Search This Blog

Friday, November 18, 2022

USILIE (DON'T CRY) - 5

 





    Simulizi : Usilie (Don't Cry)

    Sehemu Ya Tano (5)





    Hadi yanapita masaa matatu Glory alikuwa bado hajarejewa na fahamu,Deus na watu wake walizidi kuimarisha mipango yao ndani ya ile nyumba,walihakikisha kila kitu kiko mikononi mwao

    "Sasa hapa lazima tuhamishe utajiri wetu twende hata nje ya hii nchini"aliongea Deus.

    Walinzi walikokuwa wanamlinda Glory walizidi kumpepea na hawakutaka kumpereka hospital.

    "Huyu Dada lazima apate aibu,yaani utajiri wake ulikuwa umempa umaarufu leo hii anaenda kuwa maskini"alijisemea mlinzi mmoja wa kike.

    Baada ya masaa matani Glory alirejewa na fahamu,na kwa wakati huo ilikuwa saa tatu usiku,alipogeuza shingo yake alimuona Deus na wale watu wakiwa wamekaa mezani wakioneka kujadiri jambo.

    "Kweli mme wangu umenigeuka?aliuliza Glory huku akianza kudondosha machozi,hata nguvu za kutembea hakuwa nazo kabisa.

    "Sijakugeuka ila ukitaka kuanzia sasa utakuwa chini yangu na utafuata mimi nisemacho"aliongea Deus.

    "Utaanza kudeki nyumba na kuosha vyombo"aliongea Inno huku akitabasamu.

    "Hapana siwezi kukubali"alijisemea Glory baada ya kuwaza sana alipata nguvu za kunyanyuka na kwenda moja kwa moja mpaka kituo cha police.

    "Tutalifanyia kazi suala lako"aliongea Askari mmoja aliyekuwa zamu.Kwakuwa ulikuwa ni usiku alirudi nyumbani akipanga kesho yake ndo aende mahakamani,lakini Deus aliweza kuligundua hilo,moja kwa moja milion hamsini zilitimwa kwenda kwenye akaunti ya hakimu.Usiku ule hakuna aliyeweza kulala,si Glory wala wazazi wake, Glory alilia mpaka machozi mpaka yakaisha kwenye mboni zake.

    "Mungu nisaidie juu ya hili ili nikwepe aibu ninayoiona mbele yangu"alijisemea Glory wakati huo akingoja kupambazuke ili awahi mahakamani.Deus na watu wake hawakuwa na wasiwasi kabisa kwakuwa walijua kuwa kila kitu kimekamirika.Asubuhi na mapema Glory alikuwa wa kwanza kuamka na kuwahi mahakamani.

    "Mimi bado najulikana kama tajiri hivyo lazima nisikilizwe nikiwa wa kwanza"alijisemea Glory wakati huo akiwa pale mahakamani akingoja mahakama ifunguliwe.

    Saa mbili asubuhi mahakama ilifunguliwa, Glory alifurahi kuona hakimu aliyekuwa anamfahamu.

    "Utajiri ukirudi mikononi mwangu sitakuja kumuamini mwanaume yeyote mpaka naingia kaburini"alijisemea Glory.

    "Au nipo ndotoni naota?yawezekana vipi Glory mimi tajiri nirudi katika hali ya umasikini?siwezi kukubali lazima hizi mari zirudi mikononi mwangu,nimehangaika peke yangu leo hii eti mtu azichukuwe kirahisi?hapana haiwezekani"alijisemea Glory.Hakutaka kuonyesha hofu yeyote kuogopa kugundulika kwa watu.

    "Huyu mwanamke tajiri kafuata nini tena hapa?.

    "Hata sijui,kama kuna mtu kamkorofisha ujue huyo atafungwa kifungo cha maisha"

    "Kweli matajiri kama hawa sio watu wazuri,unaweza kuta ni kosa dogo lakini analifuatiria"yalikuwa maneno ya wanaume wawili waliokuwa eneo lile.Watu waliokuwa wanamjua Glory walikuwa wakimpisha na kumuachia nafasi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kweli ukiwa na pesa unaheshimika"alijisemea mwanamke mmoja baada ya kuona mme wake akimpisha Glory.

    Mda wa kesi ulifunguliwa,hakimu kwa kuwa alimjua vyema Glory alimpa nafasi akiwa wa kwanza, Glory baada ya kuelezea shida yake hakimu alizungusha kiti chake kisha akamwangilia Glory kana kwamba kuna kitu anakifikiria.

    "Shida yako nimeisikiliza,lakini kabla ya kuja hapa ulitakiwa uwe na barua kutoka kituo cha police,au unataka kuniambia huko unakokaa hakuna kituo cha police?hakimu alimuuliza Glory.

    "Nimeenda jana lakini naona hawako siliasi kushughulikia suala langu"alijibu Glory.

    "Hakuna kifungu chochote kinachoniruhusu kumhukumu mtu akiwa hajaretwa na police hapa,hivyo Dada yangu rudi kituo cha police"aliongea hakimu.Glory alichanganyikiwa sana,moja kwa moja alienda kituo mpaka kituo cha police.

    "Sawa Dada yangu lakini hatuna udhibitisho wa moja kwa moja kuwa zile zilikuwa mali zako,labda kwakuwa mmefunga ndoa tutaweza kumwambia akupe fungu kidogo kwa ajili ya kuendesha maisha yako"aliongea mkuu wa kituo.

    "Lakini nadhani hata na wewe unafahamu kuwa zile zilikuwa mali zangu,hivyo kama utanisaidia ntakupa nusu ya hizo mali"aliongea Glory.

    "Hapa hatufanyi kazi kwa ajili ya kupokea rushwa,sitaki maneno mengi kalete cheti cha ndoa ili tuone atakupa fungu gani"aliongea yule mkuu wa kituo.Glory alizidi kuchanganyikiwa hata cheti cha ndoa hakuwa nacho,kilikuwa bado kiko kwa padri.Bila kuaga Glory aliondoka huku kichwa chake kikiwa chini kwa mawazo,alijikuta akidondosha machozi mengi sana,kila alipomfikiria mwanaye aliyekuwa huko Uingereza hapo ndipo alizidi kuchanganyikiwa zaidi.

    "Mungu uko wapi kwa nini unaendelea kuruhusu haya matatizo yawe upande wangu?alijiuliza Glory huku akitembea tembea sehemu ambayo hata hakuijua.

    "Mpaka nilisahau kutembea kwa miguu"alijisemea Glory.Bado watu waliokuwa wanamuona njiani hakuna aliyeweza kumshangaa,magari mengi yalisimama mbele yake kama kumpa rifiti lakini hakuwa tayari kupanda gari la mtu,kila alipokuwa anapita sehemu zenye watu wengi alijitahidi kutengeneza tabasamu ili asigundulike.

    Huko China Issa baada ya kukosa kuharibu ndoa ya Glory alijikuta anaacha hata kufuatiria mitandao ya kijamii,yeye alizidi kufanya kazi kwa bidii,hakuacha kujipa matumaini kuwa akiwa tajiri lazima Glory arudi mikononi mwake.

    "Yaani pamoja na kutoa msaada wote huu sikuwahi hata kufanya nae tendo la ndoa harafu eti leo hii anisaliti nami nikubari?,hapana naamini ipo siku ataukumbuka upendo wangu"alijisemea Issa kwa kipindi chote alichoishi ndani ya China hakuwa kujihusisha na na mapenzi,Kama kawaida ya watu weupe kuwapenda watu weusi wasichana wengi walijaribu kuweka ukaribu na Issa lakini yeye hakuwa tayari,bado hakutaka kumsaliti Glory japo kuwa alijua vyema kuwa Glory ameshaolewa tayari.

    "Naogopa dhambi ya usalti"alijisemea Issa kila alipokuwa anaona wenzake wakiwa na wapenzi wao.

    Deus na watu wake walihakikisha kila sehemu ambayo wangehisi itawaletea matatizo walikuwa wanatoa pesa, Glory alikoswa msaada kila sehemu alipaona pagumu.

    "Sasa ni wakati wake wa kumtangaza hadhalani ili watu wote wajue"alisema Deus akiwa na wenzake,kwanza waliuza magari yote ya Glory pamoja na maduka na miradi mingine,hawakutaka kufanyia biashara zao nchini Tanzania.Katika wanaume wale kulikuwa na mwanaume mmoja alikuwa anaitwa Andrea,Andrea alikuwa na moyo wa huruma sana,mara nyingi alikuwa anawazuia wenzake wasimtangaze Glory lakini wenzake waligoma, jambo lile lilizua tafarani baina yao lakini badae wasiruhuhishana yakaisha lakini Andrea aliendelea kuwaza namna ya kuwasiliti wenzake.

    "Hawa wanar roho ya kishetani siwezi kufanya nao biashara,lazima niwaue wote huu utajiri urudi kwa mwenyewe"alijisemea Andrea.Baada ya kuuza kila kitu sasa walikusanyika sehemu moja na kupanga kwenda kuanzisha makazi yao Africa kusini,kwakuwa pesa walikuwa nayo ya kutosha hiyo haikuwapa shida.Bado Andrea aliendelea kuwaza namna ya kuwasiliti wenzake.

    "Kama nikifanikiwa kuwaua itakuwa furaha kwa yule mwanamke"alijisemea Andrea.Taarifa za kufirisika kwa Glory zilianza kusambaa kwa kasi,kwa siku nzima takribani nusu ya Tanzania ilikuwa imepata zile taarifa,watu mbalimbali walikuwa wanatumia mitandao ya kijamii waliendelea kuzisambaza zile taarifa.

    "Mimi nilisema kuwa yule mwanamke hawezi kupata utajiri wote huu bila kuwezeshwa na mtu,ona sasa kagombana na mme wake mambo yake yamewekwa wazi"

    "Nasikia yule mwanaume kauza magari yote"

    "Ndio taarifa yenyewe hii hapa"yalikuwa maneno ya vijana wakiwa kijiweni,mmoja aliongea huku akitoa simu yake na kuonyesha ile taarifa.

    Kwa siku hiyo maneno mengi yalisemwa,Safari ya Glory ilishia kwenye baa moja iliyokuwa karibu,hapo aliweza kujifunga kanga yake mpaka kichwani lengo asijulikane,hakutaka kunywa pombe kwa kuwa hakuwa na hera,alingoja hadi ulipokuwa usiku hapo aliweza kwenda mpaka kwenye kichaka kilichokuwa karibu.

    "Natamani hapa kuwe na chatu ili animeze nitoke kwenye hii dunia ya mateso"alijisemea Glory wakati akiingia kichakani.

    Asubuhi kulipopambazuka kila gazeti liliandika habari ile,kila mwandishi alijitahidi kukipamba kichwa cha habari kadri alivyoweza.

    "Hatimaye mwanamke tajiri arudi katika hali ya kuokota makopo"kilikuwa kichwa cha habari kwenye baadhi ya magazeti ikaambatanishwa na picha ya Glory.Glory alitoka kichakani aliweza kujifunga vizuri kanga mpaka kichwani hakuna mtu ambaye angeweza kumtambua,bado aliendelea kuwaza wazazi wake kuwa wataaishi vipi mjini hapo.

    Glory baada ya kusoma baadhi ya vichwa vya habari alisikitika sana.

    "Hii aibu siwezi kuendelea kuivumilia wacha nife,najua mwanangu amekuwa tayari,kuhusu wazazi watajua namna ya kuishi"alijisemea Glory,baada ya kuona gari likija kwa kasi aliingia katikati ya barabara na kulala kabsa.

    "Mungu pokea roho yangu"alijisemea Glory wakati huo alifumba macho kungoja kifo.





    Dereva wa gari baada ya kuona mtu amelala katikati ya barabara alijitahidi kubana breki mpaka tairi zikatoa moshi,gari alilibana mkono wa kulia hivyo hadi anafikia sehemu aliyokuwa amelala Glory lilikuwa limemkwepa tayari limemkwepa,watu wengi walishangaa tukio lile la Glory kulala katikati ya barabara,bado watu hawakuweza kumtambua.

    "Loooh!watu wamechoka na maisha kweli,yaani mtu anajitoa uhai hivihivi"alijisemea mwanamke mmoja aliyeshuhudia tukio lile.Watu waliokuwa eneo lile walimbeba Glory aliyejifanya kupoteza fahamu.

    "Kuna duka la dawa hapo muwahishe haraka"alisema mwanaume mmoja.Bila kuchelewa Glory alipelekwa mpaka kwenye duka la dawa.

    "Mungu wangu naenda kuaibika"alijisemea Glory.

    "Huyu anatatizo gani?aliuliza mama mmoja wa makamo.

    "Atakuwa ana tatizo labda maana amelala barabarani"

    "Wengine washachoka na maisha,sasa gharama zitakazo hitajika atalipa nani?aliuliza yule Mama mwenye lile duka la dawa,watu wote waliokuwa pale walitazanamana hakuna aliyeweza kutoa jibu,taratibu walianza kuondoka mmoja mmoja.Glory kwa macho ya chini chini alikuwa akiwatazama.

    "Hapa ni kutoroka,siwezi kuendelea kukaa hapa nitapata aibu zaidi"alijisemea Glory.Watu waliomsaidia Glory waliondoka mmoja mpaka wakaisha,yule mwanamke alingia ndani kwakuwa kulikuwa bado na wagojwa wengine anawahudumia,ile nafasi aliitumia Glory alitoka pale mbio mbio,bado hakujua atajiua kwa njia gani,aliogopa aibu,makazi yake yalikuwa vichakani huko ndo alikuwa anajificha,hata chakula chake kilikuwa cha taabu kukipata.

    "Sasa umefika wakati wa kuiuza hii nyumba,hivyo kusanya kila kilichochenu muondoke humu"aliongea Inno akiwaambia wazazi wake na Glory.Wote walitazamana hawakuwa na ujanja wa kukataa,hivyo walikusanya mizigo yao kisha wakaondoka.Ndani ya hizo siku mama Glory hakuweza kula chochote kutokana na mawazo ya Glory hakujua alipokuwa.

    "Mungu tuepushe na hii aibu"alijisemea mama Glory wakati akipanda gari kurudi kijijini.

    Andrea aliendelea kuandaa mpango wa kuwasaliti wenzake.

    "Hawa ni kuwapa sumu na kuwaua wote"alijisemea Andrea huku akiwaza jinsi ya kuwaua.Alivuta subira mpaka wauze nyumba waliyokuwa wanaishi wazazi wake na Glory.

    Matajiri kutoka jiji Dar es salaam walikuja mkoani Arusha kwa ajili ya kununua nyumba ya Glory,ilikuwa nyumba ya kisasa.

    "Million miatatu"alisema bosi mmoja.

    "Hapana ongeza million Mia ziwe mia nne"aliongea Deus.Bosi yule hakuonekana kuwa na kigugumizi hivyo aligiza pesa kutoka kwenye benk yake zihamishiwe kwenye akaunti ya Deus, Andrea alizidi kufurahi,baada ya kuhakikisha kadi ya benk ya Deus iko mikononi mwake moja kwa moja alienda mpaka kwenye duka linauza dawa za mifugo.

    "Kaka Mambo vipi? alisalimia Andrea.

    "Salama kaka karibu"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Asante nilikuwa naulizia dawa ya kuua panya kwa dakika tatu"

    "Ipo tena ni kali sana,ukiramba kidogo ujue tayari unaaga dunia"

    "Sema kweli"

    "Ndio hivyo,hakikisha unaiweka mbali na watoto"

    "Sawa nipatie"yalikuwa maongezi ya Andrea na muuza duka.

    "Made in Thailand"(imetoka ndani ya Thailand)alisema yule muuza duka wakati huo akimkabidhi Andrea.

    "Hii kweli inonekana kuwa kali,kwa heri Deus pamoja na Inno, Glory utajiri wako utarudi mikononi mwako"alijisemea Andrea wakati akizipiga hatua kurudi walipokuwa wanaishi ili akamalizie mchezo.

    Glory alianza kupoteza hadhi,mwili wake ulianza kusinyaa,weupe wake ulianza kupotea na hii ni kutokana na kuishi polini,mda wote macho yake yalikuwa mekundu sana,na kwa mda huo alikuwa hataki kula kitu chochote lengo afe kwa njaa.

    "Najua baada ya siku nane nitaaga dunia,mwanangu naomba ubaki salama"alijisemea Glory ,aliona siku nane ni nyingi kwa upande wake hivyo alijaribu kujinyonga lakini nayo ilishindikana pia.

    Andrea aliweza kufika walipokuwa wanaishi na wenzake,moja kwa moja ile dawa alipanga kuiweka kwenye pombe walizokuwa wanapendelea kunywa.

    "Oyaaa wazee leo lazima tufurahi kwakuwa ni siku yetu ya mwisho kukaa nchini Tanzania"aliongea Andrea kwa mbwembwe.

    "Hiyo kawaida yaani lazima leo nilale na walembo watatu"aliongea Inno.

    "Hiyo haina uibishi wazee,kikubwa agizeni vinywaji mnavyohitaji hata kama vitatoka nchini Kenya poa tu hera tunayo yakutosha"aliongea Deus,vinywaji vilivyokuwa pale vilikuwa vichache sana na hap Andrea ndo alipanga kuwa wenzake wakilewa sana ile dawa aiweke kwenye vile vinywaji wafe moja kwa moja, aliendelea kuwahesabia dakika.

    Deus na Inno walianza kunywa pombe,kila dakika zilivyokuwa zinasogea ndivyo walivyokuwa wanazidi kulewa.Andea alikuwa anakunywa taratibu sana baada ya kuona kuwa wamelewa sana alitoka nje na kwenda kunuua vinywaji vingine,baada ya kuleta vile vinywaji alifungua na kuiweka ile sumu,kwa wakati huo Deus na Inno walikuwa tayari wameshalewa sana.

    "Wazee Kuna pombe hapa hebu onjeni"aliongea Andrea.

    "Hatutaki pombe sisi tunataka walembo"alijibu Inno kwa sauti kilevi.

    Andrea baada ya kuona ile pombe wamekataa kuinywa aliaamua kuimimina kwenye chupa zao zilizokuwa na pombe nyingine.

    "Lazima watakunywa tu"alijisemea Andrea.Kwa kuwa walikuwa wamelewa sana hivyo hiyo pombe walianza kuinywa,kweli hazikupita dakika tano kila mmoja mapovu yalianza kumtoka mdomoni na puani,baada ya dakika kumi walikuwa tayari wameaga dunia.Andrea alifurahi kurikamilisha hilo.

    "Mali ya dhuruma huisha kwa dhuruma,wasalimie kuzimu"aliongea Andrea huku akiwavuta kutoka sebreni kwenda kuwahifadhi chumbani.Baada ya kurikamilisha hilo alitoa simu yake mfukoni na kuiweka sikioni.

    "Hallow,andaeni vijana wa kazi kuna maiti huku,hakikisha mpango unafanyika usiku huu kuna million kumi mezani"aliongea Andrea,hazikupita dakika arobaini tayari gari ilikuwa imesimama nje nyumba ya Andrea.Walishuka vijana watatu waliopakia miili ya akina Deus na Inno,hakuna aliyeweza kuitambua,mpaka wanaifikisha msituni na kuifukia hakuna aliyeweza kuitambua.

    Kazi ilibaki kwa Andrea kumtafuta Glory,kwa wakati huo Glory msituni alizidi kukonda,hata maji hakuweza kuyaweka mdomoni alikiona kifo cha mateso mbele yake.

    "Mbona nateseka hivi kwa nini nisijiue kwa uharaka zaidi?alijiuliza Glory,moja kwa moja alianza kuunganisha kanga yake,baada ya kuhakikisha imekuwa kamba ngumu,alivuta subira giza liingie.

    Andrea baada ya kuhakikisha pesa zote ziko kwenye akaunti yake kazi ilibaaki kumtafuta Glory,hakujua pa kumpatia,alizunguka siku nzima ndani ya jiji la Arusha,lakini aliambulia patupu.

    "Au tayari emepoteza maisha?nikifanya makosa namkosa"alijisemea Andrea wakati huo ilikuwainafika saa moja Jioni.

    "Lakini nikitangaza dau lazima apatikane"alijisemea Andrea.

    "Million kumi na tano kwa atakayewezesha kupatikana kwa huyu mwanamke"alikuwa ujumbe uliokuwa na picha ya Glory.moja kwa moja aliusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

    "Oya wadau huyu si ndo yule tajiri aliyefukuzwa na mme wake?

    "Ndio ndo huyu huyu kuna nini kwani?

    "Soma ujumbe kuna bonge la pesa"

    "Ati nini?million kumi na tano?

    "Ndio hii ndo pesa ya kuipata,tujiandae tuanze kumsaka"yalikuwa maneno ya vijana wawili waliokuwa wanaishi chumba kimoja,usiku huo hawakutaka kungoja walianza kuzunguka kwenye lili jii la Arusha wakimtafuta Glory.Taarifa ile kila mkazi wa Arusha aliyeipokea alihakikisha anakuwa makini kwa kila mtu aliyekuwa anapishana naye,mpaka kwenye vyombo vya habari vilitamgaza taarifa ile,wengi waliamini kuwa tayari Glory atakuwa ameshapoteza maisha.

    "Bora kuwa masikini utaishi kwa amani,lakini tajiri mda wote anaishi kwa hofu,cheki huyu kafukuzwa na mme wake lakini hatujui kama bado yuko hai"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Unayosema ni ya kweli,kajiua kukwepa aibu"yalikuwa maongezi ya wa mama wawili waliopata taarifa ile kupitia kwenye mtandao wa Facebook.

    Vifo vya Deus na Inno hakuna aliyeweza kuvigundua zaidi ya Andrea,bado hakutaka kuamini kumkosa Glory aliongeza dau usiku ule ule zikawa million therathini.Watu walizidisha umakini kuhusu kumtafuta Glory,kila mtu alihakikisha million therathini zinaingia mikononi mwake,wakati huo Glory kule msituni baada ya kusubiri giza liingie ajitoe uhai, hatimaye usingizi ulimpitia.

    Bado kila mtu alihakikisha anampata Glory ili akachukue zile pesa.





    Hadi inafika asubuhi hakuna aliyeweza kumuona Glory,watu walizidi kuangaliana.Taarifa ile iliwafikia mpaka police,moja kwa moja walianza kumtafuta mtu aliyekuwa amesambaza taarifa ile,kwakuwa ile taarifa ile ilikuwa nanamba za simu hivyo kupitia GPS(Global Positioning System)waliweza kugundua ile namba ilikuwa maeneo gani moja kwa moja walianza kufuatilia,hazikupita dakika thelathini walikuwa tayari wako nyumbani kwa Andrea ambaye hakuoneka kushtuka baada ya kuwaona wale askari aliwakaribisha vyema,baada ya maongezi ya hapa na pale Askari mmoja aliamua kumuuliza Andrea.

    "Tumekuja hapa tumesikia unamtafuta mwanamama huyu alitefukuzwa na mme wake,je kwanini unamtafuta hivyo na kuweka pesa nyingi kiasi kile?aliuliza Askari mmoja.

    "Nimeamua kumsaidia ndo maana nafanya hivyo"alijibu Andrea kwa kujiamini.Askari wote walipoa baada ya Andrea kutoa kitita cha pesa na kuwapa wale askari.

    "Jitahidi kumtafuta nanyi mkimuona million thelathini iko juu ya meza"aliongea Andrea.Wale Askari waliondoka baaada ya kupokea hongo.

    "Pesa ndo inaongea"alijisemea Andrea.

    "Dau la pesa limeongezeka million arobaini"ulikuwa ujumbe wa Andrea kwenda kwenye mitandao ya kijamii,watu walizidi kupagawa kila walipokuwa wanaona dau linaongeza.

    Kwingine kwa Glory ndo alikuwa anashtuka kutoka usingizi,alishangaa kuona jua tayari limechomoza.

    "Ahaaa tayari kumepambazuka,lakini hakijaharibika kitu hata Leo ntajimaliza"alijisemea Glory wakati huo akiangalia kitanzi chake alichokuwa amekianda,mpaka hapo mwili wake ulidhoofika sana kwa sababu ya njaa.

    Kule kijijini wazazi wa Glory waliamua kuanzisha kilimo,watu wengi waliwacheka na kuwakebehi.

    "Kiko wapi sasa mbona wamerudi"

    "Hahahahaha mama Samu unanichekesha,tangu lini upate hera kwa kujiuza halafu zidumu?

    "Kwahiyo unataka kuniambia yule Glory utajiri wake ulitokana na kujiuza?

    "Kwani hujui kuwa katibuana na bwana wake kafukuzwa kama mbwa?

    "Ahaaa mama Lea nilikuwa sijazipata hizo habari hebu nipe huo ubuyu"

    "Sindo maana wazazi wake wamerudi yeye hajulikani alipo,huenda hata alishapoteza maisha"yalikuwa maneno ya wanawake wawili waliokuwa wamekaa wanaongelea zile habari za Glory hasa baada ya kuona wazazi wake wamerudi kijijini wakiwa hawana hili wala lile.

    Jiji zima la Arusha lilikuwa makini kumtafuta Glory,vijan a walijitosa polini kuanza kumsaka Glory.

    "Million arobaini??hapana lazima nimtafute usiku na mchana ili nimpate"alijisemea kijana mmoja aliyekuwa anaitwa Ali.

    Eneo alilokuwa amelala Glory kulikuwa na kijana mmoja aliyekuwa anapendelea kuchunga mbuzi eneo lile,kijana yule alikuwa anaitwa Mudi,Mudi alikuwa na miaka kumi na saba, maisha yao yalikuwa magumu sana,aliishi na mama yake aliyekuwa hawezi hata kutembea kutokana na kuumwa ugojwa wa kisukari,Mudi alihangaika kupata pesa ya kumtibu mama yake lakini ilishindikana, mifugo waliyokuwa nayo haikutosha kabisa,ilihitajika fedha nyingi sana kwa ajili ya matibabu,mama yake Mudi alikata tamaa baada ya kuona zoezi la kupata pesa limekwenda kombo.Mudi akiwa amechunga mbuzi alimuona Glory akiwa amelala hajiwezi hata kuongea ilikuwa vugumu kwake,kwa wakati huo alikuwa na siku tano hajaweka kitu mdomoni,kwakuwa yule kijana Mudi taarifa ile aliisikia kwa majirani basi aliacha mifugo yake akambeba Glory mpaka nyumbani kwao.

    "Mwanangu huu mzoga unaupeleka wapi"aliuliza mama yake Mudi.

    "Mama huu unaouita mzigo ndo utasababisha wewe upone"aliongea Mudi kwa sauti ya upole.Kwanza kabisa Mudi alichukua uji aliokuwa ameuandaa kwa ajili ya mama yake kisha akaanza kumnywesha Glory,bado Glory hakuwa na nguvu yeyote,baada ya kumaliza zoezi lile alienda kwa jirani yake akamwambia kuwa tayari Glory kamuona, mawasiliano yalifanyika kwa uharaka zaidi,ndani ya mda mfupi gari ya Andrea ilikuwa tayari kumuchukua Glory.

    "Kijana weka mizigo yenu humu ndani ya gari pia mlete na mama yako"aliongea Andrea,moja kwa moja ndege ya kukodi ilikuwa tayari kumpeleka Glory katika hospital kuu ya mhimbili.

    "Kijana mama yako anaumwa ugojwa gani?aliuliza Andrea.

    "Ana kisukari ya mda mrefu"alijibu Andrea.

    "Usijali pesa yako utaipata pia mama yako atapona"aliongea Andrea akimwambia Mudi.

    "Kweli mungu anajibu maombi"alijisemea Mudi wakati huo akiingia ndani ya ndege kwa ajili ya kuwahi jijini Dar es salaam.Mama yake Mudi alizidi kuona kama ndoto.Baada ya kufika jijini Dar es salaam walielekea katika hospital ya mhimbili, madaktari bingwa walikuwa tayari kumtibu Glory na mama yake Mudi.Hadi inafika jioni tayari Glory alikuwa amezinduka na kupata nguvu, aliendelea kuwaza jinsi alivyofika mahari pale,wakati anabebwa kutoka kichakani hakuweza kutambua lolote.

    "Kwanini ulitaka kujiua binti?lilikuwa swali kutoka kwa Daktari aliyekuwa anamtibu Glory.

    "Kwani hapa niko wapi?aliuliza Glory kwa msahangao,baada ya kusoma mashuka aliyokuwa amejifunika aliweza kutambua kuwa alikuwa mhimbili.Yule Daktari hakuongea neno lingine zaidi alimuita Andrea.Glory baada ya kumuona Glory alimkumbuka vyema kuwa alikuwa mmoja wa watu waliomdhulumu utajiri wake.

    "Bado mnanifuatilia?kwanini hamjaniacha nikapoteza maisha nikawaachia dunia yenu hii ya mateso? aliongea Glory huku machozi yakimtoka.

    "Glory tulia Niko hapa lazima nikusaidie urudi katika hali yako"aliongea Andrea.

    "Eti unisaidie unisaidie nini wewe?kwanini hukunisaidia mwanzo kabla sijapata hii aibu?niache nife"aliongea Glory wakati huo akinyanyuka pale alipokuwa amelala na kuchomoa mpira uliokuwa unaingiza maji ndani ya mwili wake.Lakini Andrea alimuwahi kisha akamtuliza,bado Glory alionekana kuwa mbishi,lakini baada ya kutulizwa mda mrefu hatimaye alikuwa mpole.

    "Sema sasa unataka kuniambia nini?yaani nyinyi wanaume nawachukia sana"aliongea Glory huku akiyafuta machozi.

    "Glory tulia basi nikwambie"aliongea Andrea.

    "Haya nakusikiliza"alisema Glory.

    "Hapa nipo kwa ajili ya kukusaidia wewe, utajiri wako utarudi kama awali hivyo ondoa shaka kabisa yule aliyekuwa unajiita mme wako tayari tushamzika"aliongea Andrea.

    "Unasemaje?aliuliza Glory kwa mshangao.

    "Ndio hivyo subiri upate matibabu mengine yatafuatia"aliongea Andrea.Maneno yale machache yaliirudisha imani ya Glory.

    "Sasa huyu lengo lake ni lipi?alijiuliza Glory bila kupata jibu.Matibabu yaliendelea kwa mama yake Mudi.

    "Huyu sio wa kuondoka leo lazima apewe kitanda"aliongea Daktari mmoja akimwambia Andrea.

    "Hilo halina shida kabisa hakikisha mnaandika gharama zote zinazohitajika"alisema Andrea.

    Kesho yake asubuhi kulipambazuka na hali ya mvua katika jiji la Dar es salaam,kwa wakati huo Glory alikuwa tayari amemuamini Andrea,walisubiri mpaka mvua ilipopungua hapo waliaagana na Mudi aliyetakiwa kubaki pale hospital kwa ajili ya kumuangalia mama yake.

    "Sasa kaka unaniacha hapa sina chochote nitaishi vipi na mgojwa?,aliuliza Mudi.

    "Usiwe na hofu kijana gharama nimelipia zote,ukiwa na shida yeyote usikose kunitafuta"aliongea Andrea huku akitoa simu yake na kumpatia Mudi.Walikodi tax iliyowatoa mhimbili mpaka kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere,hapo walichukua ndege iliyopeleka mpaka Kilimanjaro hapo walichukuwa gari iliyowafikisha mpaka pale alipokuwa anaishi Andrea, Bado Glory alionekana kuduwaa.

    "Utajiri wangu wote huu,sasa sijui wazazi wangu wako wapi?alijiuliza Glory.

    "Karibu na utulize kichwa,hapa utaishi kama nyumbani kwako,usihofu kitu chochote,wahenga walisema kuwa ukianguka usiogope kuinuka na kusimama upya,wakati wako sasa kurudisha heshima kwa waliokucheka mda uliokuwa umepata aibu,heshima yako itarudi mda si mrefu"aliongea Andrea huku akinyanyuka na kumuacha Glory aliyebaki mdomo wazi.



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Maisha ya Glory yalianza upya,bado alishinda ndani kukwepa aibu,hakutaka kutembea sana,kama angetaka kutembea basi alikuwa anachukuwa gari yenye vioo vyeusi lengo asijulikane.Walinaza kuanzisha biashara zao kimya kimya akiwa sambamba na Andrea,pesa zote alizokuwa nazo Andrea alimpa Glory aliyehakikisha kwanza anawasiliana na mwanaye na kumtumia pesa nyingine,mwanaye huyo hakufahamu chochote kilichokuwa kinaendelea nchini Tanzania.

    "Sujui wazazi wangu watanipokeaje"aliongea Glory akiwa na Andrea.

    "Hilo usiliwaze,waache kwanza najua wako kijijini,siku ya kwenda kule wajengee nyumba nyumba huko huko,najua hawawezi tena kurudi mjini"aliongea Andrea, Glory alijikuta akivutiawa na ushauru wa Andrea.Kipindi chote hicho kila mtu aliishi kivyake japo walikuwa wanakaa nyumba moja.Siku zilisogea huku taratibu biashara zao zilianza kuua,bado Glory aliendelea kujifungia ndani,hakutaka kujulikana, biashara hizo aliamua kuzisimamia Andrea.

    "Lakini kwa nini nisimuoe kabisa huyu? alijisemea Andrea,moja kwa moja hilo wazo aliliweka kichwani.Jioni ya siku ile alimuita Glory na kumwambia yaliyokuwa moyoni mwake, Glory hakutaka kubisha kila alipokuwa anafikiria Andrea alivyo pambana kwa ajili yake naye alijikuta anainuka na kwenda kumkumbatia Andrea.Maisha yao yalianza Andrea alivyogusia suala la kufungua ndoa Glory alikataa kabisa.

    "Labda tufunge ndoa ya kimya kimya asijue mtu"lilikuwa jibu kutoka kwa Glory.Andrea hakuaka kumlazimisha sana hivyo waliitwa mapadrina ndoa yao ikawa imemalizia ndani.Wote walifurahi hivyo waliyaanza maisha upya.

    "Bado nawaza ili kurudisha heshima yangu nifanyeje ili watu waniheshimu tena"alisema Glory akiwa na Andrea.

    "Subiri kuna gari aina ya BENZI tukinunua hiyo nadhani kidogo heshima itarudi waliokuwa wanakucheka wakuheshimu tena"aliongea Andrea.

    Glory alifurahi sana,moja kwa moja mawasiliano yalifanyika mpaka nchini Ujerumani,gari aliyokuwa anaitaka Glory aliipata.

    "Sasa mme wangu hii gari tuandike maneno gani?aliuliza Glory.

    "Bado nafikiria lakini andika kuwa UKIANGUKA USIOGOPE KUINUKA TENA,hayo ndo maneno yatakayowachoma waliokuwa wanakucheka"aliongea Andrea.

    Katikati ya jiji la Arusha ndo kulikuwa na maongamano wa watu wengi sana,wengi wao walikuwa bize na shughuli zao,hapo ndipo alipanga Glory asimame ili watu waanze kumpa heshima kama zamani.Kwa wakati huo hakuna aliyefikiria tena habari za Glory.Gari la Glory lilipunguza mwendo,kila mtu aliacha kazi aliyokuwa anaifanya akageuza shingo kuliangalia,mara alishuka Glory kwa mbwembwe kabisa kila mtu alimshangaa,wengi wao walijua kuwa kwa wakati huo labda atakuwa ameshapoteza maisha tayari.

    "Habari zenu?alisalimia Glory huku akielekea kwenye duka kununua maji,ndivyo alivyokuwa anafanya kila sehemu aliyokuwa anapita akiona msongamano anasimamaisha gari,kwa siku moja jina lake lilirudi.

    "Hapa tumepata somo,wengi wanafeli kwa kuogopa kuinuka tena,nadhani mfano mzuri upo kwa huyu mwanamke"

    "Hilo ni kweli,watu wamemsema sana"

    "Kumbe kukaa kimya nayo ni faida pia huwezi kujua amekuaja amejipanga vipi"

    "Aseee vijana tufanye kazi"yalikuwa maneno ya madereva boda boda waliokuwa kijiweni,kila mtu alionekana kuongea lake hasa baada ya kumuona Glory.

    Safari ya Glory iliishia kwenye baadhi ya maduka yake,watu walizidi kumshangaa kila mtu aligeuza shingo yake kuiangalia gari ya Glory.

    "Ama kweli ng'ombe hazeeki maini"alijisemea kijana mmoja.

    Peter mwanaume aliyembebesha mimba Glory alikuwa anafanya kwenye mgodi wa melalani,kila mda habari za Glory aliendelea kuzisikia,ilifikia hatua akatamani kuonana uso kwa uso na Glory lakini bado alikuwa na aibu,hakujua Glory atamuelewa vipi lakini aliendelea kusubiri na kujipa moyo kuwa ipo siku atakutanana na Glory.

    "Najua hasira zake zilishaisha"alijisemea Peter,alijua kuwa mwanamke ni mtu ambaye hana hasira kwa mwanaume.

    "Hawa wanawake wakishapenda wanapenda kweli tofauti na sisi wanaume"alijisemea Peter.Siku zilisogea, Glory alikuwa na Andrea mda mwingi wakipangilia biasahara zao.

    "Mme wangu naona kama huu utajiri hautoshi yaani nataka zaidi ya hapa"aliongea Glory.

    "Usiwe na haraka mambo mazuri huwa hayataki haraka"alijibu Andrea.Maisha yao yaliogea,ilifikia hatua Andrea akatamani kumuona Glory akipata mimba lakini mawazo yake yalizidi kwenda kombo,Hadi inapita miezi mitatu Glory alikuwa bado hajapata ujauzito.

    Licha ya Glory kukubali kuwa na Andrea kimapenzi bado alizidi kumuwaza Issa,alijua mda wowote Issa anaweza kurejea tena na akimkuta na mtoto mwingibe.

    "Hilo kwangu haliwezekani,Issa ni mwanaume aliyenisaidia sana tofauti na hawa wengine hivyo naamini siku moja naweza kurejea na tukayaendeleza mapenzi yetu"alijisemea Glory.Hivyo mda mwingi alikuwa anatumia sindano na vidonge vya kuzuia mimba.

    Andrea aliendelea kuvumilia lakini kila siku alitamani kumuuliza Glory lakini moyo wake ulikuwa mzito juu ya hilo.

    "Au tatizo liko kwangu?lakini hapana lazima nikapime kwanza kabla sijamuuliza"alijisemea Andrea,moja kwa moja alisafiri mpaka mhimbili hapo alifanya vipimo na kukutwa hana tatizo lolote.

    "Sasa hizi mali zitatusaidia nini kama sitakuwa na mtoto?alijuliza Andrea bila kupata jibu alifika jijj Arusha huku akiwaza kutafuta mwanamke wa nje ili azae naye.

    "Mimi mwanaume lijali hivyo siwezi kumvumilia huyu sijui alipewa mtoto mmoja tu"alijisemea Andrea.

    Kule hospital ya mhimbili afya ya mama yake Mudi ilizidi kuimarika vyema,hakuacha kupiga magoti na kumshukuru mungu kwa msaada alioupata.

    "Kweli unapokaribia kukata tamaa ndo mungu hutuma majibu yake"alijisemea mama yake Mudi.

    Kama kawaida ya migodi mbali mbali kutoa madini kwa wakati ambao haujurikani ndicho kilichotokea kwenye ule mgodi wa melelani,watu wengi walikuwa wakisaka dhahabu,mkusanyiko wa watu uliongezeka sana.

    Peter akiwa miongoni aliendelea na uchimbaji huku akili yake ikiwa kwa Glory.Hakuwa na aibu tena kuwa alimkimbia.

    "Nitamdanganya kuwa nilienda kutafuta,lazima akubali"alijisemea Peter.

    Huku kwa Glory na mme wake Andrea uelewano ulianza kupungua taratibu,na hii ni kutokana na Andrea kuhitaji mtoto lakini akahisi kuwa Glory hana uwezo wa kuzaa tena licha ya kuwa alimzaa mtoto mmoja,hivyo alipunguza uaminifu baada ya kupata mwanamke aliyekuwa amechika kwa mme wake hivyo alianza kumgharamia huyo ili amzalie mtoto.Glory hilo jambo aliweza kuligundua mapema lakini hakutaka kuonyesha tofauti yeyote.

    "Mme wangu kwa nini siku hizi umebadirika?hujui kuwa unayoyafanya nayajua yote?aliuliza Glory.

    "Niko sawa ila nilikuwa naomba kuuliza kuwa kwanini hushiki mimba au una tatizo lolote?aliuliza Andrea.

    "Sina tatizo mme wangu ila najua mwenyezi mungu hajapanga hicho kitu hivyo ukae ukijua kuwa hii ni mipango ya mungu"aliongea Glory huku akitoa machozi.

    "Sawa ngoja tuendelee kumsubiri huyo mungu"alijibu Andrea kwa jeuri huku moyoni akiamini kuwa tayari anaye mtu wa kumzalia mtoto.

    "Sawa mme wangu lakini nilikuwa nataka kukwambia kuwa sahivi mgodi wa mererani unatoa sana Tanzanite kwa nini tusianze kununua? aliongea Glory.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa hilo halina shida kesho twende tukaangalie utaratibu ukoje"alijibu Andrea.

    Kesho yake asubuhi na mapema Glory akiwa na mme wake walichukuwa gari iliyofikisha mpaka mgodini,waliweza kuona jinsi watu walivyo wengi.

    "Sasa mme wangu hapa tunaanzia wapi?aliuliza Glory.

    "Ngoja nizunguke upande wa pili nikaangalie"alisema Andrea huku akishuka ndani ya gari na kumuacha Glory.Glory akiwa ndani ya gari kupitia kwenye kioo cha gari cha mbele alimuona Peter, Glory alishtuka na kushika mdomo kwa mshangao.





    "Mungu wangu!kumbe Peter yuko huku?sasa kwa nini alinikimbia?hapana siwezi hata kumsalimia"alijisemea Glory huku akiwa makini kumtazama Peter aliyekuwa hana habari.

    "Au nimsalimie?alijiuliza Glory lakini moyo wake ulikataa,kila alipokuwa anayakumbuka mateso aliyoyapata baada ya Peter kumkimbia alijikuta akipatwa na hasira ya ghafla.

    "Huyu hakuwa na upendo wa dhati hata kidogo"alijisemea Glory.

    Mda kidogo alirejea Andrea kisha wakaendelea na mpango wao wa kununua Tanzanite,hiyo ndo ikawa biashara yao hasa baada ya kuona ina faida kubwa.

    Kadri siku zilivyokuwa zinasogea ndivyo Peter alizidi kumuwaza Glory.

    "Lakini lazima nitafute pesa kwanza,nikimwendea hivi hivi hawezi kunielewa"alijisemea Peter.Hapo alizidisha bidii katika utafutaji.

    Ilikuwa siku ya juma ya tano,siku hiyo Glory alikwenda peke yake pale mgodini,kwa wakati huo Andrea alikuwa amekwenda mhimbili kumuona mama yake Mudi.

    Glory alishuka kwenye gari na kuzipiga hatua kusogea pale walikokuwa wanaoshea Tanzanite,lakini kabla hata hajafika mbali alisikia sauti ikimuita.

    "Glory"ilikuwa sauti kutoka nyuma yake.Glory aligeuka kwa haraka macho yake yalikutana na Peter, Glory alihamaki.

    "Waoooh mpenzi wangu"aliongea Peter kwa tabasamu lakini alishangaa kumuona Glory akiwa amenuna.

    "Nani mpenzi wako? aliongea Glory kwa hasira.

    "Wewe hapo Glory nikupendaye kutoka uvunguni mwa moyo wangu"aliongea Peter.

    "Hahaha eti mpenzi wako!nani mpenzi wako?mwanaume mzima huna haya"aliongea Glory.

    "Lakini kwa nini unaanza kunihukumu mpenzi wangu kabla hujaniuliza yaliyonikuta? aliongea Peter.

    "Siwezi kusikiliza chochote kutoka kwako,kwanini ulinikimbia?

    "Sijakukimbia,nami sikutegemea kuwa watakufukuza nyumbani kwenu"

    "Unaongea nini wewe?mbona sikuelewi?aliuliza Glory.

    "Baada ya kuona kuwa wewe ni mjamzito niliamua kuondoka nikaja hapa lengo nitafute pesa ili mwanagu pamoja na wewe muishi kwa raha"aliongea Peter.

    "Kwanini hukuniaga?

    "Sikutaka kukuaga kwa kuwa nilijua huwezi kukubali hivyo naomba upunguze hasira mpenzi wangu"

    "Na kwanini ndani ya kipindi hicho hukunitafuta?

    "Nilikutafuta sana,mpaka nikaenda kijijini huko niliambiwa kuwa umefukuzwa,bado sikujua ulielekea wapi,ndipo nikapata taarifa kuwa wewe unaishi hapa ila tayari una pesa nyingi hivyo nikakoswa jinsi ya kukuingia"aliongea Peter kwa hisia Kali.

    Glory alikaa kimya kwa mda akionekana kutafakari kitu.

    "Sawa lakini bado una makosa sana Peter,ulitakiwa kuniambia kuwa wewe unaenda"

    "Hilo ni kosa langu nalielewa mpenzi naomba upunguze hasira bado natamani kumuona mwanangu ambaye mpaka sasa sijui aliko"

    "Mtoto wako yupo Uingereza kimasomo,jina nilimpa jina la bahati"

    "Sawa mpenzi wangu ngoja nisikuchoshe,ukipunguza hasira zako naomba unitafute kwa hizo namba"aliongea Peter huku akitaja namba ambazo Glory akiziandika kwenye simu yake.

    "Kwa heri mpenzi pia msalimie mwanangu mwambie natamani kumuona"aliongea Peter huku akizipiga hatua kuondoka,lakini kabla hajafika mbali Glory alimuita.

    "Peter naomba urudi"aliongea Glory.

    "Nambie mpenzi wangu"aliongea Peter.

    "Mimi tayari naishi na mwanaume na ndo yule aliyesababisha mimi kurudi kwenye hii hali ya utajiri baada ya kufirisiwa,je tutaishije?

    "Hilo lisikupe shida kabisa,nalitambua hivyo hiyo haina shida mimi siwezi kuwa na wivu juu ya hilo"aliongea Peter.

    "Sawa sasa unaishi wapi nanani?aliuliza Glory.

    "Nina gheto langu ndo naishi hapo,kama vipi twende ukapaone"aliongea Peter.Glory alikaa kimya akionekana kutafakari sana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa twende,ingia ndani ya gari"Peter baada ya kuingia ndani ya gari Safari yao ilianza,haikuwa ndefu sana,ndani ya dakika kumi na tano walikuwa tayari wamefika pale alipokuwa anaishi Peter.

    "Karibu mpenzi mimi huwa naishi hapa"aliongea Peter.

    "Nashukuru kupafahamu,panaonekana pametulia sana"aliongea Glory huku akizungusha shingo yake kukiangalia kile chumba,maongezi ya hapa na pale yaliendelea.

    "Mpenzi nimekusaheme kwa moyo mmoja,hivyo basi njoo tukumbushie"aliongea Glory.Bila kuchelewa walijikuta wakifurahi,ndani ya dakika arobaini kila mtu alikuwa anatabasamu.

    "Mpenzi wangu nataka wiki ijayo mwanao aje ili akuone"aliongea Glory.Basi baada ya maongezi ya mda mrefu hatimaye waliagana kisha Glory akaondoka.Mapenzi yao yalianza upya sana,mda mwingi Glory alikuwa na Peter.

    "Kweli wanawake hawana hasira yaani nilitegemea kuwa labda ataleta ubishi lakini ndo kwanza upendo wake naanza kuuona upya"alijisemea Peter akiwa na Glory.Baada ya miezi mitatu Glory aliona kama vile mme wake huyo Andrea anamnyima raha ya kufurahi na Peter.

    "Yaani namchukia huyu mwanaume,kila dakika emenuna ndani ya nyumba hakuana amani hata kidogo"alisema Glory akiwa kifuani kwa Peter.

    "Sasa tufanyeje mpenzi wangu?aliuliza Peter.

    "Nilikuwa na wazo moja kama utakuwa tayari"aliongea Glory.

    "Wazo gani hilo,sema mimi Niko tayari"

    "Nataka tumuue huyu mwanaume ili tuweze kuishi kwa amani na furaha"aliongea Glory,hakufikiria tena msaada wa Andrea alivyo msaidia hadi akainuka tena.

    "Hilo hata mimi nilikuwa nalifikiria kwa mda mrefu,sawa mimi niko tayari"aliongea Peter,wote walikubaliana kumuua Andrea.Sumu ya panya iliandaliwa mara moja.Siku hiyo Glory alirudi nyumbani na kumkuta Peter akiwa anaongea na mtu wake yule wa nje.

    "Una mimba?asee nafurahi kusikia kwa sababu huyu kinyago ndani hataki kushika mimba nadhani alipangiwa mtoto mmoja"yalikuwa maongezi ya Peter aliyokuwa anaongea na mke wa nje yote Glory aliyasikia.

    "Mimi kinyago?yaani umefikia hatua hiyo?hata hivyo leo ndo mwisho wako"alijisemea Glory,huku akirudi nje hakutaka kuyaangilia yale maongezi alihisi ataharibu mpango wake.Baada ya kuhisi kuwa amemaliza kuongea aliingia ndani hakuonyesha kukasirika,kutokana na kutokuwa na wafanyakazi wa ndani hivyo aliaandaa chakula yeye mwenyewe,kile chakula alikitia ile sumu,maandalizi yalipokamilika alimkaribisha Andrea,kila mtu alikuwa anakula na sahani yake mkononi,hazikupita dakika tatu tayari Andrea aliiachia ile sahani ya chakula kisha mapovu yakaanza kumtoka dakika tano mbele Andrea alikaaga dunia.

    "Malipo ni hapa hapa duniani japo uliwauwa wenzio japo ulifanya haya kwa ajili yangu lakini unaenda kukutana nao"aliongea Glory,msaada alipewa na Andrea hakuukumbuka tena.Aliwasiliana na watu waliokuja wakauchua mwili wa Andrea kisha wakaenda kuuzika polini.

    Hapo Glory alianza kuishi na Peter,waliishi kwa furaha sana.

    Huko China Issa baada ya kukaa mda mrefu hajafuatiliia habari za Glory siku ile aliamua kufungua simu yake,moyo wake ulikumbwa na mshangao baada ya kuona taarifa ikimuonyesha Glory kuwa kafirisika kila kitu,hakutaka kuaendelea tena kuaangalia ile taarifa hakujua kuwa kwa wakati huo Glory alikuwa tajiri tena.

    "Nini?yaani mwanaume aliyemuoa kamgeuka tena?hapana hapa lazima niende nchini Tanzania,siwezi kukubali"alijisemea Issa kwa hasira,moja kwa moja alianza maandalizi ya haraka sana.

    "Najua bado atanipenda tu ngoja nimsaidie Tena juu ya hili"alijisemea Issa.

    Alikumbuka kuwa hakuwa na VIZA vya kusafiria lakini alichoamua ni kukodi ndege binafsi.Ilikuwa pesa nyingi ya kukodi ndege kutoka China mpaka Tanzania lakini yeye hakuhofu kwa kuwa pesa alikuwa nayo ya kutosha.

    "I will going to kill him"(Nakwenda kumuua huyu) alijisemea Issa akiwa tayari yuko ndani ya ndege.Taratibu ndege ilianza kuiacha ardhi ya China.





    Issa akiwa ndani ya ndege alitamani ndege iongeze mwendo zaidi ili awahi kufika nchini Tanzania,bado hakutaka tena kuifungua simu yake ambayo alimini kuwa itamuongezea hasira,moyo wake ulizidi kwenda kasi

    Huku Glory na Peter walianzisha maisha upya,bado watu walizidi kujiuliza kuwa Andrea kaenda wapi hasa baada ya kumuona Glory ana mtu mwingine mpya,lakini hakuna aliyedhubutu kumwambia Glory kutokan na kuwa siliasi mda mwingi.

    "Sasa mwanangu nitamuona lini?aliuliza Peter.

    "Nadhani wiki ijayo atakuja ila sina uhakika kama atakuwa bado anafahamu kiswahili,anza kujifunza kingereza mme wangu"aliongea Glory kwa utani kidogo.

    "Sasa wewe mke wangu kingereza unakijua?aliuliza Peter.

    "Oooh mimi sio mwenzako kabisa"alijibu Glory,basi utani wa hapa na pale uliendelea.Glory aliacha kabisa kutumia zile sindano za kuzuia mimba pamoja na vile vidonge,hakuvitumia tena,lakini bado alikuwa hajapata ujauzito,ndipo siku hiyo hiyo aliamua kwenda kupima,majibu aliyopewa ni kwamba kizazi chake kimeharibika kutokana na kutumia sana madawa ya kuzuia mimba,alijikuta akiangua kilio lakini alikumbuka kuwa tayari anaye mtoto mmoja hivyo ndo atakuwa furaha yake.

    "Lazima nihakikishe Bahati wangu anapata elimu iliyo bora"alijisemea Glory huku akiondoka pale hospital.Moja kwa moja alifanya mawasiliano huko nchini Uingereza na kumwambia mwanaye aombe ruhusa ili aje nchini Tanzania amuone baba yake.Bahati alifurahi kwani kwa wakati huo alikuwa bado hajahawahi kumuona, Glory alirudi nyumbani akionekana kutokuwa na furaha kabisa.

    "Nini shida mpenzi wangu mbona hauko sawa?aliuliza Peter.

    "Hapana mme wangu ila nahisi kichwa kuuma"

    "Pole mpenzi najua ni mizunguko ya hapa na pale hivyo tumia dawa"

    "Sawa mpenzi,ila mwanao anakuja wiki ijayo"

    "Waooh ntafurahi sasa sijui analinganaje"

    "Subiri utamuona"Basi maongezi yao yaliendelea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hatimaye kule hospital Mama yake Mudi aliruhusiwa,kila kitu alilipia Glory,hivyo Mudi na mama yake walianza kuishi nyumbani kwa Glory.

    Issa kwa wakati huo ndo alikuwa anafika kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere,hakutaka kusimama hapo moja kwa moja mpaka uwanja wa ndege wa KIA Kilimanjaro,baada ya kutoka hapo alikodi tax iliyomfikisha mpaka pale alipokuwa anaishi na Glory kipindi cha nyuma.

    "Glory alihama hapa sahivi anaishi hapo mtaa wa pili kwenye nyumba utakayoiona ya kifahari sana ndo nyumbani kwake"aliongea mpangaji mmoja,hapo Issa alitoa fedha kadhaa akamkabidhi yule mpangani kama shukurani.Alipanda tena tax.

    "Samahani broo, hivi unamuulizia nani?ilikuwa sauti ya dereva tax.

    "Mwanamke mmoja anaitwa Glory"alijibu Issa.

    "Glory yule tajiri?

    "Ndio huyo huyo"

    "Sahivi anaishi na na mme wake"

    "Sawa we twende tu"macho ya Issa yaligota kwenye mjengo wa kifahari sana.

    "Sasa mbona wanasema kuwa amefirisika?alijiuliza Issa.

    "Broo ni hapa hapa"alijibu yule dareva tax,baada ya kupewa ujira wake aliondoka akamuacha Issa akiwa amesimama nje ya jumba hilo.

    Issa aliamua kubisha mlango wa mbele.Glory na mme wake wakiwa sebuleni wanapata chakula walisikia mtu akigonga mlango.

    "Ninani huyo mbona sio kawaida"aliuliza Peter.

    "Subiri nikamfungulie"alijibu Glory huku akiinuka na kwenda kuufungua mlango.

    "Laahahula!!!alitaharuki Glory baada ya kumuona Issa,alijikuta akipiga magoti chini huku akitoa machozi.

    "Naomba unisamehe kwa kukutendea haya,kiukweli nimepitia mengi sana tangu tutengane,hata sikutegemea kama utarudi kwa mda huu,nilijua kuwa wewe ni kama vijana wengine wanaoenda nchi za nje na kulowea huko"aliongea Glory.Kwa wakati huo Issa alikuwa kimya hajaongea neno lolote.

    "Hilo nililijua mapema hivyo nimekuja hapa nikiwa sina kinyongo kabisa,nikaribishe ndani basi"aliongea Issa.Hapo Glory alizidisha kilio.

    "Sasa mbona unalia nimekwa..."hakumalizia sentensi Issa macho yake yaligongana na ya Peter.

    "Glory ninani huyu"aliuliza Issa kwa mshangao.

    "Nikuulize wewe nani kwa sababu umekuja nyumbani kwangu"aliongea Peter kwa sauti kibabe.

    "Mimi ni mpenzi wake na huyu"aliongea Issa huku taratibu machozi yakianza kumlenga.

    "We kama ni mpenzi wake basi mimi ni mme wake"alijibu Peter.

    "Mama Bahati huyu ninani?aliuliza Peter.

    "Huyu ndo yule aliweza kunisaidia kipindi nataka kujifungia"alijibu Glory.

    "Ohoo,hongera kwa kutoa msaada kaka lakini huyu tayari ni mke wangu"aliongea Peter.

    "Kweli ndo huyu mwenye mtoto"alijibu Glory.Hapo Issa alikumbuka maneno ya marafiki zake kuwa ukilea mtoto ambaye sio wako baba mtoto akija atamuchua na wewe utabaki kushika kichwa"yote aliyawaza Issa na kujikuta akidondosha chozi.

    "Sawa Glory nashukuru kwa malipo haya lakini mimi nilikupenda jinsi ulivyokuwa,haikutosha nikaenda mbali nakumpenda mtoto ambaye nilijua kuwa sio damu yangu lakini leo hii malipo yake ndo haya?Kama alikuwa anakupenda kwa dhati kwa nini alikukimbia baada ya kukubesha mimba?ila siwezi kulipiza juu ya hili,kwa heri na watakia maisha mema"aliongea Issa huku akigeuka na kuondoka, Glory alijiona mkosaji lakini hakuwa na jinsi,safari ya Issa iliishia uwanja wa ndege.

    "Siwezi kuendelea kubaki hapa nitazidi kuumia"alijisemea Issa wakati huo akipanda ndege kurudi zake China.

    Glory na Peter walienda mpaka kijijini kwa wazazi wake Glory aliwakuta wakiwa wameshachakaa kutokana na kulima sana, Glory aliwaomba msamaha wakamsamehee.

    "Sasa Baba na Mama jiandae twende mjini"aliongea Glory.

    "Hapana mwanangu hatuwezi kurudi tena huko aibu tuliyoipata inatosha"aliongea Mama yake Glory.Basi Glory alianza taratibu za kuwajengea nyumba baada ya kukataa kurudi mjini.

    Hatimaye wiki moja ilitimia Bahati alirejea kutoka nchini Uingereza.Ilikuwa ni furaha kwa Peter ambaye alikuwa hajawahi kumuona mwanaye.

    "Baba na mwana hao kwenye ubora wenu"aliongea Glory kwa utani.

    "Mme wangu kuna kitu natamani kukwambia ila nahisi kama utachukia"aliongea Glory.

    "Kitu gani hicho?wewe niambie tu usiwe na hofu"aliongea Peter.

    Ghafla Glory alianza kudondosha machozi,Peter alishangaa hali ile.

    "Mama Bahati nini tatizo"

    "Mme wangu mi sahivi siwezi tena kupata mimba"aliongea Glory kwa sauti ya kwiki.

    "Kwanini unasema hivyo mama Bahati?

    "Hapo zamani nilikuwa natumia dawa za kuzuia mimba kumbe zimeharibu kizazi changu"aliongea Glory.

    "Pole sana usijali kwa hilo hiyo ni mipango ya mungu hivyo kuwa na amani"aliongea Peter.

    Hapo Glory alionyesha tabasamu,wote walifurahi,likizo iliisha Bahati alirudi nchini Uingereza kuendelea na masomo.

    Kule kijijini kwa wazazi wa Glory nyumba ya kisasa ilikuwa tayari inajengwa,hivyo baada ya miezi mitatu ilikamilika,ilikuwa nyumba ya iliyovutia sana,watu kujijini walijuliza maswali mengi.Wengi wao walijua kuwa kwa wakati huo Glory alikuwa hana tena utajiri hasa baada ya kuona wazazi wake waliokuwa mjini wapo Kijijini.

    Huko China Issa aliendelea na kazi yake,hakutaka tena kurejea nchini Tanzania hivyo makazi yake yalikuwa kule.

    "Ili kumsahau Glory lazima nitafute mke nioe"alijisemea Issa,moja kwa moja mpango wake ulianza hapo alipata binti mmoja raia wa Zimbabwe ila alikuwa huko China hivyo walifunga ndoa,waliishi kwa furaha.

    Baada ya miaka mitano utajiri wa Glory na mme wake Peter ulizidi kukua,walijenga kiwanda cha mafuta ya kula mkoani Singida huko waliweza kupata pesa nyingi hivyo walizidi kuukuza utajiri wao wakiwa sambamba na mtoto wao Bahati aliyekuwa nchini Uingereza.Hawakubahatika kupata mtoto mwingine hivyo Bahati ndo alikuwa mtoto wao pekee.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mme wangu hivi kama ningeliitoa hii mimba inamaana nisingelipata mtoto mwingine,kweli mungu mkubwa"aliongea Glory.

    "Wengi wakikosa kizazi wanalalamika kumbe unakuta kizazi walipewa lakini wakakichezea kwa kutoa mimba,nakupongeza kwa hilo mke wangu"aliongea Peter,Maisha hao yalizidi kuwa ya furaha zaidi.



    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog