Search This Blog

Friday, November 18, 2022

CHUNGA SAANA LAAZIZI WANGU - 4

 





Simulizi : Chunga Saana Laazizi Wangu
Sehemu Ya Nne (4)




“Baby katika jitihada zangu za hapa na pale nimefanikiwa kupata hiki kidogo.”Alimkabidhi lile boksi lililokuwa na zawadi aliyomuandalia siku hiyo.

“Usiseme ni kidogo kwani kutoa ni moyo sio utajiria mpenzi wangu.” Tuntu aliongea huku akiibusu zawadi hiyo.Waliinuka na kuelekea kituoni ambapo walipanda gari mpaka Magomeni Mapipa na hapo walishuka.Tuntu alimsindikiza Salma mpaka jirani na nyumbani kwao kisha yeye alielekea kituoni na kuondoka nyumbani kwao.

Siku ya Alihamisi iliwadia ambapo ilikuwa ni siku ya mahafali ya shule ya sekondari Jangwani.Tuntu alivaa suruali na T-shirt alizozawadiwa na mpenzi wake Salma siku ya mahafali yake.Siku hiyo timu nzima ya Tuntu waliungana kwenda kumuunga mkono Salma.Zawadi aliyoiandaa Tuntu kwa ajili ya mpenzi wake siku hiyo,aliiweka sehemu kwa ajili ya kusubiri muda muafaka.

Muda wa sherehe uliwadia na hapo shamrashamra za burudani pamoja na michezo iliyoandaliwa na wanafunzi wa shule hiyo ilifanyika kwa ustadi Zaidi.Muda wa ugawaji wa vyeti uliwadia na hapo Salma alijizolea vyeti takribani vitano ikiwemo cheti cha somo la Book-keeping,Commerce,Geograph,uongozi pamoja vyeti vya klabu mbalimbali alizozitumikia kipindi akiwa shuleni hapo.

Familia nzima ya Salma ilikuwepo siku siku hiyo.Baada ya sherehe kumalizika,walikaa chini ya mti kati ya miti iliyokuwepo shuleni hapo.Kama ilivyokuwa ada walipata vinywaji na chakula.Wakiwa wanaendelea kupata vinywaji,Salma alichukua jukumu la kuwatambulisha wote waliokuwepo.Alianza kuwatambulisha rafiki zake kwa wazazi wake pia akafuata wazazi kwa rafiki zake.

“Huyu ndo yule kijana?Hongera sana baba!” Mama Salma aliuliza baada ya Tuntu kutambulishwa kwani alikuwa hamjui kwa sura.

“Asante sana mama”Tuntu aliongea kwa sauti ya unyenyekevu.Waliongea mambo mbalimbali mpaka kufika mida ya saa kumi,wazazi walirejea nyumbani huku wakiwaacha vijana wafanye yao.Baada ya wazazi kuondoka,Tuntu alichukua simu na kumpigia jamaa mmoja ambaye baada ya dakika kadhaa aliwasiri akiwa ameshikiria boksi lililopambwa vizuri.Alimkabidhi Tuntu kisha aliondoka.

Marafiki wa Salma na wale wa Tuntu wote walikuwepo.Walitafuta chumba cha darasa ambacho kilikuwa wazi wakaingia ili kufanya shughuli zao.Tuntu alimkabidhi Salma lile boksi na kisha walikaa chini huku marafiki wakishangilia kwa furaha.

“Naomba ufumbe macho wakati ukiwa unalifungua boksi hilo.”Tuntu aliongea kwa sauti ya kudeka.Salma alifanya hivyo taratibu na baada ya kumaliza kulifungua,aliambiwa afumbue macho yake.

Hakuamini alichokiona ndani ya boksi hilo. “Waooo! Thank you mpenzi wangu!” Aliongea huku akimkumbatia Tuntu. Ilikuwa ni keki maalumu kwa ajili yake iliyoandikwa kwa maandishi ya rangi nyekundu yenye kuvutia. “I LOVE YOU SALMA.”Salma alianza kuikata keki na kuwalisha wote waliokuwepo baaada ya wao kulishana.

Siku hiyo Salma alifurahi sana kwa jinsi alivyofanyiwa na kupewa thamani na Tuntu.Siku hiyo aliipoteza ile fikra kwamba ni masikini asiye na kitu bali alijiona ni mtu miongoni mwa watu.Walifanya yao mpaka mida ya saa kumi na mbili kamili na hapo kila mmoja alitawanyika…..





Mitihani ya kidato cha nne iliwadia.Kila mwanafunzi mtahiniwa mwaka huo,alikuwa yupo tayari katika mapambano dhidi ya baraza la mitihani la taifa.Kwa upande wa Salma na Tuntu walikuwa wamekwisha jiandaa kwa asilimia kubwa kiasi cha kuamini hakuna kipengele ambacho hawakujidhatiti.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Walifanya mitihani yote katika hali ya Amani na utulivu mpaka na kufikia wiki ya pili, walikuwa wamekwishamaliza masomo yao kwa wale waliokuwa wakichukua masomo ya sanaaa na biashara huku wakiwaacha wale wa sayansi wakimalizia.

Jumamosi iliyofuata baada ya wiki ya kumaliza mitihani,Tuntu,Salma pamoja na marafiki zao walikutana kujipongeza kwa kumaliza shule salama.Sherehe hiyo fupi waliifanyia ndani ya Mbala mwezi Beach mikocheni.

******

Kadri miezi ilivyosonga mbele ndiyo mahusiano kati ya Tuntu na Salma yalizidi kupamba moto.Miili yao muda mwingine ilipandwa na njaa ya kustarehe,lakini walijikaza kwa kujipa moyo kuwa watafanya pindi watakapopewa idhini na Mwenyezimungu.

“Hata mimi nataka ila tuvute subira mpaka tukimaliza masomo.”Ni kauli ya Salma akimpa moyo Tuntu pindi anapoomba mchezo wa kitandani.Sababu ya Salma kukataa ilitokana na usia aliopewa na mama yake kuwa awe makini na wavulana hivyo mara nyingi hofu ilimfanya kuwa makini.Tuntu hakuwa na pingamizi lolote kwani aliamini kwa asilimia mia moja Salma alikuwa wake.

Miezi takribani mitatu na nusu baaada ya kumaliza kidato cha nne mwezi wa kumi na moja ilipika na hapo baraza la mitihani nchini Tanzania lilikuwa tayari kuwarudishia majibu wanafunzi wote waliofanya mtihani.Mnamo tarehe ishirini ya mwezi wa pili,matokeo ya kidato cha nne yalitoka rasmi.

Tuntu,Salma pamoja na marafiki zao wote walifaulu kwa kiwango cha kuwapeleka kidato cha tano.Salma alifaulu kwa kiwango cha daraja la pili akiwa na alama 19 huku Tuntu akifaulu kwa daraja la kwanza alama 16.Kwa upande wao wote meno therathini na mbili yalikuwa nje.Waliimba na kuruka kwa kila aina ya mtindo walioufahamu yote ikiwa ni sehemu ya kuonesha hisia zao za furaha juu ya matokeo yao mazuri.

Wazazi wa Salma nusu wazimie kwa kutoamini taarifa walizofikishiwa na mwanao.Waliona maisha sasa kwa wakati huo yanaelekea kuwanyookea. “Yaani lazima tukuchinjie kuku ule upande mzima,”Mama Salma aliongea huku akiwa anapumua kwa nguvu kutokana na nguvu aliyotumia kurukaruka juu.

“Asanteni sana wazazi wangu ila inabidi tuombe dua maana bado safari ni ndefu.”Salma alichangia.

“Ulipotoka ni mbali sana siyo sawa na unakokwenda! Hapa ndiyo pagumu mwanangu!” Baba yake alichangia huku sura yake ikiwa na bashasha.Siku hiyo Salma hakupata usingizi hata chembe.Alikesha kutokana na maongezi marefu kati yake na Tuntu ambayo yaliwapeleka mpaka saa kumi alifajiri.Salma alimshukuru sana Tuntu kwa msaada aliompatia mpaka kufikia hatua hiyo ya mafanikio.

“Najua unafuraha kubwa sana ila tambua nafanya yote hayo kwasababu nakupenda sana.Naomba tu na wewe unipende kama ninavyokupenda.”Tuntu alichoshwa na mvua ya shukrani iliyokuwa ikidondoshwa na Salma usiku kucha hivyo aliamua kusema hivyo ili kumkatikiza Salma suala la kushukuru mpaka kupita kiasi.

“Najua baby ila nashindwa ‘kucontrol’ furaha yangu.”Salma alidondosha machozi kwani hakuwa na imani kama angeweza hata kuufanya huo mtihani kutokana na maisha yalivyokuwa magumu nyumbani kwao.Waliongea mengi huku wakijipa matumaini kuwa wanapendana na kifo ndicho kitakachowatenganisha.

******

Miezi ilizidi kusonga mbele huku wakivuta muda kusubiri wapangiwe shule za kwenda kujiunga na kidato cha tano.Wakati wote huo Tuntu aligeuka kuwa mlezi wa Salma kwa kila kitu.Alitoa kiasi chochote ambacho Salma alihitaji ili mradi kiwe ndani ya uwezo wake.

Siku moja Jamse ambaye ni rafiki wa karibu wa Tuntu aliamua kukaa rasmi na Tuntu ili kubadilishana mawazo mawili matatu.Walitafuta sehemu tulivu ambayo itawapa fursa ya kupumzisha akili zao huku wakibadilishana mawazo.Walikwenda maeneo ya Coco beach na hapo walitafuta sehemu tulivu na kuanza mazungumzo yao.

“Kwanza napenda kuomba radhi kwa haya nitakayo kuambia lakini ni moja ya jitihada za kukutakia mema kama rafiki yangu wa muda mrefu.”Jamse alianza mazungumzo na hapo alikunywa funda moja la maji ya baridi kutuliza koo.

“Unamaanisha nini kuanza kwa kuomba radhi,mara ngapi umekuwa hata ukinitukana kwa lengo la mimi nijirekebishi nimeshapigana na wewe?”Tuntu alimuhakikishia rafiki yake atakuwa mtulivu kwa yale atakayoambiwa.

“Najua unampenda sana Salma na umejitoa kwa moyo wako wote juu yake.Upo tayari hata kujinyima ila yeye apate,hivi unawajua wanawake kweli?”Jamse alimuuliza.

“Ha ha ha! Kwa hiyo una maana Salma anaweza kunisaliti?Siamini katika hilo.”Tuntu alicheka kwa kebehi kidogo huku akitikisa kichwa ishara ya kukataa.

“Una maana gani kujiamini kwa asilimia mia kuwa hawezi kukutema?”

“Sikiliza Jamse!Salma mimi ndiyo kama mzazi wake wa pili.Shule yake naijua mimi,vaa yake naijua mimi itatokea nini mpaka aniteme?”Tuntu alibishana na rafiki yake.Jamse alimsikitikia Tuntu kutokana na ubishi wake wa kujifanya anawajua wanawake vyema.

“Sikiliza rafiki yangu.Wanawake ni sawa na msitu mkubwa wenye miti ya kila aina,wanyama na majani ya kila aina,hivi ukiambiwa utaje aina za majani tu achana na miti iliyomo utaweza kujua?Kuwa makini sana rafiki yangu.”Jamse alizidi kumfungua Tuntu.

“Kwa hiyo unataka mimi nifanyeje”

“Swali zuri sana rafiki yangu.Nachotaka kutoka kwako ni jambo moja tu,Punguza kujiumiza kwa kujitwisha mzigo ambao hujui kama ni wa dhahabu au mawe.”

Tuntu alikaa kimya kuashiria kama aliyekuwa akitafakari jambo lakini kiuhalisia maneno ya rafiki yake hayakumuingia hata chembe.Alimuona Jamse kama mchawi kwa kutaka kuyavunja mapenzi yake na Salma aliyoyatengeneza kwa gharama kubwa sana.

“Sawa nimekusikiliza nitalifanyia kazi.”Tuntu aliamua kuyakatikiza maongezi hayo.Walibadilisha mada na kuendelea na mazungumzo mengine.Waliongea mpaka mida ya saa kumi na mbili jioni kisha walirejea nyumbani.

Mnamo mwezi wa sita walikuwa wamekwishapangiwa shule watakazokwenda kusoma kidato cha tano.Tuntu alipangiwa kujiunga kidato cha tano katika shule ya sekondari Minaki iliyopo maeneo ya Kisarawe.Alipangiwa kuchukua mchepuo wa HGL huku Salma akiwa amechanguliwa katika shule ya sekondari Zanaki akiwa anachukuwa mchepuo wa ECA.

Kitendo cha Tuntu kuchaguliwa mchepuo wa Sanaa hakikumridhisha baba yake.Baba yake alihitaji Tuntu asomee masuala ya biashara ili baadaye aje kuwa msimamizi wa biashara zake,lakini Tuntu hakuwa na ndoto ya kufanya biashara bali alitamani kuwa mwalimu.

“Mimi sipo tayari kukusomesha masomo ya kijinga!Midhali umeshindwa kuendana na matakwa yangu basi utajijua mwenyewe!”Baba yake alibwata sana baada ya kupokea taarifa za Tuntu kuchaguliwa mchepuo huo.

“Lakini mume wangu tumuache mtoto asome anachokipenda!” Mama Tuntu alijaribu kumtetea mwanaye.

“Kama upo tayari msomeshe lakini mimi sina muda huo.”Baba yake alichachawa aliendelea kusimamia maamuzi yake.Tuntu alirithi ubishi kutoka kwa baba yake. Waliamini katika mawazo na misimamo yao kuliko kitu kingine.

Baada ya baba yake kutoa msimamo huo,aliinuka na kuelekea chumbani na kuwaacha Tuntu na mama yake wakiwa sebuleni.

“Sasa tutafanyaje mwanangu!? Ni bora ukubaliane na baba yako ukifika kule ubadilishe mchepuo usome mchepuo wa biashara.”Mama yake alijaribu kumsihi mwanaye ili mambo ya kukwaruzana na baba yake yasiwepo.

“Mama mimi sibadilishi akitaka aache nitajua mwenyewe nafanyaje!”Tuntu aliongea kwa hamaki kisha aliinuka na kuelekea chumbani mwake akimuacha mama yake akimkodolea macho pasi na kujua lipi la kufanya kwa wakati huo.

“Mizee mingine nuksi mambo ya kikoloni unayaleta leo hii..!?”Ni maneno ya Tuntu aliyoongea akiwa anaelekea chumbani kwake.Baada ya kuingia chumbani kwake,alijilaza kitandani huku uso wake ukiwa umetawaliwa na ndita….









Ilikuwa siku ya jumamosi ikiwa imebakia wiki moja shule zifunguliwe na wanafunzi wa kidato cha tano waanze kusajiliwa.Mpaka kufikia wakati huo,Salma na Tuntu walikuwa bado hawajafanya maandalizi yoyote.Salma alishindwa kufanya maandalizi kutokana na kiasi cha fedha kilichohitajika ilikuwa vigumu kwa wazazi wake kukipata.Zilihitajika takribani shilingi laki tatu na nusu ili akamilishe mchakato wote.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Siku hiyo ya Jumamosi walikutana maeneo ya Kinondoni B kwa ajili ya kubadilishana mawazo katika moja ya mkahawa. “Kwanza nikupe pole kwa changamoto hiyo, pia nasikitika sana kwasababu hata mimi nakabiliwa na changamoto moja?”Tuntu aliongea baada ya Salma kumaliza kuelezea shida yake.

“Changamoto gani tena..!?”Salma aliuliza kwa hofu kubwa.

“Mzee anataka nisome mchepuo wa bishara na mimi masomo hayo hayapo moyoni kiivyo kwa hiyo amekataa kunisomesha.”Baada ya kumaliza kuongea,Tuntu alimuangalia Salma kuona atalipokeaje.Salma alishusha pumzi kwa nguvu ishara ya kukata tamaa kwani Tuntu ndiyo alikuwa ni tegemeo lake la mwisho baada ya wazazi wake kwa wakati huo.

“Kwanza pole sana.Kwa hiyo tunafanyaje mpaka sasa!?”Salma aliuliza kwa unyonge.Tuntu alimuangalia kwa takribani sekunde tano hivi kisha alitabasamu na kusema,“Nakumbuka siku moja nilikupeleka kwenye baadhi ya miradi yangu midogomidogo hivyo mpaka sasa nina akiba kama ya laki nane hivyo itabidi tuitumie ili kukamilisha jambo hili linalotukabili.”

Salma machozi yalimdondoka taratibu huku akimuangalia Tuntu bila ya kummaliza.Alimshika mkono na kumbusu kisha alisema,“Tuntu umekuwa mkombozi wangu mkubwa sana,siamini kama naweza kuulipa wema unaonitendea mpaka sasa.Asante sana mpenzi wangu.”

“Usijali na fanya yote haya kwasababu ya upendo uliopo moyoni mwangu juu yako.Nakupenda pia Salma.”Tuntu aliongea huku akichomoa pochi yake iliyokuwa kwenye mfuko wa nyuma.Aliifungua na kutoa kiasi cha shilingi laki mbili na kumkabidhi Salma. “Kaandae vitu vya muhimu kwanza halafu hiyo iliypobaki nitamalizia kwasababu pesa nyingine iko benki.”Tuntu aliongea huku akimfuta machozi Salma kwa kutumia kitambaa chake.

Walimalizia vinywaji vyao na hapo walielekea kituoni kwa ajili ya kila mmoja kupanda gari na kuelekea nyumbani kwao.Mama yake Salma alifurahi sana kiasi cha machozi kumdondoka baada ya kuoneshwa pesa na Salma alizopewa na Tuntu.

“Mwanangu!Ukimuacha huyu kijana kwa makusudi hakika utakutwa na makubwa! Chondechonde mwanangu nakuomba usimuache huyu kijana,”Ni maneno yaliyotoka kinywani mwa mama Salma.

******

Ilikuwa ijumaa jioni zikiwa zimebakia siku chache ili jumatatu wanafunzi waanze kuripoti mashuleni kwao.Kwa kuwa Tuntu alikuwa anaelekea katika shule ya sekondari Minaki ambayo ni shule ya bweni,aliona busara kupata muda wa kuagana na mpenzi wake Salma kwani ingewachukua muda kidogo kuonana tena.

Walipanga kukutana kwa akina Jamse rafiki yake Tuntu maeneo ya Yemen,Tandale.Kwa kuwa chumba alichokuwa akilala Jamse kilakuwa pembeni,ilikuwa rahisi kwao kuingia ndani.Baada ya kuingia ndani walimkuta Jamse akiwa anafanya baadhi ya shughuli zake.

“Vipi ndugu naona ndiyo unapanga bajeti wakati siku zimeisha,inakuwaje?”Tuntu alimuuliza Jamse ambaye alikuwa akikusanya baadhi ya karatasi zilizokuwa kitandani ili kuwapa nafasi wageni wake wakae.

“Mchongo ulikuwa unazingua,inabidi kesho nizuke Kariakoo kununua vitu.Ila nashukuru suruali imeshashonwa.”Jamse alimjibu.Tuntu na Salma walikaa juu ya kitanda kwani hakukuwa na kitu chochote zaidi ya kitanda,stuli moja ambayo Jamse aliitumia kama meza pamoja na picha za wasanii wa ndani na nje ya nchi zilizokuwa zimebandikwa ukutani.

“Jamani nawaacha kidogo kuna kitu naenda kuchukua mara moja”Jamse aliwaaga na kuondoka ili kuwa nafasi ya kufanya mambo yao.Baada ya Jamse kuondoka,Salma na Tuntu walibaki wakiangaliana kisha walitabasamu kwa furaha huku Salma akiinamisha macho yake chini kwa aibu.

“Salma nimekwita leo kwa ajili ya kuagana kabla sijaenda shule.”Tuntu alifungua maongezi baada ya imya cha muda mfupi kisha aliendelea,“Salma najua naachana na wewe kwa muda kidogo.Kwa kipindi chote hiki utakutana na marafiki wapya,utakutana na watu wapya kutoka sehemu mbalimbali,nakuomba usinisahau Salma.Nakuomba ukikaa picha yangu iwe inatawala fikra zako kiasi cha kutotamani kumuona mwingine Zaidi yangu.Salmaa…!”

“Tu..Tu..Tuntu…Naomba uishie hapo mpenzi wangu!”Salma alimkatikiza Tuntu kwani machozi yalikuwa yamekwishaanza kumbubujika. “Tuntu umekuwa nguzo yangu kubwa sana katika maisha yangu.Kuondoka kwako ni pengo kubwa kwangu.Tuntu siwezi kukusahau.”Salma alishindwa kuvumilia kiasi cha sauti ya kilio cha chini ilisikika.

“Najua upendo ulionao juu yangu kwa sasa.Ila mimi na wewe hatujui siku zijazo tutakuwa katika hali gani.Nakuomba CHUNGA SAANA LAAZIZI WANGU…!” Tuntu naye alishindwa kuvumilia na hapo machozi yalianza kumdondoka taratibu.Wakati huo walikuwa wamekumbatiana huku wakijaribu kufutana machozi.

“Nakuahidi Tuntu sitojaribu kuwaza kukusaliti.Nakupenda na nitakupenda mpaka mwisho wa maisha yangu…”Salma aliongea kwa hisia kali sana.Kabla hajaendelea kuongea,ghafla mlango ulianza kugongwa.

“Jamse! Jamse! Wee Jamse sininakwita wewe!?”Ilikuwa ni sauti ya bibi yake Jamse aliyekuwa akiita huku akigonga mlango kwa nguvu.

Tuntu na Jamse walikaa kimya kusikilizia hatima yake.Baada ya kuita bila ya kujibiwa,bibi aliondoka huku akijisemeza mwenyewe, “Nasikia watu wanaongea lakini naita hawaitikii,adabu gani!?”Baada ya bibi kuondoka Tuntu na Salma walibaki wakicheka chini kwa kutona na bibi alikuwa na mapengo hivyo uongeaji wake ulikuwa wa kuchekesha.

Tuntu na Salma walikumbatiana kwa muda wa takribani sekunde kumi na tano na hapo hisia zao zilianza kubadilika.Miili yao ilianza kusisimuka na hapo mioyo yao ilianza kuwaenda mbio huku macho yao yakianza kubadilika na kuwa mekundu.Walijikuta wamedondoka kitandani na hapo midomo yao ilikutana na kuanza kunyonyana mate.

Tuntu alianza kumtomasa sehemu mbalimbali za mwili kuanzia nywele mpaka kwenye kisigino na hapo Salma alianza kusafiri taratibu kuelekea kwenye kisiwa cha malavidavi.Baada ya dakika kama ishirini,wakiwa kama walivyozaliwa,hakukuwa na kizuizi chochote zaidi ya kulisakata kabumbu.

Kwa upande wa Salma ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo.Starehe aliyokuwa akiipta,ilimfanya kutoa miguno mbalimbali.Tuntu baada ya kuiona hali ya Salma,alijiridhisha kuwa ulikuwa muda muafaka wa kumuingiza baba watoto.Akiwa katika harakati za kutaka kumuingiza baba watoto chumbani,ghafla mlango uligongwa tena kwa mara ya pili.

“Hivi humu kuna mtu kweli?”Mara hii ilisikika sauti ya mama Jamse.

“Yumo humoo! Huoni kama hakuna kufuli?Tena wamo wawili niliwasikia kwa masikio yangu”Bibi alizidi kusisitiza.Kitendo cha bibi na mama Jamse kuwapigia fujo kwa kugonga mlango,kiliwafanya Tuntu na Salma kutoka kwenye kisiwa cha malavidavi na kurudi ulimwenguni.Tuntu aliangalia muda kwenye saa yake na hapo ilikuwa imeshatimia mida ya saa kumi na mbili na nusu jioni.

“Tulitaka kumtuma Kwa Mtogeli sasa sijui amelala?”Mama Salma alimjibu jirani yao aliyemuuliza kulikoni mbona wanagonga bila ya mafanikio. “Jamse humo hayumo maana nilimuona anatoka muda mrefu tu uliopita.”Jirani yao aliwambia.

“Sasa humu yumo nani!?”Bibi aliuliza kwa mshangao kidogo kwani aliwasikia Tuntu na Salma wakiongea. “Mh! Basi ndiyo mjiulize ila Jamse hayupo humo.”Jirani aliwahakikishia kuwa Jamse hakuwepo hivyo wajiulize nani yupo humo ndani kwani mlango haukufungwa kwa nje.

“Au marafiki zake ndiyo wamejipumzisha.”Mama Jamse aliongea kasha alimtaka bibi walielekea ndani kwa kmsubiri Jamse mpaka atakaporudi.Tuntu na Salma waliyasikia yote yaliyokuwa yakizungumzwa nje.Hamu ya kurudi kwenye kisiwa cha malavidavi iliondoka moja kwa moja.

Waliamua kuvaa nguo zao kwani disko aliingia Mmasai.Giza lilikuwa limeanza kuingia,Tuntu alifungua taratibu mlango na hapo alichungulia huku na kule kuangalia nje kukoje.Baada ya kujiridhisha kuwa mazingira yalikuwa salama,alimshika Salma mkono na kuchoropoka kuelekea nje ya nyumba.

Wakiwa wanamalizia kutoka getini,bibi alitokea chooni akiwa na haraka kuwaangalia walikuwa ni akina nani,kwani alisikia mlango ukifunguliwa. “Mama Jamse wameondoka sasa hivi!”Bibi alipiga mayoe.Bahati mbaya hakuwaona sura zao ila aliwaona wakiwa wanamalizia visogo vyao…..

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Tuntu na Salma baada ya kuchoropoka,walikimbia taratibu kuelekea kituoni.Walipita vichochoro viwili vitatu na hapo walitokea kituoni Yemen.Baada ya kufika kituoni huku wakipumua kwa nguvu,waliangaliana usoni na hapo wote walicheka japo Salma alitawaliwa na sura ya aibu.

Tuntu alichukizwa na kitendo cha bibi alichokifanya kwani alimpokonya tonge mdomoni siku hiyo kutokana kwamba ndiyo ilikuwa fursa kwake kulila tunda la Salma.

“Huyu bibi mbeya sana!”Tuntu aliongea kwa hasira.

“Hapana Mungu hajapanga usimlaumu sana bibi.”Salma alima moyo.Walisubiri gari kwa takribani dakika tano na hapo gari liliwasili.Tuntu alipanda gari lililokuwa likielekea Kawe huku Salma akipanda gari lililokuwa likielekea Gongo la Mboto ili ashuke Magomeni Mikumi.

Siku hiyo wote mawazo ya walichokifanya yalitawala fikra zao kiasi cha kutotembelewa na usingizi.Salma aliwaza ilikuwaje mpaka kujikuta katika ulimwengu wa raha ambayo hakuwahi kuipata tangu azaliwe.Alijikuta anaanza kumchukia bibi aliyeikatikiza raha yake isiyokuwa na mfano.

Tuntu naye aliona sasa kwa upande wake kuna mkono wa mtu kwani kila akipanga kulitungua Tunda la mtomto huyo mambo yanaingiliana.Aliwaza na kuwazua maana nafasi hiyo ndiyo ilikuwa ya pekee kwa wakati huo kwana kuonana naye tena ni baada ya miezi mitatu.

“Nitachukua muda mrefu kuonana na Salma,hivi kwa raha iliyompagawisha leo hatotamani kuipata kwa wajanja wengine..!?”Ntuntu alijiuliza kimoyomoyo baada ya kuyakumbuka maneno ya rafiki yake Jamse kuwa awe makini na wasichana.

Usiku kucha aliumaliza kwa mawazo lukuki.Mpaka kufika mida ya saa kumi na nusu alfajiri ndipo usingizi ulimchukua.Salma naye usingizi ulimchukua mida ya saa kumi kamili alfajiri.

Kesho yake siku ya jumamosi,Tuntu aliitumia siku hiyo kufanya maandalizi ya hapa na pale ikiwa ni pamoja na kunyosha nguo zake pamoja kupanga vifaa vilivyohitajika shuleni.Baada ya kupanga vitu vyake barabara,alimpigia simu Jamse ili waanze kuyapanga yatakayofanyika kesho yake.

“Jamse kesho mapema tu mida ya saa tisa maana nimeshachoka kukaa kitaa”Tuntu alisikika akiongea.Wakati akiendelea na mazungumzo,baba yake alikuwa amekwisha rejea na hapo alisimama nyuma yake akimsikiliza aliyokuwa akiongea.Tuntu hakujua kama ,mzee alikuwa kisharudi.

“Mwanaume inabidi uwe na misimamo yako bwana!Sio kwasababu huna hela unyanyaswe kizembe!Mzee kakataa kunisomesha mimi nitakomaa kivyangu.”Tuntu alizidi kutiririka bila ya kujua kama mzee wake alikuwa akimsikiliza.Tuntu aligeuka nyuma ili kuelekea chumbani kwake na hapo alikutana ana kwa ana na baba yake.Moyo ulidunda mithili ya mpira.

“Haya mwanaume!Huo uanaume wako umeutoa wapi!?”Baba yake aliongea kwa ghadhabu.Tuntu hakumjibu Zaidi ya kuinamisha sura chini.Baba yake alifoka sana kiasi cha koo kumkuaka.

“Kumbe naishi na mwanaume mwenzangu humu ndani eee!Sasa kwa kuwa wewe ni mwanaume,naomba usinijue kwa chochote kuanzia leo ujihudumie wewe mwenyewe!”Mzee alichachamaa kisha aliondoka na kuelekea chumbani bila ya kuhitaji maelezo yoyote kutoka kwa Tuntu.

Tuntu alibaki amenywea bila ya kujua kipi cha kufanya.Aliifikiria kauli ya baba yake mara mbilimbili bila ya kupata jibu. “Huyu mzee imekuwaje kunibadilikia hivi ghafla?Kisa kukataa kusoma anachokipenda,au mimi sio mwanaye!?”Tuntu aliwaza mpaka kufikia mbali Zaidi. “Hii mikabila mingine sio kabisa!” Aliinuka na kuelekea chumbani kwake.

Usiku mida ya saa mbili kuamkia kesho yake jumapili ambayo Tuntu alitakiwa kuelekea shuleni,Mama yake alimfuata chumbani ili kuongea naye mawili matatu kabla hajaondoka. “Mwanangu!Baba yako kiukweli simuelewi siku hizi.Hata mimi hatuna maelewano mazuri kwasababu anasema mimi ndiyo nakupa jeuri usifuate anachokisema.Ila mwanangu nakuomba ukasome kwa juhudi zako zote.Nakutakia kila la heri na uishi vyema na wenzako.”

“Mama mimi nashukuru ila kuanzia kesho nahisi hamtaniona tena kwenye hii nyumba!”Tuntu aliongea kwa hasira ya mbali kidogo.Mama yake alishtuka.

“Unasemaaa!Hiyo kauli una akili timamu kweli!?”Aliongea kwa ghadhabu huku akiwa amemkodolea macho Tuntu.

“Nina akili zangu timamu.Mzee amesema kwamba nisimjue kwa jambo lolote sasa unaona kuna haja ya kuishi naye?”

“Hamaanishi ndiyo uondoke nyumbani.Yeye anachofanya ni kukutisha ili ubadilishe maamuzi yako.”

“Sasa mimi sitaki kuishi maisha ya paka na panya,abaki na vitisho vyake.”

“We mwanangu wewe hebu acha kujitafutia radhi za bure.Una dhani sisi tutafurahi uende kuishi mtaani kama chokoraa wakati tunao uwezo wa kukuhudumia?”

“Kama mnataka mimi nirudi,baba atengue kauli yake!”Tuntu alichachamaa.Mama yake alimsihi na kumuahidi ataongea na baba yake ili wayamalize.Baada ya kukubaliana,mama yake alimkabidhi kiasi cha fedha kama laki moja ili imsaidie katika matumizi yake ya kawaida awapo shuleni.

Tuntu baada ya kupokea Baraka na zawadi kutoka kwa mama yake,alijilaza kitandani.Akiwa katika harakati za kuutafuta usingizi,mawazo yalimrudisha siku za nyuma kidogo alizowahi kukorofishana na baba yake.

Baba yake alihitaji kumpeleka shule za kulipia kwa kumuhamisha kutoka Azania lakini Tuntu alikataa.Kulitokea mvutano mkubwa sana kiasi cha Tuntu kuchelewa kuanza masomo kwa mwezi mzima lakini baba yake alilegeza na kukubaliana na msimamo wa Tuntu.

Akiwa katikakati ya mawazo hayo,ghafla simu yake iliita.Alipoiangalia alikta ni Salma ndiyo aliyempigia.Baada ya kupokea na kusalimiana,Salma alianza kwa kulaumu kwanini Tuntu hajmpigia tangu waachane siku hile ya nusu fumanizi.

“Hupaswi kulaumu kwa hilo bali inabidi tu ubvumilie maana purukushani za hapa na pale za maandalizi zinachukua fikra kubwa.”Tuntu alimpoza mpenzi wake na hapo waliendelea na mazungumzo mengine.

“Baby mi nakutakia safari njema,ufike salama na Mungu akuepushe na kila la shari.”Salma aliongea kwa huzuni kwani hakuwa tayari kuachana naye kwa wakati huo.Hakutamani kukata simu kwa wakati huo.Salma alisikika akilia.Tuntu machozi yalianza kumlengalenga kwa bali kwani kilio cha Salma kilimsikitisha.Hawakuwa na jinsi Zaidi ya kuagana na kuutafu usingizi.

*******

Kesho yake mida ya saa tisa mchana,Tuntu alichukua vitu vyake muhimu ili kuianza safari yake ya kuelekea shuleni kwao Minaki Kisarawe.Kwa kuwa baba yake hakuhitaji kutoa ushirikiano,ilibidi akodi usafiri wa tax ambao ilipidi umpeleka moja kwa moja mpaka shuleni.Baada ya kupakia vitu vyake ndani ya gari,alimuaga mama yake pamoja na wafanyakazi wa nyumbani kisha dereva alianza safari.

Walimpitia Jamse maeneo ya Magomeni Kanisani ambapo alikuwa amawasubiri kisha waliendelea na safari yao.Kwa kuwa siku hiyo hakukuwa na msururu wa magari njiani,iliwachukua masaa mawili na nusu kuwasili shuleni kwao.

Walipokelewa na mwalimu Salum Rubase ambaye alikuwa na jukumu la kuwapokea wanafunzi wapya kwa siku hiyo.Mwalim aliwaelekeza taratibu za kufanya kwa siku hiyo ili wapatiwe vyumba vya makazi yao pindi watakapokuwa hapo kwa muda wote wa masomo.Taratibu zote zilikamilika mida ya saa moja usiku na hapo wanafunzi wote walielekea kupata chakula cha usiku.

Baada ya kupata msosi,walielekea vyumbani mwao kwa ajili ya kujipumzisha.Siku hiyo mawazo yote ya Tuntu yalikuwa kwa Salma.Alihisi kama yupo gerezani kwani uwepo wa Salma pamoja na mazoea ya kusoma shule ya kutwa,vilimpa tabu sana siku hiyo.

Usiku mida ya saa tisa usiku,Tuntu aliota ndoto.Aliota siku moja alikuwa na Salma sehemu moja hivi yenye poli kubwa na miti mingi.Walikuwa wakitembea taratibu wakiifuata njia iliyonyoka sana.Walivyofika mbele kidogo walikutana na mapanda njia.Tuntu alimtaka wanyoke nayo njia hiyo lakini Salma almtaka wakatitishe njia iliyokwenda kushoto.

Tuntu ilibidi akubaliane naye na hapo walisonga na njia iliyoelekea kushoto na kuiacha ile iliyonyoka.Walipofika mbele,walikutana na mto mkubwa uliokuwa ukitembea kwa kasi.Waliusogelea na kwa mbele kidogo waliona maporomoko makubwa.Salma alimtaka waelekee kuyaangalia maporomoko hayo.

Walipofika karibu na maporomoko ya mto huo,Salma alimkumbatia Tuntu na kuanza kumpiga denda.Wakiwa katika harakati hiyo ya kupata uroda,Salma alimgeuzia Tuntu kwenye ukingo wa mto na hapo baada ya muda mfupi alimsukumia kwenye maporomoko hayo huku akicheka na kubetua midomo.

“Mamaa..!Nakufaaa…!”Tuntu alikurupuka kitandani huku akipiga mayoe.Kitendo cha Tuntu kupiga mayoe,kiliwaamsha baadhi ya wanafunzi wenzake akiwemo Jamse ambaye alikuwa kitanda jirani.Jamse aliinuka na kumfuata Tuntu ili kujua kulikoni.

“Daah! Nimeota ndoto mbaya.”Tuntu alisema baada ya kuulizwa na Jamse kulikoni.

“Ni ndoto gani tena ndugu!?”Jamse alipatwa na wasiwasi.Tuntu alimuahidi kumsimulia kesho yake aliota ndoto gani.Wanafunzi walioamka walirudi kwenye vitanda vyao kuendelea na sakata la kustarehe.Wakati wote Tuntu alikuwa akijifyonya kutokana na kujiuliza ndoto hiyo ilikuwa na maana gani.

“Salma atanifanyia jambo baya.Kwanini niote ndoto hii!?”Usiku wote Tuntu aliumalizia kwa mawazo juu ya ndoto hiyo.Mida ya saa kumi na moja waliamka ili kujiandaa kwa ajili ya kujiandaa na kuripoti shuleni kwa ajili ya usajili…



“Ndugu yangu nadhani niliwahi kukuambia kuwa muangalifu,naona Mungu ananisaidia kufikisha ujumbe.”Jamse alimwambia Tuntu baada ya kumueleza ndoto aliyoiota usiku.

“Unamaana hii ndoto inatoka kwa Mungu,au shetani ananichezea tu fikra zangu?”Tuntu bado alikuwa hana Imani kwamba ndoto ile ilikuwa ni tahadhari.Waliachana na mazungumzo hayo na kuendelea na mazungumzo mengine.

Siku zilisonga mbele takribani wiki moja ilipita.Salma alikuwa ameshajiunga na kidato cha tano katika shule ya sekondari Zanaki.Baada ya kufika shuleni hapo,alichaguliwa kuwa kiongozi wa darasa.Mambo yalimuendea vizuri ndani ya wiki hiyo kwani Tuntu alimuacha akiwa na kiasi kizuri cha fedha ambacho kingelimsukuma siku kadhaa hivi.

Ndani ya mwezi mzima Salma alikuwa mpweke.Pengo la uwepo wa Tuntu lilionekana waziwazi katika maisha yake.Maisha yalimuendea kombo kadri siku zilivyosonga mbele.Alipewa msaada na baadhi ya rafiki zake aliowapata shuleni hapo,lakini ilifikia kiwango wakaanza kumchoka kwani alikuwa tegemezi katika kila kitu.

Siku moja Salma alikuwa anatembea kwa mguu kutokea shuleni kwao Zanaki maeneo ya Posta kuelekea nyumbani kwao Magomeni.Aliamua kutembea kwa mguu kutokana na kukosa hata miambili ya nauli. Katika harakati za kutembea alifika meneo ya chuo cha DIT.

Ghafla aliona gari linasimama mbele yake kwenye kituo.Aliendelea na kutembea lakini alipolifikia gari hilo,dereva alishusha kioo na kumuita. “Unaelekea wapi binti?” Ilikuwa sauti ya kijana wa makamo ya umri wa miaka ishirini na nane.

“Magomeni Mikumi”Salma alijibu huku akiwa kama ni mwenye haraka akitaka kumjibu na kuondoka zake. “Ingia ni kusogeze hapo mbele kidogo”Jamaa aliongea kwa sauti ya upole iliyojaa huruma na ushawishi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Hapana nitafika tu maana sio mbali sana,”Salma alikaza kidogo ili aonekane wa bei.Jamaa alimshawishi mpaka Salma akalegeza kamba na kukubaliana naye.Baada ya kuingia ndani ya gari hilo,jamaa alichukuwa boksi la juisi aina ya Azam embe na kumpatia Salma ili apoze koo.

Wakiwa wanaendelea na safari,jamaa alikuwa akimdodosa maswali ya hapa na pale ili kumfahamu zaidi.Alimuuliza jina lake na wapi alikokuwa anaishi.“Nimefurahi sana kukufahamu.”Salma alijikuta anaanza kumzoea taratibu japo mwanzo alionekana kutawaliwa na wasiwasi iliyochanganyikana na haya.

“Unaitwa nani?”Salma alivunja ukimya na kumuuliza. “Naitwa Hashiim Majura.Naishi Masaki.”Jamaa alijitambulisha kwa jina hilo. “Nimefurahi kukufahamu japo hujasema unajishughulisha na nini?” Salma alitokea kumzoe ghafla.

“Mimi ni mfanyabiashara…”Jamaa alikunywa funda la mate kidogo kisha akaendelea, “Nameanzisha kampuni ya kuagiza magari kutoka Japan.Kwa hiyo tunagangaganga.”Hashimu alijibu.

“Hongera zako,”Salma aliongea huku akitabasamu.Walifika mpaka Magomeni Mapipa na hapo Salma alimuomba amuache hapo. “Wanasema nafasi hairudi mara mbili,vipi naweza kupata namba yako?”Hashim alimuomba namba Salma baada ya Salma kumuomba amuache hapo.

Salma alikaa kimya kwa muda wa takribani sekunde kumi. Aliangalia huku na kule kama ni mwenye kuona haya kisha alimtajia namba yake. “Ila usinipigie usiku”Salma alimpa masharti. “Usijali lazima nifuate unavyopenda ili nisikukwaze.” Hashimu aliongea huku akimalizia kuihifadhi kwenye simu namba aliyopewa.Waliagana na hapo kila mmoja aliendelea na safari yake.

*****

Miezi ilizidi kusonga mbele.Kwa upande wa Tuntu masomo yalipamba moto kiasi cha yeye kuanza kupunguza taratibu mawazo juu ya kipenzi chake Salma yaliyomsumbua kwa takribani miezi miwili.

Kama ilivyokawaida katika mjumuiko wa watu hawakosi watukutu.Katika chumba cha akina Tuntu alikuwepo mwanafunzi mmoja amabaye alikuwa na simu ya mkononi.Siku moja mida ya saa nne usiku,Tuntu alimuomba ili aitumie kuwasiliana.Jamaa alimkabidhi simu na hapo Tuntu aliiandika namba ya Salma na kumpigia.

“Haloo! Naongea na nani..!?”Ilikuwa ni sauti ya Salma baada ya kupokea simu. “Unaongea na baba mwenye nyumba”Tuntu alijibu. “Baba mwenye nyumba yupi! Mzee Mdigo?”Salma alizidi kudodosa.Salma aliivuta sauti kwa umakini lakini haikuwa rahisi kwani Tuntu aliongea kama ni mwenye kukoroma.

“Wewe kuwa makinii!”Tuntu aliongea kwa sauti yake ya kawaida huku akicheka. “Wewe umenishtua!” Salma aliongea kwa furaha.Walisalimiana na kuulizana hali zao huku kila mmoja akiwa na shauku ya kuongea na mwenzake.

“Yaani baby nimekumisi sana daaah!”Salma aliongea huku akiinuka kutoka alipokuwa amelala.“Huwezi kunishinda mimi ndiyo maana nimekupigia.”Tuntu alisisitiza zaidi.Waliongea kwa takribani dakika kumi,na hapo yule kijana mwenye simu alianza kumgombeza Tuntu amkabidhi simu yake.

“Oyaah! Mwanangu unazingua na mimi na shida ya kuongea na wanangu wa kitaa!” Kijana aliongea huku akijaribu kumpokonya simu Tuntu ambaye alikuwa akikwepesha kwa kugeuka huku na kule huku akiongea.

“Tutaongea kesho maana mwenye simu ameanza kuchongachonga.”Tuntu alimuaga Salma kisha alikata simu. “Oya mwanangu mbona unazingua?Nimefikia kwenye utamu halafu unakatikiza!”Tuntu alimfokea mwenye simu. “Salio linaisha au utalipa”Jamaa aliongea huku akirudi kitandani kwake.

“Kuwa makini tu na huo msauti wako Patron akisikia,itakula kwako.”Tuntu alimwambia kijana mwenye simu. “Atafanyaje?kwani yeye hajui umuhimu wa mawasiliano?”Kijana alitunisha misuli yake kuonesha ni mbabe.

Vijana wote walilala na kumuacha yeye akiongea na watu wake aliowajeu mwenyewe.Tuntu siku hiyo usingizi ulikuwa mwanana.Aliota kila aina ya ndoto nzuri juu ya Salma kipenzi chake.Aliota wakiwa baharini,mara supermarket na sehemu mbalimba wakifurahia maisha.Alipoamka asubuhi mida ya saa kumi na moja,alijikuta amekumbatia shuka lake tu huku Salma akiwa ameyeyuka.

Maisha yalisonga mbele.Wiki moja baadaye Salma alikuwa nyumbani kwao mida ya saa mbili usiku akipika chakula.Akiwa katika harakati za mapishi,mara simu yake iliita.Alipoiangalia alikuta namba ngeni halafu haikuwa namba ya nchini Tanzania.

“Naamini naongea na Salma?”Ilisikika sauti kwenye simu ikiuliza baada ya kusalimiana. “Ndiyo..!”Salma aliitika kwa wasiwasi. “Mimi ni Hashim Majura yule kijana niliyekupa lifti siku ile ukitokea shuleni.”Jamaa alijitambulisha na hapo Salma alimkumbuka.Alituliza mapigo ya moyo na kuanza kuongea naye.

“Mbona naona namba ya nje ya nchi uko wapi?” Salma aliuliza. “Nilikuambia kuwa najihusha na biashara kutoka Japan nipo huku kuchukua mzigo pamoja na kuongea na wafanyabiashara wenzangu” Hashim alimjibu.

“Sawa” Salma aliitikia kisha alikaa kimya ili kumsikiliza nini alitaka kumuambia. “Leo una muda?Nilitaka tuongee kwa undani zaidi.”Hashimu aliuliza. “Mpaka baada ya lisaa limoja na nusu.” Salma alijibu. “Basi haina shida nitakupigia.” Hashimu alikata simu.

Salma alibaki akijiuliza maswali lukuki. “Huyu anataka kuniambia nini? Au anataka kunitongoza nini?”Alijiuliza bila ya kupata majibu.Aliendelea na shughuli zake kama kawada na ilipofika saa tatu na nusu usiku walikuwa wamekwishamaliza kula na kila mmoja alielekea kujipumzisha.Dakika kama tano baada ya kujilaza kitandani,simu yake iliita tena.Alikuwa ni hashimu aliyekuwa anapiga.

“Salma kuna jambo muhimu nahitaji kukuambia ila naomba unisikilize kwa makini. Kiukweli mimi mpaka sasa sijapata mwanamke sahihi wa kumuoa.Nimekuwa nikitafakari kwa kina bila ya kupata jibu juu ya mtu sahihi anyefaa kuwa mke wangu.Ila kwasasa nimelipata jibu la swali langu.”Alipumzika kidogo.

Salma mapigo ya moyo yalianza kumuenda mbio.Alijua dhahiri kijana huyo dhamira yake kuu ilikuwa ni kumtongoza.Alikaa kimya kuendelea kumsikiliza.Kijana aliendelea na mazungumzo. “Siku ya kwanza nilipokuona kiukweli ndipo nilipopata jibu langu.Bila hata ya kwenda mbali,Salma nakupenda sana na nipo tayari kusimamia kila kitu ili mladi baadaye uwe mke wangu.”Hashim alifunguka bila hata ya kuchelewa.

“Salma!Najua utakuwa unajiuliza utaanzaje kuwa na mimi wakati bado unasoma,ila tambua mimi nimejitoa kwa moyo mmoja kukusimamia mpaka pale tutakapofunga ndoa.!”Jamaa alizidi kumshawishi Salma ambaye alikuwa kimya huku ulimi ukiwa na kilo tatu kiasi cha kushindwa kuinuka.

“Naomba unipe muda kwanza nijifikirie maana umenishtukiza.”Salma aliamua kufunguka. “Labda nikupe muda wa siku ngapi?” Hashim alimpa uhuru wa kujichagulia mwenyewe. “Kama wiki moja hivi.”

“Basi mimi ningependa nikupe siku tatu.” Hashimu aliona wiki ni kubwa. “Labda ningependa uelewe kwanini nimeongea na wewe sasa hivi.Nimekuwa nikilifikiria suala la kukuambia nafsi yangu ikawa inanisukuma nikuambie mapema ila nikawa navuta subira ila leo subira imenishinda.” Hashim alizidi kumshawishi.

“ Basi nitakupa jibu baada ya wiki moja naomba uwe na subira tena.”Salma alisimamia maamuzi yake.Hashim ilibidi akubaliane naye na hapo waliongea mambo mengine kidogo kisha simu ilikatwa.Siku hiyo Salma hakupata usingizi mapema kwani alikuwa kwenye mtihani mzito.

********

Siku zilizidi kusonga mbele kiasi cha kubakia siku moja Salma ampatie jibu bwana Hashim. Siku hiyo Salma alikuwa na mawazo lukuki. Ilikuwa ni siku ya jumamosi mida ya saa kumi na moja jioni,ujumbe mfupi uliingia kwenye simu ya Salma.Alipousoma,ulikuwa unatoka kwa Hashim akimjuza kuwa ameshawasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere akitokea nchini Japan.Salma aliamua kuifunga simu yake ili akapopigiwa na Hashim asipatikane.

“Nafsi yangu inampenda Tuntu.Tuntu yuko mbali nami na ndiyo alikuwa mtatuzi wangu mkubwa,sasa hivi napata shida sana katika haya maisha.Hashimu ana pesa nyingi sana kiasi kwamba ameahidi kunisaidia kwa kila kitu.Daaah! Ila potelea mbali tu…” Ni mawazo yaliyokuwa yakipita kichwani mwa Salma ambaye mwishoni aliamua kuinuka na kuelekea ndani……

Masaa yalisonga mbele kwa kasi mpaka kesho yake ikawadia. Siku hiyo ndiyo ilikuwa maalumu kwa Salma kumpatia jibu bwana Hashim.Kwa kuwa Bwana Hashim alikuwa na uwezo wa kifedha,alipanga maongezi hayo yafanyikie ndani ya hotel ya Holyday Inn iliyopo maeneo ya Posta.

Mida ya saa nne asubuhi Salma alikuwa akijiandaa kwa ajili ya kusubiri kuambiwa wapi wakutane.Akiwa anaendelea na kujipura,ujumbe uliingia kwenye simu yake.Aliufungua ujumbe huo na hapo alikutana na meseji ya tigo pesa akiwa ametumiwa shilingi laki moja na nusu.

Salma alichanganyakiwa.Mara meseji nyingine iliingia,hii ilikuwa inatoka kwa Hashim ilisema,“Tumia hiyo kama nauli chukua Tax njoo Holyday Inn Hotel.”Salma alihisi kama yuko nchi nyingine. “kama nauli ndo hii je nikiwa mpenzi wake?”Salma alijiuliza moyoni.Hashimu alimteka ghafla.

Baada ya kumaliza kujipamba,alitoka nje na kuelekea kituoni.Hakuwa na haja ya kuchukua Tax kwa kuhisi ilikuwa ni uharibifu wa fedha.Alipanda daladala mpaka Posta na hapo alishuka na kuelekea kwenye hotel hiyo ambayo aliishia kuiona kwa nje siku zote na siku hiyo ilikuwa zamu yake kuingia humo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alipofika nje ya jengo hilo lenye kuvutia,alimpigia simu Hashim ili ampatie maelezo.“Ingia mapokezi halafu sema una mwenyeji wako chumba namba 230.Kisha utapanda lifti ukishuka utanikuta nimekusubiri.”Sauti ya Hashim ilisikika ikimpa maelekezo.Salma alifanya kama alivyoelekezwa.

Baada ya kushuka ghorofa ambayo chumba alichokodi Hashim,alimkuta Hashim akiwa amemsubiria. Baada ya kusalimiana,waliongozana mpaka ndani ya chumba hicho ambacho uzuri wake si wa kuelezewa.Salma alikaribishwa akae kwenye moja ya sofa zilizokuwemo humo ndani.

“Umekodi chumba chote hiki kwani hata hapo nje situngeongea yakaisha!?” Salma aliuza kwa wasiwasi.“Hapana wewe una hadhi kubwa sana.Siwezi kukuweka nje ambapo kila mtu anakuona”Hashim alimtoa wasiwasi. Muda mfupi muhudumu alileta vinywaji ili wapoze koo zao wakati wakiendelea na mazungumzo.

Hasimu alianzisha mazungumzo kwa kumuliza kama ameshafikiria juu ya ombi lake.Salma mapigo ya moyo yalianza kumuenda mbio.Ulimi ukawa mzito wakati muda ,mfupi uliopita alikuwa akizungumza kwa sauti nzuri huku akikisifia chumba lakini mada ilipobadilika aliugua ububu wa ghafla.

“Kiukweli hili nimedhamiria kutoka moyoni.Sina nia ya kukuchezea.nakupenda sana Salma.”Hashim alisisitiza. Salma aliinama chini kama mtu aliyezama kwenye fikra nzito,baada ya muda aliinuka na kumuangalia Hashim huku akiwa hapepesi macho kisha alimuuliza, “Hashim!Unanipenda kweli..?”

“Kungekuwa na uwezekano wa kuufungua moyo wangu ungeona jinsi gani ninavyomaanisha ninayokuambia.”Hashim alizidi kusisitiza.

“Nakuuliza vizuri ili nikikukabidhi moyo wangu baadaye nisije kujuta.”Salma alizidi kufunguka. “Yaani naomba uniamini.”Hashimu alimuhakikishia.Salma alikaa kimya kwa mda kidogo kasha aliamua kufunguka kwa kusema.

“Nimekubali kuwa na wewe.”Salma aliamua kukunjua moyo wake. Hashim ambaye alikuwa pembeni yake,alishindwa kujizuia na hapo alimkumbatia Salma na kumbusu. “Nakuahidi kuanzia leo hautaishi maisha ya shida kabisa.”Hashim aliongea kwa furaha. “Nashukuru kusikia hivyo” Salma aliongea huku akitabasamu.

Waliongea mengi mpaka mida ya saa saba mchana na hapo muhudumu aliwaletea chakula cha mchana. “Hivi hiki chakula bei gani” Salma aliuliza maana hakikuwa chakula ambacho alitegemea kama angewahi kula katika maisha yake.“Hiki ni bei rahisi sana ambapo sahani moja huwa laki tatu mpaka tatu na nusu baadhi ya hoteli ila hawa nawapenda wanauza laki tatu.”Hashim aliongea kama anataja kiasi cha elfu moja tu.

Salma alishtuka kwani kwake pesa ya sahani mbili ni sawa na pesa ya matumizi ya miezi mitatu mfululizo. “Samahani lakini,mbona mnatumia pesa vibaya?” Salma aliuliza. “Ha ha ha! Pesa vibaya,labda tufanyeje” Hashim aliuliza kwa furaha.

“kwanini usiende sehemu ambazo ni rahisi tu?” Salma alijibu. “Hapana hadhi niliyonayo hainiruhusu kwenda sehemu hizo unazofikiria.”Hashimu alijaribu kumbadilisha fikra Salma aamini kuwa jambo la kutumia milioni moja kwa siku ni la kawaida.

Baada ya kumaliza mazungumzo yao mida ya saa tisa jioni,walitoka na kurejea nyumbani.Hashim alimbeba Salma kwenye gari lake na kumpeleka mpaka maeneo ya nyumbani kwao.Walipofika maeneo ya magomeni mapipa,hashimu aliegesha gari pembeni mwa barabara ili kumuacha hapo Salma aondoke nyumbani kwao.

Baadaya gari kusimama pembeni mwa barabara,Hashimu alimuangalia usoni Salma ambaye alikuwa kainama kwa haya zilizomjaa.Salma naye alimuangalia na hapo mioyo yao ilijikuta ikienda mbio.Hashim alikosa uvumilivu aliamua kulishika paja la Salma huku akilitomasatomasa taratibu.

Akiwa anafanya hivyo,mara alijikuta mkono unapanda taratibu kuelekea kifuani kwa Salma na hapo aliyafikia matiti yaliyosimama barabara mithili ya mwiba wa mchongoma.Aliyasikashika taratibu huku akimbusu Salma kwenye shavu lake la kushoto. Salma alianza kupagawa taratibu na hapo alianza kuushika mkono wa Hashim na kuupapasa.

Hashimu aliingiza mkono ndani ya brauzi ya Salma na kuyashika matiti barabara.Walijikuta wanaanza kupigana denda taratibu huku Salma akianza kusafiri kutoka Magomeni mpaka New York bila ya yeye kutegemea. Aliikumbuka ile raha aliyoipata siku ile Tuntu alipomchezea kwenye chumba cha Jamse.

Baada ya dakika kama kumi,Salma matiti yalikuwa wazi kutokana kwamba Hashim alimvua brauzi yake bila yaye kujua. Pia alimpandisha siketi yake mapaja yote yakawa wazi mpaka maeneo ya bi kidude aliyezuiwa na chupi tu.Mambo yalikuwa mambo ndani ya gari hilo ambalo lilikuwa na faragha kutokana na kuzuiwa kwa vioo vyeusi.

Salma alishtuka baada ya Hashim kumfungua chupi na kuingiza mkono ulioanza kumchezea bi kidude. “Nooh! Hashim tutafanya siku nyingine!” Salma aliutoa mkono wa Hashim falagha. “Mmmh! Kidogo tu maana nipo hoi!”Hashim aliongea kwa sauti ya kutweta. “Panga siku maalumu siyo leo huoni tupo barabarani?” salma aliongea kwa sauti ya ushawishi.

“Basi uje nyumbani kwangu jumamosi ijayo.” Hashim alimuomba.baada ya Salma kukubali,alichukua pochi yake na kuchomoa kiasi cha shilingi laki moja na kumkabidhi. “Basi usikose kuja jumamosi mapema.”Hashim alimsisitizia.

“Asante”Salma alimshukuru na hapo alitoka ndani ya gari na kuushika mtaa wa kuelekea nyumbani kwao.Hashim hakuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kulipasha moto gari lake na kuelekea nyumbani kwake.

Mida ya jioni Salma alikuwa amejilaza kitandani kwake akifikiri mambo mbalimbali.Alifikiria siku ya kwanza kuonana na Hashim mpaka siku hiyo.Moyo ulianza kumuingiza taratibu Hashim;lakini uzito ulikuja kila alipokuwa akimfikiria Tuntu. “Nitajua mbele kwa mbele itakavyokuwa.”Alijisemeza akilini mwake.

Maisha yaliendelea kama kawaida huku ukaribu kati ya Salma na hashim ukipamba moto zaidi.Simu zilikuwa hazikatiki mara kwa mara kiasi cha nafasi ya Tuntu kuanza kupotea taratibu kwani kama ni shida ya pesa alikuwa akikohoa tu zinamfikia kutoka kwa Hashim.Alianza kuishi maisha ya kimalkia kutokana na huduma aliyokuwa akiipata kutoka kwa Hashim.

Ilikuwa siku ya Alhamisi usiku wa saa nne zikiwa zimebakia siku chache Salma aende nyumbani kwa Hashim.Simu yake iliita na alipoingalia ilikuwa ni namba ya yule rafiki yake Tuntu aliyemuazima simu ile siku ampigie. Simu iliita bila ya Salma kuipokea. Ilipigwa tena hakupokea na mara ya tatu ilibidi apokee. “Mbona unanipigia usiku nimepumzika?Nipigie kesho.”Salma hakutaka kumsikiliza Tuntu alijifanya kuongea kama mtu aliyetoka usingizini.

“Tuntu hakutegemea kupewa jibu hilo na Salma. “Unamaanisha ni achane na wewe?”Tuntu aliuliza kwa hasira ya mbali. “Siyo hivyo naomba tu unipigie kesho mida ya jioni,nimechoka.”Salma alimjibu. Tuntu alikata simu kwani hasira ilikuwa imeanza kumtawala hivyo angefanya mambo ya ajabu.

Salma alibetua midomo kwa dharau kisha aliendelea kujibizana na Hashim kwa njia ya meseji. Waliongea mpaka mida ya saa sita usiku;na hapo waliagana kila mmoja alale salama huku wakipeana maneno ya upendo wa hali ya juu.

**********

Tuntu kwa upande wake usingizi siku hiyo haukumtembelea hata chembe.Alilala chali kitandani akiyafikiria majibu ya Salma ameyatoa wapi. “Huyu ni Salma ninayemjua mimi au?Jeuri ya kunijibu hivyo ameitoa wapi?”Tuntu alijiuliza bila ya kupata jibu. Mawazo yake yalimpeleka mpaka mida ya saa kumi na moja ambapo ni mda wa kuamka kwa ajili ya kujiandaa na shule.

Kwa upande wa Salma hakuwa na mawazo kama amemuumiza Tuntu kwa kumjibu vile.Aliendelea na harakati zake mpaka ilipofika siku ya jumamosi aliyoahidiana na Hashim aende nyumbani kwake.

Siku hiyo Salma aliamka mapema na kufanya shughuli zake kwa haraka.Baada ya kumaliza shughuli zake mida ya saa nne asubuhi,alielekea kituoni na kupanda gari ya kuelekea nyumbani kwa Hashim.Alitumia kama dakika ishiri kuwasili nyumbani kwa Hashim na hapo alimkuta Hashim peke yake.

“Jisikie uko nyumbani kabisa”Hashim aliongea huku akifungua friji na kuchukua boksi la juisi ya Azam Embe. “Unaipenda sana juisi hiyo?”Salma aliuliza. “Sana kuliko vinywaji vingine.wewe unapendelea nini?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Napendelea sana Mo passion!” Salma alijibu. Waliongea mengi kwa mda wa dakika kmi na tano kisha Hashim alianza kumtembeza ndani ya jumba hilo la kifahari.Alimuelekza kila sehemu ikiwemo jikoni.Mida ya saa sita mchana,Salma alinza kuandaa chakula cha mchana ambapo alipika wali na nyama.

Mpaka kufikia mida ya saa saba na nusu mchana chakula kilikuwa tayari.Alipakua chakula na kumpatia kijana aliyekuwa mlinzi wa ntumba hiyo kisha aliandaa chakula kwa ajili yao.Walikula chakula huku wakilishana na kunyweshana.Baada ya kumaliza kula mida ya saa nane na nusu,walielekea chumbani kwa ajili ya kujipumzisha.

“Baby nimekulekeza sehemu zote ila sehemu moja sijakuonesha.”Hashim alimwambia Salma. ‘sehemu ipi?”Salma aliuliza.Hashim hakumjibu ila alishika mkono na kumuongoza kuelekea chumbani







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog