IMEANDIKWA NA : IRENE
MBOWE
*********************************************************************************
Simulizi : Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi
Sehemu
Ya Kwanza (1)
KISA CHA KWELI ,,,,
Charlote,
mwanamke aliyeishi kwenye ndoa yake kwa miaka 5. lakini baada ya kukutana na
changamoto za ndoa ambazo alishindwa kuzivumilia na kujikuta kuwa na kisasi
rohoni, Sasa aliamua kulipiza kisasi hicho na kupelekea kuvunja ndoa
tatu.
Hembu msikilize Charlote anachokisimulia. Hii inaweza
kukusaidia sana katika maisha yako kutokuwa na kisasi
moyoni.
ONYO.. HURUHUSIWI KUNAKILI.. HAKI ZOTE
ZIMEHIFADHIWA.
SEHEMU YA KWANZA.
Nimelelewa
kwenye mazingira ya maisha ya utulivu na amani. Wazazi wangu walipendana na
kuheshimiana sana. Na kutufanya sisi watoto wote kuwa na heshima na kupendana .
lakini pia kujali jamii iliyotuzunguka na kuishi kwa adabu
sana.
Nilipata bahati ya kupata elimu nzuri na ya viwango. Wazazi wetu
walitusomesha, tena shule zenye hadhi na gharama kubwa mno.
Nikiwa
kidato cha pili , Mtoto wa mzee ambaye ni family friend na sisi aliingia kidato
cha tano katika shule niliyosoma. Hivyo kijana huyu Jones tuliheshimiana sana.
Alinipenda na nilimpenda wote tulipendana na kuhurumiana na
kuheshimiana.
Wengi shuleni walijua sisi ni family friends, na hivyo
kila mmoja ni kama alikuwa akimchunga mwenzake. Jones aliogopa kufanya upuuzi
akiamini ni lazima ningemsemea nyumbani, lakini na mimi pia niliogopa kufanya
upuuzi nikiamini kabisa jones angenisema Nyumbani.
Hivyo Jones na mimi
tukajulikana kama wana ndugu haswa haswa, na heshima ikawepo. Sikuwa na utani
wala mizaha na watoto wa kiume.. hii ni kwa Vile Jones alikuwa akinifuatilia
sana. Lakini na mimi nilimfuatilia sana kuhusu kuwa na mazoea na mabinti na
hivyo aliogopa pia nay eye.
Wengi walisema Jones na Charlote ni ndugu.
Wengi wa vijana walimtania Jones na kumwambia mwenye dada hakosi shemeji. Na
Jones alichukia sana.
Tuliendelea kupendana sana.
Baada ya
kumaliza masomo ya Secondary Jones alienda kujiunga na chuo wakati mimi
nikiendelea na masomo ya Secondary. Lakini tuliendelea kuwasiliana sana. Na
hatukutupana hata kidogo.
Alinipenda na kunikumbuka kila
mara.
Nilipomaliza kidato cha sita, yeye tayari alikuwa ameshaanza kazi
ya kuajiriwa.
Na sasa nilikuwa najiandaa na mimi kuanza
chuo.
Nakumbuka siku moja alinipigia simu na kunitaka tukutane
tuzungumze. Wana familia walijua urafiki wangu na Jones. Hakuna aliyekuwa na
mashaka juu ya urafiki wetu. Kila mmoja alitupenda na kutufurahia kwa urafiki
wetu.
Nilimpa ahadi Jones ya kukutana na mimi. Kwanza nilishangaa sana
kwa namna ambavyo alikuwa kabadilika. Alikuwa kanawiri sana, kawa na hali ya utu
uzima zaidi na pia alionekana ni kijana ambaye alikuwa na
pesa.
Tulikutana na kukaa mahali kwa ajili ya kuzungumza.
Kitu
cha kwanza aliniuliza …
Charlote,,, je una rafiki ama
mpenzi?
Nilitabasamu sana kwani moja kwa moja nilianza kuona akili yake
ikiwa inanihitaji kuwa mpenzi wake. Ni kweli sikuwa bado nina mahusiano. Na hii
ni kwa vile nilikuwa sitaki kuwakere wazazi wangu na nilitamani mahusiano
nitakayokuwa nayo yaishie kwenye ndoa ni we mke wa mpenzi nitakaye kuwa naye.
Badala ya kubadilisha mara huyu ama huyu kama nilivyokuwa nikiona wengi. Hivyo
niliamini nitakapofikisha umri mkubwa ndipo nianze mahusiano. Wakati huo
nilikuwa na miaka 20 wakati Jones akiwa na miaka 26.
Aliniuliza kwa
kusisitiza tena, je una mpenzi?
Nilimjibu hapana sina mpenzi na si
hitaji. Ni kama hakamini.
Ila akaamua kufunguka na kuniambia kwamba,,
hata yeye hana mpenzi na hana mahusiano, ila amekwua na marafiki kama marafiki
lakini amegundua kwamba marafiki hao hawana viwango avitakavyo. Na aliogopa
kunieleza kwani alifikiri tuna mahusiano ambayo yasingeweza kuruhusu sisi
kuoana.Ila baada ya kuongea na wazazi wake walimruhusu na kumueleza kama
Charlote atakubali kuwa mchumba wako haina neno. Hivyo akaamu akusitisha urafiki
wowote na hivyo kuja kuniuliza kama niko tayari.
Nilishindwa kutoa jibu
la haraka kwani sikuwa tayari ninamhitaji. Alionekana ni kijana nadhifu, msomi
na mwenye upendo. Lakini bado sikuwa na hitaji mpenzi, hivyo nilimueleza sina
mpenzi na sihitaji mpenzi. Na nilimueleza kwa nini sihitaji mpenzi, na sababu
mojawapo ikiwa ni kwamba natamani mpenzi nitakayekuwa na mahusiano naye awe mume
na sio kuwa na wapenzi wengi wa kila mara.
Jones alinitazama na
kuonyesha anamaanisha anachotaka kukisema.
Aliniambia,, Sharlote wewe ni
msichana mrembo sana, na ukweli ni kwamba nakupenda sana, na kwa vile sasa
hatuna uhusiano wa kindugu kama nilivyofikiri natamani kama ungekuwa mpenzi
wangu kisha uwe mke wangu.
Nilimtazama na nilifahamu kabisa kwamba Jones
anamaanisha mimi kuwa mpenzi wake. Sikuwa na historia mbaya ya Jones hata
kidogo. Lakini bado sikuwa na sababu ya kumkubali. Bado jibu langu lilikuwa ni
mapema sana, nahitaji kusoma na kuwa na kazi ndipo maswala ya mapenzi
niyaanze.
Aliniambia anaweza kunisubiri na kunihakikishia kwamba
nikimkubali nitasoma, nimalize nipate kazi ndipo anioe. Kama hilo ndilo
ningelihitaji.
Nilitabasamu na kumwambia ni mapema mno sina jibu la
kumpatia ila asubiri.
Aliniambia Charlote tafadhali najua mapema utaenda
chuo. Hivyo endapo utakuwa na maamuzi ya kuwa na mahusiano usinisahau,
ninakuahidi sitakuwa na mahusiano mpaka utakaponieleza msimamo wako
.
Tulimaliza maongezi yetu na kila mmoja akaondoka.
Siku hiyo
ilikuwa ngumu sana kwangu, kwani sasa nilianza kuwa na shauku ya kuwa na mpenzi.
Niliyatafakari maneno ya Jones usiku kucha. Nikiamini kabisa alikuwa anamaanisha
anachokisema.
Nilipokuwa naendelea kutafakari aliniandikia msg na
kuniambia,,, CHARLOTE TAFADHALI KABLA HUJAAMUA KUMPA MTU NAFASI NAOMBA
UNIFIKIRIE MIMI, NAKUPENDA SANA, NAKUFAHAMU NA NINGETAMANI UWE MKE WANGU . WEWE
NI MZURI SANA NA MREMBO MNO, BADO SIJAONA MWANAMKE MZURI NA MREMBO KAMA
WEWE.
Nilipomaliza kusoma msg ile niliisave ili iwe kumbukumbu yangu, ni
msg ya kwanza ya kimapenzi kuipokea yenye nguvu na heshima. Si kama nilizozoea
kusipokea za kishenzi na kipuuzi puuuzi.
Hivyo
niliisave.
SEHEMU YA PILI.
Muda wa kwenda chuo ulifika.
Wazazi wangu walinipenda sana, hivyo walinitafutia chuo kizuri na nilichokipenda
Nchi jirani. Nilianza masomo yangu ya Usekretari. Lengo langu ni niwe na kiwango
kikubwa cha taaluma hii. Wengi waliniambia Charlote wewe ni mrembo sana,
unapendeza sana ukifanya kazi kwenye maofisi makubwa. Urembo wako na kazi ya
usecretari vitakufaa sana. Kila mtu aliniambia hivyo, na hata nilipokuwa shule
ya sekondari kila mmoja aliambia hilo, hivyo nikajikuta natamani sana Taaluma
hii. Hivyo nikiwa nchini Nairobi niliisoma vyema na kuhakikisha nafaulu
vyema.
Niliipenda sana Taaluma hii, na nilifanya vizuri
sana.
Tuliendelea kuwasiliana na Jones, nilimueleza ninachokifanya. Na
bado nikiwa mwaka wa kwanza chuoni bado sikuwa nimemueleza kuhusu suala la mimi
kumkubali yeye kuwa mpenzi wangu.
Lakini nikiwa Nairobi nilikuwa na
kijana rafiki tu ambaye ni Mtanzania, isipokuwa naye alikuwa ni rafiki na si
mpenzi. Na sikumpenda kama mpenzi ila rafiki ili niwe na mtu wa karibu mtanzania
mwenzangu. Hivyo niliamua kuwa na urafiki naye wa karibu nikiamini kuwa na
mwanaume rafiki nitakuwa salama.
Nilipendeka sana chuoni, wanaume wengi
walinipenda na kunitamani, lakiini bado msimamo wangu ulikuwa pale pale sihitaji
mpenzi wa kuniacha, ila mpenzi ambaye atakuwa mume.
Muda ulipita nikiwa
chuoni , na nilisifika kwa tabia njema na kujiheshimu, wengi walinifurahia na
hawakuweza kuwa kama mimi kwani walikwua na tama sana.
Nakumbuka siku
moja nikiwa hostel. Nimejilaza. Rafiki yangu Penina, msichana wa Kinyarwanda
ambaye tulipenda sana, na wengi walisema tumechaguana warembo,, alikuja
kuniamsha na kuniambia .. Charlote,,, uko na mgeni, kijana handsome sijui katoka
wapi ila ana sound kama mtzedi… he is outside anakusubiri kwa nyumba ya wageni
ukaonane naye…
Mh… haraka nilijua huenda ni kaka zangu na si mtu
mwingine, wazo halikuwa kwa Jones kabisa.
Dah.. sikuamini kwa kadiri
nilivyokuwa nikisogeza hatua zangu.. nilimuona kabisa ni Jones,, nilianzakupata
furaha sana moyoni. Nilimsogelea na kumkumbatia kwa furaha kama mtu na kaka na
dada yake. Nilifurahi sana kumuona.
Tulizungumza na akaniambia kama
naweza kupata ruhusa ya kutoka chuoni na kwenda mjini basi nifanye hivyo na siku
inayofuata atanirudisha kwani ilikuwa ni week end. Nilizungumza na rafiki yangu
Mnywaradwa Biera na alikubali kwamba tutoke. Hivyo tukaomba ruhusa na kkwetu
ilikuwa rahisi sana kuruhusiwa kutokana na tabia zetu. Tuliondoka na Jones na
Biera mpaka mjini.
Jones alituvutisha raha za kila namna, tulikunywa,
tulikula na kufanya shorping. Kisha jioni wakati wa dinner kabla hatujaenda
kulala kwenye hotel nzuri ya kifahari aliyobook kwa ajili yetu nay eye,
aliniomba sana nimpatie jibu.
Alinieleza nia yake na lengo lake kwamba
bado anahitaji niwe mpenzi wake.
Sikuona sababu ya kukataa sasa. Moja
kwa moja kwa moyo wa hiyari kabisa, nilimwambia Jones nampenda na niko tayari
kuwa na mahusiano naye ya mapenzi , awe mpenzi wangu na kisha mume wangu. Na
nilimueleza kwamba natamani sana tuheshimiane, tupendane na kuwa mke na mume
kama Mungu akitupa maisha.
Jones alifurahi na kwa mara ya kwanza kuona
machozi ya Jones. Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwake mimi
kumkubali.
Tulilala usiku huo. Mimi na biera kwenye room yetu. Usiku
kucha tulipiga mastory na kumueleza juu ya Jones. Biera alinishauri vyema na
kuniambia nimepata kijana mwenye anaonekana ni smart, muaminifu na anayemaanisha
mahusiano. Aliniambia sio kijanahohe hahe ni kijana ambaye yuko smart na very
handsome and educated.
Tulifurahi na kulala.
Asbh tuliamka na
kuelekea kwenye chai. Kisha tukazunguka tena mjini na ndipo sasa Jones
akaturudisha chuoni. Huku akinisisitiza kwamba mimi nay eye sasa tuko kwa stage
ingine kabisa na sio ya urafiki tu, ni urafiki wa uchumba kwani tunafahamiana
miaka mingi, hivyo ni vyema sasa tukaheshimu mahusiano
hayo.
Nilimuhakikishia kwamba mimi niko salama sana na asijali, nay eye
pia awe salama.
Aliondoka na kuniacha. Nilianza kumuwaza sana, nilianza
kumuona alivyo mzuri,na kijana wa thamani sana kwangu.
Nilimfurahia sana
Jones. Lakini Biera naye aliniambia sio kijana ambaye ni chokoraa ama mang’aa.
Akaniambia kwa namna vile anaonekana kama angekuwa mang’aa angetafuta tu
msichana wa kuspendi naye na asingehangaika kuja naibori kwa ajili yangu.
Nilimuelewa Biera.
Sasa Jones alianza kunifuatilia kwa simu. Alipiga
simu kila mara, alijua natoka darasani saa ngapi na aliongea na mimi zaidi ya
lisaa kila siku mara agunduapo niko na nafasi. Wakati mwingine nilichelewa hata
kuoga ama kula. Hii ni kwa sababu alishikilia simu muda mrefu. Na kama ingekuwa
naongea na simu basi ni lazma nimueleza naongea na nani.
Jones aliingia
wazimu juu yangu. Na mimi sikushawishika kutompenda, ila nilimpenda zaidi na
zaidi.
Muda ulipita. Sasa ni mwaka wa pili niko chuoni.
Jones
ameshajulikana kila mahali, si chuoni wala nyumbani kwamba ni mpenzi wangu na
mchumba wangu.
Wasichana wengni walinionea wivu, hali kazalika vijana wa
kiume nao. Walinitamani sana na walitamani mahusiano yetu yangekuwa kamayao.
Kwani mara nyingi walikorofishana.
Biera naye alikuwa akikorofishana na
mpenzi wake kila mara.
Jones alifika Nairobi kila mara alipohitaji, hasa
siku za jumamosi na jumapili, hivyo ijumaa jioni nilitoka chuoni na kurudi
jumatatu asbh.
Tulipendana sana. Na tulpofunga chuo Jones alikuja na
kunichukua na gari yake.
Marafiki wa Tanzania walinitamani na waliomba
lift ila Jones aliniambia hakuja kuchukua chuo ila kunifuata mimi hivyo hawezi
mpatia mtu yeyote lift, isipokuwa mimi ambaye ni mpenzi wake.
Mapenzi
yalipamba moto. Tulipendana sana.
Niliporudi kutoka chuo, nilifikia kwa
Jones ambaye alikuwa na nyumba yake aliyopangisha, nilikaa kwake siku tatu kisha
ndipo nilienda nyumbani, na muda wowote alinifuata nyumbani na kutoka na mimi.
Wazazi wangu walimpenda kijana ambaye alijiheshimu sana.
Wakati narudi
chuoni kwa ajili ya kumaliza elimu Yangu, Jones aliniomba kunivisha pete.
Nilimuomba anivishe pete mara baada ya mimi kumaliza chuo. Aliniambiahapana
naomba kabisa nikuvishe pete ya uchumba, nilimuomba sana asubiri. Na
akakubali.
Nilienda chuoni nikiwa msichana mwenye furaha na kujiona ni
mwenye bahati sana.
Maisha yaliendelea kwa furaha mno. Na nilibahatika
kufanya mitihani yangu vyema.
Kabla sijamaliza chuo, Jones aliniambia
kaka yake anaoa, na angependa nihudhurie harusi hiyo. Nilimueleza situation ya
masomo, aliniomba sana kwamba nichukue ndege nifike jijini kwa harusi na baada
ya siku mbili nitarudi.
Nilimtii wkani nilimpenda. Alinilipia tiketi ya
ndege na kwa mara ya kwanza nilipanda ndege. Nilienda kwa ajili ya harusi ya
kaka yake. Alinipeleka shorping kwa ajili ya nguo za harusi. Kisha Jumamosi siku
ya harusi tukawa tuko pamoja kwa ajili ya harusi ya kaka yake
Kila mtu
alimhurumia na kumwambia huyo Charlote kakukamata haswa, na alifurahi kusikia
hivyo. Alikuwa muaminifu sana kwangu, na hakuwa na mahusiano na msichana yeyote
Yule. Mara nyingi aliambiwa ukimuamini sana Charlote iko siku atakutenda, na
mimi sikutaka kukamilisha ndoto hizo na misemo hiyo mibaya. Hiyvo nilijitahidi
kumpenda na kumuonyesha yuko mahali salama na kwenye penzi salama . na
sikushawishika na kutamani mwanaume yeyote.
Harusi ilikuwa kubwa sana na
ilifana sana.
Maharusi waliingia ukumbini kwa nderemo na
vijijo.
Kisha wageni waalikwa nasi tukaingia ukumbini.
Baada ya
utambulisho, Maharusi walifungua champagne kisha tukagongeza kuwatakia mafanikio
mema.
Baada ya Hapo Jones naye alipewa nafasi ya kuongea, sikuwa na wasi
wasi kwani nilijua anataka kusema jambo kama mwanafamilia.
Kisha Jones
alisema kwa sauti ya juu kwa kutumia kipaza sauti… CHARLOTE MY LOVE WHERE ARE
YOU?
Ukumbi mzima ulitulia kutaka kujua nini kinaendelea. Nilitoka
nilipokuwa, hofu na kutetemeka kwa aaibu kutokana na umati wa watu, na sikuwa na
ujasiri wa kusimama mbele za watu wengi. Ila kwa vile nilimpenda sana Jones
sikutaka kumuangusha, nilijikaza sana huku natetemeka.
Kisha nikafika,
na akanibusu. Baada ya sekunde kazaa alitoa kitu mfukoni mwake,, na
kusema..
Huyu hapa ni mpenzi wangu, rafiki yangu na mchumba wangu, mke
wangu mtarajiwa, naomba kusema kwamba baada ya harusi hii ya kaka inayofuata ni
yangu…
Charlote will you marry me?
Dah…. Ilikuwa mtihani,,
nilijikuta naogopa,machozi yanatoka,,, na Jones naye hali kazalika… Alipiga
magoti na nikamwambia yes,,, will marry you….
Watu walishangilia sana,
na kufungua champagne. Kisha nikaenda kukaa na wazazi wangu walikuwa harusini
kwani ni family friend wakaambiwa Jumamosi ijayo wajiandae na ugeni wa
kupelekewa mahari.
Ilipendeza sana japo nilishtukizwa
kabisa.
Harusi iliishia vyema na nikarudi
chuoni.
SEHEMU YA TATU.
Nilimaliza masomo yangu salama.
Na tayari nilikuwa na ujauzito wa miezi 2. Kwanza Jones alifurahia sana kusikia
nina ujauzito. Haraka mipango ya harusi ilifanywa na tulioana, na sasa ikawa ni
mke na mume rasmi. Harusi yetu ilifana sana, ilipenda mno. Na wengi walitupenda,
na baada tu ya mimi kujifungua tulisimamia harusi kama mbili hivi, hii ni kwa
vile waliotuomba tuwasimamie walivutiwa na maisha yetu ya ndoa na kupendana
kwetu.
Jones alinipenda sana.
Nilipata kazi nzuri nay a mshahara
mzuri kutokana na elimu yangu ilivyokuwa ya juu. Nilifanya kazi kwenye ofc kubwa
mjini na ambao wanalipa vizuri.
Haraka sana Mume wangu alininunulia gari
nzuri ya kutembelea na kuniambia hataki nipate shida.
Nilimpenda Jones
nay eye alinipenda sana.
Sikuwahi kumuwazia mambo mabaya hata kidogo. Na
pia hatukupenda kugombana wala kulumbana kwani wazazi wetu walipendana sana na
hatukutaka kujiaibisha. Mara tulipokoseana pole pole tuliambiana na
kurekebishana kabla mambo hayajawa magumu na mabaya zaidi.
Hivyo
matatizo ya ndoa yetu hakuna aliyeyajua zaidi yetu wawili.
Nakumbuka ni
mara moja tu Jones aligomba kwa tabia yangu ya kunywa pombe, na nilimuahidi
kuacha, kwani nilikuwa natumia pombe hasa balantine, na alipokuwa akisafiri
ndipo nilikunywa sana. Japo sikuwa natoka ila nilinyewa nyumbani tu. Na
alinikataza tabia hiyo. Na siku moja aliniaga anasafiri na kwa vile nilimwambia
nimeacha alitaka kuhakiki je nimeacha ama la? Na hivyo alisafiri safari feki na
kurusi na kunikuta niko bwii. Alikasirika sana na kuniitia mama yangu anionye.
Huu ndio ugomvi ambao naweza kusema kwa mara ya kwanza niliuona mkubwa na
kumuona Jones alivyobadilika. Na kuanzia siku hiyo nilimuahidi sitakunywa tena
pombe. Japo sikuweza kwa mara moja ila nilimuahidi sitakunywa tena
pombe.
Ndoa yetu na maisha yetu yalkuwa gumzo mtaani , kwenye familia ,
kwa ndugu na marafiki, hata wafanyakazi wa jones na wafanyakazi ninaofanya nao
kazi walikwua wakitushangaa sana.
WENGI WALISEMA IVUMAYO HAIDUMU….. NA
WALITUBEZA MNO.
WENGINE WALITUFURAHIA, WENGINE
WALITUTAMANI.
Ndani ya ndoa ya miaka mine nikabahatika kupata mtoto
mwinngine. Mungu akatujalia watoto 2. Tuliwapenda sana. Walikuwa wavulana wote,
walifanana na sisi sana.
Maisha ya ndoa yalikuwa matamu
haswa.
Sikuwahi kumuwazia Jones kuwa na mwanamke hata
kidogo.
Nakumbuka siku moja nikiwa natoka kazini, niliamua kumfuata ofcn
kwake ili tupitie mahali nimuonyeshe friji ili tununue. Ilikuwa ni saa kumi na
moja.
Wakati natoka napanda ngazi za ofcn kwake nilikutana na mfanyakazi
mwenzake, aliponiona alirudi kwa speed ya ajabu, nilishikwa na butwaa nini
kinamrudisha? Lakini nikasema ni ofc za watu.
Sikujali sana, nikaendelea
kupanda ngazi. Kisha ghafla nikapishana kwenye ngazi na msichana ambaye
ninamfahamu. Lakini hakunisalimia, ila alinipita kwa kasi ya ajabu, niligeuka
nyuma kumtazama na aliendelea kuziruka ngazi kwa speed ya ajabu mpaka
akamalizikia sikumuona tena, Nilipogeuzauso wangu nilikutana macho kwa macho na
Jones, alinikumbatia na kunibussu, kisha akanishika mkono na kunipelake ofcn
kwake. Akanipatia juice. , na nikamueleza kilichonipeleka kwake na tukaondoka
kuelekea madukani na kununua friji hiyo kisha kwenda nyumbani.
Siku hiyo
mume wangu alionekana kuwa busy sana na simu sana, na si kawaida yake. Na
tuliwekeana sheria hakuna kuweka simu pw, na kila mmoja ana ruhusa na simu ya
mwenzake. Na hii ilitufanya tukaaminiana sana na kutokuwa na wasi wasi kwenye
ndoa yetu.
Kwa vile ilikuwa ni sheria sikuona shida nilijua tu acha awe
busy kuna saa nitaishika simu yake na kuikagua.
Na kweli usiku kabla ya
kulala nilimuomba simu yake na nilifanikiwa kuikagua.
Nilikuta ametuma
msg na kasahau kuifuta na kasema ,, Samahani Husna naomba tuongee kesho
nimeshafika nyumbani sihitaji kukuudhi, tutaongea kesho mpenzi.
Dah,,
nilipaniki kimoyo moyo,, lakini sikumuonyesha kama nimejua, ila Husna ni binti
ambaye alinipita kwenye ngazi na speed za ajabu, Namfahamu mama yake, namfahamu
baba yake, na ninawajua ndugu zake. Dah. Kiliniuma. Kisha nikafuta ile msg wala
sikumuonyesha mume wangu kwamba nimejua kitu.
Usiku sana muda wa saa
saba nilimuamsha, nikamwambia Jones, naomba usinifiche, niambie ukweli wote
kuhusu jambo nitakalo kuuliza.
Je husna ni nani? Kwanza alisema alienda
kuomba kazi, mara mpenzi wa mfanyakazi mwenzake nk. Nilikasirika nikamwambia kwa
nini unanidanganya? Akaniambia mke wangu sio kweli sina mahusiano
naye.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment