokuwa unasema “Salma! Hivi ni lini utanipa jibu langu..?Nakupenda sana.”Tuntu alipandwa na hasira kali sana.Alijiuliza maswali na asipate majibu.

“Hivi kweli nitakuwa nagharamia wakati wenzangu wanafaidi…? Huyu kweli hana mwingine halafu mimi ananichuna tu..? Natakiwa kuwa makini…!”Kichwa kiliwanga siku hiyo.Furaha ilitoweka usoni mwake.Akiwa anaendelea kuwaza na kuwazua,Salma nae aliwasili.

Salma aligundua tofauti kwenye uso wa Tuntu.Alimshika begani na kumpapasa ili amuulize kulikoni.Tuntu aliuondoa mkono wa Salma lakini Salma alijaribu tena kuurudisha,Tuntu aliuondoa kwa jazba kidogo.

“What wrong Tuntu..!?”Salma aliuliza kwa mshangao uliochanganyika na huzuni kidogo.

“Salma naomba usinifiche chochote.Hivi una wapenzi wangapi ukiachana na mimi!?” Tuntu aliuliza kwa hasira.

Salma alishtuka kidogo moyoni. “Tu..tun..Tuntu!? Ina maana umeanza kutoniamini? Ok..Sina mwengine zaidi yako wewe.Na kama umegundua lolote labda uniambie ili nijue.”Salma aliongea huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio.

“Huyo jamaa uliyemsevu J.G ni nani na ameipataje namba yako!?” Tuntu alimuuliza huku akimuangalia bila ya kupepesa macho. “Salma kwa hali hii inaonesha kwamba kama nimemgundua huyo basi kuna wengine wengi ambao sijawajua,si ndiyo..!?”Tuntu aliwaka sana.

“Si..sii.Sikiliza nikwambie baby..!

“Nani baby wako..!Nani baby wako nasemaa..!”Tuntu alimuwasha kibao shavuni.Ilikuwa ni mida ya saa kumi na mbili ikielekea saa moja jioni giza lilikuwa limekwisha tanda huku taa zikuchukua hatamu.

“Heee!Tun..tuntuuu..!”Salma alishangaa sana kumuona Tuntu katika hali hiyo maana hakutegemea.Alilishika shavu lake kuugulia maamuvu.Alitokwa na machozi huku kwikwi za kilio zikisikika kwa mbali kutokana na kujizui asilie kwa nguvu maeneo hayo ya chuoni.Alikaa chini na kujifunuka uso wake.

Tuntu alikuwa na hasira kali sana.Hakutaka kuendelea na mazungumzo tena.Alichukua shilingi elfu tano na kuiweka karibu na begi la Salma kisha aliondoka bila ya kumuaga.Alichukua pikipiki mpaka maeneo ya Magomeni kisha alipanda gali nakuelekea nyumbani kwao.

Salma aliumia sana kwa kitendo cha Tuntu kumpiga bila ya kumsikiliza maelezo yake.Alichukua vitu vyake na kuondoka nyumbani kwao na siku hiyo hakuwa na furaha kiasi cha mama yake kuigundua hali hiyo.

“Inaonekana hauko sawa,kwanini Salma?Hata kama ni hali duni tuliyonayo inabidi uvumilie.Miezi yenyewe imebaki michache,utamaliza tu mwanangu.”Mama yake hakujua sababu iliyomfanya awe hivyo bali alihisi itakuwa ni shida ya kiuchumi ndiyo iliyompa mawazo mwanaye.

“Sawa mama”Salma aliitikia.Enzi hizo alikuwa akimsaidia mama yake shughuli ndogondogo za nyumbani.Ghafla machozi yalianza kumbubujika taratibu huku akivuta kamasi.Uchungu ulizidi kumpanda.Mama yake alistaajabu kwanini iwe hivyo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Salma mbona unalia kuna jambo lingine zaidi limekutokea..!?”Mama yake alianza kuwa na wasiwasi.

“Hapana mama..!”Salma aliongea huku akilia.Aliamua kuinuka na kwenda chumbani kwake na kujilaza kitandani.Mama yake alimfuata chumbani kwake na kuanza kumuhoji kwa kina,ila Salma hakumjibu lolote.Mama yake alitumia busara kuondoka na kumsubiri mpaka hasira itakapopungua.

Wakati wa kula Salma alikataa kutoka nje ya chumba chake.Mama yake alimbembeleza,lakini Salma alikataa kula kwa hiyo siku hiyo alilala na njaa.Mabadiliko hayo ya ghafla yaliwapa wasiwasi wazazi wake kiasi cha kuchanganyikiwa kwa maswali ya kulikoni.Walijaribu kumuuliza kama alikuwa anaumwa,lakini alijibu kuwa alikuwa haumwi ila hakuwambia ni kwanini alikuwa analia.

Kwa upande wa Tuntu,mawazo yalikuwa yanamchanganya kichwa chake.Aligundua kuwa alikosea kumpiga Salma bila ya kumpa nafasi ya kujitetea.Aliwaza jinsi alivyompiga kofi shavuni na Salma hakumrudishia,aliamini kuwa Salma alikuwa na mapenzi ya dhati kwani kwa mwingine angelimrudishia au kumtukana.

“Salma ananipenda sana.Huenda hata huyo jamaa anakataliwa kwasababu yangu mimi.Daah! Nimekosea sana kumpiga..!Kesho nitamuomba radhi.Salma usikasilikie nimefanya hivyo kwasababu ya wivu tu,nakupenda sana”Tuntu alijisemaza moyoni.Kabla ya kulala,aliona siyo vizuri bila ya kumsalimia.Alichukua simu yake ya mkononi na kumpigia.

Kwa upande wa Salma,yeye alikuwa na wasiwasi kama akimpigia Tuntu atapokea?Alibaki ameishika simu yake tu bila ya kufanya lolote huku akiichezea kwa kuigeuza huku na kule.Ghafla aliona simu yake inaita.Alipoangalia alikuta ni Tuntu ndiye aliyempigia.Alivuta pumzi kwa nguvu na kupumua kwa ajili ya kujiandaa kuipokea simu hiyo.Akiwa katika maandalizi hayo,ghafla simu ilikata.

Tuntu alisubiri kwa muda mrefu bila simu kupokelewa hivyo alihisi Salma alikuwa ameshalala,ikambidi aamue kukata simu.Akiwa anajiandaa kwa ajili ya kujilaza kitandani,ghafla alisikia mlio wa meseji kwenye simu yake.Alipoifungua na kuisoma,alikuta imeandikwa tafadhali nipigie kutoka kwa Salma.

Tuntu alikuwa na misimamo ya ajabu sana.Maamuzi yake kwa wakati huo ilikuwa ni kulala hivyo alimuandikia meseji kuwa wataongea kesho.Baada ya kuituma meseji hiyo,alijilaza kitandani kwa ajili ya kuitafuta kesho yake.

Salma baada ya kuipokea meseji hiyo kutoka kwa Tuntu,alipata nguvu kuwa bado Tuntu alikuwa na moyo wa kuwa naye.Kuachwa na Tuntu kwa wakati huo,ingelikuwa ni pigo kubwa sana kwa Salma kwani Tuntu alikuwa kama mzazi wake wa pili kwa wakati huo.Alijifuta machozi na kujilaza huku macho yake yakiangalia kwenye paa la chumba chake ambacho hakikuwa na uzio wowote juu.

Aliutafuta usingizi kwa muda mrefu bila ya mafanikio.Alijigeuza kushoto,kulia kifudufudi lakini usingizi haukuja haraka.Baada ya muda wa takribani saa moja na nusu,usingizi ulimpitia bila ya yeye kujua.....



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kesho yake baada ya masomo,Tuntu na rafiki zake walielekea chuoni Muhimbili kama ilivyokuwa kawaida yao kukutana na wanafunzi wa Jangwani kwa ajili ya majadiliano.Siku hiyo ilikuwa tofauti kidogo.Rafiki zake Salma walikuja wote,lakini Salma hakuonekana. “Salma yuko wapi..!?” Lilikuwa ni swali alilouliza Tuntu hata kabla ya kusalimiana nao.

“Tungekuuliza wewe,kwasababu ndiyo mtu wako wa karibu lazima atakuwa amekupa taarifa?”Alisema mmoja kati ya rafiki zake Salma.

“Ok..Sawa…!Tuachane nayo…”Tuntu alipotezea.Moyoni alijua kama Salma alikuwa na hasira juu yake lakini hakumwambia mtu yeyote.Baada ya kusalimiana,walikaa na kuendelea na ratiba kama ilivyokuwa kawaida yao.Wakati wote wa majadiliano,Tuntu alikuwa haelewi A wala B.Alikuwepo kimwili lakini kifikra alikuwa kwa Salma.

Jioni ilipofika,alirejea nyumbani huku njia nzima akiwa hajielewielewi.Mawazo juu ya Salama yalikitawala kichwa chake. “Au ndiyo maana alikataa kupokea simu yangu..!? Mmh! Asiwe ameamua kuachana na mimi..!?” Zilikuwa ni fikra za wasiwasi zilizojaa kichwani mwa Tuntu.

Baada ya kufika nyumbani na kubadilisha nguo zake za shule,aliingia bafuni kuoga.Baada ya kutoka kuoga aliifungua simu yake na dakika chache baada ya kuifungua simu,ujume uliingia.Ulikuwa ujumbe mrefu uliotoka kwa Salma.

“Tuntu mpenzi wangu! Najua kuwa ni wivu na hasira ndivyo vilivyopelekea unipige.Natambua kiwango cha mapenzi uliyonayo juu yangu ila nakuomba unisikilize hata kidogo nijitetee.Najua bado una hasira na mimi lakini tambua sina makosa bali tu ni fikra zako zilizokupeleka mbali Zaidi.

Tambua wewe ni mvulana wa kwanza kumtamkia neno kupenda katika maisha yangu.Na hii inatokana na msimamo wangu juu ya wavulana.Mimi kama msichana ni jambo la kawaida kutongozwa na zaidi ya wavulana hata wawili mpaka wa tatu kwa siku lakini kwangu nilijitahidi kuwaepuka kwa kuwakatalia na kuwapa onyo ila kwako wewe moyo wangu nimeufungua.Nakupenda Tuntu..!” Ujumbe uliishia hapo.

Tuntu alivuta pumzi kwa nguvu.Aliungalia ujumbe huo kwa takribani sekunde tano hivi kisha alikaa kitandani na kuanza kutafakari.Moyo ulimuuma,alijipiga kichwa na kupiga ngumi takribani mara tatu kitandani kwa nguvu. “Salma ananipenda sana..Salma naomba unisamehe.!”Tuntu alijisemeza kwa sauti ya chini.

Tabasamu lilinyong’onye usoni mwa Tuntu.Alijiona ni mwenye makosa kwa kitendo alichomfanyia Salma siku ya jana.Mida ya chakula cha usiku ilifika lakini Tuntu hakuhisi ladha ya chakula hicho kilichopikwa kwa ustadi zaidi.Alikula takribani vijiko kumi kisha alielekea kunawa.

“Baba vipi leo unaumwa?” Mama yake alimuuliza.

“Hapana mama.”

“Sasa mbona mara tu umeinuka?”

“Nimeshiba mama.” Alijibu huku akielekea chumbani kwake.Kichwa kilikuwa kimejawa na maswali yasiyo na majibu.Mwisho wa siku aliamua kuichukua simu yake na kumpigia Salma kipenzi chake.Baada ya dakika chache aliambiwa simu ilikuwa inatumika.Alisubiri takribani kama dakika tano kisha aliishika simu yake ili ampigie tena.

Kabla hajagusa sehemu ya kupiga,simu yake iliita na alipoangalia jina alikuwa ni Salma.Alisubiri kwa dakika chache ili aangalie kama alikuwa anambipu au kumpigia.Simu iliendelea kuita na hapo Tuntu alijiridhisha kuwa alikuwa anapiga hivyo alijiandaa kuipokea.Kabla hajapokea,simu ilikata na muda mfupi kidogo meseji iliingia.

“Hata kama umenikasirikia naomba upokee simu yangu.”Ilisema meseji hiyo.Tuntu aliamua kumpigia tena na mara kidogo Salma alipokea. “Kwanza naomba unisamehe kwa kile nilichokufanyia.Pili naomba kesho uje shule usifanye hivyo maana leo tulikuwa wapweke sana.”Tuntu aliongea kwa upole baada ya kusalimiana.

“Mimi nitakujaje kukaa sehemu na mtu amabaye hanipendi?”

“Nani hakupendi?”Tuntu aliuliza kwa mshangao kidogo. “Si wewe hapo.” Salama alikuwa anatikisa kibiriti.“Kwa hiyo inamaana bado hujanisamehe?”Tuntu aliuliza kwa hasira ya mbali kidogo. “Siyo hivyo mpenzi wangu kiukweli niliumia sana.”

“Najua ndio maana nimekuomba radhi.”

“Sawa nimekusamehe.”

“Nafurahi kusikia hivyo,Kesho usikose kuja shule,umesikia?”

“Ndiyo mpenzi wangu,”Salma aliitikikia huku akitabasamu na waliendelea kuzungumza mambo mbalimbali.Walitaniana kwa maneno mbalimbali yaliyowafanya warudi kwenye hali zao za kawaida.

******

Siku zulisonga mbele na hatiamaye mwezi wa kumi uliingia.Walikuwa wamekwishafanya mitihani mbalimbali ya mock pamoja na ile ya kujiandaa kabla ya mtihani wa mwisho wa taifa.Kipindi hicho cha mwezi wa kumi,walikuwa walikuwa wanakabiliwa na sherehe za hapa na pale za mahafali kwa ajili ya kuagana kwa Amani.

Zilukuwa zimebaki wiki mbili kufikia mahafali ya shule ya Jangwani.Mpaka kufikia wakati huo,Salma alikuwa bado hajalipia hata senti tano.Mchango ulikuwa ni shilingi elfu therathini kwa ajili ya gharama mbalimbali pamoja na joho.Akili ilimuwanga kwani wazazi wake walikuwa hawana kiasi cha pesa ambacho kingelimuweza kuchangia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Salma alikuwa hana tabia ya kuombaomba hivyo hakumueleza Tuntu juu ya shida hiyo.Siku moja juma mosi mida ya jioni walikutana maeneo ya Kinondoni Mkwajuni.Walikutana kwa ajili ya kujadili mambo yao mbalimbali.Walikaa kwenye mgahawa mmoja uliokuwa karibu na shule ya sekondari Ridhwaa.

“Salma sura yako inaniambia una shida nzito ni ipi hiyo?”Tuntu alimuuliza baada ya kuwa wameshapewa vinywaji na muhudumu huku wakiendelea na mazungumzo.Salma aliinamisha kichwa chini huku akiwa kimya bila ya kusema chochote.

“Sasa kama unanificha mimi utamwambia nani tena?”Tuntu alizidi kumshawishi ili amwambie. “Mwenzako nimechanganyikiwa mpaka sasa..”Salma aliongea kisha alisita kidogo baada ya kukatikizwa na Tuntu aliyeuliza, “Umechanganyikiwa kwa sababu gani.”

“Bado kama wiki mbili mahafali ifanyike na mimi mpaka sasa sijachangia hata nusu ndio maana siko vizuri.”Salma aliongea kwa kusikitisha. “Kwani mnatakiwa kuchangia bei gani?” Tuntu aliliuza. “Elfu therathini kila mtu.”

Tuntu alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha alisema, “Usijali mpaka kufika kesho tutaangalia hali ikoje.Nakuomba usiwaze ni mambo madogo madogo hayo.”Tuntu alimpa moyo. “Nashukuru sana mpenzi wangu.” Salma alilionesha tabasamu lake lote murua kiasi cha mwanya wake kuchomoza bila ya kizuizi.

Tuntu mate nusra ya mdondoke.Tabasamu la Salma lilikuwa kama maji ya baridi mwilini mwake.Alijikuta amemshika mikono Salma na kuanza kuibinyabinya taratibu.Baada ya muda mfupi Salama alihisi tofauti maana mapigo ya moyo yalianza kumuenda mbio taratibu.Waliangalizana machoni na hapo hisia zao zilianza kubadilika.Kwa upande wa Tuntu suruali ilikaribia kutoboka kutokana na hasira za bwana mkubwa wa kijiji.

“Wewe watu wanatuona bwana haifai.”Salma aliongea kwa sauti ya chini huku akiitoa mikono yake kwa Tuntu.Tuntu alibaki akimuangalia kwa jicho lililolegea lenye kutoa ujumbe wa nataka. “Tuondoke basi maana muda wenyewe unauona ulivyokwenda.”Salma alimwambia Tuntu kwani ilikuwa imeshatimia mida ya saa kumi na mbili jioni.

“Ngoja kwanza kama dakika tano hivi.” Tuntu alikataa kuondoka kwa wakati huo kwa kuhofia kuaibika mbele za watu kutokana na baba watoto wake kuivimbisha suruali hivyo alisubiri mpaka ipoe ndipo anyanyuke.Baada ya dakika kama tatu hivi,alipata afadhali na hapo alinyanyuka na walianza kuondoka.

“Baby kiukweli umeniacha hoi.”Tuntu alivunja ukimya.

“Kivipi mpenzi wangu?”

“Nahitaji mambo maana nipo hoi.”

“Mmhh! Mi sijazoe.”Salma alikuwa bado hajaonja ladha ya kitandani. “Kesho basi tuonane kidogo.”Tuntu alishindwa kusubiri na kuamua kuomba nafasi ya mechi.

“Sasa tutaonania wapi?”Salma aliuliza kwani Zaidi ya nyumbani kwa akina Tuntu wangeenda wapi tena. “Wewe nipe jibu kama umekubari sehemu ya kwenda nitajua mimi.”Tuntu alimuhakikishia upatikanaji wa kiwanja cha kuicheza mechi hiyo.Salma alikubari na waliagana baada ya kufika kituoni na kila mmoja alishika njia yake…





Jumapili na mapema iliingia.Kama ilivyokuwa ada kwa siku hiyo ndani ya jiji la Dar es salaam kutokuwa na shamrashamra hivyo ni siku ya pekee kwa mtu kutumia usafiri wa dalala na kufika mapema kule alikokusudia kwenda.Siku hiyo Salma aliamka asubuhi sana na kufanya shughuli zake ili amalize mapema na kumsubiri Tuntu walieahidiana kukutana siku hiyo kwaniaba ya kwenda kulisakata kabumbu.

Baada ya kumaliza shughuli zake za nyumbani mida ya saa mbili,alielekea kuoga.Alitumia takribani kama dakika kumi na tano na kisha alirudi chumbani kwake na kuanza kujipura.Siku hiyo aliichomoa nguo yake iliyokuwa chini ya begi kabisa na kuivaa.Wanja na shedo alizotupia zilikaa barabara mahala pake na kuionesha ile sura yake iliyokaa kiutamu utamu.Alijiangalia kwenye kioo mara tanotano yote ni kuhakikisha siku hiyo anapata asilimia miamoja za kupendeza mbele ya mpenzi wake.

Alimaliza kujipura mida ya saa tatu na dakika kadhaa.Alikaa na kusubiri kupigiwa simu na mpenzi wake ili kujua wapi wangekutana.Mpaka kufikia dakika therathini hakuna simu wala meseji yoyote iliyomfikia kutoka kwa Tuntu.Alijipa moyo mpaka saa nne asubuhi hakuna alichokipata.Aliamua kuchukua simu na kumtafuta na hapo aliambiwa simu haipatikani.Salma alishtuka kidogo kwani hakutegemea kukutana na taarifa hiyo.

Alipiga tena kwa mara nyingine vivyohivyo alikutana na sauti ya dada huyo yanye kubembekeza ikisema, “Samahani namba ya mteja unayempigia haipatikani kwa sasa tafadhali jaribu tena baadaye.” Salma alipandwa na hasira.Aliiangalia simu yake na kuirusha pembeni kwenye kitanda kisha alijilaza huku akijifinya na kujipiga kichwani. “Kwanini Tuntu ananifanyia hivi kama ameahirisha safari siangeniambia?Mbona anakuwa haeleweki jamani,”Salama aliongea kwa uchungu.

“Shosti leo naona umependeza unaelekea wapi?” Mama Salma alimuuliza mwanaye baada ya kuingia chmbani na kumkuta mwanae kang’aaa. “Siendi sehemu mama,kwani mtu anapendeza mpaka awe anatoka.”Salma alimjibu huku akiwa analazimisha tabasamu.

“Sio kawaida yako kuwa hivyo kama hautoki.”

“Leo nimeamua.”Salma alimjibu hjuku akiifungua sumu yake.

“Haya tuachane na hayo,leo tunakula nini mchana maana sina hata senti.”Mama Salma alianza maongezi.

“Mimi mwenyewe niko vibaya.Nimelipia mahafali na maandalizi mengine sina kitu.”

“Wewe mtoto hiyo pesa ya kulipia mahafali umeitoa wapi na wakati sisi tulikuambia hatuna!?”

“ Mama kwanza naomba upunguze munkali,kaa chini tuongee”Salma aliongea kwa sauti ya upole huku akitabasamu.Mama yake alishusha pumzi na kukaa pembeni yake ili kusikiliza hoja za mwanaye.Salma alimueleza kila kitu bila ya kumficha chochote juu ya uhusiano kati yake na Tuntu.

“Mwanangu vijana wengi wa sasa lengo ni kuwachezea wasichana na kuwaacha baada ya kuwaona wakoje.Nakuomba usikubali kumuonesha madhaifu yako kwa kukubali kufanya naye jambo lolote.Akisha kuchezea ni haraka kukuchoka na hatimaye kukuacha.” Mama Salma aliongea kwa sauti ya upole na yenye kunasihi.Hakuwa na nguvu ya kumkemea kutokana na kwamba hata kama angelimkemea shida zingebaki palepale

“Naomba mama niamini siwezi kufanya baya lolote.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Haya na hivyo ulivyovalia unaenda wapi tena?”

“Tulipanga kuonana leo kwa hiyo ndo naenda kuonana naye lakini mpaka sasa hajanipitia.” Salma aliongea kwa huzuni kwani mpaka wakati huo hakuna taarifa aliyoipata kutoka kwa Tuntu aidha wataenda au la.Wakiwa wanaendelea na mazungumzo,ujumbe mfupi uliingia kwenye simu ya Salma na alipofungua alikuta ni namba ngeni iliyomtumia.

“Najua umenisubiri kwa muda mrefu sana ila napenda kukuambia siwezi kuja nipo hospitali.”Ujumbe uliishia hapo.Salma moyo ulimdunda mithili ya mpira ulioshuka kutoka juu. Aliipigia namba hiyo iliyomtumia ujumbe huo na baada ya muda ilipokelewa. “Hospitali gani mpo..!? Eeee..! Nakuja sasa hivi..!?” Salma alichanganyikiwa.Mama yake alimuuliza kulikoni lakini hakumjibu kutokana na kushindwa aanzie wapi.

Mama yake alimshika begani na kumpapasa taratibu kisha alimuuliza kulikoni. “Mama Tuntu yupo hoi na amelazwa Mwananyamala Hospitali.”Aliongea huku akibadilisha nguo zake na kuvaa nguo za kawaida. “Amekutwa na nini?” Mama yake aliuliza.

“Hajaniambia..!” Salma aliongea huku akipumua kwa shida kutoka na mapigo ya moyo kumuenda mbio.Alitoka chumbani kwake na kuelekea chumbani kwa mama yake na kuchukua mtandio kisha alimuaga mama yake na kuondoka.Alipofika kituoni alichukua gari la kuelekea Makumbusho lenye kupitia Mwananyamala.

Alipofika hospitali alipewa maelekezo ya wodi gani waliokuwepo.Baada ya kuingia aliwakuta watu takribani wanne.Wakiume watatu na mwanamke mmoja wakiwa wamekizunguka kitanda alicholala Tuntu.Tuntu alikuwa amelala chali akiangalia juu.Baada ya Salma kuingia na kuwasalimia waliokuwepo,Tuntu aligeuka kumuangalia. “Pole Tuntu..!” Salma aliogea huku akimgusagusa kichwani kulisikiliza joto la mwili.

“Naa…nao...na.o.mba..mni.nya..nyu..e..!”Tuntu aliongea kwa shida huku akilishika tumbo lake.Salma na kijana aliyekuwepo pale kati ya wale wanaume watatu,walisaidizana kumnyanyua.Baaada ya kukaa na kuegemea mto,Tuntu alianza kuongea japo kwa shida.Alimtambulisha Salma kwa wote waliokuwepo pale kwa kusema ni rafiki yake,kisha aliwatambulisha waliokuwepo kwa Salma.

Yule mwanamke aliyekuwepo mahala pale alikuwa ni mama mzazi wa Tuntu na kwa wale wanaume mmoja alikuwa baba yake mwengine ni mjomba wake halafu yule aliyekuwa kijana ni mfanyakazi wa kiume aliyekuwa akishughulika na utunzaji wa bustani nyumbani kwa akina Tuntu.

Sababu ya Tuntu kupelekwa hospitali ilitokana na kuugua ghafla tumbo mida ya asubuhi saa moja baada ya kuamka.Tumbo lilimsokota kwa nguvu kiasi cha kukosa nguvu ya kuinua mguu kwa maumivu makali.Alijikunja kwenye sofa sebuleni huku akipiga kelele.

Wazazi wake walitoka chumbani mbio na kuja kuangalia kulikoni na hapo ikabidi wamkimbize haraka hospitalini.Akiwa na maumivu hayo makali,hatimaye alipoteza kumbukumbu zake na aliamka baada ya kuongezwa maji.

Baada ya kufanyiwa vipimo,iligundulika alikuwa anaumwa ugonjwa wa Taifodi. “Sasa mbona huwa hatumii maji ya kufunga au yoyote hii taifodi kaipataje?” Mama Tuntu alimuuliza Daktari. “Mama huyu haukai naye masaa ishirini na nane huko anakoshinda unajua anatumia nini?”Daktari aliuliza kisha akasema,“Kuna dawa nimemuandikia hivyo itabidi azipate na kuanzia leo atumie maji safi na salama ili kuepuka matatizo Zaidi”Aliwakibidhi karatasi iliyoandikwa orodha ya dawa.

Wakati wazazi wa Tuntu wakiwa wameelekea kwa daktari kupata maelezo Zaidi,mjomba na yule kijana walielekea nyumbani na hapo Salma alibaki na Tuntu huku akimfariji kwa maneno ya kutia moyo.

“Yaani nimezipata habari za kuumwa moyo umenienda juu juu” Salma aliongea kwa kumaanisha.Wakati huo wa maongezi yao,Salma alikuwa akimpa matunda aliyokuja nayo kama zawadi kwa mgojwa.Alimletea machungwa,maparachichi pamoja na ndizi.

“Nilimwambia Simon akutumie meseji maana simu yangu niliisahau nyumbani halafu asubuhi nilikuwa sijaiwasha,”Tuntu aliyakoleza maongezi.

“Namba yangu uliipata wapi?”

“Ninayo kichwani.”Kutokana na upendo aliokuwa nao kwa Salma ilikuwa rahisi kwake kuihifadhi namba ya msichana huyo aliyeuteka moyo wake.Salma alifarijika kwa kusikia Tuntu alikuwa na namba yake kichwani kitu ambacho ni adimu kwa mtu asiyekupenda kukaa na namba yako. Waliongea mengi na mpaka kufika mida ya saa tisa jioni aliruhusiwa na Daktari kurudi nyumbani.

Walitoka nje huku Tuntu akiwa anasaidiwa kutembea kwa kuweka mikono yake kwenye mabega ya Salma na mama yake ambapo mkono wa kulia aliuweka kwenye bega la kusho la Salma na mkono wa kushoto kwenye bega la kulia la mama yake.Tuntu alikuwa anadeka sana kutokana na kuwa mtoto wa pili baada ya kutanguliwa na dada yake ambaye kwa wakati huo alikuwa anasoma shahada ya uchumi katika chuo kikuu cha Dar es salaam.Hivyo walikuwa watoto wawili tu kwa wazazi wao.

Baada ya kufika sehemu ya kuegesha magari,waliingia ndani ya gari la baba yake na hapo mzee alilipasha moto gari kwa ajili ya safari. “Binti unaelekea wapi ili tukusogeze kidogo?” Baba yake Tuntu alimuuliza Salma baada ya kuona mpaka anawasha gari bado alikuwa yumo ndani.

“Twende naye nyumbani..”Mama Tuntu aliingilia kati kabla ya Salma kujibu.Mzee hakuwa na pingamizi Zaidi ya kuliondoa gari kuelekea nyumbani kwao….



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Baada ya kufika nyumbani na kuingia ndani,walikaa sebuleni kwa ajili ya kupunga hewa.Wazazi wa Tuntu walikaa kidogo na baada ya muda walielekea chumbani na kuwaacha Tuntu na Salma wakiendelea na mazungumzo.

Mfanya kazi wa ndani aliwaletea juisi ya maembe ili wapoze koo zao wakati wakiendelea na mazungumzo.

“Mh! Nyumba yenu nzuri!” Salma aliongea huku akipitisha macho huku na kule.Ilikuwa mara yake ya kwanza kuingia ndani ya jumba hilo lililokuwa katikati ya uzio mkubwa uliopambwa kwa bustani zilizohudumiwa barabara.Siku ya kwanza Salma kuliona jumba hilo aliishia nje kwa kuoneshwa na Tuntu kuwa pale ndiyo nyumbani kwao.

“Asante kwa kupasifia nyumbani.”Tuntu aliongea huku akikagua baadhi ya vitu kwenye simu yake baada ya kuletewa na dada wa nyumbani.Muda mfupi mama Tuntu aliingia na kujumuika nao kwenye mazungumzo.

“Kwa hiyo mnasoma pamoja?”Mama Tuntu aliuliza.

“Hapana,huyu anasoma Jangwani ila tunasoma masomo sawa hivyo tumeungana kwa ajili ya kusaidizana kwenye masomo.”Tuntu alijibu kuwa Salma alikuwa rafiki yake kwani hakutaka wazazi wake wajue kama alikuwa ni mpenzi wake kwa wakati huo.

“Karibu mwanangu jisikie upo nyumbani.”Mama Tuntu aliongea huku akitabasamu.Salma alifarijika kwa mapokezi aliyopatiwa siku hiyo.Baada ya muda mfupi walikaribishwa kupata chakula cha mchana.Baada ya kumaliza kula Tuntu alielekea bafuni kujimwagia maji.

Salma alibaki akizungumza na mama yake Tuntu. “Mwanangu unaonekana una nidhamu nimekupenda sana endelea kuwa hivyohivyo.”

“Asante mama.”Salma aliongea huku akitabasamu.Waliiongea mengi huku mama Tuntu akijaribu kumdodosa kwa maswali mbalimbali ili kumfahamu Zaidi.Baada ya dakika kadhaa Tuntu alirejea na kuungana nao.Waliongea mpaka mida ya saa kumi na moja jioni na hapo Salma aliomba ruhusa ya kurudi nyumbani kwao.Mama Tuntu alimkabidhi shilingi elfu kumi kama nyongeza kwenye nauli yake.\

Wakati huo Tuntu alikuwa ameanza kupata nafuu hivyo alikuwa na uwezo wa kutembea bila ya kushika chochote.Walimsindikiza mpaka getini na hapo Salma aliondoka kuelekea nyumbani kwao Magomeni.

******

Siku za mahafali kwa shule hizo mbili Azania na Jangwani zilifuatana.Ilianza mahafali ya Azania ambayo ilifanyika siku ya jumanne na ya Jangwani ilikuwa siku ya Alhamisi.Salma alimuandalia Tuntu zawadi ya pekee siku hiyo.Kwa kuwa alijua Tuntu alikuwa anapendelea Jeans na t-shirts,alinunua na kutia kwenye boksi maalumu.

Siku hiyo ya mahafali ilikuwa na shamrashamra kutokana na kila mtu akiwa na shughuli zake katika maandalizi ya sherehe hiyo.Mpaka kufika mida ya saa nne na nusu asubuhi,sherehe ilikuwa imeshaanza.Wazazi wa Tuntu siku hiyo walijinyima mambo yao na kuja kumuunga mkono mwanao.

Tuntu alikuwa miongoni mwa tumbuizaji wa siku hiyo.Katika wimbo wake wa siku hiyo hakusita kumsifia kipenzi chake Salma japo hakumtaja moja kwa moja.Baada ya shughuli zote za kumalizika ukumbini,kila mmoja alielekea kujumuika na ndugu zake kwa ajili ya kupata picha za ukumbusho na shughuli mbalimbali za kuendeleza furaha yao ya siku hiyo.

Tuntu,Salma,marafiki zao pamoja familia nzima walikaa kwenye moja ya vimbweta vilivyokuwa wazi sehemu hiyo.Walikuja na vyakula pamoja na vinywaji vyao walikaa na kuanza kufurahia huku wakiongea mambo mbalimbali juu ya sherehe ilivyokwenda.Tuntu alitunukia cheti cha mwanafunzi bora kwenye somo la Historia pamoja na mwanamichezo bora.

“Hongera sana baba” Mzee wake alimpa pongezi.

“Kweli ulikuwa unasoma maana wanafunzi mlikuwa wengi sana” Mama yake aliongezea.Maongezi yalinoga huku kila mmoja akichangia ili mradi tu mazungumzo yalikolea. “Asanteni sana wazazi wangu kwa moyo mlionionesha na majukumu mliyoyatimiza juu yangu.”Tuntu alitoa shukrani kwa wazazi wake.

Mida ya saa kumi jioni disko lilianza na hapo kila mmoja alikuwa tayari kulisakata rumba.Vijana wa Azania wengi walikuwa na wapenzi wao kutoka sekondari ya Zanaki,Tambaza,Benjamin pamoja na jirani zao Jangwani hivyo hawakuwa na shida kutafuta wa kusakata nao shida ilibaki kwa yule ambaye alikuwa hana mpenzi wa kucheza naye siku hiyo.

“Sisi inabidi tuondoke maana mambo ya vijana yameanza.”Baba yake alioongea huku akielekea alikoliegesha gari lake.Mama Tuntu aliwaacha Tuntu,Salma na marafiki zao wakiwa wanajiandaa kwenda kulisakata disko hilo lililokuwa la kukatana shoka.Tuntu alielekea kwenye moja ya vyumba vya madarasa kubadilisha nguo alizovaa mchana na kuvaa za kuingia nazo kwenye disko.

Wanafunzi wa kidato cha nne siku hiyo walikuwa wametupia mavazi ya kila aina.Kila mmoja alivaa nguo kadri ya uwezo wake ulivyomruhusu.Tuntu alitokelezea akiwa ametupia jinzi kali nyeusi,t-shirt nyekundu pamoja na kiatu cha raba chenye rangi nyeupe.Alimchukua Salma na kuingia naye ndani ya ukumbi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Dj Mbwax mtaalamu wa kucheza na vyombo vya muziki alianza kufanya yake.Ikitoka nyimbo hii iliingia hii ili mradi tu awapagawishe vijana.Tuntu aliiona dunia ni yake kwa siku hiyo.Alikamatia vyema kiuno cha Salma ambacho kilikuwa kikizunguka vyema mithili ya feni iliyotoka dukani.

Ilipofika mida ya saa kumi na moja na nusu,Dj mahiri alianza kupiga nyimbo za kubembeleza za mapenzi na hapo aliwapa vijana nafasi ya kuwakumbatia wapenzi wao barabara.Kila mmoja siku hiyo aliifurahisha nafsi yake kwa kadri alivyopenda.Mpaka kufika mida ya saa kumi na mbili na nusu jioni,giza lilikuwa limeshaanza kutanda hivyo ulikuwa muda wa kufunga muziki na kila mmoja kuelekea nyumbani kwao.

Tuntu na Salma walitoka nje ya ukumbi na kukaa kwenye vimbweta kwa ajili ya kupunga hewa huku wakiwasubiri rafiki zao kabla ya kuondoka.Dakika chache baada kuketi hapo,Salma alianzisha mazungumzo.




ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog