Search This Blog

Thursday, November 24, 2022

MKUKI KWA NGURUWE - 2

 

     

     



     Simulizi : Mkuki Kwa Nguruwe

    Sehemu Ya Pili (2)

     

     



    ‘Sasa mke wangu, nakuahisi kuwa mimi mume wako, ...nitajitahidi sana tuwe pamoja tuiondoe hiyo hali, au unasemaje mke wangu..?’akasema, nikakumbuka kuwa mtu huyu hatakiwi kuongea kwa muda mrefu, kwahiyo natakiwa kukubali tu, japokuwa nilikuwa sijamuelewa bado , hapo nikasema.



    ‘Usijali mume wangu, cha muhimu kwa sasa, ni kuhakikisha yale tuliyo anza nayo yanafankiwa,…kampuni eeh, hiyo nitapambana nayo, na hili la huyo mdogo wetu  achana naye, lisikuumize kichwa, au kuna nini zaidi,..hakuna achana naye, jingine ni kuhusu watoto wetu , najua familia inakua, sasa, hapa kuna kitu nataka tukiongee....’akasema



    ‘Tutakuja kuongea tu mume wangu usijali…’nikasema lakini hapo nahis kuna jambo anatakak kulisema, naogopa anaweza kusema jambo, nikaingiwa na hasira, na haitakiwi,..hapo nikasema.



    ‘Lakini mume wangu…’akanikatiza na kusema;



    ‘Huyu mdogo wangu kwa sasa hana tatizo, keshajiweka mahali ambapo hatuna haja ya kuhangaika naye tena,....na kwa watoto wetu bado wadogo, hatuna shaka nao, tutawajenga kimaadili, na umeshafanikiwa kwa hilo, kama wanaweza kuamuka asubuhi na kuwajibika hata bila kuelekezwa, tunataka nini tena mke wangu..au sio….’akasema.



    ‘Ni kweli…’nikasema



    ‘Sasa mke wangu kuna kitu kingine nilitaka tuongee…’akasema



    ‘Mume wangu unakumbuka docta alisemaje…’nikasema



    ‘Ndio nakumbuka alisema nisiwaze sana, na nisiongee sana…’akasema



    ‘Sasa hapa umeongea vya kutosha, unahitajika kumpumzika..’nikasema



    ‘Lakini niliyo nayo kichwani yananifanya niwaze sana , ndio maana nataka tuyaongee, tuyaweke sawa, yananifanya niwaze sana, na baba yako, yupo nyuma ya hili, akiona nimepona tu, atanivaa, sitaki, nataka tuyaweke sawa sisi wawili kwanza…’akasema



    ‘Tutaongea tu mume wangu usijali, sasa hivi wewe unahitajika kupumzika kwanza…unajua mume wangu nimekukosa sana, nataka upone haraka, au wewe hulioni hili, …’nikasema



    ‘Kweli mke wangu nafahamu..hata mimi naona nakutesa sana, nawazia sana hilo pia, utaishi hivi mpka lini, ndio maana naingiwa na wivu, nahisi  kama naibiwa…’akasema



    ‘Hahaha mume wangu….wivu gani huo, kwa umri huu usiwe na wasiwasi kabisa, si unanifahamu mimi sina mwili wa tamaa tamaa za ajabu ajabu, mimi najimudu mwenyewe kabisa…’nikasema



    ‘Mhh, ..ni kweli, hata hivyo wivu hauachi kuwepo,…ila kiukweli mungu alikujalia , lakini tatizo ni mimi mume wako, tamaa ni nyingi sana, ndio maana mungu kaona aniadhibu….’akasema



    ‘Oh,…. pole sana, sasa mume wangu tulia , dawa zifanye kazi, ulale sasa…’nikasema



    ‘Ngoja nikuambie ukweli kwanza kabla sijalala,…mke wangu, nataka

     

    tufurahi pamoja, tuongee pamoja,… nilishaanza kuwazia vibaya sana, hii ajali ndio imeniokoa, sasa nataka kusiwepo na uadui, kati yangu mimi na wewe na …marafiki zako pia..kama ni langu liwe langu…’akasema‘Usijali mume wangu nimekuelewa tu…’nikasema‘Hapana, wewe hujui tu…nilishaanza kufikia kubaya, na….isingelikuwa hayo mambo ya baba yako, ningelishajiandaa kufanya mabaya tu, tamaa zilishaanza kuitawala nafasi yangu,…wakati mwingine mungu anajua tu nilikuwa naelekea wapi…’akasema‘Mume wangu sasa lala…’nikasema‘Nakupenda sana mke wangu, niache nikuambie ukweli, nimekukosea sana, na kosa langu linakwenda kuathiri wengine ndio maana naogopa, sasa mdogo wangu kesho atakuwa mwingine, unaona eehe, ni vyema tukayamaliza haya sisi wenyewe achana na mipango ya baba yako, hebu sogea hapa mke wangu, nahisi sauti inakwisha, dawa hizo…’akasema hapo nilitaka kuanza kukasirika, maana ni kama unaongea na mtoto ambaye unamkanya kitu hasikii, lakini sikuwa na jinsi, nikasogea na kukaa karibu yake‘Kaa hapa kwenye miguu yangu…’akasema‘Mume wangu lala basi…’nikasema‘Ni amri ya mume wako…’akasema na mimi nikaenda na kujiegesha kwenye miguu yake, na akawa ananishika ili kunifanya nikae, huku namuonea huruma, ..kitendo hicho kikamfanya acheke..na mimi nikajikuta nacheka tu‘mke wangu kweli unanipenda, wanionea huruma sana, lakini huruma hiyo isiishie hapa,..unihurumie kabisa kabisa..usimsikilize baba yako, kila kitu alichpanga tukisahau, unanielewa, hayo niachie mimi, au sio…akanishika kama ananitekenya,......’‘Aah, mumu wangu, nini tena lala, utajiuliza…’nikasema na kucheka na yeye akacheka,   na mara nikasikia sauti ya mtu akipiga hodi, na kabla sijasema karibu mlango ukafunguliwa, ..., alikuwa ni docta.‘Kumbe ni wewe jirani…’nikasema na kujiinua haraka miguuni mwa mume wangu.‘Oh, naona leo mpo na raha, maana nimesikia kicheko, ..kicheko cha raha, ...’akasema  na mimi nikashukuru kuwa hatmaye mgonjwa atakubali kulala.‘Kwanini nisiwe na raha na mimi nipo na mume wangu..’nikasema.‘Ni kweli hayo ndio maisha,...inatakiwa  mfanye hivyo kila siku,, au mara kwa mara, au sio rafiki yangu?’ akamuuliza mume wangu huku akimsogelea na kushikilia kile kigari,..na mume akasema;‘Na wewe bwana, unakuwa dakitari wa kila kitu....’akasema‘Ni kweli natamani iwe hivyo, na nimekuja na mtu wa mazoezi, leo tunataka kumfanyisha mume wako mazoezi maalumu, na kama hutajali naomba nimchukue mume wako’akasema‘Unataka kumpeleka wapi?’ nikauliza nikimwangalia kwa uso uliotahayari.‘Ndani ofcourse, tunahitajia tuyafanyie ndani,  sehemu yenye nafasi, hasa kule maktaba au sio…docta kaja na vifaa maalumu, yupo nje,…docta ingia...’akasema, na mara akaingia docta akiwa kavalia kikazi zaidi.Mimi hapo sikuwa na jinsi…nikawaacha wao wakielekea kwenye chumba cha maktaba, na wakati wanaondoka kuingia  mume wangu akageuza kichwa na kuniangalia kwa nyuma, akasema;‘Mke wangu nakupenda sana....’akaniambia mimi sikujibu kitu, muda huo akili ilikuwa imezama kwenye mawazo, nawaza hayo mume wangu aliyoongea, inaonekana kiukweli mume wangu kakosea, na huenda, ..kuna ukweli wa hayo yanayosemwa, na …na huenda baba yangu ameshaligundua hilo…sasa itakuwaje…************* Baadae docta akarudi, naona alimuacha mwenzake akiendelea na mazoezi na mume wangu.‘Nimekuona ukimuhoji sana mume wako, ...huu sio wakati muafaka, wa hayo maongezi yako...’akasema‘Mbona sijamuhoji kitu chochote cha kumfanya awaze sana, yeye ndio anaongea mambo mengi tu…’nikasema‘Kwanini una haraka na hayo mambo, uwe na subira  na hicho unachotaka kukijua, utakifahamu na…utakuja kuniamini niliyokuwa nikikuambia.., lakini kwa hivi sasa yasubirishe hayo..wasiwasi wangu ni kuwa, unaweza ukafanya jambo ambalo utakuja kujijutia. Ukiwa umeshachelewa….unanielewa hapo…’ Akasema na mimi nikawa namsikiliza tu..‘Japokuwa namuona mume wao leo ana furaha sijui kwanini…lakini ndivyo itakwavyo, awali alikuwa akionyesha kuwa ana jambo linamkera, hata hivyo hayo ysikupe mawazo kuwazia kuna nini, hayo yaweke pembeni kwanza, mengine nakusaidia, niamini mimi…’akasema‘Kwani wewe unafikiri mimi nimemuuliza nini mume wangu kibaya,..tulikuwa tunaongea tu, ila mimi najiuliza kwanini wewe unayejua ukweli hutaki kuniambia,..’nikasema‘Kukuambia nini sasa, wakati mimi nimeshakuambia kila kitu au…?’ akauliza‘Hapana,..hujaniambia…’nikasema‘Tatizo  ..wewe unataka nikutafunie kila kitu, mimi siwezi kuvunja ndoa ya mtu, na sitaki hilo litokee, …unasikia, snitajuta sana ndoa yenu ikivunjika…’akasema‘Unajua mimi sikuelewi, wewe unajifanya kuwa unanijali, kumbe kuna mengi makubwa unanificha, hukutaka kuniambia mapema, na huenda yote yasingelitokea kama ungelikuja kuniambia mapema..’nikasema.‘Ina maana unanilaumu mimi kwa hilo, ...unanichekesha kweli, wa kujilaumu ni wewe mwenyewe, wewe umeshindwa kuihudumia ndoa yako halafu na hatimaye hayo yakatokea,mengine yameanzia huko…, umesahau eeh, ni mara ngapi ninakuja kuongea na wewe na kujaribu kukuelekeza…’akasema.‘Usijitetee bwana…, wewe ulikuwa na mume wangu wakati anafanya yasiyofaa, kama alishaanza kujihusisha na umalaya, kama alivyosema leo hii , ina maana wewe ulikuwa unafahamu,, je hukuwahi kumuona na wanawake wewe huniambii, ni nini maana ya kunijali...’nikasema.‘Na wanawake, kakumbia hivyo…hapana ….’akasema‘Kasema tamaa zilimzidi, akaanza na kutamani kufanya mabaya, hayo yana maana gani…?’ nikauliza‘Sizani kama alikuwa na maana hiyo…’akasema‘Lakini kuna kipindi nilikuambia hilo, unakumbuka kuna siku nilikuja nikakuambia kuwa mume wako naona kama ana…kuwa kuwa karibu na wanawake, kitu ambacho sio kawaida yake, lakini sio kwa ubaya, sikuona huo ubaya wa ndani …’akasema‘Anakwua nao kwa vipi,…?’ nikauliza‘Lakini nilikuambia, ukasema mimi naleta fitina, umeshasahau eeh, usinione kuwa mimi ni mjinga, nafanya haya mambo kihekima, nisingelikuja na kukuambia moja kwa moja, nilikuambia kwa namna ya wewe kulielewa, ukaniona mimi ni mbaya...’akasema.‘Swali je kuwa nao karibu ni kwa nia mbaya, kuvunja ahdi ya ndoa , au kwa vipi, nataka unijibu hapo…’nikasema‘Hilo kwa utashi wangu sijaliona, wanakunywa pamoja, kuongea inaishia hapo ila mimi niliona hilo lina muelekeo mbaya…’akasema‘Kwahiyo wewe umesahau ile ahadi yako,?’ nikamuuliza‘Ahadi gani?’ akaniuliza‘Kuwa kamwe hutakubali mtu aniumize...’nikasema.‘Na ndicho ninachokifanya...wewe mwenyewe utaona, si unajifanya mpelelezi, endelea,...lakini mimi nitajitahidi kuhakikisha kuwa hakuna mtu atakayekuumiza,ahadi yangu ipo pale pale, hata kama hunitaki niwe karibu na wewe....ila nakukanya uwe mwangalifu, usichukulie mambo kwa pupa..’akasema huku akitabasamu na kushika kidevu‘Halafu kuna ujumbe, nimeupata, kutoka eeh, kwa rafiki yako, anasema kuna mambo yameshindikana anahitajika arudi kwanza huku, ...sijui ni mambo gani, kwani hamjawasiliana naye ?’akaniuliza‘Rafiki yangu yupi tena, ooh, kwahiyo mnawasiliana naye wewe, mimi ananiona sina maana tena kwake…’ nikasema.‘Una marafiki mangapi bwana, huyo huyo,..unayemwamini kupidukia,...nahisi akija sasa mtamalizana naye na ukweli utagundulikana, ila bado nakukanya, uwe makini, hasa akija huyo rafiki yako,...’akasema‘Mimi hajaniambia, kwanza kaondoka bila kuniaga kwahiyo hata akija sizani kama nitakwua na muda wa kuongea naye…’nikasema‘Hutataka kuujua ukweli…?’ akaniuliza‘Ukweli upi…?’ nikauliza‘Kuhusu mtoto…?’ akaniuliza na ikawa kama kanitonyesha jeraha, nikakunja uso, nikabakia nimeduwaa, halafu nikasema;‘Nimeongea na mdogo wa mume wangu, anavyojikanyaga inawezekana akawa ndio yeye, au anaufahamu ukweli wote, nataka nije kuongea naye kabla huyo shetani hajarudi…’nikasema‘Leo hii inamuita shetani…’akasema‘Kutokana na wewe..ila mimi sijaamini, kama nimekosea mungu atanisamehe, ila kama ni kweli…sizani kama tutaelewana…’nikasama‘Utamzuia asirudi kusoma, wewe si ndio umemfadhili…?’ akauliza‘Hilo ni jambo jingine halihusiani kabisa na hili, siwezi kukosa fadhila za utu wema kwa ajili ya ubaya wa mtu…kama ataniambia ukweli, na ikawa hivyo ni kweli, kila kitu kipo wazi,…’nikasema‘Kwa vipi…?’ akauliza‘Mume wangu anafahamu…’nikasema Mara tukasikia docta akija na alipotufikia akasema;‘Oh mume wako kajitahidi sana leo, naona anafuraha fulani, mpaka kaweza kuinua miguu ni hatua nzuri sana, sasa jitahidini, awe na furaha kama hivyo, atapona haraka, ila mwishowe kaonekana mnyonge, …’akasema‘Kwanini docta…?’ akauliza docta rafiki‘Nahisi kuna kitu akikikumbuka kina mtesa, kuna kitu kasema, kapokea ujumbe unaompa shida sana, ujume wa simu kitu kama hicho…’akasema‘Oh, labda ni huyo mshenzi, kamtumia ujumbe kuwa anarudi..’nikasema kwa hasira‘Haiwezekani….’akasema docta rafiki.‘Huyo mtu hana jema…ikibidi hata simu msiwe mnamruhusu atumie, lakinikwa hekima zaidi…’akasema docta.‘Ni kazi, hataki kabisa kuchana na simu yake…’nikasema‘Basi lakini kwa hatua aliyofikia, ni maendeleo mazuri tu…’akasemaNa baadae huyo docta akaaga kuondoka, na mimi nikaona niende kumuona mume wangu kama kalaa…niliingia na kumkuta anachat kweye simu.‘Mume wangu hujalala..?’ nikamuuliza‘Kuna kitu nakifuta kwenye simu yangu lakini hakitaki…’akasema‘Kitu gani nikusaidie…’nikasema‘Hapana…ni ujumbe, ..haina shida, umeshafutika…’akasema na sasa akazima simu yake, na kiukweli mimi sina muda na simu yake hata sijui anatumia neno gani la siri, lakini nikawa na hamasa sana ya kujua kaandikiwa ujumbe gani.Nilipohakikisha mume wangu kalala, nikaichukua simu yake na kutoka nayo nje, nikampigia mtu wangu mmoja mtaalamu wa simu, anisaidie kuwasha simu iliyowekewa kifungo..ni mtaalamu sana, na akasema anakuja.NB:  Samahanini sana kwa kutokuwa hewani kwa kipindi cha siku tatu hivi, ni matatizo ya umeme na mtandano, na mitihani ya hapa na pale..WAZO LA LEO: Ndoa nyingi zina matatizo yake, na huenda yakawa ni matatizo madogo tu, lakini kwa wanandoa wakashindwa kuyatatua, kwa vile, hakuna anayekubali kushuka chini, kila mmoja anajiona anafahamu zaidi ya mwingine...au mmoja anaogopa kumuelezea mwenzake ukweli.....wewe kama rafikji tumia hekima kuwashauri, usitumie mwanya huo kuharibu badala ya kujenga. Hekima ya ushauri ni muhimu sana kwa watu kama hawo.‘Hakikisha umeharibu kila kitu…kila kitu, hasa mikataba, mengine nitayamaliza nikija…’Ni meseji pekee iliyokuwa imebakia kwenye simu, na imetumwa kutoka namba za nje...mume wangu alihakikisha kafuta kila kitu, hadi picha.‘Hasa mikataba, mikataba gani hiyo ya kazi, na ni nani huyu kamwandikia mume wangu, …’ nikajikuta nikisema, nikirejesha simu ya mume wangu sehemu nilipoichukulia, mume wangu alikuwa kalala kwa amani kabisa.Ujumbe huo ulinifanya niwazie kwenda ofisini, kuhakikisha kama kila kitu kipo sawa, na kuhakikisha mikataba ya kazi, na mingineyo ipo sawa sawa,…niliweza kuondoka, maana hali ya mume wangu ilikuwa sasa inaendelea vyema, na ningeliweza kumuagiza mfanyakazi wa ndani akaendelea na huduma nyingine bila shaka, muhimu ni mume wangu mwenyewe akubali,‘Mume wangu naona hali inaimarika sasa namshukuru mungu kwa hilo…’nikasema‘Kweli mke wangu nakushukuru sana…’akasema‘Sasa nilikuwa na ombi moja, nataka kesho asubuhi na mapema nifike ofisini kwangu mara moja, unaweza kuniruhusu…?’ nikamuuliza‘Ofisini eeh, …ooh, hivi kweli, samahani sana mke wangu,ina maana siku zote ulikuwa huendi kazini kwa ajili yangu, mimi nilijua upo likizo…’akasema‘Nilichukua likizo kwa ajili yako…’nikasema‘Nashkuru sana mke wangu,  sasa…, wewe nenda tu, si umeona mwenyewe siku hizi najitahidi, yaani sijui kwanini wiki hii nimeingiwa na kitu kikanifanya mwili uwe na nguvu za ajabu, nikaweza kusimama, na sasa natembea japo kwa shida…mmh, nahisi hizi ni nguvu za ajabu…’akasema‘Hongera, tumshukuru mungu…’nikasema‘Haya wewe kesho nenda tu..Basi kesho yake asubuhi nikafika ofisini.                 *****Kesho yake nilipofika ofisini, kwanza nilihangaika na maswala ya kikazi, ambayo yalinihitajia mimi kama mkurugenzi mkuu, na nilipomaliza, nikawa natatafakari kitu gani kingine nifanye kabla sijaondoka.‘Lakini usichelewe…’ nilikumbuka kauli ya mume wangu.Hata hivyo, muda ulikuwa bado, nikapiga simu nyumbani, na mfanyakazi akasema kila kitu kipo sawa, mume wangu anachukua mazoezi mwenyewe ya kutembea, ..‘Sawa naona nitachelewa kidogo…mwambie nilimpigia sikumpata sawa..’nikasemaSiku hiyo nilijiona sina raha kabisa, na ilitakiwa niwe na raha, maana mume wangu hali yake inaimarika, keshaanza kutembea kidogo kidogo....nilishangaa kumuona akiwa furaha kuliko siku za nyuma, ni kama vile amesikia jambo kubwa ambalo limefurahisaha sana Kiukweli niliombea iwe hivyo, ili apone haraka na maisha yaendelee, ila sikutaka kumdadisi sana, kujua kuna nini kimetokea, nilijitahidi kujizuia sana , kwa kutokumuongelesha au kumuuliza maswali ya kumpa mawazo, japokuwa sio kazi rahisi, kichwa changu kilikuwa na maswali mengi yasiyo na majibu na mwenye majibu ni yeye. Wakati nipo mezani nikifanya hiki na kile akili bado ilikuwa inafanya kazi, inawaza, na sasa nikakumbuka kauli ya mume wangu:Nakupenda sana mke wangu, niache nikuambie ukweli, nimekukosea sana, na ninachoogopa ni kuwa huenda kosa langu likaenda kuwaathiri wengine,  sasa umemuingilia mdogo wangu, sijui kakukosea nini, haya…kesho atakuwa mwingine, unaona eehe, ni vyema tukayamaliza haya sisi wenyewe…kama ni dhambi zangu nibebe mimi mwenyewe… achana na mambo  ya baba yako…au . Inaonekana kuna kitu kwa mume wangu…sasa ni kitu gani hicho‘Hakikisha umeharibu kila kitu…kila kitu, hasa mikataba, mengine nitayamaliza nikija…’‘Hasa mikataba….’ Nikasema hilo neno na lulirejea mara nyingi, na sijui ni kwanini kuna kitu kikanikumbusha jambo…. nikakumbuka…‘Mkataba wa ndoa…’Nilipokumbuka hivyo, nikasimama,‘Hivi kweli eeh, ule mkataba wetu wa ndoa,…ooh, afadhali, nimekumbuka, …sasa mambo yatakwisha kwa amani…sasa kama ni kweli, …mkataba ule utafanya kazi yake,...’nikasimama na kujinyosha,‘Mkataba wa ndoa…’nikasema nikichezesha mikono kuonyesha kuwa nimekumbuka jambo la muhimu sana.**********Nilipokumbuka hili nikataka kujirizisha , nilitaka nikausome tena ule mkataba…najua mume wangu atakuwa keshalisahau hilo, lakini ulikuwa ni muhimu sana kwenye maisha yetu,…na ndio ulionifanya nimuamini sana mume wangu, kwani mkataba huo ulikuwa umetufunga tusifanye makosa..‘Lakini kwa hili…wanalosema kuwa mume wangu kafanya,..ina maana kweli hakumbuki huo mkataba, hapana, watu wengelijua wasingelisema hilo, mume wangu aliuthamini sana huo mkataba, aliahidi na akawa wa kwanza kuutekeleza huo mkataba,…sasa iweje,..siamini,….’nikasema`Yah,..hili sasa litakuwa ndilo suluhisho la hili tatizo, na sizani kama mume wangu kalisahau hilo, kama kasahau, basi kakusudia kweli, na kama kakusidia kweli, basi sheria itachukua mkondo wake, maana ahadi ni deni…’nikasema kwa sauti. Hapo nikapata nguvu ya ajabu,….niliinuka kwa haraka kwenye kiti, nikasimama kwanza nikajinyosha tena na tena,…, sikuwa na haraka, sikuwa na jambo jingine muhimu kwa muda huo la kufanya, ...‘Kwenye ule mkataba ushahidi ni muhimu sana, hasa likitokea kosa, hilo lilisisistizwa sana, …’nikawaza hapo nikakuna kichwa‘Sasa mimi nina ushahidi gani, kuwa hayo waliyosema watu ni kweli, kuwa huenda , mume wangu kafanya kosa, na kosa lenyewe ni lipi, mmh…kazini, huko sina uhakika, lakini hili kosa kubwa la kuvunja masharti ya ndoa, je kweli kafanya hivyo, ushahidi upo wapi…?’ nikajiuliza‘Ok, ngoja kwanza,…nikausome vyema ule mkataba, mambo ya ushahid ni mengine, je nitauweza kuutumia muda ukifika, je …haaa, sizani, mume wangu hawezi kufany ahivyo, ina maana kasahau, haaaah, mungu wangu....’nikasema.Nikatembea hadi kwenye kabati langu maalumu, kabati hilo, huwa naweka kumbukumbu zangu muhimu, na hakuna mtu mwingine mwenye mamlaka ya kufungua hilo kabati, ….Kwanza nikafungua sehemu ya  ukutani, kuna kabati maalumu za nyaraka za ofisini, lipo ndani ya ukuta, na humo kuna sehemu maalumu, ina ufunguo wake, na kuna sehemu imejificha sana hapo ndio niliweka ufungua wa kabati… Nikafungua kabati, na ndani ya kabati kuna sehemu maalumu, humo nimeficha ufungua wa sehemu ambapo nimeweka hizo nyaraka, hakuna anayeweza kuuona huo ufunguo,… ni muda mrefu sijalifungua hilo kabati, maana vyote vilivyopo humo ndani, sio mambo ya kila siku ya kikazi. Na humo niliweka nakala zangu nyingine za mikataba ya kazi , jengo nk, pia kuna nakala za vyeti vya ndoa, na nakala za vyeti vya watoto…            ******** Wakati nimeshauchukua huo ufunguo, ndio nikakumbuka jisi gani tulifikia hadi kuamua kuwa na mkataba wa ndoa,… ilikuwa kama masihara tu, ilikuwa kama fikira zilizokuwepo kabla ya kuolewa , na baada ya kuolewa nikasahau, sikuona umuhimu wake tena.Nakumbuka ilikuwa kipindi nakaribia kujifungua, hilo wazo likanijia akilini, ikawa naliwazia sana, mpaka nikashindwa kuvumilia, ndio nikampigia simu wakili wa kazini, nikamuelezea hilo wazo.‘Muheshimiwa, kuna kitu kinanisumbua sana akilini, ni wazo tu, lakini nimefikiria sana, nikaona lina umuhimu wake,..mimi napendelea kuwa na kitu kama mkataba wa ndoa kati yangu na mume wangu....’nikasema‘ Wazo zuri sana,…basi kama mtakubaliana wewe na mume wako.., mimi nipo tayari, na nitawatengenezea mkataba mnzuri sana, na wenyewe mtaona jinsi gani utakavyowasaidia, ...ongea kwanza na mume wako mkubaliane, maana hilo ni swala la nyie wawili, kukubaliana kwanza...’akasema.Nikahamasika,na jambo hilo , niliona uwe mkataba mkubwa zaidi, ambao utagusia kila kitu,  mambo yote ya familia, kuanzia ya kifamilia hadi ya mali zetu,  na hili nililifanya makusudi, ili hata nisipokuwepo mimi, au mume wangu basi kusije kukatokea mambo mengine ya kuja kuidhulumu watoto wetu. Basi siku hiyo nilikaa nikiliwazia hilo, na jioni alipokuja mume wangu, nikaona nimwambie…ilikuwa siku ya kumbukumbu sana, na tarehe hiyo ilikuwa muhimu kwenye familia yetu.‘Mume wangu kuna kitu nataka nikuambie...’nilimwambia,  na yeye akanisogelea na kushika shika tumbo langu, huku akitabsamu , akasema;‘Usiniambia siku zinakaribia, maana nina hamu sana ya kumuona mtoto wetu huyu’akasema huku akinishika shika tumbo langu..kiukweli siku za awali, hakuna mtu angeniambia kitu dhidi ya mume wangu nikakisikiliza, nilimpenda sana mume wangu na nilikuwa namuamini sana.‘Usiwe na shaka mume wangu, siku yoyote kuanzia leo tunaweza tukaitwa baba au mama fulani, lakini sio hicho nilichotaka kukuambia.....’nikasema‘Mhh, ok…kuna nini,  niambie tu...mama watoto wangu …mama kijacho…’akasema huku akiendelea kushika shika tumbo langu.‘Kuna kitu siku nyingi nilikiwaza..awali nilichukulia kama mambo ya kishule tu, lakini jana , juzi nikaliwazia hilo, nikaona kumbe lina umuhimu wake,..na nilipoona  wazazi wetu wameanza kutkubali,  nikaingiwa na hamasa, ila sitaki wazazi wangu walifahamu hilo ni mimi na wewe tu…’nikasema‘Ehe, niambie…unazidi kunipa hamasa…’akasema‘Lakini unielewe mume wangu, ...sina nia mbaya na wazazi wangu, au jamaa zangu, au jamaa zako, lakini haya hutokea sana katika  dunia hii, na sisi kama wazazi inabidi tuwe makini kwa hili...’nikaanzia mbali.‘Kwani kuna tatizo kutoka kwa wazazi wako tena?’ akauliza akionyesha mashaka‘Hapana, hili ni kati yangu mimi na wewe, na familia yetu inayokuja, hatujui tutapata watoto wangapi, na hatujui watakuwa wakike au wakiume wangapi, ....hilo ni mimi na wewe lakini linalenga maisha ya mbeleni…’nikasema.‘Hahaha mke wangu bwana, una wasiwasi,..’akasema akiwa bado hajafahamu nataka kuongea nini.‘Mume wangu sipo huko kwenye kuzaa kwangu, nipo kwenye baada ya kuzaa, maisha yetu , mali zetu, na mipangilio yetu ya kila siku, maana hilo ndilo muhimu sana....’nikamwambia.‘Mhhh, mhh, kwahiyo watakaje labda....’akasema huku akikaa vizuri na kuniangalia machoni.‘Nataka tuwe na mkataba wa kifamilia...’nikasema na yeye akawa kama anashituka halafu akapepesa pepesa macho.‘Mkataba wa kifamilia, wa nini tena,..si sis tuna ndoa yetu tayari ndoa ni mkataba tosha au sio,… unahitajia mkataba gani tena, huniamini au kuna nini umekigundua dhidi yangu, au familia yangu au yako?’ akaniuliza kwa mashaka.‘Niliongea na wakili wetu wa kampuni,.....ambaye kama unavyojua, anashughulika kwenye kampuni zote mbili yangu na ya kwako pia, mimi sina lengo la kuingilia kampuni yako saana, lakini hili la mkataba ni kwa ajili ya mali zetu zote, zikiwemo kampuni zetu,  ili kusije kukatokea sintofahamu baadaye....’nikasema.‘Mhhh, okey, niambie maana mpaka sasa sijakupata vyema, na hata hivyo huyo wakili hajaongea na mimi... kwahiyo sijui unachotaka kusema ni nini hasa…’akasema.‘Ni hivi, katika maswala yote ya mali, kama hakuna matatizo, hakuna shida, lakini kukija kutokea matatizo, watu , binadamu tulivyo, cha kwanza kukimbilia ni mali, hutaamini, watu mlikuwa mnapendana, mnasaidiana, ni marafiki, lakini kukitokea mfarakano kidogo tu, wote akili na macho yao ni kwenye mali...’nikasema‘Ni kweli, lakini sio mimi….’akasema‘Najua, sote tutasema hivyo…lakini sio kwetu tu, na wengine wa nje, umeona visa vingapi vinatokea, baba au mama, au baba na mama wakiondoka, kunatokea nini,, watu ambao hata wahajui mali imetokea wapi ndio wa kwanza kuja kuvamia mali za mayatima,  wakitamani kila kitu..’nikasema‘Ni kweli…’akasema‘Sasa mimi nimesoma sheria kidogo, na nilitaka kile nilichokisomea angalau kije kufanya kazi kimatendo kwenye familia yetu, unaonaje hapo kwanza,…’nikasema.‘Mke wangu mbona unanitia wasiwasi, ina maana unaogopa kuwa ukienda kujifungua ....unaweza usirudi, hapana bwana,…mke wangu kuzaa ni kawaida tu, hutapata lolote baya...hutakufa bwana, usinitishe…usinitie wasiwasi na majonzi, hakuna shida, huna matatizo yoyote, docta kasema huna tatizo lolote…utajifungua salama…’akasema.‘Mimi siongei hili kwa vile nakwenda kujifungua, hapana, naliongelea hili kwa ujumla wake, ni jambo la maisha yetu,...na ukumbuke mume wangu, sisi kama wandamu, hatuna mamlaka na mungu, kuwa nitaishi muda gani au nitakufa lini,...’nikasema.‘Ni kweli…’akasema bado akiniangalia kwa mashaka.'Lakini hata hivyo ni vyema tukawa na utaratibu mzuri tu, tukajiandaa kwa lolote lile, hata kama tupo hai, bado mkataba unaweza kutusaidia katika maisha yetu, tukawa na utaratibu mnzuri tu kwa nia njema,...’nikasema‘Ni sawa, nana kukuelewa…’akasema‘Na hatuombei mabaya…, maana sisi ni wanadamu,kama kutatokea mfarakano wowote, makataba huo utakuja kutusaidia...hamna haja ya kushikana mashati, wakili yupo na mkataba upo..’nikamwambia.‘Sawa, sawa kabisa....kwahiyo ulikuwa unataka kusema nini, ..tuwe na mkataba, kuhusu nini hasa mali, au…maana ndoa ina masharti yake, kidini kisheria, imebainishwa kila kity au..sijakuelewa zaidi, ?’ akauliza akishika kichwa, nahisi alikuwa akiwazia mbali, na mimi nikamwambia;‘Eheeeh, sasa tulia nikuambia, mimi niliongea na wakili wangu, akanishauri kuwa sisi ni wanandoa na pia mungu katujalia tujaliwa kuwa na watoto, tuna kampuni, na bahati nzuri tuna kampuni mbili, yako ya ya kwangu..na baba yupo ana hisa kwetu japokuwa ni kidogo, nia ni kuhakikisha anatulinda, tulifanya hivyo kwa nia njema tu..sio kwamba kila mtu ana maisha yake, hapana, ni katika kujijenga zaidi….’nikasema.‘Sawa kabisa, na huo ulikuwa ni ushauri wako, japokuwa mimi nilitaka tuwe na hisa nusu kwa nusu kwenye kampuni yangu, hata kama sio ya kwako, maana mtaji karibu wote unatoka kwako na kwa wazazi wako...’akasema.‘Hapana hilo halikufanyika kwa nia mbaya...sote ni wazazi wetu, na uchungu wa familia ulio nao wewe ni sawa na nilio nao mimi, ndio maana hakuna aliyefikiria kuwa ukipata hisa zote hizo, utadhulumu, au utakimbia nazo, ..hilo halipo, na utambue kuwa mimi nakuamini moja kwa moja...amini hivyo...’nikamwambia.‘Sawa kabisa hata mimi nakuamini sana,...’akasema.‘Sasa ni hivi, niliongea na wakili wetu, nikamwambia atayarishie mkataba, mkataba ambao, utagusa kila kitu chetu, kuanzia, mali, watoto na hata ndoa yetu,...hii itasaidia sana, ili tuwe makini na si kwenye mali tu, bali pia na kwenye ndoa yetu, mkataba huo uainishe kuwa kama mmoja wetu atakiuka maswala ya ndoa, basi ...amevunja mkataba na mali na kila kitu chake, kinachukuliwa,..’nikasema‘Mke wangu, unajifunga wewe mwenyewe…’akasema kwa kujiamini‘Nikuulize wewe je upo tayari na kitu kama hicho , maana mimi sina shida....’hapo nikatulia.‘Una maana mtu akikiuka hata kwenye maswala ya ndoa…kama, usaliti au sio..ok, inakwenda hadi kwenye mali, mtu anakuwa hana haki na mali tena, kuachia kuchana nak….ok, …mimi sina shida na hilo,..ni sawa kabisa, lakini wewe huoni kuwa wewe ndio utadhulumiwa…’akasema‘Usijali…’nikasema‘Unajua nina maana gani, mali ni zako, mtaji umetoka kwa wazazi wako, leo umevunja mkataba mali inakuja kwangu, je wazazi wako watakubali hivyo, hapana hapo kuna walakini...’akasema.‘Ndio hivyo, kwani wewe unatarajia kukiuka masharti ya ndoa, mimi naliona kwangu ni kinga, sitaweza kukiuka, na sheria ni msimeno, nikikiuka sheria ipo una haki ya kudai haki yako..au sio..?’ nikamuuliza.‘Kwangu mimi mke wangu sina shida, mimi  nakupenda sana mke wangu, sizani kama kuna mtu anaweza kuja kunivuruga akili…, hakuna..kwahiyo mimi naunga mkono huo mkataba, tena bila wasiwasi....lakini ni wewe tu, kama ikatokea, haya utapoteza kila kitu, ila siwezi kukuacha....’akasema na mimi nikamkatisha na kusema;‘Sawa mimi nilitaka nikuweke wazi kwa hilo,na nilimwambia wakili autayarishe, halafu tutakutana sote kwa pamoja tuusome, tuone kama kuna chochote cha kubadili, au kuongeza,..na ningelipendelea ikiwezekana iwe kama katiba yetu ya familia, na nina imani kuwa hakuna atayekiuka huo mkataba, mimi sina shaka kwangu...’nikasema na kumwangalia.‘Hata mimi..mimi sina shaka na hilo, ..wewe niamini mia kwa mia...’akasema.‘Mimi nina uzoefu , mimi naheshimu sana hayo mambo ya mkataba, kwani nimeona jinsi gani unavyosaidia maswala ya kikazi, ndio maana nikaona  kwanini mkataba kama hiyo tusiitumie kwenye familia zetu, ili kukwepa makatizo mbeleni..kaa ufikiria kwanza…’nikasema.‘Hakuna shida kabisa, mimi nipo pamoja na wewe, na nipo tayari kwa hilo...naliunga mkono kwa nguvu moja.’akasema.‘Sawa kama umekubali basi, tuombe mungu, ...na ni vyema wewe ukakaa ni kuliwazia hilo kwanza, ili uone ni vitu gani muhimu vinahitajika kwenye mkataba huo, isiwe ni mawazo yangu tu, ....au  isiwe ni mawazo ya wakili wetu tu,...mkataba huo uwe kama katiba yetu..unaonaje..?’ nikasema.‘Ni sawa kabisa mke wangu‘Basi ni vyema, basi kaa ufikirie zaidi….’nikasema nikipumua, sikutarajia kuwa mume wangu atakubaliana na hilo.‘Mimi sina cha kufikiria zaidi, cha muhimu tukutane na huyo wakili tuone jinsi gani alivyoandaa, na kama kuna nyongeza mimi nitasema, na wewe pia utasema, ili mwisho wa siku tuwe na kitu kimoja cha watu wote, hilo naona lisichukue muda, hata leo, kama wakili keshaandaa, tunaweza kumuita...’akasema.‘Sawa tutamuita wakili wetu kesho,kama yupo tayari, na kama keshaandaa, nilimuambia akasema ataandaa ,lakini kwanza mimi na wewe tukubaliane....’nikasema ‘Sawa mke wangu, mimi sina shida kabisa mke wangu nakuunga mkono kwa wazo hilo la hekima, nipo tayari  kwa wakati wowote...’akasema.Na baada ya siku mbili mkataba ukatayarishwa, baada ya kukutana na kupitia kila kipengele, na tukaongezea na mengine mengi, ilimradi uwe mkataba unaogusa kila kitu kwenye maisha yetu, na tukaupitisha , ukapelekwa mbele kisheria, na mwisho wa siku ukawa ndio katiba yetu.Mwanzoni tulikuwa tukifuatilia sana, na ikawa kila mmoja ana hamasa na utaratibu wote, hadi tukawa tumeweza kushika kila jambo, na kila mmoja akawa na tahadhari , asije akavunja mkataba, na kila mara tunakumbusha,kama jambo limafanyika, sivyo ndivyo, utasikia `mkataba unasemaje...’Siku zikaenda, mambo yakwa mengi, watu tukajisahau,ikafikia hatua hakuna aliyejali kangalia mkataba unasemaje,ila kuna yale mambo ya msingi, kama ya ndoa, masilahi, na uwajibikaji,...mengine madogo madogo yakawa yanakiukwa hapa na pale, hakuna aliyejali,...ilimrdi tunaaminiana...tukajisahau lakini maisha yakaenda mbele, maana kulikuwa hakuna matatizo.`Ngoja nikausome tena ule mkataba wa familia...’ nikasema sasa nikifungua kabati, hiyo ni nakala niliificha sehemu maalumu,  hakuna mtu anayeweza kuupata.Ufunguo ulikuwepo pale pale,....nikauchukua, na kusogea kwenye kabati, nikahakikisha nimefunga mlango wa ofisini, kabla sijafungua hilo kabati, maana sikutaka mtu aingie na kuja kunisumbua. Nikasogea kwenye lile kabati, na kuchuchumaa, maana sehemu nilipoweka hizo nyaraka ni sehemu ya chini ya hilo kabati, ...Nikafungua kidroo hicho, kilikuwa na namna ya kukifungua, sio kwa haraka, ni kama unafuatilia namba, nikafuatilia kwa makini mpaka mlango wake ukafunguka...., nakumbuka kabisa wapi niliuweka ile nakala ilikuwa pembeni,..sehemu yake maalumu, niliisimamisha  maana ni mkataba mrefu, sikutaka ijikunje…Nikavuta kidroo chake, kilikuwa kitupu hakuna kitu…‘Haiwezekani…’nikasemaNikavuta sehemu yote, kulikuwa na nyaraka nyingine tu ambazo kwa muda huo sikuwa na umuhimu nazo...Hapo sasa, nikahisi moyo ukinienda mbio,....nikatulia kidogo, labda nimesahau, labda niliwahi kuuchukua huo mkataba, hapana, sijawahi, ni muda sijautumia, sasa upo wapi.‘Haiwezekani, nakumbuka kabisa huo mkataba niliuweka hapo, kwenye sehemu yake maalumu…’nikawa naongea peke yangu sasa. Na mimi ni hodari sana wa kuweka vitu vyangu kwenye mpangilio wake, na nahakikisha kila nikitoka ofisini kwenda popote, kila kitu nakiweka katika mahali pake kwa mapangilio wake, hilo sikosei hata mara moja.Nikatuliza kichwa na kutafakari, lakini hakuna dalili yoyote kichwani ya kuniambia kuwa labda niliwahi kuutoa hapo. Nikaingiza mkono ndani na kusogeza kwa ndani kabisa, kama umegandia kwa ndani, hakukuwa na kitu kama hicho, nikaanza kuhisi vibaya. Sasa nikatoa kila kitu, na kupanga upya, ili kuhakikisha, , lakini sikuona cha mkataba wala nini….Mkataba haupo, ….‘Ni nani huyu mwenye nia mbaya,kaweza kuugundua huo ufungua, na akautoa, na kufungua hili kabati, halafu akalifunga na kuhakikisha kuwa hajagusa kitu kingine chochote, ni nani huyu…’nikawazaKiukweli ufungua wa hapo ni huo huo, hakuna  akiba...na hakuna anayefahamu kuwa ufunguo huo upo wapi zaidi ya mimi mwenyewe,….na ni nani anayefahamu kuhusu huo mkataba, zaidi ya mume wangu na wakili…,nikajaribu kuangalia tena kwa makini, lakini mkataba ulikuwa haupo....Mkataba haukuwepo....!‘Hakikisha umeharibu kila kitu…kila kitu, hasa mikataba, mengine nitayamaliza nikija…’NB:  Sehemu hii ni muhimu sana, ndio maana nimeandika kwa taraibu na msisitizo, msichoke kusoma sehemu hii, itatusaidia sana kwenye maisha yetuWAZO LA LEO: Kama tutakuwa na taratibu za mikataba kwenye ndoa zetu, kwenye familia zetu, kwenye vikundi vyetu, kwenye maisha yetu,kwenye sehemu zetu za kazi, nk, tungeliepuka migongano na mfarakano, maana mambo mengi yangelitatuliwa kisheria. Familia nyingi zinajikuta kwenye matatizo,pale anapofariki mmojawapo, au pale kunapotokea tatizo, na kutokuelewana. Na mwisho wa mifarakano hiyo, au matatizo hayo, wahanga wa haya yote ni watoto na akina mama, ambao wanakuja kudhulumiwa haki zao. Je hatuoni kuwa ili kukwepa hayo yote, ni bora kukawa na mikataba katika maisha yetu? Tuliwazie hili na wanasheria watusaidie...Nilipohakikisha kuwa kweli ule mkataba haupo kwenye sehemu yake, nikamuita mmoja wa wafanyazi wangu wanaofanya usafi na kujaribu kumdadisi kama aliwahi kumuona mtu mwingine akiingia ofisini kwangu wakati nipo mapumzikoni.‘Hakuna bosi aliyewahi kuingia bila ya ridhaa yangu…’akasema‘Lakini kuna mtu aliwahi kuingia, ukiwemo‘Hakuna bosi…mtu akija namuekeleza kwa msaidizi wako…’akasema,   ‘Kwani kuna kitu kimepotea bosi?’ akauliza kwa mashaka.‘Bado sijahakikisha, kama kuna kitu kimepotea, ila kama kipo nitakuambia, na uwe na uhakika ..jaribu kukumbuka vyema kama kuna mtu ulimuona akiingia humo, au alikuomba ufunguo, ...ndicho ninachotaka kusikia kutoka kwako, nakuamini sana...? ‘nikauliza‘Hakuna kabisa mtu aliyeingia humo,,...hilo nina uhakika nalo...’akasema na kwa vile mimi namwamini sana huyu mfanyakazi wangu sikutaka kumshinikiza zaidi.‘Hamna shida,....’nikasemaNiliona hakuna haja ya kuendelea kuuliza uliza watu wengine, na sikuwa na hamu tena ya kuendelea kufanya kazi kwa siku hiyo, haraka nikaondoka zangu kurudi nyumbani maana bado nilikuwa likizo. Wakati nikiwa ndani ya gari, nilijaribu kuwaza, nifanye nini,...na sikutaka mambo haya ya ndani ya familia yangu yatoke, nje, na mtu pekee angeweza kunisaidia kwa hili ni rafiki yangu, ambaye hayupo.‘Lakini nasikia anarudi…’nikajikuta nikisema hivyo‘Hata hivyo maswala ya mkataba wangu na mume wangu hastahiki kuhusika kabisazaidi ya wakili wangu..’nikasema.Hata hivyo sikuwa na shaka sana, maana ipo nakala nyingine nyumbani , nikifika nitaisoma, ila kiukweli kupotea na nakala hiyo kulipa ni shida sana, ni nani kaichukua na kwa nini. Akili yangu ilivyo, sikuwa na dalili yoyote ya kumshuku mtu yoyote, na kila niliyemuwazia, nilijikuta nikimuondoa kwenye ushukiwa.Nafasi kubwa ilikuwa kwa mume wangu, lakini alikuwa mgonjwa,...na kabla hajaumwa, nakumbuka ipo siku niliwahi kuuchukua huo mkataba na kuusoma, na kuurejesha nilikuwa natafuta mkataba wa kampuni ya mume wangu, nilikuwa na nakala , na siku mbili baadae ndio akapatwa na hiyo ajali.‘Haiwezekani akawa ni mume wangu,, yeye ana nakala yake,Nilijaribu kumuwazia mtu mwingine, lakini sikuweza kumpata, kwani sikuona umuhimu wake na huo mkataba wetu.‘Sasa atakuwa ni nani?’ nikajiuliza bila kupata jibu.Nilifika nyumbani, nikaliendesha gari langu mbele kidogo, kuna duka langu la vipodozi, na vifaa vingine vya namna hiyo,, nikamwambia mlinzi wa pale, aniangalizie hilo gari, nitalipitia baadae, nikarudi nyumbani  kwa miguu, ni hatua chache, kwani ukuta wa sehemu hizo za duka zimeshikana na ukuta wa nyumbani kwangu.Kwa haraka nikaingia ndani, na moja kwa moja nikakimbilia chumbani kwangu, nikafungua mlango taratibu maana sikutaka kumsumbua mume wangu kwani akiwa amelala haitakiwi kusumbuliwa.‘Kwa vile kalala nitafungua kabati na kuchukua huo mkataba, nikasome huko mbele kwa mbele..’nikasema na huku nikihakikisha kama kweli mume wangu kalala. Alikuwa kalala, dawa zilikuwa bado zinafanya kazi,...nikageuka na kuelekea chumba chetu cha maktaba,  humo ndipo kwenye kabati, sehemu hiyo ni kama ofisi yetu ndogo.Nikajifungua, kuhakikisha kuwa hakuna mtu atakayekuja kunisumbua, haraka nikaliendea kabati tunapoweka nyaraka za kifamilia, huwa kila mmoja ana ufungua wa hilo kabati, lakini mimi nilikuwa na sehemu yangu nyingine, ambayo mume wangu hana ufunguo nalo, ninaweka vitu vyangu vya kike, lakini nilitengeneza sehemu ya kuhifadhia kumbukumbu zangu binafsi ambavyo .Nikafungua ile kabati, ...niliona kila kitu kipo kama nilivyokuwa nimeacha, hapo huwa napatumia mara kwa mara, nikihitajia vitu vyangu , nikasogeza vitu vingine na kuinua sehemu ambapo niliweka huo mkataba, ..sikuamini macho yanguKweupe...hakuna kitu...nikashikwa na butwaa, haiwezekani , haiwezekani, sasa hili ni tatizo, ...‘Kwa hali ilivyo, sasa naanza kumuhisi mume wangu, hakuna mwingine anayeweza kuhangaika na huu mkataba,..huyu atakuwa ni mume wangu tu..’hapo nikasema kwa sauti‘Hata hivyo kaupatia wapi ufungua wa hapa, uungua bado ninao mwenyewe na akiba yake....’nikawaza mwa kwa sauti, nikafunga kama ilivyokuwa na sikutaka kuchukulia pupa…nilipohakikisha nimefunga kama kawaida nikageuka kuondoka.Ni wakati nataka kutoka nikakumbuka kitu, sijui kwanini niliwazia hivyo, nikarudi sehemu ile tena, nikafungua, upande wa pili yake.., na kuangalai hicho nilichotaka kukiangalia...nikakuta kipo pale pale...sijui kwanini nilitaka kufanya hivyo, lakini moyo ulitaka kuhakiki, kuwa silaha yangu binafsi bado ipo, ..huwa nina kibali cha kumiliki bastola, na tangu niinunue, ni muda sasa sijawahi kuigusa. Mwanzoni nilikuwa na tabia ya kwenda kulenga shabaha hata kuwindia, lakini kutokana na majukumu, nikawa sina muda huo tena. Kwahiyo ni muda sasa sijaitumia hiyo silaha‘Hata hivyo silaha ya nini....?’ nikajiuliza, niliikagua na kuhakikisha ipo salama, baada ya kumaliza kuikagua nikafuta alama za vidole, kama kawaida yangu,..na kurudisha sehemu yake.nikahakikisha nimefunga kabati vyema, nikafungua mlango wa hicho chumbani , na kutoka, hapo akili ilikuwa kama sio yangu, hasira..lakiniNikaingia chumbani, nikajikuta nashikwa na butwaa, kitanda kilikuwa kitupu, mume wangu alikuwa hayupo kitandani,…kaamuka muda gani na kaenda wapi…nikajiuliza kwa haraka nikajua katoka nje.‘Huyu mume wangu kaamuka saa ngapi?’ nikajiuliza maana nilihakikisha kuwa alikuwa kalala, kabla sijaenda huko maktaba yetu, na kuamuka huko ni kama vile huyu mtu alikuwa macho, maana sikukaa muda mrefu pale ndani.Na mimi kwa haraka nikatoka kule chumbani na kwenda sebuleni, sehemu ya mapumziko, …lakini kwa kunyata kimia kimia…na pale sebuleni.., nikamkuta mume wangu kakaa kwenye sofa.Alikuwa hajaniona, na mkononi kashika kitu.Taratibu nikamsogelea, hadi nikamkaribia,….nahisi alihisi kuna mtu nyuma yake, kwani aligeuka,… akaniona, alishituka, mpaka nikaogopa, maana kwa hali yake, hakutakiwa kushituka kiasi hicho,....‘Oh, mke wangu umerudi saa ngapi..si ulisema hutarudi mapema?’ akaniuliza huku akiwa ananishangaa, na mkononi alikuwa kashika mkataba.Ule mkataba wa kifamilia…!!Kwanza nilijifanya kama hakuna kitu, lakini yeye aligundua kuwa macho yangu yalikuwa yameangalia ule mkataba aliokuwa nao mkononi, na nilivyomshitukizia, hakuweza hata kuuficha, akawa kaushika vile vile mkononi, na mimi nikawa namsogelea kuhakikisha kuwa ni huo mkataba wetu, yeye ana nakala yake, na mimi ya kwangu, ila mimi kuna alama niliweka kwenye nakala zangu.‘Nilikuona umelala, wakati naingia na sikutaka kukusumbua, kuna kitu nimekifuatilia huku nyumbani, na huenda nikarudi tena ofisini, ila na mimi nashangaa maana muda huu ulitakiwa ulale, kwani hujanywa dawa zako sawa sawa nini?’ nikamuuliza.‘Dawa nimekunywa, lakini sasa hivi hata nikinywa, sipati usingizi kama ule wa mwanzo...’akajitetea.‘Sawa mimi naona nisikusumbue,,..’nikasema kama vile nataka kuondoka, lakini nikamsogeela na kuangalia kile alichokuwa kashika mkononi nikasema;‘Naona unasoma mkataba vipi tena, unajikumbushia zile enzi zetu za kuishi kwa kufuata mkataba, hahaha mume wangu bwana, au unaangalia nini, na peni, kama unasahihisha jambo, kuna nini kimekukwanza mume wangu ...?’ nikamuuliza na yeye akajibaragua kama vile anataka kuuweka chini, kama vile sio kitu muhumi sana kwake, akasema;‘Aaah unajua tena ukikosa la kufanya, niliona nisome some tu kupoteza muda.....lakini ....’akasita.‘Hakuna wasiwasi mume wangu, ...hiyo naona kama ni nakala yangu au , niliiweka wapi, sijui, uliipatia wapi...?’ nikamuuliza nilipoona ile alama yangu, nakutambua kuwa ilikuwa ni nakala yangu.‘Hapana hii ni nakala yangu, sio ya kwa-kwako…kwani nakala yako haipo?’ akaniuliza akionyesha ishara ya kushangaa.‘Unavyouliza ni kama vile unafahamu kuwa nakala yangu haipo, au?’ nikamuuliza huku nikitabasamu, nilikuwa nimejisahau sasa, maswali kama hayo sikutakiwa kumuuliza.‘Ndio maana nakuuliza, maana kila mmoja ana nakala yake, au sio,...mmh, halafu mke wangu nilataka tuongee kitu muhimu, nilikuwa najaribu kupitia baadhi ya vipengele mbali mbali kwenye huu mkataba eeh, na sijui utakuwa na nafasi tukae tuongee, kwasababu mengi yamepita, na hatujawahi kuongea haya yaliyotokea...’akaanza kusema.‘Mume wangu achana kabisa na mambo hayo, wewe hujafikia muda wa kuongelea hayo mambo, hujaruhusiwa na docta kabisa…subiria kwanza upone, na hata hivyo, sioni kwanini ukimbilie kusoma katiba kwa sasa, huoni utajitakia matatizo, unakumbuka tulivyokubaliana, hata kwenye mkataba hilo lipo kuwa mtu akiumwa, mambo ya mkataba yanawekwa pembeni kwanza,mengine yote yanasahaulika mpaka anayeumwa apone..sioni umuhimu wa mkataba ukiwa kwenye hiyo hali.’nikasema.‘Swali linalonisumbua ni kuwa nikipona, itakuwaje…inanipa shida sana hiyo, na akili yangu haiwezi kutulia kama tusipolitatuia hilo, unanielewa hapo..itakuwaje sasa…?’ akauliza huku akifungua fungua ukurasa kwenye ule mkataba.‘Kwani una wasiwasi gani mume wangu,...mimi sioni tatizo, kwani ulishaniomba msamaha, nikakukubalia kuwa nimekusamehe, hayo yanatoka wapi tena?’ nikamuuliza .‘Kusamehe kwa maneno ni kitu kingine, lakini yapo mambo ya kisheria…na haya ni kati yangu mimi na wewe…sasa….’kabla hajamaliza mlango ukagongwa, nikageuka kuangalia mlangoni, na mara ukafunguliwa akaingia docta, rafiki wa mume wangu, ambaye aliponiona kwanza alijifanya kama vile hajashituka. Lakini nilimuona na dalili ya kushtuka, hakutarajia kunikuta hapo‘Nilisikia umekwenda kazini au…mbona umerudi mapema hivi,.....?’ akaniuliza docta‘Kwani tuliongea na wewe leo, kuwa nimeenda kazini na sitarudi mapema, mbona unaingilia mambo yasiyokuhusu, unakuwa kama unafahamu ratiba yangu kuwa nitarudi nyumbani kwangu saa ngapi, kwanza ukumbuke kuwa nipo likizo, kwa ajili ya kumuuguza mume wangu!’ nikasema nikimwangalia kwa makini machoni.‘Nilipiga simu kwa mumeo akasema haupo, ....nikajua upo kazini, na kama upo kazini, sizani ungelifika tu na kuondoka…’akasema na akawa sasa anamuangalia mume wangu kwa makini, nahisi kuna ishara aliona kutoka kwa mume wangu ndio akakatiza maneno, sikutaka kuongea sana au kufanya lolote litakalo wakwanza, nikasema;‘Mume wangu naazima hii nakala …mara moja…’nikasema nikiwa nimeinama kuichukua hiyo nakala, ni kitendo cha haraka, maana nilipotamka hivyo, nay eye alikuwa keshafikisha mkono kama kuishika hiyo nakala ya mkataba, lakini mimi nilihsiwahi‘Hapana nina kazi nayo…si una ya kwako…’akasema‘Ni kitu kitu kidogo, nakurudishia sasa hivi, nyie si mnaongea wewe na rafiki yako, au sio…’nikasema nikimuangalia docta, na docta akawa anaonyesha uso wa tahadhari, akimuangalia sana mume wangu‘Mhh, hapana hiyo nakala yangu ...ina mambo yangu binafsi nimeandika,....unaonaje ukaenda kuchukua nakala yako, kama hutojali mke wangu...’akasema akionyesha wasiwasi fulani.‘Usijali mume wangu, nitakurudishia tu, ....endeleeni kuongea...’nikasema huku nikiwa nimeshauchukua na kuanza kufungua sehemu za ndani za mkataba ule, niliona mistari imechorwa chorwa, kama kukata kata kata sehemu, na maneno mengine yameandikwa kwa mkono, kama vile ni rafu.Kiukweli hii ilikuwa nakala yangu , pamoja na sahihi, kuna sehemu niliandika mambo yangu, na sahihi,  lakini kwa hivi sasa naona mume wangu naye kaandika mambo yake..akifuta yale yangu…, nikageuza kuangalia juu, nikaona sahihi yangu na sehemu niliyokuwa alama ipo, kuashiria sijakosea hiyo ilikuwa ni nakala yangu...’‘Mke wangu, ...nauomba huo mkataba, tafadhali....’akasema huku akisimama kuja kuuchukua mkononi mwangu, na mimi nikasogea pembeni nikiendelea kufungua fungua, na yeye akawa hana jinsi, akatulia huku kanikazia, macho akionyesha wasiwasi,Mimi kwa muda huo  sikujali tena kuwa nitamkwaza, nikawa sasa natembea kutoka nje nikiwa bado nimeushikilia huo mkataba huku nikiendelea kufungua sehemu nyingine, na hakukua na maandishi ya kuhakikiwa kwenye sehemu nyingine zaidi ni kwenye vipengele vya ndoa.Nikafika mlangoni bila kugeuka nyuma, na huyo nikatoka nje bila ya kugeuka nyuma, nikawa sasa naelekea kule kwenye bustani, ili nikae, nitulie nipate muda wa kuangalia ile sehemu,…kwa haraka nikachukua simu yangu na kutaka kupiga picha ili niwe na kumbukumbu, lakini kabla sijafanya hivyo nikasikia sauti toka ndani;`Shemeji,...njoo haraka...’ ilikuwa sauti ya hatari kutoka kwa docta, rafiki wa mume wangu. Simu ililia mlioa wa kuchukua picha, lakini sizani kama itakuwa imelenga sawa sawa maana nilisthuka… Kwa haraka nikajizoa zoa na ule mkataba haukubanduka mkononi, nikakimbilia ndani, nilipofika nikakuta mume wangu kalala sakafuni..na docta kamuinamia akimfungua shati, na mimi nikamsogelea na kuuliza;‘Kuna nini tena jamani..?’ nikauliza, na docta akaniangalia kwa macho, yaliyoonyesha kukerwa, na kusema;‘Umefanya nini sasa...nilishakukanya, unaona sasa....’akaanza kunilaumu mimi na sikujau ananilaumu kwa lipi….**************Hali ya mume wangu ilibadilika na kuwa mbaya,na juhudi za docta hazikufua dafu, alimpa huduma ya kwanza lakini haikusaidia,  ikabidi akimbizwe hospitalini na docta huyo huyu na alipofika docta wake akamkagua, na kusema haraka aingizwe kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.‘Kuna jambo gani limemshitua?’ akauliza huyo docta baada ya kumhudumia na kurudi pale nilipokuwepo, na hadi muda huo tulikuwa hatujaongea lolote na docta rafiki.‘Kwakweli mimi siwezi kujua, labda tumuulize rafiki yake, maana mimi nilimuacha wakiwa naye, akiwa mzima kabisa, na niliwaacha hata dakika mbili hazikupita, nikasikia sauti ya huyo rafiki wa mume wangu akiniita kuwa mume wangu hali yake sio nzuri...’nikasema.‘Mhh, inaonyesha kuwa kuna kitu kimemshutua, na wewe unakifahamu ni kitu gani,...hukutakiwa kulazimisha kufanya kitu ambacho hakitaki, au alipata mshtuko fulani, mshituko kwake ni tatizo…lakini….’akasema huyo docta, na docta rafiki akamkatiza na kusema;‘Nahisi ni ule mkataba…’akasema‘Lakini mbona ni mkataba wetu mimi na yeye, na anaufahamu siku zote kuwa tunao , na haikuwa na ubaya mimi kuuchukua, na hata hivyo wewe unajuje kuwa ni kuhusu huo mkataba…?’ nikauuliza kwa mshangao.‘Kwasababu nilimuona na dalili mbaya, wakati huo mnaongea na uliuchukua mkataba akawa hataki, ile hali ikawa inazidi kumsukuma kwenye hatari…’akasema‘Usinitupie lawama kabisa…’nikasema.‘Kwani ni mkataba gani huo, inawezekena kuna kitu hakipendi kwenye huo mkataba…?’ akauliza docta anayemtibia‘Hakuna cha maana vitu vilivyopo humo ni kati yangu na mume wangu hakuna la zaidi, na sioni ni kwanini liwe ni tatizo hilo…..’nikasema.‘Una uhakika kuwa hakuna jambo linalomkwanza mume wako kwenye huo mkataba, nahisi inawezekana kuna kitu ambacho anakihofia..?’ akaniuliza huyo docta, na mimi nikasema;‘Lakini sizani hata kama kuna kitu…kipo kipo…nahisi ana lake jingine, hata sielewi, kwanini iwe hivyo, unajua nimejitahidi sana, sasa nachoka jamani…aah, basi nifanyeje jamani?’ nikasema huku nikuliza kwa mshangao.‘Muhimu, ni kumuhakikishia kuwa kama kuna lolote humo, halitafanya kazi, au kama hataki wewe uwe nao, mrejeshee, haraka iwezekanavyo…’akasema docta rafiki.‘Hivi kwanini unaongea hivyo, unajua lolote kuhusu huo mkataba maana, maana moja ya makubaliano yetu mimi na yeye ni kuwa mkataba huo ni baina yangu mimi  na yeye tu, wewe umayefahamu vipi hayo…?’ nikamuuliza docta rafiki kwa ukali, mpaka docta anayemtibia mume wangu akatuangalia kwa mshangao‘Off course, …mimi sijui lolote zaidi ya kuwakuta pale mkiwa kwenye kubiashana..eeeh, nahisi , mimi nahisi huenda mwenzako kinachompa shida kwa sasa ni kuhusu mliyoandika kwenye huo mkataba…sasa sisi hatujui ni nini kilichomo humo ndani,...je huna uhakika kuwa huenda kafanya kitu kinyume na huo mkataba wenu..?’ akaniuliza docta rafiki.‘Mimi sijui, na hakuna kitu kama hicho, huo ni mkataba wetu tu wa kikazi, hakuna tatizo, …’nikasema kuvunga ili isije kuleta maana kamili ya kilichomo kwenye huo mkataba.‘Haya, kama unaona hivyo, sawa,...ila jitahidi sana, kuwa mvumilivu, huko mnapokwenda, ni kubaya, na mwenzako yupo mahali pabaya, hajijui...na usije ukafanya mambo kwa pupa, ukaanza kujijutia, ....itakuathiri sana kwenye maisha yako...’akasema.‘Hamna shida, hilo niachie mimi,..., cha muhimu ni kutafuta njia za kumponyesha huyo mtu, na sijui nifanye nini, maana kila ninachotaka kukifanya, kwa masilahi yetu, kinakuwa na utata, nitawezaje kuishi maisha ya nama hii, ina maana mimi nakuwa kama mfungwa...’nikalalamika.‘Ni swala la muda tu...vumilia, hadi mume wako apone, na mengine yatakuja baadaye, usije ukafanya mambo, ambayo yatakuharibia, na hata ukienda kisheria ukaonekana wewe huna haki...’akasema huyo rafiki wa mume wangu na wakati huo docta alikuwa akitusikiliza tu baadae yeye akaondoka zake na kutuachia nafasi ya kuongea.Aliposema hivyo, nikaingiwa na shaka, kwani anavyoongea ni kama vile anafahamu kitu kwenye huo mkataba wetu, kuna kipengele, kuwa kama mmoja akiumwa, mambo mengine yote yasimame, hadi hadi huyo anayeumwa apone....na isitokee shinikizo la mmoja kuchukua nafasi hiyo kwa masilahi yake binafsi...‘Kwahiyo wewe unasemaje...unataka mimi nifanye nini?’ nikamuuliza, kwanza alitabasamu, kama kunidhihaki kuwa sasa naanza kumtegemea yeye, lakini hakufahamu mantiki ya swali langu.‘Kwa taarifa yako, tu, licha ya kuwa ni hatari, lakini docta kasema tukio hilo limesaidia kitu fulani, limashitua ile mishipa iliyokuwa haijashituka, na sasa hivi kila sehemu ya mwili imerejea kwenye hali yake ya kawaida, lakini kuna angalizo kubwa, tena hilo ni hatari zaidi, kuwa kama hali hiyo ikiendelea inaweza kuleta matatizo mengine makubwa zaidi...’akasema‘Kama yapi?’ nikauliza kwa hamaki‘Stroke....anaweza akapata na kiharusi,ni hiyo ikamfanya apooze kabisa...’akasema‘Mungu wangu....’nikasema‘Lakini yote yanategemea nyie wawili, kama kuna kitu unaona kinaweza kumkwanza mume wako, ni vyema ujaribu kukiwepa, jaribu kujizuia,....kwanini usiwe na subira…achana na mambo mengine yote..’akasema na mara docta akafika, na mimi nikawa na shauku ya kusikia mume wangu anaendeleaje. Na kabla hajaongea kitu rafiki wa mume wangu akasema;‘Docta mimi nilikuwa na wazo, je huyo mgonjwa hatuwezi kumpeleka mahali ambapo atakuwa hakutani na mkewe...maana naona wakiwa pamoja matatizo kama haya yataendelea kutokea na kama ulivyosema kuwa ni hatari kama akipatwa na stroke? Akauliza rafiki yangu.‘Hiyo ni mbaya zaidi, maana mume wake, hataki kuwa mbali na mkewe, niliwahi kumwambia hilo kabla, lakini alipinga kabisa,.., na kufanya kitu ambacho hakipendi kitamfanya ajisikie vibaya, cha muhimu ni mke wake, kukwepa yale yote yanayoweza kumfanya mume wake ashituke,au ahisi vibaya, ndio hivyo....’akasema docta.‘Unasikia, ....nilikuambia, uwe makini, mimi nakushangaa  una haraka gani, kuna kitu gani unakihitajia kwasasa, sasa uchague mwenyewe, mume au hayo unayoyataka wewe....’akaanza kunilaumu rafiki wa mume wangu‘Wewe hujui kinachoendelea ina maana nikae kimiya wakati naona kuna mambo yanaharibika, kuna vitu muhimu vinapotea, kwanini vipotee, kuna nani yupo nyuma ya hayo yote, unataka mimi nikae kimiya, hivi kweli mimi unaniona kuwa sina uchungu na mume wangu....’hapo nikawa nasema kwa ukali.‘Hujanielewa …’akasema docta‘Nimekuelewa sana,…nikuulize kama kuna vitu vinapotea, ambavyo vitakuja kuitahiri familia, akiwemo huyo mume wangu… , nikae kimiya tu..nisifuatilie, na hata huko kufuatilia, sijamuhusisha yeye, ila yeye anajiingiza kwenye mambo yasiyomuhusu kwasasa…ni lazima nifanye yote, nimhudumie mume wangu na wakati huo huo nilinde masilahi ya familia..’nikasema.Na mara kukatokea suti ndani ikumuita huyo docta, na docta akakimbilia ndani, na sisi tukabakia tukiwa na wasiwasi, lakini baadaye huyo docta akarudi na kusema;‘Mgonjwa anaendelea vizuri, lakini anamuhitaji mke wake..’akasema docta‘Itabidi nifuatane naye maana mimi nawajulia hawa watu…’akasema docta rafiki‘Hapana, mgonjwa kasema anataka kuongea yeye na mke wake tu...’ aliposema hivyo docta, mimi sikupoteza muda nikakimbilia huko ndani alipolazwa mume wangu…, na nilipofika ndani nilimuona mume wangu akiwa kalala huku kaweka mikono yote miwili kichwani kama vile hakuna mto, huku kaangalia juu.‘Oh, mume wangu umepona...’nikasema na yeye akajitahidi kucheka huku bado akiwa kaangalia juu, kama hataki kuniangalia machoni,na kwa sauti ya huzini, akasema;‘Yah, nimepona, lakini sasa naogopa kupona, ...’akasema‘Kwanini unasema hivyo mume wangu?’ nikaulizaNB: HAYA KWA LEO NIISHIA HAPAWAZO LA LEO: Dunia nzima, inaingia kwenye matatizo kwasababu kubwa ya mali na masilahi,. Watu wanakosana, kunakuwa na vita, migongano makazini, familia hazipatani, ukichunguza sana ni kwasababu ya mali na masilahi.Ubinadamu, utu, udugu, unasaba, ndoa vyote hivyo vinaharibika, na kuingia kwenye matatizo kwasababu ya mali, na masilahi. Tukumbuke kuwa vyote hivyo, mali na masilahi ni vitu vya kupita tu...vilikuwepo, na vitaendelea kuwepo, wewe kama binadamu mali na masilahi yako ni matendo yako mema.Matendo yako mema ndio mali na masilahi yako, itakayoweza kukusaidia hata baada ya kufa..‘Ahsante mungu…mume wangu ndio wewe, ooh,.., mume wangu sasa umepona, nashukuru sana…’nilisema hivyo, na mume wangu, hakuchelewa kunijibu akasema;‘Yah, nimepona, lakini sasa naogopa hata huko kupona, ...’akasema‘Kwanini unasema hivyo mume wangu. Usikufuru jamani…?’ nikauliza nikimuangalia kwa mashaka..Taratibu akajigeuza na kuniangalia…lakini kwa namna ya aibu …Tuendelee na kisa chetu…**************‘Nina maana yangu kubwa sana kusema hivyo mke wangu…’akasema, na mimi nikabakia kimia nikimuangalia tu, mume wangu alikuwa kadhoofu sana, uso umekunjamana, sio mwili wako, maana alishanenepeana sana.‘Mhh.., ni kweli, nimeponea tundu la sindano, ni wajibu wangu kumshukuru sana mungu…’akatulia kama anawaza jambo.‘Ni kweli nimeteseka sana, sio mchezo, hadi kufikia hapa ni kudra za mungu,…nilijua sitaweza kutembea tena, nilijua mimi ndio basi tena,..bado, kuna vitu havijawa sawa, siju…ila nimepona…’akatulia kidogo.‘Kiukweli najua nimekutesa sana mke wangu, nimewatesa sana watu wengi, nawashukuruni sana, na hasa wewe na docta rafiki yangu, siwataji madocta wanaoniuguza maana ninaweza kusema ni kazii yao..’akahema kwa kiraafu, halafu akasema;‘Lakini kwa madhaifu yetu sisi wanadamu..tunawazia ya mbeleni, maisha na tamaa zetu za kila siku, ..hapa nilipo, nawazia itakuwaje, ndio maana naishia kusema, najua nakufuru lakini nitasemaje sasa, ndio hivyo…, kupona kwangu ni kubaya zaidi, naona ni heri ningeendelee kuumwa tu...’akasema‘Mume wangu sasa unanichosha….’nikasema‘Najua …najua sana mke kuwa nakuchosha, lakini haya nitayasema kwa nani…nisamahe tu mke wangu.., nisamehe, nisamehe, nisa-mehe....hata hivyo najiuliza ni kwanini niufiche ukweli, wa kutoka moyoni mwangu, hata docta kasema nisipende kuficha ficha mambo moyoni mwangu, nikawa na duku duku, nikateseka ndani kwa ndani, sasa nimeamua nijitoe, niwe muwazi..’akatulia‘Haya fanya utakavyo, ila sipendi kuja kulaumiwa…’nikasema na yeye huku anaongea kama vile hanijali.‘Kwahiyo, ni bora niwe natoa dukuduku langu…ili mlisikie, kuliko nikae nalo moyoni, ni bora niwe na sema ukweli kwenu hata kama hamtaupenda, lakini uwe ni kwa manufaa yetu sote, sipendi kugabua,...., ndio maana naanza kuusema ukweli huu leo kwako, ila unielewe, kama kweli wewe ni mke wangu…, japo unaumia…’akasema‘Sitaki kukaa kimia alafu uje kusikia kwa wengine kunihusu mimi, au nije kusemwa na watu kuwa nipo hivyo siwezi kuendesha familia yangu, mimi…namtegemea mwanamke…nina machungu mengi moyoni, ..ni lazima niyaseme…nitayasema, nitachukiwa, lakini nitayasema…’akashika kichwa‘Mume wangu, najua akili yako bado haijawa sana, hujapona bado..na mimi ..sitaweza kufanya yale ninayojua yatakuumiza, nafahamu sana hilo,…ninachokuomba mume wangu usijiwekee vikwaza visivyo na msingi, usijitwike mzigo kabla haujatua kichwani mwako, tafadhali nakuomba…’nikasema‘Ahahahaha mke wangu huyo,..oh, oh, oh… unajua hivi sasa, kwa vile naumwa, kwa vile…eeh…utajifanya hunielewi, lakini kwa sirini, ndani ya moyo wako unafahamu nina maana gani, na ushajipanga kwa hilo, najua..haina haja ya usbishi kwa hilo…’akasema‘Haya niambie  ni kwanini kupona kwako kuwe kubaya.. maana sasa inabidi nifanye utakavyo wewe, ninaweza kukuuliza maswali ya kakuwaza, ukadondoka hapa, ni nani atalaumiwa kama sio mimi,..hata hivyo, wewe ni mume wangu lazima nikujali, ina maana hayo ninayofanya nafanya vibaya..?’ nikauliza na hapo hapo nikahis nimefanya kosa, nikageuka kuangalia kule mlangoni.‘Usiogope mke wangu, nipo sawa, sitadondoa, na nikidondoka si nipo hospitalini, una wasiwasi gani…mke wangu nimejipima kabla hujaingia humu ndani, mimi sasa…nipo sawa kabisa, nimejiandaa kwa lolote lile, leo najisikia nina nguvu,…na najua nkianza kusema ukweli utakasirika, utakuja juu, lakini kwanini nifiche eeh…’akajiinua kidogo, kama anataka kukaa, halafu akalala vile vile.‘Mume wangu, kwanini unakuwa mbishi, sisi tunahangaika kwasababu ya afya yako, afya yako ni muhimu kuliko hayo unayoyafikiria wewe…, au hutuonei hata sisi huruma, wewe hujui ni kiasi gani tunaumia tukikuona kwenye hiyo hali, wewe unajifikiria wewe mwenyewe tu..’nikasema.‘Ni kweli mke wangu, unasema kweli kabisa, wala hujakosea,...nashukuru sana kwa kunijali, na eeh, na…eeh,  siku nilipokuomba msamaha na ukasema umenisamehe, nilijua nimemaliza kazi, …kuwa sasa nipo salama, …lakini nikaja kukumbuka jambo,nilisahau kabisa…mmh, mungu mkubwa...’hapo akatulia kidogo.‘Ulikumbuka….! Ulikumbuka nini, mungu wangu sasa unanifanya nianze kukuuliza maswali, hata docta akija hapa atanikaripia mimi…’nikasema‘Usijali, wewe uliza tu…ni hivi, nashukuru ulisamehe au sio, sizani msamaha wako ulikuwa wa kugeresha, mimi nakufahamu sana…lakini kuna kitu tulisahaua, labda mimi, maana ndiye muathirika ….nlipokumbuka hilo, nikajua, msamaha wako hauna maana, hata ukitamka mara kumi,..hata ukisema umenisamahe…, ha-i-ta-sa-i-d-i-a kitu, huo ndio ukweli,…’akasema‘Kwahiyo unataka kusema nini, au wewe ulitakaje, ulitaka …nikatae kimia…au, maana unataka na mimi nianze kukueleleza, nifanya jambo, ili nionekana mimi mbaya, ili hayo uliyopanga yaonekane ni kweli kuwa mimi sikujali au sio…nakuomba tena, tafadhali, jail afya yako kwanza, umenisikia..’nikasema‘Siliza bwana…ni hivi, nimesema nin vile, eeeh, kuwa msamaha wako hautasaidia kitu, kwani kuna jambo zito ambalo haliwezi kutatuliwa kwa msamaha wako wa maneno, hata kama unatokea moyoni, na kwanini utokee moyoni wakati unajua ni nini unachokifanya, ulijua haya yanaweza kutokea, na hapa ndio namuona baba yako kuwa ni mtu mwerevu sana …ni wazee wanaoona mbali, wazee sio mchezo…’akasema‘Ok, haya niambie ni jambo gani hilo zito mume wangu, ambalo halijali msamaha wangu..?’ nikauliza‘M-ka-ta-ba …’akayatamka hayo maneno kwa uzito..na kuniangalia machoni, na mimi nilikuwa namuangalia lakini sio machoni,‘Naona hata hushtuki, hushtuki, kwa maana kuwa wewe unalifahamu hilo, …ndio maana ukaniaga kwenda kazini, hahaha mke wangu bwana,…lakini ni wajibu wako kufanya hivyo au sio, kufuatilia kuwa kila kitu kinakwenda sawa sawa....’akasema‘Mkataba gani huo, na wa nini mume wangu,…’nikasema‘Mkataba…mkataba ule uliobuni wewe mwenyewe, siongelei kitu kigeni hapa, na unafahamu fika nazungumzia kuhusu mkataba gani…wewe ulijua kama alivyojua baba yako, kuwa kwangu, …ni kunguru hafugiki, au sio, lakini sio kweli haya yangeliweza kutokea kwa yoyote yule....’akasema.‘Mume wangu sasa unanilazimisha nifanye unavyotaka wewe, nikuulize wewe una wasiwasi gani na hilo, unaogopa nini, kwenye huo mkataba, eeh, maana huo mkataba siku nyingi hautumiki…na mimi ndiye muhusika mkuu pamoja na wewe, kauli ykao na yangu inaweza ikabadili …na nikuulize umafanya kitu gani kibaya, eeh, umenilazimisha mwenyewe nikuulize hayo, sio ndio hivyo,…?’ sasa nikawa siogopi tena kumuuliza‘Sawa kabisa, nataka hivyo, uniiulize, na mimi nitakujibu, nipo tayari kwa hilo, sitaki uwe unazunguka zunguka, mara mdogo, mara kwa docta, niulize mimi mwenyewe…’akajiiunua na kukaa vyema.‘Una lako jambo, sio bure…’nikasema‘Mke wangu, kiukweli, nikuambie kutoka moyoni mwangu, mimi nina wasiwasi sana, wasiwasi ambao sijawahi kuupata awali, na nikiendelea hivi, nitawehuka, ndio maana sasa ni lazima niamue, la sivyo, …natumai utanielewa…’akasema‘Sasa hayo ni yako, na kama nia yako ni kunitesa mimi, itafikia sehemu nitashindwa, ngoja nimuite docta, ili asikie unachokitaka wewe, ili likitokea la kutokea nisije kulaumiwa mimi…’nikasema‘Utashindwa! Unasema nini, kuwa utashindwa, …hapana mke wangu,…usifikie huko, ni lazima tuwe pamoja, kama utanielewa, na docta nimeshaongea naye, kasema naweza kuendelea tu, usijali…’akatulia na mimi nikatulia, na yeye ndio akaanza kuongea;‘Unajua mke wangu, ni lazima ulijiuliza sana ni kwanini nikafikia mimi mume wako unaniyenifahamu, kuja kukuomba msamaha…kweli si kweli…usinijibu’akahema tena, nikawa namuangalia kwa mashaka, nilitamani docta aingie akatize haya mazungumzo, lakini moyoni pia nataka aongee auseme ukweli nijue moja tu.‘Nafahamu sana wewe mke wangu, umehangaika sana kuutafuta ukweli, ukazunguka huku na kule, ..lakini, hata ingelikuwa ni mimi, au sio…lakini nakupongeza sana mke wangu, kwa kitu kimoja, wewe huna haraka ya kumshuku mtu…’akasema‘Ndio maana baada ya kusubiria sana, baada ya matukio mengi, nahis na baada ya kuambiwa na watu wengi , kunihusu mimi, ..hapa naongelea yangu, eeh, wewe hukuchukulia pupa, unajua ni kwanini, kwasababu una kitu cha kukulinda, nacho si kingine, bali ni mkataba…’akasema .‘Lakini mke wangu…mengine, eeh, hayavumiliki au sio, hata ukikubali, hata ukinisamehe, hata hapa yapo au sio, lakini tulisahau jambo moja, kuwa kuna udhaifu wa kibinadamu, au sio, mimi yaliyotendeka sio kwa makusudi yangu…’akatulia, na mimi nikakaa kimia‘Unajua nafahamu baada ya leo, huenda ukanichukia sana, …lakini ni lazima nifanye hivyo, kwa vile mimi nakupenda, mimi naipenda familia yangu, nawapenda watoto wangu wote bila kubagua, sijali umasikini au utajiri…’akasema nakutilia mpaka nikaingilia kati na kusema;‘Unajua mume wangu mpaka sasa sijakuelewa, ni nini unachokitaka maana sikuelewi, ni nini shida yako, una tatizo gani, haya niambie hayo nijue mapema…’nikasema‘Najua kwanini unaniuliza hayo, najua lengo lako ni nini, wewe hutaki kuharibu, kuvunja mkataba au sio..mkataba unasema mtu akiumwa, mwenzake amuhudumia blab bla aa, eeh…..na mmoja akiumwa, mwingine eeh, asifanye kadha wa kadhaa, kama kuna tatizo, mpaka mwingine apone, kwa kufanya hivyo eeeh, utakuwa umevunja mkataba..au sio..sijui kama nimepatia…’akasema‘Mume wangu mimi sifanyi hayo kwa sababu ya mkataba, mimi ni mke wako natakiwa kuwajibika, kama ungeliwajibika wewe kwangu kam ningelikuwa naumwa kama unavyoumwa wewe..na uwepo mkataba au usiwepo, hiyo ni haki ya wanandoa…’nikasema`Ok,..ok,…labda nisipoteze muda, maana najua muda umefika, saa ngapi vile, mmh, naona kuna kuchelewa hapa, lakini itafanikiwatu..hili zoezi eeh, ni lazima lifanyike tu,..mke wangu, kabla sijasahau, naomba ile nakala ya mkataba....’akasema na mimi nikajikuta nikishikwa na kigugumizi nikasema;‘Mume wangu achana na mambo hayo  ya mkataba, huu sio muda wa mambo ya mkataba, hapa tupo hopsitalini,..nataka wewe upone kwanza, kama huo mkataba ndio unakuumiza na kufannya hayo yote basi, tuachane nao kabisa, kwangu mimi afya yako ni zaidi ya huo mkataba...’nikasema.‘Mke wangu naomba ule mkataba ile ni nakala yangu.....’akasisitiza‘Una uhakika kuwa hiyo ni nakala yako, sema ukweli mume wangu…’nikasema sasa kwa sauti ya kutokujali.‘Nimesema naomba ule mkataba…’akasema sasa akinikazia macho, nikaona isije ikawa taabu yakazuka mengine, nikafungua mkoba wangu na kumkabidhi huo mkataba, na yeye akaupokea na kuuweka kifuani, akageuka na kulala kama ilivyo kuwa awali, huku ule mkataba upo kifuani mwake.‘Kwahiyo unaendeleaje…’nikasema, nilisogea na kukaa karibu naye na akashtuka nahsi alijua nataka kuuchukua huo mkataba, akaushika na kuuweka pembeni upende wa pili ambao siwezi kuuchukua kwa kirahisi, na , akawa kimia akiwa kaangalia juu, kama vile hataki kuniangalia tena machoni, sikumuelewa, na mimi sikuwa na haraka naye, hapo nilitaka nifanya atakavyo halafu nitoke humu hospitalini.Hali ya ukimia ilitanda kwa muda, kimia kingi kina mshindo moyoni, lakini sikutaka kumghasi, labda alikuwa akiwaza jambo, na ..baadae akauvunja ukimia, kawa kusema;‘Mke wangu unisamehe sana kwa hayo yaliyopita na huenda na-yajayo, nafahamu na kukwaza sana, wewe moyoni utahisi sikujali,...lakini mengine nayafanya kwa nia njema tu...wewe hujui tu, …lakini siwezi kukufanya wewe unielewe kwa haraka hivyo, najua hilo…’akasema na mimi nikaa kimia‘Mke wangu kwa vyovyote itakavyokuwa ujue nakupenda sana, kama itafikia sehemu ya kulazimishana jambo, tukawa hatuelewani, na huenda haya yakifika kwa baba yanaweza kuleta maana nyingine na huenda ikafikia, …mimi na wewe kulazimishwa tuachane..najua hilo,, hasa kutokana na huu mikataba,  lakini sitakubali kwa hilo…’akasema.‘Mume wangu kiukweli sikuelewi, hivi unataka nini, niambie ukweli wako, ni kitu gani unakitaka kutoka kwangu ..ni mali au….niambie ukweli…ili usipate taabu sana, niambie hapa hapa, mimi nitakupatia hicho unachokitaka, ili tu uwe na amani, ni nini inachohangaika nacho, niambie?’ nikauliza sasa sijali, na yeye akabakia kimia tu.‘Utaelewa tu….’akasema hivyo‘Kiukweli mimi nimechoka…’nikasema.‘Mke wangu mimi sio mtoto mdogo, ...nilijua tu, siku nilipokubali haya maswala ya mkataba ndipo nilipokubali kuwa mtumwa, na mfungwa wa maisha yangu mwenyewe, mkataba huu ulilenga wengine, lakini hauku lenga usawa, utakuja kulifahamu hilo baadae..’akasema‘Mkataba , mkataba mkataba..mume wangu ni hicho, lete niuchane mbele yako, si ndio unakufanya uwe hivyo, mkataba unaweza kubatilishwa, lakini maisha yetu je, watoto wetu je,..hivi unafikiri dunia hii ni yetu tu mume wangu, ..’nikasema‘Hapo hapo…eeh, natumai sasa tunaanza kuelewana….’akasema sasa akikaa vizuri‘Kama ulifahamu hilo, ni kwanini ukaleta haya maswala ya mkataba, mimi nilikubali tu, kwa vile nakupenda, na nilijua haya yatakuwa kwa masilahi yetu yote, sikujuwa kuwa kuna kuteleza...sawa yametokea yaliyotokea, eeh, si hivyo,...sasa nifanye nini....nikae kimiya, na hata wasiohusika wapate taabu kwa makosa yangu.....hapana..’akatulia kidogo‘Mke wangu, nilifikia sehemu nikaona bora nife tu, mitihani ilikuwa mingi kichwani mwangu..lakini nikakumbuka kuwa mimi ni mume wa familia, nina watoto, ..nina dhima mbele ya mungu, hapo nika…eeh, nikamuomba mungu anisaidie nipone ili nibebe majukumu yangu mwenyewe...’akasema.Ikapita muda, nikaona kama anahangaika, nikaangalia mlangoni, nikitaka docta atokee, na baadae nikasema;‘Unajua mume wangu nimeliwazia hili sana, nakuona haupo vizuri, akili yako haijatulia, bado unaumwa, kwa ajili ya afya yako,. Itabidi ukalazwe sehemu ukae mpaka upone, maana kukutana mimi na wewe inakuwa ni taabu, unakuwa huna amani, sijui kwanini na....unanipa shida sana ya kukuhudumia....’nikasema.‘Hilo halitawezekana kabisa…, nitakaa na wewe hadi hatua ya mwisho, kwanza nimeshapona, unaona ...’akasema na kujiinua , akateremka kitandani,…akasimama na kuruka ruka, kiukweli hata mimi sikuamini hilo, mtu alikuwa hawezi kujiinua leo hii yupo hivyo, kweli mungu mkubwa….hapo nikasema;‘Nashukuru sana kukuona umepona, lakini bado,...docta kasema hatua uliyofikia ni hatari zaidi kama hutafuata masharti, ukipata mshtuko kidogo tu, uka…inaweza ikawa mbaya zaidi....’nikasema‘Masharti gani, masharti ya kutesana, hahaha eti masharti, …sawa. ni sawa , lakini wanajua kilichopo moyoni mwangu, kilichopo moyoni mwangu kama kisipowekwa sawa, haitasaidia kitu, na hiyo, ya mshtuko, ni kutokana na hilo…sasa kwa vile nimeweza kuuinua huu mwili, basi, ni lazima nipambane…’akasema‘Na  nani..upambane na nani mume wangu?’ nikamuuliza hapo akanitizama, na mimi nikamtizama, tukatizamana, yeye akawa wa kwanza kuangalia pembeni.‘Ni hivi mke wangu, mimi si ndio mume wako au sio, kichwa cha familia, haijalishi hali , haijalishi kuwa wewe ndiye mwenye uwezo wa kifedha, hiyo ni kweli au sio..hata kama baba mkwe ndiye anatufadhili hiyo haina maana kwenye ndoa yetu au sio…lakini vyovyote iwavyo, mimi ni lazima niwajibike kama mume, siwezi kujipweteka, unaona eeh,..dunia itanicheka…’akatuliaNa mimi nikabakia kimia tu…‘Sasa ni hivi, namshukuru mungu kuwa nimepona, ...siwezi kuendelea kukutesa tena mke wangu, ....ninachotaka ni ijulikane moja,...nataka nikitoka hapa tukae, tujue moja, nafahamu wewe utasimamia kwenye mkataba…sijui…lakini hata ikiwa hivyo, sio mbaya, mimi nipo tayari kwa lolote lile, japokuwa nafahamu ni nini kitatokea,ila kuna masilahi ya watu wengine ni lazima niyapiganie kwa nguvu zangu zote..’akasema.‘Hao watu wengine unaowataja sana , ni akina nani,na kiukweli mimi sio mtoto mdogo…hata hivyo mume wangu waonaje haya tuje kuyaongelea nyumbani, au,,,>; nikauliza, nikijaribu kujishusha japokuwa moyoni haikuw ahivyo.‘Kupona kwangu mimi ni pamoja na kufahamu hatima yangu,...nilipokumbuka kuhusu huu mkataba, nikajau kuwa kupona kwangu ni hatua tu, nina kazi kubwa mbele yangu‘Nikuambie ukweli mke wangu nimekuja kugundua kuwa kumbe huo mkataba ulikuwa ni mtego kwangu, ...sasa siwezi kulala hapa, kwa vile naumwa,….aah, nimejipima, ..nikatembea…nikaruka, nikaona sasa nipo safi, bado kuna udhaifu fulani, lakini sio hoja, sasa ni lazima nipiganie haki zangu, na za hao wengine....’akasema na mimi nikabaki kushangaa.‘Kama uonavyo ni sawa, haya, maana mimi sijui unataka kupigana na nani, na hizi haki za nani, kutoka kwa nani,…mimi sikuelewi kabisa, lakini upendavyo, siwezi kusema zaidi....’nikasema.‘Sawa kabisa hapo umenielewa na kunisikia....kwa vile huu mkataba ulikuwa mtego kwangu, utakuwa wa kwanza kuufanyia kazi…’akasema‘Sawa uonavyo,…’nikasema‘Kifupi mke wangu ni hivi, kwa vile mimi ni mume wako, natakiwa kuanzia sasa nianze kusimamia mambo yetu kama kichwa cha familia, kwahiyo kama kulikuwa  na jambo jingine ambalo linanifanya niwe mume bwege, kuanzia sasa nitaliondoa kwa mikono yangu mwenyewe…’akasema‘Unasema nini, mume bwege, hiyo kauli imetoka wapi…?’ nikauliza kwa mshangao‘Usijali, utakuja kunielewa ni na maana gani, kwanza tutaanza na huu mikataba , tuangalia vipengele vyote vya mitego mitego…ikibidi tuuharibu tuanzishe mwingine kwa masilahi ya familia yetu sote, sio kwa masilahi ya familia yangu ndani ya familia nyingine..’akasema‘Mhh..’nikaguna tu‘Utakuja kunielewa tu, akija muhusika …’akasema‘Muhusika gani. Ni nani anakuja huku hospiali…?’ nikauliza kwa mshangao‘Ndio… atakuja muhusika  na tutaweza kuyaongea yote vizuri tu, mambo yote, ya familia, yaliyotokea na hatima yake, lakini muhimu ni mambo yetu, sitaki tena kuishi kwa mashaka, nimeamua, na wewe utanisaidia ukishirikiana na huyo naye....’akasema.‘Mume wangu, ni nani huyo..?’ nikauliza‘Unajua mke wangu huu mmkataba una madhaifu mengi, ndio tutakaa pamoja watu watatu, baada ya kuhakikisha ule mkataba wa awali umefutwa, tuandika kitu kincahogusa watu wote, sisi , watoto na mali zetu,, uwe mkataba unajali familia yetu, na mambo yetu , na sio kwa kuegemea familia nyingine..’akasema‘Kuegemea familia gani…?’ nikauliza‘Hivi nikuulize mke wangu, mimi si ndio nimekuoa, kama mimi ndiye nimekuoa kwanini tuendelee kutegemea familia ya kwako,…hapo natoa mfano tu…’akasema‘Tunategemea ndio kwasababu ndio wafadhili wetu, kama isingelikuwa hivyo, hiyo kampuni ungeliweza kuianzisha, haya maisha tunayoishi sasa yangelikuwa hivyo, hebu jiulize hilo wewe mwenyewe hilo hatuwezi kulikwepa bwana unajidanganya tu, madeni kibao, ndio unataka hivyo…’nikasema‘Ni sawa, lakini kuanzia sasa tuanweza kuishi wenyewe au sio, kama kuna mapungufu, eeh hayo madeni nk… tutayakabili wenyewe, ndivyo nimejipanga hivyo, tutapambana wenyewe kufa na kupona, bila kutegemea familia nyingine…’akasema‘Hbu kwanza nikuulize maana umeyataka mwenyewe,  kuna muda ulisema hata ukiwa na mtoto nje, ulikuwa na maana gani,  ya kuwa unaye mtoto nje au, niambie ukweli…?’ nikauliza,sikutaka kuongea naye kihasira, nikiwa na maana yangu tu. ‘Hayo sasa tutakuja kuyaongea mbele  akija muhusika, huyo atayaweka kila kitu sawa….nataka kila kitu sasa kiwe kwa namna ambayo, hakuna mtu ataumia,..sio mimi wala wewe au yoyote ..nataka nitende haki, kama mume wa familia na tutakuja kuyaongea tukiwa watatu tu…’akasema‘Hujanijibu swali langu, nataka kufahamu maana haya umeyataka wewe mwenyewe, je kweli una mtoto nje…na ni nani huyo…?’ nikauliza na kabla hajanijibu,‘Mtoto sio, ngoja nikuambie….’akatulia maana mlango uligongwa na kufunguliwa Mimi pale akili yangu ilishaanza kubadilika, mume hajaweza kunijibu, inaonekana kuna kitu kama hicho, inawezekana mume wangu ana mtoto nje ya ndoa, je ni nani, je ni kweli wanayozungumza watu, kama ni kweli, itakuwaje…nikawa nawaza mambo mengi kwa muda mfupi, lakini mawazo yangu hayo yalikatizwa na hao walioingia pale mlangoniKwanza aliingia docta anayemuuguza mume wangu, akafuatia nesi wake, halafu docta rafiki wa mume wagu…usioni hakuonekana na furaha, nikahisi kuna jambo, .., lakini zaidi ya hao, kuna mmoja ambaye alinifanya moyo wake udunde, nijawe na hasira, ni kama vile kuwepo kwake huyu ndio kumetibua ile hasira niliyokuwa nayo, nikajikuta nikhema kwa shida, na uso ukabadilika kwa ghadhabu.....NB: Naishia hapa kwa leo, nikiwatakia maulidi mema....WAZO LA LEO: Tabia njema ndicho kiigizo chema katika jamii, tujipambe kwa tabia njema hata wale wanaokuiga wakuongezee fadhila zako katika maisha yako hapa duniani na kesho ahera.  ‘Hayo sasa tutakuja kuyaongea  akifika muhusika, ambaye ataweka kila kitu sawa….unajua mke wangu nataka kila kitu sasa kiwe kwa namna ambayo, hakuna mtu ataumia,..nafanya haya kama mume wa familia….‘….Je ni kweli una mtoto nje…na ni nani huyo…?’ ,  Wakati anataka kujibu swali hilo mara…wakaingia madocta na nyuma yao, akaingia mtu, mtu ambaye alinifanya nipandwe na hasira, ..Ni nani huyu…Tuendelee na kisa chetu…**************Ungeliniona nilivyokuwa nimeshikwa na butwaa ndio ungelifahamu haya ninayokuambia hivi sasa…, maana akili yangu ilishahamanika, niliposikia mume wangu kama vile anataka kukubali au kukataa kuwa ana mtoto nje ya ndoa, na huo ndio ungelikuwa ni shahidi wangu mkubwa, ama kwa heri au kwa shari..Kiukweli hadi muda huo nilishaamua moja, kama ni kweli hayo wanayoyazungumza watu basi mkataba ungelifanya kazi yake,..ama kama ni uwongo, kuna mambo mengi yangelinifanya nianza kukosana na marafiki zangu kuwa wao wanataka kuivunja ndoa yangui…ila nilichohitajia kwangu kikubwa ni ‘ushahidi..’Kauli ya mume wangu ingelikuwa ni ushahidi tosha, wa kumaliza matatizo haya yote kichwani mwangu,angekuwa mkweli, huenda ningeliumia, lakini mwisho yangelifikia muafaka, lakini kwanini hataki kuniambia ukweli, hapa nabakia na swali kubwa kichwani,  je ni kweli mume wangu kafanya hivyo, ina maana alisahau huo mkataba, na sikuwezi kupata jibu hilo, maana mbele yangu kulitokea tatizo jingine…Mawazo yangu yalikatishwa na huyo jamaa, aliyeingia, kumuona yeye tu, nilijua kuna tatizo, na tatizo hilo sio dogo,…hapo akili ilishtuka, na kuharibu mawazo yote niliyokuwa nayo kichwani…!Cha ajabu hata baada ya wale wengine kuingia ndani, wao waliingia na moja kwa moja wakaja pale tulipo kwa mgonjwa, ambapo mimi nilikuwa nimesimama karibu naye, lakini huyo jamaa yeye baada ya kuingia alipiga hatua moja , mbili, halafu akasimama karibu na mlango, na mbali kabisa kutoka pale tulipokuwepo sisi, hakusogea ..Nilibakia nimeduwaa, nikimkodolea macho huyo jamaa, kiukweli sikutatarajia kumuona huyu mtu tena katika maisha yangu…baada ya tukio lililotokea huko nyuma baina yangu mimi na yeye,..na nakumbuka kwa mara ya mwisho nilipokutana naye, hatukuachana vizuri kabisa, nikakumbuka kauli yangu kwake;‘Sitaki kuja kuonana na wewe tena, …sikutaki kabisa na ukumbuke hili, siku nikija kukutana na wewe tena, nitahakikisha nakufungulia mashitaka ya utapeli, na uwongo, na nitahakikisha, unakwenda ndani, na ukitoka jela, hutajishughulisha tena na utapeli wako huo….’nikamuambia hivyo kwa hasira.‘Na pia nakutahadharisha,..mimi nitakuwa nakufuatilia, hatua kwa hatua,…mimi nakuonya uwe mbali kabisa na mume wangu..unanisikia wewe tapeli…’nilizidi kumpa onyo na kwa muda huo hakuwa na cha kusema, bali ni kukaa kimia tu.‘Kama nikikuona upo karibu na mume wangu, nitahakikisha ninakumaliza kwa mikono yangu mimi mwenyewe…na nitaanika mabaya yako yote hadharani….’nilimwambia…kiukweli nilikuwa nimeshamfahamu alivyo na jinsi anavyofanya kazi zake, na ushahidi wote nilikuwa nao…‘Samahani sana..ni makosa yalitokea, sitarudia tena….’alijitetea hivyo‘Sina haja ya samahani yako, ondoka mbele yangu…’nilimuambia hivyo tukiwa ofisini kwangu na alitoka haraka na sikuweza kuonana naye tena, mpaka siku hii ya leo.Jamaa aliendelea kusimama pale, hakusogea hata hatua moja kuingia ndani, sasa sikufahamu ni sababu ya kuniogopa, au alikuja kwa malengo yake binafsi.Kama kawaida yake, alikuwa kavalia mawani meusi machoni, akificha unafiki wake, mkononi akiwa kashikilia mkoba wake mweusi, mkoba ambao umekuwa kama sehemu ya mkono wake, maana popote utakapokutana naye, huo mkoba upo mkononi, sijui ndani yake kuna nini!Kwa muda ule mimi nilikuwa nimeshikwa na butwaa, mwili ukinicheza cheza kwa hasira, mdomoni nikitaka kutamka jambo au kupiga ukelele wa hasira…, lakini sikuweza kufanya hivyo , nikiheshimu mamlaka ya hapo, kuwa hapo ni hospitalini.Lakini pia sikuweza kufanya jambo, nikichelea matatizo ya mume wangu…kiukweli isingelikuwa hayo mambo mawili, ungelisikia mengine, nahisi ningelipiga ukele, au kwenda kumvaa huyo jamaa kwa hasira,  lakini kwa muda huo na sehemu kaam hiyo, ilibidi ninywee tu, na kuumia na hasira zangu moyoniBaadaye  nikageuka kumwangalia mume wangu nisikie anasema nini,...kwani kwa muda huo alishamalizana kusalimiana na walioingia humo ndani kasoro huyo jamaa.Mume wangu aliponitupia jicho, akaiona hiyo hali usoni mwangu, nilishabadilika, hasira zote zilikuwa usoni mwangu, alitarajia kuwa ningelifanya jambo, la kumvaa huyo jamaa au kuongea kwa hasira, lakini hilo halikutokea, alishangaa kuniona nimesimama tu, siongei neno, ila uso wangu ulionyesha kila kitu…Mume wangu akasema;‘Mke wangu samahani sana, nafahamu hupendi kabisa kumuona huyo mtu..na nafahamu ni kutokana na yale yaliyotokea kipindi kile..na hayo yaliharibu sifa zake..lakini hukutaka kuyafuatilia zaidi kuwa yeye hakuwa na kosa, kama ni kosa basi labda ungelinilaumu mimi, unanielewa hapo, lakini hukutaka hata kunisikiliza…’akasema kumtetea huyo jamaa.‘Mimi namfahamu sana rafiki yangu huyu,…ndio kuna wakati mwingine anafanya mambo-mambo, lakini sio kwa kupenda yeye, wakati mwingine ni kutokana na mteja wake anavyotaka yeye…anajulia namna za kuweza kumsaidia mteja wake,…’akatulia‘kwa hali kama hiyo, yeye yupo tayari kuingia kwenye hatari, ili kukidhi matakwa ya mteja wake…na wakati mwingine anahatarisha taaluma yake, lengi ni kusaidiana, anatufahamu maisha yetu sisi watu wa kawaida, na anafahamu maisha ya watu wliopo kwenye dhiki..au kukwama kwa namna hii au ile, maana sisi wanadamu tuna madhaifu yetu…’akaendelea kuongea lakini mimi hayakuniingia akilini.‘Kwa namna hiyo na nyingine wale maadui zake, na wasipomtakia mema, wamefikia kumharibia jina lake…, lakini afanyeje kama mteja wake anataka hivyo, na kama mtu kaja kumlilia hali, mtu kama huyu anatusaidia sana sisi watu tuliokwama, ni vyema tukamfahamu hivyo, japokuwa upande wa pili watamsakama sana…’akatulia‘Sisemi haya kuwa wewe ulitaka kufanya mabaya, kwa kupitia kwake, hapana, ila kwa taarifa alizozipata,…’akataka kuendelea mimi nikaonyesha mkono wa kukataa hayo maelezo yake nikasema‘Please,..bsi basi inatosha,…mimi sitaki tena kusikia  hayo maelezo ya huyo mtu, mimi namfahamu vilivyo,..hakuna mtu anayeweza kunidanganya lolote, sijafanya makosa …namafahamu..kwahiyo sijui kaja hapa kufanya nini..’nikasema‘Mke wangu ..najua wewe hurudi nyuma, unamuamini sana rafiki yako, au sio…lakini nikuambie kitu,….lakini hayo tuyaache kwanza, maana hayo yalishapita au sio..’akasema na kutulia kidogo‘Hata hivyo kutokana na hayo yaliyotokea…eeh, yanaweza kuwa ni sababu, kwani huko yanapoendea, kunaweza kukazuka sintofahamu eeh..nashindwa kuelezea kiuwazi zaidi..kisheria, si unajua membo mengine yapo kwenye mkataba, yanahitajia sheria, na..na..ndio maana, nimeona huyu mtu aje kunisaidia, …, yeye, ni rafiki yangu wa siku nyingi, namuamini sana kuwa atanisaidia kwa hilo…’akatulia‘Kukusaidia, kwani una kosa gani mume wangu…..?’ nikamuuliza sasa kwa hasira , na hapo mume wangu akaonekana kunywea, lakini kwa haraka akajirekebisha kuonyesha nafasi yake akasema;‘Ndio hivyo, makosa yap ndio maana nikakuomba msamaha,..au sio, lakini haya yatasemwa baadae kwa muda muafaka, ngoja nimalizane na huyo mtu…yeye nimemuita ili aweze kulisaidia hili…’akamuangalia jamaa‘Huyu jamaa namuaminia…, yeye anajulia sana mambo ya mikataba hasa ya kifamilia kama hii ya kwetu ya kienyeji enyeji, iliyotengenezwa kimtego mtego…na pia ya kikazi, na anaweza kufahamu madhaifu ya mikataba hiyo na lipi lifanyike ili kuirekebisha, bila kuleta matatizo makubwa, anajua njia zote kwa jins tunavyotaka sisi umenielewa hapo…’akasema‘Kwanini unataka kufanya hivyo..?’ nikamuuliza‘Kama nlivyoanza kukuambia awali, mke wangu..nielewe..sitaki tuongee sana kabla sijaweka haya mambo vizuri, lakini ni hivi.., huo mkataba wa kimtego,…una mapungufu mengi, na ..ukifika kwa baba yako, kashapata panga la kukata mti..na huo mti ni nani, sio mimi kweli..ndio hivyo, sasa nikimalizana na huyu jamaa, nitakuja kuakuambia kila kitu,... ila kwa hali ilivyo inabidi kujihami, sipendi kazi zetu zote zionekane hazina maana, …na mume nipo, ni aibu jamani...ni lazima sasa nishike hatamu…’akasema akitikisa kichwa kama kukubali.‘Mume wangu unajua unajizalilisha wewe mwenyewe, mambo ya ndani unamtafuta wakili wa kazi gani, umeua..umafanya kosa gani kubwa kihivyo…’nikasema‘Hapana, ..sijaua..lakini aheri uneliua, ikajulikana moja,…nafahamu kabisa mbele ya baba yako, naweza kuonekana kama muuaji tu….nitazalilika, …na, nitakimbilia kujiua…si umeona hapo…ila mke wangu haya ni mambo ya kawaida tu,..utakuja kunielewa, wala usipate shida, niachie mimi, nitayaweka sawa, mwenyewe utakuja kuona…’akasema‘Sitakuelewa kamwe,…na kwanini unafanya hivyo, kwa hali uliyo nayo, kwanini hujionei huruma, na kama wewe hujijali, kwanini usiwajali wanaokuhangaikia, eeh, hili …mume wangu…hapana, hapa kiukweli umevuka mipaka…’akasema‘Mke wangu, niamini, …si unaniamini,..sasa endelea kufanya hivyo, utaona manufaa yake, mengine nitakuja kukuambia nyumbani,..huyu mtu sivyo kama unavyomfikiria wewe, na kutokana na hali zetu kuwa sio nzuri kibiashara, yeye kajitolea kwa gharama ndogo tu, na haya tutayayamaliza haya mambo kwa haraka iwezekanavyo...’akasema mume wangu.‘Mimi, sikuelewi na sitakuelewa, na sipo kabisa na mambo yako, samahani kama nitakukwaza, ila kwa huyu mtu, sipo tayari kushirikiana naye kwa lolote lile,…’nikasema huku nikimuangalia docta rafiki ambaye kwa muda huo naye alikuwa kama kachanganyikiwa. Wakati huo docta yule aliyekuwa akimshughulia mgonjwa alishaondoka, na alisema atarudi baadae kutuambia cha kufanya kama nikuondoka na mgonjwa, au bado anahitajika kuendelea na matatibabu.‘Mke wangu…usiwe na wasiwasi kabisa…haya nitayamaliza tu, ngoja docta aje kama ni kuniruhusu haya, kama ni kuendelea kubakia hapa , sawa , lakini kabla ya mimi kuondoka hapa, ni lazima mambo fulani yafanyike ili huyu mtu aondoke ..na kuanza kazi yake…’akasemaMimi pale nikakaa kimia,…baadae nikageuka kumwangalia docta. Docta rafiki, alikuwa bado kakaa kimia, na sasa akimuangalia rafiki yake kwa makini…, na baadae akaniangalia mimi,..na muda huo ndio na mimi nageuka kumuangalia yeye nikitaka asaidie kwa hili. Macho yakakutana…*************** Docta rafiki alipoingoa mara ya kwanza, alichofanya yeye, baada ya kusalimiana na rafiki yake, alijitenga pembeni, ..lakini pembeni mwa kitanda kama kutupatia nafasi, na muda mwingi alikuwa katulia huku kainama chini, kama vile hataki kuingilia mambo yetu, lakini akiwa tayari kutoa msaada ..na kila alipoona napandisha hasira, alikuwa akinitupia jicho,  la kunipa tahadhari…lakini kwa muda huo mimi sikujali tena,.., nikamgeukia mume wangu.‘Mume wangu huko unapokwenda ni kubaya, nakuomba tena tuyaache haya mambo mpaka upone, tafadhali, usije ukafanya mimi nikaja kuonekana mbaya…’nikasema‘Wala usijali mke wangu hakuna baya litatokea,…uwe huru tu..lakini hili lazima lifanyike…’akasema‘Hili lipi….weka wazi….na sijui kwanini mume wangu unayafanya haya yote..ina maana una kosa gani kubwa mpaka unadhamiria kuyafanya haya yote, wakili, wakili wa nini…sijakuelewa bado…?’ nikamuuliza‘Wakili ndio…ila kwa sasa usiwe na papara, utakuja kujua kila kitu…nimeshakuambia dhamira yangu kuwa ni lazima apatikane mtu wa kuyaweka haya mambo sawa, ya ndoa, mali na kadhalika, kuna mkataba au sio, je upo sawa..sasa nilazima nimpate mtu sahihi wa kunishauri…na nimeonelea mtu wa ngu sahihi huyo jamaa…’akasemaNilitaka kugeuka kumuangalia huyo jamaa, lakini hata kichwa kikasita kufanya hivyo…nikasema;‘Mume wangu kwani wewe una wasiwasi gani, mimi nipo kwa ajili yako, na kama unahisi kuna tatizo, mimi nitasaidiana na wewe kulimaliza hili au sio,....mimi sioni umuhimu wa kumleta mtu mwingine kwenye mambo yetu ya nyumbani, tulishasema haya ni yetu wawili, sasa huyu mtu ni wa nini…, jaribu kujionea huruma wewe mwenyewe kwanza, ....!’nikasema.‘Mke wangu usione nayafanya haya kwa kuwa labda nimependa, …hapana nimejikuta sina jinsi, na nikiyaachia, nitakuja kudhalilila…hapana, hapa ilipofikia ni lazima na mimi nifanye jambo…’akasema‘Ufanye jambo gani,…weka wazi,…na kama kweli kuna tatizio kubwa kihivyo, na mpaka haya yote yanatokea, utuambie ili na sisi tuweze kusaidia,..uliua, hapana, ulifanya nini basi…haya kama ni hivyo, kwanini haya yafanyike hapa hsopitalini,… basi subiria tutoke hapa, tukifika nyumbani tutakuja kuayaongea haya vizuri…’nikasema nikijaribu kujishusha‘Hapana mke wangu tulishaongea yote na huyu mtu, sasa hivi kaja ili kumalizia hili jambo kwa ujumla wake, …ukitaka unaweza kubakia, kusikiliza kila tutakachoongea, lakini kama hutapendelea, basi, nitakuja kukuambia tulichokubaliana,..lakini vyema na wewe ungelikuwepo,  maana mim nimekuwa mtu wa kuumwa, umwa,..sasa lini litafanyika hili,naona sku zinakwenda, na baba yako anazidi kuwa juu..hulioni hilo, ..ngoja tulimalize hili kabisa leo hii hii,..’akasema‘Mimi sikubaliani na hilo kabisa, unasikia, wewe kwa vile umeamua kwa masilahi yako, wewe endelea na huyo mu wako, na mimi usinihusishe kwenye makubaliano mtakayofanya na huyo…na nasema hivi kama una nia njema na hayo unayotaka kuyafanya, basi subiria tufike nyumbani kwanza...’nikasema.‘Mke wangu kwa hatua ilipofikia hatuna jinsi, inabidi tukubaliane na huyu mtu, vinginevyo, mambo yataharibika, nielewe hivyo, na niamini hivyo,mwenyewe utakuja kuona....’akasema‘Tukubaliane na yeye, una maana gani hapo na ni mambo gani hayo yataharibika…?’ nikamuuliza‘Ndio nasema utakuja kujua lakini kwa hivi sasa siwezi kukuambia lolote uniamini tu..’akasema‘Nakuuliza hivi, kwani huyu mtu ndiye anakulazimisha kufanya hivyo, au ni kwa utashi wako wewe mwenyewe, niambie kama kuna kitu nyuma ya pazia, nifanye kazi yangu, huyu mtu mimi hanibabaishi kwa lolote lile, ninamfahamu sana ni mbabaishaji tu, ni tapeli huyo, utakuja kujutia, umeshachelewa…’nikasema  ‘Mke wangu mimi nakupenda sana, na sitaweza kuachana na wewe, hilo nimeahidi , sio bab yako wala kitu gani kitavunja ndoa yetu,.. nafahamu hata wewe unanipenda pia, au sio…?’ akasema kama kuniuliza, sikumjibi kitu‘Sasa. kwa ajili ya ndoa yetu, kwa ajili ya maisha yetu na familia yetu, na watoto wetu,...mimi siwezi kukubali mambo mengine yaje kutuingilia,...nafahamu kabisa nikikaa kimiya hilo litatokea, na....sijui itakuwaje kama likitokea...ni nani wa kualaumiwa kama sio mimi,...hapana mimi siwezi kukaa kimia,  ni bora nijitetee mapema,...’akasema na akawa anakunja uso kama anahisi maumivu fulani.Nikageuka kumuangalia docta, na docta akawa naye anamuangalia mume wangu kwa mashaka...akageuka kuangalia kule wanapokaa madocta, kulikuwa hakuna mtu, halafu akaniangalia mimi...‘Mke wangu wewe niamini mimi..na sifanyi hili eti kwa shinikizo la mtu, kuwa eti labda huyo jamaa kafanya jambo kunirubuni, hapana hakuna kitu kama hicho, huyo ni rafiki yangu hawezi hata siku moja kunifanyia hivyo, haya yote nayafanya kwa masilahi ya familia, kwa utashi wangu  mimi mwenyewe…’akasema mume wangu.‘Sizani kama nitakuelewa, na aah, hata sina hamu tena ya kuendelea kukaa hapa, mimi nataka kuondoka, kama ..oh, docta alisema tumsubirie, ok, au..?’ nikasema nikiwa nataka kuondoka, nikamuangalia docta rafiki, naye akawa ananiangalia kwa uso wa kunionya kuwa niwe makini.‘Mke wangu usiondoke kwanza tafadhali…, maana sizani kama nitaendelea kulazwa hapa, kiukweli hata mimi mwenyewe nataka kuondoka hapa...,ikibidi leo hii….docta kaniambia hali yangu imeshatengamaa, sasa nikae hapa kufanya nini..mambp yangu yanalala,..na ndio maana nimemuita huyu mtu, aanze kunisaidia yale mambo yanayoweza kuleta madhara kwenye familia...’akasema. Alipoongea hivyo, nikageuka kumwangalia docta rafiki. Nilimona kainama vile vile, nikamsogelea pale aliposimama, na yeye akainua kichwa taratibu na kuniangalia machoni, huku akiwa nusu kutabasamu na nusu kuonyesha mashaka fulani, lakini bado nilikuwa sijamuelewa, kuwa yupo na mume wangu au yupo na mimi,mimi nikamwambia kwa sauti ya chini chini ili mume wangu asisikie;‘Hivi huyo mtu mumemchukulia wapi,…?’ nikamuulizaDocta rafiki akamtupia jicho yule jamaa , huku mimi naendelea kuongea‘Hivi si nyie mlionionya kuwa hali ya mume wangu haihitajii mambo ya kugandamizwa kimawazo, sasa hamuoni kuwa kwa hali kama hii tunaweza kumuathiri mgonjwa, au kuna jambo jingine mumelipanga mimi silifahamu...?’ nikamuulizaDocta rafiki,..akatulia kama anawaza jambo, halafu, akageuka kumuangalia mume wangu,…mume wangu alikuwa kainamisha kichwa chini, hatuangalii, ni kama ananiacha niongee na docta, na hakuwa na wasiwasi na hiloDocta rafiki, akageuka kumwangalia yule jamaa tena pale aliposimama karibu na mlango, alikuwa kasimama pale pale, hajasogea hata hatua moja, na vile vile alivyokuwa kasimama awali ni hivyo hivyo.. docta akawa anauangalia kwa makini, tatizo yule jamaa alikuwa kavalia mawani meusi, kwahiyo huwezi kufahamu ana hisia gani machoni…Baadae docta akanigeukia na kunitizama machoni, na kwa sauti ndogo akasema;‘Mimi sijui kabisa ni kitu gani kinachoendelea hata mimi nimebakia kuduwaa, mpaka sasa nawaza kuna kitu gani kinachoendelea...sijui kuna tatizo gani kubwa limetokea kwa rafiki yako mpaka kufikia hatua ya kumuita huyo mtu, kiukweli bado nipo gizani…’akasema‘Siwezi kuamini hilo…kuwa wewe hujui, rafiki yako hawezi kukuficha, ninajua wewe unalifahamu hili,  mumelipanaga hili, kwa dhumuni fulani, basi niambieni na mimi, ili niufahamu huo ukweli…’nikasema‘Ina maana huniamini mimi, ..mimi sijui kitu, muulize mume wako, hili ni lake yeye mwenyewe, na …kiukweli, limenishtua na mimi…’akasema docta, na mgonjwa aakinua uso kutuangalia, na docta akasema‘Tunateta kidogo na mke wako,…samahani lakini…’akasema docta‘Ongeeni tu , tena ni vizuri,..mshauri afahamu kuwa mimi ni mume wake,..na haya nayafanya kwa ajili ya familia yangu..unajua mimi nataka haya mambo tuyamalize yote leo hii hii, hebu mshauri ili tulimalize hili tatizo..., najua wewe ni rafiki mwema kwetu..’akasema mume wangu.'Ukisema hivyo unanifanya kama vile nafahamu unachotaka kukifanya....'akasema docta'Hapana,...simaanishi hivyo, nataka wewe umshauri aakubale yale ninayotaka kuyafanya, kiukweli wewe hujui lolote kuhusu hili, ni mambo ya kifamilia, lakini wewe unaweza kumshauri, akakubaliana na mimi...'akasemaDocta akaniangalia mimi...na mimi nikasema;‘Nakuapia kama unajua lolote kuhusu hili, mtapambana na mimi….nikitoka hapa naenda kuongea na baba, tuone hatima ya haya mambo itafikia wapi, maana kiukweli nimechoka, nimevumilia na kila hatua inakuwa aheri ya jana, na mimi ni binadamu jamani ….’nikasema‘Usifanye vitu kwa pupa, najua ukilifikisha kwa baba yako hivi kama lilivyo, utakuwa umeharibu kila kitu,...tafuta ni nini kinachoendelea kwanza, ili uwe na uhakika, je kama mume wako ana kusudia jambo jema,...huwezi jua, na  mwache baba yako afanye kivyake, ipo siku mtakaa meza moja mtayamaliza, nina uhakika na hilo….’akanishauri docta.‘Kwanini kwanza mkamruhusu huyu mtu kuingia ndani..hapo ndio nasema hata wewe unalifahamu hili, sio vizuri mlivyofanya…’nikasema‘Nikuambie,…huyu mtu alipofika alisema kaitwa na mume wako…nasikia mapema tu,alimwambia docta kuwa kuna mgeni wake atafika, kwahiyo, akifika aruhusiwe kuingia, kwani yeye ana mazungumzo muhimu na huyo mtu, ambayo yanamsumbua kichwa chake...’akasema rafiki wa mume wangu.‘Na wewe ukakubali kirahisi hivyo..ulitakiwa kwanza uje uongee na mume wangu, au uniambie mimi ili nikupe ushauri, maana huyo mtu namfahamu sana mimi…hebu niambie tukianza kuzozana hapa, huoni lolote laweza kutokea, maana mimi kiukweli sitakubaliana na haya mambo...’mimi nikasema.‘Mimi nakushauri uvute subira ufahamu wanachotaka kukifanya,…na mimi nisingeliweza kumzuia huyo mtu, nilijua bado ile hali tete ya mume wako bado ipo na ukizuia jambo analolitaka yeye,..inaweza ikamuathiri mume wako...’akasema‘Mhh…siamini, …kuna nini lakini…’nikasema‘Hata huyo jamaa sisi tulimtahadharisha, kuwa hali ya mume wako haitaki mawazo mengi kama kaja na mambo yenye utata, ni bora yasubirie, lakini  alichotuambia sisi wenyewe tulibakia hatuna jinsi…’akasema‘Kasema nini…?’ nikauliza‘Kasema hiyo hali aliyo nayo mume wako,  yeye pekee ndiye anayefahamu jinsi gani ya kuimaliza, keshaongea na mume wako na keshajua tatizo lipo wapi, kwahiyo yeye, kaja kumalizia makubaliano, na ana uhakika atayamaliza matatizo yanayomsumbua mume wako, hebu tuambie sisi hapo tungelifanya nini..’akasema rafiki wa mume wangu.‘Huyo ni tapeli mkubwa, anajua kucheza na hisia za watu, ni kama mchawi fulani hivi..namfahamu sana…nahisi kuna kitu..lakini ngoja tu, nitakigundua, kwa vyovyote vile, na ataishia kubaya..’nikasema‘’Usichukulie jaziba…’akasema docta,‘Wewe subiria uone…nitafanya jambo, ananitambua nilivyo, wewe subiria uone…’nikasema na sasa nikasogea pale nilipokuwa awali, na kumuinamia mume wangu…nilimuangalia moja kwa moja usoni, lakini yeye akawa ananikwepa tusiangaliane machoni…kama ananionea aibu, …sikujali, nikamuuliza;‘Mume wangu nakuomba tena, huyu mtu aondoke hadi hapo hali yako itapokuwa salama, kama kuna lolote niachie mimi, nitaongea naye, nahisi kuna kitu kakufanyia, au kakutisha nacho, huyu mtu ni tapeli, na mimi namjulia, unaisikia.....’nikamwambia kwa sauti ya chini chini, na yeye akasema;‘Mke wangu, usiwe na wasiwasi,....mimi nimeshaongea na huyu jamaa, na sivyo kama unavyofikiria wewe, nahisi uliyoyasikia kwa watu ndiyo yamekufanya ufikirie hivyo,…sikiliza  yeye kufika kwake hapa ni kwa vile mimi ndiye nimemuita. Na nilishawahi naye kabla…, na leo, kaja tumalizane…yeye kaja kwa nia njema tu, ya kunisaidia..ya kutusaidia ili haya mambo yaishe kwa amani. ..na hatakuwa na muda mrefu,…nakuomba uondoe wasiwasi dhidi yake…’akasema.Nilikaa kwa muda, nikiyawazia haya, nikainua kichwa kugeuka, kwangalia docta rafiki wa mume wangu, ambaye alikuwa akituangalia tunavyoongea na mume wangu, na aliponiona nipo kimiya,akataka kunisogelea nahisi alitaka kunisihi jambo.Mimi niliona nisipoteze muda, kwa haraka nikatoka pale na kutembea hadi pale alipokuwa kasimama jamaa…jamaa alikuwa kasimama vile vila hakujali kuwa nakuja mbele yake, hadi nilipofika pale aliposimama. Na niliona kama anataka kusogea nyuma, lakini hakufanya hivyo, akatulia, akisubiria nitafanya nini….NB: Sehemu nyingine inakuja soonWAZO LA LEO: Ukiwa na hasira usifanye jambo kwa pupa, hakikisha umetuliza hasira yako kwanza kabla ya kuchukua maamuzi, mara nyingi ndani ya hasira ibilisi hachezi mbali, na hasira inaweza kuwa ni hasara.  Nilitembea kwa haraka kama nataka kufanya jambo ...hadi nafika kwa huyo jamaa sikujua nitafanya nini, ili akilini, nilitaka nifanye jambo...nikafika pale aliposimama huyo jamaa,...nilipomkaribia tu,nikasikia mume wangu akiita huku nyuma;‘Mke wangu unataka kufanya nini…’akasema mume wangu, lakini mimi sikumjali tena, kwani sasa nilikuwa nimesimama kwa huyo jamaa tunaangaliana uso kwa uso. Tatizo yeye, alikuwa kavaa hayo mawani, mkwe usinione, nilitamani niitoe, nione anahisi nini, …lakini mkono ukawa mnzito kufanya hivyo, nilitamani, nifanye jambo, mkono unawasha, lakini mkono ukawa mnzito kuinuka,, lakini kwa haraka mkono wangu ukaenda kwenye mikono ya jamaa, nikamshika mkono na kumvuta tutoke nje, lakini hakusogea, nilipoona hivyo nikasema;‘Naomba tutoke nje, kama wewe mwanaume kweli...'nikasema hivyo'Mhh...' jamaa akaguna tu, na hakusogea'Sikiliza wewe mtu, mim nataka  tukaongelee haya mambo nje, maana hapa sio mahali pazuri pa kuongea, tutavunja taratibu za hospitali, na pia eeh…tunaweza kuleta matatizo kwa mume wangu..’ nikamwambia, na yeye kwa haraka ajaibu kwa kusema;‘Kwa leo mimi siwezi kuongea na wewe chochote, kwa maana  mimi nimekuja hapa kwa ajili ya kuongea na mume wako,...'akasema'Nafahamu hilo, ...nimeona kuwa umekuja kwa ajili yake, lakini nataka kukuambia jambo la msingi sana....'nikasema'Hapana, siwezi kufanya hivyo, kabla sijaongea na mume wako,...'akasema'Unataka nitumie nguvu...'nikasema'Hapana usifanye hivyo, kwani haitasaidia kitu...mume wako kanipigia simu anataka kuongea na mimi...kiukweli tulishaongea mambo fulani fulani,...sasa  nimekuja kuna mambo mawili matatu ya kumalizana...'akasema'Ina maana hunielewi, kwani mimi ni nani kwa huyo mgonjwa'Ni mume wako...'akasema'Kwahiyo hayo unayotaka kuongea naye mimi hayanihusu...?' nikauliza'Nitajua nikimalizana kuongea na yeye, natii alichoniomba mteja wangu...'akasema'Mteja wako...?'! nikauliza'Ndio....'akasema na muda huo yeye alikuwa akinijibu kwa sauti, kama vile anataka kila mtu asikie wakati mimi nilikuwa nikimuuliza kwa sauti ndogo‘Mliongea nini na mume wangu, mpaka akuitie huku hospitalini..au  ni ule utapeli wako wa kurubuni watu, …bado unataka kumfanyia tena mume wangu, mimi..nitakuitia polisi sasa hivi…’nikasema‘Kwanza nikuambie jambo, mimi sio tapeli..na kuja kwangu hapa sio kwa kujitakia, ni mume wako kaniita..na tuliyoongea mimi na yeye, hayawezi kusemwa mpaka nimalizane na yeye, kama anataka ndio nitakuelezea, kwanini inakuwa vigumu kuelewa….’akasema‘Kwangu mimi siwezi kukuelewa, japokuwa nakuelewa ulivyo,..na hilo unalotaka kuongea na mume wangu lazima nilichuje kwanza, kwasababu mume wangu ni dhamana yangu, lolote likitokea nitaulizwa...'nikasema, nikimuangalia moja kwa moja usoni‘Ni kweli,…lakini kwa hivi sasa hata mimi sijajua kikamilifu kaniitia nini, kwasababu kwenye simu hajaniamba, zaidi ya kusema nifike hapa hospitalini, ni muhimu sana, ..kwahiyo mpaka niongee naye ndio nitakuwa na uhakika huo,,..'akasema‘Lakini mlishaongea jambo kabla, wewe na yeye…?’ nikauliza‘Kifupi, Ndio...'akasema'Mliongea nini...?' nikauliza'Mambo mengi, yakiwemo ya afya yake, familia, kazini, na mikataba ...'akasema'Mikataba gani....?' nikauliza'Mimi naomba ukamuulize mume wako, maana yeye ndiye kaniita hapa, labda anataka nimfanyie kazi yake..’akasema‘Kazi gani sasa…?’ nikamuuliza nikitarajia jibu hilo.‘Oh, mimi nilijua nyie wawili mumeshaongea na kukubaliana, sasa kama hamjaongea kwanini ameniita,..basi huenda kaniita kwa jambo jingine, ndio maana naomba npate muda wa kuongea naye kwanza ili nijue ni kitu gani, tafadhali...’akasema.‘Huwezi kuongea naye mpaka nijua ni jambo gani, ili niwe na usalama moyoni, je mkiongea jambo likamkwanza..tafadhali...’ nikasema.‘Madamu,…siwezi kusema kitu, nitakuambia nini sasa, mimi sijui kaniitia nini, huenda ni maswala mengine,...tafadhali nielewe hapo, tutalumbana hapa bure na sitaweza kukuambia kitu…’akasema‘Sasa naona unataka na mimi nifanye kazi yangu,… hebu sikiliza, huyu mume wangu anaumwa, na mara kadhaa amekuwa akipoteza fahamu kwasababu ya shinikizo la damu..na madocta wakashauri  tusiwe tunamshinikiza kwenye mambo ya kumfikirisha sana,…sasa wewe eeh,…, hivi nikuulize..kama tukiongea hapa nisipokubaliana na nyie,akashikwa na hasira akadondoka, ....huoni kuwa utajiweka kubaya...’nikasema.‘Haiwezi kutokea hivyo madamu..nakuhakikishia hilo…halafu nikuambie kitu, mimi sijafika hapa kwa ugomvi na wewe kwanini tusielewane...eeh,..na ama kwa huyo mumeo yeye ni rafiki yangu toka siku nyingi, wewe tu ndiye uliyeingilia urafiki wetu, na kunipiga marufuku nisiwe naonana na yeye, sawa mimi nilitii...'akatulia'Sasa umefuata nini tena, nilishakupiga marufuku...'nikasema'Mumeo anaumwa, na nirafiki yangu, mimi ni binadamu, kuumwa ni kitu kingine, unanisikia sana..sitaweza kuwa na amani, bila kuja kumjuliahali..kwa hapo nilivunja agizo lako samahani sana..’akasema‘Kwahiyo kumbe ulikuwa unakutana naye mara kwa mara au sio kwa kujifanya wewe ni mwema, au sio…’nikasema‘Madamu ni wewe tu hunifahamu, mimi ni mtu mwema sana…sina ubaya na watu, mimi ni mtu wa watu hasa wale wanaotaka huduma zangu…na kwa huyo mume wako, yeye tumeshibana sana, lakini tunaheshimu tu maagizo yako…kiufupi, wewe usiwe na wasiwasi kabisa na mimi, ni wewe tu madamu....’akasema.‘Tatizo ni hivi..kauli yako na nafsi yako ni vitu viwili tofauti, mimi nakufahamu sana wewe ulivyo, upo tayari kufanya kazi yoyote inayohusiana na taaluma yako kwa ajili y pesa bila kujali kuwa ni kinyume na maadili yako...pesa kwako wewe ni kila kitu....na kwahiyo siwezi kukuamini kwa lolote lile utakaloongea na mume wangu, la sivyo, liwe halinihusu mimi, unanisikia..’nikasema‘Hamna shida, ni wewe madamu…’akasema‘Ila nakuonya, kama utafanya jambo la kumweka mume wangu kubaya, ..kama kuna njama za kumrubuni mume wangu kwa minajili ya kuchuma pesa kwa kutumia mgongo wake..., mimi na wewe tutapambana, kwanza nikitoka hapa nakwenda kutoa taarifa polisi…’nikasema‘Mimi hayo siyafahamu…nijuavyo mimi ni kuwa katika kumsaidia mume wako, nitakuwa nimechangia kwa kiasi kikubwa, kumaliza matatizo yake ya kiafya, hilo nina imani nalo, kwa kiasi kikubwa nitakuwa nimemaliza jambo linalomsumbua sana mume wako,…je huo nao ni utapeli,..’akasema‘Wewe ni docta au mganga wa kienyeji...?' nikauliza'Mimi ni wakili, wakili wa kujitegemea...'akasema'Hivi wewe hukumbuki kuwa polisi bado wanakuchunguza kwa tabia yako hiyo ya utapeli,..au unataka kufanya nini tena, unafahamu bado kesi yako ipo polisi au nikawaite polisi waje wakuchukue?’ nikamuuliza.‘Hahaha, madamu, tafadhali, ...mimi sio tapeli,....polisi, nilishamalizana nao, hakuna kesi yoyote dhidi yangu, kawaulize ...., na hilo la kuwaita, usiogope kufanya hivyo, kama unaona ni njia sahihi ya kumsaidia mume wako haya, karibu, lakini nakuhakikishia mimi nitaweza kumsaidia mume wako kwa kiasi kikubwa sana…’akasema akitikisa kichwa kidogo.'Sitaki huo msaada wako, siku zote nahangaika naye, leo umeona kapata nafuu, unataka kumpandisha tena shinikio la damu, ngoja nikaongea na docta wakutoe humu ndani...'nikasema‘Nikuambie kitu madamu, labda kwa taarifa tu, kipindi uliponishitakia, nilikwenda polisi, nikawaambia waniambie kosa langu ni nini, na kama nina kosa wanifikishe mahakamani, mbona hawajafanya hivyo hadi leo…, kwahiyo hili la kusingiziwa utapeli, achana nalo, halina nguvu kabisa, mimi najiamini, ninafanya kazi zangu kisheria, na wanaobisha twende mahakamani.....’akasema na kutulia.‘Sawa safari hii hilo litafanyika, nakuahidi hivyo…’nikasema'Sawa ...unasema unataka kumuita docta anitoe, sawa, muite tu..usijali madamu, kama itasaidi....'akasema na mimi hapo nikasita kidogo, nikageuka kule walipo mume wangu.**********  Baada ya kuongea na huyo mtu,  nikageuka kumwangalia mume wangu, nilimuona akituangalia tu, hakuonyesha dalili ya kuingilia maongezi yetu, alikuwa katulia, huku macho yake yakipepesa pepesa, kama vile anajisikia vibaya, hapo nikaona nisije nikaleta hali nyingine mbaya, nikageuka kumwangalia huyu mtu na kusema;.‘Mimi nimekuelezea niliyotaka kukuelezea na mimi nimenawa mikono, na naona hunielewi, sawa, mimi naona ni bora niondoke, ili kuepusha shari, maana mimi nina uchungu wa mume , wewe hutojali chochote kikitokea…’nikasema‘Ni wasi wasi wako tu madamu…’akasema‘Ndio lazima niwe na wasiwasi huo,…ngoja nikuachie huyo mtu uendelee kumdanganya na utapeli wako, lakini kwa masharti, kama kuna lolote litatokea,mume wangu akizidiwa, au kama kuna lolote baya, kati yako na yeye,....mimi  sitasubiria polisi, wala nani, nitahakikisha nikapasua kichwa chako kwa risasi...hilo ninakuahidi...’nikasema na yule mtu akabenua mdomo kwa dharau na kusema;‘Mbona mimi sina neno madamu…, mbona hunielewi, kwanini hayo yote huongei na mume wako tu kukuthibitishia kuwa mimi sina maana yoyote mbaya, ni kwa masilahi ya mume wako, sio zaidi ya hilo, umesema unakwenda kumuita docta anitoe, mbona hufanyi hivyo, tunapoteza muda bure, tutafukuzwa hapa na mume wako atakuwa hana amani, unajua ni nini kitatokea, ni nani atalaumiwa kwa hilo, mimi au wewe....’akasema‘Sawa, nimekuelewa…’nikasema‘Madam,..usiwe na wasiwasi na mimi, dada yangu, sina nia mbaya kabisa, mimi nimetii wito kutoka kwa mume wako, kama kuna cha kulaumu, basi mlaumu mume wako, na...nakuahidi nikitoka hapa mume wako atakuwa salama, salamini…’akasema‘Sawa …sasa nimekuelewa, hamna shida…’nikasema.‘Madamu sikiliza  nikuambie wazi, wewe ndiye unayesababisha mume wako asipone kwa haraka, jaribu kumsikiliza mume wako ni nini anakitaka, uone kama hatapona, ni ushauri wamgu wa bure tu, hapo alipo anajikakamua tu, lakini kupona vyema ni wewe tu…shauri lako....’akasemaAliposema hivyo, nikaona nisiendelee kulumbana naye, maana kwa huyu mtu ni mjanja sana, ukimtaka kwa maneno mtalumbana mpaka kesho;‘Kwahiyo kwa kifupi, mume wangu anakutakia nini wewe…?’ nikamuuluza‘Kwa ufupi, anataka mimi niwe wakili wake….’akasema‘Wakili wake kwa kesi gani…?’ nikamuuliza‘Sio kesi, ila ananihitajia mimi kuwa wakili wake wa kifamilia na hata mambo ya kazini kwake, ila hatujafikiana muafaka, labda leo ndio kaniita tumalizane, sina uhakika na hilo, madamu....’akasema‘Lakini  mbona tunaye wakili tayari, wa kifamilia na mambo ya kikasi, na unalifahamu hilo…’nikasema‘Ukamuulize yeye mwenyewe, ila sijajua alichoniitia hapa hii leo, naomba usininakili vibaya...'akasema'Ni lazima atakuwa kakuambia ni kwanini anahitajia wakili mwingine au sio...?' nikauliza kwa upole'Ndio kasema wakili huyo hawakilishi matakwa yake, na ana wasiwasi kupona kwake kunaweza kuwa ni mwanzo wa tatizo jingine,..kwahiyo ameniita mimi kuja kumsaidia, na zaidi ni kutokana na ushauri wa docta, kuwa ajitahidi kuondoa yale yote yanayomsumbua akilini...ni hayo tu ninayoweza kukuelezea, siwezi kueleza zaidi ya hapo...’akasema‘Wewe uwe wakili wake, ….hahaha, labda niwe maiti…’ nikasema.‘Madamu, kwanini unasema hivyo, mimi ni wakili au sio…sasa kuna tatizo gani nikifanya kazi za mumeo, ....cheti changu kinatambulikana kimataifa, japokuwa fitina zimepita nyingi tu..,’akasema‘Fitina au ndivyo ulivyo..’nikasema‘Hao hao watu wanaoleta fitina wakikwama chini kwa chini, wanakuja kwangu kutaka niwakwamue, na ndivyo ninavyotaka kufanya kwa mume wako...kumsaidia rafiki yangu…kwenye matatizo yake.’akasema.‘Mume wangu hana matatizo, kachanganyikiwa tu,na wewe unachukulia mwanya huo kumghilibu…’nikasema nikigeuka kumwangalia mume wangu, na wakati huo, alikuwa akiteta jambo na rafiki yake.‘Docta kanithibitishia kuwa hali yake ipo shwari, na wala hajachanganyikiwa, na nikimsaidia nitakuwa nimechangia kwa kiasi kikubwa kumtibia,na nimemuhakikishia docta kuwa mimi nitamsaidia rafiki yangu apone kwa haraka..kama unabisha, kamuuliza docta wake…’akasema‘Kwa hili tutapambana..’nikasema‘Hebu kwanza, maana naona vitisho vyako vinazidi, unaonaje… , naomba dakika kumi tu,niongee na mteja wangu, nikimalizana naye mtaongea naye, na kama atataka kuwaambia lolote,atawaambia yeye, ila baada ya mimi kuongea naye leo,kama kuna lolote la kumshutumu yeye, naomba mliwasilishe kwangu mimi kama  wakili wake...’akasema.‘Tapeli mkubwa wewe...sikia nikuambie...’nikasema hivyo na kugeukia kule alipo mume wangu, walikuwa bado wnaongea rafiki yake, na walionekana kama wakibishana jambo fulani, na rafiki yake…baadae niliona docta kama ananyosha mikono juu kusalimi amri,akasogea pembeni kama kukata tamaa.Mume wangu aligeuka kuniangalia, na mimi nikitabasamu ile ya kebehi, na yeye alipoona hivyo,akainamisha kichwa chini, na ilionekana hakuwa na furaha , sijui waliongea nini na rafiki yake,mgeukia huyu mtu na kusema;‘Nitahakikisha nayafahamu haya yote, na unanifahamu nilivyo...mimi naondoka, lakini kama kuna lolote baya linaloendelea dhidi ya mume wangu, au dhidi yangu mimi, tutapambana, ....tutaona mwisho wake, na safari hii, nitahakikisha hurudii tena...’nikasema huku najifanya natabasamu, na huyo jamaa akisema.‘Usijali dada yangu, umeshaniambia hilo mara nyingi tu, usipoteze pumzi yako, kwa kurudia rudia, kitu kisichotekelezeka,…na sioni kwa nini usiniamini,...utakuja kunipa mkono wa ahsante, lakini nilijua na wewe unatakiwa kuwepo ....’akasema na kuangalia saa yake.‘Siwezi kukaa kusikiliza utapeli wako…’nikasema Kwa muda ule nikageuka tena kumwangalia mume wangu, na mara docta akaingia, na sasa akawa anaongea na mume wangu, na dakitari akawa anaandika kitu kwenye kumbukumbu zake, halafu akageuka kuniangalia mimi na kusema;‘Kuna lolote jamani maana muda umekwiisha wa kuwaona wagonjwa, kama kuna lolote jingine basi niwapa dakika kadhaa..au kama kuna kitu cha kuulizaniulizeni, vinginevyo dakika zilizobakia ni z huyu mgeni wa mgonjwa, au sio…’akasema akimuangalia mume wangu‘Sawa kabisa docta, …na mke wangu,…’akasema‘Hapana…nahisi ni bora mkaongea na huyu mtu wako hatutaki aina yoyote ya malumbano, unasikia, bado upo kwenye masharti, vinginevyo, usibiria mpaka hali iwe sawa, kwa vipimo vyako, bado kidogo…’akasema docta.Mimi nilimwangalia mume wangu, yeye alibenua mdomo kama kulazimisha kutabasamu, lakini kwa undani zaidi machoni, niliona kama ana huzuni, nahisi mume wangu yupo kwenye matatizo makubwa..‘Huyu mtu ana nini, kwanini amchukue huyu tapeli, sio bure, kuna tatizo hapa…’nikasema kimoyo moyoHapo sikutaka kupoteza muda, au kusikia kile alichosema mume wangu kuwa na mimi natakiwa niwepo,..., nikageuka, na kuanza kutoka nje,...na kabla sijafika mbali nikasikia mtu akiniita nyuma yangu, sikutaka kugeuka kwani sikutaka kuongea naye, lakini huyo mtu hakukata tamaa, alinikimbilia na kunishika bega.‘Kwa hali ilivyo , nakushauri, acha wafanye wanavyotaka, ili kuepusha shari...naona kuna kitu kinaendelea , usipokuwa makini, utaumia, na unaweza ukampoteza mume wako…’alikuwa na docta rafiki‘Wacha itokee hivyo, mim sijali tena…’nikasema‘Lazima ujali huyo ni mume wako…na kwanini hukusubiria ukasikia wanataka kuongea nini, hasira zako zinakufanya ukose maana…’akasema‘Acha nikose hadi hapo najua nimesimama na nani, na ni nani adui yangu, ila kwa mume wangu najua kuna mtego, kategewa na huyo mtu, huyo mtu ni tapeli, sio bure,..mume wangu anafanya kwa nguvu za….’hapo sikumalizia‘Hahaha, sio kweli, mume wako anafanya hivyo kujihami, anajua akipona hapo, utaweza kumshitakia kwa wazazi wako, hiyo ni moja ya sababu  lakini pia pia kuna huo mkataba wenu, mimi sijui unahusu nini,  unaweza ukawa ni sababu nyingine kubwa sana…au..ni ..nakumbuka kuna kipindi ulipokuwa unasomea sheria ulisema ungelipenda kitu kama hicho…’akatulia akitaka mimi nisema neno, lakini sikusema kitu‘Basi kama mlifanya hivyo, mkawa na mkataba kama huo…ndio unamueweka pabaya, yategemea mumekubalinana nini, maana naona hicho ndicho mume wako anakihofia sana, hasa akitaja mkataba…’akasema‘Wala hilo kwangu sio tatizo kubwa, kama kakosea, akiri kosa, na mimi ni binadamu, tunaweza kuvumiliana kutegemeana na hilo kosa, lakini kwa jinsi nimjuavyo,…haweze kukiri kosa, atajibaragua na kutafuta uchochoro wa kujitetea, sasa hilo sitaweza kulivumilia, bora mkataba ufanye kazi yake nijue moja tu…’nikasema‘Kutegemeana na kosa,…nakunukuu, je kama  kosa ni hilo la kuwa katembea na rafiki yako, na sasa kazaa naye,utalichukuliaje hilo…’akasema docta‘Weeeh, mungu wangu, na rafiki yangu, hapana..ingelikuwa na mtu mwingine baki, hata hivyo, kwenye mkataba hilo ni kosa kubwa, halina msamaha…haaah, hapana, hawezi akafanya hivyo, maana anafahamu madhara yake…’nikasema‘Mhh…sasa hilo, nahisi ndilo linamtesa, na huko kuhangaika kwake yawezekaan ikawa ndio sababu, ..lakini sioni ni kwanini amtafute wakili, hapo ndio nakuwa na mashaka,…ina maana kweli, huwezi kumsamehe..?’ akauliza‘Kama mtu akivunja masharti ya ndoa, kama hivyo, akazini nje, ..na ushahidi ukawepo, basi kakiuka mkataba, na adhabu yake ipo wazi, hatuwezi kuchezea kiapo, tuliapa na kukubaliana, je kama ingelikuwa ni mimi angelifanyeje, mkuki usiwe kwa nguruwe, sasa akiri tuone, nita…haaaa…..’hapo sikumalizia, kwani simu ya docta iliita, na kwa haraka akaipokea, na akawa anasikiliza kwa muda, na alipomaliza, akaniangalia na kusema‘Rafiki yako ameshafika,alikuwa akikuulizia, anasema kajaribu kukupigia kwenye simu yako lakini ulikuwa hupatikani....’akasema na mimi hapo ilikuwa kama mshtuko mwingine tena kama mtu kanipiga kibao cha kushtukizia usoni..nilishtuka kweli, na muda huo nilikuwa nimeshikilia mlango wa gari, ukiwa nusu wazi,.. nikajikuta naufunga huo mlango badala ya kuufungua.‘Ka…ka…ooh, ….’nikashika kichwa na kutulia kidogoKwakweli pale nilihisi moyo ukinienda mbio, kama vile hasira, au…kutaka kufanya jambo. Nilibakia vile kwa muda, baadae docta akanisogelea akitaka kunishika, lakini kwa haraka nikaweka mkono kama kinga, asinisogelee, halafu nikauliza.‘Yupo nyumbani kwake?’ nikawa nimeinamisha kichwa chini sikumuangalia docta.‘Ndio, yupo nyumbani kwake…’akasema‘Na mtoto wake hajambo…?’ nikauliza‘Atakuwa hajambo, lakini hakuongelea lolote kuhusu mtoto wake na mimi sikumuulizia hilo....’akasema.‘Sawa bosi…’nikasema hivyo‘Hahaha mpendwa,  nimekua bosi tena, sikiliza ex-wangu,...napenda nikushauri jambo la kutoka moyoni…’akasema‘Sihitajii ushauri wako…, hivi sasa sitaki kumuamini mtu zaidi ya wazazi wangu tu, nimeona wazazi wangu …ndio wa kuamini, waliyonishauri nikawapinga sasa ndio naona matokeo yake, nayaona, lakini sitakubali…’nikasema‘Sikiliza tu… ninachopenda kukuambia ni kuwa kwa jinsi haya mambo yanavyokwenda, unanihitajia sana kuwa na mtu wa karibu sana wa kukusaidia, mtu anayeaminika, kwasababu nakuona upo katikati ya watu ambao unahisi ni marafiki zako kumbe pembeni wanakutendea visivyo…’akasema‘Na mmojawapo akiwa ni wewe…’nikasema‘Sawa kama utaamini hivyo…ila ukweli ndio huo, hao unao-ona ni marafiki zako, hao hao wanaweza kugeuka kuwa ni maadui zako wakubwa.....hebu fungua macho na masikio yako unisikilize angalau kidogo....’akasema.‘Ni kweli unayoyasema, naanza kuamini hivyo,..na hao wanaojifanya ni marafiki zangu kumbe ni maadui zangu nimeshaanza kuwaona,  akiwemo wewe mwenyewe, siwezi kukuficha hilo,..’nikasema‘Sio kweli, mimi sitaweza kuwa adui yako hata siku moja, nilishaapa kuwa nitakusaidia, na itakuwa hivyo mpaka mungu aichukue roho yangu…’akasema na mimi hapo nikageuka kumuangalia.‘Hahaha.., usijifanye kuwa wewe haupo kwenye hilo kundi, maana wewe unauma na kupulizia,...upande mmoja unajifanya rafiki upande mwingine, unajificha kwenye maadui zangu, nimeshakufahamu kuwa wewe una ajenda ya siri,..’nikasema‘Sio kweli….’akasema na kabla hajaendelea nikasema‘Hata hivyo nawaambia hivi… mimi naamini sana watu, lakini nikija kugeuka, hutaweza kuamini kuwa mimi ndio yule mtu…na kwa hili nitapambana nanyi, mmoja baada ya mwingine....hilo nawathibitishia...’nikasema nikionyesha kidole cha kuapa.‘Mhh, haya bhana, sina la kusema, lakini ipo siku utagundua huo ukweli niliokuambia,....ila, nakupa angalizo kama mtu anayekujali, usijidanganye sana na kujiaminisha kuwa utaweza kupambana na hao wtu kirahisi hivyo, muhimu tafuta muda, tuliza kichwa,… usiyachukulie haya mambo juu kwa juu, utaumia vibaya sana.....’akasema‘Hilo sio la kunishauri mimi…, nimeshajua mwenyewe, na hujui nilivyo, nimekuwa na subira sana, sijachukulia haya mambo kwa pupa, kama ningelifanya hivyo, sasa hivi tungelikuwa hatuongei…nimeonekana mjinga nisiyeona au kusikia, unajua ni kwanini…’nikasema kama nauliza na huyo docta akaongea kama vile hakunisikia‘Huyo wakili,…sio mtu wa mchezo mchezo kama unavyomfikiria wewe, ana uzoefu na kazi yake…, na huko polisi anajuana na kila mtu,…hap hapo polisi wanamtum,ia kwa mambo yao,…huyo jamaa ni mtu hatari sana...usije ukalogwa kupambana naye peke yako...’akasema na aliposema hivyo mimi nikafungua mlango wa gari na kuingia ndani ya gari langu, nikashusha kiyoo ili niweze kumuaga docta.'Kama ni mtu hatari basi kakutana na mtu hatari zaidi yake, mimi namfahamu sana, nimeshapambana naye mara mbili na zote kalilia pua...wewe hunijui tu…subiria uone vumbi langu, kwaheri, nisalimie mkeo…..'nikasema huku nikikanyaga mafuta.Niliendesha gari, kwa muda..na nilipofika mbele, nikachukua simu yangu na kumpigia mtu wangu.'Sikiliza..kama nilivyokuambia, kuna mtu yupo hospitali na mume wangu, mfuatilie, hatua kwa hatua, nataka kila kitu anachokifanya..hata ukiweza kufahamu walichoongea…, na ujue wapi atakapokwenda akitoka hapo hospitalini, unasikia, hilo ni muhimu sana..kazi njema, ..'nikasema na kukata simu.NB: Haya hiyo ya moto moto….WAZO LA LEO: Sio wote wanaoitwa marafiki ni marafiki wa kweli kwako, sio wote wanakuchekea, wana nia njema na wewe, cha muhimu, ni kujaribu kutimiza wajibu lakini pia kuwa kuwa na tahadhari, kwa kutokutoa siri zako, kwa kile unayemuona ni rafiki yako. Kumbuka adui na rafiki yako ni huyo huyo anayekufahamu sana.Nilipotoka pale hospitali, niliendesha gari kwa makini, nikichelea nisije kupatwa na ajali kama ilivyompata mume wangu, nahisi mume wangu aliendesha akiwa amechanganyikiwa, na sio kwasababu ya ulevi.Nilitaka nifike nyumbani, maana kulikuwa na mambo nilihitajika kuyachunguza, lakini pia nilihitajika kwenda kuonana na rafiki yangu, ambaye nasikia karudi kutoka huko alipokwenda kusoma, nilishindwa kuelewa ni kwanini akaamua kurudi haraka hivyo..nahisi kuna sababu kubwa sio bure…Nikaona nipitie kwake kwanza kabla sijafika nyumbani, nikakumbuka kuwa sehemu aliyokuwa akiishi awali, alikuwa amepakabidhi kwa mwenye nyumba, na alisema akirudi atakuwa akiishi kwa ndugu yake mmoja, japokuwa nilimuambia kwangu kuna nafasi akirudi anaweza kuja kuishi kwangu hadi hapo atakapomalizia nyumba yake anayojenga.Nilipofika hapo kwa ndugu yake, nikaambiwa hayupo…‘Hayupo katoka au hakufikia hapa kwako…?’ nikauliza‘Amefikia hapa, ila aliondoka muda tu, aliniaga kuwa anakwenda hospitalini…’nikaambiwa‘Anaumwa…?’ nikauliza‘Hapana kasema anakwenda kumuona mgonjwa…’nikajibiwa na hapo nikahisi mwili ukinichemka, nikajua atakuwa kaenda kuonana na mume wangu, lakini mbona hatukukutana naye njiani, au kachukua usafiri gani‘Na mtoto wake yupo wapi?’ nikauliza.‘Mtoto wake…!! ’akasema kwa mshangao, na mimi nikasema‘Ndio, si ana mtoto mdogo, au…?’ nikauliza.‘Hayo mengine utamuuliza mwenyewe, ….’akasema na alionyesha kama hataki kumuongelea ndugu yake,  nikaona hakuna haja ya kupoteza muda.‘Basi sawa akirudi mwambie nilikuja kuonana naye…kama hatajali nataka nionane naye…’nikasema‘Sawa nitamuambia….’akasema na wakati nataka kuondoka, huyo mwenyeji akaniuliza‘Kwani kuna tatizo, gani maana kuna mtu mmoja alikuja,..hata sijui ni kwanini rafiki yako anaogopa kufuatilia  …’akasema‘Kufuatilia nini…?’ nikauliza'Tuyaache hayo, hayanihusu sana...nisije kuharibu lawama ikarea kwangu...'akasema'Lawama gani kwani kuna nini kimetokea...?' nikauliza‘Kama nilivyoambiwa, maswala ya mtoto nisiseme lolote…’akasema‘Na nani, kwani mtoto yupo…?’ nikauliza‘Ndio nakuwambia, nimeambiwa nisiseme lolote kuhusu mtoto, na wala sijui lolote kuhusu mtoto…’akasema‘Sikiliza mimi ni bosi wake, na rafiki yake,…na nina wasiwasi na hali ya mtoto, ndio maana nauliza hivyo…’nikasema‘Basi akirudi nitamwambia hivyo, …samahani kwa hilo…’akasema Basi na mimi, nikaamua kurejea nyumbani kwangu, nilipofika nyumbani kwangu kwa kujirizisha tu, nikataka kujua mambo fulani fulani, kwahiyo, nikawa nawahoji tena watu wangu wa nyumbani kuanzia mlinzi hadi wafanyakazi wa ndani, kama kuna mtu yoyote aliwahi kufika hapo, kabla…Sikuweza kupata nilichokitaka, hapo nikaona nifanye jambo jingine kwa haraka kwa kujirizisha tu..., sikupendelea kufanya hivyo, lakini nikaona ndio muda pekee ninaoweza kufanya jambo kama hilo,…Nikaanza kupekua vitu vya mume wangu, sehemu zote anapoweka vitu vyake…pia kwenye chumba cha akiba ambacho alikuwa akilala akiwa kalewa, sikupata kitu cha maana, mwishowe nikaona nirejee kwenye maktaba niangalie vyema.Nikafungua tena lile kabati langu, safari hii kwa uangalifu kidogo, na cha ajabu niliona ile nakala ya mkataba wangu na mume wangu, ikiwa umewekwa pale pale nilipopendelea kuuweka,...!‘Mhh, nani kairudisha tena,…?’ nikasema kwa sauti ndogo, kwanza sikuugusa, nikachuka kitu cha kuzuia alama za vidole mkononi, nikaanza sasa kuukagua huo mkataba, kwa haraka nikagundua kuwa sio ile nakala yangu, maana ile nakala yangu ilikuwa na alama zangu maalumu, ambazo mtu hawezi kuzigundua, na hiyo nakala haikuwa nayo, kwahiyo ni nakala nyingine!‘Hii nakala imewekwa baadaye....sio ile nakala yangu.’nikasema ,Nilichukua ile nakala na kuanza kuipitia kwa haraka haraka, sikuweza kugundua mabadiliko, sijui kwa vile muda huo sikuwa nimetuliza kichwa,...nikaona nipumzike kwanza…nikatuliza kichwa kwa kupata kinywaji cha matunda…Baadaye nikaichukua ile nakala na kuanza kuipitia kwa makini kidogo nikagundua kitu, kwenye sehemu ya kipengele cha watoto naona kama kuna vitu vimebadilika, lakini bado sikuwa na uhakika , ....nikaanza kuisoma sehemu hiyo kwa makini, ilikuwa sio kazi rahisi, ila niligundua sehemu moja, inasema hivi;‘Kama wazazi watakuwa wamefariki,..Watoto wote wana haki sawa, na mali ya urithi  itagawiwa sawa,.’hili neno `wote’ sikumbuki kama ilikuwa hivyo mwanzoni, nakumbuka tulitumia neno `wetu’ na hili neno wetu kwenye ufafanuzi tuliandika, kuwa linasimama badala ya wanandoa mimi na mume wangu kwa kutaja majina. Nikafungua kwenye ufafanuzi, sehemu hiyo ya ufafanuzi, ilikuwa imeondolewa!‘Kwanini wafanye hivyo, na ni nani huyu, ni mume wangu na wakili wake nini, na kwanini wafanye hivi, hii sasa imevuka mipaka....’nikasema.Hapo nikaanza kuingiwa na ufahamu, kuwa kumbe mashaka na wasiwasi ya mume wangu ni kuhus huo mkataba, kumbe nia yao ilikuwa kubadili huo mkataba, nikaanza kusoma tena sehemu nyingine kuna sehemu zimeondolewa na kuongezwa maneno mengine ili kuleta maana fulani, sikuelewa ni kwanini walifanya hivyo.Nikafungua sehemu nyingine lakini sikuweza kugundua mabadiliko mengine, japokuwa nilihisi kuwa kuna sehemu fulani fulani zimebadilika, lakini kiutalaamu zaidi, na hapo nikaona niwasiliane na wakili wangu, nikampigia simu.Simu iliita kwa muda bila kupokelewa, na baadaye akaipokea, na kusema alikuwa akimsaidia mgonjwa, maana alikuwa kwao, akimuuguza mzazi wake, nikamwambia hayo yaliyotokea, na akasema;‘Kuna mtu ana nia mbaya, maana mimi nilipoondoka tu, nilipata taarifa kuwa kuna watu waliingia ofisini kwangu wakaiba baadhi ya vitu, sasa sina uhakika kama ni pamoja na hiyo nakala ya huo mkataba, ni mpaka nikirudi huko ndio nitaweza kulifahamu hilo.....’akasema.‘Mimi nahisi watu hao lengo lao ni kuhakikisha kuwa wameiba nakala zote, na kuziweka nakala wanazotaka wao,…je kwenye mtandao hukuhidhi chochote?’ nikamuuliza.‘Katika vitu ambavyo nasikia wameiba, ni pamoja na komputa yangu ambayo nimehifadhia mambo yote, na sijahifadhi sehemu nyingine zaidi, maana sikuwa na mashaka kuwa hali kama hiyo inaweza kutokea, hii sasa ni changamoto kwangu, kazi zote sasa nitaziweka kwenye mtandao ya kudumu..’akasema‘Ni bora uwe unafanya hivyo , maana kwa hali hii hatutakuwa na na kumbukumbu ya mkataba wetu ule wa awali…’nikasema.‘Hili nitapambana nalo nikirudi, hata wajifanye wajanja vipi…kiukweli kwa hivi sasa siwezi kufanya lolote, maana namuuguza mama, kwahiyo mambo mengine sitaweza kusaidia…’akasema‘Sasa kama nakala ya huo mkataba imechukuliwa huko kwako na komputa imeibiwa, tunawezaje kuipata nakala nyingine wapi, maana nahisi wamebadili huu mkataba kwa makusudi maalumu, na cha ajabu wameweza kutumia sahihi yangu kama ilivyo,..ina maana huyu mtu ni mtaalamu kweli wa kugushi hata sahihi za watu....’nikasema.‘Kama wameamua kufanya hivyo, basi nina imani kuwa hata huko serikalini watakuwa wameshafanya hivyo hivyo,watakuwa wameshabadili huo mkataba na kuweka huo wanaoutaka wao, na kugushi sahihi, sio kazi ngumu sana, maana wanaweza kutumia mtandao..ni shida kidogo, lakini upo utaalamu wa kuligundua hilo....’akasema.‘Lakini huko serikalini watawezaje kuipata hiyo nakala nyingine, sizani kama wamefanya hivyo hata huko…, ?’ nikauliza‘Unafahamu hali ilivyo, kama una pesa lolote linaweza kufanyika, sina uhakika sana na hilo, na sijui kwanini wafanye hayo yote,…kwakweli ni mpaka nirudi ndio nitajua cha kufanya…’akasema‘Mhh, inanitia mashaka hii hali, kwanin lakini…’nikasema‘Sasa fanya hivi kama unaweza nitumie hiyo nakala, ipige picha sehemu unazohisi zimegishiwa, unitumie, ili na mimi niupitie upya,mimi nitagundua ni sehemu gani wamebadili, na kwanini...hata kama unaweza kunitumia yote itakuwa ni vyema zaidi…si inawezekana hiyo?’ akaniuliza.‘Sawa nitakutumia, sasa hivi, hiyo ni kazi rahisi tu, ......’nikasema,‘Itakuwa vizuri, kama hatujachelewa, tunaweza kufanya jambo, usijali, ujanja ujanja wao utakuja kujulikana, japokuwa inanipa mashaka..huyo mtu anajiamini vipi…lazima kuna kitu wanategemea, lakini tutalimaliza hilo, hakuna mjanja juu ys sheria....’akasema‘Kama hatujachelewa una maana gani..?’ nikauliza na simu ikakatika, nikaona haina haja, nikaanza kazi ya kuipiga picha hiyo nalaka ya mkataba, hadi nikamaliza na kumtumia huyo wakili.***********Wakati nataka kuondoka nyumbani, nikakumbuka jambo, nikarudi kule kwenye maktaba yetu na kufungua kabati sehemu ninapohifadhia silaha yangu, niliikuta ipo pale pale, ililinijia wazo la kuichukua hiyo bastola niwe natembea nayo, ni bastola ndogo‘Kwanini nitembee na silaha…aah, haina haja…’nikasema kwa suti ndogoBaadae nikaondoka hapo nyumbani hadi ofisini kwangu, na nilipofungua kabati langu, nikakuta nakala ya mkataba ipo, imerejeshwa na kuwekwa pale pale ilipokuwa, nikaichunguza na kugundua kuwa sio ile nakala yangu ya awali!Nikaifungua na kuanza kuisoma, ni kama ile ile niliyoikuta nyumbani kwangu, na safari hii nilitulia kidogo, nikagundua sehemu kubwa ya vipengele vya umiliki wa mali, vimbebadilishwa pia.‘Huyu mume wangu anataka nini, ina maana akili yake yote ipo kwenye mali, kama ni mali si angelisema tu…kwanini anafany ahaya yote..’nikawa naongea peke huku napitia sehemu hiyo kwa uangalifu zaidi, ndio nikaona sehemu ikiwa imebadilishwa kwa kirafu zaidi‘Mume ndiye atakayekuwa muangalizi wa mali yote na mwenye mamlaka ya mali zote, na atakuwa na uhuru wa kumuingiza mtu yoyote katika umiliki wa mali kama atakavyoona yeye inafaa, hata bila ya idhini ya mke wake...’‘Oh, hii mpya…’nikasema‘Hii seehmu haikuwepo kwenye mkataba wa awali, ilitakiwa kila kitu kisifanyike bila ya makubaliano,…na awali mimi niliona iwe hivyo, kuwa mume ndiye anakuwa na mmalaka zaidi, lakini mume wangu mwenyewe ndiye alipinga hiyo hoja, akisema;‘Baba yako hatatuelewa,..atahisi mimi nataka mali yake…’alisema hivyo‘Sasa unataka tuweje..au tutamsikiliza wakili wetu, yeye akapendeleza kuwa kila kitu kisifanyike bila ya maridhiano ya pande mbili, na ikawekwa sawa kisheria, sasa hilo wamelifuta na kuweka maneno mengine.Nikasoma maelezo mengine, lakini akili yangu ilikuwa imechafuka, hasira zilianza kunipanda, hapo hapo nikampigia simu wakili na kumuulizia hicho kipengele, mbona hakikuwepo, ndipo akaniambia kuwa hawo watu wamefanya hivyo makusudi, huenda kuna mtu wanataka kumuingiza kwenye umiliki wa mali...‘Kumuingiza kwa vipi?’ nikamuuliza.‘Kwenye maelezo ya mwanzo, ilikuwa imesema kuwa hakuna mtu atakayeruhusiwa kuingizwa kwemue umiliki wa mali, au kwenye hisa za kampuni , zaidi ya wewe na mume wako na watoto wenu. Na watoto wenu ikiwa na maana mlizaa wewe na yeye.hilo wameliondoa na kuweka maneno yao…’akasema‘Kwahiyo lengo lake ni nini hapo…?’ nikauliza‘Lengo lake ni ili awe mwenye mamlaka zaidi yake na ataweza kufanya kila kitu bila ya kukushirikisha wewe, labda akiona kuna umuhimu huo…’akasema‘Kwa mtizamo huu, moja kwa moja mume wangu ndiye yupo nyuma ya haya?’ nikamuuliza.‘Kwa jinsi ilivyo inaonyesha hivyo.... nahisi anafanya hivyo kwa shinikizo fulani, ....’akasema wakili‘Kwa ushauri wako nifanye nini, nitoe taarifa polisi....?’ nikamuuliza.‘Bado huo sio muda muafaka, inabidi kwanza kuchunguza hili kwa ukamilifu wake maana hapo kuna kesi ya kugushi, je unawezake kulithibitisha hilo, wakat nakala zote zinasema hivyo…na ukitoa taarifa polisi kwa sasa moja kwa moja, atakayekamtwa ni mume wako, na kutokana na hali yake unaweza ukammaliza kabisa, ...’akasema.‘Sasa nifanyeje wakili wangu…?’ nikamuuliza.‘Ngoja kwanza niupitie huo mkataba wote, halafu nitakuwa na nafasi ya kusema lolote,...usijali hawo wamechukulia kienyeji sana, huwezi ukafanya hayo waliyoyafanya kirahisi hivyo, labda wawe na mtu fulani kwenye sehemu za uandikishaji wa mikataba hiyo…’akasema‘Ok…kwahiyo bado tuna nafasi ya kulimaliza hili, nataka tulimaze na ule mkataba wa awali ufanye kazi yake, sitaki utani tena..’nikasema‘Hii ni hatari, kama kuna watu wa namna hii kwenye taaluma yetu, wanatuharibia sana, ni lazima hili jambo likemewe, ngoja nirudi, nitahakikisha nalifanyia kazi..’akasema.‘Nahisi anaweza kuwa huyo wakili wa mume wangu...’nikasema.‘Wakili wa mume wako, ina maana mume wako keshatafuta wakili mwingine, kwanini...?’ akaniuliza‘Ni yule wakili Makabrasha.....’nikasema.‘Oh, balaa, huyo mtu tena…!!, nakumbuka nilishawaonya kuhusu huyo mtu, ...’akasema.‘Mume wangu sijui kaingiwa na wazimu gani, nahisi kuna tatizo kubwa kwa mume wangu, sio yeye, sio mume wangu ninayemfahamu,  sasa wewe, utarudi lini?’ nikamuuliza.‘Kiukweli sijui, maana hali ya mzazi wangu sio nzuri, na siwezi kumuacha katika hali kama hii, kama hali yake itakuwa hivi, nitachelewa sana, na ikibidi nitakuja naye huko kwa ajili ya matibabu zaidi japokuwa yeye mwenyewe kakataa, ningelishamchukua, nije naye huko, lakini hakubali, kabisa, yeye anasema anataka afie nyumbani kwake, kwahiyo kwa hivi sasa siwezi kusema lolote, ....’akasema.‘Sawa nimekuelewa,…’nikasema*************Nilimuita yule mfanyakazi wa ofisini ambaye ndiye anatunza ufunguo, nikamuhoji , Safari hii nikawa mkali, nikamuuliza anieleze ukweli, kama kweli hakuna mtu analiyewahi kuingia kwenye hiyo ofisi yangu;‘Niambie ukweli ni nani ambaye aliingia ofisini kwangu, maana nina ushahidi kuwa kuna mtu aliingia wakati mimi sipo kazini, na kuchukua vitu vyangu muhimu kwenye kabati langu?’ nikamuuliza.‘Bosi hakuna mtu aliyeingia,mimi nina uhakika, maana ufungua ninao mimi, na sijawahi kuuacha popote, kama ulivyoniagiza,....’akalalamika akionyesha wasiwasi.‘Sasa sikiliza, kama nitakuja kugundua kuwa kuna mtu aliyeweza kuingia ofisini kwangu, na wewe unafahamu ujue ndio mwisho wa ajira yako, na nitahakikisha unakwenda jela...’nikasema kwa ukali na yeye akaniangalia kwa mashaka, lakini aliendelea kukataa kuwa hakuna mtu aliyewahi kuingia, au  yeye kumruhusu mtu yoyote kuingia kama nilivyomuagizia.‘Sawa nitaiarifu polisi, na watafanya uchunguzi , na ujue wewe ndie uliyekuwa na mamlaka ya ufunguo kwahiyo wewe ndiye utakayekuwa mshukukiwa mkuu, utalala jela hadi hapo huyo mtu aliyeinga kwenye ofisi yangu na kuchukua vitu atakapopatikana..,kama sio wewe uliyefanya hivyo’nikasema.‘Bosi, mimi sijui lolote, na kama polisi watanikamata, watakuwa wakinionea bure, maana sijui, na sijawahi kumruhusu mtu kuingia ofisini kwako..nakuomba bosi, unisaidie, nasema ukweli sijawahi hata siku moja kufanya hayo .......’akasema kwa uchungu, huku akipiga magoti, kitu nisichokipenda mtu kunifanyia hivyo, mimi ikabidi nimwamini tu, ila nikamwambia kuwa nifanya uchunguzi kama nitagundua kuwa anafahamu sitakuwa na msamaha na yeye.Akilini mwangu nilijiuliza maswali mengi ni nani huyo angeliweza kuingia ofisini kwangu na kujua wapi nimeweka vitu vyangu vya siri, na kuweka kila kitu, kama kilivyokuwa na aliingia muda gani maana kama aliingia kwa uficho, basi itakuwa ni usiku , na kama ni usiku, walinzi walikuwa wapi. Hapo nikaona niwahoji walinzi.Niliwaendea walinzi na kuwahoji, na wote walikana kabisa kuwa hakuna mtu angeweza kuingia usiku bila ya wao kumuona,wakasema kama ni mtu kuingia huko ofisi, basi itakuwa imefanyika hivyo mchana sio usiku....nikajikuta nikikosa ushahidi wa kuwabana hawa walinzi, lakini nilihisi kwa vyovyote vile ni lazima kuna mtu wa ndani anayehusika,hakuna mtu angeliweza kuingia hadi ofisini kwangu, kama sio mtu anayenifahamu, na kufahamu taratibu zangu.Sikutaka kuwahoji wale wote ninaowahisi, kama katibu muhutasi wangu, ambaye sizani kama angelifanya hivyo,...niliona hilo swala niende nalo kimiya kimiya, na ikibidi nitatafuta mpelelezi wa kujitegemea.Nilimpigia jamaa yangu wa mambo ya komputa, nikamuomba aniwekee vifaa vya kunasa matukioa ili kama huyo mtu ataingia tena aweze kuonekana, japokuwa nilikuwa na uhakika kuwa huyo mtu hakuwa na sababu ya kuingia tena kwani walichokitaka wamekipaa, sasa ataingia ofisi kwangu kufanya nini....Hapo ndio nikamkumbuka rafiki yangu , msomi, aliyerejea kutoka nje, huyu ndiye alikuwa akinisaidia sana kwenye mambo kama haya, alikuwa hodari wa kufuatilia jambo hadi kulitatua, kiukweli ni mtaalamu, lakini kwa hili, siwezi kumtumia yeye tena.Basi hapo hapo nikaingiwa na hamasa ya kuongea naye, nikapiga simu, ikawa haipatikani, nikampigia docta, na docta akanipatia namba yake mpya, kumbe ile ya zamani haitumii tenaNilipopiga hiyo namba mpya mara moja akapokea simu, na sikutaka kumuuliza maswali mengi kwenye simu, nikamwambia‘Nilikuwa na maongezi na wewe, tunaweza kukutana wapi?’ nikamuuliza.‘Hata mimi nimekuwa nikikutafuta sana, ...kuna mambo nilitaka kukuweka wazi, kuhusu ile kazi uliyonipa kabla sijaenda kusoma,...na nimejitahidi ili tuonane, lakini imekuwa vigumu kukupata, ....’akasema.‘Kwanini ishindikane, kwangu hukufahamu ofisini kwangu au nyumbani kwangu…?’ nikamuuliza.‘Nilifanya hivyo, lakini ni kama vile imepangwa tusionane, maana nilifika kwako kwa mara ya kwanza nikaambiwa haupo, mara ya pili nikaambiwa umekwenda hospitalini niliwafuata huko, na bahati mbaya nilipofika nikaambiwa umetoka muda huo huo,…’akasema‘Ok, kwahiyo, tukutane wapi…?’ nikamuuliza.‘Kwa hivi sasa nipo uwanja wa ndege kwa jamaa yangu, maana natarajia kuondoka leo usiku, nikaona nije kulala huku kwake, ili iwe rahisi kuwahi kuondoka , ninaondoka leo usiku, na ndege ya usiku kurudi masomoni...’akasema na kuniacha hoi.‘Ina maana ulikuja mara moja tu, ,..?’ nikauliza.‘Ndio nilikuja mara moja, kwa dharura,....’akasema.‘Dharura gani?’ nikauliza.‘Kuna mkataba nilihitajika kuja kuweka sahihi yangu, ni muhimu sana kwa ajili yangu na  mtoto na mambo mengine yalikuja kujitokeza hata sikuwa nimepangilia hivyo, lakini tumeyamaliza salama..’akasema‘Huo mkataba, ni mkataba gani huo, mpaka urudi kwanini usingelianiambia mimi nikaukamilisha, unajua mimi niye mdhamini wako kwenye masomo huko Ulaya?’ nikauliza nikihisi kichwa kikizunguka.‘Ni mambo yangu binafsi, siwezi kukuambia..na kutokana na vikwazo mbali mbali nimeondoa udhamini wako, nimemuweka mtu mwingine, nimeona nisiendelee kukutia gharama wakati wewe  upo kwenye matatizo, na awali nilipata vistisho vingi, nikajua ni wewe, kumbe sio wewe...’akasema.‘Unasema nini, na kwanini hujaniambia hilo…?’ nikauliza kwa ukali.‘Samahani, kiukweli nikiwa huko nilijaribu sana kuwasiliana na wewe lakini haikuwa rahis, na hata nilipofika, imekuwa ni hivyo, kila ninavyopanga tuonane, sikupati, nikifika nyumbani, umetoka..na nilikuwa na mambo mengi ya kufuatilia, kwahiyo nikashindwa kujigawa, si unajua tena….’akasema ‘Na mtoto wako yupo wapi?’ nikamuuliza.‘Natarajia kuletewa leo......’akasema‘Sijakuelewa, kwanini unasema unatarajia kuletewa leo, kwani alikuwa wapi?’ nikamuuliza.‘Kuna mambo mengine siwezi kukuambia, ni ..aah, unajua kuna watu wananichezea akili yangu, na imebidi nifanye wanavyotaka wao, kwa ajili ya usalama wa mtoto wangu, sijui walijuaje kuwa nimerudi kwa dharura, na wakatumia mwanya huo kunifanyia waliyonifanyia,….’akasema‘Walikufanyia nini…?’ nikauliza‘Waliniibia mtoto,…’akasema‘Walikuibia mtoto kwa vipi,na kwanini…?’ nikauliza‘Ndio maana nasema, sitak kukuambia haya, yatakuchanganya bure, ngoja nimalizane nao, nione hatima yake ni nini, lakini bado sijakubali, muhimu kwa sasa ni usalama wa mtoto wangu…’akasema‘Kwa hapo ni lazima unielezee, kwanini, …unajua nasita kwenda polisi kwasababu yako wewe na mume wangu..’nikasema‘Polisi kwa kosa gani..?’ akauliza‘Niambie kwanza ni nao hao walimuiba mtoto na kwa minajili gani, na kwanini hujaenda polisi..?’ nikauliza‘Kiukweli mpaka sasa sijaelewa..ila leo ndio wananirejeshea mtoto wangu baada ya kufanya hayo waliyoyataka wao, na sikuweza kwenda polisi kwa usalama wa mtoto wangu ila baada ya hapa, nitajua la kufanya…’akasema‘Wao walitaka nini kwako..?’ nikamuuliza‘Siwezi kukuambia mpaka nimpate mtoto wangu, nielewe hivyo tu, kwani hata sasa wananifuatilia kuhakikisha sifanyi kitu kinyume na makubaliano yetu....’akasema‘Hivi mbona siku hizi unanichanganya, na hata hilo la hatari hivyo hutaki kuniambia, kwahiyo mtoto wako yupo wapi…?’ nikamuuliza‘Wanasema yupo salama watanikabidhi leo,…’akasema‘Unajua wewe..ra-rafiki yangu, ..ooh, hata kukuita rafiki tena  nasikia vibaya, maana hilo neno rafiki nahsi kwako halina ukweli tena,…hii sasa naona ni hadithi ya kutunga sikuamini tena, hebu niambie kuna nini kinachoendelea kati yako wewe na mume wangu..?’ nikamuuliza‘Mimi na mume wako, ..una maana gani, …hapo mimi sijakuelewa…’akasema‘Usinichezee akili yangu….upo uwanja wa ndege sehemu gani, ni kule kule kwa shangazi yako…?’ nikauliza‘Ndio ni kule kule…ina maana unakuja huku..?’ akauliza‘Sasa ulitaka nifanye nini….ila kuna foleni sana…nikiona vipi nitarudi zangu…’nikasema‘Mhh..tafadhali usije kuniharibia, nikamkosa mtoto wangu…’akasema‘Unajua ulipoamuakia wewe ndio mimi nilikuwa nalala siku nyingi…najua kila kitu kwa sasa, mchezo mliocheza wewe na mume wangu…’nikasema‘Mchezo gani ?…tafadhali usinichanganye, mimi hapa nipo na mashaka na mtoto wangu, wewe ni mzazi hebu jiweke kwenye nafasi yangu uhisi ungelijisikiaje kama tukio kama hili lingekukuta wewe.., yaani hapa mpaka nimpate mtoto wangu ndio nitakuwa na amani…’akasema‘Mtoto wako aliibiwa wapi..?’ nikauliza ‘Nilipofika tu pale nilipofikia, wakati nipo bafuni naoga, niliporudi chumbani kwangu nikakuta mtoto hayupo, nilichanganyikiwa, maana kwa muda huo nilikuwa peke yangu na mwenyeji wangu alikuwa hayupo…lakini kabla sijafanya kitu nikapigiwa simu, kuwa kama namtaka mtoto wangu hai basi nifanye wanavyotaka wao, nikawaulize nifanye nini......’akatulia.‘Ehe…’nikasema‘Kuna mambo mengi walitaka niwafanyie, sitaweza kukuambia yote kwa sasa, ila moja wapo ikawa kuweka sahihi kwenye karatsi walizoniletea ilikuwa mfano wa mikataba na sikutakiwa kusoma ndani ...’akasema.‘Mkataba gani huo, na una nini ndani yake, utaweka sahihi tu bila kujua kilichoandikwa…?’ nikamuuliza.‘Sikupewa nafsi ya kuusoma huo mkataba wote…, kwani ulikuwa na mambo mengi sana, alichoniambia, ni kuwa hayo yanafanyika kwa ajili ya maisha ya baadae ya huyo mtoto..’akasema‘Kwa maana hiyo huyo, kama walifanya hivyo kwa ajili ya mtoto, ina maana huyo aliyefany ahivyo ni baba wa huyo mtoto au..?’nikauliza‘Mimi sijui, mtoto wangu hana baba, ..’akasema‘Hana baba ulizaa na mti..’nikasema kwa hasira.‘Nikuambie kitu nikiwa huko collage…, kuna watu walikuwa wakinifuatilia, na nikaja kugundua kuwa huyo mtu anadai mimi nimezaa naye..anadai hivyo, na mimi najaribu kulificha hilo, keshagundua kuwa huyo ni mtoto wake, anavyosema yeye…’akasema‘Lakini wewe siunafahamu umezaa na nani, au sio…au wewe hukui, kwani wewe ulitembea na wanaume wangapi..?’ nikamuuliza‘Kuna mambo mengi ni siri yangu, lakini baada ya yale maongezi yangu ya mimi na wewe ..unakumbuka , ukanishauri kuwa nikaze na mwanaume yoyote, ilimradi nimpate mtoto, kiukweli,…sikutembea na mwanaume mmoja, hilo nilikuficha , nilitembea na zaidi ya mwanaume mmoja…’akasema‘Malaya mkubwa wewe…’nikajikuta nimesema hivyo‘Ahsante…’akasema hivyo'Hivi ni wewe yule rafiki yangu ninayekufahamu kweli…’nikasema‘Nisamehe tu, kiukweli…mambo ni mengi, mitihani ni mingi imenikuta,…sijui niliingiwa na nini… ila kwa hili nimejifunza sana, kuwa kuanzia sasa nisimame kwa miguu yangu mwenyewe maana kila kitu kina gharama yake…ipo siku nitakuhadithia kila kitu, ila kwa leo, niache tu, maana sina amani hapa nilipo…’akasema‘Je huyo mtu aliyekufanyia hivyo sio mume wangu…?’ nikamuuliza‘Kunifanyia nini?..kumchukua mtoto?, hapana, sio mume wako, ..mume wako si mgonjwa, ..si anaumwa jamani, siwezi kumsingizia, kwasababu hata mimi niliwazia hivyo awali kwa haraka.., ndio maana nilikwenda hadi huko hospitalini nikiwa namshuku mumeo, lakini sio yeye, …’akasema‘Kwanini ulimshuku mume wangu si kwa vile ulitembea naye, au…?’ nikamuuliza‘Mimi sijatembea naye….kwanini nitembee naye….hilo usimsingizie mume wako, mtakosana naye bura…’akasema‘Ulipofika hospitalini, uliongea na mume wangu..?’ nikamuuliza‘Ndio niliongea naye, lakini hakuwa vizuri,…naona kama ana matatizo, ..hana amani, sikutaka kumchanganya zaidi, nikamdanganya kuwa mtoto nimemuacha nyumbani…’akasema‘Kwani alikuuliza kuhusu mtoto..?’ nikauliza‘Ndio, ilikuwa cha kwanza, alifurahi sana kuniona, unajua shemeji ananijali sana…’akasema‘Ni kwa vile mume zaa naye au sio..?’ nikauliza‘Wewe…unasema nini bo-si, …ndio unanifikiria mimi hivyo rafiki yangu, ..hapo umevuka mipaka, na ulikirudia kauli kama hizi mimi nitakata simu samahani…’akasema‘Nataka ukweli kutoka kwako,….je umewahi kutembea na mume wangu…?’ nikamuuliza kwa sauti ya kibosi, kuwa sitaki utani‘Samahani, nasikia watu wanakuja…’akasema, lakin hakukata simuNikasikia watu wakiongea na huyo rafiki yangu alikuwa hajakata simu, labda ni ili nisikie wanachoongea na hao watu.. .Nikasikia, wakiongea lakini maneno siyanakili vyema masikioni, baadae nikasikia kama mtu anasema‘Mtoto wangu yupo wapi…’ilikuwa ni sauti ya rafiki yangu huyo.‘Mtoto yupo tumekuja naye..’sauti ya kiume ikasema‘Nipeni sasa mtoto wangu, nimefanya kila mlichotaka, …mnataka nini tena..’akalalamika rafiki‘Kuna kitu bado, kuna hizi nyaraka tumeambiwa uweke sahihi yako…’wakasema'Mimi sina ugumu wa kuweka sahihi, lakini kwanza nimuone mtoto wangu…’akasema rafiki yangu,‘Mtoto wako huyu hapa…’sauti ikasema na mara mtoto akaanza kulia, na rafiki akawa anaomba amchukue lakini wao wakasema sahihi kwanza‘Huwezu kumchukua mpaka uweke sahihihi hapa, unasikia…’akaambiwaBaadaye kukawa na ukimia,‘Haya nipeni mtoto wangu…nimeshaweka hiyo sahihi,…na, hapa pia sawa, mii sijui inahusu nini, ila…nawaonya hili mtakuja kulijutia..’akasema rafiki yangu, na mara kukawa na kilo cha mtoto, na baadae hao watu wakasema‘Sasa ulikuwa unaleta ubishi wa nini, haya yote ni kwa masilahi ya mtoto wako, bosi wetu kafanya hivyo, kwa vile anataka mtoto atabulike ni wake kisheria, …maana ni damu yake..keshathibitisha hilo…na kafurahi kweli hasa kwa vile ni mtoto wa kiume ‘akasema.‘Si akazae na mke wake…’sauti rafiki yake ikasema.‘Hayo mengine.. muhimu tumemalizana…’sauti ikasema‘Sawa tumemalizana, naomba muondoke hapa…’akasema rafiki yangu‘Sawa tunakutakia safari njema ila ukumbuke kuwasiliana na baba wa mtoto wako,ila kakutahadharisha, ukianza mambo ya sijui polis, utajitaharibia kila kitu..na hii iwe ni siri yako umeelewa shauri lako,,…’sauti zikasema na rafiki yangu hakujibu kitu.Baada ya muda simu ikakatika, na mimi nikaamua kumpigia simu huyo rafiki yangu, kwanza hakupokea, baadae yeye ndio akapiga simu.‘Haya niambie kinachoendelea…?’ nikauliza‘Wamemleta mtoto wangu, yupo salama…’akasema‘Kuna nini kinachoendelea, naona kama ni mchezo wa kuigiza, unataka nini  ..wewe na huyo mwenzako..?’ nikauliza‘Mwenzangu yupi….jamani,  naomba uniulize mambo yenye maana hapa akili yangu haipo sawa , na nipo kwenye maandalizi, kuna mambo yangu mengi yameshindikana kwa sababu ya hawa watu, kwahiyo angalau huu muda mchache niache niyamalizie, yatakayowezekana, tafadhali…’akasema**********Moyoni nilihisi huyu rafiki yangu ananidanganya kitu, huenda hayo yote aliyonieleza ni hadithi ya kutunga, lakini …yawezekana ikawa ni kweli pia, labda rafiki yangu yupo matatani, na mimi ndiye mtu ninayeweza kumsaidia, nikataka nipige simu kwa watu wangu ili waweze kulifuatilia hilo jambo, na wakati nawaza hilo  mara simu yangu ikaita,...nilipoangalia ni nani anayenipigia nikagundua kuwa ni docta rafiki wa mume wangu;'Upo wapi wewe, nakutafuta sana.....'akasema.'Unanitafutia nini..mbona simu yangu ipo hewani wakati wote?' nikamuuliza kwa sauti ya  kama mtu anayekerekwa, kiukweli sikuwa na amani na kila anayenipigia naona kama anazidi kunichanganya tu'Kuna mambo muhimu sana, nataka kuongea na wewe....'akasema kwa sauti ya kikazi zaidi‘Mambo gani?’ nikamuuliza kwa mkato, kwani kwa sauti hiyo inaonyesha kuna jambo.‘Kuhusu huyo wakili wa mume wako.....’akasema‘Wakili wa mume wangu, huyo tapeli, ana nini huyo wakili..hebu ongea moja kwa moja..kuna tatizo, au kuna jambo?’ nikauliza‘Huyu mtu ni hatari sana, kama tusipofanya haraka, utakuja kujijutia..’akasema‘Ulishaniambia hilo, au kuna jingine..’nikasema‘Ndio kuna jingine mimi…, nimegundua mambo mengi sana juu yake, na sipendi niyaongelee hapa kwenye simu, tuonane sehemu tuongee tuone tutafanya nini, ni muhimu sana, kabla hujachelewa...’akasema na sauti yake ilinitia mashaka, inaonyesha msisitizo ...’nikasema;‘Nitakuja nyumbani kwako....’nikasema.‘Hapana, usije nyumbani kwangu, … njoo ofisini kwangu....’akasema‘Sawa vyovyote utakavyo, nipo njiani, nakuja....’nikasema na kugeuza gari na kurudi nilipotoka, foleni ya kwenda uwanja wa ndege ilikua haiende kabisa, hapo sikujali tena mambo ya rafiki yangu.NB: Sehemu hii iliishia hivyoWAZO LA HEKIMA:Usalama wa majumbani kwetu, usalama wa watoto wetu, au usalama wa maofisini, ni muhimu sana, na ni vyema, vitu kama ufunguo, ulinzi, na usafi, vikapewa kwa watu wanaoaminika, kwa mkataba maalumu. Tatizo kubwa lililopo, ni kuwa watu hawo hawalipwi vizuri, na kutokana na hali ngumu za kimaisha, ni rahisi kwao kushawishiwa na kurubuniwa kwa pesa ndogo tu. Cha muhimu ni kuwajali sana hao watu, na kuwatimizia mahitaji yao muhimu, ili waione hiyo kazi kama yao.'Kuna mambo muhimu sana, nataka kuongea na wewe....'‘Kuhusu huyo wakili wa mume wako.....’‘Huyu mtu ni hatari sana, kama tusipofanya haraka, utakuja kujijutia..’‘Ndio kuna jingine mimi…, nimegundua mambo mengi sana juu yake, na sipendi niyaongelee hapa kwenye simu, tuonane sehemu tuongee tuone tutafanya nini, ni muhimu sana, kabla hujachelewa...’Kisa kinaendelea....************Ilikuwa siku ya aina yake, maana foleni likuwa kila mahali, sikuweza kufika uwanja wa ndege, na sasa nimeamua kurudi ili nionane na huyo rafiki wa mume wangu, na foleni ikanifanya nichelewe hadi usiku ukaingia.Lakini kwasababu ya kusikia ni kitu gani alichokigundua huyo docta, ikabidi nipitie kazini kwake, kwani bado alikuwa ofisini..nikafika kwenye hospitali yake, nikasimamisha gari langu kwenye eneo la maegesho ya mgari.Hiyo ilikuwa hospitali yake ambayo anaifanyia kazi baada ya muda wa kazi, kuanzia saa kumi na mbili mpaka saa sita usiku…kwahiyo muda wote huo utakuwata wagonjwa wapo.Niliingia ndani hadi mapokezi, niliangalia mlango wa kuingia kwenye ofisi ya huyo docta, nikawaona wapo wagonjwa wawili tu  wanasubiria kuonana naye. Nikaona nisubiria waishe hao wagonjwa, lakini walipoisha hao wakaongezeka wengine…Nilitaka nimpigie simu kumuelezea kuwa nimeshafika, lakini nikaona nimpe muda, maana nitawadhulumu hao watu wenye shida ya kutibiwa, wao ni waginjwa wamefika kutibiwa, na mimi siumwi, japokuwa nina mambo muhimu na huyo docta, ....Na niwakati natafakari hayo, mara mlango wa ile ofisi yake ukafunguliwa, na yeye akatoka, na kuangalia sehemu mapokezi, ambapo, nilikuwa bado nimesimama, inaonyesha alikuwa keshajua kuwa nimeshafika. Akanionyeshea ishara ya tano, nikafahamu kuwa ananiambia nimpe dakika tano, na mimi nikatikisa kichwa kumkubalia,...Nikasogea sehemu ya kupumzikia wageni, kuna masofa, nikachagua sehemu ya kukaa, ili niwe naone kule kwenye ofisi ya huyo mwenyeji wangu,nikawa naangalia runinga. Na baada ya dakika tano, nilimuona akitoka tena, na safari hii, alionekana akimuita mtu, nahisi alikuwa akimuita msaidizi wake, na huyo aliyeitwa alipofika,wakaongea naye kidogo.Walipomaliza kuongea, nikamuona akija sehemu hiyo niliyokuwa nimekaa, na aliponikaribia, akanionyeshea ishara kwa mkono kuwa twende sehemu ambayo alihitajia tukaongee, ni kwenye chumba kingine.‘Kwanini usingemalizana na mgonjwa wako kwanza...naona kuna watu wawili tu pale wamebakia, ila kila wakiisha wawili wanakuja wengine, pole na majukumu, hivi unapumzika saa ngapi..?’ nikamuuliza.‘Wale sio wagonjwa, wale ni vijana wangu wamekuja kunipa taarifa mbalimbali, hawana haraka, wanaweza kunisubiria tu..’akasema,‘Vijana wako, wewe unafanya kazi ngapi…?’ nikamuuliza‘Hahaha, ushaanza kunichimba, ..unakumbuka nilikuambia wakati nasoma nilipendelea sana kuwa mpelelezi, lakini udakitari ukazidi nguvu ile ndoto yangu y utotoni, kwahiyo chini kwa chini nimekuwa nikijifunza mwenyewe mambo ya upelelezi kupitia mitandao kwa kujifurahisha tu…’akasema akitabasamu‘Ili uwachunguze watu, na ndoa zao au…’nikasema‘Ikibidi kwa watu ninaowajali kama nyie..kama wewe…’akasema akinipiga piga mgongoni, nikawa nauzuia mkono wake.Tukafika kwenye hicho chumba, na tulipoingia, akasimama kidogo, kama vile ananipisha, lakini, nikamuona akinisogelea, kama anataka kunikumbatia, na mimi nikamsukuma;‘Jiheshimu, kumbuka nafasi yako na yangu pia....’nikasema.‘Samahani, unajua tena, kuna mda nashindwa kujizuia,…hahaha, nisamehe tu mwenzako, nisije kuongeza madhara, maana siku hizi tuwe makini sana…hata hivyo nilitaka kukusalimia, ....kwani kusalimia kwa kukumbatiana kuna nia mbaya,....usiwe mshamba bwana....’akasema.‘Sawa acha niwe mshamba, lakini nafahami ni kitu gani ninachokifanya, naheshimu ndoa yangu na wewe fanya hivyo hivyo...’nikasema.‘Ni kweli samahani….’akasema huku sasa akiwa mbali na mimi. Tukaingia ndani, akanisogeza kiti, ili mimi nikae, na nilipokaa, yeye akatembea hadi  kwenye kiti kikubwa, ilikuwa ofisi yake, maalumu, kulikuwa na kila kitu muhimu cha ofisi, alipokaa akaniangalia moja kwa moja usoni, hapo tulitengenishwa na meza. Mimi sikujali huku kuniangalia kwake, nikatulia kama vile mgonjwa anavyosubiria kuhudumiwa na dakitari.Nilisubiri kidogo, kumuachia nafasi hiyo ya kuniangalia, maana sijui alikuwa na maana gani, au ndio hulka hizo za wanaume…kwani alivyokuwa akifanya ni kama mtu anayemwangalia mpenzi wake, na hali kama hiyo sikuipenda, lakini kwa vile nilishamfahamu tabia yake, sikujali, ...nikatulia kimiya, na aliponiona nipo kimiya sicheki nimeangalia mbele, akasema;‘Nimekuita hapa sio kama mgonjwa, na sio kama nimekuitia hapa kwa maswala ya masihara, ya uchumba wetu wa zilipendwa, ila siwezi kuficha nakupenda sana, japokuwa siwezi kufanya lolote kwa sasa….hahaha, usijali,…hayo tuyaache mimi nimekuita hapa kwa jambo muhimu sana zaidi ya hilo..’akasema.‘Mhh,...niambie, najua usingelipoteza muda wako kuniita..’ nikasema;‘Kutokana na vyanzo vyangu vya habari, unafahamu ukiwa katika hali kama hii yetu ya kujiajiri, hasa ukawa na miradi yenye wateja wengi , na maadui wengi kibiashara, ni lazima pia uwe na vyanzo vyako vya kukupatia taarifa muhimu, naomba unielewe hivyo tu, mimi siwezi kukuficha kuwa nasubiria tu wateja, wakati mwingine inabidi uhangaike kama hivyo, kujua wenzako wanavyofanya..’akasema‘Sawa nakuelewa, kila mtu anafanya hivyo, kwa masilahi ya biashara yake…’nikasema‘Sawa kabisa, tuachane na mimi,..nataka kuongelea kuhusu wewe…’akasema‘Nimefanya nini tena…’nikasema‘Ni hivi, usione kama ni kwanini, kiukweli, sio siri nimekuwa nikifuatilia ndoa yenu hatua kwa hatua, sio kwa nia mbaya, bali kwa ajili ya kukulinda wewe, hujui tu..hili nimeshakuambia mara nyingi, …’akasema‘Pole sana…’nikasema‘Sasa… siku ile nilipoona mume wako yupo na huyo wakili, nikaingiwa na mashaka, sio kwa vile sikuamini wewe…lakini huyu mtu,…nimeshasikia tetesi zake na sikutarajia kuwa atakuja kuingia kwenye anga zangu….’akasema‘Ndio hajaingilia biashara zangu au maisha yangu, lakini yule anayekugusa wewe kanigusa mimi..sisemi kinafiki, ila kutoka moyoni, na wazazi wako wanalifahamu hilo, kuwa  mimi ndiye mlinzi wako,..tuliache hilo hivyo.Mimi huyo mtu, nimesikia sifa zake nyingi,..mbaya na nzuri, mimi awali sikulichukulia hilo maanani, kwasababu sikuwa na sababu yoyote na mtu huyo...kabisa kabisa….’akasema.‘Sawa ..naogopa kukatali, lakini naomba yasiwe ya kujirudia rudia endelea...’nikasema.‘Nafahamu una kazi nyingi sana, nafahamu angelikuwepo yule rafiki yako yupo hili  ungelimtumia yeye, na mimi nisngelikuwa na nafasi hii tena, kwa vile hayupo basi mimi  nikaona nikusaidie kwa hili, na kwa vile rafiki sasa kakugeuka, hilo utakuja kuligundua mwenyewe baadae , sio sasa, sasa hivi nataka kukuweka wazi ni kwanini nimekuwa nikikufuatilia hivyo…’akasema na mimi hapo sikusema kitu.‘Pole sana na foleni, ya kutoka uwanja wa ndege, natumai ulikwenda kuonana na rafiki yako, na nashukuru hukuweza kuonana naye , vinginevyo mtego uliotayarishwa, ungekunasa, na sijui ni nini kingelitokea baada ya hapo..’akasema.‘Umefahamu vipi kuwa nilikwenda huko kumfuatilia huyo rafiki yangu, mbona unapenda kunifuatilia sana nyendo zangu, unanitafutia nini wewe ?’ nikamuuliza.‘Nimeshakuamba kuwa mimi nina vyanzo vyangu vya kunipatia taarifa kama nina umuhimu na jambo fulani, na kufuatilia nyendo zako ni kwa ajili ya kuhakikishia usalama wako, na nitahakikisha nafanya hivyo,utake usitake, kwani niliahidi mbele ya wazazi wako, na kwako pia, kuwa nitafanya hivyo, ...’akasema‘Yatakushinda,  wewe niambie ulichoniitia masaa yamekwenda sana , unajua nimechelewa kufika nyumbani, kama mume wangu angelikuwepo nyumbani, ningekuwa na kesi ya kujibu…lakini hata kama hayupo nyumbani isiwe ndio ababu ya kuvunja miiko ya ndoa, sitakiwi nifanye mambo ya kunivunjia heshima yangu, unanielewa hapo…’nikasema huku nikiangalia saa yangu.‘Ni kweli kabisa kwa hilo mimi nakuvulia kofia, …sina shaka na wewe.., hata mimi sijafanya hivi kwa nia mbaya, hili ni muhimu sana..’akasema na kukaa vyema, halafu akaniangalia tena machoni, na kusema;‘Haya nitakayokuambia sasa hivi, ni muhimu kuliko hayo unayoyafuatulia wewe…nakuomba unielewe hivyo’akasema‘Sawa , mima nakupa robo saa, nakusikiliza, baada y ahapo naondoka zangu…’nikasema‘Kuna mambo bado hayajathibitishwa, ila ya kikamilika, nitakuambia ila kwasasa nataka kukuelezea jambo kubwa tuliloligundua....kwa kukutahadharisha, na kukuomba usifanye hayo uliyoyakusudia kuyafanya hadi hapo utakapoambiwa, kwa manufaa yako na ya watu wengine wanaokujali...’akasema, na mimi nikatulia kusikiliza.Akaangalia saa yake halafu akasema‘Robo saa sio, inatosha kabisa baada ya hapo utakuwa huru kuondoka, naahidi hivyo…’akasema akiandika kwenye karatasi yake.‘Mhh..haya, yaseme…’nikasema nikiona kama ananipotezea muda, kiukweli pale nilipo bado nilikuwa namuwazia huyo rafiki yangu je kumeendelea nini huko, isije ikawa yupo matatani..sikufikiria ubaya wake zaidi..niliwazia ubinadamu, hasa mtoto wake.‘Mpendwa, sio kwamba nakulaumu, na mimi kama walivyo wazazi wako, tulishakuambia kuhusu mume wako, kwani tabia za watu za asili, kizalia, huwa hazibadiliki sana, labda mtu mwenyewe aamue kiukweli kufanya hivyo, ila akipata mwanya, kurudia asili yake haichelewi, mtu habadili kwa hivyo kama mwenyewe hatataka kujibadili...’akasema.Mimi nikakaa kimia, najua huyu ni mtu wa wazazi wangu, nilishamzoea,…‘Na nafahamu hali uliyo nayo kwa sasa, kwani mume unampenda sana hata pamoja na hayo yaliyotokea...lakini huko kunapoelekea, itabidi ufikirie hilo mara mbili, sio kwamba nakushauri uachane naye, hapana,..hautakiwi kufanya hivyo, …hata wazazi wako hwataki ufanye hivyo…’akatulia kidogo‘Ni kweli wazazi wako wamelifikiria sana hilo ya kuwa, mna watoto, nakadhalika… sio vyema mkaachana, lakini sasa mtaishije kwa hali kama hiyo, hilo ni lenu wawili,..muhimu uishi naye ukiwa na tahadhari tofauti na awali, sasa kwa hayo waliyopanga, itakuwaje, ni kazi ambayo inafanyiwa kazi,..‘Kwangu mimi kwa hivi sasa nataka kukuelezea yale tuliyoyagundua ambayo, yatakushtua,..maana hata mimi sikuamini, lakini ukweli ni ukweli tu, na ukweli huo hatutaweza kuupata zaidi , ikiwa wewe utachukulia jazba, nafahamu itafikia sehemu utasema basi liwalo na liwe, hapana, kwa vita hivi, bado tunahitajia uvumiliv wako....’akasema.‘Kwanini unazunguka, unanipotezea muda, na kuniweka roho juu, niambie ulichoniitia, nina mambo mengi ya kufanya…’ nikasema kwa hasira.‘Huo ni utangulizi mpendwa, nilazima nikuambie hayo kama ilivyotakiwa nikuambie.....’akasema‘Ulivyoambiwa na nani, na wazazi wangu au…?’ nikauliza‘Kwanza ni kuhusu huyo wakili wa mume wako, anayejiita wakili wa kujitegemea, ni kweli kitaaluma ni wakili..na sio kwamba hana fani hiyo, anayo na kaisomea kweli, vyeti anavyo na kazi pia anaifahamu, akisimama mahakamani sio mchezo,  ila yeye n ndumilakuwili,…na tabia isiyopendezahula na tabia yake ndivyo vinamkosoa...’akasema Nilitaka kumuambia hayo nayafahamu lakini nikaa kimia ili nimsikilize zaidi, huenda kuna kitu cha zaidi sikifahamu‘Sasa huyo anataka kuwatumia marafiki zako,…bila ya wao kujua, kuhakikisha anakamilisha lengo lake , akiwemo huyo mume wako…huyu jamaa ni mjanja kweli kweli ..na hutaamini keshafanikiwa…’akasema‘Marafiki zangu..!!’nikasema kwa mshangao.‘Ndio…marafiki zako wameshatekwa kimawazo, na kwa jinsi ilivyofanyika, hawana ujanja, na kiukweli huenda hata wao hawafahamu ni kwanini, wameingizwa huko, ni ujanja wa hali ya juu,….na usione mengine yanatokea ukaona ni bahati mbaya, ni mpango wenye masihali fulani ya kisiasa…’akasema‘Mhh..sasa ni siasa, awali ilikuwa ni maswal ya kindoa, mimi simjali mume wangu, ikaja …mume huenda kasalitio ndoa, sasa imekuwa ni mambo ya kisiasa, kweli mnahangaika sana, nikuambie kitu, hili hebu niechieni mwenyewe, nafahamu sana, kuwa wazazi wangu wananijali, lakini nimeshakuwa mtu mnzima, najua kujitetea, kwanini niendelee kuwatesa wazazi wangu, waacheni wapumzike, nitapambana kivyangu…’nikasema‘Mtoto hakuwi mbele ya wazazi wake, ilimradi wapo hai, hata kama ni vikongwe, unasikia, msidharau wazazi wenu hata siku moja…pamoja na yote unayofanya, usifikirie kuwa utakuja kuwazidi wazazi wako, ….kumbuka wao wamepitia mengi, na utu uzima wao ni dawa..wao wana hekima ambayo hujaipata…mungu huwapa watu wazima maono ambayo wewe huwezi kuyafahamu…’akasema‘Sikatai, hilo siwezi kupinga lakini pia wanahitajika kumpumzika, niwasaidie na mimi, nitawasaidia lini, eeh…’nikasema.‘Haya ninayokuambia sio kwamba naongea tu,… ni kitu kilichofanyiwa uchunguzi na nina ushahidi wa kikao hicho kilichofanywa na maadui zenu…, ukitaka nitakupatia…ni hujuma zimepangwa kisayansi ya kisiasa…, na ni kweli zilianzia ndani ya familia yako, na sasa zimekwenda zaidi ya hapo, siasa imeshaingizwa..’akasema‘Mimi sio mwanasiasa na sitarajii kuingia huko, sipendi siasa kabisa…’nikasema‘Lakini baba yako ni mwanasiasa, kajiingiza huko pamoja na shughuli zake,  je humjali…?’akasema kuniuliza‘Hayo ni maisha yake, mimi sipo huko ndio maana nikajitenga naye, na nimekuwa mbali naye, na nilishamuambia, sitaki tuingiliane, ili nisije kumuharibia mambo yake…’nikamwambia docta‘Sikiliza, kwenye uwanja wa siasa, kila kitu ni silaha kwa adui yako, …na wengi wanakimbilia kuangalia familia zinavyoishi hilo kwa upande mmoja japokuwa huku kwetu Afrika sio sana, lakini zaidi ni vitega uchumi, mali nak, je havina mkono wa pesa chafu, je hakuna ukikuwaji wa maadili, kwenye zabuni nk, rushwa na vitu kama hivyo…’akasema‘Najitahidi sana kukwepa hayo…nikasema‘Baba yako alijitahidi sana kuwasaidia, na alijitahidi sana kuona kuwa nyie mnaendesha biashara kimaadili, sasa huo msaada unafuatiliwa, ulitokaje, na je huko unapokwenda, umefanyia nini,…unaona mtego uliopo hapo, msaada unageuka kuwa mtihani…’akasema‘Ni kweli , mimi sijavunja miiko ya biashara, nafuata sheria, kwahiyo baba hastahiki kuogopa kwa hilo, sijafanyia vibaya mtaji alionipa kwenye biashara zangu, kama kuna ubaya, niambieni…’nikasema‘Je mume wako anafanya hivyo..anafuta sheria, analipa kodi, anafanya biashara halali kwenye zabuni na serikali, je, matumizi yake, je..hajafanya mambo yasiyo mema kwenye jamii, kimaadili..nyie wote mnamulikwa kihivyo..?’ akaniuliza‘Mimi sijui…’nikasema‘Wewe hujui lakini maadui wa siasa wanilijua hilo, hebu nikuulize kwa hivi sasa mume wako ikatokea tatizo kwake, wewe utaziba masikio yako kuwa hayakuhusu, angalia huo ugonjwa wake, umefanya nini, ulilala kitandani…chukulia kafanya madhambi, unafikiri jamii itasemaje, hasa maadui wa kimaisha, hasa katika Nyanja za kisiasa maana mabo yako ni ya kisiasa, kuongea, kutoa propaganda potofu, watasemaje hapo, je wanataja jina la baba yako au jina la baba wa mume wako…kisiasa…?’akauliza‘Ndio maana nilimuambia baba, mimi anichie maisha yangu, sikutaka kabisa yeye ajiingize kwangu, mtaji wake uwe ni mkopo kwangu nikiurejesha ajitoa kabisa na mimi, wala asitambulikane, ..lakini hajataka kunisikia..’nikasema‘Je uliwahi kurejesha huo mkopo, ..?’ akaniuliza‘Nitaurejesha, mambo hayajakaa sawa..’nikasema‘Mpaka muda huo, unafikiri mangapi yamefanyika …nakuambia haya kwa mawazo mapana,…, huyo jamaa , wakili wa mume wako, ndio jembe la mpinzani wa baba yako, unielewe hapo, yeye alipikwa akasomeshwa na mpinzani mkubwa wa baba yako kisiasa,..sasa natakiwa kulipa fadhila, ndio hayo anayafanya je anayafanya bure bure tu, kuwa anataka masilahi ya pesa tu, jiulize kwa makini, ..’akatulia‘Mimi sijui…’nikasema‘Kitu kikubwa watu walikuwa wakijiuliza bila kupata jibu ni kwanini huyu jamaa anajiamini hivyo, ni kwanini hakamatwi, na akifunguliwa mashitaka hapatikani na hatia, ni kwanini…n hebu sikia alivyokuwa akikujibu pale hospitalini ni kwanini alijiamini hivyo, jiulize hapo…’akasema‘Na wewe ni jembe la baba yangu, au…?’ nikauliza‘Usifanye utani, hili ni jambo nyeti sana, sivyo kama unavyofikiria wewe, achana na hulika yako kuwa labda nafanya haya kwa vile, …hapana hili ni jambo nyeti na ukicheza, utajiharibu wewe na familia yako yote, kuanzia kwa wazazi wako, na  utakuja kujuta wakati umeshachelewa…’akasema‘Kwa mume wangu ulisema hivyo hivyo, na huyo ni rafiki yako, sasa umemgeuka, sasa ni kwa wazazi wangu, ni nini, siasa au sio, lakini mimi zipo huko, na baba akipatwa na matatizo, wasinisingizie mimi, ..niakuambie kitu…’nikasema‘Tunamuongelea huyo jamaa, tusipoteze muda, najua umenipa dakika ngapi, au umeziongeza ….sikiliza sasa…’akasema‘Natumai huyu jamaa unamfahamu kwa juu juu tu, nitakuelezea sifa za huyu mtu, ambaye kitaaluma ni wakili wa kujitegemea, na polisi wamekuwa wakitafuta kila njia kumnasa, kutokana malalamiko ya watu wengi, waliowahi kufanyiwa utapeli na huyu mtu, akitumia mgongo wa taaluma yake hiyo, lakini kutokana na ujanja wake hajawahi kukamatwa.....’akasema.‘Unaposema huyo jamaa una maana wakili Makabrasha...?’ nikauliza.‘Nisingelipendelea kumtaja jina lake kihivyo, lakini ndio huyo,...mtu huyu ni rafiki wa mume wako toka utotoni, na tabia zao  zinafanana, japokuwa mume wako alikuja kubadilika baada ya wewe kuolewa na yeye, huo ndio ukweli,....’akatulia kidogo.‘Mume wako, alikuwa akishirikiana na huyu jamaa kabla, jamaa akitoka ulaya, rafiki yake mkubwa alikuwa mume wako…wakawa wanashikirikiana  kwenye mambo mbalimbali, ya kutafuta maisha… kipindi hicho mume wako alikuwa akihangaika tu kazi yoyote anafanya, maisha yalikuwa magumu sana kwake, kwa hiyo tunaweza tusimlaumu moja kwa moja, japo sio sababu ya kufanya mabaya kwenye jamii..’akasema....‘Mkaja kupendana,…na hatimaye kuvuruga uchumba wetu,…sio nakulaumu, ila nakuelezea hali ilivyoweza kubadilika, ni kweli ulimsaidia sana, na kweli kipindi hicho aliamua kubadilika kiukweli, lakini kunguru hafugiki.‘Watu wanasema huenda, rafiki yake huyo wakili, ndiye aliyemshauri rafiki yake afanye kila awezavyo mpaka akuoe, ili baadae iwe ni chambo, au mlango wa kuingilia, lakini sio kweli…huyu jamaa alikupenda kiukweli, ila tamaa ndio iliyomuharibu,sio tamaa tu, bali hulka ya kuzaliwa, ilikuw na nguvu zaidi…’akasema‘Una ushahidi gani..?’ nikamuuliza‘Kila kitu kipo, mpaka nimeamua kukuita hapa nimeshahakikisha kila kitu kipo kiushahidi, maana mimi nakufahamu wewe ulivyo, lakini kwa leo nitakuelezea tu, ili kwanza nitimize wajibu wangu kama mimi na pili, niwakilishe ujumbe kutoka kwa wazazi wako, japokuwa hawajanituma nikuambie hivyo…’akasema‘Endelea…’nikasema‘Ulipoolewa na huyo jamaa, rafiki yake akawa anakusoma, anawasoma kufahamu madhaifi yenu,…kwanza alitaka kumweka sawa mume wako ili apitie kwake, kwa kujifanya anamjenga ili lolote likitokea asija kuadhirika..akajaribu akashindwa, …kwasababu ulishamweka sawa mume wako…;lakini jamaa alishajua kuwa kuna muda muafaka utafika, kunguru hafugiki, unanielewa hapo …’akatuliaJamaa akaja kwa mgongo wa taaluma yake, akitaka awe wakili wenu, mume wako alimkubalia, lakini wewe ukaja kuvuruga, lakini hakukata tamaa, akawa anatafuta njia ya kuwaingilia,….. lakini kwanini afanye hivyo, jiulize ni kwanini, ni mali tu..,..au kuna nini cha kumfanya ahangaike hivyo…’akatulia‘Mali ni nyenzo mojawapo, lakini sio sababu kubwa sana, hili hata polisi walikuwa hawajaligundua wao macho na masikio yao ni kwenye mali,..rejea niliyokuambia kuwa wakili huyu alipikwa na mwanasiasa adui, mpinzani wa baba yako…ukirejea huko ndio utanielewa vyema…’akasema‘Je atawezaje kuingilia ngome iliyojengwa imara, kimaadili, kisomi, na mnajitahidi kila namna kuhakikisha kuwa hamna kashfa, …sasa nikuambie kitu baada ya kuona bado ni shida kuingilia ngoma ya baba yako zikapikwa kashfa…‘Zikapikwa kashfa kwa vipi…?’ akauliza‘Haya mambo ya dunia hii, yaone tu, usione nchi zinapigana ukafikiri ni wao tu propoganda potofu, kashfa, hujuma, jamii kuchonganishwa, bila wao kujua, wanakuja kukosana,…kashfa nyingine hutengezwa, na kwa ushahidi…, kashfa imeshaingia kwenye familia yenu, sasa ni ya kutengenezwa au ni kweli ilifanyika kiuzembe, ndio nilichokuitia hapa, ili ulifahamu hilo, kuwa sio jambo dogo kihivyo, limeshakwenda zaidi ya kifamilia, sasa chagua kuwasaidia wazazi wako, au ..…’akatulia hivyo hakumalizia, akaangalia saa ‘Kashfa gani unayozungumzia hapa, ni huyo mtoto wa rafiki yangu, si ndio hiyo, lakini nimegundua kitu...na nilikuwa nakifuatilia, huko uwanja wa ndege, ndio ukaniwahi, nina uhakika ningelilimaliza hilo, na utata wote ungeliisha…?’ nikauliza na kusema'Hahaha, hujua kuwa unajipeleka kwenye mdomo wa ..kenge,..huo ni mtego ulitayarishwa, inajualikana ulitakiwa uende huko, ukajinase...najua nia yako ni kupata damu ya huyo mtoto ukapime DNA,lakini usingeliweza kumpata...kuna mchezo ulitakiwa ufanyike, lakini sasa...'akaangalia saa yake‘Ahadi ni deni, dakika ulizonipa zimekwisha, unasemaje, tuendelee…’WAZO LA LEO: Ukisikia taarifa yoyote ifanyie kazi kwanza, hata kama unaona kuwa ni taarifa yenye masilahi kwako, usiwe na papara nayo, inaweza ikawa nzuri kumbe ndani yake kuna ubaya, kuna mitego, walimwengu sio wema…, inaweza ikawa kama asali yenye sumu ndani yake, kumbuka kuwa sio kila taarifa ina lengo jema kwako... Ipokee taarifa, ichunguze ukweli wake, na angalia athari zake, je inaweza kupokeleka, vinginevyo, ipuuze, weka subira, mola yupo pamoja nawe, na muda utasema ‘Ndio …nataka niwahi uwanja wa ndege…najua sasa hivi hakutakuwa na foleni, anaondoka saa tatu na mimi ni lazima nionane naye, sasa hivi saa ngapi…’nikasema‘Kufuata nini huko, ina maana hujanielewa nilichokuambia..?’ akauliza akiniangalia kwa uso uliotahayari.‘Pamoja na yote uliyoniambia, ni lazima nihakiki baadhi ya habari, kwanza sina uhakika kuhusu rafiki yangu, kiubinadamu natakiwa nifanye jambo, kwa vile kaniambia yupo matatani…..je kama ni kweli, unafikiri mimi nitaelewekaje, ni lazima nifanye jambo au sio..?’nikasema‘Una watu wako watume, na foleni zilivyo huwezi kufika huko kwa wakati, utakuwa unapoteza muda wako bure, na hata hivyo, kiusalama sio vyema, unanielewa hapo…?’ akasema kana ananiuliza‘Hili sio tatizo lako,  mimi ni vyanzo vyangu vya habari, naondoka, …japokuwa hujanimalizia kuhusu hiyo kashafa ni ipi hasa ambayo hata baba yangu anaogopa itamuharibia sifa yake..,?’ nikauliza‘Sikiliza,…ok, muda umekwisha, lakini kitu muhimu ni kuwa kila jambo linatumiwa kama silaha, sisi tutatumia hilo tukio kama silaha yetu, ni mambo ya kuwhiana, atakaye muwahi mwenzake atashinda, na …., kama wameamua kuwachukua watu wako wa karibu kama watu wao, tunaweza kuwatumia hao hao kama njia ya kufanikisha mambo yetu…’akasema‘Sitakuelewa…saa ngapi…?’ nikauliza‘Ngoja nikuulize kitu…’akasema‘Uliza nataka kuondoka..najua unapoteza muda, ili nisiweze kufanya kazi yangu..’nikasema‘Ni kweli, lengo moja wapo ni hilo, licha ya kuwa , nilitakiwa kukuelezea hayo niliyokuelezea, lakini pia kukutoa mbali na hatari iliyopangwa kutokea kwako, ukibisha hilo, ukifika nyumbani kwako muulize mlinzi wako, kulitokea nini..nani alikuja nyumbani, utaambiwa,…’akasema‘Unataka kusema nini, uliza mimi nataka kuondoka..?’ nikauliza‘Ni hivi kuhusu huyo wakili , unajua pamoja na kusomea uwakili jamaa huyo kasomea taaluma za nyota…kumsoma mtu, na kosomea nje, watu wanajiuliza ni kwanini alisomea mambo hayo…’akasema‘Hayo ni ya kweli jamani au mnataka kumpakazia kila ubaya…?’ nikauliza‘Hata vyeti anavyo, ndio maana nakuambia huyo mtu sio kama unavyomfikiria wewe, kuwa unaweza kumshinda kirahisi, kasomea taaluma nyingi mojawapo nyingine ni uaskari kanzu, na watu wengine wanamuhis kuwa ni usalama wa taifa, lakini sio kweli…’akasema‘Umejuaje kuwa sio kweli..?’ nikauliza‘Siwezi kukuambia hilo, lakini kiukweli hayupo huko,…’akasema akiangalia saa yake na mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake akausoma, halafu akaniangalia.‘Sawa nafahamu, sasa kitu kinachowashangaza wengi, ni jinis gani anavyoweza kuwalaghai watu, wakamuamini, na kumpa kazi, jinsi anavyoweza kumuingiza mtu katika anga zake, na mwisho wa siku mtu huyo analizwa, na bado jamaa huyu hapatikani na makosa.....’akasema.‘Ni utapeli tu, mimi sizani kama anashindikana kukamatika kama kweli ana makosa…’nikasema‘Mimi nilipoona huyo jamaa kaingia kwa mume wako,....ikabid nianze kumfahamu vyema kwa  haraka nilikimbilia kwa jamaa yangu mmoja, ofisa upelelezi, na nikamuelezea hayo niliyoyaona na hisia zangu....’akasema, hapo nikamkatisha na kusema;‘Kwahiyo ulikwenda kunielezea matatizo yangu polisi bila kuniambia..?’ nikamuuliza‘Sio kuelezea mambo yako, nia ni kupata ushahidi na taarifa za huyu jamaa, na ni kwanini hawajaweza kumchukulia hatua huyu mtu…’akasema‘Najua hayo yote unayafanya kwa kivuli cha wazazi wangu, kweli si kweli…?’ nikauliza‘Na kwa taarifa yako wazazi wako, walishakuacha, hawataki kuingilia mambo yako tena, wakijua wewe sio mtoto tena, unaweza kujimudu, walikupima wakaona unaweza kujimudu, ila kwa hili hawawezi kukuacha,ni kweli wazazi wako waliniomba mimi niwe nakusaidia saidia, kuhakikisha hupotoki, na kukuonya kuhusu maadui zako , lakini bado walikuwa na mashaka na mume wako,..na ndio maana nalifanya hili…’akasema‘Nashukuru..’nikasema sasa nikawa nasimama kutaka kuondoka‘Kwahiyo unataka kwenda nyumbani sio……’akasema‘Ndio…’nikasema kumdanganya, lakini akilini mwangu nilikuwa sijawa na uhakika.‘Jana niliitwa na baba yako, akanielezea mambo mengi waliyoyagundua, ..mengi tu ambayo hata wewe huyafahamu…wamesema wao wanasubiria kuona ni nini wewe utakifanya baada ya hili tukio, ambao limefunikwa na mambo ambayo yanaonekana kuwa ndivyo lakini sivyo…’akasema‘Wazazi wako wanazidi kusisitiza kuwa hawataki kashfa, hilo alilolifanya mume wako ni nzito…halivumiliki, lakini je wewe utachukua hatua gani..wamekupa nafasi ya kukupima, kuona ukomavu wako katika mambo haya ya biashara..’akasema, na ilionekana alikuwa akinipotezea muda tu.‘Kwahiyo kuniita kwako kote na kuzunguka kwako kote kuhusu wakili na maelezo yake kumbe mwisho wake ni kuwa wewe umetumwa na wazazi wangu kunionya au sio, japokuwa awali ulikataa hilo, sasa umekubali mwenyewe, sawa nimekuelewa..?’ nikauliza na kusema.‘Ina maana hayo niliyokuelezea hayana maana…wewe subiria uone huo ushahidi, utakuja kugundua kuwa huyo wakili sio mtu wa mchezo, usiamue kupamba naye wewe mwenyewe, huko nyuma, alikuachia tu, kwa vile muda ulikuwa haujafika, usifikiri ulimshinda, kama ulivyoona, unajua kuwa alipanga kukushitaki kwa kumuharibia jina lake…’akasema‘Sawa nashukuru kwa hiyo taaarifa, kwanini hakufanya hivyo basi kama kweli ndivyo alivyo, …’nikasema kama kuuliza‘Nilipoongea na mpelelezi, alisema, hakuendelea kufungua mashitaka baada ya kuombwa asifanye hivyo na watu wake wa karibu, inaonekana ni sehemu ya mikakati yao, kujionyesha kuwa wao sio watu wa ugomvi...’akasema‘Sawa… mimi naondoka…’sasa nikawa nachukua mkoba wangu‘Wao bado wanamfuatilia, wanasubiria muda muafaka, maana ana watu wake wakubwa wanamlinda, lakini watu hao na wao hawana muda, wameshamulikwa, na awali hii ya utawala haina mchezo, wewe utakuja kusikia tu…’akasema.‘Hilo la kusema kuwa eti ana mtu mkubwa anamlinda siliafiki, ....hamsini zake hazijafika, na kama kaingilia anga zangu tena, mimi sitajali huyo mtu wake, sizani kama kuna mtu ana uwezo juu ya sheria, sitaki kukuambia mengi, lakini ngoja nione nitakachokifanya, najua mnanidharau, lakini ngoje muone....’nikasema kwa kujiamini.‘Wote wanasema hivyo, hata huyo mpelelezi anasema hivyo hivyo, lakini tujue kuwa hata huyo jamaa mwenyewe anajua hilo, na ndio maana anakuwa makini kwa kila analolifanya, huyo jamaa alivyo mjanja, hajipeleki kwa mtu ovyo ovyo, mambo yake ni kimiya kimiya, taratibu, kama tai anavyomvizia adui yake. ‘Ukiona anafanya kazi fulani ujue, keshapitia kila njia, na huwezi kumuona akijipeleka ovyo ovyo tu, ... mara nyingi wateja wake, ndio wanamuita....na kila anayemuita, anahakikisha anafuata taratibu zinazokubalika kisheria, ..yupo makini sana kwa hilo...’akasema.‘Umakini gani wa kufoji mikataba ya watu, kuibadili, na kuiba nyaraka kwenye maofisi ya watu...’nikasema‘Unasema nini, kaiba nyaraka,...una uhakika na hilo…usikurupuke….usije ukalisema hilo kwake,…huna ushahidi, au unao….liache kama lilivyo…’akasema ‘Sina uhakika wa moja kwa moja na hilo, ..lakini kwa mtizamo wa haraka haraka, atakuwa ndio yeye tu, na sitalala mpaka nihakikishe nimemuweka ndani, na kama analindwa, basi mimi nitajua jinsi gani ya kumfanya mlinz wake asalimu amri...’nikasema.‘Kuwa makini na kauli zako, kauli zako zinaweza kukufunga...na usije ukatamka maneno kama hayo kwake,...nilikuona ulivyokuwa ukiongea naye pale hospitalini, na kwa vile nilikuwa sijamjua, sikuweza kuingilia mazungumzo yenu, lakini kauli kama zile,...usizitamke tena kwa huyo jamaa,..tamka kitu kama una ushahidi nacho...yeye anajihami, na kwenye ule mkoba wake, ana vifaa vya kurekodi, mazungumzo’akasema‘Kwani nimesema nini kibaya hapa...ndivyo ilivyo..’nikasema‘Mimi ninachokushauri ni kuwa ujue unapambana na watu walio makini kisheria,wao wanasubiria kosa dogo, wanakunasa,  huyo mtu tuachie sisi, tumeshamfuatilia, na tunajua jinsi gani ya kumnasa, kwasasa hivi wewe hangaika na afya ya  mume wako tu na ujifanye hujui lolote, timiza wajibu wako, ili kusitokee sababu...’akasema.‘Nitahangaika vipi na mume wangu, wakati huyo jamaa keshasema ni wakili wake, halafu wanaponiacha hoi, na pale anaposema kuwa, hata mimi siwezi kuongea na mume wangu mambo muhimu, yenye mlengo wa kisheria, mpaka huyo jamaa awepo, hapo, ina maana gani, ni kuwa mume wangu na mimi sasa ni kama watu wawili tofauti...’nikasema.‘Ndio maana ya ule utangulizi wangu wa mwanzo, sasa hivi mume wako anaanza kuyaonyesha makucha yake, maana anahisi kile alichokuwa akikitaka kwako, kitapotea....na akirudi mitaani, ataadhirika, ...sasa afanye nini, ndio maana kaamua kujiunga na rafiki yake huyo....sina nia mbaya na rafiki yangu huyo, lakini ndivyo ilivyo, ....mimi nakujali wewe zaidi....’akasema.‘Nimeshakuambia kuwa mimi sihitaji msaada wa yoyote yule, usijiingize kwenye maswala yangu, ukafikiria kuwa nitakuunga mkono, sitaki kuja kumbebesha mtu lawama, niachieni hayo ni mambo yangu, msije mkaanza kusema, `ooh, tulikuambia....’nikasema.‘Usilichukulie hili swala juu juu, ...wewe unaliona kama ni swala dogo, lakini ujue hata watu mashuhuri wameshindwa kumkamata huyu mtu, unafikiri wao ni wajinga, ya kuwa hawana njia ya kumnasa, wanasubiria muda muafaka, na utafika hivi karibuni,.....’akasema.‘Sawa tutaona...hao watu waliopo juu ya sheria..’nikasema.‘Kama nilivyokuambia hawa watu ni wajanja sana, wameliweka hilo jambo lionekane hivyo linavyoonekana, wameanzia mbali sana,...lilianza kuonekana ni swala la mapenzi, …lakini kuna kitu kiliwashinda, ni huo mkataba wenu..’akasema‘Mkataba wangu uliwashinda nini, wakati wameugushi..’nikasema‘Ndio, hilo linafanyiwa kazi, usijali, kila jambo ni silaha kwetu, kama ilivyo kwao, tukinasa ushahidi, hapo jamaa hatoki, ..kaharibu meza yake mwenyewe, lakini hilo hakulifanya yeye, hutaamini hilo…’akasema‘Nani kafanya sasa..?’ nikauliza‘Yeye mkataba uliofika mezani kwake ndio huo wa kugushi, huo wa awali hajawahi kuuona, …mtu aliyefanikisha kugushi huo mkataba ni mtu mbali kabisa na yeye, na huyo mtu kwa hivi sasa hayupo hapa nchini, alishaondoka,…sio mzaliwa wa hapa, karudi kwao…’akasema‘Ok, nimekuelewa, sasa unataka mimi nifanye nini?’ nikamuuliza.‘Kunielewa haitoshi, muhimu ni kukubali tulifanye hili jambo kwa pamoja bila ya kujionyesha kwa watu kuwa mimi na wewe tuna shikirikiana , na pia na muhimu sana, usimwamini mtu yoyote kwa hivi sasa, hata hao watu wako, na huyo rafiki yako kuanzia sasa achana naye...hilo ni muhimu sana...’akasema‘Nafahamu sana, kuanzia sasa simuamini mtu tena, sina rafiki tena, kama wapo sitawaamini tena,.....’nikasema.‘Unaweza kusema hivyo, ila kwa hili, mtu pekee unayetakiwa kumwamini, kwa sasa ni mimi,...upende usipende ...mwenyewe utaona...’akasema.‘Sifanyi makosa hayo tena…’nikasema‘Sasa sikiliza, wakati tupo hospitalini, huyo wakili wa mume wako, alionekana akiongea na rafiki yako nje ya jengo,..unalifahamu hilo,...?’ akaniuliza.‘Rafiki yangu, huyu huyu anayesafiri…?’ nikauliza‘Huyo huyo ..ndio maana nakuambia uwe makini…’akasema‘Mhh…kwahiyo hilo la kuwa mtoto wake katekwa na nini..ni hadithi ya kutungwa..’nikasema‘Hilo bado tunalifanyia kazi, siwezi kukujibu kwa sasa, ila jiulize alikuja kuweka sahihi ya mikataba gani , na tumefuatilia, ndio kweli visa yake na mikataba yake ya kusoma huko nje ilikuwa na kasoro, akahisi ni wewe umefanya hivyo, ndio maana akaamua kutafuta mdhamini mpya, kwahiyo kuja kwake hapa imechukuliwa hivyo..’akasema‘Ina maana unalifahamu hilo..?’ nikauliza‘Ndio maana nakuambia utulie, mimi nina vyanzo vyangu, vitakusaidia, na kama unataka tuwe timu moja utaona jinsi gani tutaliharibu hili kundi, sasa ni hivi, kilichofanyika ni mbinu, ili ionekane hivyo, na kuna watu wamecheza na udhamini wake, na sasa wamemuweka mtu wao, unafahamu ni nani huyo….’akasema na kuuliza‘Mimi sijui…’nikasema‘Ni adui ya baba yako..yeye huwa anasomesha wanafunzi nje…au watu wasiojiweza, kwahiyo rafiki yako yupo kwenye orodha yao, na inasemakana kuna ajenda kuwa wewe ulimtelekeza ndio maana akatafuta mdhamini mwingine, hilo limefichwa…’akasema‘Mhh..ina maana gani hiyo yote..?’ nikauliza‘Sasa nikuambie kitu, huyo rafiki yako alipofika hapo hospitalini, hakuteremka kwenye gari,alifika na gari la kukodi,lisiloonyesha ndani, magari haya ya bei mbaya, jiulize kwanini alikodi gari hilo la bei mbaya…’akasema‘Na alipofika hapo hospitalini, hakuteremka, alihakikisha kuwa hakuna mtu anayefahamu kuwa ni yeye, aliyekuja kuongea naye ni huyo wakili wa mume wako, na huyo wakili wa mume wako, …alijifanya anakwenda kwenye gari lake akasimama kama analikagua, huku anaongea na rafiki yako…’akasema‘Walipomaliza kuongea, rafiki yako huyo akarudi ndani kuongea na mume wako, na rafiki yako akaondoka bila kuteremka kwenye gari, hebu jiuliza hapo kuna nini...na kwanini hakuenda kumuona mgonjwa moja kwa moja, wakati aliaga kuwa anakwenda kumuona mgonjwa.....!’akasema.‘Vijana wangu wakamfuatilia, awali hawakufahamu kuwa ni yeye, si umafahamu rafiki yako alivyo, anaweza kujibadili usifahamu kabisa kuwa ni yeye, vijana wakataka kuhakiki‘Hilo gari liliendeshwa hadi mjini, kwenye hoteli za kitalii, mdada akateremka kama kaja kutafuta chumba, akaingia ndani, na huko akaongea na watu wake, akabadili nguo, akatoka akiwa mtu mwingine kabisa, akachukua usafiri wa taksi za kawaida, uliompeleka hadi sehemu , na akateremka na kuingia kwenye daladala, iliyomfikisha hapo anapoishi, watu wangu walimfuatilia, na wakamgundua kuwa ni yeye....’akasema.‘Mhh, nafahamu kuwa alifika hospitalini, aliniambia mwenyewe..’nikasema japokuwa sikuwa nina habari zote hizo.‘Lazima angekuambia hivyo, ili kuficha ukweli zaidi,... sawa hakuna shida, ila ninachotaka kukuambia hapo ni kuwa huyo wakili, ana kitu kinachowaunganisha, rafiki yako na mume wako, kwahiyo wakili huyo anaongea na mume wako, halafu huyo wakili anapeleka taarifa kwa rafiki yako...mume wako na rafiki yako wameamua kuwa mbali mbali, na hawatakubalia lolote linalohusiana na wao wawili…’akasema.**********Kiukweli hapo niliona kuna mambo ambayo mimi sijaweza kuyapata na wenzangu wameshayapata, japokuwa kuna mambo mimi nayafahamu na nina uhakika wao hawayafahamu, lakini sikutaka kuongea nao lolote, akili ya kumuamini mtu ilishaanza kunitoka, …‘Kwa vile hukuwahi kufika uwanja wa ndege, kuna watu walitumwa nyumbani kwako kufanya lolote, hatuna uhakika nia yao ni kufanya nini, maana hawakukuta,..tatizo lao, hawakulifikira hilo mapema....kiujumla, upo kwenye hatari, sasa ni wajibu wangu kufanya kila jitihada kukulinda…kwa hivi sasa njia ipo salama unaweza kwenda…’akasema‘Je mna uhakika gani kuwa mume wangu ndiye aliyetembea na rafiki yangu,..?’ nikauliza‘Hilo lisikutie shaka…ukweli upo wazi, ila kuna ajenda ya siri ambayo siwezi kukuambia kwa sasa…ninachokuomba ni wewe kuendelea kujifanye hivyo hivyo..unavyofanya, hujaamini kuwa tendo limefanyika hivyo watu wanavyosema, nia ni kuja kunasa jambo ambalo litakuwa ushahidi…kuna DNA, imetoka, lakin hatuna uhakika nayo bado,hawataki kuionyesha mpaka sasa…’akasema‘DNA, ya huyo mtoto, mliwezaje kuipata, …niambie inasemaje…?’ nikauliza kwa hamasa‘DNA, imefichwa, na kuna tetesi kua huenda hiyo DNA, inasema kuwa huyo mtoto, sio wa mume wako…’akasema‘Mnasema, 'huenda, kwanini msiende kuulizia hapo ilipotolewa, kwani walipimia wapi.....mimi bado nina mashaka na hilo,...lakini .., mumeona sasa, na hakuna mtu anayeweza kugushi kitu kama hicho, kwahiyo ni kweli, sio mtoto wa mume wangu…’nikasema‘Usijali, hilo linafanyiwa kazi…jiandae kwa lolote lile, na hata ikihakikiswa, wala usichukue maamuzii ya haraka maana mkataba huo mpya, utakufanya usifanye lolote, kuna maswali mengi bila majibu, kama ni hivyo, kuwa DNA kama yaonyesha kuwa, rafiki yako hajazaa na mume wako, hiyo mikataba ni ya nini, je labda alitarajia jambo sasa limekuwa kinyume chake, je hayo yanayoendelea ni kwa masilahi ya nani…’akasema‘Hapo sijui…nahisi kuna jambo jingine sio kwa sababu ya huyo mtoto…’nikasema‘Hizo ni silaha zetu zitatumika kwa wakati muafaka, wewe vuta subira, sasa unaweza kwenda, na nenda moja kwa moja nyumbani kwako, kupo salama, usije kwenda kinyuma na makubaliano yetu, sawa…’akasema, na kabla sijaondoka, akaniuliza swali‘Hivi wewe unafahamu wapi Makabrasha anaishi?’ akaniuliza‘Huyu mtu sijui anaishi wapi , ni mtu wa kuhama hama, na nijuavyo mimi ofisi yake ipo mikononi, popote ni ofisi yake,..wakati mwingi ukitaka kumpata, nenda ofisi za wanasheria, alikuwa anapenda sana kukaa hapo, lakini baadaye akawa anatumia hoteli, leo hii kesho ile,..kwa ujumla anahama hama, hana sehemu maalumu, ila ana nyumba kama tano hivi,, hutaamini hata mke wake, hayupo hapoa Dar...’nikasema.‘Ndivyo unavyomfahamu hivyo, au sio…hahaha….’akasema na kucheka‘Kwani sio kweli…?’ nikauliza kwa mshangao.‘Huyu mtu anaishi maeneo ya uwanja wa ndege...kuna nyumba mpya ipo karibu na majumba sita, ina ghorofa hivi...inasadikiwa kuwa Makabrasha ana hisa nayo...ndipo ofisi zake zipo humo ndani,  …makazi yake ndio hayo ya kuhama hama, kwa vile ana nyumba nyingi, leo yupo hapa kesho yupo kwingine, anajihami kila mara…’akasema‘Eti nini...unasema ofisi zake zipo uwanja wa ndege…una uhakika na hilo?’ nikauliza huku nikisimama‘Sasa unataka kwenda wapi..?’ akaniuliza huku akinishangaa‘Kuna kitu ….ina maana basi huyo rafiki yangu alikuwa kwa Makabrasha au sio...’nikasema‘Ndio maana tukakuzuia usifike huko, haya yote yanafanyiwa kazi, kwa usalama wako...’akasema.Nikakumbuka jinsi rafiki yangu huyo, alivyokuwa akiongea kwenye simu, na sauti yake ilikuwa sio ya usalama,kama vile anakwazwa kuongea kwa sauti, ilikuwa kama ya kunong’ona,simu ikakatika, kama vile kuna mtu alimnyang’anya...Hapo akili yangu ikaniambia kuwa huenda rafiki yangu huyo ananificha jambo, au alikuwa hatarini, lakini hakuweza kuniambia, yote mawili yanawezekana, ..lakini kwa namna nyingine huenda rafiki yangu kaamua kunisaliti..sikutaka kumwambia lolote docta kuhusu mawazo yangu hayo mapya, nilitaka nikitoka hapo niwaulize watu wangu, ambao nilishawatuma huko.‘Tutaongea siku nyingine naona muda umekwenda...’nikasema.‘Umesikia nilipokuambia, uende moja kwa moja nyumbani kwako,, sawa tumeelewana hilo..’akasema‘Sawa hamna shida...’nikasema‘Haya ukijifanya mkaidi usije kunilaumu…’akasema akiangalia saa yake‘Huyu rafiki yangu anajifanya mjanja,..kumbe walikuwa na huyu wakili wakati anaongea nami kwenye simu, na nina uhakika ndipo alikuwa muda wote huo.., ila sina uhakika maana aliniambia yupo kwa shangazi yake,..je hilo la kutekwa mtoto wake ni kweli, au alikuwa akinidanganya..? ’nikasema kumuuliza‘Kuna kitu unatakiwa ukijue, huo mkataba aliolazimishwa rafiki yako kuweka sahihi ni wa nini, na  kwa masilahi ya nani, ndio ni kwa ajili ya mtoto, kama alivyodai, au kama alivyoambiwa, sasa ni kwa baba yupi…kwanini huo mkataba haujawekwa wazi mpaka sasa, ina maana unasubiria jambo fulani, unaona hapo…?’ akaniuliza‘Hilo siwezi kujua, maana hata mimi sijauona huo mkataba, watu wangu wanafuatilia, lakini haujapatikana, labda haujatolewa bado na kufikishwa sehemu husika, lakini tutajua tu,…’nikasema na kuanza kuondoka‘Sawa, ila nakuahidi mpaka kesho utakuwa umepatikana, mimi nimepanga kuonana na makabrasha nataka kuongea naye, tumakubaliana kesho, kwahiyo usiwe na haraka na hilo, sawa wewe …ukitoka hapa rudi nyumbani kwako….’akasema‘Nimekuelewa, sawa..,’nikasemaUsiku ulikuwa umetanda, giza, na mihangaiko ya watu wakirejea makazini na wengine kwenda kwenye starehe, mimi sikuwajali hao..akili ilikuwa ina mengi ya kufanya, niliona nje barabarani kupo shwari nikaangalia saa…'DNA, inasema huenda mtoto sio wa mume wako...kama sio mtoto wa mume wangu ni wa nani, basi atakuwa wa mdogo wa mume wangu...je ni kweli hili au ....hapana ni lazima nipate uhakika, kabla huyu mtu hajaondoka...na kama hivyo, basi rafiki yangu atakuwa kweli matatani...ni nani huyo yupo nyuma ya hili jambo...' nikawa nawaza sana, baadae nikaangalia saa.Nikawapigia simu watu wangu na walichoniambia kikanifanya nizidi kuwa na hamasa:‘Ni kweli madam, mtoto wa rafiki yako alichukuliwa na watu, na amekuwa akihangaika kumkomboa, …'wakaniambia'Keshaingia uwnja wa ndege...?' nikauliza'Bado, hajulikani wapi alipo mpaka sasa..tumejaribu kumtafuta hajaonekana, alitupotea wakati anahangaika kumalizana na hao watu waliokuwa na mtoto wake...'wakasema'Je hamjasikia lolote kuhusu DNA, nasikia wamepima hicho kipimo..?' nikauliza'Bado madamu, tutafuatilia tutakufahamisha, hilo ni jambo dogo tu...'wakasema'Sawa endeleeni kumtafuta huyo mtu mjue kama keshaingia uwanja wa ndege au la...'nikasemaNikaangalia saa yangu tena....‘Huu muda naweza kuwahi, ninaweza kumuwahi rafiki yangu , ni lazima niongee naye, uso kwa uso, nijue ukweli. hiyo DNA, inasemaje,..ni lazima nilifahamu hilo kabla hajaondoka, ni lazima .…’nikasema hivyo.Hapo hapo, nikageuza gari kulia...na sasa nikawa naendesha gari kuelekea uwanja wa ndege, akili ilishaamua hivyo, ni lazima nifike huko, ....Nikakanyaga mafuta, huko moyoni najipa matumaini'Nitawahi tu....'WAZO LA LEO: Maisha ya ujanja ujanja, na kujiona una akili zaidi ya wengine, ukawa unafanya mambo ya dhuluma, na bahati ukawa unafanikiwa, sawa utafanikiwa leo…na ukajipa matumaini kuwa hakuna anayekuwea. Lakini nafsini hutaweza kuwa na amani. Dhuluma inamfanya mtu aishi kwa wasiwasi, hata kama atajificha vipi, au hata kama atakuwa na walinzi wa kimataifa. Tusisahau kuwa wanaodhulimiwa wapo wanamlilia mola wao, na ipo siku kilio chao kitajibiwa, kama sio leo, basi muda baadae kidogo.‘Nahisi labda rafiki yangu yupo matatani, au hata kama hayupo matatani lakini naweza kukutana naye akaniambia ukweli kuhusu hiyo DNA, Je matokeo yanasemaje..nitamuomba sana..ili nafsi yangu itulia…hata kama…‘Na ni lazima nifanye lolote,kuonyesha utu, hata kama mtu kakufanyia ubaya, lakini keshaniambia yupo matatani, hayo mawazo yaliuteka ubongo wangu na sikuwa na sababu nyingine ya kuacha kwenda huko uwanja wa ndege....Endelea na kisa chetu.....********Usiku una mitihani yake, japokuwa nilikuwa na nia ya kumsaidia rafiki yangu, lakini moyoni, nilikuwa na mashaka ya usalama wangu, kiukweli mimi sio mtu wa kuogopa ovyo, lakini wakati mwingine unahitajika kuwa na tahadhari, kwani huwezi kujua wenzetu wamejiandaa vipi, ....Wakati mwingine nikafika kujilaumu, kwanini sikumsikiliza docta, rafiki wa mume wangu pale aliponisihi nisije nikaenda huko uwanja wa ndege, nahisi kuna kitu wameona ambacho sio kizuri, kuna hatari, lakini hatari gani.Japokuwa sikutaka kumwambia naenda wapi, lakini ingelikuwa vyema akajua,...‘Nakufahamu sana unataka kwenda huko uwanja wa ndege, ...usije ukafanya hayo makosa, mimi kama mtu ninayekujali, nakukataza kabisa usiende huko....’akasema.Kawaida yangu na huyu mtu, tunakutana, inakuwa hivyo, huwa hatukubaliani kirahisi, yeye ananifahamu hivyo, na mimi namfahamu sana tabia yake, mimi na yeye ni kama mafahali wawili, ...na sikupenda anione mimi sijui ni nini ninchokifanya hata hivyo, nilishamfahamu kuwa mengine anayafanya ili nimuone kuwa ananijali, au anafanya kuwarizisha wazazi wangu..sikupenda kufanyiwa hivyo.‘Hivi kwanini rafiki yangu alipofanyiwa hivyo, hakuwapigia simu polis, lakini yeye ni mpiganaji anafahamu lipi jema, siwezi kumlaumu hasa inapofikia kwenye familia yako…’nikasema kimoyo‘Hao watu sio mchezo, ikibidi kufanya unyama wanafanya, wakijua wana watu wa kuwalinda, kwahiyo uwe makini sana nao…’hiyo ilikuwa moja ya kauli za docta akinitahadharisha.‘Mimi sijaona uhatari wao…’nikasema na nilisema hivyo, kutokana na kauli ya docta, yeye kaona kuwa watu hao wanafanya hivyo huenda kwa vile wana watu ambao wanaweza kucheza na vifungu vya sheria na kufanya wapendavyo, na pia labda ni kwa vile wana mtu mkubwa wanayemtegemea..’nilijikuta naongea peke yangu kwenye gari.Safari ya kwenda uwanja wa ndege inaweza ikakufanya hivyo, ukaongea peke yako, ukawaza mengi, na kama huna mtu, utawaza na kuwazua peke yako, na vinginevyo, ukutane na madereva wa daladala, mtukanane,…yaani ukifika sehemu unayokwenda, kama umefika salama ushukuru mungu, ni mtihani kwa kweli.‘Je kama nikutana na hao watu , na wana silaha, nitawezaje kujihami, kama sina silaha..’nikajiuliza, hivi kwanini sikuchukua bastola yangu kwa ajili ya kujihami, ili wakinitishia na silaha na mimi nawaonyesha kuwa nina silaha na pia naweza kuitumia…oh, sasa nifanye nini, nirudi, hapana siwezi kuwahi, …hapana, siwezi kurudi…’ nikawa naongea huku gari linakwenda.Niliona kuwa kama nitakwenda nyumbani kuifuata hiyo silaha yangu, nitakuwa nimechelewa sana. Haitakuwa na maana tena, …‘Hamna shida ngoja niende huko huko, sio lazima nipambane nao kwa silaha, hata hivyo sizani kama kutakuwa na haja ya kutumia silaha, ikibidi, nitatafuta njia nyingine...pale kuna kituo cha jeshi, nitafanya lolote wajue kuwa nipo kwenye hatari, ila tatizo ni usiku…hata sijui, mungu nisaidie tu....’nikasemaNilipokaribia uwanja wa ndege, nikampiga simu ya rafiki yangu, tena na tena lakini simu yake ilikuwa haipatikani. Labda atakuwa keshaingia uwanja wa ndege, au …labda watu hao bado wamemshikilia,..lakini kwanini waendelee kumshikilia, kuna ni nini hajawatimizia,…mmh,  ngoja niwapigie watu wangu kujua kinachoendelea..’nikasema na kuwapigia watu wangu.‘Hatujampata mpaka sasa hivi, hata uwanja wa ndege hayupo, hajaingia kabisa …’wakasema‘Muna uhakia, basi Ina maana labda bado wamemshikilia sehemu..?’ nikauliza‘Yawezekana, maana kwa mara ya mwisho kuna kitu walikuwa hawajaelewana, kukatokea kitu kama vurugu, baada ya hapo mdada akatoweka, na wale watu aliokuwa nao, wakawa wanamtafuta…hadi sasa huyo mdada hajaonekana yeye au mtoto wake, na wale watu bado wanamtafuta…’wakasema‘Basi yupo kwenye wakati mgumu angalau angelinipigia, nikajua nimsaidie vipi au ndio keshanizarau……sijui nitampataje sasa..’nikasema‘Madam, tuachie hilo, tutampata tu…’watu wangu wakasema na mimi hadi hapo nilikuwa sijawajulisha kuwa nipo njiani nakuja huko huko, nilitaka hilo lisijulikane mpaka nifike maeneo ya hapo. ‘Mtoto wangu aliibiwa…, wakati nipo bafuni naoga, walifika watu nisiowafahamu, wakamchukua mtoto wangu..nilichanganyikiwa…,lakini baadaye wakanipigia simu, kuwa kama namtaka mtoto wangu, akiwa hai basi nifanye wanavyotaka wao, nikawaulize nifanye nini...’Nilikuwa najaribu kuyakariri maneno yake kuona kama kuna uwalakini wa udanganyifu, lakini niliona huenda ni kweli…..*********Nilishafika maeneo ya uwanja wa ndege sasa, nikawa najiuliza niingie ndani moja kwa moja au…nikaona niwapigia watu wangu tena kuhakiki bado wakaendelea kusema kuwa hawajamuona,  hajaonekan ndani ya uwanja wa ndege, na muda wa watu kuingia kwa ajili ya ndege anayoondoka nayo umeshafika..na bado haonekani.‘Inawezekana kaahirisha safari yake…?’ nikauliza‘Hapana, tumelichunguza hilo, hajaahirisha bado…’wakasemaNikawa sasa nimefika sehemu niamua kuingia ndani ya uwanja wa ndege au …kwa mbele nikaliona lile jengo nililoambiwa kuwa Makabrasha ana ofisi zake humo ndani,..kumbe unaweza kuliona bila kupata shida. Baada ya kuliona hilo jengo tu, akili yangu ikanituma nifike kwanza kwenye HILO jengo, kwani huko ndani ya uwanja wa ndege wapo watu wangu wanafuatilia, aanglionekana kama alikuwa keshaingia huko, basi bado atakuwa kashikiliwa sehemu na sehemu ninayoishuku mimi ni kwenye hilo jengo.‘Au watakuwa sehemu gani nyingine…hawa watu wangu kama wamemtafuta kila mahali hajapatikana, basi…hapana ngoja nikahakikishe mwenyewe..’nikasemaNikawa sasa nimefika eneo la hilo jengo, ni jengo kubwa la ghorofa tatu…na ukiliangalia kwa mbali ni kama halijamalizika kujengwa, lakini nilipofika sehemu yenyewe nilikuta shughuli zinaendelea kama kawaida, Sehemu kubwa ya chini imechukuliwa na waendesha biashara za vinywaji, kwahiyo kwa wakati huo watu walikuwa wamekaa kwenye viti vilivyopangwa kwenye miti iliyopandwa kwenye bustani ya eno hilo, wakinywa, na mziki ulikuwa ukipigwa....Mimi nilipoingia eneo hilo na gari langu, wakaja wapokezi, wakinikaribisha kwa bashasha, huku wakinielekeza sehemu ya kuegesha gari langu, nami nikafanya hivyo, na kutoka nje ya gari, na wale wahudumu, wakaendelea kuonyesha ukarimu wao, inaonekana walisomea hiyo kazi, kwani walijua jinsi gani ya kumkaribisha mgeni, mpaka unavutiwa ..‘Unakaribishwa mgeni, hapa kuna huduma mbalimbali, kuna vinywaji, kuna chakula, au kama unahitaji kumpumzika kuna sehemu ya kupumzika, vipo vyumba, na huduma nyingine ...’nikashangaa, maana sikujua kuwa jengo hilo lina mambo yote hayo. Kiukweli lilikuwa limekamilia kama jengo la ofisi, burdani na vyumba vya wageni.‘Kwani hapa kuna vyumba vya ofisi na hata vyumba vya kulala wageni?’ nikauliza‘Ndio vipo vingi tu, vyumba vya wageni vipo juu na chini, ni wewe tu, unahitaji chumba, kwa muda gani je upo peke yako?’ wakaniuliza.‘Hapana sihitaji chumba, mimi nataka kumuona mtu fulani…sijui kama ninaweza kumpata humu mmh, sasa ni saa mmh…?’ nikauliza nikijifanya kujibaragua hivyo, kwani sikuwa na uhakika nisemeje, maana nilitakiwa niwe na tahadhari. Hizi kazi za watu, hizi zilimfaa rafiki yangu, sio mimi mtu wa ofisini.‘Ni mtu gani huyo je ana ofisi hapa, au mteja wa mara kwa mara hapa, tunaweza kukusaidia kumpata…?’ akaniuliza‘Ndio anaitwa Makabrasha...’nikasema‘Oh,…kumbe ni muheshimiwa,…mhh, ulikuwa na ahadi naye..?’ akaniuliza‘Ndio…’nikadanganya hivyo.‘Basi itabidi uingie sehemu ya ndani, sehemu ya mapokezi, huko ndani watakuelekeza, sisi huku tunashughulika na wateja wan je, na ofisi za chini, karibu sana…’akasema‘Ahsante,….’nikasema‘Lakini naona ajabu, muda kama huu, mara nyingi, anakuwa huku chini,  anapenda sana kujichanganya na watu, sasa sijui kwanini hajateremka, na leo siku nzima sijamuona huwa ni rafiki yangu akija hapa lazima tuongee na kutaniana…’akasema‘Oh kumbe, kwahiyo labda ana wageni, ni mwanamke na mtoto au…?’ nikauliza‘Yeye kila mara ni mtu wa wageni..ofisini kwake kama huna miadi naye sio rahisi kumpata analindwa utafikiri muheshimiwa gani vile, sikumbuki kumuona huyo mtu mwanamke na mtoto, hata..labda maana sio muda wote ninakuwa hapa, mimi nimeingia jioni hii …’akasema‘Ok…ngoja nikaonane naye tu nitajua huko mbele kwa mbele…’nikasema‘Sawa…;lakini sio kawaida yake..kutokuonekana huku chini…, nahisi ana kazi nyingi....ingia ndani watakuelekeza ofisini kwake, karibu sana...’akasema huyo mpokeaji wageni.‘Nashukuru hamna shida, na gari langu naweza kuacha hapa… , hapa kuna usalama....?’nikauliza‘Aah , ndio hakuna shaka, ila kama unahitaji ulinzi binafsi inabidi ulipie pale, kwa yule mlinzi, vinginevyo, liache hapo hapo, ..’akaniambiaNa mimi kwa vile sikujua nitakaa huko ndani kwa muda gani, nikaona ni bora nipate hiyo huduma ya ulinzi binafsi, nikaenda kwa yule mlinzi, nikaandikisha, na kulipia. Baada ya hapo nikaingia ndani..Sikutegemea sehemu ya ndani imejengwa kiofisi kweli, kuna sehemu nzuri za kusubiria wageni, runinga, na vyumba vya huduma za vinywaji…na kulikuwa na wahudumu kutegemeana na ofisi unayokwenda.Haraka nikaenda kwa muhudumu nikamuelezea shida yangu, na nilipomtaja huyo Makabrasha, akanielekeza kwa askari mmoja…‘Yule ndiye mtu wake…’akaniambia Nikamsogelea huyo askari,  alikuwa kakaa na mbele yake kuna meza, na kitabu kikubwa, alikuwa anasinzia, na aliponiona akasimama na kunikaribisha, nikamuelezea shida yangu.‘Oh, kwa muda kama huu, mara nyingi huwa hataki wageni, ....lakini mmh, ngoja,  maana alisema hataki usumbufu, …alikuwa na wageni muhimu…mmh, sijawaona wakitoka,…eeh, ok,…unasema una miadi na yeye, jina lako,..maana natakiwa kumpigia simu kuhakiki...’akachukua simu yake na kupiga, ikawa inaita tu, akaniangalia, na kusema;‘Unaona hataki hata kupokea simu, tafadhali hebu wewe nenda,….si umesema una miadi naye au sio…basi nenda, maana muda umekwenda, ukifika rosheni ya pili, upande wa kushito utaona ofisi yake, na maandishi ya ofisi yake sio sehemu yenye utata,…lakini samahani, natakiwa nikukague kama huna silaha yoyote ni kawaida usijali..’akasema akinipitishia mashine ya kukagua, na aliporizika akasema‘Ok, sasa unaweza kwenda...’akasema hata bila ya kunipa muda wa kumuuliza nilichotaka kumuuliza, …na mimi hapo nikawa huru, hata kama nitachukua muda mrefu huko ninapokwenda, kwani yaonyesha kuna utaratibu mnzuri wa usalama, kuanzia nje hadi ndani… Nikaelekea kwenye ngazi za kupanda, juu, ..jengo halikuwa na lifti…ni mwendo wa zoezi, sikujali hilo,  maana hata mimi ni mtu wa mazoezi.Nilipoanza kupanda ngazi ya kwanza simu yangu ikaita, nikaangalia ni nani mpigaji, nikaona ni docta rafiki wa mume wangu, sikutaka kuipokea simu yake kwa muda huo, nikaikata, na kuanza safari ya kwenda juu, huku nikiwa na mawazo mengi mengi kichwani.‘Hivi haya aliyoniambia docta rafiki wa mume wangu kuwa wakili huyu ni jasusi fulani inaweza kuwa ni kweli..na kwanini mume wangu akamchukua mtu kama huyu, nataka nikikutana naye nimuulize kuhusu huo mkataba na mume wangu, mimi kama mke wa mteja wake nina haki ya kufahamu hilo.‘Hata hivyo muhimu wangu ni kuhakikisha kama rafiki yangu hayupo naye huko, …’nikasema huku nikiangalia saa, na kwa muda huo kama ni wasafiri wa kuondoka, watakuwa wameshaingia ndani, ..sijui kama huyu rafiki yangu ataweza kusafiri leo..au …yupo matatani.’nikawa naongea kimoyo moyo. Wakati natembea sasa kupandisha ngazi ya mwisho ili nifike eneo la ghrofa iliyopo hiyo ofisi …ya makabrasha, mara akatokea mtu akiwa na haraka, karibu anipige kikumbo kwa jinsi alivyokuwa na haraka, ni kama anakimbia, alikuwa kavaa kofia kubwa, kiasi kwamba huwezi kuona sura yake, mpaka, ainue kichwa kidogo.Yule mtu aliponiona, kwanza aliinua kichwa ili aweze kuniangalia usoni, ni kama kashtuka kuniona na alitaka kuhakiki, akainua kichwa kuniangalia vyema…akataka kuongea jambo… akasita, kama anataka kuniongelesha, lakini akasita, na kunipita kwa haraka na kukimbilia chini, mimi sikumjali nikaendelea na safari yangu ya kwenda juu.‘Huyu mtu ni nani, mbona anakuwa kama ana mashaka…’ nikajiuliza na hapo nikaanza kuingiwa na mimi na wasiwasi, kiujumla kulikuwa kumetulia maana muda huo ofisi nyingi zilikuwa zimefungwa.‘Huyu wakili yaonekana sio mtu wa kawaida mpaka anaweka walinzi wa kukagua watu, lakini labda ni mlinzi wa ofisi zote za huku juu..na ofisi nyingi zimefungwa yeye bado yupo kazini…’nikasema‘Ni lazima nikaongee naye, nitapambana naye uso kwa uso, atashangaaa kuniona muda kama huu..’nikasema kimoyo moyo. Na nilijipa matumaini kuwa hawezi kunifanya lolote, kwa jinsi walivyoweka taratibu zao, mtu anayeingia anajulikana na akitoka  halikadhalikaHata hivyo kutokana na familia yangu watu wengi wakisikia kuwa mimi ni mtoto wa , basi kuna kuogopwa au kuheshimiwa kwa namna fulani, baba yangu alikuwa na umaarufu fulani hivi…kwahiyo sihitajiki kuwa na mashaka..hata hivyo moyo wa mashaka bado nilikuwa nao..Sasa kiusalama nikaamua niwapigia watu wangu niwaambia kuwa nipo sehemu hizo wakaribia hapo kama lolote likitokea,..nilishangaa kuona simu yangu haina mawasilinai mtandao haushiki…, hii ni kuashiria kuwa eneo hilo, wameweka vitu vya kuzuia mawasiliano, sasa wao wakitaka kupiga simu nje inakuwaje.Nikaona haina shaka nisipoteze muda,  nikatembe akwa haraka haraka , maana sasa nilikuwa kwenye korido,.. sehemu ile ya kutembea ili uitafuta ofisi ya huyo muheshimiwa,..hapo nikajiwa na mawazo, nikimuwazia mume wangu, jinsi gani alivyotekwa kimawazo na huyu mtu hadi akukubali kuwa huyu jamaa awe ni wakili wake.‘Hii inaashiria kuwa mume wangu kafanya makosa, na sasa anajihami, sasa kafanya hivyo ili kujitetea, kwa vile anafahamu fika kosa alilolifanya litamfanya akose kila kitu, na kiukweli mimi sitaweza kukubali, ni lazima sheria ifanye kazi yake.‘Lakini kafanya kosa gani, ..la uzinzi au….kavunja miiko ya ndoa, hahaha, kama hilo sitaweza kumsamehe kamwe..anafahamu hilo kabisa, sasa kama alifahamu hivyo kwanini akafanya hivyo…na kinachotakiwa ni ushahidi, na ushahidi mnzuri ni huo wa mtoto, kumbe ndio maana,….‘Na baya zaidi kama wanavyodai watu , kama ni kweli kuwa katembea na rafiki  yangu…mbona nitaumia sana, …hapana..hili sitawasamehe kabisa, ni lazima nifanye jambo, ni lazima nimuonyeshe baba yangu kuwa ninaweza kushika hatamu zake…’nikasema‘Kwa vyovyote iwavyo, …mume wangu ana makosa, na kama alitembea na rafiki yangu, basi wote wamenisaliti,..na bahati nimkute …kwanza nitamuokoa na hao watu, lakini la pili ni lazima akapambane na adhabu ambayo hataweza kuishau maishani, hataamini kuwa mimi ndio yule rafiki yake..’nikasemaNilikumbuka kuwa mikataba imebadilishwa, kwahiyo sitaweza kuchuku hatua yoyote kwa sasa, hasa kwa mume wangu maana ndio maana pale kwenye ule mkataba waliandika kuwa:`....mume ndiye atakuwa na mamlaka ya mali yote, na maamuzi yote.....’ thubutu, mali yangu mwenyewe, mtu aje aniamulie..hilo halikubaliki, tutapambana hadi tone la mwisho, na ikibidi, nitachukua hatua ambayo watu hawataamini kuwa ndio mimi, mtoto wa muheshimiwa baba.‘Na huyu rafiki yangu nitamfanya nini..maana nsipomfanya kitu kwa hivi sasa hataniheshimu kamwe, ooh, lazima kila nilichopanga na yeye kimkute, haijaslishi yeye ni ni rafiki yangu...’nikasita hapo kidogo nikiwazia adhabu yake.‘Lakini....’hapo nikatulia kidogo..‘Ushaidi upo…mtoto anafanana na nani…na mume wangu, kwahiyo…lakini cha muhimu ni hicho kipimo, cha DNA, nikikipata tu, basi…na lazima watakuwa wamempatia huyo wakili kama wameamua kuandikishana kisheria…‘Na kuna ushahidi wa DNA, unaonyesha kuwa huyo mtoto sio wa mume wako ni wa mtu mwingine ambaye hajatambulikana…’ nikakumbuka maneno ya docta Kwa vyovyote iwavyo, mume wangu kanisaliti,..kawahi kutembea na rafiki yangu vinginevyo asingelikuwa na mashaka hayo, hata kama sio mtoto wake, ..kwanini akawa najihami, hapo hata iwavyo, bado anastahiki adhabu kubwa, …‘Na huyu rafiki yangu kama kweli hajaondoka, kaahirisha safari, basi…nitamuonyesha kuwa mimi ni nani…kuja kwake atakujutia, ni lazima apambane na kile nilichokiahidi…Nilipowaza hivyo nikachukua simu yangu ..nikaanza kuipiga huku natembea mwendo wa kawaida, simu hazitoki, basi nikaona niandike ujumbe wa maneno;‘Mimi ni yule dada niliyekuambia unitafutie wale mabaunsa wa ile kazi, ...nitakuarifu pindi, ..ndio, kuna dada mmoja, kama nikithibitisha kafanya hivyo, nataka tumfunze adabu, ...kabisa kabisa, waweke tayari tayari, nitakuambia yupo wapi, wewe subiria simu yangu.....’nikaandika hivyo na kuutuma huo ujumbe.Mara nikasikia king’ora cha polisi kikisikika kwa mbali sana…‘King’ora cha polisi, kuna nini  tena usiku huu, oh na muda umekwenda, huyu rafiki yangu sio muendaji tena, ngoja, nitamuokoa, lakini usiku huu huu atakipata cha moto…’nikasemaKing’ora cha polis kikanikumbusha yule mtu niliyekutana naye akikimbia.‘Nahisi kuna hatari, kwanini nisirudi tu huko nilipotoka..mbona moyo wangu unakuwa na mashaka…’nikajiuliza lakini sikutaka kushindwa, sikurudi nyuma, nikajikakamua, na kuendelea kutembeaNa kwa muda huo king’ora kilikuwa wazi ni cha polisi, nikasimama kidogo kusikilizia, kuhakiki, kama king’ora hicho kilikuwa kikitokea mjini, au njia ya kutokea Gongolamboto, sikuweza kukisia vyema, maana kulikuwa na sauti kubwa ya mziki. Nikajipa moyo kuwa huenda hawo askari watakuwa na safari zao,...Nikawa nimeshafika eneo nililoeleekezwa,na nilipotupa macho kushoto, nikaona kwenye mlango, maandishi, `WAKILI WA KUJITEGEMEA, MH. MAKABRASHA..‘Mr. Mkabrasha...’nikasema kwa sauti ndogo, huku nikitabasamu.Nikatulia kidogo, maana sasa huenda naingia kwenye matatizo, na nisipokuwa muangalifu ninaweza kuhatarisha maisha yangu, japokuwa watu wengi walioniona na watakuwa mashahidi wangu, kama likitokea lolote, lakini kama wataniua je, itasaidia nini hapoHata hivyo siwezi kujiaminisha sana, kuwa kuna watu wameniona nikipanda juu, kwani watu wote hawo wanaweza kuwa watu wake...wakamtetea yeye.Kwahiyo sasa nifanye nini, na mimi nimeshafika hapo…Kwanza nikavaa soksi za mikononi, maana ukiwa unakwenda sehemu zenye mashaka, ni vyema ujenga tabia ya kujihami, na mimi tabia hiyo nimekuwa nayo mara nyingi, hasa unapokwenda sehemu unazohisi kuwa zinaweza kuwa na hatari ni vyema pia ukajihami na alama za mikononi, lolote linaweza kutokea.Kwa haraka, ..nikazitoa soksi za kinga za mikono nilikuwa nazo kwenye mkoba wangu, Mara nayingi nakuwa na hizi soksi kwenye mkoba wangu.Na nilipohakikisha nimezivaa , ni kitendo cha haraka hapo, japokuwa moyo wangu ulikuwa ukinienda mbio.Nikauendea huo  mlango, ulioandikwa jina la huyo muheshimiwa, nikajaribu kusikiliza kama kuna sauti yoyote inatokea ndani, lakini kulikuwa kimiya, kimiya kabisa,unachoweza kusikilia kwa mbali ni hizo sauti za ving’ora na mziki toka chini,....nikaona nispoteze muda, nikaugonga huo mlango mara tatu...kimiya, mara nyingine tatu kimiyaMwili ukaanza kujenga hisia nyingine, nywele zikaanza kunisisimuka, nikawa nahisi uwoga fulani,....nikakumbuka wale watu chini, waliniambia kuwa huyo muheshimiwa yupo juu, kwenye ofisi yake, kwanini nagonga mlango wake mara nyingi, bila ya yeye kutokea au hata mtu mwingine kuja kunifungulia mlango, nikagonga tena na tena kimiya..Nikaona isiwe taabu nikashika kitasa cha mlango nikakizungusha taratibu, nikaona mlango unafunguka...nikausukuma polepole, ukafunguka kiasi cha mimi kupita, nikaona hapana, nikausukuma, ukafunguka kwa mapana, kiasi cha kuona ndani, nikaona kwe mbele sehemu ya mapokezi, ..kumbe ni ofisi kubwa tu, nikaangalia nje kama kuna mtu anakuja ...hakuna, nikaingia ndani.Na wakati huo vile ving’ora vya polisi, vilikuwa vimeshafika eneo karibu na hilo jengo ni kama vile wanakuja eneo hili, nikaona afadhali, kama rafiki yangu yupo matatani, nitapata wasaidizi, nikapata nguvu, nikaingia ndani, na kuangalia huku na kule nikaona mlango mmoja umeandikwa:OFISI YA WAKILI..., nikaangalia saa yangu ilikuwa saa mbili na nusu, nikausogelea ule mlango, nikagonga,...kimya nikagonga tena, kimiya....mara simu yangu ikaita, nikaizima bila kuangalia mpigaji, nikashika kitasa na kufungua mlango, mlango ukafunguka....Kwanza nilisimama huku nikiangaza macho kukagua hicho chumba na kama kuna usalama,, ilikuwa ni ofisi nzuri tu, ikiwa na kila kitu kinchoweza kupatikana kwenye ofisi za mawakili,na macho yangu yakaenda moja kwa moja kwenye meza, niliona mtu kakaa huku kalala kwenye meza.‘Mhh, huyu jamaa kalewa mpaka kalala kwenye meza..ni kawaida yake nini..’nikajisema hivyo.Alikuwa kalala kichwa kakiweka mezani, lakini ulalaji ule sio wa kawaida, ni kama mtu kalazimishwa, na macho yangu yakatua pembeni yake, nikaona nakala za mikataba, na mmoja kati ya hizo nakala za ni ule mikataba wangu ... nahisi ni ule  waliyotengeneza wao, lakini jamaa anaonekana hajitambui, labda kalewa sana, au ni usingizi gani huo..Hasira zikanipanda, nilitaka nifike kwa huyu mtu nimuinue nimsuke suke, nikifahamu kuwa kalewa, hatakuwa na ubavu wa kupambana na mimi,...na hapo inaonekana kanywa hadi kapitiliza maana pembeni kwake kulikuwa na chupa kubwa ya kinywaji cha pombe kali, na gilasi mbili,....kuonyesha kuwa hakuwa peke yake, nikaachia mlango, na kusogea kuingia ndani, huku king’ora cha polisi kikisikika kwa nguvu, kuashiria kuwa sasa askari wapo chini ya hili jengo.Hata hivyo, akilini mwangu nilikuwa na mashaka, nikijiuliza hawo maaskari wamefuata nini hapo...kusije kuwa kuna matatizo.....nikaona nimalizane na kilichonileta, kwanza nikasogea hadi pale kwenye meza, kwa haraka nikauchuku aule mkataba na kuukagua…ni nakala ya mkataba wangu, ..‘Nahisi walikuwa wakiufanyia kazi…’nikasema kimoyo moyo‘Sasa walikuwa na nani, …?’ Pale mezani kuna gilasi mbili, na zote zipo nusu… kuashiria hawa watu walikuwa wanaongea, alikuwa na mtu mwingine,.Nikaone nisipoteze muda, nikaona nimuamushe huyu mtu nimuulize rafiki yangu yupo wapi, na kwanini, kaingilia maswala ya familia yangu kwa kuharibu mkataba wangu na mume wangu,...nilipofikia hapo kimawazo sikujali mambo ya polisi, nikasogea upande ule aliokaa huyo jamaa ili kukabiliana naye....Ni wakati huo huo, nasogea na mara macho yangu yakatua pale alipolala huyo jamaa, nikaona kitu kilichonishitua, nikaganda, nikarudi kinyume nyume na kugonga ukuta, nikafanya vitu vilivyokuwa nyuma kwenye kimeza kidogo kudondoka,..ule mlio wa kudondoka hivyo vitu ukanishtuaKwa haraka , nikashika mdomo,...kujizuia,..lakini haikuwezekana, nikajikuta nimepiga yowe, unafahamu yowe, sijawahi kupiga yowe kama hilo....na mara nikasikia mlango wa hiyo ofisi ukifunguliwa, .....Tuendelee kidogo, mmh, kidole kinauma......wikiendi njemaNB: Kwa leo,..hapa hapaWAO LA LEO:Kila kazi ina utaalamu na utendaji wake, na pia kuna taratibu zake, ndio maana watu wanakwenda kuzisomea hizo kazi, tusijifanye kuwa tunafahamu kila kitu, eti kwa vile ulipitia pitia shuleni, kuna vitabu umesomasoma , hiyo peke yake haitoshi ...Ndio maana kuna taaluma tofautitofauti, na kila taaluma, ina mabingwa wake, ina wataalamu wake, ina watu wanapewa madaraja na nyazifa mbalimbali, kuonyesha kuwa hizo ni fani zinazojitegemea, tusipende kujiingiza kwenye kazi za watu ambazo huenda ni za kitaalamu zaidi, na kujifanya tunaufahamu nazo, ilihali hatujazisomea, tujue kuwa  kuongea na kutenda ni vitu viwili tofauti,..tuweni makini na fani za watu jamani.Sikuamini, sikutarajia kuwa siku moja na mimi nitaionja jela, mtoto wa muheshimiwa, familia ya kitajiri,  pamoja na elimu yangu yote, pamoja na ujanja wangu wote…, pamoja na sifa ya familia yangu, hayo yote hayakusaidia kitu, ...nikajikuta na mimi naingia ile sehemu niliyoifahamu mimi kuwa ni sehemu ya wahallifu, ....‘Jela….’‘Siwezi kwenda jela mimi, kwa kosa gani, ..’nakumbuka siku moja nilikuwa nabishana na rafiki yangu  nikamwambia hivyo, ....ilikuwa tunaongea mambo yanayofanana na  maswala ya jela, na yeye akaniambia, katika dunia hii huwezi kujithibitishia moja kwa moja kuwa huwezi kuingia jela, maana hujafa hujaumbika lolote laweza kutokea‘Kwanini niende jela wakati natii sheria, nijiepusha na makosa, maana mpaka mtu uende jela, ina maana umetenda makosa makubwa, au sio…’nikajitetea hivyo.‘Unaweza ukajitahidi hivyo, unaweza ukajihakikishia hivyo, lakini ukumbuke una watu wapo chini yako, wenye kaliba tofauti tofauti, pia wewe mwenyewe unaweza ukajitolea kufanya jambo kwa huruma zako,.., kumbe unajipeleka kwenye makosa bila kujijua...’akasema‘Lakini hapo sheria si ipo, nitajieleza, au sio…?’ nikasema‘Inaweza ikatokea bahati mbaya sio wote waliopo kifungoni wana makosa kwa asilimia mia..wengine ni hiyo bahatio mbaya tu, au dhuluma tu za watu wenye masilahi yao…’akasema‘Mhh, mungu aniepushia na hiyo bahati mbaya....’nikasema.**********‘Unashikiliwa kwa kosa la mauaji ya Makabrasha…’sauti hiyo ilijirudia sana kichwani mwangu‘Mimi sijamuua Maka-brasha…’nilijitetea lakini haikusikilizwa.***********Nikakumbuka jinsi polisi walivyonikamata…‘Simama, upo chini ya ulinzi….’ilianzia hapo, wakati huo natetemeka nimeshikilia mdomo kukwepa nisiendelee kupiga kelele..Waliingia askari polisi wakafanya upekuzi wao, baadae wakanijia na kusema;‘Tuambie ilikuwaje..’akaanza huyo askari‘Mimi sijui, niingia hapa kama nyie, nikamkuta hivyo hivyo..’nikasema‘Ulikuja kufanya nini usiku, huu ni muda wa kazi..?’ akaniuliza, na mimi nilitaka kumjibu kijeuri kuwa kama sio muda wa kazi yeye alikuwa akifanya nini ofisini, lakini muda kama huo ilitakiwa niwe mpole.‘Kuna mtu nilikuwa namtafuta, na niliambiwa yupo hapa, nilipofika ndio nikamkuta huyo mtu yupo hivyo..’nikasema‘Madam inabidi tukushikilie kwa utaratibu wa kipolisi, wewe utaisaidia polisi kwa vile umepatikana hapa kwenye tukio, kwahiyo unakuwa mshukiwa namba moja wa kifo cha Makabrasha....’nikaambiwa‘Eti nini, ....’nikang’aka!‘Ndio hivyo, tafadhali tulia pale, kila maelezo yako hapa yatachukuliwa kwa mujibu wa sheria…’nikaambiwa sasa kwa sauti kama vile mimi ndiye muuaji.‘Mimi sio mhalifu, kwanini hamtaki kunielewa, nimeshawaambi kuwa nilifika hapo ofisini kwa Mkabrasha, nikimfuata rafiki yangu, ambaye nilihisi yupo matatani, na nilipoingia humo kwenye ofisi ya Makabrasha nilikuta kama mlivyomkuta nyie,sijui lolote zaidi, tusipoteze muda, mhalifu anapata mwanya wa kutoweka ..’nikasema‘Sawa, hatupotezi muda hapa, tunafanya kazi yetu, na sio sisi tu wapo wengine wanafuatilia kila mahali kuhakikisha mhalifu aliyefany akitendo hiki anapatikana, kama ni wewe au yoyote yule..’akasema‘Mimi nina ushahidi waulizeni walinzi, huko chini nilipita bila hata silaha, walinzi wake walinikagua, mimi sijui aliuwawaje huyu mtu, kama ni kosa lianzie kwa hao walinzi, silaha ilipitaje ...’nikajitetea.‘Usiwe na shaka hayo yote yatafuatiliwa,…’akasema na mara akatupa macho chini akaiona ile bastola, mimi nilishaiona , niliiona wakati ndio wanaingia na kuamrisha kuwa niweke mikono chini, lakini sikuweza kufanya kitu, bastola ilikuwa karibu na migu yangu imefunikwa kidogo na kitu sio rahisi kuiona kwa haraka, na hata wakati wanakagua walikuwa hawajaiona, sasa kaiona huyu polisi.‘Hii bastola ni ya nani?’ akaniuliza akinionyesha ile bastola, ikiwa karibu sana na miguuni yangu, wengine wakaiona wakaja wakapiga picha,...baada ya tukio hilo, polisi akiwa na tahadhari, akaichukua alikuwa kavaa kinga, akaikagua na wakati anafanya hivyo na mimi ndio nikapata mwanya wa kuikagua..!Pale pale nilihis moyo ukilipuka , bastola, ilionekana kama yangu,..lakini nina uhakika bastola yangu ipo kabatini, sizani kamaa hiyo silaha ni yangu;‘Mimi sijui..itakuwa labda ya huyo mhalifu au ya huyu huyu marehemu, ni kwanini unaniuliza hivyo, mimi sikuingia na silaha humu ndani..’nikasema‘Hii bastola ilikuwa miguuni mwako, au sio, ina maana uliidondosha wakati tunaingia au sio..wewe unamiliki bastola..?’ akaniuliza‘Ndio…namiliki bastola lakini mimi sijafika na bastola humu ndani,..’nikasema‘Hebu iangali vizuri hii silaha, haiwezi ikawa ni yako..?’ akaniuliza‘Kwanini unaniuliza hivyo, mimi sijaingia na bastola humu ndani, na …nimeiona wakati maningia, sikuwa nimeiona kablsa..’nikasema kwa ukali.‘Nimekuona ulivyobadilika baada ya kuiangalia hii bastola, na hisia zangu zinanituma hivyo, kuwa hii silaha unaifahamu, tuambie ukweli, hii bastola ni ya nani..?’ akauliza kwa sauti ya ukali‘Nimkuambia mimi sijui…usinilazimishe kwa kitu ambacho mimi sikijui,..’nilisema Kiukweli ningekuwa nimeiona mapema, nisingelisimama karibu yake, au ningeipiga teke iende mbali na migii yangu..na mbona hiyo bastola inaonekana kama yangu wakati bastola yangu ipo nyumbani.‘Na kwanini umevaa hizo gloves mkononi..?’ akaniuliza‘Ni kawaida yangu, hata nikiwa ofisini wakati mwingine unaweza kunikuta hivi hata nyumbani kwangu ni hali niliyojijengea ya kujihami, kiafya..’nikasema.‘Umesema unamiliki silaha, …si ndio?’ akaniuliza‘Ndio…’nikajibu‘Na una uhakika kuwa silaha hii sio hiyo silaha yako unayomiliki…maana tutakwenda kuhakiki…?’akasema‘Mimi nina uhakika kuwa silaha yangu ipo nyumbani..’nikasema‘Silaha yako ni aina gani..?’ akauliza akiwa kaishikili hiyo bastola sasa wakihifadhi kwenye mfuko wa plastic, ni baada y akupiga picha sehemu ilipokuwepo na baadae wakaipiga picha bastola yenyewe ikionyesha namba zake.‘Ni bastola..nikama hii..lakini…’hapo nikasita nikiichunguza vyema, lakini sikuishika‘Aaah, kumbe unajua eeh, huku unajifanya hujui, kumbe hii ni bastola yako eeh, ....’akasema.‘Nimesema inafanana..’nikasema‘Sisi ni lazima tuchukue maelezo yako yote haya, na uweke sahihi …’akasema‘Siwezi kufanya hivyo, kwa vile mimi nina wakili wangu, sitafanya lolote kwa hivi sasa mpaka afike hapa ..’nikasema‘Wewe umesema huna kosa, wakili wa nini..?’ akaniuliza‘Ni haki yangu kufanya hivyo, ..wakili nimemuajiri wa nini..’nikasema‘Hebu muweke pingu…’akasema huyo askari, akimuarisha mwenzake.‘Kwanini mnanivalisha pingu, mimi sio mhalafu, niacheni ..siwezi kuvaa hiyo pingu mnanielewa ...’nikalalamika, na yule kiongozi wao, akaniangalia kwa makini na kuonyesha uso wa kushangaa, halafu akasema;‘Mwacheni msimtie pingu, nimeshamfahamu huyu mwanamke, wewe si ndio yule tajiri wa kampuni ya…, ile kubwa inatwaje vile...na baba yako ni…ok, ni wewe eeh?’ akaniuliza huku akijaribu kufikiria na mimi sikutaka kujulikana kwa watu,nikasema;‘Nimeshawaambia kuwa mimi sijui lolote kuhusiana na hili, ....’nikasema huku nikikwepa kuangalia pale alipolala Makabrasha, na niliona nisipokuwa mwangalifu , nitazalilika, tajiri mkubwa, …Tajiri mkubwa, leo kakamatwa kama mhalafu, je vyombo vya habari vikifahamu hili itakuwaje, nikajaribu kuwazia jinsi gazeti litakavyoandika, kwa maandishi makubwa wakikolzea uwongo, ili tu gazeti linunuliwe, ...na kama wakiniona nina pingu mkononi, watanipiga picha na kuiweka ukurasa wa mbele, hapana, ....hapana....‘Twendeni huko kituoni kwenu mimi nitaongea na mkuu wenu....’nikasema kwa kujiamini.‘Hamna shida mama, huko tutakwenda lakini kwa hivi sasa tuna kazi ya kufanya, kama hutaki matatizo, subiri hapa, tumalize kazi yetu, ukileta matata, tutakufunga pingu...’akasema huyo kiongozi wao, na mimi nilikaa pembeni nikiangalia wanavyofanya,nikatulia kimiya hadi walipomaliza kazi yao, na kuanza kunihoji tena..‘Mimi siwezi kuongea lolote mpaka wakili wangu awepo, na mtu ninayeweza kuongea naye ni mkuu wenu ,sio watu kama nyie...’nikasema kwa nyodo.‘Sawa madam, hakuna shida utaenda kuongea naye...’wakasema na kunichukua hadi kituoni cha polisi.., bila ya kufungwa pingu. Nashukuru kuwa nilipotoka pale nje, sikuonana na watu wengi, nilijitahidi kuficha uso wangu, ..sizani kama kuna mtu anayenifahamu au kuona sura yangu.********* Nilionana na Mkuu wa hicho kituo kesho yake, alikuja  na kuniambia kuwa kiutaratibu inabidi nipelekwe Segerea kwa vile mimi ni mshukiwa wa mauaji, na hapo kituoni kwao, sio sehemu ya kuweka washukiwa wa uhalifu mkubwa kama huo, wa kesi ya mauji.‘Lakini mimi sio muuaji, na wakili wangu bado hajafika..’nikalalamika.‘Sisi kwa utaratibu inabidi tukushike, kama mshukiwa , hadi hapo tutakapothibitisha ukweli wa mauaji hayo, kama huhusiki, utaachiwa huru, kama unahusika, basi sheria itachukua mkondo wake, hizi ndizo taratibu zetu, na kama unasema huwezi kuongea lolote mpaka wakili wako afike, basi utakutana na wakili wako huko Segerea , hatuwezi kukuweka hapa....’akasema mkuu wa kituo ambaye nilipopelekwa hapo kituoni usiku huo niliomba nionane naye, nikijua kuwa yeye ataweza kunisikiliza, lakini wapi...‘Hamuwezi kunipeleka huko kabla sijaonana na wakili wangu…’nikasema‘Lakini mwenyewe nasikia umekiri kuwa bastola iliyoonekana mle ndani, ni mali yako,..na hiyo bastola ndiyo iliyotumika kwenye mauji..na pia kuna kumbukumbu za kurekodiwa zilizogunduliwa, zilizoachwa na marehemu zilizokuwa zikonyesha kuzozana kati yako na Marehemu ukimtishia usalama wake, uzuri ni kuwa yeye alikuwa na tabia ya kutembea na vyomvo vya kunasia sauti , na hii itatusaidia sana kama ushahidi.....’akasema mkuu wa kituo.‘Hayo yalikuwa ni mazungumo tu, unaweza ukaongea kwa hasira, huyo jamaa alikuwa kifanya hivyo kwa mbinu zake, za kuwatishia watu, lakini sivyo kama mnavyofikiria nyie, kama mngelimfahamu vyema huyo mtu, msingalijisumbua kumtafuta muuaji, huyo mtu ana maadui wengi...’nikasema.‘Kila raia ana haki yake, hata kama ni jambazi, bado atalindwa na sheria hadi hapo itaapothibitika kuwa ni mhalifu,....hayo tuachie wenyewe, ila wewe kama mshukiwa, unastahili kutendewa mambo kadhaa, ili sisi watendaji wa vyombo vya usalama, tuweze kufanya kazi yetu vyema....na kama ulivyosema huenda alikuwa na maadui wengi, na mmojawapo anaweza kuwa ni wewe kutokana na ushahidi tulioupata....’akasema.‘Kukamata watu wasio na hatia ndio mnajisifia kutenda kazi yenu vyema, muda ule mngahangaika huku na kule mngeliweza kumkamata huyo mhalifu, nyie, mnakimbilia kunishika mimi, na mnampa mhalifu mwanya wa kukimbia mbali au kujificha kabisa...’nikasema.‘Nikuulize tena, Je silaha iliyopatikana mle ndani, ni silaha yako au sio yako?’ akaniuliza.‘Sio silaha yangu silaha yangu ipo nyumbani,…’nikasema‘Unaweza kunitajia namba za silaha yako…’akasema‘Sijaikariri kwa kichwa…’nikadanganya hivyo, wakati hiyo silaha naifahamu namba yake kwa kichwa.‘Silaha yako nyumbani inaiweka wapi, ..?’ akaniuliza‘Naiweka kwenye kabati, na nina uhakika itakuwa huko huko,…’nikasema.‘Hebu iangalie vizuri hii silaha, , ...na namba yake siunaikumbuka namba yake,..hii hapa iangalie vizuri, ni silaha yako au si yako?’ akaniuliza, na mimi nikaiangalia kwa makini, ilikuwa ni silaha yangu, kulikuwa na alama yangu, hakuna ubishi, nikasema;‘Inaonekana kufanana na silaha yangu,  lakini ili nirizike mpaka nifike nyumbani ....kwani inanipa mashaka, ni nani aliyeweza kufungua kabati langu la siri, na kuichukua hiyo silaha,...siwezi kuhakikisha hilo, mpaka nifike nyumbani nione wa macho yangu...’nikasema.‘Mama, kila mtu anapopewa silaha, wengi wanazikariri nambe zake, nah ata kuweka alama ya siri, hii silaha ni yako au sio ya kwako?’ akaniuliza.‘Jibu langu ni hilo hilo, inaweza ikawa ni silaha yangu, siwezi kukataa, maana namba japokuwa sikumbuki vyema, lakini inakuja kuja kama namba yangu, sina uhakika…’nikasema‘Tungelipenda utoe ushirikiano, kama kweli wewe sio mhaifu, ukizidi kutudanganya ndivyo utakavyozidi kushukiwa, hata kama huenda sio wewe uliyefanya hayo mauaji..’akasema‘Nimesema hivi, hiyo silaha inafanana kama silaha yangu, lakini silaha yangu ilikuwa kwenye kabati, naona ajabu imefikaje hapo, hiyo sio silaha yangu, ni kufanana tu….’nikasema na huyo mkuu akacheka kuonyesha kuwa mimi najaribu kudanganya.‘Kama ni silaha yako, imefikaje kwenye tukio la uhalifu,..hebu tuambie ni nani mwingine anayefahamu wapi unapoiweka hiyo  silaha yako?’akaniuliza.‘Mume wangu, lakini yeye ni mgonjwa...yupo hospitalini.’nikasema.‘Na kwahiyo anabakia wewe mwenye kuweza kujua wapi silaha ilipo na kuichukua na kuitumia, kwa hali kama hiyo inabidi tusikuachie, na dhamana yako itakuwa ngumu kupatikana...’akasema‘Mnafanya kama kunikomoa au..?’ nikauliza‘Kwanini tufanye hivyo,…ila usijali sana bado tunafanya uchunguzi wa kina, kuthibitisha hilo, kama risasi iliyomuua marehemu imetoka kwenye hiyo bastola, kwa ujumla mama una kesi ya kujibu, ...’akasema kwa upole‘Niitieni wakili wngu, siwezi kuongea zaidi..’nikasema‘Ni kwanini ulikuwa umevaa kinga za mikononi,…?’ akaniuliza‘Ni kawaida yangu kuvaa hivyo, ninapokwenda sehemu nisiyokuwa na uhakika nayo, kiusalama na kiafya..’nikasema‘Ni kawaida yako…ina maana una uzoefu na mambo hayo…’akasema kwa upole‘Kwahiyo nyie mlitaka niseme uwongo, kuwa silaha sio yangu au?’ nikawauliza kwa ukali.‘Ukweli wako ndio unaoonyesha kuwa wewe unaweza kuwa mshukiwa wa maujai hayo..na vielelezo vilivyopatikana kwa muda mfupi vinathibitisha hivyo, ili kuokoa muda, ungetuambia ukweli wote kuwa wewe ulimuua huyo jamaa kwasababu kadhaa, kama hasira au kisasi, na sisi tutaona jinsi gani ya kukusaidia,....’akasema huyo mkuu wa kituo, na wakati huo alikuwepo mpelelezi aliyenikamata‘Sijafanya hivyo hamnielewi, sikuwa na haja  yoyote ya kumuua Makabrasha, na sikuwa na silaha ningelimuuaje, angalieni na muda wa mauaji , mimi nilifika yameshafanyika, ...nyie naona hamtaki kujisumbua kumtafuta huyo muuaji, na naona hamtaki kunielewa,  naona tumsubiri wakili wangu, sitaki tena kuongea lolote....’nikasema.‘Sawa lakini mwisho wa siku ukweli utadhihiri...’wakasema.******Baadaye alifika mkuu wa upelelezi akawa anaongea na mkuu wa hicho kituo, na huyu mpelelezi, wakawa wanaonyeshana vidhibiti, ikiwemo hiyo silaha, na soksi za mkononi,…na ushahidi wa vyombo vya kunasia sauti walivyovipata kwenye nifa vya Makabrasha, na baadaye wakasema kuwa inabidi mimi nipelekwe Segerea huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.‘Mimi Siwezi kwenda huko Segerea kwa kosa gani....?’nikalalamika.‘Utakwenda tu …hakuna ubishi, sisi tunatimiza wajibu wetu ....’akasema huyo mkuu wa kituoa. Na hapo nikawa sina la kufanya,ikabidi nitii amri, na baadae wakaniingiza kwenye karandinga, eti kama mshukiwa wa mauaji, hadi huko Segerea.Ndio ikawa mara ya kwanza kuingie jela…usiombee hili likukute jamani jela sio seehmu ya mchezo, hata ukiitwa mahabusu,…sikuona tofauti ya mahabusu na mfungwa wote tulichanganywa humo..Itakuwaje sasaWAZO LA LEO: Ni kweli Jela ni kwa wakosaji, lakini je ni wote wanafikishwa huko wana makosa. Kuna ambao wanafikishwa huko kwa sababu tu ya kutetea haki, wengine kwa chuki binafsi, je hawa ni nani atakuja kuwalipa haki zao. Huu ni mtihani mkubwa sana kwa wanaoshika dhamana hii, na mtihani zaidi kwa yule aliyekutanika na adhabu hii ambayo hakuitenda, na mtihani tena sana kwa wanafamilia wa huyu mhanga.Tumuombe mola atuepushie na mitihani hiyo na wale waliofikwa na mitihani hiyo mola awape subira na awajalie waweze kuishinda mitihani hiyo na haki iweze kutendeka. Aamin Usiku sikulala,.nilimuomba sana mola....hadi kunapambazuka macho mazito, usingizi hakuna, lakini macho yanataka kulala...akili haitaki..na hatimaye kukapambazuka, na kama ilivypangwa...baada ya muda, gari likaja huyo ..ikawa safari ya kwenda Segerea..sikuamini..lakini ndivyo ilikuwaTuendelee na kisa chetu...************Nilipitiwa na usingizi njiani, tahamaki nikafikishwa Segerea.,!Tulipofika huko nikashangaa kuona gari la docta rafiki wa mume wangu, limeshafika, hapo nikajiskia faraja kidogo, japokuwa nilikuwa kwenye wakati mgumu, na kujutia kwa nini nilimkaidi, nilifahamu maneno gani yatamtoka huyu mtu, nikamuanza  mimi kuongea pale aliponisogelea;.‘Sasa ndio umefuata nini, muda wote ulikuwa wapi, umeacha mpaka naletwa Segerea, kwanini hukufika mapema nikiwa kituo cha polisi,....huku unasema unanijali, eti unanilinda?’ nikaanza kumlaumu.‘Wewe hujui tu, tulivyohangaika, kwanini ulikuwa hupokei simu..?’ akaniuliza na mimi sikuwa na la kusema nilitaka kusikia tu kuwa labda wamefanya jambo lolote ili nisilale hapo Segerea.‘Ina maana mlikuwa mnafahamu kuwa Makabrasha kauliwa?’ nikauliza.‘Nilijua baadae sana…yaani we acha umetupa wakati mgumu sana, sasa hata sijui lakini ngoja tuone…’akasema‘Ina maana…’nikataka kusema‘Niliamini kuwa utakwenda nyumbani kwako maana muda ulishakwisha, japokuwa bado nilikuwa na mashaka moyoni, lakini bahati akaja mgonjwa, ikawa nipo kwenye heka heka za kumhudimia,..nilipata mwanya nikakupigia ukawa hupokei, yaani mpaka namalizana na huyo mgonjwa, muda umekwenda, ndipo napokea simu kutoka kwa watu wangu wananielezea kuhusu hilo tukio..’akasema‘Aaah, hata sijui …’nikasema na yeye akanikatisha kwa kusema;‘Lakini hayo tutaongea baadaye, ila nahisi hawa watu wa usalama hawakutaka nifahamu wapi ulipo mapema…, kwani nilipopata taarifa usiku huo huo, nilianza kukufuatilia mimi mwenyewe, nikafika hadi hapa ulipokuwa umeshikiliwa nikaambiwa haupo…’akasema‘Kwanini walifanya hivyo..?’ nikauliza‘Sijui…usiku huo huko nikaenda hadi makao makuu ya polisi, ...nashukuru jamaa yangu, alipopata hiyo taarifa, alifuatilia na kugundua kuwa upo huko nilipotoka, nikarudi tena hapo sikuruhusiwa hata kukaribia hicho kituo....’akasema.‘Ok, ok…Sasa niambie umefikia wapi au umechukua hatua gani?’ nikamuuliza.‘Kwanza niliwasiliana na mkuu wa upelelezi wa anayeshughulikia kesi yako, na akasema kuwa kiukweli vithibitisho vilivyopatikana vinaonyesha kuwa wewe ni mshukiwa muhimu, na sio rahisi kukwepa hilo, na hata dhamana inaweza kuwa ngumu kupatikana, ....’akasema‘Kwanza nikuulize wewe ulifahamu muda gani kuwa huyo mtu alishafariki, ..?’ nikauliza‘Nilifahamu baada ya kupigiwa simu na watu wangu wakati huo umeshakamatwa…’akasema‘Kwanini sasa ulikuwa ukinipigia simu, ni kama vile unafahamu kilichopo mbele yangu au sio..?’ nikauliza‘Ulipotoka hapa nikapata huyo mgonjwa nikawa bize, na nilipopata nafasi ndio nikawa nakupigia simu, kuhakikisha kama umefika nyumbani na muda huo nilikuwa sijajua lolote, unielewe hapoa..’akasema‘Sasa mtafanya nini, mnakubali mimi nilale huku Segerea..?’ nikauliza‘Polisi wanadai bado wanafanya uchunguzi, kujirizisha kuwa kweli wewe ni mshukiwa muhimu au kuna watu wengine, wanasema wanaogopa ukipewa dhamana utatumia utajiri wako kuharibu ushahidi, ....na kinachowatatiza  ni muda wa hayo mauaji....’akasema.‘Muda…eh, wanasemaje hapo , najua hapo nitawashinda, ..hawataki kufany akazi yao vyema, mimi nilifika mtu keshauwawa…hata damu zinaonyesha …zilikuwa kama zimeganda…sikuweza kutazama vyema lakini ndio hivyo..na kama vipimo vyao vipo sahihi wataligundua hilo..’nikasema‘Vipo sahihi…wameshaligundua hilo…’akasema‘Na hapo ndipo inaonyesha wazi mimi wamenishika kimakosa...na kama wanalifahamu hilo kwanini wanileta huku, …aah, sijui ni nani kafanya hayo mauaji, kaharibu kila kitu, kaniharibia …hata sijui nisemeje,  aheri ningelifahamu,...au unafahamu lolote kuhusiana na huyo muuaji.?’nikamuuliza  nikimwangalia, nay eye akatabasamu na kusema.‘Wanasema kuwa ni kweli wewe ulifika wakati Makabrasha keshauwawa, hata hivyo, wao wanadai kuwa inawezekana wewe ndiye uliyetuma mtu au watu kufanya hivyo, na wewe ukafika hapo kufuatilia ili kuthibitisha, au kuchukua baadhi ya nyaraka,ulizozitaka..’akasema‘Hawo watu wana wazimu, nyaraka gani nilikuwa nazifuatilia mimi, wakati nilikuwa nakwenda kumuangalia rafiki yangu, kama nilivyokuambia nahisi yupo kwenye matatizo, ni wema na huruma vimeniponza, ooh ...’nikasema kwa ukali na kabla hajajibu kitu nikasema.‘Yah, wema na huruma zako, pole…’akasema‘Wakili wangu hajafika maana wewe sikuoni kama utaweza kunisaidia lolote kwa hivi sasa..?’ nikauliza.‘Tatizo wakili wako hayupo hapa Dar, ila keshapigiwa simu, anaweza akafika leo hii, kaambiwa apande ndege ili awahi kufika sasa sijui maana anauguza mzazi wake, si unalifahamu hilo…’akasema‘Sasa wanaposema nilifuata nyaraka , nyaraka gani hizo…?’ nikauliza‘Wanasema kuna Mikataba miwili ilionekana juu ya meza, mmoja ni mkataba kati yako na mume wako, na kuna mkataba mwingine, huo mkataba mwingine hawakutaka kuusema unamuhusu nani, wanasema kwa hivi sasa itakuwa siri yao, kwani unaweza kutumika kama ushahidi mahakamani ...’akasema‘Ni siri yao kwa vipi..?’ nikauliza‘Kwa mtizamo wao wewe huenda ulikuwa ukitafuta hiyo mikataba au mambo yanayohusiana na hiyo mikataba. Na kuna vielelezo wamevipata vinavyoonyesha kuwa wewe na marehemu mlikuwa hamuivani,…’akasema‘Vielelezo gani hivyo..?’ nikauliza kwa haraka maana askari alionekana kuja kunichukua.‘Ni vielelezo vya kurekodiwa,  ni kazi ya Makabrasha, yaonekana alishajiandaa vyema kukuharibu, kuna ushahidi mwingi, wa sauti yako ukigombana nay eye, na wewe ukitoa kauli za vitisho dhidi yake, na kuna CD siunajua tabia yake ya kurekodi mazungumzo ya watu, kwenye mkoba wake ana mitambo hiyo ya kurekodi, anatembea nayo....’akasema.‘Ni kweli niliona hiyo mikataba pale mezani wakati naingia kwa Makabrasha, lakini sikupata muda wa kuisoma, ila nahisi mmoja kati ya hiyo mikataba ni ule mkataba waliouchakachua,....sikupata ujasiri wa kuusoma kwa haraka.., kwani kwa muda huo ndio niligundua damu, zikiwa zimatuama juu ya meza, kuashiria kuwa Makabrasha kauwawa...........’nikasema.‘Na ni wakati wanaingia hawo maaskari polisi nahisi kuna mtu aliwapigia simu waje..na wakati wanaingia ndio nikaona bastola ipo karibu kabisa na miguu yangu, imefunikwa kidogo na kiti, ilikuwa sio rahis kuiona mpaka ufike pale niliposimama…’nikasema‘Wakaionaje sasa..?’ akauliza‘Kwa muda huo watu wao walikuwa wakichunguza, na muda wote walikuwa hawajafika pale niliposimama, unajua pale nilikuwa kama nimeganda, siamini ninachokiona…kashfa, kashfa…ni mpaka pale aliponisogelea huyo askari wao, ni kiongozi wa hilo kundi lililofika, akaanza kunihoji…Wakati anafanya hivyo ndio akaiona hiyo bastola..’nikasema‘Una uhakika hukuwa nayo silaha yako wakati unafika hapo kwenye tukio..?’ akaniuliza na mimi nikamuangalia kwa jicho baya.‘Ina maana huniamini, sijamuua, mimi…silaha sikuwa nayo bwana, ..’nikasema‘Sio sikuamini, unaweza ukawa ulitembea nayo, au sio, si ulisema kuwa kutokana na hali ilivyo usiku utakuwa unatembea na silaha..?’ akaniuliza‘Sijawahi kuichukua tokea siku ile nilivyokuambia, niliongea tu,..na silaha yangu muda wote ipo kabatini, nimeifungia hapo, na mimi ndiye mwenye ufunguo wake…’nikasema‘Je mume wako hana nakala ya ufunguo huo wa kabati..?’ nikauliza‘Hapana kuna makabati yeye hana nakala ya funguo zake…, na hilo nimojawapo, lakini yeye anafahamu , akitaka kulitumia mimi huwa ninampatia ufunguo..mara nyingi hana kazi yoyote na hilo kabati, maana vitu vilivyopo ni vyangu vya kike kike tu, unasikia…, hana haja na hilo kabati kabisa, hata hivyo yeye yupo hospitalini, anaumwa, huwezi kumshuku kwa hilo…’nikasema‘Na ndio hapo inapokuwa kesi ngumu kwako, na inakuwa vigumu kuwathibitishia viginevyo, vipi funguo unazo, kabati lifunguliwe na..…’akasema‘Hapo hata mimi sijui kwakweli..’nikasema na niliona kama docta ana mashaka na mimi.‘Ulipofika chumba cha Makabrasha, uliiona hiyo silaha kabla polisi hawajaingia au ilikuwa wapi, ..?’ akaniuliza‘Ilikuwa sakafuni, nilishtuka naikanyaga wakati huo polisi wameshaingia na kuniamrisha niweke mikono juu, ndio hapo na mimi nikaiona hiyi silaha, muda wote nilikuwa sijaiona,..ilikuwa hapo sakafuni, karibu kabisa na mguuni kwangu, yaani hapo ndio nguvu zikaniishia ....’nikasema‘My, my….miguuni mwako na usiione wakati wote,…hapo inaashiria nini, kuwa muuaji, alifanya hivyo, akaiacha hiyo bastola hapo ili polisi waione, lakini sasa mbona ilikuwa miguuni mwako…’akasema‘Mimi sijui..nilikuwa natembea kumshtua marehemu nilijua kalewa, kulikuwa na chpa kubwa ya pombe mezani na gilasi mbili..’nikasema‘Mhh …uone hapo sasa, ilikuwaje ikawa miguni mwako,…hapo itaonekana ulikuwa nayo, ukaidondosha sakafuni, kwa kuchanganyikiwa.....’akasema.‘Mbona unakuwa kaam huniamini jamani, kama wewe huniamini polisi itakuwaje…’ nikasema sasa nikichezesha chezesha miguu kitoto vile..‘Mimi nataka kufahamu ukweli ..na kudadavua jinsi gani ya kuweza kusaidia…siokwamba sikuamini, mimi ninaamini unachoniambia ndio ukweli, au sio…’akasema‘Najiuliza  ni nani ambaye alifahamu kuwa nitafika huko, zaidi yako wewe, maana hata watu wangu sikuwahi kuwaambia?’ nikamuuliza.‘Kuna mtu utakuwa uliongea naye kwenye simu labda au alikuwa akikufuatilia, bila ya wewe kufahamu, …au…’akasema na mimi nikamkatili kwa kusema;‘Mtu niliyeongea naye ni rafiki yangu, nilimtumia ujumbe wa maandishi, hakuna mtu mwingine niliyemwambia kuwa nakwenda huko, kwa Makabrasha ...na sijui labda simu yake ilikuwa mikononi mwa hao watu, hususani marehemu, kama alikuwa nayo.....’nikasema.‘Kabla hujafika kwangu uliongea na rafiki yako..?’ akaniuliza‘Ndio, …ndio yeye alinielezea kuhusu kuibiwa mtoto wake, na baadae wakampigia simu kuwa mtoto wanaye wao, na …katika kuhangaika wakaukubaliana na hao kuwa atimize matakwa yao, akaletewa mikataba aweke sahihi na kukubaliana nayo…’nikasema na hapo nikakumbuka jambo‘Mkataba..mkataba gani huo…?’ akaniuliza‘Mim sijui maana sijawahi kuuona na…ndicho kilinisikuma sana nifike nionane na huyo rafiki ili nifahamu kinachoendelea…’nikasema‘Hebu kumbuka vyema wakati unaongea na huyo rafiki yako aliongea ni ni zaidi cha kusaidia labda…?’ akaniuliza‘Unajua nimekumbuka kitu wakati naongea na huyo rafiki nilisikia mtu kama anamkatiza kuongea jambo, ni sauti ya mtu yaonekana alikuwa karibu yake,…ndio hapo simu ikakatika…’nikasema‘Huenda atakuwa ni huyo huyo Makabrasha, kama walikuwa naye karibu au kama kulikuwa na mtu kamshikilia..hilo bado halisaidii kitu..’akasema‘Mimi nahisi  kuna mtu mwingine,alitokea wakati unaongea nami, hakuzima hapo hapo, nikawa nasikia wakiongea mambo, lakini sikuyasikia vyema,..baadae ndio akazima hiyo simu ...’ nikasema.‘Hiyo yote yawezekana ikawa ni geresha tu ya rafki yako, mimi bado sijamuamini kihivyo..’akasema‘Lakini hapo ilikuwa mapema sana, kwenye saa kumi na moja hivi....sina uhakika sana ilikuwa ni saa ngapi, ila ilishaanza kuingia jioni...na muda huo huyo muuaji anaweza alikuwa hajafikia, kama ni mtu aliyekuja baadaye kufanya hayo mauaji..’nikasema‘Mauaji yalifanyika baadae…usiku..wanasema ni kati ya saa moja hadi saa mbili hivi, saa mbili na nusu…na hili linakuweka mbali kidogo na hayo mauaji, lakini hoja hiyo bado haitii nguvu kukuweka mbali na kadhia hiyo kwani wanakushuku bado ni wewe unahusika kwa namna moja au nyingine..’akasema‘Mimi nahisi mle ndani kulikuwa na mtu alikuwa akiongea na Makabrasha, maana nilikuta gilasi mbili..sasa huyo ndiye anaweza akawa ndiye kafanya hayo mauaji, je polisi wanasemaje kuhusiana na hilo,..?’ nikauliza‘Hilo hawajaliongelea..sijasikia hilo.nahisi mengine wameyaweka kama akiba yao…kwanza ni kuthibitisha kuwa je wewe ndiye muaaji au la..akiba yao nyingine kama sio wewe ni nani mwingine,..kwahiyo hizo gilasi, ..yawezekana ni wewe ulikuwa naye, mkinywa wanaweza kuhisi hivyo..’akasema‘Mimi sikuwa naye, na wala Marehemu hakujua kuwa nitafika hapo, japokuwa niliwadanganya walinzi kuwa nina miadi naye, je hizo..gilasi hazina alama za mikono za watu…?’ nikauliza‘Hilo litafuatiliwa, lakini kama ni muuaji mwenye ujuzi atakuwa kazifuta..vinginevyo polisi wangekuwa wameliongelea hilo, kukaa kwao kimia ina maana halina nguvu, mle ndani kila kitu wamechukua alama za mikono, wamepiga picha kila kitu …’akasema‘Kama ni hivyo basi kwanini wananishikilia mimi, sina makosa, unaonaeeh, hawana nguvu ya kunishikilia mimi, pambana nipate dhamana yangu nitajua jinsi gani ya kujitetea mwenyewe…’nikasema‘Aaah, sema sio kukulaumu, ungelipokea simu yangu,..kwanini hukupokea..’akauliza akiniangalia‘Kupokea,..sikuwa na wakati mnzuri, nilikuwa napambana na muda…ooh, nimekumbuka kitu..’nikasema‘Sema umekumbuka nini..?’ akaniuliza‘Nimekumbuka..kuna mtu nilikutana naye akikimbia ehee, kwanini nilipitiwa na hili, yaani hata polisi walipokuwa wakinihoji sikulikumbuka kabisa hili,.., kuna mtu jamani, atakuwa ndio yeye muuaji, kabisa kabisa ndio yeye..’nikasema‘Mhh…alikuwaje..?’akaguna hivyo na kuuliza.‘Anaweza akawa ndiye yeye muuaji, ooh, sasa nimekumbuka ndio yeye, tena alikuwa kavalia kofia pana kuficha sura yake, kuna muda aliinu au uso, kunitizama, kiukweli sikumuangalai vyema, lakini, nikimuona tena nitamkumbuka ndio yeye bwana..’nikasema‘Anaweza akawa sio yeye pia…’akasema na kunifanya nishikwe na mshangao‘Kwanini..?’ nikauliza‘Wewe ulimuona sura yake vyema..?’ akaniuliza‘Hapana..’nikasema‘Polisi umeshawaambia kuhusu huyo mtu..?’ akaniuliza‘Hapana, yaani hilo lilinitoka kabisa ndio nakumbuka sasa hivi, nitawaambia,...lakini sasa kiukweli sikuiona sura yake vyema, yule mlinzi atakuwa anamfahamu bwana..hawezi kutoroka kihivyo.....si lazima atakuwa kpitia hapo..kaandikisha au...kwa taratibu za pale huwezi kukwepa, hata ukiandikisha jina la uwongo, sura je... atakuwa ndio yeye, wakambane yule mlinzi vyema…’nikasema‘Kama watakuhoji tena, sawa waambie tu, ila sizani kama ndio yeye …’akasema na kunifanya nishtuke tena na kumangalia docta kwa mashaka‘Kwanini…?’ nikauliza ‘Kama rafiki yako angelikuwepo, ..tungelisema mengine,kuwa yeye ndiye kafanya hivyo, au katuma watu kufanya hivyo, ...’akasema na nilihisi hasira kwanini haniungi mkono hoja yangu ya huyo mtu niliyemuona anaongea kitu kingine.‘Huyo mtu bwana ndio yeye,…, anaweza kuwa ndio yeye…kwanini husemi lolote kumuhuu huyo mtu, au..mbona kama vile unamkwepa huyo mtu.., mbona sikuelewi au unafahami kitu hutaki kuniambia…?’nikasema‘Wewe unasema hukumuona sura yake sio…ukiwaambia polisi kwa sasa watasema unatunga , wewe utamuambia wakili wako huyo mtu alikuwaje...sawa muembie kila kitu..., na yeye atajua jinsi ya kulifuatilia hilo, hata mimi nalifanyia kazi, unanielewa, kwa hivi sasa huna haja ya kuwaambia polisi chochote zaidi ya wakili wako, umenielewa hapo…’akasema‘Mhh huanimbi kitu kwangu huyo mtu anaweza akawa ndio yeye,...kwanini nililisahu hilo,...'nikasema'Sawa kumbuka kila kitu, ..jaribu kukumbuka sana...'akasema'Unajua niliwaambia polisi wanapoteza muda, mhalifu anaweza kupotea hivi hivhi, hapo ningelikumbuka hilo, lakini cha ajabu sikulikumbuka hilo kabisa,..unajua wangelimkamata huyo mtu kwa haraka iwezekanavyo..., tatizo pale nilikuwa nimeshachanganyikiwa ..nikasahau..ooh, atakuwa ndio yeye huyo, polisi wakinipa nafasi mimi nitampata huyo mtu....’nikasema‘Hiyo ni kazi yao, wala huwezi kuiingilia, kesi kama hii ni ngumu sana, tunatakiwa kuwa wangalifu sana...'akasema'Lakini umeniamini, eeh, kuwa ndio huyu mtu, au sio..'nikasema'Yawezekana,..au kuna mtu mwingine pia, huyo mtu kama ndio yeye, unasema alivaaje...?' akauliza.'Nguo za khaki khaki hivi kichwani kavaa kofia pana..ana mwili wa kishujaa,..kama askari askari hivi...'nikasema'Umeonaeeh...huyo mtu alifika wakati Makabrasha ameshauwawa, na yawezekana ndio yeye alitoa taarifa polisi..lakini sina uhakika kama ndio huyo uliyemuona wewe, vyovyote yawezekana , muhimu ni kulielezea hilo kwa wakili…’akasema‘Kasema kuwa yeye alifika kabla ..ndivyo alivyosema na polisi wakamuamini, kwanini wamuamini na mimi wasiniamini...hapa kuna kitu maana yeye alifika kabla yangu au sio...basi yeye awe ndio mshukiwa muhimu, na wala sio mimi..vinginevyo , atakuwa ndio yeye, kwanza wamuhoji, na natamani niwepo wakimuhoji,.’nikasema‘Ndio hivyo, ila kwa akili ya haraka haraka sio yeye…kama angelikuwa ndio yeye, angelishakamatwa, polisi watakuwa na habari naye,..lakini ngoja tuone,..kila kitu kwa sasa ni muhimu sana...’akasema‘Sikukutana na mtu mwingine zaidi ya huyo mtu…unasikia, ndio yeye, vinginevyo waniambie ni kwanini wananikamata mimi na huyo mtu anaonekana hahusikia...’nikasema'Wewe unakamatwa, kwa sababu kwanza ulipatikana kwenye tukio, pili, silaha iliyotumika tatu, vielelezo vilivyopatikana...wana vigezo hivyo, na ya kuwa kama hata sio wewe  wa moja kwa moja, lakini unahusika kwa njia nyingine , wanahis wewe unaweza ukawa kiongozi wa tukio zima..hayo ni maelezo ya mpelelezi, huyo rafiki yangu...'akasema'Hapana...kuna kitu wanaficha...wana lao jambo, kuna mtu wanambeba, na ningelipata nafasi ya kutoka hapa ningelifahamu hilo...ninawezaje kuwapata watu wangu sasa..'nikasema'Watu wako mimi siwajui, na..kwa hili, wala usiwahusishe, maana utawafanya wajulikane, au haijalishi wakijulikana..?' akauliza'Inajalisha, sitaki wajulikane,..ok, nimekuelewa...'nikasema‘Kwangu mimi,akili yangu inamshuku sana rafiki yako, lakini najiuliza ni kwanini afanye hivyo, kama Makabrasha ni mwenza wake, wa kukamilisha hicho kilichomrejesha huku, unajua yeye, ndiye kamsaidia mambo mengi hata hiyo njia nyingine ya kumpata mfadhili mpya, mikataba ..nk....kwahiyo Marehemu alikuwa msaada wake,...'akasema'Msada wa masharti, kiukweli sio kumsemea vibaya marehemu, lakini hakuwa na rafiki wa kudumu, rafiki kwake ni yule anayekidhi haja zake kwa muda huo, nina mashaka hara rafiki yangu atakuwa kaingizwa huko kwa kushinikizwa kinamna fulani,...'nikasema'Sasa ni hivi kwa taarifa za uhakika rafiki yako alitoweka mapema, na watu wake wanathibitisha hilo…’akasema‘Alitoweka kwa vipi na akaenda wapi..?’ nikamuuliza‘Alikuwa kajificha humo humo ndani ya uwanja wa ndege mpaka anaondoka, alikuwa na watu wa usalama aliwaambia kuna watu wanataka kumdhuru, kwahiyo wakamuwekea ulinzi , kwahiyo yeye ana ushahdi kamili kuwa hahusiki, ...’akasema‘Hata mimi siwezi kumshuku yeye, mimi akili yangu kwa huyo mtu niliyemuona , kwanini alikuwa akikimbia , tena alionyesha kuwa ana wasiwasi , akawa kama anataka kuongea na mimi, akaghairi, ni nani huyo..?’ nikauliza‘Sio yeye, alitaka kukutahadharisha tu..’akasema‘Wewe umejuaje hayo..?’ nikauliza‘Nimekuambia kuwa nimeongea na mpelelezi, anafahamu yote hayo, huyo sio yeye, alifika muda mchache kabla yako na huyo ndiye kakuokoa usishikwe moja kwa moja kama muaji, ila umekamatwa kama mshukiwa wa kufanikisha mauaji hayo, unanielewa sasa, huyo achana naye kabisa,…’akasema‘Lakini yeye ni nani..?’ nikauliza, na docta akaonekana kama anakerwa na hiyo hali yangu ya kumshinikiza huyo mtu ndio akasema;‘Ni polisi…ni mtu wa usalama…’akasema‘Mhh…mbona hukiniambia, ..kwani yeye hawezi kuua...?'’nikaguna bado nikiwa sijarizika na hilo jibu, lakini nikaona niachane nalo ndio nikamuuliza docta;‘Je rafiki yangu wakati yupo huko na watu wa usalama alikuwa na mtoto wake…?’ nikauliza.‘Kwa muda  huo hakuwa naye,… mtoto aliletwa uwanja wa ndege baadae sana, kwa kificho, watu wa uwanja wa ndege wamelithibitisha hilo pia....’akasema.‘Watu wangu hawakuwahi kumuona …alikuwa kajificha wapi..?’ nikauliza‘Mhhh,...ndio hivyo, yule sio mwenzako hizo ndio anga zake,..na..na.. kwahiyo, inaonyesha kuwa mtoto wake alikuwa sehemu nyingine, na hayo yote ya kuwa mtoto alikuwa ametekwa inaweza ikawa sio kweli...'akasema'Kwanini..?' nikauliza'Mimi nahisi alifanya hivyo ili watu wasimuone huyo mtoto, ...unaonaeeh, anajitahidi sana kumficha huyo mtoto na ndio akaamua kutumia mbinu hiyo...kuwahadaa watu, hasa wewe na wengineo wanataka kumuona huyo mtoto…’akasema‘Mhh kwanini sasa…?’ nikauliza.‘Hivi wewe hujawafahamu hawa watu, kuna mchezo walioucheza, na huenda mtoto sasa anatumiwa kama chambo cha hayo yote mengine, huwezi jua, ....ila ninachoshindwa kufahamu ni kwanini wamemuue Makabrasha ..’akasema‘Mhh..’nikagua na yeye akasema‘Hapo kuna mawili, moja ni usaliti, au kuna kutokuelewana hapo, au pili, kuna maadui wa makabrasha waliona watumie mwanya huo kum-maliza kabisa..labda kwa ajili ya masilahi fulani, lakini ni akina nani hao, hao maadui zake ni akina nani,...maana ukisema maadui zake basi unakwenda kwingine, na hapo ndipo wewe unapoingia kutokana na ushahidi uliopatikana ...’akasema.‘Mimi ndio naingia, …acha huo utani, mimi sijui lolote na sihusiki, sikuwa na hata na lengo la kumdhuru huyo mtu , kabisa kabisa, japokuwa nilikuwa namchukia…’nikasema‘Tunajaribu kudadavua tu, najua wewe huhusiki, lakini ni lazima tuone njia zote jinsi ya mtizamo wa polisi, na jinsi gani ya kuzivuka hizo hisia zao, na hasa mbele ya  muhehimiwa hakimu…’akasema‘Hapo hata sielewi kitu naona kama unanichanganya tu, na hata hivyo hayo yote yatanisaidia nini mimi kwa hivi sasa, muhimu kwangu kwa hivi sasa ni kutoka hapa, kukwepa kwenda jela, sitaki kulala humo ndani, na yaani usiku huo mmoja kwangu ilikuwa kama mwaka,..je huku sasa itakuwaje.…nitachanganyikiwa, naweza kupoteza fahamu…’nikasema nikuna kuna kichwa changu kilikuwa kikiniwasha kwa mawazo.‘Nakuomba tena sana jitahidi kuwa mvumilivu, nafahamu hali unayopitia, lakini hakuna jinsi, mimi nitajitahidi kadri ya uwezi wangu, ..utatoka tu…vuta subira..’akasema‘Nivute subira, unajua hali niliyopambana nayo usiku wa jana, sasa sijui huko ninapokwenda kulala leo kupoje, mimi sistahili kukaa sehemu hii, mimi sio mhalafu, na hadhi yangu inaharibika, jingine la kufanyia uchunguzi wa haraka ni kuhusu silaha yangu ilifikaje hapo,au ...'nikasema'Hilo ndio swali hata polisi wanajiuliza, na ndipo unapowekwa wewe matatani.'Mimi nahisi huenda wamefanya mbinu tu,..wameua kwa silaha nyingine na hiyo wakaja kuileta baadae, huyo huyo mtu wako unayesema wa usalama labda alitumwa kuja kuiweka,...'nikasema'Vipimo vitalithibitisha hilo..'akasema'Kama muuaji sio huyu aliyekuwa akikimbia, basi, ..kuna mtu, kuna mtu kuna mtu, kuna mtu ku-ku......’nikasema huku nikirudia rudia hayo maneno mpaka docta akanishika.‘Hii inaonyesha kuwa muuaji ni mtu wa karibu sana, anayekufahamu, na anayefahamu wapi unaweka silaha yako, na anafuatilia nyendo zako mara kwa mara...sasa ni nani mtu mwingine anafahamu mambo yako?’ akaniuliza.‘Mimi sijui, kama angelikuwepo rafiki yangu ningelisema ni yeye, lakinji huyo yupo mbali kabisa na tukio hili, au sio, mwenyewe umelithibitisha hilo, sasa anayebakia ni nani, ni mume wangu, hapana, mume wangu ni mgonjwa...sasa ni nani mwingine,labda nikushuku wewe...’nikasema.‘Hahaha, nishuku tu, ....lakini...mimi nina ushahidi na wala usipoteze muda wa kunifikiria mimi,, ...anyway, tuyaache hayo kwasasa, muuaji atapatikana tu, ila cha muhimu kwa sasa ni dhamana yako....hili ndilo tulipe kipaumbele, na unafahamu mambo ya nchi yetu, ikishindikana, tutatakiwa kupenyeza rupia, hilo ujiandae nalo....’akasema.‘Utaweza hilo,...mimi sijali gharama, ila kuwe na uhakika na kila unachokifanya isije ikawa janga jingine, sitaki kufanya makosa juu ya makosa,..kama huwezi hilo nimtafute mtu mwingine wa kukusaidia, nina watu ninaweza kukuelekeza wakatoa huo msaada hadi dhamana ikapatikana, angelikuwepo rafiki yangu hii ingekuwa kazi rahisi sana....’nikasema‘Nimejaribu kila njia, hayo unayoyafikiria wewe nimeshayafanya, nimeshakuambia nina rafiki yangu wa kushibana, yupo ndani ya mtandao wa serikali, hana shida, na kama kuna uwezekano wowote angelianiambia, nimeongea na mkuu wa upelelezi, na  huyo mkuu wa kituo ambaye anafahamiana sana na baba yako, wamesema kwa leo hutaweza kupata dhamana, maana hayo ni mauaji, ila watahakikisha unakaa sehemu salama, ..’akasema.‘Eti nitakaa sehemu salama, toka lini Jela kuna sehemu salama.....nikitoka humu, nitahakikisha huyo muuaji namtafuta mimi mwenyewe, na wote wanaohusika na hili nitahakikisha nawawajibisha,...siwezi kuingia matatani kwa sababu ya tamaa za watu wengine, najua kabisa haya yote ni kwasababu ya mali zangu, kwanini wasitafuta mali zao....’nikasema kwa hasira.‘Pole sana mpendwa,…ni zaidi ya hilo unalolifikiria wewe, lakini kwa hivi sasa sio rahisi kujulikana kirahisii hivyo, na hata likijulikana, sio rahisi kulitetea kiushahidi..ila nakuahidi kitu kuwa mimi najitahidi sana, na nitahakikisha kesho hulali hapa, ila kwa leo, nakuomba uvumilie tu…, tuliza kichwa chako...’akasema.‘Huna maana kabisa, kulala hapa ni kuniharibia afya yangu hadhi yangu na hii sasa ni kashifa, ndicho wazazi wangu walikuwa hawakitaki…nasikia waandishi wa habari wameshaipata taarifa na walitaka kuja kunihoji,…sitaki kuonana na hao watu kabisa…’nikasema‘Nitajitahidi kuwaeleza walizuie hilo, mengine niachie mimi..’akasema‘Na jingine nisingelitaka wazazi wangu pia waje huku, ..nafahamu hili limeshafika kwao, fanya ufanyavyo wao wasije hapa kabisa, na je mume wangu ana taarifa?’ nikauliza.‘Sina uhakika wa hilo, sijaongea na mume wako bado, ila nijuavyo mimi hali yake inandelea vyema tu.., lakini kwa wazazi wako, …ni vigumu kidogo, hawawezi kukaa tu, ngoja tuone..hayo niachie mimi..’akasema.‘Kama mume wangu atataka kuja huku kuniona mzuieni kabisa, sitaki kuonana na yeye, kiujumla sitaki kuonana na watu wangu wa karibu,...zaidi ya wewe na wakili wangu, basi...’nikasema.‘Wakili wako atakuwa  keshafika, mtaonana naye leo hii hii…’akasema‘Sawa huyo ni muhimu kwangu…’nikasema na docta akaondoka akionekana mnyonge zaidi hata zaidi ya mimi. Na hapo nikajua hali sio rahisi, hali iliyopo mbele yangu ni ngumu,..sijui itakuwaje kwa wazazi wangu, ikizingatiwa kuwa baba ndio yupo kwenye kampeni..WAZO LA LEO:  Tunaweza kujitahidi kuwa na tahadhari za kila namna, za majanga, za kashfa za maradhi na mitihani mingine tu, lakini kwa lile lililopangiwa kukupata, hata ufanyeje, litakupata tu,..muhimu tukumbuke mola ndiye mpaji, na ndiye anayefahamu ya ghaibu, mengine ni kujitahidi tu. Lilipangwa kukupata litakupata tu. Tumuombe mola atulinde, atusaidie, atuongeze kwenye njia sahihi, na kutuepusha na mabaya yote kwa mapenzi yake.‘Na je mume wangu ana taarifa?’ nikauliza.‘Sina uhakika na hilo, sijaongea na mume wako bado, ..’akasema. ‘Wakili wako atakuwa  keshafika, mtaonana naye leo hii hii…Alikuwa docta rafiki wa mume wangu , na baada ya hapo akaondoka, na mimi nikawa mikononi mwa askari wa Magereza…Tuendelee na kisa chetu….*************Nikaingia jela, na kuonyeshwa hiyo sehemu niliyoambiwa ni ya usalama zaidi na kuahidiwa kuwa hapo sitasumbuliwa na kitu chochote…‘Nataka nionane na wakili wangu haraka iwezekanavyo…’nikasema‘Akija utaonana naye hakuna shida, lakini hata akija dhamana sio rahisi kupatikana kutokana na kosa lenyewe..’nikaambiwa.‘Dhamani ni haki yangu, sina kosa, hata nyie mnalifahamu hilo, mnafahamu kabisa mimi sijaua, mnachofanya ni kunizalilisha tu mimi, hamjui na nyie ipo siku mtazalilishwa hivi hivi, …’nikasema‘Sisi hatujui hayo, hapa kazi yetu nikuhakikisha tumekupokea kama mfungwa, mengine hayatuhusu, muhimu tii sheria za hapa, kuna kitu kingine unahitaji,..maana tumeambiwa tuhakikishe upo salama, na nakuhakikishia hutapata tatizo lolote hapa,.. …’akasema askari mmoja.‘Sihitaji kitu…’nikasema na mlango ukafungwa nikabakia peke yangu.*******Nilibakia mle ndani, kiukweli niliwekwa mbali na wafungwa wengine,lakini hakukuwa na amani, akili iliteseka, na unawaza mambo ambayo hayana mtu wa kukusaidia, huna vitendea kazi, huna simu…inabakia kuwaza tu.Hata hivyo, niliona sina jinsi, nikubali ukweli kuwa sasa nipo jela, ..je nifanye nini, kwanza nikaanza kuliwazia hili tukio kiundani,  nakujiuliza je nimekosea wapi, tatizo ni nini hasa, ni mimi au ni walimwengu,…au ni mume wangu…na ni kwanini nafikwa na mitihani hii yote,..nilijiuliza hadi kichwa kinauma, maana awali nilikwuwa nawaza tu bila mpangilio‘Ni kwanini wamemuua Makabrasha..?’ hapo nikatulia na kujaribu kupata usingizi. Hakukuwa na usingizi baadae nikagundua kuwa mtu mwingine kaletwa upande mwingine wa chumba, naye alikuwa akihangaika kivyake, hakutaka hata kuniangalia….yeye baadae nikamuona kalala, ni kama mzoefu vile‘Ni nani kamuua Makabrasha..?’ ilikuwa ndilo swali langu la mara kwa mara Huenda haya mauaji yanatokana na matukio ya nyuma, ...ambayo yameanzia kwa mume wangu, au kwangu, mtu akayafuatilia na baadae akaona huu ndio muda muafaka wa kulifany ahilo , ili kuichafua familia yangu, sasa ni nani huyo‘Ni adui zake…’ ndivyo polisi wanavyoamini hivyo, na adui za Makabrasha wanavyoona polis kwa ushahidi ni mimi….‘Kwa mume wangu haiwezekani kwa maana kuwa  Makabrasha alikuwa rafiki ya mume wangu, na ndiye anamtumia kufanikisha malengo yake, kama hiyo mikataba na…hapana kwa mume wangu haiwezekani, kwanza mtu mwenyewe yupo hospitalin, na sizani kama ana watu anaoweza kuwatumia, pesa ya kufanya hivyo ataipatia wapi..’nikawa naongea kwa kimoyo moyo.‘Je ni mambo ya kisiasa…’nikasema na kuinua kichwa, nikagundua kuwa yule mtu mwingine alikuwa kalala, lakini sasa anakuwa kama ananichunguza kinamna fulani, sikumjali,…nikaendelea kuwaza.Kutokana na maelezo ya rafiki yangu hili jambo limekwenda zaidi na kuingiza siasa ndani yake, kwahiyo haya yanaweza yakawa yamepangwa kisiasa, lakin kwa vipi, ili iweje, wakati huyo ni mtu wao muhimu sana, hapana kwa upande huo sizani kama wanaweza kumuaa, sasa ni nani...‘Huyu Makabrasha kama anatumiwa, na hao wanasiasa ni kwanini wamuue…?’ nikajiukuta nimeongea kwa sauti mpaka nikajishutikia, na niligundua yule mtu mwingine upande ule alikuwa kama ananisikilizaNikamzarau na sasa nikawa makini ili nisiongee kwa sauti, ..jamani ukiwa mahali kama hapo, unakuwa kama umechanganyikiwa fulani hivi, usiombe kukaa sehemu kama hizo, hakuna mawasiliano na wanadamu wenzako.‘Mkataba…eeh’ nikasema na kukuna‘Kuna huo mkataba wa pili, wa huyu rafiki yangu aliotakiwa yeye kuweka sahihi, je huo mkataba ulikuwa malengo gani, kwanini uwe wa kulazimishana,...ili iweje, kwa manufaa ya nani, kama ni Kwa Makabrasha kwanini wakamuua, na kama Makabrasha alikuwa jembe la wanasiasa kwanini wamuue…hapa ina maana gani, ..kuwa aliyemuua Makabrasha sio hao wanasiasa, ni watu ambao hawana umuhimu naye sasa ni akina nani’‘Hapo ndio wewe unaingia..na kushukiwa kuwa huenda ndio wewe ulifanya mauaji hayo…’ nilikumbuka kauli ya docta rafiki wa mume wangu.‘Hapa kwa vyovyote iwavyo, rafiki yangu anafahamu mengi yanayohusiana na huu mkataba,..namfahamu ni mjanja sana, atakuwa keshafahamu kitu, …na huenda na yeye ni muhusika mkuu, na anaweza akafahamu lolote kuhusiana na huyo mtu aliyekuwa akiongea na Makabrasha, na huyo mtu ndiye muuaji, sasa ni nani huyo…’nikawaza kimia kimia.‘Rafiki yako hahusiki kwa vile aliondoka  kwa Makabrasha..akatoweka, ushahid upo kuwa alikuwa uwanjani kajificha,…mmh, kajificha wapi…‘Hayo mauaji  yalifanywa baada ya yeye kuondoka kwahiyo yeye hahusiki kwa hayo mauaji, labda awe katuma watu wake waje kufanya hivyo...na watu wake ni akina nani,...watu wake wengi nawafahamu,...nitaongea nao,....lakini kwa vipi ...hapa si mpaka mimi nitoke humu, lini... na muda ni muhimu sana...’nikajikuna kichwa huku nikiwaza.Nikasimama, na kujinyosha, niliona yule jamaa kule akijiinua kuniangalia, mimi sikumjali..nilijinyosha nikachukua mazoezi kidogo, ilimradi mwili ufanye kazi, hadi nikachoka na kujilaza.‘Ni nani mwingine anaweza kuhusika, labda docta, rafiki wa mume wangu, lakini kwa nini ahusike, ana nini na huyo mtu, hapana, huyu haweze kabisa, ..sasa  ni nani….mhhh, ?’ nikajiuliza bila majibu.Kichwa sasa kimechoka kuwaza, nitaka kama nipate dawa ya usingizi, nitaipataje, maana kwa hali kama hii nitawehuka…nikasimama, nikakaa, nikasimama nikaaa..yaani kiukweli akili ilikuwa sio sawa..baadae nikajilaza tena na wakati nataka kupata usingizi..mara… Nikasikia nikiitwa, na kuambiwa wakili wangu ameshafika, na wamemruhusu nikaongee naye kwa muda mfupi tu, kwani muda wa kuongea na watu wa nje ulishapita ila nimepata upendeleo tu..Kwa haraka nikasimama na mlango ukafunguliwa, nikatoka hadi sehemu ya kuongea na wageni, nikamkuta wakili wangu akinisubiria, na aliponiona tu akaanza kuongea;.‘Samahani sana, ilibidi kwanza nihakikishe kuwa mzazi wangu yupo sehemu stahiki, si nilikuambia anaumwa, kwahiyo kutokana na hili tukio, ikabidi tubadilishe mipangilio yetu yote,..ikiwemo kumchukua mgonjwa, nije naye huku Dar, hili halikuwepo kwenye mipangilio yetu.‘Anaendeleaje..?’ nikamuuliza‘Ni hivyo hivyo, na uzee nao..lakini uzee sio tija ya kuwa mtu aumwe, ni maradhi tu, na kwa vile mwili ni mzaifu, madawa yanachukua muda kufanya kazi yake, tunapambana, huku tukimuomba mungu..’akasema‘Poleni sana…’nikasema‘Ilikuwa ni kazi kubwa sana kumshawishi hadi akakubali tuje naye huku, hakunielewa ni kwanini najali kazi zaidi, hakuelewa umuhimu wa hili tukio, lakini mwisho wa siku akakubali,‘Haya...., sasa tuingie kazini, maana nimejitahidi kupitia kwa watu wote muhimu, kuanzia kwa wale  waliokukamata,…mpaka nimefika eneo la tukio…nikaongea na watu mbali mbali mle kwenye lile jengo, nikaja kuongea na wapelelezi nia ni kupata picha na hali halisi, na mtizamo wa watu kabla sijafika kwako ....’akasema.‘Wamekudanganya nini hao watu?’ nikauliza.‘Kiufupi ni kesi ngumu..’akasema‘Lakini mimi kiukweli sijaua, siwezi kukuficha hilo…’nikasema‘Najua, hujaua, polisi bado wanahisi unaweza ukawa umefanya hivyo, unajua kazi ya polisi ilivyo, ni mpaka wajirizishe, shuku shuku ni moja ya kazi zao ili kumpata muuaji, na kukushikilia kwako ni njia moja wapo ya kumpata muuaji,..’akasema‘Kwanini wanitese mimi,maana huku nikutesena, napata hasara kiasi gani,..nazalilika, familia yangu inaingie kwenye kashfa, hawalioni hili...’nikasema‘Ushahidi mkubwa wanao kuwa wewe unaweza kuhusika,...lakini kinachowachanganya, ni muda wa muaji,..muda ndio imekuwa kikwazo kwao, kukuweka wewe kuwa mtuhumiwa mkuu…’akasema‘Wanajua hilo..’nikasema‘Sasa kutokana na hilo wanakuja kukuona huhusiki moja kwa moja na mauaji hayo, ila wanafikiria kuwa wewe utakuwa ulimtuma mtu, ayafanye hayo mauaji , na ulifika hapo kuchukua nyaraka fulani hapo ofisini ndio wakakuwahi…swali kwanini ujipeleke mwenyewe…’akatulia.‘Nilijipeleka, mimi nilikuwa sijui lolote ni waongo hao…’nikasema‘Pili, silaha yako ndiyo iliyotumika kwenye hayo mauaji, japokuwa hakuna alama zozote za vidole kwenye hiyo silaha, ya kwako au ya mtu mwingine, silaha haina alama yoyote, na wewe walikukuta umevaa kinga za mikononi.‘Kwahiyo, swali ni kwanini ulivaa kinga,…na silaha haina alama za vidole , ina maana ulifany ahivyo makusudi…’akasema‘Wanasema pia ulipofika ulisema una miadi na marehemu…lakini kwenye kumbukumbu cha kitabu cha marehemu haupo, yeye ana kitabu cha kumbukumbu cha watu alitakiwa kukutana nao, hakuna jina lako, na imegundulikana kuwa ukurasa wa siku hiyo umechanwa, na hawajaona ukurasa huo mahali popote huenda ingesaidia jambo…’akasema‘Kwahiyo bada ya kumtafuta muuaji, wanahangaika na mimi au sio…’nikauliza‘Wanasema kwa wadhifa wako unaweza ukawa uliwatuma watu wako, ukawapa silaha yako, na huenda kilichokupeleka hapo ni kuharibu ushahidi pamoja na kuchukua nyaraka ambazo alikuwa nazo Makabrasha, swali ni kwanini uende mwenyewe wakati..umeagiza mauji yafanyike, na kwanini ukadanganya kuwa ulikuwa na miadi na huyo mtu, …’akasema‘Unaona eeh, wao wanajikanyaga tu kutaka kuniharibia jina langu, kama wanatumiwa basi wataumbuka wenyewe…’nikasema‘Swali jingine ni kwanini uliwadanganya kuwa ile bastola sio silaha yako…wakati silaha yako unaifahamu…hapo wakahisi kuna kitu unawaficha..’akasema‘Lakini ni kweli, mimi nilikuwa sina uhakika bado, maana silaha yangu niliicha kabatini…’nikasema‘Uliposema silaha yako ipo kabatini walikwenda kuhakiki,  wakaona kabati lako limefungwa, hakuna dalili zozote za uvunjwaji, kwa maana huyo mtu aliyeichukua hiyo silaha yako ana ufungua, ni nani mwingine mwenye ufunguo wa hilo kabati unapoweka hiyo silaha..?’ akaniuliza.‘Hakuna mwingine…nakala zote ninazo mimi, mume wangu hakuwa na haja ya ufunguo wa kabati hilo…’nikasema.‘Kwahiyo huyo mtu aliyeichukua hiyo silaha yako,ndio huyo huyo, aliyeweza kuiba mikataba,..yawezekana mtu huyo anafahamu siri zako za ndani, sasa ni nani huyo, unaona hapo, kwahiyo ni lazima wawe na shaka na wewe..’akasema‘Kiukweli hata mimi mwenyewe nashindwa kuelewa hapo, ni nani huyo..?’ nikawa kama namuuliza wakili‘Ndio hapo polis hawataki kukuachia....’akasema wakili.‘Zaidi ya mume wangu ..hakuna anayejua kuhusu hizo funguo, hata rafiki zangu hawajui hilo, ..wafanyakazi wa ndani hawafiki huko, huko nafanya usafi mimi mwenyewe…na mume wangu ni mgonjwa, asingeliweza kulifanya hilo, japokuwa hajambo lakini bado hajaweza kutembea vyema, na asingeliweza kutoka hospitalini wasimuone….’nikasema‘Na hii inafanya jambo hili liwe gumu kidogo, kwani watu tunaowafahamu waliopo karibu na wewe na wanaoweza kufahamu nyendo zako ni mume wako, mwingine kwa mbali ni rafiki yako, ambaye yupo mbali sana na tukio lenyewe, kiushahidi, maana muda wote alikuwa na watu wanaoaminika, mwingine ni nani unayemuhisi....?’ akaniuliza.‘Sana sana ni docta, rafiki wa mume wangu, ambaye hawezi kuhusika kabisa....’nikasema.‘Kwasasa kila mtu anaweza kuhusika, cha muhimu ni kukusanya ushahidi, ...lakini kwa sasa, kwa vile nimepewa muda mchache tu, ngoja nikafuatilie kuhusu dhamana yako kwanza, na kwa hivi sasa unatakiwa kukumbuka kila kitu,  ili  tukikutana tena, uniambie kwa uwazi, usinifiche chochote, ni muhimu sana kwa sasa...’akasema wakili.‘Nasikia dhamana imekataliwa...ni kweli…?’ nikauliza.‘Mimi ni wakili wako, kama imekataliwa nitakuambia mimi mwenyewe, usiwasikilize watu wengine, na kwa tahadhari, usiongee na mtu mwingine yoyote kwa hayo yaliyotokea, zaidi yangu mimi,  unanielewa hapo..tukishirikiana vyema.., hili litakwisha japokuwa lina ugumu wake kidogo...’akasema na kutaka kuanza kuondoka.‘Ni ni kweli kuwa haya mambo yamekuwa ya kisiasa zaidi….?’ Nikauliza‘Yawekana ikawa hivyo, ila kwa hivi sasa ni mapema kulisema hilo, maana kwangu mimi natakiwa niwe na ushahidi unaoweza kumtosheleza hakimu, sio maneno ya kusikia ..unanielewa, nia ni kukuondoa kwenye makosa kisheria, sio kupambana na makundi…’akasema‘Inasemwa hivyo kuwa huenda ni maadui wa baba yangu wa kisiasa wanatumiwa mwanya huo kujenga kashafa,kwa vile baba yupo kwenye siasa, ..’nikasema‘Nikuambie kitu, hadi hivi sasa upande huo wana kundi limeundwa kwa ajili ya kutafuta ni nani kamuua mtu wao, ..Marehemu alikuwa mtu muhimu sana kwao, na wametumia pesa nyingi kumgharamia , kwenye masomo nk..haiwezekani wao, wakamuua..lolote laweza kutokea, ..kama ni kisiasa, lakini kiushahdi haina mshiko..’akasema‘Kwahiyo…?’ nikauliza‘Kwa hivi sasa acha nifuatilie mambo ya dhamana yako kwanza, ni muhimu sana hilo,  kabla siku haijaisha, .., mengine yanaendelea kufanyiwa kazi, unasikia wewe kwa leo nakuomba tu, utulie kwanza, najua upo kwenye wakati mgumu lakini kwa kosa kama hili, hatuna ujanja wa kulazimisha mambo, niamini mimi,…’akasema‘Nakuomba kitu kimoja, usije ukamwambia mume wangu, najua wazazi wangu wameshafahamu lakini mume wangu ni mgonjwa, haya mambo yatazidi kumchanganya,...’nikasema.‘Wote hawo wanashafahamu, wazazi wako walinipigia simu, japokuw mtu wa kwanza kunipigia simu alikuwa ni mume wako, niliongea naye na yeye , na akaniomba sana niweze kukusaidia upate dhamana haraka iwezekanavyo...’akasema‘Haiwezekani, ni nani alimuambia mume wangu kwa haraka hivyo alijuaje, kwanini watu wanachukua mambo kwa haraka hivyo, hwafahamu kuwa huyo mtu ni mgonjwa, na docta, amesema hakuwahi kuongea naye leo, ni nani huyo..?’ nikauliza.‘Ndio hivyo, ili ujue kuwa, dunia sasa hivi haina dogo....wa kwanza kunipigia simu alikuwa ni mume wako, na baadae ndio wakanipigia wazazi wako, wazazi wako ndio walionifanya nihangaike kumchukua mgonjwa nije naye…’akasema na kuondoka.Nb: Tulikuwa tunamalizia sehemu hii, ilikuwa ndefu kidogo, ndio tukaigawa sehemu tatu, tukijaliwa tutaingia sehemu nyingine, kufichua utata huo, ni nani kamuua Makabrasha na kwa nini.... Swali,: bashiri ni nani anaweza akawa kamuua Makabrasha, kati ya wahusika hawa: Mdada(mke wa mgonjwa), mgonjwa (mume wa mdada), Rafiki wa mdada(anayesafiri masomoni), Docta rafiki wa mume, wanasiasa ili kujenga kashfa...toa maoni yako, na ni kwanini unaona hivyo.Tuzidi kuwa pamoja.WAZO LA LEO: Ukiona mtu anafurahia madhila na taabu za wengine , na anatamani watu hao hata wafe, watu ambao wasio na hatia, wanateseka, wazee , akina mama na watoto ambao hata hawajui kinachoendelea, wewe unafurahia, unatoa maneno ya dharau, chuki, unadhihirisha ile chuki yako ya ndani…eti kwa vile sio wenzako, ujue mtu huyo ana roho ya shetani ndani yake. Haijalishi mtu huyo anayeteseka, anayedhulumiwa haki yake yupo kwenye kundi gani, ilimradi hayo yanayompata sio stahiki yake, na hakuna hukumu kisheria iliyopitishwa dhidi yake, ilibidi watu wapaze sauti ya kuwatetea,…lakini watu wanafurahia, wengine wakiuwawa, wakiteseka, wakidhulumiwa, utafikiri hao wanaofurahia hivyo wataishi milele,..hakuna atakeyeishi milele, marejeo yetu ni kwa yule aliyetuumba, na siku itafika hukumu ya kweli itatimilizwa.Tukumbuke sisi sote ni wana-wa -Adamu, na chanzo chetu ni kimoja, sasa iweje damu ya ndugu yako inamwagwa, watu wanadhulumiwa haki zai, sisi tunafurahia, kwa kisingizio cha makundi, bado tunaiona ni wacha mungu…hapana huo sio ucha mungu,na wenye tabia hiyo, sio mtoto wa Adamu, na kama wewe sio mtoto wa Adamu, utakuwa mtoto wa nani..  Ilikuwa asubuhi na mapema, nikiwa najua leo ndio siku ya dhamana yangu, kiukweli usiku mmoja wa hapo ulikuwa mateso yasiyovumilika, sikuweza kulala kabisa,   Mara nikasikia nikiitwa, nikajua sasa ndio muda umefika, lakini mbona ni asubuhi sana, ni nani huyo kafikaNikajitayarisha kwa haraka na kutoka nje baada ya mlango kufunguliwa‘Kuna wageni wako…’nikaambiwa‘Ni wakili wangu..?’ nikauliza‘Hapana nenda tu utawaona mwenyewe, wanakusubiria…’nikaambiwaBasi kwa hamasa nikaelekea sehemu ya kukutana na wageni, hata kabla sijawakaribia, nilianza kuangusha kilio,sikuweza kuvumilia..Mama naye aliponiona alishindwa kujizuia, akaanza kulia, ikageuka kuwa kilio tena.. mama akanivamia na kunikumbatia, alitamani anibebe, tukalia mpaka hamu ikaisha,.. huku mama akinishika mashavuni, mwilini, kama kuhakikisha kuwa hakuna sehemu nilyoumia, halafu akasema;‘Mwanangu upo salama kweli..?’ akauliza‘Ni kama unavyoniona mama, nipo salama, japokuw ani hi mitihani tu mama, lakini msijali wazazi wangu haya yatakwisha tu…’nikasema‘Lakini mwanangu kwanini hutaki kutuelewa sisi wazazi wako, ujue mzazi wako anaona mbali, tulishakuamba huyo mume wako hakufai, unaona sasa yanayokutokea hapa hata baba yako hajawahi ku-kufika, leo wewe umeanza, ni nuksi gani hii jamani...’akasema.‘Mimi sitaki hata kukumbushia hilo, cha muhimu, ni jinsi gani ya kukusaidia utoke hapa, tuambie mumefikia wapi, maana tulitaka tufuatilie lakini nikaambiwa kila kitu kinashughulikuwa na wakili wako, sasa niambie mumefikia wapi...’akasema baba.‘Wazazi wangu msihangaike, hilo linafanyiwa kazi, wakili wangu yupo huko, na taarifa za awali ni kuwa dhamana imeshakubaliwa, iliyobakia ni taratibu ndogo ndogo...’nikasema hivyo, japokuwa bado sikuwa na uhakika na hilo.‘Tatizo lako ni hilo la kujiamini kupita kiasi, una uhakika kweli kuwa dhamana yako imekubaliwa, au unatudanganya sisi wazazi wako, ili kutupa matumaini, unafikiri mimi sizifahamu kesi za namna hii zilivyo, haijalishi wewe ni mtoto wa nani, kesi kama hizi ni ngumu…je una uhakika na hilo?’ akaniuliza.‘Sasa mimi baba ningekudanganya , ili iweje, dhamana imeshakubaliwa, ka taarifa za juu juu, kilichobakia ni taratibu ndogo ndogo, hapa namsubiria huyo wakili aniambie wamefikia wapi, kwahiyo wazazi wangu....msiwe na wasiwasi, wakili analifanyia kazi hilo...’nikasema.‘Lakini umeonaaeeh, tuliyokuambia kuwa tabia ya mtu huwa haijifichi, sasa unaanza kuonja joto ya jiwe, na kama hutakubaliana na sisi, utaone mengi zaidi ya haya, sio nasema hivi kwa kukuombea mabaya hapana, lakini ndio hali halisi ya watu kama hao..…tabia ya asili sio rahis kubadilika kirahisi, sasa sijui tukusaidieje binti yetu...’akasema baba.‘Baba kwanini unakimbilia huko, una uhakika gani kuwa hayo yote ni kwasababu ya mume wangu..?’ nikauliza.‘Mimi sio mtoto mdogo, usione nimekaa kimiya ukafikiria sifuatilii nyendo za maisha yako, hata kama unajimudu vipi…’akasema na mimi nikamkatisha na kusema.‘Baba msijali, hizi ni changamoto za maisha yatakwisha tu, …’nikasema.‘Binti yetu sio tunasema hayo kwa kutokupenda furaha yako, ..hatuna nia ya kuvuruga ndoa yako,lakini tunaangalia mbali, kipi kilicho bora, furaha ya muda, au furaha ya kudumu, eehe…?’ akawa kama anauliza‘Ni ya kudumu baba..lakini…’nikasema‘Ya kudumu hutaipata kwa hali kama hii,  haya yanayotokea hayafurahishi kamwe yanatutesa na sisi, jea upo tayari kuishi maisha kama hayo hadi unashuka kaburini, je huwaonei huruma watoto wako...?’ akaniuliza sasa mama.‘Lakini wazazi wangu haya yanaweza kumpata yoyote, hata awe na mume kipenzi cha wazazi, bado, mitihani kama hii inaweza kumpata. Na sioni kwanini nikate tamaa na mume wangu kwa kufikiria kuwa kuna makubwa yanakuja..’nikasema‘Sisi hatutaki wewe ukate tamaa, ila changamoto ndio hizo zimeanza, na maadui zangu wameshajua kuwa hapo kwako ndio kichaka cha kuniharibia mimi kisiasa na ndicho nilikuwa najaribu kukuweka au labda wewe hutaki nifanikishe malengo yangu ya kisiasa, unajua siasa ilivyo, kashfa ndio silaha ya adui yako..’akasema baba‘Lakini baba, sijachunguza na kuamini kuwa hayo yaliyotokea ni kutokana na mume wangu, na sizani kama mume wangu anaweza kuhusika na kifo cha Makabrasha,  na hakuna mwenye ushahidi mpaka sasa kuwa mume wangu kafanya mabaya fulani yote ni tuhuma tu.., au sio…’nikasema‘Kuuwawa kwa Makabrsha hilo tuwaachie polisi, sisi tunachokiongelea hapa ni tatizo la familia yako, ambalo linaweza kuwa ni chanzo cha yote hayo mengine, kashfa ndani ya familia yako inanigusa na mimi, sasa tusipoziba ufa tutazidi kukarabati nyumba, na haitadumu, hili mimi sitakubaliana nalo…’akasema baba‘Baba ni sawa nimekuelewa, lakini yameshatokea eeh, sasa tufanyeje …maana mimi nimeshakuwa mke wake..je kama tatizo ni hilo, tatizo ni mume wangu,tufanyeje sasa, niachane naye, au nifanyejeje ?’ nikawa kama nawauliza.‘Sisi hatuwezi kusema uachane na mume wako, hayo tulikushauri mapema sana, ukakaidi, hatua iliyofikia, sisi hatuna uwezo nayo, ni wewe na mume wako mtakavyoamua ,  lakini sisi kama wazazi ni wajibu wetu kukuonya na kukumbushia hilo…’wakasema‘Lakini baba…’nikataka kusema na baba akaendelea kuongea‘Mume wako, akishirikiana na huyo marehemu, ndio wamekufikisha hapa, na hatujui hatima yake itakuwaje, kwa vile walichotaka kukifanya wao ni kujenga kashfa dhidi yangu....’akasema‘Sasa baba mimi sio mwanasiasa hayo yanafanyika kwa kukuharibia wewe au sio, ukiangalia kwa makini hilo linamweka mbali mume wangu na hilo, kwasababu, mume wangu akifanya hivyo kukuharibia wewe si ndio amejiharibia na yeye mwenyewe na familia yake, ina maana yeye hana akili hiyo ya kufikiria…’nikasema‘Mume wako anatumiwa..huenda hata bila ya yeye kujua.., wamemchota, akawa anatoa siri za ndani, na siri za ndani ndio hizo zimetumiwa kisiasa,..sasa utasema chanzo hapo ni nani, sio, … mume wako..tuelewe hapo, mume wako angekuwa mkweli akasema ukweli,..tungelijua jinsi gani ya kumlinda…’akasema baba.‘Je baba hayo yana ushahidi, maana kiukweli baba kukiwa na ushahidi hata mimi nitajua jinsi gani ya kufanya, mimi sitakubali hayo yafanyike kuniharibia familia yangu, lakini ushahidi upo…’nikasema‘Ushihidi!!!... ina maana hata sisi wazazi wako tukikuambia jambo huwezi kutuamini mpaka tukupatie ushahidi..?’ akauliza mama‘Sio hivyo mama, ..ushahidi sio kwa kutokuwaamini nyie, ushahid ni jinsi gani mimi nitaweza kupambana na mume wangu, .. kuna mambo yetu ya kifamilia tuyaliyaweka, na yatambana mume wangu, lakini ni lazima kuwe na ushahidi…’nikasema‘Ndio huo mkataba..ulioibiwa na kuchezewa, hahaha, ..?’ akauliza baba na kucheka‘Ndio baba, huo utanisaidia sana, kama nitapata ushahidi..’nikasema‘Binti,… uwe makini sana…, kama bado hujaamini, basi subiria, lakini sasa yamegusa familia yangu, sitaweza kuvumilia tena, sitajali kama wewe ni binti yangu au huyo ni mkwe wangu.., walichokitaka kwa hivi sasa wamekikosa…lakini je wamejiandaaje baada ya hili kushindwa, kwangu mimi wameshanitangazia vita..’akasema baba kwa sauti ninayoijua , huwa akiongea hivyo hatanii.‘Sawa baba nimekuelewa, lakini usichukulie jazaba, tafadhali na kuomba ....’nikasema na mama akasema;‘Hebu tuambie, ukweli, ...rafiki yako, kazaa na nani?’ akaniuliza mama.**************‘Mama jamani hilo litasaidia nini kwa hivi sasa…?’ nikauliza na mama akauliza tena‘Nauliza hivi rafiki yako kazaa na nani,..nakuuliza hivyo nikiwa na sababu zangu…?’ akauliza tena mama.‘Mama, kiukweli hilo hadi hivi sasa, mimi sijajui, kwasababu hajawahi kuniambia ukweli...’nikasema.‘Hajawahi wakati alikuwa mtendaji wako, na rafiki yako unayemuamini, hapo kuna kitu unatuficha,..lakini sasa hilo tunakuachia wewe kama homework, ukija kuligundua hilo inaweza ikawa mwanga kwako wa kujua hayo tuliyokuwa tukikuambia, na inaweza ikawa mwanga kwako, kuwa sio kila rafiki ni rafiki kweli,..’akasema mama‘Sawa wazazi wangu nimewaelewa, ..’nikasemaBaba ghafla akabadili azungumzo tukawa tunaongelea maswala mengine nia ni kunifanya nisichoke sana kiakili, na kwa vile nimeshawaambia swala la dhamana lipo wazi hawakuwa na wasiwasi huo tena…baadae ikabidi waondoke, na wakati wanaondoka wakasema;‘Kama unaona unahitaji msaada wetu tuambie, mimi nitafuatilia nihakikishe unapata dhamana, nina wakili wangu ....lakini hawezi kuingilia taratibu zako maana wewe una wakili wako, tusije tukaonekana watu wa ajabu, sio unajua taratibu zilivyo, au hata kama yeye anahitaji nguvu nyingine aseme tu...’akasema baba.‘Msiwe na wasiwasi wazazi wangu, dhamana ilishakubaliwa, hapa nasubiria tu kuondoka...’nikawaambia, maana wakili wangu na rafiki wa mume wangu walinithibitishia hilo, kwahiyo sikuwa na wasiwasi na hilo japokuwa nilikuwa sijawa na uhakika wa moja kwa moja..**************** Wazazi wangu wakaondoka..Saa zikawa zinakwenda, simuoni wakili au rafiki wa mume wangu,...hata wale maaskari nilizoeana nao, wanaonipa taarifa za mambo yangu sikuweza kuwaona, ilikuwa kama vile watu wameambiwa wasinikaribie,..na mchana huo, ukawa ukapita, ikawa inaingia jioni, simuoni mtu.Bado niliendelea kutokuvunjika moyo, nikidhania labda kuna mambo bado yanafuatiliwa na watu wangu hao, hasa wakili, .Ni wakati nimeshakata tamaa kabisa, nikiwa nahangaika kumtafuta mlinzi ili nimtume kwa wahusika ili angalau nijue ni nini kinachoendelea , mara nikasikia nikiitwa, na hapo nikajau ni muda wa kuondoka, dhamana imeshakubaliwa, japokuwa wamenichelewesha lakini sasa naondoka.Hapo sasa nikawa najiweka sawa, kwani najua sitarudi tena kwenye hicho chumba, nilipokuwa tayari, nikatoka hadi chumba cha kupokea wageni.Nilimkuta wakili wangu akiwa amekaa kwenye kiti, na aliponiona kama kawaida yake akasimama na kuja kunisalimia, nikamuitikia, lakini kwa jinsi nilivyomwangalia usoni, nikahisi kuna tatizo,… nilimuona kama hana raha, kanyong’onyea, nikahisi labda mzazi wake…nikatulia kusubiria taarifa, na yeye alipoona nimetulia akaanza kwa kusema;‘Yaani hapa nilipo naogopa hata kusema kitu, maana huyo mkuu wa kituo, na yule mpelelezi anayeshughulikia kesi yako,  sijui wana dhamira gani,...ni aheri wangelianiambia mapema, lakini walichofanya ni kuchelewesha muda, kila nikiwafuta wananiambia subiri, subiri… na baadaye wakaja kuniambia kuwa mambo hayajawa safi....’akasema.‘Unataka kusema nini?’ nikamuuliza nikiwa nimeshitushwa kwa kauli yake hiyo.‘Wamekataa kukupa dhamana,...’akasema‘Hakimu au wao..?’ nikauliza‘Unajua haya mambo tulishaongea na hakimu, nahakimu alikuwa akisubiria taarifa zao hao watendaji, kauli yake inawategemea sana wao, sasa kumbe wao walikaa kikao, wanavyodai, ..kwenye kikao hicho, wakaona kuwa wewe huwezi kupewa dhamana…’akasema‘Kwanini sasa mimi sina makosa, sijaua, ushahidi wanao…kwanini sasa, umeshindwa kazi…’nikasema kwa ukali‘Sikiliza walioweka pingamizi hilo ni  mkuu wa kituo na huyo mpelelezi, wanasema kuwa, kupewa kwako dhamana kunaweza kukaharaibu baadhi ya mambo wanayoyafuatilia, wakasema wewe kwa jinsi wanavyokujua una watu wako ambao utawatumia waingilie kazi zao na kuweza kuharibu ushahid na kazi yao,..’akasema.‘Hapana, hapana, ..wana nia gani na mimi, .....,halafu sasa ikawaje..?’ nikamuuliza, nikijua dhamani haiwezekani tena leo.‘Baadaye tukaona twende ngazi za juu, ndio tukajipanga, docta, rafiki wa mume wako, na yule ofisa wa polisi, rafiki yake docta, wakasema wao wanakwenda kuonana na uongozi wa juu, na mimi nikawa naendelea kufuatlia mambo ya kisheria , tuligawana hivyo…’akasema‘Wanasemaje hao waliokwenda huko..?’ nikauliza‘Yaani ndio hapo naona kifo cha nyani… wenzangu tangu waende huko, hawajawasiliana na mimi, na cha ajabu kila nikipiga simu zao, hawapokei, zinaita tu..’akasema.‘Mimi bado sijawaelewa, kwanini  mlipoona hivyo, hamkuja kuniambia mapema, mumesubiri hadi saa hizi, unafikiri mimi nitachukua hatua gani kwa sasa, kama mngelijuwa hilo limeshindikana mungelikuja hapa na kuniambia mapema, mimi ningejua ni nini cha kufanya, sasa muda kama huu, mnafikiria mimi nitafanya nini, ....au mnataka niendelee kusota huku jela, mnafikiri huku ni kuzuri sana  au...?’nikasema kwa hasira.‘Sio kusudio letu, bosi, kila kitu kilikuwa kinakwenda vyema, na hatukutarajia kabisa kuwa kutatokea pingamizi kama hilo, mwanzoni tulijua kuwa wanafanya kupoteza muda tu, lakini dhamana ilishakubaliwa, ..’ akasema‘Na hakimu au sio..?’ nikauliza‘Ndio, hakimu yeye hakuona tatizo, kwa vile ushahid unaonyesha kuwa wewe huhisiki moja kwa moja, ila aliwapa tahadhari wajirizishe kwanza…’akasema‘Sasa taarifa ya kukataliwa imekuja baadaye sana..jioni hii, kwahiyo tukaona tukimbilie ngazi za juu, na kiukweli dhamana ipo, lakini kwa leo...itakuwa vigumu, maana hawo viongozi wawili wenye pingamizi ambao ni muhimu sana kwenye kesi hii hawapatikani kabisa...’akasema.‘Kwahiyo nyie mnataka nilale hapa tena, na huenda hata hiyo kesho ikashindikana, maana kama wameweka pingamizi, hata huko ngazi za juu watafanya nini, hawawezi kuwahini watendaji wao, au sio?’ nikauliza‘Nimeona nije nikufahamishe hivyo, halafu mimi mwenyewe nitaende  huko ngazi za juu nionane na mwanasheria wao, kwasababu waliokwenda huko hawapokei simu, na hawajaweza kunipa yaliyotokea huko, na sheria inaona una haki ya dhamana, …’akasema‘Sizani kama utafanya lolote kwa hivi sasa…’nikasema‘Ningelijua kinachoendelea ningelijua nifanye nini….’akasema.‘Mimi nahisi huko walipokwenda wamekwama, ndio maana hawataki kupokea simu yako...wanachofanya na wao,  ni kupoteza muda tu, ili wakija hapa, wasipate hata muda wa kuongea na mimi, hamna shida, nitasota tena hapa leo, lakini kesho nataka kuwasiliana na hizo ngazi za juu…nikasema‘Wewe usijali , mimi kesho naamukia huko…’akasema‘Utakavyoona, mimi sina imani na nyie tena..’nikasema.‘Kulikuwa na jambo jingine nataka kukuulizia...’akasema.‘Sitaki kuongea lolote na nyie tena, ninachotaka kusikia ni dhamana yangu imekubaliwa, basi, kama hakuna jibu kama hilo, sitaki kuongea na nyie, mumeshanivuruga akili yangu, wamefika wazazi wangu hapa wataniona  mimi kama mtoto mdogo, ...nitakuja kuwaambia nini,..’nikasema kwa hasira.‘Wazazi wako nimeongea nao, na wao wakasema kama kesho itashindikana watafuatailia na wao waone tatizo lipo wapi, ...lakini nina uhakika kesho dhamana itapatikana....’akasema.‘Hata kama umeongea na wazazi wangu,  haina maana tena kwangu, tumeshathibitisha kwao, kuwa hatuwezi kujitatulia mambo yetu wenyewe, mpaka wao wahusike, kitu ambacho sikutaka kabisa kitokee, ina maana wewe umeshindwa kazi, na wao watamuweka wakili wao, je unakubali hilo, mimi ninakulipa gharama zako za nini,kama kazi imekushinda....’nikasema.‘Kazi haijashikana madam.., usiwe na wasiwasi, ...ni mbinu zao za kupoteza muda tu, wazazi wako wamenielewa, na sio kwamba watamuweka wakili wao, ...nitaendelea kufanya hii kazi, kama wakili wako, na hata kama wakili wao akifika hawezi kufanya miujiza, taratibu ni zile zile....hata hivyo, ... ‘nikamkatisha na kusema;‘Ulitaka kuniuliza nini mwanzoni nisamehe maana akili yangu haipo sawa...’nikauliza huku nimesimama, nikiwa simuangalii, nimempa mgongo, niliona nimeongea kwa jaziba,na huyu ni wakili wangu natakiwa kumuheshimu.‘Nilitaka kukuuliza je Mume wako alifika hapa leo kukuona?’ akauliza‘Mume wangu, ...!!’ nikasema kwa kushangaga,‘Ndio…’akasema ‘Hapana hajafika hapa…, mbona nasikia hali yake sio nzuri, ..?’ nikauliza‘Ni kweli hali yake kuna muda ilibadilika, ikawa mbaya, unajua yeye ni mbishi sana, hataki kufuatilia baadhi ya mambo, sasa akaanza kudai kuwa anataka kuja kukuona, akakataliwa, na alipokataliwa akatoroka, na wakajua kuwa huenda amekuja huku kukuona....’akasema.‘Katoroka,!!.. kwani kashikiliwa kama mfungwa, mimi ninavyojua yupo hapo hospitalini kwa ridhaa yake mwenyewe, ...’nikasema huku nikimgeukia na kumwangalia.‘Ndivyo ilivyo, lakini kama mgonjwa akitaka kutoka nje,au kuondoka hospitalini kwa muda, ilibidi aondoke kwa kibali maalumu, kama ni lazima, na alipomuomba hivyo docta, akamkataliwa kutokana na hali yake ilivyokuwa, yeye akaondoka kwa siri, huko ni kutoroka, kavunja masharti ya hospitalini..’akasema.‘Mimi nilishawaambia msimwambie huyo mtu, alitakiwa asifahamu kabisa kuwa kumetokea hivi, sasa mnaona, watamfanya sipone haraka…, sasa  katorekea wapi, yupo wapi, nyumbani au…?’ nikauliza.‘Kesharudi, na hata mimi sijui ni nani alimwambia, nahisi, ni wazazi wako walipopata taarifa, labda walikupigia simu na ulipokuwa hupokei ndio wakampiga yeye, na hapo ndipo alipokuja kufahamu kuwa umekamatwa na hatimaye kueletwa huku Segerea, ’akasema.‘Na sikukumbuka kuwauliza hilo wazazi wangu, na je wazazi wangu walipewa taarifa hiyo na nani..?’ nikauliza.‘Sijui...labda rafiki ya mume wako, ....’akasema.‘Hapana rafiki wa mume wangu tulikubalina naye kuwa wazazi wangu na mume wangu wasijue lolote kwanza, …hadi hapo muda muafaka utakapofika, na nilitarajia kuwaambia hilo baada ya kupata dhamana, kama ni lazima,..nahisi kuna kitu kimejificha hapa…kuna mtu anatuchezea akili akiwa na maana yake....’nikasema.‘Mimi sioni kama kuna kusudio maalumu hapo, ni watu waliona kufanya hivyo, wanatenda wema, ...cha muhimu kwa sasa ni kutuliza akili zetu tuone ni jinsi gani tutalimaliza hili, na mimi nataka kuongea na mume wako, nina imani kuwa ninaweza kupata taarifa muhimu kutoka kwake, zitakazo tusaidia kwenye hii kesi,.....’akasema.‘Kwa vipi wakati yeye ni mgonjwa, atakusaidije, hajui lolote utazidi kumuumiza tu?’ nikauliza‘Kwa jinsi ilivyo, inabidi tuongee naye, hata kama ni mgonjwa, maana kila ukiangalia ni nani angeliweza  kuingia ndani kwako na kufungua  kabati, ...na kama ulivyosema hata ufungua wako, unao wewe mwenyewe…, na kule ofisini uliuficha mahali pa siri, hapa inaleta mashaka, maana kama ulivyosema wanaofahamu wapi unapoweka hata hiyo bastola yako ni wewe na mume wako tu, .....’akasema.‘Kwahiyo unataka kusema nini hapo…?’ nikauliza‘Inawezekana mume wako aliwahi kumwambia mtu mwingine, na huyo mtu mwingine akatumia mwanya huo kuingia na kuchukua hiyo bastola,...maana yeye ni mgonjwa, hatuwezi kusema kuwa yeye ndiye aliyefanya hivyo...’akasema.‘Mimi bado sioni umuhimu wa kumuuliza mume wangu, tunaweza kufanya uchunguzi mwingine na kugundua ukweli hata bila kumgusa mume wangu,..tatizo nipo hapa jela, siwezi kufanya lolote kwa sasa, lakini kama ningelikuwa nje, ningelishagundua kitu...je kuna mtu kawasiliana na rafiki yangu, huyo msomi..,?’ nikauliza.‘Ndio , mimi mwenyewe nilitaka kuongea naye, lakini muda niliompigia alikuwa yupo darasani, ufahamu aliondoka wakati wenzake wanaendelea na masomo, kwahiyo alipofika tu, akaingia darasani, ...bila hata kupumzika, sijaweza kumpata tena ila kuna muda aliongea na docta, rafiki wa mume wako, sijapata muda wa kumuuliza waliongea nini zaidi maana tulikuwa tunakimbizana na muda.’akasema.‘Namfahamu sana rafiki yangu huyo ni mtu mwenye bidii sana, na akiamua kitu chake ni lazima akipate, na hayo masomo kwake ni muhimu sana, lakini kinacho nishangaza ni kutokunijali mimi, hafahamu kuwa hayo yote yasingelipatikana kama isingelikuwa ni mimi....nina hamu sana ya kuongea na yeye, na safari hii nataka anijibu maswali yangu yote kwa uwazi...’nikasema.‘Mimi nahisi rafiki yako huyo, kaingizwa huko upande wa pili bila kupenda, kwani ninavyomfahamu ni mtu anayekuheshimu sana, isingelikuwa rahisi kuvunja uaminifu wake kwako,..lazima kuwe na kitu kikubwa cha msingi, kwake,..yule ni kama ndugu yako au sio, unafikiri anaweza kukusaliti...’akasema‘Labda …kitu gani anaweza kunaswa nacho mpaka akubaliane nao, atakuwa mjinga basi, mimi sijui kwa sasa ila nitakuja kufahamu tu..’nikasema .‘Kwa jinsi marehemu anavyojulikana, tunahisi, huyo jamaa alikuwa kwenye kazi zake za kitapeli, na huyo rafiki yako alikamatika kwenye jambo fulani, akapewa masharti kufanya hivi, usipofanya hivi, nitakuharibia, ni tabia ya marehemu pia kujishughulisha na biashara ya mlungula, ‘ blackmail.’.na hilo polisi wanalifanyia uchunguzi....’akasema.‘Na kwanini tusubiri mpaka polisi waingilie undani wetu, nataka tufahamu ni nini kilitokea kabla polisi hawajagundua zaidi najua wawo wamerizika …ya kuwa mimi ndiye nahusika…, je unaweza kulifanyia kazi hilo ukagundua undani wake, kabla ya polisi, najua nakupa kazi ambayo sio yako?’ nikamuuliza.‘Linaweza kufanyika kama wahusika watatoa ushirikiano, akiwemo mume wako, na rafiki yako,...nahisi hawo wanaweza wakawa ufunguo muhimu wa kulijua tatizo hili , chanzo chake na hatima yake...na nahisi kwasasa itakuwa ni rahisi kwao kuongea kila kitu, maana yule mtu waliyekuwa wakimuogopa, keshafariki, kama ndio yeye aliwashinikiza ...’akasema.‘Kwahiyo unahitajia msaada gani kutoka kwangu?’ nikamuuliza‘Msaada wako mkubwa ni kunipa ruhusu ya kuongea na mume wako, na ikibidi nitafanya uchunguzi nyumbani kwako, kwahiyo nahitajia ufunguo zako zote...’akasema.‘Kwa hivi sasa nakuruhusu uongee na mume wangu, lakini kwa ufunguo, hebu kwanza subiria mpaka kesho kama nikitoka humu, mimi mwenyewe nitaifanya hiyo kazi, nikisaidiwa na wewe...kuna mambo nahitaji mwenyewe niyafanyie uchunguzi, sitaki yatoke nje, unanielewa hapo ...’nikasema‘Sawa hamna shida…’akasema‘Kama mna uhakika kuwa dhamana ni kesho, sioni kwanini nikupatie kila kitu,..na mengine nitakuambia hiyo kesho, kwahivi sasa fuatilia mambo ya dhamana yangu, na natumai kesho itapatikana , kama itakosekana, sitaki nikuone tena ukija hapa, na hao wenzako, waambie hivyo…umenielewa...’nikasema na kuanza kuondoka.‘Kuna jambo jingine muhimu kabla hujaondoka, unahitajika kulifahamu...’akasema‘Hilo jambo lisubiri kesho tafadhali...’nikasema.‘Ni muhimu ulijue, ...kuna mtoto wa marehemu sijui kama unamfahamu, kaja kutoka nchi za nje…amekuja kwa ajili ya msiba wa baba yake anahitajia kuongea na wewe....’akasema‘Kuhusu nini, kwanini anataka kuongea na mimi, kwa kazi gani, mimi sio ndugu yake hatuna mahusiano naye au anafikiri mimi ndiye niliyemuua baba yake..au mimi nitamshauri  mambo ya mirathi, baba yake hana mafungamani na sisi , kuwa labda alikuwa na hisa na mimi au....hapana sina haja ya kuongea na yeye, sitaki asije kunichanganya….’nikasema.‘Anasema kwenye mirathi, aliyoachiwa na baba yake kuna mkataba unaoonyesha kuwa baba yake alikuwa na hisa kwenye kampuni yako na ya mume wako, kwa mume wako ni hisa nyingi kidogo, na kwako ni hisa chache tu, kwahiyo ni haki yake kulifahamu hilo...’akasema‘Eti nini?’ nikasimama kama mtu aliyegusa na umeme.‘Lakini hilo niachie mimi nitapambana naye nahisi ni kutokana na ule ubadhirifu wa ule mkataba wa awali, na sasa mkataba wao mpya unataka kuanza kuleta chokochoko, ..hilo niachie mimi hiyo kwangu ni kazi ndogo tu...’akasema.‘This...oh,.... I can’t believe this,  its too much,....sitaki kusikia hayo maneno,...mwambie huyo mtu, asimchokonoe nyoka mwenye sumu shimoni, kama wanaishi kwa njia ya ulaghai, kama yeye ni sawa na baba yake, wasijidanganye kuwa wanaweza kufanya hivyo kila mahali...hakikisha unalimazliza hilo bila ya mimi kukutana na huyo mtu, sijui ana umri gani...’nikasema huku nikishika kichwa changu na kuvuruga nywele kwa hasira.‘Huyo ni mtoto wake wa kwanza, ni mkubwa tu, mtoto huyo alizaliwa mapema sana, wakati marehemu bado anasoma, alimpa uja uzito binti wa watu..ambaye akaja kuwa mkewe,...kwahiyo ni mkubwa,. .’akasema‘Basi ni mkubwa…sijawahi kumsikia..’nikasema‘Mimi nilishamwambia kuwa kama ni maswala ya mikataba, anatakiwa kuongea na mimi, kwani mimi ndiye wakili wako, lolote linalohusiana na hiyo mikataba nalifahamu mimi, lakini kasisitizia kuwa anataka kuonana na wewe ili muelewane....’akasema‘Tuelewane..ndio hayo siyataki,...naogopa kuwa ,nitafanya kitu ambacho sitapenda kukifanya, ...okey, tutaona naye hiyo kesho, ...fanyeni haraka nipate hiyo dhamana...’nikasema‘Tutafanya hivyo madam…’akasema‘Mimi sitaweza kuvumilia kubakia hapa ndani tena, ..ikishindikana nitatoka humu kwa nguvu..na wewe kazi hakuna...hii ni ahadi....’nikasema na kuanza kutembea kuondoka niliona wakili akitaka kuniuliza jambo jingien lakini sitakuata kusbiria tena…na wakati nafika mlangoni ili nigonge mlizi anifungulie mara kitu kikanigonga kwa nyumba kichwani, na giza likatanda,.....nikadondoka, na kupoteza fahamu.NB:Ni nini tena hiki kinakuja....WAZO LA LEO: Siku hizi kuna watu wanaishi kwa njia za ulaghai, uwongo, lugha za matusi, kejeli nk, watu wanaona ni kitu rahisi kuandika tu mitandaoni, hawajui dhamana yake na matokea yake kwenye jamii, ...hili ni changamoto kwetu, wakati huu jamii, zetu zinapojiunga kwenye kijiji kimoja cha utandawazi. Ni muhimu tukawa makini katika kutoa taarifa zetu, majina, anuani, namba za akiba zetu na maneno ya siri kwa watu, kwani huwezi kujua ni lini bahati mbaya itakuangukia.  Na kwetu watumiaji, tukumbuke kuwa maandishi(kalamu) ni hatari sana, ukishatuma kitu ujue hiyo taarifa ni kitu cha kudumu, ..leo kesho au baadae inaweza ikawa sumu kwako au kwa vizazi vijavyo, jiulize kwanza kabla ya kutuma, ninajenga au ninabomoa, ..Ni wakati nafika mlangoni ili nigonge mlinzi anifungulie mara kitu kikanigonga kwa nyumba kichwani, na giza likatanda,.....nikadondoka, na kupoteza fahamu….Tuendelee na kisa chetu…**********Nilizindukana na kujikuta nipo hospitalini, akili ilipotulia nikagundua kuna mtu kakaa pembeni ya kitanda, …ndio nikamgundua kuwa alikuwa ni mume wangu, wakati huo alikuwa kajiinamia, nikajaribu kujiinua, lakini nikahisi maumivu ya kichwa, nikashikilia kichwa, na mara ndio mume wangu akagundua kuwa nimezindukana, kwa akanisogelea na kujaribu kunisaidia, nikainuka na kukaa vizuri,‘Pole sana mke wangu unajisikiaje...’akasema kwa unyenyekevu.‘Kwani kumetokea nini…mbona….oh, kuna kitu kilinigonga kichwani, ni nani kafanya hivyo…?’ nikauliza‘Inaonekana kuna watu walitaka kukuumiza huko jela...’akasema‘Kuniumiza kwasababu gani,…ni akina nani hao?’ nikawa nauliza maswali kwa mfululizo.‘Hayo maswali kwasasa hayana msingi, cha muhimu ni kuwa upo salama, na hilo limesaidia kupatikana kwa dhamana yako haraka, kwani kuna watu walishaiwekea pingamizi, wakidai kuwa upo mahali salama, ungeliachiwa ungekuwa kwenye hatari zaidi...’akasema.‘Oh, kumbe....’nikasema huku nikishika kichwa, sehemu ambayo nilifungwa bandejii na mume wangu akaniangalia kwa mashaka na kuuliza‘Kwani unajisikiaje?’ akaniuliza huku akiweka mkono sehemu ile iliyowekwa bandeji na mimi nikawa najihami asije akanitonesha, na akaondoa mkono wake, na kuniangalia machoni. Alionekana huruma machoni…‘Maumivu ya kichwa kwa mbali, lakini sio sana, haya niambie na wewe unaendeleaje, maana mgonjwa anamuuguza mgonjwa, nani zaidi sasa...?’ nikamuuliza‘Mimi kwasasa sijambo, sina wasiwasi kabisa, nipo tayari kupambana na yaliyopo mbele yangu, japokuwa nachechemea, lakini sio kivile…na muhimu kwa sasa ni mazoezi tu...’akasema huku akijiweka vyema, kama vile anajiandaa kuongea.‘Unajiandaa kupambana na yaliyopo mbele yako, yapi hayo mume wangu, unavyoongea ni kama umemlanga mtu au ni maswala ya kazi na maendeleo...?’ nikamuuliza‘Dunia hii ilivyo, maisha yetu wanadamu yalivyo, kila siku ni mapambano, au sio, huwezi kulala tu, ukafanikiwa, ni lazima upambane, na mimi nimejifunza jambo hapo, ili ufanikiwe hakuna kulala..’akatulia kidogo.Nilimuangalia kwa makini, na hayo maongezi yake nikahisi kama hayupo sawa, kwahiyo nikaogopa kuendelea kumuuliza maswali ya kumkwanza, nisije nikaharibu nikataka kubadili muelekeo wa maongezi kwa kusema;‘Hivi huyu wakili wangu yupo wapi...maana nataka kujua mambo yanaendeleaje...aniambie kulitokea nini..nakumbuka nilikuwa mimi nay eye tu mle ndani, sasa…hapana, lakini sawa…labda…’ nikawa kama nauliza huku nikitafuta simu yangu, sikujua ipo wapi.‘Wameondoka muda mfupi uliopita, watarudi, kuna mambo wanafuatulia, walisema zoezi limekamilika, sikuwaelewa,…kwani ....unatafuta simu yako, nahisi ipo kwenye mkoba wako, nikuletee?’akaniuliza.‘Mkoba wenyewe upo wapi, hata sijui…maana akili haipo..’nikasema‘Mkoba wako huu hapa, walikuchukulia kila kitu chako, haina haja ya kurejea huko jela, kumbe ni uzembe wa watu tu, hukutakiwa kupelekwa huko…’akasema‘Nilijua tu, walitaka kunikomoa, kuijengea kashfa, lakini hawatafanikiwa ukweli utabakia kuwa silaha ya mkweli,…’nikasemaWakati huo mume wangu aliinuka kuchukua mkoba wangu uliokuwa umewekwa kwenye meza, alionekana akiinuka kwa shida, yaonyesha bado hajapona vyema ila anajikakamua tu. Akanipa simu yangu, nikaiwasha kwani ilikuwa imezimika, nikawa nimeishikilia mkononi.‘Oh, hamna shida, ..hivi leo tarehe ngapi, ...’nikasema huku nikiangalia simu, akaniambia tarehe na saa, nikasema;‘Ahsante sana mume wangu,..nikamtaja kwa jina lake, na yeye akatabasau na kusema‘Ahsante mke wangu,…’ na kunitaja jina langu, siku nyingi sijasikia ukinitaja jina langu na mimi nikatabasamu, halafu nikasema;‘Kama dhamana imepatikana basi iliyobakia ni kuangalia kesi hiyo itakwenda vipi, na huyo muuaji ajulikane ni nani, ili niwe huru kabisa....’nikasema.‘Mke wangu, kuuwawa kwa Makabrasha kumenishitua sana, sikutegemea kabisa, ni kama bado namuona vile , yaani jana tu mtu mlikuwa naye, leo hayupo, keshatoweka duniani, hatutamuona tena,..na zaidi kafaje mpaka afikie adhabu hiyo.., hapo ndio inatisha zaidi…’akasema‘Ni kweli pole sana, najua alikuwa wakili wako tegemezi na rafiki yako mpenzi, lakini yote ni mapenzi ya mungu..’nikasema‘Mhh ndio hivyo,…kazi ni kazi ukiwa hai, hayupo tena, natakiwa kupambana mwenyewe…unajua nawaza sana baada ya hilo tukio kuwa sisi wanadamu si chochote...na wengine wanajiona wana nguvu, kwa vile tu wana mali….’akasema.‘Mhh…mali,…. ni kweli mali ni mtihani, na usipokuwa na mali ni mtihani pia, au sio...’nikasema kama namuuliza.‘Ni kweli,..hilo nimeliona ni mtihani kweli ukiwa huna kitu, na …ukaoa mke mwenye uwezo, unajikuta mwanaume huna kauli, …sikuongelei vibaya  mke wangu, ila nimekuwa nikiliwazia sana hilo…nafahamu wewe huna shida, mke wangu wewe ni mtu tofauti na wanawake wengine, lakini wewe utafanyanini, kama wazazi wanataka uwe watakavyo, eeh...’akasema‘Kwanini unaongea hivyo, kwani kuna kitu gani kibaya umekiona dhidi yangu, au wazazi wangu, tulishaongea hayo sana tukayamaliza, au…kuna nini cha zaidi?’ nikamuuliza huku nikimwangalia usoni.‘Haya yanayoanza kujitokeza, yananipa shida kweli kweli, ndio maana hata nilipokuwa hospitalini, nilikuwa nikihangaika kujua jinsi gani ya kuyaweka sawa, na nikawa natafuta njia ya kuyasawazisha, lakini mwili ulikuwa haukubali,..nilikuwa kwenye mtihani mkubwa sana...lakini sasa naona kila kitu kitakuwa sawa , ni swala tu la kukubaliana...’akasema.‘Kukubaliana?? Ukiwa na maana gani hapo, kwani hatukuwa tumekubaliwana awali, mambo yalikuwa shwari au sio, au kuna tatizo, mume wangu nakuomba uniambie ukweli, kuna nini kinachoendelea…?’ nikauliza bila kujali lolote.‘Kukubalina ni muhimu hasa kwa wote wanaohusika, ili mambo yaishe tu, kwani tunataka nini zaidi, alikuwepo Makabrasha aliyejiaminisha, msomi, tena wa nje, mjanja kweli kweli, ..anajua sheria, anajua mbinu za maisha, mbona kashindwa kujilinda, leo yupo wapi,…mmh,hapo ndio mimi naogopa sana..’akasema‘Umeliona hilo eeeh, vyovyote utakavyofanya, ukatumia ujanja ujanja wa maisha, mwisho wake ..sote itakuwa hivyo, hakuna mjanja mbele ya mungu, sasa kama ulidhulumu , kama ulifany madhambi itakuwaje, inatakiwa mimi na wewe tuliwazie hilo, au sio mume wangu…’nikaongea , kuuma na kupilizia.‘Ni kweli mke wangu, sasa tufanyeje ili mambo yawe sawa, ili tuwe kama zamani, unakumbuka tulivyokuwa tunaishi, …eeh, japokuwa kiundani, nilikuwa najihisi mnyonge…unanielewa hapo, mume nakuwa hivo hivyo…’akasema‘Mume wangu tatizo nahisi kuna mtu kakuharibu akili yako, kwani mimi nilikunyanyapaa, kila kitu tulifanya kwa makubaliano au sio…na nilikubali kuwa pamoja na yote wewe ndiye mume wangu mwenye mamlaka ya mwanaume, haijalishi kitu, na kukufanya uwe na nguvu zaidi tukafungua kampuni yako mwenyewe, ili usiwe mnyonge…’nikasema‘Ni kweli lakini bado ilikuwa sio kama yangu…nilikuwa sijalifahamu hilo..lakini nilipogundua kuwa ni mimi tu, nilikuwa sifuatilii mambo, …unajua hapo ndio namshukuru sana Makabrasha, kanionyesha mambo ambayo sikuwa nayafahamu, mola ampe makazi mema peponi…’akasema.‘Mume wangu pamoja na yote hayo, kwanza nakuomba kama upo tayari, uniambie ukweli, sawa uliniomba msamaha, lakini kwa kosa gani, hujaniambia hilo, lakini pia haya yanayotokea, …mpaka wewe kutafuta wakili yana ishara gani, ni kwanini ukafanya hivyo..kama upo tayari nakuomba uniambie…’nikasema‘Nipo tayari sana mke wangu na ndilo nililojiandaa nalo, sitaki tena kupoteza muda…’akasema‘Sawa..msamaha mnzuri ni ule unakiri kosa ulilolifanya au sio…kiukweli na mungu ni shahidi au sio..sasa mume wangu nataka uniambie ukweli umefanya kosa gani, mpaka ukafikia kupatwa na ajali, ilikuwa ni tatizo gani…?’ nikamuuliza‘Mke wangu kweli unataka kuambiwa ukweli..utavumilia huo kweli, hutanichukia, huta… lakini hata hivyo, mbona ukweli wote upo wazi tu,…mimi nakumbuka nilishakuambia na kukuomba msamaha au sio…lakini anyway, hilo halina shida, ila ukweli mara nyingi unauma, naogopa kukuumiza mke wangu ...’akasema‘Mhh, kwanini ukweli uume, ..labda kama una mashaka, ...lakini kama una nia thabiti,ya kujua na kukubali kwa nia njema sizani kama utaumiza,...tatizo ni kuwa watu wengi hawataki kusema ukweli, wakichelea yatakayotokea baada ya ukweli…’nikasema tukichezeana akili hapo, kwanza nikitaka kumweka sawa nisije kumuathiri.‘Hapo ndio kwenye mtihani,lakini kwetu sisi sizani kama kutakuwa na matatizo au sio mke wangu, sasa hivi hata nikiongea ukweli, najiamini, hakuna shida mke wangu kwahiyo leo ni siku ya ukweli, ukweli wote kutoka kwangu…’akasema‘Kwanini sasa ujiamini, kwani zamani kulikuwa na kikwazo gani..?’ nikamuuliza‘Nilikuwa sijafahamu haki zangu, lakini nashukuru kwa ushauri wako, na ushauri wa wakili wetu…unajua mke wangu una akili sana, wewe unaona mambo vyema kabisa, na ushauri wako unakuwa wenye manufaa sana, ingelifaa wewe uwe mshauri wa watu…’akasema‘Una maana gani..?’ nikauliza‘Hata rafiki yako anakusifia sana, …unajua kushauri mambo, bila kujali ..maana ukimshauri mtu eeh, akifanya inamsaidia na unajua tena …na mengi uliyomshauri yamemsaidia, na hata ukiangalia mengi uliyoyashauri kwenye familia yetu, tukayafuata imekuwa ni faraja sana…wewe unaangalia mambo kwa usawa, ukiwajali wenzako, marafiki zako, familia yako, unaonaeeh, na zaidi hasa ushahur huo ukiwa kwenye maandishi, ya kudumu ..yaani mimi sikuwa na mawazo hayo kabisa hata marehemu alisema wewe ni jembe…’akasema‘Kwahiyo sasa umepona upo tayari kwa haya,…?’ nikamuuliza kwa mashaka‘Ndio mke wangu, wala usiogope, kama huamini mpigie simu docta wangu, nimepona wewe tuongee , maana hili ni la muhimu sana, ili tuyamalize haya tuwe huru, nina imani baada ya haya, hakutakuwa na tatizo tena, ..kabisa niamini mke wangu…’akasema‘ Mume wangu…mimi japokuwa bado nina mashaka na afya yako, lakini kiukweli nilikuwa nasubiria hatua hii, nilikuwa natamani sana, upone ili tuyamalize haya matatizo, japokuwa sasa yamezuka haya mambo mengine, ni shida kwakweli..sijui yataishaje, lakini tukimpata huyo muuaji, basi nina imani mambo tayakwisha, nina imani..nikitoka hapa tutalimaliza hili...’nikasema nikimwangalia, na yeye akawa akiangalia pembeni, nikamuuliza‘Yah, hilo tutalifanyia kazi, kama mume , nina wajibu wa hilo…mke wangu niamini hilo tutalimaliza,…’akasema akitikisa kichwa.‘Vipi hali yako kwa ujumla, kweli umepona vyema, maana tusije kanza kuongea hapa likazuka jingine,..?’ nikamuuliza tena….‘Hahaha , mke wangu huamini, mimi nimepona, nilifuata masharti yao,kama walivyotaka, japokuwa ilikuwa kazi nzito, maana nilikuwa kama mfungwa, lakini kiukweli ilinisaidia sana, na waliponipima kwa mara ya mwisho waliniambia nimepona kabisa, walisema kila kitu kipo safi, hakuna matatizo tena, usiwe na wasiwasi na mimi mke wangu....’akasema.‘Kwahiyo upo tayari kusema yote yaliyotokea, kuanzia yaliyotokea, ukaja kupata ajali, baadae nakumbuka ukaja hata kuniomba masamaha, nimekuwa nikijiuliza huo msamaha ulikuwa wa kosa gani, sasa je upo tayari kwa hilo , ....?’nikamuuliza.‘Hilo ndilo nataka tuliongelee leo kama na wewe upo sawa,..maana wewe unaumwa, au tusubiri kwanza hayo mengine ila kuna hili la muhimu kidogo, mimi kama mume ninawajibu wa kuomba ushauri kwako, au sio, ni la haraka, halihitajii kusubiria, kama upo tayari, tuyajadili mimi na wewe...’akasema‘Sawa itakuwa vyema…’nikasema nikiwa sijui anataka tujadili nini, zaidi nilitaka yeye aniambie ukweli‘Mke wangu kuna mengi yametokea, na muda umepita, na shughuli nyingi zimesimama, kiasi kwamba mtu unashindwa uanzie wapi…lakini kuna haya yetu wenyewe, haya ndio msingi, na nazidi kushukuru kwa mawazo yak o ya kuona mbali,..sasa ni hivi,…’akatulia kidogo, na mimi nikasubiria.‘Mimi nataka tuyamalize ikibidi leo, …ila nitakuwa mtomvu wa shukurani kama nitamsahau Marehemu, na ndio maana naona umuhimu wa kikao chetu, ili mengina yaishe , Marehemu alikuwa msaada wangu mkubwa, kiushauri, ....kanifungua macho, hasa kwenye maswala ya maandishi,....’akatulia kidogo.‘Una maana gani maana naona unatumia maneno hayo ya maandishi, maandishi…?’ nikamuuliza‘Hapo namaanisha mikataba...’akasema‘Mikataba…mmh, tuna mkataba mmoja wangu mimi na wewe, au mingine ni ya kikazi au?’ nikauliza na kabla hajajibu nikaendelea kuongea‘Au wewe una maanisha mkataba huo wa hiari ..?’ nikauliza‘Huo huo, ..yah, hiyo mikataba ya hiari, …’akasema‘Lakini,..unajua nilishindwa kukuuliza kwa vile ulikuwa unaumwa, nimeoana ajabu kubwa sana, mbona mkataba ule wa hiari, haupo tena, na sasa upo mkataba ambao sio ule wa awali…?’ nikauliza‘Mke wangu, unasema nini…hapana, mkataba ni huo huo, au…?’ akauliza‘Hahaha, nilijua tu, ni janja yako wewe na Makabrasha, au sio…ule mkataba wa hiari wa awali, umetoweka, na sasa upo mkataba wa kugushi, sasa niambie maandishi au mkataba unaozungumzia wewe ni upi, wa kugushi au ule wa awali…?’ nikauliza.‘Mkataba wa kugushi!? Mke wangu hakuna mkataba wa kugushi, hilo neno kugushi limetokea wapi tena …na unasema umetoweka kwa vipi , ni kitu hakiingii akilini mke wangu, una…aah,..una- taka kusema nini hapo…’ akaniuliza na maneno ya mwisho akaigiza lafudhi ya kizungu sijui alikuwa na maana gani.‘Kwahiyo unajifanya hujui kuwa wewe na Makabrsaha ndio mliofanya hayo!’nikamwambia huku nikimwangalia nikiwa na mashaka nisije nikazua balaa, lakini sikuona mabadiliko,, yeye kwanza akainamisha kichwa chini, na baadaye akasema;‘Mke wangu nakupenda sana, .sitaki kukudanganya, kama nilivyosema huu ni muda wa kuambizana ukweli, na…kiukweli kuanzia sasa sitaki nikufiche kitu.,..nitakuambia kila kitu kilichofanyika, na nina imani utanielewa.’akasema‘Sawa ukifanya hivyo, mbona tutaelewana tu, mimi sina shida, mwenye shida ni wewe tu ambaye ulihangaika na hadi kubadili mikataba, na ajali ikaja kukuta, nahisi ni katika kuhangaika huko, sijui ulikuwa unaogopa nini..’nikasema‘Najua,…hilo sio siri, sasa ni hivi, kiukweli ilibidi nifanye jambo, maana nisingelikubali mimi na wewe tuje kuachana, kisa mkataba, hapana mimi nakupenda sana mke wangu,..bila kujali hayo…unasikia, mkataba na nini, ni katika kujihami tu, au sio… na mimi naahisi kuwa, nitailinda ndoa yangu kwa kila hali, hilo nakuahidi, mke wangu, ..’akasema‘Sawa, nimekusikia..’nikasema‘Na ndoa hapa nina maana ya kila kitu, familia, mali, na..maisha yetu ya kila siku, kufungwa kwako ilikuwa moja ya pigo kwangu, ..sikuwepo nyumbani, nilikuwa naumwa, nilitakiwa kama ni kufungwa nifungwe mimi…’akasema‘Kwani wewe ndio uliua..?’ nikamuuliza‘Hapana, wewe wanakushuku tu, kama wanakushuku, na mimi nipo, ningeliwaambia wanifunge mimi,…hadi hapo ukweli utakapopatikana, lakini nilikuwa sijiwezi, naumwa, nipo hospitalini,ningelifanya nini..ni mtihani..lakini sasa nipo ngangari, tutapambana na hao watu…’akasema‘Kwahiyo kwa kifupi ni kweli kuwa uliubadili mkataba wetu kutoka ule wa asili na kutengeneza mwingine wa kitapeli..’nikasema nikimuangalia, maana hapo nilitumia lugha ya kumkwanza, lakini hakubadilika, alikuwa vile vile wa kujiamini.‘Mke wangu, usitumie lugha hiyo, ‘kubadili’ …maana kiukweli hakuna kitu kama hicho, kwa lugha yako hiyo ya kubadili, au kugushi hakuna kitu kama hicho eeh,....mimi kama mume wako niliona ni heri nifanye jambo, kuilinda ndoa yetu, na nilichofanya ni sahihi kabisa, kwa mujibu wa mkataba unavyosema.. ‘akasema‘Kwahiyo ulibadili mkataba kwa kutaka hayo unayoyataka wewe, na kujiwekea hayo mamlaka ya kufanya utakavyo.., nataka jibu tu hapo, kweli au si kweli, je wewe na mkabrasha mlibadili kitu kwenye mkataba, niambie ukweli tu hapo..?’ nikauliza‘Mke wangu…’akataka kujitetea‘Hilo ni muhimu kwangu, kauli yako ni muhimu sana, ni kweli au si kweli, ukijibu hilo itakuwa ni faraja kwangu, niambie ukweli,..mlibadili huo mkataba au sio, ni kwanini mlifanya hivyo, nataka jibu la ukweli, kwasababu umesema leo utaniambia ukweli..sio ndio hivyo..?’ nikamuuliza‘Ndio..leo nitakuambia kila kiu ..muda ukiruhusu, ni wewe tu..’akasema‘Haya jibu swali langu…’nikamwambia..NB: Muda umekwisha, sehemu hii itaendelea…kuna tukio muhimu sana hapa hutaamini..ngoja niliweke sawa, lakin ngoja nitangulize kipande hiki.WAZO LA LEO: Mkataba ni kitu cha makubaliano, na mkataba ulio sahihi ni ule pande mbili zinahusika, na kukubaliana,..mikataba mingi hasa ya ajira, inakuwa ya pande moja, na muajiriwa anakuwa hana hiyari, ni kukubali tu, huu sio mkataba sahihi.Kuna mikataba ya mauziano ya bidhaa, kusiwe na ujanja ujanja wa kutapeliana, hii ni dhuluma, hata kama ukishinda kumshawishi mwenzako ukamdhulumu hili ni deni kwako. Lakini pia kuna mikataba ya hiari kati ya pande mbili, ni lazima kila pande irizike na kila kipengele. Tukumbuke mkiwa wawili mwenyezimungu yupo kati yanu, au hata mkiwa wengi mwenyezimungu yupo analithibitisha hilo, hadi kwenye nafsi zetu, kudanganyana ni kujidanganya wenyewe. Tusipende kudhulumu kwa njia hii dhuluma ni dhuluma na madhara yake ni makubwa .‘Sikiliza nikuambie sasa, eeh,..mimi sikufahamu au kuukariri mkataba  kabla, kwahiyo sikuwa makini kwa kipengele kwa kipengele…mengi nilikuwa nafanya kuhakikisha nakufurahisha, eeh kwasababu nakupenda mke wangu.…’akasema‘Watu wakawa wana..fikia hatua sasa hata ya kuniuliza, umeoa au umeolewa, unaona eeh vitu kama hivyo, mimi sikujali,..sasa matatizo yakaanza, kuna mambo mengine, nitakuja kukuelezea baadae, ..’akatulia‘Marehemu nikakutana naye ndiye akanifungua macho, aliniuliza tatizo ni nini, awali sikumuambia, baadae kutokana na hayo matatizo …unajua, ikabidi nimuambie, kuwa kuna mkataba, na mkataba umekuwa ni mnyororo kwangu,..’ hapo akakaa kidogo, baadae akasema‘Akaomba aupitie,nikampa, samahani kwa hilo…akausoma , akasema, mbona kila kitu kipo sawa, ni wewe tu hutimizi wajibu wako, unaogopa nini, hiki kipengele hapa kimekupa mamlaka, ..ilikuwa kama ndio naanza kukiona,…unaonaeeh..’akasema‘Sasa kama ningelikaa kimia, huo mkataba ukafika kwa  wazazi wako, hicho kipengele sikuwa nimekiona eeh cha mamlaka ya mume, na vingine vingine,lakinikwa leo ni hiki cha mamlaka… mimi nina uhakika wazazi wako wangelikimbilia kuniwajibisha, na hapo ndoa ingelivunjika tu,..’akasemaNilimuangalia tu, na aliponitupia jicho na kuiona hiyo hali niliyokuwa nayo usoni, haraka akajibaragua na kama anatabasamu hivi, halafu akasema;‘Kwahiyo mke wangu, sasa mambo yote yapo shwari, usiwe na wasiwasi kabisa, sasa nitajitahidi kutimiza wajibu wangu, ..nimeshajielewa, na makosa yaliyopita ..si ndwele, tugange yajayo, na nachukua fursa hii kukushukuru sana wewe mke wangu,  uliona mbali sana…hata Marehem alikusifia kwa hilo…’akasema‘Hahaha, mume wangu usinifanye mimi ni mjinga kiasi hicho, kuwa mumeweza kubadili mkataba, na mumetengeza mkataba mwingine ambao ndio huo unakufanya ujiamini saana..’nikasema‘Kwanini unasema hivyo mke wangu..?’ akauliza‘Hebu nijibu swali langu , ni kwanini mlibadili huo mkataba…najua mliubadili na marehemu kwa masilahi fulani…, sasa nataka kauli yako wewe, ni kwanini ukafanya hivyo, maana unaongea kama vile..hata sikuelewi…’nikasema sasa kwa ukali.‘Ninachosema mke wangu ni hivi, kama wazazi wako eeh...wangeliuchukua ule mkataba, kabla ya mimi sijaupitia vyema, wangeliweza kutoa maamuzi na mimi nikakubalia tu, maana sikuwa na uelewa …maana wangeliangalia kosa, na adhabu ya kosa, lakini je vipengele vingine, vya kutulinda, mimi na wewe , je kipengele cha mamlaka yangu...’akasema.‘Kwahiyo wewe ulikwenda kwa marehemu ukamwambia umefanya kosa, na mkataba unasema ukifanya kosa adhabu yake ni hivi, sasa ufanyeje, si ndio hivyo, ukampa mkataba, yeye akafany alichofanya, akakurejeshea na kusema sasa kila kitu kipo sawa, ..mume wangu wewe hujui hilo ni kosa mnagushi mkataba halali..haya ulipofanya hivyo mlikubaliana  malipo gani sasa, maana pesa huna, ulimlipa nini..?’ nikamuuliza‘Mke wangu sio hivyo, hebu kwanza rejesha akili yako nyuma…’akatulia kidogo, na mimi nikatulia sikusema kitu.‘Hili la kupata ushauri kutoka kwa marehemu, ililikuwa ni kama hitimisho la mambo mengi yaliyokuwa yamejificha, huenda hata mimi sikuwa na mawazo hayo kabla, na sikuwa na uelewi wa kisheria kivile, unanielewa hapo, na sitakosea nikisema, matatizo yameanzia kwetu…sikulaumu,…wakati mwingine..inatokea, na hatuwezi kumkufuru mungu,.. labda nijilaumu mimi mwenyewe kwa kutokujua majukumu yangu...’akasema‘Unasema….’nikasema hivyo tu‘Kiukweli mke wangu Marehemu alikuwa rafiki yangu mkubwa sana, na mengi alikuwa akinishauri yeye, hata kabla ya hilo, na sikuwa na mtilia maanani kipindi ch aawali, niliona kama ananionea wivu,..lakini sasa yalipotokea matatizo…, ikabidi nimkumbuke…’akasema‘Matatizo gani sasa, niambie..?’ nikamuuliza ‘Matatizo,….yah, ndio nikafikia kukuomba msamaha, lakini hayo nitakuja kukuambia kwa wakati muafaka, usiwe na wasiwasi mke wangu, kwanza ni kwanza, hili lililipo mbele yetu....’akasema‘Kwahiyo sasa hivi unataka tuongelee nini hasa, hiyo kwanza ni kwanza ni nini..?’ nikamuuliza ilibidi nijishushe tu twende sawa na atakavyo yeye‘Kuna mambo kidogo, tunahitajika kukubaliana hapa leo hii, ni muhimu sana, nataka tuyaongee, ni kuhusu mikataba tu, tukakubaliana basi kinachofuata ni utekelezaji tu...’akasema, na mimi  kwa vile sikujua anataka kuongelea jambo gani, nikasema;‘Mhh, haya mambo gani hayo, mimi nakusikiliza wewe sasa...lakini mimi nitafurahi sana nikiusikia ukweli wote…’nikasema‘Ukweli,…! Mke wangu usijali,..mimi nipo tayari, nitakuambia kila kitu hatu akwa hatua, sitaki nikuchanganye, lakini hili kwanza la muhimu, ambalo ni msingi wa mengine yote, na sio kubwa kihivyo, ni kukubaliana tu, na ni wajibu wangu kufanya hivyo, na wewe kunishauri, kwa vile wewe ni mke wangu..’akasema‘Haya ongea ,..’nikasema‘Kuna mambo kwenye mkataba yalikuwa yamekaa kimtego-tego  kwangu,…’akasema‘Mambo gani sasa…?’ nikauliza kwa sauti mpaka akashtuka na kuniangalia machoni, halafu akasema‘Yapo kwenye mkataba tutakuja kuyaona,lakini haina shida saana,…’akasema‘Unaelewa ni nini maana ya mkataba, mkataba ni makubaliano ya watu wawili au zaidi au sio…sasa iweje mmoja achukue hatua ya kurekebisha mkataba uliokubalika bila ya idhini ya mwingine kwa masilahi yake…’nikauliza‘Sio hivyo mke wangu, naona kama hujanielewa, hakuna kitu kilichobadilika, mke wangu…’akasema‘Una uhakika hakuna kitu mumebadilisha, …usiseme uwongo mume wangu maana nitakuja kulithibitisha hilo,na nikifikia huko sheria itachukua mkondo wake,…’nikasema‘Sheria itasimamia kwenye makubaliano yetu..au sio, haiwezi kuvuruga yale tuliokubaliana, na yapo wazi kwenye huo mkataba au sio..na mimi sijasema kuwa nitafanya kinyume cha makubaliano yetu, na kama ilitokea tutarudi kwenye kipengele cha msamaha, nilishalifanya hilo, na wewe ukanisamehe au sio, tena mbele ya mashahidi…’akasema ‘Kuna kipengele gani kilisema kuwa wewe kama mume unaweza kubadili mkataba bila ya mimi kuwepo, au cha kukupa mamlaka ufanye wewe uonavyo ni sahihi, bila ya mimi kuwepo, eeeh hata kama inanigusa na mimi..?’ nikauliza‘Mke wangu kuna mambo yakitokea mimi kama mume ni lazima niwajibike…na hilo sio kwa mujibu wangu, mkataba unasema hivyo, mimi nina wajibu wa kuhakikisha familia yangu ipo salama, hebu ona mpaka watu wanafikia kuua,.. ujue watu hao hawana nia njema, sasa kama nisiposimama kiume itakuwaje…ilibidi mambo yawekwe sawa…’akasema.‘Unaposema hivyo, mambo yawekwe sawa una maana gani hapo,?’ nikamuuliza‘Nina maana gani eeh…ina maana mke wangu hulioni hilo, hebu jiulize ni kwanini Makabrasha akauwawa,…alichofanya yeye ni ushauri tu, na hatukuwa tumefikia mahali pa …undani zaidi, kabla hatujamalizana, kauwawa, masikini wa mungu…’akasema kiuonyonge.‘Mume wangu upo sawa kweli wewe, mbona nakuuliza hivi unapindisha hivi upo sawa au ulikunywa kidogo leo , ulishaambiwa usinywe pombe …?’ nikamuuliza maana nilimuona anaongea sasa kama kalewa, lakini hana harufu ya pombe‘Nipo sawa kabisa mke wangu, nafanya hivi ili unielewe, ili nikitoka hapa , mimi naenda kufanya kazi, usije kusema aah, nimekiuka mkataba, hapana…mkataba sasa ufanye kazi yake, mimi najiuliza hapo ni kwanini wakamuua Makabrasha…?’akasema‘Kwanini unauliza hivyo, hata mimi sijui…’nikasema‘Unaona eeh, wewe ni mke wangu , mambo kama hayo mimi ndiye nilitakiwa niwajibike, …lakini kwa pupa na tamaa za watu,  ndio ikafikia hapa,…kuna mambo yanahitajia umakini, sio jaziba, …’akasema‘Una maana gani hapo kuwa unanishuku mimi,…  eeh mimi nimejikuta katikati ya mambo haya, na hata kushutumiwa kuwa mimi ndiye niliyemuua, wakati sijui kabisa ni nini kinachoendelea, lakini ukweli utajulikana tu…’nikasema‘Umeonaeeh, sasa hiyo ni hatari..ina maanisha watu hao wapo tayari hata kuua, kisa ni nini, ..kwa vile kagusa kwenyewe, kwenye mali, au…labda walihis kuwa tumeingilia mambo yao hapana hatukuwa na lengo hilo, basi kama ni hivyo watakumaliza sote, next ni mimi…’akasema‘Kwahiyo kumbe wewe kuna  watu unawashuku tayari je umeshawaambia polisi..?’ nikauliza‘Aaah,..hiyo ni kazi yao bwana, sijaongea lolote na polisi, usiwe na wasiwasi kabisa na hilo…lakini kiuhalisia si inajionyesha, ni kwanini wamuue huyo wakili, ni kwanini…ina maana kuna sababu, na jiulize ni kwanini itokee kipindi hiki ambacho anahangaika kuyaweka mambo yetu sawa..’akasema‘Mambo gani yetu..?’ nikamuuliza‘Kama huo mkataba..’akasema‘Ehee..mkataba una nini labda ambacho yeye alitaka kuweka sawa..?’ nikamuuliza‘Yeye alishajitolea kuusimamia, kwa masilahi ya familia…unaona, hata kama ni kusimama mahalamani, ilimradi tu masilahi ya familia yetu yalindwe, na mimi nilikubali kushirikiana naye, na ndio tulikuwa kwenye mipango ya kukufafanulia hayo hatua kwa hatua, nina imani ingelimuelewa tu…sasa wamemuua..’akasema sauti kama ya kutaka kulia.‘Kwahiyo unataka kusema kuwa kauliwa kwa vile alikuwa akihangaika kuyaweka mambo yenu sawa, kutengeza mkataba wenu wa kugushi, kwahiyo waliomuua ni hao ambao hawakubaliani na huo mkataba wenu wa kugushi, au sio..?’ nikamuuliza‘Usiseme mkataba wenu wa kugushi, rekebisha kauli yako, huo ni mkataba wetu na wewe ndiye uliyebuni hayo, au sio, na kiukweli sio mkataba wa kugushi kabisa, niule ule mkataba, au umeshakuwa mkuki kwa nani…eeh, hapana usiwe na wasiwasi mke wangu, …na kiukweli hao wanaoupinga ni kwa mashaka yao tu, na na..ulikuwa hauwahusu au sio,…’akasema‘Na ni nani hao…ambao mnawashuku kuwa hawatakubaliana na mkataba wenu wa kugushi,..ukisema hivyo moja kwa moja unamnyoshea mtu kidole, maana mkataba ule wa asili ulikuwa kati yangu mimi na wewe…‘Sio swala la kushuku,..uhalisia unaonyesha..’akasema‘Sasa ni nani, maana ukiacha wewe , mwingine kwenye mkataba huo ni wakili wetu, na mimi…kwahiyo unataka kusema nini hapo, kuwa ni mimi nimemuua Makabrasha si ndio hivyo..?’ nikamuuliza‘Hapana, sio wewe mke wangu, wewe hauwezi kufanya hivyo, wewe ndio mimi, wewe ni familia yangu, mimi nawashuku wale wasiotaka mimi na wewe tuishi kwa furaha na amani….maadui wa ndoa yetu…’akasema‘Akina nani hao sasa..ni, wazazi wangu au..?’ nikauliza‘Sijawataja wao, na mimi siwezi kuwashuku wakwe zangu kihivyo, acha polisi wafanye kazi yao…na ..ni hivi mke wangu, shaka shaka ni lazima ziwepo au sio, inawezekana kabisa wakawa watu wengine tu, wakitumia mgongo wa watu tunaowafahamu, na hilo ni lazima tulifanyie kazi, tuwatafute ni akina nani hao, sisi kwa upande wetu tutakuwa tumenawa mikono au sio…’akasema‘Sasa niambie ukweli, unataka nini sasa….maana kama hutaki kuniambia ni kwanini ukachukua maamuzi ya kubadili huo mkataba..sizani kama tutaelewana, kwa hali kama hiyo sitaweza kukuamini kamwe..?’ nikamuuliza.*********‘Hata mimi mume wako huniamini, hahaha, utaniamini tu, wewe ni mke wangu, huwezi kwenda kinyume na mimi, au sio, na ukweli upi basi, ndio huu ninaokuambia, tulianzia kwenye hii fitina ya mkataba, hii haikuja hivi hivi tu…lakini marehemu akaigundua, na kunionya kwa hilo, ahsante marehemu…’akasema.‘Mume wangu utaniambia ukweli au uondoke zako..?’ nikamuuliza.‘Mimi ni mume wako, nitakuambia ukweli wote usijali, si ndio nimeanzia hapo kwenye mkataba, kuwa hauna shaka, mimi nilikuwa sifahamu yaliyomo, sasa nimeyafahamu na ndio maana nimeanza kuufanyia kazi au..?’ akasema na kuuliza. ‘Sikiliza mume wangu, usije ukajidanganya na huo mkataba wa kugushi, ukajiona kuwa upo salama, huo mkataba ni wa kugushi, ni ukiukwaji wa sheria, na hilo tunaweza kulithibitisha  kisheria, kuwa huo mkataba wa sasa ni wa kugushi...hata kama kila mbinu zimetumika,… kuubadili na kusambaza nakala kila mahali husika,.. haisaidii kitu , kwani wakili aliyesimamia hiyo hayupo, ..’nikasema.‘Hakuna kosa kwenye huo mkataba mke wangu, kila kitu kipo sawa-sawa, na sijui kwanini unauita mkataba wa kugushi, wakati ni wewe mwenyewe ulikuja na wazo hilo,iweje leo maneno yako uyapinge, au una ogopa nini, usiogope mke wangu mimi nipo ...’akasema.‘Huo mkataba mpya mimi siutambui, maana sikushirikishwa,..kwanza ni mkataba wa nani na nani, ...nasema hivi ukinielewa nina maana gani,  na usinione mimi ni mjinga kihivyo….sasa ni hivi ili tuelewane mimi na wewe, nauhitajia ule mkataba wa mwanzo kwanza…’nikasema‘Mkataba wa mwanzo upi tena mke wangu…?’ akauliza‘Mume wangu usitake tubishane hapa, nikuuliza tu, kama uliona kuwa kuna marekebisho, ilikuwa ni haja gani kuhangaika hivyo, ungelianiambia tu, kuwa kuna sehemu hupendezwi nazo, basi mimi na wewe tungelikaa tuone tufanye nini au, huo ndio uungwana ...’nikasema.‘Na mimi narudia tena kukuambia mke wangu, mimi sijui kama kuna mkataba uliogushiwa, upi huo uliogushiwa, kwani kuna mikataba mingapi, mkataba niujuao ni huo huo, na kama kuna kitu basi tutakaa tutaongea , hilo halina shaka, ila kwa leo eeh...!’akasema na kunifanya sasa nianza kukasirika, nilishaona mume wangu kadhamiria.‘Mume wangu acha hayo maneno...kwa kauli yako ya kuzunguka zunguka, kuna muda ulisema kama wazazi wetu waneguchukua kama ulivyo, ndoa yetu ingelivunjika, je hivyo vipengele vya awali vya kuuvunja  ndoa, ni vipi na hivyo vya sasa vya kufanya isivunjike ni vipi, mume wangu nakuona kuwa mkweli tuyamalize haya mambo kwa amani,....’nikasema.‘Mke wangu, mimi sijui mambo ya kugushi mkataba,...mimi sio mwanasheria, nitagushi vipi mkataba, na mkataba huandikwa na wanasheria, baada ya mimi na wewe kukubaliana, tulikubaliana au sio…na mwanasheria akafanya kazi yake, na ndio mkataba ninao ufahamu mimi,...’akasema.‘Una uhakika na hayo unayoyasema…mume wangu usitake tupelekane kubaya, mimi sipo hivyo, kawaida yangu ni haki na ukweli, kwanini tusiwe hivyo mume wangu unataka nini lakini, niambie…?’ nikamuuliza na yeye kwanza akaniangalia, halafu akaangalia chini na kusema;‘Mke wangu, mimi nina uhakika na hilo ninalolisema, nimeshakuambia kuwa mimi nakupenda sana kweli si kweli,…, na hayo yaliyofanyika, yalifanyika kwa nia njema tu, ya kuilinda ndoa yetu,  na nakuhakikishia kuwa mkataba wetu upo vile vile na mambo yake mazuri tu…, na mimi nitakuwa mume mwenye mamlaka kama mwanaume, sio mwanaume jina tu...’akasema‘Una maana gani kusema hivyo?’ nikamuuliza.‘Mkataba ndivyo unavyosema hivyo...kuwa mimi kama mume nitakuwa na mamlaka ya uongozi wa familia, nitaweza kupitisha maamuzi, kama nionavyo ni sahihi kwa masilahi ya familia, hilo halihitajii mjadala, au sio…hata bila kuwa na mkataba hilo lipo wazi, kwanini hunielewi…?’ Akaniuliza‘Huo mkataba  wa kugushi ndio unasema hivyo, hicho kipengele ni kigeni kwangu ..’nikasema‘Na...wewe utakuwa msaidizi wangu, na hiyo ndio kawaida ya mume na mke, mambo mengine ni ya kuiga tu, ..hayana maana kwetu, ndio hata Marehemu aliyaona, lakini sio kitu kikubwa sana, maana mimi ndio nilitakiwa nilione hilo, na mimi ndio natakiwa kusema..au sio,…’akauliza na mimi nikaa kimia‘Mke wangu, kikawaida eeh, mimi ndio natakiwa kuwa kiongozi wa familia,na ikibidi kurekebisha jambo kwa masilahi ya familia, sihitaji kibali au sio…ili kuikoa familia, na kila kitu, huo ndio ukweli, zaidi ya hayo, mimi natakiwa kuilinda familia yangu, ukisaidiwa na wewe mke wako, kwani hapo kuna makosa, ni maneno yale yale...’akasema.‘Haya unayoyaongea wewe yapo kwenye huo mkataba wa kugushi au sio sio kwenye mkataba sahihi tuliainisha wazi kuwa, ili kuondoa utata,  kila jambo litafanyika kwa makubaliano,….na hili uliliongeza wewe siku ile ya majadiliano,…na tulikubaliana kabisa kuwa asilimia kubwa ya mambo yetu yapo kwenye mkataba, kwahiyo kama kuna kasoro, au jambo lolote limejitokeza lenye sintofahamu basi, tukae tujadiliane..’nikasema‘Sawa kabisa,…’akasema‘Na hii ina maana gani, mkataba hauwezi kubadilika mpaka kuwe na kikao cha kukubaliana, akiwemo wakili wetu, sasa hayo ya mume kujiamulia mwenyewe akiona kuna sababu, yanatoka wapi,, na kwanini kuwe na mabadiliko, kuna nini kilitokea,…?’ nikamuuliza‘Mkataba ni ule ule mke wangu, hakuna kilichobadilika, hata ukiuangalia, eeh, ni mambo yale yale, na yote…tulikubaliana mimi na wewe ..na wakili wetu…wewe ni wasiwasi wako tu’akasema.‘Tatizo lako, Makabrasha alikuingiza kwenye anga zake za ulaghai, na umesahau kuwa wewe sio mwanasheria, huyo mtetezi wako sasa hivi hayupo tena duniani, kuna mambo ya kisheria huyafahamu,...na hayo yatakupeleka pabaya,...mkataba  uliokubalika kisheria ni ule tuliokaa mimi na wewe tukakubalina sio huo uliokaa wewe na mwanasheria wako, ....’nikasema.‘Ndio huo huo mke wangu, wewe una nakala yako, na mimi nakala yangu, nenda unapoziweka ukazichukue,…lakini mimi nina nyingine hapa, na nisisahau nakala nyingine ipo huko kwenye vyombo vya sheria… hakuna mkataba mwingine...kila kitu kipo vile vile, hakuna kilichobadilika, na wewe na mimi tuliweka sahihi zetu na ya mwanasheria wetu, ndio hivyo...’akasema.‘Mwanasheria gani?’ nikamuuliza.‘Mwanasheria wetu wa familia, ..ngoja nikuonyeshe mkataba wetu, ninao nakala yetu hapa..hakuna kitu kilichobadilika, ni mambo madogo madogo tu ulikuwa huyajui labda, ndio yanakuchanganya, eeh, usijali kabisa, hata kama wamemuua Makabrasha kuwa labda, nitakosa mtetezi, mimi mwenyewe nitajitetea,..na haya yote mke angu ni kwa ajili ya masilahi yetu sote...’akasema huku akiutoa huo mkatabaNa wakati anafanya hivyo macho yangu yakahisi kama kuna mtu kasimama kwa nje, nahisi alikuwa akisikiliza tunachoongea, akasogea kidogo, …sikuweza kumtambua ni nani,...nikataka kumpa ishara mume wangu, lakini hakuwa makini na yeye akawa ananionyesha sehemu zile za sahihi akasema;‘Huu ndio mkataba wetu,..unaona hii hapa ni sahihi yangu, hii ni ya kwako, hii ni sahihi ya mwanasheria wetu wa familia, mkataba ni ule ule, utabadilishwaje na nani afanye hivyo...hakuna kilichobadilika kabisa , ...unaonaeeh...’akasema huku akifungua fungua huo mkataba, na mimi nikawa namuangalia tu‘Mume wangu usitake tufikishane huko..huko unapokwenda ni kubaya, usikubali hayo mambo aliyokudanganya Makabrasha, ..huyo jamaa anajulikana sana kwa hadaa na ulaghai, hata watu wa usalama wanalitambua hilo..sasa na wewe usiwe mshirika wake, tunachotakiwa kwasasa ni kusahihisha yale makosa yaliyotokea, ili tuanze pale tulipoishia, ..’nikasema‘Ndio hivyo mke wangu ndio maana hata kama unataka basi hata huu mkataba tuachane nao au sio, na mimi niwe na mamlaka yangu kama mume wako au sio, mbona wengine wanaishi tu  bila hata ya mikataba unaona eeh, ni kwanini sisi, sababu ya mali au...’akasema‘Sikiliza mume wangu,….tusilazimishe migogoro isiyo na msingi, na tusitake kulazimisha chuki na uhasama, wakati kuna njia nzuri ya haki, yenye kuleta mariziano na maafikiano,...hebu nikuulize hivi wewe unachotaka hasa ni kitu gani, niambie ukweli ?’ nikamuuliza mwishoni.‘Nakupenda sana mke wangu , sitaki mimi na wewe tuachane, mimi nataka ndoa yetu idumu na tuishi kwa amani na upendo...’akasema‘Ni nani kasema hatupendana na hiyo hoja ya kuachana inatoka wapi, eeh, kuna nini kimeileta hiyo hoja ya kuachana?’ nikamuuliza.‘Mkataba…eeh, …je ikiingia fitina, na wewe ukaridhia nayo, wakaja wazazi wako ukasema mkataba huu unasema hivyo, itakuwaje, fitina ni mbaya mke wangu, kuna watu walishajenga majungu, na hata rafiki yako analifahamu hilo, nina uhakika hadi anaondoka bado mlikuwa hamjawa sawa, kweli si kweli, na wewe ndiye ulikuwa mshauri wake mkuu, kila jambo anafanya kutokana na ushauri wako,…lakini hayo yamepita kila kitu kipo sawa sasa, au sio,...’akasema‘Ndivyo alivyokuambia kuwa kila alichokifanya kinatokana na ushauri wangu..?’ nikamuuliza‘Rejea hoja yetu , kuhusu mkataba ni nani alitoa pendekezo hilo, lengo lake hasa ilikuwa ni nini, sema ukweli wako wote, na je sio kweli kuwa wewe na rafiki yako, mlikuwa mnashauriana mambo mbali mbali, tatizo lako wewe mke wngu unasahau, unashauri baadae ikigeuka unakana, usiwe hivyo, mkuki usiwe kwa nguruwe tu…’akasema‘Sawa, tuwe wa kweli sote, je kuna vipengele kwenye mkataba mlivirekebisha wewe na Makabrasha tumalizane na hilo…?’ nikauliza‘Hapana, hakuna kilichobadilika, …zaidi ni kuhakikisha kuwa mume ana mamlaka yake, mimi hizo sehemu nilikuwa sijazisomi, nilipozisoma na kuziona nikajua kumbe nilikuwa siwajibiki..’akasma‘Haya sawa, sasa nikuulize ni nini lengo la hayo yote , ni ndoa au ni mali…?’ nikamuuliza na hapo akashituka na kuniangalia machoni.‘Mke wangu nimesema kuwa nakupenda sana....sipiganii mali hapa.., ninachopigania ni ndoa yetu,ndoa ni kila kitu humo..ni kwanini  niipiganie mali wakati ipo , mali tunayo au sio, tuna vitega uchumi vingi, ni swala tu la kuviendeleza....huwezi kupigania kitu chako, eti mke wangu, mbona sikuelewi...’akasema.‘Kwa hatua mliyofikia, hakuna jinsi, ni lazima ule mkataba wa asili uwepo, na huo wenu uwepo, tuangalia je ni kweli hakuna kitu kilichobadilishwa, najua kuna madhambi umeyafanya, na kulikuwa na vipengele vya kukuwajibisha, ukaogoa, ndio maana ukakimbilia huko kwa Makabrasha.’nikasema‘Usimsingizie marehemu uwongo, yeye sio kazi yake kuondoa kitu kwenye mkataba, maana sio yeye aliyeutunga,..kazi yake kubwa ilikuwa ni kunifafanua na kunishauri, yeye ni kweli, alipitia mkataba wetu, akausoma, na kuniambia upo safi kabisa, akanionyesha hivyo vipengele muhimu ambayo mimi nilikuwa sivitilii manani, vya mamlaka yangu...’akasema.‘Kwahiyo ndio ukafanya ulivyoona kuwa ni sahihi,..hata kama mimi sijarizia, ?’ nikamuuliza‘Nimefuata mkataba unavyosema, au sio mke wangu, na .., kama ilitokea kukosea huko nyuma, ni kwa bahati mbaya, ndio maana nilikuomba msamaha kipindi kile, unakumbuka,… sisi kama wana ndoa wakati mwingine tunakosea kama wanadamu, na kama mkataba unavyosema mtu ukikosea unatakiwa kutubu, na kuomba msamaha, nilitimiza hayo au sio ...’akasema‘Mume wangu sitaki kusikia hayo tena, tafadhali, nakuomba uondoke, nataka kupumzika, naona unazidi kunichanganya tu, hayo ni mambo yenu na marehemu, naomba usiongelee tena kuhusu huo mkataba wenu wa kugushi....’nikasema‘Lakini mke wangu kuna jambo jingine muhimu kabla sijaondoka, ...kuna mtu anasubiri, maamuzi yangu mimi na wewe’akasema‘Nani anasubiri hayo maamuzi yangu mimi na wewe, na hapa tulikuwa tunaongea tu, na wewe mwenyewe ulisema kuwa haya ni mimi na wewe,huyo mtu mwingine inamuhusu nini hapa …na nikuambie kitu,hakuna maamuzi yoyote yamepita hapa, ..hatujakubaliana lolote hapa.mimi siutambui huko mkataba wenu, nitakubaliana na mkataba wetu ule wa awali zaidi ya hapo mimi sipo.’nikasema.‘Kuna mtu muhimu sana, alikuwa anasubiria haya maamuzi yetu, ni haki yake lakini, na mimi nilikuja kutimiza wajibu wangu, kuomba ushauri wako…’akasema‘Mtu gani huyo, na ana haki gani hiyo…?’ nikauliza‘Ni mtoto wa marehemu, anahitajia maamuzi yetu, ...’akasema, na hapo nikahisi moyo ukiniruka, ni kama mtu kakushtua ukiwa hujui‘Nimeshakuambia hakuna maamuzi yoyote yaliyopitishwa hapa, kama una lako jambo endelea kivyako, na kama umedhamiria hayo uliyokusudia, basi tutapambana mbele ya sheria, wewe si mjanja, sawa endelea na mpango wako huo, kila la heri ..’nikasema‘Mke wangu usifike huko…’akasema‘Usipoleta mkataba ule wa awali tutafika huko, maana nakuona hutaki kunielewa,  na hutaki kusema ukweli, usihadaike na tamaa za watu wengine, kumbuka tulipotoka, na kila mara nilikuwa nakuasa, acha tamaa, tushikamane, tuwe kitu kimoja, sasa haya yote yanatoka wapi, unataka nini husemi…, au kuna kitu gani kimetokea, hutaki kuniambia ukweli,…kwa hali hii bora uondoke, hapa sijisikii vyema nataka kupumzika,…’nikasema‘Sawa kama umechoka hujisikii vyema mimi nitafuata mkataba unavyosema, au sio, mkataba umenipa mamlaka ya kufanya yale yaliyosahihi kwa masilahi ya familia, na na nilichokuja kuonana na wewe ni kupata ushauri, …wewe pumzika, mambo mengine niachie mimi, au sio mke wangu…’akasema. ‘Au sio kuhusu nini…mimi sijakushauri kitu hapa..’nikasema kwa hasira‘Mke wangu si umesema niondoke,unataka kupumzika, au?’ akaniuliza huku akigeuka kuniangalia.‘Sina cha kuongea na wewe hadi hapo utakapoleta ule mkataba wa zamani, na kuniambia ukweli wote, vinginevyo hatutaelewana...’nikasema.‘Hamna shida mke wangu, ..tutaongea tu, wewe pumzika,  mimi ni mume wako wa halali, hakuna kibaya kitakachotokea, yote niachie mimi, mimi nitatimiza kila kitu kama tulivyoainisha kwenye mkataba wetu..’akasema kwa kujiamini.Na mara mlango ukafunguliwa,kwa nje, lakin hao watu hawakuingia, ulionekana mkono tu,..nahisi ni zaidi ya mmoja maana nilisikia wakiongea, walikuwa wakibishana jambo …mara mlango ukafunguliwa wote sasa, nikaweza kuwaona wapo watu wawili, kwa upeo wangu. Huyu mmoja alikuwa karibu sana na mlango, nilipomchunguza kwa makini nikaona kama anafanana sana na marehemu nahisi atakuwa ndio huyo mtoto wa marehemu, kwa muda huo alikuwa akitaka kuingia ndani, na mume wangu akawa kamuwahi na akamzuia,akisema;‘Mke wangu kachoka, naona mambo yote nitayamaliza mimi mwenyewe, tunaweza kuongea huko mbele ya safari, au ulikuwa unasemaje…?’ akauliza sasa wakiwa wamesimama mlangoni kwa nje.‘Huyu ndiye yule wakili wangu niliyekuambia, atachukua nafasi ya baba yangu..’sauti yule ambaye nahisi ndio mtoto wa marehemu ikasema. Na hapo hapo nikachukua simu yangu kwa siri, nikawaweka sawa kwenye kiyoo cha simu na kuwapiga picha, huku nikimchunguza huyo mtu mwingine ambaye ni wakili kwa kauli ya huyo mtoto wa marehemu, kwa hisia zangu nilimuona ni kama aina za Marehemu, kwa hisia zangu tu.‘Habari yako muheshimiwa, …’ mume wangu akasalimia, na wakati anasalimia ndio akagundua kuwa mlango bado upo wazi, akasogea na kushika mlango na kuufunga. Hata hivyo nilikuwa tayari nimeshawapiga picha.Na mimi nilipohakikisha mlango umefungwa,   kwa haraka nikampigia simu wakili wangu.‘Sikiliza kama ulivyonishauri haya ni mazungumzo yangu mimi na mume wangu nimeyarekodi, na picha zao nakutumia sasa hivi, yasikilize na wewe utajua ni nini cha kufanya , wahi kabla hawajafanya lolote, sawa...’NB: Doa la tamaa limeshagusa mtima, ibilisi hachezi mbali hapo,...je itakuwaje, Kwa leo inatosha.WAZO LA LEO: Imani ya kweli ya ucha mungu ni pale upomjali mwenzako, na ukawa tayari kutoa hata kile unachokipenda kumsaidia mwenzako, na ukajali jirani zako, lakini hayo yote kwa ajili ya mwenyezimungu sio kwa ria. Je ni wangapi wapo tayari kuona mwenzake anapata kabla yake, au zaidi yake, ni wangapi wanayajali matatizi ya wengine, ni wangapi wanaona mali ni kitu tu cha kupita, awe tayari kusaidia wengine, hapa ni mtihani! Kiukweli ndoa yangu ilianza kuwa na wakati mgumu, na ikafikia mahali nikaona nianze kufanya yale ambayo sikutaka kabisa kuyafanya katika maisha yangu, na katika ndoa yangu, na hata ikafika mahali sasa nianza kuamini kuwa mume wangu hakuwa mwaminifu kwangu, kifupi kasaliti ndoa yetu, lakini bado nilitaka nisikia kauli yake mwenyewe akikiri ..‘Nimetoka hospitalini, lakini sina amani..’nikasema‘Kwanini mke wangu, …upo huru, hiyo kesi isikutia mashaka, haina nguvu, mimi nitaifuatilia na kuhakikisha imekwisha…’akasema‘Sio kuhusu kesi,…ni kuhusu hayo yaliyosababisha hadi tufike hapa tulipo, sijafahamu ukweli wake bado..’nikasema‘Kama yapi..eeh, niambie mke wangu nitakuambia kila kitu..’akasema‘Kwa hili ilivyo yaonyesha wazi, kuwa wewe umenisaliti,..umeenda kinyume cha makubalianio yetu, na nilikuambia tokea mwanzo, kuwa tunaoona, lakini tuchunge milaka ya ndoa yetu, nikakuuliza je kweli unanioa kwa mapenzi au kwa mali, unakumbuka ulisemaje…?’ nikamuuliza‘Kwa mapenzi…nilikahidi na ni kweli…’akasema‘Sivyo ilivyo, kidogo kidogo inaanza kudhihiri..naanza kuhisi kuwa huenda nilifanya makosa, naanza kuuona ukweli wa wazazi wangu…’nikasema‘Lakini sasa mke wangu ulitaka mimi nifanye nini, tuangalia ukweli na uhalisia, mimi sio mume wako…eeh, hebu angalia maisha tuliyokuwa tukiishi je kweli mimi nilionekana kama mume wa familia, swali ni kwanini mpaka ikafikai kubuni hiyo mikataba, wangapi wana hiyo mikataba kaam mume na mke eeh…’akasema‘Jibu na swali lakini ni kuwa nilitaka kuwe na kitu cha kuhakikisha kauli yako, maana wazazi wangu walisema mengi, kukuhusu wewe, na sio kukusema tu lakini rejea maisa yako ya nyuma yalivyokuwa na zaidi nilitaka kuhakiki kauli yako, na sasa je umetimiza ahadi yako…?’ nikamuuliza‘Mke wangu ulitaka nifanye nini zaidi ili uonye kuwa mimi nimetimiza ahadi yangu, nimekuwa mwanaume mtiifu kwako, kila utakacho mimi nakifanya, lini nilikukaidi eeh, na wewe je..umetimiza kila nilichokitaka..sema ukweli wako…’akasema‘Kitu gani ulitaka kutoka kwangu mimi nikakukatalia,…?’ nikamuuliza‘Mke wangu karibuni hapa, nimekuomba ukubaliane na mikataba , tukianzia na huo ulioubuni wewe mwenyewe, umekataa…huo ni mfano tu, haya maisha ya ndani ya familia, nilikuomba tujitahidi tupata motto mwingine,…mungu angejalai tupate sasa wa kiume, uli…ulileta vipingamizi..sasa ulitaka mimi….’hapo akatulia.‘Kuhusu mkataba, hilo sitaweza kukubaliana na lo, huo mkataba wa kugushi mimi siutambui,, unasikia,…na hilo ni muhimu katika mustakabali wa maisha yetu, usiporejesha huo mkataba wa zamani, basi ….’nikatulia‘Mkataba mkataba…unaona mke wangu, huo ndio unaona ni muhimu kuliko ndoa yetu au sio..’akasema‘Mkataba huo ulikuwa wa hiari, tulikubaliana sote, ukakubali mbele ya wakili, kwanini ulikubali, na kwanini sasa uupinge, na kwanini ugushi ..ina maana kuna jambo umelifanya lipo kinyume na mkataba …na huenda kinyume na ndoa yetu..’nikasema‘Mkataba ulitusaidia sana tokea awali, maana ndani ya huo mkataba tuliweka yote ambayo yatamlinda kila mtu, na kulinda mali zetu kwa ajili yetu na familia zetu, na hili nilitaka kuwaonyesha wazazi wangu kuwa wewe kweli umebadilika, nilitaka kujithibitishia hilo mimi mwenyewe …ili niishi kwa amani…’nikasema‘Hebu mke wangu tusilumbane zaidi, mimi nakuuliza hivi kwani kuna tatizo gani.‘Tatizo ni kuwa wewe hutaki kuniambia ukweli, …’nikasema‘Ukweli upi mke wangu..?’ akauliza‘Najua hutaweza kuusema wote, nafahamu kuwa hapo ulipo unajiaminisha kuwa vyovyote itakavyokuwa mkataba wa kugushi utalikulinda, lakini hebu fikiria, je ulichofanya ni sahihi, je sio kweli kuwa umeisaliti ndoa yako, na bado, hukutaka kutubu, ulichofanya wewe ni kutafuta mbinu za kunufaisha matamanio yako,…’nikasema‘Mke wangu kumbuka, kule hospitalini,nilifanya nini..sikukuomba msamaha mie.. ukasema umenisamehe…’akasema‘Kwa kosa gani sasa…?’ nikauliza‘Makosa yote ya kibinadamu, mimi sio malaika, mimi ..ni mwanadamu tu, nateleza, sasa siwezi kusema kila kosa nililolofanya, ..unajua mke wangu, eeh mimi ni mtu mnzima, kuna makosa mengine nilifanya kwasababu maalumu,..japokuwa huenda wewe unaweza kuona sio sahihi, lakini nilikuwa na sababu ya msingi sana…’akasema‘Makosa kama yap hayo ya msingi kwako,…?’ nikamuuliza‘Hilo ni moja ya mambo ambayo nahitajia kukaa na wewe , najua utanielewa, vuta subira, lakini nakuhakikishia sio kwa nia mbaya kabisa, ni katika kuhakikisha ndoa na mali zetu zinabakia mikononi mwetu, wewe hulijui hilo kwa vile umefunikwa na …wazazi wako…’akasema‘Je ni kweli kuwa umenisaliti…?’ nikauliza‘Kwanini unasema hivyo mke wangu, hapana sijakusaliti kwa maana hiyo unayoitaka wewe, najua kwako wewe utaona ni makosa, lakini mke wangu nilifanya hayo nikiwa na sababu za msingi, sikufanya hayo kwa kupenda kwangu, ..najua labda hutaweza kunielewa, ndio maana nikakuomba msamaha..’akasema.‘Nikuulize tena je ni kweli kuwa una mtoto nje ndoa..?’ nikaona nimuulize hivyo‘Mtoto nje ya ndoa una maana gani mke wangu, …unajua nilishakuambia kuna mambo mengine nisingelipeda kuyaongea kwa sasa, kwa sababu yanaweza kuleta picha mbaya, kutokana na ushauri wa wakili wetu, alinishauri marehemu na sasa huyu wakili mwingine hayo yanahitajia , tukae tuyajadili mbele yake, ili kila kitu kiwekwe sawa…’akasema‘Sizani kama tutakuja kuelewana…mimi nasema hivi, nataka ule mkataba wa awali kama kweli una nia njema, ..na ukiwepo, nitakaa na huyo wakili wako, …vinginevyo, kuanzia sasa sitaki maongezi na wewe…’nikasema na kuondoka kuendelea na shughuli zangu.***********Pamoja na hayo aliyoyafanya mume wangu kugushi mkataba, lakini kuna kitu walishindwa..na hapo ikabidi kila mara aje kwangu kuniomba na kila akija kwangu tunaishia kwenye malumbano tu…Siku moja akaja na kuniomba tukae tuongee, mimi sikuwa na shida, kuongea tu, ..‘Mke wangu kuna mambo yanakwama, hatuwezi kufanya mambo ya maendeleo..’akasema‘Mambo gani…?’ nikamuuliza‘Ya kibenki…’akasema‘Kwani kwenye huo mkataba wenu wa kugushi, hamuwezi kufanya na hilo…?’ nikamuuliza‘Mke wangu…’akataka kusema ‘Kama unataka tuelewane, rejesha ule mkataba wa awali, hapo tutakaa meza moja kama mke na mume, lakini kama utaendelea na mkataba wenu huo wa kugushi, basi, nitakuacha uendelee na maisha yako na mimi nitaendelea na maisha yangu...’nikasema.‘Hapana, siwezi kukubali hilo, mimi ni mume wako na mimi ndiye kiongozi wa familia, na natakiwa kuhakikisha familia yangu ipo pamoja, ...nataka watoto wetu watuone tuna upendo na mshikamano,..’akasema.‘Wewe ndiye uliyesababisha haya yote, kashifa imeingia kwenye familia  , tumeanza kwenye ulevi, ndoa isiyo na masikilizano, ..kuzaa nje, imekwenda hasi kushutumiwa kuua, kugushi, ulaghai, hivi hayo ni maisha geni unayoyataka wewe, mimi sijakulia kwenye maisha ya namna hiyo, familia yangu ni safi....’nikasema‘Ina maana unaninyanyapaa kuwa familia yangu ni chafu, ndio maana haya yote yanatokea?’ akauliza‘Usiongelee kuhusu familia yako ongea kuhusu wewe mwenyewe,...kwasababu wewe una uwezo wa kujibadili na kuwa mtu mwema, mwaminifu, mkweli ....unaweza kabisa, lakini kama unataka kuishi kwa ujanja ujanja...hutafika mbali...’nikasema.‘Mke wangu mimi kama mume wako, naomba kauli hiyo, ya kuiniona mimi mchafu, tapeli mlaghai,..iishie,tafadhali, maana sasa unataka na mimi niwe mkali eeh,  ..’akasema huku akinitolea macho, na mimi nikatabasamu na kusema;‘Itaisha pale utakapoleta mkataba wetu wa awali, tuliokubalina kwa ridhaa moja,....’nikasema.‘Mkataba ni mmoja tu, hakuna mkataba mwingine, mkataba ni ule ule,...ila wewe unataka kunipanda kichwani, ili nisiwe na sauti kama mume..hili mimi siliafiki,...na nakuomba mke wangu, jaribu kuniangalia na mimi, unielewe na mimi...kwani nimefanya nini kibaya’akasema kwa sauti ya upole.‘Wewe sio mkweli, ...’nikasema‘Kwa vipi, mbona nimekuambia ukweli, kuhusu mkataba wetu, ...sijaukiuka, ..kuna jingine  mke wangu, hakuna, nimejaribu kuwa mume mwema, silewi tena, hilo huliungi mkono, unataka nianze kuelewa tena, unafahamu madhara ya kulewa, eeh, unataka nikafanya nini sasa...’akasema.‘Usibadili mada, mkataba wetu wa zamani upo wapi,..pili huyo mtoto uliyezaa nje ni nani, na umezaa nani, nijibu hayo maswali, na hayo ukiyaweka wazi, tutakubaliana, ...’nikasema.‘Mkataba hauna shida, mkataba ndio huo, mimi sijui mkataba mwingine, na ni nani huyo mtoto niliyezaa nje eeh nionyeshe..’akasema‘Una uhakika na hilo, maana likija kutokea kuwa haya ninayoongea ni kweli, sitarudi nyuma tena...’nikasema.‘Mke wangu matendo yako ndiyo yaliyonisukuma hadi nikafika huko, sikuwa na raha kama mume, wewe muda wote upo na kazi zako, sikuwa na raha kama mume, sikuwa na sauti kama mume, nilikuwa nipo nipo tu,....nikawa natafuta njia ya kijiliwaza,...nikaona pombe atakuwa mpenzi wangu, kumbe pombe ina mitihani yake..je sasa watana nianze tena hayo maisha.’akasema huku natamani kumzaba kibao, nilimuona kama mtoto mdogo vile.‘Hivi wewe hujitambui hayo unayoyaongea, unaongea kama mtoto mdogo, ..ulewe kwasababu ya kujiliwaza, ....sikuelewi, ulienda kulewa kwasababu ya starehe zako, mimi muda wote nilikuwa hapa ndani, kwanini hukuniambia unachokitaka wewe...?’ nikamuuliza.‘Mke wangu mke wangu, ya kale yamekwisha, nakuomba mke wangu tuishi kama mke na mume, tupendane kama zamani, tugange yajayo....’akasema.‘Hujanijibu huyo mtoto uliyezaa nje, ni nani na ulizaa na nani?’ nikamuliza.‘Hilo nitakuambia pale utakapokubaliana na mkataba wetu, maana kila kitu kipo wazi, na kama unachosema ni kweli basi tutaambizana....’akasema. ‘Unanichefua,...nashindwa hata kukuelewa, sikiliza, mimi ninakupa wiki moja, nataka mkataba wa zamani uje, kama hautapatikana basi, ...tutaita mawakili wetu, tutaangalia haki ilipo, na ikibidi tutafikishana mbali,...nisingelipenda kuwashirikisha wazazi wangu kwa sasa...ila baada ya wiki moja hiyo kwisha, kama utaendelea na ujinga wako huo....hutaamini kuwa ni mimi...’nikasema.‘Mke wangu, kwanini unakasirika,...kwanini yote hayo, mbona mimi nakupenda, na nafanya haya yote kwa mapenzi ya dhati...jaribu kunielewa na mimi....mbona hutaki angalau kuusoma huo mkataba hakuna kichobadiliak kabisa, na ukweli ni kuwa eeh, mke wangu, mimi nailinda ndoa yangu, mimi sitakubali kamwe ndoa yetu ivunjike, ....nakuhakikishia hilo....’akasema.‘Kama umekiuka mkataba, ambao tulikubaliana mbele ya wakili, na kauli yako na yangu ilitoka kuwa likifanyika hili au lile ndoa haipo, basi haipo, kaulize mawakili kaulize hata watu wa dini, hukulazimishwa, tulikubaliana…kwa maandishi…’nikasema‘Ni sawa, si kila kitu kipo kwenye mkataba au sio, mbona unaogopa wewe…’akasemaMimi sikutaka kuongea naye siku hiyo, nikaondoka kuendelea na shughuli zangu nyingine***********Siku zikawa zinakwenda, na mimi nikaendelea na msimamo wangu wa kutokuutambua mkataba huo waliotayarisha wao, sikutaka kulifuatilia kisheria zaidi, hata wakili wangu aliyetaka kulifuatilia kisheria, nilimwambia anipe muda kwanza nijaribu kivyangu, ikishindikana, itabidi tuingie kisheria.Ikafika mahali mimi na mume wangu hatuongeai, sikutaka hata kuonana naye, mimi niliweka agizo langu kuwa nitakaa meza moja na yeye pale tu huo mkataba wa zamani utakapopatikana. Nikaanza kumwekea shinikizo, kwanza nikakata mawasiliano ya kuongea naye, na kutokushirikiana naye kwenye shughuli zozote alizozifanya kimkataba.Ikafikia hatua hata hundi za benki ambazo nilihitajia mimi kupitsha nikazizua, kwahiyo akawa hana uwezo wa kipesa zaidi ya kiasi kile alichoruhusiwa kukutoa kwenye kampuni yake, kwani kiasi kikzidi sana ilitakiwa sahihi yangu na yake, kutokana na kumbukumbu za kibenki.Hali ilivyozid kuwa mbaya, akaona amtumie rafiki yake, ili aonge na mimi na siku hiyo akaja docta rafiki yake…akasema ana maongezi na mimi, akaanzia mbali na baadae akaja kwenye jambo aliloniitia, akasema.‘Shemeji pamoja na mengine, lakini kuna mambo ya kikazi, ukiwa na msimamo wako huo kazi zitasimama, na kampuni ya mumeo itakufa kabisa...’akasema huyo rafiki wa mume wangu.‘Kama analiona hilo ni wajibu wake, kuleta huo mkataba wa awali, na kama anajiona kuwa anauwezo wa kufanya anavyotaka basi aendelee, na siku nitakapo kamilisha uchunguzi wangu na kuwa na ushahidi wa kutosha kuwa kweli kavunaj mkataba wa hiari, kuwa yeye alishirikiana na marehemu kufanya hayo yaliyotokea, nitampeleka mahakamani....’nikasema.‘Lakini mambo ya kampuni msiyaingize kwenye mambo yenu ya kifamilia’akashauri.‘Sisi tulikuwa na utaratibu wetu mzuri tu, yote hayo ya kikampuni , ya kifamilia, tulikuwa tumekubaliana, ili kulinda mali za familia, ...kama tusingelifanya hivyo, kampuni hizo zisingelikuwepo, angalia sasa anavyofanya yeye, nasikia kuwa ana mtoto nje, na kama ana mtoto nje, ina maana ana kimada nje, ni nini kitaendelea hapo, kama sio kuanza kugawa mali halali za ndani ya ndoa kwa watu wasio na haki hiyo…’nikasema.‘Sitaki nikukumbushe ..lakini inabidi nikuambie, hayo umeyataka wewe mwenyewe...nilikuambia mwanzoni jaribu kuwa karibu na mume wako, jaribu kuangalia ana shida gani anataka nini, ujue kuwa binadamu wote sio sawa, kuna utofauti wa kuwaza, unavyowaza wewe, sio sawa na anavyowaza mwingine na uvumilivu wako sio sawa na uvumilivu wa matamanio kwa mwingine.’akasema.‘Nakufahamu sana, huenda hayo mliyapanga pamoja, ili kujionyesha kuwa nyie ni wanaume, mnaweza kufanya mpendavyo, au sio...mlewe , mtembee ovyo na wanawake , mzae ovyo, si ndio,...?’ nikamuuliza.‘Sina maana hiyo..ila maisha ya ndoa,msipovumiliana, mkaweza kukaa pamoja, mkajaribu kuziangalia zile tofauti zenu za kifikira, mkazitafutia suluhu, siku mambo yakiharibika inaweza ikaleta shida sana kujirudi, kwasababu muda huo kila mmoja atajiona yupo sahihi...kama mngelikaa na kujuana, na kuangalia mwenzangu anataka nini, mgeliweza kulizuia hilo....’akasema.‘Mwambie rafiki yako, suluhisho la haya ni mkataba wetu wa awali, kwasababu siwezi kukubali huo mkataba wa kugushi, wamekaa na mwenzake, marehemu, wakatunga mambo yao, mimi sikuwepo, na humo wameweka mambo ambayo mume wangu atajifanyia apendavyo, bila hata kibali changu....huoni kuwa ni hatari, kutokana na hilo, nasikia kuna mkataba mwingine, ambao, yeye kama mume, kutokana na mkataba huu, ana hiari ya kuuza hisa kwa mtu mwingine...’nikasema.‘Mhh, una uhakika na hilo?’ akaniuliza.‘Ndio maana sitakubali huu mkataba wao, ..kamwe, kwani nikikubali tu, kampuni yake, hatakuwa na hiari nayo, kwani hata marehemu kauziwa hisa, ...ni nani alipitisha hilo, ....hebu niambie, mimi nikubali tu, ‘nikasema‘Hilo sio kweli…’akasema‘Wewe si unanichunguza, wewe si ulitumwa kunichunguza mbona hilo hujaligundua,,,,sasa hiyo ni kazi yako, chunguza na utakuja kuniambia..’nikasema‘Mhh..kama imefikia huko,…unajua mimi nilishaachana na mambo yenu, tuliacha ili mjenge suluhu, lakni kwa hali hiyo, kama ni kweli, mmh, ‘akasema‘Sasa niambie mimi nifanya nini...ina maana gani kuhangaika, kutokulala, usiku na mchana tulihangaika, leo matunda yamepatikana, yachukuliwe na watu wengine kirahis rahisi tu....na japokuwa hajakubali moja kwa moja, yeye ana mtoto nje, na kwenye huo mkataba wao wa kugushi, motto huyo na mama yake, wana haki, na watachukua sehemu ya mali...’nikasema.‘Huyo mtoto ni nani na mama yake ni nani…?’ akauliza‘Hiyo kazi nakuachia wewe..’nikasema‘Unajua siwezi kulifanya hilo kwa sasa, wewe mwenyewe ulinipiga marufuku kufuatilia mambo ya ndoa yako, nilishakuambia kama unanihitajia ni kusaidie,nipo tayari,ukasema hutaki mim niingilie ndoa yako, kwani lengo langu ni kuvunja ndoa yako, ilinikera kwakweli, je bado una msimamo huo, je bado hutaki nikusaidie…?’ akaniuliza.‘Kama nilivyokuambia toka awali, wewe endelea na familia yako,mimi hili nitalimazia mimi mwenyewe, yupo wakili wangu, nikishindwa nitamkabidhi, na hapo itakuwa ndio mwisho wa haya yote maana kila kitu kilikuwa wazi kwenye mkataba...’nikasema‘Upo tayari kuvunja ndoa yako kwasababu ya hilo?’ akaniuliza‘Wewe unaliona hili ni dogo eeh, ikifikia hapo, hutaamini, kwanza huo mkataba wa zamani ukipatikana tu,...kama tulivyoahidiana, hatua kwa hatua, tutatekeleza, na kuna ahdi yangu kwa huyo mwanamke wake waliyezaa naye, mimi nitamuonyesha kuwa mimi ni nani...huwa nikiahidi kitu sirudi nyuma,....’nikasema.‘Ndio maana mume wako anaogopa kuuleta huo mkataba wenu wa zamani, anakufahamu ulivyo...’akasema.‘Huo ni uwoga,...yeye kama ni mwanaume, anatakiwa aingie uwanjani, apambane kiume, na asipofanya hivyo, akaegemea  mawazo ya wenzake, atakosa yote....hajui mimi ninawaza nini, hajui nina mipango gani kichwani, ..hajui...kwani nimetoka naye wapi,...hakumbuki hilo,...’nikasema.‘Haya mimi sitaki tena kuingilia mambo yenu, nitakuja tu pale mtakaponihitajia, kama ulivyowaambia wazazi wako, kuwa wasiingilie mambo yenu, sisi tunawaangalia lakini kama mkikwama, sisi tupo tayari kuwasaidia..’akasema na kuondoka.Siku moja wakati nipo nyumbani nimepumzika, nikaambiwa kuna mgeni anataka kuongea na mimi, nilikuwa sitaki kuongea na mtu, lakini nikaona ni vyema kumsikiliza huyo mgeni, kibusara, nikauliza;‘Ni mgeni gani huyo?’ nikauliza.‘Ni mtoto wa marehemu Makabrasha..’akasema msaidizi wangu wa ndani.‘Huyo tena, nilishasema sitaki kuonana na yeye, kama anataka kuongea akaongee na huyo huyo mwenzao, sio mimi…’nikasema‘Kasema hawezi kuondoka, bila ya kuonana na wewe, kwasababu huenda akasafiri, na hawezi kuondoka bila ya kuhakikisha ameyamaliza mambo yote aliyotakiwa kuyafanya,…kwahiyo yupo nje anasubiria kukaribishwa…’akasema bint msadizi wangu wa nyumbani.Nikawa kimia nikitafakari,…je dawa ni kukimbia jambo au kukabiliana nalo…nikikataa kuongea naye ina maana nimekimbia..nimeogopa, nikiongea naye je…huenda kuna mitego, kuna jambo wamepanga,na huenda ikawa ni sababu ya kuniumiza zaidi kimawazo.Nikachukua simu yangu na kumpigia wakili wangu wangu..nikamuelezea, wakili wangu wangu akasema‘Fanya kama nilivyokuambia…NB: Jamani hapa nimeazima laptop ya mtu, kuonyesha jinsi gani nawajaliWAZO LA LEO: Siri ya mafanikio, ni kujibidisha kwenye shughuli unayoifanya, na siri ya kushinda vita sio kukimbia, ni kukabiliana na adui yako, na siri ya matatizo sio kulalamika tu, bali ni kujitoa muhanga na kukabiliana na matatizo hayo. Mitihani mingi ipo kwa minajili ya sisi kufunguka akili zetu na kutafuta njia bora zaidi ya kukabiliana na matatizo hayo. Tuifanye mitihani hiyo kama sehemu ya daraja la kuvuka na kusonga mbele..lakinii tujitahidi kupambana na mitihani hiyo kwa njia za heri, huku tukimuomba mola wetu.‘Ni mtoto wa marehemu Makabrasha anataka kuongea na mimi…’ nikamwambia wakili wangu naye akasema‘Ongea naye ila fanya kama nilivyokuelekeza…’akasema wakili.Nikachukua simu yangu maalumu na kuhakikisha ina chaji ya kutosha.******   ‘Mkaribisheni kule bustanini, nakuja kuongea naye…’nikamwambia binti wangu wa kazi, sikutaka kuongea naye ndani, kwani sikuwa na amani naye kabisa, nilihisi kivuli cha baba yake kipo pembeni yake. Huenda mtoto kama baba, hulka hazitengamaniWalimkaribisha bustanini, na mimi nilipohakikisha kila kitu kipo sawa, nikamfuata huko bustanini, nikafika na kusalimiana naye, sikutaka kumuonyesha jinsi gani nilivyochukia, maana moyoni niliona kuwa wao, kutokana na baba yao, watakuwa wamepanga jambo la kuifisidi familia yangu, na nilitakiwa niwe makini kwenye kauli zangu kama alivyonishauri wakili.'Karibu mgeni....'nikasema na alisimama na kusalimia kwa adabu tu, baadae sote tukaa kwenye viti, mimi ndio ni nikaanza kuongea;‘Haya niambie una shida gani na mimi?’ nikamuuliza huku nikimwangalia moja kwa moja usoni, maana tulikaa tukiwa tunaangaliana na kati kati yetu kulikuwa na meza. Nilitaka nimuone usoni, kwani mtu unaweza kumpima ukweli wake, au ujasiri wake, kwa kumwangalia usoni.‘Samahani sana kwa usumbufu wangu, wa kutaka kuongea na wewe...maana nimejaribu mara nyingi bila mafanikio, na leo nilipanga, kama ikishindikana basi sitaondoka,maana...siku zangu za likizo zimeisha, natakiwa kurudi kazini...Ulaya...’akasema.‘Sawa pole sana,na pole sana kwa msiba, kwani sijapata hata muda wa kukupa pole yangu..ila salamu za rambi rambi nilizifikisha kwa kupitia mume wangu , natumai ulizipata’nikasema‘Hamna shida, nashukuru sana nilizipata, sina cha kuwalipa ila mola atawalipa zaidi, ….’akasema‘Kiukweli imebidi iwe hivyo kutokana na hulka zenu,..kiukweli japokuwa marehemu haongelewi vibaya, alichokifanya baba yako kimenivunja nguvu, ..namafahamu sana kutokana na tabia yake, lakini sikutarajia atakwenda kwa kiasi hicho,..sasa kauwawa, sijui ni nani wamefanya hivyo….imezidi kunivunja nguvu, haya niambie ulikuwa unanitafutia nini, maana kila mara napaat ujumbe kuwa unataka kuongea na mimi..?’ nikauliza.‘Mimi sina nia mbaya kama unavyofikiria wewe,..huenda ungelisikiliza toka awali tungelishamalizana mapema tu, na kila mtu akashika hamsini zake. Hapa nilipo nakwama kuondoka maana mambo mengi bado hayajakaa sawa, na mimi nimeachiwa majukumu mengi na marehemu baba, na familia yote inanitegemea mimi, kiukweli sikulipenda hili, lakini nitafanyaje....’akasema.‘Hayo majukumu uliyoachiwa, yananihusu nini mimi, hayo si mambo yenu ya kifamilia au sio…?’ nikauliza na yeye bila kujali swali langu akaendelea kuongea.‘Mhh..ni hivi, mimi nilipofika hapa Dar kutoka nje kutokana na kifo cha baba...nilitarajia mengi, maana mimi namfahamu sana baba, yeye na mimi hatukuwa sambamba kutokana na mitizamo yetu, hata hivyo yeye alinijali kama mtoto wake wa kwanza, na mamambo yake mengi aliyaweka wazi kuwa mimi ndite nitakuwa msimamizi wa kila kitu..’akatulia kidogo.‘Kifo chake kimenishtua sana, maana kuna mambo mengi tulikuwa hatujawekana sana…sikuwa tayari kwa haya majukumu kabisa....lakini ndio hivyo, mapenzi ya mungu hayapingiki…’akashika leso yake na kufuta machoni, lakini sikuona dalili ya machozi‘Nilipofika kiukweli kwanza kabisa nilitaka kujua ukweli wa kifo cha baba, na nilipewa taarifa yote kutokana na uchunguzi wa polisi. Na kwa matizamo wangu wa haraka kutoka na taarifa za watu hata kabla ya taarifa ya polisi,..nilihisi nyie mnaweza mkahusika, ...na kiukweli kama mngelikuwa nyie mnahusika, ningesimama kidete kuhakikisha haki inapatikana, bila kujali maagizo ya baba..’akashika kichwa, kama vile kinauma.‘Sasa uchunguzi wa polisi unaonyesha tofauti, imeonekana hauhusiki, na kwa kujirizisha, nikafanya uchunguzi wangu binafsi, na kuhakiki taarifa niliyopewa, nikagundua kuwa mambo ni yale yale, hauhusiki..'Sawa hausiki kwa moja kwa moja, lakni bado nikawa na dukuduku, ni kwanini,…baada ya baada ya baba kuwa wazi kwenu, ndio kifo chake kitokee, hapo ulipa maulizo mengi, na sikupendelea sana kuunganisha haya na mambo ya kisiasa japokuwa hilo limebeba uzito wake , lakini kwa vile ushahidi waonyesha kuwa upende wenu haupo, sasa nihangaike nini tena na nyie...bado swali mpaka sasa ni kwanini…tuliache hilo hapo....’akasema.‘Ngoja nije kwenye hoja...mimi ninamfahamu sana marehemu baba yangu, nafahamu sana mbinu zake za kupata mali, baba ni mjanja na alichukua kazi hiyo ya uwakili akijua kuwa itakuwa ni kinga ya ujanja wake…ni sawa kasoma, na kiukweli kaiva, lakini kwanini asifanye kitaaluma yake zaidi, hilo mimi sijui, na hata tukikutana naye huwa tunaishia kulumabana juu ya hilo.....’akasema.‘Kutokana na tabia hizo, niliposikia kuwa baba kafariki cha kwanza nilichouliza kafa kwa kifo cha kawaida au kauwawa, nikaambiwa kapigwa risasi, nikajua tu ni yale yale, na nikauliza ni nani kashukiwa, nikaambiwa ni wewe..nikatamani sana kwanza nije niongee na wewe niujua ukweli.'Unajua kazi za namna hiyo, tabia ya namna hiyo,..ni lazima ujue kuwa kifo chako kipo pembeni, mimi naishi nje, na nimeona watu wa aina hiyo wanavyouwawa, bila kufa, watu uliowatendea hivyo hawawezi kuwa na amani, amani yao ni kufa kwako...’akasema‘Blackmail,ni kazi ya hatari sana, sio mchezo, kumghilibu mtu, na kupata kile alichokihangaikia kwa jasho lake kwa shida, wewe uje ukichukue kilaini,sio rahisi kihivyo, sikuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa hilo, ila nishaambiwa na watu naa hata na polisi kuwa alikuwa akishukiwa hivyo…’akatuliaNilitaka nimkatize lakini alikuwa akiongea kwa haraka sana, na nikaona nimuache tu aendelee..‘Mimi nilikuwa sielewani  na baba tangu niwe na fahamu naye, japokuwa sikuwahi kuishi naye kikaribu hivi, maisha yangu, nililelewa na babu na bibi, maana mama alikuwa akiishi huko ,....na hata nilipokuwa nasoma hapa nchini, nilikuwa kwa babu, baadae wakati nipo elimu ya juu, ndio nikapata muda kidogo wa kuishi na baba, hatukuwa tunaelewana, damu zetu hazikuendana kabisa....‘Baba akataka nisomee uwakili, lakini mimi siupendi uwakili mambo yangu sayansi, mitandao, komputa, ni hivyo,..ndio ndoto zangu, yeye aliona ni mambo ya tamaa yasiyo na umbele zaidi'Mimi nikamwambia moja kwa moja baba, mimi sitaki kuja kutegemeamali zake nataka kuja kuishi maisha yanayotokana na juhudi zangu na dua zangu zikakubaliwa, nikafaulu mitihani yangu, nikaomba kwenda kusomea nje ya nchi, na bahati nikapata nafasi hiyo ..’akatulia akiangalia saa‘Na nikuambie ukweli, kwenda kwangu kusoma nje, hakukuwa na mkono wake, nilihangaika kivyangu, nikafanikiwa kivyangu, na huko nikasoma kwa shida sana, na aliposikia nasoma kwa shida, ndio akanitumia pesa...nilizikataahizo pesa zake kabisa...nikamrudishia, hakuamini hilo, na akaniuliza kwanini, nikamwamba iweje sasa ndio ananijali, ..kwanini alinitelekeza utotoni mwangu, hayo yana storia yake…’akasemaHapo nikamuuliza;‘Kwanini ulifanya hivyo?’ nikamuuliza nikimwangalia machoni, huyu mtu huwezi kumhisia vyovyote, hajionyeshi tabia yake usoni,..ni watu wachache wenye tabia hii.‘Kikubwa ni kuwa nilishamfahamu baba, nilijua pesa zake ni chafu na mimi sitaki pesa chafu, ndio maisha yangu nilivyoamua yawe hivyo, wewe hujiulizi kwanini baba alikuwa hakai na mama, mama ni mtu wa dini, na alifahamu tabia ya baba, akaona akae mbali na yeye, na mimi kiukweli nimerithi tabia ya mama, japokuwa sijasomea mambo ya dini...ila mimi nataka niishi kwa jasho langu, sio kama alivyokuwa akiishi baba...’akasema.'Kwahiyo kwa kauli yako mwenyewe unakiri kuwa baba yako hakuwa mwaminifu au sio..?' nikauliza'Ni kweli, mola amsamehe madhambi yake tu...hilo siwezi kukukatalia...'akasema'Sawa endelea maana mpaka sasa sijakuelewa mimi nahusikanaje hapo ...'nikasema‘Kifo cha baba, kikatufanya tukutane kama familia, nashukuru sana kuwa wanafamilia wote walikuwa wakimfahamu sana baba, hakuna aliyetaka kuingilia mambo yake, kila mmoja aliona kuwa akigusa huko huenda damu za watu, dhuluma za watu zitawaandama. Mimi nikapewa jukumu la kusafisha jina la baba, maana keshafariki sasa tutafanyaje na maisha  lazima yaendelee, ..je tutaendelea kukumbatia hiyo hali, au tutaishije.. ni lazima jambo lifanyika..’akatulia.'Niliongea na mama, na mama akasema tusaidie japokuwa ...ili roho ya baba iwe na amani, na hilo..likawa jukumu langu la kwanza,...kuisafisha familia yetu na kuhakikisha kuwa hatueleweki vibaya, .....'akasema'Kwa vipi sasa..?' nikajiukuta nimeuliza hivyo‘Kazi yangu kubwa, ilikuwa kufuatilia kwa kila aliyeumia kutokana na baba...wapo wanaojulikana, na tulitangaza kama kuna mtu kwa namna moja au nyingine alipata athari, kutokana na utendaji wa baba ajitokeze,..watu waliona kama ni utani,..mimi nikafanya kazi ya zaida ya kuwafuatilia kwa kila niyekuja kuambiwa, au kuona kwenye kumbukumbu za baba...na ili hayo yafanikiwe, tulimtafuta mwanasheria ambaye alisaidia kisheria....’akasema.‘Sasa pamoja na yote...ikabakia wewe, kwa maana ya kisheria, sijui kama kuna baya aliwafanyia, sijui, ...ila kuna mambo ya kisheria, ambayo ni muhimu sana nikae na wewe tuone tutafanyaje, nielewe sana nimechukua muda mrefu wa maelezo ili uelewe dhamira yatu….’ Hapo sasa akaniangalia usoni moja kwa moja.'Mambo gani hayo ya kisheria..?' nikauliza‘Kwanza nianze kwa kuingilia ndoa yako, niligundua kuwa …wewe na mume wako hampo sawa, hilo sihitaji wewe kukubali, ila nilipoongea na baba ...mume wako hata bila kuniambia nikaligundua..lakini kuna mikataba  imeachwa, inakuhusu wewe na mume wako, inahusu mali nk...unajua  mimi sikutaka hata kuingilia undani wake, nikawa nimeongea na mume wako kuwa kama kuna lolote baya ndani yake aniambie tuachane na mikataba hiyo kabisa…’akatulia‘Mume wako akasema kila kitu kipo sawa, na,yeye atasimamia kama ilivyo..,..sasa pamoja na huo mkataba, eeh,..unajua nikuambie ukweli mimi namfahamu sana mume wako mimi namtambua kama baba yangu mdogo, kwa jinsi familia yao na yetu zilivyokuwa karibu, na baba yangu na mume wako walikuwa marafiki sana japokuwa baba yangu alikuwa mkubwa  kwa mume wako.‘Kwahiyo nilitarajia msaada mkubwa kutoka kwake, na kiukweli sikutaka mimi nifanye lolote kwa jinsi mkataba unavyosema bila ya ushauri wake..na sio ushauri wake tu, ila kiukweli mimi sikutaka kabisa..nilimuambia uwanja huo mume wako, afanye anavyoona ni sahihi…’akatulia‘Kiukweli kwa jinsi mkataba unavyosema kama sisi tungelikuwa ni watu wa tamaa, basi tungelifaidika sana na vitega uchumi mlivyo navyo nyie..., maana sisi ni warithi halali wa baba na mkataba unasema wazi warithi wa mali yake ni nani,…kuna kumiliki hisa zake ndani ya kampuni ya mume wako, na mume wako anadaiwa pesa nyingi na mkataba unasema hivyo, na ulibaisniha kuwa malipo ya deni hilo ni kupewa hisa zaidi kwenye kampuni ya mume wako, na zaidi pia kuna mkataab mwingine kuwa marehemu anatakiwa kupewa hisia kwenye kampuni yako, kwa kupitia kwa mume wako,....’akasema‘Matapeli wakubwa nyie....Huo mkataba upo wapi?’ nikamuuliza hapo na nikagundua kuwa nimekiuka ushauri wa wakili, lakini hasira tena‘Huna haja ya kukasirika, nikuambie tena, sisi hatuna nia mbaya na nyie,..na huo mkataba ninao, kila kitu kipo wazi....’akasema‘Nautaka huo mkataba niuone kwanza...’nikamwambia.‘Bado anao mwanasheria wetu, ....’akasema‘Anao kwa ajili gani sasa?’ nikamuuliza‘Kuna mambo bado hayajakaa sawa, na hili linatokana na mume wako, kama mume wako angelikubaliana na sisi, basi tungelishamalizana, na kuhakikisha kuwa tatizo hili limekwisha kabisa,...’akasema‘Mambo gani hayo mume wangu hajakubaliana na nyie?’ nikamuuliza‘Kuna vipengele vingi vipo humo, vikionyesha kuwa mume wako ndiye anamiliki kampuni yake na yako kwa asilimia fulani za hisa, lakini katika mkataba aliouacha baba , kuna kipengele walishindwa kukubaliana, kwa idadi ya hisa, kwa maana kuwa wewe kama mshirika, hujaridhika...’akasema‘Kipengele gani hicho?’ nikauliza‘Kutokana na deni lilivyo, baba alitaka kumiliki zaidi ya aslimia hamsini ya hiza za kampuni ya mume wako, na pia kwa vile baba atakuwa anamiliki zaidi ya asilimia hamsini yeye alitaka hata jina la kampuni libadilike....na hapo kukatokea sintofahamu, nahisi hata kifo cha baba kilitokea siku walipokuwa wakibishana kuhusiana na hilo, japokuwa walikuja kukubaliana kuwa jina libakie hilo hilo...’akasema‘Wewe umejuaje hayo, na wakati hukuwepo....?’ nikamuuliza‘Baba alikuwa na kawaida ya kuhifadhi kumbukumbu za matukio yote, ..tulichokuja kuona ni ajabu ni kuwa mle ndani kwenye hicho chumba ofisini kwa baba kulikuwa na kifaa cha kunasia matukio, lakini sehemu kubwa imefutwa, kwahiyo haikuweza kuonyesha tukio la kupigwa risasi kwa baba, sehemu hiyo haipo, ina maana huyo muuaji, alirudi na kufuta sehemu hiyo, na ina maana kuwa huyo mtu anafahamu siri nyingi za baba.'Mimi ni mtaalamu sana wa komputa, nikafanya mambo yangu,  nikagundua sehemu ndogo iliyofutwa, inayoonyesha jinsi ya kifo cha baba kilivyokuwa, lakini kwa bahati mbaya sikuweza kuipata sura ya huyo muuaji, au umbile lake kwa ujumla zaidi ya kichwa kilichojitokeza na mkono uliokuwa umshika bastola, ndio nikagundua kuwa aliuwawa na watu wake waliokuwa hawaelewani naye...’akasema‘Ni watu gani hao?’ nikauliza‘Imeshindikana kuwagundua ni akina nani, naomba iendelee kuwa hivyo, na kwa vile huyo muuaji hakuonekana sura, ...na alitokeza kidogo tu, kiasi cha kuweza kulenga shabaha..na, kwa vile alikuwa kavaa kitu usoni, na kuacha macho tu,hata polisi hawajafahamu sehemu hiyo,…’akasema‘Ina maana polisi hawakupata hiyo video…?’ nikauliza‘Polisi walipata sehemu hiyo ambayo haionyeshi lolote, ila mimi kwa vile ni mtaalamu , ndio nikagundua hiyo sehemu iliyokuwa imefutwa,…lakini pia kuna kumbukumbu za baba nilizokuja kuzigundua zilikielezea watu mbali mbali, lakini hazielezei uhasimu wowote, ila kuna vitisho vya hapa na pale,..ikiwemo wewe na wengineo, sasa nani ni nani..sikutaka kuendelea zaidi, hilo niliwaachia polisi.‘Sasa ulipofanya utundu wako na kuligundua hilo, uliwafahamisha polisi?’ nikamuuliza‘Hapana, na nina sababu za kutokufanya hivyo…’akasema, na kunifanya nishangae kidogo,'Oh, kwanini...?' nikamuuliza ‘Kwasababu kuna sehemu inamuonyesha mume wako...'akasema na kunifanya nishtuke'Mume wangu, kwa vipi...?' nikauliza'Ndio mume wako yupo kwenye hiyo kumbukumbu ya video ya matukio, yaliyotokea siku ile,..., na polisi wangeliona hiyo sehemu mume wako angelikuwa kwenye hatia, mtu mwenyewe mbovu, halafu ashikwe na kuwekwa ndani itakuwaje...niliona ni heri tu ibakie hivyo hivyo, kwa vile sio yeye aliyefanya hayo mauaji…’akasema‘Mimi sikuelewi hapo mume wangu… hapo kuna makosa, unajua kipindi hicho mume wangu  alikuwa kalazwa hospitalini, anaumwa, ataonekanaje kwenye hiyo video ya matukio, uliyoiona humo ndani, usije ukatumia ujanja wa kimtandao, na kumweka mume wangu…?’ nikauliza kwa mshangao‘Siku huyo mume wako alikwenda kumuona baba, marehemu baba, ndivyo inavyoonyesha, sasa alifikaje na kwanini, hilo kwangu sio muhimu, ila kwenye hiyo video ya matukio, mume wako alionekana akibishana na baba, ipo wazi kabisa, na walikuwa wakibishana kuhusu mkataba…’akasema‘Mkataba gani huo…?’ nikauliza.‘Kuna mkataba wa hisa za kibiashara, nina Imani umeshalipata hilo kuwa baba ana hisa kwenye kampuni ya mume wako, na huo mkataba ulikuwa unaelezea hayo…’akasema‘Hebu samahani kidogo, kwanini baba yako awe na hisa kwenye kampuni ya mume wangu, na unafahamu wazi kuwa kampuni ya mume wangu inatokana na wazazi wangu ndio wao walimpatia mume wangu mtaji…?’ nikauliza‘Hiyo ni historia ndefu kidogo, ila hapo kwenye matukio, ilisikika marehemu akimuambia mume wako kuwa anadaiwa pesa nyingi tu na baba, …’akasema‘Pesa nyingi kiasi gani cha kupewa hisa nyingi hivyo, ni hayo malipo ya uwakili wake, kwani hayo malipo yalikuwa kiasi gani..?’ nikamuuliza.‘Kama nilivyokuambia awali hiyo ni historia ndefu kidogo nahisi kuna zaidi ya hilo, na mume wako analijua zaidi,..ila mimi naongea kutokana na ilivyosikika kwenye video, kuna maongezi kuwa mambo mengi kuhusu kampuni ya mume wako yalitokana na juhudi za marehemu baba, na tangia awali baba aliwekeza kiasi cha hisa ndani ya kampuni hiyo kwa siri, sasa alitaka iwe bayana kwenye huo mkataba, sasa mpaka kufikia kiasi hicho kikubwa cha hisa..hilo utamuuliza mume wako....’akasema.‘Hapo sizani kama ninaweza kuelewa,..ni udanganyifu mkubwa tu huo, kampuni hiyo  ilianzishwa kwa mkopo kutoka kwa wazazi wangu,na mpaka leo huo mkopo haujalipwa sasa iweje marehemu ajiingizie huko,…lakini… anyway, endelea....’nikasema.‘Siku ile mume wako, alifika kwa baba, alionekana ana haraka, na mashaka, na alionekana mwenye maumivi nahisi ni kutokana na kujilazimisha kupanda ngazi au kitu kama hicho, sijui labda kuna mtu alimpatia msaada,... ila yaonyesha keshaingia amekaa kwenye kiti wanatoleana mikataba..’akasema‘Je mumeshaongea na mume wangu kuhusu hayo uliyoyagundua, kuwa wewe unayafahamu hayo yote..?’ nikauliza‘Anafahamu kama ilivyo kwenye mikataba, lakini hafahamu kuwa mimi nimegundua kilichotokea siku ile baba alipouwawa..hilo sijamuambia,… ...haya hayafahamu mume wako na mpaka leo nikimuuliza kuwa aliwahi kuonana na baba siku ile ya tukio, ananikatalia,...kwahiyo yeye hayajui kama walivyo polisi, nimeona nisimuambie…’akasema‘Kwanini…?’ nikauliza‘Mume wako hana tofauti na baba kwa tabia zao, za tamaa ya mali, bila kujali uhalisia wake, iwe dhuluma au halali kwao ni sawa, nawafahamu sana kwa hilo, na sisi hatutaki kuwa miongoni mwa hilo, na nina amani kama tungelimuambia angetukataza kabisa kuliongelea hilo kwako, sis hatutaki uhasama, sisi tunataka kulimaliza hili kwa njia ya heri…’akasema na sikumuelewa hapo lakini nikaona nisubiria kwanza, nikasema‘Ehe ilikuwaje sasa maana hapa unaongea wewe, siwezi nikakuamini mpaka nione huo ushahidi…’nikasema‘Nitakuonyesha kila kitu madam, ila mpaka huo muda ukifika…’akasema‘Muda gani…ukifika..?’ nikauliza sasa kwa mashaka‘Ngoja kwanza nikuelezee ilivyokuwa, au hutakii kujua zaidi…’akasema‘Haya elezea…’nikasema‘Basi mume wako alipofika  wakaanza kuongea, na nahisi siku hiyo walipanga iwe ni kuhitimisha makubaliano yao, nahisi kuna mambo yalikuwa hayajawa sawa kwani kuna sehemu marehemu alimuulizia je mke wako kakubali, na mume wako akasema haina shida, yeye tu anatosha, kwa vile mkataba upo wazi, na kukawa na kubishana kwa hilo na baadae marehemu akasema…’a hapo akautulia kidogo‘Pamoja na hili kuna mambo ya kibenki, hayo hatuna ujanja nayo je una uhakika utaweza kumshawishi mke wako..na mume wako akasema, muda utasema kwanza wamalizane na hilo la mikataba,....’ hiyo ilikuwa ni kauli ya marehemu na mume wako, ipo wazi...‘Sasa kuna mambo mengi walijadiliana hapo, hayo utakuja kumuulizia mume wako, lakini nakuomba kwa hili nililokuambia usimuambie kwanza mume wako, utakuja kuharibu kila kitu…muhimu kwako kufahamu ni kuwa mume wako baadae waliwekeana sahihi rasmi kuwa hisa za marehemu zitakuwa kiasi gani, na za mume wako kiasi gani, ni unu kwa marehemu na iliyobakia sehemu ni yako na ya mume wako, kama minajili jhiyo baba anakuwa ana hisa kubwa zaidi na anakuwa maamuzi zaidi, hapo sijui ni kwanini..’akasema‘Mhh,hayo yote yanaonekana kwenye hiyo video…?’ nikauliza‘Ndio…kila kitu kipo wazi, lakini hayo hayaonekani kwenye ushahidi walio nao polisi..sijui kama wana utaalamu kama niliufanya mimi hadi kuligundua hilo na kama wangelikuwa nao basi mume wange angelishakamatwa, au sio…’akasema‘Hiyo video sio ya kugushi kweli…?’ nikauliza‘Kuna vitu vya kugushi,…madam,.. lakini sio vitu kama hivyo, unaweza kwenda kwa wataalamu wakakuthibitishia hilo, lakini naomba hili liendelee kuwa siri kati yangu mimi na wewe…’akasema‘Sawa endelea…’nikasema‘Basi, walipomaliza,  na wakati wanapeana mikono ya kuagana, ndio hapo tukio la mauaji likajitokeza…’hapo akatulia kidogo‘Mara mlango ulifunguliwa kwa ghafla…lakini mtu hakujitokeza, marehemu akawa anauliza wewe ni nani… na mtu aliyekuwa kajifunika sehemu zote za  usoni,akajitokeza kichwa tu usingeliweza kuiona sura yake, na hapo hapo akampiga baba risasi, kifuani kwenye moyo, na baba  akaguna na kuwea kichwa mezani, nahisi  alifariki hapo hapo..’akatulia kidogo.‘Kwanini sasa usiwape polisi huo ushahidi ni muhimu sana kwangu, maana mpaka sasa sijasafisha jina langu kuwa mimi sihusiki na mauaji hayo…’nikasema‘Watu hao walitaka kumuua na mume wako…lakini wakati huyo muuaji anataka kufanya hivyo, ikasikika sauti ya mtu akiita kwa nje, kuwa waondoke wapo kwenye hatari ya kukamatwa, ndio hapo mlango ukafungika, lakini kidogo hapo, kabla ya kuondoka, huyo muuaji alirusha hiyo bastola kwa ndani....’akasema‘Ikawaje maana mume wangu alikuwa humo ndani …?’ nikauliza‘Ukiangalia hiyo sehemu utaona vyema jinsi gani mume wako alivyochanganyikiwa, kuonyesha kuwa hakuwa anafahamu hilo tendo, labda kama alihusika,...maana ungelisema labda ni mtu wake, aliyempanga kuja kufanya hivyo, lakini utajiuliza kwanini..ili iweje,…na ukiangalia ilivyo, utaona kabisa mume wako hakuhusika, alicvhanganyikiwa, akawa anahangaika huku na kule..na kama ni yeye, basi angeliondoka na hiyo mikataba, lakini hakukumbuka kuichukua wakati anatoka kukimbia…’akasema.‘Bado hapo …’nikasema‘Ni hivi huyo jamaa alitokeza kichwa, na mara ikasikika tufu tufu…risisi zikimpiga marehemu, yeye akainama na kuweka mikono usoni hivi..yaani kichwa kakilanza mezani huku kaweka mikono kuzuia machoni,…, kama vile mtu anavyoogopa kupigwa na yeye,Alikaa hivyo kwa muda hadi hao watu walipoondoka..baadae ndio mume wako akainua kichwa taratibu, halafu akageuka kuangalia mlangoni, akajihakikishia kuwa yupo salama, sasa ndio akamtizama marehemu akagundua kuwa marehemu keshafariki..‘Utaona jinsi gani alivyochanganyikiwa, akawa anahangaika, akishindwa afanye nini...baadaye, sijui alijiwa na wazo gani, akafungua mlango, na kutoka nje, hapo alikuwa akitembea kwa shida sana, ni kama alitojitonesha au hali..inaonekana hivyo,...huwezi kuona kitu nje ya chumba, sasa sijui alivyoweza kutembea hadi kutoka eneo hilo…’akasema.‘Kwahiyo wewe unasema sura ya huyo muuaji haikuonekana, na huyo mtu alitaka kumuua pia mume wangu, inaonyesha hivyo, na inaonyesha kweli kuwa mume wangu hahusiki au sio…na huyo mtu hajulikani kuwa ni mwanamke au ni mwanaume?’ nikauliza‘Haonekani, huwezi kufahamu...'akasema‘Bado mimi najiuliza ni kwanini usiwaonyeshe polisi, maana ingewasaidia kujua zaidi?’ nikamuuliza.‘Tunafuata maagizo ya marehemu baba, licha ya kuwa sikuwa na mahusiano mema na yeye, lakini nakumbuka jinsi alivyokuwa akiniambia kuwa kwa vyovyote itakavyo kuwa awe hai au mzima, mume wako nimuheshimu kama baba yangu mdogo, kwani amewahi kumsaidia sana katika maisha yake na sisi tumlinde na kumsaidia..’akasema‘Ok…’nikasema hivyo‘Na ..hata mimi alinisaidia sana mume wako nikiwa mdogo..na alimsaidia sana mama, kipindi mama alikuwa anaumwa sana, hana pesa, yeye alijitolea kuuza mbuzi wake, aliyekuwa naye, mmoja, kwa ajili ya kumtibia mama,...mimi nilimwahidi baba kuwa mume wako atakuwa baba yangu mdogo, na sitaweza kumvunjia heshima. Hili niliahdi na ndio maana nayafanya haya…’akasema‘Sijakuelewa hapo, ina maana hata kama itaonekana kuwa yeye ni mhalfu, utamtetea tu, na huenda akahusika na kifo cha baba yako?’ nikamuuliza.‘Mume wako hahusiki na kifo cha baba yangu, hilo nina uhakika nalo...usuhuba wao ni wahali ya juu, kifo cha baba kimemuumiza sana mume wako, ..wewe hujui tu, marehemu baba alikuwa ndiye kichwa cha mume wako, kila uliloliona mume wako akilitenda lenye tija…, mara nyingi, alikuwa akifuata ushauri wa baba...’akasema.‘Hata kuzaa nje ya ndoa?’ nikamuuliza‘Kuzaa nje ya ndoa…haaah, nani kasema?!’ akauliza kwa mshangao kidogo‘Unajifanya hulijui hilo…kama kweli yote aliyokuwa akiyafanya baba yako kuwa anaweka kumbukumbu nina Imani hata hilo lipo, au sio…?’ nikauliza‘Kuna mambo mengi nimeyagundua ya baba, lakini hilo,...mmh...lakini nikuambie kitu, nataka haya tuje kuyamaliza...kuna mambo mengine siwezi kukuelezea kwa sasa mpaka hapo tutakapokuja kukubaliana, ndio maana nimekuja na maombi yangu kwako...’akasema‘Maombi gani?’ nikamuuliza‘Kwanza na lenye muhimu nakuonmba umsikilize mume wako...mkubaliane naye..mkisha kubaliana naye , mkawa kitu kimoja,basi sisi tutajitoa kabisa kwenye huo mkataba ulioandaliwa kuwa baba alikuwa na hisa, hatutaki hizo hisa, lakini huwezi kuziondoa kihivi hivi, ni mambo ya kisheria au sio,  ...’akasema‘Hahaha..nilijua tu…’nikasema‘Ninasema hivyo kwa moyo safi , nielewe madam..., sina shida na mali zenu kabisa, hatuna shida na mali za dhuluma…ila mimi nina deni kwenu, maana kama kuna pesa zilitoka kwenu, zikanisaidia mimi, natakiwa nifanye lolote kulipa fadhila au sio..sasa furaha yangu ni kuona wewe na mume wako mnaishi vyema.'Hilo halikuhusu au..kwanini unataka kuingilia ndoa yanu...?' nikamuuliza‘Kwa kifupi madam, sisi hatutaki kujihusisha na ndoa yako au mali zenu, hatutaki kupata mali isiyo halali,...lakini tunahitajika kumsaidia mume wako, kwani ...wema wake kwetu ni mkubwa sana, ndio mume wako ana tabia kama hizo..., lakini ni mwepesi kujirudi, nampenda sana kwa hilo, sio kama baba, baba alikuwa haambiliki, sasa tunakuomba umsaidie mume wako, nina Imani atajirudi na mambo yenu yatakuwa sawa,...hata ukiongea na mama atakuambia hilo…’akasema.'Mama yako sio...yupo...?' nikauliza'Yupo ndio, kaja kwa ajili ya huo msiba, wapo wanafamilia karibu wote...'akasemaMimi hapo kwanza nikatabasamu moyoni nilihisi kupata jambo la kunipa faraja, japokuwa bado nilikuwa sijawa na uhakika, maana hayo ni maongezi tu, ushahidi upo wapi,..nikajaribu kumuangalia huyo jamaa usoni kwa makini sana, kama nilivyokuambia sio rahisi kumtambua huyu mtu  hisia zake kupitia usoni je ni mkweli au ni muongo, na baadae  nikasema;‘Naweza kuonana na mama yako.....nataka niongee naye ?’‘Kuonana na mama yangu sio tatizo na mkiongea naye atakuuliza kama umekubaliana na mimi, na mimi ndiye muamuzi..sasa nataka kauli yako kuhusu ombi langu, je upo tayari kushirikiana nasi ili tulimalize hili jambo, ni muhimu sana kwangu?’ akauliza.‘Kwanza nataka niongee na mama yako…..’nikasema, na mara gari la mume wangu likafika, nilimuona yupo na mtu ndani ya gari, nikagundua kuwa ni wakili wake.NB: Inatosha kwa leoWAZO LA LEO: Urafiki ni mzuri, unajenga mahusiano mema, lakini tujaribu kuangalia aina gani ya marafiki zetu,kuna marafiki wengine wanaweza wakawa ni sumu ya maisha yatu, kutokana na tabia na matendo yao..utawafahamu kutokana na hulka na matendo yao, hao sio marafiki, hata kama mumeshibana vipi,…ikiwezekana ni bora utengane nao kabisa, kwani ukiungana nao, hata kama hutafanya wanachokifanya wao, lakini ubaya wao unaweza kukuleta matatizo kwani ukikaa na muuza uturi, utanukia uturi....au sio?Mtoto wa marehemu alionekana mtu mwema kwangu…, na alikuwa tayari kuniambia mengi ambayo huenda yangelifanikisha malengo yangu, ya kutaka kujua ni kitu gani kinachoendelea, kitu gani kilichoweza kumbadilisha mume kiasi hicho..na je ni kweli ana mtoto nje ya ndoa..huo kwangu ungelikuwa ni ushahidi mkubwa sana...tatizo huyu mtoto wa marehemu akatoa sharti ambalo lilinipa wakati mgumu kulikubali,Sio kwamba simpendi mume wangu, sio kwamba…simuamini, lakini kama ni kweli kayaafanya hayo ninayoyasikia, na kavunja mkataba, je haiwezi ikawa ndio njia, na sababu ya kutenda mengine makubwa zaidi ya hayo.....na je nikikubaliana naye si ndio sababu ya kupoteza mali na  juhudi zangu zote, je wazazi watanielewa kweli….‘Nataka umsikilize mume wako..mkubaliane naye..mkisha kubaliana naye , mkawa kitu kimoja,basi sisi tutajitoa kabisa kwenye huo mkataba ulioandaliwa, mkataba huo ulionyesha kuwa baba ana hisa kwenye kampuni zako, ...’‘Naweza kuonana na mama yako.....?’ nilimuomba hivyo..akili ikiwa imechanganywa na sharti hilo....Endelea na kisa chetu....... Mara mume wangu akaja na gari lake, na ndani ya hilo gari alikuwepo mtu mwingine alikuwa ni wakili wake, walifika na hawakutaka hata kutusalimia, wakaingia ndani,..na mimi sikutaka kuwafuata, japokuwa ni adabu mgeni alifika umkaribishe, lakini kwa hali ilivyokuwa, ..sikujali tena….‘Mume wako anaonekana hayupo vizuri…’akasema‘Ni kawaida ..nahisi ni majukumu ya kazini kwake, ila sijui kwanini kamleta huyo wakili hapa nyumbani, ..kama watanihitajia wataniita..’nikasema‘Yah….basi…kama haupo tayari, mama anaweza kuja wakati mwingine..’akasema‘Kwanini, …nipo tayari,..hao wana mazungumzo yao, hayawezi kuzuia hili, kama wangenihitajia wangeniambia..si umeona..hawakutaka hata kusalimia, ina maana wana mazungumzo yao binafsi…’nikasema‘Sawa…kiukweli mama, atashukuru sana kuongea na wewe, kwani hata yeye alikuwa na hamu sana ya kuonana na wewe, lakini kweney haya, yeye hana zaidi ya kuamua, zaidi ya yote ananitegemea mimi, yeye ni muwekezaji tu wa huko kijijini ...’akasema.‘Kwanini alitaka kuonana na mimi, ni kuhusu mambo hayo hayo…?’ nikamuuliza‘Pamoja na hayo yaliyotokea, yeye alishasikia sifa zako, za uchapa kazi wako, na kwa vile yeye ni mjasiriamali, alikuwa na hamu sana ya kuonana na mtu kama wewe, ajifunze mengi kutoka kwako, na ni muongeaji, atakusimulia mengi ambayo hata hukuyaka kuyafahamu, uwe mvumilivu tu...’akasema.‘Kwani mama yako huko kijijini anafanya kazi gani hasa?’ nikamuuliza‘Amejiajiri, ana miradi yake, ni mmoja wa viongozi wa akina mama, na hamu yake kubwa ni kuja kuwekeza hapa Dar kama itawezekana, lakini sio rahisi kama ujuavyo, gharama, masomo …, lakini hiyo ni mipango ya baadaye...’akasema.‘Nahisi kwa mtizamo wangu, mumepanga kufanya hivyo kwa urithi wa baba yako, au sio..na baba yako ana vitega uchumi vingi, nasikia ana nyumba zaidi ya tano, .....?’nikauliza.‘Nyumba zote tumepiga mnada, kwa ajili ya kulipa watu, waliopata madhara kutokana na mambo yake, ...sisi kama sisi, hatutaki chochote kutoka kwake,mali zake na miradi yake, kwetu sio muhimu, muhimu ni kulisafisha jina lake ili mungu amsamehe makosa yake,..’akasema.‘Mnaonekana hamtaki ubaya wa baba yenu uwangilie na nyie au ni mbinu tu za kuataka kunihadaa, kiukweli mimi siwaamini, nikuambie ukweli kutoka moyoni mwangu, yaliyonikuta…yamenipa fundisho?’ nikauliza‘Ndivyo tunavyotaka, lakini watu wengine wanaonekana kutokutuamini, sioni ajabu na wewe ukisema hivyo, lakini dhamira yetu ipo pale pale, hata kama hamtatuamini sisi tutafanya yale tunayoona ni sahihi, tukimaliza hayo, basi wale wenye nia njema na sisi watatuamini tu...’akasema‘Mimi sina ubaya na nyie, kama kweli mna nia hiyo njema, ila sitaki mtu kuniingilia kwenye mambo yangu, ....baba yenu alianza hivyo, akajitahidi, na nilimkanya sana, bado hakuchoka, akatafuta mbinu mpaka akaweza kuingia kwenye mambo yangu hata bila ya mimi kufahamu..kama kweli mna nia njema mumeliona hilo, lakini nina iamni kuwa sio yeye, kuna mtu anamtumia…’nikamwambia.‘Hayo mimi siyaamini sana, kuwa kuna mwanasiasa anamtumia, hapana,..mimi namfahamu baba, ni hulka yake, sawa anaweza kuwa anatumiwa, lakini yeye si ana akili….sijui lakini, maana huko mimi sija..paangalia sana..’akasema‘Sawa pamoja na sharti lako hilo, ambalo mimi kwangu ni gumu, na mimi nina sharti langu, kama tutakubaliana, basi nitajua na nyie mpo na nia njema,…’nikasema‘Sharti gani,…niambie tu , maana nia yetu ni kujenga…’akasema‘Ili kweli niwaone kuwa hampo nyuma yake, na hamna nia njema, nawataka kwanza, nipate mkataba wangu, upo mkataba wangu wa asili kati yangu na mume wangu, baba yako aliuchukua, akaugushi na kutengeneza mkataba huo ambao mnao sasa…yeye aliyeubadili, na najua kabisa anao, ule wa asili, sasa nipeni huo, ....’nikasema na yeye akanikatiza kwa kusema;‘Sisi hatujui lolote kuhusu mkataba wenu wa asili, na hatuna haja nao,  sisi mkataba tulioupata ambao hata wakili wetu anaufanyia kazo ndio huo, unaoonyesha  kuwepo kwa hisa za baba kwenye kampuni zenu, na ndio maana kwanza tulitaka kulithibitisha hilo, …’akasema‘Mtathibitishaje, kwasababu kulithibitisha hilo ni kuwaona wahusika, je mumelifanya hilo…?’ nikamuuliza‘Ndio…tumeongea na mume wako, amelithibitisha hilo...ila alisema kuwa hiyo ya umiliki wa hisa zaidi ya nusu, ya hisa, haikuwa ni hiari yake, ..kulikuwa na shinikizo fulani kwake, juu ya uwezo wake,, ila yeye alikubali tu ili mambo yaishe..na tukamuuliza ni shinikizo gani..’akasema.‘Je yeye aliweza kuwaambia  ni kutokana na shinikizo gani?’ nikamuuliza‘Hakutaka kusema ni shinikizo gani, lakini kwa vile tunamfahamu baba, kuwa akiwa anatafuta kitu, hasa mali, hajali aliyepo mbele yake, hatukutegemea kuwa watafikia hatua ya kushinikizana kiasi hicho, kwani haiingii akilini, mume wako akubali kumpa nusu ya hisa baba, kwa sababu ya deni, na ni kweli madeni yapo..kuna hati hizo,..lakini kwanini kuwe na shinikio..madeni ni madeni au sio…sasa ni nini, sisi hatukutaka kumlazimisha mume wake atuambie...’akasema.‘Wewe hukugundua ni kitu gani, si ulisema ulifanya uchunguzi wako au sio…?’ nikamuuliza.‘Hapana, sisi hatukutaka kuingilia huko kwa undani zaidi, ili iweje, kwani tunataak nini, …mmh, mimi naona yale niliyotaka kukuambia kwa sasa yanatosha, na kwa vile unataka kuongea na mama, ngoja nikamuite, muongee naye, nitamsubiria kwenye gari...na mume wako naona anaongea na wakili wake, sijui watanihitajia au la..nisingelipenda kuongea naye kwa leo…’akasema‘Ina maana mumekuja na mama yako kumbe mbona hukuingia naye..yupo wapi…!?’ nikamuuliza kwa mshangao.‘Tulikuwa naye, alikuwa na mambo yake, nikamwambia napitia kwako kwanza kujaribu kama utakubali kuongea na mimi, na yeye akawa anawasiliana na wateja wake kwenye simu, nikamuacha nje kwenye gari, yeye muda wote ni kuongea an simu, si unajua ujasiriamali ulivyo...’akasema‘Sawa nitafurahi nikiongea naye, na samahani sana, kama sitaweza kukubaliana na ombi lenu, nalisema hili mapema, uelewe msimamo wangu, muhimu ni mkataba wangu wa awali, huo ndio utakuwa ufunguo wa makubaliano mengine bila huo, sizani kama tutaweza kukaa meza moja na mume wangu...’nikasema.‘Hamna shada, ..nimefurahi sana kuongea na wewe nahii iwe ni mwanzo tu wa mazunguzmo yetu, na nina imani tutashirikiana kulimaliza hili jambo…na kama upo huo mkataba mwingine, kwanini usitolewe..usijali tutalimaliza hilo…haya ngoja mimi nikamuite mama aje muongee naye..’akasema na kusimama, tukashikana mkono, na akaondoka na kuniacha nikiwa nimesimama nikimwangalia anavyoondoka.**********Mke wa marehemu alikuwa wale akina mama wahangaikaji, wake wa shoka, hata jinsi alivyokuwa akitembea kuja pale nilipokaa alionekana ,mama mchapakazi kweli,...mwendo wake sio ule wa kike kike wa kutembea kimikogo, anatembea kama mwanajeshiAlipofika pale nilipokaa mimi nikasimama kwa adabu na kwanza , akasimama hatua chache kutoka pale niliposimama, kwanza akaniangalia kama ananikagua, halafu akanisogelea tukakumbatiana, na kusalimiana.‘Siamini kama ni wewe..’akasema‘Kwa vipi dada...?’ nikamuuliza‘Unafahamu, nimeziona  picha zako kwenye magazeti tu, kwenye majirida mbali mbali yakitangaza biashara zako, ..lakini unavyoonekana kwenye picha, sio sawa na nilivyokuona leo, leo upo kihalisia zaidi...’akasema‘Kwani leo nipo vipi na huko kwenye magazeti naonekana vipi?’ nikamuuliza kwa mshangao kidogo‘Tuyaache hayo, maana sisi akina mama tukikutana mengi tutakayoanza kuzungumzia,ni  mavazi, muonekano , sura, hata tutasahau jambo muhimu, na majukumu ya kila siku, mimi siku hizi sitaki kupoteza muda tena, na tangu nije hapa Dar, naona napoteza muda wangu bure tu na mambo yasiyonisaidia kitu...’akasema huku akikaa kwenye kiti.Akaletewa kinywaji, na matunda…akapiga mafundo mawili, halafu akainua uso na kuniangalia, akasema;‘Haya niambie kulikoni, hivi Samahani kidogo, hivi wewe na mume wako mna matatizo gani?’ akakimbilia kuniuliza hilo swali. Na kunifanya niingiwe ni tahayari kidogo‘Mhh, kwanini…oh, kwanza nikupe pole za msiba wa mumeo,maana hatujaweza kukutana kwa sababu ya haya mambo yanayoendelea kwa sasa, pili sio kweli kama watu wanavyodai kuwa eti mimi ndiye nimemuua mume wako…, kwanini mimi nimuue mume wako..’nikasema.‘Ni kweli kibinadamu, hisia hizo zipo, japokuwa mimi na mume wangu tulikuwa mbali sana, huwezi amini hilo, nimeishi kama sina mume,   lakini ki ndoa yeye ni mume wangu eeh…,siwezi kumkataa hadi kesho, japokuwa sasa ni marehemu..ila hutaamini yeye, kwa kauli yake, alishanifanya mimi sio mke wake....inasikitisha…’hapo akatulia kidogo.‘Kwahiyo mlishatalikiana au..?’ nikamuuliza‘Hamna talaka,..mimi sikukubaliana na hilo, …, kwahiyo bado alikuwa ni mume wangu, ndio maana sasa nimepewa cheo cha mjane, na hata kwenye mirathi yake sikuamini,kuona na mimi nipo kwenye orodha ya warithi,…ni ajabu kabisa, alikumbuka kuniweka nahisi hili kalifanya baade sana, sijui ni nani kamshawishi kufanya hivyo..hata hivyo kinafsi yangu, sikutaka chochote kutoka kwake,…mengine tuseme yote ni mapenzi ya mungu..’akasema akionyesha huzuni.‘Je wewe ulikuwa ukimpenda mume wako?’ nikajikuta nikimuuliza hivyo.‘Sana tu...huwezi amini, mimi nilikuwa nampenda sana mume wangu, na nikuambie ukweli,..hili watu hawalifahamu na hata mume wangu akitoa kauli zake hizo za kuwa hanitambui kama mke wake..alikuwa akisema hivyo akiwa kalewa tu…kuwa  mimi ndiye niliyemtaka yeye…awe mume wangu...’akasema na kunifanya niingiwe na hamu ya kuyafahamu maisha yao.‘Hebu niambie ina maana wewe ndiye uliyemtongoza mume wako…au kwanini alikuwa akisema hivyo…, nisamehe kwa kuuliza haya, maana imenipa hamasa tu ya kufahamu…?’nikamuuliza‘Hahaha, ndio hivyo, siwezi kulipinga hivyo..lakini sio kwamba alikuwa hanipendi, kihivyo, hapana, kipindi hicho tulikuwa kwenye ushindani wa kumpata yeye, unajua tena kijijini, na sisi tulijiona wasomi fulani..hivi, tukiwa darasa la sita, mwili na sura vilitudanganya…’akatabasamu.‘Kulikuwa na kundi la mabint warembo wa hapo shuleni na kijini, nikiwemo mimi..unasikia…sasa, unajua tena, naongea haya..aah....tulikuwa mabinti watatu, warembo…kila mmoja anataka yeye ndiye ampate huyo mwanaume, kipindi hicho yeye ni kijana mtanashari eeh, na ana majigambo fulani, kiingereza mdomoni hakimtoki, ..’akatulia.‘Mrembo..?’ nikauliza na yeye akacheka, halafu akasema‘Kijijini bwana,..mwanaume akionekana msomi, kiingereza kingi…si unajua tena, huyu jamaa alikuwa msomo, kiukweli…na …ndio hivyo..basi bwana, sisi ni mabinti wadogo warembo wa hapo kijijini...ilikuwa hapatoshi, kushindana ni nani atachukuliwa na huyo msomo,..hahaha, ..lakini ndio hivyo, mwisho wa siku nikasimama mimi kidedea, ..tukawa wapenzi, japokuwa ni upenzi wa kijijini...’akasema.‘Hongera, ...’nikasema‘Unafahamu, mimi tangu nikiwa mtoto, nililelewa kwa shida, sikuwahi kupata raha, ...wazazi wangu hawakunidekeza, hawakuwa na kitu, kwahiyo ilikuwa ni maisha ya suluba, ..kula na kulala kwa shida, ..unajua maisha tena ya kijijini..basi ikatokea nikamfahamu huyo mwanaume…, kiajabu ajabu tu..’akasema huku akitabasamu.‘Yeye nakumbuka tangu nimfahamu, alikuwa ni mtu wa kusoma vitabu tu...hata alipokuja huku mjini, na baaadaye akawa anafika fika, alikuwa muda mwingi ukimuona  kashikilia kitabu, hivi vitabu vya hadithi, alikuwa anapenda sana kusoma vitabu vya kizungu, nakumbuka kuna vitabu vyake, aliwahi kunionyesha, hata mimi baadaye nilipojiendeleza nimekuwa nikivisoma, hivi vinaitwa, eeh, Jemsi Hadley Chase, na Peri Masoni, nahisi ndio maana akajikita kwenye uanasheria...’akasema.‘Siku ya kwanza kukutana kwetu, ilikuwa kama vile wanavyoonyesha kwenye sinema, maana ilikuwa ni kwenye shughuli, mimi nilikuwa kasichana, na bahati mbaya mwili wangu ulikuwa haraka, ni baadhi ya wasichana kijijini kwetu tuliokuwa kimwili haraka, ...ilikuwa siku hiyo nafanya usafi kuwaandalia wageni, mara wakati nawapelekea watu maji ya kunywa, nikagongana naye, ..akadondosha kitabu chake, kikalowana maji...maana kulikuwa na maji maji sakafuni, mimi nikakiokota na kukifuta kwa kitambaa changu cha mtandio. Picha ndio ilianzia hapo…Nilipomaliza nikamkabidhi kitabu chake, kumbe mwenzangu wakati wote huo nahangaika kukifuta kile kitabu, alikuwa akinitizama, na hata namkabidhi hicho kitabu, bado alikuwa akinitizama tu machoni....hapo mimi bado mbichi nasoma, vititi saa sita..’akasema.Nilishamuona kabla, na tulikuwa tukimuongelea shuleni, wasichana na tama zetu…lakini hilo la kukutana kihivyo, ilikuwa siku hiyo, na ndio nikaweza kujuana naye, na kuanza kujenga urafiki, na urafiki ukatibua nyongo…’akatulia‘Kwa vipi…?’ nikauliza‘Alinibebesha mimba..na kunifanya nifukuzwe nyumbani kwa wazazi wangu..’akasema‘Mungu wangu…’nikasema hivyo‘Nilikwenda kuishi kwa bibi, mpaka nikajifungua...hebu fikiria, darasa la sita enzi hizo, unabebeshwa mimba,hata darasa la saba sikumaliza, ingawaje baadaye nikijisomesha, kujiendeleza,…usinione hivi , nilijisomesha hadi sekondari, kiaina aina.‘Basi aliponipa mimba, wazazi wangu wakafahamu, palikuwa hapatoshi jamaa huyo akakimbilia mjini, sio kweli kuwa alikuja huku mjini kwa ajili ya masomo, hapana,..ni lugha ya kudanganya , kuficha ukweli, yeye alikimbia kuogopa balaa la wazazi wangu....’akasema‘Lakini umesema yeye anasema ni wewe ndiye uliyemtongoza, naona hapo inaonyesha yeye alikupenda pendo la awali,...au sio, lile pendo watu mnaonana hapo hapo, kunajengeka hisia za kupendana au sio...’nikasema.‘Baada ya pale,…kwenye shughuli… siunajau tena mambo ya shule, nikawahadithia wenzangu, basi, marafiki zangu kila mmoja akataka ampate yeye, na kila mmoja akawa anajibaragua kwake, kijinsi ajuavyo yeye, mimi ikaniuma sana, wivu tena… ina maana kuwaelezea wenzangu ndio imekuwa nongwa..basi nikaona nisilaze damu, ...’akasema.‘Nilipoona wenzangu wanambana sana huyo kijana, kila mara wapo naye, nikaamua kumwambia ukweli, ilikuwa ni kazi nzito kujielezea si unajua tena wasichana…, lakini mwisho wa siku alikubali kuwa hata yeye ananipenda sana tangu siku ile kwenye shughuli, ya kudondosha kitabu,...mambo yakakolea sasa kuanzia hapo, ikawa mimi na yeye, nikawa nachapwa nyumbani kwa ajili yake, sikusikia,...haniambii  mtu...na asiyesikia la mkuu huvunjika mguu...ikatokea kama mchezo tu, mimba hiyo...’akatulia.‘Kiukweli mimba ilikuwa ni bahati mbaya, maana pamoja na urafiki wetu huo, hatukuwa na mambo ya kisasa, haya ya kimjini mjini, hapana...ilikuwa ni kukaa pamoja kuongea, kutaniana, kukimbizana,...ila siku hiyo sikumbuki ni kitu gani kilitokea, na tukajikuta tumefanya jambo ambalo ndilo lilimleta huyu mtoto wangu duniani, mliyetoka kuongea naye....’akatulia kidogo.‘Nilitenda hilo mara moja, na ikawa ndio tiketi ya shida, ...shida kweli...na nikuambie ukweli, mtoto huyo alinitesa kweli kweli…ilikuwa ni mimba ya fundisho, na sikutaka kuzaa tena..licha ya mimba yake, na hata malezi yake…, nilimlea kwa shida sana, huwezi amini. Siwezi hata kukusimulia, ....hata hivyo.. mungu hakunitupa mja wake, mateso hayo yalinijenga..nikawa mke-dume, aliyejengeka kijasiri, unaniona nilivyo hata kutembea kwangu..na nilitaka mtoto wangu awe hivyo hivyo, sikupenda awe mtoto wa ovyo ovyo, nilijitahidi kumlea kihali niliyoona ni njema kwake..’akasema.‘Ina maana ulipomzaa huyo mtoto, hukupata msaada kutoka kwa mume wako?’ nikamuuliza.‘Msaada gani, angelipata wapi pesa za kunisaidia wakati huo, wakati huo wa awali, yeye mwenyewe alikuwa kula kulala..hana mbele wala nyuma, na aliponipa mimba akakimbilia mjini kujificha, hakuonekana, hadi nilipojifungua na alifika kwa mara ya kwanza mtoto anatembea,hamjui ,.....na sikutaka hata kuongea naye..’akasema.‘Ikawaje sasa mpaka mkafunga ndoa?’ nikamuuliza‘Wazazi wangu waliweka shinikizo..kuwa ni lazima anioe...huoni , hata nikiwa naye naonekana mimi ni mkubwa kuliko yeye, lakini ni kwasababu ya maisha, na mwanamke mara nyingi anaonekana mkubwa, kama mkiwa umri karibu sawa..sisi wanawake tunakuwa haraka haraka, na ukizaa ndio basi tena...’akasema.‘Basi ikabidi kweli anioe, kuepusha shari,  japokuwa hakutaka, alishaniona sifai tena..japokuwa mimi nilikuwa nampenda kweli kweli,...hata tulipoona hatukuweza kuishi kwa upendo, ilionekana kama ndoa ya lazima, akawa ananinyanyasa, ...yaani sikuwa na raha na yeye, na hakutaka hata kutembea na mimi, yaani kutembee mitaani kama mke na mume, haikuwahi kutokea....aliniona simfai, mwanamke wa kijijini, mshamba,  asiyejua kujiremba...na yeye keshakulia mjini, anawafahamu warembo wa mjini, eeh..’akasema akibenua mdomo kwa dharau.‘Basi bwana, ..mimi nikawa mama wa kijijini, sikujali, bado nilimtambua yeye kama mume wangu, yeye akawa anishi mjini , mimi kijijini, sikujali, nikawa napigika kijijini, maisha ya shida, anakuja mara moja au mbili kwa mwaka, ..hanitumii pesa, akibahatisha ni mara moja kwa miezi mitatu, ni pesa yenyewe pesa basi, nikawa nahangaika kivyangu kumlea mwanangu, sikujali na wala sikukata tamaa...’akasema.‘Nikawa naletewa taarifa za ajabu ajabu kutoka huko mjini, kuwa mume wangu ana wanawake, sio mwanamke, ana wanawake, anawabadili kama nguo...ikafika mahali nikamuuliza, na kumshitaki kwa wazee, nilivyosikia, hutaamini kibao kiligeukia kwangu, kuwa mimi nasikiliza majungu, ni wapi nilimuona na hawo wanawake,...iliniuma sana, kwani mmoja wa wanawake zake, namfahamu, alikuja kuniambia yeye mwenyewe, kuwa mimi nitabakia huko kijijini yeye atakuwa akistarehe na huyo mume wangu, eti sababu mimi nilimuibia yeye...’akasema.‘Mwanzoni nilipata shida sana, na ikafikia hatua nikaamua kumwendea huko mjini, ili nikapate huo ushahidi wanaoutaka wazee, najuta kwanini nilifanya hivyo, maana nilizalilika,....sitasahau, kwani siku hiyo nikiwa nimevalia zile nguo zetu, kwetu kijijini niliziona za maana , gauni refu...mikono mirefu, kitambaa kichwani,...nikaingia dar, ilikuwa ni mara ya tatu, nilishawahi kufika kabla.‘Nilikuwa nafahamu wapi mume wangu huyo anaishi, nikafika bila hata ya yeye kufahamu, ilikuwa saa kumi kumi hivi, nikafika nyumbani kwake, ...kulikuwa na mvua mvua inaanza kunyesha, nikafike eneo alikopanga chumba, alikuwa na chumba kimoja, maisha muda huo hayajamnyookea,…anasoma na kufanya kazi, nikagonga mlango , mara akatokea mwanamke na khanga moja kiunoni, akafungua mlango, huku akisema kwa nyodo.‘Hivi nani hawa wanaharibuu starehe za wenzao, ni Malaya gani wewe...’akasema huku akinifungulia mlango, na kuniona mimi, akashikwa na butwaa, maana ananifahamu, ndio huyo aliyeniambia, kuwa mimi ndiye nilimuibia mchumba wake..kiukweli, yeye alionekana mrembo kwa maisha aliyokuwa akiishi ya mjini, mimi nimeshachakaa na maisha magumu ya kijijini, na kuzaa .‘Ni wewe....?’ akauliza kwanza kwa aibu lakini baadaye akabadilika na kugeuka kuangalia ndani, na kusema kwa sauti iliyojaa dharau;‘Haya wewe bwana, kuna mgeni wako nje..’akasema na kuingia ndani, na mimi nikaingia na kumkuta mume wangu akiwa na taulo kiunoni, kakaa kwenye sofa, akageuka na kuniona, hakuonyesha ile dalili ya kushituka akasema;‘Wewe mwanamke ni nani kakuambia uje bila taarifa, bila ya kibali changu, nataka nikiinuka hapa haupo ..rudi huko, huko ulipotoka..’akasema huku haniangalii usoni...’‘Mume wangu niende wapi, ..wakati nimekuja kwako, ..nitapata wapi basi muda kama huu?’ nikamuuliza kwa adabu zile za kijijini, huku moyo unaniuma kweli.‘Utajua mwenyewe....kwani ni nani alikuambia uje, nilishakuambia kuwa mimi sikutaki...unang’ang’ania tu kuwa wewe ni mke wangu, hebu jiangalie wewe ulivyo, una hadhi gani, na shepu gani ya kuwa mke wangu, ...huoni aibu, eti kusema `mume wangu’, sikiliza rudi huko huko ulipotoka,unasikia...’akasema na kusimama,Mimi sikusogea nikasimama pale pale, na yeye bila kujali kuwa kavaa taulo, akaanza kunisukumia nje huku yule mwanamke wake, akiniangalia kwa nyodo kashikilia kiuno...sikuona taabu, awali nikapambana naye , lakini mwanaume ni mwanaume,…akanitoa nje..nilikaa pale nje, kibarazani hadi walipomaliza mambo yao, ...’akasema huku akitabasamu tu.‘Ina maana hawakujali, na bado walikuwa wakiendelea na starehe zao?’ nikamuuliza. 


    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog