Simulizi : Facebook Imeharibu Maisha Yangu
Sehemu Ya Nne
(4)
Mnamo mwezi wa kumi na moja familia yake
yote ilisafiri kuelekea jijini Mwanza kusheherekea kwa pamoja mahafali ya mtoto
wao,Eveline ambaye tayari alikuwa kazini baada ya kuwa amemaliza miaka yake
mitatu chuoni na kufaulu vizuri pia alijumuika katika kukamilisha furaha hii ya
rafiki yake mpenzi huku akiongozana na mchumba wake Benjamin
Simon.
Reshmail alifurahishwa sana na ujio wa Eve kwani alizidi
kudhihirisha kuwa ni kiasi gani yeye ni rafiki wa
kweli.
Yalikuwa ni mahafali makubwa na ya kipekee kuliko yote
yaliyowahi kutokea ambapo chuo cha Mt.Augustino kilifanya mahafali ya pamoja na
matawi yake yote Tanzania,yaani Iringa,Mtwara na Tabora. Kwa ufupi yalikuwa
yamefana.
Ni katika pirikapirika na pitapita za huku na huko za
sherehe hiyo ndipo Reshmail akiwa na Eveline ana kwa ana anakutana na familia ya
Adam yaani baba na mama yake,aliwatambua kwa uwepo wa Rosemary yule mdogo wake
Adam.
Rosemary alikuwa ndio kwanza amehitimu shahada ya elimu
katika chuo kikuu cha mtakatifu Augustino tawi la mtwara hivyo yeye na familia
yake pia walikuwepo katika viwanja vya Raila Odinga kusheherekea mahafali
yale.
"Mchawi...mchawi!" alianza kupiga kelele mama yake Adam
wakati Reshmail akisogea taratibu katika eneo walilokuwepo kwa
furaha.
"Uuuwii" alipiga makelele kwa sauti ya juu jambo
lililovuruga usikivu katika eneo lile na watu kuanza kumwangalia yeye kama mtu
aliyechanganyikiwa, Reshmail na Eve walikuwa wameganda tu na mama Adam akizidi
kupiga kelele,
Jitihada za baba yake Adam kumtuliza mkewe
hazikufua dafu,mara ghafla mama Adam akakurupuka akiwa na chupa iliyokuwa na
soda ambayo haijafunguliwa bado na kwa kasi akaenda kumkabili Reshmail ambaye
akili yake ni kama ilikuwa imesimama na umati uliokuwa umemkazia macho kwa
kitendo cha kuitwa mchawi ulimzidishia hofu na fedheha kwake, Eve alimshika
mkono Reshmail na kujaribu kumvuta watoke eneo lile lakini tayari mama Adam
alishawafikia na kwa nguvu kabisa akaituliza chupa ile juu ya kichwa cha
Reshmail palepale akaenda chini huku damu nyingi ikimtoka
kichwani.
Wanaume watatu akiwemo pia baba yake Adam walifika na
kumbeba juu juu,mama Adam ambaye alionekana dhahiri kuwa bado hajaridhika na
kipigo alichotoa kwa Reshmail kwani bado alikuwa anaangaza huku na huko kama
palikuwa na silaha nyingine. Alikuwa kama mwendawazimu.
Wengine
walimbeba Rshmail ambaye joho lake la kipekee kabisa lilikuwa limechafuliwa
vibaya na vumbi la uwanja wa mpirawa miguu wa Raila Odinga ambapo ndio sherehe
zilifanyika. Hali ya sintofahamu ilitawala sherehe zile kwa takribani nusu saa
nzima hadi Reshmail alivyoondolewa na familia yake kuelekea hospitali na mama
Adam kutiwa katika nguvu ya dola
***
Halikuwa
jeraha kubwa sana nyuzi mbili zilipita katika kichwa chake kushona jeraha
lile
?kwa nini mama mkwe wako akutende hivi? eve alimuuliza
Reshmail akiwa pale kitandani
?ni haki yake hata kunipiga
risasi mimi ni chanzo cha maumivu haya wanayoyapata? alijibu Resh huku
akilazimisha tabasamu
?kwa hio hapa amenionea huruma sana mimi
ni sawasawa na muuaji tena wa kukusudia na haki yangu ni kuuawa pia? aliendelea
Reshmail huku akitoa tabasamu hafifu tena
?usiseme hivyo mamii
sio wewe uliyetaka iwe hivyo ni Mungu pekee? aliongea kwa upole Eve huku
akivibinyabinya vidole vya Reshmail
?mama mwambie baba afatilie
mama mkwe asije kulazwa selo hata kwa saa moja hana kosa lolote? Reshmail
alimwambia mama yake alipoingia katika chumba cha hospitali ya Agha khan
aliyokuwaelazwa kwa ajili ya matibabu maneno hayo yalimshangaza sana mama yake
aliyetegemea Reshmail atakuwa na hasira ya kutendwa vile mbele ya
hadhara
Nafsi ilikuwa inamsuta sana mama reshmail,moyo uliomba
msamaha lakini mdomo ulikuwa mzito sana kufanya hivyo. Hali hiyo ilimkondesha
sana na kumkosesha raha ndani kwa ndani unene wake wa asili uliyafunika yote
hayo na hakuna aliyejua jambo zito alilobeba mama huyu.
Kweli
badala ya bwana na bibi Manyama kuegemea upande wa mashtaka ili mama Adam apewe
adhabu la wao waliunga mkono kwamba Reshmail alikuwa na makosa mahakama
ikatupilia mbali mashtaka hayo na mama Adam akawa huru,jambo hilo badala ya
kurudisha undugu liliongeza chuki na uadui
?si nilikwambia
ukabisha?? Kama hawajamtoa mwanetu kafara kwanini sasa wamekubali niachiwe
huru??? mama Adam alimwambia mumewe jambo ambalo wakati huu hata yeye
alikubaliana nalo kuwa motto wao mkubwa wa kiume(Adam) alitendwa vibaya na
familia ya reshmail .
kuamini kwa mzee Michael baba yake Adam
ni sawa na familia nzima kuamini kabisa na sumu ya chuki ikamwingia kila
mwanafamilia na kuwa aadui wakubwa wa familia ya mzee
Manyama.
Siku mbili alizokaa pale hospitali hakuja
hata mwanafunzi mmoja kutoka pale chuoni kuja kutoa pole kwa Reshmail wote
waliogopa wakiamini alikuwa mshirikina .
Eve hakukubaliana hata
kwa mbali na shutuma hizo kwani alimwamini sana Reshmail hivyo aliendelea kuwa
pale hospitalini pamoja na mchumba wake kumuuguza Reshmail ambaye alitoka siku
tatu baadaye.
?baba mimi nitaenda na Eve kwake nitakaa siku
tano ndio nitakuja huko? Reshmail alimpa taarifa hiyo baba yake naye hakupinga
kwani amani aliyokuwa nayo Resh akiwa na Eve ilikuwa kubwa mno hali iliyowapa
faraja hata wazazi wake hivyo walimruhusu bila kusita.
Siku
hiyohiyo walipanda ndege kwa gharama za mchumba wa Eveline aitwaye Benjamin
Simon,kuelekea Iringa ambapo Eve alikuwa amepata ajira katika benki ya N.B.C
tawi la hapo.
Maisha yao yalikuwa mazuri sana kwani Benny
alikuwa mwalimu wa shule ya sekondari hivyo katika majukumu waliweza kusaidiana
na upendo wa dhati kati yao ulipendezesha zaidi nyumba yao.Reshmail alivutiwa
sana na maisha hayo na kumkumbuka sana Adam wake ?laiti angekuwepo tungeishi
hivi siku moja ? alijiwazia Reshmail wakati akiwaangalia Eve na Benny wakiwa
kwenye kochi wamebebana kwa furaha huku wakitaniana
Ilikuwa
jioni moja Reshmail na Eve wakiwa katika mizunguko ya hapa na pale mizunguko
ambayo kwa namna moja au nyingine iliibua ghafla safari ya kuingia
sokoni,waliingia hapo kununua matunda matunda,zilikuwa zimepita siku tano na
tofauti na alivyowahaidi wazazi wake hata hakuwa amefikiria kurudi Dar maisha ya
Iringa yalikuwa yamempendeza sana .
?Eveline ona eveline jamani
angalia kale katoto!!!? Reshmail alimgusagusa begani Eveline huku akimwonyesha
kikundi fulani cha watoto pale sokoni
?wewe achana hao
machokoraa walionikwapua pochi langu sina hamu nao hata kidogo,kisimu changu cha
mchina na shilingi elfu thelathini zikapotelea hewani looh!! Wabaya hao?
aliongea kwa hasira Eve huku akisitisha zoezi la kula chungwa aliliokuwa
anafanya kwa wakati ule.
?mh!! Eve jamani achaga uongo yaani
katoto kama kale jamani hebu kaone kale kadogo ?Reshmail alizidi kusisitiza
lakini Eve alionyesha bado ana uoga na uchungu moyoni wa kuibiwa vitu vyake na
watoto aliowaita machokoraa
?Reshmail shauri zako vitakuliza
hivyo we endelea kusema ni vitoto???..mh!! Resh lakini kale kadogo kazuri kweli?
aliongea Eve alipokaona kale katoto ambako Reshmail alisisitiza
sana.
?toto zuri jamboo!!?
?sijambo shkamoo!!?
kalijibu katoto kale kwa uchangamfu sana baada ya Reshmail na Eve kukasogelea na
kukasalimia.
?marahaba mtoto mzuri mbona upo hapa! Mwenyewe au
hawa ni kaka zako?? Resh alimuuliza
?a a sio kaka zangu mi
namsubiri mama ameondoka na watu wameenda huko amesema anarudi nimsubiri?
alijibu tena kwa sauti ya kitotototo
?umekula??? aliuliza
Eve.
?looh!! Eve hujaacha tu maswali yako ya kichoyo ya
uchagani kwenu mh! Unataka aseme amekula ili umnyime au ?? Reshmail alimshushua
Eve kiutani
?mh! Limeniganda shoga,una mashushu wewe!!? alijibu
Eve kiaibuaibu huku akimpa yule mtoto chungwa lililokwisha menywa
tayari.
?mama anarudi saa ngapi??? Reshmail alimuuliza yule
mtoto tena
?sijui nimemsubiri hata hajaja amenipa chai tu akaondoka na
wale wanaume wawili? alijieleza vizuri motto yule
?mh!! Mjini
mjini tu katoto kanajieleza utadhani mtu mzima dah!? Eve alimnon?goneza
Reshmail
?haya twende ukale eti motto mzuri!? Reshmail
alimwambia yule motto naye akakubali kwa ishara ya kichwa,akiwa pekupeku
akafuatana na Reshmail hadi kwenye mgahawa ulioandikwa ?MAMA FRED MGAHAWA?
uliokuwa pembeni kidogo ya soko kuu la Iringa.
?utamsalimia
mama eeh!!? baada ya kumnunulia chakula walilipa na
kumuaga
?haya mamdogo!? alijibu yule
mtoto
?unaitwa nani vile?Eve
akamuuliza
?naitwa Christian motto wa mama Bite? alijibu na
wote kwenye mgahawa wakacheka
Kuifananisha na picha ya
Adam, dimplez za yule mtoto zilimfananisha kabisa na Adam, achilia mbali rangi
yake ya maji ya kunde na ucheshi wake.
"Eve hapana,mbona kesho
naenda kumtafuta Christian ili nimjue baba yake anavyofanana,haiwezekani
kufanana kwa kiasi hchi hapana "Aliongea Resh huku akiifunika album ile
.
Eve alikubaliana naye na siku iliyofuata majira ya saa
nne,walikuwa katika hoteli ya yule mama ambapo walimwacha
Christian.
"Nyie watoto ni kesi gani hyo mmetaka kuniachia
jana" mama mnene kiasi mmiliki wa mgahawa wa Mama Fred aliwapokea kwa maneno
hayo makali huku akifunga kanga yake vizuri kiunoni.
Resh na
Eve hawakuwa na jibu la kutoa walidhani amewafananisha
labda
"Mama ni nini tena,mbona sisi...." alijaribu kujieleza
Eve huku akiishiwa maneno ya kujieleza.
"Mmenitekelezea mtoto
hapa anaanza kunililia hapa usiku he! jamani mnataka mniuwe kwa presha mkurya wa
watu mie" aliongea kwa ghadhabu na mshangao mkubwa sana yule
mama.
"Mama sisi tumempata hapo sokoni,ndio kumleta hapa kwako
kwa ajili ya kupata chakula tu mama yangu" Reshmail alinyanyua mdomo wake na
kuzungumza kwa sauti iliyojaa mshangao pia.
"He! mauzauza gani
haya jamani,mi nimempeleka pale kituo cha polisi usiku uleule
ndugu
Baridi kali ya Mbeya ilikuwa imemkataa motto wa
Bite (Christian) kwa hali hiyo alipotimiza miaka miwili waliondoka na kurudi
tena Iringa ambapo Bite alitaka kukaa kidogo halafu aende Mwanza kuweka makazi
mapya huko.
Jambo la kushangaza licha ya baridi ya Iringa hali
ya Christian ilianza kuwa njema kama awali jambo lililosababisha Bite aendelee
kukaa katika mkoa huo.
Hadi anatimiza miaka mine hali yake
kiafya ilikuwa njema sana na tayari Bite alikuwa amesahau suala la kwenda
Mwanza. Akaanzisha genge la kuuza uji na karanga mida ya jioni na mihogo ya
kukaanga majira ya asubuhi.
Ilikuwa biashara ndogo lakini
iliyomuingizia kipato kizuri tofauti na matarajio yake.aliweza kupanga nyumba ya
chumba kimoja na sebule aliyoishi na mwanae kwa furaha sana tu bila masumbufu
yoyote hadi siku hiyo asubuhi alipokuwa anauza mihogo yake ambapo wanaume wawili
ambao sura zao hazikuwa ngeni machoni pake walipofika eneo la biashara
yake.Aliwapokea kwa furaha sana na bashasha kama wateja wengine aliozoeana
nao.
?Bite tukuone pembeni kidogo samahani lakini? wawili wale
walimvuta pembeni Bite
?mh! Mikopo asubuhi asubuhi hamna
kwakweli mtadhalilisha hizo suti zenu? aliongea Bite kwa utani huku akiwafata
walipo wawili hao
?funga biashara tunaondoka na ukithubutu
kupiga kelele au kukimbia nasambaratisha ubongo wako nadhani hujawahi kufikiria
kifo cha namna hiyo,hivyo basi fanya kama unavyoagizwa? aliambiwa Bite na wale
wanaume huku mmoja akifunua koti lake jeusi la suti na kumwonyesha Bite kitu
ambacho hakujiuliza mara mbili mbili kuwa ile ilikuwa ni
Bunduki,
Kwa kuutambua uoga alioupata Bite,yule mwenye bunduki
alimbandika kitu mfano wa kishikizo cha nguo na kumwambia ?hiyo ni sound
recorder nenda ukawaambie wateja wako sisi ni ndugu zako tumekuletea taarifa za
msiba nitakuwa nakusikiliza hapa, ole wako nasema ole wako usifuate maelekezo?
alipewa masharti hayo ya uongo Bite ambaye laiti isingekuwa pensi yake ya jinsi
ambayo huwa anavaa kwa ndani ili kuhifadhia pesa zake za mauzo basi mkojo
uliopenya bila yeye kujua ungemwagika palepale hadharani na wala asingepatwa ma
aibu yoyote ile.
Kama alivyoagizwa aliwaeleza wateja wake
wawili waliokuwa wanamalizia kuitafuna mihogo waliyokuwa wameinunua,wakampa pole
za dhati .
jasho lilikuwa linamtoka alitamani kutumia ishara
kuwaambia kwamba yupo katika hatari lakini alipowazia mdomo wa bunduki alikaa
kimya kabisa,bila kificho Bite aliiogopa sana bunduki na hakupenda kumwacha
Christian katika umri ule.
Tayari akili ilisharudi nyuma
akatambua hasa,hao watu alikutana nao wapi,walikuwa ni baadhi ya wafanyakazi
katika ile ngome aliyekaa miaka miwili na ni hao waliomleta Adam pale
ngomeni
?nimekwisha mimi Beatrice? alijiwazia Bite huku
akitetemeka.
Baada ya kuifunga biashara yake aliwafuata akiwa
na mwanae amemshikilia mkono.
?nadhani unajua hatuhitaji
mtoto!!! Tunakuhitaji wewe tena sasa hivi? aligombezwa Bite na bila kujijua
akajikuta akimwacha mwanae pale
?Christian narudi sawa
nisubirie pale sokoni sawa mwanangu!
?haya mama alijibu
Christian kwa furaha kwani alijua amepata fursa kubwa na ya kipekee kwenda
kucheza na watoto wenzake pale mtaani
?ulidhani unaweza
kutuzidi ujanja sisi,umepotea sisi hatupimiki hata kidogo umeumia tena umeumia
sana aliambiwa Bite na wale wanaume wakiwa kwenye gari kuelekea kwenye gari
kuelekea kule katika ngome jambo hilo Bite hakulitamani hata kidogo,japo
alimpata Christian kwa bahati mbaya lakini alikuwa akimpenda sana kutoka moyoni
na hakuwa tayari kutenganishwa naye kwa namna yoyote
ile.
Alijiuliza maswali mengi sana ni nani atakayempa chakula
mwanaye siku hiyo na nyingine zitakazoendelea wakati yeye hayupo,michezo ya
kukimbizana aliyoipenda Chriss pia ilimtia hofu Bite na kuhisi huenda mwanae
anaweza kupoteza uhai wake kwa kugongwa na gari.
Funda la
hasira lilimkaba kooni alitamani kufanya lolote lile wakati huo lile jambo liwe
ndoto kwake, machozi yaliyotoka ndio yaliyeyusha lile fundo japo kidogo,hasira
kali ilikuwa imemkaba Bite aliyekuwa amekaa siti ya nyuma na jamaa mwenye
Bunduki katika koti lake lakini maskini hakuwa na la kufanya hadi gari
lilipoingia ndani ya ngome ile
* * * *
*
Macho ya Reshmail yalitawaliwa na taswira ya yule mtoto
Christian, zilikuwa ni siku nyingi zimepita tangu afungue album yake kumwangalia
mpenzi wake (Adam) aliyeaminika kuwa tayari ni marehemu.Ni katika usiku huu
alipokuwa akipitia album ya Eveline ndipo tena anakutana na picha ya Adam ambayo
yeye (Adam) alimpa Eveline walipoenda
Mwanza.
?Eveline,Eveline,Eve???.huyu hapa ni
nani????
?we umechanganyikiwa tena eti hebu acha mambo yake ya
ajabu huyu Adam? Alijibu Eve kwa uoga.
? na tuliyemwona leo
kule sokoni ni nani??? aliuliza Reshmail
?we Reshmail jamani
wanafanana Mungu wangu mbona wamefana hivyo lakini eeh!! Eve alijikuta picha ya
mtoto Christian ikiumbika kichwani mwake na Zangu kwa sababu nimekaa naye hadi
saa nne tumemsubiri huyo mama yake aje wapi!! Nikaona isiwe shari ngoja
nimpeleke polisi penye usalama kuepuka balaa kumbe na nyie hamjui ni wa nani
he!!? alitoa maelezo hayo yule mama na kueleweka vyema kwa Reshmail na
Eveline.
?hicho kituo cha polisi umesema kipo wapi?? aliuliza
Eve
?kile pale kinaonekana hata kwa hapa,lile jingo la bluu
nyuma yake? alielekeza yule mama
Ndani ya dakika tano tayari Reshmail na
shoga yake walikuwa mbele ya mapokezi ya kituo cha polisi Iringa mjini, na
walikuwa kwenye foleni wakisubiri zamu yao ya kuhudumiwa
ifike.
?nyie ni ndugu zake? Au mmoja wenu ndio mama
yake??
?hapana sisi si ndugu zake ila???aliishia njiani katika
maongezi yake Resh baada ya kukatishwa na yule askari ?ila nini? Yaani nyie
wanawake wa siku hizi suala la kujali watoto wenu hamtaki kabisa kulisikia
mnachojali ni urembo tu wa sura zenu?
?jamani sio kwamba kuna
ndugu yake hapa kati yetu ila sisi tumemkuta jana kule sokoni ndio tumemnunulia
chakula halafu tukajiondokea zetu,leo hii ndio tunapita pale kwa mama Fred yule
mwenye mgahawa yeye ndiye ametupatia taarifa hiyo tukaona sio vibaya nasi
tukifika kumwona huyo motto? aliongea Eve aliyeonekana kutokuwa na hofu na kituo
cha polisi lakini Reshmail alikuwa ana uoga kwa mbali kama vile anatuhumiwa kwa
lolote lile.
?haya yupo tumemuhifadhi na tumepeleka taarifa
kwenye vyommbo vya habari wataanza kutangaza kama mama yake bahati mbaya haya
atakuja kumchukua na kama amemtelekeza akajiandae kwenda kuishi kwa watoto
yatima sisi hatuna uwezo wa kuhifadhi watu hapa zaidi ya mahabusu? alijieleza
askari yule huku akijipepea joto kwa kutumia kofia yake
iliyochakaa
Majuma mawili yalipita bila mama wala
ndugu wa motto kupatikana licha ya kituo cha redio maarufu mjini iringa cha Ebon
fm kutangaza kila siku bila kukoma
?Eve naenda kumchukua yule
motto nafsi yangu inanishauri hivyo na ni lazima nifate ambacho nafsi yangu
inaniamuru? Reshmail alimwambia Eve siku moja wakiwa wamekaa sebuleni
wakiangalia habari katika luninga.Eve alikuwa amejenga tabia ya kutobishana na
rafki yake huyo kwani furaha yake ilikuwa ni kumwona Reshmail akiwa na furaha
tele
?lakini Resh,mama yake si atamtafuta
ssana???
?Eve yaani imetangazwa hivyo redioni na hajajitokeza
leo hii mie tu kumchukua ndipo ajitokeze? Looh! Acha nae ahangaike kidogo?
alijibu Reshmail kwa jeuri
?mh! Haya sikuwezi mwanasheria
wangu?
Polisi hapakuwa na usumbufu ni wazi kwamba walikuwa
wamechoshwa na matukio ya watoto kutelekezwa na wazazi wao pasipo sababu zilizo
wazi,hivyo kitendo cha Resmail kuamua kumchukua Christian ilikuwa ahueni
kwao.aliandiokishwa maelezo mafupi tu kabla ya kuruhusiwa kondoka na mtoto
ambaye alikuwa dhaifu tayari kutokana na lishe duni na upweke wa kutomuona mama
yake kwa siku hizo zote.
Reshmail alikuwa ameyafurahia sana
maisha ya Iringa,kampani kubwa kutoka Eveline na mchumba wake ilibeba nusu ya
furaha yake huku nusu nyingine ikikamilishwa na uwepo wa Christian mikononi
mwake,mara kwa mara alipenda kuwa naye karibu huku akimwita mume wako jambo
lililompa faraja kubwa moyoni
?Eve jamani nitakumiss kipenzi
changu lakini nitarudi tena asanteni sana kwa ukarimu wenu mlionionyesha tangu
mwanzo nimeishi kwa furaha kubwa sana hapa? Reshmail aliyazungumza hayo
alipokuwa anawaaga Eve na Benny usiku ambapo kesho yake alitegemea kurejea
Dar-es-salaam akiwa ameandamana na Christian mtoto aliyempata katika mazingira
ya kutatanisha
Kwa Christian safari ya kutoka Iringa kwenda Dar ilikuwa
safari yake ya kwanza ndefu zaidi kuwahi kusafiri
Siku
iloyofuata wawili hawa walikuwa ndani ya basi la ?budget? litokalo Mbeya kwenda
Dar likipitia Iringa.
?Mama alisema baba yupo pale kwenye ile
nyumba, tushuke nikamsalimie!? Chriss aliongea hayo huku akielekezea kidole
chake kwenye jingo lililoonekana kwa mbali mno kutokea pale barabarani na
hapakuwa na dalili ya kuishi mtu pale hivyo Reshmail akachukulia kuwa ni akili
ya utoto imemtuma Chriss kuzungumza akaamua kupuuzia
?chriss
alikwambia nani we muongo!!?
?alinambia mama siku moja hivi
tulipita hapa ,halafu mama alinikataza kusema uongo ni dhambi? alijieleza
Christian haraka haraka
?mh! Haya tutakiuja siku nyingine sawa
mfalme wangu? Reshmail alimjibu Chriss ili kumlidhisha kwa aliyokuwa
anasema
** ** ** **
Nyumba tulivu
kabisa ya mh.Manyama ililipuka kwa furaha kwa kurejea kwa Reshmail akiwa mwenye
furaha tele ?umetuletea na mjukuu!!? alitania mama Resh.
?mtoto
wa Eve huyu anamwita mama mdogo? Resh naye akadanganya
?kazuri
kweli kama??????? alisita kumalizia baba yake
?ni kama Adam
baba usiogope kufananisha wamefanana kweli? alimtoa baba yake wasiwasi huku
akimkumbatia baba yake kasha mama yake.
?mh!! Tulikuwa wapweke
kweli jamani dada? msaidizi wa kazi za ndani aliyeitwa Fatuma alimwambia
Reshmail huku akimkumbatia na kumbusu shavuni
?na huyo mtoto
kama mwanao vile hebu kaone? aliendelea Fatuma
?sio kama wa
kwangu ila ni wa kwangu humwoni alivyonifanana?? alijibu kimzaha na wote
wakacheka kwa pamoja
** ***** *****
Hali ya
sintofahamu iliwakumba wale wafanyakazi wa lile jumba (ngomeni) alipokuwa
anatunzwa Adam. Mkuu wa ngome hiyo bwana Lwebe alikuwa na ghadhabu kubwa
sana,kila mbua alikuwa na ghadhabu kubwa sana,kila kitu kilikuwa shaghala
baghala kila mara aliongea kwenye simu hukuakitoa vitisho vikali sana na hata
kutishia kuua.
Wafanyakazi hawakumwelewa lolote walizitambua
hasira za bosi wao huyo ambaye mara chache anazokuwa katika hali kama hiyo
humalizia hasira zake kwa kutoa roho ya mtu
?mlete Adam hapa
mara moja !!? aliamrisha huku akijikuna ndevu zake kwa kutumia mdomo wa bunduki
aliyokuwa nayo
?maskini Adam sijui amekosa nini? alijiuliza
aliyekuwa anaenda kumwita. Bila wasiwasi wowote Adam akamfikia Lwebe D kwa
ishara ya mkono akamwamrisha kumfuata,pamoja na mabaunsa wawili waliotinga suti
nyeusi .
lwebe hakuongea neno lolote hadi walipofika kwa
nje,tayari kigiza cha saa mbili kilikuwa kimetawala
?mlete na yule
mwingine wa nyumba ya chini? alitoa amri nyingine tena baada ya tano walioagizwa
wakarejea na mtu mwingine
?we kinyamkera una bahati sana
aliyekuleta hapa amesema haujasambaza taarifa zozote mbaya laiti kama
ungethubutu ningeiondoa shingo yako sasa hivi.
Nakuacha uende
tena lakini tambua mtandao wangu upo popote katika nchi hii sasa ole wako
uthubutu kunyanyua mdomo wako kutangaza ujinga? aliambiwa yule binti aliyeletwa
pale huku akionyeshwa njia ya kutokea
?we kidume kwa jeuri ya
bosi wako kujaribu kunidhurumu pesa yangu wakati wewe unakula na kulala bure
hapa;lazima nimwonyeshe mimi ni nani na ni wewe utakayeumia? aliongea Lwebe huku
akipuliza moshi wa sigara
hewani.
**********
Ilikuwa ni mwezi mmoja
tangu Bite arejeshwe kwenye ile ngome lakini katika chumba kingine,hakuwa
msaidizi wa kazi tena bali mtuhumiwa na hakupata fursa ya kuonana na Adam hata
siku moja .
siku alipotolewa nje usiku na kwa mahesabu ya miaka
mitano ambayo Adam angekaa pale machale yalimcheza,alivyopewa uhuru wa kuondoka
hakwenda mbali sana alifika eneo moja kwenye mtaro na kuanza kusubiria ni nini
kitatokea japo hakusikia vizuri maneno lakini alisubiri hata
vitendo
**********
Mkataba
wa miaka mitano alioandikishana Bi.gaudensia na Lwebe wa Adam kuhifadhiwa pale
ulikuwa umeisha tayari na miezi mitatu zaidi ilikuwa imepita,suala hilo la
kuchelewesha pesa lilimkera sana Lwebe na pia ahadi za uongo kutoka kwa
Gaudencia zilichochea sana hasira za Lwebe kufikia hatua ya kuamua kuzipooza kwa
huyo Adam aliyehifadhiwa hapo.
Ni usiku huo alipoamua kwa mkono
wake mwenyewe Adam duniani kama kisasi kwa Bi.Gaudensia
?paa!!
Paa!!? mlio mkali wa risasi ulisikika na kumzindua Bite ambaye alikuwa amepitiwa
na usingizi pale kwenye mtalo, kidogo apige kelele lakini viganja vya mkono wake
vikawahi kuuziba haraka sana. Hakusikia hata chembe ya kilio na baada ya dakika
kama saba akasikia milango imefungwa
Kwa ujasiri na tahadhari
kubwa Bite akajisogeza hadi karibu kabisa na eneo ambalo aliamini hakika ndipo
mlio wa risasi umetokea huku kichwani kwake akiwa ana jibu la ?nimesahau saa
yangu? iwapo atakutana au kushtukiwa na mlinzi, kwa hofu alizurura katika lile
eneo dakika tatu bila kuona chochoten?au wameingia nae ndani??? alijiuliza bila
kupata jibu
?koh!! Koh!! Alishtuliwa na sauti ya kikohozi nyuma
yake, mawazo yake alidhania ni mlinzi eneo lile lakini alipogeukz hakuwa mlinzi
tena ni mwili wa binadamu ukiwa chini,hakutambua mara moja yule ni nani hadi
macho yake yalipolizoea giza la pale ?Adam!!!!!?
?we ni nani???
alijibiwa kwa sauti ya chini sana iliyokuwa inaunguruma kama mnyama
anayechinjwa
?Bite mimi jamani Adam?
?ondoka
watakuua hao Bite ondoka niache mi nife hapa? alijibu
Adam
?hapana Adam usife,usife Adam twende tukamtafute mwanetu
Chrstian anatamani sana kukuona,usife Adam tafadhali? Bite
alibembeleza
**********
Risasi
mbili zilizopenya katika paja lake la kulia zilikuwa zimemsababishia Adam kuvuja
sana damu na mbele yake alichokitarajia ni kifo hakuna kingine lakini maneno ya
Bite.
Nguvu zilirejea upya kabisa tena kwa kasi?Bite
ulijifungua, mtoto wangu yuko wapi? Ni wa kiume au wa kike?? alihoji maswali
mfululizo Adam huku akijitutumua kusimama kwa nguvu alizokuwa
amezipata
?ni stori ndefu na hapa sio mahali pake
tuondoke tafadhali jitahidi kuna hatari kubwa kama unampenda mwanao jitahidi
tuondoke? aliongea Bite huku akiuweka mkono wa Adam katika bega lake na kuanza
kumkongoja kutoka eneo lile huku (Adam) akitumia mguu mmoja na ule uliojeruhiwa
ukiwa juu juu.
Kutoka pale walipokuwa hadi barabarani haukuwa
umbali mrefu sana na walifanikiwa kufika,kwa giza nene lililokuwepo hawakuweza
kuonekana na mtu yeyote,nguvu zilikuwa zinamwishia Adam kutokana na kuvuja damu
lakini alijikaza kijasiri sana na kuendelea
mbele
********* *******
*******
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment