Search This Blog

Friday, November 18, 2022

MUHANGA WA MAPENZI - 2

 






Simulizi : Muhanga Wa Mapenzi 
Sehemu Ya Pili (2)




*****

Usiku ulikuwa ni mrefu kwa Athuman alikosa kabisa usingizi kwa mawazo, alijiona naonewa bila kosa lolote. Alijua ni yote sababu ya jeuri ya fedha, Alijiuliza kuhusu ujio wa yule binti anayedai ananipenda, ni kweli alikuwa na mapenzi ya kweli au alitumwa na baba yake kumuingia matatizoni ili wanifunge.

Hakujua kosa lake nini alilowakosea hata hata yule binti mwenyewe hakuwa amemfanya kitu chochote cha kumfanya afikie hatua ile. Alikumbuka hata siku ya kwanza alipokutana naye hakumjibu lolote pamoja na kukashifiwa.

Akiwa katikati ya wimbi la mawazo alishtuliwa na sauti ikimwita.

“Athuman ndiye nani?” Ilikuwa sauti ya askari, kabla ya kuitika kwanza Athuman alijiuliza ni nani anayemuita au ndiyo kwenye mahojiano mengine na mkuu wa polisi.

“Nipo afande,” Athuman aliitikiahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

”Unaitwa nje.”

Mlango ulifunguliwa na Athuman alitoka nje ili akamuone anayeniita. Alitoka hadi nje ya jengo, ilikuwa tofauti na wengi huishia kaunta na kuzungumza na wageni wao. Alijiuliza nani aliyekuwa akimwita.

Nilipotoka nje alishtuka kumkuta ni Rachel, bila aibu mtoto wa kike alimkimbilia na kumkumbatia. Kitu kile kilichowashangaza askari wote waliokuwa pale kituoni.

” Pole sana mpenzi, vyote ni vizingiti vya penzi letu, lakini tutavivuka, “ Rachel alisema akiwa bado amemkumbatia. Athuman hakujibu kitu alitulia tuli ili ajue nini nitachoendelea.

“Athuman mpenzi tunaweza kwenda, nimeisha kuwekea dhamana.”

Alisema Rachel huku akijitoa kifuani na kumshika mkono, waliongozana hadi katika BMW aliyokuja nao Rachel alimfungulia mlango kwa heshima. Athuman aliingia kisha Rachel naye alizunguka upande wa pili na kuingia.

Baada ya kila mmoja kufunga mkanda safari ilianza ya kumrudisha nyumbani.

Njiani Rachel alimpa pole nyingi Athuman na kumuomba msamaha kwa yote yaliyonitokea.

“Mpenzi pole sana, lakini usijali.”

“Asante Rachel,” Athuman alijibu kwa upole.

“Athuman mapenzi yangu ni mazito kwako nakuahidi kukulinda kwa nguvu zangu zote,” Rachel alijisahau kama anaendesha gari na kuanza kunitomasa Athuman nusra wapate ajali.

Wakiwa njiani Rachel aliliona gari la baba yake likija kwa mbele alimuamulisha Athuman alale chini.

“Athuman lala chini baba huyo!”

Athuman aliona bwawa limeingia luba, moyo ulimpasuka pa! alijua shughuli imeiva . Aliamini kama Baba Rachel akiniona tena yupo na mwanaye angemfanya kitu kibaya hata kumpiga risasi.

Alitii amri kwa kufungua mkanda haraka na kuinama chini mara Rachel aliaimamisha gari ili kuzumngumza baba yake aliyemuwashia taa asimame.

“Vipi unatoka wapi saa hizi?” Ilikuwa sauti ya mzee Mulisa.

“ Natoka kwa shoga yangu Joyce,” Rachel alijibu kwa kujiamini.

“Mbona hukuaga, mama yako alikuwa anakutafuta wahi nyumbani… Pia nilisahau kamwambie leo naweza kuchelewa kurudi.”

“Baba naye yaani umeshindwa kumpigia mama simu?” Rachel alimwambia baba yake.

“Nitafanya hivyo ila na wewe fikisha ujumbe.”

“Sawa baba.”

Rachel aliagana na baba yake na kukanyaga mafuta.

“Nyanyuka mpenzi, pole kwa usumbufu pia naomba univumilie kwa yote yaliyokutokea au yatakayokutokea.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nimekuelewa mpenzi.”

Athuman muda wote alijikuta akijiuliza maswali mengi juu ya yote yaliyomtokea na jinsi Rachel alivyomtoa polisi na hatima ya penzi lao ambalo kwake aliiona hatari mbele yake.

Rachel alisimamisha gari mbele ya nyumba anayoishi Athuman, waliteremka pamoja na kuingia ndani. Baada ya muda Rachel aliniaga na kuondoka na kumuhaidi atampitia jioni ili waende sehemu tulivu kwa maongezi zaidi. Athuman alishindwa kumkatalia alimkubalia.

******

Kengele ya mlangoni ilimuashilia Athuman nje kuna mtu, alisogea hadi mlangoni na kufungua hakuwa mwingine ila Rachel alikuwa amependeza sana . Kwa vile naye alikuwa tayari amejiandaa waliongozana hadi katika gari moja la kifahari la wazi na kuelekea pembeni ya bahari ya Hindi.

Athuman na Rachel walielekea ufukweni, walipofika hawakutelemka haraka ndani ya gari. Upepo mwanana wa bahari uliwalipepea, Rachel alifungua kifuko kidogo na kutoa soda mbili za kopo pamoja na sambusa ambazo ambazo alizinunua kwa ajili ya kutafuna wakati wa maongezi.





Rachel, pamoja wa ugeni kwa Athuman hakuonyesha woga wowote kama ilikuwa siku yao ya kwanza kuwa karibu na kwa nafasi kama ile. Alipitishia mkono shingoni huku ukitetemeka ikionesha hajiamini Athuman alitulia tuli alimwacha afanye atakacho.

“Athuman vipi, mbona huoneshi kama tupo pamoja au bado unawaza ya baba?” Rachel alimuuliza Athuman huku akimtazama usoni.

“Nikweli Rachel hata kama nitaonyesha mapenzi juu yako ni kazi bure,” Athuman alijibu kwa sauti ya upole.

“Aah! Kwanini unasema hivyo ?“Rachel aliuliza akionesha ameshtuka sana kutokana na kauli ya Athuman.

“Rachel wewe ni mtoto wa tajiri hivyo sina ubavu wa kushindana na baba yako.”

“Ni kweli usemayo lakini penzi halifundishwi shule wala toka kwa wazazi , ni upendo unaotoka ndani ya moyo wa watu wawili walio shibana. Hivyo msimamo wetu ndio siraha pekee ya kuwafanya wazee wangu kulikubali matakwa yetu, nami nipo radhi kwa hali na mali kuona penzi letu linadumu milele,” Rachel alisema huku machozi yakimtoka.

“Usemayo ni kweli, kumbuka baba yako ana uwezo wa kunifanya chochote ili kuhakikisha ananishikisha adabu. “

“ Athuman mpenzi, kumbuka mimi ni mtoto wa tajiri ambaye napata kila kitu ninachotaka kwa wazazi wangu. Na wazazi wangu wananipenda sana vyote wanaweza kunipa sio mapenzi,” Rachel alisema huku akimtazama Athumani kwa jicho la huruma.

“Rachel hakuna kinachokosekana kwa wazazi hata mapenzi ukifika muda wake utayapata.”

“Penzi nilipate vipi kwa wazazi wangu, sasa Athuman naona tumechokana kwa muda mfupi,” jibu la Athuman lilimkwaza Rachel.

“ Samahani Rachel naona hujanielewa vizuri, sina maana unayofikiria. Maana yangu kutapata mchumba ambaye atapokelewa na wazazi wako bila vikwazo,” Athuman alitetea hoja yake.

“Aah! Lakini anaweza kuwa sio chaguo langu siku zote ndege hutua mti aupendao, nami tayari nilishatua kwako.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Maneno mazito yale yalimfanya Athuman akose cha kuzungumza na kubakia akimkazia macho Rachel ambaye macho yake yataka ujabari kumtazama yalijaa majaribu matupu.

“Athuman japo mimi ni mtoto wa tajiri lakini nipo kizuizini na mkombozi wangu ni wewe, nimeukabidhi moyo wangu mikononi mwako tafadhari nipokee nipo chini ya miguu yako.”

Rache aliliomba penzi la Athuman kwa sauti tamu ya kinanda

ya kubembeleza huku machozi yakiweka michirizi juu ya mashavu.

“Rachel siwezi toa jibu haraka kutokana na kichwa changu kutingwa na mambo mengi, nipe muda,” Athuman alijibu kwa sauti ya upole.

“Jamani Athuman, kwanini usiseme tu upo tayari kunipokea ili niwe wako. Kama mimi nilivyojitolea juu yako?”

Hali aliyokuwa nayo Rachel ilimtia huzuni Athuman, kama kawaida yake machozi yalizidi kumtoka.

“Rachel mpenzi nami nipo radhi kukupokea ili uwe wangu,” Athuman alijikuta akisema bila kutambua nazungumza nini.

“Waaaooo! Kweli Athuman?” Rachel alimkumbatia kwa furaha na kujikuta wakigusanisha midomo yao katika mapenzi mazito.

Walifungua vinywaji vyao huku wakigonganisha kopo zao, walikunywa huku wakinyweshana na kulishana keki kwa mdomo kama ndege na kinda lake. Rachel aliniona ni kiumbe kilichozaliwa upya katika ulimwengu wa wapendanao, kila mmoja alilifurahia penzi lile jipya.



*****

Mzee John Mulisa na mkewe mama Rachel wakiwa sebuleni waliendelea na mazungumzo yao, baba Rachel alimuuliza mkewe:

“Mama Rachel huyu mtoto mbona simuoni amekwenda wapi?”

“Amekwenda kwa shoga yake Joyce,” Mama Rachel alijibu bila wasiwasi wowote.

“Mbona leo amechelewa sana kurudi?”

“Sijui nini kimemchelewesha, ningekuwa na wasiwasi kama yule mwanarahamu angekuwa nje... Tena kweli baba Rachel umefikia wapi na yule fisadi?”

“Kwa kweli leo nilikuwa bize lakini mwache apate adabu, wiki ijayo lazima afikishwe mahakamani na hukumu siku hiyo hiyo tena ngoja niwasiliane na mkuu wa kituo cha polisi nijue amefikia wapi,” Mzee Mulisa alichikua simu ya mkononi na kubonyeza namba za kituo cha polisi, haikuita muda mrefu simu ilipokewa.

“Haloo kituo cha polisi makao makuu hapa, tukusaidie nini?”

“ Mulisa naongea.”

“Ahaa! Mzee shikamoo kumbe wewe, “ mkuu wa kituo alijibu kwa adabu.

“Ndiyo mimi, vipi ile shughuli mmefikia wapi?”

“Mzee ile shughuli tuliona haina umuhimu wowote kwa hiyo hatukuishughulikia.”

“Kwa nini useme hivyo?” Mzee Mulisa aliuliza.

“Tutafanyaje wakati mtu mwenyewe yupo nje.”

“Yupo nje? Mbona sikuelewi ina maana mmekaidi amri yangu?” Aliuliza kwa ukali.

“Sio sisi mzee ni mwanao ndiyo kaja kumtoa leo asubuhi,” mkuu wa kituo alijitetea.

“Kwa nini mmemruhusu amtoe?” Alizidi kupamba moto.

“Sio sisi ila ni wewe mzee ulishasema tusiikatalie lolote familia yako hata mbwa wako.”

Kauli ile ilimfanya Mzee Mulisa ashushe pumzi ndefu kama mtu aliyetua mzigo mzito na kumshtua mkewe aliyekuwa akifuatilia mazungumzo yale.

“Mume wangu mbona hivyo?”







“Tunafanya kazi ya bure kubeba maji kwenye gunia.”

“Kwa nini mume wangu?”

“Yaani Rachel anavunja amri yangu?”

“Kafanya nini?”

“Amemtoa yule kijana, leo akirudi atanitambua na huyo kijana atajuta kuzaliwa,”Mzee Mulisa alisema kwa hasira.

“Basi inawezekana hata kwa huyo Joyce hakwenda yupo na huyo kijana, kuna umuhimu wa kupiga simu kwa kina Joyce ili kupata ukweli wa mambo.”

“Sawa,” Mzee Mulisa aliitikia kwa unyonge hata nguvu hakuwa nazo tena. Mama Rachel aliamua kupiga simu ili kupata ukweli. Baada ya simu kuita kwa muda ilipokelewa upande wa pili na mama Joyce.

“Haloo naomba kuzungumza na Joyce mimi mama Rachel.”

Baada ya muda Joyce alikuwa katika simu.

“Haloo mama shikamoo.”

“Marahaba mwanangu, eti Rachel leo amefika huko?”

Wakati huo Rachel alikuwa ndio kwanza anaingia sebuleni kwao, swali alilisikia kabla Joyce hajajibu kitu aliiwahi simu ya mama yake na kuikata.

“Rachel kwa nini uikata simu?”

“Simu ya nini wakati mimi mwenyewe nimekwisha ingia,” alijibu kwa kujiamini.

Mama yake alishindwa kuzungumza chochote na kumtazama mwanaye. Mzee Mulisa alishtuka pale kwenye kochi baada ya kupitiwa na usingizi. Alinyanyuka kwa hasira alimshika mwanaye na kumuuliza.

“Wewe mwana haramu kwa nini umemtoa yule shetani polisi? ”

“Lazima nimtoe kosa lake nini? Kama mwenye makosa ni mimi nifungeni mimi sio mtoto wa watu asiye na hatia, “ jibu lilikuwa kama kufuli katika mdomo wa Mzee Mulisa na kuzidi kumchosha zaidi baada ya kuyasema yale Rachel alikwenda chumbani kwake kulala na kuwaacha wazazi wake wakiwa vinywa wazi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mke wangu kuna umuhimu wa kumdhibiti yule kijana.”

“Kuna haja ya kufanya hivyo.”

***

Siku ya pili Rachel alikutana na Joyce shuleni, wakati wa mapumziko shoga yake alitaka kujua sababu ya mama yake kukata simu. Rachel alimpa stori kamili juu ya kufanikiwa kumpata Athuman.



“ Hongera shoga, mambo si hayo ulikuwa unaogopa nini, lakini ipo kazi kati yako na Mzee Mulisa.”

“Atatuliza boli tu,” Rachel alisema kwa kujiamini.

“Ehe! Tuachane na hayo vipi kuhusu pepa, maana imebakia wiki, sijui umejiandaa vipi?” Joyce alimuuliza shoga yake.

“Sio siri toka Athuman aingie akilini, sikupata tena muda wa kusoma zaidi ya kumuwaza yeye.”

“Sasa ndiyo itakuwaje?”

“Joyce mtihani wangu mkubwa maishani mwangu naamini ulikuwa kumpata Athuman, kwa vile nimefauru sina tena haja ya mtihani mwingine.”

“Ina maana hufanyi tena hata huo mtihani?” Joy alishtuka.

“Nitafanya kutimiza wajibu lakini sitegemei kwenda popote zaidi ya ndoa yangu na Athuman.”

“Shoga una makubwa, mara hii mipango ya ndoa?”

“Yote tuna kamilisha kesho tena shoga nitakualika ili ushuhudie tukivalishana pete ya uchumba lazima uwepo kupiga picha.”

Muda wa kutoka shule ilipotimu Toyota VX V8 ili simama mbele ya shule na kuwachukua Rachel na Joyce.

***

Athuman alijikuta katika kipindi kigumu cha kulikubali penzi na mtoto wa tajiri, wakati baba yake anawaka mithili ya moto wa tiper. Alijiuliza ni kweli akishilikiana na Rachel wataweza kuuzima moto wa mzee Mulisa mtu mwenye pesa kama mchanga. Alijikuta akipiga moyo konde na kuwa radhi kukabiliana na ushindani toka kwa mzee Muliza kutokana na mapenzi ya dhati Rachel aliyoonesha kwake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Vilevile alijua kwa kipindi kile Rachel angemsaidia kutatua matatizo yake kwa kumweleza matatizo yake ambayo yote yalitatuliwa na Rachel ambaye alimuahidi kumfanya aishi maisha ambayo kwake mwanzo aliona ni njozi.

*****

Kwa vile mtoto wao alikuwa karibu na kufanya mtihani wa mwisho wa kidato cha nne, Mzee Mulisa na mkewe walionelea lazima awekwe chini ya ulinzi mkali ili ajiandae vizuri na mtihani. Walimuhamisha chumba chake na kumuhamishia chumba cha self conteiner ili ashinde ndani akijisomea baada ya muda wa shule.

Pamoja na hatua waliyofikia ya kumdhibiti vile ili ajiandae na masomo hilo halikumfanya Rachel asimuwaze Athuman. Rachel aliwaomba wazazi wake awe karibu na Joyce ili wasaidiane kusoma, hawakumkatalia. Joyce aliombewa ruhusa kwa wazazi wake na kukubaliwa na kuhamia nyumbani kwao Rachel kwa kipindi kile cha maandalizi ya mtihani.



Wito ule ulimfanya Joyce ashangae jinsi Rachel alivyobadilika kuonesha mabadiliko ya maandalizi ya mtihani alijiuliza ni kweli Rachel ameamua kujikita kwenye masomo. Lakini kumbe ilikuwa tofauti, ilipotimu usiku Rachel hakuwa katika masomo zaidi ya kumpa shoga yake story za mapenzi hasa zaidi za Athuman. Ikawa mara aibusu picha kubwa ya Athuman ya passport size.

“Rachel bora niendoke zangu nyumbani sina muda wa story zaidi ya kujisomea,” Joy alishtuka na tabia za shoga yake.

“Joy usiwe hivyo shoga yangu unajua saa hizi nipo kizuizini nina hamu ya kumuuona mpenzi wangu Athuman.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Sasa mmi uliniitia nini, si bora ungeniacha nyumbani nijisomee mwenyewe,” Joy alimlalamikia Rachel.

“Joyce hiyo ilikuwa kuwafunga macho wazee, muda si mrefu nitatoka kwenda kwa Athuman,” Rachel alionekana kutojali chochote zaidi ya kuzama katika mapenzi kuliko masomo.

“Kwenda kwa Athuman! Usiku wote huu?” Joy alishtuka.

“Eeh, kipi cha ajabu.”

“Rachel usiku wote huu anafuata nini? Baba yako akija nitamjibu nini?”

“Hakuna mtu wa kuja muda huu wakilala wamelala”

“Kwanza utapitia wapi milango yote imefungwa?”

“Nitapitia dirishani.”

“Rachel mbona una makubwa! Utateremkaje toka hapa hadi chini?” Joy alizidi kumshangaa shoga yake.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog