Search This Blog

Friday, November 18, 2022

MASKINI MAYASA - 4

 






Simulizi : Maskini Mayasa

Sehemu Ya Nne (4)





Siku moja Damaso alipigiwa simu na bibi yake akimhitaji aende huko kijijini. Damaso alipanga safari ya kwenda huko, alipofika alikaribishwa kwa furaha sana na bibi yake. Hata Damaso alishangaa sana.

"mmmh bibi leo una furaha sana,kulikoni? Au kuna zawadi yangu nni,?"

"ulijuaje? Kuna bonge la zawadi ipo kwa ajili yako"

"Weee, iko wapi niione?"

"usiwe na papara, zawadi ipo na nakisubiri"

"Aya nasubiri"

"vipi mnaendeleaje na mkeo?"

"salama kabisa"

"Nasikia mkeo ana mimba nyingine..!"

Hapo Damaso akashtuka sana, kwani jambo la mimba hakuna yeyote anayejua zaidi ya yeye na Mayasa tu.

"Aaah ni kweli bibi, leo ndio nilipanga nije kuwaambia lakini kumbe mnazo taarifa! Aliwaambia Mayasa?"

Bibi Damaso akacheka kisha akasema kuwa ni Mayasa ndiye aliyesema kuwa ni mjamzito.

Damaso alishangaa moyoni mwake,lakni baadae akaona pengine kweli aliwaambia. Waliongea mambo mengi sana, Damaso aliwaaga ili aondoke mjini siku hiyohiyo lakini bibi yake alimwambia alale alafu asubuhi ndipo aondoke. Damaso alikubali kwa heshima ya bibi yake.

Usiku ulipofika,kuna muda bibi Damaso alitoka na kwenda kwa jirani yao ,ndiko ambako anakaa Neema,mwanamke ambaye bibi Damaso ndiye anayemtaka awe mke wa Damaso. Kuna mipango yao waliipanga, bibi Damaso na Neema kwa siri walienda hadi katika chumba cha Damaso bila hata babu na Damaso kujua chochote.

Bibi Damaso alimwacha Neema chumbani alafu akamsisitizia kuwa hodari na mipango yao itimie kama walivyopanga. Neema naye akajawa na ujasiri mkubwa sana na kujiapiza kufanya kila linalowezekana ili kumteka Damaso.



Neema alibaki katika chumba hicho huku akiwa hana nguo hata moja katika mwili wake. Neema alipanda kitandani na kujifunika shuka vizuri kiasi kwamba mtu akiingia ni vigumu sana kubaini kama kuna mtu amelala mpaka ukisogelee kitanda ndipo utabaini.

Damaso baada ya kumaliza kula aliingia chumbani kwake.Hakuangalia kitadani na wala hakuhisi chochote ingawa alikuwa anahisi kuna harufu nzuri ya mafuta.

Damaso alivua nguo zake na kusogea kitandani. Alishangaa baada ya kuona kama kuna mtu hivi,lakini alipuuza kwani bibi yake hakusema kama kuna mtu chumbani mwake.



Damaso alizima taa na kupanda kitandani, hapo ndipo akagundua kuwa kuna mtu. Akampapasa akagundua ni mwanamke maana alimgusa maeneo ya kifuani.

"Nani wewe?"

"Neema"

"Neema ndio nani?"

"Si jirani yako hapa..."

"Umefuata nini humu,?"

"Nimekufuata wewe..."

"Mimi? Ili iweje,?"

"Aaah Damaso maswali gani hayo?"

Damaso akatoka kitandani na kwenda kuwasha taa.

"Haya uliyekuambia uingie humu ndani ni nani?"

Neema hakujibu, alitoka kitandani na kusimama mbele ya Damaso huku akiwa hana nguo hata moja mwlini mwake.



Damaso alibaki ameshangaa na huku akimkodolea macho Neema.Wakati Damaso anaendelea kushangaa, Neema alitumia muda huohuo kumvamia Damaso mzimamzima.

Damaso akaanza kujitoa mikononi mwa Neema, Katika purukushani za hapa na pale walijikuta wameangukia kitandani tena.







Baada ya wote kuwa kitandani, Damaso akajikakamua tena, akahoji tena maswali kama aliyomuuliza mwanzo. Neema hakutaka kujibu ,aliendelea kujiweka karibu na Damaso ili adhma yake itimie. Damaso baada ya kuona Neema anazidi kuwa king'ang'anizi ,alimsukuma kwa nguvu alafu akasogelea suruali yake na kuivaa harakaharaka kisha akatoka nje ya chumba chake na kwenda kumgongea bibi yake .

Bibi yake aliamka na kuja kumsikiliza Damaso ambaye wakati huo alikuwa yupo tumbo wazi.

"Bibi ndio mambo gani haya umenifanyia?"

"Yepi tena Damaso?"

"Chumbani umemweka nani?"

"Hee kumbe ndio hilo tu?"

"Sasa wewe unadhani lipi? Unamweka yule mwanamke ili kitokee kitu gani, bibi naomba nenda kamwambie aondoke kabla hata sijaenda kumdunda mangumi"

"Damaso...Damaso...unaniabisha sana, hivi yule mwanamke akiondoka hivi hivi si atakudharau? Ni mwindaji gani wewe unayemuona swala amekatiza mbele yako na kumuacha bila hata kumkata hata mkia?"

“Anidharau...asinidharau hiyo ni shauri yake, mimi ninachotaka nenda kamwambie aondoke kabla mashetani yangu hayajaamka”

“Damaso ukimwacha huyo basi kesho siku nzima atakutangaza kijiji kizima na watu watajua kuwa wewe hamna kitu”

“Mwache atangaze, sina hofu na hilo nina mke wangu ametulia tu, ila bibi leo umenichukiza sana, sasa naenda kumzaba vibao yule mwanamke na utasikia vilio muda sio mrefu ikiwa ataendelea kuwa mbishi na kutokubali kuondoka”

Baada ya kusema hayo, Damaso akatoka hapo na kuingia chumbani ambako alimkuta Neema akiwa amelala kifudifudi na kuyaacha makalio yake makubwa yakiwa wazi.

Damaso alipoingia alitulia kwanza kwanza mlangoni akimkodolea macho Neema ambaye alikaa kimitego sana.

Damaso wazo lake la kutaka kumtimua liliyeyuka ghafla, akajikuta anaanza kuyaodolea macho makalio ya Neema.

Wakati anaendelea kuyakodolea macho, simu yake iliita, alikuwa ni mke wake Mayasa. Alikuwa anamuulizia kama amekula na kumtakia usiku mwema. Baada ya kumaliza kuongea naye, akili za Damaso zikarudi katika hali yake ya kawaida. Akasogea kitandani na kumwamsha kwa nguvu huku akimwamuru atoke nje.

Neema aliamka alafu akaanza kuvaa nguo zake lakini huku akisema maneno yenye kuumiza,

“kumbe ndio maana....Yale tuliyosikia ni kweli kabisa, na leo nimethibitisha mwenyewe, kesho nitasimulia kwa mashoga wangu........haahaaa”

“Wewe ondoka tu na nenda kawasimulie kadri utakavyoona inafaa”

“Ndio naondoka,siwezi kubaki na kisu butu,kisu ambacho hata nyasi hakiwezi kukata, na ndio maana hata mkeo watu wanamchukua kila siku ,kumbe shida ni wewe, hata bibi kaniambia mkeo kazi yake ni kukupikia tu kazi zingine unafanyiwa na vidume.....hahaaaaa polee Damaso”

Maneno ya Neema yalikuwa mwiba moyoni mwa Damaso, Damaso alijisikia vibaya sana, akaona amedhalilishwa sana,akamshika Neema mkono na kumvuta kitandani. Damaso alifanya hivyo ili kuonesha kuwa yeye yupo vizuri na wala hana shida yeyote.

Usiku huo walilala wote hadi asubuhi. Mtu wa kwanza kuja kugonga mlango alikuwa ni bibi Damaso, Neema ndiye aliyewahi kufungua mlango.

Bibi Damaso alimuuliza kwa sauti ya chini kama washamaliza mchezo, Neema aliitikia kwa kichwa kuwa teyari mambo yameenda vizuri. Babu Damaso aliamka ,wakati anapita maeneo hayo alishangaa kumuona Neema akiwa hapo tena asubuhi na mapema kama hiyo.

Bibi Damaso ndiye aliyejibu kuwa amefika kwa bwana wake, babu alishangaa sana, akajisemea moyoni akimuona Damaso atamuuliza juu ya mambo haya.

Neema alirudi chumbani na kumkuta Damaso akiwa amekaa kitandani. Damaso alimwambia Neema kuwa hiyo ndio iwe mwanzo na mwisho wa wao kukutana kwani hakufanya hilo kwa kupenda bali ni shinikizo tu la bibi yake. Neema akamuaga Damaso na kuondoka.

Wakati wanakunywa chai, Babu alimwambia Damaso,

"Yaani mjukuu wangu kitu ulichokifanya sijapenda hata kidogo,unatambua fika kuwa una mke alafu unakuja huku unalala na mwanamke mwingine, umefanya ujinga mkubwa sana"

"Aaah! Babu mimi sija....."

Bibi akaingilia kati na kumkatiza Damaso,

"Mmmh! Wewe naye ! Mambo ya watoto hayo tuwaachie tu, mimi sijaona ubaya wowote ule uliotokea,kwanza hawa ni majirani na ukumbuke wamecheza wote tangu wakiwa watoto wadogo sana,sasa hapo mzee Nongwa unashangaa kitu gani?"

"Heee! Kumbe mulipanga hili? Hivi wewe Damaso hujui kama una mke?"

Damaso alikaa kimya,hakujibu kitu. Alikubali kubeba mzigo wa lawama wa bibi yake. Babu Damaso alimsema sana Damaso kwa jambo ambalo alilifanya. Damaso alikubali kosa na alijutia mbele ya babu yake. Baada ya kumaliza kunywa chai, Damaso hakutaka kuendelea kusubiri zaidi ,aliwaaga na kuondoka zake mjini.



Damaso alifika mjini na kuendelea na shughuli zake kama kawaida. Mwezi mmoja mbele , Mayasa akiwa na miezi miwili tangu ashike ujauzito, siku moja wakati amebaki peke yake katika nyumba waliyopanga. Alikuwa amelala, alianza kusikia sauti za ajabu sana, hakujua ni sauti za watu ama wanyama. Akaamka na kuchungulia dirishani, hakuona kitu zaidi ya watu tu ambao walikuwa wanakatiza na safari zao.

Akaanza kuhisi kizunguzungu, alipojaribu kuangalia mbele aliona giza tu, hakuona mbele. Dakika moja mbele alianza kuhisi kuna mtu anamshikashika katika tumbo lake. Hapohapo akaanza kuyahisi maumivu ya tumbo chini ya kitovu.

Maumivu hayakuwa ya kawaida, yalimtesa sana, alilia kwa uchungu sana, na wakati huo Damaso alikuwa mbali sana na kwao, maumivu aliyoyapata hakuweza hata kuinuka,alitamani kumpigia simu Damaso lakini hakuweza kutokana na maumivu makali ambayo yalimwandama ma mbaya zaidi watu wote hawakuwepo, alibaki yeye tu siku hiyo.

Mayasa alianza kukiona kifo kinakuja mbeleni mwake, zilipita dakika thelathini ,bado Mayasa hakupata msaada wowote. Ndipo mama mmoja ambaye ni jirani yao alirejea, wakati anapita jirani na chumba cha Mayasa ndipo akamsikia mtu analalamika. Ikabidi aende ndipo akamkuta Mayasa hajiwezi kabisa, analia huku akiwa ameshika tumbo.

Akatoka nje na kuita bajaji, wakampeleka hospitali ya wilaya. Daktari baada ya kupata maelezo ya Mayasa kuwa ni mjamzito, alimfanyia vpimo na akabaini kuwa tatizo ni mimba imetungwa nje ya tumbo la uzazi.

Daktari akasema kuwa hakuna namna nyingine ya kumsaidia zaidi ya kuitoa mimba hiyo kwa njia yeyote ile ili maumivu yakome. Damaso alipata taarifa za Mayasa kuwa hospitali ,hivyo naye hakukawia sana kufika hospitali ,alimkuta Mayasa akiwa analalamika. Daktari alimpa maelezo Damaso, Damaso alichanganyikiwa sana, hakuelewa shida iko wapi hadi hayo yote yanatokea.

Daktari alifanya uwezekano wa kuitoa mimba na alifanikiwa kufanya hivyo. Hapo ndipo maumivu ya tumbo yakakoma.

Baada ya siku mbili Mayasa aliruhusiwa kurudi nyumbani . Kila mmoja alishangaa sana, si Mayasa wala Damaso. Damaso aliamua kumpigia simu bibi yake na kumpa taarifa hizo, bibi yake alishangaa sana,

“Mmmh! Damaso Damaso, huyo mwanamke ataendelea kutoa mimba zako hadi lini? Huyo mwanamke hakufai hata kidogo, ukiendelea naye huyo mambo yako mengi yataaribika, inaonesha huyo mkeo ni mchawi maana sio kawaida hayo mnayoyapata katika maisha yenu”

Maneno ya bibi Damaso yalimwingia vilivyo Damaso ,akaanza taratibu kuamini kuna namna inayofanyika hadi mimba zinaharibika. Damaso akaanza kutengeneza chuki kwa Mayasa. Hata jinsi wanavyoongea Damaso hakuonesha ushirikiano kwa Mayasa. Ilifika hatua ,Damaso alikuwa hashiriki kabisa tendo la ndoa na Mayasa. Hata muda mwingine hakula chakula kilichopikwa na Mayasa. Inaweza ikatokea usiku wote Damaso hasemi kitu chochote labda tu aulizwe swali hapo ndipo atajibu.

Mayasa aliona mambo yanazidi kuwa magumu sana kwa upande wake, aliamua kufunga safari hadi kwa dada yake, na kumweleza jinsi mambo yanavyooenda kombo. Dada yake baada ya kutafakari sana, aliona bora ampeleke Mayasa kwa Mtaalamu ambaye ataweza kugundua shida inayomkabili Mayasa.

Mayasa alikuwa anaogopa sana mambo ya waganga lakini hakuwa na jinsi alikubali jambo aliloambiwa na dada yake. Waliambiana na kukubaliana kuwa jambo hilo watalifanya kwa siri bila mtu mwingine kujua chochote ,hata waume zao hawakutaka kuwashirikisha.

Mama Vumi alimuaga mume wake kuwa anaenda kumuona shangazi yake na akamuombea ruhusa Mayasa naye kwa Damaso kuwa wanaenda kumuona shangazi yao, walisingizia kuwa ni mgonjwa. Walikubaliwa, na wakaanza safari yao ya kwa mtalaamu. Walikodi pikipiki maana mtalaamu huyo alikuwa anakaa mbali na mjini.





Safari ilifanikiwa walitumia mwendo wa dakika kama thelathini hivi hadi kufika kwa mtalaamu.

Walipofika walioneshwa sehemu ya kukaa,baada ya kukaa, mganga alianza kupiga ramli. Akayapandisha maruhani yake. Akaanza kuongea kwa lugha yake ambaye aliifahamu yeye mwenyewe lakini pembeni yake palikuwa na msaidizi wake ambaye alikuwa anamwitikia kila alilokuwa analisema.

Baada ya dakika kumi hivi, mganga akatulia kwa dakika moja na baadae akarejea katika hali yake. Yule msadizi wake akamwambia yale yote ambayo alikuwa anayazungumza. Alipomaliza kumwelezea, mganga akawageukia akina Mayasa na kuanza kuwaambia.

“Binti upo kwenye matatizo sana, upo katika sehemu mbaya sana, mimba zako zote zilizotoka sio kwa ajili ugonjwa wala chochote kile, kuna mtu hakupendi, hataki uendelee kuishi na mume wako, ndio maana anakutengenezea majanga kila siku”

“Mtu gani huyo babu? Naomba unisaidie nipate dawa ya kujikinga na huyo mtu”

Kama ilivyo kawaida ya waganga wa kienyeji,akacheka sana alafu akasema,

“Binti usiwe na papara,mtamjua na nitakusaidia, hii ndio kazi yetu kusaidia watu,nitakusaidia ,ondoa hofu kabisa,kila kitu kitakaa sawa tu”

Baada ya kauli hiyo mganga akavuta kioo chake alafu akaimba nyimbo mbili tatu na baada ya hapo akamwambia Mayasa aangalie kwenye kioo. Mayasa akiwa na uoga ,alichungulia kioo. Baada ya kuchungulia aliiona sura ya bibi yake Damaso,alipigwa na butwaa sana, baada ya kuiona akamuuliza mganga kama huyo ndiye mtu anayesababisha matatizo au la.

Mganga akacheka sana kisha akamwambia huyo ndiyo chanzo cha matatizo yake yote, kwani hataki kabisa kuwa na mjukuu wake Damaso.Mayasa alitaka kuhamaki lakini mganga akamtuliza na kumwambia kuwa atampa dawa lakini hapaswi kumwambia mume wake hata kidogo.

“ Unatakiwa utulie wala usiwe na papara, ukiwa na papara utaharibu kila kitu, na maisha yako yatakuwa hatarini sana, na unaweza ukapoteza maisha ukifanya mchezo, nitakupa dawa ambayo itaenda kuwa kinga yako, dawa hiyo hakikisha mumeo haioni”

Baada ya kuyasema hayo mganga,akatoa dawa na kumkabidhi Mayasa. Alafu akamwelekeza namna ya kufanya.

Baada ya kumaliza kila kitu,Mayasa na dada yake wakajiandaa kwa ajili ya kurejea nyumbani kwao. Mayasa alimwambia dada yake inabidi dawa za mganga zikakae nyumbani kwake kwani zikikaa kwake anaweza kuziona Damaso alafu ikawa tatizo juu ya tatizo Mama Vumi naye hakutaka kuzichukua kwa kuhofia bwana wake naye kuziona.

Mayasa ikabidi azibebe yeye mwenyewe na ataenda kuzitunza kwa uangalizi mkubwa sana. Walipata usafiri na kurejea nyumbani kwao. Walipofika mjini kila mmoja akaelekea njia yake, lakini kabla hawajaachana mama vumi alimsisitizia sana Mayasa kutojionesha anajua chochote kuhusu bibi yake Damaso kama walivyoambiwa na mganga.

Mayasa alifika nyumbani kwake na hakumkuta Damaso, akaificha dawa vizuri sana katika begi lake, alifunua katikati ya nguo zake na kuiweka.

Damaso aliporudi hakuweza kubaini chochote, alimkuta Mayasa akiwa anapika chakula cha jioni. Jioni walipokula, walipanda kitandani teyari kwa kulala. Usingizi ulipowachukuwa na kuwapeleka katika ulimwengu mwingine kabisa wa ndoto.

Bibi Damaso aliwatembelea kwa njia zake anazozijua, alitumia usafiri ambao hautumiwi na watu wa kawaida. Baada ya kuja katika nyumba hiyo, aliingia katika chumba cha akina Damaso. Alipoingia ndani hakuona kitu chochote wala mtu yeyote. Chumba kilikuwa cheupee yaani hakikuwa na kitu hata kimoja. Bibi Damaso kila alivyojaribu kufanya madawa yake hakufanikiwa kuona kitu.

Bibi Damaso akang'amua kuwa kuna dawa ambazo ziliwekwa kwa ajili ya kudhibitiwa. Alijaribu mara nyingi ila alishindwa kumuona Mayasa. Akaamua kurudi kwake, siku ya pili yake bibi Damaso alienda kwa wazee wenzake kwa ajili ya kuongezewa nguvu.

Mzee mmoja ambaye ndiye kinara wa mambo ya mazingara katika kijiji chao, baada ya kuangalia darubini yake ya asili, akabaini kuwa dawa ipo katikati ya begi la nguo la Mayasa. Bibi Damaso akapata wazo la kumkomesha Mayasa.

Muda huohuo akachukua simu yake na kumpigia Damaso,

“Mjukuu wangu,mimi bibi yako sitaki upate matatizo hata kidogo, jana usiku nimeoteshwa ndoto mbaya sana, nimeota huyo mwanamke wako ameenda kwa mganga kuchukua dawa ya kukuangamiza wewe”

“Mmmh! Wewe bibi.....kuniangamiza kivipi tena?”

"Yaani baada ya kuangamiza viumbe vyako viwili sasa anataka kukuangamiza wewe,mjukuu wangu sisi bado tunakupenda”

“Sasa bibi yangu,yaani ndoto tu imekufanya uniambie hayo maneno? Aaah bibi mbona unakuwa hivyo?”

“Sasa ni hivi Damaso,hebu fuatilia kwanza uone kama kweli au si kweli,mimi niliota hiyo dawa ameiweka katikati ya begi lake la nguo,kwa hiyo kama upo mbali na kwako basi kimbia urudi nyumbani ukaangalie hata kabla mkeo hajarudi”

“Mmh bibi wewe na hizo ndoto zako za ajabu ajabu mmmh”

“Damaso fanya kama nilivyokuambia na utaamini maneno yangu, mimi siwezi kukuambia habari za uzushi wakati wewe ni damu yangu”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Bibi Damaso akakata simu, Damaso alikuwa yupo kazini na hata Mayasa naye alikuwa yupo anakoshona nguo zake. Damaso akamsimulia rafiki yake wa karibu sana. Rafiki yake akasema,

“Damaso, siku zote wakubwa ni jalala na kama ujuavyo jungu kuu halikosi ukoko, mimi nadhani wewe nenda haraka nyumbani alafu kaangalie katika begi lake kama hivyo vitu vipo au la, maana unaweza kupuuza kumbe kweli hivo vitu vipo, na unaweza pia usivikute maana sio kila ndoto ina uhalisia ,wewe nenda kaone tu”

Damaso akachukua bodaboda na kuelekea nyumbani kwake. Alipofika alikuwa na shauku kubwa ya kuangalia kilichomo kwenye begi kama atakuta hivyo vitu alivyoambiwa. Alianza kupekua kwa shauku kubwa sana, kweli kama alivyoambiwa akakutana na irizi pamoja na dunguri zingine alizopewa kwa mganga. Damaso alifadhaika sana ,akatoa vitu vyote alivyovikuta na kuviweka juu ya kitanda.

Akaanza kuyakumbuka maneno ya bibi yake kuwa Mayasa anataka kumuua ,aliingiwa na jazba pamoja na hasira sana. Muda huohuo akampigia simu Mayasa akimtaka aje nyumbani. Mayasa alishangaa kwani haikuwa kawaida yake kumuita nyumbani wakati huo. Mayasa akachukua usafiri wa bodaboda hadi kwao. Alipofika hakujua kuna nini maana hakuangalia kitandani.

“Hivi wewe mwanamke unataka uiotoe roho yangu kwa kosa gani? Nimekukosea nini mimi?”

Mayasa ni kama alikuwa haelewi hivi,

“Kwani kuna nini Damaso? Mbona sikuelewi? Mbona siku hizi huishiwi visa jamani....”

“Unajifanya hujui eeeh? Hebu angalia hapo kitandani.....”

Mayasa akageuza shingo ili kuviangalia kuna kitu hapo kitandani.





Mayasa alipogeuza shingo na kutazama kitandani alikutana na vitu vyake vyote alivyopewa na mganga. Mayasa alifadhaika moyoni mwake hakujua Damaso amevionaje. Alichoshangaa zaidi ni jambo la Damaso kupekua begi lake wakati hakuwa na tabia hiyo hata siku moja.

“Mmmh! Hivi huyu alikuwa anatafuta kitu gani hadi akafikia hatua ya kupekua begi langu? Au nimuulize? Lakini huyu ni mume wangu ,siwezi kumwekea mipaka katika chumba chake,ila amezionaje hizi?lakini ngoja nimuongopee maana nikikubali hapa itakuwa tatizo kwa upande wangu”

Mayasa aliwaza moyoni mwake huku akiendelea kuangalia vitu hivyo. Damaso akasema,

“Aya ulidhani mimi narogeka eti? Haya nini hivi?”

Mayasa hakujibu kitu, akajifanya naye kushangaa sana, akasogea hadi kitandani na kuvishika shika vitu hivyo huku akiuliza swali kwa Damaso,

“Mmmh Damaso! ndio mambo gani haya? Mbona sielewi ni vitu gani hivi? Umevikuta wapi? Ameleta nani hapa?”

“Unajitoa ufahamu na kujifanya hujui kinachoendelea eti, umezoea sana kunifanya mimi mpuuzi sana? Hili begi ni la nani?”

“Ni langu”

“Vitu vilivyomo katika begi hili ni vya nani?”

“Ni vyangu”

“Aliweka nani?"

“Mimi”

“Sasa unashangaa nini?”

“Ninashangaa hivi vitu sivijui, sasa hata kama ni vyangu kama unavyoasema, mimi nimevipata wapi vitu kama hivi wakati kila siku mimi ninashinda kazini?”

“Kwa hiyo unataka kusema hivi vitu vimejileta vyenyewe katika begi lako?”

“Hapo sasa ndio sijui ”

Mayasa aliivaa sura ya ukweli, hata Damaso akaanza kuingiwa na wasiwasi na juu ya ukweli wa vitu hivyo. Mayasa aliikausha sura kau kau, kwa wakati huo hakuna ambaye angeweza kudhani kuwa Mayasa anasema uongo. Damaso kwa utulivu sana akamuuliza Mayasa,

“Sasa Mayasa kama ndio ipo hivyo, wewe unahisi huu mzigo umeingiaje humu ndani? Au ndio tumeanza kurogwa?”

“Kwakeli hili ni jambo la kushangaza sana, kama kati yetu hakuna ajuaye huu mzigo ni wa nani na umefikaje humu basi kuna mtu atakuwa ameleta, na kama ndio hivyo basi ni lazima atakuja kufuata mzigo wake”

Damaso kila alipojaribu kumwangalia usoni Mayasa ,ndipo Mayasa alivyozidi kujikausha ,Damaso akaona hana sababu ya kubishana sana na Mayasa wakati hata yeye mwenyewe hana uhakika wa akisemacho. Wakakubaliana kuwa kesho yake asubuhi na mapema kabisa wataenda kwa dada yake kuwaonesha vitu hivyo ili wakapate ushauri wa jambo la kufanya.

Waliendelea na shughuli zao hadi usiku ulipofika wakapanda kitandani na kujilaza. Mayasa hakulala mapema ,wazo ambalo lilifika kichwani mwake lilikuwa ni kuamka na kumsubili Damaso alale alafu achukue vitu vyote na kwenda kuvifukia mahali ili kupoteza ushahidi. Maana alimkumbuka mganga wakati anampa masharti kuwa dawa yake hairuhisiwi kuonwa na mtu mwingine zaidi ya yule aliyeenda kwa mganga, na ikiwa kama kuna mtu mwingine ataiona kwa bahati mbaya basi inabidi afanye kila linalowezekana kuificha dawa hiyo sehemu au kuifukia ardhini, na kama hilo halitafanyika basi atadhurika.

Mayasa aliogopa sana,aliona bora akaifukie nje kwa siri ili kujiepusha na madhara ya kukiukaa masharti. Alimsubiri Damaso hadi akiwa ameanza kukoroma kabisa. Baada ya kujihakikishia kuwa amelala fofofo, Mayasa akaamka taratibu sana na kwa tahadhari kubwa sana kwa hofu ya kumwamsha Mume wake na mpango wake ukashindikana.

Alipofanikiwa kuteremka kitandani, akavichukua vile vitu vya mganga na kutoka navyo nje kabisa ya nyumba yao. Alichukua na jembe,. Alichimba shimo ambalo lilikuwa linatosha kabisa kwa kuvizika vitu hivyo bila hata mtu mwingine kujua kuna kitu gani mahala hapo.

Alipomaliza kuchimba shimo ,kwa haraka sana alivitia katika shimo hilo na kuvifukia harakaharaka. Alipomaliza zoezi hilo akapumzika na kushukuru kwa kumaliza salama. Akachukua jembe lake teyari kwa kuondoka, alipogeuka tu nyuma alikutana na mpangaji mwenzake ambaye alikuwa anaitwa Sunir. Sunir alikuwa na asili ya kihindi lakini alikuwa ni Mtanzania wa kuzaliwa.

“Kumbe wewe binti ni mchawi kiasi hiki? Nimekufuatilia tangu unatoka ndani hadi unafukia ndumba zako hapa, sasa kesho nakutangaza kwa wapangaji wote haya mambo yako wayajue”

Moyo wa Mayasa ulichachawa kwa woga na mfadhaiko ambao hakuwahi kuupata hata siku moja, Mayasa akaona njia pekee ya kujiokoa kutoka katika aibu hiyo ni kumdanganya Sunir,akamwambia,

“Hapana Sunir huu sio uchawi,ni takataka tu nimetoa ndani ndo nimekuja kuzifukia hapa”

“Weeee! Nimekuona mwanzo mwisho, na kama ni uchafu kwa nini usisubiri asubuhi ndipo ukautupe?”

“Asubuhi huwa ninaamka mapema sana,ndio maana nimekuja kuvitupa sasa hivi ili kesho niwahi kazini"

“Sasa ili nihakikishe kama kweli ni takataka basi ngoja tufukue ili tuone, maana kila siku watu wanalalamika wanachawiwa hapa na watu ambao hawajulikani"

Mayasa aliishiwa nguvu ,kila alilojaribu kumweleza Sunir wala halikueleweka hata kidogo, Wakati huo teyari Sunir alishaanza kufukua hata kabla Mayasa hajakubali. Kwa kuwa shimo halikuwa refu sana ,Sunir alivikuta vile vitu, akawasha tochi yake ya simu na akaviona vitu vyote vizuri sana.

“Haya hivi vitu ndio takataka kweli hizi? Huu si ushirikina kabisa huu? Asee ama kweli siku za mwizi ni arobaini......leo nimekubamba, sasa hapa mguu wako mguu wangu,tunaenda kuwaamsha wapangaji wote ili wamjue mtu wao ambaye anawaroga kila siku”

Mayasa macho yalimtoka na akaanza kutetemeka,akamsogelea Sunir kwa karibu sana. Kwa haraka sana, akamsimulia kuhusu vitu hivyo,

“Sunir....sikutaka kusema ukweli mapema kwa sababu haya ni mambo ya siri, hivi ni kwa ajili ya mimi mwenyewe wala sio uchawi, kama mjuavyo nimelazwa hospitali mara mbili kwa ajili ya mimba kuharibika ,sasa hizi ni dawa kwa ajili ya kinga yangu tu”

Sunir akamuuliza kama jambo hilo analijua Damaso, Mayasa alijibu kuwa Damaso hajui chochote na ndio maana hata hapo amekuja peke yake. Mayasa akumuomba Sunir kumtumzia siri hiyo na akihahidi kumpa chochote atakachohitaji ili tu asiseme. Sunir hakuwa ameoa,alikuwa anakaa peke yake. Wakati huo walikuwa wamekaribiana sana huku upepo wa baridi ukiwa unapuliza kwa mbali. Mayasa alikuwa amevaa kanga moja tu kwani alijua hatakawia kurudi kitandani. Sunir alianza kuingiwa na matamanio ya mwili. Akajisogeza karibu zaidi na kujigusanisha na mwili wa Mayasa.

Mayasa baada ya kuona hivyo akajitoa haraka mikononi mwa Sunir na kusogea pembeni.

“Ndio nini sasa Sunir,unataka ufanye nini.......”

"Si umesema utanipa chochote? Sasa mimi nataka mwili wako mara moja tu leo, sitamwambia mtu yeyote”

Mayasa alilikataa sana jambo hilo katakata, na akasema kuwa kama atasema kwa wengine kuhusu aliyoyaona basi bora iwe hivyo kuliko kuongeza makosa mengine. Mayasa akaokota vitu vyake na kuanza kuondoka kwenda chumbani kwake.

“Kumbe wewe mwanamke unajitia jeuri eeeh,Ok ngoja tuone hasira za mkizi zitakavyomfurahisha mvuvi.....”

Mayasa hakugeuka nyuma alizidi kusonga mbele. Akaingia chumbani kwake ,alimkuta Damaso bado amelala. Alitulia kama dakika mbili hivi huku akitafakari namna ya kufanya ili aweze kuficha vitu hivyo na asivione tena Damaso. Alipanda kitandani na kijilaza kidogo, baada lisaa limoja mbele mishale ya saa tisa,Mayasa aliamka tena na kwenda kuvichimbia sehemu nyingine. Safari hiyo alihakikisha hakuna mtu yeyote aliyemuona. Alifanikiwa kurudi chumbani kwake, wakati anaingia Damaso alikuwa teyari ameshaamka.

Damaso alimuuliza alikuwa wapi ,Mayasa alijibu kuwa alikuwa mariwatoni. Akapanda kitandani na kulala. Asubuhi ilipofika wakajiandaa kila mmoja kwa ajili ya kwenda kwa dada yake Mayasa ili kuwaonesha vitu hivyo vya ajabu. Walipomaliza kujiandaa, Damaso akaangalia vile vitu lakini hakuviona. Mayasa naye akaungana na Damaso kushangaa. Walitafuta kila sehemu ila hawakuona.

Wakati wakiwa katika mkanganyiko wa mawazo na mihangaiko ya kutafuta vitu hivyo,Sunir aliodisha chumba cha kina Mayasa. Aliingia ndani baada ya kukaribishwa na Damaso. Mayasa alishtuka sana,lakini akatulia ili kusubiri kitakachoendelea chumbani humo.





“Vipi bwana Sunir,mambo vipi?”

Damaso alimsalimu Sunir, Sunir naye akarudisha salamu,

“Mambo poa japo si sana”

“Mmmh! Vipi tena mambo yasiwe poa kwa bishoo kama wewe ,nyumba nzima wanakujua....”

“Aaah kaka bishoo wapi bana! , sema jana kuna tukio la ajabu sana limetokea....”

Damaso akajiweka vizuri ili kusikiliza jambo gani. Wakati huo Mayasa tumbo limshaanza kupata moto kwa wasiwasi. Mayasa akatafuta mpenyo na akaweza kumkonyeza Sunir huku akiashiria wazi asiseme kitu kuhusu yeye. Sunir akajifanya hajamuona Mayasa alivyomkonyeza. Sunir akaendelea mbele,

“Hivi kaka wewe unaamini kama uchawi upo?”

“mmmh! Sunir mbona hili mpya? Hujawi kuniuliza kitu kama hiki,kuna nini kwani?”

Mayasa akamkonyeza tena Sunir ili aache kuendelea kusema na akionesha waziwazi kuwa yupo teyari kumpa chochote atakachohitaji. Sunir akaendelea kujifanya hajamuona ,

“Hamna kitu kikubwa sana ila jana ,nimeona kitu cha ajabu sana, Niliamka usiku kwenda msalani, sasa wakati natoka hivi nilivyoangalia nje kupitia dirishani, kuna mtu nilimuona hapo nje akifanya mambo ya ushirikina, alikuwa anachimba na kuweka vitu vya ajabu sana....”

Damaso akamkatiza huku akiwa mtu mwenye taharuki sana,

“Eeeh kaka ni mtu gani huyo maana kuna mambo yametokea hapa kwetu.....”

Mayasa akapiga jicho tena kwa Sunir huku akionesha hofu kubwa aliyonayo juu ya jambo hilo, jicho hilo liliashiria kabisa lipo teyari kwa lolote, Sunir akatabasamu moyoni mwake na huku akianza kuamini kuwa teyari ndege mjanja amenasa katika mtego mdogo sana ambao hauhitaji hata uwe na bunduki kubwa ndipo umpige.

Sunir akaendelea mbele,

“Basi kaka yule mtu alikuwa mwanamke, nimeenda asubuhi hii kweli nimekuta shimo ila sijakuta chochote,kaka wakati wewe unalala kuna watu huwa wanakesha kukuchezea, amini usiamini tunaishi na wachawi humu ndani au jirani na hapa”

Damaso akamwangalia Mayasa na kusema,

“Unasikia mambo hayo mke wangu? Inawezekana hata vile vitu vya jana ambavyo sasa vimepotea bila shaka ndio hao hao wanaotuchezea”

Sunir hakuendelea kuongea zaidi ,baada ya hapo akawaaga na kwenda zake. Mayasa na Damaso safari yao ya kwenda kwa mama Vumi iliisha asubuhi hiyohiyo. Damaso aliona ni mambo ya kawaida hakutaka kuyaendeleza tena baada ya kuona vitu vimepotea na hata hivyo alivyosikia habari za kuonekana mtu anavichimbia chini basi akaamua kupuuza.

Kwa upande wa Mayasa jambo hilo kwake lilikuwa kama hauheni kwake kwani aliamini teyari limeshaisha na sasa ataendelea kuishi vizuri na mume wake Damaso. Baada ya safari kuhairishwa kila mmoja alielekea kazini kwake.

Mayasa akiwa njiani(wakati anatembea kwa miguu) ,ghafla akatokea Sunir kwa nyuma.

“Sasa Mayasa inakuwaje?”

“Inakuwaje nini?”

“Aaah! Mayasa! Ina maana hujui ninachokuulizia?”

“Kipi Sunir?”

“oooh! Kumbe unaona nimeshakuokoa kule teyari sasa unaanza kuleta nyodo sio?”

“Nyodo zipi tena Sunir? Haya sema unataka nini.....”

“Tukafanye mara moja tu leo kama tulivyokubaliana”

“Sasa wewe Sunir kweli unitake mimi kimapenzi ? Mimi ni shemeji yako, hivi huo ujasiri unautoa wapi? Yaani huoni hata aibu?”

“Mimi sio shemeji yako, pale tumekutana tu kama wapangaji, sasa mimi nilikusaidia kuokoa ndoa yako,kwa nini moyo wako unakuwa mgumu kusaidia wenzako?”

“Lakini Sunir mambo yameshaisha sasa kwanini bado unaendeleza? ”

“Ahadi ni deni Mayasa.....kwani ukinipa siku moja tu atajua nani?Au wewe utaumia wapi? Si kawaida tu”

“Kwako ni kawaida ila kwangu sio kawaida,na kitu kama hicho siwezi kufanya hata siku moja”

Wakati Mayasa anaendelea kuongea, Sunir akachukua simu yake na akampigia Damaso kisha akaweka loud speaker.

“Sasa kaka Damaso kuna lile jambo ambalo nimekuambia muda mchache uliopita hili la uchawi....kumbe mchawi yupo palepale”

“Eeeh ni nani tena huyo maana nina hasira naye sana.....”

Mayasa alikuwa anasikia kila kitu, akaanza kusema kimyakimya akimwambia Sunir asiseme kitu na atampa anachotaka. Damaso akauliza tena baada ya kuona Sunir yupo kimya,

“Vipi kaka mbona kimya....ni nani?”

“Aaah mbona nilikuwa naongea? Basi itakuwa mtandao unasumbua....kaka kuna jamaa yetu jirani pale alipandisha mashetani ndio akaanza kuropoka kuwa mchawi yupo palepale mtaani, ila hakumtaja jina”

Baada ya kujibu hivyo ,Damaso akamwambia Sunir kuwa watawasiliana baadae maana muda huo teyari alikuwa ameshafika kazini kwake. Sunir alikata simu na kumgeukia Mayasa kisha akamuuliza,

“Kwa hiyo?”

“Mimi nawahi kazini,nitakutafuta baadae sasa”

“Saa ngapi?”

“Saa nane”

“Poa, ukizingua hapo tusilamiane baadae”

Mayasa akachukua namba ya Sunir na kuifadhi katika simu yake kisha akaelekea kazini.

Mayasa alipofika kazini kwake, alitulia kidogo kutafakari juu ya uamuzi ambao alitaka kuuchukua, alifikiria kumpigia simu dada yake lakini akaona hakuna haja ya kufanya hivyo kwani aliona mambo yatakuwa mengi, wazo ambalo lilikuja kichwani mwake ni kulimaliza kimya kimya jambo hilo ili aendelee kuishi na Damaso.

Mayasa alikuwa anaamini kuwa Damaso ndiye mwanaume pekee ambaye anaweza kuishi naye kutokana na tabia yake kuwa nzuri. Sifa zake nyingi ndizo zilizomfanya Mayasa aendelee kuvumilia kwani mambo ambayo yamempata mengi , sababu ni kuwa na Damaso, aliona yote ayavumilie ili Damaso aendelee kuwa wake.

Moyo wake ulikuwa umegubikwa na mawazo tele,alifikiria kukataa lakini aliona atasababisha mfarakano kati yake na Damaso na aibu ya yeye kuonekana ni mchawi basi itakuwa kubwa sana.

“Bora nimpe tu mara moja alafu maisha mengine yaendelee, jambo hili simwambii mtu yeyote hata dada yangu simwambii, nitafanya siri kwa lengo kuokoa mapenzi yangu kwa Damaso”

Mayasa alijisemea moyoni mwake, alafu akaendelea na kazi zake.

Saa nane ilipofika, Mayasa akamtafuta Sunir na kumuuliza wakutane sehemu gani. Sunir alimwambia achukue pikipiki alafu ampeleke hadi katika gest ambayo ipo nje kidogo na mjini. Ilijificha mafichoni, akamwelekeza jina la gesti hiyo.

Mayasa akaomba ruhusa kwa bosi wake Mr Makalanga fundi mkuu huku akimuhaidi kurudi kabla ya saa tisa. Safari ya Mayasa hakuna ambaye aliijua ,ni Mayasa pekee ndiye aliyejua.

Mayasa alifika hadi sehemu aliyoelekezwa na kumkuta Sunir ambaye teyari alishafanya booking ya chumba. Baada ya kumpokea Mayasa ,moja kwa moja waliongozana hadi chumbani. Mlango ukafungwa na wote wakakaa kitandani.

Sunir akaanza manjonjo yake katika mwili wa Mayasa,Mwili wa Mayasa ulionekana hauko teyari kwa ajili ya tendo ambalo Sunir alikuwa anataka kulifanya,alienda hapo kwa sababu hakuwa na jinsi, moyo wake ulikuwa unamuuma sana juu ya jambo ambalo alikuwa anaenda kulifanya muda mchache ujao.

Sunir alidhamiria kutimiza alichopanga, ndani ya dakika moja,alibakiwa na boxer tu huku akianza kusaula nguo za Mayasa ambaye alionekana mwenye wasiwasi sana na hakuonesha ushirikiano kwa Sunir. Wakati Sunir akiendelea na zoezi hilo, mlango wa chumba chao ukagongwa.

“Ngo....ngo...ngo....ngo”

“Nani?"

Sunir aliuliza.

“Fungua mlango”

Sauti ya nzito ya kiume ilisema.

Moyo wa Mayasa ulifanya paaaaaa kama risasi iliyokosa shabaha na kupaa hewani. Hata Sunir naye aliingiwa na hofu.

“Fungua mlangoo”

Sauti ilirudia tena kusema.







“Nani huyo”

Kwa sauti ya chini sana ,Sunir alimuuliza Mayasa.Mayasa naye akajibu ,

“Unaniuliza mimi? Si wote tupo ndani? Mimi sijui, nenda kafungue....”

“Asee fungua mara moja....”

Sauti ikajirudia tena kusema vilevile , Sunir akiwa amejawa na uoga akausogelea mlango kisha akaufungua. Akakutana na dada wa mapokezi na wanaume wawili ambao hakumfahamu ni akina nani na hajawahi kuwaona hata siku moja. Baadae watu wakajitambulisha kuwa wao ni polisi ,kuna majambazi wanawatafuta. Waliingia katika chumba hicho wakapekua kila mahali. Baadae wakasema waendelee kisha wakaondoka zao. Sunir alibaki na Mayasa preasure ikiwa imeshuka. Wakatulia kama dakika mbili hivi bila yeyote kusema kitu.

Baadae wakaingia uwanjani kucheza mpira kama walivyopanga. Mashambulizi yalikuwa kwa timu moja kwani timu nyingine haikuwa teyari kwa mechi hivyo iliingia uwanjani kwa lazima tu kwa sababu ilipangwa kucheza mechi.

Kwa kuwa mechi ilikuwa ya upande mmoja, hata timu ya Sunir nayo iliboreka na mechi, mechi ilimalizika kwa ushindi mnono upande wa Sunir kwani yeye ndiye aliyecheza hasa.

Walipotoka hapo kila mmoja alielekea anakokujua. Mayasa alirudi kazini kwake, akatulia na kuendelea na kazi zake. Kila alipokumbuka alichotoka kukifanya na Sunir roho yake ilihudhunika sana,alijawa na kujilaumu na majuto ambayo hayakuwa na kifani.

Mayasa alipotoka kazini kwake alirejea nyumbani kwake kwa hudhuni sana, hakujua ni kitu gani kilimfanya aende kukutana na Sunir. Lakini siku zote wahenga husema majuto ni mjukuu, ndio maana huwa inasemwa sana kufikiri kabla ya kutenda.

Damaso naye aliporudi alibaini kuwa Mayasa ana tatizo maana alionekana mwenye wasiwasi iliyochanganyika na hudhuni.

“Vipi mke wangu kuna jambo lolote baya limekupata?”

“Mmmh!....hata hamna ila nawaza tu mambo yaliyotokea katika maisha yetu haya.....”

Damaso akamsogelea Mayasa huku akimshika shika kichwani na mabegani na kumwambia,

“Usijali mke wangu, wewe ndio wangu,na mimi ndio wako, haya mengine tumwachie Mungu, yale yameshapita, usiogope wala kuhuzunika kwani matatizo yanapotokea ndipo uimara unapotokea. Naamini kwa haya matatizo yanayotokea yanatufanya tuzidi kuimarika, sahau kila kitu,sikuja kwako kwa bahati mbaya....Nakupenda sana Mayasa!”

Mayasa alitokwa na machozi kwa maneno ya Damaso ,machozi yake yaligubikwa na mambo mengi sio tu maneno ya Damaso, alikumbuka pia usaliti aliotoka kuufanya siku hiyo. Machozi yalikuwa mengi hadi sura yote ililowana. Damaso aligeuka na kuwa kama mama afanyavyo anapokuwa anambembeleza mtoto usiku wa manane.

Mayasa alitulia kidogo na akaendelea na kazi nyingine ,aliingia jikoni na kuanza kupika kwa ajili ya chakula cha jioni.

Kuanzia siku hiyo, Damaso alikuwa anaonesha upendo wa kiwango cha kupitiliza, upendo wao ulioanza mwanzo ulirudia tena kama kawaida tena ulipita ule wa mwanzo. Mayasa alisahau kabisa matatizo ambayo alikumbana nayo hapo mwanzo.

Mwezi mmoja ulikatika, bibi Damaso alimwita Damaso aende kijijini kwao ,ingawa Damaso alijaribu kukataa kwa njia za mzunguko. Damaso alimwambia bibi yake kuwa yupo bussy na kazi,bibi yake akamwambia Damaso kuwa kuna jambo la muhimu sana inabidi aende akaambiwe.

Damaso alikosa jambo la kujitetea, ikabidi apange safari ya kwenda kwa bibi yake ili akamsikilize. Alipofika kwa bibi yake, babu yake hakumkuta . Alipouliza kuhusu babu yake akaambiwa kuwa ameenda kijiji cha jirani kwenye shughuli za mazishi. Damaso akatulia kusubiri aambiwe jambo la muhimu kutoka kwa bibi yake.

Bibi alimuuliza Damaso,

“Vipi lile jambo ambalo nilikuamibia kuhusu mke wako kuwa na dawa kwenye begi lake kwa lengo la kukuroga limeishia wapi ? Mbona hujanipa mlejesho?”

“Aaah bibi....yale yameisha”

“Kivipi?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Yameisha bibi hayana hata umuhimu,kwa sababu mimi mjukuu wako sijaumia popote wala kurogwa , kwa hiyo mimi naona kama halina umuhimu wa kulizungumzia....”

Bibi akatulia kidogo huku akijifanya ameelewa kilichosemwa na Damaso. Baadae bibi akamuuliza Damaso,

“Umewahi kuwasiliana na Neema?”

“Hapana....”

“Heee! Kwa nini?”

“Kwanini! Sasa mimi niwasiliane kwa lengo gani?”

“Yaani umemsahau Neema au unamaanisha nini?”

“Sasa bibi yangu nimkumbuke yeye kwa lipi hasa, mimi nitamkumbuka mke wangu na ndugu zangu wengine, sina sababu itakayonifanya nimkumbuke huyo mtu”

Bibi Damaso akiwa amekasirika akasema,

“ Yaani tangu umeanza kukaa huko mjini umebadirika sana,yaani umekuwa jeuri sana, ndio maana niliwahi kukuambia kuwa huko mjini kumekuaribu sana.....”

Damaso akajitetea kuwa hajabadirika, yupo kama zamani.Damaso alikuwa na shauku ya kutaka kujua alichoitiwa na bibi yake, bibi yake alimwambia atulie tu ataambiwa. Muda wa chakula cha mchana ulishafika, Damaso alihisi njaa, akamwambia bibi yake kama kuna chakula ampatie, bibi akasema kuwa kinaandaliwa na baada ya muda kitakuwa teyari. Damaso alishangaa jibu la bibi yake kwani muda wote alikuwa yupo naye hivyo alivyosema kinaandaliwa alishangaa sana.

Baada ya dakika tano kupita, Neema alifika akiwa amebeba chakula. Alifika nacho hadi kwa bibi Damaso na kukiweka sehemu ambayo alielekezwa na bibi Damaso. Neema akamsalimia Damaso ambaye alikuwa bado yupo katika mshangao wa anachokiona. Damaso aliitikia. Bibi Damaso akamwambia Damaso aende kula, Damaso alisita kidogo, alitaka kughairi kula ila baadae akasogea kwenye chakula.

Damaso alivyomuangalia vizuri Neema alibaini kuna utofauti katika tumbo lake, alionekana dhahiri ni mjamzito. Damaso akaanza kula huku akiwa mwenye mawazo tele.

Baada ya kumaliza kula, Damaso akatulia kwenye kiti, Neema akatoa vyombo alafu baada ya dakika mbili akarejea tena hapo kwa bibi Damaso. Bibi Damaso akaanza kwa kumpa hongera Damaso kwani anakaribi kuwa baba. Bibi alieleza kuwa tangu mimba inaanza mwezi wa kwanza mpaka ilipofikia ,yeye ndiye amekuwa karibu na Neema ,Damaso alipouliza kwanini hakuambiwa mapema juu ya jambo hilo hadi mimba inafikia kubwa kiasi hicho ,alijibiwa kuwa hata kama angeeambiwa mapema bado mambo yangebaki vilevile.

Damaso alitaka kujaribu kuikataa lakini bibi Damaso alitoa shinikizo na kumuhakishia Damaso kuwa mimba ni yake na hiyo ni bahati yake kuwa naye.

Wazazi wa Neema nao walijua kuwa Damaso amefika nao wakaja hapohapo kwa bibi Damaso. Wazazi hao walipofika walidai kuwa kwa mila na tamaduni zao ni kwamba mtoto wao baada ya kuwa mjamzito inatakiwa akaishi na mume wake kwani kwa mila zao mwanamke mwenye mimba kuishi na wazazi wake ni hatari na ni kinyume kabisa na mila zao. Kwa hiyo wakamtaka Damaso kumchukua Neema na kwenda kukaa pamoja. Damaso kila alipojaribu kuwakwepa lakini bado alikuwa anabanwa.

“Sote tunatambua kuwa una mke lakini hili jambo linatakiwa lifanyike kimila, leo hii watu wanapomuona mwanangu ni mjamzito alafu mume hajulikani ni aibu kubwa sana, kwa hiyo sisi tunakukabidhi huyu ukaishi naye hukohuko mjini”

Baba Neema aliongea, Damaso aliwajibu kuwa hayupo teyari kwa hilo kwani yeye teyari ana mke na hata hivyo hana hela ya kuweza kumpangia chumba kwani kipato chake ni kidogo sana. Bibi naye akakazia hapohapo kwa kumshawishi Damaso kwa sifa kedekede za Neema. Bado Damaso alionesha kutokubaliana nao. Baba Neema akamuuliza Damaso,

“Kijana hii mimba wakati unampa hukujua kama una mke?”

“Mimi sikumwita ,alikuja mwenyewe,muulizeni vizuri huyo mtoto wenu....”

“Hata kama alijileta mwenyewe, hivi wewe hukuwa na akili za kukataa? Kwanini unataka kumwacha mtoto wangu katika mazingira magumu? Nani unamwachia huyu wakati wewe ndiye muhusika? Kijana usipende kuchezea familia za watu,utaumia, mimi naondoka hapa kesho asubuhi nataka jibu ili nijue cha kufanya”

Baba Neema alipomaliza kusema hayo akaondoka na mwanaye Neema na akamwacha Damaso na bibi yake. Damaso mipango yake ya kurudi mjini siku hiyohiyo ilikwama. Akalazimika kumsubiri babu yake arudi alafu wajadili suala la Neema. Damaso alimpigia simu Mayasa na kumwambia hatarudi siku hiyo.



Kwa upande wa Mayasa naye alikuwa katika wakati mgumu sana kwani mwezi ulipita alafu siku zake zilipita bila kuziona. Damaso alipoenda kwa bibi yake naye akapata wasaa wa kwenda kupima kama ni mjamzito. Majibu yalionesha ana mimba ya mwezi mmoja. Mayasa alipojaribu kuhesabu siku, aligundua kuwa mwenye mimba ni Sunir. Mayasa alichanganyikiwa sana, Sunir alikuwa ni mhindi. Kwa hiyo mtoto naye atakayezaliwa lazima atakuwa na asili ya kihindi hivyo lazima itajulikana kuwa alitoka nje Damaso. Mayasa alichanganyikiwa sana,majuto ni mjuu,! . Mayasa sasa akaamua kumpigia simu dada yake na kumwambia kuwa ana matatizo hivyo alimuomba dada yake aende kwake siku hiyo hiyo ili akamweleze.





Dada yake alitaka kukataa mwito huo lakini Mayasa akalazimisha sana hadi ikamfanya dada yake ajue kweli tatizo ni kubwa sana. Akapanda bodaboda na kufika nyumbani kwa Mayasa kwa haraka sana. Baada ya kuhodisha aliruhusiwa kuingia na alimkuta Mayasa akiwa amelala lakini macho yakitazama juu.

“Vipi mdogo wangu kuna nini? maana umenishtua kweli....”

Mama Vumi alisema mara baada ya kuingia ndani tu. Mayasa hakujibu kitu zaidi ya kutikisa kichwa tu. Mama Vumi akauliza tena,

“Shemeji yuko wapi au hajarudi kazini?”

Mayasa akajiinua na kumwonesha karatasi ya majibu ya vipimo vya mimba. Mama Vumi aliisoma na kuanza kufurahi sana.

“Jamani Mayasa unanishtua na mimi nakuja hapa mkukumkuku bila hata kujiandaa kumbe jambo lenyewe ni la heri hivi! Sasa mimba ndio tatizo?”

“Dada yangu ni majanga juu ya majanga, tulia kwanza nikuambie majanga yenyewe, Shemeji yako yupo Kijijini kwa bibi yake,sijui hata nianzie wapi kukueleza.....”

“Heee mbona unanitisha, ni matatizo gani yamekukumbuka ndugu yangu.....?”

Mayasa akaanza kumwelezea dada yake matukio yote kuanzia siku ile wanatoka kwa mganga hadi kukutana na Sunir na matokeo ya kukutana kwao.

Baada ya kumaliza kusema tu ,hapohapo mama Vumi akadakia,

“Heee! Yaani wewe Mayasa ndugu yangu, mbona umekuwa mjinga kiasi hicho? Kwa nini hukuniambia mapema haya mambo?”

“Aaah! Dada yangu hili limeshatokea hata kama ukiongea hadi mwakani hakuna utakachobadirisha, mimi nimefanya makosa teyari na siwezi kubadirisha labda kama siku zingekuwa zinarudi nyuma hapo angalau ningekuwa na uwezo wa kutofanya ujinga nilioufanya. Yaani hadi leo sijui kwanini nilifanya mambo yale tena mbaya zaidi sijui kwanini sikukuambia jambo hili dada yangu pengine ungenishauri na nisingefanya kitu kama hichi, dada naomba unisaidie nifanye nini maana hapa akili yote imeruka,yaani hata sijui itakuwaje.......”

“Kwani Damaso anajua kama wewe ni mjamzito?”

“Hapana hajui ,sijamwambia jambo hili”

“Na huyo Sunir anajua?”

“Hata yeye hajui ,kwanza sijawahi kumuona kwa takribani majuma matatu hivi...

Mama Vumi akatulia kidogo kama dakika moja hivi,alafu akamuuliza tena Mayasa,

“Unampenda Damaso?”

“Ndio....”

“Kabla sijasema ninachofikiria, naomba uniambie wewe unawaza nini juu ya haya?”

“Dada hapa nilipo sijui hata nikuambie kitu gani......Yaani kichwa changu hata hakina kinachowaza nipo nipo tu.....”

“Na huyo Sunir yupo wapi sasa hivi?”

“Mimi sijui ila niliwasikia wapangaji wenzetu wakisema kuwa ameenda Dar es salaam kwa jamaa zake wengine, na ilisemekana kuwa amehama moja kwa moja kwa hiyo hapa hawezi kurudi tena”

“Heeee! Majanga! Sasa itakuwaje?”

“Ndo hapo sasa nahitaji msaada wako....”

“Lakini wewe Mayasa una hatari kweli yaani mambo yameshaharibika ndio unasema ,alafu ulikubali vipi kufanya hivihivi si angalau mngetumia hata kinga .......Mmmh! Yaani wewe ndugu yangu duuuh, huu mtihani sasa......”

“Dada nimeshakuambia teyari kuwa nilifanya makosa ,mbona unazidi kunilaumu tu?”

“Yaani hapa najaribu kuangalia njia ya kukusaidia hata siioni, pengine kama huyo Sunir angekuwa bado yupo hapa basi ningekuwa na kitu cha kusema ila hapa hakuna njia nyingine ya kufanya zaidi ya kuitoa tu, maana hapo kama haitoki maana yake ukijifungua mtoto lazima atakuwa mhindi na hapo sasa mambo ndio yataharibika zaidi kwani Damaso lazima atakuacha na huyo mtoto utalea peke yako na aibu hii itaikumba ukoo wetu wote”

Mayasa alikubali wazo hilo kwa haraka sana, aliona ndio njia pekee ya kutatua tatizo hilo kwa njia hiyo. Wote wakakubaliana siku hiyo hiyo waende kwa hospitali kabla hata Damaso hajarudi. Mama Vumi akampigia simu daktari fulani ambaye anajuana naye tangu zamani. Daktari aliwaambia waende nyakati za jioni wakati yupo huru kidogo. Walisubiri hadi jioni na ilipofika wakatoka na kwenda kwa daktari. Walipofika kwa daktari , akawasikiliza shida yao na baadae akauliza swali kwa Mayasa kwamba kwanini anataka kuitoa mimba.

Mayasa akalazimika kumuelezea kila kitu daktari ili ajue kwa nini anataka kutoa mimba. Baada ya maelezo yake daktari alimuonea huruma Mayasa. Daktari akasema,

“Kutoa mimba inawezekana sana ila kuna jambo ambalo unatakiwa ulijue kabla hujafanya maamuzi”

“Ni jambo gani hilo dokta?”

“Iko hivi....utoaji wa mimba muda mwingine unaweza kusababisha ugumba, na kama ulivyosema kuwa umewahi kutoa mimba mara baada ya kugundua ipo nje ya mfuko wa uzazi, sasa hili jambo litakufanya uwe katika hatari ya kutoshika ujauzito tena, sasa kama upo teyari kwa hili sema tufanye kazi”

Mayasa akagutuka, akaogopa sana aliposikia kuwa anaweza asishike tena ujauzito. Mayasa akajikuta anamuuliza daktari kwa haraka sana,

“Sasa daktari nitafanyaje?”

Daktari akatabasamu kidogo huku akiumauma peni aliyoshika mkononi, baadae akasema,

“Binti uamuzi ni wako ,kama umenielewa nilivyokuelekeza basi hivyo ndivyo ilivyo, mimi huwa napenda sana pesa maana najua lazima mtoe ila nimekutahadharisa tu kwakuwa nimekuona una matatizo mazito, mimi sikushauri uitoe,ila kama wewe wenyewe utakuwa umeridhia.............”

Mayasa alizidi kuchanganywa na maelezo ya daktari, muda wote huo mama Vumi alikuwa yupo kimya sana, alipoona mambo yanazidi kuwa mengi akamwambia Mayasa bora waondoke na wasitishe zoezi hilo . Mayasa na mama Vumi wakatoka hospitali na kurudi kwao . Walipofika kwao walijadili sana ,mwishowe wakaona bora mimba iachwe iendelee. Kitakachotokea mbele ya safari watajua tu hapohapo cha kufanya. Mama Vumi akaondoka kwake na kumwacha Mayasa. Wakati huo teyari giza lilianza kuingia.



Kwa upande wa Damaso ilipofika usiku,ulikuwa ni wakati wa kujadili cha kufanya kuhusu Neema. Bibi Damaso alitumia nguvu zake za kumshawishi Damaso akubali kukaa naye na aikubali mimba ya Neema. Wakati huohuo babu naye alirejea kutoka kwenye mazishi. Baada ya kutulia akaambiwa kuhusu Neema. Alishangaa sana habari hizo kwani yeye hakuzijua hata kidogo na hii ni kwa sababu habari zote za Neema zilikuwa chini ya bibi Damaso.

Mara nyingi bibi Damaso alikuwa na nguvu sana za ushawishi, kila analosema ndilo linaloenda kufanyika hata Mzee Nongwa mwenyewe amekuwa akilazimishwa baadhi ya mambo na mwishowe huyakubali hata kama hakupenda.

Ingawa babu Damaso naye alitaka kutia ngumu ila baadae akaungana na mkewe na mwishowe wote wakakubali kama ujauzito ni wa Damaso na kuanzia muda huo atakuwa anauhudumia. Hata asubuhi ilipofika ,baada ya familia akina Neema kuwasili, Damaso hakuwa mbishi tena, alikubali moja kwa moja kuwa atahusika kwa asilimia mia moja kwakuwa kiumbe kilichopo tumboni ni chake.



Siku hiyohiyo jioni Damaso aliwaaga ili arejee mjini na kuhaidi mara baada kufika huko ataandaa mipango kwa ajili ya kumuita Neema mjini. Damaso alifika mjini na kuendelea na kazi zake kama kawaida. Hakuna aliyemwambia mwenzake kuhusu jambo ambalo amelifanya. Kila mmoja nafsini mwake alihudhunika na kujiona mkosaji mbele ya mwenzake. Moyo ni kichaka, kama mioyo ya watu ingekuwa inafunguka na kuonekana na kila mtu basi hakika wale uliowadhani ndio wenyewe ukiwaona unaweza ukatoa machozi hadi ukatengeneza mto au ziwa kwa yale utakayoyaona ndani ya moyo wake.

Usaliti uliofanywa na kila mmoja kwa mwenzake ulipelekea kila mtu kuongeza upendo kwa mwenzake ili tu asionekane au asilete hofu mpaka akasababisha kutiliwa wasiwasi. Mapenzi yao yalikuwa mazito hadi ikapelekea Damaso akamsahau kabisa Neema. Neema kila alipojaribu kumpigia simu Damaso, Damaso hakupokea na hata sms hakuzijibu.

Kimya kilipozidi , Neema alifunga safari hadi mjini anakoishi Damaso kwa lengo la kuonana naye. Alielekezwa mitaa anayoishi ila nyumba ndio hakuijua. Neema alipofika mitaa aliyoelekezwa ,akaanza kuulizia jina la Damaso na kazi yake ili iwe rahisi kumpata. Katika kuzunguka zunguka, alikutana na Mayasa.

“Samahani dada, ninamuulizia mtu mmoja hivi anaitwa Damaso,nasikia anaishi mitaa hii”

“Yupoje huyo?”

“Ngoja niseme hivi ,yeye ni fundi selemala”

Mayasa aliposikia hivyo akajua kuwa mwanamke huyo ni mteja anamtaka Damaso kwa ajili ya ufundi, akaongozana naye kuelekea nyumbani kwake ili akamuone Damaso kama ndiye yeye au la.







Hakuna aliyewaza chochote kwa mwenzake ,kila mmoja alijua amekutana na mtu ambaye anamfahamu Damaso kijuujuu na wala sio kiundani. Waliendelea na safari bila kuongea. Hatimaye walifika kwa Damaso. Damaso alikuwa yupo ndani, wa kwanza kuingia chumbani alikuwa Mayasa. Baada ya kuingia akamwambia Damaso kuwa kuna mgeni wake yupo nje. Damaso bila kujua chochote akamwambia Mayasa amruhusu mgeni aingie ndani.

Mayasa akafanya kama alivyoambiwa,Neema alipoingia,Mayasa akasema,

“Dada.... huyu ndiye Damaso ,sasa sijui ndio huyu au nimekosea....”

Damaso alipomuona Neema, alichanganyikiwa sana. Hofu ilimjaa lakini akajaribu kujikaza ili Mayasa asijue chochote kinachoendelea na wakati huo alikuwa anawaza amefikaje hapo. Kwa upande wa Neema alibaini kuwa Mayasa ndiye mke wa Damaso ila kwa upande wa Mayasa yeye alikuwa kipofu, hakujua chochote. Mayasa aliendelea na kazi zake nyingine bila hata kuwaangalia Neema na Damaso. Neema akasema,

“Damaso nimeamua kukufuata baada ya kukuona upo kimya, nataka nijue mustakabali wa suala letu.. ...”

Mayasa aliposikia kauli hiyo akatulia , akatega sikio kusikiliza sasa Damaso atasema kitu gani.Damaso naye alipomuona Mayasa ametulia na kuwa makini kwa alichozungumza Neema,akaanza kuingiwa na hofu,akatafuta njia ya kujikomboa kutoka katika dhahama iliyopo mbeleni mwake, akaona bora sasa adanganye,Damaso akasema,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Aaaah! Dada yangu lile suala usione kimya ,nipo kwenye mchakato wa kulimalizia, nafikiri jumamosi hii kila kitu kitakuwa teyari, naomba univumilie kidogo dada yangu.....”

“Damaso mimi ni dada yako?”

Neema aliuliza swali ambalo likamfanya Damaso amwangalie Mayasa kwa jicho la wizi. Damaso akajibu,

“Neema hebu punguza hasira, kila kitu kitakaa sawa tu wala usihofu...”

Mayasa ambaye alikuwa yupo kimya muda wote aligundua kuwa Neema ni mteja wa Damaso. Mawazo ya Mayasa yakampelekea kuamini kuwa Damaso alipewa kazi na Neema na hajaikamilisha kwa wakati. Mayasa akamwambia Neema,

“Dada naomba umsamehe tu, Mume wangu alikuwa na matatizo huko kijijini kwao, ndio kwanza amerudi jana tu, mvumilie tu ataikamilisha kazi yako na utaipata”

Neema akamwangalia Mayasa huku akijisemea moyoni kuwa kama angejua yeye ni nani basi wala asingethubutu kusema kitu kama hicho. Neema akafungua mdomo wake ili aseme kitu kuhusu kauli ya Mayasa ,lakini alikatishwa na Mayasa ambaye aliwaaga kuwa anatoka nje kwenda kuosha vyombo. Mayasa akili yake haikufunguka na kuwaza kingine chochote, kwa asilimia mia moja alijua kuwa Neema ni mteja wa Damaso.

Baada ya Mayasa kutoka nje hapo ndipo Damaso akapata wasaa wa kupumua kidogo, akaanza kumuhoji Neema amefikaje hapo na kwa nini afike hapo bila hata taarifa. Neema kwa kujiamini sana tena miguu yake akaipandisha juu kitanda na huku kiwiliwili kikiwa juu ya sofa, Neema akasema,

“Dawa ya moto ni moto, wewe si ulidhani umenikomoa sana, sasa mimi ndio nimekuja hivi,tutalala wote kitanda kimoja na utaanza kunipa huduma na kukihudumia hiki kiumbe chako”

“Sasa wewe unajua kabisa mimi ninakaa na mtu hapa,kilichokufanya wewe uje moja kwa moja hadi hapa ni kitu gani? Si bora ungenipigia hata simu?”

“Heee! Kuna kosa kwani? Mimi nimekuja kwa mume wangu sasa nipige simu ya nini? ”

“Neema nakuomba uondoke usije ukaniletea balaa hapa.....”

“Niondoke? Niende wapi? Nyumbani wamenifukuza kwa ajili yako ......sasa unaniambia niondoke ili niende wapi ....Nakuambia mimi ndio nimeshafika hivi na hapa siondoki”

Maneno ya Neema yakamvuruga kabisa Damaso, walibishana hadi Mayasa akamaliza kuosha na kurudi tena chumbani na kuwakuta bado wababishana. Mayasa akamuuliza Damaso,

“Kwani Damaso kuna shida gani? Muda wote huo bado hamjaelewana tu? ”

Damaso akiwa mtu mwenye tahadhari sana akasema,

“Aaah! Mayasa sijui hata nifanyaje hapa, mimi nimemwambia kuwa asubili hadi kesho au keshokutwa nitakuwa nimemaliza kazi yake lakini yeye ananiambia hadi tuende ofisini akaone kama nimeanza kutengeneza”

“Sasa hilo tu Damaso ndio mnabishana muda wote huu? Si bora ungeenda kumuonesha tu hiko kitu chenyewe?”

“Yaani nimechoka kweli ila ngoja niende tu nikamuoneshe ili aridhike.....”

“Ndio ni kweli, bora ufanye hivyo”

Damaso akafurahi moyoni, akaona ameshakivuka kiunzi hicho. Kwa upande wa Neema alikuwa anawaza kumshushua Damaso hapo hapo kuwa yeye sio mteja kama Mayasa anavyodhani bali yeye ni mpenzi wa Damaso. Damaso alivyomwangalia Neema alimuona ana kila dalili za kukataa kutoka hapo. Damaso ikabidi atumie mbinu mbadala,akanyanyuka huku akimuhimiza Neema naye aamke ili wawahi ofisini. Neema akaona kwakuwa ameshapajua kwa Damaso basi bora atoke na Damaso alafu akamsikilize atakachokisema.

Neema na Damaso wakatoka, walipoiacha nyumba yao,Damaso akaanza kufoka kama nyoka,tena akitamani na kumpiga na makonde ila maneno ya Neema yakamtuliza Damaso na kumfanya atulie na kuwa mpole kama pale ambapo bahari hutulia na kuwa shwari.

“Kwa hiyo Damaso busara zangu za kutosema mimi ni nani kwa yule kinyago wako ndio sasa unaanza kunipanda kichwani eti? Sasa ngoja nikuoneshe kuwa mimi ni jeuri ngoja niende kule nikamwambie ukweli yule kinyago wako”

Damaso alikuwa mpole kwa kauli ya Neema, alipomuuliza amefikia wapi hapo mjini ,Neema alijibu kuwa mjini hakuwa na jamaa mwingine zaidi ya Damaso. Wakati huo teyari ilikuwa jioni,Damaso akalazimika kwenda kumtafutia chumba katika nyumba ya wageni ili alale kwa siku hiyo. Damaso alifanya hivyo baada ya kusikia Neema anasema hana ndugu mwingine hapo mjini. Hivyo alifanya jambo hilo ili ajipumzishe kwa siku hiyo na asubuhi aondoke kwakwe kijijini. Baada ya kupata chumba ,Damaso akamuaga Neema ili arudi kwake. Neema akang'aka kama mbogo akiwa nyikani baada ya kujeruhiwa,

“Hivi wewe mwanamume ni chizi au? Sasa hapa unataka uondoke alafu mimi nibaki na nani? Una akili kweli wewe? Kama unaondoka basi tuondoke wote.....”

“Heee! Neema jamani, wewe si umemuona mke wangu pale nyumbani sasa nikibaki hapa itakuwaje,tafadhali naomba uniache kesho mimi nitakuja hapa na tutazungumza vizuri ”

“Aya nenda.....ila kama umeamua leo tulale watu watatu kwenye kitanda kimoja basi wewe niache tu hapa,matokeo utayapata baada ya muda mfupi tu”

Damaso akasita kidogo,akajaribu kumshawishi kwa kila njia lakini alishindwa, Neema alikuwa king'ang'anizi kama kupe. Damaso akalazimika kutulia na Neema mpaka ilipofika saa tatu usiku. Mayasa alimsubiri sana Damaso lakini hakutokea. Ilipofika majira ya saa nne usiku Mayasa akaamua kumtafuta kwenye simu. Wakati Mayasa anapiga simu, Damaso alikuwa yupo bafuni kwa hiyo simu aliiacha chumbani ambako yupo Neema. Neema alivyosikia simu inaita akaona jina la Mke Wangu, akaiopokea,

“Haloo”

“wewe nani umepokea simu ya bwana wangu?”

“Na wewe ni nani unayepiga simu ya bwana wangu?”

Damaso alikuwa anasikia, alipoona hivyo akatoka mkukumkuku na kumnyang'anya simu Neema, alipoangalia jina akaona ni Mayasa. Damaso akatumia akili za kuzaliwa nazo na za mtaani kutatua tatizo hilo haraka sana,

“Helo Mayasa.....”

“Heloo nani? Yaani wewe Damaso mpaka sasa hujarudi nyumbani? Umeamua leo kuwapa simu hao malaya wako?”

“Mayasa....Mayasa...malaya niwatoe wapi mimi!”

“sasa huyo aliyepokea simu ni nani?”

“Aaaah! Mayasa huyu ni yule mwanamke ambaye nimetoka naye hapo nyumbani, nakuambia amenikomalia hapa hadi nimalize kazi yake, daah mambo ya kuchukua kianzio haya sio mazuri asee, alikuwa anakutania tu......”

“Sasa kwa nini apokee simu yeye wakati simu ipo mfukoni mwako?”

“Simu niliiacha karibu naye wakati mimi ninaendelea na kazi, sasa simu iliita muda mrefu hadi ikataka ikatike ndipo nikaamua kumwambia apokee......”

“Ooooh! Hapo sawa! Maana moyo ulikuwa unaenda mbio kweli kweli, sasa utarudi kweli?”

“Lazima nirudi mke wangu, ila kama nikichelewa sana basi nitalala kwa jamaa yangu hapa maana yeye huwa anaishi jirani tu na ofisi yetu, wewe funga mlango ,nitakaporudi nitakushtua.....”

“Aya poa... ”

Damaso akamaliza mchezo, akajua sasa hatakuwa na lawama zozote hata kama akirudi kesho yake. Baada ya kukata simu akamgeukia Neema na kuanza kumlaumu kwa alichokifanya. Neema alikuwa hana wasiwasi hata kidogo, alipomaliza kusema tu, Neema akasema,

“Sasa ndugu yangu tabu yote hiyo unayojipa ya nini? Si umwambie tu ukweli kuwa upo na mke wako mwingine? Hivi utaendelea kudanganya hadi lini? Ukweli humfanya mtu kuwa huru , wewe kama huwezi kusema ukweli ngoja mimi nikaseme ukweli kulekule,hiyo kazi nitaifanya kesho mimi mwenyewe.......”

Damaso akajishusha na akajinyenyekeza ili kumtuliza Neema,Neema akajifanya kumsikiliza na kumwelewa Damaso haliyakuwa moyoni alikuwa akisema,

“Funika kombe mwanaharamu apite”

Usiku ulipita Damaso akiwa na Neema, walilala wote kitanda kimoja. Asubuhi ilipofika , Damaso akalazimika kumpa nauli Neema ili arudi kwao. Neema alikataa katakata huku akimlazimisha Damaso ampangie chumba mjini huko huko na sio kurudi kijijini kama Damaso anavyotaka. Neema alipoona Damaso anazidi kuwa king'ang'anizi,ikabidi akubali ili amfurahishe lakini Moyoni akiwa na jambo ambalo alihisi akifanya basi atamkomoa Damaso.

Damaso akamsindikiza Neema hadi kituo cha mabasi ya kwenda kijijini kwao. Alipoona amepanda kwenye gari,Damaso akaondoka na kurejea nyumbani kwake. Alimkuta Mayasa akipika chai,Mayasa alimuonea huruma sana Damaso maana alikuwa anaonekana dhahiri kuwa amechoka. Haraka haraka akaanda maji ya kuoga. Damaso akaingia bafuni na kuoga. Alipomaliza ndipo Damaso akaanza kuurudia uongo wake wa jana.

Wakati anaendelea kuongea,kwakuwa alikuwa usawa wa dirishani alikuwa anawaona watu wote wanaopita nje. Alimuona mtu kama Neema, akaangalia vizuri na akajihakikishia kuwa yeye ndiye mwenyewe. Neema hakwenda kijijini,kumbe wakati Damaso anaondoka naye muda huohuo akashuka na kuelekea kwa Damaso. Damaso akamwambia Mayasa kuwa akija huyo mtu basi amwambie kuwa Damaso hayupo.

Neema alitia timu hadi nyumbani kwa Damaso, akahodisha,Mayasa akatoka nje ili kusikiliza hodi ya aliyehodisha.









Mayasa alipotoka nje akakutana na Neema ambaye alionekana wazi kuwa yupo kishari shari. Mayasa akamsalimia Neema,Neema aliitikia na kuunganisha swali la kuulizia kuhusu Damaso. Mayasa bila kujua kuwa anajichimbia kaburi mwenyewe, akadanganya na kusema kuwa Damaso hayupo.

Neema akauliza swali kwa Mayasa,

“Ina maana hajarudi?”

“Ndio hajarudi ,kwani wewe ulimuacha wapi?”

“Jana nimekesha naye mbona na nimeachana naye asubuhi hii....”

“Umekesha naye? Kivipi?”

“Heee! Unashangaa kukesha? Je nikikuambia tuliyokuwa tunayafanya hadi tukaamua kukesha si ndo utachanganyikiwa?”

Majibu ya Neema yalimstajaabisha sana Mayasa, hakujua kwa nini Neema alikuwa anamjibu majibu kama hayo. Wakati huo huo Damaso alikuwa anasikia kila kitu kilichokuwa kinasemwa hapo nje. Damaso alijua teyari mambo yameharibika ,hakutaka kujitokeza haraka,aliendelea kusubiri ili aone kitakachojili kati ya Neema na Mayasa.

“Kwani wewe nani mbona unajibu majibu ya jeuri sana kuhusu mume wangu?”

Mayasa akaamua kumuuliza swali Neema baada ya kuona majibu yake ni ya kiukorofi tupu,Neema huku akiwa na sura ya dharau akajibu,

“Mimi nani? Kweli wewe chizi tena chizi haswaaa!....Yaani mpaka hapo hujui mimi ni nani? Duuh! Pole sana na kukaa kote mjini hapa bado tu unashangaa na kujiuliza mimi ni nani....haahaa kweli wewe umechelewa sana asee...”

“Wewe si ulifika jana hapa na kusema ulimpa kazi mume wangu? Mbona leo unaongea mambo yasiyoeleweka?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nani alisema maneno hayo? Si yule bwana wetu aliyesema vile kwa lengo la kukupoteza wewe,na wewe jinsi ulivyo mjinga ukakubali eti mimi ni mteja wake, sasa kwa taarifa yako usiku wote tulikuwa tunaponda raha tu wakati wewe ukiteseka na baridi peke yako, na hapa sitoki hadi arudi ,si unaona kitumbo changu kilivyojaa? Basi hii ni kazi yake nzuri aliyoifanya kwangu, hatujaanza leo wala jana ,sisi ni wa kitambo sanaa maana nakuona umeanza kuchanganyikiwa teyari, vipi una swali lingine nilijibu?”

Mayasa alichoka kwa majibu ya Neema, yalikuwa kama mwiba katika chemba ya moyo wake, alijisikia maumivu makali sana, machozi yakaanza kumlengalenga Mayasa, Damaso alichungulia kwenye mlango akaona Mayasa ameanza kutokwa na machozi, Damaso alitamani kutoka nje ili kumfuta machozi Mayasa lakini alihofia kuchanganya mafaili zaidi na kusababisha dhahama kubwa.

Neema akamwambia Mayasa,

“Yaani maneno kidogo tu unalia hivyo,je hapo utakapoambiwa kuwa sasa ondoka alafu mimi niingie si ndo utajinyonga kabisaa? Mbona mimi najua wewe ni mke wake lakini silii?.....ndivyo ilivyo kucheka na kulia si kwa mmoja tu”

Damaso hakuwahi kufikiria kama Neema ana maneno mengi kiasi hicho kwani mwanzo wakati anamuona kule kijijini alikuwa anadhani ni mpole sana lakini kwa siku hiyo Damaso aliduwaa kabisa. Neema alionekana mtoto wa mjini haswa kwa maneno yake hadi Damaso akaanza kuingiwa na hofu kwamba pengine Neema amewahi kuishi mjini.

Maneno ya Neema yakamfanya Mayasa ashikwe na hasira, alivumilia mwishowe akashindwa kuvumilia alimrushia konde moja la nguvu ambalo lilimpata mgongoni mwake na likamwangusha chini moja kwa moja. Neema alipoamka naye akamvamia Mayasa ,wakaanza kushikana shikana. Wakati huohuo wapangaji wengine wakaanza kutoka nje na kuja kuwaamua. Damaso naye alikuwa ameshatoka nje, akamshika mkono Mayasa na kumwingiza ndani. Alafu wakajifungia ndani.

Neema naye hakukubali, akaanza kugonga mlango kwa nguvu huku akimtusi Mayasa. Ilikuwa ni kituko cha aina yake, kwa jinsi Damaso alivyokawa anaheshimika katika nyumba hiyo kila mmoja alishangaa sana,hakuamini kama Damaso waliyemfahamu ndiye huyo ambaye amewagombanisha wanawake. Kila mmoja aliongea lake, na maneno yote Damaso na Mayasa walikuwa wanayasikia vizuri.

Mayasa kwa utulivu sana ,akamwambia Damaso afungue mlango na amruhusu Neema aingie ndani ili afanye analotaka maana kelele za Neema zilikuwa nyingi sana hadi zilikuwa zinavuka hadi ng'ambo ya barabara. Damaso akafungua mlango, Neema hakutaka kuingia ndani, badala yake alimtaka Mayasa atoke nje ili wapigane.

Damaso sasa akaamua kuitoa aibu yote na kuanza kutumia ubavu wake ili kutatua tatizo hilo. Akamshika mkono Neema na kumvutia ndani ,Neema alijitoa na mikononi mwa Damaso na kurudi tena nje. Bado Neema alizidi kupiga kelele ambazo zikapelekea sasa hata wapita njia nao kusimama na kujongea karibu na nyumba hiyo. Damaso akaona anazidi kuumbuka, akafanya maamuzi magumu akaamua kumshika mkono Neema na kutoka naye nje ya nyumba yao. Wakati huo alikuwa anamwambia maneno ya kulegeza na kulainisha. Damaso alifanikiwa kumtoa Neema na kumpeleka mbali kidogo na hapo kwake.

Damaso akajaribu kumuuliza ana shida gani na anataka kitu gani hasa hadi akaamua kufanya ujinga kama huo,Neema akajibu kuwa ameamua kufanya jambo alilolifanya kwa lengo la kumjulisha Mayasa kuwa asijione yeye ndiyo yeye hivyo anatakiwa atambue kuwa na Neema naye yumo. Damaso alikuwa na hasira sana, alitamani kumpiga ngumi zisizo na idadi lakini alihofia hali ambayo alikuwa naye.

“Damaso mimi sirudi nyumbani nimeshakuambia teyari, yaani hapa nataka nami unipangie chumba ili niwe karibu yako”

Neema aliongea huku akiwa anadeka sana ,Damaso hakujibu kitu,akachukua simu yake na kumpigia bibi yake. Alimuulizia habari za Neema kama ana taarifa naye. Bibi Damaso akamjibu kuwa watu wote huko kijijini wanajua kuwa Neema ameenda kwa Damaso ,bibi yake akamsihi sana Damaso ,akamwambia akubali anachosema Neema. Baada ya kuongea na bibi yake,ndio ikawa kama amelainishwa vile, Damaso alisahau kila kitu, akajikuta anakubali jambo alilosema Neema. Akampigia simu dalali wa nyumba.

Siku hiyohiyo chumba kilipatikana, Damaso alinunua godoro na kuliweka chini. Neema akaamia. Damaso akatoa akiba yake yote na akakamilisha baadhi ya vitu ambavyo vilimwezesha Neema aweze kuishi. Baada ya kukamilisha kila kitu,Damaso akarejea nyumbani kwake ili akayamalize kwa Mayasa. Alimkuta Mayasa akiwa na furaha kama kawaida, Damaso alishangaa sana, baadae Mayasa akamuuliza Damaso ,

“Vipi yule binti umemuacha wapi?”

“Ameshaondoka......”

“Kwa hiyo yule ni nani sasa?”

Damaso akaamua kumwambia ukweli kuhusu Neema. Kuanzia jinsi walivyokutana huko kijijini kwao hadi tena siku hiyo wakiwa mjini. Ingawa alimwambia ukweli kuwa ni kweli ni mtu wake ila alimficha kama bibi yake ndiye aliyesababisha wakutane na Mayasa na hata hivyo kuhusu kumpangia nyumba pia hakusema ukweli ,hapo napo alimficha na alimwambia kuwa yupo kijijini kwao mpaka muda huo wakiwa wanaongea.

Mayasa alikuwa anamsikiliza tu Damaso huku naye akifikiria kuhusu swala lake, mimba ya Sunir. Mayasa hakumhoji sana kwani hata yeye nafsi yake ilikuwa inamsuta sana kwa hiyo hata hamu ya kuendelea kuhoji hakuwa nayo. Mayasa alimsamehe moja kwa moja Damaso na jambo hilo alilikubali ,Damaso alishangaa sana kwani Mayasa hakuonesha hata hali ya kupinga wa kuleta utata.



***

Siku zilizidi kusonga huku Neema na Mayasa nao mimba zao zikizidi kukua. Neema alizoea mtaa mpya na baadae akaanza shughuli za kuchoma maandazi na sambusa. Alijizolea umaarufu mkubwa, watu wakaanza kumiminika kwake kuja kununua sambusa na maandazi.

Miongoni mwa wateja wake siku moja alifika mteja ambaye ambaye alikuwa anafahamiana naye.

“Heee! Wewe Neema....”

“Mmmh! Wewe upo?”

“Nipo sana, nilikuwa nakutafuta sana nimeenda hadi kijijini kwenu sijakupata, asee kweli binadamu hukutana ni milima tu ambayo haikutani”

“Ni kweli, unaishi wapi sasa?”

“Oooh! Hapo nyuma tu,yaani kila siku mimi huwa ninakula mgahani sasa leo nimeamua nipike chai mwenyewe,ndio nikasikia wapangaji wenzangu wanasema kuna dada anauza maandazi laini sana,nikasema ngoja nije....daaah! Kumbe nakukuta wewe?....Heee! Ajabu sana,kwa hiyo upo wapi Neema?”

“Hii nyumba unayoiona ndio naishi humo, nakaa huko nyuma ,nimepanga chumba kimoja”

Kijana huyo akanunua maandazi na baadae akamwachia namba yake na kuhaidi jioni akirudi katika mishemishe zake atamtafuta ili waonane na waongee zaidi. Neema naye akampatia namba yake, wote wakaagana na kukubaliana wakutane hiyo jioni.



***



Kwa upande wa Mayasa siku hiyohiyo asubuhi wakati Damaso na yeye wanajiandaa kwenda kazini kwao. Mayasa alimwambia Damaso kuwa anataka kumuuliza swali,Damaso alishtuka sana akatulia kwenye sofa na kumsikiliza Mayasa. Mayasa akaanza kwa kutabasamu kisha akasema,

“Hivi Damaso nikikuuliza kitu unaweza kusema ukweli?”

“Yeah,nitasema ukweli kwanini niseme uongo kwako?”

“Oooh! Nashukuru sana, swali langu ni hili, hivi Damaso ingekuwa wewe ndio mimi je ungenisamehe kwa uliyoyafanya?”

“Yaani mimi niwe wewe kivipi?”

“Yaani maana yangu ni hii, yaani wewe si umempa mimba Neema....Sasa kwa mazingira kama yako ingekuwa na mimi nimepewa mimba na mtu mwingine ambaye sio wewe na kisha ningekuomba msamaha ,je ungekuwa teyari kunisamehe?”



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Damaso akashtuka,hakujibu moja kwa moja naye akaamua kumtupia swali Mayasa,

“Mmmh! Hivi umefikiria nini hadi uniulize swali kama hilo?"

“Hata hamna kitu, kwani kuna ubaya nikikuuliza swali kama hilo?”

“Hapana sio kwamba kuna tatizo ila mifano ambayo sio mizuri na inataka kugusa hisia zetu haifai , mimi najua hilo ulilosema haliwezi kutokea hata siku moja kwa hiyo sioni hata umuhimu wa kujibu hilo”

Damaso akalikwepa swali la Mayasa,hakulijibu hata kidogo na jambo hilo likafungwa mjadala wala halikuendelea tena. Lengo la Mayasa lilikuwa kujua msimamo wa Damaso upoje kwani teyari ana mimba tumboni mwake ambayo sio ya Damaso. Mayasa alishindwa kujua msimamo wa Damaso kuhusu jambo hilo,aliendelea kuacha moyoni mwake huku akiendelea kusubiri kitakachotokea siku za usoni lakini alikuwa katika wasiwasi mkubwa sana, kila siku ipitayo alikuwa anafikilia sana kitakachotokea mara baada ya kujifungua.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog