Simulizi : Kilio Changu
Sehemu Ya Pili (2)
"We kijana unafanyaje hapo mlangoni,simama hapo hapo usiingize miguu yako ndani" Genes aliskia sauti nzito nyuma yake wakati ndio anaanza kuingia chumba ambacho aliona miguu ya mtu ikiwa chini ikimaanisha mtu kajiegesha tu,ila Genes alishindwa kujua kwa nini kakoromewa hivo na alipomwangalia mbaba mwenyewe alikua kajifunga shuka la kimasai na alikua kama anahema sana kwa hofu fulan kana kwamba anafukuzwa au kuna kitu anataka kufanya cha hatari,
"hapana baba nilikua naangalia huku chumbani maana nimeandikiwa niingie chumba namba tisa ila nimepewa funguo za chumba namba sita hivyo nikataka kujua huku ndani kama kuna mtu" Genes alijibu kwa hofu
"kwanza we mtoto mdogo unakuja Kulala huku kwani huna kwenu?" Genes aliulizwa kwa hasira ila hakujibu kitu zaidi ya kurudi mapokezi ili kujua kama ni dada wa mapokezi kajisahau.
"Samahan baba, huyo uliyekua unaongea nae hapo nje ni nani ?" Miriam alimuuliza msamaria wake aliemdhamini sehemu ya kulala,
"ni mtoto mmoja mshenz kweli hata cjui anafuata nini huku usiku huu,ila nishamtimua alitaka kutuharibia raha zetu"
"raha gani tena baba kwani ulinambia naletewa chakula nashangaa wewe ndo unakuja" Miriam aliongea kwa hofu kwani pale tayari alijiwa na kumbukumbu ya sauti ya Genes na alitaka kujua kama ndie yeye au ni nani na kama ni yeye amekuja kufuata nini pale,
"sasa wewe binti sikia mimi nimekuja huku ndani kwa ujanja ujanja tu sijajiandikisha huko mapokezi hivo naomba tutulie sauti isitoke nje" msamaria wa Miriam alimwambia Miriam kwa kumnong'oneza,
"kwa kweli baba mimi sipo tayar kulala na wewe maana nilichokimbia huko nilikotoka ni hiki na wewe unataka kunifanyia tena hichohicho hivyo heri nirudi tu" Miriam alijibu kwa hasira huku akisimama na kuanza kuelekea mlangoni ila huyo baba alimshika na kimvutia kitandani na hapo walianza kuvutana huyo baba akitaka kumvua nguo kwa lengo la kumwingilia kimwili.
*******
"Dada samahan mbona sijaelewa kuhusu huu ufunguo ulionipa na chumba ulichoniandikia" Genes alimpata dada wa mapokezi,
"kwani vipi mdogo angu" dada nae alimjibu kwa kumbembeleza mteja,
"huu ufunguo ni wa chumba namba sita ila umeniandika niingie chumba namba tisa,sasa chumba namba tisa kuna mtu ila pia kaja mtu mwingine ambae sijamuelewa hebu fanyeni uchunguzi,
"ahaa kweli mdogo wangu samahani sana nimekumbuka chumba namba tisa kuna dada mmoja kaletwa hapa na baba yake ila pia huyo baba aliondoka ili huyo binti alale hapa hivyo smahani ngoja nibadilishe chumba hapa niandike namba sita, samahani sana dogo shemeji yako ananichanganya"
"sasa dada kama hicho chumba ni binti yupo huko ndo ujue kuna mbaba kaingia huko sasa nendeni mkachunguze maana kila kukicha naskia vifo kwenye vyumba vya wageni hivyo huenda hata huyo ni muuaji" Genes aliongea kws msisitizo.
Walinzi waliitwa kuelekea chumba namba tisa ambapo Genes pia aliandamana nao kushuhudia.
********
"We baba niacheeeeee niache unaninyonga niache nakuambia niache,hata kama ni hela yako uliyonilipia basi kachukue nikalale nje mimi sihitaji msaada wako" Miriam aliendelea kujitetea ila alizidiwa nguvu na kuvuliwa nguo,
"aliekwambia mjini kuna vitu vya bure ni nani" huyo baba alimwambia Miriam kwa kumkoromea na hapo alikua akimuweka mkao mzuri wa kumwingilia ila kabla hajafanikiwa kuanza kumwingilia kimwili aliskia mlango ukigongwa kwa kishindo,
"Nyie fungueni mlango mbona mnapigana humo ndani,mmeskia hivo vitanda ni uwanja wa mieleka?" Mlinzi aliejulikana kwa jina Chipolo aliongea kwa ukali,
"sinimesema huyu ni muuaji,sikiliza huyo anaelia huko ndani," Genes aliongea kwa kunong'oneza,
"alooo nyie hamfungui niingie na huu mlango ?" mlinzi Chipolo alizidisha mikwara,
"mimi nataka kufungua ila huyu baba ananishika na kuninyonga hataki nifungue" Miriam aliongea kwa sauti ya juu huku akiwa bado uchi ila alijitahid kufungua mlango ili aweze kupata msaada,hakujali yupo uchi kabisa hata blauz aliyokua amevaa alivuliwa hivyo mwili wake wote ulikua unaonekana.
Mlango ulifunguliwa na hapo Miriam alijitupa miguuni mwa mlinzi kutaka msaada,
"Hebu binti kwanza kaa pembeni tunamtaka huyu mhalifu kwanza" mlinzi Chipolo aliongea kwa ukali na kumwamuru Miriam asogee pembeni.
Mhalifu alikamatwa na askari waliitwa na kumtia mikononi tayar kwa uchunguzi pamoja na Miriam alichukuliwa kupelekwa kituoni kwa ajili ya uchunguzi.
Genes alipomuona Miriam mazingira yale alishindwa kuelewa ni kwa namna gani Miriam kule na kufanyaje ,ingawa mimi ndio nimemwokoa lakini kafuata nini huku,
" basi huyu demu atakua malaya tu mimi nilijua nimepata demu kumbe kahaba tu anajiuza sasa itakua wamerushana pesa" Genes alijisemea kimoyomoyo huku akifungua chumba alichopewa ili alale,
" kesho asubuhi hata siendi nyumbani ili nikaende shule nitalala hadi saa mbili asubuhi maana kweli nimekubali usilolijua ni sawa na usiku wa giza"Genes alijiongea kwa sauti hata mtu angemuoa angedhani anaongea na mtu.
Baada ya dakika ishirini Genes alipitiwa na usingizi.
********
"Yaani kweli Genes ndo mwanaume wakuja kunioa kama ameweza kuniokoa kupatwa na majanga yaleo basi ndio mwanaume nitakaemkabidhi moyo wangu hata kama atakua na maisha ya namna gani, yaani nilikua nishakata tamaa ila mungu mkubwa kanioneshea tena,kazi ni moja tu kesho asubuhi lazima nitamtafuta katika hotel niliyomwacha ili niweze kuongea nae machache pamoja na kumshukuru kwa kuniokoa" Miriam aliwaza hayo wakiwa njiani kuelekea kituoni kwa ajili ya mahojian na polisi kwani kwa kipindi hicho kulikua na matukio mengi yalikua yakitokea kwenye nyumba za kulala wageni hivyo kesho la polisi lilikua makini kupambana na matukio hayo ili yasiendelee kutokea.
"we mtoto mbona unaonekana mdogo sana na mnakuja kwenye vyumba vya wageni kutishiana kuuwana?" askari mmoja alimuuliza Miriam wakiwa bado njiani kuelekea kituoni,
"kwa kweli afafande mi mimi cjajauwawana na huhuyu ila yeye ndio alilitaka kunibaka" Miriam alijibu huku akitetemeka kwa woga kwani kitendo cha yeye kukaa na askari wakiume pamoja na mhalifu wake kulimpa wasiwasi wasije mgeuka na kumbaka tena,
"aha we kama unasema ulikua unabakwa uliingia chumbani kufanyaje?" askari alizidisha swali ila Miriam alipofika kituoni alieleza yote ndo hapo walipowekwa chini ya ulinzi hadi pakuche ambapo ndipo Genes alitakiwa kuitwa kituoni kutoa ushahidi kwani Miriam alisisistiza huyo Genes atafutwe kumbe nia yake ilikua kuja kumuona na kumshukuru na kumuahid panzi la dhati kwani alimuona kama mkombozi wa maisha yake.
********
"aha saiv saa kumi na mbili kumbe bado hapajakucha vizur" Genes alijisema pale aliposhtuka na kuangalia saa yake.Alivuta blanketi ila usingizi haukumjia tena zaid ya kuwaza tu kuhusu Miriam,
"lakin huyu mwanamke hivi jana hajalala hapa tena kweli,au itakua alienda kulala sero na huyu bahasha wake walioshindwana bei, ingawa nilisema nalala mpaka saa mbili aise silali tena maana anaweza amka tukutane na mimi sitaki kuonana nae kabisa hata watu wakiona nasalimiana nae watanicheka sana,kumbe ningempa hii misimbazi yangu ningekua natunza mali ya watu pumbavu zake ngoja nitoke saivi kwanza asije kuniona hapa"Genes alijisemea kimoyomoyo huku akiamka kuingia bafuni ili aweze kutoka kwani alitokea kumchukia Miriam ghafla sana hivyo hakutaka hata waonane,
"ngoja niweke hizi hela zangu zilizobaki hapa maana nikienda nazo bafuni zinaweza kulowa na mimi sipendi kutembea na pesa chafuchafu" Genes alijisemea hayo huku akiinua godoro na kuweka hapo pochi yake.
*******
" jaman wahini kule hotelin kabla yule Genes hajatoka ili aje kuelezea jinsi alivyoonana na huyu mhalifu alietaka kunibaka" Miriam aliongea kwa ukali kupitia dirishani alipomwona askari akikatiza njia karibu na chumba chake maalumu cha watoto alimohifadhiwa
"we turia mtoto acha mawenge yako" askari alitoa jibu kwa Miriam,
"kweli yule ataondoka na mtakosa ushahidi tena jitahidini kuwahi saivi" Miriam alisisitizwa na hapo alisikilizwa na askari waliwasha gari kuelekea hotel Aquline kumtafuta Genes.
Miriam alifurahi sana kuona Genes atakua nae baada ya muda mfupi ili aweze kumwonesha hisia zake.
******
"Me nilijiuliza kwa nimpe namba ya simu alafu asinitafute kumbe ndo kazi yake hii hadi akasahau kunitafuta,sasa kama jana yupo na baba yangu kabisa si hatari kabisa yaani mahali wababa wanapita na mimi nipite? asante mungu kwa kuniepusha na hili janga" Genes aliongea maneno hayo huku akifunga mlango ili akakabidhi ufunguo mapokezi tayari kuelekea nyumbani.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Broh vipi hapo Mianzini shilingi ngapi?" Genes alimuuliza dereva pikipiki kwani alitaka kupanda pikipiki hadi kituo cha Mianzini ambapo angeweza kupanda daladala hadi kwako,
"Hapo buku jero tu boss wangu" dereva pikipiki alijibu,
"aah nawewe acha hizo,sinitembee na miguu" Genes nae aliongea kumaanisha kiasi alichotoswa ni kikubwa kulingana na umbali wa kutoka Aquline hotel hadi Mianzini,
"haya basi leta hiyo buku chap nikurushe kama fast jet" dereva pikipiki aliongea huku tayar kashawasha pikipiki,
"siuna chenchi ya msimbazi?" Genes aliongea huku akipanda kwenye pikipiki kwani alijua amebaki na elfu arobaini na ni elfu kumi kumi zote,
"aise asubuhi hii bado cjakamata mpunga huo labda ulete nicheki kwa marafiki zangu hapa kijiweni" dereva pikipiki aliongea huku akijiandaa kupokea pesa na ndipo Genes alipoingiza mkono mfukoni na kushtuka hajachukua pesa zake pale alipoziweka kuelekea kuoga,
"mama yangu nimesahau pesa pale chumbani" Genes aliongea huku akitimua haraka kurud hotelini,
"cheki huyu bwege ananitia gundu asubuhi hii yote" dereva pikipiki alijisemea huku Genes akiishia.
"sijui kama nitazipata mungu angu kama ashaingia mtu huko ndo basi tena" Genes alijisemea huku akipiga hatua kubwa kubwa kuelekea hotelini.
*******
"Kweli huyo kijana wakati anaingia jana ni mwenzangu alikua hapa mapokezi ila kwa taarifa za hapa kwenye daftari zinaonesha aliingia mda sawa na huyo Miriam, alafu mngewahi kidogo tu mngemkuta maana kaondoka kama dakika kumi na tano zimeisha saivi" hayo talikua maneno ya dada wa mapokezi alikua anawaelezea askari walioenda kumchukua Genes kwa ajili ya ushahidi wa tukio la Miriam ila kwa bahati mbaya wakakuta kashaondoka.
"sasa dada hebu kama inawezekana tukafungue chumba cha huyo Genes tuangalie kama kuna kitu chochote cha kuchunguza maana pia kwanza kwa nini mtoto mdogo hivo aje kukodi chumba huku hotelini" aliongea askari mmoja kwa sauti ya kushauri,hapo wote waliandamana kuelekea chumba namba sita ambacho ndicho Genes alicholala.
********
"Miriam akiwa kituoni aliendelea kumuomba mungu amsaidie tu ili aweze kuonana na Genes
" hakika huyu Genes nisipomwona nimshukuru na kumwonesha hisia zangu itakua nimefanya kosa kubwa ila naamini kwa uwezo wa aliye juu lazima nitafanikiwa kuonana nae leo tena mda sio mrefu"Miriam aliendelea kujipa natumaini kwa kiasi kikubwa kwani nia yake sio kuhitaji ushahidi bali ni kumwona Genes tu basi.
**********
"cheki huyu Miriam ndo mkosi wa haya yote hadi namkosa huyu dada wa mapokezi hakika huyu mwanamke anganiletea balaa kwenye maisha yangu" Genes alijisemea hayo akiwa mapokezi ili aweze kutoa maelezo ya chumba alichotoka nakusahau huko pesa zake ila hakumkukuta dada aliyekua zamu kwa mda huo ila hakujua kama kwa mda huo ndio chumba alichotoka kinafunguliwa.Baada ya kusubira kwa dakika mbili aligundua akili aliyopewa na rafiki ake aitwae Deo kua kama ukisahau kitu cha thamani ndani alafu ukapotea ufunguo wa kufungua chumba chenye hicho kitu cha thamani basi haraka inakupasa ukachunge hapo mlangoni ili mtu hata akiokota huo ufunguo asiweze kuja kufungua,hivyo baada ya wazo hilo aliamua kuelekea karibu na chumba alichotoka hadi dada wa mapokezi arudi.
"Haya yote ni Miriam anasababisha" Genes aliendelea kumtupia Miriam lawama huku akitoka mapokezi kuelekea chumbani ila ghafla alishangaa kuona mlango wachumba alichotoka ukiwa wazi na kwandani kukiwa na watu na hapo aliona sare ya askari.
"mmmh sio kuzuri hata kidogo" Genes alijisemea na kuwaza labda kuna namna amehusishwa katika patashika ya jana,
"hapa heri ipotee tu hiyo pesa" Genes alijesema kwani aliogopa kuhusishwa na kesi yeyote kwa maana aliogopa nyumbani akijulikana hayupo kwa shangazi ambapo jana yake aliaga kuenda huko basi nyumbani patawaka sana,ila wakati akijishauri kugeuka basi alionekana na dada wa mapokezi,
"we Genes njoo hapa unatafutwa"Dada aliongea kwa sauti kubwa ila Genes alijifanya hajaskia na akataka kukimbia ila askari mmoja alitoka na kimkamata.
Hapo wote walijiuliza kua kafuata nini kwa sababu alishakabidhi funguo na kuondoka,
" huyu itakua ana lakwake jambo"askari mmoja alijisemea kwani mda huo nae akawa anachunguzwa ingawa walimfuata kwa ajili ya kuenda kutoa ushahidi ila nae walimhisi kama mhalifu kwani alipoulizwa kuwa kafuata nini alidai kaja kumsalimia mdada wa mapokezi kitu ambacho askari walimtilia mashaka.
Gari ya police iliondoka na Genes huku Genes akiwa anaumi moyoni kwani alizidi kumchukia Miriam kwa yote yaliyokua yakitokea,
"sasa hapa nakamatwa ni lazima baba yangu atajua na mama yangu pia na jamii yote inayonizunguka itajua kua nimekamtwa mazingira ya quest tena wakati wa masomo kisa huyu Miriam na alaaniwe na hela zenyewe zitapotea aah shenzi kweli huyu mwanamke" Genes alijisemea kimoyomoyo huku gari ikiwa kasi kuelekea kituoni na mda huo ilikua ni saa moja asubuhi.
********
Hapo kwanza Genes alianza kutumika katika kutoa ushahidi juu ya kesi ya Miriam ila askari walishanga kusikia Miriam akisema,
"jaman huyu baba ingawa alitaka kunibaka nimemsamehe ila chakufanya anilipie nauli ya kurudi nyumbani"
"we binti unajua utaratibu wa mahakama au unaongea tu" askari mmoja alimjibu Miriam,
"siujui ila naomba mimi ni mtoto sitaki kupambana na kesi hivyo yaishe" Miriam aliongea kwa msisitizo mkubwa kwani alikua na uso wake wake ulimwangalia Genes kwa furaha ila Genes alimkazia sura hakuamini kabisa kama mwanake huyo ndo anamletea balaa zote hizo.
Askari walishikwa hasira na hapo wakaitana pembeni na kujadiliana ambapo mkuu wa upepelezi aliongea,
"hii kesi me siielewi kabisa hapa tuchukue hapo hela ya chai tupite zetu kushoto hawa mara mshtaki hataki kesi mara wote hawaeleweki" baada ya kusema hayo walirudi na kuwataka kiasi cha pesa ili waweze kufuta makosa hayo ambao mhalifu wa Miriam alitoka shilingi elfu sitini kunyamazisha yote pamoja na kumpa Miriam elfu 50 kwa ajili ya kusafiria jinsi alivyodai na kesi ikawa imeisha.
"sasa nyie kila mtu aondoke kwa amani hapa ila wewe dada tutakurudisha hadi pale Aquline hotel maana tulikutoa hapo" aliongea askari mmoja kwani kufanya hivo kungeimarisha usalama wa Miriam,
"na wewe kijana utabaki hapa hadi wazazi wako waje kutoa maelezo yako maana kwanza bado unaonekana unasoma ila mara unatoka hotelini na kurudi hivyo wewe utabaki hapa" askari mmoja aliongea huku akiinuka kwa kumwita Miriam ili aweze kumrudisha Aquline hotel,
"sitaki nimwache huyu Genes mikononi mwa askari" Miriam aliongea kwa sauti mbele ya askari wote kwani Miriam alipandwa na hasira kuona akili aliyotumia hadi Genes akafika pale inataka kuzuiwa tena wasiongee hivyo Miriam aling'ang'ania kuondoka na Genes yaani warudishwe pamoja pale Aquline hotel.
Baada ya mvutano wa muda basi askari walimtosa Genes shilingi elfu 30 ili waweze kimruhusu atoke ila Genes alidai hana hela na hapo Miriam aliamua kutoa elfu 30 kwenye elfu 50 aliyopewa ili kumlipia Genes kisha wakarudishwa wote pale Aquline hotel.
"Hata unichangie figo sitaweza kukaa na wewe" Genes akijisemea moyoni.
Genes aliwaza kua atafikaje nyumbani kwani alishatoa sadaka zile pesa alizoacha chumbani sababu aliogopa sana hata kukaa mazingira ya pale hotelini.
"Yaani hii gari ikisimaa tu natoka nduki leo natembea kwa miguu hadi nyumbani" Genes alijisemea alipoona geti la hotel Aquline,
"yaani mungu mkubwa leo nitaongea na mume wangu kila kitu" Miriam nae alijisemea moyoni kwa furaha gari ilipokua ikiingia getini.
Baada ya kushuka askari waliwaaga kwa amani ila Miriam kwa haraka alitoa ile elfu 20 iliyobaki na kumkabidhi Genes elfu 10,
"Mume wangu tugawane hii" Miriam aliongea kwa tabasamu huku akimkabidhi Genes hiyo pesa ambapo baada ya Genes kupokea alianza kuondoka kwa kasi,
"kumbe ulijua sina hata nauli?" Genes alijisemea baada ya kumshinda Miriam mbio na kupanda pikipiki ambapo alimwacha Miriam pale getini.
Miriam hakuamini macho yake kwani aliona kama mtu aliyeokota dhahabu na kuipoteza,
"sasa hii elfu kumi haitoshi hata kunifikisha nyumbani Manyara" Miriam alijisemea huku akiwaza kurud hotelini na kuomba msaada mwingine lengo lake likiwa kuongea na Genes tu,hivyo alielekea mapokezi.
Miriam aliongea na dada aliyekua mapokezi kwa mda mrefu ambapo Miriam aliongea historia yote ya maisha yake na hapo huyo dada alimfanyia mpango akapata kazi ya kufua mashuka na kufanya usafi katika vyumba, na hapo Miriam aliwenza kuanza kazi siku hiyo hiyo.
"We Miriam ukifanya usafi uhahikishe unainua magodoro na kuangalia kwenye machaga vizur kwani kuna wanaume wengine wasio wastarabu wanaweza lala na mwanamke alafu wanaficha huko mampira yaliyotumika" Miriam aliambiwa huku akiwa kubeba maji na dekio kuelekea kwenye baadhi nyumba ambavyo tayari watu washatoka.
"Tena naanza na hiki chumba mme wangu alicholala" Miriam alijisemea huku akifungua chumba alicholala Genes.
"Sasa pochi yangu itakua imepotea na kitambulisho changu cha shule kimepotea ila kwa kua kile kitambulisho kina picha yangu na jina langu basi mtu akikipata ni rahisi kunipata,ila namkumbuka rafiki yangu Deo ananipaga ushauri kua napopoteza kitambulisho niende kituo cha polisi kutoa taarifa maana mtu mbaya akikiokota alafu akaenda kufanya tukio la kihalifu kisha akitupe hicho kitambulisho basi lazima nitafutwe ila kama ukienda kutoa taarifa wala hutahisishwa na tukio hilo"
Genes alijisemea akiwa Kwenye daladala kurudi nyumbani.
Kuanzia siku hiyo Genes aliyachukia mapenzi na aliapa kutopenda tena kizembe kwani aliona kama vile kupenda ni kujiingiza katika matatizo maana kupenda ndiko kulimsababishia yote hayo.
"Hadi shuleni nimeanza kupoteza raman kwa ajili ya mapenzi, saivi shule nitakua nasoma kwa bidii mapenzi yapo tu nitaja yakuta tena nitampata msichana mwaminifu sio huyu Miriam muuza mwili" Genes aliendelea kujisemea kwani alikua na mawazo sana na hapo alipanga akifika nyumbani atadanganya anaumwa ili aweze kukaa tu ndani.
********
"Hii pochi itakua ya nani?" Miriam alijiuliza huku akikaa kitandani ili aweze kuchunguza vizuri pochi aliyoikuta kwenye chumba Genes alicholala,
"heee ina hadi pesa nyingi hivi,zinatosha kwenda Manyara,ngoja nikamwoneshe dada Anitha"
Anitha ndo dada alimchorea kazi hivyo ndo alikua rafiki yake kwa mda huo,Miriam alijisemea huku akiinuka ila kabla ya kutoka nje alirudi kukaa kwani aliona kitambulisho ikabid akitoe na hapo hakuamini kukutana na picha ya Genes katika kitambulisho ambacho kilikua ni bima ya afya pamoja na cha shule hapo aliibusu sura ya Genes katika hivyo vitambulisho ,
"sasa hapa mungu mkubwa jaman hata napata faraja ya maisha yangu kua na picha ya huyu mwanaume" Miriam alijisemea moyoni na hakutaka tena kumwonesha Anitha,
"sasa Genes itakua ni mganga wa kienyeji nini?,kwani alijulia wapi kua nitakuja kufanya kazi hapa ndio aache vitu hivi vyote?,au itakua kuna sababu nyingine yayeye kuacha?,ngoja nitamuuliza dada Anitha" Miriam alijisemea hayo wakati akificha pochi hiyo ndani ya mfuko wa sweta kubwa alilovaa kutokana hali ya ubaridi mkoani Arusha.
********
"We Genes hebu fungua mlango wako nataka nijue kwa nini hutaki kuenda shule,na nataka kujua hela zangu nani kaiba hapa chumbani kwangu" mama yake Genes aliongea kwa sauti kubwa iliyomfanya Genes ashtuke na kujifuta machozi yaliyokua yanamtiririka.
"Mama mimi naumwa",
"Unaumwa wapi",
"kichwa naskia yani homa inanijia mama"
"ahaa pole mwanangu hebu ile bima yako ya hospitali niangalie kama imeisha ila tufanye utaratibu wa kuenda kukutibu"
"Mama ile bima niliweka hapa ndani hata siioni,"
"sawa mwanangu jiandae tuende basi hapo kituo cha afya na kitambulisho chako cha shule"
"hata hicho sikioni mama"
"mwanangu siku hizi umepetwa na nini mbona sikuelewi maana hata walimu wako shuleni wanalalamika umekua mzembe,na huku nyumbani umekua mzembe nini shida mwanangu unajua mtihani wa kuhitimu masomo ya msingi ndio unakaribia?".
Genes na mama yake waliongea mengi na kutokana na mama kua na moyo wa huruma basi aliacha masuala ya kupotea kwa hela na kumhudumia mwanae.
"Ila usikute unanionea mimi mama yako kwakua baba kasafiri ?"mama Genes alimuuliza Genes kwa utani huku akimpa maji ili ameze dawa aina ya panadol kwa ajili ya kutuliza maumivu.
"Yaani haya yote ni huyu mbwa mwitu aise Miriam siutoe huu mkosi unaoniachia kumbe hadi maza kashasanda kuwa shuleni nimekua mbulula aise" Genes alijisemea baada ya mama yake kumuacha alale.
******
"Hivi dada Anitha, leo asubuh yule kijana aitwae Genes ilikuaje hadi akaja kukamwatwa?" Miriam alimuuliza Anitha baada ya kumaliza usafi,
"aah kale katoto bhana kajinga sana kalianza kukabidhi ufunguo kakaondoka ila baada ya mda kakarudi tena ndipo kalipokamatwa" Anitha alijibu huku akicheka,
"kwa hiyo kalirudi kufanyaje" Miriam aliongeza swali,
"hata cjui maana kana mambo ya kitoto bhana maana kalikuja kakawa kanachungulia ndo wakamshika ila mwanzo alikua ashakabidhi ufunguo kwangu"Anitha alijibu ila uso wake ulionesha kuchokwa na maswali.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sasa dada Anitha huyo ndie mume wangu" Miriam alimwambia Anitha kua Genes ndie mume wake tena kwa kujiamini,
"wee kale katoto kula kwa mama yake kulala kwa mama yake hata nguo za ndani itakua anapewa na mama yake,katakupeleka wapi sasa mdogo wangu? sema mimi nikutafutie bonge la bwana likuvalishe na kukugharamia kila kitu,tena wewe mdogo mdogo hivi na mwili wako unavovutia na huo weusi wako wa asili lazima tupige pesa hadi za watalii" Anitha aliongea kwa kumsihi Miriam,
"hapana dada yule ni mtoto ndio ila thamani yake niliiona siku moja tu na nikatokea kumpeda sana na sitomuacha hata kama hatanipa kitu mimi nitampa" Miriam alijibu kwa kusistiiza,
"mdogo angu itakua umechanganyikiwa, yaani hapa mjini ni mipango hivyo unavyotaka kufanya huwezi tembea na mtoto kama yule,we kwanza unavyoniona mimi nina wanaume sita tena wazito kihela acha hizo michepuko na hawanitoshi bado,mungu amekupa mwili wenye tundu hivyo basi litumie mdogo wangu,yaani we unatembea na mgodi hivyo uliona wapi watoto wakiingia mgodini?, hivyo mdogo wangu angalia mwenye pesa sawa?", Anitha alimwambia Miriam ambae kwa mda huo aliinamisha kichwa chini na kutafakari juu ya maisha yake,
"mungu nitie nguvu kama kila mtu nakaa nae ananishauri juu ya kujiuza tu nitaishi na nani?,Genes pekee ndie wakunioa milele sitomsaliti na nitafanya kazi yoyote kwa malengo" Miriam alikua anajisemea kimoyomoyo huku kichwa kikiwa chini,na hapo aliwaza baada ya mda akamwambia Anitha,
"mimi huyo Genes ni mtu muhimu sana katika maisha yangu siwezi kumwacha ingawa hata mahusiano hayajaanza maana sasa kama ukinambia niwe na wanaume wengi nitaweza kupata ukimwi" Miriam aliongea kwa uso wa huzuni,
"mdogo angu ukimwi sio wa kuogopa bali inabidi uogope mimba kwani ndo itakuzuia kuendelea na kazi zako alafu ukute mbaya zaidi imekuja kipindi huna hela ya kutoa,ila ukimwi hata ukipata bado utapiga pesa tu mdogo angu saivi wanasema hapa kazi tu sasa wewe lala ule ndoto zako,hapa mshahara ni mdogo sana hivyo ukiutegemea wala hutoki milele" Anitha alizidi kutoa maneno yaliyompasua Miriam kichwa hadi akashindwa kujua ni wapi atapa mtu mwenye malengo ya kufanya kazi kwa bidii,
"Dada Anitha mimi nitajitahidi kufanya kazi kwa bidii hadi nifanikiwe, maana mimi nauogopa sana ukimwi ingawa wanasema kuna kinga ila mimi heri nisifanye kabisa kwani mtu akiamua kukuambukiza ukimwi atakuambukiza tu hata akivua hizo mipira utajulia wapi ?, we hujui wanaume wengi wana malengo mabaya na sisi kinadada ?,na pia hata kama mshahara wa hapa ni mdogo nitajitahid kuufanyia kazi uwe mkubwa kwani hela nikipata nisipotumia ovyo nikikusanya na kufuga hata kuku sinitakua na kuku wengi nikija kuwauza nitakua tajiri tu," Miriam aliongea kwa kujiamini kwani hakutaka kufanya kitu cha kujiharibu mwili wake, yeye aliamini kazi yoyote inaweza kukufanya kuwa tajiri na hata hapo aliwaza kuhusu watu wanaodharau kazi za ndani eti ni za kijinga na mshahara mdogo,
"hivi kwa mfano hata ukifanya kazi za ndani kama unakula na kulala bila kukatwa mshahara alafu ukalipwa elfu sabini ina maana ukinunua kuku wa elfu arobaini na chakula cha elfu ishirini ukatafuta kaeneo ka kufugia siutafanya hivyo kila mwezi na hatimaye utakua tajiri? kikubwa ni kufanya kazi kwa bidii bhana na kuepukana na kutumia hela ovyo kwa kujiepusha na starehe na anasa" Miriam alijikuta akiwaza kwa hasira moyoni kwani alikua na moyo wa kufanya kazi kwa bidii.
"Mdogo wangu ila wewe jitahidi kujitunza na kufanya kazi kwa bidii tuone kama utatoka,wewe mimi nitakusaidia sehemu ya kulala baada ya kutoka hapa kazini" Anitha alimwambia Miriam,
"nitashukuru dada Anitha kwa kunipa hifadhi mimi nitafanya kazi kwa bidii nakuomba unihifadhi kwa miezi miwili tu", Miriam aliongea kwa kushukuru kwani kupata sehemu ya kulala ilikua furaha sana kwake,
"Ila kama ana wanaume sita tena wazito kihela basi atakua ana nyumba yake" Miriam alijisemea moyoni kwa kuhisi Anitha atakua tajiri sana kwa kua ana wanaume wengi wenye pesa wanaoutumia mwili wake.
Jioni ilifika ambapo Anitha na Miriam waliongozana kuelekea nyumbani ambapo Anitha alipanga chumba chake maeneo ya Sekei karibia na hotel ya Mount Meru.
Wakiwa njiani Miriam alikua na mawazo ya kwa jinsi gani ataweza kuonana na Genes kwa mara nyingine ili aweze kumkabidhi pochi yake yenye pesa na vitambulisho kwani alishajua aliisahau ndo maana alirudi kuichukua ndipo akakamatwa.
Wakiwa wamefika Mount Meru hotel hapo Miriam aliona karatasi iliyochanwa vipande viwili na kuviringishwa pamoja,kutokana na tabia yake ya kupenda usafi basi aliliokota ili kulitupa,sehemu husika ila alitembea umbali kidogo bila kuona sehemu ya kulitupa hivyo akajikuta analifumua ili aweze kusoma kilichoandikwa,
"ha mbona jina langu?" Miriam alijisemea baada ya kukutana na neno
"Dear Miriam" ambalo ndio neno la kwanza aliloona katika kipande cha kwanza cha karatasi na hapo akasema,
"ngoja nikifika nyumbani nitasoma vizur" kisha aliviweka vipande hivyo mfukoni na kua na hamu ya kufika nyumbani kwa Anitha mapema ili kuweza kuona faida ya kuwa na wanaume wengi jinsi Anitha anavyodai kua na watu wazito pamoja na kujua nini kilichoandikwa katika karatasi aliyoiokota njiani..
"Miriam hapa ndipo nyumbani karibu sana utakaa hapa hadi upate mahali pako pa kuishi,jiskie nyumbani" Anitha aliongea huku akimkaribisha Miriam aweze kukaa katika godoro lililowekwa chini,
"Asante dada nashukuru" Miriam alijibu kwa furaha kwani alimuona Anitha kama mwanake mwenye roho nzuri.
Waliendelea kuongea huku wakipika chakula cha jioni ili waweze kula na kulala.
"Yaani wewe mpuuzi tu mwenyewe yule msanii yule cjui nani tena na hela zake zote na umaarufu wake ila ameimba kua anajua hata demu wake kuna siku atamkimbia sembuse wewe na hicho kitambi chako tu unasema eti siwezi kukuacha nyoooo! pumbavu" Yalikua maneno ya Anitha akimfokea mtu aliekua akiongea nae kwenye cm wakati Miriam akiskia yote hayo,na wakati huo ndio walikua wanamalizia ugali waliopika,
"nani tena huyo dada Anitha" Miriam aliuliza kiuchokozi akitaka kujua nani ameambiwa maneno hayo,
"huyu ni kinyago fulani ana kitambi ila hana pesa na ananing'ang'ania kama kupe siheri nimfute kwenye list yangu maana hata shughuli hawezi sababu ya kitambi chake ukimuona utazania mkuu wa UN (United Nation) kumbe ovyoo" Anitha alijibu na kumalizia kwa kicheko cha zarau,
"nae Miriam alicheka ingawa hakufurahia maneno hayo ila ilibidi ampe ushirikiano mwenzake.
Baada ya kula Anitha alikua wa kwanza kueda bafuni,
"sasa nisome ile barua" Miriam alijisemea huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa zile karatasi mbili akaziunga tayari na kuanza kwa makini.
Dear,Miriam.
Natumai unaedelea vizuri mpenzi wangu Miriam,mimi tokea ile siku nimekuja kwako ndo nikapigwa na mama yako hadi leo nimekua silali wala sili chakula kwa ajili yako hata shuleni siwezi tena kusoma kwani nakupenda sana na wewe umekataa kunipenda,sasa naomba nikuambie tena nakupenda sana naomba nikubalie nitakupa pesa kwa sababu baba yangu ni tajiri na mama yangu ni tajiri.Hata usiku nakuona ndotoni unanijia hadi natamani kukugusa mwili wako ila nashtuka,hivyo naomba tu unikubalie niwe mpenzi wako ili niwe na raha maana hata saivi nilikunywa maji kwenye glasi nikakuona sasa nateseka sana moyoni,Miriam ukinikubalia nitakuja kulala na wewe nikufanyie kama wafanyavyo wacheza tamthiliya za kifilipino kwani nafurahi sana pale wanapokumbatiana na kutomasana sehemu mbali mbali za mwili huku wakipigana mabusu kila mahali.Miriam naomba nikubalie jaman ila kama hutakubali basi usinichukie kwani bado nina nia ya kukusaidia kurudi nyumbani.Ukimaliza majibu yaandike nitakuja siku ingine hapa ndo unipe au unitafute kwenye namba ile ya simu niliyokupa natumai unayo.Nakupenda sana Miriam I LOVE YOU Mwaaaah.
Wako nikupendae,
Genes.
Hayakua maneno mengi sana hivyo aliweza kumaliza kabla hata Anitha hajarudi.
"mungu wangu jaman hii barua imetoka wapi na kwa nini niliiokota mazingira yale tena ikiwa kama imetupwa vile mbona nashindwa kujua" Miriam alijisemea huku akijizungusha zungusha kwenye godoro kwani tokea azaliwe alikua hajawahi kuandikiwa maneno mazuri kama hayo tena kilichoyafanya yakawa mazuri ni kwa vile alijua imetoka kwa Genes mwanaume wandoto zake, hapo hadi alijihisi kuloa baadhi ya sehemu za mwili wake kwa furaha aliyoipata ingawa alishindwa kujua kwa nini itupwe mazingira yale?
"labda aliniona nikija ndo akaitupa ili niokote?ila hapana mbona karibu hapakua na mtu ?na kama aliitupa ili niokote aliitupa lini mbona inaonekana imechafuka kidogo pia inaonekana haijatupwa siku hiyo.
Miriam alifurahi sana hapo akatoa kitambulisho katika pochi ya Genes na kuibusu mara tatu huku akitoa machozi ya furaha kwani tokea avunje ungo ndo aliskia hisia zimempanda hadi kumloanisha nguo ya ndani,
"huyu mwanaume nampenda jamani ila yeye sijui kama ananipenda au la maana mara anaacha pochi yake chumbani naikuta mara anatupa barua njiani naipata sasa kwa nini anafanya haya ? na je anakua na uhakika gani kama mimi ndie nitakaeipata ?" Jaman mme wangu Genes nakupenda"Miriam aliongea huku akirudisha barua kwenye mfuko wa koti na pochi akaificha kwenye nguo ya ndani kwani nguo yake ya ndani ilikua yakumbana hivyo haikua shida pochi kukaa sawa mahali hapo kwani aliamini ndipo mahali salama,
"hawa wanawake wanajiita watoto wa mjini wanaopenda pesa zaidi ya utu hawachelewi kuzichukua" Miriam alijisemea aliposkia vishindo vya Anitha akitokea bafuni.
"haya ndoo hiyo hapo mimina maji hapo jikoni bafuni ni nyuma ya chumba hicho hapo cha mbele" Anitha aliongea huku akimwelekeza mahali bafu ilipo.
Miriam alivua nguo na kujifunga kaka kisha kumimuna maji jikoni
"Miriam una viziwa mchongoma wewe mwanaume gani atavinyonya ?" Anitha aliuliza kwa uchokozi,
"heee mamae vina mwenyewe wakuja kuvimeza kabisa" nae Miriam alijibu kwa furaha,
"yule dogo mwenzako unamwita sijui Genes?"Anitha alizidi kuuliza,
" haswaaa kama ulikuepo vile"Miriam alijibu kwa kuringa huku akimwonesha Anitha maungo yake yalivyoumbika kwa kuchezesha kiuno kwa kumringishia Anitha kisha kutoka na maji na kuenda bafuni.
"ila ukae makini hiyo bafu haina bati kwa hiyo ukiweka sabuni hapo juu watapita nayo njia" Anitha aliongea kwa sauti,
"Powa dada" Miriam alijibu nae kwa sauti akiwa anasukuma mlango wa bati ili aweze kuoga.
Kama kawaida yake ya kujijali kiafya basi alianza kwa kumwaga maji bafuni ili kuua baadhi ya bakteria,
"sina baba wala mama mjini hivyo lazima nijitahidi kujikinga na haya magonjwa kwani nikija kushikwa na haya wanayoita sijui UTI na mengineyo hadi nije kupata msaada ni mbali sana"Miriam alijisemea kwa kujijali na kuanza kuoga.
Anitha alibaki chumbani ila hapo akapata wazo,
"hivi kwenye mfuko wa koti la Miriam kuna nini? maana hawa watoto wanaweza kua na fungu ila wakawa wanakuchora" Anitha alijisemea huku akilivuta koti la Miriam na kuanza kulipekua,
"haa kweli huyu mtoto siyo barua hii kaletewa wapi duh, hebu ngoja niisome Anitha aliongea huku akiunganisha vipande viwili na kuanza kusoma.
"Jamani huyu dada Anitha ananambia ana wanaume sita tena wazito kipesa sasa mbona maisha yake ni ya chini tu,au wanampa hela yeye anapeleka wapi, chumba chake hakina hata kitanda jaman simcheki ila kwanini anakubali kujiumiza sehemu zake za siri bure ? maana hata wasomi wanakwambia kama biashara unayofanya haikulipi basi achana nayo" Miriam alijisemea kimoyomoyo kwa kumhurumia dada Anitha kwa maisha anayoishi,
"ila ngoja nitaenda kuongea nae maana anaonekana ni mtu anaependa maongezi tushauriane namna ya kutumia mishahara yetu kwa kuifanya izalishe pesa nyingi" Miriam alijisemea akipiga hatua za madoido kwani hakutaka anapotoka bafuni achafuke hata kidogo.
"Dada nishamaliza kumuoshea Genes tunda lake" Miriam aliingia ndani na kuanza kuongea utani ila kwa wakati huo Anitha hakumjibu kitu zaidi ya kumkazia jicho,
"We dada Anitha unataka kusema mwanaume kakuuzi unaniletea hasira hadi mimi?unaloo" Miriam alizidi kuongea utani wa kumchokoza Anitha ila alishangaa Anitha kuzidi kumkazia jicho.
Miriam alipomwangalia Anitha mkononi alishtuka kumuona na vile vipande viwili vya karatasi ambavyo vilikua na ujumbe kutoka kwa Genes..
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"yaani hii barua imekujaje hapa ndani kwenye mfuko wa koti langu?" Anitha alimuuliza Miriam kwa hasira,
"hapana dada Anitha hiyo barua kwa kweli nimeiokota tukiwa njiani kuja huku na hadi mwenyewe sijaielewa ila atakua yule mchumba wangu Genes" Miriam alijibu huku akionesha uso wa kusononeka sana.
Baada ya Anitha kuelezwa jinsi Genes alikwishawahi kumpa Miriam namba ya simu kipindi cha nyuma basi aliamini kweli barua imetoka kwa Genes ila je kwa nn ipatikane kwenye mazingira yale?.
"Waliandaa kitanda na kujilaza ila kwa kua walikua wawili hivo usingizi ulichelewa kwa sababu walianza utani wao kwa Anitha kuanza
" kwa hiyo Miriam una uhakika Genes atakuoa ?"
"ndio dada lazima atanioa tu,nitajitahid kumtunzia tunda lake lisije guswa na nyoka"
"kwa uchumi gani Miriam mdada mzuri kama wewe hustahili kuolewa hata siku moja kwani wanaume umekosa Miriam yanini kuenda kunyimwa uhuru bure"
"hapana dada Anitha mimi lazima nitaolewa na Genes kwa maana maisha huwa yanabadilika mfano mimi nakumbuka nikiwa mdogo mama yangu alishawahi kuumwa malaria kwa mda mrefu ila kwa kua alikua na mume basi mume ndie alietupikia na kumuogesha mama pamoja na uangalizi wake tu kwa mama ulikua mkubwa sasa kama mama yangu angekataa kuolewa angesaidiwa na nani wakati wazazi wake walishafariki na ndugu zake wote wapo na familia zao ? nisikudanganye dada Anitha vijana tulio wengi tunaringia uwepo wa wazazi wetu na ndugu zetu ambao hawajaanza maisha na familia zao kwani kila mtu akiwa na familia yake hataweza kuja kukusaidia kama mpenzi wako, pia hata ukizeeka watoto wako watakuangalia je sasa usipokua na mtoto nani atakuangalia?".
Miriam aliongea maneno mengi zaid ambapo mwisho alipouliza swali hakujibiwa zaidi ya kuskia Anitha akikoroma kwa mbali kuashiria usingizi umechukua.
Baada ya Miriam kuona Anitha amelala basi Miriam aliichukua ile barua na kuweka chini ya mto wake huku mawazo yote yakiwa ni kwa jinsi gani atamuona Genes wake.
******
"dada Anitha amka tuwahi kazini" ilikua saa kumi na mbili asubuh ambao ndio mda Miriam aliozoea kuamka kipindi akiwa mpishi hivyo akamwamsha Anitha,
"alaa! na wewe Miriam ndo wenge la kazi au yaani nahisi umelala macho" Miriam alijibu huku akijigeuza na kuweka sawa nguo yake ya kulalia ambayo kwa mda huo ilikua imeacha mapaja wazi,
"Mmh, huyu dada Anitha ana sura mbili nini mbona naona mguu unang'aa hadi gizani ila mapaja mbona meusi?"Miriam alijiuliza moyoni,
"ahaaa ni yale mafuta yanayochubua mwili jaman itakua kajipaka huyu dada na wakati niliskia yana madhara mengi sasa huyu anaweza kosa hata uwezo wa kuzaaa mtoto kwa kuathiriwa na haya madawa" Miriam alijisemea moyoni huku akivaa koti kubwa ili aweze kutoka nje kwani aliona kukaa kitandani zaid ni kujichosha tu bure.
*********
Genes nae aliona mapenz ni kitu cha ovyo hivyo aliamua kutulia shule na kusoma kwa bidii na hapo ndipo alipoanza kurudi katika hali yake ya zamani.
********
Baada ya miezi miwili tayari Miriam alishakua na hela za kuanza kupangisha chumba na kujitegemea kulipia kodi kwani mshahara wake alituumia vizuri na hapo tayari alishaanza ufugaji wa kuku kwa kutumia ile pesa ya Genes aliyoiacha kwenye pochi kwani aliona kukaa nayo tu nikuweka hela chini hivyo alifanya vile ili izalishe ila hakuacha utani wake kazini awapo na Anitha,
"dada Anitha leo umekuja kazini na hasira kwa nini au kuna mwanaume kakuamsha vibaya kama kawaida yako?"
"acha tu Miriam yani kuna mwanaume alikua ananilipia kodi sasa saivi kagoma kanambia eti simridhishi hivyo kama hatalipa kweli siunamjua yule mzee Kimario mwenye nyumba atanitoa ndugu sijui nitakuja kwako unihifadhi" Anitha alijibu kwa majonzi makubwa kwani hakuamini kumuona Miriam aliempokea mjini akiwa tayari anajitegemea kodi mwenyewe,
"tena alikuja me nikilala chini lakini yeye analala kitandani na mimi bado najilaza chini,itakua mkosi" Anitha aliendelea kuwaza kimoyomoyo huku akiinamisha kichwa chini,
"dada Anitha ila me sinilikuambia hawa wanaume ukiwategemea sana unaweza kufa masikini ?"Miriam alimwambia Anitha huku akimwinua kichwa alichokua amekiinamisha chini,
"mdogo wangu maisha haya naona nishakosea tayari" Anitha alijibu kwa aibu
"apana dada bado hujakosea na pia bado hujachelewa sana unaweza jirekebisha na kuja kua na maisha mazuri tu"Miriam alijibu kwa sauti ya kumtia mtu moyo,
"kwa kweli mdogo wangu nimejichezea sana kama ni starehe nimefanya sana na waume za watu saingine nimekua nimekua nikiwadharau hadharani wake za mahawara wangu saivi nahisi dunia inanicheka"Anitha alimjibu Miriam huku machozi yakianza kumtoka,
"hapana dada kikubwa ni kumuomba mungu akusamehe na uweze kuacha tabia hiyo na hapo utaanza kuona mafanikio ya kazi", Miriam alimpa Anitha moyo na hapo Anitha aliinamisha kichwa chini na kuanza kumlilia mungu amsamehe kwa aliyofanya mabaya,
" wewe ni dada angu kabisa siwezi kukuacha ukiteseka kwani umenipa malazi kwa mda na kunionesha upendo na sitosahau utani wetu tukianza kutaniana jaman" Miriam alisema hayo huku akiingiza mkojo kwenye sidiria na kutoa shilingi elfu hamsini na kumkabidhi Anitha kwa ajili ya kuenda kulipia chumba.
Miriam aliweza kujipatia pesa nyingi kwa sababu ya uchapaji kazi wake kwa moyo kwani hata mwenye hotel alipokuja na kumuona anavyopambana hakusita kumuita pembeni na kumpa kitu kidogo na kwakua Miriam hakupenda starehe basi alitunza fedha kuliko kitu chochote na wakati huo alizidi kupedeza tu kwani alichomoza chuchu zake na kiuno kilikua chembemba huku akiwa na mguu wa saizi wenye weusi wa asili na ulaini wa mafuta ya mgando hakika kila mwanaume alitamani kumuoa pia kwa heshima aliyokua nayo mzee Massawe mwenye hotel alizid kumpeda na hadi siku moja alimuita ofisini kwake na kumuambia,
"hakika mwanangu uchapaji wako kazi unakufanya uje kimiliki hotel kama yangu na zaidi"
"aaah boss na wewe kwa utani, nambie kazi gani umeniitia niifanye maana kuna mashuka nimeloweka nataka nifue kabla jua halijatoka" Miriam alijibu kwa kucheka kwani ashazoea boss wake kumtania mara kwa mara,
"hapana mwanangu sijakuitia kitu kingine, nenda kaendelee na kazi ila tambua siku moja utaja miliki biashara kubwa sana" Mzee Massawe alisisitiza,
"haya boss ngoja me niende kuyafua haraka maana tukikaa hapa ofisini wewe unanitania tu", Miriam aliongea huku akiinuka na kuwahi kufua.
*** ******
Baada ya miaka mitatu Miriam alikua kashaendelea zaidi ila wakati huo alikabidhiwa kitengo cha kukagua usafi wa kila kitu hapo hotelini, na bado mawazo yeke yote yalikua juu ya Genes,
"nitakufa na usichana wangu kuliko nitembee na mwanaume mwingine" Miriam alijisemea akiwa nje ya hotel a kukagua mazingira yakoje.
Ghafla alishtuka kuona mtu kwa mbali,
"yule sio Genes kweli ?" Miriam alijisemea huku akisugua macho ili aweze kuona vizur kwani hakuamini macho yake.
Baada ya Genes kuweka pembeni mapenzi na kuzingatia masomo alifanikiwa kuhitimu masomo yake ya msingi nakufaulu kujiunga katika shule ya sekondari ya Arusha iliyokua ikijulikana kwa umaarufu Arusha sec,ambayo ni shule aliyosoma waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa na wengineo kwani ni shule kongwe sana.
Genes alipoanza kidato cha kwanza ndipo alipoanza tena kuwaza mapenzi kwani aliona wanafunzi wakike walivyovutia kwani wengine walivaa sketi juu ya magoti na wengine walijipaka mafuta ya kujing'arisha nyuso zao nakuonekana walaini kama watoto wadogo.
"hakika sekondari sijui kama hawa watoto wanasoma" Genes alijisemea baada ya kuona mdada mmoja wa kidato cha pili akiongea na simu chooni.
Genes aliendelea kusoma kwa bidii na katika mitihani ya muhula wakwanza alikua wakwanza kwa alama kubwa kitu kilichompa umaarufu shuleni hata wanafunzi wa vidato vya juu kumfuata kwa ajili ya kusomea nae.
"Genes mbona we unafaulu sana darasani" Genes aliulizwa swali na msichana wa kidato cha pili aitwae Angel,
"kwa sababu nasoma kwa bidii pia napenda kuuliza maswali darasani" Genes nae alijibu kwa ucheshi,
"yaani nataman niwe kama wewe" Angel aliongea kwa tabasamu huku akimuonesha Genes mwanya wake wa wastani na kwa kua walikaa kwa kuangaliana basi Genes alijikuta akimkagua kila kitu kwa mbele ambapo alianzia paji la uso akafurahi kuona mwanya na na meno masafi meupe,lips nyekundu zisizo hitaji make up, shavu pana kiasi.Alihamia kifuani akafurahi kuona Angel akiwa na maziwa madogo yaliyosimama na kuchongoka vizuri ukizingatia na shati alilovaa kuyaonesha vizur ila ghafla Genes alishtuka kuona Angel alipandisha sketi yake na kuacha mapaja wazi,
"mmh huyu ni malkia au binadamu" Genes alijisemea baada ya kuona mapaja meupe yaliyoendana na nguo aliyovaa ndani yenye rangi ya pinki.
Hapo Genes alishindwa kuendelea kuangalia ikabidi arudishe macho yake usoni kwa Angel na hapo Angel alizid kumchanganya Genes kwa kuonesha tabasamu zaid huku akipenyeza ulimi wake wenye kidoti cha rangi nyeusi kwa mbali kwenye lips zake.
Genes alisisimka mwili wote na hapo alikumbuka filamu za kizungu mwanamke anapomwonesha mwanaume ulimi hivo mwanaume humfuata na kumbusu ila kwakua walikua darasani basi Genes alibakia kula kwa macho,
"ama kweli kuna wanawake huku duniani, sasa yule Miriam kitu gani mweusi kama mkaa ?" Genes alijisema huku Angel akisimama tayari kuondoka kuelekea darasani kwake kwani mda wa mapumziko uliisha ila alipoanza kutembea na Genes kuangalia jinsi Angel alivyokua na makalio mazur yaliyobinuka basi Genes aliita,
"we Angel"
"abee" Angel aliitikia kwa heshima huku akimsogelea Genes kiasi cha baadhi ya viungo vya Angel kumgusa Genes,
"aise ukitembea una makalio mazuri yanadundika kinoma" Genes aliongea kwa utani,
"Uzuri wa nyumba choo eti" Angel alijibu kidogo kwa uso wa aibu na kugeuka kuelekea darasani kwake, hapo alizidisha manjonjo ya kutembea, kwani aliamini tayari ashamteka Genes akili yake na atafanikiwa kutimiza kazi aliyopewa na marafiki wa Genes waliokua na wivu wa kuongoza kwake kiakili darasani hivyo waliamini wakimtumia mwanamke wakumteka atajisahau na kudorora.
*******
Ilipita mwaka na nusu bila Genes kumuonesha Angel kua amempenda ingawa bado Angel alizid kumtega kwa kila njia ila Genes aliogopa sana kujihusisha na masuala ya kupenda kwani alihisi yanaweza yakaja kutokea kama ya Miriam.
Alipofika kidato cha tatu huku Angel akiwa kidato cha nne basi akina Genes katika somo la biology walifika mada ya Human Reproductive System (mfumo wa uzalishaji wa binadamu) ambapo kila mwanafunzi alitega sikio kwa makini ili kusikia jinsi mwalimu alivyoongea mambo ya wakubwa nao wanafuzi wa kike walikaa makini kusikiliza jinsi ya kujikinga na mimba zisizotarajiwa kwa kuzingatia kalenda iliyochorwa ubaoni ikieleza namna ya kuzingatia mzunguko wa hedhi,
"dah kumbe ni rahisi hivi namimi nitajaribu kufanya maana yule boy wangu ananisumbua tufanye kila siku nambania kuogopa mimba ila saivi nitakua nazingatia huo mchoro"
"aaah mimi boy wangu hatakagi kutumia kondom ananilazimisha tuende kavu kavu nambania ila saivi naanza kumpa kavu ili afurahi kwani nitakua nazingatia hili duara vizuri".
Hayo yalikua baadhi ya maneno ya watoto wakike baada ya mwalimu kutoka darasani wengine ambao hawajawahi kujaribu kufanya mapenzi basi walitamani kuanza kufanya kwani walipatwa na mvuto fulani kuhusu mada hiyo.
Genes pia aliingiwa na ile mada kichwani na kukumbuka miaka minne iliyopita alivyoota akiwa amelala na Dany alivutiwa sana na kitendo cha mwanaume kutoa shahawa na akawaza kujaribu nayeye kuonja penzi.
"Leo mmesoma ule mchoro pale ubaoni?" Angel alimuuliza Genes alipoingia darasani kwake,
"ndio tumesoma" Genes alijibu huku akifunika kitabu chake alichokua akisoma,
"vipi umeionaje hii mada" Angel aliuliza kwa tabasamu kama kawaida yake,
"aise kwa kweli hii mada ya reproduction ni nouma sana" Genes alijibu kwa uso wa aibu,
"hata sisi kipindi tunaisoma tulifurahi sana tena mwalimu wetu alitufundisha kipindi cha likizo kwa kutuchangisha hela kwa sababu alijua atapata pesa nyingi maana wanafunzi wote waliipenda sana" Angel aliongea huku akizidi kusogea karibu na Genes hadi wakakaa kwa kugusana,
"wewe Angel usinisogelee hivo bhana unajua unanipandishia stem ?" Genes alimnong'oneza Angel,
"mimi mwenyewe stem zimenipanda mbona kitambo" Angel nae alijibu kwa kunong'oneza,
"basi ngoja tutajua cha kufanya" Genes aliongea kwa sauti ya chini na hapo kengele iligongwa kuashiria mda wa mapumziko umeisha hivyo Angel alinyanyuka taratibu na kurudi darasani kwake.
********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Aise Genes huu mlupo ni wako nini maana naona unauimbisha zaidi ya mwaka sasa" Genes aliulizwa na rafiki yake aitwae Jesophat,
"wala mwangu huyu demu ananishobokea kichiz yani,ila saivi nataka nimuwekee heshima maana nikimuacha hivo anaweza enda nitangaza kwa wanawake wenzake kua mimi ni bwege" Genes alijibu,
"ila mwangu angalia maana hivi vident vizuri vizur hapa skuli vinatoka na waalimu sana sasa ukija kugonganishwa na master lazima ufukuzwe shule man siunajua tena hiki kidemu kina mashauzi sana kila mtu maarufu hapa shule anamshobokea hata yule mcheza mpira maarufu wa kidato cha pili naskia anatoka na huyu demu tena hivyo kaa makini man" Josephat aliongea kwa kumshauri rafiki yake,
"sawa Jesophat nitakaa makini kwani mimi sitacheza peku" Genes alimjibu rafiki ake,
"powa leo nataka tupite maeneo ya stand aise nikanunue mkanda kisha tupandie gari Mianzini" Josephat alimuomba Genes kampani,
"Ahaa mwangu ule mtaa mimi sipiti kabisa maana kuna msala ulinipata nikiwa nasoma la sita pale hotel Aquline, hivyo mimi sitofika kule,
"haina kwere mkuu wangu wewe kama unapaogopa hotel Aquline basi utapitia hii road ya kaloleni tukakutane pale corner Florida" Jesophat aliongea huku akimwelekeza njia atakayopitia ili asipite pale Aquline.
********
"Samahan kaka",
"bila samahan ",'
"nilikua nimekufananisha",
umenifabanisha na nani maana nilikuona kwa mbali unanitazama tu",
"nimekufananisha na mwanaume mmoja anaeitwa Genes"
"Genes yupi? kwani wewe ni nani?"
"Mimi naitwa Miriam huyo Genes nilijuana nae kipindi cha nyuma sana ila nina picha yake hii hapa" Miriam aliongea huku akitoa kitambulisho cha Genes chenye picha ya passport ambayo Jesophat alishangaa kuona,
"ahaa mimi pia naitwa Josephat, hiki kitambulisho umekitoa wapi maana huyu jamaa namjua nasoma nae tena ni rafiki yangu sana" Jesophat aliongea kwa mshangao,
'sasa nitakupa zawadi yako kama kesho utanipitia hapa jioni nikupe ujumbe wake' Miriam aliongea kwa furaha,
'sawa nitapitia hapa sema sasa wewe mida kama hii utakua wapi?au ni hapa hapa utakua?"Jesophat aliuliza,
"ndio nitakua hapa hapa we pitia nitakuona" Miriam alijibu kwa furaha,
"sawa sawa" Jesophat alijisemea huku akiagana na Miriam.
Jesophat aliongeza mwendo ili kuenda kumpa Genes taarifa kwani aliamini mda huo Genes atakua Florida akimsubiria kwani alikuwa amegoma kupitia hotel Aquline.
"itakua huyu demu amemfanyaje?Jesophat aliwaza baada ya kumuona Genes akimsubiria kwa mbali.
"Waaoooooooh! dada Anitha yaani mungu ananipigania kila kukicha na nilikuambia lazima Genes atakua mume wangu tu" Miriam aliongea huku akirukaruka baada ya kumfuata Anitha aliyekua mapokezi,
"nawe Miriam mbona mara nyingine unachizika mwenyewe" Anitha alimjibu huku akimtuliza kwani Miriam alikua anarukaruka kwa furaha.
"apana dada sio ukichaa bali nimefanikiwa kumnasa tena Genes niliejua ashanipotea ila nimefanikiwa kujua namna ya kumpata" Miriam aliongea kwa sauti iliyoandamana na mihemo mikubwa,
"kivipi Miriam sikuelewi maana huyo Genes wazaidi ya miaka mitatu leo umempata wapi?"
"we dada Anitha usiku wa leo itabidi uje kwangu unisaidie kazi moja tu" kutokana na Miriam kutojua kusoma na kuandika vizuri alimuomba Anitha msaada wa kuja kuandika barua ya kumpeleka Genes.
*******
"mmh nawe Genes kiwembe kweli kweli aise kama unamiliki tena hiki chuma cha mjapani nilichokutana nacho hapo Aquline" Jesophat aliongea huku akitabasamu kwa kumsifia Genes,
"kivipi man?" Genes aliuliza kwa mshangao,
"ngoja kesho nisubirie huo ujumbe wako,maana kuna kademu fulani keusi hivi wanaita black beauty aise hapo Aquline kakanambia kanakujua hadi kitambulisho chako cha shule ya msingi kanacho,alafu naona kavaa sare ya uhudumu wa hapo hotelini kanambia kesho nipitie hapo anipe ujumbe wako" Josephat alimuelezea Genes kila kitu na jinsi Miriam alivyomuita,
"achana na huyo kahaba tu bhana anajiuzaga hapo nae anataka kuniua mimi, temana nae wala usihangaike kumpitia hapo maana nitaja mzibua bure" Genes aliongea baada ya kuelezewa,
"apana man ila kako powa kama Nick Minaj,yaani anamzidi Angel sema Angel mweupe tu" Josephat aliongea kumsifia Miriam,
"eti Nick Minaj," Genes alimjibu Jesophat kwa kumzarau Miriam.
Baada ya Genes na Josephat kukubaliana kua wasihangaike na Miriam yeye Jesophat alitaka kujua ni ujumbe gani Miriam anataka kuutuma kwa Genes,
"lazima nimpiteia huyo msichana nione ni ujumbe gani" Josephat aliwaza kisha kuagana na Genes kwani walifika njia ya kutawanyika kila mtu kuelekea nyumbani kwake.
*******
"Sasa yani nataka unisaidie kumuandikia huyu mpenzi wangu barua moja hiyo hadi akisoma aniote usiku" Miriam alimwambia Anitha huku akiwa na uso wa aibu kwani alijidharau mwenyewe kwa kutojua kuandika vizuri,
"haya nitakusaidia best, maana nyie watu mnasema mmekufa macho eti hamuwezi kuandika ila kuhesabu pesa mbona hamtuambii tuwahesabie" Anitha nae aliongea utani huku akichana karatasi katika daftari la Miriam alilotumia kuandikia mapato na matumizi yake kwani aliandika hata hela ya maji aliyonunua kwa siku,
"sasa mimi nitaandika nini au wewe ndio utasema mimi niandike tu" Anitha aliuliza
"Ndio mimi nitakuambia cha kuandika ila kwanza hebu jaribu kuandika (mama anapika chakula kitamu) ili nione mwandiko wako kama una mvuto" Miriam aliongea huku akicheka na hapo Anitha bila ubishi aliandika,
"ndio ila uongeze bidii kidogo" Miriam aliongea kwa kuridhishwa na mwandiko wa Anitha,
"sasa siunajua hatua za uandishi wa barua?" Anitha aliuliza huku kalamu ikiwa tayari kuanza kazi,
"we hapa hakuna cha kufuata kanuni za uandishi ila cha kuzingatia ni uandike nachokwambia mimi,kwani siataelewa?" Miriam aliongea na kuanza kutamka maneno ambayo Anitha alikua akisikiliza kwa makini na kuandika na maneno hayo baada ya kuandika yalisomeka hivi,
Kwako mpenzi Genes,
Natumaini wewe ni mzima wa afya na unaedelea vizuri na shughuli zako ikiwemo masomo.
Napenda kukujulisha bado upo moyoni mwangu na pia nakutunzia penzi lako la dhati lililopo ndani ya nafsi yangu japo tumeonana mda mrefu ila bado upo kichwani mwangu hadi siku tutakayofunga ndoa na kuishi wote milele nakuahidi hakuna mwanaume nitakayempenda zaidi yako nishaapa kufa na usichana wangu kuliko niishi na mwanaume mwingine zaidi yako Genes,we umekua zaidi ya mwanga moyoni mwangu kila napokuwaza napata moyo wa kufanya kazi kwa bidii.pia nataka nikuone kuna ujumbe wako mwingine ambao nadhani utafurahi sana kuuskia.
Genes sijui nikulezeje juu ya upendo wangu kwako ila napenda kukujulisha tu usome kwa bidii kwani mimi sikubahatika kupata elimu kama wewe ila najitahid kufanya kazi kwa bidii.Mpenzi wangu zingatia sana masomo ya hesabu maana nina hasira yakupambana hadi nije kua na mahoteli mengi wewe uwe mkaguzi wa mahesabu hivyo ndani ya bahasha hii naweka elfu ishirini ununue nayo kitabu cha hesabu kama zawadi kutoka kwangu.Mimi nipo katika ile hotel tuliyokutana miaka mitatu iliyopita na saiv nafanya hapo kazi kama mkaguzi wa usafi wa mazingira na vyumba.Pia ukiwa shule nakuomba ujiepushe na wasichana wenye nia mbaya na wewe kwani wengi wao hawana mapenzi ya dhati kwako tambua mimi nipo kwa ajili yako na nitajitunza na kuliheshimu penzi langu kwako.
Wako nikupendae,
Miriam.
"haa mtoto wewe unatoa wapi maneno haya yote?" Anitha aliumuuliza Miriam ambae kwa mda huo alikua analia kwa hisia kali,
"ichore zile alama za upendo basi" Miriam alimsihi Anitha,
"Ah zile ni za watoto hii inatosha" Anitha alijibu na kumkabidhi Miriam barua yake.
Miriam aliichukua na kuikunja vizur kisha kuchukua bahasha na kuweka huko elfu ishirini kisha kuifunga vizuri pia hakutaka kumwambia chochote kuhusu kuokota pochi yake kwani alihofia Anitha kujua masuala ya pochi.
"Haya sasa dada Anitha kumekua usiku nami ushamaliza kazi yangu nkupe zawadi gani?" Miriam alimuuliza Anitha,
"hapo Castle lager mbili tu" Anitha alijibu kwa furaha kwani siku nyingi hajaonja tokea Miriam amshauri kuachana na masuala ya kugawa mwili wake ili apewe bia hivyo alikua na kiu sana,
"jaman dada pombe nilikuambia acha kabisa,mimi nakupa mtetea mmoja ukamfuge" Miriam alimjibu kwa huzuni,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sina banda la kufugia jaman mdogo wangu" Anitha alijibu kwa aibu,
"we njoo nkuoneshe kuku wako alafu tufanye utaratibu wakutengeneza banda" Miriam aliongea huku wakielekea kwenye banda la kuku,
"unamuona yule mweupe pale tena ashaanza kutaga mayai mawili utachukua vyote na nitakupa jogoo pia huyo mwekundu hapo" Miriam aliongea huku akielekeza kidole kwa kila kuku aliyemtaja,
Baada ya Miriam na Anitha kuagana basi Miriam alirudi chumbani kwake akaandaa chakula baada ya kula akalala huku barua ikiwa chini ya mto akisubiria kesho yake kwa hamu kubwa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment