Simulizi : Kazi Za Ndani Nchini Oman Zilivyonikutanisha Na Kifo
Sehemu Ya Tatu (3)
Hussein Jabal na Zakia mke wa Abdallah Mustapha walikuwa uchi wa mnyama kitandani.
Niliduwaa mbele yao, macho yalinitoka pima. Mikono yangu ilifunika mdomo wangu uliokuwa wazi kwa mshangao!
Wao pia, walipatwa na taharuki, wakakurupuka kitandani na kunyakua nguo zilizokuwa kando na kujiziba. Tukatizamana bila yeyote kati yetu kusema kitu. Ilikuwa ni picha mbaya kwenye macho yangu.
“Unaona sasa. Haya yote nilikueleza.” Hussein aliongea kibwege akiwa na wasiwasi usoni. Zakia hakutia neno zaidi ya kuanza kuvaa nguo zake upesi upesi.
“We mbwa umetoka chumbani kwako kuja kunifumania humu chumbani?” Zakia alisema, safari hii macho yake hayakuwa na wasiwasi tena, yakawa ni macho yenye chuki na hasira dhidi yangu.
Nakuuliza wewe Malaya mweusi....” alisema. Na pale pale alinichapa kibao ambacho hakikunifanya niyumbe wala kupepesa macho.
Nilikosa cha kumjibu yule mke wa bosi wangu, nikabaki nimeganda kama sanamu huku moyo wangu ukiteketea kwa dhuruma ile.
Yanii nidhulumiwe penzi langu na mitusi nitukanwe na makofi nipigwa!! Niliwaza kimoyomoyo nafsi yangu ikizidi kukaangika kwa maumivu.
“Hussein, why this black bitch come in here ?” Zakia alimuuliza Hussein kwa ghadhabu, kwamba kwa nini mimi Kahaba mweusi niko pale.
“Kahaba ni wewe Kisonoko wa Kiarabu.” nilisema huku nikimwangalia Zakia kwa jicho la chuki.
Alinitandika kibao kingine. Nilipepesuka na kuhisi shavu likifukuta kwa joto kali la maumivu, lakini safari hii na mimi sikukubali, kwa wepesi wa ajabu nilimrukia nikampiga kibao cha uso kilicho mpeleka chini, sura yake ikawa imejaa mshangao wa kutotegemea jambo lile.
Akanitizama kwa ghadhabu na kunifuta kwa hasira huku akiunguruma kama paka vidole amechanua tayari kwa kuniparua kwa makucha. Ndani ya sekunde zilezile mlango wa chumba kile ulisukumwa, bila kutegemea mumewe aliingia.
Tukabaki tumeduwaa, ndani ya nukta chache sana. Akili ya Zakia alifanya kazi mithili ya kompyuta, hapohapo alimkimbilia mahali aliposimama mumewe Abdallah Mustapha na kumkumbatia kifani, akaongea kwa mideko:http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“These two people want to kill me just because I found them sexing” alisema kwa Kingereza chepesi kwamba tunataka kumua kisa ametukuta tikifanya mapenzi.
Lilikuwa ni shambulio la moja kwa moja kwa upande wangu, na ikawa zamu yangu kutaharuki.
“What!.” Abdallah alihamaki. Akatutizama mimi na Hussein kwa zamu, macho yake yakiwa na hasira. Ghafla alinirukia na kunipiga ngumi ya uso, nikaanguka chini huku damu zikinitoka puani. Akamvaa Hussein na kumpiga mateke ya tumboni.
“Mnazini ndani ya mji wangu, kama haitoshi mnataka kuondoa uhai wa mke wangu!!!..” alisema kwa ukali ndita zilizojichora kama mkeka wa kizaramo zilionekana.
“Watu weusi mnataka kuua mtu mweupe..! tena kwenye ardhi ya nchi yake..!Hii ni kali kuliko zote nilizowahi kuziona!” jitu hilo la Kiarabu liliunguruma.
Mefanya makosa makubwa sana, hili ni taifa la Warabu, siyo Afrika... huko kwa wapumbavu...” alisita, akaacha kumpiga Hussein, akatutizama kwa zamu kisha akasema tena:
“Jiwekeni tayari kunyongwa hadhalani washenzi weusi ninyi,” sauti yake ilikuwa ya kunong’ona lakini yenye kutisha.
Walitoka mule ndani kisha wakatufungia mlango kwa nje na kutia kufuli.
“Get ready for wriggle! Black bitch” Akiwa nje ya chumba walichotufungia alirudia rudia kusema hayo maneno kwa msisitizo, akiwa na maana kwamba tuwe tayari kufa.
“Ulijuaje kuwa hawa washenzi wako huku wakifanya huu ujinga?” nilisikia Abdallah akimuliza mkewe.
“Niliona dalili za mahusiano tangu zamani, ndipo nilipoanza uchunguzi wa siri.”
“Lazima tuwasiliane na polisi na kuwaeleza juu ya haya ili watu hawa wapewe adhabu ya kifo.”
“Lini?”
“Sasa hivi.”
Nilisikia mazungumzo hayo yaliyozungumzwa kwa sauti kubwa, kila neno nililisikia vizuri kabisa.
Muda mfupi badae nilimsikia tena Abdallah akiwasiliana na polisi na kuwaeleza kisanga chote kilichotokea pale nyumbani kwakwe.
“Ndio...Wamo ndani.......hawawezi....kutoroka....Tanzania na Somalia” Abdallah aliendelea kutoa maelezo kwa polisi, kisha nikasikia akiwamiza polisi kufika ndani ya dakika ishirini.
Niliketi chini, donge zito likinikaba kooni, machozi yalinitoka, nilijiona ni kimbe niliyedhulumiwa haki yangu kwa kiwango kikubwa, kwa wakati huo sikuwaza madhala yanayoweza kutokea kutokana na lile tukio, lililokuwa akilini mwangu ni MAPENZI.
“Alinilazimisha....” hatimaye Hussein alisema kwa sauti ya upole akiniangali kwa macho ya upole.
“Nini!”
“...alinilazimisha kufanya mapenzi...” alisema tena huku akinitizama kwa huruma.
“Unafikiri naweza kuwa hayawani wa kiwango hicho? tangu lini mwanaume akalazimishwa kufanya mapenzi na mwanamke! tafuta uongo mwingine wa kuniongopea siyo huo”
“Haki ya Mungu nakuapia, Zakia amekuwa akinitaka kimapenzi kwa siku nyingi sana na nimekuwa nikitishiwa kwa mambo mengi, najua ni ngumu kunielewa, muhimu kwa sasa tufanye mpango wa kujinasua kwenye hili songombingo kwani nijuavyo sheria za nchi hii, kesho asubuhi tutanyongwa hadhalani kwa makosa ya uzinifu na kutaka kuua.”
Kauli ile ndiyo iliyozindua ufahamu wangu na kuelewa hatari iliyokuwa inaninyemelea. Wivu uliokuwa umegubika nafsi yangu uliyeyuka kama bonge la balafu kwenye jua, hofu ikachukua nafasi.
“Hussein umeniponza, ona maisha yangu ulivyoyaingiza matatani...”
“Hayo tutayaongea badaye, muhimu kwa sasa ni kuhakikisha tunatoweka eneo hili”
Huko nje tuliendelea kuwasikia Zakia na mumewe wakiendelea kutujadili kwa namna kifo chetu kitakavyokuwa funzo kwa watu wengine hususani wafrika waliko nchini Oman.
Dakika chache nilisikia ngurumo za magari ambayo haikuhitaji kuuliza ni magari ya nani, upesi nilifahamu yalikuwa ni magari ya polisi.
“Wako wapi?” nilisikia sauti ikisema huko nje.
“Tumewafungia chumba hiki” Abdallah alijibu, mlango wa chumba ulifunguliwa askari kama saba wenye bunduki wakaingia mule ndani.
Hatukuulizwa chochote na wale askari zaidi ya kupigwa, tulipigwa na kupigwa tukapigika kweli kweli.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila sehemu ya mwili wangu kulikuwa na maumivu. Sikuweza kusimama kwani nilikuwa na maumivu makali.
“Wasilianeni na ndugu zao waliopo huku kwa ajili ya kuja kuchukua maiti zao.” Askari mmoja aliyeonekana kama kiongozi wao alisema.
Tuliondolewa mule ndani tukiwa tumefungwa pingu mikononi, tukapandishwa kwenye gari la polisi, safari ya kuelekea mahali ambapo sikupaelewa ikaanza, muda wote nilikuwa nikilia kwa uchungu, maisha yangu yalikuwa yamebadilika ghafla mno.
“Nisamehe Agripina” Hussein alisema, akionekana kukata tamaa. Aliongea hayo tukiwa ndani ya ‘defender’ la polisi
“Najua hadi kesho, muda kama huu, miili yetu itakuwa mochwari ndani ya friji lenye baridi kali, ikingojea kuzikwa kwenye makaburi mawili tofauti. Nataka moyo wako ufahamu kuwa sikukusudia safari ya mahusiano yetu iwe hivi.
Ndoto zangu za kukupeleka Mogadishu zimegonga mwamba. Naumizwa na hilo Agripina, lakini naumizwa zaidi na mtoto aliye tumboni mwako” alisema huku akinionyesha kipimo changu cha mimba alichokuwa amekimata mkononi, machozi yakijikusanya machoni mwake.
Sikujibu chochote, zaidi ya kutiririkwa na machozi, polisi walikuwa wametuweka kati huku mitutu ya bunduki ikitutizama kwa uchu.
Tulipelekwa hadi kwenye eneo moja lenye uwazi mkubwa, kukiwa na majengo yaliyokuwa kama mabweni, ukingoni mwa eneo hilo kukizungushiwa ukuta mrefu wenye mitambo yenye shoti za umeme.
“Teremka” tuliamriwa.
Taswira ya kunyongwa ikawa inanitesa akilini, kwakweli niliogopa sana, tukiwa kwenye lile eneo ambalo badae nilifahamu kuwa ilikuwa gereza.
Tuliingizwa kwenye ofisi ndogo tuliyo andikisha majina yetu na kuandikiwa makosa mawili yanayotukabili, kwa maana ya kufanya mapenzi kabla ya ndoa, sanjari na kujaribu kuua.
Baada ya hapo, Hussein alichukuliwa na kupelekwa eneo ambalo sikujua ni wapi. Nilitolewa mule kwenye kile kiofisi kidogo na kuingizwa kwenye chumba pweke ambacho hakikuwa na kitu chochote, kulikuwa na mwanga hafifu wa njano uliotokea kwenye balbu ndogo iliyokuwa ikining’inia kwenye dari.
Niliegemeza mgongo ukutani, taswira ya kijiji cha Makose mkoa wa Tanga huko nchini Tanzania ikanijia, kwa mara nyingine nililia mno kuona ndoto zangu za kuikomboa familia yangu katika maisha duni zimegonga mwamba huku nikisubiri kunyongwa hadi kufa masaa machache yajayo.
Nilikaa ndani ya kile chumba hadi asubuhi, mwanga wa jua la asubuhi ukapenya kupitia matobo ya kwenye bati na kuingia hadi ndani ya chumba kile.
Niliumia nilipo baini kuwa jua hilo ndio jua la mwisho kuliona duniani, masaa mawili badaye, mlango ulifunguliwa. Wakaingia askari wawili na wakanitaka nitoke nje.
Nilitolewa nje na kupelekwa tena kwenye ile ofisi ndogo ambayo niliingizwa jana usiku nikiwa na Hussein Jabal.
“Yuko wapi Hussein?” niliuliza.
“Unamuuliza nani maswali ya kijinga, nyamaza kimya” askari mmoja alinifokea.
“Nifanyie ikhisani ya jambo moja,” nilimwambia kwa upole huku machozi yakinilenga.
“Jambo lipi?”
“Naombeni msaada wa kuwasiliana na ubalozi wa nchi yangu ili nipate msaada wa kisheria. Pia yupo mwenyeji wangu aitwaye Mariamu ambaye anaishia hapa hapa Muscut maeneo ya Deira...”
“Tunasikitika hilo pia hatuwezi kufanya , taarifa zitakazo mfikia huyo Mariamu ni kuja kuchukua maiti yako.” alisema tena yule askari.
Nililia nikalia na kulia, hofu ya kunyongwa kwa kamba ilisambaa ndani ya kifua changu vibaya sana.
Walinifunika kitambaa cheusi usoni, mikono yangu ikiwa kwenye pingu. Nikachukuliwa na kupelekwa mahali ambapo nilisikia wakipataja kuwa panaitwa ‘slaughuter place’
Nilifikishwa ‘slaughuter place’ na kufunguliwa kitambaa, mbele yangu nikajiona nipo eneo lenye uwazi kama uwanja wa mpira, kulikuwa na jukwaa kubwa ambalo lilitengenezwa kama goli la mpira wa miguu, kamba nyingi zenye vitanzi zilikuwa zikining’inia kwenye goli lile nikabaini eneo hilo ndipo eneo lililohusika kwa kunyongea watu.
Katika kutazama huko nikaendelea kuona kitu kingine kilicho upasua moyo wangu vibaya mno, nilimwona Hussein akiwa kando ya jukwaa lile la kunyongea akiwa anafanya ibada kwa imani ya dini ya Kislamu.
“Husseiiiin!!” niliita kwa nguvu huku nikiamini kivyovyote vile Hussein amepewa nafasi ya kusali sala ya mwisho kabla ya kuning’ininzwa kwenye kitanzi. Wale askari wa kijeshi walinikaba shingoni.
“Wewe!!!. Kuleta ghasia kwa mtu anaye fanya ibada ni jambo baya...Eeh!!”
Nilishindwa kujibu kwa kuwa tayari nilikuwa nimefungwa kitambaa mdomoni, nikaishia kulia, wakati huo nilimwona Hussein akiwa amemaliza kufanya ile ibada na sasa askari walimfunga pingu mikononi mwake. Aligeuka akanitizama huku akitoa tabasamu lenye kila dalili ya kukata tama.
“Agripina naenda kunyongwa, nisamehe kwa kushindwa kukupeleka Mogadishu, nisamehe hata kwa kukusababishia kifo ilihali ukiwa na mtoto tumboni mwako. Nisamehe kwa kukusaliti na kutembe na mwanamke mwingine, nisamehe kwa kila kitu Aglipina.
Naamini tutaonana badaye. Inshallah...” Hussein alipaza sauti kunieleza.
Nibubujikwa na machozi mdomo wangu ukiendelea kuzibwa kwa tambala gumu.
Walimvalisha soksi nyeusi usoni wakamwongoza kumpandisha kwenye jukwaa la kunyongea. Askari wawili walimvisha kitanzi cha kamba ngumu shingoni na kuhakikisha wamekaza vizuri kisha wakashuka chini wakimwacha peke yake kwenye jukwaa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliendelea kulia nikimwomba Mungu kimoyomoyo afanye mujiza wake kubadilisha kile kilichokuwa kikiendelea wasaa ule, lakini haikuwa hivyo. Askari aliyehusika na kubonyeza swichi ya kupandisha kamba juu alikuwa akingojea amri kutoka kwa kamanda mkuu.
“Kill him.”
Amri ya kunyonga ilitoka.
Mnyongaji alibonyeza swichi, kamba ikaanza kujiviringisha taratibu kwenda juu. Ilivyokuwa ikijivingirisha ndivyo ikawa inamnyanyua Hussein taratibu na hapo ikawa inamkaba shingoni kwa nguvu.
Sekunde kumi badaye Hussein alikuwa akining’inia juu na kutapatapa huku na kule. Miguu yake ilikuwa ikirukaruka huku kiwiliwili chake kikitetemeka kama anapigwa na shoti ya umeme. Hussein alijikojolea na wakati mkojo huo unapita sekunde tano zilizofuata Hussein alitulia tuli.
Tayari alikuwa MAITI!!!!!.
Bila kutegemea nilijkuta na mimi nikijikojolea kwa mara ya pili, nilikuwa na woga usiyo mithilika, niliona mwili wa Hussein ukiendelea kubembea kwenye kamba. Maisha ya Hussein hapa duniani yaliashia hapo. Kilichokuwa kimebaki kwakwe ni kushushwa kupelekwa mochwari kisha kuzikwa.
“Anayefuata kunyongwa ni wewe,”
Sauti ya kamanda ilisikika nyuma yangu. Tumbo likinichafuka nikahisi kutapika, bila kutarajia nikajisaidia haja kubwa na ndogo kwa pamoja.
Nilifunguliwa kile kitambaa mdomoni na kusogezwa eneo lilitandika zuria dogo kando kukiwa na maji kwenye ndoo ambayo nilitakiwa kunawa kabla ya kusali sala zangu za mwisho kisha kunyongwa kama ilivyokuwa kwa mpenzi wangu Hussein Jabal.
“Niacheni nirudi nyumbani, sitaki kufa mimi...sitaki.” nilisema kwa hamaniko kubwa huku nikilia. Hakuna aliyenijali, wote walinitaka nijinawishe kwa maji kisha waninyonge.
Niliendele a kuwasihi waniachie nirudi nyumbani kwetu Tanzania, lakini nao waliendela kunisihi nisali sala zangu za mwisho kwani muda wa mimi kufa utakapo wadia hawatakuwa na cha kusubiri zaidi ya kunitundika kweye kamba na kuninyonga.
Muda wa kunyongwa ulifika. Walinikamata askari wawili waliokuwa na nguvu na kunisukumiza kwenye jukwaa tayari kwa kunivisha kitanzi na kunyongwa.
“Mungu uko wapi wewe Mungu...Fanya kitu kwa ajili yangu baba, fanya sasa hivi Mungu wangu, nisaidie.” nilitamka maneno hayo kwa nguvu nikiwa nimechanganyikiwa vibaya sana.
Hata hivyo, fikra hizo zilibakia kuwa kichwani mwangu tu. Nilivishwa kitambaa cheusi kisha kitanzi, kamba ikakazwa shingoni mwangu na askari anayebonyeza swichi inayoruhusu kamba kunivuta kwa juu aliiendea swichi na kuibonyeza.
Kamba ilianza kuivuta shingo yangu na kunining’iniza kwa juu. Pumzi ziligoma kutoka huku maumivu makali ya kubanwa na kamba yakiniumiza. Nikawa natapatapa huku na kule, nikatamani ninyanyue mikono yangu ili nizuie kamba isiendelee kunikaba, ila mikono yangu ilikuwa imefungwa pingu.
Giza la ajabu likazikumba mboni zangu na wakati huohuo nikajiona nikiwa naelea angani, nikiwa kwenye hali hiyo, nilijiona naanguka kwa kasi kueleka kwenye shimo ambalo lilikuwa na giza, kwenye shimo hilo sikuona mwisho wake. Hapo nikaendelea kubaini kuwa zile ni dalili za kifo.
‘Kumbe ndiyo hivi mtu akiwa anakufa inavyokuwaga niliwaza.
Nukta zilezile sikujua tena kilicho endelea ingawa kabla sijajua kilicho endelea tayari nafsi yangu ikakubali kuwa mimi ni maiti!!!
******
NILISHITUKA ghafla nikajikuta nipo kwenye eneo lenye baridi kali na ukimya wa ajabu. Nilikuwa nimelala chali huku nikiwa kama nilivyozaliwa, nilikuwa natetemeka kutokana na baridi.
Niligeuza shingo kutizama kulia na kushoto, nikajiona nipo kwenye kitu kama box kubwa lenye kuzalisha baridi, sikuhitaji muda mrefu zaidi kutambua kuwa nilikuwa nimewekwa kwenye jokofu la kuhifadhia maiti ndani ya Mochwari!.
Ndani ya nukta zilezile nilikumbuka kila kitu. Kichwa changu kikabaki na maswali mengi ambayo majibu yake sikujua pakuyapatia. Katika mengi niliyojiuliza, swali kubwa lilikuwa ni vipi nipo hai ilihali nilinyongwa kwa kamba hadi kufa!.
Wakati nikiwa naendelea kujiuliza swali hilo mara nilisikia mlango wa Mochwari ukifunguliwa, nikasikia sauti za watu wawili wakizungumza, mmoja mwanaume mwingine wa kike.
Almanusura nipige kelele baada ya kusikia sauti ya mtu ninaye mfahamu. Niliweka utulivu nikajionya kutokurupuka kwa namna yoyote ile. Nilitulia huku nikifuatilia mazungumzo.
Wakawa wanazungumza huku wakisogea karibu zaidi na jokofu nililokuwa nimelazwa. Nikasikia yule mwanaume akimuhadithia songombingo lilitokea nyumbani kwa Abdallah Mustapha hadi kupelekea mimi na Hussein kunyongwa.
“Kikawaida huwa hatuna utaratibu wa wanawake kuingia kwenye chumba cha kuhifadhia maiti na kutizama miili, lakini kwakuwa umeniomba sana, utamwona ndugu yako.”
“Nitashukuru sana.”
“Uko tayari kuona maiti ya ndugu yako?” mlinzi wa Mochwari alimuuliza Mariamu kwa msisitizo.
“Ndiyo niko tayari,” baada ya jibu hilo kutoka kwa Mariamu, ndani ya jokofu, mate mepesi yakajaa mdomoni, hofu ikanitawala. Wakati huohuo droo ya jokofu nilimolazwa ikavutwa.
Shiiit!!.
Nilijikuta nakosa utulivu ambao nilikuwa nimeutengeneza. Bila kutarajia nikafumbua macho. Tendo la maiti kufumbua macho mbele ya Mariamu na yule mlinzi wa mochwari iliibua kizaazaa.
“Mamaaaa. Uwiiii!! Maitiiii...Imefufuka..,Waiii...Uwiiii...Mzimu...Mzimuu..”
Mariamu na mlinzi yule wa mochwari walipiga kelele huku wakikurupuka na kuuparamia mlango wa kutokea nje.
Kwa upande wangu nilijitoa ndani ya ile droo ya jokofu nikasimama katika ya chumba kile nikaona nimezingirwa na maiti nyingi zilizokuwa zimelazwa chini huku zimefunikwa kwa mashuka meupe.
Wakati huohuo nikasikia kelele nyingi zilizopigwa na Mariamu na mlinzi yule zikishadadiwa na watu wengine huko nje.
Nilibaki nimeduwaa kama teja aliyekosa kidonge cha methadon, katika kuduwaa huko nikavutiwa na maiti moja iliyokuwa imelazwa chini huku kukiwa na kibao kidogo kilichowekwa juu ya mwili wa ile maiti kikiwa na maandishi ya kingereza yaliyosomeka ‘Today buria’
Mpenzi msomaji, hadi leo ninapo simulia mkasa huu nashindwa kuelewa ni msukumo gani ulionikumba na kufanya kile nilichofanya, kwani pamoja na kulindima kwa kelele huko nje zenye kushadadia kufufuka kwa maiti ndani ya mochwari, ndiyo kwanza mimi nilipiga hatua kuusogelea ule mwili, kisha nikaufunua. Sukuamini nilicho kiona.
Kwa mara nyingine nilijikuta nikiduwa baada ya kuona kitu kilicho nifanya nihisi mwili wote ukipata ubaridi. Mpenzi wangu Hussein Jabal alikuwa amelala chali akiwa amekufa, uso wake ulionyesha kama mtu aliyepatwa na maumivu makali kabla ya kukata roho.
Shingoni mwake kulikuwa na alama na michumbuko ya kamba iliyomnyongea.
Machozi yalinitoka, donge kavu likanikaba kooni, kwa mara nyingine nilimlaumu mno Mungu, niliona sitendewi haki kwenye dunia. Maisha yangu yalikuwa yamevurugika vibaya mno.
Kamasi jepesi lilichungulia kwenye tundu za pua yangu huku machozi yakiendelea kumiminika mashavuni mwangu.
“Mzimu, mzimu, mzimu!!!” ghafla nikashitushwa na kelele zilizo endelea kulindima kwa kasi ya ajabu kutokea huko nje, hapo akili yangu ikazinduka, bila kufikiri mara mbili nikachomoka kufuata malango wa kutokea nje na kutoka.
Nilipojitokeza tu nje nikashangaa kukuta mlundo wa watu waliokuwa umbali wa hatua kama ishirini wakiwa wamezunguka jengo lile la mochwari wakiwa mkao wa kusubiri kuona mzimu ulioibuka ndani ya mochwari.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kujitokeza mbele ya mboni za macho yao nikabutwaa kuona kukizuka taharuki nyingine ya aina yake.
Kelele na mayowe ya hofu yalilindima huku kila mmoja akishika njia yake, bila kupoteza muda na mimi nikaanza kutimua mbio bila kujua wapi ninapokimbilia. Ndani ya nukta hizo hizo nikagundua jambo jingine lililonifanye nizidi kuchangaikiwa.
Kwenye mwili wangu nilikuwa sina chochote nilicho vaa, nilikuwa uchi wa mnyama.
Nikazidi kuhamanika, nikageuka na kurudi ndani ya chumba cha mochwari kisha nikakwapua shuka moja miongoni mwa zile zilizokuwa zimefunika miili ya watu wengine, nikajifunika na kutoka tena nje.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment