Simulizi : Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi
Sehemu Ya Pili
(2)
Nikamwambia poa haina
neno.
Tulilala, asbh nikakasirika sana, nikampigia Husna simu kumuuliza
ana nini na mume wangu, alipokea simu na kusema hana mahusiano yoyote ila ni
kama shemeji yake. Nilinyamaza na nikamuuliza anatoka na nani akaniambia anatoka
na Damson. Nikamkumbuka Damson. Nikampigia simu, nikamuuliza shem samahani,
Husna unamfahamu? Akasema ndio namfahamu, nikamuuliza ni nani? Akasema kwa nini
shem unaniuliza hivyo? Nikamwambia mbona kasema ni demu wako? Kwani wewe
umemuacha prisca? Maana alijua namfahamu prisca, akasema aa shem vunga. Kisha
akakata simu, na mara simu yake ikawa busy sana, nikajua anaongea aiza na Husna
ama Mume wangu. Haraka nikampigigia mume wangu, simu ikawa busy sana.
Nikanyamaza.
Jioni mume aliporudi home akawa kaweka simu pw. Tena kwenye
kila kitu, nikamuuliza kulikoni? Akasema naona tu tutakosana kisa simu, naona
niweke pw. Na mimi nikamwambia so na mimi niweke sio? Na mimi nikaweka. Kisha
nikaanza kugombana naye, kwanza nikampigia Prisca nikamuuliza kuhusu Husna,
akaniambia Charlote naomba tu nikuambie kweli, Husna anatoka na mumeo, ila
wanatabia ya kusame ni demu wa Damsosn ili usijue. Lakini Husna anatoka na
mumeo, ila wewe tulia nitakukamatisha naye. Wewe nyamaza.
Prisca
akanihakikishia kuwakamata. Na kweli akachonga njia mpaka akanipigia simu siku
moja na kuniambia niende ofcn.Nilifika ofcn na kweli hamadi, Husna na mume wangu
hawa hapa . Sikuamini, kwanza aligoma kufungua ofcn lakini nilisukuma mlango wa
alminium ambao niliwaona kwa ndani .
Jones hakuamini, aliogo pa sana,
niliomba tu wafungue, mwisho akafungua. Kiliniuma sana, nikamwambia Husna ni
nini hiki? Hakunijibu, nikataka kumshika nimpige
akaniponyoka.
Nikamwambia mume wangu ni nini unanifanyia? Akaanza kuomba
msamaha, mwisho nikaona sina sababu ya kuendelea kulumbana naye, nikaondoka na
kwenda nyumbani, kufika nyumbani nikalia sana, kikaniuma sana.
Akaja na
kuniomba msamaha, nikamuuliza kulikoni nini anakosa? Hakuwa na jibu. Nikamuuliza
mimi nikifanya hivi utajisikiaje? Hakujibu pia.
Alikuwa mpole sana.
Akaniambia nisamehe mke wangu sitarudia tena naomba yaishe.
Nikamwambia
poa haina neno, ila asante sana.
Kuanzia hapo nikaanza kujiuliza
inakuwaje mume anabadilka hivyo. Mume niliyemjali kiasi hicho na
kumuamini.
Niliogopa kuwapa watu faida, nikasema sitaondoka wala kufanya
lolote, ila nitaenda kumshtaki Husna kwa mama yake.
SEHEMU YA
NNE:
Nilijua mama yake Husna alipofanyia kazi. Nilimfuata asbh sana,
kabla hajaingia ofcn kwake.
Nilimsalimia na kumwambia mama samahani
nataka kuzungumza na wewe.
Namna alivyonitazama ni kama aliyenibeza na
mwenye kujua jambo, niligundua hilo mapema sana.
Nilimwambia shikamoo
mama, alinitazama chini juu, hakuniitikia. Ni mwanamke mweusi mnene na mfupi.
Hivyo hata aliponitazama ilikuwa ni rahisi mimi kujua ananitazama yani
kunishusha kwani ilibidi anyanyue sana shingo kunikuta
nilipo.
Sikkujali, alisema enhe unasemaje?
Nilimwambia mama
samahani,, nimegundua mwanao ana mahusiano na mume wangu.
Akaguna, na
kusema ninao watoto wengi ni nani?
Moja kwa moja nilisema ni Husna….
Alicheka kwa kejeli,, akaniambia,,,
Uliwashika ama ni umbea umekusanya
mtaani?
Nikamwambia niliwashika.
Akaniambia uliwashika wapi?
Nikamwambia niliwashika ofcn kwa mume wangu.
Akaniambia kwa hivyo huyo
mumeo haruhusiwi kufanya kazi na wanawake? Kwani uliwakuta wako uchi
ama?
Mh.. hii ilinishangaza,, nilijiuliza huyu ni mama ama ni Jini?
Mbona hana huruma kama hajaolewa?
Nilimwambia mama nina uhakika ndo
maana nimekuja ili umuonye mwanao.
Akaniambia naona huna jipya mama,,,
sikia,, naomba sisikilizi umbea, Nenda kamtosheleze mumeo sawa.
Alivuta
hatua na kuniacha nikiwa nimeshangaa nisijue la kufanya, kiliniuma
sana.
Nilienda kazini kwangu huku nina mawazo debe zima.
Nililia
sana, ila kwa vile sikutaka ofcn wajue kisa changu nilijikaza sana na kunyamaza
tu.
Sikuongea lolote.
Baada ya muda kidogo Husna akaniandikia
msg na kuniambia,,, Umeongea na mama yangu ili nini? Itakusaidia nini? Mchunge
mumeo usinifuatilie.
Niliisoma ile msg bado nikajikaza, nikasema sina
sababu ya kushindana kwa maneno, nahitaji matendo zaidi.
Nikanyamaza
kimya sikuijibu.
Nikamaliza kazi nikaenda home kama hakuna kilichowahi
kutokea.
Nikaanza kujidunga balantine moja. Kila siku lazima soda moja
ya ginger lemon na glass ya balantine.
Kila jioni, ili kupoteza mawazo.
Na jones alishindwa Kunizuia kwani sasa alikuwa na kosa na hakutaka kukubali
kosa. Kuomba msamaha anashindwa, kuniambia nisinywe pombe
anashidwa,
Akaniambia mke wangu naomba tufungue simu
zetu.
Nikamwambia sio tu kufungua yani yangu hata chini sitakaa niiache.
Nitaenda nayo mpaka chooni. Nikaweka pw kila kona, japo sikuwa wala na baya la
kufanya.
Nikawa nawaza nifanye nini ili roho yangu isikie
raha?
Miezi mitatu nilikuwa nikinywa tu pombe huku nawaza nifanye
nini.
Je nimpige ama kumfanyizia Husna? Je nimfanyeje? Nikaona haya yote
hayamfai.
Nikajikausha kama sio mimi, nikaanza kumpotezea, na kuanza
kuishi maisha yangu mimi kama mimi.
Mume wangu akaanza kuwa na wasi wasi
akasema anaomba nisifunge simu yangu, nikamwmabia poa.
Nikafungua pw
zote na nikamwambia simu hii hapa.
Maisha yakaenda.
Baada ya
miezi mitatu kuuisha nikafuatilia nikagundua mume wangu na Husna wameachana.
Hawana mahusiano kabisa, na Husna kapata mpenzi wake.
Nilianza
kumfuatilia Husna kujua mpenzi wake ni wa wapi, na nilijua na kujua ofcn
anayofanyia kazi.
Na baada ya muda nikasikia husna kavishwa pete ya
uchumba. Kwangu ilikuwa ni shangwe siku hiyo. Nilifurahia sana, nilijisikia rah
asana, Nilikunywa sana usiku huo. Husna alikuwa na miaka 25 hivi. Na mpenzi wake
kama miaka 28. Na mimi nilikuwa na miaka 28 na mume wangu miaka
34.
Baada ya kuhakiki kweli husna ana mchumba nilitulia kidogo huku
napanga mbinu zangu za kulipiza kisasi.
Siku moja nilikuwa
nimekaa ofcn,, nikakumbuka Babayake Husna mzee Zuberi Muarabu anapofanyia kazi,
niliinua simu yangu na kutaka kuongea na Huyo mzee nimsikie ni wazee wa aina
gani?
Nilimpigia simu na kuongea naye, alikuwa ni boss wa kampuni Fulani
mahali Fulani. Nikamwambia samahani Baba mimi naitwa Charlote, naomba nije na
cv’s zangu ili kama unaweza unisaidie kazi.
Aliniambia sasa hivi hawana
nafasi za kazi. Nilitumia akili ya kike ya kumshawishi aniruhusu tu nizipeleke
ili likitokea la kutokea basi anisaidie. Alikataa sana, lakini badae
alikubali.
Na ndipo nilisema sasa njama zangu za kulipiza kisasi
zimekamilika.
Siku ya jumatano asbh saa nne nilitoka nyumbani nikiwa
nimevalia vizuri sana kwa heshima, tena kwa kujitanda. Nilienda moja kwa moja
ofcn kwa mzee Zuberi, nilifika nikaomba kuingia ofcn kwake.
Secretary
aliniambia naweza kuingia. Nilingia, ni mtu mzima, nilimsalimia,
nilijitambulisha, Na akanisifia sana na kusema dah, umevalia vyema sana,
sikuwaza kama wewe ni Charlote, pengine ungesema unaitwa Hidaya… nilicheka na
kumueleleza nina shida na kazi. Alishangaa inakuwaje kwa elimu ile sina kazi?
Nilimwambia ninafanya kazi ila sipati mshahara mzuri. Nilimdanganya. Aliniambia
kwa saa hana nafasi za kazi, ila akaniomba nimpe wakati kisha atanitafutia kazi
yeye mwenyewe kwa elimu yangu.
Nilifurahi sana na
kuondoka.
Wakti naondoka alinitazama na kuniiita, Charlote,,, niligeuka
na kusema abee baba.. Aliniuliza umeolewa? Nilimwambia ndio
baba.
Akaniambia, dah,, mumeo ana mke mrembo sana, Nilicheka kwa
kujishebedua kisha nikamfinyia jicho na nikatoka. Lengo langu lilishakuwa la
kishetani, sikuwa na mswalie Mtume tena, nilishajivika uibilisi, sikwua na
huruma hata kidogo.
Nilipokuwa natoka nilipofika reception, Yule dada
aliniambia Umeambiwa urudi.
Ni mara ya kwanza tu nimeonana na mzee
Zuberi, aliniambia Charlote, naomba kesho ninaenda kwenye mkutano mkoani,
tafadhali kama hutajali naomba uongozane na mimi ukafanye kazi zangu.
Ukanisaidie kazi. Nilimueleza kwamba atanilipaje maana nina shida na pesa
nadaiwa kodi ya nyumba, nilidanganya.
Aliniambia unadaiwa shilingi
ngapi? Nilimwambia nadaiwa laki saba na nusu, kodi ya miezi mitatu.
Mzee
zuberi alinitazama kisha akaniambia subiri hapa. Alipiga simu accounts na
kuitisha pesa hiyo. Mh, sikuamini, nilipatiwa Laki Saba na nusu na kuniambia
basi kalipe hizi ili uwe na uhakika usije haribu kazi.
Niliondoka hapo
nikiwa na kicheko cha hali ya juu, na kuanza kuona mission zangu
zikitiki.
Nilifika nyumbani nikiwa na rah asana, nikachukua balantine
yangu na kujidnga kama kawaida.
Mume waangu alirudi na kunikuta niko
njwii. Alianza kuongea na mimi, nilimwambia wala usijali mpenzi, ulilianzisha
wacha nilimalize, mimi sitafanya umalaya ila nitafanya umalaya na balantine,
sitaacha kunywa pombe, ukitaka niache.
Mume wangu alikuwa akiwaza sana
na kujuta kunikosea, ila azma yangu ilikuwa kulipiza kisasi.
Asbh
nilimuaga nasafiri . Aliniuliza naenda wapi sikumjibu.
Niliondoka
nimejiandaa vyema, na kupitia hoteli niliyoambiwa nitafuatwa pale na gari la mr
Zuberi. Kweli muda ule nilikuwa nimeshafika pale, na mr zuberi na dereva wake
waliwasili.
Tulianza safari nje kidogo ya mji, haikuwa mbali sana ni
kama km 60. Na kufikia kwenye hotel ya kifahari, nilifika hapo na Mr Zuberi
aliniambia Charlote wewe ni msichana wa kwanza mimi kukutamani tangu nimeoa, na
sijui kwa nini umenivutia, ila nakupenda sana tafadhali naomba uwe mpenzi
wangu.
Kwangu hii haikuwa na shida kwani ndicho haswa
nilitaka.
Sikujali hata kidogo, nilijivunga na kulalamika shida ya
maisha, na aliniambia atanisaidia kwa chochote nitakacho. Na akanihakikishia
uhakika wa maisha.
Tulilala hotelini hapo siku tatu, kisha siku ya nne
tukarudi.
Mume wangu niliporudi aliniuliza nilikuwa wapi, nilimwambia
aniache, alishikwa na hasira na kunipiga, nikamwambia umeharibu sana kunipiga,
nikaanza kufungasha niondoke.
Alipogusa pochi yangu alikuta pesa taslimu
milioni moja na laki mbili, akaniambia pesa hizo nimetoa wapi? Nilimwambia ni
zangu na asinibabaishe, alizichukua pesa zile,na kisha kunifungia chumbani kisha
kumuita mdhamini wa ndoa yetu na mkewe.
Walikuja na tukakaa kikao.
Tuliongea sana na nikasema nilikuwa nimeenda kupumzika kwa hasira, hivyo aniache
kwani alikwua na mahusiano na husna. Mume aliomba msamaha sana na kusema anaomba
yaishe, na akaomba nifungue simu yangu.
Nilifungua na akanirudishia pesa
na kuniambia yaishe , nikamwambia poa. Ila bado nilikuwa na
kisasi.
Tuliishi maisha ya mimi kumficha sana mume wangu tabia zangu na
hakuwezi kunikamata kabisa.
Mwezi mmoja kabla ya harusi ya Husna,
nilihama kwa mzee Zuberi, na sas nilitaka kuwasiliana na Majidi, mpenzi na
mchumba wa Husna, hii ilikuwa ngumu kidogo. Kwani Majidi alikuwa ni mfanya
biashara na alikuwa na duka kubwa la kuuza tv, simu na vifaa vya umeme, hivyo
ningeenda pale ningeonekana. Na pengine Husna angepewa
taarifa.
Nilijiuliza nitawezaje kumpata Majidi? Ohoooni rahisi sana. Ni
rahisi sana, Niliangalia bango la tangazo la biashara yake, na namba za simu
niliziona.
Nilichukua namba za simu na nikasema nitampigia, ila
nitamwabia nini? Hiyo ilikuwa juu yangu.
Wakati huu mzee Zuberi
alishanieleza kamba binti yake anaolewa siku za usoni. Na nilikuwa namsifia sana
na kumwambia una bahati kuozesha binti kwani sio kila mtu anaozesha
bintiye.
Na yeye alifurahia sana na kunipenda sana, sikuwa mapepe na
alinisifia namna ambavyo namheshimu yeye na mkewe kwani huwa sipigi simu wala
kumsumbua kabisa akiwa nyumbani.
Mzee wa watu maskini asijue nini lengo
langu.
Charlote, baada ya mume wake kujihusisha na mapenzi na
msichana aitwaye Husna, Charlote anaamua kumtafuta mama wa Husna ili kumueleza
juu ya swala hili akiamini kwamba ni mama mwenye busara ambaye anaweza kumuonya
bintiye kuacha mahusiano na Jones, mumewe Charlote. Lakini kwa bahati mbaya
anakutana na mama ama mke ambaye hana busara wala hekima na kumjibu Charlote
majibu ambayo kwayo sasa anaamua kulipiza kisasi.
Tayari
Charlote ameshaanza mahusiano ya mapenzi na mume wa mwanamke huyo yaani baba wa
Husna, na mapenzi yao yamepamba moto , isipokuwa Charlote anafanya kwa siri sana
ili isijulikane, sijui nini azma yake.
Je kisasi chake
kitafanikiwa ama la?Endelea kujisomea katika sehemu hii ya
Tano.
SEHEMU YA TANO;
Kwa Majidi nilipata mtihani
kidogo mkubwa, sikujua nimuingilieje, na lengo langu ilikuwa kuvuruga na
kuharibu haswa, niliamua kulipiza kisasi ambacho si mama yake Husna wala Husna
ambao wataumia maishani mwao mwote,
Kitendo cha Mume wangu Joe kuwa na
mahusiano na Husna kiliniuma sana, niliumia kwani nilikuwa msichana ambaye
nilikuwa najitunza, nampenda na kumheshimu sana, lakini niliamini pendo lake la
dhati kwangu.
Hiyo haitoshi , kiliniuma zaidi pale ambapoo nilipomuuliza
alikataa na kunifanya mimi ni kama mtoto mdogo na asiyetambua
jambo.
Hizi fikara ndizo ambazo zilikuwa zikizidisha chachu katika
kisasi change, na hata pale akili zinaponirudia na kuona nakosea ninapokumbuka
hayo, hasa maneno ya mama yake Husna eti, KAMTOSHELEZE MUMEO… haya yalinifanya
nishikwe na hasira kama swira aliyepigwa jiwe likamkosa.
Kumtosheleza
ndio nini? Alikuwa na uhakika gani kwamba simtoshelezi? Ohooo,, hivi kumbe
mwanaume akitoshelezwa hatoki eeee.. sasa Jones kilichomtoa ndani ni nini na
kumfuata Husna msichana ambaye kila nilipojaribu kuangalia na kufananisha namna
tunavyoonekana mimi nay eye wala hakunifikia kwa lolote, si umbo, sura , elimu
wala Tabia, nilijiuliza na kukosa jibu.
Kisha nikapata jibu kwamba kuna
wakati wanaume wanapenda wanawake wabaya. Hili ndilo jibu nilipata.
Kwa
uzuri niliokuwa nao, kwa heshima na utii kwa mume na urembo kamwe
usingenifananisha na Husna.
Sura umbo wala tabia ya husna havikuwa
vizuri, na wala hakuwa msichana mrembo. Nilipata jibu kwamba wanaume hupenda pia
wasichana wa SURA MBAYA.
Nilishikwa na hasira kila mara nilipokuwa
nikitafakari haya.
Lakini msaidizi wangu Balantine alikuwa pembeni
akiniliwaza kila nilipokuwa ninapata mawazo.
Mapenzi ama mahusiano yangu
na Mzee zuberi hayakuwa ya furaha wala sikuyafurahia hata kidogo, ni kwa vile
nilikuwa nalipiza kisasi tu.
Jones kilimuuma sana kwa namna
nilivyobadilika , alikuwa akijuta kwa nini nakunywa pombe kiasi kile, nilipenda
pombe sana, niliifurahia, nilikunywa nililala na kuridhika kabisa.
Jones
alianza kukonda na kuwa na mawazo mengi sana, sijui kwa nin…
Kuna wakati
nilimueleza bila kumficha, Husna si yupo, go, nenda she is
available.
Kila nilipomueleza hivyo alichukia sana na mimi
kilinichekesha sana.
Muda ulipita,
Nikiwa nimekaa sebuleni
nilipata wazo jipya, ilikuwa ni siku ya Jumatatu asbh nikiwa namalizia kunywa
juice ili nielekee ofcn.
Nilifika ofcn, baada ya kufungua ofc na
kuangalia kazi zangu za siku hiyo nilijiona nina nafasi.
Mara moja
nilichukua simu ya ofcn na kupiga kwa Majidi.
Halooo.. upande wa pili
ulipokea.
Haloo… nilijibu.
Kisha nikajitambulisha…. Kwamba mimi
ni mteja nahitaji flat screen za sumsang kama pc 10 hivi kwa bei
nzuri.
Majid alionekana kwenye simu kufurahi sana, alitaka kujua
napatikana wapi,,
Nilimueleza kwamba anipatie kwanza bei , nilimpa aina
ya screen na ukubwa.
Aliniambia zinauzwa milioni
1.2.
Nilimuambia nikichukua pc 10 atanifanyia punguzo la bei? Alikubali
akasema ndio atafanya punguzo la bei.
Aliniomba sana tuonane ili tuweze
kuzungumza kwani hana dukani kwa sasa ila ameziagiza na mzigo wake utafika
Zanzibar bandarini muda si mrefu.
Nilimueleza niko na shunguli nyingi,
isipokuwa nitamjulisha nitakapokuwa na nafasi
Alinihoji ni za matumizi
gani,, nilimueleza ni mepata oder kwa mwenye hotel , anataka pc zaidi ya 30. Ila
kwa kuanzia anahitaji pc 10 kwanza.
Majid ni kama aliingia uchizi, kwani
nilimchizisha pia kwa kumwambia nitahitaji simu za mezani extentions, friji za
vyumbani na mazulia.
Aliniambia hivi vyote ana uwezo wa
kuvipata.
Nilikubaliana naye nionane naye siku inayofuata jioni. Na
kumuomba sana hii deal asijaribu kuongea na mtu kwani sitaki kuipoteza, hivyo
asishirikishe mtu ili tusije kosa pesa.
Aliniambia
nisijali.
Nilikata simu na kuachia tabasamu kwani tayari nilishajua
ndege kanasa kwenye mtego wangu, sina haja ya kikimbia pole pole namkuta kwenye
mtego. Maskini Majid bwana harusi mtarajiwa.
Tulikubaliana kukutana
kwenye hotel Fulani na baadae nilikata simu huku nikiwa na furaha
sana.
Siku iliyofuata nilijua fika ninatakiwa kukutana na
Majid, ninamfahamu kwa sura na muonekano wako. Ni kijana mdogo ambaye anaonekana
kujiheshimu, kujipenda na kusaka pesa. Ni kijana mwenye asili ya Kiarabu, ni
mwenyeji wa Tabora, hupendelea kumuita Majidi Muarabu wa Nzega… hivi ndivyo
ilikuwa ukitaka kufika dukani kwake lazma utumie jina hili. Ni kijana ambaye
anapenda maendeleo sana, anajishughulisha mno, mpenda dini yake sana . Na hata
baada ya kuanza kuwa na mahusiano na Husna , husna naye alianza kuvalia vyema,
kwa kujitanda na kujifunika sana, sio husna Yule niliyemuona amevaa leggings na
dress top siku ile niliyopishana naye kwenye ngazi, lakini pia siku nilimkuta
ofcn kwa mume wangu alikuwa kavalia kigauni kifupi sana kilichoacha paja zake
wazi. Nilipokumbuka hili nilianza kupata tena hasira.
Ohooo, sasa
nitafanya hivi, najua umbo langu ni zuri, linavutia, nitavalia vyema kama Salha,
nilimkumbuka Salha, mwanachuo mwenzangu miaka hiyo iliyopita, alinifundisha
kuvalia kama yeye mara kwa mara. Aliniambia nina umbo zuri sana sipaswi
kuliachia ila kulihifadhi kwa ajili ya mume wangu. Mara zote aliponiambia hivyo
tulicheka. Hivyo nilisema sasa nitavalia hivyo.
Nilikumbuka kwamba nina
sketi nzuri ndani, nilikumbuka nina mtandio, nilipoamka ashb
nilijiandaa.
Nilivalia vyema sketi ndefu, sendoz zilizoacha vidole
vyangu vya miguu wazi, na blauzi ya mikono mirefu, kisha nikafunga kitambaa
kichwani na kutupia ushungi, Manshalah,, ungeniona katu usingeniita Charlote,
ungeniita pengine Hidaya jina alilonibatiza Mzee Zuberi.
Pole pole
nilitoka ndani. Jones mume wangu alinitazama, akaniambia wewe… niligeuka
akaniuliza umevaaje hivyo? Nilimtazama na kumwambia kwani
nimevaaje?
Akasema unaenda wapi? Nikamwambia naenda
ofcn.
Akaguna,,, kisha akasema subiri tuongozane. Sikukataa,
nilimsubiri,
Geti lilifunguliwa kisha tukaondoka
kuongozana.
Nilitangulia mbele akafuata nyuma.
Nilifika ofcn
nikashuka, akaniaga na kuniambia siku njema, nilimwambia asante.
Niliona
namna ambavyo Jones anaumia kwa kunikosea.
Lakini hata nilipojaribu
kumhurumia nilikumbuka neno la mama yake Husna,, KAMTOSHELEZE MUMEO… nilijiuliza
tena, hivi wanaume wote ambao wanamahusiano nje ya ndoa huwa hawatoshelezwi?
Nikajichekea tu nikasema ohooo,, kumbe mama husna hamtoshelezi mzee Zuberi ndo
maana akanipenda eee…. Nikacheka na kuingia ofcn na kuanza kazi
zangu.
Nikiwa kati kati ya kazi, nilishtuliwa na binti ambaye
hutuhudumia chai , akiniambia dada Charlote chai tayari
nikuletee..
Niliinua uso wangu kwani nilikuwa busy na kazi, nilimtazama
na kumuachia tabasamu kisha nikamwambia asante, nipatie chai, kisha vitumbua
viwili.
Aliniambia haya dada. Ni binti mzuri anajipenda ana heshima na
hutuhudumia kwa heshima sana, na huwa hunipenda mno. Na mara zote huanza
kuniuliza kama nitahitaji chai. Na wengi humtania na kumwambia Ni miss kampuni
yetu.
Aliniletea chai, nikiwa nakunywa chai, simu yangu ya mezani
iliita, nilipokea.
Mume wangu, alinipigia…. Charlote mke wangu
habari….
Mh… niliguna kwanza,, kisha nikamwambia
salama.
Akaniambia,, tafadhali naomba tutoke wote kwa lunch leo nina
maongezi na wewe.
Nilimwambia sawa haina tatizo.
Kisha nikakata
simu.
Baada ya nusu saa alinipigia tena simu akaniambia nichague nataka
kula nini.
Nilimjibu na kumwambia, unajua choice zangu naomba
nichagulie.
Alicheka kwenye simu kicheko cha furaha, nikajua kapata
faraja.
****************************************************************************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment