Search This Blog

Friday, November 18, 2022

PAIN OF LOVE - 1

 






IMEANDIKWA NA : SADARI KISESA



*********************************************************************************



Simulizi : Pain Of Love

Sehemu Ya Kwanza (1)



UTANGULIZI....

Mapenzi ni nini?. Mapenzi si kitovu cha uzembe kinachouma mfano wa donda ndugu, kinachofukuta wakati wa joto. Mh, sidhani ninachojua kuwa katika mapenzi kuna upendo na usaliti. Katika upendo na usaliti mwanadamu yote anapitia. Upendo huleta chachu ya kupendana kati ya mwanaume na mwanamke. Usaliti huleta chachu ya kuchukiana kati ya mwanaume na mwanamke. Aisee, omba yasikukute wala asikuambie mtu kuhusu usaliti. Usaliti ni mbaya, lakini huwa binadamu tunakaza moyo ili mradi kuzitendea haki hisia zetu. Lakini mbona nazidi teseka sababu ya mapenzi?, kwani kuna mwingine anayeteseka katika mapenzi?. Loh, sidhani maana nikiangalia wenzangu wao naona mapenzi yameshamiri hadi naona wivu. Katika mapenzi kwanini iwe mimi wa kudumbukizwa kwenye dimbwi la moto na mkombozi wangu akizidi kufungulia bomba la petroli nizidi kuteketea bila huruma, ni lini nitakuwa na furaha kama wenzangu au mimi nimeandikiwa kulia kwa kusaga meno hadi mwisho wa uhai wangu katika mapenzi. Hebu...Coletha nipe nafasi nisiumie nizidi kupata furaha ya kudumu, usinifanyie ukatili huo Coletha. Mimi ni binadamu si mnyama ambaye anapigwa na silaha, mimi ni udongo muda wowote naweza kumong'onyoka kwa maji uyafunguliayo kwa kasi. Pia mimi ni mdhaifu kama yai ukinipasua moyo utaniachia maumivu, hebu...Coletha naomba rudisha moyo nyuma unionee huruma mwana wa mwenzio unipende nipate kuishi kama wengine. Coletha ukweli ni kwamba nitaona fahari sana kama utaweza kurejesha furaha yangu, Coletha jaribu kunipenda hata kidogo moyo wangu utulie. Kwanini hunielewi au kwako furaha kuona nadondosha chozi kwaajili yako. Coletha kwanini uruhusu niendelee kulia kwasababu yako?, na kwanini unazichezea hisia zangu kama Mpira wa kandanda unaochezwa na wachezaji uwanjani. Bora niwe kichwa ngumu leo nichukue maamuzi sahihi yatakayo tuliza mtima, huelewi?...yaani namaanisha sitaki tena kukupenda Coletha, sitaki tena kuumia moyo na sitaki tena kuteseka Coletha.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

SONGA NAYO...

Mathias ni kijana mchapakazi na mwenye upeo wa maisha, pia ni kijana anayejitegemea katika maisha yake. Amepanga chumba Mabibo Loyola na anajishughulisha na kazi ya kukodisha na kuuza CD. Ofisi yake ipo maeneo ya Kigogo Post, ofisi yake hiyo inamuingizia pesa na ina kivutio sana kwa wateja wa rika zote. Wadogo kwa wakubwa, vijana kwa wazee na wake kwa waume. Mathias hakuwa mvivu alipenda kuwahi ofisini kwaajili ya kuuza na kukodisha CD ili jioni iwe mahesabu, hivyo siku hiyo Mathias aliwahi ofisini akafungua ofisi kisha akasubiri wateja kama kila siku afanyavyo. Haikupita muda wateja wakamiminika kwa wingi walifurika banda la CD kama siku zote hadi wakati wa chakula cha mchana Mathias ukampita. Wateja kweli siku hiyo walifurika kwa kasi ya ajabu hadi ikambidi Mathias kuletewa chakula pale ofisini na msichana wa Mama Bonge ambaye ni maman'tilie maarufu pale Kigogo Post kwa mapishi hatari yanayosifiwa na makapela na masela Mambo Mathias salamu ilitolewa na msichana wa Mama Bonge mara baada ya kukabidhi chakula kwa Mathias. Poa tu...naona leo umeamua uniletee chakula ofisini Mathias alisema huku akihudumia wateja. Ndiyo nimekuletea, maana kisije kuisha ukatulaumu Sasa umeniletea chakula gani...ugali? Nimekuletea wali na nyama...si kitakufaa? Kitanifaa, maana ugali nimeula mno mpaka nishauchoka.

Mathias akiwa kwenye mazungumzo na msichana wa Mama Bonge huku akiwa bize na wateja, kwa mbali sauti ya upole ikapenya masikioni mwake ikitokea nje ya ofisi, Mathias alimtazama aliyeongea akaduwaa mara baada ya kumuona msichana mlimbwende mbele ya macho yake. Mathias macho yake yalipogongana na macho ya mlimbwende yule moyo wake uliripuka hadi akashikwa na kigugumizi cha ghafla, akamruhusu msichana wa Mama Bonge aende aje baadae kufuata pesa ili apate nafasi ya kuongea na mlimbwende. Msichana wa Mama Bonge alipoondoka Mathias akamchangamkia mlimbwende yule kama anavyowachangamkia wateja wengine. Karibu dada Asante...hapa mnakodisha CD? Ndiyo dada...tunakodisha na tunauza Nilihitaji unikodishie CD...unakodisha kwa bei gani? Nakodisha kwa shilingi elfu moja, pia nauza kwa shilingi elfu mbili Okay...CD za kihindi unazo? Za season, au? Zozote tu, ili mradi iwe ya kihindi Oooh, zipo Kama zipo...CD ya KUCH KUCH HOTA HAI utakuwa nayo? Ninayo...subiri kidogo aliongea Mathias kwa kumjibu mlimbwende yule huku akiwahudumia baadhi ya wateja wengine.

Mathias alipohakikisha wateja waliotangulia kuja kabla ya mlimbwende yule wameisha, akamkodishia mlimbwende yule CD, mlimbwende yule akatoa pesa na akampatia Mathias mara baada ya huduma hatimaye akataka kuondoka. Mathias akashindwa kabisa kujizuia akaropoka kwa kupaza sauti kumuita mlimbwende. Dada.!! Abeeh!!! Mlimbwende yule aliitika na akarudi kusikiliza wito. Hivi, jina lako ni nani? aliuliza Mathias kwa hofu. Naitwa Coletha...kuna shida?" alijibu na kuuliza Coletha kwa kumkazia macho Mathias. Hakuna shida yoyote...nilitaka tu kufahamu jina lako, kwani kuna ubaya? Hakuna ubaya...haya mimi naenda alijibu na kuaga Coletha mara baada ya kusikiliza wito. Lakini hakufika mbali akasikia anaitwa tena kugeuka kuangalia anayemuita akaona anayemuita ni Mathias akarudi. Nisamehe, kwa usumbufu alisema Mathias mara baada ya kurudi Coletha. Bila samahani, ulikuwa unataka kusema nini? aliuliza Coletha huku akiweka kofia aina ya cap vizuri kichwani. Nilikuwa naomba unisaidie, namba zako za simu kama hutojali Za, nini wewe? Coletha aliuliza kidogo kwa sauti ya ukali. Wateja zangu wote ni lazima nichukue namba zao, ili nipate wepesi kumpata pindi CD isiporudishwa mapema alieleza Mathias huku akionyesha sura ya hofu. Haya andika, 0688110311 Asante Sawa...naenda tutaonana wasaa mwingine Coletha aliaga na kuondoka huku akimuacha Mathias akimalizia chakula.



*****

Coletha ni mzaliwa wa Arusha, alizaliwa pekee katika familia ya Mzee Deus Swai, kutokana na wazazi kukwaruzana kwa sintofahamu za hapa na pale ikawapelekea wazazi kutarakiana. Coletha aliishi na baba yake angali alikuwa mdogo hadi anakua na kuwa Binti kabisa, aliishi na baba yake katika nyumba yao ya Kigogo Mapera akasomeshwa hadi kufikia chuo kikuu na kuhitimu pale UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM. Akapata stashahada ya udaktari na hatimaye akachaguliwa kuwa Daktari katika hospitali ya taifa ya MUHIMBILI, siku anayokodisha CD ilikuwa ni siku ya mapumziko ambayo hakwenda kazini bali alitoka matembezini na akiwa anarudi nyumbani akaona ni heri aende na CD ili akapotezee muda. Alipofika nyumbani, Coletha akaingia chumbani mwake na kuchukua laptop kisha akaketi kitandani na kuiwasha laptop yake na kuanza kuitazama filamu ile katika CD, alitazama filamu mpaka ilipofika usiku, akatoka kwenda kutafuta chakula mgahawani. Muda ule Mzee Deus Swai baba yake Coletha alirejea kutoka kazini akaingia chumbani kwake kubadili nguo kisha akauvesha mwili taulo tayari kwa kwenda kuoga, alipotoka kuoga baada ya kujiweka sawa akavaa nguo na akatoka chumbani na kuelekea moja kwa moja dinning kupata (chajio) yaani chakula cha usiku, lakini alipofika dinning na kufunua hotpot hakukuta chakula alikasirika sana na akamuita mwanae kwa ghadhabu.

Coletha, Colethaaa aliita mzee Swai bila mafanikio yoyote ya kujibiwa na mwanae hapo ndipo alipogundua kuwa mwanae hayupo ndani.

Huyu mtoto sijui kaelekea wapi...akirudi atanieleza hawezi kunikalisha na njaa mimi" Mzee swai alifoka kwa hasira huku akijisemesha nafsini mwenyewe pale dinning kama mtu aliyerukwa na akili. Kitendo cha mwanae Coletha kutoandaa chakula kilimkasirisha sana Mzee Deus Swai, kwa kuipunguza jazba yake na kijazube akaamua kwenda sebuleni kutazama runinga.Kipindi akiwa anatazama taarifa ya habari ya saa mbili usiku mara akasikia mlango wa sebuleni ukigongwa kwa haraka akanyanyuka sofani kwenda kumlaki agongaye lango, alipofungua mlango alikutana uso kwa uso na mwanae ghafla alikunja ndita kwa hasira kisha kuanza kuuliza.

Coletha, umetoka wapi?

Nimetoka mgahawani, kununua chakula alijibu Coletha kwa kusuasua.

Ushaanza uvivu wa kupika sio?...sasa hicho chakula umekipata?

Nimepata

Umepata chakula, gani?

Chipsi, yai

Nami, umeniletea?

Yaah, daddy

Okay...ingia ndani ukatenge tule alisema mzee Swai kwa kuonyesha uso wa bashasha mara baada ya mwanae kujieleza kwa weredi wa hali ya juu.

Baba na mwana waliingia ndani.Coletha akatenga chakula dinning hatimaye wakala na walipomaliza Mzee Swai akaingia chumbani kwake kujipumzisha, akamwacha mwanae sebuleni akiangalia filamu yake kwenye laptop yake.

Coletha alinogewa na filamu mpaka usingizi ukamteka na kumuweka na kumsweka kabisa himayani mwake na alikuja kushtuka muda mwingine kabisa, akiwa na kimuhemuhe nafsini mara anazama katika jambo la kufikirisha kwa kuanza kuiwazia huruma ya baba yake laiti angemkuta usiku ule pale sebuleni aking'atwa na mbu ingekuwaje??



Mmh, hivi mzee Swai angenikuta sijui ningemwambiaje

Halafu na kesho nahitajika kuwahi kazini, kwa namna hii nitawahi kweli

Sasa huu ujinga...naomba kabisa usiendelee tena ukiendelea kazini kutadorola Coletha alijifikiria huku akiinuka kuelekea chumbani mwake kujipumzisha.

*****

Mathias baada ya kazi yake ya kila siku alirudi nyumbani alipofika kwenye chumba chake akafungua mlango na kuingia ndani.Akavaa taulo na kwenda bafuni kuoga, baada ya kuoga akarejea tena ndani kula chakula alichonunua mgahawani, alipomaliza akaiwasha feni impepee ili baada ya muda apate hata lepe la usingizi.

Kweli baada ya muda Mathias alipata usingizi kulala fofofo, alikuja kushtushwa na Jogoo wa alfajiri alipowika, alikurupuka kitandani na kufikicha macho mfululizo kuondoa ukungu uletao giza machoni.Akachukua ndoo ya uani na kuitia maji ya kuoga kisha akaelekea kubafu na alipomaliza akarudi ndani kujiandaa, Baada ya kujiandaa alitoka na kuelekea moja kwa moja kufungua ofisi yake.Alipofika ofisini hakuweza kuamini alichokuwa anakiona kwani aliikuta kadamnasi ikimsubiri bila shaka walikuwa wanahitaji huduma, alifungua ofisi chapchap na kuanza kutoa huduma kwa wateja wake, akiwa anaendelea kutoa huduma kwa wateja alishangazwa kwa kuona jambo fulani mbele yake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alimuona mama mmoja kabeba mtoto mchanga mgongoni mwake huku akiwa kavalia dela kuu kuu akija katika ofisi yake na baada ya kumwangalia kwa makini Mathias anagundua kuwa ni ombaomba wa mtaani kutokana na jinsi muonekano wake ulivyokuwa, yule mama alifika ofisini mwa Mathias akaomba chochote kitu kwa kijana Mathias kweli kwa mtu mwenye upeo anaweza kutambua ni jinsi gani yule mama alivyogubikwa na shida.Alionekana kweli ni mwenye shida maana mdomo wake ulikauka na kujenga utando mweupe mithili ya mwathirika wa maradhi sugu au uraibu wa madawa yote kutokana na njaa aliyokuwa nayo, miguu yake ilitoka magaga sugu kutokana na kutembea kwa muda mrefu bila kupumzika mara kwa mara, mwili wake ulijaa vipele vya ukurutu bila shaka kutokana na kutokuoga kwa muda mrefu. Baba, naomba msaada nikapate chochote kitu alisema yule mama kwa uso na sauti ya huruma.

Samahani Mama yangu, mimi ndiyo kwanza nafungua biashara sijaingiza chochote aliongea Mathias kwa upole.

Nisaidie hata elfu mbili kama unayo, itanitosha tu mwanangu alisema mama yule huku safari hii akiwapunga nzi katika mkono wake waliokuwa wanamzonga kupata shibe kwenye vipele vyake vya ukurutu.

Mathias huruma ilimjia kwa yule mama na kuanza kujipapasa kwenye mifuko ya suruali kama ataweza kukutana na chochote.

Hamadi! akakutana na shilingi elfu tano katika mfuko wa suruali yake na moja kwa moja bila ya hiyana akaamua kumpatia yule mama ile pesa yote ili imsaidie kwa siku ile, yule mama alimshukuru sana Mathias kwa msaada aliompatia kwani aliamini bila kuomba msaada siku ile njaa ingempelekea hata angepoteza maisha siku si zake kwaajili ya baa gumu la njaa.

Mwanangu, asante sana; Mungu aIbariki kazi ya mikono yako kwa unyenyekevu na busara yule mama alitoa fanaka zake kwa kijana Mathias.

Usijali mama, nawe pia nikutakie utakaswe na kupatiwa wepesi katika maisha yako alisema Mathias kwa kumfariji yule mama huku akimshika mkono begani.



Asante baba, naamini ipo siku Mungu atakisikia kilio changu

Ukimuamini yeye tu, atatenda.”

Amina...lakini baba mimi si mkaaji acha niende tutaonana tena siku nyingine aliaga yule mama hatimaye akaondoka huku nyuma akimwacha Mathias akiendelea kutoa huduma kwa wateja wake.

Mathias alizidi kutoa huduma kwa wateja mpaka muda wa mchana pale wateja walipotulia kuja, ndipo akafunga na kwenda kupata chakula cha mchana kwa mama Bonge ambaye ndiye maman'tilie aliyezoeana naye kitambo kidogo.

Karibu, mteja wangu alikaribishwa Mathias na mama Bonge mara baada ya kuwasili mgahawani hapo.

Nishakaribia...kuna nini leo? aliuliza Mathias huku akijaribu kutazama mahali sahihi kwa kwenda kukaa.

Kuna wali nyama na kuna ugali samaki, sijui wewe katika hapo unakula nini leo alijibu mama Bonge huku akiwa na pilika pilika za kuwahudumia wateja.

"Ugali wenyewe, dona au sembe?

Ni, sembe

Niwekee, ugali

Mabinti, muwekeeni Mathias ugali aliagiza mabinti zake mama Bonge huku yeye akiwa bado anahudumia wateja wengine.

Mathias alitengewa chakula taratibu akaanza kula kile chakula bila ya kukimbizana wala kukimbizwa na mtu, baada ya kumaliza kula alilipa pesa na kuaga kisha akarejea ofisini kwake huku akijikongoja kutokana na shibe na alipofika ofisini akashtuka kumuona Coletha akiwa nje ya ofisi yake.

Moyoni alifurahi sana kumuona tena Coletha japo hakujua kilichomleta.

Coletha, umekuja muda? aliuliza Mathias huku usoni akimuonea haya Coletha.

Muda kidogo, nimekusubiri mpaka miguu yangu imekufa ganzi alijibu Coletha huku akijifuta jasho usoni kwa leso yake.

Pole

Nishapoa, ndiyo unafungua sasa hivi?

Hapana, nimetoka kula chakula

Okay, mimi nimeleta CD yako

Mbona umewahi kurudisha, wakati muda wako bado

Mh, nimeogopa mwenzangu kulala na CD ya watu

Lakini, si umemaliza kuangalia?

Yaah

Basi sawa...asante kwa kuniwahishia CD yangu

Okay, kuna CD nyingine ya kihindi ya love story?

CD zipo, uchoke wewe tu

Nichagulie iliyokuwa nzuri, nikaangalie

JEET, naona itakufaa

Inaitwaje?

JEET

Kaigiza, nani?

Kaigiza SANNY DEOL, KARISMA KAPOOR na SALMAN KHAN ukiona ni nzuri alisema Mathias kwa kupigia promo biashara yake kwa mlimbwende Coletha mtoto wa chuga. Coletha alipochaguliwa CD aliaga haraka na kuondoka huku nyuma asijue kama ameacha simu kwenye ofisi ya Mathias.Mathias kutokana na usingizi aliokuwa nao kwasababu ya shibe ikambidi atandike kirago alale, usingizi ulimchukua kama alivyo na baadae kuja kushtushwa na mlio wa simu ya Coletha, alipoamka akashangaa kuona simu ya Coletha ipo ofisini kwake. Akaamua kuichukua na kuanza kuipekua na moja kwa moja alienda kuufungua ujumbe mfupi wa maandishi uliokuwa umetumwa wasaa mchache ambao mlio wake ndio uliompelekea akurupuke kutoka usingizini ni ujumbe aliokuwa ametumiwa Coletha lakini ulimpagawisha sana mathias alipousoma na alihisi kama kichwa kupasuka.

Lakini Mathias alijikaza kama mwanaume japo kichwani mwake alikuwa bado anauwazia ule ujumbe, Mathias alizidi kujifikiria huku akikuna kichwa chake utafikiri kama kuna chawa wanamtambaa.”





Kweli, huyu mpenzi wa Coletha?

Haiwezekani...msichana nimpendae nimkose kirahisi hivi

Coletha, moyo wangu mbona unakupenda kiasi hiki?

Moyo wako, nawe unanipenda?

Moyo wangu, una wivu sana nikiona upo na mwanaume mwingine

Hivyo naomba uje kunipenda mimi, moyo upate tulia

Coletha, nasema sitokubali kukukosa nitapambana mpaka tone la mwisho ili nikupate

Naamini ipo siku utakuwa wangu, Coletha alijifariji moyoni Mathias kisha kupotezea ule ujumbe.

Mathias aliihifadhi simu ya Coletha vizuri akijua dhahiri kwamba mwenyewe atarudia kuichukua, baada ya kuihifadhi simu hakurejea tena kulala bali aliamua kujipa jukumu la kupanga CD zake vizuri kwaajili ya kuwavutia wateja.

Coletha akiwa yupo nyumbani aligundua kama simu yake hana akakumbuka kwamba kaisahau ofisini kwa Mathias ikambidi arudi kuifuata simu yake na safari hii alikaza mwendo apate kufika haraka, alipofika akamkuta Mathias anamalizia kupanga CD.

Nimerudi, tenahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kuna, nini?

Simu yangu, nimeisahau hapa bandani kwako

Mh, mbona sijaona simu

Hujaiona!!!?

Yaah...labda umedondosha njiani

Hapana, nakumbuka nimeiacha hapa

Hapa, hamna sasa

Basi sawa, acha ipotee tu

Pole, sana

"Asante...mimi naenda alipiga hatua kadhaa Coletha kisha akaitwa na Mathias.

Usiondoke, nilikuwa nakutania

Unamaanisha, nini?

Simu yako, ninayo

Loh, utani gani huo?

Nisamehe Coletha na wala usikasirike, maana utani nimezoea...naomba nawe unizoee tu

Okay...nilichanganyikiwa sana maana kazi zetu hizi bila simu utafeli

Ni kweli, kabisa

Haya, kwa heri aliaga Coletha huku akipekua simu yake sehemu ya missed call na sehemu ya ujumbe mara baada ya kupewa simu.

Coletha alipopekua kwenye ujumbe ndiyo akauona ujumbe aliousoma Mathias ulikuwa umeshafunguliwa.Akaufungua tena ujumbe ule ili asome na ujumbe ulisomeka hivi:

Habari mrembo wangu, natumai ni mzima wa afya mimi huku ni mzima ingawa nimechoka kuishi South Africa kwasababu ya utafutaji wa pesa ulivyo mgumu.Kwahiyo nimetuma ujumbe huu ili kukujulisha kuwa mwakani baada ya kumaliza masomo yangu ya uanasheria nitarejea nyumbani Tanzania alisoma Coletha ujumbe ule mpaka mwisho kisha akatoa tabasamu huku akikamata barabara ya kurudi nyumbani

Mathias aliachwa ofisini kwake akiendelea na shughuli zake huku akiwa na huzuni.Aliona siku ile ni mbaya kwake ila atafanyaje ilimbidi kujikaza kisabuni na kuzidi kujipa moyo tu ili asiweze kuamini alichokiona aone kama ndoto za alinacha.

*****

Coletha aliendelea kuwa na furaha kwa upande wake hadi alipofika nyumbani, ule ujumbe ulimfanya kutofanya lolote na alipofika nyumbani.Aliingia moja kwa moja chumbani kubadili nguo na baada ya kubadili nguo aliamua kuelekea mtaani kununua chakula mgahawani, hakutaka kujichosha kuingia jikoni bali alinunua wali samaki hatimaye akarudi nyumbani.Kabla ya kula chakula akamtafuta yule mtu wake aliyemtumia ujumbe akiwa ameisahau simu kwenye banda la CD la Mathias, alimtafuta kupitia kwenye simu ya mkononi lakini hakufanikiwa kumpata bali alisikia sauti ikimwambia: Simu ya mteja unayempigia haipatikani kwa sasa, jaribu tena baadae au bonyeza kitufe chochote kumuachia ujumbe wa sauti na utatozwa gharama uliyorekodia sauti ilimalizika kuongea kisha simu ikakata.

Coletha hata hivyo hakukata tamaa alipomaliza kula akamtafuta tena lakini jitihada zake bado zikagonga mwamba alitokea kukasirika sana mpaka akaamua kuzima simu.Akaiweka kwenye droo ya meza kisha akatoka chumbani mwake na kuelekea sebuleni kufanya baadhi ya kazi alipomaliza akarudi chumbani kupitia nyaraka za hospitalini, kidogo nyakati zile Coletha alikuwa bize kwa kupitia nyaraka usiku wa saa mbili kama kawaida mzee Deus aliwasili nyumbani, akakuta mlango wa sebuleni upo wazi na hakuona dalili ya uwepo wa mwanae.

Huyu mtoto kwa kuzurura, sijui kaenda wapi? alinung'unika mzee Swai.

Halafu mlango kaacha wazi, sijui anategemea nini?

Haya yote, ni malezi ya mama

Mtoto anakuwa kama mbwa koko bwana, atulii nyumbani kama kachanjia vile

Ona ananifanya kila nikirudi niongee, nionekane baba mbaya kumbe anajitakiaga mwenyewe alinung'unika kwa kufoka mzee Deus Swai huku akiingia ndani.

Akaketi kwenye sofa kumsubiri mwanae kwa hamu, lisaa halikufika mara ghafla akashikwa na taharuki kwa kumuona mwanae akiwa anatokea chumbani mwake.

Shikamoo baba alisalimu Coletha.

Marahaba aliitikia salamu mzee Swai kisha akatoa leso akajifuta taka mwili hatimaye kuendelea kuongea.

Kumbe, muda wote upo ndani?

Yes, daddy

Nisamehe, sana

Kwa, kipi?

Nimekushutumu bure kuwa unazurura, lakini kumbe upo ndani

Nilijichokea, nikaingia chumbani kujipumzisha kidogo

Okay...umepika nini?

Sijapika

Kwanini?

Nimeenda mgahawani, kununua chakula

Nilijua tu cha uvivu...sasa umepata chakula?

Ndiyo, nimepata

Umepata, chakula gani?

Ndizi, nyama

Waooh, umenifurahisha sana unajua umenikumbusha mbali sana

Nimekukumbusha, wapi?

Umenikumbusha kipindi nipo mdogo, chakula hiki alipenda sana kupika mama yangu ambaye ni bibi yako wewe

Alaah, inaelekea unakipenda?

haswaaa

Basi twende, nikakutengee ule alisema Coletha kisha akaelekea dinning kumtengea baba yake chakula.



*****

Benson ndiye kijana aliyetuma ujumbe mwanzo kwenye simu ya Coletha, alipoiwasha simu yake ndipo alipokutana na ujumbe wa Coletha kwamba alimtafuta.Akatafuta namba ya Coletha, akapiga simu mara ya kwanza ikakatwa, akapiga mara ya pili ikakatwa hakuchoka akaja akapiga mara ya tatu.Coletha akiwa bado yupo na baba yake kwa mbali akasikia simu yake ikiita tena alipotazama kizinza cha simu yake akaona namba ngeni ikipiga pole pole akanyanyuka kwenye kiti na kuelekea chumbani kupokea simu.Coletha alipofika chumbani akapokea simu iliyokuwa inaita kwa muda mrefu.

Hellow alizungumza mara baada ya kupokea simu.

Hellow sauti ya upande wa pili nayo ilisikika ikiongea.

Nani, mwenzangu? aliuliza Coletha.

Mathias

Mathias, yupi?

Wa, CD

Oooh!!!, unahitaji CD yako?

Hapana, nimeona nikujulie hali tu

Asante...kesho alisema Coletha kisha akataka kukata simu.

Usikate simu, nahitaji nikuambie kitu Mathias alimzuia Coletha asikate simu.

Kitu gani, hicho!!!? aliuliza Coletha kwa taharuki.

Coletha, una kila sifa ya kuitwa mwanamke una kila vigezo vya kumshawishi mwanaume akazitamka hisia zake kwakohttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Sijakuelewa

Coletha wewe ni mzuri, Mungu kakupa urembo uliotukuka kwenye macho ya wanaume

Ebu acha utani, yaani una maanisha mimi ni mzuri kiasi hicho?

Yaah, wewe ni mzuri mno yaani nikielezea uzuri wako tutakesha

Lakini mbona mwenyewe, najiona wa kawaida

Huwezi kujiona mwenyewe, sisi wa pembeni ndiyo tunayekuona

Mmmh, haya asante...ushafunga ofisi? alisema Coletha kisha akabadilisha mada ili kumsimamisha Mathias asiendelee anapotaka kwenda. Nimefunga, muda kidogo

Kesho, utafungua saa ngapi?

Kesho nitawahi sana, kwenye saa kumi na mbili kasoro ya alfajiri nitakuwa nishafungua

Okay, nikienda kazini nitakupitishia CD yako

Utakuwa, ushaimaliza?

Yes

Kama itakuwa bado kumaliza, usihofu endelea kutazama

Nishaimaliza

Basi sawa, kesho niletee

Okay

Coletha, hivi una boyfriend? aliuliza Mathias kwa kurudisha mada ya mwanzo aliyoikwepa Coletha.

Yaah, ninaye alijibu Coletha kwa madaha.Jibu lile liilipenya vyema sikioni mwa Mathias na kumsababishia Mathias kuumia moyo pia likamfanya moyo kwenda kasi na kudunda kama kitenesi.

Ushamtambulisha, kwa wazazi?

Mbona una maswali mengi, kipi kinachoendelea?

Nataka kufahamu tu, Coletha

Ukishajua?

Pengine roho yangu, itapona

Kivipi?

Kwa kutokuwa, na maswali yasiyo na majibu

Eeeeh, umenishinda tabia...usiku mwema akakata simu Coletha.

Hallow, hallow...shiiiiit amekata simu wakati hata jambo langu sijamwambia daah alilalamika sana Mathias mara baada ya Coletha kukata simu.

Coletha alipokata simu akarudi sebuleni kuangalia CD baada ya mzee Swai kwenda kulala baada ya kumaliza kula.Coletha aliachwa huru kwa muda ule mara ghafla wakati anaangalia CD akasikia simu yake inaita tena kuangalia namba ilikuwa ni ngeni, hivyo akajua ni Mathias bado anamsumbua akakata simu mpigaji naye akujikatia tamaa aliendelea kupiga lakini ikawa bado inakatwa.Coletha akiwa yupo bize na CD simu ikaita tena akataka kukata tena lakini alipolisoma jina la mpigaji akaona linasomeka kwa jina la Benson akapokea kwa kutabasamu na kwa furaha zote.



Hello aliongea Coletha kwa shauku ya kutaka kusikia sauti ya Benson.

Hello, kipenzi sauti ya upande wa pili ilisikika nayo ikiongea kwa mapozi.

Nimekumiss

Hunishindi mie, mpenzi

Mpenzi kwasasa, una Diploma au Certificate?

Nina Degree, hizo zote nishapita

Oooh, hongera

Asante mpenzi...nawe ushamaliza chuo?

Nishamaliza, kwasasa ni daktari wa mama wajawazito na watoto

Hongera sana, naona ushatimiza ndoto zako

Kweli, lakini bado ndoto moja tu

Ipi, hiyo?

Si ndoto nyingine, bali ni kuolewa nawe mpenzi wangu

Usijali, omba nirudi salama

Nitakuombea

Haya bye, mpenzi

Bye, nawe alimalizia kwa kuaga Coletha kisha akakata simu.

Coletha baada ya kuongea na simu alijihisi mwenye furaha kwa kusikia sauti ya Benson tu, hata haja ya kuangalia CD tena hakuwa nayo alizima kila kitu kisha akaingia chumbani kulala.

*****

Mathias tokea akatiwe simu na Coletha hakuwa na amani kabisa hata usingizi wenyewe aliutafuta kwa mazonge kwani kuna nyakati aliupata na muda mwingine hakuupata kabisa.

Mara baada ya kuumwa na mbu kwa muda mrefu wakati akiutafuta usingizi.Coletha kutokana na furaha aliyokuwa nayo ya kuongea na mwenzi wake hivyo alikuja kupata usingizi majogoo.Hata mzee Swai alipodamka kujiandaa kwenda kazini alikuwa bado hata lepe la usingizi hajalipata na usingizi ulikuja kupatikana saa kumi na moja ya alfajiri, bado hakulala sana kwani lisaa limoja mbele alikuja kugongewa mlango wake wa chumbani na baba yake mara baada ya baba yake kukuta simu ya mwanae pale sebuleni imesahaulika.Coletha alinyanyuka kitandani akitaka akamfungulie baba yake aliponyanyuka tu ghafla akakumbuka kama simu yake aliacha sebuleni jana, akili ikamruka akachanganyikiwa akaenda kufungua mlango kinyonge kufungua tu akakutana ana kwa ana na baba yake mapigo ya moyo yalikwenda kasi kwa uoga, mawazo yake haraka yakafikiria mbali jinsi alivyomwona baba yake kafura pale mlangoni.

Mungu wangu!!!, simu yangu kaiona nini?

Mmmh, kama kaiona halafu kakuta mambo yasiyoeleweka nimekwisha

Duuh!!!, mbona ya leo kali maana si kawaida yake kuja kuniamsha...kuna kitu sijui kakiona

Mmmh Coletha akiwa bado ameduwaa pale mlangoni akijifikiri mara akashtuka akiitwa na baba yake.

Coletha aliita mzee Swai huku akiupiga mlango kwa kutumia mkono kwaajili ya kumzindua mwanae toka kwenye lindi la mawazo. Abeeh! Coletha aliitika kwa mshtuko.

Mbona unaonekana, una mawazo kulikoni? aliuliza mzee Swai mara baada ya kugundua mwanae kuwa alikuwa na mawazo.

Hamna alijibu Coletha kwa hofu.

Hamna!!!...kweli?

Kweli

Haya, lakini kumbuka mficha maradhi kifo humuumbua shauri yako alisema mzee Swai huku akimkabidhi mwanae simu.Akatembea hatua kadhaa akarudi tena kwa mwanae kisha akasema kwa kuhabarisha.

Kuna jumbe karibia tano za mama yako kwenye simu...sijui anashida gani?”

Nimeziona aliongea Coletha mara baada ya kuipekua simu yake aliyokabidhiwa na baba yake.

Kama umeziona sawa...ngoja nami niende kazini sasa alisema mzee Swai kisha akamuaga mwanae na akatoka nje kuelekea ofisini.

Mara baada ya mzee Swai kwenda kazini Coletha akarudi chumbani kujiandaa, baada ya kujianda akaelekea kazini nae kutimiza majukumu yake.

*****

Benson aliendelea na masomo akiwa ughaibuni, alitokea kupendwa na wahadhiri kutokana na juhudi zake za darasani pia akatokea kupendwa na baadhi ya wanafunzi wenzake wa kutoka vyuo mbalimbali pindi walipozipata sifa zake katika chuo chake cha MANDELA.Alipata marafiki wengi sana pale chuoni wanaume kwa wanawake bila yeye kutegemea.Marafiki wengine walimfuata kwa dhumuni la ushawishi mzuri, wengine walimfuata kwaajili ya kufundishwa kujadili midahalo wa chuoni, wengine baadhi ya wanawake walipenda kutoka naye sehemu mbalimbali za starehe pia wanawake wengine walipenda kutoka naye kimahusiano bila ya wao wenyewe kujijua kama wanachangia bwana mmoja.Siku moja Benson akiwa hosteli na rafiki yake anayekaa naye hosteli moja ghafla alishtuka kwa kushangazwa na ujumbe uliojaa vitisho, aliogopa sana alihema kwa kasi kisha akatokwa na jasho jembamba kwa uoga.



*****

Kama kawaida Mathias aliamka mapema akajiandaa kisha akatoka kwenda kutafuta vitafunwa kwaajili ya staftahi alifanikiwa kupata vitumbua na kurudi navyo nyumbani kwaajili ya kupata staftahi yake, alipofika nyumbani akachemsha chai.Chai ilipochemka akanywa na punde kabla hajamaliza kunywa chai akasikia mlango wake ukigongwa kwa nguvu alishtushwa na hali ile maana si kawaida lakini kama mwanaume alijipa ujasiri, akashusha pumzi kisha akaenda kufungua ule mlango kufungua tu mlango mara ghafla akakutana na mama mwenye nyumba.

Eeeh, afadhali nimekukuta alisema yule mama kwa kuhema huku akionyesha sura ya jazba.

Kwani, kuna nini? aliongea Mathias kwa upole.

Unajifanya, hujui?

Sijui

Hujui eeh, hii zamu ya nani kufanya usafi...si yako?

Ni yangu, ndiyo

Haya tokea wiki inaanza, ushawahi fanya hata siku moja?

Hapana

Ndiyo maana mnaambiwa wapangaji ni wakorofi kwaajili ya haya...wiki yote hii niilikuwa nakufanyia usafi yaani wewe hata hujali

Nilipitiwa mama, tusameheane

Ulipitiwa!!! sawa...sasa nahitaji posho yangu ya kukufanyia usafi

Ni shilingi, ngapi?

Ni, elfu saba...kila siku ni elfu moja kwahiyo siku saba bei yake ndiyo hiyo

Sawa aliongea Mathias kisha akaingia ndani kuchukua pesa amlipe yule mama.

Mathias alimlipa yule mama bila kikwazo, mara baada ya kulipwa yule mama akachapa mbaliga kurudi ndani kwake.Mathias alipomalizana na yule mama mwenye nyumba akarudi kumalizia chai alipomaliza akafunga mlango wake na mwisho akaondoka kuelekea ofisini kwake, lakini kabla hajafika ofisini akiwa bado yupo njiani simu yake ikawa inaita kuangalia anayepiga ni nani alipoangalia namba ya mpigaji aliachia tabasamu akifikiri ni Coletha anayepiga.”



**********

“Coletha alipofika ofisini akamtafuta mama yake ili ajue mama yake ana shida gani kubwa ya kumfanya amtafute kwa siku ile.



“Hallo” alizungumza Coletha huku akiweka simu yake vizuri sikioni.



“Mwanangu, upo wapi?” sauti ya Mama Coletha ilisikika ikimuuliza mwanae.



“Nipo, kazini.”



“Unaweza, kuja kwangu?.”



“Kuna, shida gani?.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Wewe, njoo.”



“Mbona, unanitisha...kuna nini?.”



“Nakufaaa!!!” alipiga ukunga Mama Coletha kwa tabu sana.



Ukunga ule ulimshtua Coletha roho yake ikajenga hofu akawa anatetemeka na kukosa nguvu kabisa. Coletha pindi nguvu ziliporejea haraka akakata simu na upesi safari ya kuelekea kwa mama yake ikaanza, kabla ya kwenda kwa mama yake kwanza akapitia katika ofisi ya Daktari mkuu kutoa taarifa.



**********

Mathias alizidi kufurahi baada ya kuona ile namba ngeni akajua si mwingine itakuwa ni Coletha kamkumbuka kupitia namba nyingine. Bila kukawia Mathias aliipokea simu ile kwa shauku akaiegesha sikioni kumsikiliza apigaye.



“Naitwa Anitha...na imani wewe ndiye mtangazaji wa kipindi cha WANAWAKE LIVE” ilisikika sauti ya Anitha kama alivyojitambulisha hapo awali ikiongea.



“Hapana...mimi si mtangazaji dada yangu utakuwa umekosea namba” alisema Mathias kwa kumkatisha mazungumzo Anitha.



“Uuuuh!!!, samahani kaka yangu kwa usumbufu” alisikika Anita akishusha pumzi polepole na akasema kwa upole.



“Bila, samahani” alimalizia kusema Mathias kisha akakata simu.



Baada ya mazungumzo ya kwenye simu, Mathias akaendelea na safari yake mdogo mdogo akiwa bado yupo njiani alisikia tena simu yake inaita. Akaitoa simu mfukoni akaangalia kwa makini kwenye kioo cha simu amtambue huyo anayepiga, kuangalia tu jina la mtu anayepiga barabara nzima akacharuka kwa kuruka ruka kama kitenesi hakuamini hata kidogo hivyo ikamlazimu angalie tena kwa mara ya pili apate kuamini. Mara ya pili ndipo aliamini kuwa apigaye si mwingine bali ni Coletha ni yule msichana ampendaye, pale pale akashikwa na kitete na moyo wake ukawa na wasiwasi kwa uwoga kwa vile alikuwa na kitete hivyo basi simu ikaita hadi ikakata bila kupokelewa ilipokatwa haraka sana Mathias akataka kupiga ila ikamkatisha sauti ya kike iliyokuwa inasema;

Samahani salio lako halitoshi kupiga simu hii, ongeza salio ndipo ujaribu kupiga tena simu hii” ile sauti ilipenya vyema sikioni mwa Mathias. Upesi upesi Mathias hakutaka kungoja muda akaingia dukani.



“Vocha, zipo?” aliuliza Mathias mara baada ya kufika dukani.



“Bila shaka, zitakuwepo” alijibu muuza duka kisha akaingia dukani kumhudumia mteja.



“Kama zipo, nigee.”



“Vocha, ya aina gani?.”



“Tigo.”



“Ya shilingi, ngapi?.”



“Elfu, moja.”



Mangi alimpatia Mathias vocha aliyoihitaji kisha Mathias akaondoka zake, Mathias mbele kidogo alisimama ili kuikwaruza taratibu vocha na kuziingiza tarakimu kwenye simu hatimaye akajiunga kifurushi. Cha kwanza akamtafuta Coletha kwa shauku lakini alipopiga simu ya Coletha iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa akajaribu tena kupiga ikaita simu kwa muda mrefu hadi Mathias akakata tamaa alitaka kukata tu mara ikapokelewa.



“Hallo,” Mathias aliisikia sauti ya Coletha ikizungumza kwenye simu.



“Mambo” alitoa ushirikiano Mathias wa kuongea na kumsikiliza Coletha.



“Poa.”



“Eeeh, niambie.”



“Kwasasa, upo wapi?.”



“Nipo njiani, ndiyo naelekea ofisini.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Okay...sasa nimepata dharura CD yako nitaipitisha kesho.”



“Sawa, wee usijali.”



“Basi poa, kesho.”



“Coletha, subiri usikate simu...,” Mathias kabla hajamaliza kuongea Coletha akabonyeza kitufe chekundu na kukata simu.



Mathias aliachwa katika njia panda hakutarajia kama kweli Coletha atakata simu alidhani Coletha atampa muda hata kidogo wa kuongea lakini sivyo alivyofikiri, alinywea akawa mdogo kama pilitoni.



**********



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog