Search This Blog

Friday, November 18, 2022

PAIN OF LOVE - 2

 






Simulizi : Pain Of Love

Sehemu Ya Pili (2)





Benson aliogopa sana na moyo wake ulizidi kwenda mbio kama injini, muda kidogo kupita ndipo taratibu akatuliza moyo pia akatuliza na akili na hapo hapo akili yake ikamtuma apige simu kwa yule mtu aliyetuma ujumbe wa vitisho. Baada ya kukubaliana na akili yake akachukua simu akapiga kwa mlengwa.



(Aaah!, you f*ckinguy that is just a warning)

“Aaah!, kijana hilo ni onyo,” Benson alisikia sauti yenye bezi ikimwambia mara baada ya kupiga simu.



(Who are you?)

“Wewe, nani?” aliuliza Benson kwa sauti ya ujasiri.



(You wanna call yourself f*ckinmachine to date with peoples loverokay soon you know gonna me, son of bitch)

“Wewe si fundi wa kutembea na wachumba za watu...utanijua tu hivi punde” yule mtu alizidi kumpa vitisho Benson.



(Who is that shityou are talking about?)

“Yupi huyo, unamzungumzia?.”



(You dont know haa? Soon you gonna know her)

“Humtambui eeeh?, ipo siku utamtambua.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

(Why are you scaring me? or youwanna talk like that in order to be scared of?)

“Mbona, unaongea kwa vitisho au unaongea hivyo ili uogopwe?.”



(Better threats than doing badshits to your living and coming regret later)

“Bora vitisho, kuliko kukufanyia kitu mbaya katika maisha yako ukaja jutia.”



(I think youve called wrong number)

“Nahisi, umewrong number si bure.”



(Ive ever wrong number, I know you well from A to Z and Ive spied on you since way back. So youve to watch your step before destroying your face because of that bitch, stay away with my lover)

“Sijawahi kosea namba, mimi nakujua A to Z pia nimeanza kukufuatilia muda sana...sasa ndugu jiangalie sana nisije siku kukuharibu sura kisa mwanamke kaa mbali na mchumba wangu” alitoa tahadhari yule mtu kwa Benson.



(Aaah Aaah destroying my face haa? I dont think so)

“Aaaah, aaah uniharibu sura sidhani kama utaweza” alijaribu kuongea kwa dharau Benson kwa kujionyesha naye ni kidume mbele ya mwenye mali.



(You despised haa?, you gonna send me to jail)

“Unajibu dharau?...sasa wewe utasababisha nifungwe.”



“Ahaaaa haa, haa” alizidi kucheka Benson kwa dharau.



(What gives you power?, you do think you are a patriot South Africa has their owners, so you refugee continue to act you are knowing youll getback just a name to your land)

“Unajiamini nini?...au unajiona mzaliwa wa hapa, hii South Africa ina wenyewe sasa wewe mlowezi endelea kujifanya unajua kama kwenu hujarudi jina tu” aliongea yule mtu kwa sauti ya kufoka, kisha akakata simu. Akamuacha Benson akifikiri na kutafakari.



“Huyu, ni nani?...na anamzungumzia mchumba wake gani?”



“Aaahaa shit...kichwa kinauma” yale manung'uniko ya Benson, Peter rafiki wa Benson aliyasikia. Akasogea hadi alipokaa Benson akamshika bega kisha akamuuliza rafiki yake.



“Benson, una nini?.”



“Hamna, kitu” alikataa Benson kinafiki ili rafiki yake asijue kinachoendelea.



“Nakuona unapayuka hapo, halafu unaniambia hamna kitu” alisema Peter huku akikaza macho kwa Benson.



“Niamini, ningekuwa nina kitu kinanitatiza ningekuambia.”



“Haya, lakini kaa ukijua mficha maradhi siku zote kifo humuumbua” aliongea Peter kwa mkazo na kuonyesha sura ya kumuonea huruma rafiki yake.



Benson alifikiria ule msemo wa rafiki yake akaona ni kweli kabisa anachosema, akiendelea kuficha ficha mwishowe maradhi yaje kumuumbua na kupata fedheha na mwisho kuonja umauti bila ya mtu yeyote kujua. Basi hakuona tena sababu ya kumficha rafiki yake alimueleza rafiki yake ukweli wote bila kumficha chochote ili kama kuna ushauri ampatie.



“Kumbe ndiyo yaliyokukuta...pole sana” alisema Peter mara baada ya kutambua kitu kinachomtatiza rafiki yake.



“Kwa hapo utanipa ushauri gani, rafiki yangu?” aliuliza Benson na kuonyesha dalili ya kutaka msaada kwa rafiki yake.



“Ninachoona, umjue kwanza huyo mwanamke anayemzungumzia kisha ukimjua haraka sana achana naye.”



“Rafiki yangu, wanawake niliotembea nao hawana idadi kifupi nitapata tabu tu ya kumtafuta.”



“Acha upate tabu, lakini ilihali uwe tayari ushamjua.”



“Sasa hapo, nitaanza na hatua ipi?.”



“Anza hatua ya upelelezi, upate kumjua huyo mwanamke.”



“Upelelezi, nianzie wapi?.”



“Anzia kwa huyo mwanaume, kumuuliza baadhi ya maswali kuhusu huyo mwanamke.”



“Nitaanzaje?...wakati namba yangu anaijua.”



“Rafiki yangu unakuwa kama si mjanja...nunua laini nyingine kisha mpigie au mtumie ujumbe na hapo ndipo utaanza upelelezi wako bila ya yeye kujua.”



“Okay...hapo sasa nishakuelewa,” Benson aliongea huku akionyesha ishara ya kukubali kwa kutingisha kichwa. Akakuna kidogo nywele kisha akauliza kwa sauti iliyobeba tafsiri ya furaha.



“Hivi rafiki, pale mtaa wa Zingo si kuna mawakala?.”



“Wapo wengi, na pale huwezi kukosa kabisa.”



“Basi ngoja nifanye mchakato wa kwenda sasa hivi, nikasajili hiyo laini,” Benson aliongea haraka na upesi akamuaga rafiki yake na kuondoka kusajili hiyo laini.



Benson kabla ajafika mtaa wa Zingo akiwa bado njiani kwenye barabara ya vumbi, akahisi gari limesimama kando yake kugeuka kuangalia kweli akaona gari aina ya LANDCRUISER nyeusi imesimama kando yake. Akiwa bado anashangaa haelewi chochote akaona kioo cha gari lile kikishushwa taratibu na hapo ndipo akamuona kijana wa kisomali akimuamuru aingie ndani ya gari kwa lafudhi ya kisomali, yule kijana wa kisomali sababu alibarikiwa sauti nzito iliyomuogopesha Benson basi kipingamizi hakikuwepo kwa Benson. Aliingia kwenye lile gari bila mkukumkuku wowote alipoingia tu taharuki ikaugubika moyo wake alishangaa kuona yule kijana wa kisomali amemtolea bastola na kumlengeshea kwenye mbavu.



**********

Mathias aliumia sana lakini ikafika muda alijikaza kama mwanaume huku akijifariji kuwa Ipo siku Coletha atakuwa wake. Alituliza akili yake Mathias akamsahau kabisa Coletha kwa muda hule aliweka simu yake mfukoni akaendelea na safari, alifika ofisini akaendelea kufanya kazi kwa umakini na punde wateja walimiminika kwa wingi katika kibanda chake cha CD.



“Mathias niwaishie CD yangu, niondoke” sauti ya mama mmoja ilisikika ikimuongelesha Mathias.



“Nitakuhudumia, lakini nakuomba mama yangu twende kwa utaratibu wa kupanga foleni” aliongea Mathias kwa sauti ya unyenyekevu wa kazi yake.



“Nisaidie Mathias, mwenzio nimeacha mboga jikoni” alizidi kubembeleza yule mama.



“Naweza kukusaidia, ila ningependa uongee na wenzako waliokutangulia wakiridhia nikuhudumie sawa nitakuhudumia,” Mathias alimueleza yule mama kwa ustaarabu wote.



Kwa kumwangalia yule mama alikuwa kachoka kupita maelezo yote kutokana na ujauzito aliokuwa nao, kwa kuwa yule mama alichoka sana kusimama pale kwenye banda la CD na alikuwa ana nia kweli ya kuondoka kuwahi mboga yake ikabidi asikilize ushauri wa Mathias. Akajishusha na akaomba kwa wateja wenzie waweze kumruhusu ahudumiwe aondoke.



“Kwa vile umetuomba, hatuna tatizo wewe hudumiwa tu uende,” Dada mmoja ambaye ni mmoja wa wateja alimueleza yule mama kwa kumpatia ruksa.



Baada ya muda kupita wateja wote walikuwa washahudumiwa. Mathias aliendelea na kufanya kazi zake nyingine ilipofika nyakati za mchana tumbo la Mathias likawa linakwangua kuashilia njaa imechachamaa, ikabidi afunge ofisi mara moja na kwenda kupata chakula kwenye mgahawa anaokulaga siku zote.

Habari yako, mama Bonge alitoa salamu Mathias kwa Mama Bonge mara baada ya kufika mgahawani.



“Salama...kwema?,” Mama Bonge aliitikia salamu kisha aliuliza kwa kutaka kujua hali ya Mathias.



“Kwema...leo kuna chakula gani?.”



“Ugali, wa dona.”



“Niwekeeni, hilo dona.”



Mathias alitengewa chakula huku mama Bonge akiwa amekaa pembeni akimpigisha stori mbili tatu, Mathias akiwa bado anapata chakula ghafla alihisi kichwa kinauma kwa kugongagonga kama nyundo.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

**********

Coletha aliwasili kwa mama yake mapema kidogo. Akagonga mlango kwa muda mrefu bila majibu kwa kuona hamna majibu yoyote akazungusha kitasa. Mlango ukafunguka akaingia ndani la haula!! kuingia ndani hakuamini alichokiona alimkuta mama yake akiwa sakafuni akiwa anavuta pumzi kwa kasi. Alikimbia kumuwahi kumuinua pale sakafuni alimuinua akamkalisha sofani kisha akakimbia kuleta maji apate kunywa, mama Coletha alikunywa maji kwa wingi na taratibu hali yake kidogo ikawa ahueni.



“Mwanangu, bora umekuja« alisema Mama Coletha huku akishika kifua na kusikiliza mapigo ya moyo jinsi yanavyodunda.



“Kwani kimekupata nini?...mbona nimekukuta kwenye hali ile?” aliuliza Coletha huku akimpepea mama yake kwa khanga yake aliyoitoa kwenye kipima joto (handbag) yake.



“Hali yangu sio nzuri kiukweli, ubongo wangu kuna...” kabla hajamaliza kuongea Mama Coletha ghafla hali yake ikaibuka tena.



Safari hii hali yake ndiyo ilikuwa mbaya zaidi alikuwa anatapatapa kwenye sofa kama mtu mwenye kifafa au kuku anayekata roho. Coletha alimweka mama yake vizuri pale sofani huku akionekana kuchanganyikiwa kwa ile hali ya mama yake, baadae kabisa wazo la kumpeleka mama yake hospitali likamjia akatoa simu yake aina ya IPhone X2 kwenye handbeg kisha akatafuta namba ya dereva taxi kwenye simu yake ambae kila siku huwa anampeleka kazini. Alipoipata hiyo namba akapiga ikaita mara moja na kisha ikapokelewa.

Hallo ilisikika sauti ya dereva taxi upande wa pili ikizungumza.



“Eeenh, kijana...upo wapi?” aliuliza Coletha kwa kuweweseka.



“Dada, nipo Karume.”



“Unaweza fika Ilala, tumpeleke mgonjwa hospitali.”



“Bila shaka...nakuja.”



“Wahi kidogo, maana mgonjwa mwenyewe hali yake mbaya.”



“Usijali, dada” yule dereva taxi alipomaliza kuongea tu akakatiwa simu na Coletha.



Coletha baada ya kukata simu, likapita lisaa mpaka yule dereva taxi kuwasili wakasaidiana na Coletha kumpakiza mgonjwa kwenye gari kisha wakaanza safari ya kwenda hospitali.



“Dada, mgonjwa wetu tumpeleke hospitali gani?” aliuliza dereva taxi wakiwa njiani.



“Tumpeleke hospitali ya MUHIMBILI, pale kwasababu nafanyia kazi na huduma tunaweza pewa kwa haraka.”



“Sawa,” Dereva taxi alikubaliana na Coletha kisha akazidi kukanyaga mafuta.



Basi hawakuchukua masaa mengi kufika hospitali ya Taifa, Coletha na dereva taxi wakasaidiana tena kumshusha mgonjwa. Mgonjwa aliposhushwa dereva taxi akalipwa pesa kisha akaondoka nyuma akamuacha Coletha akiita wauguzi waje kumsaidia kumpeleka mama yake wodini, mama Coletha akapakizwa kwenye kiti cha magurudumu cha wagonjwa wasiojiweza kisha akakokotwa hadi wodini. Coletha aliacha majukumu yote kwa wauguzi waliokuwa zamu siku hiyo yeye akaongoza kwenye ofisi ya daktari mkuu kuripoti.



“Coletha, mama yako kapatwa na tatizo gani?” ndilo lilikuwa swali la kwanza la yule daktari mkuu wa Muhimbili mara baada ya Coletha kuwasili ofisini kwake.



“Sifahamu” alijibu Coletha kwa kuonyesha kutojua chochote kinacho msibu mama yake.



“Kwani, hakuwahi kukugusia kama yeye anaumwa?” alizidi kuuliza yule daktari mkuu.



“Hajawahi...leo asubuhi nikiwa ofisini nilishangaa alivyonipigia simu na wakati si kawaida yake kupiga simu nikiwa kazini, nadhani kuna kitu alitaka aniambie.”



“Unahisi ni kitu gani, alitaka akuambie?.”



“Sikujua, ila nilipofika kwake aliniambia kuwa hali yake sio nzuri.”



“Ukumdodosa?.”



“Sikupata nafasi ya kumdodosa, kwa maana nilimkuta katika hali mbaya nami nilichanganyi...,” Coletha kabla hajamaliza kuongea akakatishwa kuongea na muuguzi mmoja ambaye aliyeingia mkukumkuku kwenye ofisi ya daktari mkuu bila hata ya kubisha hodi.



“Wewe!!!, kulikoni?,” Daktari mkuu ikabidi aulize kwa mshangao.



Samahani, mgonjwa kule kazidiwa alijibu yule muuguzi huku akihema kwa hofu kubwa.



“Mgonjwa, yupi huyo?” aliuliza daktari mkuu.



“Mama yake, Co Co Coletha” yule muuguzi alijibu kwa kigugumizi.



“Eti, nini?,” Coletha alidakia yale mazungumzo na kuonyesha hajaelewa kilichoongelewa na muuguzi.



Mara ghafla akanyanyuka kitini kwa kuchanganyikiwa moja kwa moja akakimbilia kwenye wodi aliyolazwa mama yake.”





**********

“Mathias kichwa kiliuma hadi akasikia kizunguzungu. Chakula chote alichoagiza akakiona si kitamu lakini akajitahidi kujikaza ili Mama Bonge aliye pembeni yake asijue lakini ikashindikana Mama Bonge akaona ile hali na akajua, akamsogelea Mathias jirani akamshika bega na kuuliza.



“Mathias, kuna nini?.”



“Kichwa kinaniuma,” Mathias hakuficha ikabidi amueleze Mama Bonge ukweli kitu kinachomtatiza.



“Kimekuanza, muda?.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Kimenianza sio muda mrefu...kwa hapa duka la madawa lipo maeneo gani?” alijibu na kuuliza Mathias.



“Duka la madawa lipo mbali kidogo...unataka kuagiza dawa?.”



“Ndiyo.”



“Ngoja basi, nikuitie mtoto umuagize.”



“Sawa.”



“Ulikuwa, unataka dawa gani?.”



“Panadol, zitanifaa” alijibu Mathias huku akitoa pesa mfukoni.



Akatoa shilingi elfu mbili mfukoni akamkabidhi Mama Bonge kwaajili ya pesa ya chakula na kwaajili ya hiyo dawa. Baada ya Mama Bonge kupewa pesa akampatia ile pesa mtoto aliyemtafuta kwaajili ya kununua hiyo dawa, yule mtoto akapokea ile pesa kisha akaenda kununua alichoagizwa dakika chache tu yule mtoto alikuwa kasharudi akamkabidhi chenji Mama Bonge pamoja na panadol hatimaye akaondoka. Mama Bonge mara baada ya kupatiwa chenji na dawa akakata pesa yake ya chakula kisha pesa iliyobaki akamrudishia mwenyewe, akamrudishia na akampatia maji ameze dawa zake. Mathias alipopokea chenji, dawa na maji kwa Mama Bonge akainywa ile dawa kisha akapumzika kidogo kwa kujilaza kwenye benchi. Baadae kabisa akaja kuamka kuangalia juu ya anga akaliona jua linazama kuashilia jioni imeingia akiwa ametulia akisikilizia kichwa kwa mbali akasikia kichwa kinauma na kilikuwa kizito.



“Umeamka?,” Swali lilitoka kwa Mama Bonge mara baada ya kuona Mathias kashaamka.



“Nimeamka...lakini mbona hukuniamsha umeniacha nimepitiwa mpaka saa hii?.”



“Nilikuwa najali kwanza afya yako, ningekuamsha ningekusumbua angali unaumwa.”



“Ahsante...ngoja niende.”



“Kichwa, lakini si kimepoa?.”



“Kwa mbali, maumivu nasikia.”



“Sasa unaweza kwenda mwenyewe?, au niite mtu akusindikize?.”



“Acha tu, nitajitahidi kwenda mwenyewe” alijibu Mathias kisha akanyanyuka kwa kujikokota na mwisho akaondoka.



Mathias polepole akatembea akielekea nyumbani maana kurudi ofisini muda ulikwenda sana, akiwa yupo njiani kwenye barabara ya vumbi ghafla akaona kizunguzungu na mbele yake akaliona giza limetanda papo hapo akadondoka chini.



**********

Benson akatoa macho kwa uwoga kama mjusi aliyebanwa na mlango na akatetemeka kama mtu anayeumwa na ngiri. Yule kijana wa kisomali hakuonyesha kabisa sura ya huruma wala hakutaka kucheka kabisa na Benson, akaonyesha sura ya kukasirika kweli hadi Benson akaogopa.



“Kijana, si ulikuwa mjanja kwenye simu?” aliuliza yule kijana wa kisomali kwa hasira.



“Ndi ndi, ndiyo” alijibu Benson kwa wasiwasi.



“Sasa nishakutia mkononi, chagua moja nikupige bastola au uachane na Yulietha” alisema yule kijana wa kisomali.



“Yulietha!!!,” Benson alijifanya kushtuka mara baada ya kutajiwa lile jina na kujifanya kama hamjui huyo Yulietha.



“Unashangaa, inamaana humjui sio?.”



“Namjua.”



“Huyo, ni nani yako?.”



“Ni rafiki yangu tu, pia ni mwanafunzi mwenzangu ninayesoma naye darasa moja.”



“Stupid,” Kijana yule wa kisomalia alifoka na kumpiga kibao cha nguvu Benson. Kisha akaendelea kuongea kwa kuuliza.



“Yulietha nani yako?...rafiki yako!!!, hizi picha za kukisiana zimetoka wapi?,” Kijana yule wa kisomali aliuliza huku akimwonyesha baadhi ya picha Benson.



“Ukweli kuwa, Yulietha kabla hatujawa marafiki tulikuwa wapenzi... kwasasa tushaachana” aliongopa Benson mara baada ya kujua kuwa yule kijana wa kisomali kashajua uhusiano wake na Yulietha.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Oooh, najua unajitetea sasa nasema hivi kuanzia leo nikikuona sehemu yoyote na Yulietha nakumaliza...umenielewa?” alifoka yule kijana wa kisomali kwa kuyatoa macho kwa hasira kisha aliuliza.



“Ndi ndi ndi, ndiyo” alijibu Benson kwa uwoga.



“Haya haraka telemka kwenye gari langu, na upotee machoni mwangu kabla sijakufanya kitu mbaya” aliongea yule kijana wa kisomali na kuonyesha vitisho kwa Benson.



Benson akateremka kwenye gari alipoteremka tu akatoka mbio kama mwanariadha, hakusimama sehemu yoyote hadi alipofika kwenye hosteli yao kuingia tu hosteli akamkuta rafiki yake akijisomea. Peter alipomuona rafiki yake karudi huku akiwa anahema akajawa na shauku ya kutaka kujua yaliyojiri huko atokako rafiki yake.



“Benson mbona tunashtuana?, nini kinachokukimbiza?,” Peter akauliza.



“Rafiki yangu, wee acha tu,” Benson alijibu huku akiwa bado anahema.



“Siwezi acha kwa hili, wee niambie.”



“Yaliyonikuta, ni makubwa balaa.”



“Kimekukuta, nini?.”



“Si nimekutana, na yule jamaa.”



“Jamaa, gani?.”



“Yule, ambaye niliekueleza muda ule.”



“Aaah...eeenh imekuaje ulivyokutana naye?.”



“Mh...kumbe ni msomali bwana.”



“Eeeh, kweli!!!?.”



“Kweli, na hapa unavyoniona nimeponea chupuchupu kwenye tundu la sindano.”



“Kivipi?.”



“Si, alinishikia bastola na kunipa vitisho kuwa niachane na yule mwanamke.”



“Huyo, mwanamke mwenyewe ushamjua?.”



“Yaah.”



“Ni, nani?.”



“Ni, Yulietha.”



“Mh, rafiki yangu kama ushamjua huyo mwanamke bora uachane naye, maana wasomali kuua hawaoni tabu asije akakudhuru rafiki” aliongea Peter kwa kumsihi rafiki yake kuwa aachane na Yulietha mwanamke anayedaiwa ni mchumba wa msomali.



Wakiwa wanaendelea na mazungumzo mara ghafla ikazuka taharuki, mara baada ya wote kusikia mlango wao ukigongwa. Peter taratibu akaenda kufungua mlango kwa kunyata alipofungua akatahamaki na kushikwa bumbuwazi kukutana uso kwa uso na mgongaji ambaye alikuwa ni mwanamke. Peter akashangaa kwa kuduwaa bila kumkaribisha mwanamke yule ndani akawa anajifikiria kwenye mfumo wake wa ubongo jinsi yule mwanamke alivyomfanyia usaliti rafiki yake akatokea kumjengea chuki mazima.



“Benson, nimemkuta?” lilikuwa swali alilouliza yule mwanamke.



“Benson katoka, kaenda kumsindikiza mpenzi wake maabara,” Peter akadanganya.



“Unanidanganya, Benson ana mwanamke yeyote zaidi yangu” aliongea mwanamke yule kwa kujikweza.



“Unasema hana mwanamke mwingine zaidi yako, unaona uliyomfanyia ni mazuri?.”



“Kitu gani, nilichomfanyia?.”



“Wewe, una mpenzi msomali?.”



“Msomali!!!, msomali atoke wapi?.”



“Unajua ni siri, kwa taarifa yako Benson anajua kila kitu.”



“Kuhusu, nini?.”



“Anajua kuhusu mahusiano yanayoendelea, kati yako na msomali wako.”



“Kwahiyo ndiyo, kaamua kudate na mwanamke mwingine?.”



“Yaah.”



“No...msomali aliniapproch tu lakini sikumkubalia.”



“Unadhani, Benson atakuamini...wakati msomali alimfuata akamthibitishia na kumpa kitisho kikali.”



“What?.”



“Unachouliza nini?...au ni unafiki?.”



“Najua hamtoamini, ila ninachojua kuwa ukweli ni kwamba huyo msomali aliniapproch full stop.”



“Ingekuwa msomali wako kafanyiwa kitu mbaya ungesema hiyo full stop, au kwasababu kafanyiwa Benson kwako ni furaha.”



“Hapana, Peter sina maana hiyo...Benson kwani kaenda maabara ipi, ya hosteli au?.”



“Unauliza, ili iweje?.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nikaongee naye, tuyamalize.”



“Yulietha, Yulietha usijisumbue maana huyo Benson hataki hata kukuona.”



“Sawa naenda, lakini nitarudi tena kuomba msamaha japo sijatenda kosa...nampenda sana na sitaki kumpoteza Benson” alisema kwa majonzi mwanamke yule aliyetambulika kwa jina la Yulietha.



Yulietha hakukaribishwa ndani kabisa na Peter akaishia nje mpaka anapoaga na kutaka kuondoka bado alikuwa nje, lakini akiwa anataka kuondoka akasikia kwenye hosteli ya kina Peter mtu akipiga chafya mfululizo akagundua ndani mule kuna mtu. Yulietha ikabidi ahairishe kuondoka kwa kutaka kujua aliyepiga chafya ni nani angali Peter alimwambia kuwa Benson hayupo.



**********

Mathias akiwa yupo chini amedondoka hajielewi, ikatokea gari aina ya TOYOTA RAUM ndani ya gari hilo akashuka binti mwenye mwonekano wa kiwadhifa. Yaani ni mwanamke mwenye pesa zake akasogea hadi kwenye mwili wa Mathias.



“Huyu kaka, kimemkumba nini?” alijiuliza moyoni Binti yule.



“Kapatwa na ajali, nini?” alizidi kujiuliza.



“Ngoja nitoe msaada wa kumpeleka hospitalini, naona mapigo yake ya moyo bado yanadunda” alisema Binti yule mara baada ya kushika eneo la kifuani mwa Mathias.



Moja kwa moja dada yule akampakiza Mathias kwenye gari lake kisha akamuwahisha kumpeleka hospitali ya MUHIMBILI, muda ulikwenda sana hivyo binti yule alivyompeleka Mathias hospitali hakukaa sana. Akatoa maelekezo kwa madaktari kisha akaondoka akitegemea kurudi kesho kuja kumwangalia mgonjwa. Mathias akaendelea kutibiwa vyema na matabibu wa pale hospitalini, kesho yake kama ilivyonenwa na mnenaji binti yule akarudi tena kumjulia hali mgonjwa wake. Baada ya kufika akaingia kwenye ofisi ya madaktari alipofika akamkuta daktari mmoja akipitia baadhi ya x rays za watu na muuguzi akiwa kando yake akifanya usafi.



“Habari, daktari” alimsalimu daktari Binti yule mara baada ya kuketi kwenye kiti.



“Salama, nikusaidie nini?” aliitikia daktari huku akivua miwani yake.



“Kuna mgonjwa wangu, nilimleta jana na nikamuacha kwaajili ya matibabu...sijui nimemkuta?.”



“Wa kike, au wa kiume?.”



“Wa kiume, ni mwenye rangi ya maji ya kunde na ni mrefu kiasi...kwani umemuona asubuhi ya leo?.”



“Nilimuona, ila mbona kasharuhusiwa.”



“Muda, gani?.”



“Si, muda mrefu hata kwenye lango kuu sijui kama kafika.”



“Okay, mlivyo mpima mmekuta anasumbuliwa na nini zaidi?.”



“Hana ugonjwa wowote, ni mawazo tu yanayomsumbua” alicheka kidogo daktari kisha akaendelea kuongea.



“Kijana yule anahitaji sana, mtu wa kumfariji maana nilivyomwangalia kichwani kuna mambo mengi yanamtatiza.”



“Nimekuelewa Daktari, acha niende” alikatisha maongezi Binti yule na kuondoka kumuwahi Mathias.



Binti yule hakuchelewesha muda haraka akatoka kwenye ofisi ya daktari na kukimbia mbio mbio kumkimbilia Mathias, alipofika nje ya hospitali akajaribu kung'aza macho kila pahala labda ataweza kumwona tena Mathias lakini kwa wingi wa watu ikawa ni vigumu kumwona kirahisi.



**********

Daktari mkuu wa hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI hakuamini taarifa zilizoletwa na muuguzi, akanyanyuka na kumfuata Coletha wakathibitishe walipofika kwenye wodi aliyolazwa Mama Coletha wakakuta wauguzi wakiwa wamekizunguka kitanda alicholazwa Mama Coletha. Wakifikiri jinsi gani wafanye mgonjwa apate ahueni. Daktari mkuu alipofika akakasirika sana kuona madaktari kumi wote wameshindwa kumtibu Mama Coletha ipasavyo.



“Stupid, huu ni uzembe usioelezeka,” Daktari mkuu alifoka huku akiwasukuma baadhi ya madaktari nyuma apate nafasi ya kusimama mbele angalie ujuzi gani afanye ili Mama Coletha apone.



“Mapigo ya moyo yanafanya kazi, ila tumetumia mbinu zote lakini hatuoni dalili ya kuamka” alizungumza Daktari mkuu msaidizi kwa upole.



“Mmecheki, vipimo?” aliuliza Daktari mkuu kwa kuwakazia macho baadhi ya madaktari.



“Oooh, shit tumesahau” alijibu Daktari mkuu msaidizi kwa masikitiko.



“Umeona uzembe...hebu nipisheni nifanye vipimo mnaweza kuua mtu hivi hivi” alizidi kufoka Daktari mkuu huku akimsukuma nyuma msaidizi wake kwa hasira.



Daktari mkuu alivyopokea jukumu lile akaanza kuchukua vipimo kwenye mwili wa Mama Coletha alichukua vipimo vyote kisha akawatawanyisha madaktari wote waliokuwa kwenye chumba kile wakaendelee na majukumu mengine na yeye mara baada ya kumaliza vipimo wakaongozana na Coletha hadi ofisini kwake akampatie majibu ya mama yake.



“Tafadhali, kaa kitini” aliongea Daktari mkuu mara baada ya kufika ofisini kwake na Coletha. Coletha akakaa chini kwaajili ya kusikiliza anachotaka kuambiwa na daktari mkuu.



“Pole sana...nastahili kukuambia kuwa vipimo vya mama yako vinaonyesha kuwa amepooza mwili,” Daktari mkuu alianza kwa kuongea hivyo.



“Eti!!!” alisema Coletha kwa mshtuko na hapo hapo akakosa nguvu na kuzimia.



Daktari mkuu haraka sana akamuwahisha Coletha wodini akapumzike kwa muda, akamsubiri pale wodini kwa muda baada ya masaa mawili mbele Coletha akarudisha fahamu. Aliporudi katika hali yake daktari mkuu akampa ruhusa ya kwenda nje akapate upepo zaidi, Coletha akajikongoja hadi mapokezi akaenda kuketi kwenye kiti huku akijisikilizia hali yake lakini akiwa ameinamisha kichwa chini pale mapokezi, akatahamaki kumwona Mathias mbele ya uso wake akashangaa sana huku asijue Mathias kaja kufanya nini pale hospitali.



“Mathias, unafanya nini hapa?,” Coletha akauliza.



“Nimekuja, hospitali.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Unaumwa?.”



“Ni uchovu tu umepelekea kudondoka njiani...lakini msamaria mwema aliniokota inavyosemekana ndiyo akanileta hospitalini kwaajili ya matibabu.”



“Pole, sana.”



“Asante...wewe je mbona nawe hupo hapa nini kilichokukuta?.”



“Mimi ndipo ninapofanyia kazi hapa, ila nimemleta mama yangu atibiwe maana anaumwa sana.”



“Aisee, nini zaidi?.”



“Amepooza, mwili.”



“Daah, pole sana.”



“Nishapoa...huyo msamaria bado yupo?.”



“Aliondoka sema, daktari aliniambia kuwa atarudi tena leo kunichungulia hali yangu.”



“Oooh, ndiyo unamsubiri hapa mapokezi?”



“Hapana, naondoka maana nishamsubiri sana kwenye ofisi ya daktari lakini hakutokea.”



“Lakini, huoni kama ukiondoka nyuma atakuja kukutafuta.”



“Lakini ni kweli, ngoja nivute subira kwa kumsubiri...naweza nikaungana na wewe hapa?.”



“Usijali, wewe kaa tu.”



“Kwa hiyo, leo hujaingia kazini?” aliuliza Mathias mara baada ya kuketi naye kitini.



“Niliingia, lakini kwa kuwa mama anaumwa inabidi nisiingie tena kazini.”



Mathias na Coletha wakiwa bado kwenye mazungumzo yao ya kawaida, wakaja kukatishwa mazungumzo yao na binti yule aliyetoa msaada kwa Mathias ambaye kwa muda wote alikuwa anamtafuta Mathias.



“Habari, yenu,” Binti yule alikatisha yale mazungumzo kwa kusalimu.



“Safi tu, karibu tukusaidie lolote?” aliuliza Coletha mara baada ya kuona sura ile ngeni kwa upande wake.



“Najua wote hamnijui, mimi naitwa Anitha ndiye niliyemsaidia huyo kijana” alijibu Anitha kwa kujitambulisha.



“Oooh, mimi naitwa Mathias na huyu ni Coletha ni daktari katika hospitali hii...shukrani sana dada yangu,” Mathias aliongea kwa kudakia kwa furaha mara baada ya kujua Anitha ndiye aliyetoa msaada kwake.



“Nashukuru kuwafahamu...mimi nilitoa ahadi leo ya kuja kuona hali yako lakini sikukukuta ndipo daktari kaniambia alikuruhusu,” Anitha akasema.



“Ni kweli aliniruhusu, na hapa unionapo nilikuwa nakungoja nitoe shukrani” alisema pia Mathias.



“Okay...tunaweza tukatafuta sehemu tuongee,” Anitha alitaka kidogo kutoka na Mathias sehemu tulivu wakaongee.





“Sawa, tu,” Mathias akakubali.



“Dada, sisi ngoja tukuache,” Anitha alimgeukia Coletha na kumwambia kwa kumuaga.



“Sawa, kwaherini” aliaga Coletha kisha akaachwa pale mapokezi peke yake mara baada kuondoka Anitha na Mathias.



Anitha akaongozana na Mathias moja kwa moja hadi kwenye parking walipofika eneo la parking wakapanda gari na kuanza safari, ukimya ukatawala kwa muda ndipo ukimya ukaja kuvunjwa na Anitha kwa kuanzisha mazungumzo.



“Eti, sehemu tulivu ni wapi?.”



“Naona, hotelini.”



“Mmmh, hotel ya LANDMARK tukienda si itapendeza?.”



“Yaah.”



Wakakubaliana kwenda hivyo Anitha akatembeza gari hadi kwenye hoteli waliyokubaliana, walipofika wakashuka ndani ya gari kisha wakaingia ndani ya hoteli na Anitha akamuita mhudumu wa hoteli ile baada ya kuketi kitini. Mhudumu hakuchelewa kwa kuwa ni wajibu wake kumsikiliza kila mteja hivyo akaenda kusikiliza wito wa mteja.



“Kuna, chakula gani?,” Anitha aliuliza mara baada ya mhudumu kufika kwenye meza yao.



“Kuna chipsi kuku, chipsi yai na kuna ndizi nyama choma” alijibu Mhudumu kwa uchangamfu.



“Niletee chipsi kuku...unakula nini Mathias?,” Anitha alisema na kisha akamuuliza Mathias.



“Nitakula, chipsi yai,” Mathias akajibu.



“Kuna, vinywaji gani?,” Anitha alimuuliza tena mhudumu mara baada ya Mathias kujibu.



“Kuna Safari lager, Serengeti lite na Ndovu, upande wa soda kuna Fanta orange, Mirinda orange na Pepsi pia kuna maji makubwa ya Hill,” Mhudumu akajibu.



“Nigee maji makubwa...unakunywa nini Mathias?,” Anitha alimuuliza tena Mathias.



“Nitakunywa, Fanta orange,” Mathias alijibu huku akipepesa macho yake kwa watu waliokuwepo pale.



Mhudumu baada ya kuwasikiliza wateja akaenda moja kwa moja kuleta vyakula vilivyoagizwa, akatoa huduma akalipwa kisha akaondoka kwenda kutoa huduma kwa wateja wengine huku nyuma akimwacha Mathias na Anitha wakiongea mazungumzo yao binafsi.



“Nashukuru sana, kwa msaada wako umetoa mchango mkubwa juu yangu” alitoa shukrani Mathias kwa Anitha kwaajili ya msaada aliompatia.



“Usijali, nimetoa msaada kwa moyo na kwa huruma yangu hivyo huna budi ya kunishukuru sana,” Anitha alisema huku akiendelea kupata chakula.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Lakini ni binadamu wachache wenye moyo na huruma kama wako, hivyo nisipokushuru nitakuwa sijakutendea haki.”



“Naelewa hilo, ila hapa sijakuleta kwaajili ya kunishukuru nimekuleta hapa kwaajili ya maongezi yetu ya faragha.”



“Maongezi gani hayo, ya faragha?” aliuliza Mathias kwa kustaajabu kidogo.



**********



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog