Search This Blog

Friday, November 18, 2022

KAZI ZA NDANI NCHINI OMAN ZILIVYONIKUTANISHA NA KIFO - 4

 






Simulizi : Kazi Za Ndani Nchini Oman Zilivyonikutanisha Na Kifo
Sehemu Ya Nne (4)




Nikashika uelekeo wa upande wa kusini mwa hosptali ile, nikawa nakimbia huku nimejifunika shuka jeupe.

Lile shuka jeupe la mochwari lilinifanya nizidi kufanana dhahili na mzimu, nilikimbia nikiwa nimechanganyikiwa vibaya sana, katika kukimbia huku na kule nakajikuta nimetokeza upande wa nyuma wa hosptali ile, eneo lile kulikuwa na bustani ya mauwa iliyopandwa kiusatadi, bahati nzuri lilikuwa ni eneo ambalo halikuwa na mtu yeyote.

Kando ya mauwa kulikuwa na pipa la kuhifadhia takataka, nikaamini hapo ndiyo maficho sahihi kwa wakati ule, nikafunua mfuniko na kutumbukia ndani ya pipa lile kisha nikajibanza humo.

Nilikuwa nimejikunyata huku nikitweta, nafsi yangu ilikiri kuwa nilikuwa ni kama mwanakondoo aliyezingirwa na kundi la mbwa mwitu. Sikutaka kujiongepea kama nikikamatwa tena, nitanusurika kifo kama ilivyo tokea siku hiyo.

Tukio hilo lilinifundisha jambo kubwa kuhusu ukuu wake baba wa mbinguni. Mungu acheni awe Mungu jamani, utukufu na sifa anastahili yeye. Kama yeye hajakukadiria jambo fulani, hakuna pigo litakalo kuangusha daima. Jifunze hili ndugu msomaji.



Uhai wangu ulikuwa mashakani, niliamini kama nitaingia kwenye mikono ya serikali ya nchi ya Oman kamwe hawawezi kuniacha nikiwa hai, niliendelea kuamini kuwa endapo nitatiwa nguvuni jeshi la nchi hiyo liitahakikisha ninanyongwa hadi napoteza uhai wangu.

Kiu ya kuwa mtu huru ilizidi kutanda kwenye fikra zangu, shauku ya kurudi nyumbani Tanzania ilipozidi kutekenya hisia zangu.

Nilikaa ndani ya pipa lile la takataka kwa makisio ilikuwa ni zaidi ya masaa saba ama nane, eneo lile liliendelea kuwa kimya, sikusikia michakacho wala chakarachakara yoyote.

Nilijinyanyua taratibu na kuchungulia, nilishangaa nilipona giza lilikuwa limeingia, nikajivuta na kuruka nje ya pipa lile. Nitembea kuelekea gizani. Wakati napiga hatua ya kwanza ya pili, nikabaini jambo jingine lisilo la kawaida mwilini mwangu.

Njaa kali ilikuwa ikiniuma, nikagundua nilikuwa nina muda mrefu sijapata chochote, na nilikuwa sina nguvu, kukaa sana kwenye jokofu kukanifanya niwe na kiu cha maji.

Hata hibyo sikutaka kuwaza sana juu ya njaa niliyo kuwa nayo, nilichokuwa nahitaji ni kurudi nyumbani kwetu Tanzania.

Akili yangu nikairejesha kwenye kujinasua kuingia kwenye mikono ya serikali ya nchi ya Omani. Nafsi yangu ikakiri kuwa hatua ya kwanza ya kuwa mtu huru ilikuwa ni kutoka nje ya hosptali ile.

Nikawa natembea kwa kupepesuka lakini kwa umakini wa kutooenekana na mtu yeyote, mwilini nikiwa nimejifunika lile shuka nililotoka nalo mochwari, nilitokeza kwenye eneo ambalo lilinipa faraja zaidi, nikaona kwa kutokea eneo lile ni hatua nyingine muhimu ya kunitoa ndani ya hospitali.

Ilikuwa ni eneo la kufulia nguo na nguo nyingi zilikuwa zimeanikwa katika kamba.

Nilinyata na kuanua gauni moja na mtandio, upesi nikavaa gauni lile na kujitanda mtandio kisha nikatoka nikiwa natetemeka, miguuni nilikuwa peku.

Nilipishana na watu wawili watatu hapakuwa na yeyote aliyenijali na hatimaye nikatokeza kwenye geti kuu la hosptali hiyo.

Kulikuwa na wanajeshi wenye bunduki waliokuwa wamezagaa kwenye geti lile. Nilizidi kutetemeka, lakini sikuacha kujongea kuufauta mlango wa kutokea.

Hatimaye nilifika getini na kutoka nje, jasho liliendelea kunitoka huku mwili wote ukinitetetemeka, hatua ya kwanza....Ya pili...Ya tatu. Mara nikasikia sauti kali ya kiume ikiniita nyuma yangu.

“Agripina...”

Bila kufikiria mara mbili, nikageuka. lilikuwa ni kosa kubwa sana. Ulikuwa ni mtego, hapo hapo nikaona sura za wale wanajeshi zikimakanika bunduki zao wakazielekeza mbele yangu.

“Nimekwisha!!!!..”





Ndani ya sekunde chache amri kutoka kwa mwanajeshi mmoja ilitoka:

“Kamata! Huyoo ndiye yeye, msimwache akatoroka..” sikupoteza muda hapo hapohapo nikakurupuka na kutimua mbio.

“Paaaaaaa!..PAA!”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Sauti kali ya risasi ilisikika nyuma yangu, Kukazuka kizaazaa kingine , watu wachache waliokuwa eneo lile la lango la hospitali kila mtu akashika njia yake huku sauti za taharuki zikiwatoka.

Nilifahamu wazi risasi ilikuwa imepigwa angani ili kunitisha nisikimbie, nilikuwa tayari kufa nikiwa nakimbia nikijaribu kujiokoa kuliko kusimama kisha nikatiwa nguvuni kikondoo.

“Simama wee mwanamke Simamaa!!” sauti za amri zilizidi kunishurutisha. Sikujali nilizidi kukimbia kwa nguvu zangu zote, nilibahatika kuona kichochoro mbele yangu, mita kama kumi, nikaona pale ndiyo mahali sahihi pakuwapoteza wale mafala waliokuwa wakinifuata nyuma yangu kwa kasi.

Kwa mbio za farasi, nilikifikia kile kichochoro na kutokomea ndani yake, nikakutana na mazingira ambayo yalizidi kunipa nguvu ya kukimbia. Nilikuwa ndani ya makazi ya watu hohehahe kwetu Tanzania hupaita ‘Uswahilini’ Nikapita kwenye vichochoro viwili vitatu, hatimaye nikajikuta nimetokea katika eneo ambalo halikuwa na njia.

Risasi zilizidi kulindima nyuma yangu.

Nikatazama kulia kwangu nikajiona nipo katika nyumba eneo la uwani, nikaona kuna vyumba kadhaaa katika eneo lile la uwani vikiwa wazi. Nikakimbia na kuingia kwenye chumba kimoja.



Nilisukuma mlango kwa nguvu na kuzama ndani kisha nikaufunga. Kwa mwonekano chumba hicho kilikuwa kikikaliwa na mvulana wa Kiarabu. Naye alikuwemo humo ndani!.

Bahati nzuri ni kwamba, amelala fofo! Alikuwa mwanaume mrefu na mwenye nywele nyingi kichwani.

Pamoja na kwamba nilisukuma mlango kwa nguvu na kuingia ndani kwa fujo lakini mtu yule aliyekuwa amelala fofo hakushituaka!. Nilijikunyata nikiwa nahema kama nimetoka kwenye mbio za marathoni.

Ukimya wa ghafla ukashika hatamu. Sauti za risasi huko nje sikuzisikia, Nikawa najiuliza maswali mwenyewe mule ndani kama natakiwa nitoke ndani ya chumba kile nitimkie mahali pengine ama niendelee kubaki mule ndani hadi hapo mwenyeji wa chumba kile aliyekuwa akikoroma kitandani atakapo amka na kunikuta mule ndani.

Katika kuwazawaza huko nikapata wazo ambalo niliamini ni zuri. Bahati mbaya bado kivuli cha bundi kiliendelea kunifuata, kwani kabla sijalifanyia kazi wazo langu mara nikashuhudia kitu cha ajabu.

Yule mtu aliyekuwa amelala kitandani alikuwa anatoa mkoromo usio wa kawaida, nikasimama na kumtizama.

Sikuamini kile nilicho kiona.

Mtu yule alikuwa akitokwa damu puani, masikioni na mdomoni damu ile ilichanganyika na povu lililokuwa likimtoka mdomoni.

“Ngo ngo ngo...” ndani ya sekunde hizohizo nikisikia mlango wa chumba kile ukigongwa kwa nguvu!.

Nilibaki nimeganda kama sanamu, nilihisi akili yangu ikisimama kufanya kazi kwa muda, wakati nikiwa nimeduwaa mbele ya mtu yule aliyeonekana yupo kwenye hekaheka za kuipigania roho yake nikashitushwa tena na sauti kali ya mlango ukigongwa.

Hapo ni kama akili yangu ilikurupuliwa ilipokuwa imelala, nikatambua hatari iliyokuwa inaninyemelea.

“Ngo,ngo,ngo!..Open the door..” Sauti ya mtu ilisikika ikisema kwa wahaka huku akiendelea kuugonga mlango kwa nguvu, jasho lilinichuruzika maungoni mwangu, nikaona hatimaye ninaingia kwenye mikono ya serikali ya nchi ya Oman, sikutaka kujiongopea kwamba siwezi kuhusishwa na kifo cha yule jamaa aliyekuwa akiweweseka kitandani huku damu ikimtoka puani na mdomoni.

Nikaamini kabisa hilo ni jumba bovu jingine linalokwenda kuniangukia, nikajionya kama nisipofanya kitu lazima nitaingia kwenye mikono ya serikali na sikuhitaji mwalimu wa kunieleza kuwa kama nikingia kwenye mikono ya dola nini kitatokea.

“Ngo,ngo,ngo...”

Mgongaji aligonga tena safari hii kwa nguvu zaidi, nikatizama kulia na kushoto nikaona mahali pekee pakujificha ni kuingia chini ya uvungu wa kitanda. Lakini kabla sijazama uvunguni mara mlango ulisukumwa kwa nguvu na ukafunguka.

Aliingia msichana mmoja wa kiarabu akanikodolea macho yenye mshangao kisha akayahamisha macho yake kwa kwa mvulana aliyekuwa hoi pale kitandani, nikamwona akibutwai baada ya kuona hali ya yule mtu pale kitandani.

Nilikuwa nimesimama nikiendelea kumwangalia yule dada namna alivyo taharuki kwa kile alichokuwa akikishuhudia mbele yake, nikawa makini na yule msichana kufuatilia kila tendo alilokuwa akifanya, akayatupa macho yake tena kwangu, akanitizama kwa chati kisha akasema kitu, lakini sikumwelewa kwakuwa alizungumza kwa lugha ya Kiarabu.

Ingawa sikumwelewa lakini nilibaini alichokuwa ananiuliza ni nini. Alitaka kufahamu mimi ni nani,kwa nini nipo mule ndani na nimemfanya nini mtu yule anayetokwa na damu nyingi.

Kitendo cha mimi kubaki kuwa bubu huku yeye akiniuliza maswali lukuki kilimkera vibaya sana yule msichana, nikaona anatoa simu yake ya mkononi kisha akapiga namba fulani na kuanza kuzungumza na mtu upande wa pili. Sikutaka kujiongopea kwamba haiti polisi.

Machale yakanicheza, hapohapo nikamrukia na kumkwapua ile simu na kuitupa, baada ya kufanya kitendo kile kilichofuata kilikuwa hakielezeki, tulikamatana na yule msichana na kuvingirishana huku na kule, pamoja na kwamba nilikuwa na njaa lakini niweza kumthibiti msichana yule.

Nilimvuta nywele nikamkandamiza kwa chini huku nikiwa nimemkanyaga kifuani.

“Kimyaa!! nasema kimyaa, nyau wewe nani aliyekwambia uite polisi? Umeniona mimi ndiyo nimemua huyu fala wako aliyelala hapa kitandani...Eeh?” nilisema kiwazimu nikiwa nimevurugwa vibaya sana.

Nilichofanya ni kumfunga kwa kamba mikono na miguu yake kisha nikamsachi mifukoni mwake, nikamkuta na kiasi cha fedha ambazo sikumbuki zilikuwa ni shilingi ngapi, nilizikomba pesa zote nikiamini zitanisaidia mbele ya safari, baada ya tukio hilo niliyatupa macho yangu kwa yule bwana pale kitandani. Nilichanganyikiwa baada ya kumwona mtu yule akiwa amekodoa macho huku akiwa ahemi. Mtu yule alikuwa amekwisha fariki dunia...

“Hapanifai tena hapa”

Sikupoteza muda, niliondoka mule ndani upesi nikimwacha yule binti akijizoazoa pale sakafuni, niliingia mtaania na kuendelea kukimbia, niligeuka kuwa mkimbizi katika nchi ya watu.

Nakumbuka baada ya kutoka mule ndani nilichofanya ni kwenda katika hoteli iliyokuwa mafichoni kidogo, ilikuwa karibu na pwani ya bahari, haikuwa hotel ya kitalii ila nakumbuka jina la hotel hiyo iliitwa ‘Kuruthumu’ ingawa ilikuwa ni usiku nilipata stafutahi ya chai ya maziwa na mkate wa siagi ambao kwa hakika ulijaza tumbo langu.

Na katika kipindi chote ambacho nilikuwa nikipata stafutahi ile nilikuwa nimekwishapata wazo moja ambalo niliamini kama nikiliweka katika uhalisia ni wazi litaleta matunda na kuweza kutoroka kabisa katika nchi ile na kurudi nyumbani Tanzania.



Na katika kipindi chote ambacho nilikuwa nikipata stafutahi ile nilikuwa nimekwishapata wazo moja ambalo niliamini kama nikiliweka katika uhalisia ni wazi litaleta matunda na kuweza kutoroka kabisa katika nchi ile na kurudi nyumbani Tanzania.

Baada ya kushiba nilinyanyuka na kuanza kuyafanyia kazi mawazo yangu, nilitoka na kutembea kwa mguu3 ukingoni mwa fukwe ile.



Nilifika katika wigo bandari ya Muscut, uliozungushiwa seng’eng’e. Nilisimama katika uzio wa bandari hiyo nikawa natizma huku na kule kama nitamwona mtu yeyote.

Wakati huo kwa makisio ilikuwa yapata kati ya saa nne ama saa tano usiku. Nikaelendelea kusimama kwa muda hadi badae niliposhituliwa na sauti kali iliyotokea nyuma yangu:

“We ni nani na unafanya nini?” sauti ya amri ilisikika, nilipogeuka nikamwona mtu mmoja mzee wa makamo kasimama huku akiwa amekamata bunduki aina ya ‘bolt shotgan’ Kimwonekano alikuwa ni kama mlinzi wa eneo lile la bandari.

“Naitwa Agripina, shida yangu ni kupata meli yoyote inayoelekea Afrika. Nisaidie baba yangu niko kwenye matatizo makubwa. Nitakupa chochote utakacho.”

Yule mlinzi alinitizama kwa chati tochi yake ikiendelea kunimulika, kisha akavuta pumzi ndefu halafu akasema:

“I’ve never seen you in my life but you seem like you need some help...” Aliongea kwa sauti ya kukoroma, alionekana ni mzee ambaye amekubuhu kwenye biashara za magendo.

“We have a cargo ship, Zaghol 153 which travels to Mombasa this night. Captain can take you there in one condition...” aliongea tena kwa Kingereza, akisema ipo meli ya mizigo ya, Zaghol 153 inayosafiri kwenda Mombasa usiku huu ila nahodha anaweza kunipeleka kwa sharti moja.

“Sharti lipi?” niliuliza kwa kiherehere.

“Nifuate. ”

Badala ya kunijibu yule mtu alisema huku akifunua wavu wa seng’eng’e na mimi kupita ndani ya bandari, tukanza kutembea kuingia ndani ya bandari hiyo.

Niliendelea kumfuata huku nikiwa na mashaka, nilikuwa na wasiwasi kwa sababu niliona kama jambo nililoliomba kwa mtu yule lilikubalika kirahisi mno. Machale yakawa yananicheza, nikawa njia panda, nilifikiria kwa muda mwisho wa siku nikajiambia potelea mbali litakalo kuwa na liwe. Nikamfuata.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alinipeleka hadi kwenye ofisi moja ndogo ambayo ilionekana ni kama ofisi ya walinzi waliyoitumia kwa kufanyia mambo yao ndani ya bandari ile.

“Ningoje hapa.” Aliniambie yule mzee na kunipa kiti, aliniacha pale na kwenda mahali ambako sikujua ni wapi, dakika chache badae alirejea na kunitaka nimfuate.

Nilimfuata. Swali kuu kichwani mwangu lilikuwa ni vipi mtu yule ajitoe kunisaidia mimi kiasi kile, kwa malipo gani? Kwa ushawishi upi? Na kwa huruma gani aliyonayo juu yangu mtu ambaye nimekutana naye si zaidi ya dakika ishirini.

Pamoja na kuyawaza hayo, bado sikutaka kabisa kurudi nyuma, nilitaka nishindwe nikiwa kwenye harakati za kujaribu kujiokoa kuliko kuogopa kufanya nikingoja kukamatwa kibwege.

Agripina, adui namba moja wa maisha yako ni HOFU, sauti moja kichwani iliniambia.

Safari yetu ilishia kwenye kontena moja ambapo baada ya kuingia ndani nilishangaaa nilipoona mandhali ya ndani yakiwa ni mithili ya sebule nzuri ya kisasa yenye kila kitu ndani yake.

“Anaitwa Casper ndiye atakaye kusadia kukupeleka kwenu,” alitoa utambulisho yule mwenyeji wangu.

“Sawa.”

“Mimi naondoka, mambo mengine atakueleza mwenyewe,” yule mlinzi alisema tena huku akituangalia kwa zamu.

Nilitikisa kichwa kumkubalia, alinyanyuka na kusogea kwa yule jamaa kisha yule jamaa akatoa burungutu la pesa na kumpa yule mlinzi.

Isije ikawa ndiyo unauzwa Agripina, sauti nyingine iliniambia akilini.

Tulibaki na yule jamaa aliyetambulishwa kwangu kama Casper nahodha wa meli ya mizigo ‘Zaghol 153’

Tulikuwa kimya kwa dakika nzima, hakuna aliyeanza kumsemesha mwenzake, jamaa alikuwa bize na sigara zake, akionekana kutokunijali hata kidogo. Hata hivyo nilibaki kimya nikisubiri niambiwe ni nini malipo ya kusafirishwa kutoka Muscut hadi Mombasa.

“Una mzigo wowote au ndivyo hivyo ulivyo utakavyo safari?” hatimaye jamaa aliniuliza.

“Ndivyo hivi nilivyo, sina mzigo”

“Ok, twende kwenye meli.”

Tulitoka ndani ya kontena lile na kupita katikati ya makontena mengi tukipishana na watu lukuki waliokuwa wakiendelea na majukumu yao mule bandarini.

Safari yetu ikaaishia mbele ya meli kubwa ya rangi ya kijivu, ilikuwa ni meli kubwa kama mlima. Ubavuni mwa meli hiyo kukiwa na maandishi makubwa yaliyosomeka ‘Zaghol 153’

Nilijichoma ndani ya meli ile, nikapelekwa kwenye moja ya vyumba vilivyokuwa mule ndani nikatulia mule nikingoja kupewa maelekezo mengine.

Saa tisa kamili usiku Meli ile kubwa ilipiga honi kali. Dakika chache badaye ikaanza kuondoka. Bado nilikuwa siamini kama hatimaye naweza kuiacha nchi ya Oman, nilisali na kumshukuru Mungu kimoyomoyo.

Nilikuwa nimekaa ndani ya chumba kile juu ya kitanda huku nikijiona ni mwenye furaha isiyo ya kawaida kwa kuona narejea nyumbani kwetu Tanzania.

Nikifika Mombasa, Kenya ni kama tayari nimefika Tanga, Tanzania. Siwezi kuisahau hii Oman. Nilijiambia kimoyomoyo.

Nakumbuka nilikaa ndani ya chumba kile ndani ya Meli kwa masaa mengi mno hadi usingizi ukanipitia, nililala masaa mengine mengi mno hadi nilipo amshwa na njaa kali.

Kwa mujibu wa saa ya ukutani iliyokuwa mule ndani ilikuwa ni saa sita mchana wa siku mpya. Njaa ilikuwa inaniuma mno.

Hadi wakati huo bado Casper hakuwa ameniambia ni jambo gani nitakalo stahili kumlipa kama malipo ya kunisafirisha Mombasa.



Nikiwa bado natafakari mara mlango wa chumba kile uligongwa kiustarabu, na kuvaa nguo, kisha nikauendea mlango na kuufungua. Alikuwa ni Casper.

Alikuwa amesimama sigara ikiwa mdomoni mwake, mkononi akiwa ameshika sahani lililokuwa na chakula aina ya British Beef and Ale na glasi yenye sharubati nzito ya nanasi.

“Nimekuletea chakula,” alisema huku akitoa moshi wa sigara katika tundu za pua yake. Nilipokea chakula kile huku nikitoa tabasamu lililosema ahsante kwa wema wako.

“Kula, ukishiba tutazungumza,” alisema tena Casper.

Nilikula upesi upesi, baada ya kushiba nikaketi kitako kumsikiliza yule jamaa.

“Kwa nini unakimbia Oman kwa kujificha...Umeua?” Casper aliuliza.

Swali lilikuwa kama mjeledi wa moto kifuani mwangu mate mepesi yalinijaa mdomoni nikapatwa na kigugumizi. Na hata kabla sijajibu akasema tena:

Hata hivyo siyo kazi yangu kujua kwa nini unakimbia nchi ile ya kishenzi ya Kiarabu, kazi yangu ni kukupeleka unakotaka kwa malipo ya penzi tu.”

Kwa mara nyingine nilibaki tena nimeduwaa baada ya kauli hiyo. Nilijiona ni mjinga kwa kutohisi jambo lile kama linaweza kunitokea.

Nilibutwaa baada ya Casper kuanza kunishikashika matiti yangu yaliyokuwa wima, vidogo dogo kama vipera.

Akawa ananivutia kwakwe, macho yake yakionesha ananjaa kali ya penzi. Nilendelea kuduwaa nisijue kama nilitakiwa kukataa ama kukubali.

Ningewezaje kumkatalia mshenzi yule ilihali ni yeye alikuwa ameshikilia hatma ya maisha yangu, nilikuwa kwenye himaya yake, angeweza kunifanya chochote hata kunitosa baharini.



Casper akaendelea kunibinyabinya matiti huku pumzi zikimtoka kwa kasi. Akanivua gauni, nikabaki na nguo ya ndani, niliendelea kuganda kama sanamu machozi yakijikusanya machoni.

Mara akavua surauli yake harakaharaka kama anakimbizwa, nikaona kitu cha ajabu kwenye sehemu zake za siri.





Sehemu zake za siri zilikuwa kubwa na zilikuwa wima kama mnara wa mashujaa wa vita ya pili ya dunia, zilikuwa zimekakamaa huku zikinitizama kwa uchu. Kwenye mdomo wa mnara huo kulitoka chozi la uchu. Jamaa akawa anahema kwa tabu, mzimu wa ngono ulikuwa ushampanda vibaya sana.

Hatimaye akawa ananiingilia kimwili. Sikuhisi chochote zaidi ya maumivu makali sehemu zangu za kike. Kwa lugha nyepesi naweza nikasema alikuwa akinibaka. Alinibaka, akanibaka na kunibaka, alinifanya anavyotaka mpaka hamu yake iikakwisha.

Alipotoka juu ya mwili wangu nilikuwa nahisi kama nimetiwa kwenye bani ya kukaishia tumbaku. Koo lilinikauka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Sikuwa na la kufanya kwakuwa kitu nilichokuwa nakitaka kwa wakati huo ni kurudi nyumabni kwetu Tanzania, nilikubaliana na udhalilishaji wote sanjari na maumivu yote yatakayo nisibu ilimradi nifikishwe nyumbani.



“Bila shaka utanifikisha nyumbani salama, ” nilisema kwa sauti ya upole mbele ya yule mwanayme mwenye asili ya Kigiriki.

Alinitizama kwa chati kisha akasema:

“Nina kisasi na wanawake wote kwenye hii dunia, sijawahi kumpenda mwanamke yeyote tangu nilivvyopata akili. Tangu nilipogundua viumbe hao walinifanyia mambo ambayo sikupaswa kufanyiwa niliwachukia mno.

Niliapa kuwaliza na kuwaumiza kisha kuwamaliza popote watakapo ingia kwenye anga zangu...”

Aliwasha sigara yake, akavuta na kunipulizia moshi mwingi usoni mwangu huku akinitizama kama kikaragosi. Akaendelea kusema:

“Hadi sasa nimekwisha ua mademu wengi na bado nina kiu ya kuua zaidi. ..”

Alivuta tena, akaendelea kuongea.

“Hata wewe tayari nisha kuua....”

“Casper!!!” nilimaka.

“Kwa nini unaongea maneno hayo mbona unanitisha..”

“Sikiliza we’ mbwa mwanamke. Hapo ulipo tayari nishakuambukiza Ukimwi na kwa taarifa yako siwezi kukusafirisha hadi huko unakotaka kufika. Umebakiza muda mfupi wa kuendelea kuishi kwenye hii dunia, kitu cha msingi ni kusali sala zako za mwisho...”

Toba!!

Ilikuwa ni kama ndoto mbaya ya kutisha inayonipitia nikiwa nimelala usingizini. Nilitamani iwe hivyo ili nishituke na kujikuta kitandani, chumbani mwangu huko kijijini kwetu Makose maisha yangu ya upendo na amani yakiendelea kama kawaida.

Pamoja na umasikini ulizingira familia yangu na nchi yangu, lakini amani na upendo wa Tanzania yangu ilikuwa ni tunu niliyoitaka kwa udi na uvumba katika maisha yangu ya kusaka fedha kwenye nchi za watu.

Nilijikuta nikianza kulia kama mtoto aliyetelekezwa na mamaye, mambo aliyonieleza mzungu yule, Gaspaer, yalikuwa ya kutisha mno.

“Umeniambukiza Ukimwi!!!”

“Ndiyo nimekupa Ukimwi kwa makusudi,” alisema huku tabasamu la kifedhuli likimtoka usoni mwake.

“Kwa nini lakini! Eeeh! nilikukosea nini kwenye maisha yako mimi.”

“Kimya!!Kenge wewe, kimya unamlilia nani hapa fala wewe!.”

“ Umeniambukiza Ukimwi!!!”

"Nasema kimya we’ mtu mweusi huelewi...Alaa!”

“Nimekukosea nini?” niliendelea kulalama huku mifereji ya machozi yakilowesha mashavu yangu.

“Nikwambie mara ngapi mbwa wenzio wanawake, walinifanyia mambo mabaya maishani. Na nikwambie mara ngapi niko kwenye oparesheni ya kulipa kisasi kwa mbwa wote wa kike!!!!!” aliongea kwa kuofaka vibaya sana.



Ghafla hali ya hewa mule ndani ilichafuka, yule jamaa alitoka akiwa na hasira dhidi yangu, nilimwona mtu yule kama alipandwa na majini kichwani mwake, sikutegemea kabisa kwa ukarimu alionionyesha awali kama angeweza kunibadilikia muda mfupi kiasi kile.

Nilibaki chumbani nikilia kwa uchungu, kwakweli sikujua nini hatma ya maisha yangu, kwa dakika zile chache nilijikuta nikikata tamaa vibaya mno, sikuona thamani ya uhai kwenye huu ulimwengu, kitendo cha kuambukizwa UKIMWI kiliniuma mno.



Nikiwa sijawa vizuri kiakili mara Casper akarudi akiwa kama mbogo aliyejeruhiwa na jangili kwa risasi.

“Toka toka humu ndani toka...” alisema huku akinisukuma, alikuwa kifua wazi, mkononi alikuwa ameshikilia kamba pamoja na kisu chenye makali.

Nilitoka nje, nikiwa nimeghafirika kwa tukio hilo. Nje nilikutana na watu wengine ambao kwa mwonekano walikuwa ni wafanyakazi wa meli ile, walionekana ni watu wenye kumwogopa sana Casper.

“Mfunge kamba huyu mwanamke mbwa.” Amri ilitolewa na Casper, upesi vijana wale walinidaka kama sungura dhidi ya kundi la mbwa mwitu wenye njaa.

Walininifunga kamba miguu na mikono, haikuishia hapo, walinifunga mwilini na chuma kizito.

Nilitambua nini kinacho kwenda kutokea. Kutupwa baharini nikiwa nimefungwa mikono na miguu, sanjari na chuma kizito mwilini wangu.

Nilikuwa kiumbe mwenye bahati mbaya kwenye maisha, nilizaliwa kwenye familia masikini na nimekuwa ndani ya umasikini huo kwa muda mrefu, katika kipindi ambacho niliamini nakwenda kubadilisha historia ya maisha yangu mara mambo yanabadilika kwa kufanya kosa dogo sana, ambalo limeniletea majanga mazito na yenye kuogopesha.

Machozi yalinibubujika, picha ya familia yangu ilijitengeneza kichwani mwangu, hasa nilipogundua nakwenda kufa pasina wao kuona mifupa yangu.

Siku zote familia yangu itakuwa na amani kwa kuamini mtoto wao niko nchini Oman nikifanya kazi za ndani na mwisho wa siku nitarejea nyumbani na kubadilisha hali ya maisha ya nyumbani.

Nikaendelea kuona taswira ya wazazi wangu watakapo kaa kwa muda mrefu bila kunipata na kuamua kufuatilia kwa wakala aliyenipeleka Oman, wataambiwa nilikutwa na misukosuko ya kifo kabla ya kufufuka mochwari, baada ya hapo watambiwa nilitokomea kusiko julikana.

Niliyaona machozi ya wazazi wangu, niliona mfadhaiko mkubwa nyoni mwao, mimi nilikuwa mtoto wa pekee na nguzo yao ya badaye. Hawatoona japo unywele wangu daima dumu.

Niliumizwa na nililia sana juu ya hilo, uchungu uliokuwa kifuani kwangu ulikuwa haumithiliki, niliamini mambo yote hayo chanzo chake ni umasikini na sasa nilikuwa nikionja chungu ya umasikini.

Mpenzi msomaji pengine haya ninayo simulia leo unaweza kuona ni kama riwaya za kubuni, amini nakwambia, mambo yote haya yemenitokea na hakuna hata moja la kubuni wala kuongeza chumvi.

Nikiwa nimejinamia, nimfeungwa kamba na chumba mwilini, mara nikashitushwa na sauti ya Casper ikisema:

“Mtupeni baharini huyo mbwa mwanamke.....wanawake wote duniani ni mbwa, hadi mama yangu mzazi, naye ni mbwa, tena mbwa koko...” mwendawazimu yule aliongea.

Hapohapo wakanibeba juu tayari kunitosa baharini, wakawa wanasogea ukingoni mwa meli tayari kwa kunibwaga majinii. Niligeuka kuangalia chini nikaona bahari ikiwa na mawimbi mazito yaliyokuwa yakijipiga katika kuta za meli ile kubwa na kutawanyika kila mahali.

Nikaona ubuluu wa maji, nikabaini kuwa sehemu ile ilikuwa na kina kirefu. Agripina mimi sikuwahi kujua kuogolea ingawa hata kama ningekuwa najua kuogelea bado nisingeweza kufanya lolote kwani mikono na miguu yangu ilikuwa imefungwa kwa kamba huku shingoni nikiwa nimefungwa kwa kamba nyingine iliyo unganishwa na chuma kizito.

“Moja...mbili...” wale jamaa walihesabu”

“tatu.. twendee!”

Hapohapo wakanirusha baharini! Nilijibamiza kwenye maji ‘pwaaa’ maji yakaruka na kusambaa kila mahali, nikaanza kuzama kuelekea chini huku nikinywa vikombe kadhaa.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

nilikuwa siwezi kufurukuta kwakuwa chuma kizito kilikuwa kimefungwa shingoni mwangu, mikono na miguu ikiwa imefungwa kwa kamba, nilipojaribu kuvuta hewa kwa ndani nikajikuta navuta maji mengi puani na mdomoni tendo hilo likanifanya nianze kutapatapa kwa namna halisi ya mfa maji.

Nilibwia vikombe vya maji huku nikiwa sipati pumzi, hatimaye nikawa nazama kwa kasi kuelekea chini kabisa ya bahari, sikuwa na la kufanya zaidi ya kusubiri mauti, nafsi yangu ilikuwa tayari kabisa kufa.

Nilibwia vikombe vya maji nikiwa sipati pumzi, nikaanza kuliona giza la ajabu mbele yangu, hatimaye sikujua tena kilicho endelea. Na kabla sijajua kilicho endelea nafsi yangu ilikiri kwamba mimi tayari ni maiti.



******


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog