Simulizi : Sitoweza Kukusahau
Sehemu Ya Nne (4)
“Nataka nione sura za hao jamaa mara moja la sivyo wote wananyonga,sitaki upumbavu katika jumba langu” Mzee Kibangara akafoka kwa hasira huku chembe chembe za mate zinarukaruka toka kinywani,ni hasira zilizopea,mkononi mwake akiwa ameshika bastola,akaendelea kusema.
“Tena nawapa masaa matano tu,niwe zimesiona sura hizo hapo,kama kuna mtu ameshindwa kazi basi aseme nimfute kazi,mimi sioni hasara kufukuza kazi mtu.Kama kuna aliyechoka kazi apite mbele” Mzee Kibangara akafoka mno,mara mmoja wa wafusai wake akapita mbele huku akiwa ameweka mikono nyuma kama ni ishara la heshima kwa mzee huyo.
“Wewe ndio umechoka kazi?”
“Ndio bosi” jamaa huyo akajibu kwa ukakamavu huku akionesha wasiwasi mwingi.
“Hahaha kwa hiyo nikupe msharaha wako uondoke?” Mzee Kibangara akauliza.
“Ndiyo bosi”
“Vizuri kijana,kuna mwengine?” akauliza tena,tena mwingine akatokea.Mzee Kibangara akastaajabu kwa nini wafuasi wake ambao wamekula mazoezi ya kutosha na mikutuo ya aina yake,halafu leo wanataka kuacha kazi kirahisi namna hii.Akawapatia kisawasawa.
“Hey come with brificase” Mzee Kibangara akaamulu mfuasi wake mmoja na baada ya sekunde tano akawa amefika na brifikesi,akalitazamisha kwa bosi wake,likafunguliwa na kukuta kuna noti za elfu kumi kumi zikiwa zimejaa brifikesi zima.
“Ni zaidi ya bilioni mia tisa na hamsini za kitanzania,je mnataka niwape kiasi gani?” Mzee Kibangara akawauliza jamaa hao,lakini wakabaki wakitazamana tu na wasijue cha kujibu.
“Nawauliza kwa mara ya mwisho,MNATAKA KIASI GANI?” safari hii akasema kwa sauti kubwa na kuwafanya wafuasi wake wote washtuke.Bado wakaendelea kutazamana,haikuchukua sekunde tano,Mzee kibangara akainua mkono wake ulio na bastola na kufyatua risasi mbili zilizomfikisha mpaka chini mmoja wa wale wa kuacha kazi.Akabaki mmoja akiwa anatetemeka sana.Wakaotwa wanawake watatu huku wakiwa na nguo zilizowaacha wazi sana kwenye miili yao,wakaambiwa wamchukue jamaa huyo na kwenda kummaliza taratibu.Kwa kweli hakukuwa na mtu ambaye alifanikiwa kuacha kazi na kujikuta anatoka katika jumba lile akiwa salama,wote waliambulia kifo cha kikatili.
Muda wote huo wakati zoezi la Mzee Kibangara na wafuasi wake ambao walikusanywa kwenye ukumbi wao,Ramso na Mtoto wake Gadna,wakapata kutoka kwenye chumba kile na kujivuta mpaka kwenye mlango mmoja wa lile hekalu,kabla hawajafika mahali popote,wakashtukizwa kwa kuwekea bunduki nyuma ya vichwa vyao.
“Tulia hakuna kupiga kelele,tulieni hivyohivyo”Inspekta Makurumla akasema huku akiwa ameishika bunduki hiyo kwa umakini sana.
“Piga magoti wote” Ramso na Gadna wakapiga magoti na kukaa kimya huku wakitetemeka kwa hofu.
“Naomba funguo za geti,haraka sana”
“Funguo za geti!” Ramso akashangaa sana,akajua kuwa na jamaa huyo pia alikuwa ametekwa kwenye lile hekalu na anataka kutoka nje kama alivyo Ramso na mtoto wake Gadna.
“Leta funguo eboo! nitakumwaga ubongo” Inspekta Makurumla akasema kwa mnong’ono mkubwa uliojaa hasira.
“Kaka mimi pia nataka kutoka sina funguo zozote kaka” Ramso akajaribu kujitetea lakini akapigwa na kitako cha bunduki na kumuangusha chini.
“Usimuue dady” Gadna akawa anasema huku machozi yanamtoka.
“Shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Kelele wee mwanaharamu” Inspekta Makurumla akafoka.Ni kweli hakujua kuwa Ramso na mtoto wake nao wapo katika harakati za kutoka kwenye jumba hilo,hakujua kabisa kuwa Ramso ndiye mtu ambaye alikuwa anamtafuta toka zamani sana kwa tuhuma za ujambazi na uharifu akishirikiana na Zulfa.Akili ya Ramso ikaanza kucheza mara mbili mbili na huku akijaribu kuikumbuka sauti ya Inspekta Makurumla,ni sauti ambayo sio ngeni masikioni mwake.Akainuka na kunyoosha mikono juu na kuanza kusema.
“Najua unataka kutoka humu ndani mr,lakini hata sisi pia tunataka kutoka humu ndani,wewe ni mateka na sisi ni mateka,suala la kuanza kupigana na kutoaminiana linaweza kutumaliza maisha yetu sisi sote na hawa binadamu wanyama,tumeteswa sana,kwa kweli,tafadhali shusha silaha yako chini na kuanze kuajadili jinsi gani tunaweza kutoka kwenye jumba hili.” Maneno hayo yakamuingia vizuri Inspekta Makurumla na kumfanya aanze kushusha bunduki yake chini taratibu,akaanza kuamini maneno ya Ramso.
“Unaitwa nani?” Inspekta akauliza.
“Franko” Ramso akajibu.
“Haya tunaazaje kutoka humu ndani?” akauliza,wale askari wenzake waliojificha kwenye sehemu ile,wakachomoka na kwenda pale alipo mwenzao mara baada ya kumuona ameshusha silaha yake chini.Ramso akainuka na kumbeba mtoto wake vizuri akaanza kutembea.
“Nifuateni huku” Ramso akajibu.Katika siku za nyuma,kipindi anafanya kazi katika jumba lile,akaweza kuabini kuwa kuna njia za siri ambazo hutumiwa na wafuasi wa humo ndani,ni milango midogo ambayo sio rahisi kwa mtu mgeni kuigundua.Wakaanza kutembea huku wakiwa makini sana.Inspekta Makurumla yeye ndiye aliyekuwa nyuma huku akihakikisha kuna ulinzi wa kutosha kwa upande wao.Kazi ya kutoka nje kupiti milango ya siri ilikuwa rahisi sana kwani wafuasi wote wakati huo wamekutanishwa na mzee Kibangara kwenye ukumbi wao.Hata wale ambao wanashungulika na kuliendesha jumba hilo kwa kutumia kompyuta zilizo katika chumba maalumu hawakuwa na muda wa kuendelea na kazi zaidi ya kuja kumsikiliza mkuu wao anasema nini na ndio sheria moja wapo ya Mzee Kibangara.
Wakapenya wote na kujikuta wamefika nje kabisa,wakaanza kutoka mbio kusudi wasije kuonekana na kamera za CCTV.Wakakimbia na kuacha eneo hilo mita nyingi bila kukutana na mtu wa aina yoyote.Wakafika mahali kwenye mti wenye kivuli,wakaamua kuketi na kupumzika kabla hawajaanza tena safari yao.Kitu cha ajabu kilichomshangaza Ramso,ni kitendo cha Inspekta Makurumla kuikoki bunduki yake na kumuelekezea Ramso ambaye wakati ameketi na kujiegemea kwenye shina la mti huo.
“Upo chini ya ulinzi” Inspekta Makurumla akasema huku macho ameyakaza……………
“Kuna nini mkuu?” askari mmoja akauliza kwa mshangao,kwani ni kitendo cha ghafla sana kwa Inspekta Makurumla kubadilika namna ile.
“Huyu tulikuwa tunamtafuta kwa muda mrefu sana,ni jambazi sugu alikimbia miezi mitano iliyopita,na sasa nimempata leo” Inspekta Makurumla akasema huku akimuarisha Ramso asimame juu.Ramso akiwa katika mshangao wa kipekee,akainuka huku akihisi kama ndoto au mkanda wa muvi unazunguka kwenye kichwa chake,lakini haukuwa kama alivyodhania.Akaambiwa anyooshe mikono juu,ndipo akatii amri,wakaanza kutembea huku mtoto Gadna akiwa ameshikiliwa,hakika alistaajabu sana.
****
Jiji zima Zulfa akawa anatafutwa na wafuasi hao ambao walitaka kumtia mikononi mwao na kumpeleke kwa kwa mkuu wao Mzee Kibangara.Wakati wote Zulfa yupo katika mavazi ambayo yanamziba mwili mzima ili asiweze kuonekana kabsa na watu wanaomtafuta.Akapanda gari lake mpaka Buguruni kwa rafiki yake Jamila,kwa bahati mzuri akamkuta yupo anatazama TV kwenye sebule yake.Akakaribishwa na kupewa juisi.
“Shosti kulikoni na haja maguo yako?” Jamila akauliza kwa mshangao.
“Mmmh we acha shoga yangu”
“Ehee niambie,niache namna gani?”
“Ni stori ndefu mno” Zulfa akasema huku anameza fundo la juisi,kisha akamtazama Jamila ambaye muda wote amemkazia macho Zulfa.
“Au umeibiwa?”
“Bora ningeliibiwa ningelishukuru kuliko huu msala nilio nao” akasema Zulfa kwa unyonge sana,akaanza kumuelezea kitu kinachomsumbua kuanzia mwanzo mpaka mwisho.Jamila akamzam mara mbili mbili Zulfa,kisha akasema.
“Itakuwa kuna kifaa wanakitumia kukutafutia na kama sio kifaa basi kuna mtu wa karibu yako anawapa taarifa” akasema Jamila kwa umakini sana,maneno hayo yakamuweka katika usikivu mkubwa mno Zulfa.
“Ahaa sasa hapo nimekumbuka” Zulfa akasema
“Umekumbuka nini?”
“Kila kiniwasha simu yangu,GPS inawaka na kuna kijialama chekundu kinawaka” Zulfa akaeleza.
“Ehee mimi kuna rafiki yangu wa Kariakoo,anauwezo wa kuhack hao jamaa wanaokusumbua,subiri nimpigie simu” Jamila akatoka na kuingia chumbani kwake,akarudi na simu yake,akabonyeza namba na kuiweka simu sikioni,baada ya sekunde chache simu hiyo ikapokelewa.Jamila akaeleza kila kitu na ndipo alipoambiwa kuwa waende ofisini kwake.
Hawakutaka kuchelewa wakachukua gari na safari ya kwenda Kariakoo ikaanza.
“Usiwashe simu yako,maana hao jamaa yako wanaweza kutuibukia sasa hivi” akasema Jamila na safari kuendelea.Baada ya kufika Kariakoo,wakaingia kwenye ghorofa moja iliyochakaa kidogo,wakaanza kupandisha ngazi kuelekea juu,ila kabla hawajafika wakasimamishwa na njemba mbili ambazo zimeshika bastola mkononi,Jamila akaeleza kuwa anamiadi na bosi wao,bila kipingamizi wakaruhusiwa na wote wakaingia ndani.Wakakuta mlango ambao ulitakiwaq ufunguliwe na namba za siri hapo ndipo walipokwama,ikawalazimu wapige sim,wakafunguliwa na kuingia ndani.
Ndani humo wakakutana na mtu ambaye ni mwembamba kiasi ambaye anaendesha chumba kizima kilichojaa kompyuta huku akisaidiwa na jamaa mmoja ambaye nae yupo bize na kazi zake.Kwa jinsi chumba hiko kilivyojaa kompyuta,Zulfa hakuamini kabisa kama mtu huyo mwembamba mwenye umbo dogo ndiye anayecheza na mitambo hiyo.
“Karibu Qeen Jamila,leo umekuja na mtoto mzuri eeh” Jamaa huyo akasema
“Aaaah huyu rafiki yangu bana,anaitwa Zulfa,ndio yule mwenye matatizo niliokuambia” Jamila akasema na kumfanya jamaa huyu amtazame Zulfa ambaye amevaa baibu huku uso wake akiwa ameuachia kwa kujifunua ijabu yake.
“Ahaa okay karibu sana mgeni wangu,naitwa Prince”
“Asante nimekaribia” Zulfa akajibu.
“Hebu nipe simu yako” jamaa huyo akapewa simu na Zulfa kisha akaiwasha,ile simu inakaa vizuri tu GPS ikajiwasha na baada sekunde kama tano kijitaa chukundu kikawaka kwenye simu hiyo,akachukua waya wa USB ana kuinganisha kwenye kompyuta yake na kuanza kubofya sehemu anazozijua yeye mwenyewe.Wakati wote huo Zulfa na Jamila wakawa wanashangaa tu kile chumba,kwani kilikuwa kidogo na kimetapakaa kila aina ya mitambo,kompyuta zipatazo kumi zikiwa zimezunguka chumba kizima huku zimewashwa ,wakaendelea kushangaa vingi mno,katika kompyuta moja iliyo upande wa kushoto kwao,hiyo ikawa inaonesha mandhari ya nje,inaonesha jinsi watu wanavyoendelea na kazi zao za kila siku mjini Kariakoo.Kompyuta ya pili kutoka ile ya kwanza ikawa inawaonesha walinzi waliokaa nje huku wakiwa makini mno katika suala zima la kuweka ulinzi ndani humo.
“Umesema unaitwa nani vile?” Prince akauliza huku akimtazama Zulfa.
“Zulfa”
“Ahaaa,kwenye simu kuna mtandao mkubwa sana unakufuatilia,ni zaidi ya kompyuta saba zinakutafuta popote uendapo,yaani hapo ulipo ukiwasha simu tu basi wanajua mahali ulipo na lazime wakupate”
“My God,nitafanyaje?”
“Usijari hapa ndio umefika bibie nataka niwafunge wasiwe wanakuona kabisa”
“Sawa nitashukuru sana”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jamaa huyo anayejiita Prince akaendelea kuichambua simu ya Zulfa kiutaalumu zaidi,lakini wakati zoezi hilo linaendelea,mara wakashtuka kuona watu wakiwa wamevalia mizula iliyowaziba vichwa vyao na kubakiza macho tu,wakiwa wameshika bastola zao,kwa kupitia kwenye kompyuta inayoonesha walinzi wa nje,Prince akashtuka na kuiendea Kompyuta hiyo.Walizi wote wawili wakapigwa risasi na kupoteza maisha yao hapohapo,ikawa ni taharuki ndani ya chumba hiko cha Prince.Bila wasiwasi Prince na mwenzake wakaanza kubonyeza kompyuta zao na kufungwa mageti muhimu ya kuingilia chumbani humo,baada ya kumaliza wakakaa kwenye viti vyao huku wakitoa pumzi ndefu.
“Wakina nani hao” Jamila akauliza kwa wasiwasi.
“Mmmh sijajua ila ngoja niwatazame kwa kupitia mashine yangu” Prince akaendelea kubofya mashine yake lakini alipokuja kushtuka mlango wao unagongwa,kimya kidogo ikaingia huku wakiwa wanatazamana tu,wote macho yao yamewaivwa utadhani wamebugia debe la pilipili.
*******
“Hakika binadamu hatuna shukurani,nimewaokoa kutoka kwenye tundu la sindano lakini leo hii unataka kunihukumu kwa kosa ambalo sio la kwangu,kosa ambalo limesababishwa na yule ambaye mmemkimbia,hakika huwezi kutokomeza ujambazi na ugaidi pasipo kumnasa yule anayesababisha ugaidi na ujambazi,kunifunga mimi sawa sawa na kuongeza vijana elfu moja kwenye ugaidi hapa duniani…” Ramso akawa anatoa ya rohoni huku mikono yake ikiwa kichwani na mtutu wa binduki ukiwa nyuma ya kichogo chake.Maneno ya Ramso yakaanza kumuingia vizuri Inspekta Makurumla lakini akakumbuka vizuri miiko ya kazi yake,akajikuta anamkaza sauti na kumsukumia mbele Ramso.
“Acha kuongea upuuzi wako,utaenda kueleza huko kituoni,na lazima umtaje aliyekutuma uwe jambazi” Inspekta Makurumla akfoka huku macho yake yakiwa mekundu mno.
“Nitakutajia hata sasa hivi,tena ukitaka hata anakokaa nitakupeleka tu” Ramso akajibu kwa hasira,kitu ambacho kikamfanya Inspekta Makurumla apandishe jazba,akampiga na kitako cha bunduki sehemu ya mgongoni,Ramso akaanguka chini kwa mara ya pili kama mzigo.
“Nitakuwasha risasi ya kichwa upotee duniani,paka wewe,ongoza mbele” Inspekta Makurumla akaanza kumsukuma Ramso na safari ya kutoka kwenye msitu huo mdogo ulipo bunju ikaendelea.Haikuchukua muda wakajikuta wanaibukia barabara ya vumbi,wakaendelea kusonga mbele huku kila mmoja akiwa kimya.Kwa mbali wakaiona gari inatokea nyuma yao.Mmoja wao akasimama katikati ya barabara na kunyoosha mkono juu kwa ishara ya kulisimamisha gari hilo.Haikuwa rahisi kwa gari hilo kusimama lakini haikuwa bahati yao,gari hiyo ndio kwanza ikaongeza kasi na kukata barabara hiyo huku vumbi jingi likiwa linawafunika.
Ramso akawa anayazama tu yote hayo,lakini akaanza kuvuta picha endapo atafungwa gerezani,hali ya mtoto wake Gadna na mke wake watakuwaje.Je ni nani atawapa huduma muhimu,maswali mengi yakaanza kuingiwa kwenye kichwa cha Ramso bila kupatiwa majibu.Hakutaka kitu kama hicho kitokee,amekwishapia mambo mengi sana tangia mama yake mzazi afariki dunia,mikutuo aliyoipata ikaanza kumtia hasira na hapo ndipo mwili wote ukaanza kuchezwa na vijidudu wenye dukuduku kubwa la kumgeukia Inspekta Makurumla ambaye anasimamia misingi ya kazi yake ya upolisi…………
Kwa kasi,Ramso akajigeuza kumrukia Inspekta Makurumla na kumpiga roba ya nguvu,lakini roba hiyo haikuchukua muda sana kwani wale askari wengine wakawa wamemvamia Ramso na kuanza kumshushia kipigo.Mpaka wanakuja kumuacha damu nyingi zikawa zinamvuja kupika kiasi,Gadna hakuwa na jinsi zaidi ya kulia tu humu akimtingisha baba yake ambaye kwa muda amezimia kwa kipigo cha askari wale.Punde ikatokea gari nyingine aina ya Fuso kubwa,walipoipungia mkono ikakubali na dereva mwenye ndevu nyingi akashuka huku akitazama tazama huku na huko.
“Tunaomba utufikishe mjini mwana mkubwa” Inspekta Makurumla akasema na bila kupinga jamaa huyo akawaruhusu na safari ya kutoka kwenye eneo hilo ikakamilika.Walipofika bunju ndipo fuso hiyo inapoishia wakashuka na kuomba mawasiliano.
“Jambo afande”
“Jambo jambo”
“Mkuu Inspekta Makurumla naongea nikiwa Bunju tunaomba msaada wa gari mkuu” Inspekta akasema na maongezi yao yakaisha.Wakamchukua Ramso ambaye hajitambua kabisa na kumsogeza mpaka hosptali,hapo ndipo akawa amepatiwa huduma ya kwanza kabla ya kuchukuliwa kwenda hosptali nyingine akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi akishikiliwa kama jambazi mkubwa.Insp Makurumla akachukuliwa na gari mpaka kwake Mbezi na huko akakuta familia yake ikiwa na huzuni lakini baada ya ujio wake wakaanza kufurahi,kwani ulikuwa muda mrefu sana.
“Hubby tulikumisi sana” mke wake akasema huku akiwa amemkazia Inspekta Makurumla usoni.
“Mke wangu,nilikuwa na majnga makubwa mno,yaani namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kutoka huko ndani” Inspk Makurumla akasema huku akinywa bia yake.
“Mmmh pole mume wangu,Mungu ni mwema siku zote”
Mazungumzo yao yakadumu kwa muda wa nusu saa mzima,ndipo wakajikuta wanatoka sebleni ikiwa saa tatu na nusu usiku,wakaingia chumbani na kujilaza huku Inspekta Makurumla akiwa na uchovu wa aina yake,majeraha ya mijeredi ambayo aliadhibiwa na wafuasi wa Mzee Kibangara.
******
Mlango wa chumba kilichosheheni kompyuta tele ukaendelea kugongwa bila kupoteza matumaini,Prince akaiseti kamera moja inayoonesha mandhari ya nje ya mlango huo kisha akawaona walinzi wake wawili wengine wakiwa wamewashika kabali adui zao.Taratibu mlango ukafunguliwa kwa kuruhusiwa na kompyuta,wakaingia walinzi hao wakiwa na jamaa mmoja aliyeshikwa kabali bila huruma.
“Wengine wako wapi?” Prince akauliza.
“Tumewamaliza basi” jamaa moja akasema.Mfuasi huyo aliyeshikwa kabali kisawasawa akakalishwa kwenye kiti na kufungwa mikono kwa nyumba kwa kutumia mnyororo mgumu,wakawa wanamuhoji mambo kadhaa.
“Nani kakutuma?” Prince akauliza.
“Hakuna” jamaa huyo akajibu kwa kiburi,kitu ambacho kikamfanya jamaa aliye pembeni yake kuchomoa kisu na kumchoma nacho kwenye paja,ukelele mkubwa ukatokea kwa jamaa huyo huku akiumanisha meno yake kwa maumivu makali anayoyapata,wakaendelea kumuhoji kwa maswali mengi mno.
“Tunakuuliza tena,umetumwa na nani?”
“Mz…ee” akaongea huku akitoa kelele ya maumivu.
“Mzee gani ongea vizuri”
“Mzee Kiba..” akakomea hapo,hakutaka kumalizia jina hilo kwani ni moja ya kuvunja masharti ya Mzee Kibangara.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kumbe wewe umetumwa na mzee Kibangara!” Zulfa akahamaki na kuinuka kwenye kiti chake,akarusha teke moja lilimfikisha mpaka chini jamaa huyo huku mikono yake ikiwa nyuma akiwa amefungiwa na mnyororo.Akainuliwa tena na kupigwa maswali mengine,mpaka anajikuta anatoa siri ya jumba hilo la Mzee Kibangara.Wakamtoa nje ya chumba hiko na kumpelekea kwenye chumba kingine cha mateso.Zulfa alipomaliza kazi yake,wakaondoka na Jamila kuelekea kwao,lakini wakafika njiani wakabadilisha maamuzi mara baada ya Jamila kusema kuwa anataka kwenda hospitali ya Mwimbili kumtazama Shangazi yake amabaye anaumwa.
“Shoga,naomba tupitie Muimbili nikamtazame Anti yangu,ni mgonjwa”
“Ahaa sawa usijari” Zulfa akageuza.Safari ya kuelekea hosptalini hapo ikaanza.Kwa kuwa hakukuwa na msongamano wa magari,wakawa wametumia muda machache sana kuweza kufika kwenye hospitali hiyo ya Taifa.Wakaingia mpaka kwenye wodi ya wanawake na kumkuta mama mmoja akiwa na ndugu zake pembeni,mama huyo ambaye amekonda kiasi,inaonesha wazi kuwa ni mgonjwa kupita kiasi,hata kuongea nako aliongea kwa shida sana.Jamila akawa anasalimiana ndugu zake huku Zulfa anaye akifanya hivyo.
“Shangazi pole sana”
“Asante sana mwanangu,Mungu atasaidia tu siku moja”
“Kweli Anti,Mungu atakuponya na utarudia katika hali yako ya zamani”
“Ameen”
Baada ya kumaliza maongozi hayo na kumfariji shangazi yao,Zulfa na Jamila wakatoa pesa ambayo itamsaidia shangazi yao kwa siku za mbele zijazo.Wakatoka na kuelekea nje,lakini kabla hawajalifikia gari lao,wakakutana na mtoto Gadna,akiwa amelala chini ya sakafu,pembeni yake wamesimama asakri wawili nje ya mlango.Gadna akiwa ameshikwa na baridi,baada ya kuwaona Zulfa na Jamila akainuka na kutaka kuwafuata,ukurupukaji wake huwezi kuutofautisha na mtu ambaye alikuwa anaota toka usingizini.Askari hao wakamkamata Gadna na kurumdisha mahali pake huku aking’ang’ania baibui la Zulfa.
“Kwani vipi,huyu mtoto mbona yupo hivi?” Zulfa akauliza.
“Huyu mtoto ni mtoto wa mtuhumiwa ambaye ni mgonjwa,yupo humu ndani”
“Ahaa kwahiyo mbona anaonekana kuwa na homa huyu?”
“Ebuu kelele,hujui kuwa sisi ni polisi?”
“Haijalishi,huyu ni mtoto mdogo sana,anahitaji huduma na sio kumtesa eti kisa baba yake mtuhumiwa” Zulfa akasema kwa sauti ya uchungu mno,maneno hayo yakawafanya askari hao watazamane kisha wakatingisha kichwa kuashiria kuwa kuna ukweli ndani yake,mtuhumiwa na mtoto wake ni vitu viwili tofauti sana,mtoto anahitaji kutunzwa bila kuangalia kosa la baba yake.
“Haloo dada,kwa kweli sisi tumeagizwa tu,na tumeambiwa tukae naye huyu mtoto pamoja na kumlinda baba yake asije akatoroka,maana ni jambazi sugu aliyetafutwa kwa miezi sita” polisi mmoja wapo akajieleza
“Jambazi sugu?”
“Ndio”
“Haya ninaweza kumuona huyo jambazi?”
“Aisee hapana huwezi,kwanza tunafanya makosa kuongea na wewe hapa” polisi akasema
“Basi naomba nimsaidie huyu mtoto wake” Zulfa akaendelaea kuongea kwa huzuni,hali ya Gadna ikamfanya awe na huruma huku akiwa na uso wa unyonge pale anapomuangalia mtoto huyo.Hakufahamu huruma juu ya mtoto huyo imetokea wapi,hakika hakupenda kitu anachofanyiwa mtoto Gadna na askari hao.
“Huwezi kuondoka naye kirahisi hivyo,mpaka aje mkuu wetu hapa”
“Ok sawa” Zulfa aliposema hivyo mlango wa chumba hicho ukafunguliwa na daktari wa makamo akatoka.Zulfa ana Jamila wakaanza kumfuata nyuma na hatimaye wakamfikia.
‘Samahani dokta tunaweza kumuona mgonjwa liye kwenye chumba unachotoka?”
“Mmmh mimi sihusiki kabisa na hilo,labda mzungumze na hao polisi” Dakatari huyo akasema na kuanza kuondoka kwenye eneo hilo.Zulfa na Jamila wahakuwa na jinsi,wakajikuta wanageka walikotoka,wakawa wanamtazama Gadna ambaye analia machozi,sura yake imekuwa nyeusi kwa kutopta maji kwa muda mrefu,vipere na mabaka mbalimbali kwenye mwili wake havikuisha,kutokana na mbu ambayo wanamshambulia usiku kucha.
“Shoga tuondoke,huyu mtoto atakusaidia nini?” Jamili akasema
“Hapana,nimejikuta namuonea huruma mtoto huyu,nataka nikamchukue nikaishi naye.Halafu kuna kitu nahisi hapa” Zulfa akasema huyu amemkazia macho Jamila.
“Kitu gani hicho”
“Subiri utaona mwenyewe,kama ni kweli”
Walipotazama muda wakabaini kuwa imekwishatimia saa kumi na nusu jioni,wakaaanza kushusha nagzi kuelekea kwenye gari la Zulfa,lakini muda wote Zulfa akabaki anamtazama Gadna ambaye anamlilia kwa uchungu pale kwa askari.
“Nichukueee,nakuomba nichukue Dady anaumwaaa” Gadna akalia kwa uchungu mno kiasi kwamba Zulfa akashindwa kuingia kwenye gari yake,akabaki akaimtazma mtoto kwa uchungu,taratibu akafunga mlango na kuanza kumfuata tena.
“Sasa Zuu unaenda wapi jamani,muda umekwend nataka kwenda kupika miee” Jamila ambaye tayari yupo kwenye akaongea huku akimshangaa Zulfa.Kabla hakumfikia mtoto huyo akashangaa polisi hao wanapiga saluti na kumkalibisha mkuu wao ambaye ni Inspekta Makurumla.Zulfa hakuweza kuisahau sura hiyo,moja kwa moja akajigeuza na kuficha sura yake……
“Vipi usalama upo?”
“Ndio mkuu”
“Ok wacha nimcheki huyu jamaa” Inspekta Makurumla akaingia ndani ya chumba hicho alicholazwa Ramso,akafunga mlango na kuketi pembeni ya kitanda.
“Unaendeleaje?” Inspekta akamuuliza Ramso ambaye yupo macho pale kitandani huku akiwa na pingu mkononi.
“Naendeleaje kuhusu nini?” Ramso akajibu kwa dharau huku akitazama upande mwingine.
“Haha haha nilijua tu lazima nikutie mikononi mwangu,huwezi kunikimbia”
“Naomba nimuone mwanangu”
Inspekta Makurumla anamuita Gadna na kuingia ndani,akaa pembeni kwa baba yake huku machozi yakimtoka.
“Dady nataka Mumy,where is Mumy” Gadna akawa analia na machozi yakaanza kulowanisha mashavu yake,Ramso akainuka japokuwa ana pingu mikononi akajikaza na kukaa.
“Usijari Mwanagu nitakupeleka usijari” Ramso akawa anamfariji mtoto wake japokuwa haelewi kama ndio atakuwa amefungwa ama laah.
Nje Zulfa akaingia kwenye gari lake na kuutazama mlango wa chumba kile alicholazwa Ramso,hakujua mtu ambaye anaumwa mule ndani ni mmoja kati ya watu aliowahi kufanya nae kazi.
“Tuondoke basi Zuu mbona hivyo?” Jamila akasisitiza sana,lakini Zulfa hakutaka kabisa kuondoka kwenye eneo lile,kikubwa anachokitaka ni kujua ni mgonjwa gani aliye ndani ya chumba hicho na pia anataka kuondoka na mtoto huyo ambaye anateswa na wale askari wasiopenda kusikiliza watu.
“Shoga subiri basi” Zulfa anasema hivyo mara mlango ukafunguliwa na Inspekta Makurumla akatoka akiwa na Gadna,huku nyuma yake kuna Ramso mwenye pingu mkononi pamoja na daktari.Zulfa akawa kama aliyepigwa na shoti ya umeme,hakuamini mtu anayemuona mbele yake,alijua fika kuwa Ramso yupo Afrika Kusini,lakini leo hii amekamatiwa mikononi mwa polisi,hakujua kwa kweli Ramso kakamatwaje.Akataka kutoka nje na kumkimbilia,lakini Jamila akawahi kumzuia na kumsisitiza asifanye kitendo kama hicho.Inspekta Makurumla,Ramso,Gadna pamoja na askari wawili wakaongozana na daktari mpaka ndani ya ofisi yake.Baada ya dakika kama tano wakatoka kwenye ofisi hiyo na kuingia ndani ya gari.Ikawa inatoka kwenye eneo hilo,Zulfa hakutaka kuliacha nae akawa analifuata kwa nyuma mpaka walipokuja kusimama kwenye kituo ambcho Zulfa hakuweza kukisahau kabisa,ni kile kituo cha kwanza alichowahi kuwekwa akiwa na Ramso pamoja na Peter.Wakaiweka gari pembeni na kushuka.Imekwishahitimu saa moja na nusu ya usiku,giza likaanza kufunika jiji la Dar es salaam.Ramso akawekwa rumande na Inspekta Makurumla akamchukua Gadna kisha akaondoka nae mpaka nyumbani kwake Mbezi.Zulfa akawasha gari yake na safari ya kumrudisha Jamila ikaanza.Njia mzima kichwa chake kikajaa mawazo ni kitu gani kimemkuta Ramso mpaka amekamatwa na sehemu gani.
“Au itakuwa hakwenda Madiba?” maswali mengi yakaanza kujaa kwenye kichwa chake huku asielewe aanze lipi kujijibu,hakika fumbo hilo likawa mtihani kwake kuweza kulifumbua.Tayari alikwishafika barabara kuu ya kwenda Morogoro,na sasa akawa anavuta moto kuelekea Mbezi mwisho.Alipofika tu hakutaka kuchelewa akaingia chumbani kwake na kufungua kabati lake kisha akatoa nguo zake,jinsi ya kipira nyeusi,tisheti nyeusi,mzula wa kuzuia uso mweusi,grovusi za mikononi nazo nyeusi,buti nyeusi zenye muundo wa kijeshi,akachukua na kisu kisha akakichomeka kwenye buti lake,bastola ikafichwa kiunoni na kumalizia na koti ndefu.Muonekano wake ukawa tofauti kabisa na muonekano wake wa kila siku,leo muonekano wake sio tofauti na ule muonekano wake wa kwanza kule msituni ambako alikuwa na Ramso wakikimbizwa na polisi.Akatoka mpaka nje na kupanda gari yake.Madhumuni makubwa kwake ni kumuokoa Ramso kutoka kwenye mikono ya polisi.Saa yake ya mkononi ikasomeka kuwa ni saa tatu na dakika arobaini na tano,akatumia muda wa lisaa limoja mpaka akufika kwenye eneo hilo la kituo cha polisi.Hakutaka kufanya tukio hilo kwa majira hayo,ikamlazimu asubiri mpaka pale itakapohitimu saa sita sita ndipo aanze kazi yake,akavua koti lake na kuliweka pembeni kisha akatoa bastola yake na kuweka magazini,akachukua kifaa kinachoweza kuzuia sauti ya mlio wa risasi kutoka anakipachika kwenye silaha yake.Sasa akawa anatazama saa yake iliyo mkononi huku akiwa na shahuku ya kumkomboa rafiki yake Ramso.
*****
Kitendo cha Ramso na mateka wake wengine kutoroka ,kikamuweka Mzee Kibangara kwenye wakati mgumu sana,anajua fika kuwa siku na muda wowote atakwenda kuanguka kutokana na siri kadhaa kufichuka,hii kutokana na mtu yoyote ambae amebahatika kuingia kwenye hekalu hiyo basi lazima ataona kitu fulani ambacho akijui.
Mzee Kibangara akaingia kwenye chumba chake kikubwa na kufungu jokofu kisha akatoa pombe kali,akajimimia kwa hasira na kujilaza kitandani huku muda wote akili yake ikicheza ni jinsi gani anaweza kukabiliana na matatizo yaliyojitokeza.Akili yake ikaamia kwenye mteketezi wa mabilioni ya pesa ambazo alitumia kununulia silaha,lakini silaha hizo hazikufika salama nchini Somalia ambako kuna ngome yake ya pili,akajikuta anakunywa tena pombe ile na kuchukua simu toka kwenye meza yake ndogo.
“Hey Mr, I need to bomb Eastern Kenya(Hei bwana,nahitaji kulipua mashariki mwa Kenya” akameza mate kisha akaendelea “Wamenitia hasara kubwa sana na siwezi kuwasamehe hata siku moja aisee,they must pay” Mzee Kibangara akaongea kwa hasira huku misuli ya kichwa chake imejichora dhahiri kabisa,ni kutokana na hasira alizokuwa nazo.
“No worry Sir,we have Hydrogen Booms,na lile la nyuklia lipo,tutalitumia pia” Sauti kutoka upande wa pili ikasikika vyema kwenye masikio ya Mzee Kibangara.
“Yes,kesho nitakuwa hapo”
“Sawa haina neno”
Mzee Kibangara akakata simu na kuitupa kitandani,akajimimia tena fundo la pombe ile kali na kuvumba macho kama ishara ya ukali wa pombe hiyo.Akavaa shati lake lililo pana na kichwani akavaa Pama,akaingia kwenye chumba cha kompyuta na kuketi pembeni huku akimtazama mmoja wa wafanyakazi wake.
“Umefanikiwa kitu gani mpaka sasa?” Mzee Kibangara akauliza.
“Yaa bosi,nimegundua kuwa,mateka waliotoroka juzi wamepitia kwenye mlango mdogo wa dharula ila sijajua wamepotelea wapi mpaka sasa hivi” mfuasi huyo akaeleza.
“Okay endelea kufanya utafiti kisha niambie nini kinaendelea”
“Sawa bosi”
“Na wale waliokwenda kumtafuta yule binti,wamefikia wapi” swali hilo la Mzee Kibangara likamfanya mfuasi huyo akae kimya kidogo bila kujibu.Mzee Kibangara akarudi na kuketi tena kwenye kiti.
“Where are they?(wako wapi?)”
“There opereshion failed(oparesheni yako imefeli)”
Mzee Kibangara akatoka na kuondoka kwenye chumba hicho,mambo yake yakaanza kuharibika,kila alichokifanya sasa kikawa kinafeli.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Usiku wa saa nane akajiandaa vizuri na kuchukua brikesi yake,akaingia kwenye ndege yake ndogo ya kutembelea huku akiongozwa na wafuasi wake kadhaa kuelekea Somalia.Akili yake ilikuwa ni juu ya kulipua Kenya na kufanya kitu ambacho anaweza kurudisha pesa zake kwa haraka ili mpango wake wa kutawala nchi ya Tanzania usiyayuke.Akafika Somalia kwenye ngome yake na taratibu za kuandaa mabomu mazito ambayo yataiteketeza ardhi ya Kenya.
“Hydrogen bomu imekaa poa sana mkuu” Jamaa mmoja akasema huku akivuta stendi ya bomu na kuliweka juu yake huku akisaidiwa na wenzake watatu.
“Nataka nipige pale kwenye Chuo kikuu chao”
“Ahaa ila bosi naona haitakuwa na mashiko”
“Kwa hiyo unatakaje?”
“Nataka tuelekeze kabisa kwenye bunge lao,au tufanye kama mwanzo,tulipue jiji la Nairobi”
Mzee Kibangara akakaa kimya kisha akamtizama mfuasi wake,kisha akarudisha macho kwa mzee wa Kiarabu,akatoa pumzi na kukaa vizuri.
******
******
Saa sita kamili ilipohitimu,Zulfa akavaa koti lake na kushika bastola yake mkononi kisha akaanza kutafuta sehemu ya kuweka kumpitisha ndani katika kituo hicho.Wakati wote alihakikisha kuwa anapita sehemu ambayo haina mwanga wa taa,hatiamaye akafanikiwa kupita ndani kwa kupenya kwenye waya uliozungushiwa fensi,akafikia kwenye bustani ya maua,kisha kaanza kunyata kuelekea mbele zaidi,kwa mbali akamuona askari ameshika bunduki yake huku akivuta na kutoa moshi mwisho wa sigara.Hakutaka kabisa kuipoteza nafasi hiyo,akamnyatia na kuwa karibu naye zaidi,akakichomoa kisu chake toka kwenye buti na kumrukia polisi huyo bila kusikika kishindo chochote kile.Akamvuta pembeni kabisa kwenye giza na kumkandamiza kisu kwenye shingo yake na kumfanya polisi huyo aanze kufulukuta kwa maumivu anayoyapata.
“Shiiiiii! Nitakukata kolomeo”Zulfa akafoka kwa sauti kali ya mnong’ono.
“Niambie wapi alipo mtuhumiwa wenu?” akauliza
“Sij..ui” polisi akajibu na Zulfa akaongeza kumkandamiza kisu shingoni,hali ambayo ikamfanya polisi huyo atahaluki huku akisisitiza kuwa atamuambia alipo.
“Nita..kuambia”
“Niambie haraka”
“Yupo nda..ni” askari huyo akasema huku akihemea juu juu.
“Nipe funguo haraka sana” Zulfa akafoka na askari yupo akatoa funguo toka kwenye mfuko wake,akampatia Zulfa kisha akaiweka mfukoni mwake.Akachukua pingu zilizo kwenye kiuno chake na kumfunga nazo kwenye mlingoti wa chuma,akatoa kitambaa chake na kukipengea kamasi zito kisha akamshindilia nacho mdomono ili asitoe sauti itakayowashtua askari wenzake.Baada ya kuhahakisha kuwa amebadilisha nguo zake na kuvaa sare za askari huyo,akatoka na kueleke sehemu husika huku nyuma akimuacha askari kwenye mlingoti akitweta kwa kasi ya ajabu.Njiasi baadhi ya maaskari wakawa wanaendelea kuweka ulinzi,hawakuwa na wasiwasi wowote juu ya ujio wa Zulfa.Akaingia ndani na moja kwa moja akafika kwenye chumba alichofungiwa Ramso.
“Ramso” akaita kwa kunong’ona na kumfanya Ramso ashtuke.Hakutaka kuitikia badala yake akainuka huku bado mikononi akiwa na pingu zake.
“Zuu” akajikuta anaita jina bila kutegemea.
“Shiiiii,kelele basi” Zulfa akanong’ona huku na kuchukua kijifunguo kidogo cha kufungulia pingu.Akamfungua na wakaanza kutoka nje huku kila mmoja akiwa makini kila kona.Hawajafika nje tu mara mlango wa kutokea nje ukafunguliwa na askari mmoja akaingia akiwa na kirungu mkononi.Giza tupu limetanda ndani ya kituo hicho,ikamlazimu askari huyo kuwasha taa,lakini haikuwa bahati yake,Ramso akamrukia na kumpiga roba kali ambayo ikamlazimu polisi huyo kuachia harufu mbaya katika ukumbi huo.Ramso akafanya vile mpaka alipohakikisha kuwa askari huyo afulukuti tena,tayari ameshaua polisi mmoja,wakaendela na safari yao.Nje wakakutana na askari mwingine,huyu ndiye akashtuka badla ya kumuona Zulfa akiwa kwenye sare za kiaskari wakati jioni hiyo hawakuwa na askari yeyote wa kike.
“Hey simama hapo hapo” Zulfa na Ramso wakasimama.
“Jambo afanye” Zulfa akapiga saluti ili mradi amzuge askari huyo lakini haikuwezekana kabisa,tayari amekwisha waweka chini ya ulinzi na mtutu wake wa bunduki aina ya AK 47.Ramso na Zulfa wakatazama na kuoneshana ishara ya kitu fulani ambacho wanatakiwa kukifanya ndani ya dakika chache kabla ya askari huyo kusababisha maafa yoyote mbele yao.Walipotazama pande zote hawakuona askari mwingine zaidi ya yule aliyewasimamisha.
“Nataka nnieleze kuwa sare hizi umepata wapi na huyu mtuhumiwa unampeleka wapi?” akaongea kwa sauti ya juu mno.Zulfa akaanza kutetemeka kwa hofu,akaamua kukaa kimya bila kujibu swali hilo.
“Naongea na wewe mala…..” Askari huyo kabla hajamalizia sentensi yake akaanguka chini na sauti ya maumivu ikawa inamtoka,ngumi mzito iliyotoka kwa Ramso na kumpata chini ya kidevu.Wakachukua bunduki yake na kuanza kukimbia mpaka pale kwa askari aliyefungwa na Zulfa.Zulfa akachukua nguo zake haraka na kuanza kukimbilia kwenye mpenyo alioingilia nao mara ya kwanza.Wakati huo wote polisi walikwisha sikia sauti ya vishindo vya watu na sauti ile ya askari aliyepigwa ngumi ya kidevu.Risasi zikanza kulia huku tochi zikiwamulika Zulfa na Ramso ambao wapo katika harakati za kutaka kupenya na kutokomea pasipojulikana.Wa kwanza kutangulia kupenya kwenye huo alikuwa ni Ramso huku akifuatiwa na Zulfa,ila kabla hajamalizia kutoka nje,akahisi maumivu makali toka kwenye mguu wake.
“Mamaaaaaaa” ukelele wa maumivu ukatoka kwa Zulfa ambaye amepigwa risasi ya mguuni na askari aliyekuwa anaendelea kuwakabili waalifu hao.Ramso akapigwa na bumbuwazi kwani ni ghafla mno kwa tukio hilo kutokea.Akamnyakuwa Zulfa na kuanza kukimbia nae huku bado askari hao wakiendelea kuwarushia risasi.
“Tunapata wapi usafiri maskini!” Ramso akajiuliza huku amemshika Zulfa kwa umahiri.
“Nimekuja na gari yangu,funguo hizi hapa” Zulfa akatoa funguo na kumpatia Ramso.Wakafanikiwa kuingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi ya ajabu.Hali ya hewa imetulia na mji mzima upo kimya kabisa,sauti iliyokuwa inasikika ni sauti ya gari hilo dogo la Zulfa ambalo linapasua ardhi.Sauti ya ving’ora kutoka kwenye gari za polisi,zikatokea ghafla nyuma ya gari walilopanda Zulfa na Ramso na kuwafanya waanze kupagawa.
“Ra..mso nakufaaa mi..mi” Zulfa alilalamika huku machozi yanamtoka kama mtoto mdogo.Maumivu makali ya risasi yanamtesa ku[ita maelezo.
“Jikaze Zuu tutafika salama”
“Simamisha gari Ramso naumia” Zulfa anaendelea kulalamika na sasa anadai gari isimamishe na wakati gari gari za polisi zinawafukuza.
“Noo Zulfa polisi wanakuja kwa kasi” Ramso akasema na kuongeza mwendo wa gari.Umahiri wa madereva wa gari hizo za polisi wakafanikiwa kulifikia gari hilo ndogo kwa ukaribu zaidi.Wakaanza tena upya kurusha risasi kwenye gari hiyo.Ramso akanyonga breki ya ghafla na kuwafanya polisi hao wakose kona hiyo,wakajaikuta wananyoonga moja kwa moja.Ramso akaendelea kufinya mafuta huko mara nyingi akitazama nyuma na kubaini kuwa amewaacha vya kutosha.Akakata kona nyingine na safari ya kuelekea Buguruni kwa rafiki wa Zulfa ikaanza.Wakafanikiwa kufika kwenye nyumba hiyo salama,lakini bado hali ya Zulfa imekuwa mbaya kuliko ile hali yake ya mwanzo.
“Hodii” Ramso akagonga mlango kwa nguvu sana,baada ya dakika kadhaa akatoka Jamila akiwa amevalia vazi lake la kulalia.
“We nani?” akauliza.
“Nitakuambia naomba unisaidie kumtoa Zulfa amepigwa risasi?” Ramso akasema huku akihema mno.
“Mungun wangu Zulfa risasi!?”
“Ndo hivyo njoo basi” Ramso akisaidiwa na Jamila wakamtoa Zulfa nje gari gari na kuingia nae ndani kisha Ramso akaingia ndani ya gari na kulificha sehemu ambayo sio rahisi kwa gari hilo kuonekana na mpitanjia yeyote.
“Sasa itakuaje na mimi sina dawa hapa?” Jamila akasema huku akionesha kuchanganikiwa na asijue la kufanya.
“Atii unasemaje?” Ramso akashangaa,hofu ikawatanda na wasijue nini kitakachotokea mbele yao kama sio kumpoteza Zulfa ambaye mguu wake bado umefumuka kwa risasi.
“Sasa hakuna daktari yeyote hapa wa jilani?” Ramso akauliza
“Ok nimekumbuka” Jamila akasema na kutoka nje.
“Ra…mso nao..mba univue hili jinzi” Zulfa akaongea kwa shida sana na tena kwa sauti ndogo.Ramso akafanya hivyo kama alivyoambia.
“Asssssiiih taratibu unaniumiza” Zulfa akalalamika huku akiumanisha meno yake kwa nguvu.
“Jikaze Zulfa” Ramso akafanikiwa kumtoa jinzi na Zulfa akabakiwa na taiti tupu.Dakika chache baadae akaingia Jamila akiwa na msichana mdogo kiumri akiwa amebeba begi ndogo.Bintii huyo akatoa vifaa vyake toka kwenye begi na kuanza kumtibia Zulfa.Ramso akatoka nje na kuchungulia barabarani,ghafla akaziona gari hizo za polisi zikiwa zimezimwa king’ora,zikapita kwa kasi sana na kuwaacha wakina Ramso.Akarudi na kuketi kwenye sofa huku akishisha pumzi nyingi.Akili ikaanza kumcheza tena juu ya mtoto wake Gadna,hakuelewa yupo mahali gani mpaka sasa,je ni mzima au amekufa?.Hakupata jibu la aina yoyote.Akaamua kutoka tena nje.Ni kama mtu aliyechanganyikiwa au mgonjwa kichaa,kazi yake ni kuingia ndani na kutoka nje.
“Haiwezekaniiii” akajisemea mwenyewe huku akijipigapiga kichwani.Wakati anaendelea kuwaza nini atakifanya ili aweze kumpata mtoto wake,ghafla akasikia sauti ya ikipiga simu sehemu.Akaelewa simu hiyo ni ya yule binti aliyekuja kumtibu Zulfa.
“NDIO NINAWATIBU HAPA,MMOJA KAPIGWA RISASI YA MGUUNI,MFANYE HARAKA SASA”
Ramso akainuka na kwenda sehemu alipo binti huyo.Akamkuta anaweka simu yake kwenye taiti yake huko chooni.
“Lete simu malaya wewe” Ramso akafoka kwa hasira huku akimshika roba binti huyo.
“Haaa hii huku” binti huyo akasema huku akitoa sauti ya maumivu makali.Ramso bila kusita akaiingiza mkono kwenye tatiti ya binti huyo na kuchomoa simu.
“Haya niambie kakutuma nani upige simu?”
“Mmmh”
“Nyoooo nini nani kakutuma malaya wewe nitakuua sasa hivi” Ramso akaongeza kasi ya roba na kumfanya binti huyu aanze kurusha miguu yake huku akikoroma kama paka.
“Nasemaaa” akasema kwa shida na Ramso akalegeza ugumu wa kabali hilo la kukata na shoga…………
“Nime…tumwa na…naaaa”
“Na nani sema nita..” Ramso akamfuta nywele zake,akaanza kutoa ukelele wa maumivu,ila haukutoka nje kutokana na kuzibwa mdomo wake kwa nguvu na Ramso.Binti huyo akaendelea kusema.
“Nimetumwa na PUNK G”
“PUNK G ndio nani?”
“Ni…jambazi mmoja hivi” binti huyo akaendelea kusema kila kitu huku akiwa na hofu ya aina yake.
“Jambazi gani nyoosha maelezo,nitakufinyanga sasa hivi”
“Ni mtu wa mzee mmoja anaitwa Kimba…ngara sijui”
“Mzee Kibangara!?” Ramso akajikuta anasema kwa nguvu na hapo akajua muda wowote lazima wafuasi hao watakuwa wamewasili kwani huwa hawakawihi hata sekunde moja.Akamrudisha mpaka kwenye sebule na kuwakuta Zulfa na Jamila.Ikabidi washangae kuona kitendo kama hivyo.
“Kwani vipi Ramso?”
“Tuondokeni pamenuka hapa” Ramso akasema na tena kwa msisitizo “haraka sana jamaa wanakuja sasa hivi”.
“Na huyu mbona umumpiga kabali hivyo,hajamaliza kumtibu Zulfa”
“Tutamtibu mbele lakini hapa sio,nimemfuma huyu anapiga simu kwa watu hatari huko chooni” Ramso akasema.Haraka Jamila akaenda kuvaa nguo zake na kurudi kwenye sebule,wakati huo Ramso amekwisha mfunga kamba mikononi na miguuni,pamoja na kumziba kwa bendeji mdomoni,Wakachukua kamba zingine na kumfungia kwenye sofa ndogo.Ramso akambeba Zulfa na kutoka nae nje huku Jamila akiwa nyuma yake.Wakapanda mpaka kwenye gari na kuanza kutimua sehemu salama.Safari hiyo ikapamba moto kuelekea Mbezi mwisho kwa Zulfa,walipofika tu wote wakshuka na kuingia ndani.Taratibu za kuendelea kumtibu Zulfa akachukua Jamila huku Ramso akahangaikia jinsi gani ataweka mambo sawa ikiwemo suala la kumpata mtoto wake Gadna.
******
“No! no! sitaki kujitetea,huo ni uzembe wenu,haiwezekani watu wote sita,mnashindwa kuwamiliki watu wawili” Inspekta Makurumla akafoka kwa jazba huku jasho linamtoka,cheche za mate zinamtoka kutokana na hasira alizonazo.
“Upuuzi huu siwezi kuvumilia,tuliwakama mara ya kwanza,wakatoroka na hii mara ya pili mmewatolosha,sasa basi nawapa masaa manne,niwe nimeiona sura ya Mtuhumiwa huyo hapa ofisini kwangu,la si…” Inspekta Makurumla akameza mate na kusema “KAZI HAMNA”,maneno hayo yaliwavunja sana moyo aslkri hao ambao wamesimama mbele ya mkuu wao,hofu zimewatawala,macho yamewatoka.Kitendo cha Ramso kutoroshwa na Zulfa.
“Ndio mkuu” wakaitikia wote kwa pamoja na kutoka kwenye ofisi hiyo.Inspekta Makurumla akabaki peke yake huku kichwa kikimchemka asijue wapi pa kuanzia.
“Hivi huyu mtu jini au,mbona kila tukimkamata anatoroka,tena lazima aue polisi,kama sio mmoja au wawili” akajisemea peke yake.Hakika alichanganyikiwa mno.Baada ya kutaharuki kwa muda mrefu bila kupata jibu,mara simu yake ikaanza kuita.
“Mme wangu” sauti kutoka kwenye simu ikapenya kwenye sikio la Inspekta Makurumla.
“Naam mke wangu,kwema huko?”
“Sio kwema” kusikia sauti huyo Inspekta Makurumla akainuka kwenye kiti na kusimama huku akivua miwani yake.
“Kuna kitu gani?” akahoji.
“Mtoto uliyemleta haonekani kabisa”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“UNASEMAJE?” Inspekta akahamaki na kubweruka kwa sauti kubwa,hakuamini kabisa kile kitu anachoambiwa na mke wake.
“Hapana,sio kweli,hebu jaribu kumtazama kwenye mpera huko nyuma ya nyumba”
“Kote hayupo”
Inspekta Makurumla akabaki amechoka,kama presha imepanda na kushuka,sasa kilichobaki ni haja kubwa ambayo inapiga hodi na kurudi mara kadha bila mafanikio.Mawazo ya kufukuzwa kazi yakaanza kumjia kichwani mwake,ni kesi ya pili sasa ya mtuhumiwa huyo anaipoteza kabisa,ni bora angelikuwa na mtoto wa mtuhumiwa ili aweze kukamilisha kazi ya kumpata Ramso lakini,mtoto mwenyewe nae katoroka kama baba yake.Akajikuta ameishiwa nguvu kabisa,akaa kwenye kiti huku akitweta kwa kasi.
******
Kitendo cha mke wa Inspekta Makurumla na mtoto wake wawili kushangaa tu,Gadna akapata mpenyo mzuri wa kutoroka kwenye jumba hilo huku akimpita mlinzi ambaye amelala fofofo.Akiwa pekupeku kabisa akaanza kushuka mabondeni huku akikimbia na kutazama nyuma.Alidhamilia kabisa kwenda mbali kabisa na jumba hilo,kwani kuendelea kukaa kwenye jumba hilo ni hatari.Hakuwa na viatu kabisa,akashuka bondeni na kukanyaga maji machofu yapitayo kwenye mfereji.Akakimbia kwa mwendo wa masaa matatu bila kupumzika,lakini ghafla njaa ikaanza kumtafuna,akajikuta tena kukimbia wala kutembea,akaa chini ya mti wenye kivuli na kupumzika.Hakuweza kujua anakokwenda kutokana kutokuwa mwenyeji wa jiji hilo la Dar es salaam,Mungu pekee ndiye anayemnusuru,akainuka huku akishikilia tumbo lake ambalo halina kitu kabisa.Safari yake kuelekea mahali asipopajua ikaendelea.Mpaka giza likaingia hakuwa na kitu chochote ambacho amepata kuingiza tumboni.
****
“Unajisikiaje kwa sasa?” Ramso akauliza huku akimshika kichwa Zulfa ambaye yupo kitandani.Zulfa akageuka na kumtazama Ramso kwa macho ya huruma.
“Sijambo kidogo” Zulfa akaongea kwa sauti ndogo mno.
“Pole utapona tu,hata mimi nilivyokapigwa risasi ya bega,nilijikaza sana na mpaka sasa nimepona”
“Ehee hivi ilikuaje baada ya kuanguka kwa ule ndege?” Zulfa akauliza na sura yake ikaachia tabasamu zito lenye matumaini.
“Aaah acha tu,yaani ilikuwa pata shika nguo kuchanika” Ramso akasema huku akimtazama Zulfa usoni,akaachia tabasamu na tabasamu zao zikakutana.Akaaanza kuadithia kuanzia pale alipotoka uwanja wa J.K Nyerere mpaka hapa alipo.
“Mmmh umepitia maisha ya shida sana,yaani mpaka ukadandia ndege!” Zulfa akastaajabu mno,ni ujasairi wa hali ya juu ambaoa ameuonesha Ramso kwenye maisha yake ya nyuma.
“Yaani bila yule Bi mkubwa aliyeniokota kule porini,basi ningelikufa kabisa” Ramso akasema.
“Historia yako inasisismua sana”
Wakaenedelea kupiga soga,mpaka pale Jamila alipoingia akiwa ameshika chumba ya chai na vitafunwa,akaandaa na kuanza kunywa .Baada ya kumliza,Ramso akaaga kuwa anaenda mjini kidogo na kuwahaidi kuwa atarejea muda sio mrefu,akavaa nguo zingine kabisa ambazo alinunua siku iliyopita,kichwani akanunua kofia ya Pama nyeusi,miwani nyeusi,huku kidevumi akchonga nywele zake na kubadilika kabisa kimuonekane wake.Hakutaka kuchukua gari ya Zulfa,akaingia kwenye kituo cha taksi na kuingia ndani yake.Dereva akaingiza gia na kukanyaga mafuta kuelekea kule alipoelekezwa na mteja wake.Kitu cha kwanza baada ya kufika ndani kabisa ya Mlimani City ni kununua simu,alipomaliza malipo yake akachukua laini yake na kuiweka kwenye simu hiyo.Baada ta sekunde kama ishirini,mara kifaa cha GPS kikawaka bila Ramso kujua na kuonesha kijitaa chekundu.Hakukitilia maanani kabisa,akafungua kwenye majina ya simu na kupiga.
“Hello,sasa mimi nipo Mlimani City nitakupigia nikitoka ndugu yangu”Ramso akasema huku akianza kutembea kwa hatua ndogondogo.
“Kwani uko wapi wewe?” Ramso akaliza.
“Ahaaa Liberia,basi poa siku yoyote nitakukuta ndugu yangu” wakati wote huo anaendelea kuongea hakujua kuwa GPS yake inasomwa na wafuasi wa Mzee Kibangara.Alipomaliza kuongea akaiweka simu mfukoni bila kuizima na kuendelea na mizunguko yake ndani ya jengo hilo maarufu.Hatimaye akamaliza mizunguko yake,akaamua kuondoka akitumia taksi.
“Nipeleke Mikocheni”
“Sawa” Dereva akaitoa gari na kuanza safari ya Mikocheni.Wakati wako njiani,mara ikawapita gari moja kwa kasi,hawakuelewani ni watu gani,wakapuuzia na kuendelea na safari yao,mara ikapita nyingine aina ya Mercedez Benz yenye namba ya usajiri T 345 DFP kwa kasi.Hapo ndipo Ramso alipogundua kuwa kuna kitu kinaendelea mbele yao,alichokifanya ni kufungua kioo na kutazama nje,jicho likaenda moja kwa moja kwenye gari hiyo ambapo anakumbuka vizuri sana kuwa gari za mzee Kibnagara zote lazima ziwe na herufi DFP kwa usajiri wake.
“Hawa watu wengine maboya sana,wanaendesha kama wamenunua barabara” dereva huyo akasema.Ramso akabaki kimya huku akipanga jinsi gani ya kuwaepuka watu hao.
“Simamisha gari” Ramso akasema,mara baada ya kuliona gari moja wapo limesimama mbele yao mita chache kutoka pale walipo.
“Naam”
“Paki gari pembeni haraka” Ramso akasema kwa msisitizo na dereva huyo akafanya alichoambiwa.
“Vipi chifu,hapa sio Mikocheni lakini!” dereva akaongea kwa mshangao.
“Unanidai shiling ngapi?”
“Ni elfu kumi na mbili za kitanzania Chifu” dereva akajibu……………
Ramso akatoa shiling elfu kumi na tano na kushuka ndani ya gari haraka sana.Akaanza kufuatia mchochoro uliopo mita chache huku akikimbia na kumuacha dereva wa taksi ashangae asijue nini kimetokea.Kitenso cha Ramso kukimbia,kikawafanya wafuasi hao wamuunganishie.Bila kutazama nyuma Ramso akaendelea kukimbia mpaka pale alipokutana na ukuta mbele yake,akarudi nyuma na kuruka juu ya ukuta huo na kuendelea kukimbia.
****
Mzee Kibangara alipofika tu somalia,utaratibu wa kutega bomu ndipo ulipoanza.Wategaji mahili kutoka uswisi,walialikwa kwenye shughuli hiyo na sasa,mabomu mawili yalikwishategwa,moja litasambatalisha ardhi ya Mashariki mwa Kenya na lingine ni Sudan,nchi ambazo zimesababisha mali zake kutetekea.Mzee Kiabnagara alidhalia kweli katika zoezi hilo.
“Mzee hapa tayari,rimoti kontrol hizi hapa” Jamaa mmoja mwenye asili ya Kikorea akazungumza kwa lunga la Kiingereza.
“Sawa sawa kijana,kazi mzuri” Mzee Kibnagara akasema hivyo na kuchukua rimoti hizo.Baada ya kuyaelekeza mabomu hayo kwenye sehemu husika,wakafungua ramani ya nchini Kenya na Somalia kisha wakaanza kuweka mambo sawa.Ndani ya dakika thelathini wakawa tayari wamepata eneo ambalo litawawezesha mabomu hayo kufikia.
“Hebu nitazamishe hiyo kioo kwangu” Mzee Kibangara akasema na kompyuta kubwa kuliko zote kwenye chumba kile ikaelekezwa kwake.Wataalamu waliobobea katika fani ya uchezeaji wa Kompyuta,wakazima mitambo yote ya televisheni ya nchini Kenya na Sudan,sasa akawa anaonekana yeye peke yake.Mzee Kibangara amabaye sasa amevaa kilemba na kuziba uso wake huku pembeni ameshika RPG.Mzee Kibangara akatoa vitisho ambavyo vimewachanganya sana wakenya na wasudan.Wamepewa dakika kumi tu wawe wamerejesha pesa ambazo zilitumika kununlia silaha zake.
Ndani ya dakika nane tu nchi ya Kenya alikwisharudisha pesa kwa kuhofia nchi yao kuliouliwa na kusasabisha machafuko nchini humo,kiasi kingine cha pesa kilitakiwa kilipwe na Sudan lakini wakakataa katakata.Mzee Kibangara akapandwa na hasira na muda huo huo akalituma bomu moja na kusambalatisha makao makuu ya nchi hiyo.Vituo mbalimbali vya televisheni vikaanza kuripoti tukio hilo la kikatili lilisambalatisha watu zaidi la laki tano.
“Haiwezekani kabisa,lazima nilipe kisasi” rais wa Sudan akaamaki na kujikuta anaanza kuunda mitambo yake kwa lengo moja tu,ni la kulipa kisasi.
*****
Usiku umeingia,mtoto Gadna haelewi wapi anakwenda zaidi ya kutalii tu sehemu asiyoijua.Akafika kwenye nyumba moja ambayo imeezekwa na bati kuukuu,akahodika na kuitikiwa na bibi mmoja anayeonekana kuwa na umri mkubwa sana.
“Chikamoo” Gadna akasalimia
“Marhaba wewe nani?” bi mkubwa huyu akauliza huku akimkaribia Gadna
“Naitwa Gadna,naomba unisaidie bibi”
“Nikusaidie nini usiku hii mjukuu wangu?”
“Pa kulala,sina sehemu ya kulala”
“Eeeh kwani unatoka wapi sasa hivi?”
“Mi sijui”
Bi mkubwa huyo akamshika mkono Gadna na kuingia nae ndani,akampatia maji ya kunywa na kumpa chakula,baada ya kumaliza kula ndipo alipoenda kuoneshwa kitanda cha kulala.Katika chumba hiko ndiko kuna wajukuu zake wawili nao wamelala.Gadna akajilaza kiunyonge na baada ya nusu saa mbele akachukuliwa na usingizi wa aina yake na kujikuta analala fofofo!.
*****
Katika purukushani za kukimbia huku na huko Ramso akajikuta anaanguka chini na kujibamiza kwenye paja lake,sehemu ambayo kahifadhia simu,ndipo simu yake ilipoharibika kabisa.Kutokana na kuzimika,wafuasi wa Mzee Kibangara hawakuweza tena kuifuatilia GPS yake,wakajikuta wanashindwa kuendelea na msako huo.
Baada ya kukimbia kwa muda mrefu sana,Ramso akafanikiwa kupanda taksi na sasa safari yake ya kurudi Mbezi ikaanza.Ndani ya dakika chake akawa amefika kwenye nyumba ya Zulfa akafungua geti na kuingia ndani,lakini akashangaa baada ya kukuta damu zimetapakaa chini,mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio huku akihema kwa kasi,hakujua aanzie wapi katika kuvumbia kitu kilichopo mbele yake.
“Shiiiiit My God,nini tena hiki?” akahamaki.Akasukuma mlango kwa teke na kujibanza pembeni,huku bastola yake ipo mikononi mwake ameishika kikamilifu.Kitu kilichoendelea kumshangaza zaidi ni baada ya kukuta simu ya Zulfa ikiwa imewaka.Kitu cha kwanza kukifanya ni kuanza kuchunguza chumba kizima na kuhakikisha hali ya usalama inakaa sawa,baada ya hapo akachukuwa kitambaa chake na kujivisha kwenye kiganja cha mkono,akaishika simu ya Zulfa na kuiwasha,hakuweza kuichezea kwa sababu ilikuwa imewekwa namba za siri,wakati anaendelea kuitazama simu hiyo,ikaanza kuita na jina lililosomeka kwenye kioo cha simu hiyo ni Jamila,akabonyeza kwenye kipokeo na kuiweka sikioni huku akihakikisha kuwa simu hiyo haigusi ngozi yake,inaweza kuwa ametengwa na ile simu na ndio maana yupo makini mno.
“Helooo”
“Oooh asante Mungu,nani Ramso au?” sauti kutoka kwenye simu ikasikika
“Yah” Ramso akaitikia kwa sauti ndogo.
“Ok ni hivi,nipo hospitalini hapa Zulfa alizidiwa ghafla,zimemuaisha hapa hali yake ni mbaya sana”
“Ooppss nia…mbi…e mpo hos..pitali gani?” Ramso akauliza huku ameshikwa na kigugumizi.
“Mwananyamala wodi ya wagonjwa mahututi”
Ramso aliposikia hivyo tu akakata simu na kuchomoka nje huku anakimbia kuwahi Mwananyamala.
“Oyaa niwaishe hosptiali ya mwananyamala haraka” Ramso akaimiza.
“Poa ni elfu kumi na tano”
“Endesha gari”
Dereva akaiwasha gari na kutimua mbio wakielekea Mwananyamala.Kichwa kizima cha Ramso kimevurugika kutokana na kuwaza vitu vingi sana,kikubwa ni mwanae Gadna na mke wake,hakujua kama mke wake na Gadna wako salamu ama laa,bado matatizo yanaendelea,rafiki yake kipenzi Zulfa ambaye amewahi kufanya nae kazi moja na kusaidia kwa kila hali na mali,leo hii yupo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi,hakika alimuia kichwa kwa mambo mengi.Sio mambo hayo tu bali hata nchi yote ya Tanzania inamtafuta kwa tuhuma za kujihusisha na ujambazi wa kutumia silaha.
“Tumefika kaka” dereva akasema huku akimshtua Ramso ambaye amejiinamia kwenye goti lako kwa mawazo mengi.
“Ahaa okay” Ramso akashuka kwenye gari bila kujua kuwa hajalipa pesa ya usafiri.
“Oyaa brooh,hujalipa hela bana” dereva akamshtua Ramso na kumfanya ageuke haraka na kutoa pesa na kumpatia.
“Chenji ya….” Dereva hakumaliza kuongea kwani mbele yake tayari hakukuwa na Ramso.Baada ya Ramso kufika mapokezi akawauliza wahusika wa mahali.
“Samahani ninaomba kuuliza,kuna mgonjwa kaletwa hapa wa kike amediwa sana?” Swali la Ramso likawaacha kinywa wazi wahusika hao ambao ni wasichana.
“Mmmh anaitwa nani?”
“Zulfa” Ramso akajibu na mmoja akaanza kufunua daftari yake mpaka alipokuta jina la Zulfa kwenye orodha ya majina ya wagonjwa wa leo.
“Ok huyu hapa,yupo wodi namba nane ya wagonjwa mahututi”
“Asante sana” Ramso akajibu haraka haraka na kuondoka kwenye eneo lile.Jamila akiwa nje ameketi kwenye benchi,akamuona Ramso kwa mbali anakuja,akamkimbilia na kumrukia huku akilia.
“Nini Jamila,kuna usalama kweli?” Ramso akauliza.Jamila hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kulia tu.
“Nyamaza basi,you know unaniweka kwenye wakati mgumu,kama unalia namna hii,sasa ni nani ataniambia kitu gani kinaendelea?” Ramso akaendelea kulalamika huku akimbembeleza Jamila bila kuwa na matumaini.Naye mwenyewe akaanza kuangusha chozi,picha ya Zulfa akiwa amekufa ikamwingia kwenye ubongo wake.Akaanza kukumbuka jinsi Zulfa alivyomsaidia kwa kila hali na mali na kumtumia pesa baada ya kupata matatizo nchini Msumbiji.Hakukaa vizuri wakamuona daktari mmoja akitoka kwenye chumba kimoja alicholazwa Zulfa,wakaanza kumfuata na kuaanza kumuhoji.
“Vipi dokta,mgonjwa wangu anaendeleaje?” Ramso akauliza lakini daktari akavua miwani na kumtazama Ramso kwa jicho la huzuni.Hapo ndipo akagundua kuwa Zulfa kuna uwekano kuwa amekufa lakini daktari anashindwa kusema………………
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Talk to me doctor(niambie daktari)” safari hii Ramso akafoka kwa hasira zilizojaa uchungu.
“Tulia basi,njooni ofisini” daktari akasema na kuanza kupiga hatua kuelekea ofisini kwake.Walipofika Ramso hakukaa kwenye kiti,akabaki anatembea tembea ofisi mzima.
“Mgonjwa wenu yupo hai,ila inaonekana amewekewa dawa yenye sumu kwenye jeraha lake,na ndio maana yupo katika hali ile”
“Yupo hai?”
“Yes Mr”
Ramso akashusha pumzi ndefu na kuketi kwenye kiti,jasho jembamba likawa linamvuja kutokana na hofu aliyokuwa wayo.Mara akaingia nesi akiwa na kijisahani kidogo cha kuifadhia vifaa vya kutibia.
“Dokta mgonjwa wako ameshtuka na kuamka” nesi huyo akasema.
“Okay,kamtoeni sasa,mpelekeni kwenye wodi ya kawaida,kuna ndugu zake wanataka kuja kumuona” daktari akasema.Mioyo ya Ramso na mwenzake Jamila ikaanza kutulia na mapigo yake yakawa yanatembea kwa upole sana,hofu juu ya Zulfa tena hawakuwa nayo tena.
“Mmesikia?” daktari akauliza.
“Ndio dokta”
“Kwa hiyo kuweni na amani kwa sasa”
Baada ya kuondolewa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi(ICU),Zulfa akaingizwa kwenye chumba cha kawaida.Dakika chache wakaingia Ramso na mwenzake Jamila.Jamila rafiki kipenzi wa Zulfa akajikuta anamkumbatia Zulfa kwa hisia kali huku machozi yanamtoka.Hakuamini kabisa kama kweli Zulfa anaendelea kuishi mara baada ya kuzimia na kupelekwa kwenye chumba hatari cha ICU,
“I love my Zulfa”Jamila akatamka neno hilo huku chozi lake linaendelea kumwagika na kulowanisha mashavu yake.
“Me too Jamila” Zulfa akaongea kwa sauti ndogo sana.Baada ya muda wakatulia na sasa wakawa wanapiga stori za kawaida.Ramso akachukua simu ya Zulfa na kumpatia mwenyewe,kisha akaitoa simu yake ambayo imevunjika kioo,akaisha na kutazama majira,akakuta ni saa kumi na mbili na nusu za jioni.Hakika hakujua kabisa kama laini ya simu yake imeunganishwa na mtandano wa kigaidi wa Mzee Kibangara,GPS yake ikaanza kusoma na kumuonesha mahali alipo.
“Natoka nje,niwabebee nini sijui?” Ramso akauliza.
“Beba machungwa na juisi ya embe” Jamila akasema kwa niaba ya Zulfa.Ramso akatoka nje na kuanza kutembea kuelekea nje kabisa ya hosptalini hiyo huku alama ya GPS inamuonesha.
*****
Bi mkubwa ambaye alimpokea Gadna na kumpatia hifadhi,macho yamemtoka,machozi yanamtoka,hii mara baada ya Gadna kupigwa na wajuu zake mpaka kuzimia.Kitendo hicho kikamuweka katika wakati mgumu sana bi mkubwa hiyo.Kama kumpepea,alimpepea sana lakini haikuwezekana.Ni baada ya kulia sana ndipo akatokea jirani yake na kumsaidia kumpelekea hosptalini.Ndani ya taksi Bi mkubwa anapita kulia tu,ikafika sehemu akaanza kujuta kwa nini alimpokea mtoto huyo,hisia za kufungwa jela zikaanza kumjia,akajikuta anaangusha chozi mara mbili zaidi ya hapo.
“Bi Kinono taratibu basi,atapona tu huyu”jilani huyo akasema na kumfariji Bi Kinono ambaye bado analia
“Aaaah mbona haemi?” Bi kinono akauliza huku anajifuta machozi.
“Anahema lakini kwa mbali,usijari bibi ni mzima huyu”
Maongezi hayo yakaendelea mpaka walipofika hosptiali ya Mwananyamala.Wakamshusha Gadna na kumuingiza mapokezi,baada ya taratibu zote za kupokelewa,wakamuingiza kwenye chumba chake na huduma ikaanza rasmi.Manesi waliobobea katika fani ya kuwatibu baadhi ya wagonjwa,wakaanza kumshughulikia Gadna.Bi Kinono na jilani yake wakabaki nje wanasubiri majibu ya mgonjwa wao.Wakati wote huo wanaendelea kusubiri matokeo,mara akatokea msichana mmoja mita chache kutoka sehemu walipo,hatua ya kwanza ya pili mpaka ya tatu akajikuta anagongana na mwanaume aliye mwembamba ambaye ni Ramso.
“Sorry sorry” Ramso akasema huku ameshika kimfuko kidogo kilichojaa machungwa.Hofu ikamtanda Ramso na mara nyingi akiwa anatazama nyuma alikotoka.
“Unatembea boya wewee?” msiachana huyo akagoma kwa ukali lakini Ramso akawa mpole kwani ni yeye ndiye aliyemkuwaa kutokana na kutazamatazama nyuma.Msichana huyo akaondoka na kumuacha Ramso akiokota machungwa yake na kuyatia tena kwenye mfuko.
“Mama vipi mtoto anaendeleaje?”
“Ninyamazie,watoto wako ndio waliosababisha mtoto wa watu awe katiak hali hii,na kama akifa basi hayo mashtaka utachukua wewe” Bi Kinono akafoka kwa jazba na kumuacha msichana huyo akiwa ameshika tama.Hata dakika tano hazijapita mbele yao kwenye lile kordo,wakapita watu watatu waliovalia suti na miwani,mwendo wao ulikuwa wa haraka sana,hawakujua kama ndio wafuasi wa Mzee Kibangara wanamfuatilia Ramso,baba wa Gadna waliomleta kwenye hosptali hiyo.Wakabaki wakiwasindika jamaa hao mpaka walipozama kwenye upeo wa mboni zao.
“Zulfa wale jamaa wanakuja,wapo huko nje daah”
“Jamaa gani?”
“Jamaa wa Mzee Kibangara”
“Heee,wamejuaje?”
“Hata mimi sijui”
“Mmmh,hebu simu yako” Zulfa akasema na Ramso akatoa simu yake na kumpatia.Zulfa alipoiona tu akaizima kwa haraka na kuitupa pembeni.
“Simu yako imeunganishwa na mtandao wa Mzee Kibangara,yaani hapo ukiwasha tu GPS yako inatoa taarifa kwa hao jamaa na kukubaini wapi ulipo” Zulfa akaongea na kumuacha Ramso akishangaa,kwani jambo hilo kwake lilikuwa jipya.
“Umejuaje?”
“Hata mimi yangu ilikuwa inasoma GPS na kunionesha wapi nilipo,ndipo nilipoenda kuitegua kwa mtaalamu wa Kompyuta Kariakoo”
“Aaah ndio maana jana walinifuatilia na kuanza kunifukuza” Ramso akashikwa na mshangao wa aina yake.
“Ndio hivyo”
“Kwa hiyo hapo ukizima ndio hawakuoni?”
“Hapo wamepotea kabisa hawawezi kujua upo sehemu gani”
Baada ya kupeana taarifa zote wakatoa machungwa na kuanza kula.Akaingia Jamila akiwa ameshika kimfuko kidogo kilichojaa chipsi.Wakaanza kula kwa pamoja bila wasiwasi.
“Niazime simu yako” Ramso akamuambia Zulfa,akachukua na kubonyeza namba anazozijua,kwa bahati mbaya namba hizo hazikupatikana.
Taratibu akaanaza kunyati na kutoka nje,alipochunguza kwa umakini akabaini kuwa hakuna mtu mbaya yeyote.Akili yake ni kurudi kwa yule mdada ambaye aligongana nae ili amtake radhi.Kweli akafika na kumkuta akiwa amekaa na Bi mkubwa mmja na jamaa mmoja.Sura zao hazikuwa na matumaini kabisa,kila aliyemtazama hakuwa na furaha kabisa.
“Samahani dada” Ramso akasema “shikamoo mama” akamsailimia Bi Kinono na kumalzia jamaa aliyekaa pembeni.
‘Samahani dada yangu,kulikuwa na jamaa wananikimbiza ndio maana nikakosea kukukuwaa”
“Sawa nimekusamehe”
Ramso akamtazma Bi mkubwa huyo ambaye hana kabisa tabasamu.
“Mama kuna mgonjwa wenu hapa?”
“Ndio mwanangu” Bi Kinono akasema kwa sauti ya kukwaluza.
“Oooh poleni anaumwa nini?”
“Alipigwa tu na wenzake”
Baada ya kuongea nao machache bila kujua kuwa aliye ndani ni motto wake Gadna amelazwa,akainuka na kuondoka huku akiwaaidi kuwa atakuja kuwazama baadaye.
“Oooh My son Gadna where you are?” akajikuta anaongea peke yake.lakini wakati anaendelea kuwaza hayo akakumbuka kuwa mara ya mwisho motto wake Gadna alikuwa kwenye mikono ya Inspekta Makurumla.Akawaza jinsi gani anaweza kumpata askari huyo bila kufanikiwa kupata jibu la fumbo lake.
“Hivi nawezaje kumpata yule Inspekta Makurumla?” Ramso akauliza na Zulfa akajibu.
“We wa nini?”
“Yule ndio mtu wa mwisho kumchukua mtoto wangu,nataka nimpate yeye ili iwe rahisi kujua wapi alipompeleka” Ramso anasema huku misuli ya kichwa ikiwa imemsimama kwa uchungu wa mtoto wake.
“Huyo jamaa kumpata ni rahisi tu?” Jamila akasema.
“Mmmh kwani wewe unamjua?” Ramso akashangaa kumsikia Jamila akisema hivyo,kwani hajui hata kitu kimoja kuhusu yeye.
“Nitakusaidia kumpata,nipe malekezo yake tu”
‘Haya kama unaweza”
“Mimi ni mwanamke wa shoka bana”
Ramso hakuwa na chaguo lingine zaidi ya kumpatia maelekezo yote kuhusu askari huyo anayeitwa Inspekta Makurumla.Akamtajia na jina la kituo chake na muda ambao anakuwepo kituoni hapo.
“Usijari nitakucheki kwenye simu,kesho majira ya saa saba za mchana”
“Poa nakuaminia J”
“Haina mbaya”
Jamila akaaga na kutoka nje ya hospitali hiyo akachukua taksi ikampeleka moja kwa moja nyumbani kwake magomeni,huko akajitayarisha kwa kazi ya kesho ya kumtia mkononi Inspekta Makurumla.
*****
********
Jamila hakutaka kabisa kupoteza muda,tayari amekwisha panda kwenye pikipiki ambayo ikamoeleka mpaka Mbezi katika jumba la Inspekta Makurumla.Akashuka na kuanza kupuga hatua kuelekea kwenye geti la nyumba hiyo.Hakutaka kusita kabisa,akaanza kugonga geti mara kadhaa na mlinzi akaafungua geti.
"Mambo"Jamila akasalimia kwa sauti iliyojaa ushawishi kwa mlinzi.
"Safi ehee mtoto nzuri unasemaje?"
"inspekta Makurumka nimemkuta?"
"Unamuhitaji wa nini?" Mlinzi akaanza kuuliza maswali bila ya kujiba maswali anayoulizwa.
"Ni mfanyakazi mwenzangu"
"Ahaa bosi katoka kidogo mpaka...."kabla hajamalizia sentensi yake gari ndogo ikatokea nyuma yao na kusimama.Akashuka Inspekta Makurumla akiwa amechoka mno.Tai yake imekaa vibaya shingoni,hakika alikuwa katika mvulugiko wa aina yake,akavuta hatua na kuwafikia Jamila pamoja na mlinzi.
"Vipi mbona unamuweka mlinzi nje?"Inspekta Makurumla akauluza huku akintazama Jamila ambaye amevalia kijisketi kifupi kilichochora umbo lake la kiuno kwa muonekano angavu kabisa.
"Samahani bosi,nilikuwa najaribu kumuhoji kama anamiadi na wewe" mlinzi akajitetea.
"ok hebu mpishe aingie ndani" Inspekta aksema.
"Hapana hapa hapa inatosha"Jamila akadakia kwa uharaka.
"Sawa haina neno,hebu tupishe,endelea na kazi yako"Inspekta akamwambia Mlinz na wakawa wamebaki wawili pale nje.
"Samahani tunaweza kukaa sehemu,kuna jambo kubwa nataka kukujuza Inspekta"
"Jambo gani hilo?"
"Ndio maana nikakuambia tutafute sehemu ili nikuambie,najua una tatizo kubwa sana"
Jamila akasema na kumuacha Inspekta Makurumla katika mshangao wa aina yake.Hakuwa na chaguo lingine zaidi ya kuingia kwenye gari na kuanza safari yao.
****
Ramso na Zulfa bado wapo katika chumba alicholazwa Zulfa huku wakiongea mambo kadha wa kadha juu ya mustakabali wa maisha yao.
" Hivi unajua bado tunatafutwa na pande mbili?" Lilikuwa swali la Zulfa ambaye amekaa juu ya kitanda.
"Najua hilo,nafikiria maisha haya yatakuja kuisha lini"Ramso akasema huku akijipiga kichwa kofi.
"Lazima tufanye kitu,ama sivyo tutaangamia"
"Nataka kuama kabisa Afrika Kusini,nataka niamie Liberia kwa rafiki yangu"
"Mhhh huwezi kwenda peke yako lazima namimi nije unataka nikafie jeela au kwa yule mzee"Zulfa akazungumza na sekunde chache mbele simu ya Zulfa ikaanza kuita.
"Jamila huyooo"Zulfa akasema.
"Hebu nipe niongee naye"Ramso akasema na kupewa simu.
"Njoo haraka maeneo ya Magomeni,yuke mtu nimemkamata hapa" sauti kutoka upande wa pili wa simu ikasikika.
"Ok nakuja" Ramso akakata simu,akajiweka sawa na kumuaga Zulfa kuwa atarudi baadae.
Akafika nje na kuchukua bodaboda iliyomfikisha mpaka Magomeni Mapipa.Akachomoa simu na kuipiga,lakini cha ajabu ikakatwa,baada ya dakika moja ujumbe ukaingia kwenye simu yake.
'Usipige yule jamaa atashtukua' ujumbe wa Jamila ukamtaadhalisha Ramso naye pia akatuma ujumbe mpaka wakaweza kuelewana na Jamila akamuelekeza sehemu waliopo.
"Nipo kwenye Gardeni hapa upande wa kushoto" Ujumbe wa Jamila ukamfanya Ramso aanze kuangaza huku na huko na kuwaona.Uzuri wa sehemu hiyo kuna maua makubwa kiasi ambacho mtu akijificha hawezi kuonekana kabisa na watu.Akawaona Jamila na Inspekta Makurumla wakiwa wamekaa na mezani wamejaza pombe kali.Ramso akaenda kwenye upande wa kamera ya simu na kuwavuta kisha akaanza kupiga picha.Alipoona zinamtosha akamtumia ujumbe Jamila na kumuambia aingie nae ndani.
'INGIA NAYE NDANI,TUKAMBANE VIZURI'
Jamila akafanya kama alivyoambia na ndani ya muda mchache wakawa wameingia ndani kisha Ramso akafuata nyumba.
Katika chumba namba kumi na nane ndimo Jamila na Inspekta Makurumla walimoingia.Inspekta Makurumla pombe imemkolea kichwani hakuwa anakijua anachokufanya,akaanza kumvamia Jamila na kupiga mabusu huku macho yake yakiwa mekundu,laiti kama angelijua kuwa ule ni mtego,asingelifanya kitendo kama hicho.
"Hebu subiri basi" Jamila akasema na kumgandua Inspekta Makurumla kwenye mwili wake.Akamsukumia kitandani na kumkalia juu yake.Akatoa blauzi yake ya juu na kubakiwa na sidilia.Inspekta Jicho limemuiva kama nyanya kwa ule utundu wa Jamila.Wakati yote yanafanyika Ramso yupo nje ya chumba hicho akiwa anajiweka tayari.Akavaa maski yake ya kitambaa,akavaa pia na glovusi mikononi,akachomoa bastola yake na kuishika mkononi mikamilifu.Kitendo cha haraka akasukuma mlango na kuingia hadi ndani,akasukuma mlango kwa teke na kujifunga.Inspekta Makurumla akiwa katika dimbwi la huba na Jamila,akashtuka na kujibwaga chini.
"Tulia hivyo hivyo nitakumwaga ubongo"Ramso akafoka na kumuelekezea bastola kichwani Inspekta Makurumla.Jamila akachukua blauzi yake na kuivaa kisha akaenda mlangoni na kuufungwa kwa ufungua.
"Haya niambie mtoto wa bosi yupo wapi"Ramso akazungumza kwa hasira na ghazabu huku akitumia njia ya kumdanganya Inspekta ili asigundue kama yeye ndio Ramso ambaye amemkimbia kituoni.
"Mtoto wa bosi!" Inspekta akashangaa baada ya kusikia kauli hiyo.Mshangao wake ukampandisha hasira Ramso,hapo hapo akamfumua teke la kifuani na Inspekta Makurumla akaachia ukelele wa maumivu lakini hakuchukua muda mrefu akainuliwa na kuwekwa sawa.Akapigwa ngumi ya pua na kupachikwa na maswali.
"Mtoto Gadna umemuweka wapi?"
"Mi si...jui ka..bisa ame...toroka nyumbani" Inspekta Makurumla akajieleza kwa hofu ya kipigo anachogawa Ramso dhidi yake.
"Unasemaje?"
"Sina mtoto wenu" safari hii Inspekta Makurumla akasema kwa kujiamini japokuwa anavuja damu za puani.Ramso akashikwa na ghazabu tena,akaanza kumpiga Inspekta Makurumla kwa mfululizo bila kumpa nafasi.Jamila alipoona hivyo,akaanza kumtoa Ramso kwenye mwili wa Inspekta bila mafanikio.Akajitahodi mpaka alipofanikiwa kumgandua kwenye mwili huo.
"Niache nimuoneshe kazi huyo bwege"Ramso akajaribu kujipokonya kwenye kwenye mikono ya Jamila lakini bado Jamila akawa hataki kumuachia kwani kumuachia kwake kunaweza kusababisha mauti ya Inspekta.Purukashani zikaamia kwao,wakti huo Inspekta Makurumla amelala chini hajitambui damu zinamvuja sehemu mbalimbali za mwili wake.Mara Ramso akajikuta anaangusha bastola yake chini na kuendelea na vurumai zao baina yake na Jamila.
"Nimekuambia niache Jamila"
" Sikuachi" Jamila amemng'ang'ania Ramso habanduki.Wakaangushana chini na vurugu likaendelea.Inspekta Makurumla akaanza kuvuta hewa kwa mbali na kujaribu kufumbua macho.Akajaribu zaidi ya mara tatu hatimaye akafanikiwa kutazama.Kitu kilichopo mbele yake ndicho kilichompa faraja moyoni mwake,Waswahili wanasema 'MBUZI KAFIA KWA MUUZA SUPU'.Akanyoosha mkono wake kwa shida na kuikamata bastola iliyo pembeni yake.Akajiinua taratibu na kukaa.
"Hivyohivyo mlivyo mikono juu" Inspekta Makurumla akasema kwa sauti ya juu na kuwashtua Ramso na Jamila ambao walikiwa katika ugomvi mkubwa chumbani humo.
"Haya mikono juu haraka sana"
Machovya Ramso na Jamila hayakuamini kabisa kitu kinachotokea mbele yao.Inspekta Makurumla amezinduka na sasa ana mguu wa kuku aliouangusha Ramso.
"Simama juu" Inspekta Makurumla akafoka na wote wakasimama juu mikono yao ikiwa imeelekezwa juu.
"Naanza na wewe malaya,vua nguo zako zote"
" M...imi?" jamila kauliza kwa kutoelewa nani wa kuvua nguo kati yao.
"We nitakumwaga ubongo sasa hivi" Inspekta Makurumla akamfokea Jamila jwa hasira na kumfanya aanze kusaula nguo zake huku mwili wake umejawa na hofu.Mpaka anakuja kubakiwa na chupi ya ndani,Inspekta Makurumla akamtazama tena usoni na kumuambia.
"Vua na hilo chupi lako"Inspekta akafoka.Jamila akamakizia kuvua na chupi na kubaki kama alivyozakiwa.
Inspekta Makurumla akamgeukia Ramso ammbaye amevaa mzula wa maski usoni.
"Vua hilo ngago lako baladhuri wee" Insepkta Makurumla akasema na Ramso akaanza kutetemeka.Kwa mara nyingine hisia za kukaa gerezani zikaanza kumtawala.
"Vua,haloo unajitia ununda?"Inspekta hakuwa na utani kabisa,si Ramso hata Jamila,hawakujua nini dhamira ya Inspekta huyu kuwataka wavue nguo zao...............
"Hapa mmeingia choo cha kike,toa zula lako"Inspekta Makurumla akafoka na Ramso akavua maski yake.
"Eeeeeh kumbe wewe boya?" Inspekta Makurumla akahamaki baada ya kuona sura ya Ramso iliyopo mbele yake.Ramso akainamisha kichwa chake chini kwa mfadhaiko mkubwa.
'Ama kweli leo nimeingia choo cha kike' Ramso akawaza na akajikuta anaafikiana na Inspekta huyo kuwa Wameingia choo cha Kike.
"Na wewe fanya kama huyo malaya alivyofanya" sauti hiyo ikanshtua sana Ramso.Kitendo hicho cha kuvua nguo bila kujua dhamira ya Inspekta kikamchanga kichwa sana.
Hakuwa na budi kukubaliana na maneno ya Inspekta.Akaanza kuvua nguo moja moja huku akifikiria kitu gani cha kufanya kwa haraka ili aepukane na tukio lililo mbele yake.Akavua nguo zote za juu na kubakiza za chini,akamtazama Inspekta lakini akaoneshwa alama ya kumalizia nguo za chini.Akafungua mkanda taratibu na kuanza kuporomosha suruali yake huku anamkata jicho la hasira Inspekta huyo.Ni kama alipandwa na mzuka kichwani mwake,Ramso akamrushia suruali ile Inspekta Makurumla na kumpiga teke la mkononi.Inspekta Makurumla akaangusha bastola chini na hapo ndipo Ramso alipojipindua na kuirukia bastola hiyo.Sasa ikawa mikononi mwake.
"Okay put your hands up!(nyoosha mikono juu)" Ramso akaamrisha na Inspekta akafanya kama alivyoambiwa.Sasa ikawa zamu ya Inspekta huyo kuenya na kutweta kwa mazoezi magumu anayopewa na Ramso,mazoezi ambayo hakuwahi kuyapata tangia anaanza mafunzo yake ya upolisi mpaka anafikia cheo cha uinspekta.
"Utanionesha mtoto au hunioneshi?" Swali hilo likawa mtihani mkubwa sana kwake.Hakujua mtoto huyo ameelekea wapi,kazini kwake amesimamishwa kazi mpaka pale atakapokuwa amewakamata waalifu.Jasho linamvuja kwa wingi,anatamani dunia ipasuke ili atoweke asionekane mbele ya Ramso lakini haikuwezekana kabisa,ni sawa na mtu anayeota amejenga nyumba angani.
"Vua nguo haraka sana"Ramso akafoka na Inspekta Makurumla akamtazama Ramso kwa sura ya huruma lakini Ramso hakujali huruma yake.
"Vua haraka"
Inspekta Makurumla hakuwa na la kufanya kwani mtutu wa bastola upo mbele yake na akifanya mzaa anaweza kupoteza maisha yake.Akaanza kuvua nguo zake na kubaki kama alivyozaliwa.
"Jamila mpande huyu Kwa juu nichukue picha"
Ramso akasema hivyo na Jamila akapanda juu ya kutanda.Akaanza kumuwekea style za kutandani huku Ramso akichukua picha kwa kutumia simu mfululizo.
"Kama hautanipatia mtoto wangu picha hizi nitamuonesha mke wako na nitazisambaza kwenye mtandao.Na hii video niliyorekodi nitaenda kuweka mtandao,kupona kwako basi lazima unaoneshe mtoto wangu Gadna tu na sio kingine" Ramso akazungumzo sana na hatimaye akafungua mlango na kuondoka akiwa na Jamila huku nyuma Inspekta Makurumla ameachiwa namba ya mawasiliano.
****
Wafuasi wapatao sita wakamchukua bosi wao Mzee Kibangara na kuingia nae kwenyw ndege inayoelekea Tanzania.Dhamira kuu ni kuja kuongea na Waziri mmoja nchini Tanzania kwa dhumuni la kuanza mipango ya kuipindua serikali ya sasa iliyopo madarakani.
Ndege ndogo maalumu ya Mzee Kibangara ikatua katika hekalu yake iliyopo kwenye msitu mdogo huko Bunju.Hakutaka kukawia,ndipo akawasiliana na Waziri huyo na kupanga jinsi ya kukutana.Walipomaliza Mzee Kibangara akaingia ndani ya gari yake ya kufahari na safari ya kwenda sehemu waliyopanga ikaanza.
Kutokana na uwezo mkubwa wa gari hilo dereva wa Mzee huyo akatumia dakika arobaini peke yako kufika kwenyw jumba kubwa lililopo Masaki.Wakaingia ndani na kupokelewa na walinzi wa Waziri huyo kisha baadae akaingia mpaka ndani ya jumba hilo na kukutana na Waziri.
"EHEE nipe habari mheshimiwa"Waziri huyo akazungumza huku akimpa mkono Mzee Kibangara.
"Safi harakati zinaendaje?"
"Kwema kabisa,kwa kweli mipango yetu inakwenda vizuri sana"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ehee umefikia wapi?"
"Aaah mpaka sasa nimezishikilia nyaraka muhimu za wizara zote"
"Vizuri sana" Mzee Kibangara akasifia,akachukua maji yaliyo kwenye glasi na kunywa.
"Bado tumtoe uhai mheshimiwa rais.Huyu kazi yake ndogo tu,tutamuwekea sumu kwenye kipaza sauti,maana wiki ijayo anahutubia bunge" Waziri huyo ambaye hana masihala akazungumza huku akiwa amekunja sura kuashilia yupo siriazi mno.
Wakapanga mikakati jinsi ya kuichukua serikali hiyo Tanzania pamoja na kuiweka mipango ya kuishikilia dola.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment