Search This Blog

Friday, November 18, 2022

SITOWEZA KUKUSAHAU - 3

 






Simulizi : Sitoweza Kukusahau
Sehemu Ya Tatu (3)




Wafuasi hawa walikaa zaidi ya nusu saa chini ya mto huku wakimsubiria Zulfa aliyekuwa kwenye gari lakini hakutokea.Zulfa baada ya kuhisi gari imemshinda alifungua mlango na kuruka mpaka nje ambapo alifanikiwa kujikamatia kwenye chuma la daraja hilo.Nusu aliachie kutokana na maumivu aliyokuwa anayapata.Akajipindua na kurudi juu ya dalaja.Akakutana na gari mbili zilizokuwa zimesimama.Kitendo cha sekunde mbili tu alivunja kioo na kufungua mlango wa gari moja kati ya yale.Hakukua na funguo,aliamua kutotoa waya unaonganishwa kutoka kwenye swichi na kuliwasha gari hilo.Akachomoa na gari hiyo huku akikoswakoswa na risasi na watu hao.Alihakikisha kuwa lazima awaache kwa umbali mrefu,kwani wanaweza kumteketeza na risasi.

Jamaa hao hawakuwa nyuma waliingia kwenye gari yao moja iliyobakia na kuanza kumfukuzia Zulfa ambapo muda huo alikuwa yupo mbali na wao.Gari hiyo ililalamika vya kutosha kutokana na kufinywa kwa mafuta mpaka mwisho,hata sehemu iliyokuwa na tuta dereva hakujari aliruka nao na kutua chini kama wanashindana.Askari barabarani walipojaribu kuwapungia mkono walikoswakoswa kugongwa na gari hiyo bado ilikuwa motobati.Hasira za askari hao wakajikuta wanapanda kwenye pikipiki zao kubwa zenye ving’ora na kuanza kuwafuatilia watu hao waliokuwa wanavunja sheria za barabarani.

“Hei simama” walifoka polisi hao ambayo walikuwa kwenye mwendo sawa na gari ya watu hao katili.

“Nimesema simamisha gari” waliendelea kufoka.Katika hali isiyo ya kawaida kwako,wakajikuta wanaachia stelingi baada kupigwa kwa risasi za kichwa.Wafuasi hawa walionekana hawana mzaha katika suala hilo.

“Maliza gia ya mwisho wewe acha ufala” alikuwa mmoja wa watu hao,akimtaka dereva aongeze mwendo.Gia ikaongwezwa bila hiyana.

“Weka spidi 120,maliza kabisa spidi au hujui unipishe?” alifoka kama chura aliyemeza panzi.Dereva hakutaka shali.Akakanyaga moto na gari sasa ikaanza kupaa huku ikitoa moshi mwingi sana.Hatimaye wakaikuta gari aliyopanda Zulfa,nayo ilikuwa kwenye mwendo kasi,zikawa zimekurubiana kwa kiasi kikubwa.Watu hao waliokamata bunduki mzito wakafungua vioo vya madirisha na kuanza kuimiminia gari hiyo risasi za kutokwa nyuma ya gari.Kioo cha nyuma kilikuwa nyang’anyang’a.Zulfa kuona hivyo akaanza kuikwenpeshakwepesha kwa mtindo wa kuilaza gari pande zote yaani ZIG ZAG.Akalikwepa roli lililokuwa linakuja mbele ya kwenye mkono wa kulia na kukaa sawa.Ghafla mlio mkubwa ukatokea nyuma ya gari yake.Ilikuwa uso kwa uso kati ya gari hiyo wafuasi na roli kubwa,zikiwa zimegongana vilivyo.Gari yao ikarushwa mbali na mlipuko ukasikika,tayari walishakwenda na maji.

****

Mipango ya kutekeleza kuvamia katika maeneo yaliyo na rasilimali kubwa,ilianza mara moja.Mzee Kibangara alikwisha weka wafuasi wake nchini Sudani tayari kwa kwenda kuvamia maeneo hayo.Walikuwa wapo kwenye msitu uliokuwa umetenganisha Sudan kusini na Sudani Kaskazini.Wakiwa wanaendelea kubadilisha mbinu mbalimbali za kuingilia maeneo hayo ambayo nayo yalikuwa katika ulinzi mkubwa mno.Ulinzi huo ambao ulisukwa na wanajeshi wa Raisi wa nchi hiyo wakishirikiana na wanajeshi wa Marekani,ulikuwa umesukwa na kusukika.Mitego kila sehemu walihakikisha inakuwepo kwa wingi.Mabomu ya kurusha kwa mikono nayo ikahusika.

Bado wafuasi hawa walikuwa wanaendelea kusuka mipango yao,mpaka giza likaingia palepale.Lakini hawakuonesha dalili zozote za kulala.Asubuhi yake,vikaanza kuja vifaru na magari ya kivita yaliyojaa silaha.Tayari walikuwa wanasubiria ruhusa kutoka kwa mkuu wao.

“Nimelekezwa kuwa tuataanza kazi usiku wa saa sita,hii itatusaidia sisi kuwavamia kwa urahisi,bado watakuwa katikati ya usingizi” walijadili jinsi watakavyowavamia wanajeshi hao wa Sudan Kaskazini.

“Ok,sawa”

Wote wakaitwa na kupanga mistari miwili iliyonyooka.Ujembe kutoka kwa mkuu wa Mzee Kibangara likatangazwa.Mkuu anayesimamia kikosi hicho,aligawa jeshi lake kwenye makundi matatu.Kikundi cha kwanza kitakiwa kupita upande wa kulia,kingine kilipita upande wa kushoto na kilichobakia kilipita katikati.Baada ya kufanya hivyo,wakatulia na kusoma ramani sehemu gani wakutane huko mbeleni.

Usiku ukaanza kuingia taratibu na hatimaye saa sita usiku ikahitimu.Kila kikosi kilijiweka tayari,walipeki mabomu ya mikono,bunduki mbili moja ikiwa migongoni na moja nyingine mikononi mwao,kiuno waliweka bastola pamoja na visu.Magazini za kutosha waliweka kwenye mifuko yao ya gwanda za kijeshi.Tayari safari ya kuvamia maeneo hao ikaanza huku nyuma yao kukiwa na vifaru vyenye makombola ya adabu.

Upande wa pili,majeshi ya Sudan kusini aliimalisha ulinzi vizuri na ilipotimu usiku,walilala kambini hapo huku wakiwa tayari kwa mashambulizi ya aina yoyote ile.Usiku wa manane ndani ya kandi hiyo,ghalfa mlipuko ukatokea ni mita chache kutoka kambini hapo.Sekunde tano wanajeshi wote walikwishajipanga ipasavyo.Mitutu yao ya bunduki ilikokiwa na kulenga sehemu husika.

“SIDE A go right hand and SIDE B go left hand(kund A nenda upande wa kulia na Kundi B nenda upande wa kushoto)”alitoa maelekezo mwanajeshi huyo wa kizungu,mara moja oda yake ikatekelezwa.Wakaanza kunyatia kuelekea mbele huku wakiwa na uangalifu mkubwa sana juu ya mabomu na mitego waliyoitega.Hawakukaa vizuri wakasikia mlipuko mwingine mbele yao.Sasa wafuasi wa Mzee Kibangara walikuwa wanavamia mitego na kujikuta wanalipuliwa kama ndege anayechomwa.Wafuasi waliokuwa wanalipuka ni haswa wale wa upande wa kulia.Kitendo kile kikawashtua wanajeshi wa Sudan kaskazini na hapo wakaanza kumimia risasi kwenye vichaka vyote vilivyozunguka upande huo wa kulia.Wakaa kimya zaidi ya sekunde sita mzima.Mara wafuasa hao wakaanza kujibu mashambulizi kwa kurusha mabomu ya mkono.Wanajeshi wa Sudan kaskazini walijikuta wanakufa kama kuku walioshikwa na mdondo.Ilikuwa ni ghafla sana kwao.Haikutosha sasa vifaru vikaanza kazi yake ya kuchalaza makombola kwenye kumbi hiyo.Kitendo kile kilimfanya mkuu wao achanganyikiwe ghalfa.Macho yake yakaanza kuiva na kuwa mekundu mithili ya mtu aliyekula pilipili kali.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Go and take a plane?” aliamuru watu wake,mpaka kwenye dakika mbili helkopta zilikuwa angani na mashambulizi yakaanza mara moja.Ikaongezwa helkopta nyingine.Kilichoendela hapo ni kunyongana kwa mabomu mazito kati yao.Kwa kuwa wafuasi wa Mzee Kibangara walikuwa bize kuzishambulia helkopta hizo,wanajeshi wa sudan wakapata wasaa mzuri wa kujipenyesha karibu yao na kuanza kuwamimia risasi kama mchele kwenye kuku.

“Songa mbele hakuna kurudi nyuma” ilikuwa sauti ya mkuu wa kikosi wa wafuasi hao waliooneskana kuzidiwa nguvu na wanajesho imara wa Sudan.Wakawa wanasonga mbele huku kifaru kilicho nyuma yao kikiachia mabomu ya hatari.

“Weka vizuri boya wewee” alifoka mmoja wa wafuasi hao ambaye alikuwa ameshikilia mzinga wa kudungulia ndege .

Bomu likawekwa ndani ya RPG yaani Rapid Propelled Grenade na kuiruhusu.Helkopta iliyokuwa inamimina risasi na mabomu ikawekwa kwenye tageti na mfuasi huyo na kitu kikafyatuliwa na kuisambalatisha helkopta hiyo,hapo hapo ikageuka na kuwa jivu tupu.Mapambano yaliendelea huku kila upande ukitoa mashambulizi ya aina yake.

Wakati wote huo Mzee Kibangara alikuwa na mwenzake mzee wa kiarabu mwenye sharaf ndani ya chumba cha mawasiliano.Walitazama mapigano hayo ambayo yanaendelea.

“Tuongeze nguvu au?” aliuliza mzee wa kiarabu.

“Hapana wacha tuone itakuwaje,washaanza kuzidiwa hawa” Mzee Kibangara alisema.

Mara wakati wanaendelea na mzungumzo,kikasikika king’ora kidogo kutoka kwenye mashine moja ndani humo,taa ndogo iliyowaka kwa rangi nyekundu ilimaanisha kuna hatari.Wakasogea haraka haraka na kuipokea.Kilikuwa ni kipande cha video kilichokuwa kinarushwa moja kwa moja kutoka kwenye eneo la mapigano msituni.Aliyekuwa mbele ya kamera alikuwa ni mkuu wa wafuasi hao ndani ya vita.

“My interest never die” Mzee kibangara alijikuta anaongea kwa sauti mzito iliyojaa hasira

****

***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Upepo uliendelea kumtesa Ramso ambaye bado alikuwa nje ya ndege hiyo.Mkono wa upande aliopigwa nao risasi sasa ukaanza kumuuma.Ramso hakukata tamaa akajikaza na kuhakikisha kuwa lazima aingie ndani ya ndege hiyo.Baada ya kuhangaika sana,akabahika kuukamata mlango wa buti.Alipojaribu kuusukuma ulikuwa umefungwa kwa ndani.Upepo unaenda kumshinda kwani ndege ilikuwa imepaa juu mno.Kasi yake ikaongezeka mara dufu.Akawa anaendelea kupiga mlango kwa nguvu zake,mpaka pini ya loki ikafyatuka na kufunguka.Ghfla upepo ukaanza kuvuma kwa kasi ukiingia ndani.Joto lililosababishwa na injini lilianza kumfunika Ramso ambaye alikuwa anahangaika kuingia ndani humo.Kitendo cha kushika chuma lililokuwa ndani yake,hapo hapo akajisokomeza ndani na kufunga mlango huo.Ramso akaanza kukohoa kwa nguvu huku akishika kifua chake.Upepo uliokuwa unampiga kwa muda mrefu ulimtesa sana kifua.Akajikuta anaingia ndani ya chumba kinachokaa injini ya ndege hiyo kinachotoa joto kufuru. “Katazame kuna mlango haujafungwa vizuri huko nyuma” alisema kepteni wa ndege hizo ambaye alikuwa anaitazama taa nyekundu ya HAZARD iliyokuwa inawaka. “Chumba gani?” “Cha injini,ila naona sasa kimetulia,lakini lazima ukahakikishe”.Mmoja wa marubani hao akatoka na kuanza kutembea kuelekea kwenye chumba cha injini.Akawatazama abiria waliokuwa wametulia tulii ndani ya ndege hiyo,vyuso zao zilionesha kuchoka mno na safari hiyo.Akafika na kufungua chumba hiko na kuwasha taa.Ukaguzi ukaanza kufanyika huku akiwa makini mno.Ramso alibana sehemu ndogo iliyojificha,haikuwa rahisi kwa rubani huyo kumuona.Wembamba wake ndio uliomsaidia kwa kiasi kikubwa.Alipohakikisha hakuna mtu yoyote akafunga mlango na kutoka zake.Ramso akazinduka pale alipojificha na kutoka kwenye chumba kile.Akafungua chumba kilichoandikwa STORE na kuingia ndani yake.Huko akakutana na mizigo mbalimbali,mikubwa na midogo,taratibu bila kelele ya aina yoyote akaanza kutafuta begi lake. “Litakuwepo kweli humu?” alijiuliza mwenyewe hukua akiendelea kuchambuachambua mizigo.Mara akajikuta anaachia tabasamu la nguvu mara baada ya kuliona begi lake likiwa limelala chini ya mizigo mingine.Akalichukua na kulifungua. “Oooh Mungu mkubwa” alijisemea peke yake huku akizitoa baadhi ya pesa na kuzipeleka puani,akazinusa na kuzirudisha.Alipogeuka tu akahisi mapigo ya moyo yanamuenda mbio.Alikutana uso kwa uso na mhudumu wa kike ambaye alikuwa kavalia nguo zake za kikazi.Hakuamini kabisa tukio lile.Hakika alikuwa katika hali ya kupigwa na butwaa. “Umefuata nini huku?” aliuliza mhudumu yule kwa shauku. “Nimekuja kuchukua mzigo wangu” alisema na kumuonesha begi lake. “Nani kakutuma?,ahaa kumbe nyie ndio wezi eeh” alihamaki mhudumu huyo. “Hapana sio mwizi,mimi ni abiria safi tu” alijitetea Ramso.Mhudumu huyo akachukua simu yenye mkonga nje na kubofya namba,ila hakubahatika kuipiga,tayari alikuwa kazuiliwa na Ramso na kushika shingoni. “Ukifanya huo ujinga nakumaliza sasa hivi” Ramso alifoka kwa sauti mzito iliyojaa ukatili.Roba ilikuwa mzito na kumfanya mhudumu huyo kuhema kwa shida huku akishindwa kuongea.Ikamlazimu Ramso apunguze kumkaba,akamvutia pembeni kabisa na kumkandamiza ukutani. “Ukipiga kelele nakunyonga sasa hivi” alisema Ramso kwa mnong’ono mkubwa.Mhudumu hakuwa na jinsi,aliitikia kwani kifo sio rafiki sana kwa binadamu,hasa ukizingatia mtu aliyekuwa mbele yake alikuwa na sura iliyojaa ukatili na mwenye nguvu kushinda yeye. “Sikiliza,nataka unisaidie kutoka humu baada ya ndege kutua,sawa?” ‘Ndio”Mhudumu huyo alitia huruma.Alinywea kama maji jagwani.Ramso akajikuta kuwa na moyo wa upole kwa binti yule aliyekuwa amevalia sketi fupi na shati jeupe,kichwani alivaa kofia ndogo yenye nembo ya kampuni ya ndege hiyo.Akamshika kidevu chake japokuwa mwili wa binti huyo ulikuwa unatetemeka kama simu iliyowekwa vibration. “Usiogope” alisema Ramso kwa sauti ya upole,lakini haikuwa rahisi kumtuliza mtetemeko huo uliojawa na woga.Taratibu mdomo Ramso akaugusanisha na mdomo wa mhudumu huyo.Akanyonya mdomo wake wake juu,kitu ambacho kilimpelekea mhudumu huyo kuanza kutoa ushirikiano.Ghalfa safari ya huba ikawakolea kilichoendelea hapo ni kuvuana nguo zao huku wakishikashika kila sehemu ya miili yao.****Zulfa akaacha gari hiyo maeneo ya Mbezi na kuanza kutembea kwa mguu huku akiwa anahema kama bata.Akafika nyumbani kwake na kuingia ndani.Giza ilikuwa limeingia haswa na sasa ilikuwa saa tatu za usiku.Akaingia bafuni na kujimwagia maji.Alipomaliza akarudi chumbani kwake na kuvaa mawazi mengine.Akatoka mpaka sebleni na kuiwasha TV yake huku akijituliza na juisi ya parachichi.Taarifa zilizokuwa zinaendelea kwenye vituo mbalimbali vya TV ni juu ya suala zima la machafuko ya nchini Sudan.Mabomu na makombola yaliendelea kulindima katika eneo hilo la msitu.Hakukaa dakika tano mara matangazo yaliokuwa yanaruka laivu kutoka kwenye runinga yale ya ajari ya gari lililokuwa linamkimbiza.Moshi mwingi ulitanda sehemu hiyo,ilionesha dhahiri ilikuwa ni ajari kubwa tena kubwa mno.Zulfa akaizima na kuingia chumbani kwake,mpaka ilipotimu saa sita usiku akapitiwa na usingizi moja kwa moja.**** “Go ahead(songa mbelee)”sauti ya mkuu wa wafuasi wa Mzee Kibangara alifoka huku akiwa amejishika mguu wake ambalo amepigwa nao risasi.Wakaendelea kusonga mbele japokuwa mageshi ya Sudan yaliwazidi nguvu. “We need support Sir(Tunahitaji msaada mkuu)” akatoa taarifa kutoka makao makuu.Kwa kweli walikuwa wamezidiwa mno,hakukua na hata mfuasi ambaye aliweza kumudu vita ile.Ikawalazimu wajifiche sehemu ambayo sio rahisi sana kwa wao kuonekana.Kikosi kikapagwa upya,ila wengi wao walikuwa wamejeruiwa vibaya sana. “Sasa wote,tunaenda msitari mmoja,hakuna kurudi nyuma,nyie wa vifaru,sasa hivi mnatangulia,ila muda si mrefu tutapata msaada kutoka makao makuu sawa?” “Ndiooo mkuu” wote waliitikia kwa pamoja.Mara moja vifaru vikaanza kusonga mbele na kuvunjavunja miti iliyoonekana kuzuia vifaru hiko kisipite.Wafuasi hawa wakawa wanafuata nyuma katika mstari mmoja mrefu.Silaha zao zilipekiwa vizuri na kukaa sawa.Ghafla vifaru vikaanza kushambulia mbele na upande wa mbele ukawa unajibu mapigo,kilichokuwa kinawapoteza kwenye ramani ya mapigano haya ni vile wanajeshi wa Sudan alivyokuwa wanatumia chopa kupiganaChopa zilikuwa na uwezo wa kurudi nyuma na kuwadhibiti adui zao,hapo alifyekwa kama nyama buchani.Haikuchukua muda mrefu ndege helkopta mbili zikawasili kwa kasi ya ajabu na kuanza mashambulizi.Mapigano yakawa yamegeuka angani ambapo chopa moja inapigana na helkopta mbili.Uwezo wa chopa ulikuwa mkubwa zaidi ya helkopta hizo za wafuasi hawa wa kibangara.Ilikuwa pata shika nguo kuchanika.Huku chini nako kuliendelea kulindima,hakuna hata upande mmoja uliommpa mwenzake nafasi ya kumpiga.Punde si punde Helkopta moja ikaanguka na kulipuka,mara baada ya kudunguliwa na kombola lililotoka kwenye Chopa.Sasa ilikuwa imebakia helkopta moja kwa upande wa wafuasi na Chopa ya wanajeshi wa Sudan.Mapigano yaliendelea huko angani ni zaidi ya vita vya pili vya dunia.Haikupita tena dakika kumi helkopta ya pili ikaanduka chini na kulipuka.Wafuasi wakaanza kuchoka,hakukua tena na msaada,kilichofuata hapo ni kurudisha nyuma majeshi na kujipanga upya.Lakini watawezaje na wamewekwa kwenye tageti na ile Chopa inayotawala anga. “Tumekwisha mkuu” alipita simu makao makuu na kumueleza Mzee kibangara. “Dakika tatu nimetuma chopa mbili na helkopta tatu zenye wanajeshi,endeleeni na pambano” “Sawa”.Akakata simu na kuwatazama wenzake. “Hatuendi popote,sisi tutakaa hapahapa,chopa zinakuja na wanajeshi wengine”.Wakaamua kukaa sehemu walijificha kimya huku wakiugulia maumivu ya majeraha yao.Kwa mbali sana wakaanza kusikia mlio wa ndege zinakuja kwa kasi kutoka upande wa kusini mashariki mwa upande wao,na bila kupepesa macho sana,wakaziona chopa mbili zikiwa zina na helkopta tatu zinatumia umbali mrefu kidogo kutoka pale walipo.Simu ikapigwa na kuambiwa kuwa ndio wao waliokuwa kutoa msaada wamewasili tayari.Wakawa wanajikongoja kuelekea mahali hapo.***Mtanange ukaendelea kati ya Ramso na mhudumu wa ndege huku kila mmoja akiwa anamvutia pumzi mwenzake.Hawakukamilisha mambo yao ambayo muda huo waliwaweka kwenye hali ya ubize,mara mlango ukafunguliwa na mmoja wa mhudumu wa kiume ambaye naye pia alivalia sare zake akaingia katika chumba kile cha kuhifadhia mizigo.wakasitisha mipango ya na kukaa kimya katika ule mpenyo waliojificha.Punde akaingia mhudumu mwingine wa kike huku akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa. “Eeeeh umemuona Josephina?” akamuuliza yule mhudumu wa ndege huku akiwa na wasiwasi mno. “Hapana kwani hayupo huko?” akajibu jamaa. “Hayupo,itakuwa kapotelea wapi sijui maskini!” akajikuta anaishiwa nguvu sana kwani hofu ya kupotea kwa Josephina ambaye mpaka dakika hiyo yupo mule mule ndani na tena anawasikia wahudumu wenzake wanavyohangaika kumtafuta,maana ni muda mrefu sana tangia wamuone.Mioyo yao ikawa inaenda mbio kama gari lililofeli breki.Walichopagawa zaidi ni baada ya kumuona jamaa huyo anakuja upande waliokuwepo wao.Hapa Ramso alihisi kutokwa na haja kubwa kwani tumbo lote likawa linawaka moto kwa hofu.Wakasogea tena pembeni huku mkono wa Ramso upo mdomoni mwa mhudumu huyo,ili asipige kelele.Kumbe jamaa huyo hakuwa na muda wa kuingia sehemu walipo wa tu hawa.Akachukua mzigo wake na kutoka nje ya chumba. “Sikiliza sasa,mimi siwezi kuendelea na haya mambo,naomba unisaidie kitu kimoja sawa?” akasema Ramso kwa sauti ya kunong’ona “ndege ikifika uwanjani nitakuomba uwe wa mwisho kutoka ili mimi nitoke na wewe,nadhani wataamini kuwa mimi ni msafiri wa kawaida sawa?” “Kwanza we umeingiaje huku afu umenitia nyege hutaki kuzishusha” “Hilo swala ondoa kwa sasa au hutaki pesa wewe?” akauliza Ramso huku amemkazia macho mhudumu huyo. “Hela ukawa nazo wewe?” mhudumu akajibu kwa dharau.Kitendo hicho kikamfanya Ramso achukue begi yenye pesa na kumfungulia. “Eeeeh!” akastaajabu kuona lundo la dola limejipanga kwenye begi. “Usipige kelele sasa,utafanya kama nilivyokuelekeza?” “Ndioooo” akaitikia mhudumu huyu kwa haraka mno. “Haya nenda sasa wenzako wanakutafuta ila usinitaje kama ulikuwa na mimi sawa!” “Sawa sina shida” akavaa nguo zake na kutoka katika chumba kile huku akiwa anatazama tazama nyuma.Ni muda mchache baadae ndege hiyo ikawa anga ya uwanjani.Ikatanguliza taili zake za nyuma na kumalizia za mbele,ikaanza kukimbia kwa kasi na hatimaye ikaanza kupungua mwendo na kusimama kabisa.Ngazi iliposhushwa,watu wakaanza kutoka wakiwa na mizigo yao midogo midogo na kupokelewa na ndugu zao,wengine wakapanda kwenye taksi zilizopo kwenye uwanja,ila michakato hiyo waliifanya baada ya kupitia sehemu ya ukaguzi na kuonekana hawana magendo.Ramso bado huyo kwenye chumba cha mizigo akisubiri mdada mhudumu aje kumtoa,akasubiria kama dakika kumi mpaka kumi na tano,ndipo mlango ulipofunguliwa na kutokea mhudumu.Akamuita Ramso na wakatoka kwenye kile chumba huku wakiwa makini ili wasije wakaonekana na wahudumu wengine wanaoweza kuwatilia wasiwasi.Wakawa wametoka salama salmini kwenye ndege hiyo,ndipo wakapanda kwenye moja taksi iliyopo uwanjani hapo na kuanza kupeana mishiko kama walivyoaidiana. “Unanipa dola ngapi?” “Hebu tulia basi nawe,shika hizo zinakutosha” Ramso akampatia dola ambazo aliona kuwa zinamtosha na mhudumu huyo akaonesha kufurahi mno.Akajikuta anamuacha Ramso na busu la mdomoni huku wakibadilishana namba za simu zao..Wakati huo wote dereva wa taksi hiyo alikuwa anatazama mchezo mzima uliokuwa unafanyima nyuma ya gari yake.Kuanzia dola zilizojaa kwenye begi na mabusu yale. “Nakuja kidogo kaka,dakika sifuri” akaaga dereva huyo na kumuacha Ramso ndani.Akajificha sehemu na kutoa simu yake,akawa anawasiliana na watu wako. “Oyaa kuna mchongo wa pesa ndefu hapa nimemgumia mteja mmoja hivi,yaani kajaza kwenye begi” akasema huku akiitazama gari yake mara kadhaa. “Ndio,nyie kaeni hapo njia ya kwenda kwa ZULU HOTEL mimi nampitisha hapo,ila msisahau na ile mashine yenu ya MP5 inanikoshaga sana mlio wake” “Basi poa msizingue sasa,na mimi lazima nile mshiko mrefu leo” akamaliza maongezi na kuikata simu kisha akarudi kwenye gari. “Samahamu braza kwa kukuweka”………………………..

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Dereva huyo akaingia ndani ya gari yake na kuondoka uwanjani pale huku mara kadha akimtazama Ramso kupitia kioo cha kati.Kichwani mwa Ramso hakukuwa na kingine anachowaza zaidi ya familia yake aliyoiacha miezi miwili bila mawasiliano ya aina yoyote.Leo anrejea salama akiwa na fuko la pesa mkononi,akajifariji kuwa baba alienda kutafuta na amerejea na kitu fulani chenye maana.Hakujua kwamba pesa zile zinamendewa na vijambazi vilivyotonywa na dereva taksi.Gari hiyo ilikuwa inaenda kasi kidogo lakini baadae ikaanza kupunguza mwendo wake,hakufika mbali sana akakuta gogo limetandikwa barabarani.Dereva akajua hapa ndio penyewe,ni sehemu ya kuvuma matundu kwa kumpora Ramso begi la pesa,laiti wangelijua begi hilo alivyopata nalo shida mpaka kufika nalo sehemu alipo,halafu wanataka kumkatili,wasingelifanya kitendo hicho.Ramso akashangaa kuona goyo lile kubwa lililozuia barabara,maswali mengi yakawa yanajigonga kwenye almashauri yake ya kichwa lakini hakupata jibu.

“Oyaa vipi?” akauliza kwa wasiwasi.

“Hata mimi nashangaa bosi” kabla hawajamaliza kuuliza,mbele yao akatokea jamaa aliyeshika bunduki aina ya MP5,akaikoki na kuitazamisha mbele ya kioo hicho cha gari.Kwa kuzuga tu dereva akawa anajifanya kutetemeka na kunyoosha mikono juu,kitendo kile kikamfanya jamaa huyo kuja upande wa dereva hiyo.Haikutosha wakatokea jamaa wapatao tano wakiwa na marungu,hapo ndipo Ramso alipoanza kuhisi haja ndogo inataka kutoka bila breki.Alichokitafakari kwa haraka haraka,akapindukia mbele kwa dereva kwa spidi kama umeme na kukishika kindoka kisha akakisogeza kwenye herufi R,akamtoa mguu dereva aliyekuwa mikono juu na kuanza kufinya moto.Gari ikawa inarudi nyuma kwa kasi huku risasi zikawa zinamimika kwa kasi mbele ya kioo.Akamsukumia dereva nyuma ya siti na kuukalia msukani.Akapiga resi ya nguvu na kuiweka gari sawa.Jamaa hao ambao bado walikuwa wanamimina risasi wakajikuta wanafeli na kuishia kutukana tu.Wakawa wanarudi wanakotoka huku gari ikiwa kama imetengenezwa miaka ya sabini kwani ilikuwa imechakazwa vya kutosha.Katika hali ya kushangaza wapo njiani,mara dereva aliyekuwa nyuma,akachomoa bastola na kumuoneshea Ramso aliyekuwa bize kwenye msukani.

“Simamisha gari fala wewee,unakimbiza pesa,unataka tukale wapi?” akatamka maneno hayo dereva huyo huku akiwa ameikamata kikamilifu bastola yake.Ramso akasimamisha gari pembeni ya barabara.

“Mikono juu” akaamrishwa,Ramso hakuwa na tabu akaweka mikono juu.Muda wote alikuwa anausoma mchezo wa dereva huyo ambaye alikuwa na uchu wa pesa ya haraka.

“Toka njee,hara….”hakumaliza hata sentensi yake,akahisi anavujwa na damu puani,maumivu makali yakawa yanamtawala.Ramso alikwishafanya yake,alimpiga kisigino chake cha mkono wa kushoto kwa nguvu zote,dereva akaiachia bastola na kuishikia pua yake ambayo ilikuwa kwenye breeding.Haraka Ramso akaishika bastola na kumuweka kwenye mikono yake.

“Unajua hizi pesa zimetoka wapi,unapenda sana pesa za haraka eeeh,sasa utaeleza leo” Ramso akasema na hapo hapo akawa akamuongezea kumtwanga ngumi zikiwa za sikioni na zingine za kichwani,alipompiga ngumi ya shingo akapoteza kabisa netiweki,akawa amezimia na hajielewi kabisa kama yupo dunia au sehemu gani.Akashuka fasta na begi lake na kuanza kukimbia kurudi mjini.Alipofika akachukua mabasi yaendayo mji ungine.Baada ya lisaa limoja akawa amefika maeneo ya nyumbani kwake,akaanza kutembea huku akiwa na tabasamu zito kwenye uso wake.Matumaini ambayo yalipotea kwa muda mrefu,sasa yakawa yametimia.Akafika hadi mlangoni kwake,taratibu akaanza kugonga mlango.Zaidi ya mara tatu mlango ulikua kimya.Akaendelea kuugonga bila kukata tamaa.Mwishowe akasikia sauti ya mke wake akifurahi mno ndani.Ramso tabasamu lake likawa linaongezeka usoni.Kwa kweli aliimisi kuisikia sana sauti ya mke wake,akajitayarisha tayari kwa kukumbatiwa ni kama kawaida ya mke wake huyo.Mlango ukatolewa loki na ghafla uso kwa uso na mke wake ambaye wakati huo alikuwa amevalia vazi laini mno,vazi ambalo lilimchora vziuri umbo lake.Kilichomtia wasiwasi Ramso hakuona ile hali ya kukumbatiwa,hakuona sura ya furaha kwa mke wake.Hapo ndipo tabasamu la Ramso likawa linapotea taratibu.

“Mke wangu vipi kwani,mimi mume wako nimerudi” akasema hivyo lakini cha kushangaza mlango ukabamizwa NDIII na Ramso kubaki nje akiwa na msahngao wa kutosha.Kinachotokea machoni mwake ni kama miujiza fulani au ndoto aliyokuwa anaota katikati ya usingizi mzito.

“Lakini kama ndoto,mbona najaribu kuamka siamki,hapana hii sio ndoto,mbona macho yangu yamefumbuka?” alijiuliza maswali mengi sana.Moyo ukawa unamuuma kweli kweli,kitendo cha mke wake kumfungia mlango,kilimfanya ajihisi kuwa amekosa amani yote kwenye dunia,akatamani sana dunia iishe siku hiyo ili kila mmoja afe na chake.

“Mama Gadna,mimi mume wako,tafadhali nimerudi fungua mlango basi eeh” akalalamika pale nje kama mtoto mdogo maskini lakini hakukuwa aliyejibu ndani yake.



Mama Gadna alikuwa amejiinamia nyuma ya mlango huku anaangusha chozi la huzuni,kitendo cha kumsaliti mume wake kilimuuma mno,ukizingatia mwanaume huyo yupo ndani humo akiwa amejificha sehemu,tena baada ya kutoka kufanya ngono.Kadri alivyokuwa anaisikia sauti ya mme wake Ramso,alitamani ardhi ipasuke aingie ndani ili asionekane kabisa na Ramso.Akajikuta anajifuta machozi na kufungua mlango.



****

“Wapange mstari mmoja haraka sana” ilikuwa sauti ya mkuu wa kikosi cha Wafuasi wa Mzee kibangara,kikiwa kimewafyeka wanajeshi wengi wa Sudan.Sasa wakawa wanahakikisha kama kweli wameshapoteza maisha kabla hawajaingia rasmi kwenye eneo husika lenye rasilimali zinazoitajiwa na tajiri mkubwa wa Sudan kusini.Kweli wakapanga maiti zipatazo ishirini na tano kwenye mstari mmoja.

“Chukua bisibisi” ikachukuliwa bisibisi ndefu “haya anza kuchoma hizo maiti jicho moja moja,tunahakikisha wote wamepoteza maisha.Kweli kwa ukatili iliozidi mipaka yake,jamaa huyo akaanza kuzichoma maiti hizo na kifaa chenye ncha kali,ili kuhakikisha kama kweli wanajeshi hao wamekufariki au wameigiza.Michomo ikawa inaendelea na sasa jamaa alikuwa kwenye maiti ya kumi na sita,akamchoma hakutingishika,akaendelea na kumi na saba,hapo ndipo maiti moja ikaruka juu,alikuwa ameigiza kufa.Wakamkatama na kumuamrisha kuwa akae mita chache.Jamaa aliyekuwa anashughulikia RPG mashine ya kudungulia helkopta,ndege na kadhalika,akaambia amlipue mwanajeshi yule ambaye alidanganya kifo.Wakati amewapa mgongo mwanajeshi huyo wa Sudan huku akiwa hailewi kinachoendelea ndani nyuma yake,moshi ndani ya sekunde mbili ukawa umetawala eneo lile na kusambalatisha kila kiungo chake na kugeuka kuwa jivu,akawa ameenda na maji.Walipomaliza zoezi hilo,wakapanda kwenye ndege zao na kuelekea kwenye eneo walilokuwa wanapigania ndani ya siku mbili mzima.Wakatua kwenye moja ya eneo hilo na wote wakashuka.Mawasiliano yakafanya moja kwa moja kwa Mzee kibangara.

Mpaka kwenye siku tano,Mzee kibangara akajipatia mshiko mkubwa na wenye thamani kushika watu wote Afrika mashariki na kati.Hii baada ya kupewa share yake kutoka kwa tajiri huo na zoezi hilo likawa limefikia tamati.

***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Oparesheni ya askari na baadhi ya wanajeshi kadhaa wa Tanzania,wapo kwenye gari zao maalumu wanaelekea bunju,mara baada ya kugundua kuwa kuna hekalu kubwa ya kigaidi iliyopo chini ya ardhi.Wanabaini kuwa,kambi hyio ndio inayosadikika kuwa na majambazi wa kila aina hapa jijini Dar es salaam.Matukio mengi yanayotokea kwenye benki tofauti tofauti ni sababu ya kuwepo kwao.Katika upande wa maaskari kuna Inspekta Makurumla ambaye amevalia sare zake huku kifuani na sehemu ya tumbo ameweka gamba la kuzuia risasi ‘BULLET BROOF’ na upande wa jeshi la wananchi(JW) linaongozwa na keptein Masalo Maktosh,wanaoneaka wamebeba silaha mzito mzito kama vile RPG,AK 47,BARRETT.50cal na zingine nyingi,wamepania kwa kweli kwenda kuing’oa hekalu hiyo hatari inayoshirikiana na kikundi cha kigaidi cha nchini Somalia.Gari zipatazo saba zikiwa zimebeba wanajeshi na polisi zinateleza kwa kasi kwenye barabara kuu ya kwenda Bagamoyo.Zinapita maeneo ya Makondo sekondari,japokuwa watu walishangaa lakini msafara ukaendelea kusonga mbele.Pikipiki iliyokuwa mbele kabisa ya msafara,ikiwa imewashwa taa nyekundu kuashiria kuna haraka mno ya msafara huo,ikawa na kazi ya kupangua magari kadhaa yaliyoonekana mbele.Wanafika Tegeta,wanaongeza mwendo,lakini walipokaribia bungu ving’ora vyote vilivyokuwa vinalia vikazimwa na pikipiki hiyo ya polisi ikageuza na kurudi ilikotoka.Majira ya saa 12 jioni,gari hizo za wanajeshi na polisi zikafunga breki kwenye pori dogo la maeneo hayo ya Bunju ikiwa ni umbali kutoka kwenye makasi ya watu.Wakaamua kuweka kambi yao ndogo huku wakijipanga kuingilia hekalu hiyo ya hatari ambayo inaogopwa mno.Wakaanza kupanga mipango yao huku wakitumia mbinu mbalimbali za kijeshi na za kiaskari.Kila mtu akachukua silaha yake na kuiweka vizuri,wakachukua mapomu ya kurusha kwa mkono na kuyaifadhi vyema mahala sitahiki,kila mmoja pia akavaa Bullet broof bila kusahau kofia zao zile mfano wa plastiki zenye rangi ya kijani iliyoendana sare na gwanda za kijeshi,hiyo ni kwa upande wa wanajeshi.Upande wa askari polisi,wamevaa gwanda zao za kijani huku nje wamevaa jaketi lenye kukinga risasi kupita mwilini,wakawa wametimia na kuwa imara tayari kwa mapambano.

Majira ya saa mbili usiku,wanaanza kusonga mbele huku wakiwa kimya,kila mmoja yupo tayari kumbalia kwa kile kitu kitakachojitokeza mbele yao.Kwa mwendo wa kobe wananyata kuelekea sehemu ambayo wanahisi ndio sehemu yenyewe.Haraka Inspekta Makurumla,akawaita baadhi ya wanajeshi na askari.

“Kuna kitu nahisi katika eneo lile pale la mbele” Inspekta Makurumla anasema na kuonesha eneo lililo mbele yao “Sasa tulizunguke na kuliweka kati,tukajue kama kweli ndio sehemu yenyewe?” akasema hivyo kisha wakaafikiana kila kitu na kutawanyika.Wakaanza kunyatia eneo hilo huku kila mmoja wao ameiweka silaha yake ipasavyo kwenye mikono yake.Wakatengeneza duara kubwa,wakaanza kusonga mbele na hatimaye wakajikuta wametengeneza duara hilo.Cha ajabu walipofika kwenye eneo hilo hawakuona hata dalili zozote za kuwa na kitu ardhini.Walitarajia kuwa lazima kutakuwa na kitu katika eneo lile.Wakati wanaendelea kustaajabu mara kijidirisha kidogo kikafunguka bila wao kujua na kutokeza tundu la kutokezea risasi,ilikuwa na bunduki ambayo imesetia kwa kompyuta ndani yake na kuelekezwa kwa wanajeshi hao.Hawakujua kabisa kwamba sehemu walioyopo ndio kwenye kini kabisa cha hekalu hiyo,wamekanyaga zulia gumu lililotengenezwa kwa zege zito.Silaha hiyo iliyotokeza kwenye kidipenyo cha dirisha,ikaaanza kutema risasi,hapo wote wakaanza kusaliti eneo hilo na kuingilia kwenye pori.Usiku huo walikuwa wameshtukizwa mno kwa mashambulizi yao,palepale askari wapatao wanne wakafariki dunia kwa kupigwa risasi.Wakaanza kujipanga upya,wakajua kuwa eneo lile ndio limekaliwa na magaidi hao.



Tayari kwenye hekalu hiyo ya Mzee Kibangara imeshagundua kuwa juu ya ujio wa askari hao.Kupitia kamera zilizotengwa kwenye maeneo hayo,ndipo wakabaini kuwa kuwa kuna hali isiyo ya kawaida na bila kusita wakawa wanatoa mashambulizi.





“Haraka toa silaha zote,hakikisha mnatega geti ili wanase ndani wenyewe” mkuu wa hekalu hiyo ambaye ameachiwa na Mzee Kibangara akasema huku na yeye mwenyewe ameshikilia USAS-12.Haraka kama walivyoelezwa wafuasi hao wakapakia silaha zao na kuvaa gwanda za kazi,wakachukua na Bullet Proof na kijivesha,tayari wapo kimapambano.Wawili wao wakaseti geti kuu lililopo juu kwa kutumia kompyuta.

“Ngoja wanakuja taratibu,fanyeni haraka watano mkakae pale pembeni ya geti,mimi nitabofya hapa ili waingie nalo hili geti,maana wanakaribia kulifikia” Mkuu huyo akatoa Oda na kisha watano kati yao wakafuata oda hiyo.Kwa kweli pande hizi mbili walijizatiti kikamilifu mno,hakukuwa na hata upande mmoja uliokuwa na wazo la kushindwa katika akili zao.Walipoakikisha kila kitu kimeenda sawa,wafuasi hawa wakakoki mashine zao na kujificha sehemu ambazo sio rahisi kwa adui kuwaona.



Inspekta Makurumla na wenzake,wakazidi kusogea kwenye usawa wa geti lililopo chini ya ardhi hiyo bila kujua kuwa wanakwendwa kukanyaga mtego hatari wa wafuasi hao.Bunduki zao ziko mbele,macho yao yakiwa yamelenga kwenye sehemu husika,pale kwenye mashine iliyotegwa na kuwasambalatisha mara ya kwanza.Wakafika mpaka kwenye geti bila kujua pale waliposimama ni getini kabisa.Ghafla bila kutegemea wakajikuta wameangukia ndani ya hekalu hilo,mtego umewanasa kwa asilimia zote.Kile kitendo cha kufika ndani tu,mashambulizi ya wafuasi hao yakaanza kuwaandama kwa mfululizo.Ni idadi kubwa mno ya wanajeshi na polisi walioshiriki oparesheni hiyo,wamelala chini wakivujwa na damu,wamepoteza maisha yao.Inspekta Makurumla na wenzake tano wakiwa wamejibanza kwenye sehemu ambayo ilikuwa sio rahisi sana kwa adui hao kuwaona,wakawaona wafuasi hao wakiwa wanachomoka kutoka kwenye sehemu zao walizojificha,wakawasha taa na kuanza kutazama maiti ya askari hao ambao wamejitoa sadaka kujaribu kuingia kwenye kambi hiyo.

Inspekta Makurumla akaanza kuwazama wenzake huku machozi kwa mbali yakawa yanamvuja bila kutoa sauti ya kilio.

“Inspekta tunafanyaje,tumekwisha,hawa jamaa sio wa kuwachezea namna hii,wana silaha mzito mno” akasema mmoja wao kwa sauti ya chini.

“Tunatakiwa tupa….” Inspekta Makurumla kabla hajamaliza kuongea wakashtukizwa na sauti ya bunduki ikikokiwa juu ya vichwa vyao.Aliyesimama nyuma yao alikuwa mkuu wa hekalu hiyo,mkononi ameshika bunduki moja yenye uwezo mkubwa kupita maelezo,kilichofuata hapo kila mmoja akawa amevyoosha mikono yake juu na huku wakimuomba Mungu wasije wakatandikwa risasi.

****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ramso hakuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kushusha kipigo kwa mtu Yule ambaye amemsababisha mke wake awe msaliti,kwa kweli Ramso amepandwa na hasira,hakukuwa na mtu ambaye angeweza kumpunguza hasira hizo.Ngumi na mateke ya tumbo yakawa yanamuandama jamaa huyo ambaye muda wote anavuja damu kichwani na kutapika damu tupu,mke wake Mama Gadna alijitahidi sana kumtoa mume wake kwenye mwili wa jama huyo ambaye anaelekeza kupoteza fahamu lakini wapi,hakuweza kuamlia ugomvi huo,Ramso amechachawa na hasira zilizochanganyika na wivu ndio zimetawala ubongo wake.Mama Gadna hakuwa na jinsi tena zaidi ya kuchukua kifaa kidogo tena kigumu na kumpiga nacho mume wake Ramso kichwani maeneo ya kisigo,hapohapo Ramso akadondoka chini na kupoteza fahamu kabisa.Mama Gadna hakuamini kama kweli mume wake amepoteza maisha kwa ujinga wake mwenyewe kisa kumtetea mwanaume ambaye amekutwa nae ndani ya nyumba yake,ulikuwa ni usaliti na ukatili wa hali ya juu uliofanywa na Mama Gadna.Akakimbia mpaka kwenye simu ya mezani na kubofya namba za kuomba msaada kituo cha polisi na baada ya dakika kumi tayari gari maalumu ya polisi ikafunga breki nje ya nyumba hiyo.Hali walioikuta kwenye nyumba hiyo ikawashngaza kidogo,kwani Ramso pamoja na jamaa aliyekuwa anapigwa na Ramso,wote wamezimia,hakukuwa na hata mmoja aliyeweza kujitambua.Haraka wakachukua maelezo na kuwawaisha hosptali kwa matibabu huku wakiwa chini ya jeshi la polisi.Mama Gadna akachukuliwa na polisi ili akatoe maelezo zaidi.



Ramso akiwa amelazwa hospitalini huku kichwa cahke kikiwa kimefungiwa bandeji,mikononi kuna dripu ya damu,hakuwa anajiweza kabisa,yote yanayotokea katika maisha yake,alihisi kama ni ndoto ambayo anategemea usingizi utakapoisha ndipo azinduke,lakini haikuwa kama alivyowaza,kila kitu katika maisha yake ndio kinakwenda kama vilivyo.

“Nesi samahani,naomba niku...lize” Ramso akajaribu kusema japo kwa sauti ya chini sana.

“Sawa uliza usijari”

“Mke wangu yuko wapi?”

“Mmmh mi mbona simjui yukoje,maana hapa unasimamiwa na polisi tu”

“Polisi?”

“Ndio”

“Kwani nimefanya nini mimi?” Ramso akawa anauliza maswali mengi asijue kabisa kilichotokea siku za nyuma.Akajaribu kuinuka akakuta mikono ipo sawa imeungwanishwa,akajitingisha na kutazama mikono yake na kukuta kuna pingu.Wakati akiwa kwenye mshangao polisi wawili wakaingia huku wakiwa na daktari.Wakaanza kuongea bila kumhusisha Ramso katiak maongezi hayo.

“Atapona lini dokta?”

“Aaah sijajua labda siku mbili tatu mbele”

“Ahaa maana kesi yake inatakiwa ianze mara moja”

Mazungumzo hayo yakamuacha hoi Ramso ambaye yupo kitandani na jeraha leke kichwani.Mawazo kuhusu mtoto wake Gadna yakaanza kumjia,tangia akanyage kwenye nyumba yake hajapata kumuona mtoto wake wa pekee,kwa mbali akaanza kububujikwa na machozi.Akataka kuinuka lakini akashindwa kabisa,akajikuta amelala huku maumviu ya kichwa yakiwa yanamchaanga ipasavyo.

****

Mzee kibangara akiwa na mtoto wa makamo ambaye amefungwa kitambaa usoni,bado anaendelea kumuhoji na kumpa adhabu mbalimbali tena zilizo kali.Hakuonesha kuwa na sura ya huruma hata kidogo kwa mtoto huyo ambaye ndio kwanza kwa kumuangalia unaweza kusema ana miaka tisa au kumi.

“Baba yako yuko wapi?” Mzee Kibangara akauliza.

“Si…jui” mtoto huyo akasema huku akilia machozi ya uchungu yaliyochanyika na maumivu ya adhabu anayopewa.

“Kwanza unanijua vizuri wewe mtoto,bila baba yako kuwepo hapa huwezi kuondoka” Mzee kibangara amepania kisawa sawa.Siku ya pili sasa Mzee huyu mwenye roho mbaya na ya kiukatili yupo kwenye jiji la Durban nchini Afrika Kusini.Amemteka mtoto wa Ramso anayeitwa Gadna,lengo lake lilikuwa ni kumnasa Ramso ambaye alichoropoka kutoka kwenye mikono yake miezi kama miwili mitatu nyuma huko jijini Dar es salaam baada ya kukaa kuendelea na kazi aliyopewa.Alipania kurudisha pesa alizopoteza na kuondoa uhai wa gwiji huyo aliyemsaliti.Mzee Kibangara akachukua kisu na kukilamba huku akiyatoa macho yake,kitendo hicho kilimfanya mtoto Gadna aogope mno,akajua ndio mwisho wa maisha yake.

“Unakijua hiki?”

“Nd….io”

“Nini?”

“Kisu”

“Kazi yake nini?”

“Kukatia keki” Gadna akasema huku akibubujikwa na machozi.

“Pumbavu zako keki ya bibi yako?” Mzee Kibangara akafoka na kutoka sehemu hiyo huku mtoto huyo akiwaachia vibaraka wake.Wakamchukua na kumtupia kwenye chumba kidogo na kufunga mlango.

Mzee kibangara akaingia kwenye chumba kidogo,huko nako kuna mawasiliano yanayoendeshwa na wafanyakazi wake,akatoa kijisimu chake kidogo na kuchukua USB kisha akakiunganisha na kompyuta iliyokuwa inatumiwa na jamaa yake mmoja.Baada ya kuweka simu hiyo ikaanza kuunganishwa kwenye satelaiti ambapo ikawaonesha ndege mmoja ikiwa na rubani wawili tu,ndege hiyo ilikuwa inatoka nchini Marekani inaelekea Somalia,huku ikiwa na shehena kubwa ya silaha za kivita.

“Hebu niunganishe nao niweze kuongea nao” Mzee Kibangara akasema na mara moja simu hiyo ikaunganishwa kwenye ndege ambayo ipo angani tena ikiwa na kasi ya aina yake.Baada ya kuunganishwa rubani mmoja aliyekuwa na kofia mfano wa elementi na bomba lililokuwa limetoka mdomoni mwake,akapokea mawasiliano hayo na kumuona ni Mkuu wao Mzee Kibangara ndiye anayepiga.

“Yes boss”

“Mmechukua mizigo yote?”

“Ndio bila shaka bosi”

“Na yale mabomu ya nyuklia je?”

“Nayo pia na tutaingia nchini somalia ifikapo majira ya saa sita usiku?” rubani huyo akatolea maelezo.

“Sawa kuweni makini angani,punda afe mzigo ufike”

“Haina tabu bosi”

Wakamaliza maongezi hayo kisha Mzee Kibangara akatoka kwenye kompyuta hiyo,akavuta kiti na kuketi huku akizungumza na jamaa mmoja wa kizungu.Wakaletewa mzinga mmoja wa pombe na kuanza kunywa.

“Inatakiwa tumalize hii oparesheni tuimalize mapema,tunatakiwa tupige pesa ya ajabu” Mzee Kibangara akaongea.

“Na ule mpango wa kuipindua serikali ya Tanzania,umefikia wapi bosi?’ mzungu huyo akauliza huku akivuta fundo la sigara.Mzee Kibangara akashusha pumzi kidogo na kusema “Yaah lazima serikali ya Tanzania iwe mikononi mwangu,ila kwa sasa nitaweka bomu la nyuklia kwenye ikulu,nataka kuhakikisha inabadilika na kuwa jivu mara moja,sitaki ikulu ikae pale,na makao makao makuu ya nchi lazima yawe Lindi” Mzee Kibangara akaongea huku sura yake akiwa ameikunja kuashiria kuwa hana mzaha katika suala hilo.

“Very nice boss(vizuri sana bosi)” mzungo huyo akaitikia.

“Yaah kwa sasa nimewapandikiza baadhi ya mawaziri,hao ndio watakaoshuhulikia kumpindua raisi aliye madarakani” Mzee Kibangara akizidi kuongea mengi na mzugu huyo.Walipomaliza mazungumzo yao,mzee Kibangara akachukua tena simu yake na kuiunganisha kwenye kompyuta.Sasa ikawa inaonesha hosptitali ambayo amelazwa Ramso,pembeni ya kitanda kukiwa na polisi ya kitanda pamoja na daktari mmoja,wakawa wanachukua vipimo kwenye mwili wa Ramso.Kitu ambacho kimesababisha Ramso kuonekana ni kuwepo kwa kamera na mitambo mbalimbali inayoizunguka hospitali hiyo,kutokana na mitambo ya kisasa na ya hali ya juu ya mzee Kibangara,mitambo hiyo ina uwezo wa kubaini mtu yeyote ambaye anayefanya au aliyewahi kufanya kazi chini yake kujulikana mahali popote alipo duniani.Hakika alikuwa na mtandao mkubwa mno mzee huyu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“P Jimmy na wenzako watano,mnamuona huyu mtu hapa kitandani?” akauliza.

“Ndio mkuu tumemuona” wakaitikiaa kwa pamoja.

“Namtaka hapa mara moja,huyu kala pesa zangu nyingi sana?” akasema Mzee Kibangara na kuwafanya watu hawa waanze kujiandaa tayarikwa kuvamia hosptitalini hiyo bila kuonekana na madaktari.Mzee Kibangara tena akatafuta kitu kingine na hapo ikaonekana na picha ya Zulfa ambaye yupo kwenye swimming pool anaogelea.Haraka akatoa mawasiliano kwa vijana wake wa Tanzania na kuwaambia juu ya uwepo wa Zulfa sehemu alipo na anahitaji akamatwe mara moja iwezekanavyo.

“Yes,nimemuona hata mimi hapa” akajibu jamaa huyo kupitia kwenye kioo cha komyuta.

“Nataka nimkute hapo kesho mchana”

“Sawa,ila kuna wanajeshi na polisi tumewakamata hapa,walitaka kuvamia kambi”

“Ahaaa okay wapeni adhabu niwakute kesho wakiwa chakali,mimi sio wa mchezo kabisa” Mzee Kibangara akasema kwa msisitizo kisha akakata mawasiliano hayo.

P Jimmy na wenzake kata watatu,wamekwisha jiandaa kwenda kumteka Ramso amabyae amelazwa kwenye hosptali moja iliyopo kwenye mji huo huku ikiwa akiwa chini ya uangalizi wa polisi,wakachukua bastola zao ndogo na kuziweka sehemu husika,wakaingia kwenye gari ya gharama aina ya BMW kisha wakaondoka zao kuelekea hospitalini huko.

****





****

Inspekta Makurumla na wenzake wakaendelea kupata vipigo na mateso ya hali ya juu,damu zinawachulizika mwili mzima,wapigaji hao waliobobea kutembeza mkong’oto wakwa wanapokezana zamu kwa zamu.Mpaka inafika saa saba asubuhi wakafunguliwa kamba ambazo walifunga nazo na kuingiza kwenye chumba kikubwa kilichokuwa na giza nene,ndani yake kuna bwawa kubwa.Wakafungwa vitambaa usoni huku wote wapo kama walivyozaliwa.Wakatupiwa katika bwawa hilo.Maji hayo yaliyo ya moto yakaanza kuwaunguza,vidonda walivyokuwa navyo vikazidi kuwaumiza mno.Kila mmoja akawa anajuta kwanini amekuja katika oparesheni hiyo.

“Sasa mkuu tunafanyaje,tutakufa humu ndani” akauliza askari mmoja.

“Kaka hapa tusali sala ya mwisho,huoni yule jamaa aliyeshika mjeredi?” Inspekta Makurumla akajibu huku anatazama mbele,jamaa aliyesimama mbele huku akiwa ameshika mjeredi.Jamaa huyo akasogea karibu yao na kuanza kurusha mjeredi huo uliowapata vizuri miilini mwao.Wakatolewa kwenye maji hayo huku wakiwa wamevimba migongoni na kulowa damu kila sehemu yao,wakapelekwa kwenye sehemu nyingnine ambayo ina shimo lililo na giza kama kwenye ukubwa mkubwa wa bwawa walilikuwa wanateswa kwa mara ya kwanza.Shimo hilo lilijaa Nge wakali ambao wana sumu kali mno,hapa Inspekta Makurumla ana wenzake wakaanza kulia kama watoto wadogo mara baada ya kuingizwa na Nge hao wakaanza shughuli yao mara moja,yalikuwa ni mateso ya kikatili sana kufanywa na binadamu wa kawaida.Wakawekwa ndani ya shimo hilo zaidi ya dakika tano,walivyokuja kutilewa miili yao yote ikawa imebadilika uso na kuwa weusi kutokana na sumu ya Nge hao.

****

Ramso wakati amejibanza sehemu ambayo sio rahisi kuonekana kwenye hospitali hiyo,ilikuwa na baada ya kuwatoloka askari ambao walikuwa wamemuweka chini ya ulinzi.Ramso wakati huyo tumbo wazi huku asijue atapata wapi shati,akaanza kunyata kuelekea nje kabisa ya hospitali hiyo.Kwa kuwa ulikuwa usiku akaweza kupita kwenye vichaka vya maua ya hosptali hiyo bila kuonekana na mtu yoyote huku akiwaacha askari hao wakilumbana na mauuguzi walio zamu siku hiyo kuhusiana na kutoloka kwake,askari hao wamechanganikiwa kupita kiasi,hawakujua Ramso ametoloka muda gani na hali hiyo inaweza kuzua kesi kwao.

Ramso akatoka mpaka nje na kuanza kukimbia kwa kasi,safari ya kwenda nyumbani kwake ikaanza huku akiwaza pesa na mtoto wake tu,kichwani mwake akawa anamchukulia mke wake kama adui kwani kitendo cha kumpiga na chuma kwa lengo la kumtetea na mgoni wake,hakika kitendo hicho ni cha kinyama kufanywa na mwanamke aliyeolewa,Mama Gadna ameonesha dhahiri kuwa hana mapenzi ya dhati.Ramso akafika nyumbani kwake ambapo papo kimya,hakukuwa na dalili zozote zile za kuonesha uwepo wa familia yake,akachukua begi yake ya pesa ambayo aliiweka kwenye sofa mara kabla hajapigwa na chuma kizito kichwani akalivaa na kuingia chumbani,akazivaa nguo zake kisha akaanza kutoka nje,wakati anaelekea mlangoni akasikia sauti ya mlio wa gari unasimama nje ya nyumba hiyo,haraka akafunua panzia na kutazama nje ili aweze kuona nini kinaendelea.Nje gari aina ya BMW imepaki na watu kama watatu wametoka kwenye gari hiyo huku wakiwa na bastola zao mikononi mwao,Ramso alipoona hivyo akatoka mbio kasi na kuingilia kwenye mlango wa dharula(Emeregence door),akatokea upande wa pili na kutimua mbio huku akitazama nyuma.Akafika mjini huku akiwa amechoka mno,akaingia kwenye duka linalouzwa simu na kununua,akaweka na laini yake tayari kwa kufanya mawasiliano na watu wake.Alipohakikisha kuwa amelipia simu hiyo akatoka nje na kuendelea na safari yake.Hakujua ni kosa kubwa kwake kuwa na simu tena ambayo inaweza kuwapa mawasiliano watu wa mzee Kibangara.Hakutembea umbali mrefu tayari alishazungukwa na gari mbili nyeusi,hapohapo akakamatwa na kuingizwa ndani ya gari zao,wakamfunga kitambaa machoni ili asijue wanakompeleka.Kimya kikazidi kutandaa ndani ya gari hiyo ambapo baada ya dakika kama ishirini gari hizo zikaingia kwenye jumba moja lilio na ulinzi mkali na kila kona kukiwa na taa pamoja na kamera za CCTV zinazochunguza watu wanaotoka na kuingia.Wakamshusha na kuingia nae ndani huku wakimburuza kwenye sakafu kama mzigo wa kuni.

Mzee kibangara akiwa na wafuasi wake walioketi kwenye viti wakamtazama Ramso ambaye sasa anavuja damu mno.Wakamzunguka na kuanza kumpatia kipigo,tena kile kipigo sitahiki kwa mkosaji.Kelele za maumivu anazozitoa Ramso zikamfanya Gadna ambaye amefungiwa kwenye chumba kidogo aanze kulia huku akimtaja baba yake Ramso.Ramso naye alivyosikia sauti ya mtoto wake Gadna akaanza kuita kwa sauti ilichanganyika na sauti za kulia,akaita kwa uchungu huku damu zinamtoka mdomoni lakini jamaa hao wakakutaka kumuachia.

“Gadnaaaaa my son,I never let you die,I will fight because of you my blood son(Gadnaaa mwanangu,kamwe sitokuacha ufe,nitapambana kwa sababu yako mwanangu wa damu” Ramso akaendelea kupiga kelele huku wakati mwingine akijaribu kutambaa ili akiendee kile chumba lakini wapi,jamaa hao wasio na huruma wakamzuia na kupiga kwa nguvu mpaka pale alipotulia tuli huku sehemu mbalimbali za mwili wake zinavuja damu,hakika kilikuwa kipigo cha aina yake.

Mzee Kibangara akasimamisha zoezi la kumshughulikia Ramso na kuwaamuru wampeleke kwenye chumba kingine ambacho ni tofauti na cha mtoto wake Gadna.

“Atakapoamka,mtaniambia haraka sana”Kibangara akasema na kutoka kwenye eneo lile,akaingia kwenye chumba chake maalumu na kuitoa simu yake,ni ndogo lakini imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu mno.Akaiwasha na kuanza kubonyeza vibonyezo vyake.Ndege mbili zikawa zinaonekana angani,ndani yake kukiwa na mabomu pamoja na silaha za viwango vya juu,zinakanyaga anga ya Kenya sasa na kuendelea kuisaka anga ya Somalia ambako ndio makao yao.Mzee Kibangara wakati anaendelea kuzitazama ndege hizo huku akiwasiliana na rubani wake ghafla akaiona ndege moja inalipuka na kuteketea kabisa,ikabaki moja ambayo sasa ikaanza kurusha mabomu na risasi bila kuwa na mpangilio maalumu.Haikuchukua dakika tano tayari na ile ndege nyingine ikadunguliwa na kutetekea kabisa.Mzee Kibangara hakuamini macho yake kama kweli kile anachokiona kwenye simu yake ni kitu halisi au ni ndoto tu,alipojaribu kufikicha macho yake na kuitazama tena simu yake bado aliuona moshi uliotanda kwenye kioo hicho cha simu ikiwa na maana kuwa hakukuwa na ndege iliyo salama,kile anachokiona pale ndiyo chenyewe na sio ndogo kama anavyodhania.

Akashuka kwenye ngazi haraka haraka na kuingia kwenye chumba maalumu cha mawasiliano,kila kompyuta ya chumba hicho ilionesha tukio la udunguaji wa ndege hizo mbili zilizokuwa zimebeba mabomu na silaha zingine za mzee Kibangara.Ndani ya hekalu hilo hakukukalika kabisa kila mmoja alionesha sura ya kuchanganikiwa zaidi ya kumpita mwenzake.

“My God whats happen,ina maana dola bilioni mia mbili zote zimeteketea kihurahisi namba hii?” Mzee Kibangara akajiuliza kwa sauti huku jasho linamvuja,japokuwa ndani ya chumba hicho kulikuwa na kiyoyozi lakini bado Mzee Kibangara akawa anavuja jasho tena bila kizuizi.

“Kenya Watalipa pesa zangu,na lazima nidungue makao makuu yao,ndani ya masaa 45” Mzee Kibangara akasema kwa ghadhabu huku akivua koti lake,kwani hakuweza kuistaimili joto lililopo ndani yake kwa muda huo.

“Evansi na Tinno,naomba mviongoze vikosi vyenu kuelekea anga ya Kenya kwenye eneo la tukia na kisha mtanipa taarifa kamili kesho,na pia nahitaji kujua nani kahusika na shambulizi hili lililonitia hasara namna hii” Mzee Kibangara alivyosema hivyo akatoka na kuwaacha wafuasi wake wakitazama bila kusema chochote,kazi iliyotolewa kwa mkuu wao huyo haikuwa ya kitoto,ni kazi ya kiutu uzima na yenye kuitaji ufundi na akili za hali ya juu katika kulifanikiwa zoezi hilo,hakika wote wameshikwa na butwaa kwa kazi waliyopewa.



Wakati wafuasi hao wanaendelea kujadiliana katika kazi hiyo,Ramso aliye ndani ya chumba chake,akiwa amelowa damu mwili mzima,akafumbua macho yake kiuchovu huku akiugulia maumivu makali aliyokuwa amepatiwa na jamaa wenye ukatili mkali ndani ya jumba hilo.Kutukana na vyumba hivyo walivyofungiwa yeye na mtoto Wake Gadna,vilikuwa na dilisha dogo lililo juu kidogo,ikawa ni rahisi kwa kila mmoja wao kusikia sauti ya mwenzake.Sauti ya kukohoa ya Ramso ndio iliyomshtua Gadna kutoka kwenye usingizi wa mang’amng’amu kwenye ile sakafu iliyo na baridi mithili ya barafu.

“Daady” akaita mara moja lakini hakuna sauti ya kujibiwa.

“Daady iam Gad…na” akasema tena ila safari hii akasikiwa sauti ya kukohoa na sauti ya chini sana iliyosema.

“My son,naku…penda sana,usijari tuta…..tutatoka humu ndani” Ramso akasema kwa sauti ya chini kutokana na maumivu anayoyapata kwenye kichwa chake.

“How you can Dady?(Utawezaje Baba?)”

“Trust me my son(Niamini mimi mwanangu)” Ramso akasema huku anajivuja kulisogelea lile dilisha liliwatenganisha yeye na mtoto wake,akasimama kwa msaada wa kujishikilia kwenye dilisha hilo na kuanza kuchungulia,ila kabisa hajamuona mtoto wake akashtukia teke zito la mbavuni lililomfanya aanguke chini tena na maumivu upya yakaanza kutawala mwili wake.

“Unataka kujifanya Jet Lee sio?” akafoka jamaa huyo ambaye amempiga teke Ramso.Akamtwanga tena teke la kifuani na hapo hapo Ramso akatulia tuli huku damu kutoka mdomoni na puani zikaanza kuvuja.Mtoto wake Gadna ambaye hakuweza kabisa kulifikia dilisha lile akaanza kuita mfulilizo jina la baba yake lakini hakuweza kujibiwa,mawazo yakampeleka mbali na kudhani kuwa baba yake amekwishakufa,kwa sababu hakukuwa na dalili zozote zilizoashiria kuwa baba yake yupo hai ndani ya chumba hicho.Akaanza kulia kwa uchungu huku akitaja jina la baba yake Raamadhani(Ramso).

Tayari Helkopa aina ya Chopa zipatazo tatu zimepaa angani majira ya saa nane usiku huku zikiendeshwa na marubani mahiri wa vikosi hivyo.Safari ya kwenda Kenya katika eneo la tukio imeiva na sasa wanawasiliana kupitia radio call zao maalumu.Kwa jinsi helkopta hizo zinavyopaa angani na kupishana bila kugongana zikatoa taswira kama zile muvi za kimarekani zinazochezwa na wasanii mahiri wa nchini humo,kila rubani alionesha umahiri wake wa kuendesha helkopta hizo za kisasa.

“We are in Mozambique along the coast right now(tupo pwani ya msumbiji sasa)”

“Ok nice(Sawa vizuri)”

“Yeah we are on fire sir”

“Ok call me later”

“Thanks sir” Mazungumzo hayo yalivyokwisha helkopta hizo zikaongeza kasi zaidi kulekea kwenye eneo la tukio.Mpaka ilipohitimu saa kumi na robo,zikawa zimekanyada pwani ya Tanzania,pembezoni mwa bahari ya hindi,zikapita kwa kasi na kuwaacha hoi wavuvi walikuwa wanaendelea na shunguli zao za kuvua samaki kwenye bahari hiyo.

******





****

“Lazima msande leo,leta kisu” sauti ya mkuu wa hekali la mzee Kibangara akasema huku mbele yake kukiwa na askari watatu na akiwemo Inspekta Makurumla ambaye ameshiriki kwenye oparesheni hiyo ya kuangamiza ngome hatari ya mzee Kibangara,lakini kazi hiyo ikawa kinyume chake,sasa wakawa wanateswa na kufanyiwa ukatili wa aina yake.Kisu kikafika na jamaa huyo mwenye sura ya kutisha,akamshika mmoja sikio na kulikata.Hakika ulikuwa ni ukatili wa hali ya juu mno,sauti ya maumivu ndio iliyotawala ukumbi huo,Inspekta Makurumla na wenzake waliobakia wakaanza kutetemeka huku wakisali kimoyomoyo ili waepushwe na ukatili ule,kukatwa sikio sio jambo la kitoto,ni la maumivu kweli kweli..Baada ya kumaliza kumkata sikio hilo akaweka kisu mezani na kulilamba sikio hilo.

“Mimi ni Mfia zaidi ya udhaniavyo” akasema jamaa huyo huku akitabasamu kwa dharau,mara kigola cha hatari kikaanza kulia na kila mmoja wao akaaanza kwenda kwenye eneo la king’ora hicho.Ni katika chumba maalumu cha kompyuta ambacho kinatoa mawasiliano na mahekalu yote ya Mzee Kibangara.Wakaona jinsi rubani wa helkopta mbili wanavyoendesha kwa kasi huku,mawasiliano katika hekalu zote tatu yaani hekalu ya Tanzania,Somalia na Afrika Kusini zikawa zinatazama tukio zima na jinsi helkopta hizo zinavyoendeshwa kwa kasi kuelekea anga ya Kenya.Katika jitihada za kutaka kutoka kwenye eneo lile walilofungwa kamba,mara Inspekta Makurumla akafanikiwa kujifungua kamba kwa kutumia kile kisu kilichotumiwa na jamaa huyo katika kumkata sikio askari mwenzao.Wakafanikiwa kutoka kwenye eneo lile huku askari mmoja akisaidiwa katika kutembea.Kimya kimya wakaingia kwenye kijichumba kidogo ambacho hakikuwa na mtu.Wakajibanza mahali hapo na kukuta nguo zao zimetundikwa juu,wakvaa haraka haraka na kukaa kimya,bila kutegemea akaingia askari mmoja akiwa na silaha yake mkononi,bila kusita Inspekta Makurumla akarusha ngumi nzito iliyompata vizuri kwenye taya la jamaa huyo na kumfanya aanguke chini bila kupiga kelele,wakachukua silaha yake na kuanza kutoka nje kwa umakini mno.Wakafika mpaka kwenye geti ambapo hawakukuta mtu hata mmoja,wakaanza kujiuliza watafunguaje geti hilo kwani sio la kufungua kwa kawaida,huwa linafunguliwa na rimoti maalumu tu.

“Tutafanyaje sasa mkuu?” akauliza mmoja wa askari hao.

“Mmmh hapa wanatumia rimoti kufungua hili geti,sasa sijui tutatokaje humu ndani masikini” Inspekta Makurumla akaumiza kichwa katika kulifumbua fumbo la kufungua geti la hilo.

“Ooooh Mungu tusaidie sisi waja wako” mmoja wap akajikuta anaomba Mungu ili waweze kutoka katika lile jumba la chini ya ardhi.Wakati wanaendelea kujadiliana kivipi wanaweza kutoka nje mara ndege ikasikika toka juu,hii iriashilia kuwa Mzee Kibangara sasa anatua kwenye hekalu hilo.Wakaanza kurudi nyuma kwa kasi na kujificha kwenye sehemu isiyo rahisi kuonekana,wakajibanza huku wakitazama nani ataingia kwenye hekalu hilo.Taratibu geti hilo likaanza kufunguka na ndege ndogo ikaanza kutumua na kukimbia kwa kasi kwenye maegesho yake.Baada ya hapo ikatulia na mzee Kibangara akashuka akiwa na watu kama tano aliofuatana nao.Watu hao wakafungua mlango wa nyuma wa ndege hiyo na kumtoa mtu mmoja akiwa na mtoto mmoja huku jamaa huyo akiwa amelowa damu tupu mwili mzima,hakuwa mwingine bali ni Ramso akiwa na mtoto wake Gadna sasa wameletwa Dar es salaam kwa mara nyingine.Ramso alikimbia kipindi kifupi kilichopita kwa tuhuma kuwa yeye alikuwa jambazi sugu sana na alimjeruhi polisi mmoja jijini hapo.Wakakashikwa kwa ukatili na kuingizwa kweny chumba kimoja.Insapekta Makurumla na wenzake wakawa wanatazamana na kuishiwa nguvu kabisa hasa pale walipoliona geti hilo linajifunga tena na giza kutanda.

“Inatakiwa tufanye kitu tena kwa haraka zaidi sana kabla hakijatokea kitu kingine humu ndani” Inspekta Makurumla akasema huku akiwatazama wenzake ambao kwa muda huo wakiwa wamekata tamaa kabisa ya kutoka kwenye jumba hilo la kutisha lililosheheni ukatili wa aina yake.

“Sasa itakuwaje?”

“Subirini hapo hapo” Inspekta Makurumla akasema na kuanza kunyata kueleke kwenye chumba kile alimpiga jamaa na kuchukuwa silaha yake,akakuta bado jamaa kalala hajitambui kabisa kutokana na kupigwa ngumi nzito ya kwenye taya.Akampapasa na kuitoa simu,moja kwa moja akatoa kijikadi kinachounganishwa kimawisiliano katika lile jumba na kuanza kupiga simu makao makuu ili apate msaada.Kweli Inspekta akafanikiwa kupata mawasilino na sasa akawa anaongea na mkuu wake wa kazi hiyo.

“Yeah mkuu hatuna jinsi na hatujui humu ndani tutatokaje kwa kweli”

“Oka natoa taarifa kwa jeshi la wananchi ili waje kuwaokoa” sauti kutoka kwenye upande wa pili ikasema.

“Okay boss fanya hivyo ila wawe waangalifu sana,maana hili jumba sio zuri sana,wanaua kama kuku aisee”

“Sawa ndani ya dakika kama kumi na tano watakuwa hapo”

Mazungumzo hayo yapoisha akakata simu na kutoka nayo nje ya chumba hicho huku bunduki aliyopola ikiwa mikononi mwake.Mara wakaanza kusikia sauti ya risasi inapigwa kutoka kwenye upande waliokuwa Mzee Kibangara na wafusai wake,kitendo ambacho kikawafanya waanze kutetemeka na kushindwa cha kufanya.

****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Anga ya Kenya pembezoni kabisa mwa jiji la Mombasa ndipo ndege ambazo zilibeba silaha zilipoangukia,wanajeshi kutoka Kenya wakishirikiana na jeshi la Sudan tayari wamefanikiwa kuzinasa ndege hizo na kuchukua uamuzi wa kuzitungua ndege hizo na kuacha jivu tupu.Baada ya dakika kama ishirini baada ya tukio kufanyika,ndipo wanajeshi hao wakawa wanatalii eneo hilo huku wakichunguza kama kutakuwa na watu wa aina yoyote katika eneo hilo.Wafuasi wa kibangara ambao wapo katika helkopta,sasa baada ya kukanyaga tu arthi hiyo wakashusha helkopta mita ndefu kutoka kwenye eneo lile la tukio.Wakaaanza kunyatia huku mikononi mwao wakiwa na silaha mzito,wakaendelea kulisogelea eneo lile ambalo kwa muda likiwa limetawaliwa na wanajeshi wa Kenya na Sudan.Ikawalazimu watazame kwa makini sana ili wagundue nini kinaendelea katika eneo hilo.Baada ya kubaini kuwa ni wanajeshi,mmoja wao akatoa kifaa kitumacho mawasiliano kwa Mzee Kibangara na kumpa taarifa.

“Bosi,tumefika eneo la tukio na sasa kwenye eneo la tukio kuna wanajeshi wengi,hatujajua wanafanya kitu gani” akatoa maelezo jamaa huyo.

“Okay endeleeni kuwafuatilia kisha nipeni data kamili,ni nani kasababisha ajari hiyo na wahusika wote niwapate” Mzee Kibangara akasema.

Mpaka inakuja kuhitimu saa kumi na moja alfajiri ndipo walipotambua kuwa wanajeshi wale ni wa Kenya na Sudan kutokana na kuziona nembo za bendera zao kwenye sare zao.Wakatoa taarifa tena kwa mkuu wao na hapo ndipo walipoamrishwa waanze mashabulizi.Hawakuchukua muda wakaanza kujipanga vizuri na kujiweka tayari.Wadunguaji zaidi ya watatu wakakaa sehemu husika ambayo sio rahisi sana kuweza kuonekana na wanajeshi hao.Bila kugundua kitu chochote wanajeshi hao wa Kenya na Sudan wanaochukua baadhi ya mabaki ya silaha zilizo kwenye ndege hizo,wakashtukia wenzao wawili wanaanguka chini na kuanza kuvuja damu,tayari walikwisha pigwa risasi na wadunguaji hao mahiri wa Mzee Kibangara.Tukio hilo likafanyika ndani ya sekunde tatu tu,wanajeshi hao wakaanza kupiga risasi ovyo huku wakioneshwa wasiwasi mwingi mno.Kitendo cha wao kurusha risasi ovyo kikawafanya wafuasi wa Mzee Kibangara waanze kuja kwa kasi kama ya nyuki kwenye eneo lile.Baada ya kuingia tu kwenye eneo husika wakaanza kurusha risasi na mabomu ya mkono kwa kasi ya ajabu mpaka wakajikuta wanawamaliza wote ndani ya muda mchache.

*****

Zulfa akiwa anapunga upepo maeneo ya JANGWANI SEA BREEZE huku akichezea simu yake bila wasiwasi wowote ule.Taratibu akatoa nguo zake na kubakia na nguo yake ya ndani tu huku juu akiwa na sidilia akiwa amejiweka tayari kwa kuogelea,akasogea mpaka kwenye swimming pool na kujitosa kwenye maji huku akiyasakata maji kama samaki tena aina ya nguva.Hakujua kuwa simu yake ambayo anayotumia huwa inatoa taarifa kwa wafuasi wa Mzee Kibangara.Ndani ya dakika kama tano watu wapatao watatu wakiwa wamevalia suti nyeusi huku masikioni mwao wamevaa vifaa vya mawasiliano.Wakawa wanachunguza huku na kule pamoja na kufuata alama ya simu ya Zulfa ilipo.Zulfa bado yupo kwenye swimming pool anaendelea kuogelea na sasa amekolea na maji,hana wasiwasi wowote kwani anajua pale ni sehemu pazuri na akafiria kuwa hawawezi kutokea watu wabaya,kumbe fikra zake hazikuwa sahihi kabisa.Jamaa hao wamekwishafika kweny kitanda kidogo cha kubalizi,na ndipo Zulfa ameweka simu yake na nguo zake.Wakasimama hapo na kuanza kutazama huku na huko wakiwa wanamtafuta Zulfa………………



Zulfa alipoona amechoka akatoka kwenye maji na kuanza kuelekea kwenye kitanda chake alichoweka simu na nguo zake,lakini kabla hajakifikia mita chache akawaona watu watatu waliovalia suti nyeusi wamesimama pale kwenye kitanda chake,akasita na mapigo ya moyo yakawa yanamuenda mbio mno.Akamkumbuka mmoja wao kuwa alikwishawahi kumuona kwenye hekalu la Mzee Kibangara kabla ya kuvunja mkataba wao.Kwa kasi akaanza kutembea huku akitazama tazama nyuma kuelekea ndani.Na jamaa hao nao wakamuona Zulfa anaingia ndani wakaanza kumfuata hukohuko ndani,wamepania kweli kweli.

Zulfa akafika kwenye sehemu ambapo watu hupenda kukaa na kunywa vinywaji,akapiliza mpaka kwa wahudumu ambao wanahudumia wateja wafikao kwenye eneo hilo.

“Dada vipi mbona na chupi mpaka huku?” Mhudumu wa kike mmoja akauliza kwa mshangao sana,kwani haikuwa kawaida kwa wateja kuingia ndani humo.

“Samahani naomba unisaidie kama kuna nguo yoyote hapo ya kujiziba mpaka usoni” Zulfa akasema,mhudumu akamtazama Zulfa kwa umakini kisha akafungua kabati ndogo na kuutoa mfuko,akazitoa nguo nyeusi na kumpatia,akaanza kuzivaa haraka haraka na hatimaye baibui hilo likafunika vizuri mwili wake.

“Asante sana dada” akashukuru

“Kwani kuna nini unachokimbia?” akauliza

“Hamna nguo zangu hapo nje zimeibiwa,na mimi nataka kuondoka” Zulfa akasema huku akijua mwenyewe kitu anachosema sio cha kweli,bali ni kuepukana na watu ambao wanamtafuta wasiweze kumuona.Akaanza kutoka nje huku akipiga jicho pande zote mule ndani na kuweza kuwaona jamaa hao wakiwa wanashangaa shangaa kila bila mafanikio yoyote.Akafanikiwa kutoka nje na kuchukua simu yake,akapanda kwenye gari ndogo aina ya Vtz akaondoka zake huku kiwaacha wafuasi wa Mzee Kibangara wanang’aa macho.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

*****

Mlio wa risasi uliosikika ndani ya hekalu la mzee Kibangara ukawaongezea sana hofu Inspekta Makurumla na wenzake kwenye sehemu ambayo wamejificha.Risasi hiyo ambayo ilifyetuliwa na Mzee Kibangara,ikamfumua ubongo mfuasi wake mmoja ambae alipewa jukumu la kulisimamia hekalu hilo pamoja na kuwahakikisha kuwa mateka ambao waliwateka wasiweze kutoroka mpaka pale atakapowakuta pindi atokapo Afrika Kusini.Wafuasi waliobakia wakaanza kutetemeka na wengine kwa mbali mikojo ikawa inawavuja bila kujielewa,wanajua kuwa mzee Kibangara hana mchezo kabisa katika swala la kazi,hakuwa na mzaha hata kidogo,pale mfanyakazi wake anapotaka kuvurunda basi lazima akawasalimie kuzimu.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog