Simulizi : Fundo La Umivu
Sehemu Ya Tatu (3)
Sababu moja wapo iliyomfanya asiwe na msichana wa malengo naye, wasichana (wanawake) wote awapatao walikuwa wakubwa zaidi yake. Pili, aliihofia jamii, kwamba msichana aliyetokanaye ni mbaya kwa sura, atachekwa. Kuhofia kuchekwa ndiyo sababu iliyoenea zaidi akilini. Huku akisahau mahusiano yadumuyo huangalia tabia. Ilivyowadia saa 4 asubuhi, akiwa ameketi bandani kwa Mkumba akibadilishana mawazo na vijana wenziye, aliitwa na mmoja wa kaka zake. Naye alitii wito. Kwa kumfuata muitaji kisha wakasogea pembeni kuteta.
“Vipi mbona mbiombio kulikoni?” aliuliza Vumilia.
“Kuna taarifa nimezisikia huko nitokako zikuhusuzo. Hivyo nikaona vyema, nikufuate ili unithibitishie.”
“Zipi hizo?”
“Nimesikia kuwa jana usiku ulikuwa na Mama Moza.”
“Yeah! Nilikuwa naye maeneo hayahaya ya sokoni. Kuna nini?” Vumilia alimuongopea.
“Kama una nia ya kumtongoza huyo mwanamke, ghairisha. Maana afya yake haiko vizuri. Inasadikika kaathirika.”
Hali fulani ya mshitiko ilimpata Vumilia. Ila hakutaka kuuweka wazi. Alionyesha ungangari kisha akaendelea na maongezi, wakati huo akili ikiwazua ujumbe alioupata. Huku akivuta na taswira kwa kina kumchambua mwanamama huyo.
“Hamna shida. Nimekuelewa,” alisema Vumilia mara baada ya maongezi kumalizika kisha akarejea pale alipokuwa ameketi.
Amani ya moyo ilitoweka. Taaarifa ya usadiki, ya kuathirika kwa yule mtu aliyelala naye jana ilimuathiri. Kila avutapo kumbukumbu, hujiona naye ashajiunga katika orodha ya watu wauguwao tatizo hilo.
“Yawezekana kweli, ndiyo maana alinikubalia kiurahisi vile. Sasa itakuaje kuhusu ajira, kama nimeathirika?” aliwaza. Huku akiendelea kumdadavua Mama Moza taswirani namna alivyo.
Vikovu vikovu vya chunusi vilivyokauka usoni, vikamthibitishia, na kumuongezea hisia yake kuwa ni ya kweli. Pasipo kupata vipimo. Ambavyo ndivyo tiba pekee ya utambuzi wa ugonjwa. Naam! Vumilia aliteseka. Mawazo yalimtesa. Kuwa kaathirika ama lah. Hadi mwili ukaanza pungua, kidogo kidogo. Lakini hakuwa na budi alilazimika kusubiri matokeo mbeleni. Kila awapo hakukosa mawazo juu ya jambo hilo. Tena amuonapo Mama Moza huongezeka zaidi, na hulianzisha wazo lingine, kuwa mama huyo kamuangamiza. Kumuuliza mwenyewe alishindwa. Kwani anaweza muuliza akamuongopea, na mwishowe tatizo akalishuhudia, itakuwa sawa na bure. Alilazimika kupambana kiume, na mawazo yote yahusuyo jambo hilo. Vyovyote itavyokuwa ajiandae kupokea matokeo. Lakini wazazi watamuelewaje? Wakati yeye ndiye tegemezi lao la baadaye? Alikuwa na mtihani mgumu. Uliomkaba koo, hivyo kuufahamu ukweli ilimlazimu. Ili apate japo amani kidogo.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kaka eh! Nasikia yule mama kaathirika?” aliuliza Vumilia, kumuuliza Mkumba, wakiwa bandani kwa Mkumba wakipiga soga za hapa na pale.
“Siwezi kuhakikisha hiyo kauli, sababu mimi sio daktari. Ila maneno ya watu wengi husema hivyo. Sababu alishawahi ishi na mwanaume aliyefariki kwa ugonjwa huo. Ukimwi!”
“Dah! Dada mzuri vile. Halafu...” alisema Vumilia lakini hakuweza malizia kauli yake. Baada ya kubanwa na chafya.
“Ndiyo hivyo ndugu yangu. Ulimwengu huu sio. Unavyoanzisha mahusiano hupaswi ingia kichwa kichwa,” Mkumba akasema pasipo kujua maneno ayaongeayo humuumiza Vumilia kwa kiasi kikubwa.
Juu ya maumivu, lakini kwa kiasi fulani alipata unafuu, baada ya huyo mtu kudhaniwa, na sio kama wana uhakika juu ya hicho kisemwacho. Siku zilizidi kusonga mbele. Mwishowe ile siku ya safari aliyohitajika kuianza safari kuelekea mafunzoni, mkoani Kilimanjaro ikawadia. Alijiandaa. Maandalizi yalivyokamilika aliondoka, hadi mjini Mtawara, ambapo alijumuika na wenziye kuianza safari pamoja. Aliondoka! Ila wazo kuhusu kuathirika halikubanduka akilini. Alienda huku akiwa anajiaminisha, ataenda na kurudi siku za karibuni, pindi akishabainika kuwa muathirika. Upande wa pili ukamuaminisha hatorudi. Atafanikiwa kumaliza mafunzo na hajaathirika. Waliondoka Mtwara na Basi la Maning Nice, lililojitahidi kuchanja mbuga na kuwawezesha kuwasili jijini Dar es salaam saa 8 mchana. Katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani. Ubungo. Walipumzika kwa muda mchache, kupata chakula kisha wakaunga safari, kwenye Basi nyinyinge iliyokodiwa kwa nguvu ya pesa waliyochanga. Kakore Trans. Kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Moshi. Safari waliianza saa 9 alasiri baada ya watu wote walivyorejea toka sehemu walizoenda kupatisha tumbo zao shibe. Wakaungana na baadhi ya raia kadhaa, kujazilizia siti zilizobaki wazi.
Safari ilikuwa tulivu. Macho yaliangaza huku na kule kushuhudia jiografia ya nchi ilivyo. Kwani ilikuwa ndiyo mara yake ya kwanza kusafiri ukanda huo. Basi lilienda kasi, wajitahidi japo kuwahi, wasifike kiza kinene. Maeneo mengine dereva alivunja sheria zitakiwazo barabarani, ili awawahishe abiria wake. Mnamo saa 6 usiku, ndipo Basi liliwasili mjini Moshi. Katika chuo cha polisi. Likapakiwa lango kuu, kisha vijana wote kuteremka. Walivyoteremka waliongozwa mapokezi, kwa mienendo ya kijeshi kuendelea na taratibu zingine. Rasmi akawa ndani ya himaya ya utawala wa chuo. Kusubiri hatma ya maisha yake, itakuaje.
Kabla mafunzo hayajaanza walishughulika na kazi mbalimbali, zilizowachukua muda mwingi, na kuwaachia muda mchache wa mapumziko. Shughuli moja wapo ni usaili. Vijana wote walisailiwa upya. Kuhakikisha nyaraka walizoingia nazo ndizo sahihi, au kuna magumashi yamefanyika. Walivyokamilisha kwenye nyaraka, walihamia kwenye vipimo vya mwili. Sehemu iliyombadili Vumilia na kumfanya mwenye majuto, mawazo mengi na unyonge uliokithiri. Hakubahatika hata chembe ya furaha pindi zoezi hilo linaendelea. Akili yake ilikuwa njia panda, upande upi atakuwepo. Kwa waathirika ama wasioathirika. Hofu tele iliongezeka, zamu yake ya upimaji ilipomfikia. Iliyoinua mapigo ya moyo na kuwa maradufu zaidi ya ilivyokuwa awali.
“Vipi kijana, mbona unatetemeka sana? Ondoa hofu chukulia ni jambo la kawaida,” alisema daktari ampimaye. Wakati huo akiwa amekamatia sindano, maalumu kwa ajili ya kumchoma Vumilia katika moja ya kidole chake, ili aweze kupata damu ya kufanyia vipimo.
Vumilia hakujibu. Alimuangalia tu yule daktari usoni, kisha kuangalia namna sindano hiyo inavyoenda kutoboa kidole chake. Namna ambavyo alizidiwa na hofu, hadi kijasho chembamba kilimtoka. Ilhali kulikuwa na kiyoyozi kilichokuwa kinafanya kazi muda wote.
“Unaweza kutoka,” alisema daktari mara baada ya kumaliza.
Aliinuka. Fikra zikiwazua matokeo. Alivyofika nje alitafuta eneo tulivu na kwenda kuketi pekee. Na kuanza upya kufikirisha akili yake toka mwanzo wa tukio hadi hatua aliyofikia.
“Lakini! Ile siku si nilitumia kondomu,” alikumbuka jambo. Lililompa ahueni, takribani sekunde thelethini baada ya hapo akarejea tena katika hali aliyonayo awali.
“.........Ndiyo nilitumia. Ila, ilipasuka pindi niko mchezoni,” aliendelea kukumbuka. Kumbukizi chungu, iliyokosesha amani ya moyo. Na raha ya maisha kwa ujumla.
Novemba 02, 2014 walianza mafunzo rasmi. Matokeo ya vipimo walivyofanya yakiwa bado hayajatoka. Huku yakikadiriwa kutoka miezi ya katikati ya mafunzo yao. Kwa kiasi fulani ilimpa matumaini. Lakini si matumaini ya kumfanya asahau tatizo limkumbalo. Alilikumbuka sana, tena zaidi ya mafunzo. Kwani, hilo ndilo lilikuwa mustakabali wa kuamua maisha yake yatakuwa vipi baadaye. Kama kujiunga katika orodha ama lah! Kufanya mafunzo na kuishia kati, hakuona kuwa na maana yoyote, pale atapobaini chanzo kilichomfanya asitishiwe mafunzo yake ni hilo tatizo. Kuathirika! Wazo jipya likaibuka. Atoroke. Ili matokeo yatapotoka, awe tayari ashaikimbia aibu, na macho ya watu, ambao watakesha kumuonesha kidole.
“Eeh! Sina njia nyingine. Inanilazimu kutoroka,” alisema kimoyomoyo, jioni moja akiwa tuli kaketi bwenini kwao pekee.
****
Mwenyezi Mungu ni muweza wa yote. Mpaji na mtoaji aamuwapo. Husimamia riziki ya mtu, kwa namna yoyote mtu huyo atayotumia ili afanikiwe kuipata. Atahakikisha inatua mikononi mwake, hata kama atafanyiwa hila na njama za ajabu ajabu na watu wenziye. Huleta kila kitu ulimwenguni. Kwa kutumia mawakala wa aina mbalimbali, na vinginevyo kwa kudra zake. Walimwengu hunena, baada ya dhiki ni faraja. Ila faraja hii haiji bure, bali ni kwa kupambana na dhiki. Hata uteseke kiasi gani, ipo siku utaonja, nuru ya unafuu, iondoayo mateso uyapatayo. Kuondoka kwake sio kwa kukaa, ili usubiri kudra zikushukie. Hapana. Njia sahihi siku zote ni kukabiliana na kile kiletacho adha. Ukishakabiliana nacho, kudra zitafuatia, kupitia kwa mawakala sahihi ambao Mwenyezi Mungu atapenda kuwatumia.
Naam! Baada ya mateso ya muda mrefu, yaliyodhoofisha mwili na uwezo wa akili, nafuu ilimvaa Vumilia. Furaha ilianza rejea, tabasamu muda wote, na uchangamfu haukubanduka. Fikra zilizokuwa zinamsumbua awali, mbali alizifukuzia. Baada ya kupata marafiki sahihi waliomfanya awakumbuke kila dakika, kutokana na wema wamtendeao. Pia, hali hiyo ilizalishwa, siku waliyofolenishwa vijana wote wa mafunzoni chuo kizima, kisha kusomewa majina ya vijana wanaopaswa kusitishiwa mafunzo baada ya kubainika wana matatizo mbalimbali ya kiafya na vyeti. Pindi majina hayo yanasomwa alikuwa kwenye fukuto la utulivu, na lundo tele la fikra, jina langu linafuatia baada ya kusomwa hilo jina. Ila hadi msomaji anahitimisha, jina lake halikuwemo. Furaha aliyonyanyukanayo hapo haikuwa ya kawaida. Alifurahi mno, ilhali wenzake walijawa na masikitiko, wenzao wanasitishiwa mafunzo, siku za mwishoni kabisa. Kuanzia siku hiyo hadi endelevu, ndipo alianza rejea kwenye ukawaida wake. Hali iliyowashangaza hata wenziye alionao kombania moja, kwanini kipindi cha nyuma alikuwa mnyonge na sasa ni mwingi wa furaha. Alivyoulizwa kulikoni. Hakusita kuwahadithia. Toka mwanzo na muendelezo wa siku nyingine pia. Simulizi iliyowapa msisimko hadhira. Na kuwashawishi kutoa pole nyingi kwake.
“Dogo, Mungu mkubwa. Usimsahau,” alisema kijana mmoja aitwaye, Tenende. Kiongozi wa kombania yao.
“Tena sana. Sasa kanifundisha kuwa makini, kwenye haya mambo. Siwezi fanya ujinga,” Vumilia akasema. Huku akitoa cheko la dhihaka.
Aliojenga nao matani waliishia kumtania. Matani yaliyozidisha furaha kwake, kuona anapendwa na kukubalika na wenziye. Hatimaye siku zilizidi yoyoma, na kuifikia ile ya kuhitimisha mafunzo yao. Ambayo ni Julai 15, 2015. Jumatano! Siku iliyozidisha faraji maradufu. Kwa kufurahia kuachana na mateso na shida walizokuwa wanazipata. Sherehe kubwa iliandaliwa, katika kusherehekea kuhitimisha mafunzo yao. Ambayo Waziri wa mambo ya ndani, Mhe. Dkt. Hijira Chambali, ndiyo alikuwa mgeni rasmi. Sherehe ilikuwa ya siku nzima. Kuanzia saa 12 asubuhi hadi, saa 12 jioni. Mara baada ya mgeni rasmi na ugeni wake kuondoka, na wageni waalikwa, wazazi na ndugu wa wahitimu nao walitawanyika maeneo ya viwanja vya chuo. Shughuli za uwanjani hazikuwa hitimisho. Hitimisho lilikuwa disko. Walilopigiwa usiku kucha, kusherehekea zaidi kumaliza kwao.
Siku iliyofuata, walipangiwa maeneo ya kazi. Ambayo kila mmoja alipaswa kwenda kuyatumia mafunzo aliyopata. Baada ya kusomewa vituo vya kazi, waligawiwa vyeti vya kuthibitisha kuwa ni wahitimu wa mafunzo ya awali ya jeshi la polisi, pia walianza rudisha vifaa vya chuo. Vitanda, godoro, vyombo vya chakula na nguo za mazoezi. Kwani walipatiwa sare mpya. Waliianza safari kesho yake, kuelekea walikopangiwa kwa Basi zilizokodishwa na uongozi wa chuo ili wakaanze rasmi majukumu. Si wote, ambao waliondoka. Wengine walisalia. Kuongezewa mafunzo maalumu walivyosomeka wapo kitengo hicho. FFU (Field Force Unit). Vumilia alikuwa mmoja miongoni mwa wasalia. Kusubiri mafunzo hayo, ambayo hayakuchukua siku nyingi kuanza. Siku moja tu, toka ile waliyoondoka wengine, yalianza. Yalikuwa mafunzo maalumu, kwenye vijana wote walioteuliwa ndani ya kikosi hicho maalumu, cha kutuliza ghasia, almaarufu fanya fujo uone, wengi wao walivyozea kuita mtaani. Walifanya mafunzo hayo kwa muda wa miezi mitano. Baada ya hapo wakasafiri kuelekea mikoani walimosomwa wakatumikie majukumu yao.
Vumilia alikuwa mmoja wa vijana waliochaguliwa kwenda kufanya kazi mkoani Dodoma. Alikuwa mtu mwenye ari ya juu, kufurahia kitengo alichopo. Kiogopwacho sana mtaani. Kutokana na sifa na tabia kemkem walizonazo pindi wawapo kazini. Maisha yalianza vyema ndani ya mji wa Dodoma. Aliifurahia kazi yake, kazi nayo ilimfurahia.
“Sasa nishapata kazi. Awali nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa ufanikishaji huu. Majukumu yanaanza rasmi sasa, katika kuitengeneza familia niitakayo,” aliwaza. Akiwa ghetoni kwake alikopanga maeneo ya Kisesa.
Umri ulizidi kumtupa mkono. Mpenzi alistahili. Ili aifikie safari ndefu ya kimaisha. Katika ukabilianaji wa takwa hilo, akawa mteja mzuri wa chakon’ chako sehemu maarufu iwapayo wadada wa mjini fursa ya kuinadisha miili yao, pale akumbwapo na haja. Kila hisia zilivyokuwa zinamtuma uhitaji wa kutoa haja zake, kimbilio lake la kwanza lilikuwa huko, kisha baada ya hapo alimtafuta msichana, wa kushinda naye siku mojamoja na sio maalumu kwa malengo ya kimaisha. Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya Vumilia, mwajiriwa mpya ndani ya jeshi la polisi.
Ilikuwa ni Januari 03, 2016. Ukongwe na uzoefu wa mazingira ulishakithiri kwa Vumilia. Au Afande Vumilia. Hakuna mtaa alikosa ufahamu, ndani ya mji huo wa Dodoma, yote ni kutokana na majukumu yao ya kazi kuwataka kuangalia usalama wa mji unavyoendelea kila baada ya saa ama siku fulani. Kaubaridi kwa mbali, ndiyo hali iliyosheheni siku hiyo. Jamapili! Jua lilimezwa mawinguni, hivyo kuwapa watu kazi ya ubashiri muda wowote mvua inaweza nyesha. Toka kulivyopambuzuka, hadi kufikia saa hilo, 3:46 asubuhi ni hali hiyo pekee ndiyo ilitamalaki. Iliyoibua mateso kwa wengi na kuwapa ulazima wa kutafuta nguo nzito kujikinga. Haijalishi wapi mtu yupo. Ndani au nje, kujikinga na nguo nzito alilazimika. Wakati huo Vumilia alikuwa ghetoni kwake. Chumba kimoja alichopanga. Kwa mkataba wa miezi sitasita, akiwa ndani ya prova kubwa lenye rangi ya uzurungi. kichwani alivaa boshori nyeusi, pasi na sahau unyayoni, alivaa soksi. Kutoruhusu baridi impige kirahisi. Muda wote alikuwa kakamatia simu ya kisasa mkononi mwake. Akiwa kitandani kaketi, akipitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuangalia yanayojiri ulimwenguni.
Alianza kupitia Instagram, akafuatia Twitter mwishoni alimalizia na Facebook. Sehemu iliyomchukua muda mwingi kuiangalia tofauti na mitandao mingine aliyoianza mwanzo. Akiwa huko, takribani dakika kumi na tano toka alivyoingia, mlio wenye uashirio wa ujumbe kuingia ulisikika. Na muonekano wa ile kurasa aliyopo ikabadilika. Baada ya namba moja kusoma sehemu yenye alama inayomaanisha ujumbe. Aliifungua. Mshangao ukamshika, kutoamini kitu akionacho. Jina la mtu aliyetuma ujumbe huo. Ila baadaye alipiga moyo konde, alifungua kisha kuanza kusoma ujumbe alioandikiwa. Upendo Mgumu, ndilo jina alilokutana nalo. Lililompa mshituko. Hata alivyosoma ujumbe alioandikiwa uliendeleza mshituko wake kwa kutoamini akionacho.
“Mambo Vumi? Wapi upo kwa sasa?” ulisomeka ujumbe huo.
Naye pasi na hiyana aliujibu. Mambo yalianza hivyo. Taratibu, pasipo haraka, wawili hao wakajikuta wameingia kwenye mawasiliano ya kina baada ya kupeana namba za simu ya mkononi. Maongezi yao yalikuwa mazuri, yaliyojaa msisimko na shauku ya kuwafanya wasiishe kuwasiliana. Kila wakumbukanapo walipigiana simu ama kutumiana ujumbe, kutakiana hali na kuelezana dhamira ya mawasiliano kwa muda huo. Kipindi hicho Upendo alishakuwa mwajiriwa ndani ya jeshi la wananchi. Kikosi cha askari jeshi wa ardhini jijini Dar es salaam. Sio kwa upande huo pekee. Upande wa pili ni mitandao ya kijamii, hasa Whatsapp. Nako walitumia kuwasiliana, na kutumiana vitu vingi vyenye kuleta faraja. Video, picha za mnato na makala mbalimbali.
“Lini unakuja Dar es salaam?” ilisikika sauti ya upendo. Akiongea na Vumilia kwa njia ya simu.
“Sijajua ni lini. Ila hakika mwaka huu, nitafika tu huko. Maana nitakuwa na safari ya kuelekea nyumbani.”
“ Fanya uje. Maana nimemiss kukuona jinsi ulivyo sasa,” alisema Upendo. Kwa sauti nyororo, legevu isisimuayo na kukonga moyo wa kidume.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hamna shida, nitajitahidi.”
Mbano wa sauti, uliotoka kwa Upendo ulipelekea kusimamisha mwenge wa Vumilia. Hisia fulani zilimshika. Zilizochangia kwa kiasi kikubwa kumwacha kwenye tafakuri kuhusu Upendo. Imekuaje msichana aliyekosa mazoea naye kipindi cha nyuma aanze kumtamkia kauli kama hizo. Alitafakari, tena kwa muda mrefu sana, hadi kufikia maamuzi sahihi, si chini ya muda wa nusu saa alioutumia. Hakikuwa kitendo cha siku moja. Kila siku lazima kifanyike. Na wala hawakushibana, kwamba mmoja tayari ashamchoka mwenziye kisa wanaongea kila siku. Hapana! Hali ilichanua kila leo, na kuwapa fursa ya kutengeneza urafiki kwa ukaribu wenye mashaka. Haikupita siku, pasipo wawili hawa kuwasiliana. Muda wote, asubuhi, mchana na usiku, tena ni usiku wa kiza kikali. Kuanzia saa 4 na kuishia saa 9 usiku, bali ilitegemeana na afya walizonazo kwa siku husika. Wakiwa na uchovu sana huongea kwa muda mfupi tu.
Akili ya Vumilia ikajenga tegemeo. Upendo ni msichana anayeweza kuwa sahihi kwake, katika safari ya kimaisha ya kutengeneza familia.
“Sipaswi kumtamkia kwa haraka. Acha kwanza nijenge mazoea ya kutosha, na nione hisia zake kama navyohisi. Endapo zitakuwa waziwazi kama hivi alivyoanza nitamalizana naye,” aliwaza.
Hisia za kumpenda Upendo zilianza ibuka. Msichana wa kisabato, wenye utawaliwo na dini. Hivyo kila kukicha walivyokuwa wanazungumza, Vumilia hakumaliza taswira kumtathmini, na kufikiria namna atavyoanza mtamkia maneno yatayomshawishi akubaliane naye. Ilikuwa shughuli pevu. Dini ikiwa chanzo. Kilichomfanya muda mwingine akate tamaa ya kufanya vile anavyohitaji. Ila moyoni aliendelea kusukumwa, atoe kero yake, nafsi iache kutapa. Itulie. Pindi akili yake ikiwa na shehena kubwa ya mawazo yamhusuyo, Aprili 16, 2016 jumamosi. Alipokea ujumbe mwingine Facebook toka kwa Sabina. Uliomtaka aeleze sehemu aliyopo, kazi afanyayo na mafanikio ya usaili yalikuaje. Maswali hayo hayakuwa kero kwake, aliyajibu, tena kwa uharaka na baadaye akaombwa namba.
“Kama una namba za Tizo naomba unipatie. Yule kijana mfupimfupi, aliyekuwa anapenda sana matani pindi tunafanya usaili. Halafu yuko wapi?”
“Yupo Zanzibar, namba yake ni...”
Maongezi yao na Sabina yaliishia hapa. Baada ya hapo, Vumilia aliwasiliana na Tizo siku zijazo kufahamu chochote kiendeleacho baina yake na Sabina.
“Ndugu vipi kuhusu Sabina?”
“Acha haraka kaka. Sina papara naye. Nitakujulisha tu siku akishaingia Zanzibar. Naamini hawezi chomoka.”
“Nami nakukubali, maana hayo ni mambo yako. Kama umezaliwa nayo vile,” alisema Vumilia kisha kikafuatia kicheko toka kwa wote.
Siku zilizidi kata. Majuma yakawadia na hatimaye mwezi. Mawasiliano baina ya Vumilia na Upendo nayo hayakuacha kuendelea. Tena yalizidi kuongeza matani, toka kwa Upendo kumuendea Vumilia, sambamba na kumbukizi nyingi ya mambo waliyofanya nyuma, pindi wako kikosi cha mafunzo Mafinga na kile cha malezi Itende.
“Mmmmh! Vumi. Ulikuwaga pono sana mafunzoni,” alisema Upendo. Kama ilivyo ada kwa sauti nyenyekevu, aliyosadiki kuwa ni mapozi pindi aulizwapo kwanini huongea hivyo.
“Acha matani yasiyo na msingi. Ulikuwa unaniona vipi? Wakati mimi nawe tulikuwa kundi tofauti?”
“Nilikuwa nakuona. Kwani kombania si ileile?”
“Sawa. Kinachonishangaza hatukuwa na ukaribu huo wa kuniambia ulikuwa unafahamu namna nilivyo.”
“Basi mimi nafahamu tambua hivyo.”
Taarifa hizo zilimtatanisha Vumilia. Ilikuwaje hadi Upendo awe na umakini wa kumfuatilia. Jambo lililomhimiza apatwe na hisia zingine. Kuwa yamkini Upendo alikuwa na mapendo naye toka muda, ila alishindwa kuweka wazi hisia zake kutokana na mazingira yalivyo kwa wakati huo. Hisia hizi alikuja zithibitisha, kwa matendo afanyiwayo kila uchao. Yaliyoongeza ukaribu, na kumpatia uhuru Upendo wa kufanya mawasiliano kwa Vumilia muda wowote ajisikiao. Waonao hawakuacha kuwa na mawazo mbalimbali kuwahusu. Kuwa ni wapenzi, ilhali wenyewe walijitambua kama marafiki. Na ndiyo kauli pekee waliyokuwa wanaitumia wakisitisha kuitana majina yao, na my dear hasa kwa Upendo achokapo kutumia majina hayo mawili ya awali.
Hiyo ndiyo ilikuwa kawaida. Iliyowaunganisha watu wengine wafahamiane zaidi kwa kutumia mgongo wa mawasiliano yao. Madam Cecy na Mwanjaa, kwa upande wa Upendo, ilhali kwa Vumilia, Upendo aliweza wafahamu Tulizo, Semeni na Lyanga. Watu hawa nao walizidi chochea, mahusiano yao yazidi kukua kwa kuwahamasisha baadhi ya mambo. Kuhakikisha hakuna utengano utaojitokeza kati yao. Ilikuwa ni Mei 25, 2016. Vumilia alipata kuwa ndani ya likizo ya dharura. Akafunga safari toka mkoani Dodoma kuelekea nyumbani kwao Mangaka mkoani Mtwara. Alionekana mwenye furaha, kwani ilikuwa safari yake ya kwanza toka awe ajirani kuelekea kwao. Kingine kilichomfurahidha zaidi. Huo ulikuwa muda mahususi wa kwenda kuonana na yule aliyekuwa anawasiliana naye. Mapema tu alivyoingia basini akamfahamisha, yuko safarini kuelekea ndani ya jiji alilopo. Achilia mbali Upendo, Sabina naye alifahamishwa ujio wa safari yake.
“Lini unakuja?” lilikuwa swali toka kwa Sabina, punde alivyotumiwa ujumbe mfupi facebook, yeye akaamua kumpigia baada ya kuchukua namba zake za simu kwenye mtandao huo.
“Hivi niongeavyo niko ndani ya basi, tushaanza safari.”
“Saa ngani unaweza wasili?”
“Nahisi kuanzia saa 8 mchana.”
“Karibu sana!” alisema Sabina, kwa sauti yenye bashasha kufurahia maongezi yao.
“Ahsante!”
Baada ya hapo wakakesha kuchati. Kwa ujumbe mfupi, kila baada ya dakika kadhaa kufahamisha wapi alipofikia. Mnamo saa 8 mchana kama alivyohisi alilifikia jiji la Dar es salaam. Na kupokelewa na mmoja wa rafikiye wa sehemu atayofikia kuishi kwa siku kadhaa ndani ya jiji hilo. Alivyopokelewa walielekea eneo husika, Kawe! Ambako hawakuchukua muda mwingi sana kuwasili juu ya foleni zilizopo jijini hapo. Walitumia usafiri binafsi wa pikipiki. Kutokana na uchovu wa safari, alioga kisha kupata chakula na mwishowe kupumzika, unyong’onyo umtoke. Alijibarazua pale kitandani, kwa mitindo mbalimbali katika hali ya kunyoosha viungo vya mwili wake na kuutafuta usingizi mororo. Muito wa simu, uashirio alikuwa anapigiwa ndiyo uliokuja kumzindua. Masaa matatu baadaye. Saa 1 usiku! Hima aliamka, alifuta uso kwa mikono yake miwili kisha alipokea.
“Mmmmmh!” alisema, punde alivyopokea simu na kuweka sikioni.
“Nishatoka kazini. Wapi nashukia ili nifike uliko?” ilisikika sauti ya Sabina.
Kwakuwa Vumilia hakuwa na ufahamu wa kutosha, alimuuliza rafikiye, alivyofahamishwa ndipo akarudisha jibu kwa Sabina.
“Naomba uje unipokee basi. Ili tuongozane sote huko ulipofikia.”
“Hamna shida.”
Akakata simu.
Haikuchukua dakika ishirini toka alivyokata siku. Muito wa kupigiwa ulisikika kwa mara nyingine. Ila awamu hii alikuwa hajalala, hivyo mapema tu aliipokea alivyobaini mpigaji ni nani.
“Nimeshafika kwenye kituo ulichoniambia. Mbona sikuoni?”
“Subiri niko karibu na hapo.”
“Fanya haraka basi ili niweze kuwahi kurudi nyumbani.”
Rafikiye, aitwaye Lupeto ndiye alienda kumpokea na kuja naye. Tabasamu lililowatoka halikuelezeka. Walitokwa na tabasamu, mithili ya watu wenye mazoea ya kina kwa muda mrefu. Walianza kwa kumbatio. Kumbatio lililochukua takribani dakika tatu kila mmoja kuachia mwili wa mwenziye, huku joto walilopata likichangia kusababisha kugandana kama ruba kwa muda mrefu. Lupeto aliwaachia uwanja. Uliowapa fursa ya kujimwayamwaya watakavyo mpaka pale wataporidhika kuhitimisha wafanyacho. Walisabahiana, kisha maongezi kuhusu mambo mengine kufuatia. Waliongea mambo mengi, habari za kipindi cha nyuma na walichopo na maulizano ya watu wengine. Wakati huo jicho lenye uchu halikuisha kumtoka Vumilia. Jicho lilikuwa pima kumuangalia Sabina namna alivyonona hali iliyoibua hisia kali za matamanio.
“Hivi nimuache kweli jinsi alivyo hivi? Nisipate japo raha murua ampazo mtu wake?” alijisemeza kimoyomoyo. Domo likiwa limejaa mate ya uchu, aliyoyameza meza kila baada ya muda fulani.
“Ila Tizo si aliniambia anataka kufanya mambo ya kikubwa na huyu binti. Wacha kwanza nimuulize, kama hilo lengo bado analo nitajua namna ya nami kutumia nafasi yangu, nipate uroda wake,” aliendelea kujisemeza macho yakiwa yametua kifuani, kuzitathmini skonzi zilivyochanua, kisha kuyapeleka macho yake kiunoni. Kuyaangalia mapaja yalivyojengeka kimvuto na ushawishi wa kumtamanisha mwanaume yeyote amuonaye.
Dhahiri! Tamanio lilimjaa. Koo likamkaba, akatapatapa akilini aanze vipi kulitamka. Hisia za kuhitaji penzi lake zilimtwaa. Lakini alishindwa kuzungumza. Hadi wanafikia ukomo wa maongezi. Ambapo Sabina aliaga na kuondoka.
“Vipi ushamaliza?” aliuliza Lupeto, punde alivyowasili baada ya Sabina kuondoka.
“Naanzaje kumaliza leoleo, ilhali ndiyo kwanza tumekuwa na mazoea ya kuongea kwa muda mrefu.”
“Humu wanawake wakija hawabanduki hivihivi. Acha uboya fanya mambo na mtoto huyo.”
“Siku bado zipo, naamini nitapata nafasi hiyo.”
Alivyomaliza tu maongezi na Lupeto alinyanyua simu na kumpigia Tizo. Alimueleza mkasa mzima kisha kumuulizia yake nia kwa Sabina kama bado ipo.
“Unaweza mchukua, mimi bado sijamtilia sana maanani,” alisema Tizo.
“Hamna noma mwanangu. Acha nikaze, nipate uhondo wa huyu kigori,” alisema Vumilia na kukata simu.
Usiku wa saa 4 wakawa kwenye ulimwengu wa mawasiliano. Kwa njia ya ujumbe mfupi. Sabina akiwa tayari ashafika nyumbani kwao. Na wote wawili wakiwa kitandani kuutafuta usingizi. Vumlia alianza kumchombeza kwa maneno matamu matamu yenye kummwagia sifa kemkem mrembo huyo, zilizompandisha kichwa na kuupa moyo nafasi ya utambuzi wa Vumilia. Chombezo lilichombezeka. Mtiririko wa majibu, juu ya maswali aulizayo, Vumilia akang’amua jambo.
“Naamini utakuwa mwenyeji wangu wa kila kitu hapa jijini,” alianza kwa kusema hivyo.
“Ondoa shaka kuhusu hilo. Wewe tena. Siwezi nikakutupa,” alijibu Sabina.
“Nafurahi sana kusikia hivyo. Na nashukuru kwa kutambua hitajio langu.”
“Hamna shida. Upo ndani ya himaya ya moyo wangu. Kuwa na amani.”
Vumilia alifurahi. Lakini swali moja likatua kichwani na kumkosesha amani. Imekuaje kawa mwepesi wa kukubali? Ama alikuwa na mapendo naye toka muda? Alikosa jibu. Kwa namna fulani ilimtengenezea tafakuri, japo kuna wakati alikuwa anapotezea. Ila kiuhalisia ilimchukua muda mwingi kupambanua ukweli ni upi. Alihofia yasije mkuta kama yaliyotokea kwa Mama Moza, ukizingatia hapo ni jijini kumejaa kila aina ya starehe. Afikiriapo habari za kinga yote hupuuzia na hamasa ya kutoka na Sabina huongezeka. Sasa Sabina naye mambo yakawa moto. Mawasiliano ya kila muda, na kila atokavyo kazini humpitia kumuona. Aligeuka kuwa faraji ya moyo wake, asipomuona haridhiki. Siku ambazo alikuwa haendi kazini, mapema tu humtembelea. Kuondoka hadi kiza kiingie. Siku kama hizo hugeuka watoto, kwa kufanya michezo mingi na yenye mahadhi ya utoto na kiasi fulani ile ya ukubwani mioyo ichangamke. Kwa siku hizo zote, ule mchezo halisi wa kiutu uzima bado haukutendeka. Kutokana na Sabina kuwa kwenye matatizo ya tumbo. Lile la kawaida kwa wanawake.
“Nenda Mangaka, ukirudi tutafanya yetu. Ama unaseamje kipenzi changu?” aliuliza Sabina akiwa kalaza kichwa kifuani kwa Vumilia.
“Sawa. Ila natamani sana ningepata uhondo wako kabla sijaondoka.”
“Sijakataa. Tatizo lililopo si umeliona. Ukisharudi, nitakuwa niko vizuri, hivyo utatumia mwili wangu utakavyo.”
“Dah! Mzuka nilionao si wa kuondoka pasipo...” alisema Vumilia ila hakuweza malizia kauli, baada ya Sabina kuufunga mdomo wake kwa kidole.
“Shiiiiii! Nenda urudi.”
Pindi hayo yote yanaendelea kwa Vumilia. Katu hakuacha mawasiliano na Upendo. Msichana pekee aliyeuteka moyo wake kwa kasi iliyokosa kifani. Mawasiliano yao yalikuwa palepale, tena ndiyo yalizidi maradufu, ila uwingi wa kazi alizonazo Upendo, ikamuwia ugumu wa kuonana.
“Vumi! Natamani nikuone, lakini nina mambo mengi sana. Hivyo nenda kwanza nyumbani. Ila uwahi kurudi kabla siku tatu hujafunga safari ya kuanza rejea Dodoma,” alisema Upendo. Pindi wakiwasiliana kwa njia ya simu.
“Unahisi kama sasa hivi imeshindikana, hiyo baadaye itawezekana?”
“Niamini Vumi. Lazima tuonane, maana kazi zitakuwa zishapungua.”
Hakuwa na budi. Pia hakutaka kuwa sehemu ya kikwazo kwa Upendo. Alihitaji apate kuwa sehemu ya faraja pekee, hivyo aliridhia matakwa aliyoambiwa. Alifunga safari hadi Mangaka, na kukaa kwa siku alizopanga baada ya hapo akaelekea Nyangamara, nako akakaa kwa siku kadhaa. Chache, kisha kurejea jijini Dar es salaam. Siku iliyofuata toka ile aliyowasili alianza wasiliana na watu wake wa karibu. Sabina na Upendo. Wa kwanza alikuwa ni Sabina. Alivyoambiwa alifurahi mno. Na kuahidi akishatoka kazini kupitia alipo apate kumuona. Upendo, alivyoambiwa, aliahidi kumtembelea jioni ya kesho yake.
Kiza kilivyoanza ingia, Sabina alitii ahadi yake. Aliwasili, huku akionekana mwenye furaha mno. Kufurahia uwepo wa Vumilia karibu yake. Kwa muda huo mchache waliojenga mazoea, Sabina alikuwa haambiliki kuhusu Vumilia. Alishatekwa akili, moyo ukamridhia, nafasi tele akatunukiwa. Ni yeye tu kuitawala atakavyo. Lupeto aliwaachia nafasi. Wawili pekee wakasalia. Nguvu za mvutano zikaanza majukumu, kuwasogeza karibu, na kugandiana. Haifahamiki ni baada ya muda gani walivua nguo na kuwa watupu, huku baadhi ya maungo yao yakikazana kutomasa tomasa sehemu mbalimbali za mwili zilizoinua msisimko zaidi na uhitaji wa kuingiliana. Sabina alilegea. Tepetepe, kila aambiwalo alitingisha kichwa kukubali ama kukataa, sauti ilimshinda kutoka. Kwani alinyong’onyea kiasi kwamba hata uwezo wa macho yake kuona ulipungua. Muda wote akiwa kakamatia jogoo anang’ang’aniza apande ulingoni kuanza pambano.
“Ingiza basi,” alisema Sabina akiwa hoi, kalegea. Jicho tepetepe, nguvu pungufu, sauti mithili ya mtu aliyeishiwa.
“Mbona una haraka hivyo?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimechoka mpenzi wangu. Pia naumia. Kwani mambo yamejazana, yanahitaji kutolewa.”
“Subiri basi, muda si mrefu nalianzisha.”
“Mmmmnnnh! Sasa hivi bana.”
“Sawa!”
Ni sauti za kimahaba pekee, ndizo zilisikika. Ulimwengu wa raha uliwagubika, ya duniani waliyasahau kwa muda. Vumilia hakuremba. Baada ya uhitaji mwingi alipanda ulingoni mtanange wa kukatana shoka ukaanza. Kila mmoja na ufundi wake, walivyokuja changanya, mambo yalinoga. Ni miguno tu ilisikika toka kwa Sabina, na milalamo ya kuomba kasi ipungue, pamoja na kubadili sehemu ya upigaji. Hasa sehemu imuumizayo aguswapo. Haina uhakika. Kama ni raha au maumivu ndiyo yalichangia sauti ya miguno na malalamo itoke. Ila nyuso zilionesha kufurahi, tena pale shambulizi la nguvu lilivyotoka na kushambulia kwa mgandamizo wa moto, walifanya kumbatio la mapokezi shambulizi lirutubishe vyema. Shambulizi lilienda sawia, pasi na kikwazo chochote. Glavus hazikutumika. Kwa kuhofia zitaharibu ladha ya pambano. Lilikuwa pambano la kavukavu.
Hadi wanafika hatimani, lilitoa matokeo ya goli mbili, zilizochangamsha mwili na kuupa wepesi. Baadaye walipata chakula, kisha Sabina alisindikizwa kuelekea nyumbani kwao mara walivyohitimisha kula. Kwa ufundi stadi alioutoa, Vumilia aliomba kurejea pambano kesho yake, ili apate uhondo zaidi.
“Kesho si tutarudia pambano?” aliuliza, wakiwa barabarani kuelekea kituoni, Sabina akapande daladala aelekee kwao.
“Hujaridhika?”
“Ndiyo. Tena ikiwezekana kesho unalala kabisa.”
“Mmmmh! Kulala tena? Sidhani kama nitaweza kulala. Nitamuagaje Mama yangu?”
“Muongopee vyovyote vile ilimradi uje kulala huku. Tufanye yetu pasipo hofu ya muda.”
“Haya nitajaribu. Ikishindikana, nitakujuza.”
“Naamini uwezekano utakuwepo,” alisema Vumilia. Kauli iliyoambatana na kusikika kwa mlio wa simu yake. Wenye kumaanisha ujumbe umeingia.
Aliitoa katika mfuko wa suruali ambako aliiweka. Alifanya ufunguzi wa vitufe na kukutana na jina la mtu aliyetuma ujumbe huo. Upendo! Hakukawiza, aliufungua, maneno machache alikutana nayo, yaliyosomeka; ‘Vumi! kesho jioni naja.’ Alivyomaliza aliirejesha mfukoni. Safari iliendelea hadi kituo cha daladala, ambapo walisubiri kwa muda mfupi, daladala ilipowasili, Sabina alipanda kisha gari ikaondoka.
“Mmmh! Itakuaje Upendo akija na Sabina naye akifika?” alijiuliza, kwa muda mwingi pasipo kulipatia ufumbuzi swali hilo. Aliichakarisha akili kufikiri. Lakini kila aling’amualo halikuwa sahihi katika halmashauri ya kichwa chake. Hatimaye ilimlazimu kumshirikisha Lupeto ampatie msaada wa mawazo.
“Kwa kuwa Sabina ushapita naye, msitishe kesho asije, ili upambane na huyo Upendo,” alisema Lupeto baada ya kuhadithiwa mkasa mzima.
“Lakini Upendo ni rafiki tu. Si mpenzi wangu.”
“Hata kama. Si unampenda?”
“Yap! Nampenda sana. Tena zaidi ya Sabina.”
“Basi fanya nilivyokuambia. Ama la sivyo, acha waje wote. Mmoja utamleta hapa mwingine, utampeleka kwa Rashid kule juu.”
Hakika! Vumilia alikuwa njia panda. Uamuzi gani auchukue juu ya kupata ushauri toka kwa rafikiye. Tamanio lake liliwahitaji wote wazuru alipo, ila wasionane. Na afanye jitihada za kubahatika kuingia himayani mwa Upendo, mwanamke aliyopo moyoni mwake. Japo kwa muda huo walitambuana kama marafiki. Kwani hakuna aliyetoa hisia za mapenzi kwa mwenziye.
“Acha wote waje,” alisema. Baada ya kufikiria kwa muda mrefu.
Jioni ya siku iliyofuata Sabina ndiye alikuwa wa kwanza kuwasili. Vumilia alifurahi, ila si sana. Akili yake ilikuwa inamfikiria na kumsubiri kwa hamu kubwa sana Upendo. Mwanamke aliyenaye mapendo ya dhati. Japo ni rafiki. Aliishi kwa imani, mahusiano ya kweli huanzia mbali. Hivyo aliamini naye, ipo siku atakuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti huyo. Yumkini, hiyo siku ndiyo mwanzo. Alipiga stori huku macho yakiwa hayabanduki simuni, juu ya skrini, kutazamia jumbe toka kwa Upendo itayomfahamisha kawasili. Ni mara chache sana, aliinua macho yake kumtazama Sabina. Ambaye aliketi mbele yake, akiandaa mboga maalumu kwa chakula cha usiku. Saa 1:10 usiku mshawasha wake ukakata. Ujumbe toka kwa mtu aliyekuwa anamsubiri ulivyoingia simuni, uliomfahamisha kashawasili. Hamu ya kuendelea na maongezi na Sabina iliishia hapo, hatimaye alimuaga kwa kumuongopea na kuondoka, kumfuata Upendo alipofikia.
Jinsi alivyotawaliwa na shauku, kutembea aliona hakumfai. Alikimbia ili awahi kufika na kufanya maongezi na mgeni wake ndani ya muda mzuri. Alivyomfikia, kumbatio ndiyo kitu cha kwanza. Walikumbatiana, huku Upendo akitomasa tomasa baadhi ya sehemu za mwili wa Vumilia. Tukio lililoambatana na kauli.
“Vumi!...Vumi!...nafurahi kukuona.”
“Nami pia.”
“Mmmmh! Mbona hujaanza niambia?”
“Hamna kilichoharibika, hata ulivyotangulia kunitamkia.”
“Haya bana. Twende tusipoteze muda.”
Walianza ondoka kwa mwendo wa mikogo. Mithili ya kinyonga. Huku mkono wa kushoto wa Upendo akiwa kaupitisha chini ya kwapa, usawa wa mbavu za Kulia za Vumilia. Maongezi muruwa, yalisindikiza mwondoko wao, vicheko na maangaliano nayo yakiwa sambamba katika hilo. Baada ya hatua kadhaa, rasharasha ilianza teremka. Iliyomhimiza Upendo kutoa khanga kwenye begi dogo alilokujanalo kisha kufunika kichwa, na sehemu ya bega zisilowane. Pia iliwafanya wakaze mwendo, kidogo na kubadili mada.
“Vumi!” aliita Upendo.
“Naam!” Vumilia aliitika na kugeuza macho kumuangalia Upendo kusubiri atachoambiwa.
“Mungu ni mkubwa. Ona anabariki upendo wetu.”
Ilikuwa kauli iliyoinua msisimko moyoni mwa Vumilia. Hakuamini, wala hakuwahi kuwa na matarajio mapema tu walivyokutana angelisikia neno hilo toka kwa binti huyo. Alishindwa hata kujibu. Aliishia kumuangalia baadaye akageuza macho yake kuangalia kule waendako. Mwendo wa robo saa walilifikia jengo husika, analoishi kijana aliyoelekezwa na Lupeto. Rashid! Vumilia alifungua na kuingia ndani. Sebuleni ndipo walifikia. Waliketi sofani kisha kutulia kwa muda, na kufanya mhemo wa nguvu, kuchangamsha mwili, baada ya hapo walianza upya stori. Mambo waliyohadithiana yalikuwa mengi, kwani hawakutulia kwenye mada moja. Mada zilikuwa nyingi, toa hii weka ile muda nao ukiwapokea kwa kuruhusu uendaji wa sekunde na kuongeza hali ya kiza. Huku utamu wa stori ukiwahimiza kuendelea.
Wakati wote Upendo ndiye alionekana kuwa muongeaji mkubwa. Vumilia alikuwa msikilisaji na kuchangia kwa kiasi kidogo pale alipohitajika. Kichwani alijawa na tathmini, kumtathmini Upendo, na kuzitathmini hisia alizonazo juu yake. Aanze vipi?
“Vumi! Muda wa kuondoka unakaribia. Ila kuna jambo ningependa kukushirikisha ili nawe unipatie mtazamo wako katika hili.”
“Lipi hilo?”
Upendo alihema kwa sekunde kadhaa, kisha alianza elezea mada husika, ya mwisho kabla ya kuondoka.
“Hivi, kufanya tendo la ndoa ni vigumu ama sio vigumu?”
“Mmmmh! Sijui hata nikujibu vipi. Kwanini umeniuliza hivyo?”
“Kuna watu wengi sana nimekutana nao wananiambia kitu hicho ni rahisi kufanya, ila huwa napingana nao. Vipi kuhusu mtazamo wako?”
“Hakika, siwezi kukujibu kwa sasa. Labda unipe muda. Una hoja ipi ya utetezi inayokufanya uamini hivyo?”
“Vumi! Tendo la ndoa ni maridhiano. Itakuaje rahisi kama hamna maridhiano? Wengine huenda mbali kabisa kwa kusema; unaweza kutana na msichana leo ukatongozananaye halafu kesho yake mkafanya tendo la ndoa. Mfano, tuchukulie sisi hapa tulivyokutana. Tunaweza fanya tendo la ndoa?” aliuliza Upendo, huku akiinuka pale alipoketi na kuanza kuzunguka zunguka pale sebuleni, pindi akisubiri jibu toka kwa Vumilia.
Vumilia alijibaragua pale sofani. Kwa kukuna kichwa, na kukizungusha huku na kule akifanya tafakuri ya jibu gani atoe kuhusu kile alichoulizwa. Akiwa katikati ya tafakuri, ghafla! Alishtushwa na mwanguko wa kitu kifuani kwake. Alivyotoa macho kuangalia ni kitu gani, alikumbana na sura ya Upendo. Kajilaza juu yake.
“Naomba tuondoke. Muda umeshakwenda sana, hilo swali utanijibu siku nyingine,” alisema Upendo, taratibu akinyanyuka.
Baada ya wote kunyanyuka, waliondoka. Moja kwa moja hadi kituo cha daladala kusubiri usafiri utaomrudisha Upendo atokako. Daladala ilivyowadia Upendo alipanda na Vumilia alirejea nyumbani kwa Lupeto alikofikia. Alimkuta Sabina akiwa kanuna, kisa kuchelewa. Halikuwa tatizo sana. Alimlaghai kwa maneno kadhaa kisha kumrudisha kwenye ukawaida wake. Japo hakufanikiwa, kutusua ngome ya Upendo, ila aliona dalili za mafanikio. Na kuamini, ipo siku, atajimwayamwaya juu ya ngome ya msichana huyo aliyeteka moyo wake kwa kiasi kikubwa. Upendo pekee ndiye aliyetawala kwa wakati huo. Ijapokuwa si mpenzi. Sabina alikuwa naye basi tu, kufurahisha haja zake. Usiku wa siku hiyo, waliutumia pamoja na Sabina, kwa kulala kitanda kimoja na kujifunika shuka moja. Hivyo walitumia vyema kwa mara nyingine nafasi hiyo kuburudisha yao mioyo. Waliingia ulimwengu wa huba kila mzuka ulivyopanda. Tena ili mambo yaende kiurahisi, Sabina alilala mtupu. Pale ahitajikapo, awe na shughuli moja tu, ya kugeuka ama kunyanyua maungo ya mwili wake katika mtindo wataoridhia kuutumia. Hadi kunako mapambazuko mambo yalinoga. Walipandisha vilima na kuteremka zaidi ya mara tatu, hadi harufu ya uchubuko wakahisi ipata, baada ya kilainishi kuanza kukauka.
Asubuhi kulivyopambazuka walianza pongezana kwa kile walichofanya usiku. Baada ya hapo walifanya usafi wa mwili kisha kila mmoja kuingia kwenye mihangaiko yake aliyopanga kuifanya siku hiyo. Sabina alielekea kazini kwake, na Vumilia alifunga safari kurejea mjini Dodoma. Safari iliyomuondoa jijini Dar es salaam saa 4 asubuhi baada ya kuagaaga baadhi ya rafiki na wengine alioanza nao kujenga mazoea kwa muda huo aliowasili. Muda wote pindi yuko safarini alikesha kuwasiliana na Upendo, kumtaarifu wapi kafikia na hali gani aliyonayo. Sabina ilikuwa kwa nadra sana, yote ni kutokana ni kiasi kidogo alichonacho kwa msichana huyo. Mwingi ulisheheni kwa Upendo, na ndiye alipewa nafasi kubwa. Japo alimtambua kama rafiki, huku akitumia njia hiyo kumsogeza karibu aingie himayani. Hata upendo, alionekana kuwa na mapendo kwa wingi kwa Vumilia. Kwani unyenyekevu aliouonesha, ni zaidi ya rafiki. Tena kwa sauti yake ileile aipendayo kuitumia pindi wawasilianapo. Aliyosadiki kuwa ni mapozi. Kila baada ya nusu saa, alipiga simu ama kutuma ujumbe mfupi kumtaka Vumilia amueleze maendeleo ya safari naye kumpa hamasa asitawaliwe na uchovu.
“Usisahau kupata chakula na kunywa maji mengi. Umenisikia Vumi, my dear?”
“Yeah! Nimekusikia na kukuelewa pia.”
Hadi anawasili mjini Dodoma saa 4 usiku, wawili hao waliendelea kuwasiliana. Basi alilopanda lilichelewa kuwasili baada ya kupata hitilafu njiani, mbele kidogo ya maeneo ya Chalinze.
“Vipi kuhusu kula chakula cha usiku?” aliuliza Upendo baada ya kutaarifiwa kashawasili nyumbani.
“Kuna rafiki yangu nilimuomba anisaidie juu ya hilo. Na nashukuru kaweza kunitekelezea. Nimekuta chakula kaniandalia.”
“Kula basi, kisha upumzike. Ama utahitaji tuzungumze japo kwa uchache?”
“Kwa leo hapana. Tufanye kesho.”
“Ok! I miss you!”
“I Miss you too!”
“Uwe na usiku mwema.”
“Nawe pia.”
“Bye!”
“Bye!”
Simu ikakatwa.
****
Kutoka siku hiyo mawasiliano yalianza zaidi baina ya wawili hawa. Upendo alijivika uhuru wa kufanya maongezi muda wowote atakao. Si usiku si mchana. Na pale alipokosa mrejesho mapema, wa kupokelewa ama kujibiwa ujumbe hulalamika kana kwamba wamekaa mwaka mzima pasipo kuwasiliana. Muda huohuo apigao, ndiyo muda aliohitaji simu yake ipokelewe. Isipopokelewa, akapiga kwa mara ya pili ikapokelewa, basi huanza na malalamiko.
“Vumi! Ushanichoka?” aliuliza Upendo, siku moja baada ya kupiga simu takribani mara tatu pasipo kupokelewa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hapana, siwezi kukuchoka, wala kuruhusu hiyo hali moyoni mwangu.”
“Kwanini sasa nakupigia simu mara zote hizo hunipokelei?”
“Sikusikia awali ulivyopiga. Naomba uniwie radhi.”
“Muongo Vumi. Mara zote hizo?” aliuliza Upendo, kwa sauti iliyoonekana kujaa kasiriko moyoni mwake.
“Kweli Upendo. Niamini, siwezi kukuongopea.”
Hiyo ndiyo ilikuwa kawaida yao kila uchao. Pale simu isipopokelewa kwa wakati. Na endapo Vumilia hatopatikana, malalamiko huwa maradufu ya kutopokea kwa wakati. Hasa kutopatikana wakati wa usiku.
“Kwanini ulinizimia simu jana usiku?”
“Simu haikuwa na chaji Upendo. Ilijizima, na luku ilikuwa imekata. Hivyo sikuwa na sehemu mbadala ya kupeleka kwa ajili ya kuchaji.”
“Toka lini simu yako haipatikani? Mbona unaanza nifanyia mambo ya ajabuajabu Vumi siku hizi. Eeh!...kama ushanichoka niweke wazi.”
“Hapana. Usinihisi vibaya. Amini nikuambiacho.”
Naam! Chembe chembe za mapendo thabiti, baina ya wawili hawa zilionekana wazi, ila kila mmoja hakutaka kuzibainisha kwa mwenziye kwa kutamka, bali ni kwa vitendo. Na daima ijulikanavyo siku zote, mtoto wa kike huwa ni mgumu kumtongoza mtoto wa kiume. Hata awe na upendo naye kiasi gani, atatumia vitendo kuonesha hisia zake. Vumilia alikuwa katika wakati mgumu. Matendo atendewayo dhahiri, yalimsukuma, azidishe hisia za kumhitaji Upendo, awe mpenzi wake. Kila uchao, alifikiria namna ya kutoa kauli, ila aliingiwa na hofu nyingi kila atakapo kuzungumza. Udini, ilikuwa sababu moja wapo. Upendo ni mkristu, yeye muislam. Itakuaje akihimhitaji awe mama wa familia? Lilimuumiza sana akili swali hilo. Kingine kilichomzidishia kumpatia maumivu, alikuwa na uhitaji wa kumtamkia kauli za hitajio hilo waonanapo. Ana kwa ana na si njia nyingine. Alishindwa kujiongeza kabisa. Alibaki na maumivu yake, huku siku zikizidi yoyoma.
Pindi hayo yakiendelea, upande wa pili napo mambo yaliendelea vivyo hivyo. Upande wa Sabina. Walikuwa wanawasiliana kama kawaida na kwenye shida za hapa na pale hawakukosa saidiana. Hasa za kifedha. Na kihisia pia. Japo si sana kama ilivyokuwa kwa Upendo. Pale ilipotokea Sabina kulalamika kwanini, hali iko hivyo, hakukosa cha kujibiwa. Majukumu ya kazi yalikuwa chaka la maswali aulizwayo. Ila Sabina hakuchoka. Aliendelea na dhamirio lake. Naye alijipambanua kuwa na mapenzi ya dhati kwa Vumilia. Ilhali Vumilia, hata chembe ya mapenzi kwake hakuwanayo. Upendo alimteka akili.
Ilikuwa ni Septemba 16, 2016. Vumilia alipokuwa na haja kwa kiasi kikubwa kuwa juu ya ngome ya mwanamke. Haja zilirundikana, miezi kwa miezi, kwani toka apambane na Sabina jijini Dar es salaam hakukutana na msichana mwingine. Hivyo kukutana na huyohuyo ikamlazimu. Kwani kwa wakati huo alishaacha habari za kwenda kuwatembelea wadada wajiuzao na kumaliza haja zake. Alimpanga. Kisha kumueleza hitajio lake. Lililokubaliwa kwa furaha sana na Sabina. Alimuahidi, amtafutie nauli tu, kuja lazima. Vumilia naye pasi na hiyana alitii. Jitihada alizifanya. Kumsafirisha mbeba mizigo wa haja zake, alishageuka hivyo. Kwa sababu hakuwa na mapendo naye. Mapendo yalikuwepo pale tu apandwapo na nyege. Pesa ya nauli iliandaliwa. Usiku wa saa sita akaituma, kisha kusubiri mrejesho wa kumhakikishia ujio ndani ya Dodoma.
Siku iliyofuata Sabina, akampatia uhakika. Wa ujio wake ndani ya mji huo na kujenga matumaini ya nguvu. Kwamba haja zimsumbuazo, zinakuja ondolewa. Tena kwa kumuaminisha zaidi, kuna muda alipigiwa simu kuulizwa Dodoma sehemu gani anakoishi, naye kumfungukia kwa ufasaha. Dakika saba baadaye toka aulizwe mahali anakoishi, Sabina alipiga simu kumtaarifu jambo.
“Niambie mrembo wangu,” alisema Vumilia kumpamba mambo yasiharibike mara baada ya kupokea simu.
“Niko poa. Kuna jambo nahitaji baadaye nikueleze mpenzi wangu.”
“Jambo gani hilo, unaloshindwa kulitamka sasa?”
“Baadaye ndiyo vizuri. Kuwa na uvumilivu.”
“Sawa. Wala hamna shida,” alisema na kukata simu.
Punde, machale fulani yakamjia. Alihisi jambo. Aliloahidiwa kuambiwa, lakini wazo lake hakulipa nguvu sana. Lakini lilimchukulia muda kulitafakari.
“Hamna jambo lingine zaidi ya kuniambia safari kaghairisha,” aliwaza.
Kweli! Jioni ilivyowadia, alipigiwa simu. Kama alivyohisi mchana, maelezo ya Sabina yakapita humohumo. Alighairisha safari. Kwa kigezo cha Mama atabaki katika mazingira magumu. Kauli iliyompandisha hasira, na kutapakaa kooni, rundo si ya mchezo, laiti huyo amuambiaye angelikuwa karibu angelichezea vitasa vya kutosha. Hata kumjibu ilimuwia ugumu. Aliamua kukata simu na kuendelea na shughuli nyingine. Sabina alivyopiga mara ya pili kuulizia kulikoni. Alipatiwa jibu jepesi lenye maneno machache na kuombwa akate simu. Kauli iliyokuwa ngumu kutekelezwa kwa Sabina kiurahisi.
“Kwa hiyo umekasirika?”
“Hapana kuwa na amani. Niko kawaida.”
“Amani ipi wakati unaonekena kubadilika?”
“Huo ni mtazamo wako tu. Ila niko vilevile nilivyokuwa awali.”
Baada ya majibizano ya muda mrefu yaliyokosa jibu muafaka, Sabina akakata simu. Simu ilivyokatwa, ilimpatia nafasi ya upembuzi. Zipi mbichi, zipi mbivu.
“Huyu ananiona sina akili. Kwa hiyo kaamua kula hela yangu kirahisi hivyo? Kama kuhusu mambo ya mama mwanzoni hakutambua hilo? Katambua baada ya kutumiwa pesa? Hapana! Huo ndiyo mwishowe wake. Asahau kuhusi mimi,” alisema kimoyomoyo.
Uchungu wa kuteswa, hasa mapenzi ulikuwa mgumu kutambulika kwa Vumilia. Hakujua maana ya kuteswa. Kwa sababu hakuwa na mpenzi wa kudumu maishani mwake. Hivyo lile aliamualo, haraka mno, hujidhatiti kulitekeleza. Akiapa, kaapa. Kamwe havunji mwiko wa kiapo chake.
Habari za yeye na Sabina akaziweka kuwa mapisi. Kwani kila alivyokuwa anapigiwa simu, alikuwa hapokei, atumiwapo ujumbe hajibu na hata akibadilishiwa namba akapigiwa akigundua kuwa ni Sabina humkatia simu.
Mapenzi yao yakawa yameishia kwa namna hiyo. Japo Sabina alijitahidi sana kuomba radhi, kwa njia za ujumbe mfupi na kuwatumia baadhi ya marafiki zake na wale wa Vumilia aliobahatika kufahamiana nao. Kwa kuwa mapendo juu ya huyu binti hayakuwa ya kina sana, kama ilivyokuwa kwa Upendo, radhi zake hakuzijadili. Alizipotezea na kuendelea kumpoteza fikrani. Sasa alihamia rasmi kwa Upendo. Zile hisia chache zilizokuwepo kwa Sabina awali, alizihamishia moja kwa moja kwa Upendo. Tena mazima pasipo bakisha ya akiba pembeni, itayotumika kumliwaza endapo mambo yataenda vibaya baadaye. Upendo naye alizipokea kwa mikono yote miwili, kisha kuzionyesha za kwake pia zipokelewe kwa kadri atavyoweza. Ili waende sambamba hadi hatua ya mwisho watayothubutu kufikia.
Haja ya kutoa makamanda wake waliorundikana kwa muda mrefu ikaanza msumbua. Kwa namna yoyote alilazimika kupata msichana, atayekuwa kwenye mahusiano naye kwa kujishikiza, wakati huo akiendelea na mipango ya kumvuta karibu Upendo awe himayani. Katika kulitimiza hilo, alibahatika kupatiwa namba ya msichana, na mmoja wa rafikiye anayefanya naye kazi pamoja. Ajulikanaye kwa jina la Maguta. Kisha kutunishiana misuli, waoneshane nani mwenye kisu kikali. Punde alivyopatiwa, Vumilia aliruka hewani kuwasiliana na msichana huyo, aliyetambulika kwa jina la Zamzam, mwenyeji wa Kondoa, mkoani Dodoma. Hapa hakukawiza. Mapema tu, alijieleza. Kisha kupatiwa jibu siku kadhaa mbeleni. Alikubaliwa, jambo lililopelekea kumsahau Sabina moja kwa moja. Hakuhitaji kuwa na mazoea naye tena.
Raha ya mahusiano matumu yaanzapo. Yakishakwiva, huibua hali zingine. Ndivyo ilivyokuwa. Kwa Vumilia na Zamzam. Baada ya mahusiano yao kuchukua muda mrefu, mdudu aharibuye, mahusiano akaingilia kati. Imani potofu! Ile raha ya mapenzi waliyokuwa wanapeana awali, ilianza dorora. Upendo akiwa chanzo. Vumilia hakuonesha dalili za kumthamini wala kumjali Zamzam. Alimthamini pale alipohitaji kutimiza haja zake, ila hilo halikumfanya Zamzam apunguze mapendo yake. Alimpenda sana, tena sana. Na alithibitisha mapendo yake kwa kauli na vitendo lakini Vumilia hakuambilika.
Ilikuwa kawaida, Zamzam kuachwa kitandani usiku, kisha Vumilia kutoka nje kuongea na Upendo zaidi ya masaa mawili. Amalizapo ndipo hurejea. Ilimuumiza, wakati mwingine alitamani kupokea simu Upendo apigapo, lakini alikatazwa kufanya kitendo hicho lengo asiharibu mahusiano yaliyopo. Vumilia alikuwa anampenda sana Upendo, zaidi ya wasichana wote aliobahatika kuwanao. Zamzam alivumilia yote. Katika kuhakikisha mahusiano yao yanadumu. Hakuruhusu manyanyaso, yadhoofishe afya na akili ya mwili wake. Juu ya hayo matukio alilazimisha kuipata furaha na amani ya moyo maisha yaendelee.
Matendo aliyokuwa anatendewa na Upendo, yalimhakikishia Vumilia kuwa huyo ni mwanamke pekee wa maisha yake. Aliendelea na imani hiyo, iliyowadharau wasichana wote alioshuhudia usichana wao, kwa kuwaona si chochote, na kuwafanya watumwa kisa tu kagundua asilimia kubwa wengi wao wanampenda. Maisha yaliendelea. Kwa namna hiyo. Zamzam kujipendekeza na Sabina naye hakuwa nyumanyuma kuendelea kuombeleza mahusiano ya awali yarejee. Lakini mambo yalikuwa tofauti. Upendo alipatiwa nafasi kubwa kadri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele. Dalili za waziwazi ziliwabainisha, zilizowatambulisha kwa kila mmoja aliyefahamu mawasiliano yao kuwa ni wapenzi. Hasahasa maongezi yaliyozidishwa usiku wa manane. Vilevile kitendo cha Upendo kulia afanyiwapo vibaya, ama ashindwapo kusikilizwa, kilichangia pia. Kuwapatia hisia nyingi watazamaji. Kwani ilifikia hiyo hatua. Upendo kuangusha chozi, mbele ya Vumilia simuni, kutoa machungu yake akosewapo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Vumi!” aliita Upendo, usiku mmoja majira ya saa tatu.
“Naam!” aliitikia Vumilia kwa sauti iliyojaa bashasha.
“Mbona unanijali sana? Ama unanipenda?” aliuliza Upendo. Kisha kufuatia kimya kwa muda mfupi.
Vumilia alitulia kwa muda kutafakari, baada ya hapo ndipo alijibu swali aliloulizwa.
“Ndiyo Upendo. Nakupenda!”
“Mbona hukuniambia?”
“Nilikuwa nasubiri siku tu. Ila nilikuwa na imani ipo siku ningekupatia ujumbe huu.”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment