Simulizi : Usilie (Don't Cry)
Sehemu Ya Tatu (3)
Glory aliinuka kwenda kumsikiliza Fikiri.
"Naomba ndizi"aliongea Fikiri.
"Ngapi nikupe?aliuliza Glory.
"Zozote ntakuwa nakula wewe unahesabu,pia nawe kula unazozitaka"aliongea Fikiri.
"Hawa wanawake wanadanganyikiza kwa kitu kidogo kabisa"alijisemea Fikiri.Glory akiwa anakula ndizi huku macho yake yakiwa makini kusoma simulizi,ghafla simu yake iliita hakuwa mwingine bali alikuwa ni Issa,Glory alijikuta akisonya hakupenda kupigiwa simu kwa wakati ule.Siku hiyo hata maongezi yao hayakuwa mazuri.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mke wangu nini shida mbona leo hauko kama siku zote?aliuliza Issa baada ya kuona tofauti kidogo.
"Kichwa kinaniuma harafu mtoto alikuwa analia sana"alijibu Glory.
"Pole basi ngoja mimi nikuache ntakupigia badae"alisema Issa.
"Haya sawa mme wangu kazi njema"alijibu Glory.Yote hayo aliyaona Fikiri.
"Nishajua pa kumnasia huyu mwanamke"alijisemea Fikiri.Zogo la hapa na pale liliendelea huku Fikiri akiwaza yake moyoni.Usiku wa siku ile Issa alipiga tena ,Glory alipokea kwa uchangangamfu mkubwa,waliongea mengi sana,kila maongezi yao Issa hakusita kumwambia Glory kuwa awe makini,aliamini wanawake ni rahisi sana kubadilika hivyo alizidi kumsisitiza.Kesho yake Fikiri alirudi tena,alinunua ndizi kisha akaondoka,Glory aliendelea kufuatiria mitandao ya kijamii.
"Sijui nilikuwa wapi siku zote kwanini sikuijua hii mapema"alijisemea Glory.Licha ya Issa kumuachia Glory pesa ya kutosha lakini alihakikisha kila mwisho wa wiki anamtumia pesa ya kutosha,bado genge lake lilizidi kuwa kubwa,kila hera aliyokuwa anatumiwa alihakikisha anaongezea vitu.Baada ya wiki mbili kupita Glory alikuwa ashajua kila kitu kwenye mitandao ya kijamii,bado alitumia mda mwingi kuwa kwenye mitandao ile hasa kila alipokuwa anakutana na simulizi nzuri.katika pita pita zake alikutana na simulizi moja inaitwa UTANIKUMBUKA,simulizi hiyo ilimvutia na kujikuta akitoa namba na kumpigia mtunzi wa simulizi hiyo.
"Kaka simulizi zako nzuri,nimezipenda"aliongea Glory baada ya kutoa namba ya mwandishi.
"Asante dada kwa kunisifia"ilikuwa sauti ya upande wa pili.
"Sasa nikitaka iliyokamirika naipataje"aliuliza Glory.
"Labda nikutumie WhatsApp yule mtunzi alimjibu,baada ya kujiunga na lile kundi alikutana na simulizi nyingine iliyoitwa USALITI,nayo ilimvutia.
"Hivi nami naweza kumsaliti Issa?asee siwezi ila usaliti kama huu upo,yaani hawa waandishi wanaandika kitu kilichopo kabisa"alijisea Glory.Siku ile hakuweza hata kumkumbuka Issa.
"Huyu mwanamke vipi hata kunijulia hali?mbona sio kawaida yake?alijiuliza Issa baada ya kuona imepita siku nzima Glory hajampigia na sio kawaida yake.Kila alipokuwa anampigia Glory hakuweza kumpata kabisa,basi alijipa moyo.Kadri siku zilivyokuwa zinasogea ndivyo Glory alizidi kukutana na mambo mengi mitandaoni.
Ilikuwa siku ya Ijumaa,majira ya mchana,Glory kama kawaida yake alikuwa bize,Fikiri alifika gengeni kwake,baada ya salamu Fikiri aliamua kumuomba Glory namba ya simu.
"Sijaiweka kichwani,labda nipe yako nikupigie"aliongea Glory,baada ya kumaliza kupeana namba Fikiri aliondoka.
"Nishamjua huyu mwanamke anapenda simulizi"alijisemea Fikiri.moja kwa moja alianza kuwasiliana na waandishi waliokuwa wanamuuzia simulizi kisha yeye anamtumia Glory kwa njia ya WhatsApp.
"Kaka kwani mwandishi ni wewe?aliuliza Glory.
"Ndio ni mimi ,soma jina la mwandishi"Fikiri alijibu.Alichokuwa anakifanya Fikiri,kila alipokuwa anatumiwa simulizi yeye alifuta jina la mwandishi na kuweka lake,ile njia aliiona nyepesi kumnasa Glory. Siku zilisogea huku Fikiri njia yake ikiwa ni ile ile,Glory alianza kumpenda Fikiri kutokana na simulizi zenye uhalisia ambazo aliamini kuwa mwandishi ni yeye.Hadi inapita wiki moja Glory alikuwa bado hajawasiliana na Issa,Issa bado hakuelewa yale mabadiliko ya ghafla,hakutaka kumhukumu Glory.
"Au labda alidondosha simu?alijiuliza Issa bila kupata jibu.Fikiri baada ya kuhakikisha amemteka Glory aliamua kumwambia ukweli.
"Pole sana mwandishi,umechelewa mimi nina mtu tayari na siwezi kumsaliti kabisa"alijibu Glory.
"Najua lakini huyo mtu wako umesema yupo China sasa unajua China atarudi lini?funguka akili Glory"alisema Fikiri.
"Hapana kwa hilo siwezi kabisa"alijibu Glory.
"Usiseme hivyo Glory hebu jiulize mimi natumia mda gani kukaa na kutunga Simulizi ili nikuburudishe wewe?bado hujauona upendo wangu tu"aliongea Fikiri kwa sauti ya huzuni.
"Najua kuwa ni kazi ngumu pia inachosha,lakini Kama nilivyokwambia kuwa umechelewa,Mimi tayari niko ndani ya mahusiano"aliongea Glory.
"Najua lakini tambua kuwa nakaa ndani mda wote naumiza kichwa ili nikuandikie simulizi ufurahi,yote haya nayafanya kwa ajili yako,jaribu kutafakari,ukituliza kichwa utaona jinsi upendo wangu ulivyo mkubwa kwako"aliongea Fikiri.
"Siko tayari kumsalti Issa"alijibu Glory kisha akakata simu,hapo alimkumbuka Issa,bila kuchelewa aliingia mtandaoni na kujaribu kumtafuta Issa.Issa akiwa amejiinamia kwa mawazo alisikia simu yake inaita.
"Waoooh mke wangu, jamani nini kilitokea?aliongea Issa kabla hata ya salamu.
"Yaani mme wangu simu ilidondoka kwenye maji na mafundi wa huku unawajua walivyo wasumbufu kwahiyo simu nimeichukua leo"aliongea Glory huku akitunga uongo ambao Issa aliukubari.
"Pole sana,vipi Bahati hajambo na vipi hera za matumizi bado mnazo ndani"aliuliza Issa.
"Bahati hajambo na yupo anakusikiliza hapa,hera bado zipo Mme wangu vipi kazi zinaendaje lakini"aliuliza Glory.Basi waliongea mambo mengi sana,huku Issa akifurahi kuongea na Glory.Ndani ya kipindi hicho Fikiri aliacha kumtumia Glory Simulizi bado Glory hakutaka kumsaliti Issa.
"Issa ni mwanaume aliyenisaidia kwenye matatizo makubwa ambavyo bila yeye huenda ningelipoteza maisha"alijisemea Glory huku akikumbuka maneno ya Fikiri.kwa kipindi hicho Glory kila mda alikuwa akiwasiliana na Issa,bado Simulizi alizipenda lakini hakuwa tayari kumuacha mtu aliyemsaidia.Majira ya saa sita usiku Glory akiwa bado anapitia kwenye mitandao ya kijamii,kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake kwa njia ya WhatsApp,alipoufungua alikuta ni Simulizi iliyokuwa inaitwa MAISHA YANGU,ilitoka kwa Fikiri,baada ya kumaliza kuisoma ilimvutia kweli.
"Waooh ni nzuri hongera kwa kipaji ulichopewa na mungu"Glory aliandika hayo maneno kisha akayatuma kwa Fikiri,bado hakujua kuwa Fikiri zile Simulizi alikuwa anazinunua kisha anafuta jina la mwandishi,Fikiri alitabasamu baada ya kuyasoma hayo maneno.
"Lazima nikukamate"alijisemea Fikiri.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Siwezi kukubali"bado aliendelea kuongea Fikiri,alitoa simu yake na kuiweka sikioni akampigia Glory,simu haikuita sana ilipokelewa.
"Hallow Glory, hapa nina mawazo mapya yamenijia kichwani"aliongea Fikiri.
"Mawazo gani hayo?aliuliza Glory.
"Kama uko tayari nataka niandike Simulizi ya maisha yako kisha nitoe kitabu,naamini kitapokelewa kwa kasi pia ndo kitakuwa chanzo cha sisi kupata hera pia wewe nitakuweka kama mwandishi"aliongea Fikiri.Glory alifakari kwa sekunde kadhaa.
"Mmh itawezekana kweli"aliuliza Glory.
"Ndio itawezekana ni wewe tu kuwa tayari"aliongea Fikiri.
"Nipe mda nimuulize Mme wangu kisha nitakujibu"aliongea Glory.
"Naam ninachojua mimi hakuna mwanamke mgumu kwenye hii dunia"aljisemea Fikiri,aliamini kabisa Glory hawezi kuruka lazima atakubari.
Glory atakubari?harufu ya usaliti hiyooooo..
Glory aliyatafakari yale maneno ya Fikiri,kila alipofikiria kumwambia Issa moyo wake ulikuwa mzito kabsa.
"Hivi namimi naweza kujulikana kama waandishi wengine?alijiuliza Glory kila alipowaza maneno ya Fikiri kuwa yeye atahusika kama mwandishi.Siku nzima alishinda Fecebook akiangalia baadhi ya waandishi na kuona walivyo na wafuasi wengi.
"Cheki kama huyu Juma Hiza yaani anapata like zaidi ya elfu mbili,asee hapa nimekubali"alijisemea Glory bado hakujua kuwa ile njia Fikiri aliitumia ili amnase,Fikiri hakuwa mwandishi.
"Sawa nimekubali lakini kwenye Simulizi utaniweka mimi kama mwandishi"ulikuwa ujumbe alioutuma Glory kwenda kwa Fikiri.
"Nilisema toka mwanzo kuwa hakuna mwanamke mgumu kwenye hii dunia,vijana wengi wanakoswa mbinu"alijisemea Fikiri baada ya kuona njia aliyoitumia itakuwa nzuri kumteka Glory kimapenzi.Issa alianza kuwa na hofu kadri siku zilivyokuwa zinasogea,mda wa kuongea na Glory ulikuwa mchache sana,kila mara Glory alikuwa na sababu zilizosababisha mawasiliaono yao kushuka.
"Yaani tulikuwa tunaongea hata masaa matatu leo hii hata dakika tano haziishi?nini kimesababisha yote haya?mbona mapema mno huyu mtu kabadirika hivi?Issa alijiuliza,kila alipokuwa anakumbuka mahusiano yake na Glory mwanzoni yalivyokuwa alidondosha chozi.Ikiwa imepita miezi mitatu tangu Issa aende China,huku Tanzania Glory alianza mazoea taratibu na Fikiri.
"Ujue nini Glory"aliongea Fikiri akiwa na Glory.
"Eeeh nambie"alijibu Glory.
"Kitabu nitakachokiandika kitapendeza kama mimi na wewe tutashiriki kama mke na Mme"aliongea Fikiri kwa uchokozi.Glory alishusha pumzi kisha akatulia kwa sekunde kadhaa akionekana kutafakari jambo.
"Sawa basi andika hivyo"alijibu Glory.Fikiri alifurahi moyoni.Wahenga walisema kuwa mazoea hujenga tabia,ndicho kilichotokea kwa Glory,alijikuta akimpenda Fikiri na kumsahau Issa,kijana aliyejitahidi kumuokoa kipindi anataka kujifungua,Glory alosahau msaada wa Issa,mbaya zaidi hadi Issa anasafiri kwenda China hakuwa amefanya tendo la ndoa na Glory.Issa huko China mda mwingi alionekana kuwa mnyonge,alifikiria kilichompata Glory hadi akabadirika ghafla jibu hakulipata,sasa ilipita wiki mbili Glory akiwa hajamtafuta Issa,upendo wa Glory na Fikiri ulianza kukua.
"Hivi kweli unanipenda?aliuliza Fikiri.
"Ndio nakupenda nipo tayari kwa lolote"alijibu Glory kwa kujiamini.
"Kama kweli upo tayari nikikwambia kitu utakubari?aliuliza Issa.
"Ndio wewe niambie niko tayari"alijibu Glory.
"Sawa nataka utoe hiyo laini kwenye simu kisha uitupe motoni,harafu mimi nakupa ya kwangu ndo uiweke humo"aliongea Fikiri.Glory hakutaka kusubiri aliitoa ile laini na kuitupa motoni.
"Kuna kingine nifanye?aliuliza Glory.
"Hapana hakipo hapo nimeamini kweli unanipenda"aliongea Fikiri huku moyoni akifurahi,alijua kabisa kuwa Issa hatampata tena Glory. Mapenzi yao yaliendelea kuwa mazuri,hata glory alianza kukoswa mda wa kwenda gengeni kwake mda mwingi alikuwa ndani na Fikiri.
"Yaani nataka utangaze ndoa kabisa unioe"aliongea Glory.
"Kwahilo usjali kabisa niko tayari"alijibu Fikiri,Fikiri hakuwa na makazi ya kuishi mara nyingi aliishi na washikaji.
"Lakini Mme wangu natamani nipaone unapoishi"aliongea Glory kwa sauti ya kubebeleza.
"Jamani usjali tutaenda sahivi kuna mdogo wangu yuko likizo"alijibu Fikiri.
"Kwahiyo unaishi na mdogo wako?aliuliza Glory.
"Hapana yuko likizo katoka Uingereza hivyo kafikia ninapo ishi"Fikiri alitunga uongo uliozidishi kumvimbisha kichwa Glory .
"Kwahiyo huyo mdogo wako anasomea Uingereza?aliuliza Glory.
"Ndio na ada mda mwingi namlipia mimi"alijibu Fikiri.Glory alizidisha upendo bila kujua kuwa Fikiri hakuwa na mbele wala nyuma,Glory kila alipokuwa anamwambia Fikiri kuwa akapoone alipokuwa anaishi bado Fikiri hakukosa sababu hadi inapita miezi miwili Fikiri alikuwa anaishi kwa Glory.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Issa baada ya kuona namba ya Glory haipatikani kwa mda mrefu aliamua pesa aliyokuwa amepanga kumtumia Glory alizidi kuiweka kwenye akaunti yake.Bado utendaji kazi wake ulionekana kuwa wa chini mno,kila alipomfikiria Glory alikoswa nguvu.
"Kwani kosa langu liko wapi?alijiuliza Issa.
"Ila naamini kama kweli Glory kanisaliti ipo siku ataukumbuka upendo wangu"alijisemea Issa.Aliendelea kufanya kazi kwa badii,pia hakuwa na matumizi mengi.
"Ngoja nizidi kuweka akiba ili siku nikiingia Tanzania nimuone huyu anayemmiliki Glory anafananaje"alijisemea Issa.
Mama mwenye nyumba alizidi kushangaa Glory na Fikiri,alikumbuka siku za nyuma Glory alikuwa anaishi na Issa,lakini ghafla anamuona na mtu mwingine.
"Haka kadada kanaonekana hakajatulia kweli"alijisemea mama mwenye nyumba.Alikumbuka kodi ya miaka miwili aliyokuwa amelipia Issa.
"Ngoja nijaribu kumpigia simu nione kama anayajua haya"alijisemea mama mwenye nyumba huku akipiga namba ya Issa,lakini haikupatikana.
"Natamani kuuona mlima Kilimanjaro"aliongea Glory akiwa na Fikiri.
"Usjali jioni ya leo tutaenda"alijibu Fikiri.Jioni ya siku ile walienda mpaka kwenye ule mlima,watu wengi waliokuwa wanamjua Glory walipigwa na bumbuwazi walipomuona na Fikiri.
"Huyu binti ndo maana alibebeshwa mimba anaonekana mcharuko kweli"aliongea kijana mmoja.
"Lakini ujue sio vizuri,Issa na Fikiri walivyokuwa wanaishi lakini leo hii Fikiri kamchukulia mchumba wake,asee rafiki yako ndo adui yako"yalikuwa maneno ya kijana mwingine,hapo hapo alitoa simu yake na kumpigia Issa lakini hakumpata.
Huko China Issa,alijaribu kutafuta namba za Tanzania lakini hakuzipata,alikumbuka kuwa kwenye simu yake alikuwa na namba ya Glory pekee.
"Mama kwanini aliniambia niwasaidie wanawake wajawazito wasio jiweza?alimanisha nini,mbona huyu nimemsaidia lakini mwisho wa siku kanisaliti?hawa watu mungu aliwaumbaje?yalikuwa maswali kichwani kwa Issa,bado hakutegemea mtu kama Glory angeweza kumsaliti tena kwa kipindi kifupi.
"Yote sawa,huwezi kujua mungu kaniepusha nanini"alijisemea huku akifuta machozi ambayo hayakukauka kwenye mboni zake.
Maisha ya Glory yalizidi kusogea ndani ya kipindi hicho Fikiri hakutoa hera kabisa,hera waliyokuwa wanaitumia ilikuwa ya Glory aliyokuwa ameachiwa na Issa.Fikiri alizidi kuongeza upendo huku moyoni akifurahi kulelewa.
"Zikishaisha hizi pesa hanioni tena"alijisemea Fikiri,alipanga kumtoroka Glory.
"Tayari nilichokuwa nakitaka nishakipata tayari,hivyo hainisumbui tena"alizidi kujisemea Fikiri baada ya kuona pesa waliyokuwa wanaitumia ikianza kupungua.Glory alizidi kujiuliza kazi aliyokuwa anaifanya Fikiri.
"Mbona simuoni akienda kazini?kazi gani anayoifanya huyu?kila siki yuko hapa"alijiuliza Glory.Mtoto wa Glory mpaka kwa wakati huo alikuwa akitambaa,Fikiri hakuwahi kumbeba hata siku moja alimchukia sana,yote hayo yalikuja baada ya kumshiba Glory.
"Wanawake bhana sasa alichokuwa analingia kiko wapi,yaani mwanzoni nilikuwa namuona wa maana sana lakini sasa hivi wa kawaida,hata hivyo mimi mwanaume lijali siwezi kung'ang'ania mwanamke mmoja"alijesemea Fikiri.
Siku moja Glory alimuita Fikiri na kumwambia.
"Mme wangu uliniambia tutaandika kitabu,na mpaka sasa sioni maandalizi yeyote kuhusu hilo uliloniambia,je ni kitu gani ulichokuwa unatumia kuandika Simulizi?Glory alimuuliza Fikiri aliyebaki kutoa macho.
"Mme wangu sasa ule mpango uliokuwa umeniambia kuwa utaandika kitabu vipi umefikia wapi,maana sioni maandalizi yeyote"Glory alimuuliza Fikiri.Fikiri aling'ata kidole kana kwamba kuna kitu anakifikiria.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Usjali kuhusu hilo,mdogo wangu aliyetoka Uingereza ndo alikuwa anaitumia kompyuta yangu nayoitumia kuandika,hivyo akiondoka kila kitu kitakuwa sawa"alijibu Fikiri,uongo ule uliweza kumtuliza Glory.Kadri siku zilivyokuwa zinasogea ndivyo mapenzi ya Fikiri yalizidi kupungua kwa Glory,baada ya pesa kuisha ndipo Glory aliweza kukumbuka genge lake,alikuta baadhi ya vitu vimeshaanza kuoza,bado Fikiri aliendelea kuishi kwa Glory,alitegemea pesa iliyokuwa inatoka kwa Glory.
"Huyu mwanaume vipi?mbona Simulizi aliyokuwa ameshanitumia nusu ndo hii nayoiona anaiposti MKAPA JR?kuna nini hapa katikati,au alitumia njia hiyo ili anipate?alijiuliza Glory bila kupata jibu,bila kuchelewa alitoa namba za yule mwandishi na kuziweka kwenye simu yake kisha akapiga.
"Hallow,mambo"aliongea Glory.
"Powa naongea nanani"sauti ya upande wa pili ilisikika.
"Glory hapa kutoka Arusha,wewe ndo MKAPA JR?
"Ndio nambie"
"Ahaaa nimeona story yako nikaipenda"
"Ooh asante sana"
"Vipi mwandishi ndo wewe?
"Ndio ni mimi?
"Sasa nikitaka iliyokamirika naipaje?
"Lipia elfu mbili nikutumie"
"Sawa nitumie basi namba nikutumie"
"Namba ndo hiyo"
"Ok sawa natuma sasa hivi,jina litatoka nani?
"Jina ni Mkapa tofili"
"Ok sawa,asante"yalikuwa maongezi ya Glory na mwandishi wa Simulizi.
"Ndo ntajua ukweli wa huyu mwanaume"alijisemea Glory baada ya kumaliza kutuma pesa hazikuisha hata dakika tano,Simulizi alitumiwa yote.
"Inamaana alikuwa ananidanganya?alijiuliza Glory huo ndo ulikuwa mwanzo wa kugundua uongo wa Fikiri.Siku hiyo Glory alianza kumchukia Fikiri,aliona anafuga mzigo ndani usiokuwa na maana,moyo wake ulianza kuwa na hasira,kila alipokuwa anakumbuka Fikiri alivyomdanganya na kumshawishi kumuacha Issa,ghafla moyo wake ulianza kumkumbuka Issa,tatizo lilikuja kwenye namba alizokuwa ameshazipoteza tayari.
"Sasa namba ntazipaje?nimemkumbuka kweli mwanaume mwenye upendo sio hawa wengine"alijisemea Glory,alijukuta akijutia kitendo chake cha kukubali kushawishika tena ikiwa bado mapema kabisa.
"Sasa namba yake ntaipata wapi ili nimuombe msamaha?alijiuliza Glory alikumbuka laini iliyokuwa na namba za Issa jinsi alivyoitupa motoni mbaya zaidi hata namba ya Issa alikuwa hajaiweka kichwani,yote hayo kumfurahisha Fikiri.
"Mungu anisamehe kwa usaliti huu"alijisemea Glory,hata nguvu za kuendelea kukaa kazini kwake hakuwa nazo kabisa,alirudi nyumbani na kumkuta Fikiri akiwa amelala,hasira alizokuwa nazo hakuongea,hadi inafika jioni Glory hakutamka kitu chochote.
"Mke wangu vipi kwani leo"aliuliza Fikiri.
"Sina mme muongo kama wewe"aling'aka Glory huku machozi yakianza kumtoka.
"Muongo?mbona sikuelewi"aliuliza Fikiri.
"Ziko wapi simulizi ulizokuwa unanitumia?kumbe simulizi zenyewe ulikuwa unazitoa kwa mtu muongo mkubwa wewe"Glory aliongea kwa uchungu.
"Hahahahahaha,ujue Glory unanichekesha sana bado sijakuelewa"aliongea Fikiri kwa kebehi.
"Kikuchekeshasho ninini?hujui kuwa wewe umesababisha nikamsahau mtu aliyekuwa ananipenda?bado unacheka kitu gani?Glory aliongea kwa uchungu.Fikiri alizidi kucheka,baada ya kucheka mda mrefu aliinuka kitandani kisha akamsogerea Glory.
"Hivi wewe na akili zako zote mtu anakudanganya kwa kitu kidogo kama hicho na wewe unakubali kumuacha mtu unayempenda?hivi nyinyi wanawake mbona mnakuwa wepesi hivyo?ona sasa mimi nishakutumia ninavyotaka na sasa nimekushiba,bado sijajua huwa mnalingia kitu gani"aliongea Fikiri kwa jeuri.Glory alijikuta akimpiga kofi Fikiri lakini yeye aliishia kucheka.
"Nakuomba utoke ndani kwangu,mwanaume gani wewe unayependa kulelewa,tokaaa!!tokaaa!uondoke"aliongea Glory huku akilia kwa sauti.
"Sawa mimi naondoka lakini tambua nimekutumia nitakavyo hata ukinitemea mate au kunipiga mawe haisaidii,ndo maana ulibebeshwa mimba ukakimbiwa akili zako finyu"Fikiri alimalizia na matusi kisha akachukua baadhi ya nguo zake na kuondoka.Yote hayo aliyaona mama mwenye nyumba.
"Nilisema tangu mapema kuwa huyu binti hajatulia"alijisemea Mama mwenye nyumba.Maisha ya Glory yaliyumba kwa mda mfupi,siku hiyo alijifungia ndani kisha akaanza kutoa machozi.
"Issa naomba nisamehe huko uliko mimi bado nakupenda"Glory aliongea kwa sauti,mawazo yalimpeleka kwa Peter.Pater aliyemuachia huu msala kisha yeye akaenda kusiko jurikana.
"Wanaume wote ndo wale wale waongo,labda Issa mwanaume aliyekuwa ameshushwa na mungu kwa ajili yangu,lakini nimemlipa haya kweli nasitahili adhabu"Glory aliongea kwa uchungu wa hali ya juu.Maisha ya Glory yalianza kuwa magumu kutokana na msongo wa mawazo,genge lake lilianza kupungua kutokana na kukosa pesa ya kuongeza vitu,bado umeme na maji alikokuwa amepanga vilimpa changamoto kubwa,hera kidogo aliyokuwa anaipata iliishia kwenye matumizi madogo madogo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mzee vipi nasikia ulikuwa umeolewa"alikuwa kijana mmoja akimwambia Fikiri.
"Wewe acha tu yaani kwa kipindi cha miezi kama mitano nilikuwa nakula na kulala bure"aliongea Fikiri.
"Sasa imekuawaje mbona umetoka"
"Ahaa unajua hiyo manzi imeishiwa ndo nikaamua kutoka"aliongea Fikiri kwa kujisifu,alianza maisha akiwa na marafiki zake aliokuwa anaishi nao tangu mwanzo.
"Unajua kwenye hii dunia ya sasa bila kuongea uongo huwezi kupata kile unachokihitaji"aliongea Fikiri huku akianza kuwasimulia mwanzo mpaka mwisho ilivyokuwa.Wote walimsifia kwa uongo ule alioutumia.
"Vijana tunakoswa mbinu tu ila hakuna mwanamke mgumu"kijana mmoja aliongea.Basi zogo la kijiweni liliendelea kata ya Fikiri na baadhi ya vijana wengine.
Ilikuwa siku ya jumapili,siku hiyo Glory hakuwa hata na hera ya akiba ndani,ghafla mtoto wake alianza kutapika ,ilikuwa homa ya ghafla iliyokuwa imemkumba mwanaye,Glory alichanganyikiwa sana ndani hakuwa na hera yeyote,mtoto wake alizidi kutapika,mpaka alianza kutapika damu,hali ile ilimtia wasiwasi Glory hakujua atapata vipi msaada,alipojaribu kwenda kuazima pesa kwa mama mwenye nyumba alipewa majibu yaliyomfanya azidi kudondosha machozi.
"Kwani vipi uliyekuwa unamlea humo ndani leo hajakupa pesa?yalikuwa maneno ya mama mwenye nyumba akimwambia Glory.Glory alimbeba mwanaye mpaka kwenye duka la madawa lililokuwa karibu.
"Huyu mtoto inaonyesha kaishiwa maji,na sisi hapa hatuna huduma hizo mpaka kwenye hospital kubwa,fanya haraka umuwahishe vinginevyo utampoteza"yalikuwa maneno ya mama ya mama mmoja akiyekuwa unauza kwenye duka la dawa.Maneno yale yalizidi kumchanganya Glory hakujua msaada ataupata wapi,mwanaye alizidi kutapika huku akionekana kulegea kabisa.
"Mungu wangu msaidie mwanangu,hapa ndo naanza kuuona umhimu wa Issa,mungu ampe adhabu Fikiri kwa kunipotosha"alijisemea Glory huku akijaribu kusimamisha boda boda ili awahi kwenye hospital ya Mount Meru.
"Kaka niwahishe hospital mwanangu yuko hali mbaya"Glory aliongea huku akihema kwa kasi.
"Elfu moja dada nilipe kabisa"yule kijana aliongea.
"Kaka ntakulipa nikitoka mwanangu apone kwanza,nisaidie kaka angu"Glory aliongea huku machozi yakimtoka.
"Kumbe huna hera,asubuhi asubuhi hii huwa sifanyi biashara hizo"yule kijana alijibu kisha akaondoka eneo lile akimuacha Glory ameshika kichwa,huku mgongoni mtoto alizidi kutapika huku hali yake ikionekana kuwa mbaya zaidi.
Malipo ya usaliti ndo haya,kina dada nadhani mnaendelea kunielewa vyema...
Glory aliendelea kuomba msaada lakini hakuna aliyemsiliza,wengi wao walionekana kuwa bize na mambo yao.
"Mwanangu anakufa hivi hivi kweli sina hata wa kunisaidia?alijiuliza Glory huku taratibu akianza kutembea kuelekea ilipokuwa hospital kwa mwendo wake alitakiwa kutumia masaa mawili,mtoto baada ya kutapika mda mrefu hatimaye aliacha hata kutoa sauti.
"Kapoteza maisha nini?alijiuliza Glory huku akimweka chini na kuanza kumkagua,lakini alikuta bado akiwa anapumua hasa baada ya kutasikilizia mapigo ya Moto wake.
"Mungu msaidie mwanangu"alijisemea Glory huku akikaza mwendo.Baada ya kutembea kama nusu saa alijihisi kuchoka lakini bado alikaza mwendo,kila mara alimshika mwanaye kifuani kusikilizia mapigo ya moyo.
"Bado anapumua kwa mbali"alijisemea Glory huku akizidi kutembea.Gari aina ya Land Lover ilikuwa imepaki kando ya barabara,Glory alipofika karibu na lilipokuwa gari lile,mara mtoto aliachia matapishi yaliyotua kwenye lile gari,Glory alisimama kwanza na kutoa leso yake kisha alianza kuyafuta yale matapishi,ghafla mwenye lile gari alifika.
"Achana nalo ntalipeleka wakalioshe"aliongea yule mwanaume.
"Asante sana kaka angu"aliongea Glory.
"Usjali kwani mtoto anaumwa nini"
"Ni homa ya ghafla imemshika mpaka naogopa maana anatapika damu"aliongea Glory.
"Pole sana sasa unaenda wapi?
"Nawahi hospital ya Mount Meru"
"Ndo unatembea kwa miguu?kwani usafiri hakuna?
"Usafiri upo kaka ila wamegoma kunipeleka"
"Kwanini?
"Ahaa,sina nauli ya kuwalipa"
"Oooh,mungu wangu,kwani baba wa huyo mtoto yuko wapi?hapo Glory alianza kutoa machozi,yule mwanaume aliyekuwa anaitwa Dulla alishangaa.
"Kipi kinakuliza?aliuliza Dulla.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Umenikumbusha mbali kaka angu"aliongea Glory huku machozi yakizidi kumtoka.Ndipo alipoanza kumsimulia mwanzo mpaka mwisho.Dulla alishusha pumzi kisha akamwambia Glory aingie kwenye gari,safari yao iliishia hospital,Dulla alijitoa kulipia kila kitu,baada ya masaa matatu mtoto Glory alipata nafuu kidogo ilihitajika damu yote hayo aliyalipia Dulla.Dulla alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya baba yake,baba yake umri kidigo ulikuwa umesogea hivyo utajiri wote alimkabidhi mwanaye Dulla.Dulla alikuwa mtu wa kuwasaidia watu,hakupenda kujiweka juu,kila binadamu alimuona kwake sawa.
"Dada unaishi maeneo gani?aliuliza Dulla.
"Naishi pale uliponikuta kwa mbele kidogo naishi na mwanangu huyu"Glory alijibu kwa sauti ya chini.
"Sasa vipi kodi ya nyumba na chakula"
"Kodi bado miezi mitatu labda chakula ndo shida"aliongea Glory.
"Pole sana,hiyo ndo mitihani ya maisha yakupasa uishinde,nisubiri kidogo"aliongea Dulla kisha akaingia benk iliyokuwa karibu,alitoa pesa na kumpa Glory.
"Ooooooh mungu akubariki kaka angu asante kwa kunisaidia"aliongea Glory akiwa amepiga magoti chini.Lakini Dulla alimsimamisha na kumwambia kuwa anayestahili kupigiwa magoti ni mungu pekee.Saa kumi na moja za jioni Glory alipewa ruhusa ya kutoka pale hospital,mwanaye kidogo alipata nafuu,pesa alizopewa alizihesabu na kukuta ni laki nne,moyo wake ulifurahi sana.
"Ntaenda kujaza genge langu"alijisemea Glory huku akimshukuru mungu kwa kumkutanisha na Dulla.
Huko China Issa ilizidi kupungua kutokana na mawazo,bado hakutaka kuamini kuwa Glory ndo alikuwa amemsaliti,bado aliendelea kufanya kazi kwa bidii zote.
"Ipo siku atanikumbuka"alijisemea Issa baada ya kuwaza mda mrefu,alijitahidi kulazimisha moyo umsahau Glory lakini ilishindikana.
"Sawa nimeumia ila nitazoea,laiti ningeliwasikiliza rafiki zangu kuwa mke mwenye mtoto sio wa kuoa,leo hii nisingeliweza kukonda kwa haya mawazo"alijisemea Issa.
"Glory baada ya kufika nyumbani alinunua mahitaji kidogo yaliyokuwa yanahitajika.Kesho yake alienda sokoni na kununua mahitaji ya gengeni kwake kidogo palijaa.Fikiri baada ya kuachana na Glory hakuwa na kazi yeyote,aliishi mitaani huku akifanya kazi ndogo ndogo ndani ya jiji hilo la Arusha.Kila mara aliwaza jinsi ya kumkomoa Glory.
"Sijawahi kutukanwa na mwanamke hata siku moja,najua jeuri yake ipo kwenye kile kigenge chake anachokitegemea"aliwaza Fikiri,njia aliyoona sahihi ya kumkomoa Glory ni kuvamia kwenye lile genge ikiwezekana vitu vyote avisambaratishe.Usiku wa siku ile aliamka saa sita za usiku na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye genge la Glory hapo alivunja mlango na kuanza kupakia baadhi ya vitu.
"Kumbe alikuwa ameongeza vitu vingine pole sana,mimi siwezi kutukanwa na mwanamke"alijisemea Fikiri.Baada ya kupakia vitu vya kutosha hapo alitoa vingine na kuanza kuvirusha rusha,mpaka alipohakikisha genge limebaki tupu alitoka nje na kuvibeba vile akavipereka alipokuwa anaishi na marafiki wengine.Asubuhi Glory aliamka mapema sana,kutokana na kuongeza vitu aliamua kwenda mapema,lakini alipofika karibu na lilipokuwa genge lake alipigwa na butwaa,hakuamini kuona genge lake liko tupu.
"Mungu wangu nimeibiwa"alijisemea Glory alisogea mpaka karibu alianguka chini na kupoteza fahamu kabisa.Majilani wa karibu walijitokeza eneo lile lakini hakuna aliyeamini kuona genge lote limebaki tupu.
"Ninani aliyefanya haya mbona kwenye mtaa huu hakuna vitendo hivi kabisa"alijisemea bibi mmoja.Baada ya masaa matatu Glory alilejewa na fahamu,bado alilia kwa sauti hakujua ataishije kwani alichokuwa anakitegemea kilikuwa hakipo tayari.
"Laana ya kumsaliti Issa ndo hii naipata,ntaenda wapi Glory mimi"alijisemea Glory huku akikumbuka kipindi chote alichoishi na Issa hakuwahi kuteseka kabisa.Majilani walijitahidi kumfariji lakini haikusaidia kitu Glory bado aliendelea kulia.Hadi inafika jioni Glory hakula chochote.
"Nisingekuwa na mwanangu ningejiua ili niondokane na hizi shida za dunia"alijisemea Glory huku akimwangalia mwanaye aliyekuwa hajapata unafuu.Baada ya wiki tatu kila kitu ndani kwa Glory kiliisha,hakujua msaada mwingine ataupata wapi tena,ndipo alipoanza kuzunguka ndani ya jiji la Arusha kuomba kazi.Alizunguka siku nzima hakuweza kupata kazi,akiwa na mwanaye mgongoni alizipiga hatua kurudi nyumbani,siku hiyo alilala njaa,aliomba uji kidogo kutoka kwa wapangaji na huo uji alikunywa mwanaye.Maisha yalizidi kuwa magumu,Glory aliukumbuka upendo wa Issa lakini hakujua atampata wapi.
Glory hakuchoka kuzunguka ndani ya jiji hilo kuomba kazi.
"Dada habari"alisalimia Glory.
"Salama karibu"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Asante sana,nilikuwa naomba kazi yeyote ntaifanya"aliongea Glory.
"Pole Dada yangu ungelipata kazi ila ndani ya huu mgahawa kuna wafanya kazi wasio na watoto,kawaida ya mwanamke mwenye mtoto huwa mchafu kwahiyo bosi haruhusu labda sogea kule mbele"aliongea yule mwanamke akimulekeza Glory kwa mkono kuwa asogee kwenye mgawaha wa uliokuwa mbele kidogo.Glory aliishiwa maneno alisogea mbele na kujaribu kuomba tena,bahati nzuri kazi aliipata.Alianza kufanya kazi kwa bidii zote,wiki moja iliisha bado alijitahidi sana kufanya kazi, licha ya kuwa na mtoto,mwezi mmoja uliisha hapo alipewa hera yake elfu therathini,alifurahi sana,kidogo mateso alianza kuyasahau.Baada ya miezi mitatu Glory alikuwa mwenyeji tayari,watu wengi walimpenda kutokana na upole wake,jambo lile lilianza kuvuta wateja,wateja walizidi kuongezeka kila kukicha na wote hao walivutiwa na Glory.Baada ya miezi sita Glory kuna kitu alikiona ndani ya ule mgahawa kilichoanza kumpa hofu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment